Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Page 1

Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur'ani Tukufu

Kimeandikwa na: Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani

4:14 PM

Page A


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

Š Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 06 - 5 Kimeandikwa na: Sheikh Abdul-Karim Al-Bahbahani Kimetajumiwa na: Hemedi Lubumba Selemani Kimehaririwa na: Abdallah Mohammed Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab. Toleo la kwanza: Augasti, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

4:14 PM

Page B


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page C

YALIYOMO Utangulizi....................................................................................................2 Maana ya laana Kilunga na tofauti iliyopo kati yake na maana ya Tusi na Kashifa...................................................................................................... 2 Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu..................................................................4 Kwa muibu na Sunna Tukufu......................................................................4 Si za laana na mlaanifu kwa mujibu wa kitabu na Sunnah.........................5 Laana ni dharura ya kiitikadi.......................................................................9 Msimamo wa kambi ya Kisunni katika suala la laana..............................16 Msimamo wa kambi ya Ahlul-Bait katika suala la laana.......................... 18 Muhtasari wa Uchambuzi..........................................................................74


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page D

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya AHLUL-BAYT ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanachuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa Ahlul-Bayt. Wanachuoni waliyokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikra kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt imefanya hima kutetea tukufu za ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bayt na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanachuoni wa kambi ya Ahlul-Bayt katika dhamira hii ni vya aina ya pekee, kwa sababu una nguzo ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na uzalendo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanaharakati wenye fani maalumu mazungumzo ambayo yanaituliza akili na yanapokewa na maumbile sala-


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page E

ma. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bayt limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya nchi zenye chuki dhidi ya uislamu na waislamu. Jumuiya imejiepusha na udadisi uliokatazwa na ni yenye kuhangaikia kuzidadisi akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalum toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tunachokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulio nao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aidhihirishe juu kuliko dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. JUMUIYA YA KIMATAIFA YA AHLUL-BAYT KITENGO CHA UTAMADUNI


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page F

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la, Mafhumu ‘l-La’na wa ‘s-Sabb fi ‘l-Qur’ani l-Karim. Sisi tumekiita, Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu, kilichoandikwa na Sheikh Abdul Karim al-Bahbahani. Kitabu hiki, Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu, ni matokeo ya kazi ya kielimu iliyofanywa na mwanachuoni huyu wa Kiislamu. Kitabu hiki ni majibu kwa wale wanaowashutumu Mashia kwamba wanawatukana masahaba, shutuma ambazo zimekuwa zikitolewa kwa karne nyingi sana licha ya wenyewe Mashia kukana shutuma hizi kwa nguvu sana. Kwa bahati mbaya, shutuma hizi zilikuwa zikijibiwa kwa lugha za kigeni, hususan Kiarabu na Kiingereza, na kuwaacha wasomaji wa Kiswahili wasijue chochote kuhusu suala hili. Basi kitabu hiki ni moja ya vitabu vinavyotoa majibu ya shutuma hizo kwa lugha ya Kiarabu, ambacho tumekitarjumi kwa lugha ya Kiswahili. Kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masu-


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page i

ala ya kidini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba Selemani kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania

i


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

ii

7/1/2011

4:14 PM

Page ii


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

1

7/1/2011

4:14 PM

Page 1


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 2

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

UTANGULIZI Shia wa sasa na wa zamani, wote wametuhumiwa kuwatukana maswahaba na kuwalaani, na kwa ajili ya tuhuma hii wamepatwa na matatizo na machungu mengi baada ya kuhukumiwa kuwa wao ni makafiri. Jambo ambalo limefanya suala la laana na kulaani lifuatiliwe na watu wengi na wajiulize kuhusu ukweli halisi wa laana ndani ya sheria, hukumu yake na mipaka yake mbalimbali. Ewe msomaji mpendwa! Somo lililomo mikononi mwako ni jaribio makini katika mwelekeo huu ambalo ndani yake tunajaribu kuangazia macho maana ya kulaani kilugha (kiarabu) na kwa mujibu wa Kitabu na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na tutazame msimamo wa kambi mbili: Kambi ya Sunni na kambi ya Ahlul-Bayt kuhusu suala hilo. Hayo yote ni kwa lengo la kutaka kufikia matokeo halisi katika suala hili, na muhimu zaidi ni kuchunguza ukweli wa tuhuma ya kuwatukana maswahaba wote ambayo Shia wanatuhumiwa nayo.

MAANA YA LAANA KILUGHA NA TOFAUTI ILIYOPO KATI YAKE NA MAANA YA TUSI NA KASHIFA Ar-Raghibu Al-Isfahan amesema: “Laana: Ni kufukuza na kutenga mbali kwa njia ya kuchukizwa. Na ikitoka kwa Mwenyezi Mungu ni adhabu ya Akhera na kutokupata rehema Zake na tawfiki Yake duniani. Na ikitoka kwa mwandamu ni kumuombea mabaya mwenzake.”1 At-Tarihi amesema: “Laana: Ni kufukuzwa kutoka kwenye rehema…. Na waarabu zamani ilikuwa mtu miongoni mwao anapoasi humtenga mbali na wao na kumfukuzia mbali ili madhara yake yasiwapate, hivyo husema: Laana ya kizazi cha fulani…”2 1 Al-Mufradat: 471. 2 Majmaul-Bahrain 6: 309.

2


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 3

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Ibnu Athir ndani ya kitabu An-Nihayah amesema: “Asili ya laana ni kufukuzwa na kutengwa na Mwenyezi Mungu. Na kutoka kwa viumbe ni tusi na dua mbaya.”3 Pia maana hii imetajwa na Al-Jawhar ndani ya Sahih yake4. Hii ndio maana ya laana kilugha. Ama kuhusu tusi, Ibnu Athir amesema: “Tusi ni kashfa.”5 Na hiyo ndio kauli ya Al-Jawhar6, At-Tarih7 na Ibnu Mandhur8, kama kwamba maneno hayo mawili yana maana moja, isipokuwa aliyetaja tofauti yake ni Al-Isfihan ndani ya Al-Mufradati, nayo ni: “Tusi ni kashifa iumizayo.”9 Na kashifa kwa At-Tarih ni: “Kuelezea kitu kwa kuonyesha fedheha na upungufu.”10 Na kwa Ibnu Mandhur ni: “Maneno machafu yasiyo na laana.”11 Kwa muhtasari ni kuwa laana ikiwa ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu maana yake ni kufukuzwa kwenye rehema, na ikiwa ni kutoka kwa binadamu maana yake ni kuomba dua ili utengwe. Hivyo yenyewe ni kitu kingine kisichokuwa tusi wala kashifa ambayo yenyewe humaanisha maneno machafu yanayotumika katika kufedhehesha na kuaibisha. 3 An-Nihayah 4: 255. 4 As-Sahahu 4: 2196. 5 An-Nihayah 4: 330. 6 As-Sahahu 1:144. 7 Majmaul-Bahrain 2: 80. 8 Lisanul-Arab 1: 455. 9 Al-Mufradat: 225. 10 Majmaul-Bahrain 6: 98. 11 Lisanul-Arab 12: 318.

3


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 4

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

KWA MUJIBU WA QUR’ANI TUKUFU Kama ambavyo lugha (Kiarabu) imetofautisha kati ya laana na tusi na kashifa pia Qur’ani tukufu nayo imetofautisha kati ya maana hizo mbili, kiasi kwamba utaikuta imetumia neno (laana) mara thelathini na saba ikinasibisha na Mwenyezi Mungu na mara moja ikinasibisha na watu. Matumizi haya yenyewe tu yanaonyesha kuwa asili yake imeruhusiwa kisheria. Wakati neno (kutukana) limepatikana mara moja tu tena katika muundo wa kukataza, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wala msiwatukane wale ambao wanawaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, wasije wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila kujua.” Sura Al-Anam: 108. Kukatazwa huku kunaonyesha ubaya wa kutukana na kukashifu, na laiti kama laana ingekuwa inashirikiana nayo katika ubaya huo basi Qur’ani tukufu ingeikataza, hivyo kitendo cha Qur’ani tukufu kutokuikataza, kisha kuitumia na kuinasibisha na Mwenyezi Mungu ni dalili kuwa yenyewe ni jambo sahihi kwa mujibu wa sheria na linahitajika

KWA MUJIBU WA SUNNA TUKUFU Tunapokuja ndani ya Sunna tukufu tunaikuta imejaa mamia ya maelezo ambayo ndani yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia laana dhidi ya maadui wa ujumbe wakiwemo mushirikina, wanafiki na watu wa kitabu, na dhidi ya hali mbalimbali kutoka kwa waislamu akionyesha kukasirishwa kwake sana na makosa wanayoyatenda, au akiwapa tahadhari kali dhidi ya kukurubia makosa makubwa na yenye kuangamiza. 4


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 5

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Mwandishi wa kamusi ya misamiati ya Hadithi za Mtume katika neno (laana) amekusanya karibu anuani mia tatu za Hadithi za Mtume zote zikianza kwa neno (laana)12, japokuwa hakuwafikishwa kukusanya Hadithi zote za mlango huu, hivyo akapitwa na baadhi ya Hadithi mashuhuri kama ile ya Mtume (sa.w.w.) kumlaani yule aliyetengana na jeshi la Usama.13

SIFA ZA LAANA NA MLAANIFU KWA MUJIBU WA KITABU NA SUNNAH Tunapozitazama Aya zinazozungumzia laana ndani ya Qur’ani tukufu tunazikuta katika makundi manne: Zipo zilizoelekeza laana kwa Ibilisi, mfano kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na hakika laana Yangu itakuwa juu yako mpaka siku ya Malipo.” Sura Swad: 78. Na nyingine ni Aya zilizoelekeza laana kwa makafiri wote, mfano kauli ya Mwenyezi Mungu

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto uwakao.” Sura Al-Ahzab: 64. 12 Mawsuat Atraful-Hadithi An-Nabawi, Juzuu ya sita: 594 – 707. 13 Imenukuliwa kutoka kwenye kitabu As-Saqifah Wafadak cha Abu Bakr AlJawhari (mwaka 30 A. H.).

5


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 6

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na zipo zilizoelekeza laana kwa watu wote wa kitabu na kwa mayahudi tu, mfano kauli ya Mwenyezi Mungu

“Wamelaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa wana wa Israeli kwa ulimi wa Daud na wa Isa bin Mariam.” Al-Maidah: 78. Na za kundi la nne zimemwaga laana juu ya anuani za mienendo bila kubagua na hivyo kuwajumuisha waislamu, mfano anuani ya waongo, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na mara ya tano kwamba: Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.” Sura Nur: 7. Na anuani ya madhalimu, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sikilizeni! Laana ya Mwenyezi Mungu iko juu ya madhalimu.” Sura Hud: 18. Na anuani ya wenye kumuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Kwa hakika wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, Mwenyezi Mungu amewalaani katika dunia na Akhera.” Sura AlAhzab: 57. Na anuani ya wenye kuwasingizia wanaojiheshimu, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu: 6


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 7

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Bila shaka wale wanaowasingizia wanawake wanaojiheshimu, wasiojua, walio waumini, wamelaaniwa katika dunia na Akhera.” Sura Nur: 23. Na anuani ya wenye kuua, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na mwenye kumuua muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo ataishi milele, na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” Sura AnNisai: 93. Na anuani ya wanafiki, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wanafiki wanaume na wanafiki wanawake na makafiri Moto wa Jahannam watakaa humo milele. Huo unawatosha na Mwenyezi Mungu amewalaani na wana adhabu ya kudumu.” Sura Tawba: 68. Na anuani ya wenye kufanya uharibifu na kukata ujamaa, hiyo ni katika kauli ya Mwenyezi Mungu:

7


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 8

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Na kama nyinyi mkipata utawala ni karibu mtaiharibu nchi na mtaukata ujamaa wenu. Na ndio Mwenyezi Mungu amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao.” Muhammad: 22 – 23. Kama kwamba Qur’ani tukufu katika laana inaanzia kwenye alama ya shari inayowakilishwa na Ibilisi na kuendelea mpaka kwenye makundi ya wanadamu ambayo yanamkubali na kuitikia wito wake, hivyo inaanza na makafiri kama kundi la kwanza kisha watu wa kitabu kama kundi la kati, na makundi yote mawili ni maadui wa nje wa Uislamu, kisha inaendelea hatua kwa hatua mpaka ndani ya wigo wa Uislamu na hapo inaanza kuelekeza laana kwa maadui wa ndani wa Uislamu kama vile wanafiki, kisha inahama mpaka kwenye kundi la mwisho la msitari wa shari nao ni madhalimu, wauaji, wanaowasingizia waliyojiheshimu na wanaokata ujamaa, yaani kundi ambalo linatishia kusambaratisha muundo wa jamii. Hivyo Qur’ani inaendelea kuulaani msitari wa shari kuanzia makundi yake yenye kupiga vita Tauhidi na Uislamu kwa nje mpaka makundi yake yenye kupiga vita kwa ndani na kuendelea mpaka kwenye makundi ya kijamii ambayo yanatishia na kuhatarisha jamii ya kiislamu huku yakipotosha sera zake na harakati zake za njia ya wema na mafanikio. Na atakayefuatilia kwa makini kwa kulinganisha kati ya Kitabu na Sunna tukufu katika suala hili atafumbukiwa kwa uwazi kabisa kuwa Sunna tukufu imejikita sana na kwa mapana zaidi katika kulilaani kundi la mwisho kuliko makundi mengine, na dalili juu ya hilo ni kuwa laana ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imeshuka juu ya anuani za kijamii, kama vile laana dhidi ya pombe, riba, rushwa, mzuia sadaka na Zaka na mengineyo, kama ilivyo wazi kutoka kwenye anuani za mlango huu wa Hadithi za Mtume zilizomo 8


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 9

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kwenye vitabu vya Hadithi.14

LAANA NI DHARURA YA KIITIKADI Kutokana na maelezo yaliyotangulia imebainika kuwa laana kiasili ni suala la kiimani la dharura ambalo jamii ya kiislamu inalihitaji ili kuimarisha na kumakinisha misingi ya Uislamu kama inavyopasa, na kuondoa makapi kutoka ndani yake na kudhihirisha kuchukizwa na kutoridhishwa na kila kinachopeleka upande wa shari na batili kwa mahusiano yoyote yale, kama vile makafiri kwa upande wa nje na wanafiki kwa upande wa ndani, na sababu za kusambaratika jamii ambazo husaidia harakati za maadui kwa ndani na nje kufikia malengo yao machafu na kuzuia harakati za jamii za kiislamu zisifikie malengo yake. Na yenyewe ni tamko la kiimani juu ya haja ya kumakinisha kitenganishi cha kinafsi na kitamaduni na kilugha ndani ya maisha ya mwislamu kati ya Uislamu upande mmoja, na msitari wa ukafiri, unafiki na uovu ambao unapambana na Uislamu kwa ndani na nje upande wa pili. Laana kwa maana hii na ufahamu huu haina uhusiano wowote ule na tusi ambalo lenyewe ni msamiati wa maadili yanayopingana kwa ukamilifu na maadili ya kiislamu. Bali maana yake kiimani kwa upande mmoja ina uhusiano wa karibu sana na ile maana ya utawalishaji na kujitoa katika dhima, na kwa upande wa pili ina uhusiano wa karibu mno na faradhi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Hiyo ni kwa sababu laana anashushiwa yule mtu ambaye kiimani inapasa mwislamu kutangaza kujitoa katika dhima yake, kama vile makafiri na wanafiki. Na juu ya sababu za uovu wa kijamii na anuani zisizokubalika katika mwenendo wa kijamii ambazo kisheria ni wajibu kwa mwislamu kuziondoa kwa mujibu wa faradhi ya kuamrisha mema na kukataza mabaya. Hivyo yenyewe ni tamko la kilugha 14 Rejea Mawsuat Atraful-Hadithi An-Nabawwi 6: 594 – 606.

9


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 10

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu juu ya faradhi mbili: Ya kiimani na kisheria, ndani ya wakati mmoja. Wala kutokana na maelezo hayo haimaanishi kuwa Uislamu na jamii yake unategemea laana kama silaha tegemezi katika kupambana na njia ya ukafiri, unafiki na uovu bali silaha tegemezi ndani ya Uislamu ni dalili na hoja na mantiki yenye hoja za kiakili ambayo Qur’ani imeielezea kwa lugha mbalimbali. Na tukifuatilia matumizi ya matamshi ya kilugha ndani ya Qur’ani yenye uhusiano na fikra, akili, dalili, hoja, elimu, uandishi na mfano wa hayo tutayakuta ni zaidi ya mara elfu mbili mia moja na tisini, ilihali matumizi ya neno laana ni mara thelathini na nane. Hivyo dalili na hoja ndio kanuni kuu ya imani ndani ya Uislamu, ama laana si chochote bali ni maelezo ya kilugha juu ya silaha ya kujihami ya ulinzi wa kuzuia mashambulizi, ambayo huikimbilia muislamu pindi anapohisi hatari, na mwenye kulaani hulaani baada ya kuwa na ushahidi wa wazi na hoja juu ya haki na baada ya kuthibiti ukaidi na upinzani toka upande wa pili. Ndiyo, imekatazwa laana isiwe ni tabia ya kudumu na njia ya kuendelea ambayo daima muislamu anapita juu yake, kama aliposema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Muumini si mtukanaji mno wala si mtiaji mno dosari wala si mwenye kulaani mno.”15 Na kauli yake (s.a.w.w.): “Muumini huwa hawi mwenye kulaani mno.” 16 Ni wazi kuwa anayeitwa mwenye kulaani mno ni yule ambaye laana inatoka ulimini mwake kwa namna ya kuendelea kwa sababu maalumu au bila sababu yoyote, ama ambaye analaani kwa kadiri ya mahitajio husika haitwi mwenye kulaani mno, kwa sababu tamko hilo (mno) hutumika kwa yule ambaye mara nyingi amekuwa katika hali hiyo, na hivyo mara nyingi hutumika kwa ambaye anafanya kitendo fulani kuwa kazi na shughuli yake, kama vile seremala na mchinjaji na wengineo, na ni wazi kuwa ambaye anachinja kichinjwa kwa dharura tu huwa haitwi mchinjaji, bali jina hili 15 Kanzul-Ammal 1: 146, Hadithi ya 720. 16 Kanzul-Ammal 3: 615, Hadithi ya 8178.

10


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 11

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu hupewa yule ambaye kazi hii ni shughuli yake ya kuendelea kila siku kama jukumu lake la kudumu kwake, hivyo laana ya namna hii na kukatazwa kwake hailazimishi asili ya laana ikatazwe. Hivyo asilan hakuna mgongano kati ya mambo hayo mawili. Al-Faydhu Al-Kashan amesema: “Ama Hadithi ‘Msiwe watoa laana mno,’ huenda alikataza kutukana kusiwe tabia yao kwa sababu ya kukithirisha kufanya hivyo, kiasi kwamba wanamlaani kila mtu kama inavyoonyeshwa na kauli yake (s.a.w.w.): ‘Watoa laana mno.’ Hivyo haimaanishi kuwa alikataza kulaani wenye kustahiki, kama si hivyo basi angesema: Msiwe watoa laana, kwani kati ya sentensi hizo kuna tofauti kubwa anaijua yule mfasaha wa lugha.” Ama ile iliyopokewa kuwa kiongozi wa waumini (a.s.) alikataza kuwalaani watu wa Sham ikisihi basi huenda (a.s.) alikuwa anataraji kuwa watasilimu na kumfuata, kama ilivyo kwa Rais mwenye huruma kwa raia wake, ndio maana akasema: “Lakini semeni: Ewe Mwenyezi Mungu suluhisha kati yetu,” na hii inakaribiana na kauli ya Mwenyezi Mungu katika kisa cha Firaun: “Na kamwambieni maneno laini.”17” Ndiyo, kiongozi wa waumini (a.s.) aliwakataza maswahaba wake kuwalaani watu wa Sham, na hili limetajwa ndani ya Nahjul-Balagha kwa anuani ya: “Maneno yake alipowasikia watu miongoni mwa maswahaba wake wakiwatukana watu wa Sham siku za vita vyao vya Siffin.” Na Ibnu Abil Hadid ameongezea kwa kusema: “Ambalo (a.s.) hakupendezwa nalo kutoka kwao ni kuwa walikuwa wakiwakashifu watu wa Sham na wala hakuwa akichukizwa na laana yao kwao na kujitenga nao, si kama wanvyodhani watu wa mtazamo wa chini, kwa kusema: Hairuhusiwi kumlaani yeyote mwenye jina la Uislamu na hawapendezwi na anayelaani. Na yupo anayevuka mipaka zaidi ya hapo kwa kusema: Simlaani kafiri wala simlaani Ibilisi kwani Mwenyezi Mungu hatomuuliza mtu siku ya Kiyama 17 Sura Twaha: 44.

