Umaasumu wa Mitume

Page 1

Umaasumu wa Mitume (‘Ismatu ‘l-Anbiyaa’) FAIDA ZAKE NA LENGO LAKE

SEHEMU YA KWANZA

Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani

Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili


ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 427 - 66 - 6 Kimeandikwa na: Sheikh Ja’far Subhani Kimetarjumiwa na: Sheikh Harun Pingili Kimehaririwa na:

Hemedi Lubumba Selemani Kimepangwa katika Kompyuta na: Ukhti Pili Rajab Toleo la kwanza: Machi, 2008 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax:

+255 22 2127555

Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info


YALIYOMO Manabii na Mitume ndani ya Qur’an Tukufu.............................................2 Tafiti ya Ismah ina mafungamano na maisha...............................................4 Mwanzo wa kujitokeza kwa fikra ya Ismah...............................................10 Qur’an yaleta suala la Ismah......................................................................12 Ismah ya Nabii ndani ya Qur’ani Tukufu..................................................13 Kujadili dhima ya Ahmad Amin................................................................16 Ismah ni daraja ya upeo wa mbali kabisa wa takwa................................25 Ismah hutokana na elimu ya uhakika juu ya matokeo yamaasi................27 Roho ambaye huwa weka sawa mawalii..................................................33 Hivi Ismah ni kipaji cha kiungu au ni jambo la kujichumia......................35 Ismah ya kutumikiwa ni ukamilifu kwa aliyetumikiwa.............................40 Maneno ya Sayyid Murtaza...................................................................... 44 Daraja za Ismah na dalili zake...................................................................50 Hatua ya pili: Ismah ya Manabii dhidi ya maasi........................................70 Uthibitisho wa Mutadha............................................................................75 Kujibu swali lingine..................................................................................78 Qur’an yazungumzia Ismah ya Manabii dhidi ya maasi.........................79 Hoja ya wapingao Ismah...........................................................................92 Tafsiri batili za Aya..................................................................................118


NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako, ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kwa jina la “Ismatul Anbiya” sisi tumekiita “Kuhifadhiwa kwa Manabii” kilichoandikwa na Sheikh Ja’far Subhani. na tumekigawa katika sehemu tatu na hii uliyo nayo sasa ni sehemu ya kwanza ambayo tumeiita: Faida na Lengo Lake. Sehemu ya pili tumeiita: Majibu ya Aya Zenye Utata. Sehemu ya tatu tumeiita: Umaasumu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.). Suala la ismah ya Manabii ni nukta ambayo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wanachuoni na miongoni mwa madhehebu. Upande mmoja unasema Manabii ni binadamu ambao wamehifadhiwa kutokana na dhambi na makosa ya aina yoyote. Upande mwingine unasema hapana, Manabii wanaweza kukosea na kufanya dhambi. Upi ni ukweli; mwandishi ya kitabu hiki ambaye ni mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu analifafanua suala hili kwa urefu kwa kutumia dalili za kielimu, Qur’an na Sunna na kuhitimisha pasina shaka yoyote juu ya Umaasumu wa Mitme. Sisi tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu. Hivyo, tunakitoa katika lugha ya Kiswahili ili wasomaji wetu wa Kiswahili wapate kufaidika na kulielewa suala hili vilivyo na kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu Sheikh Harun Pingili, kwa kukubali juku-


mu hili la kukifanyia tarjuma kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.


F



Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

MANABII NA MITUME NDANI YA QUR’AN TUKUFU Kwa kweli mtizamo wa udadisi kuhusu ulimwengu, maisha, mwanadamu wathibitisha kuwa uumbaji kamwe haukuwa mchezo na bila faida yeyote, na kwamba mwanadamu hakuumbwa bila ya lengo na kusudio. Ukweli ni kwamba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ame muumba na amemleta kwenye ulimwengu huu wenye wasaa kwa lengo la hali ya juu la kiroho, na ili aufikiye ukamilifu wa kiroho uwezekanao. Qur’an Tukufu imeuelezea ukweli huu kwa ibara tofauti, amesema (s.w.t.):

Hatukuziumba mbingu na ardhi na vilivyo kati ya hivyo viwili bure (bila ya faida) hiyo ndio dhana ya waliokufuru, ole wao waliokufuru na (adhabu ya) moto. (Swad-27). Pia amesema (s.w.t.):