11


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 12

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kwa nini haujalaani? Bali atamuuliza kwa nini ulilaani? Hakika maneno yao haya ni kinyume na maelezo ya Kitabu kwa sababu Mwenyezi amesema:

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewalaani makafiri na amewaandalia Moto uwakao.” (Sura Al-Ahzab: 64.) Na akasema:

“Hao hulaaniwa na Mwenyezi Mungu na hulaamiwa na wenye kulaani.” Sura Al-Baqara: 159. Na akasema kuhusu Ibilisi:

“ Na hakika laana Yangu itakuwa juu yako mpaka siku ya Malipo.” (Sura Swad: 78.) Na akasema:

“Wamelaaniwa popote waonekanapo.” (Sura Al-Ahzab: 61.) Na Aya kama hizo ndani ya Kitabu ni nyingi sana. Itawezekanaje kwa muislamu achukie kujitenga na mtu ambaye ni wajibu kujitenga naye? Hivi hawa hawajasikia kauli ya Mwenyezi Mungu:

12


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 13

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Hakika nyinyi mna mfano mzuri kwa Ibrahim na wale waliokuwa pamoja naye, walipowaambia watu wao: Kwa hakika sisi tu mbali na nanyi na hayo mnayoyaabudu kinyume cha Mwenyezi Mungu, tunakukataeni na umekwishadhihiri uadui na bughudha ya daima kati yenu na yetu.” (Sura Al-Mumtahinah: 4.) Na dalili inayothibitisha kuwa aliye muislamu atakapotenda dhambi kubwa inaruhusiwa kumlaani, bali inawezekana katika baadhi ya mazingira ikawa ni wajibu kumlaani kama ilivyo katika kutoleana laana kati ya mume na mke. Mwenyezi Mungu anasema katika kisa cha laana:

“Basi ushahidi wa mmoja wao utakuwa kushuhudulia mara nne kwa kiapo cha Mwenyezi Mungu, kwamba: Bila shaka yeye ni katika wasema kweli.* Na mara ya tano kwamba: Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.” (Sura Nur:67.) Na akasema kuhusu mwenye kumtuhumu mtu kwa zinaa:

“Bila shaka wale wanaowasingizia wanawake wanaojiheshimu, wasiojua, waliyo waumini, wamelaaniwa katika dunia na Akhera.” (Sura Nur: 23.) 13


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 14

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Aya hizi mbili zinawahusu waisilamu na Aya za kabla yake zinawahusu makafiri na wanafiki na kwa ajili hii alimwombea dua mbaya Muawiya na kundi la wafuasi wake ndani ya kunuti na akawalaani baada ya Swala. Na alilolikataza kiongozi wa waumini ni kuwakashifu baba zao na mama zao, kwani baadhi yao walikuwa wakiiaibisha nasaba ya kundi fulani miongoni mwao na mwingine akiwataja kwa uduni wa nasaba na mwingine akiwafedhehesha kwa uoga na ubahili na kwa baadhi ya michambuo ambayo washairi huchambuana kwayo, na namna yake inajulikana18, hivyo (a.s.) akawakataza hilo kwa kusema: “Mimi sipendi nyinyi muwe watukanaji lakini bora zaidi ni muelezee matendo yao na mtaje hali zao….” 19 Na kwa kutumia Hadithi zinazokataza kulaani tunaweza kuthibitisha kuwa zinaashiria lile tulilobainisha mwanzo kuwa silaha ya asili ya sheria ya kiislamu katika kuamiliana na msitari wa ukafiri na unafiki na uovu ni dalili na hoja, bali laana yenyewe ni kama silaha ya kujihami ambayo anaihitajia kila kiumbe hai na kila nidhamu ya jamii ili kujihami mwenyewe kimaadili na kijamii dhidi ya anayemfanyia uadui kwa nje na dhidi ya anayepotosha mwenendo wake kwa ndani. Maneno ya kustaajabisha sana ni yale aliyotamka Al-Ghazalii katika suala hili, pale alipodai kuwa: “Katika kuwalaani watu kuna hatari hivyo mtu ajiapeshe, na wala hakuna hatari katika kunyamaza bila kumlaani Ibilisi sembuse mwengine.” Kisha akasema: “Hakika tumesema haya kutokana na watu kutolitilia uzito suala la laana na kulitamka ulimini, na muumini huwa si mwenye kulaani mno, hivyo haipasi ulimi wake utamke laana ila juu ya aliyekufa akiwa kafiri, au makundi ambayo yanajulikana kwa sifa zao bila kuwataja watu binafsi, hivyo kujishughulisha na utajo wa 18 Kama lugha ya kejeli na kuchamba tunayoishuhudia ndani ya mashairi na beti za wanataarabu na mipasho ambayo kwa sheria ya dini ni haramu na uovu mkubwa kwa muislamu - Mtarjumi. 19 Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid 11: 22 – 23, Hadithi ya 199.

14


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 15

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Mwenyezi Mungu ni bora, na kama si hivyo basi kwenye kunyamaza kuna amani.”20 Katika maneno yake kuna eneo la uchunguzi litokanalo na maelezo yaliyotangulia, nalo ni kuwa laiti laana ingekuwa na hatari ndani ya jamii basi ingelazimika Qur’ani isiitowe na Mtukufu Mtume asiitowe na kuitekeleza. Maneno haya ya Al-Ghazalii yana aina fulani ya uzalendo wa chuki, kwani kwa ajili ya kumtetea Yazid na kuharamisha kumlaani amekimbilia kwenye kauli ambazo zinakomea kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila kutaka. Qur’ani tukufu inamlaani Ibilisi, hivyo laiti kusingekuwa na masilahi yoyote ya kiimani basi zisingepatikana Aya mbili zikimlaani, na maslahi ya kwanza kabisa ambayo tunaweza kuyajua ni kuimarisha na kukomaza ndani ya nafsi hali ya kuchukizwa na kutokupenda alama za shari, batili na uovu, jambo ambalo litasaidia kuwa katika msimamo na kuweka msitari mkubwa tenganishi kati yake na uovu, lakini pamoja na hayo yote bado AlGhazalii anadai kuwa ‘hakuna hatari yoyote katika kuacha kumlaani Ibilisi sembuse mtu mwingine.’ Huoni matokeo ya maneno yake haya ni kuondoa hekima ya Qur’ani?! Ama suala la watu kutolitilia uzito, hilo ni suala jingine na chanzo chake ni ujinga wa watu au siasa za watawala waovu ambao walimlaani kiongozi wa waumini na wafuasi wake mimbarini, mfano wa Muawiya na Yazid bin Muawiya na watawala ambao walikuwa wanapotaka kuwatendea baya wafuasi wa Ahlul-Bayt basi huwatuhumu kuwa wanawatukana mashekhe wawili21 ili iwe wepesi kwao kuwatendea watakalo kama utakavyoona huko mbele.

20 Ihyau Ulumid-Dini, 3:134 – 135, chapa ya Darul-Fikri. 21 Abubakr na Umar – Mtarjumi.

15


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 16

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Ama kutofautisha kwake kati ya kulaani makundi na kulaani watu binafsi jibu lake na uchambuzi wake vitakuja mbele. Ama kauli yake kuwa: “Hivyo kujishughulisha na utajo wa Mwenyezi Mungu ni bora, na kama si hivyo basi kwenye kunyamaza kuna amani,” ni rai binafsi juu ya suala husika, kwani kinacholazimu ni kuweka wazi hukumu ya laana, hivyo ikiwa kisheria inahitajika basi haina maana yoyote kusema kuwa: Kwenye kunyamaza kuna amani, na kama kisheria haihitajiki basi hapo ni lazima kuweka wazi kutokuruhusiwa kwake kisheria, hivyo maneno yake haya ni sawa na mawaidha binafsi juu ya hukumu za kifiqhi.

MSIMAMO WA KAMBI YA KISUNNI KATIKA SUALA LA LAANA Ukweli ni kuwa suala hili halina utata kati ya waisilamu upande wa asili yake, bali utata kati yao umejitokeza pale ufahamu wa laana yenye maana hiyo tuliyoibainisha ulipogongana na kanuni ya msingi miongoni mwa kanuni za kambi ya kisunni, nayo ni kanuni ya uadilifu wa kila swahaba ambaye aliishi zama za uhai wa Mtume (s.a.w.w.) akasuhubiana naye huku akiwa anamwamini. Hivyo kwa ajili ya uzito wa kanuni hii na kuitanguliza kwao mbele kabla ya kanuni nyingine wamelazimika viongozi wa kambi hii kuleta maana nyingine katika kila kinachopingana na kanuni hiyo miongoni mwa fikira na ufahamu, na hata matukio ya wazi ya kihistoria ambayo yanathibitisha uovu wa wazi juu ya baadhi ya maswahaba, na makosa ya wazi ambayo Qur’ani imeyathibitisha juu ya baadhi yao. Basi wakajaribu kutaka kuyakimbia kwa hoja ambazo hakuna yeyote mwenye akili anayeafikiana nao, na ni vigumu sana hata kwa wao wenyewe kukinaika nazo. Isipokuwa walipopita njia hii na kujizibia njia nyingine walijikuta wanalazimika kurukia kila neno ambalo wao wanadhani kuwa litawasaidia kutoka kwenye matokeo mabovu ya lazima yatokanayo na kanuni hiyo, japokuwa bora zaidi kwao ilikuwa ni kuyafanya matokeo hayo batili dalili ya ubatilifu wa kanuni hiyo. Na ufa16


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 17

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu hamu wa laana ni miongoni mwa mambo ambayo yanapingana na kanuni hii, hivyo wakazidi kung’ang’ania humo kwa kujikaza juu ya kanuni hiyo ambayo kwa ajili ya kuilinda na kuitetea wamepanda kila la uasi na baya, japokuwa sehemu kubwa ya maswahaba wa Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) wametenda matendo ambayo Qur’ani imeyaelekezea laana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) yeye mwenyewe akawalaani baadhi ya maswahaba kupitia sifa jumuishi, kama pia alivyowalaani wengine kwa kuainisha na kwa majina. Na japo haya yote ni sehemu ya historia isiyopingika lakini bado kambi ya kisunni inaamini kuwa:

Maswahaba wote ni waadilifu. Yote yanayopingana na uadilifu yaliyotokea kati yao vyovyote yatakavyofikia ni lazima kuyaletea maana nyingine yoyote inayonasibu kama ijtihadi na mfano wa hilo. Kuhukumu kwa mujibu wa makosa haya na kuyafanyia kazi matokeo ya kisheria na kiakili na kutoyaletea maana nyingine nzuri kunapelekea kuwatia dosari maswahaba walioyatenda na kufungua mlango wa kuwalaani na kuwaweka kwenye uovu. Kuwatia dosari baadhi ya maswahaba ni dhambi kubwa inayopelekea mwenye kuwatia dosari ima kuwa muovu au kafiri.22 Nukta hizi baadhi yake zinatokana na nyingine na kila moja kati ya hizo ni mbaya zaidi na mbovu kuliko ya kabla yake na zote zinakomea kwenye kanuni yao kuu inayohusu uadilifu wa maswahaba hata yule aliyetenda makosa ya wazi, bali hata yule ambaye Qur’ani imethibitisha uovu wake!!! Kuanzia hapa ndipo utata kati ya kambi mbili ulipoanza: Kambi ya kisunni na kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.) katika suala la laana, kwani kambi Ahlul22 As-Sawaiqu Al-Muhriqah: 375 – 389, chapa ya Darul-Kutub Al-Ilmiyyah.

17


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 18

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Bayt (a.s.) wanaamini kuwa watu wote katika sheria ya Mwenyezi Mungu ni sawasawa na kuwa yeyote atakayetenda kitendo chochote ambacho ndani ya Kitabu na Sunna kimeambatanishwa na laana na himaya basi matokeo haya yanamkuta sawa awe sahaba au mwanafunzi wa sahaba au mtu wa karne za baadae, na hasa kwa kuwa Qur’ani imethibitisha hilo juu ya baadhi ya maswahaba na ikawatolea laana hiyo, na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) imekusanya ushahidi mbalimbali juu ya kutuhumiwa, kulaaniwa na kutengwa kwa baadhi ya maswahaba. Ufuatao ni ufafanuzi wake:

MSIMAMO WA KAMBI YA AHLUL-BAIT KATIKA SUALA LA LAANA Ili tulifafanue vizuri kabisa suala hili kwa upande wa Ahlul-Bayt na liwe na uwazi utoshelezao ni lazima tulizungumzie kwa kufuata vipengele vifuatavyo:

Tofauti kati ya laana na tusi Kutokana na maelezo yaliyotangulia imebainika kuwa laana ni dharura ya kiimani ambayo jamii ya kiislamu yenye imani inaihitaji ili kulinda misingi yake ya kiimani dhidi ya maadui wa Uislamu wa ndani na wa nje, na dhidi ya baadhi ya tabia za kijamii ambazo zina hatari inayotishia kusambaratisha muundo wa jamii ya kiislamu, ilihali tusi ni msamiati wa kimaadili usiotakiwa na ni neno la kilugha lisilokubalika kwa mtazamo wa Qur’ani na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimamu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (a.s.).

Nadharia ya uadilifu wa kila sahaba si sahihi Maudhui hapa haijawekwa ili kujadili nadharia ya uadilifu wa kila sahaba, kwani maudhui hiyo inahitaji nafasi pana yenye kulingana na kitabu kizima au zaidi ya kitabu kimoja, lakini kwa sababu mada yetu ina uhusiano 18


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 19

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu na maudhui hii tumedharurika kuigusia kwa kiwango kinachonasibiana. Miongoni mwa kanuni za kiakili zinazokubalika kwa wenye akili ni kuwa dai lazima lilingane na ukubwa wa dalili, lakini likiwa kubwa kuliko dalili basi linageuka na kuwa dai lisilokuwa na dalili, na pindi unapopimwa ukubwa wa dai hutazamwa pamoja na matokeo yote ya lazima ya dai husika kisha ndipo linapopimwa lenyewe kati yake na dalili husika. Tunapokuja kwenye nadharia ya uadilifu wa kila sahaba tunaikuta inalazimu kupatikana matokeo mengi ya lazima ya kiakili na ya kisheria na yote si sahihi, miongoni mwa matokeo hayo ni: Hakika kuamini uadilifu wa sahaba kunalazimu kuamini kuwa sababu ya uadilifu kwa sahaba ni ule tu usuhuba wake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na wala si vitendo vya sahaba, hivyo maadamu yeye ni sahaba basi ni mwadilifu hata kama atatenda atakayotenda miongoni mwa makosa. Hakika makosa ya maswahaba ni lazima kuyaletea maana nyingine inayonasibiana, na kila inapokuwa vigumu kuleta maana na ikadhihiri kuwa tunalazimisha maana hiyo basi kipengele husika cha sheria hudhoofika na kupoteza hadhi yake na hukumu yake. Hivyo kutafsiri kuwa maswahaba ni mujtahidina, na mwenye kukosea kati yao hupata thawabu moja na mwenye kupatia thawabu mbili, jambo hilo linashusha hadhi ya ijtihadi ndani ya sheria ya kiislamu. Ni ijtihadi ipi hii inaruhusu maswahaba wauane wao kwa wao? Basi kuna tofauti gani kati yao na wanadamu wengine ambao wanauana wao kwa wao, na mengineyo, hivyo kuyatafsiri yote kwa maana ya kisheria kunashusha hadhi ya maana hiyo ndani ya sheria. Hakika imani ya uadilifu wa maswahaba inapingana na tamko la wazi la Qur’ani tukufu inayoonyesha kuwa miongoni mwao wamo wanafiki, waovu na wenye kumuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama itakavyokuja. 19


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 20

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Hakika imani ya uadilifu wa maswahaba inapingana na tamko la wazi la Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inayoonyesha kuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakasirikia na kuwaghadhibikia baadhi ya maswahaba zake kama itakavyokuja. Hakika imani ya uadilifu wa maswahaba inapingana na maana ya laana inayopatikana ndani ya Qur’ani tukufu kwa kuhusiha baadhi ya hali ambazo baadhi yake zimepatikana katika mwenendo wa baadhi ya maswahaba. Hakika imani ya uadilifu wa maswahaba inapingana na kanuni za tabia za binadamu ndani ya jamii kwani mwanadamu ambaye kabla ya kumwamini Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimpiga vita, tena mwenye kubobea kwenye ujahili kwa kila aina ya ubaya na uchafu itawezekanaje akili ikubali kuwa amekuwa mwadilifu kwa kutamka tu shahada mbili na kumsuhubu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.)? Hatukatai kuwa ni jambo linalowezekana lakini uwezekano huo ni kwa baadhi ya watu ambao ushahidi wa kivitendo umethibitisha kupatikana uadilifu kwao kivitendo, na si kwa jamii nzima kama jamii, kwani uwezekano ni kitu kingine na upatikanaji ni kitu kingine, kwani nadharia ya uadilifu wa maswahaba haizungumzii uwezekano bali yenyewe inazungumzia upatikanaji wa uadilifu kwa kila sahaba bila kujali matendo yao bali ni bila kukubali uchunguzi juu ya hilo. Na tunaweza kusema kwa yakini kabisa kuwa nadharia ya uadilifu wa maswahaba inapingana kwa ukamilifu na elimu za historia, jamii na saikolojia ambazo hazikubali kutoa hukumu za mjumuisho wa moja kwa moja zinazosifia kundi la watu fulani, kisha ukatafsiri matendo yao kwa namna inayooana na hukumu hizo. Na jambo ambalo linasisitizwa na tabia ya maisha pamoja na elimu hizi ni kuwa: Hukumu ya sifa nzuri au mbaya inatokana na matendo na wala matendo hayatokani na hukumu, na kwa ajili ya hukumu kutokana na matendo ni lazima tuchunguze matendo ya 20


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 21

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kila mmoja mmoja na tumtolee hukumu kila mmoja kwa kile anachostahiki, ima tumhukumu kwa sifa nzuri au mbaya. Wenye akili wemezoea kutoa hukumu juu ya kundi fulani la watu kwa kuangalia uwingi na aghlabu, Qur’ani imeridhia utaratibu huu hivyo nayo ikatoa hukumu juu ya baadhi ya makundi kwa namna hii, lakini maarufu ni kuwa katika hali kama hizi hukumu ya kundi haimgusi mtu mmoja mmoja, mfano inaposemwa: Wanaume wana nguvu kuliko wanawake, katika hukumu kama hii haimaanishi kuwa kila mwanaume ana nguvu kuliko wanawake wote, kwa sababu hukumu kama hii na mfano wake zimetokana na kigezo cha uwingi na aghlabu na wala haitokani na uchunguzi na laiti mtu akidai imetokana na uchunguzi basi dai lake litakuwa ni uwongo. Nadharia ya uadilifu wa maswahaba inahimiza uadilifu wa kila sahaba wala haikubali dhana ya uwingi na aghlabu, na hiki ni kielelezo cha wazi kabisa kinachobainisha ubovu wake. Baada ya kubainisha baadhi ya nukta juu ya nadharia ya uadilifu wa kila sahaba upande mmoja, na kuangalia mkazo wa kambi ya kisunni juu ya nadharia hii upande wa pili, sasa mchunguzi mwadilifu ana haki ya kujiuliza: Ni kwa ajili ya dalili ipi tunalazimika kuamini nadharia ambayo inalazimu kutenda mambo yote haya ya mfarakano na matokeo batili? Je, dalili juu ya nadharia hii imefikia nguvu, uwazi na mkazo wa kiwango hiki? Kiasi kwamba kutenda mambo haya ya mfarakano na matokeo batili ni suala jepesi kimantiki kuliko kuamini uadilifu wa baadhi ya maswahaba? Na je, kuamini uadilifu wa baadhi ya maswahaba na si wote kunalazimu makosa na mambo ya mfarakano yaliyo makubwa kuliko hayo? Kiasi kwamba tulazimike kuamini kuwa maswahaba wote ni waadilifu? Ukweli ni kuwa sisi sote tunapozitazama dalili wanazozileta juu ya nadharia ya uadilifu wa kila sahaba tunazikuta ni kundi la baadhi ya Aya na Hadithi zisizothibitisha dai hili, mfano: 21


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 22

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Waliotangulia ndio waliotangulia.* Hao ndio watakaokaribishwa.” (Al-Waqiah: 10 – 11.) Na Aya

“Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu na walio pamoja naye ni imara mbele ya makafiri na wenye kuhurumiana wao kwa wao.” (Sura Al-Fat’hu: 29.) Na Aya

“Kwa hakika Mwenyezi Mungu amewaridhia Waumini.” (Sura AlFat’hu: 18.) Na kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Karne bora ni karne ambayo nimepewa utume nikiwa miongoni mwao, kisha wanaowafuata kisha wanaowafuata.”23 Ni wazi kuwa lengo linaloonyeshwa na dalili hizi ni kukisifia kizazi cha maswahaba na kuwasifu kwa juhudi walizozifanya katika kuinusuru dini na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na hilo ni jambo linalokubalika kiakili hata kabla ya Qur’ani kwani maswahaba wa Mtukufu Mtume wao kama kizazi walikuwa ni mbegu ya jamii ya kiislamu duniani na ndio mwanzo wa kusambaa Uislamu ndani ya maisha, hivyo wao ni kipimo bora cha imani kuliko jamii yoyote ile ya wanadamu katika ardhi zama hizo, lakini hiki ni 23 Al-Fatawa Al-Kubra 4: 217.