Je mumedhania tulikuumbeni kwa mzaha na kwamba ninyi hamtorudishwa kwetu!. (al-Mu-uminuun-115). Isipokuwa kulifikia lengo hilo litakiwalo kwahitajia mambo mawili:

2


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Utayarifu wa kimaumbile wa dhati umejificha ndani ya kuwepo kwa mwanadamu, wampeleka kwa msukumo wa ndani ya dhati yake kwenda akiuelekea ukamilifu. Viongozi wenye nguvu wenye elimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na waliotumwa na Yeye ili kumwongoza mwanadamu alifikiye lengo ambalo kwa ajili yake ameumbwa. Kwa hiyo endapo sababu mbili zimeafikiana, ya ndani na ya nje kumwongoza afikiye lengo litakiwalo, kutatimia. Na hili ni miogoni mwa mambo ambayo yashuhudiwayo na akili iliyo salama, na kitabu chenye hekima. Lakini kumuongoza mwanadamu kwenye ambalo manabii kwa ajili yake wametumwa si jambo rahisi liweze kutekelezwa na kila mwenye kuinuka na kutambaa. Isipokuwa mwanadamu awezaye kutekeleza hilo lazima awe mtu wa mfano kwa watu katika elimu, matendo, ni wajibu awe anasifika na sifa bora na kamilifu na zenye nguvu mno, na awe ametakasika yu mbali na kila uongo dosari na kila aina ya aibu, na katika utangulizi wa yote hayo ni wajibu awe mtendaji wa ayasemayo, mtekelezaji wa anayowaita watu kwa ajili yake, mwenye kuamrika na ayatoleayo amri, mwenye kujikataza na awakatazayo wengine, kama si hivyo maneno yake yata teleza mioyoni, kama vile ambavyo mvua itelezavyo kutoka jiwe gumu na wala lengo la kupelekwa manabii na Mitume halingethibiti, kwa sababu watu kulingana na tabia za kimaumbile huwaelemea watu wasifikao na sifa bora na wampenda miongoni mwao anayeambatanisha elimu na kazi, hali wakiwa kwa tabia zao kimaumbile huwachukia wanao kinzana na aina hii ya tabia miongoni mwa watu japo watu hao wawe kileleni katika nguvu za kifikra na utamu wa maneno.

Na hili ndilo ambalo limewafanya Waislamu waseme kuwa manabii na 3


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

mitume wa Mwenyezi Mungu ni wajibu wawe maasumu (wamehifadhika) hawatendi kosa, kuteleza, na kutenda dhambi, pia na maimamu – (a.s). Na hilo wamelitolea ushahidi kwa kitabu chenye hekima, na kwa hukumu ya akili iliyo salama ambayo kitabu kitukufu hakitengani nayo. Kwa minajil hiyo mas’ala ya ismah (kuhifadhika) yamechukuwa nafasi makhsusi katika vitabu vya elimu ya kalaamu-scholasticism- na tafsiyr. Wa hakiki wame kithirisha maneno kuhusu hilo, hata hivyo katika Waislamu kuna ambao wamekuwa na msimamo wa pekeyao hawaelezei ismah ya manabii.

TAFITI YA ISMAH INA MAFUNGAMANO NA MAISHA Kwa kweli utafiti kuhusu (Ismah) sio utafiti wa mas’ala iliyo kando na mafungamano ya maisha ya mwanadamu, hususan upande wa kiakili, bali ni miongoni mwa mambo ambayo yanaambatana kwa uthabiti na elimu na maisha ya Kiislamu ya wakati uliopo. Kwa kuwa utafiti kuhusu ismah ni utafiti kuhusu mambo ambayo yana chukuwa dhamana ya elimu hii, na uthabiti wake, zaidi ya hivyo ni utafiti unaochukuwa dhamana ya yale yanayoambatana na maisha yetu ya wakati uliopo pamoja na aliyoteremsha Mwenyezi Mungu miongoni mwa sheria, na aliyoyaacha Nabii wake mtukufu miongoni mwa Sunnah. Kulingana na hayo inakuwa miongoni mwa yanayopendeza kwa mkazo kabisa, bali ni miongoni mwa ambayo ni lazima kutiliwa maanani katika maisha ya manabii na sera zao, na kuzizingatia Aya zilizokuja kuhusiana na nafasi yao, zaidi ya hapo ni kuwa ina ainisha ufahamu wa kweli wa (ismah) na watilia mkazo mafungamano yake na usalama wa elimu ya kiis4