22


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 23

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kitu kingine; na kuhukumu uadilifu kwa kila mtu miongoni mwao ni kitu kingine. Na tayari tangu mwanzo tumeshasema kuwa hukumu ya pamoja haimgusi mtu mmoja mmoja kwa sababu yenyewe inatokana na kigezo cha uwingi na aghlabu, ilihali hukumu ya mtu mmoja mmoja inahitaji uchunguzi wa pande mbili: Upande wa watu na upande wa matendo ya kila mtu muda wote wa maisha yake ndipo itasihi kwetu kusema: Watu wa kundi hili wote ni waadilifu. Aya zilizotajwa hazionyeshi uchunguzi wowote si katika upande huu wala upande ule, bali hapo uchunguzi haukubaliki kiakili kwa sababu maisha ya maswahaba wanaohutubiwa kwa Aya hizo bado hayajatimia mpaka tuseme kuwa: Zinaonyesha uadilifu wao, kwani baada ya hotuba hii au baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huenda watatenda mambo yanayokhalifu uadilifu, na tayari Aya nyingine zimeshatupa habari kuwa baadhi ya maswahaba wanaweza kuritadi na hilo ni kosa kubwa sana miongoni mwa mambo yanayopingana na uadilifu na hilo lilitokea kivitendo kama itakavyokuja. Na kwa kuwa uchunguzi hauwezekani basi tunaweza kusema kuwa: Hakika Aya zilizotajwa si kwamba hazionyeshi tu uadilifu wa maswahaba bali pia dalili hii yenyewe binafsi haijiwezi, kwani yenyewe ni tasa kwa sababu ya kutoweka mlengwa, kwani hakuna maana mbili: Moja inaonyesha uadilifu wa maswahaba na nyingine inaonyesha kusifiwa kwao tu, hata tuhitaji kuchagua iliyo bora zaidi kwa mujibu wa vielelezo na dalili. Bali maana ni moja katika Aya hizi nayo ni kuwa Aya hizi zinawasifia maswahaba kwa kuzingatia wao ni kizazi na kundi moja bila kujali mtu mmoja mmoja miongoni mwao, na maana hii imetamkwa wazi ndani ya maelezo na urithi wa kifikra wa Ahlul-Bayt (a.s.) kama tutakavyoona katika kipengele kifuatacho.

23


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 24

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Tunakiri ubora wa maswhaba kwa sura ya ujumla Imamu Ali (a.s.) anawazungumzia maswahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kusema: “Hakika niliwaona maswahaba wa Muhammad (s.a.w.w.) na sijamwona yeyote anayefanana nao miongoni mwenu, hakika walikuwa wakiamka na kutawanyika kama vumbi ilihali walilala wakiwa ni wenye kusujudu na kusimama huku wakijigeuza kati ya vipaji vyao na mashavu yao, na wakisimama kama wako juu ya kijinga cha moto kwa ajili ya kukumbuka marejeo yao, kati ya macho yao kukiwa kama magoti ya mbuzi kutokana na urefu wa sijida zao, Mwenyezi Mungu anapotajwa macho yao hububujika machozi mpaka vifua vyao vinalowa na wananepa kama unepavyo mti wakati wa upepo mkalli kwa ajili ya kuogopa adhabu na kutaraji thawabu.”24 Na anasema: “Wako wapi ndugu zangu ambao wamepita njia na wakapita juu ya haki? Yuko wapi Ammar, yuko wapi Ibnu At-Tayyhan, yuko wapi mwenye shahada mbili? Wako wapi mfano wao miongoni mwa ndugu zao ambao waliisoma Qur’ani kisha wakaiimarisha, na wakaizingatia faradhi kisha wakaisimamisha, walihuisha Sunna na wakaua Bidaa, waliitwa kwenye jihadi wakaenda na wakamwamini kiongozi kisha wakamfuata.”25 Na Miongoni mwa dua za Imam As-Sajjad Zaynul-Abidina Ali bin Husein (a.s.) ambazo zinapatikana ndani ya kitabu maarufu kwa jina la As-Sahifatu As-Sajadiyyah ambacho wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) hukitumia katika ibada mbalimbali ni dua hii: “Ewe Mola, wabariki wafuasi wa Mitume na wale wenye kuwasadikisha katika mambo ya ghaibu, wakati wapinzani wao wanapowapinga kwa kuwakadhibisha……. Ewe Mola, na maswahaba wa Muhammad hasa, ambao waliandamana naye kwa wema na ambao walipigana kishujaa kati24 Nahjul-Balagha – Subhi As-Saleh: 91. 25 Nahjul-Balagha – Subhi As-Saleh: 264 Hotuba ya 182.

24


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 25

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu ka kumnusuru, wakamsaidia na kufanya haraka katika kuunga mkono ujumbe wake na kuuitikia mwito wake, waliomwitikia mara tu alipowasikilizisha hoja za ujumbe wake, wakajitenga na baba zao, wake na watoto katika kudhihirisha neno lake, wakapigana na baba zao na watoto katika kuthibitisha Utume wake na wakanusurika kwaye. Na wale waliozama katika kumpenda yeye, waliotarajia biashara isiyoweza kuharibika ya mapenzi kwake. Na wale ambao jamaa zao waliwahama pale waliposhikamana na kishikio chake na akraba waliwakimbia pale walipokaa chini ya kivuli cha akraba zake. Basi usisahau ewe Mola yale waliyoyaacha kwa ajili yako katika njia yako. Wape radhi zako….. Uwalipe kwa kuyahama majumba ya watu wao kwa ajili yako….. Ewe Mola uwafikishie bora ya malipo yako wale walioandamana nao kwa wema ambao husema: “Mola wetu Mlezi tusamehe sisi na ndugu zetu waliotutangulia katika imani…..”26 Maana hii inaonekana kutoka kwenye urithi wa wanachuoni na wanaharakati wa kambi ya Ahlul-Bayt (a.s.), mmoja kati ya wanachuoni wa zama zetu naye ni Sheikh Muhammad Husein Ali Kashful-Ghitai anasema: “Sisemi maswahaba wengine – Na ndio wengi ambao hawakuwatawalisha Ahlul-Bayt – walimkhalifu Mtume na hawakushika ushauri wake, si hivyo, tunajikinga kwa Mwenyezi Mungu tusiwadhanie hivyo ilihali zama hizo wao ndio walikuwa watu bora kuliko wote waliyokuwa juu ya ardhi, lakini huenda maneno hayo hawakuyasikia wote na baadhi walioyasikia hawakujua makusudio yake. Na maswahaba wa Mtukufu Mtume wako juu zaidi kuliko hadhi zao kuzungukwa na dhana chafu.”27 Ali Kashif Al-Ghita baada ya kutaja baadhi ya yaliyowapata Ahlul-Bayt zama za ukhalifa uliofuatana anaongeza kwa kusema: “Usisahau kuwa hii 26 As-Sahifatu As-Sajadiyyah – Dua namba 4 (Kuwaombea baraka wafuasi wa Mitume na wenye kuwasadikisha.). 27 Aslus-Shia Wa Usuliha: 84 – 85.

25


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 26

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu haimaanishi kuwa sisi tunataka kukanusha mema waliyo nayo hao makhalifa na baadhi ya huduma zao kwa ajili ya Uislamu ambavyo havikanushi ila mwenye kiburi, na tunamshukuru Mwenyezi Mungu sisi si wenye kiburi wala si watukanaji wala si wenye kukashifu, bali sisi ni wenye kushukuru wema na kusamehe makosa.” Na anasema tena: “Huo ni umma uliotangulia una yake uliyoyachuma na ni juu yake yale uliyoyachuma na malipo yake ni juu ya Mwenyezi Mungu, akisamehe basi ni kwa fadhila Yake na akiadhibu basi ni kwa uadilifu Wake.”28 Haya ni kwa ufafanuzi, ama muhtasari wa wasifu wa maswahaba ameufupisha As-Sayyid As-Shahid Muhammad Al-Baqir As-Sadri kwa ibara ya kupendeza akasema: “Hakika maswahaba kwa sifa yao ya kuwa kundi la mwanzo lenye imani na lenye kuangazia wengine walikuwa wabora na mbegu bora zaidi katika kuanzisha umma wa kiislamu mpaka historia ya mwanadamu haijashuhudia kizazi cha kiimani kizuri, bora na kisafi kuliko kizazi alichokianzisha Mtukufu Mtume kiongozi.”29 Vielelezo vya Qur’ani, Hadithi na historia vinathibitisha ukosefu wa uadilifu kwa baadhi ya maswahaba Na sisi hapa tutaeleza hilo kwa ufafanuzi kidogo. Vilidhihiri baadhi ya vitendo vya unafiki kwa baadhi ya maswahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Madina tukufu na Qur’ani ikasajili vitendo hivyo kwa ibara mbalimbali zilizorudiwa ndani ya Sura kumi na mbili, na moja ikatengwa mahususi kwa ajili ya kuwafichua, kuwatahadharisha, kufichua njama zao na siri zao na kubainisha sifa zao na mwenendo wao, na ikawaashiria kwa kutumia neno unafiki au wanafiki mara thelathini na saba, na bila shaka hawa walimsuhubu Mtume (s.a.w.w.) na kabla ya hapo walikuwa miongo28 Aslus-Shia Wa Usuliha: 94. 29 Al-Majumuati Al-Kamilah namba 11 mada kuhusu utawala: 48.

26


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 27

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu ni wanaoshiriki naye katika vita mbalimbali na huenda baadhi yao walikuwa na imani ya kweli kabla unafiki haujaingia ndani ya mioyo yao. Miongoni mwa maswahaba yumo aliyemuasi Mtume (s.a.w.w.) katika sadaka, na yupo aliyemuudhi na kumwambia yeye ni (Sikio), na miongoni mwao yupo aliyejenga msikiti kwa ajili ya kuwadhuru na kuwafarakisha waumini, na miongoni mwao yupo aliyekuwa na ugonjwa moyoni mwake na wapo wenye kuwazuia watu, na miongoni mwao wapo waliotoa udhuru ili wasiende vitani kwenye vita vya Tabuk, na hao walikuwa watu themanini30 na wakaapa mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) naye akakubali kiapo chao ndipo kwa ajili yao Mwenyezi Mungu akateremsha

“Watakuapieni Mwenyezi Mungu mtakaporudi kwao ili mjitenge nao. Basi jitengeni nao, kwani wao ni najisi, na makazi yao ni Jahannam ni malipo ya yale waliyokuwa wakiyachuma.* Wanakuwapieni ili muwe radhi nao, na kama mkiwaridhia, basi hakika Mwenyezi Mungu hatakuwa radhi na watu wavunjao amri.” (Sura Tawba: 95 – 96.) Na katika vita hivi wanafiki kumi na nne walinuia kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye giza huko kwenye ufa wa mlima.31 Na alipoondoka Mtume kutoka kwenye vita hivi kwenda Madina njiani kulikuwa na maji yanayotoka kidogo kidogo kwenye bonde lenye mpasuko, basi 30 Fat’hul-Bari 8: 113, mlango wa 79, Hadithi ya 4418. 31 Dalailun-Nubuwwah 5: 256, 262.

27


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 28

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Atakayetutangulia kufika kwenye maji yale asinywe hata kidogo mpaka nifike.” Basi kundi la wanafiki likamtangulia na wakanywa maji, Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipofika alisimama na hakuona maji hata kidogo, basi Mtume alipojua walilolifanya wanafiki alisema: “Hivi hatukuwakataza wasinywe maji hata kidogo mpaka nifike?” kisha akaanza kuwalaani na kuwaombea dua mbaya.32

“Na miongoni mwao wako wanaomuudhi Nabii na wanasema: Yeye ni sikio….. na wale wanaomuudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu watakuwa na adhabu iumizayo.” (Sura Tawba: 61.)

“Kwa hakika wale wanaomuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na Akhera na amewaandalia adhabu yenye kufedhehesha.” (Sura Al-Ahzab: 57) 33 Na miongoni mwao wamo wanaodanganya na ambao wanadhihirisha imani, Mwenyezi Mungu kawaelezea kwa kusema:

32 Tarikhu At-Tabari 2: 186, kuelezea habari za vita vya Tabuki: Matukio ya mwaka 9 tangu kuhama. 33 Rejea Tafsiril-Mawsarid 4: 422 kwenye tafsiri ya Aya hii.

28


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 29

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Na miongoni mwa watu wako wasemao: Tumemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya Mwisho, hali wao si wenye kuamini.* Wanataka kumdanganya Mwenyezi Mungu na wale walioamini lakini hawamdanganyi ila nafsi zao na hawatambui.” (Sura Al-Baqara: 8 – 9.) 34

“Na wanapokutana na walioamini husema: Tumeamini, na wanapokuwa peke yao kwa mashetani wao husema: Hakika sisi tu pamoja nanyi, sisi tunafanya mzaha tu.” (Sura Al-Baqara: 14.) 35

“Na miongoni mwao wako waliomwahidi Mwenyezi Mungu akitupa katika fadhili Zake lazima tutatoa sadaka na bila shaka tutakuwa miongoni mwa watendao mema. Lakini alipowapa katika fadhila 34 Rejea Al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani 1: 192 – 197 kwenye tafsiri ya Aya hizi mbili. 35 Rejea Tafsir Al-Baydhawi 1: 175 – 177 kwenye tafsiri ya Ayah hii.

29


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 30

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Zake wakazifanyia ubakhili na wakageuka na huku wakipuuza. Kwa hiyo akawalipa unafiki nyoyoni mwao mpaka siku ya kukutana naye kwa sababu ya kumkhalifu Mwenyezi Mungu ahadi waliyomwahidi na kwa sababu walikuwa wanasema uongo.” (Sara Tawba: 75 – 77.) Aya hizo ni kisa cha Thaalabah yule sahaba mkata aliyemwomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amuombee kwa Mwenyezi Mungu ili amruzuku mali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Ole wako ewe Thaalabah kichache unachoshukuru ni bora kwako kuliko kingi usichokiweza.” Thaalabah akasema: “Naapa kwa yule aliyekupa utume, iwapo utamwomba Mwenyezi Mungu na akaniruzuku mali hakika nitampa kila mwenye haki ile haki yake.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mola mruzuku Thaalabah mali.” Ndipo Mwenyezi Mungu alipomruzuku mali na kumzalishia. Basi Mtukufu Mtume alipomwomba atoe Zaka ya mali yake Thaalaba alikataa huku akitoa kisingizio kuwa Zaka hii ni kodi, hivyo akagoma kutoa; na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akafariki ilihali Thaalabah akiwa bado hai, basi ndipo alipopeleka Zaka ya mali yake kwa Abu Bakr naye akaikataa, akaipeleka kwa Umar akaikataa, na Thaalabah akafariki zama za Uthman.36 Na miongoni mwao yupo aliyezungumziwa na Qur’ani kuwa:

36 Rejea Tafsir Fat’hul-Qadir cha As-Shawkan Ali bin Muhammad 2: 185. Tafsir Ibnu Kathir cha Ismail bin Kathir Ad-Damashki 2: 373. Tafsir Al-Khazin cha Alaud-Din Ali bin Ibrahim Al-Baghdad 2: 125. Tafsir Al-Baghawi Muhammad ibnu Al-Hasan bin Masuud Al-Fara 2: 125 kwenye maelezo ya Tafsir Al-Khazin. Tafsir At-Tabari cha Abu Jafar Muhammad bin Jarir At-Tabari 6: 131.

30


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 31

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

“Je, muumini anaweza kuwa sawa na yule aliye muovu? Hawawi sawa. Ama wale walioamini na wakafanya vitendo vizuri basi watakuwa nazo Bustani za makazi ndio pakufikia kwa waliyokuwa wakiyatenda. Lakini wale waliofanya uovu, basi makazi yao ni Motoni, watakapotaka kutoka humo watarudishwa humo na wataambiwa: Onjeni adhabu ya Moto ambayo mlikuwa mkikadhibisha.” (Sura As-Sajdah: 18 – 20.) Muumini hapa ni Ali bin Abi Talib, na muovu hapa ni Al-Walid bin Aqabah na yeye alikuwa Gavana wa Uthman huko Kufa na Gavana wa Muawiya na mwanae Yazid huko Madina.37 37 Rejea Tafsir At-Tabari 21: 107. Tafsir Al-Kashaf cha Az-Zamakhshar 3: 514. Fat’hul-Qadir cha Al-Shawkan 4: 225. Tafsir Ibnu Kathir 3: 462. Asbabun-Nuzul cha As-Suyut kimechapwa pambizoni mwa Tafsir Al-Jalalayn: 550. AhkamulQur’ani cha Ibnu Arab 3: 1489. Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abil Hadid 4: 80 na 6: 292. Ad-Durul-Mathur cha As-Suyut 5: 178. Zadul-Masir cha Ibu AlJawaziyu Al-Habaliyu 6: 340. Ansabul-Ashraf cha Al-Baladhari 2: 148 Hadithi ya 150. Tafsir Al-Khazin 3:470 na 5: 187. Maalimu At-Tanzil cha Al-Baghawi AsShafi kwenye maelezo ya Al-Khazin 5: 187. As-Sirat Al-Halbiyyah cha Al-Halbi As-Shafi 2: 85. Takhrijul-Kashaf cha Ibnu Hajar Al-Asqalan kilichochapwa mwishoni mwa Al-Kashaf 3: 514. Al-Intisaf fi ma tadhammanahu Al-Kashaf kilichopo mwishoni mwa Al-Kashaf 3: 244.

31


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 32

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na miongoni mwao yupo aliyezungumziwa na Mwenyezi Mungu kwa kusema:

“Na ni nani dhalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo na hali anaitwa kwenye Uislamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (As-Saf: 7.) Aya hii iliteremka kwa ajili ya Abdullah bin Abu Sarhi naye ni Gavana wa Uthman huko Misri, yeye ndiye aliyemzushia Mwenyezi Mungu uongo na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akahalalisha damu yake hata kama atang’ang’ania nguzo za Al-Kaaba kama anavyoelezea hilo As-Shafiy mwandishi wa kitabu As-Sirat Al-Halabiyyah kwenye mlango wa ukombozi wa Makka, na siku ya ukombozi Uthman alikuja naye akimuombea amani kama anavyoeleza mwandishi wa As-Sirah, lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinyamaza akitaraji atauwawa ndani ya muda wa ukimya wake kama alivyofafanua hilo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini hakuuwawa na hivyo akapewa amani.38 Na miongoni mwao yupo aliyezungumziwa na Mwenyezi Mungu:

“Wamefanya kiapo chao kuwa ngao, wakaepuka njia ya Mwenyezi Mungu basi itakuwa kwao adhabu ifedheheshayo.” (Sura AlMujadalah: 16.) 39

38 Rejea As-Siratu Al-Halabiyyah mlango wa ukombozi wa Makka. 39 Rejea Tafsir Al-Khazin 4: 262 kwenye Tafsiri ya Aya hii, chapa ya Darul-Kutub Al-Ilmiyyah.

32


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 33

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na yupo aliyesema:

“Hakika wanafiki wanataka kumdanganya Mwenyezi Mungu, naye atawaadhibu kwa sababu ya udanganyifu wao. Na wanaposimama kuswali husimama kwa uvivu, kujionyesha kwa watu, wala hawamtaji Mwenyezi Mungu ila kidogo tu. Wanayumbayumba huku na huku, huku hawako wala huku hawako. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemwacha katika upotovu basi huwezi kumpatia njia.” (Sura AnNisai: 142 – 143.) 40 Na Kitabu Kitukufu kinatamka waziwazi kuwa lipo kundi linalomsikiliza Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) lakini Mwenyezi Mungu amepiga mihuri kwenye nyoyo zao kwa sababu wao walifuata matamanio, Mwenyezi Mungu akasema:

“Na wako miongoni mwao wanaokusikiliza hata wanapoondoka kwako wanawauliza wale waliopewa elimu: Amesema nini sasa? Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewapiga muhuri nyoyoni mwao na wakafuata tamaa zao.” (Sura Muhammad (s.a.w.w.): 16.) 41 40 Rejea Tafsir Al-Maragh 2: 186 – 188 kwenye tafsiri ya Aya hizi mbili, chapa ya Darul-Fikri. 41 Rejea Safuwat-Tafasir 3: 209 – 210. Chapa ya Darul-Qalam kwenye tafsiri ya Aya hii.

33


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 34

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Kama Mwenyezi Mungu alivyotangaza kulilaani kundi miongoni mwao nao ni wale ambao ndani ya nyoyo zao mna ugonjwa na ambao wanaofanya uharibifu ardhini na kukata ujamaa wao, Mwenyezi Mungu akasema: “Na ndio Mwenyezi Mungu amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao. Je, hawaizingatii Qur’ani au nyoyo zina kufuli?” (Sura Muhammad (s.a.w.w.): 23-24.)42 Na miongoni mwao yupo Dhuthudayyah ambaye alikuwa miongoni mwa maswahaba wenye kushikamana na ibada, ibada yake pamoja na juhudi zake vilikuwa vikiwashangaza watu, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisema: “Hakika yeye ni mtu mwenye doa jeusi kutoka kwa Shetani.” Na akamtuma Abu Bakr ili akamuue lakini alipomkuta akiswali akarejea. Akamtuma Umar naye hakumuuwa. Kisha akamtuma Ali (a.s.) lakini hakumkuta.43 Na yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa waasi na aliuliwa na Ali kwenye vita vya Nahrwan.44 Baadhi ya kundi la maswahaba lilikuwa likijikusanya kwenye nyumba moja wakiwazuia watu dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndipo akamwamuru aliyewaunguza kwa kuwachomea nyumba hii.45 Na miongoni mwa waliomsuhubu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Qazman bin Al-Harth aliyepigana bega kwa bega na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye vita vya Uhud tena kwa ushujaa mpaka maswahaba wa Mtukufu wa Mtume (s.a.w.w.) wakasema: “Hakuna yeyote aliyetuwakilisha kama 42 Rejea Safuwat-Tafasir 3: 211 – 212, kwenye tafsiri ya Aya hizi mbili, chapa ya Darul-Qalam. 43 Rejea Al-Isabah fi Tamyizi As-Sahabah 1: 484, namba 2446. Fat’hul-Bari 6: 617, Hadithi ya 361, kwa tamko lingine. 44 As-Sirat An-Nabawiyyah cha Ibnu Haban: 546. MurujuDhahab 2: 425. AlKamil fi Tarikh 3: 348. Al-Bidayat Wan-Nihayah 7: 235. 45 Rejea Sirat Ibnu Hisham 3: 235.

34


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 35

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu alivyotuwakilisha fulani.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Bila shaka yeye ni miongoni mwa watu wa Motoni.” Na alipopatwa na jeraha na kudondoka wakamwambia: “Hongera ewe baba Al-Ghaydaq.” Akasema: “Pepo kutoka kwa Harmal! Naapa kwa Mwenyezi Mungu hatukupigana ila kwa ajili ya nasaba.”46 Na miongoni mwao wapo waliojenga msikiti kwa ajili ya kuwadhuru na kuwafarakisha waumini na wakasema: Hakika wao wamejenga msikiti huu kwa ajili ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na hawa walikuwa ni watu kumi na mbili wanafiki miongoni mwa maswahaba. Ibnu Hajar Al-Haythami ametoa kutoka kwa Abu Dardau amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: “Bila shaka kwenye Hodhi nitajua atakayofanyiwa mmoja wenu, kisha nitasema: Huyu ni miongoni mwa maswahaba zangu. Nitaambiwa: Hakika wewe hujui ni kitu gani walizua baada yako”47 Na kutoka kwa Abu Dardau amesema: Nikamwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, imenifikia habari kuwa umesema: Hakika watu katika umma wangu watakufuru baada ya imani yao.” Akasema: “Ndiyo, ewe Abu Dardau, na mimi si miongoni mwao.”48 Na Imam Ahmad ametoa kutoka kwa Abu Bakrah amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Watanikuta kwenye Hodhi watu miongoni mwa walionisuhubu na kuniona, basi watakapoinuliwa na nikawaona, watasogezwa mbali na mimi. Hapo nitasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hawa ni maswahaba zangu! Hawa ni maswahaba zangu! Nitaambiwa: Hakika wewe hujui ni kitu gani walizusha baada yako.”49 Na ametoa Imam Ahmad kutoka kwa Anas bin Malik kutoka kwa Mtukufu 46 Al-Isabah 3: 235. 47 Maj’mauz-Zawaid 9: 367. 48 Maj’mauz-Zawaid 9: 367. 49 Musnad Imam Ahmad 5: 50 chapa ya kwanza.

35


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 36

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kuna watu watanikuta kwenye Hodhi basi nitakapowaona watainuliwa kuletwa kwangu lakini watasogezwa mbali na mimi. Hapo nitasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Hawa ni maswahaba zangu! Hawa ni maswahaba zangu! Nitaambiwa: Hakika wewe hujui ni kitu gani walizusha baada yako.50 Na Imam Ahmad ametoa kutoka kwa Said bin Jubayri kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisimama kutuwaidhi akasema: “Hakika ninyi mtafufuliwa kuelekea kwa Mwenyezi Mungu mkiwa peku, uchi na mkiwa mazunga kama tulivyoanza mwanzo wa umbile tutalirudisha ikiwa ni ahadi juu yetu hakika sisi tulikuwa ni wenye kufanya.” Hivyo kiumbe wa kwanza atakayevishwa nguo ni Ibrahim kipenzi cha Rahman kisha kundi miongoni mwenu litapelekwa upande wa kushoto.” Na Ibnu Jafar amesema: “Watu miongoni mwa umma wangu watachukuliwa na kuelekezwa upande wa kushoto51, kisha mimi nitasema: Ewe Mola Wangu Mlezi, maswahaba zangu! Nitaambiwa: Hakika wao hawakuacha kurudi nyuma tangu ulipowaacha, basi nitasema kama alivyosema mja mwema ‘Nilikuwa shahidi juu yao pale tu nilipokuwa bado nimo miongoni mwao.’ Hakika Wewe ni Mshindi, mwenye hekima.”52

Qur’ani na Sunna vinawalaani waziwazi baadhi ya maswahaba Ama kuhusu Qur’ani tukufu tayari tumeshasema maeneo ya laana ndani ya Qur’ani tukufu yamegawanyika katika mizunguko minne nayo ni: 50 Musnad Imam Ahmad 3: 281. 51 Ili wafikishiwe sehemu inayowafaa wao, Mwenyezi Mungu anasema: “Na watu wa kushoto, watakuwa vipi watu wa kushoto. *Watakuwa katika upepo wa moto na maji yachemkayo. * Na kivuli cha moshi mweusi sana. * Si baridi wala si starehe.”- Sura Waqia: 41. - Mtarjumi. 52 Musnad Imam Ahmad 1: 235.

36


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 37

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Makafiri wote, mayahudi peke yao, wanafiki na sababu zinazotishia kusambaratika muundo wa jamii ya kiislamu. Mzunguko wa kwanza na wa pili ni ya nje na wa tatu na wa nne ni ya ndani inaishi ndani ya jamii ya kiislamu, na pindi Qur’ani inapomwaga laana yake juu ya wanafiki ni kuwa inawalaani watu ambao walisilimu na wakamsuhubu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na maana ya usahaba ikatimia kwao, na hivyo hivyo katika mzunguko wa nne. Na Aya kinara kabisa katika kuwalaani baadhi ya maswahaba ni kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tulipokuambia: Hakika Mola wako Mlezi amewazunguka watu. Na hatukuifanya ndoto ile tuliyokuonyesha ila kwa kuwajaribu watu, na pia mti uliolaaniwa ndani ya Qur’ani tukufu. Na tunawahadharisha lakini haiwazidishii ila uasi mkubwa.” (Sura Al-Israi: 60.) Wafasiri wamesema kuwa mti uliolaaniwa ndani ya Qur’ani tukufu ni mti wa Al-Hakam bin Abul-Aas, na ndoto ni ndoto aliyoiota Mtukufu Mtume kuwa kizazi cha Mar’wan bin Al-Hakam watapeana mimbari yake.53 Ama laana ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa baadhi ya maswahaba ni mlango mkubwa sana wenye mambo mengi, na mashuhuri zaidi ni laana ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumlaani Al-Hakam na kulaani kizazi chake 53 At-Tafsir Al-Kabir 20: 237. Al-Jamiu Liahkamil-Qur’ani 10: 281 – 287 kwenye tafsiri ya Aya hii ya sitini ya Sura Al-Israi. Ruhul-Maan cha Al-Alus 15: 105 – 107 kwenye tafsiri ya Aya hii.

37


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 38

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu mpaka akasema: “Ni balaa kubwa kwa umma wangu kutokana na kilichopo kwenye mfupa wa mgongo wa huyu.”54 Na kwa mujibu wa Hadithi ya Aisha ni kuwa yeye alimwambia Mar’wan: “Nashuhudia ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimlaani baba yako nawe ukiwa kwenye mifupa ya mgongo wake.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamfukuza na kwenda Maraj karibu na Taif na akamharamishia kuingia Madina, lakini alipofariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Uthman alimwendea Abu Bakr akimuomba amrudishe Madina lakini Abu Bakr alikataa, na Abu Bakr alipofariki Uthman alimwendea Umar ili amruhusu kurudi Madina naye Umar akakataa, ndipo Uthman alipochukua ukhalifa akamwingiza Madina kwa heshima na taadhima na akampa dirhamu laki moja na kumfanya mwanae Mar’wan kuwa mshauri wake mkuu, na mwishowe alisababisha khalifa kuuawa na ukhalifa kuharibika. Nasru bin Muzahim Al-Man’qar ametoa kutoka kwa Abdul-Ghaffar bin Qasim kutoka kwa Adi bin Thabit kutoka kwa Al-Barau bin Azib amesema: “Alikuja Abu Suf’yan akiwa na Muawiya basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Mola, mlaani mfuasi na mfuatwa, ewe Mola mlaani mwana.” Ibnu Barrau akamuuliza baba yake: Ni nani mwana? Akasema: Muawiyya.”55 54 Chanzo kilichotangulia. Na Fakhru Ar-Raz amefanya Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Aisha kuwa ndio dalili ya kusihi tafsiri hii ya mti uliolaniwa kuwa ni Al-Hakam na kizazi chake. Pia tazama Al-Mustadrak Alas-Sahahain cha AlHakim 4: 481 na amesema riwaya hiyo ni sahihi. As-Sawaiq Al-Muhriqah: 179 chapa ya Al-Muhammadiyyah na ukurasa wa 108 chapa ya Al-Maymaniyyah Misri. Tat’hir Al-Jinan kilichochapwa pamoja na As-Sawaiq: 63 chapa ya AlMuhammadiyyah na kwenye maelezo yake: 144 chapa ya Al-Maymaniyyah. AdDurrul-Mathur cha As-Suyut 4: 191 na 6: 41. Maqtaluk-Husein cha AlKhawarazim Al-Hanafiy 1: 172. Siratu Aalamu An-Nubalai 2: 80. Usudul-Ghaba cha Ibnu Al-Athir 2: 34. Al-Istiab cha Ibnu Abdul-Bar mwishoni mwa Al-Isabah 1: 317, chapa ya Misri na juz 1, uk 318. As-Siratul-Halabiyyah 1: 317. As-Siratu An-Nabawiyyah cha Zayni Dahlan kwenye maelezo ya Siratul-Halabiyyah 1: 225, 226. Al-Ghadir cha Al-Amin 8: 245. 55 Waq’at Saffayn: 217, uhakiki na ufafanuzi wa Ustadh Abdus-Salam Muhammad Harun, chapa ya Misri.

38


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 39

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na Nasru ametoa kutoka kwa Ali bin Al-Aqmar mwishoni mwa Hadithi yake: “Mtume akamtazama Abu Suf’yan akiwa juu ya kipando na Muawiya na ndugu yake mmoja amekaa na mwengine anaendesha, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowaona akasema: “Ewe Mola mlaani kiongozi, mwendeshaji na mpandaji.” Tukasema: Wewe ulimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ndiyo, na kama si hivyo basi masikio yangu mawili yazibe kama yalivyopofuka macho yangu mawili.”56 Tazama barua ya Muhammad bin Abu Bakr ambayo alimtumia Muawiya ndani yake aliandika: “Na nimekuona unataka kujilinganisha naye ilihali wewe ni wewe na yeye ndiye mwenye nia njema kuliko watu wote na ndiye mwenye kizazi bora kuliko watu wote na ndiye mwenye mke bora kuliko watu wote na ndiye mwenye binamu bora kuliko watu wote, ndugu yake aliiuza nafsi yake siku ya vita vya Muuta, na ami yake ni bwana wa mashahidi siku ya Uhudi na baba yake ndiye aliyejitolea kumhami Mtume wa Mwenyezi Mungu na sisi ni wanafunzi wake. Na wewe ni mlaanifu mwana wa mlaanifu wewe na baba yako mliendelea kumfanyia kila tatizo Mtume wa Mwenyezi Mungu na mkijitahidi kuzima nuru ya Mwenyezi Mungu mkikusanya makundi ili kutimiza hilo na mkitoa mali na kumkusanyia makabila na baba yako akafariki akiwa katika hali hiyo na wewe umemrithi katika hilo.” Muawiya hakukataa laana yake wala laana ya baba yake japokuwa aliandika barua ya kujibu barua hii.57 Na ushahidi huu wa Qur’ani, Hadithi na historia unathibitisha kwa yakini kabisa ubatilifu wa nadharia ya uadilifu wa kila sahaba, na pia unathibitisha kuwa maswahaba wao wenyewe hawakuwa wanamuona kila sahaba mwenzao ni mwadilifu kama ilivyo kwenye kauli ya Aisha kumwambia Mar’wan: “Nashuhudia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimlaani baba yako na wewe ukiwa bado kwenye mifupa ya 56 Waq’at Saffayn: 220, chapa ya Misri. 57 Muruj Ad-Dhahab 3: 14 – 16.

39


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 40

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu mgongo wake.” Na matokeo haya yanatiwa mkazo na neno lake mashuhuri kuhusu Uthman: “Muuweni Naathal hakika yeye amekufuru.” 58 Ubatilifu wa kanuni ya kutofautisha kati ya sifa jumuishi na mtu binafsi Ushahidi huu pia unathibitisha ubatilifu wa kanuni aliyoiweka Abu Hamid Al-Ghazalii na wengine waliomfuata katika hilo, kuwa laana inayoruhusiwa ni laana ya kulaani makundi kwa kuzingatia sifa jumuishi akaandika akisema: “Hakika laana inayoruhusiwa ni kulaani kwa kuzingatia sifa jumuishi kama vile kusema: Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya makafiri, watu wa bidaa, madhalimu na wala riba… Ama kumlaani mtu binafsi kwa kumuainisha katika hili kuna hatari, kama vile kusema: Mwenyezi Mungu amlaani Zaydu, japokuwa yeye ni kafiri au muovu au mtu wa bidaa.” Na kwa ufafanuzi ni kuwa kila mtu binafsi ambaye kisheria imethibiti laana yake basi inaruhusiwa kumlaani kwa kumuainisha, kama vile kuse58 Rejea Tarikh At-Tabari 4: 459. Al-Kamil fi Tarikh cha Ibnu Athir Al-Jazri AsShafiy 3:206. Tadhkiratul-Khawas cha As-Sibtu bin Al-Jawzi Al-Hanafiy: 61 na 64. Al-Imamah Was-Siyasah cha Ibnu Qutaybah 1: 49 humo mna “kawa muovu” badala ya “kakufuru” chapa ya Mustafa Muhammad ya huko Misri. As-Sirat AlHalabiyyah cha Ali Burhanud-Din Al-Halbiy As-Shafiy 3: 286, chapa ya AlBahiyyah Misri mwaka 1320 A.H. Na ameinukuu Al-Askar ndani ya kitabu Ahadithi Ummul-Muuminin Aishah, juz 1, uk. 105 kutoka kwenye kitabu Tarikh Ibnu Aatham: 155 chapa ya Bombay, rejea huko. An-Nihayah cha Ibnu Al-Jazri As-Shafiy 5: 80 uhakiki wa Mahmud Muhammad At-Tanahi chapa ya Daruihyai At-Turath Al-Arabiy huko Beirut. Tajul-Arus Min Shar’hul-Qamus cha AzZubaydiy Al-Hanafiy 8: 141. Lisanul-Arab cha Ibnu Mandhur 14: 193. Sharhu Nahjul-Balagha cha Ibnu Abu Hadid 2: 77 chapa ya kwanza Misri na 6: 215 chapa ya Misri uhakiki wa Muhammad Abul-Fadhlu, na 2: 408 chapa ya MaktabatulHayat Beirut, na 2: 121 chapa ya Darul-Fikri.