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

lamu ikiwa ni kutekeleza kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je hawaizingatii Quran” na kauli yake:

“Kitabu tumekuteremshia ili wazingatiye Aya zake na watiye akilini wenye akili” Hivyo basi mtizamo wa kitafiti kuhusu Aya zilizo kuja kuhusiana na hali ya manabii, pia visa visemwavyo kuwahusu kwa sura ya jumla, na Aya ambazo zarejea kwenye ismah yao ya kutofanya kosa, kuteleza, dhambi na maasi kwa sura makhsusi huzingatiwa kuwa ni ibada ya kimatendo ambayo mwanafikra mzingativu hupata thawabu kwa ajili yake. Lakini yasikitisha kuona baadhi ya waandishi wenye pupa wamechukuwa msimamo wa upinzani dhidi ya wanachuoni waliofanya utafiti kuhusu (ismah) ndani ya tafsir zao au vitabu vyao vya kiitikadi.Wasema katika hali ya kukanusha na kushambulia: “Hatujamsikia yeyote miongoni mwa maswahaba kuwa alimjadili Nabii kuhusu jinsi Adam alivyokula mti. Na eti ilikuwaje alimuasi Mola wake, wala hawakumjadili rasuli kuhusiana na Mtume mwingine mbali na Adam (a.s.) miongoni mwa manabii kwa mwelekeo huu ambao wameufanya walio kuja nyuma. Wallahi maswahaba hao hawakuwa wachache wa maarifa ya nafasi za manabii ukiwalinganisha na hao waliokuja nyuma wala hawakuwa wachache wa heshima na utukuzo wa hadhi zao kuliko hao wenye kujikalifisha yasiyo na manufaa kwao na wajiingizao kwenye mambo yasiyowahusu. Ama nyoyo ndwele, ni nyoyo za waliokuja nyuma ambao Mwenyezi Mungu amewafungulia mlango wa shetani ulio mpana wa fani za

5


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

mjadala, na wingi wa imesemwa, yasemekana, na malumbano ya matamko na kauli za Ah’lul-kitaabi miongoni mwa Mayahudi ambao ni watu huwachukia sana manabii, huwatweza, huwa taabisha, huwakufurisha na huwauwa.”1 Sisi hatutadhihirisha maoni yetu kuhusiana na maneno haya kwa kuwa ni duni na yana unyonge, kwa sababu iko wazi hali ya mwenye kuwasema wanachuoni wa kiislamu ambao Mwenyezi Mungu amewafanya kuwa mawakala wa kuuongoza umma wa kiislamu, kuwa wame athiriwa na fitna ya shetani, na ambaye amekufanya kuzingatia Aya za Kitabu kitukufu kuwa ni wahyi wa shetani na kufuata nyayo za Ahlul-kitabi miongoni mwa Mayahudi. Lakustaajabisha ni kwamba huyu mwandishi (asiyejulikana ) amekitoa kimoja tu miongoni mwa vikundi vya kiislamu kuwa wao wamelindwa wasipatwe na vitimbi vya shetani na ushawishi wake na fitna yake hao ni “Ahlul-hadith wenye kufuata athari, ambao wameziweka akili zao na rai zao chini ya hukumu ya yale aliyoleta Mtume (s.a.w.) ikiwa ni kushikamana na kishiko madhubuti na kamba thabiti”. Imefichika kwake kuwa mmoja katika waislamu haachani na Sunnah na kukiendea kitu kingine baada ya Qur’an Tukufu na kwamba kuikanusha Sunnah ni kukanusha unabii wa Nabii ambaye ni Nabii wa hitimisho baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na ju ya kizazi chake daima milele. Lakini maneno hapa yanahusika na kuipambanua (Hadithi) iliyo sahihi na isiyo sahihi, iliyozushwa na isiyozushwa. Kwa sababu historia hivi sasa inafichuwa kuwa Hadiithi zimeangukia kwenye matatizo mengi, kwani dhana hii ya Mungu kuwa na mwili na kumshabihisha Mungu (s.w.t.) na viumbe wake, hutegemea Hadithi kama hizi zilizosajiliwa ndani ya vitabu vya swihahi, sunani na masanid. 1. Kutoka Utangulizi(Ismatul-anbiya) cha Raziy kwa kalamu ya mwandishi asiyejulikana identity yake kimetolewa na Darul-matbuuatil jadiidah.