40


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 41

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu ma: Mwenyezi Mungu amlaani Firaun, na Mwenyezi Mungu amlaani Abu Jahl, kwa sababu tayari imeshathibiti kuwa hawa walikufa wakiwa makafiri na likatambulika hilo kisheria. Ama kumlaani mtu binafsi katika zama zetu hizi kama vile kusema: Mwenyezi Mungu amlaani Zaydu, eti kwa kuwa tu yeye ni Yahudi hili lina hatari kwani huenda atakuja kusilimu na akafariki akiwa amejikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu, sasa vipi ahukumiwe kuwa ni mlaanifu? Ukisema: Analaaniwa kwa kuwa hivi sasa ni kafiri kama ambavyo muislamu anavyoombewa rehema: “Mwenyezi Mungu amrehemu” kwa kuwa hivi sasa ni mwislamu japokuwa huenda akaritadi, basi jua kuwa tunaposema: “Mwenyezi mungu amrehemu” tunamaanisha Mwenyezi Mungu amuimarishe ndani ya Uislamu na ndani ya utiifu ambavyo vyenyewe ndio sababu ya kupata rehema hiyo, na wala haiwezekani kusema: Mwenyezi Mungu amuimarishe kafiri ndani ya kitu ambacho ndio sababu ya kupata laana, kuuombea ukafiri ombi hili na kwenyewe ni ukafiri, bali inaruhusiwa kusema: Mwenyezi Mungu amlaani iwapo akifa ndani ya ukafiri na Mwenyezi Mungu asimlaani akifa ndani ya Uislamu, na hilo ni jambo la siri halijui isipokuwa Mwenyezi Mungu, na hali isiyojulikana yenye kutaradadi kati ya pande mbili ina hatari lakini kuacha kulaani hakuna hatari. Ukijua hilo kwa kafiri basi lenyewe kwa Zaydu muovu au Zaydu mtu wa bidaa ni bora zaidi kuliacha, kwani katika kuwalaani watu binafsi kuna hatari kwa sababu hali za watu hubadilika ila yule ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtambulisha kwani inaruhusiwa kutambulishwa yule atakayefia ndani ya ukafiri, na kwa ajili hiyo aliainisha baadhi ya watu kwa kuwalaani akawa akisema ndani ya dua yake juu ya makurayshi: “Ewe Mola, mlaani Abu Jahli bin Hisham na Ut’bah bin Rabiah.” Na akiwataja baadhi ya watu waliyouwawa ndani ya ukafiri mpaka alikuwa akimlaani yule asiyejuwa mwisho wake na ndipo akakatazwa. Kwani imepokewa kuwa: Alikuwa akiwalaani mwezi mzima ndani ya kunuti yake wale waliowaua watu wa kisima cha Muuta ndipo ikateremka 41


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 42

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Aya ya Mwenyezi Mungu: “Huna neno katika shauri awakubalie toba yao au awaadhibu, maana hakika wao ni madhalimu.” Inamaanisha kuwa huenda wao watasilimu na itajulikanaje kama wao ni walaanifu? Na pia inaruhusiwa kumlaani yule aliyebainika kufia ndani ya ukafiri iwapo tu kufanya hivyo hakumuudhi mwislamu lakini kama kunamuudhi hairuhusiwi, kama ilivyopokewa kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimuuliza Abu Bakr kuhusu kaburi moja pindi walipopita kuelekea Taif, akasema: “Hili ni kaburi la mtu aliyekuwa kafiri dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake naye ni Said bin Al-As.” Basi mwanae Amr bin Said akakasirika na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hili ni kaburi la mtu aliyekuwa mtoaji mno wa chakula na mkarimu mno kuliko Abu Quhafa.” Abu Bakr akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hivi huyu ndiye anayeniambia mimi maneno haya?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Nyamaza dhidi ya Abu Bakr.” Akaondoka, kisha Mtume akamgeukia Abu Bakr na kumwambia: “Ewe Abu Bakr, mnapowataja makafiri watajeni kwa sifa jumuishi kwani mtakapoainisha watoto watakasirika kwa ajili ya baba zao.” Akawazuia watu kufanya hivyo. Nu’man alikunywa pombe na akaadhibiwa mara nyingi tu mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) basi sahaba mmoja akasema: “Mwenyezi Mungu amlaani kwani mara kwa mara analetwa.” Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Usiwe msaidizi wa shetani juu ya ndugu yako.” Na katika riwaya nyingine: “Usiseme haya hakika yeye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Akamzuia kufanya hivyo, na hili linaonyesha kuwa hairuhusiwi kumlaani muovu kwa kumuainisha, na kwa ujumla ni kuwa kuwalaani watu binafsi kwa kuwaainisha kuna hatari hivyo mtu ajiepushe na wala hakuna hatari katika kunyamaza bila kumlaani Ibilisi achia mbali mwingine. Ukisema: Je, inaruhusiwa kumlaani Yazid kwa kuwa alimuua Husein au aliamuru auwawe? Tunajibu: Asilan hili halijathibiti, hivyo hairuhusiwi 42


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 43

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kusema kuwa yeye ndiye aliyemuuwa au aliamuru kwani haijathibiti achia mbali kumlaani. Kwa sababu hairuhusiwi kumnasibisha mwislamu na madhambi makubwa bila uchunguzi. Ndio, inaruhusiwa kusema Ibnu Muljimu alimuuwa Ali (a.s.) na Abu Luuluu alimuuwa Umar kwani hilo limethibiti kwa wingi. Hivyo hairuhusiwi muislamu kuzushiwa uovu au ukafiri bila uchunguzi, kwani Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Mtu hamzushii mwenzake ukafiri wala uovu ila ni lazima umrudie mwenyewe iwapo mwenzake hana sifa hiyo.” Na akasema (s.a.w.w.): “Mtu hathibitishi ukafiri wa mwenzake ila ni lazima utamrudia mmoja kati yao, akiwa kweli ni kafiri basi yeye ni kama alivyosema, na kama si kafiri basi yeye (mwenye kuthibitisha) amekufuru kwa kumzushia ukafiri mwenzake.” Na hii maana yake ni kuwa amkufurishe ilihali anajua kwa yakini kuwa yeye ni mwislamu, lakini iwapo akidhania kuwa yeye ni kafiri kwa sababu ya bidaa au nyingine atakuwa mwenye makosa na si kafiri. Maadh amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniambia: “Nakukataza kumkashifu mwislamu au kumuasi Imam mwadilifu na kuwachunguzachunguza sana maiti.” Masruq amesema: “Niliingia kwa Aisha akasema: “Fulani laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake amefanya nini?” Nikasema: Amefariki. Akasema: “Mwenyezi Mungu amrehemu.” Nikasema: vipi hili? Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: “Msiwatukane wafu kwani hakika wao wameyafikia waliyoyatanguliza.” Na akasema (a.s.): “Msiwatukane wafu mtawaudhi waliyo hai.” Na akasema (a.s.): “Enyi watu! Nilindieni heshima yangu kwa maswahaba zangu, ndugu zangu na wakwe zangu na wala msiwatukane, enyi watu! Maiti anapofariki mtajeni kwa heri.” Ukisema: Je, inaruhusiwa kusema: Mwenyezi Mungu amlaani muuwaji wa Husein, au Mwenyezi Mungu amlaani mwamrishaji wa mauwaji yake? Tunasema: Sahihi ni kusema: Mwenyezi Mungu amlaani muuwaji wa Husein ikiwa amekufa kabla ya kutubu, kwani huenda amekufa baada ya 43


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 44

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kutubu, kwani Wahshiya muuwaji wa Hamza ami ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimuuwa akiwa kafiri lakini baadae akatubu na kuacha ukafiri na uawaji vyote pamoja, na wala hairuhusiwi kumlaani, kuuwa ni dhambi kubwa lakini halifikii daraja la ukafiri, hivyo laiti lisipowekwa sharti la kutubu na ikaachwa bila sharti kuna hatari, lakini katika kunyamaza hakuna hatari hivyo kwenyewe ni bora. “Hakika tumesema haya kutokana na watu kutolitilia uzito suala la laana na kulitamka ulimini, na muumini huwa si mwenye kulaani mno, hivyo haipasi ulimi wake utamke laana ila juu ya aliyekufa akiwa kafiri, au makundi ambayo yanajulikana kwa sifa zao bila kuwataja watu binafsi, hivyo kujishughulisha na utajo wa Mwenyezi Mungu ni bora, na kama si hivyo basi kwenye kunyamaza kuna amani.”59 Ibnu Taymiyyah naye akaandika akiunga mkono hilo: “Ndani ya Sahih Bukhari yamethibiti yenye kumaanisha kuwa kulikuwa na mtu mlevi mno akinywa pombe na kila alipopelekwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichapwa viboko, basi siku moja mtu mmoja akasema alipoletwa: “Mwenyezi Mungu amlaani kwani mara kwa mara analetwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Msimlaani hakika yeye anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Na kila muumini anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na asiyempenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake basi si muumini japokuwa wanatofautiana katika imani na wana mapenzi juu ya kitu kingine. “Alikataza hilo bila kujali kuwa yeye mwenyewe (s.a.w.w.) alilaani pombe, mtengenezaji wake, mnywaji wake, mnyweshaji wake, mbebaji wake mpelekewa na mlaji wa kipato chake. Na alikataza kumlaani huyu mtu binafsi kwa sababu laana ni sehemu ya ahadi ya adhabu hivyo hutolewa kwa sura ya ujumla. Na huenda ahadi ya adhabu ikaondolewa kwa mtu binafsi kutokana na toba sahihi au mema yenye kufuta au matatizo yenye 59 Ihyau Ulumid-Dini 3: 133 – 135, chapa ya Darul-Fikri.

44


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 45

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kufidia au shufaa yenye kukubalika au mengine yasiyokuwa hayo miongoni mwa sababu ambazo madhara yake huondoa adhabu kwa mwenye dhambi.”60 Na imenukuliwa kutoka kwake kauli: “Na ukweli wa mambo katika hilo ni kuwa kauli inaweza kuwa ukafiri, na itolewe kauli ya kumkufurisha msemaji wake, isemwe: “Atakayesema kadha wa kadha yeye ni kafiri.” Lakini mtu mwenyewe aliyesema hakufurishwi mpaka ithibiti dalili juu yake ambayo inamkufurisha atakayeiacha, kama vile maelezo ya hukumu ya kisheria kutoka kwa mtawala au kiongozi mwenye kutiiwa kama ilivyoelezwa ndani ya vitabu vya sheria. Hivyo sheria itakapomtambulisha na akajulikana ndipo dalili itakapokuwa imethibiti, hili ni kama lilivyo ndani ya ahadi za adhabu kutoka ndani ya Kitabu na Sunna, nazo ni nyingi mno. Na kusema kwa mujibu wa dalili hiyo ni wajibu lakini kwa sura ya ujumla bila kumuainisha mtu binafsi, hivyo haisemwi: “Huyu ni kafiri au muovu au mlaanifu au mwenye kukasirikiwa au mwenye kustahiki moto” hasa inapokuwa mtu ana fadhila na mema, kwani wasiokuwa Manabii wanaweza kutenda madhambi madogo na makubwa, zaidi ya hapo inawezekana mtu huyo akawa mkweli au shahidi au mtu mwema kama ilivyoelezwa katika sehemu nyingine kuwa husamehewa matokeo ya dhambi kwa toba au kuomba msamaha au mema yenye kufuta au matatizo yenye kufidia au shufaa yenye kukubalika au kwa utashi binafsi wa Mwenyezi Mungu na rehema Zake. Ukisema: Ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mwenye kumuua muumini kwa makusudi…” (Sura An-Nisai: 93.) Na kauli Yake: “Hakika wale ambao wanakula mali ya yatima kwa dhulma bila shaka wanakula moto matumboni mwao na wataingia Motoni.” (Sura An-Nisai:10.) Na kauli Yake: “Na anayemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kuiruka mipaka Yake….” (Sura An-Nisai: 14.) Na 60 Al-Fatawa Al-Kubra 4: 220.

45


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 46

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kauli Yake: “Wala msiliane mali baina yenu kwa batili..” (Sura AlBaqarah:4) Na kauli Yake: “Na mwenye kufanya hili kwa uadui na dhuluma...” (Sura An-Nisai: 30.) Na Aya nyingine kama hizo zinazotoa ahadi ya adhabu. Tunasema: Ni kwa mujibu wa kauli ya Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Mwenyezi Mungu amemlaani mlevi wa pombe.”61 Au “Asiyewatimizia haki wazazi wake wawili.”62 Au “Atakayebadili minara ya ardhi.”63 Au “Atakayechinja kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu.”64 Au “Mwenyezi Mungu amemlaani mwizi.”65 Au “Mwenyezi Mungu amemlaani mla riba, mwakilishi wake, shahidi wake na mwandishi wake.”66 Au “Mwenyezi Mungu amemlaani mwenye kupinga sadaka na mwenye kuzifanyia uovu.”67 Au “Atakayezua tukio Madina au akamsaidia mwenye kuzua tukio basi laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika Wake na watu wote itakuwa juu yake.”68 Na Hadithi nyingine kama hizo za ahadi ya adhabu, lakini hazijaruhusu kumuainisha mtu yeyote miongoni mwa watu binafsi waliofanya matendo hayo na kusema: Huyu mtu binafsi amepatwa na ahadi hii ya adhabu. Hilo ni kwa sababu anaweza akatenda chochote kinachofuta adhabu kama toba au jambo lingine.” 61 Majmauz-Zawaid 4: 90, humo anasema kuwa (s.a.w.w.) alisema: “Mwenyezi Mungu ameilani pombe, mtengenezaji, mnywaji na mnyweshaji….” 62 Musnad Ahmad 1: 317. 63 As-Sunan Al-Kubra cha An-Nasai 3: 67. 64 Al-Mustadrak Alas-Sahihain 4: 153. 65 Sahih Bukhar 8: 15. 66 Sahih Muslim 5: 50, humo mna: “Mwenyezi Mungu amemlaani mla riba, mwakilishi wake, mwandishi wake na shahidi wake.” 67 Musnad Ahmad, 1:464 – 465. 68 Sahih Bukhar 4: 69, humo mna: “Madina iliyo tukufu ni eneo kati ya Air mpaka Kadha, basi atakayezua tukio Madina au akamsaidia mwenye kuzua tukio basi laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika Wake na watu wote itakuwa juu yake.”

46


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 47

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Akaendelea mpaka akasema: “Atakayefanya matendo kama haya kwa kudhani kuwa ni halali kutokana na ijitihadi au ufuasi na mfano wa hayo basi atakuwa na kinga ya kutokupatwa na adhabu kutokana na kizuizi kama ilivyoshindikana kwao kupata adhabu kutokana na toba au mema yenye kufuta au matatizo yenye kufidia au kama hayo. Na njia hii ndiyo ambayo tunawajibika kuifuata kwani hakuna njia nyingine ila mbili mbaya: Ya kwanza: Kusema kuwa kila mmoja atapatwa na adhabu kama ilivyo. Na pili ni kudai kuwa amefanya kwa mujibu wa maelezo ya Aya au Hadithi, na hili ni baya sana kuliko hata kauli ya Makhawariji wanaowakufurisha watu kwa madhambi, ya Muutazila na wengineo, na ubovu wake unajulikana kwa dharura na dalili zake zinajulikana huko sehemu yake. Hivyo maelezo ya ahadi ya adhabu kama haya na mengineyo ni haki, lakini mtu binafsi ambaye amefanya vitendo hivyo hathibitishiwi moja kwa moja kuwa atapatwa na adhabu hiyo, hivyo kwa muislamu hathibitishiwi Moto kwa kuwa sharti halijatimia au kwa kuwa kuna kizuizi. Na hivyohivyo upande wa kauli zinazomkufurisha msemaji wake, kwani huenda msemaji huyo hajafikiwa na maelezo yanayomlazimu kuijua haki, na huenda yamemfikia lakini hayajathibiti kwake au hajaweza kuyajua na kuyafahamu ipasavyo, au huenda amepatwa na mkanganyiko ambao Mwenyezi Mungu atamsamehe kwawo. Basi atakayekuwa anamwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake mwenye kudhihirisha Uislamu mwenye kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake Mwenyezi Mungu anamsamehe hata kama atatenda baadhi ya madhambi kwa maneno au vitendo, sawa aitwe mshirikina au muasi. Hili ndilo wanaloliamini maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na maimamu wote wa Uislamu, lakini makusudio ni kuwa madhehebu ya maimamu yamejengeka katika imani hii ya kutofautisha kati ya sifa jumuishi na mtu binafsi.”69 69 As-Sawaiq Al-Muhriqah fi radi Alal-Wahabiyyah, Sulayman bin AbdulWahab: 86 – 88 uhakiki wa Darul-Hidayah.

47


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 48

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Maneno haya tumeyaleta kwa urefu wake na mapana yake kutokana na uzito wa utata huu na haki kufichikana sana, na tunaweza kuufikia ukweli kwa njia ya kubainisha baadhi ya nukta muhimu zinazopatikana katika kanuni hii katika nukta mbalimbali nazo ni: Hakika kulaani si kutoa habari za hali ya mlaanifu mpaka tuseme kuwa huenda mtu anayelaaniwa atatubu na kuomba msamaha na hivyo huenda akapatwa na rehema ya Mwenyezi Mungu. Bali kwenyewe kama tulivyosema tangu mwanzo kuwa ni kuomba mtu huyo aondolewe kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu, hivyo huenda Mwenyezi Mungu akajibu dua au asijibu, na huenda kweli mtu huyo baadaye akatubu na kuwa miongoni mwa waja wema na huenda asitubu, hivyo Mwenyezi Mungu anatenda kwa vipimo Vyake na muumini anatekeleza jukumu lake. Basi mtu atakapomuona mtu mwenye kutenda vitendo vilivyolaaniwa na Kitabu na Sunna ya Mtukufu Mtume anawajibika kuamrisha mema na kukataza mabaya kwa kufuata hatua zake tatu, kwa mkono wake, ulimi wake na kwa moyo wake, na laana ni miongoni mwa hatua ya ulimini na moyoni, hivyo akiweza kuidhihirisha na kuitoa nje na kuitangaza waziwazi hiyo ni katika hatua ya ulimimi. Na kama hawezi kufanya hivyo basi hiyo ni katika hatua ya moyoni. Na katika laana hii hakuna kitu kinacholazimu kufichua na kutoa habari za hali ya mtu mlaanifu mbele ya Mwenyezi Mungu kama ililivyo wazi, ila tu pale Mwenyezi Mungu atakapokuwa kamlaani mtu binafsi ndani ya Kitabu Chake au kupitia maneno ya Mtume Wake, laana kama hii ina aina fulani ya habari zinazofichua hali ya mtu huyo mbele ya Mwenyezi Mungu. Na kanuni ya kutofautisha kati ya kulaani kundi kwa kuzingatia sifa au kumlaani mtu binafsi imetokana na kuchanganya kati ya muumini kumlaani mtu binafsi na kati ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kumlaani mtu huyo, kwani laana ya watu kumlaani mtu binafsi haina habari yoyote, kinyume na laana itokayo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, na 48


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 49

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu tunayozungumzia ni laana ya watu kumlaani mtu binafsi isiyokuwa na chembechembe yoyote ya habari za Akhera, hivyo haina hoja yoyote kauli ya Al-Ghazalii kuhusu muumini kumlaani Yahudi kuwa: “Hili lina hatari kwani huenda anaweza kuja kusilimu na akafariki akiwa amejikurubisha zaidi kwa Mwenyezi Mungu, sasa vipi ahukumiwe kuwa ni mlaanifu?” Kwani maana ya kumlaani ni kuwa Mwenyezi Mungu amesharuhusu alaaniwe kulingana na hali yake ya sasa, na hukumu ya kuwa ni mlaanifu mbele ya Mwenyezi Mungu? Au hapana inabakia kwa Mwenyezi Mungu kulingana na vipimo Vyake vikuu alivyonavyo na vielelezo kamilifu, wala katika hilo hakuna hatari yoyote bali huenda hatari ipo katika kuacha kwani kunadhoofisha kwa muumini hisia za kufuata haki na roho ya kuikataa batili, na hii ndio hatari ya kuacha kulaani laana ambayo AlGhazalii anaikanusha. Hakika Aya: “Huna neno katika shauri awakubalie toba yao au awaadhibu, maana hakika wao ni madhalimu.”70 Ambayo imesemekana kuwa ilishuka kumkataza Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akiwalaani ndani ya Swala yake mwezi mzima wauaji wa maswahaba kwenye kisima cha Muuta, yenyewe haionyeshi kuwa Mwenyezi Mungu anamkataza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) dhidi ya laana hii, na kikubwa kinachoonyeshwa na Aya ni kuwa laana si kipimo halisi cha mafikio ya watu waovu, kwani huenda Mwenyezi Mungu atawasamehe na huenda atawaadhibu, na hili halilazimishi laana ikatazwe kama alivyotafsiri Al-Ghazalii. Na hili linaoana kabisa na tukio la mlevi wa pombe ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu alimuadhibu mara kwa mara na akakataza asilaaniwe71, kwani kukutaza huko huenda kunatokana na utambuzi wake binafsi aliokuwa nao Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) juu ya matokeo ya mustakabali wa mtu huyo na mbele ya Mwenyezi Mungu, hivyo ndio maana Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) 70 Sura Al-Imran: 128. 71 Sahih Bukhari 8: 14, chapa ya Darul-Fikri.

49


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 50

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu akawakataza maswahaba zake wasimlaani, ikiwa ni ishara kuwa huenda dua zao zisipokewe na kuwa wao wanamuombea mtu mwenye matokeo mazuri, hivyo Hadithi hii inakuwa sawa na hukumu kwenye tukio maalumu linalomuhusu mtu pekee bila kuwajumuisha wengine, na kutafsiri vile (alivyotafsiri Al-Ghazali) na kuacha tafsiri hii ni kuchagua bila kigezo, kwani zote mbili zinawezekana: Tafasiri ya kukataza kumlaani mtu binafsi, na tafsiri ya kuwa katazo la hapa (kwenye kisa) ni hukumu ya tukio binafsi. Na tayari imeshasemwa (na wataalamu) kuwa: Uwezekano wa pili unapopatikana basi dalili inabatilika. Ufafanuzi huu ni iwapo tu kanuni ya kutenganisha kati ya makundi na watu binafsi ni sahihi. Ama ikithibiti kuwa yenyewe ni batili na kuwa haina dalili yoyote kama ilivyo sahihi, basi haki inabakia imezingirwa kwenye tafsiri ya pili tu na hamna njia nyingine na wala zamu haifiki kwenye uchaguzi wa tafsiri iliyo bora. Tunaweza kukubaliana naye kuwa kuwalaani watu binafsi ni hatari lakini hatukubaliani naye kuwa kwa ajili ya hatari hii tujiepushe kulaani, bali linalotakiwa ni kuwa makini mno juu ya mtu tunayetaka kumlaani, hivyo asilaaniwe ila yule tu ambaye kwa yakini kabisa anastahili kulaaniwa, kustahili kusikokuwa na shaka yoyote. Wala hatumuafiki kuwa hakuna hatari katika kunyamaza bila kumlaani Ibilisi sembuse mwingine, kwa sababu laana ni silaha ya kilugha na kielimu ambayo jamii inaweza kuitumia kujilinda yenyewe dhidi ya uovu na kujihami yenyewe dhidi ya sababu za ubomoaji na uharibifu wa ndani, na kunyamaza bila kulaani kunamaanisha kuiua silaha miongoni mwa silaha za asili zenye kuhami ambazo zinaihakikishia jamii usalama wake na unyoofu wake, na kwa ajili hiyo ndio maana Mwenyezi Mungu aliwalaani watu binafsi ndani ya Qur’ani kama vile Ibilisi, na mti uliyolaaniwa ambao ni Al-Hakam bin Abu Al-As na wanawe.

50


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 51

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na maneno ya Al-Ghazali kuhusu muuaji wa Imam Husein (a.s.): “Sahihi ni kusema: Muuaji wa Husein Mwenyezi Mungu amlani iwapo alikufa kabla ya toba, kwa sababu huenda alikufa baada ya kutubu…” ni kukiri kuruhusiwa kuwalaani watu binafsi miongoni mwa waisilamu kwa sababu toba haihusiani na laana, kwa sababu kosa lake linajulikana waziwazi kuwa yeye ndiye aliyeamuru Husein auwawe na ndiye aliyetoa tamko la kumuuwa na wala haijulikani kama alitubu, hivyo ikiwa kitendo hicho kimetoka kwake basi sisi hatujui kama toba yake imekubaliwa, na muhimu zaidi ni kuwa ndani ya hesabu za Al-Ghazalii Yazid si miongoni mwa watu waliofia ndani ya ukafiri, lakini cha kushangaza imekuwaje ameruhusu alaaniwe ilihali yeye kasema hairuhusiwi laana ila juu ya aliyefia ndani ya ukafiri? Ama maneno ya Ibnu Taymiyyah kuwa hairuhusiwi: “Hazijaruhusu kumuainisha mtu yeyote miongoni mwa watu waliyofanya matendo hayo na kusema: Huyu mtu binafsi amepatwa na ahadi hii ya adhabu. Hilo ni kwa sababu anaweza akatenda chochote kinachofuta adhabu.” Ikiwa ni kwa kigezo cha ahadi ya Mwenyezi Mungu Akhera na zitakavyokuwa hali za watu binafsi siku ya Kiyama, maneno yake ni sahihi wala hayana tatizo lolote, kwani hakuna mtu yeyote anayeweza kuwa na yakini juu ya hali za watu binafsi siku ya Kiyama kwa sababu mambo hayo ni siri na nafsi zimefichwa kwetu. Ama kwa kigezo cha athari za kidunia zinazotokana na matendo yao, maneno hayo kisheria hayakubaliki, kwani haiwezekani kuyaamini achia mbali kuyatekeleza, kwa sababu ni wazi kuwa kuritadi na unafiki na baadhi ya mambo ya uovu husababisha athari za malipo ya kisheria, kama vile wajibu wa kumuuwa aliyeritadi, basi iwapo tukitekeleza kanuni hii na tukaacha kutekeleza adhabu ya malipo ya kisheria kwa watu binafsi, (kama anavyosema kuwa) haturuhusiwi kumuashiria mtu fulani na kusema: Yeye ameritadi au muovu au mlaanifu, basi hatutoweza kutekeleza hukumu za adhabu za malipo ya kisheria ya kiislamu zinazotokana na anuani hizi za matendo. 51


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 52

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na dalili juu ya hilo ni kitendo cha khalifa wa kwanza, ikiwa kweli hakuwaainisha watu fulani kwa madai ya kuritadi na kutoka kwenye dini, ni kwa kigezo kipi aliruhusiwa kuwauwa? Hivyo kitendo cha khalifa wa kwanza ni jibu la wazi kabisa ndani ya kambi ya kisunni juu ya ubatilifu wa kanuni ya kutenganisha kati ya sifa jumuishi na watu binafsi katika ahadi za adhabu. Ni wazi kuwa kutekeleza malipo ya adhabu na mengineyo juu ya aliyeritadi, muovu na munafiki huwa ni kwa kuzingatia hali ya nje ya mtu, na wala hali hiyo hatuwezi kuifanya kuwa ndio dalili juu ya matokeo mabaya ya Akhera kwani Akhera ina hesabu zake ambazo zenyewe zimefichikana kwetu, na ahadi ya adhabu za Akhera za watu hawa hatuna njia ya kuzijua ila kwa habari za Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume Wake kuhusu watu hawa kama ilivyo wazi tangu mwanzo. Pia ni wazi kuwa kutekeleza athari hizi za kidunia zinahitaji ushahidi makini kwa sababu kumhukumu muislamu kwa ukafiri au unafiki au uovu ni jambo zito sana si la kudharau kama yalivyokubaliana madhehebu yote ya kiislamu isipokuwa watu wachache kama vile Makhawariji. Matokeo ni kuwa kanuni iliyotajwa ikiwa ni kwa kigezo cha Akhera basi yenyewe ni sahihi isipokuwa tu wale ambao Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wametoa habari kuwa watu hao binafsi watapatwa na adhabu. Na kama ni kwa kigezo cha athari za duniani basi yenyewe si sahihi na wala hatuwezi kuiamini, ndiyo kuthibitisha athari hizi za kisheria juu ya watu binafsi kunahitaji sharti za uthibitisho tena zilizokamilika, na kuwa makini sana katika kuchambua ni nani mfano halisi wa ukafiri, kuritadi, unafiki na uovu, na wala isiwe kwa namna ya kubahatisha na shaka. Na miongoni mwa ushahidi unaothibitisha ubatilifu wa kanuni hii ni athari za kihistoria zinazoonyesha kuwa maswahaba walikuwa wakiwaambia watu binafsi na kuwaashiria kwa ukafiri na unafiki, kama vile habari ya 52


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 53

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Aisha kuhusu Mar’wan na baba yake72 na maneno yake ambayo AlGhazali ameyataja huko nyuma, na maneno yake kuhusu Uthman73 na maneno maarufu ya Abu Said Al-Khudri aliposema: “Hakika sisi tulikuwa tunawajua bila shaka wanafiki kwa kumchukia Ali bin Abi Talib.”74 Yenyewe ni maneno yanayowagusa watu binafsi maalumu ndani ya dhamiri ya muongeaji na anawaita watu binafsi kwa sifa ya unafiki. Ibnu Aqil Al-Alawi amemjibu Al-Ghazali kwa kusema: “Nasema: Nashangaa imekuwaje Ibnu Al-Munir na Al-Ghazali na aliyewafuata watafsiri kitendo cha Mtume (s.a.w.w.) kukataza maswahaba zake kumlaani mlevi wa pombe mwenye kumpenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kuwa amekataza kuainisha, ilihali katazo lililopo kwenye Hadithi hiyo lina sababu maalumu nayo ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake tena limetokea baada ya kuadhibiwa, na wala kutoka ndani ya ibara za Hadithi haifahamiki maana yoyote ya kuainisha au kutokuainisha. Na hoja yenye nguvu sana katika uhalali wa kumlaani muislamu binafsi ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kwani anasema kuhusu yamini ya mwenye kulaani:

“Na mara ya tano laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake ikiwa ni miongoni mwa waongo.” (Sura An-Nur: 7.) Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) mara nyingi alimuapisha mwenye kulaani na akafanya hilo kuwa ni sheria ya kudumu ndani ya umma wa Muhammad (s.a.w.w.) mpaka siku ya Kiyama, na uainishaji kwa dhamiri ya mzungumzaji hapa una nguvu sana kuliko kuainisha kwa kutaja jina la mtu 72.Usudul-Ghaba cha Ibnu Athir 2: 35, mlango wa herufi Hau na Kaf. At-Tafsir Al-Kabir cha Ar-Raz 20: 237, kwenye tafsiri ya Aya ya 60 ya Sura Al-Israi. 73 Al-Kamil fi At-Tarikh 3: 105, amesema: “Muuweni Naathal bila shaka yeye amekufuru.” Tarikh At-Tabari 3: 12, matukio ya mwaka 36 A.H. 74 Sunan At-Tirmidh 5: 593, kitabu cha fadhila, mlango wa 20 fadhila za Ali (a.s.) Hadithi ya 3717.

53


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 54

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu binafsi, kama inavyoelezwa kwenye vitabu vya lungha ya kiarabu, na wala hakuna yeyote aliyesema kuwa aliye muongo kati ya wenye kutoleana laana ni kafiri hata ioane na kauli ya Al-Ghazalii na waliomfuata kuwa hairuhusiwi laana kwa mtu binafsi ila kwa kafiri. Na Mtukufu Mtume (s.a.w.w) aliwalaani watu aliyowataja kwa majina na walifia ndani ya Uislamu kama vile Abu Suf’yan bin Harbu, Suhayl bin Amr, Amr bin Al-As, Abu Al-Aawar As-Salmiy, Al-Hakam bin Abul-As na mwanae Mar’wan na wengineo, na akawalaani maswahaba wakubwa watu aliowataja kwa majina yao kama vile Muawiya, Amr bin Al-As, Habib, Abdur-Rahman bin Khalid, Dhahak bin Yazid, Basru bin Artaah, Al-Walid, Ziyad, Al-Hajjaj bin Yusuf na wengine wengi ambao ni vigumu kuorodhesha idadi yao. Na pia Hasan bin Thabit alimlaani Hindu binti Ut’bah na mumewe Abu Sufyan zama ambazo yeye (Abu Suf’yan) alikuwa akimtetea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dini yake lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w) hakukataza bali aliridhia. Alisema katika beti zake: “Laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu ya Hindu pamoja na mumewe.”75 Na Umar bin Al-Khattab alimlaani Khalid bin Al-Walid alipomuuwa Malik bin Nuwayrah.76 Na Ali (a.s.) akamlaani Abdullah bin Zubayr siku aliyouawa Uthman kwa kuwa hakumhami.77 Na Abdullah bin Umar alimlaani mwanae Bilal mara tatu kama alivyoeleza Ibnu Abdul-Bar amesema: Imepokewa kutoka kwa Abdullah bin Hubayrah As-Sabaiy amesema: “Alitusimilia Bilal bin Abdullah bin Umar kuwa baba yake Abdullah bin Umar siku moja alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu 75 Ad-Daywan 1: 384 Chapa ya Dar Sadir. 76 At-Tabari 3: 241 kwa matamshi yake mbalimbali, na katika baadhi yake: “…Akamkashifu Muhammad bin Talha na kumlaani Abdullah bin Zubayr.” AlKamil fi Tarikh 3: 358 – 359. Sharhu An-Nahju 1: 179. 77 Murujudh-Dhahab 2: 54.

54


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 55

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu (s.a.w.w.) alisema: “Msiwazuie wanawake kupata mafungu yao kutoka msikitini.” Nikasema: Mimi nitaendelea kumzuia mke wangu na anayetaka amruhusu mkewe. Basi akanigeukia na kuniambia: Mwenyezi Mungu akulaani, Mwenyezi Mungu akulaani, Mwenyezi Mungu akulaani. Unanisikia nasema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kaamuru wasizuiliwe, kisha akasimama akiwa amekasirika.78 Na imesihi kutoka kwa Imam Malik kuwa alisema: Mwenyezi Mungu amlaani Amru bin Ubaydu - yaani mtawa mashuhuri. Na akasema Muhammad bin Hasan sahaba wa Abu Hanifa Mwenyezi Mungu awarehemu wote wawili kuwa, nilimsikia Abu Hanifa akisema: “Mwenyezi Mungu amlaani Amr bin Ubaydu.” Na Ibnul-Jawzi amenukuu kutoka kwa AlQadhi Abu Yaal kwa kuitoa kwa Salih bin Ahmad bin Hambal alisema: “Nilimwambia baba yangu: Watu wanatunasibisha na utawala wa Yazid, akasema: Ewe mwanangu mpendwa! Hivi yeyote anayemwamini Mwenyezi Mungu humtawalisha Yazid, na kwa nini tusimlaani aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake? Nikamwambia: Ni wapi Mwenyezi Mungu kamlaani Yazidi ndani ya Kitabu Chake? Akasema: Kauli Yake “Na kama nyinyi mkipata utawala ni karibu mtaiharibu nchi na mtaukata ujamaa wenu.* Na ndio Mwenyezi Mungu amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao.”79 Je kuna uharibifu mkubwa kama mauwaji haya.” Na katika riwaya nyingine: “Ewe mwanangu mpendwa, nitasema nini kuhusu mtu aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Kitabu Chake.”80 Na Bukhari amenukuu kuhusu kuumbwa kwa vitendo vya waja akasema: Wakiu alisema: Bashru Al-Maraysiyyu laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake, je ni myahudi au mkiristo? Mtu mmoja akamjibu: “Baba yake au babu yake alikuwa mkiristo.” Wakiu akasema: “Laana ya Mwenyezi 78 Jamiu Bayanl-Ilmi Wafadhluhu 16: 414, Hadithi ya 45174. 79 Sura Muhammad: 22 – 23. 80 Ameinukuu Ibnu Hajar ndani ya kitabu Tat’hir Al-Jinan Wal-Lisan: 50.

55


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 56

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Mungu iwe juu yake na juu ya wafuasi wake.”81 Na Bakru bin Hammad, Al-Qadhi Abu Tayyib, Abu Al-Mudhaffar AlAsfarainiy na wengineo walimlaani Imran bin Hattan katika jibu lao mashuhuri juu ya beti zake ambazo alimsifia muovu wa waovu Ibnu Muljim laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake.82 Na Yahya bin Mu’in alimlaani Husein bin Ali Al-Karabis As-Shafiy Al-Baghdad kama ilivyoelezwa ndani ya kitabu Tahdhibut-Tahdhib83 na bado laana imetapakaa baina ya waislamu pindi wanapogundua maasi kutoka kwa mtu binafsi, maasi yanayostahili kumlaani. Na utakapofuatilia vitabu vya Hadithi, sira na historia utavikuta vimesheheni hilo, na kwa ajili hii namwambia mtafiti wa haki kuwa yasikushitue maelezo mengi ya hawa ya kukataza kuainisha, japokuwa zimepatika riwaya nyingi zinazowakhalifu wao kutoka kwa Mtume wao na maswahaba wengi na kutoka kwa mashekhe wakubwa wa zamani, basi furahia kwani uongofu ni uongofu wa Muhammad na maswahaba zake.”84 Laana haimpeleki mtu kwenye ukafiri Wanachuoni wa kiislamu wamekuwa wakali kuhusu kumkufurisha mtu miongoni mwa waislamu na wala hawajaruhusu hilo ila kwa kutimia masharti maalumu na kwa ugumu sana, hiyo ni kutokana na taathira za kisheria zinazotokana na kitendo hicho, na pia Sunna ya Mtukufu Mtume imekuwa makini sana na jambo hilo, hivyo umashuhuri wake na kutapakaa kwake kunatutosheleza dhidi ya ufafanuzi wake na dhidi ya kuleta ushahi81 - Khulqu Af’alil-Ibad: 20. 82.Nurul-Absar cha Shablanji: 199. Katika beti za mwanzo za Bakri bin Hassan amesema: "Mwambie Ibnu Muljim na nguvu zilizoshinda umeubomolea Uislamu na dini nguzo. 83. Tahdhibut-Tahdhib 2: 360, namba 608. 84.An-Nasaihul-Kafiyah: 33 - 36, chapa ya Muassasatu Al-Fajri

56


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 57

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu di wa maneno ya wanachuoni wa sheria na wanatheolojia. Na la muhimu sana kwetu katika mlango huu ni kusema kuwa miongoni mwa sharti maarufu katika kumkufurisha mtu ni kitendo kinachompeleka mtu kwenye ukafiri kisiwe kimetokana na ijtihadi ya kimakosa kwani mwenye kufanya ijtihadi amesamehewa na yale yanayotokana na ijtihadi yake, na wala mujtahid mmoja hana njia juu ya mujtahid mwingine. Na hili ndilo linalofanyika katika mlango wa laana, yule ambaye juhudi zake za kielimu na madhehebu yake vitampelekea kuwalaani baadhi ya maswahaba bali akaona hilo ni bora, hatuwezi kumhukumu kuwa ni kafiri au muovu hata kama asili ya laana inawajibisha awe hivyo, kwani ijtihadi ni miongoni mwa mambo yanayozuia hukumu hiyo ya kidhana. Na vifuatavyo vi vipande vya rai za Sheikh Ibnu Taymiyyah na Sheikh Ibnul Qayyim Al-Jawziyyah kuhusu dhamira hii, kauli hizo zimenukuliwa na Sheikh Sulayman bin Abdul-Wahab kaka mpendwa wa Sheikh Muhammad bin Abdul-Wahab mwasisi wa Uwahabi ndani ya kitabu chake “Vimondo vya Mwenyezi Mungu katika kuwajibu Mawahabi.” Humo ameandika: “Na kwa kuchukulia kuwa haya mambo mnayodai ni ukafiri, yaani nadhiri na kinachohusiana nayo, basi hapa kuna msingi mwingine miongoni mwa misingi ya Sunni ambao wote wameukubali kama alivyotaja Sheikh Taqiyyud-Din na Ibnul-Qayyim kutoka kwao, nao ni kuwa asiyejua na mwenye kukosea ndani ya umma huu hata kama atatenda jambo la ukafiri na shirki ambalo mwenye kulitenda huwa kafiri au mshirikina basi yeye atasamehewa kutokana na ujinga na makosa mpaka dalili imbainikie, mwenye kukufurishwa ni yule mwenye kuiacha waziwazi na kwa ubainifu usiochanganyikana na mwingine, au anayeacha lile linalojulikana kwa dharura ndani ya dini ya Uislamu, ambalo wote wamekubaliana kwa yakini na uwazi kabisa, analolijua kila mtu miongoni mwa waislamu bila kufikiria wala kusita.85 85 As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 33, uhakiki wa Darul-Hidayah.