6


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Muongo hana kumbukumbu. Ninalodhani ni kuwa utangulizi huu umeandikwa kwa lengo makhsusi nalo ni kuteremsha chini daraja ya Ahlul bayt wa Mtume na maimamu wao ambao Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amewajibisha juu ya watu kuwapenda na amejaalia kuwapenda wao ndio ujira wa kuwafikishia risala aliposema: “Sema: Siwaombeni ujira kwa(ajili ya kazi) hii isipokuwa upendo kwa ndugu wa karibu�. 24:23 Kwa kweli mwandishi huyu (asiyejulikana) mara atambulisha kuwa Mayahudi ni watu wenye chuki sana na manabii na ni wenye kuwadharau sana..... mpaka mwisho wa aliyosema. Dharau hiyo inalazimu manabii kutokuwa na ismah kwa mtazamo wao, bali ni wenye kuraruwa heshima ya Mwenyezi Mungu. Na mara nyingine anawashabihisha na Mayahudi wale wafuatao athari za Ahlul- bayt, eti kwa sababu tu wao wanaithibitisha ismah kwa maimamu wao kama ambavyo Mayahudi wanathibitisha ismah kwa manabii kuonyesha heshima kwao na kuitukuza hadhi yao! Basi oh! wenye maoni! Mnasemaje kuhusu maelezo yenye kupingana waziwazi kama kama ya ibara mbil hizi. Ikiwa Mayahudi wapo hali ile aliyoieleza katika ibara ya mwanzo kuwa ni wenye chuki sana, dharau na uadui kwa manabii basi hawangeithibitisha ismah kwa manabii, ambayo ni miongoni mwa kipaji kitukufu mno cha kiungu apewacho mwana wa Adam. Na ikiwa Shia ni kama Mayahudi kuhusiana na kauli ya ismah basi nini maana ya kuwa Mayahudi ni wenye chuki sana, dharau na uadui kwa manabii!? Zaidi ya hayo ni kuwa, ni kwa dalili ipi Mayahudi wanahusishwa na usemi wa ismah! Bali wao kulingana na matamko ya Taurati wana dhana kinyume na dhana hiyo.

7


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Ili kuwapa hadhi manabii na kuwaheshimu, na kwenda bega kwa bega na kauli yake (s.w.t.): “Ili wazingatie....” tumeazimia kukusanya baadhi ya Aya zinazo husiana na ismah ya manabii na Mitume, zile ambazo zijulishazo ismah yao na zile ambazo zinazodhaniwa kinyume chake. Nasi twa jaribu kwa hilo kuziba pengo lionekanalo katika maktaba za kiislamu kwa sura iwezwayo kuguswa. Ingawaje kulikuwa na kundi la wanachuoni wa kiislamu wa hapo zamani mfano wa Sharif al-Murtadha (355-436 A.H.) Na al-Khatiiybu, al- Fakhru Raaziy (543-6006 A.H.) na wasiokuwa hao wawili waliitosheleza suala hii kwa utafiti na darasa, ila ni kuwa kila utunzi una vipambanuzi vyake, kama ambavyo kila mtungaji hulingana na zama zake na taaluma ya mazingira yake. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) atuhifadhi tusiteleze, na atupe tawfiki kwa alipendalo na aliridhialo. Qum—Al- hawza Al- ilmiyah Dhul Qaadah 1408 (A.H.) Jafar as-Sub’haniy.