57


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 58

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Imenukuliwa kutoka kwa Ibnul-Qayyim kuwa alisema: “Ukafiri wa kupinga una namna mbili: Ukafiri wa kupinga kitu kizima na ukafiri wa kupinga sehemu maalumu ya kitu kizima, wa kitu kizima ni kupinga yote aliyoteremsha Mwenyezi Mungu na ujumbe wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na wa sehemu ya kitu kizima ni kupinga faradhi yoyote miongoni mwa faradhi za Uislamu au haramu yoyote miongoni mwa haramu zake au sifa miongoni mwa sifa alizojisifu mwenyewe Mwenyezi Mungu, au habari miongoni mwa habari alizozitoa Mwenyezi Mungu, afanye hivyo kwa kusudi au kwa kutaka kumshinda mpinzani wake kwa ajili ya lengo lolote miongoni mwa malengo, kwa kusudi huku akiwa anajua. Ama akifanya hivyo kwa ujinga au kwa tafsiri fulani, anasamehewa na hivyo mwenyewe hakufurishwi kutokana na riwaya iliyomo ndani ya Sahih mbili, Sunan na Masanid iliyotoka kwa Abu Huraira, amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Alisema mtu mmoja ambaye alikuwa hajaifanyia kheri yoyote familia yake – Na katika riwaya nyingine: Mtu mmoja alifanya uharibifu juu ya nafsi yake – basi ulipofika wakati wa kifo aliwausia wanawe kuwa atakapofariki wamchome moto kisha nusu yake waiweke nchi kavu na nusu yake baharini, naapa kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu Mwenyezi Mungu alimkadiria kumwadhibu adhabu kali ambayo hajawahi kumwadhibu yeyote miongoni mwa viumbe, basi alipofariki wakafanya kama alivyowaamuru, ndipo Mwenyezi Mungu alipoiamuru bahari ikakusanya iliyonayo na akaiamuru nchi kavu ikakusanya iliyonayo, kisha akamwambia: Kwa nini ulifanya hivyo? Akajibu: Ewe Mola Mlezi! Ni kwa ajili ya kukuogopa na wewe unajua. Basi akamsamehe.” Huyu ni mkanushaji wa uwezo wa Mwenyezi Mungu juu yake na mkanushaji wa ufufuo lakini pamoja na haya yote Mwenyezi Mungu alimsamehe na kumkubalia udhuru wake kutokana na ujinga wake, kwa sababu hicho ndicho kiwango cha elimu yake na hakupinga hayo kwa kiburi, na hicho ndicho kitenganishi katika ubatilifu wa kauli ya anayesema: “Hakika Mwenyezi Mungu hakubali udhuru wa ujinga kwa viumbe katika kuwaon58


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 59

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu dolea adhabu iwapo hicho ndicho kiwango cha elimu yake.”86 Imenukuliwa kutoka kwa Ibnu Taymiyyah kuwa alisema: “Na miongoni mwa bidaa mbaya ni kulikufurisha kundi maalumu na linginelo lolote miongoni mwa makundi ya kiislamu na kuhalalisha damu yao na mali yao, na hili ni kosa kubwa kwa sababu mbili: Ya kwanza: Hakika hilo kundi jingine huenda likawa halina bidaa kubwa kuliko ile ya kundi lile lenye kukufurisha, bali huenda kundi lenye kukufurisha likawa na bidaa kubwa kuliko lile lenye kukufurishwa, na huenda yakalingana au likawa chini, na hii ndio hali ya watu wote wa bidaa na matamanio ambao wanakufurishana wao kwa wao, na hawa ni miongoni mwa wale aliowazungumzia Mwenyezi Mungu kwa kusema:

“Hakika wale waliofarikisha dini yao na wakawa makundi makundi huna uhusiano nao wowote.” (Sura Al-An’am: 159.) Ya pili: Lau ikijaaliwa kuwa kundi moja limo ndani ya bidaa na jingine limo ndani ya Sunna basi Sunna hii haijamkufurisha kila anayesema kauli yoyote yenye makosa, kwani Mwenyezi Mungu anasema: “Mola wetu Mlezi usitushike kama tukisahau au tukikosa…” (Sura Al-Baqara: 286.) Na imethibiti ndani ya Sahihi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa Mwenyezi Mungu “Alisema: Tayari nimeshafanya.” Na Mwenyezi Mungu akasema:

“Wala si lawama juu yenu katika hayo mliyokosa, isipokuwa katika yale ziliyofanya nyoyo zenu kwa kusudi…” Sura Al-Ahzab: 5. 86 As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 8.

59


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 60

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Na imepokewa kutoka kwa (s.a.w.w.)87 kuwa alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameusamehe umma wangu yatokanayo na makosa, usahaulifu na waliyoshinikizwa.” Nayo ni Hadithi nzuri ameipokea Ibnu Majah na wengine. Na maswahaba na waliowafuata kwa wema na viongozi wengine wa waislamu wote wamekubaliana kuwa si kila anayesema kauli yenye makosa basi anakufurishwa kwa kauli hiyo, hata kama kauli yake inakhalifu Sunna, lakini watu wana utata katika suala la kukufurisha nalo limeelezwa kwa upana sehemu nyingine.”88 Na pia imenukuliwa kutoka kwake kuwa: “Hakika mimi nakiri kuwa Mwenyezi Mungu ameshausamehe umma huu makosa yake, na hilo linajumuisha makosa ya kwenye masuala ya kihabari na masuala ya kielimu, na waliyopita bado wanazozana kuhusu masuala mengi miongoni mwa masuala haya na hakuna yeyote miongoni mwao anayemthibitisha mtu binafsi kwa hilo, si kwa ukafiri wala uovu wala maasi, kama Sharihu alivyokanusha usomaji wa: “Bali unastaajabu, na wao wanafanya mzaha.” (Sura As-Saffat: 12.) Akasema: Hakika Mwenyezi Mungu hastaajabu.” Mpaka akasema: “Mzozo huu umepelekea kuuwana kati ya waliotangulia japokuwa Sunni wameafikiana kuwa makundi yote mawili yana imani, na kuwa kuuwana hakuzuii uadilifu uliothibiti kwao, kwa sababu muuwaji hata kama atakuwa ni dhalimu lakini yeye ni mwenye kuleta maana nyingine na kuleta maana nyingine kunazuia uovu. Na nilikuwa nikiwabainishia kuwa yaliyonukuliwa kutoka kwa waliotangulia na viongozi kuwa kutoa tamko la ujumla la kumkufurisha mtu anayesema kadha wa kadha pia nako ni haki, lakini ni lazima kutofautisha kati ya mjumuisho na muainisho, na hili ndilo suala la kwanza ambalo umma ulizozana miongoni mwa masuala makubwa ya misingi, nalo ni 87.As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 85, uhakiki wa Darul-Hidayah. 88 As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 80 – 81.

60


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 61

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu suala la ahadi ya adhabu, kwani hakika maelezo ya ahadi ya adhabu ndani ya Qur’ani ni ya mjumuisho yasiyokuwa na mipaka, kama kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale ambao wanakula mali ya yatima kwa dhuluma..” (Sura An-Nisai: 10). Na vilevile mambo mengine kama atakayefanya hivi basi atapata hivi au yeye ni hivi, hakika maelezo haya ni ya mjumuisho yasiyokuwa na mipaka na yenyewe ni sawa na kauli ya mwenye kusema miongoni mwa waliotangulia: “Atakayesema kadha basi yeye ni kafiri.” Mpaka akasema: “Na kukufurisha ni miongoni mwa ahadi ya adhabu, hivyo japokuwa kauli hiyo itakuwa ni kupinga aliyoyasema Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) lakini inawezekana mtu huyo ni mgeni ndani ya Uislamu au amekulia kijiji cha mbali, na huenda akawa ni mtu ambaye hajasikia maelezo hayo au ameyasikia lakini kwake hayajathibiti au yamekinzana kwake na kitu kingine, au amewajibika kuyaletea maana nyingine japokuwa ni mwenye makosa. Na daima hukumbuka Hadithi iliyomo ndani ya Sahihi mbili inayomhusu mtu aliyeiambia familia yake kuwa: “Nitakapofariki mnichome moto…” kwani mtu huyu alishakia uwezo wa Mwenyezi Mungu na uwezekano wa kumrudisha baada ya kuwa chembechembe za udongo bali aliamini kuwa hakuna ufufuo, na huu ni ukafiri kwa itifaki ya waislamu wote, lakini alikuwa mjinga hajui hilo na alikuwa muumini akiogopa Mwenyezi Mungu asimuadhibu, basi ndipo Mwenyezi Mungu akamsamehe. Na maana iliyoletwa kutoka kwa watu wa ijtihadi wenye pupa ya kumfuata Mtukufu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) inafaa zaidi kusamehewa kuliko mfano wa hili.”89 Imenukuliwa tena kuwa Ibnu Taymiyyah aliulizwa kuhusu watu wawili waliozungumzia suala la kukufurisha, basi akajibu na kurefusha jibu, na mwisho wa jibu akasema: “Tukijalia kuwa mtu huyo alitetea ukafiri dhidi 89 As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 83 – 84.

61


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 62

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu ya mtu anayeamini kuwa si kafiri ili amhami na kumnusuru ndugu yake muislamu basi lengo hili ni zuri tena la halali, na yeye iwapo amefanya ijtihadi katika hilo na akapatia basi ana thawabu mbili na kama atakosea ana thawabu moja.”90 Vifungu hivi ni sehemu ya mitazamo ya waasisi wa Salafiyyah mpya, vinatosha kabisa kuonyesha mitazamo ya wanachuoni wengine wa sheria japokuwa hatumkosi aliyezidiwa na chuki yake na akatoa fatwa ya kumkufurisha yule anayewatukana maswahaba na hivyo kumsababishia matatizo makubwa yule aliyetuhumiwa kwa hilo kama tutakavyoona katika nukta ifuatayo.

8-Chanzo cha kisiasa cha kumkufurisha yule aliyetuhumiwa kuwatukana maswahaba Ufafanuzi mzuri mno katika dhamira hii ni ule aliouandika Ustadhi Sheikh Asad Haydar pindi alipoandika akisema: “Hakika tuhuma ya kuwatukana maswahaba dawa yake imeshindikana hivyo imekuwa vigumu kutibika, hukumu yake imetekelezwa hivyo imekuwa vigumu kuitengua na madai hayo yameenea ndani ya jamii huku hisia zisizoona na chuki iliyofura vikiichafua, na ukweli ukiwa umesimama huku umekunja mikono mbele ya mazingira hayo ya kuumiza, mbele yake umewekewa nguo za kuuvuruga na umezungukwa na aina mbalimbali za vizuizi, na katika njia ya kuufikia ukweli kumewekwa maelfu ya adhabu huku silaha ya nguvu ikiwa juu yake, kwani utawala ulipitisha utaratibu wa kutekeleza ukafiri na uzindiki juu ya wale wanaoipinga siasa yake. Na hawakuweza kutimiza hilo ila kwa kutuhumu kuwatukana maswahaba au Abu Bakr na Umar katika sura ya pekee, na pindi wanaharakati wanapojaribu kusimama kwenye ukweli na uhalisi wa mambo basi huwatuhumu kwa tuhuma hizo na utawala huo muovu huwazingira, hivyo serikali 90 As-Sawaiq Al-Ilahiyyah: 84.

62


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 63

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu ilikuwa inapotaka kumuadhibu Shia yeyote kwa ajili tu ya madhahebu yake ilikuwa haikumbuki jina la Ali bali hufanya sababu kuu ya kumuadhibu ni kuwa yeye amewakashifu Abu Bakr na Umar. Hilo limesemwa ndani ya kitabu Al-Muntadhim, na Ibnu Athiri katika matukio ya mwaka 407 A.H. Amesema: “Ndani ya mwaka huu Shia wengi waliuwawa katika nchi zote za kiafrika na tuhuma ya kuwatukana mashekhe wawili ikafanywa ndio sababu ya kuwauwa.”91 Ni mengi sana matukio hayo ya fedheha na matendo ya unyama ambayo utawala wa kisiasa uliyatekeleza na wala hayana uhusiano wowote na Uislamu ambao unamhukumu mtekelezaji wake kuwa ametoka ndani ya Uislamu wenyewe. Na hakika suala liko wazi halihitaji maelezo ya ziada ya kubainisha na kufafanua sababu ambazo zilipelekea kutokea matukio hayo ya kuumiza na kutenda makosa hayo ya aibu na kuamiliana na wafuasi wa kizazi cha Mtukufu Mtume muamala mbaya mno. Hakuna anayeshakia kuwa uhuru wa Shia kiroho na kutokukubali sheria ya mtawala asiyeheshimu kanuni za dini na wala hafuati amri za sheria ndio uliowafanya wawe wapinzani wa utawala, hivyo tatizo la ufuasi wa kizazi cha Mtume lilikuwa ndio tatizo kubwa kati ya matatizo ambayo dola ilipambana nayo. Hivyo Shia kwa sababu ya upinzani wao na dola na kuwapinga watawala waovu walikutana na vikwazo katika njia ya kueneza wito, kama vile walivyopata ushindi pale vikwazo vinapokuwa haviwarudishi nyuma au haviwaweki kwenye mbinyo wa kufeli na kukata tamaa ya kuendelea katika njia ya kudhihirisha imani yao. Hakika walikuwa na ari na imani imara iliyowasaidia kuendelea kurudisha nafasi yao katika historia ili wabebe ujumbe ambao wanalazimika kuufikisha na ni wajibu kwao kuendeleza mapambano ili kutimiza ujumbe huo nao ni ujumbe wa Uislamu chini ya kivuli cha wito wa kizazi cha Mtukufu Mtume (a.s.), hivyo wakawa na taathira kubwa katika kueneza mwamko 91 Al-Imam As-Sadiq Wal-Madhahib Al-Ar’baah 2: 614 – 623.

63


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 64

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu wa kiislamu na kuzikomboa fikra kutoka kwenye mgando. Vyovyote vile ni kuwa maadui zao hawakupata utatuzi wa tatizo hili ila ni kuwabambikizia tuhuma ambayo jamii itaikubali hivyo wakazama ndani ya tuhuma na wakafanya njia ya kutimizia malengo hayo, wakasema: Hakika Shia wanawakufurisha maswahaba wote wa Muhammad (s.a.w.w.) na kuwatia dosari na kwa ajili hiyo dosari hizo zinafika mpaka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwa wao wanawasingizia mama wa waumini zinaa, na mengineyo. Wakaweka kanuni waliyoipitisha wanachuoni waovu nayo ni: Ukimuona mtu anamkosoa yeyote miongoni mwa maswahaba wa Muhammad (s.a.w.w.) jua kuwa ni zandiki, kwa sababu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni haki na Qur’ani ni haki na hakika aliyetufikishia Qur’ani hii na Sunna ni maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), hivyo wanataka kuwatia dosari mashuhuda wetu ili wabatilishe Kitabu na Sunna hivyo kuwatia dosari wao ni bora na wao ndio mazandiki.92 Na wakamhukumu kuwa ni kafiri yule mwenye kuwatukana mashekhe wawili, hivyo haoshwi wala kuswaliwa na wala tamko la kuwa hapana Mola wa haki ila Allah halimnufaishi chochote, na hivyo atabebwa kwa jeneza na kufukiwa ndani ya shimo lake.93 Na kuwa atakapoomba toba haikubaliki bali ni wajibu kumuuwa,94 na baadhi yao wakasema kuwa kichinjwa chake ni haramu na ni haramu kumuoza. Kutokana na haya na yale ikaenea fikira ya ukafiri wa Shia kwa sababu dola kwa utaratibu wake iliamua kuwamaliza na kukitafutia kitendo hicho kigezo cha kisheria, lakini siasa haina macho na haki haina thamani kwa wanachuoni waovu ambao walijitokeza kuutia nguvu utawala na 92 Al-Kifayah cha Khatibu Al-Baghdad: 49. 93 As-Sarim Al-Maslul: 575. 94 Rasail Ibnu Abidin 1: 364.

64


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 65

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kuwapoteza watu wa kawaida. Na hapa tunapenda kidogo kugusia uchambuzi wa Imam Kashif Al-Ghitau kuhusu tofauti ya msingi kati ya makundi mawili. 95 Baada ya kutaja tofauti kuhusu ukhalifa akasema: “Pia huenda hili lisiingie kwenye maasi wala kuwajibisha uovu iwapo linatokana na ijtihadi na imani hata kama amekosea, kwani miongoni mwa mambo yaliyokubalika kwa wote katika mlango wa ijtihadi ni kuwa mwenye kukosea ana thawabu moja na mwenye kupatia ana thawabu mbili.” Maimamu wa kisunni wamesihisha vita ambavyo vilitokea kati ya maswahaba zama za mwanzo, kama vile vita vya Jamal na Siffin na vinginevyo kwa sababu Talha, Zubayr na Muawiya walifanya ijtihadi, japokuwa walikosea katika ijtihadi yao lakini hilo halitii dosari uadilifu wao na hadhi yao, na ikiwa ijtihadi inahalalisha na wala haikatazi kuuwa maelfu ya nafsi na kumwaga damu zao, basi ni bora kuhalalisha na kutokukataza ushushaji wa heshima na hadhi unaofanywa na baadhi ya wapinzani (kutokana na ijtihadi). Hatuna uwezo wa kunukuu maneno ya wanachuoni wa kishia juu ya nukta hii muhimu ambayo ina athari kubwa katika kuchafua udugu wa kiislamu na hivyo ikawa ndio njia ya maadui wa dini ya kuingizia malengo yao.” Kisha akaongeza kwa kusema: “Hakika wazo la kuwatuhumu Shia kuwatukana maswahaba na kuwakufurisha kuliasisiwa na siasa chafu na watu duni waliouza dhamira zao kwa thamani duni wakaendelea kuliimarisha na wakazidisha uongo kwenye milango ya madhalimu wakijikurubisha kwao kwa kuwatuhumu Shia. Maadui wa dini waliitumia fursa hii hivyo wakapanua wigo wa mpasuko ili wapate malengo yake na waponye vifua vyao dhidi ya Uislamu na waislamu, wafitinishi wakaendelea 95Tazama uchambuzi huu wa thamani ambao ulisambazwa na jarida la RisalatulIslam lililotolewa na Darut-Taqrib Baynal-Madhahib Al-Islamiyyah chini ya kichwa cha habari “Uwazi wa Waisilamu” uk 227 – 228 mwaka wa pili, toleo la tatu.

65


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 66

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu kuhamasika ili kueneza fitina na kuwasha moto wa chuki kati ya waislamu bila uchunguzi na mazingatio na nyoyo zao zikiwa zimejaa chuki. Na kwa uamuzi wa siasa na utawala wake Shia wakawa ndiyo wenye kutupiwa kila baya na kushambuliwa kwa mashambulizi ya ajabu na wakasimama wenye tamaa na kuonyesha mapenzi yao kwa dola hiyo kwa kuunga mkono utawala huo na kuukubali na tayari umekuwa ni sehemu ya akili za umma ilihali wao wanajidanganya. Hawajafungua mlango wa mjadala wa kielimu na wakawaharamishia watu uhuru wa kuhoji na wakawafumba mdomo ili waweze kuamini ukafiri wa Shia na wajitenge na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.), na laiti mtafuta ukweli akiwahoji na kuwataka wamfafanulie hilo basi hawana jibu ila ni utawala huo kumuadhibu. Hivyo sisi tunawauliza: 1. Upo wapi umma huu unaowakufurisha maswahaba wote na kujitenga nao? 2. Upo wapi umma huu unaodai kuwa Maimamu wa nyumba ya Mtukufu Mtume (a.s.) ni sawa na Mola Mlezi? 3. Upo wapi umma huu ambao mafunzo yake umeyachanganya pamoja na mafunzo uliyoyachukua kutoka kwa waabudia moto? 4. Upo wapi umma huu ambao umepindisha Qur’ani na kudai upungufu wake? 5. Upo wapi umma huu ambao umezua madhehebu nje ya Uislamu? Bila shaka hawawezi kujibu hayo, kwa sababu dola imeamua tuhuma hizi basi wao hawawezi kuzikhalifu na wala haiwezekani kuwakinaisha kwa lugha ya elimu, na hakuna njia fupi mno ya kuutambua ukweli kama wangekuwa angalau na sehemu ndogo ya fikra na mabaki ya upendo wa kutaka kudadisi, kumuogopa Mwenyezi Mungu na kuhami dini. 66


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 67

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Hivi Ushia si imani inayojumuisha idadi kubwa ya maswahaba wa Muhammad (s.a.w.w.) na wao ni miongoni mwa watu wa vita vya Badri na watu wa kiapo cha ridhaa? Miongoni mwa watu waliomtawalisha Ali (a.s.) na kuamini ukhalifa wake?!! Je, miongoni mwa Mashia si wamo wanachuoni ambao hadhi yao ya juu na wingi wa elimu yao vimekubalika na wote, huku watu wakiwahitajia na wao wakiwa miongoni mwa mashekhe wa wanachuoni wakubwa na waandishi wa Sahih Sita kama vile Abu Hanifa, Shafi’i, Ahmad, Bukhari na wengineo?! Na waandishi wa Sahih Sita wametoa idadi kubwa ya wapokezi Mashia ambao idadi yao ni zaidi ya wapokezi mia tatu, na wala nafasi hii haituruhusu kutaja majina yao hivyo hilo tunaliacha kwa ajili ya fursa nyingine.96 Hivi miongoni mwa mashia si wamo watu waliobeba ujumbe wa Uislamu na kuvumilia matatizo katika kuufikisha wakiwemo waliobeba Fiqhi na laiti kama si wao basi Fiqhi ingepotea na mafunzo ya Uislamu kutoweka?! Na hakika Shia wana mchango katika kuhifadhi urithi wa Uislamu na kuulinda dhidi ya mchezo wa kisiasa.”

96 Baadhi yao amewataja Sayyid Sharafud-Din ndani ya kitabu chake AlMurajaat, ametaja wapokezi mia moja. Allamah Al-Amin ndani ya kitabu chake Al-Ghadir ndani ya juzuu ya tatu ametaja idadi kubwa miongoni mwao. Na sisi tuna orodha takriba ya wapokezi mia tatu ambao waandishi wa Sahih Sita wamewategemea “Kwa kalamu ya Asad Haydar ndani ya kitabu chake Al-Imam AsSadiq Wal-Madhahib Al-Ar’baah” na hayo yote ameyakusanya Sheikh Muhammad Jafar Al-Murawwaj At-Tabas An-Najaf ndani ya kitabu chake

“Rijalus-Shia fiasnadis-Sunnah” yaani “Wapokezi wa kishia ndani ya upokezi wa kissuni.” 67


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 68

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Kisha akasema: “Hatujazama katika kubainisha mada hii kwa mchezo tu au kwa ajili ya kuzua mada mpya, na pia hatukusudii kuzama ndani ya uchambuzi usiokuwa na mahusiano yoyote na kitabu hiki, bali ukweli halisi ni kuwa mada hii ni miongoni mwa mada muhimu ambazo ni lazima kuzigusia ndani ya kitabu hiki ambacho tumekitoa ili kubainisha madhehebu ya wafuasi wa kizazi cha Mtukufu Mtume (a.s.), na hakika tatizo kubwa lililopo mbele ya mtafiti ni suala la Shia kutuhumiwa kuwatukana maswahaba au kuwakufurisha. Na tayari mara nyingi tumebainisha kuwa hilo linatokana na sababu za kisiasa ambazo hazina ukweli wowote, kwa sababu jina Shia ni kufungamana na watu wa nyumba ya Muhammad (s.a.w.w.) na wao ndio watetezi wao, na watu wa nyumba ya Muhammad ndio mfupa uliokwama kwenye koo za hao watawala ambao waliugandamiza umma kupitia utawala, hivyo kutokana na sababu za kisiasa ukaota chuki ndani ya nyoyo za watu dhidi ya yule anayewapinga na kupambana nao au asiyewaunga mkono huku akisimama msimamo wa kupinga vitendo vyao. Je, kuna shaka yoyote katika upinzani wa Shia na kutokuunga mkono dola yao, na kuwa wao zama hizo hawakubali utawala wao kwa sababu wao hawataki kukiri kuwa Ahlul-Bayt ndio wenye haki na ukhalifa kutokana na kuwa na nafsi safi na kujitolea kwa ajili ya maslahi ya watu wote, na wao ndio wanaofaa zaidi kwa jambo hilo na waadilifu mno katika hukumu, na kwa ajili hiyo ndio maana tunaona kuwa fitina za utaratibu wa utawala juu ya yule anayetuhumiwa kuwatukana maswahaba inalenga kuwaadhibu Shia tu, ama wengineo wao hukumu hii haiwagusi hata kama ni mpagani! kama tulivyoeleza. Na huenda wanaodanganywa kwa mambo ya juu juu wakaharakisha kukubali na wakasimama kutekeleza na hivyo kuwahukumu Shia kwa uovu mara moja na ukafiri mara nyingine, natamani wangeliwekea hili mipaka maalumu ili watu wajue namna ya kuhukumu, lakini wao wamepanua wigo na kutofautisha picha, kama pia walivyopitisha kuwa 68


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 69

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu toba ya mwenye kutuhumiwa kuwatukana maswahaba au mashekhe wawili katika sura maalumu haikubaliki, na wakaamua kutekeleza rai za mtu binafsi juu ya umma wote bila kuchunguza hukumu wala kujidhibiti katika mada hii. Kwa ajili hii vibaraka miongoni mwa wanachuoni ambao walikuwa ndio chimbuko la fatwa na wakuu wa idara ya sheria, walichukua dhamana ya kuwapotosha watu na kuwapeleka kinyume na haki, hivyo walikuwa makada wa mfarakano na viongozi wa upotovu, basi wakawahukumu Shia hasa bila kueleza chanzo cha hukumu na dalili ya fatwa ya kuwa kuwauwa Shia ni jihadi kubwa na atakayeuawa wakati wa kuwapiga vita basi yeye ni shahidi. Na anasema mwisho wa fatwa kuwa: “Atakayeshakia ukafiri wao basi yeye mwenyewe anakuwa kafiri.” Na mwingine anasema: “Shia kama anawatukana mashekhe wawili na kuwalaani basi ni kafiri na kama anamfadhilisha Ali kuliko wao wawili basi ni mtu wa bidaa.”97 Hivyo ndivyo watu walivyopambiana wao kwa wao wapende tukio hilo na wakahalalisha muislamu kuuawa kwa mkono wa nduguye muislamu bila kuchunguza hukumu na kusimama mbele ya heshima hiyo, hawana lengo lolote ila ni kuuridhisha utawala hata kama Mwenyezi Mungu atawakasirikia. Wala hatuna haja ya kunukuu ibara zinazoonyesha uwezo wa akili za wasemaji wake na kiwango cha ujuaji wao wa mambo hivyo hatusimami sana kwenye uzushi huo na batili hizo bali tunaziwekea pazia. Lakini ni lazima tuchunguze nukta mbili:

97 Rasail Ibnu Abidin 2: 169.

69


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 70

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Ya kwanza: Je, kulitia dosari kundi la maswahaba kunawajibisha hukumu hizi mbaya? Au kuna tofauti na kitenganishi? Ikiwa hukumu hii ni kwa kila anayewatia dosari maswahaba au kuwasifu kwa sifa isiyofaa, basi kwa nini hawajamhukumu yule aliyewatia dosari maswahaba wengi na akawasifu kwa sifa isiyowafaa? Na wao ni miongoni mwa maswahaba wakubwa na halisi kwa sababu wao walimpinga Uthman kuhusu mazingira ya kinyume ya Bani Umayyah na kuwakumbatia kwake, au walimukhalifu Muawiya Ibnu Abu Suf’yan, hivi huoni miongoni mwa dosari na kuwatia aibu maswahaba ni kuwasifu kuwa: “Hakika wao ni miongoni mwa watu wapumbavu mabaradhuli, bila shaka wao ni waharibifu ardhini wenye kumuasi Imam.”98 Na Ibnu Taymiyyah anasema: “Hakika wao ni waasi wenye kufanya uharibifu ardhini.” Mpaka akasema: “Na wala halikumuuwa ila kundi dogo ovu la kidhalimu. Ama waliokwenda kumuua wote ni wenye makosa bali ni madhalimu waovu waliovuka mipaka.”99 Ibnu Hajar anasema katika kuwasifu waliompinga: “Hakika mujtahid hapingwi katika mambo yake ya kiijtihadi lakini hao walaanifu wenye kupinga hawana fahamu yoyote bali hawana akili yoyote.”100 “Na katika mada ya uaidilifu wamepitisha kuwa maswahaba ni waadilifu mpaka kutokee fitina. Ama baada ya hapo ni lazima tumzungumzie yule asiyekuwa kielelezo cha uadilifu, hii ndio moja ya kauli.”101 Na wala hatutaki kugusa kauli zote ambazo kwazo wamewasifu maswahaba ambao walishiriki katika kumpinga Uthman na kuwahimiza watu dhidi yake.

98 Tarikh Ibnu Kathir 1: 176. 99 Min’hajus-Sunnah 2: 191 – 206. 100 As-Sawaiqul-Muhriqah cha Ibnu Hajar: 68. 101 Sharhu Al-Fiyya Al-Araqiy 4: 36.

70


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 71

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Ya pili: “Hakika Shia hawajifichi katika kumchukia kila anayemfanyia uadui Ali (a.s.) kwani hakika amchukiaye Ali (a.s.) ni mnafiki kwa mujibu wa maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Ali! Hakupendi ila muumini na wala hakuchukii ila mnafiki.” Na hakika wanafiki watakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni, na tayari imeshathibiti kuwa baadhi kati ya waliokuwa na alama za usahaba walikuwa wakimchukia Ali (a.s.) na wakimtukana na hilo ni mashuhuri kwao: Bila shaka Mwenyezi Mungu anashuhudia hakika sisi hatuwapendi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, katika hilo hatumuhofii yeyote atakayechukia. Na bila shaka ni kuwa Muawiya na kundi lake walikuwa wakidhihirikiwa waziwazi na sifa ya kumchukia Ali (a.s.) na watu wa nyumba ya Mtukufu Mtume wote, na walimkabili kwa uadui na kutangaza vita juu yake. Kama Muawiya alivyotangaza na kufanya Sunna na akawafuatilia wafuasi wao kuanzia maswahaba hadi tabiina, na hivyo akawaonjesha kila aina ya maudhi na matatizo akawanywesha sumu na kuwauwa chini ya kila jiwe na changarawe, suala ambalo hatuna haja ya kulifafanua, ilihali matendo yake haiwezekani kuyanyamazia na wala hakuna njia ya kuyatafsiri kwa maana ya usahihi. Si uadilifu kusema: Hakika Muawiya ni mujtahid aliyeleta maana, ilihali ameacha sheria na kubatilisha ushahidi na ameuwa nafsi zilizo haramu kuziua, kawateka wanawake wa kiislamu na kuwatangaza kwenye masoko na kufunua miundi yao, hivyo yeyote mwenye muundi mkubwa hununuliwa kulingana na ukubwa wa muundi wake102. Na mengine mengi miongoni mwa matukio ya fedheha na ya huzuni. Huyu hapa Abu Al-Ghadiyyah Al-Juhni, alikuwa miongoni mwa maswahaba na miongoni mwa waliomsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akapokea kutoka kwake na yeye ni miongoni mwa wapokezi wa Hadithi: “Ewe Ammar litakuuwa kundi ovu.” Na yeye mwenyewe ndiye aliyemuuwa Ammar radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake. Watu walim102 Al-Istiabu 1: 157.

71


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 72

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu chukia kwa kutenda kosa hili na yeye mwenyewe akakiri kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa Motoni, na alikuwa akisema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu laiti Ammar angeuliwa na watu wa ardhini basi wangeingia Motoni.”103 Inakuwaje anatuhumiwa kuwa katoka ndani ya dini yule mwenye kujitenga na mtu muovu kama huyu ambaye yeye mwenyewe amekiri kuwa ni adui wa Mwenyezi Mungu, lakini baadhi ya wasimulizi wamemtafsiri vingine na kuwa yeye ni mujtahid aliyekosea na ni lazima kuwa na dhana nzuri na maswahaba.104 Sisi hatujui ni mantiki ipi hii inayopitisha kutupiliwa mbali hukumu na Kitabu kuhamwa kwa hoja ya kuwa na dhana nzuri na maswahaba na kunyamazia yale waliyoyatenda. Na je, inaruhusiwa kwetu kunyamazia matendo ya Basri na maangamizi yake? Pindi tu atakapokuwa na alama ya usahaba, ilihali yeye ndiye kiongozi wa jeshi la Muawiya na hakika alitenda makosa ambayo unyama wake bado historia haijauona mfano wake, mpaka wanawake wakamkana pindi alipoingia Yemen, akauwa wazee na watoto na kuteka wanawake. Mwanamke mmoja kutoka kabila la Kinda akamwambia: “Ewe mwana wa Artaah! Hivi mtawala hadumu ila kwa kuuwa watoto wadogo na wazee vikongwe na kung’oa rehema na kuwatendea vibaya ndugu wa damu, hakika yeye ni mtawala muovu.”105 Vipi iruhusiwe kwetu kunyamaza dhidi ya vitendo vya Basri na tuzibe masikio yetu dhidi ya sauti ya mama mfiwa ambaye sauti yake inasukuma mawimbi ya haki na kupeleka dhuluma aliyofanyiwa kwa wanaume waadilifu huku akiomba akiwa amechanganyikiwa hajui la kufanya?!

103 Usudul-Ghaba: 5 – 267. 104 Al-Isabah: 4 – 151. 105 Al-Kamil cha Ibnu Kathir 3: 195.

72


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 73

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu “Ewe ambaye umehisi kuhusu wanangu wawili wapendwa ambao wao ni sawa na nyota mbili zilizoachana pande mbili. “Ewe ambaye umehisi kuhusu wanangu wawili wapendwa ambao wao ni sikio langu na akili yangu, leo akili yangu imekwapuliwa. “Atakaye muonyesha mzazi wa kike aliyechanganyikiwa asiyejua cha kufanya juu ya watoto wadogo wawili waliodhalilika, kesho atapata malipo. “Niliambiwa habari za Basri na si kuamini waliyodai kutokana na uongo wao na kosa walilolitenda. “Naihurumia mishipa ya shingo za wanangu wapendwa iliyonolewa na kulainishwa na lile kosa linalotendwa.” Hii ni sauti inayopeleka maumivu moyoni na kijiti jichoni inatoka kwa mama mwenye huzuni kali naye ni mke wa Abdullah bin Abbas aliwakosa wanae wawili nao ni Qutham na Abdur-Rahman, aliwachukua Basri bin Artaah ilihali wakiwa bado wadogo, akawachinja mbele ya mama yao, basi akachanganyikiwa bila kujua la kufanya, hivyo akawa akija msimu huo na kusoma shairi hili bila kujua afanye nini.106 Hivyo sio haki kabisa kumtuhumu mwislamu kuwa ni zandiki na mpagani akichukia pindi anaposikia sauti yake na kunasibisha dhuluma kwa yule aliyewauwa wanae, eti kwa sababu tu kamtia dosari Muawiya, kwani mauaji yalifanyika kwa amri yake na yeye ni sahaba, na katika hilo ana ijtihadi inayokubalika au tafsiri sahihi, hivyo Muawiya aingie kwenye uwanja wa maisha na kutenda lolote atakalo mwenyewe.

106 Al-Istiabu 1: 156. Al-Kamil cha Ibnu Kathir 3: 195.

73


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 74

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu Bila shaka usahaba umewekewa ngome inayouzuia usihukumiwe na hivyo ukakingwa na kila hatari, na umwage damu na uuwe kwa kigezo cha dhana na tuhuma, mbele yake vizuizi vyote vimeondoka na vikwazo vyote vimeyayuka hivyo haumhusu ule utaratibu na hukumu zilizowekwa na sheria tukufu zenye wema kwa wanadamu na utaratibu wa maisha kwa sababu tu yeye ni sahaba na ana uhuru wa kufanya chochote ndani ya hukumu. Na laiti angekuwa na haki ya kufanya hivyo basi matendo yake yasingepingwa na maswahaba, na kinara wao ni sahaba mkubwa Abu Dharr Al-Ghaffar, bila shaka alitangaza waziwazi mbele ya kadamnasi upinzani wake dhidi ya mwenendo wa Muawiya na uendaji wake kinyume na dini. Pia Aisha alimpinga Muawiya kwa kitendo chake cha kumuua Hajar na wafuasi wake na akamkasirikia na akamkataza asiingie nyumbani kwake na wala hakukubali udhuru wake pale aliposema: “Hakika katika kuwaua kuna masilahi kwa umma na kuwaacha waendelee kuishi kuna uharibifu kwa umma.” Aisha akamwambia: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: “Kuna watu wataua kwa hoja za kitoto na Mwenyezi Mungu na watu wa mbinguni watawaghadhibikia.”107

MUHTASARI WA UCHAMBUZI Hakika laana ni suala lingine lenye maana tofauti na tusi na kashifa kilugha hata kisheria, na bila shaka laana ni dharura ya kiitikadi inayoimarisha maana ya mapenzi kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu na uadui kwa maadui wa Mwenyezi Mungu. Na hakika Qur’ani tukufu imeitumia kwa watu wa kitabu na mara nyingine kwa makafiri wote na mara ya tatu kwa 107 - Tarikh Ibnu Kathir 8: 55. Tazama Aslus-Shiah Wa-Usuliha cha marehemu Kashif Al-Ghatau.

74


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 75

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu wanafiki na mara ya nne kwa waisilamu wenye kutenda makosa ya kisheria yaliyo makubwa. Na hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitumia mara nyingi kwa ajili ya kundi la nne tu kwa waislamu kuliko makundi mengine, na maswahaba wana athari zilizomo ndani ya historia. Na laana inatumiwa kwa kundi la watu wenye sifa moja na kwa mtu binafsi, na hakika wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) hawalaani maswahaba wote kama walivyotuhumiwa kwa hilo, bali humlaani yule tu aliyelaaniwa na Mwenyezi Mungu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na kumlaani mtu binafsi kukiwa kunatokana na ijtihadi basi kwenyewe hakuingii kwenye mlango wa maasi achia mbali kumpeleka mtu kwenye ukafiri. Na hakika kuwakufurisha Shia kwa tuhuma ya kuwatukana maswahaba ni kitendo kisichokuwa na msingi wowote wa kisheria ndani ya Uislamu, bali kilitekelezwa na baadhi ya wanachuoni vibaraka wa watawala ili wajipendekeze kwa watawala na kuzua fitina kati ya waislamu. Mwisho wa dua zetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu.

75


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi 76

Page 76


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53.

Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto 77

Page 77


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78.

as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s)

78

Page 78


Hatukashifu bali tunalaani chk Lubumba Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:14 PM

Page 79

Maana ya Laana na Kutukana katika Qur’ani Tukufu

BACK COVER Shia wa sasa na wa zamani, wote wametuhumiwa kuwatukana masahaba na kuwalaani; na kwa ajili ya tuhuma hii wamepatwa na matatizo na machungu mengi baada ya kuhukumiwa kuwa wao ni makafiri. Jambo hili limefanya suala la laana na kulaani lifuatiliwe na watu wengi na wajiulize kuhusu ukweli halisi wa laana ndani ya sheria, hukumu yake na mipaka yake mbalimbali. Ewe msomaji mpendwa! Somo lililomo mikononi mwako ni jaribio makini katika mwelekeo huu ambalo ndani yake tunajaribu kuangazia macho maana ya kulaani kilugha (Kiarabu) na kwa mujibu wa Kitabu na Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na tutazame msimamo wa kambi mbili: Kambi ya Sunni na kambi ya Ahlul Bayt kuhusu suala hilo. Hayo yote ni kwa lengo la kutaka kufikia matokeo halisi katika suala hili, na muhimu zaidi ni kuchunguza ukweli wa tuhuma ya kuwatukana masahaba wote ambayo Shia wanatuhumiwa nayo. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

79


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.