8


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Ismah ya manabii ndani ya Qur’an Tukufu: Kwa kweli limetumika neno: (al-Ismah) ndani ya Qur’an Tukufu mara kumi na tatu katika Sura zake tofauti huku likiwa halina zaidi isipokuwa maana moja, nayo ni kujishika na kujizuia, hata likitumika maeneo tofauti lakini ni kwa kuizngatia maana hii. Ibn Farisi amesema: “(aswama) ina asili moja sahihi, yajulisha kujishika na kujizuia na kujilazimisha, na maana katika hayo yote ni maana moja. Miongoni mwa maana hiyo ni ile (al, ismatu) ambayo ni Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kumuhifadhi mja wake kwa kumuepusha na uovu uwezao kumkabili. Na litumikapo kwa upande wa mja mathalan: (iitaswamal abdu billaahi) amejihifadhi mja kwa Mwenyezi Mungu, ni pale ajizuwiapo. Na (is,ta,aswama): Amekimbilia. Na waarabu husema: (ii,taswamtu fulaanan) yaani nimemuandalia fulani kitu ana jihifadhi nacho kimlinde dhidi ya alicho kichuma kwa mkono wake, yaani anakimbilia na kushikamana nacho. 2 Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anawaamuru waumini wajihifadhi kwa kamba yake katika kauli yake:

“Na mujihifadhi kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala musi farikiane”. (Imran-103). Na maana yake ni kushikamana nayo na kuichukuwa kwa nguvu na uthabiti. Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ananakili kutoka kwa mke wa mfalme kauli yake: “Kwa kweli nilimshawishi kinyume na utashi wake akajihifadhi” (Yusuf-32).s Kwa hiyo neno hili limetumika katika Aya ya kwanza kwa maana ya Al-maqayiisu,Juz.4,,uk3 (Kutoka utangulizi (Ismatul ambiya) 2.

9


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kujishika na kujihifadhi, na katika Aya ya pili kwa maana ya kujizuia na kukataa na maana zote zinarejea kwenye maana moja. Kwa minajili hiyo twawaona waarabu huiita kamba ambayo hutumika kwa kufungia mizigo (al—Iswaam ) kwa sababu ina hifadhi na kuzuia mizigo isianguke na kutawanyika. Bw. Mufidu amesema: “Kwa kweli al ismah katika asili ya lugha ni kitu ambacho mtu amejihifadhi nacho katika vitu, inakuwa kama kwamba amejizuia nacho asiingiye kwenye jambo linalochukiza. Na miongoni mwayo kauli yao: (Iitaswama fulaanun bil’habli.-fulani amejihifadhi kwa kamba) Akijiziwia kwayo. Na kutokana na matumizi hayo milima mirefu imeitwa (al-Iswam) kwa sababu ya kuzuilika kwake nayo.3 Na ismah kutoka kwa Mwenyezi Mungu ni tawfiqi ambayo kwayo mwanaadamu anasalimika nayo kwa kuyaepuka anayoyachukia endapo atatekeleza utii. Na hivyo ni kama tumpapo kamba mtu anayezama ili aishike asalimike kwa hiyo yeye endapo ataishika na kujihifadhi nayo, huitwa kitu kile ismah kwake kwa kuwa alikishika na akahifadhika asizame, na lau kama asingehifadhika nacho kisingeitwa Ismah).3 Kwa kadiri itakavyokuwa makusudio ya maana ya ismah ni uhifadhi wa mtu na makosa, maasi, bali uhifadhi katika fikra na azma kwa hiyo maasumu wa moja kwa moja ni yule asiyekosea maishani mwake, na wala hamuasi Mwenyezi Mungu katika umri wake wala hataki kutenda maasi wala hafikirii kabisa kuasi.

MWANZO WA KUJITOKEZA KWA FIKRA YA ISMAH Kwa kweli vitabu vya theiolojia vya zamani na vya sasa vimejaa tafiti kuhusu ismah, ukweli wa maneno ni:Ni kujua mwanzo wa kujitokeza fikra 3. Awailul’maqalati, uk. 11 10


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

hii kati ya Waislamu, na je! tafiti hizi zimeanzia wapi na vipi walizindukana wanachuoni wa theiolojia kwenye asili hii? Hapana shaka kuwa wanazuoni wa kiyahudi sio walioanzisha fikra hii. Kwa sababu wao wanawaambatanisha manabii wao na maasi mengi, agano la kale linaelezea madhambi ya manabii baadhi yao yanafikia viwango vya madhambi makubwa, huenda kalamu ikaona haya kuyataja baadhi yao. Kwa mantiki hiyo basi, manabii ni waasi watenda makosa, kutokana na hali hiyo suala hili halikuanzishwa na wanazuoni wa kiyahudi. Naam wanazuoni wa kinaswara japokuwa wanamtakasa Masihi na kumweka kando na aina zote za aibu na dosari, lakini utakaso huu sio kwa kumzingatia Masihi akiwa mtu miongoni mwa binadamu ametumwa ili kumwongoza mwana wa Adam na kumwokowa, isipokuwa yeye kwao ni ( Mungu aliye ndani ya mwili wa mwanadamu) au yeye ni mmoja wa watatu (yaani mkusanyiko wa Mungu baba mwana na roho mtakatifu ). Hivyo basi haiwezekani wanachuoni wao wawe ndio waanzilishi wa suala hili katika tafiti za elimu ya theiolojia, kwa sababu maudhui ya ismah ni kwa ajili ya mwanadamu. Na Bw. Donaldson anasema kwamba: “Fikra ya ismah ya manabii katika Uislamu asili yake ni Madina na umuhimu wake uliofikia, na baada yake ukaendelea ndani ya (theiolojia- scholasticism) ya Shia, na wao ndio wa kwanza kufanya utafiti wa itikadi hii na kuwasifu nayo maimamu wao. Na yawezekana fikra hii ilijitokeza zama za As-Swadiq hali ikiwa hapajatajwa ismah kwa Ahlus-Sunnah ila katika karne ya tatu ya hijira baada ya kuwa al- Kulaini amekwishatunga kitabu chake (al—Kaafiy fiy usulidiyn) akaongelea sana maudhui ya ismah”. Na Bw. Donaldson anaeleza sababu kuwa: “Ili Shia wathibitishe madai ya maimamu mbele ya makhalifa wa kisunni wameidhihirisha itikadi ya 11


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

is’mah ya mitume kwa kuwa wao ni maimamu au viongozi.”4 Uchambuzi huu haukujengeka juu ya msingi thabiti bali ni miongoni mwa dhana na hekaya zilizobuniwa na utashi wa mtu na uadui wake kwa Uislamu na Waislamu kwanza, na pili kwa Shia na maimamu wao. Na hapa unapata kwa ukamilifu chanzo cha kujitokeza kwa fikra hii.

Qur’an yaleta suala la Ismah Kwa kweli ismah kwa maana ya uhifadhi wa kutofanya makosa na maasi bila kujali inamuhusu nani, ni suala lililokuja ndani ya Quran Tukufu, na hata Malaika waliokabidhiwa Jahannam wamesifiwa kwa maelezo haya, Al-lah (s.w.t.) amesema:

“(Juu yaJahannam) kuna Malaika wakali hawamuasi Mungu (kwa kufanya kinyume na) aliyowaamrisha na wanatenda waliyoamrishwa”.Tahrim-6 Katika kuuwekea mpaka ukweli wa maana ya ismah, uhalisia wake na kumzindua mtu mwenye kutafiti fikra hii na asili yake ndani ya Qur’an, basi mtu hawezi kulipata neno la wazi zaidi kuliko kauli yake Allah (s.w.t.):

“Hawamuasi Mungu aliyo wa amrisha na wanafanya wanayoamrishwa.” Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaielezea Qur’an Tukufu kwa kauli yake:

4. Aqiidatu Shi'a, kilichotungwa na mustashriq- orientalist- Donaldoson) uk. 328. 12


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Haijiwi na ubatilifu si mbele yake wala nyuma yake, ni uteremsho kutoka kwa mwenye hekima, mwenye himidi.” Fuswilat:42 Kama ambavyo anaisifu pia kwa kauli yake:

“Kwa kweli hii Quran yaongoza kwenye kile ambacho ni thabiti na yawabashiria waumini.” (al—Israa-9). Hakika sifa hizi zaelezea kuhifadhika kwa Qur’an mbali na kila kosa na upotovu. Na kwa mujibu huo ismah ikiwa na maana yake pana bila kujali ni nani anasifika kwa sifa hiyo ni suala lililozungumziwa na Qur’an tukufu na kuvuta mitazamo ya waisilamu bila ya kuhitaji kuichukua fikira hii toka kwa makuhani wa kiyahud na watawa wa kikristo. Ndiyo wasifika katika Aya hizi ingawaje ni Malaika au Qur’an Tukufu, hali ikiwa lizungumziwalo na wanazuoni wa theiolojia ni ismah ya manabii na maimamu, lakini tofauti hii ya maudhui haitii dosari kuwa Qur’an ndiyo mwanzilishi wa fikra hii, kwa sababu linalotakiwa ni kujua chanzo cha fikra hii, kisha kuendelea kwake kwa wanatheiolojia, na yatosha kuwa Qur’an imelileta suala hili ikiwazungumzia Malaika na Qur’an yenyewe. Maelezo haya yana thibitisha kuhifadhika kwa Qur’an dhidi ya kila aina ya kosa na upotovu.

Ismah ya Nabii ndani ya Quran tukufu Kwa kweli ismah ina daraja nne, Qur’an imechukuwa dhamana ya kuzibainisha daraja hizi katika nafasi za manabii kwa sura ya jumla, na katika nafasi ya Nabii mtukufu (s.a.w.), khususan, ubainifu wa daraja hizo utakujia kikamilifu na dalili zake za Qur’an. Ikiwa Qur’an ndiyo ya kwanza kuleta suala hili kwa daraja zake na dalili zake, basi itakuwaje sahihi isemwe kuwa Shia ndio wahusikao, na izin13


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

gatiwe kuwa wao ndio asili ya kuibuni fikra hii! Na ukiwa na shaka na tuliyoyasema humu ichunguze kauli yake (s.w.t.) kumhusu Nabii mtukufu vile alisifiavyo tamko lake tukufu kwa kauli yake:

“Hatamki kwa- hawaa- utashi wa nafsi yake isipokuwa ni wahyi hufunuliwa”.(Annajmu:3-4). Waona Aya hizi mbili kwa wazi zinaishiria kuwa Nabii hatamki kwa mujibu wa msukumo wa utashi wake binafsi, anategemea katika tamko lake wahyi ana kuwa mwenye kuhifadhika kwa kutoteleza katika ngazi ya uchukuwaji na upokeaji na ngazi ya ufikishajina ubainishaji. Zaidi ya hapo ni kuwa Aya za Qur’an zinausifu moyo wake na macho yake kuwa ni vitu viwili visivyokosea wala havipotoki wala havivuki mpaka aliposema (s.w.t.): “Moyo -wa Mtume(s.a.w)- haukukosea ulicho ona jicho halikupotoka wala kuona kisicho cha kweli.” Annajmu:11—17). Je ni sahihi baada ya Aya hizi za Qur’an, kuyasadiki aliyoyasema huyu mustash’riqi (Orientalist) myahudi au mustash’riqi mnaswara yale waliyo yadhania kuwa Shia ndio walioanza kuleta suala la ismah juu ya busati la mjadala, na kuwa ni matunda ya ukamilifu wa elimu ya theiolojia kwa Shia katika zama za Imam Swadiq (a.s.), hali twaona suala hili lina asili ndani ya Qur’an. Shia hawalaumiwi wakifuata nyayo za kitabu cha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) endapo wataeleza kuhusu manabii wake na Mitume wake yale ambayo ameeleza Mwenyezi Mungu wenyewe kuhusu manabii hao kitabuni mwake.

Ismah, kwa mtizamo wa Imam Ali(a.s.): Baadhi ya wamisri, mfano wa Ahmad Amin na waliokwenda mwendo wake wanashikilia kuwa Shia wamechukua njia yao kifikra kuhusu suala la uadilifu, ismah na mengine miongoni mwa fikra kutoka kwa Muutazila 14


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kwani wamesema: Kwa kweli Shia katika maswala mengi ya misingi ya dini {usulu-dini} wanasema kama usemi wa Muutazila, kwa kweli Shia wamesema kama walivyosema Muutazila kuwa sifa za Mwenyezi Mungu ni ileile dhati yake, na ya kuwa Qur’an ni kiumbe na wanakanusha (Alkalamunnafsiy), na kukanusha kumuona Mwenyezi Mungu kwa macho duniani na Akhera, kama ambavyo Shia wanaafikiana na Mutazila katika usemi wa “uzuri na ubaya ni vitu viwili vya kiakili” na uwezo wa mja na uchaguzi wake, na kwamba uovu hautoki kwake (s.w.t.) na kwamba matendo yake (s.w.t.) hutokea kwa sababu zenye lengo. Nimepata kukisoma kitabu Al-Yaqutu cha Abiy Is-haqah Ibrahim ambaye ni miongoni mwa wanatheiolojia wa Shia imamiyah wa zamani…5 basi nilikuwa kama nasoma kitabu miongoni mwa vitabu vya Muutazilah isipokuwa katika maswala machache, kama mlango wa mwisho katika uimamu na uimamu wa Imamu Ali na uimamu wa maimamu kumi na mmoja baada yake, lakini je! Nani amechukuwa kwa mwezake ! Ama baadhi ya Shia wanadhania kuwa Muutazila wamechukuwa kutoka kwao, na kwamba Waasilu bin Atwaa amesoma kwa Jafar As-Swadiq. Na mimi natilia uzito usemi kuwa Shia ndio ambao wamechukuwa taaluma yao kutoka kwa Muutazila. Na kuzaliwa kwa madh’habu ya I’itizali kwajulisha hilo. Na Zaidu bin Ali mkuu wa kikundi cha Shia Zaidiya amesoma kwa Waasilu, na Jafar As-Sadiq alikuwa anawasiliana na ammi yake Zaidu, Abul-Faraji anasema ndani ya kitabu Muqatilu twalibiyna: “Jafar bin Muhammad alikuwa anamshikia Zaidu bin Ali ngamia, na kumtandikia nguo zake juu ya mnyama wa safari6, hivyo endapo aliyoyasema 5. Ahmad Amiin amesema akitoa maelezo ya jumla hii: Nayo ni muswada (man-

uscript) hupatikana kwa nadra rafiki yangu Al-ustadhu Abu Abdillahi Azzanjaniy alinizawadiya hiyo: (manuscript). Ninasema:Kwa kweli kitabu hiki kimepigwa chapa mwishoni Iran kikiwa na sherehe ya Allamah Hiliy. 6. Muqatilu Twalibiina,uk93 15


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Shah’ristaniy na wengine yatakuwa sahihi kuwa Zaidu amesoma kwa Wasilu, basi haiingii akilini sana kuwa Wasilu asome kwa Jafar. Na walio wengi katika Muutazila walikuwa wanauukubali ushia, kwa hiyo ni dhahri kwa njia ya hao zimeingia usulu za Muutazila kwa Shia.7

KUJADILI DHANA YA AHMAD AMIN Aliyoyasema mwandishi wa kimisri ni ijitihadi kukabiliana na tamko la Muutazila wenyewe kuwa: Wamechukuwa misingi yao kutoka kwa Muhammad bin Al- Hanafia na kwa mwanawe Abu Hashim na hao wawili wamechukuwa (elimu yao) kutoka kwa Ali bin Abiy Twalib mzazi wao mtukufu. Baadhi ya matamko yao ni haya: Al-Ka’abiy amesema: “Yasemekana kuwa Muutazila na madh’hebu yao wana njia inayoungana na Nabii hali ikiwa hakuna yeyote miongoni mwa vikundi vya umma huu mfano wao, Na haiwezekani kwa mahasimu wao kuwakanusha, na kwa kweli Wasilu njia yake ni kwa Muhammad bin Ali bin Abiy Twalibi na mwanawe Abu Hashimu (Abdullah bin Muhammad bin Ali) na kwamba Muhammad amechukuwa kutoka kwa baba yake Ali na Ali amechukuwa kutoka kwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu.”8

Pia amesema: “Na Waasilu bin Atwaa alikuwa katika watu wa Madina aliyelelewa na Muhammad bin Ali bin Abi Twalib na alimuelimisha na alikuwa pamoja na mwanawe -Abu-Hashimu katika madarasa kisha alikuwa naye muda mrefu baada ya kifo cha baba yake, na imeelezwa kutoka kwa baadhi ya watu wa kale kuwa aliambiwa: “Vipi ilikuwa elimu ya Muhammad bin Ali?” Husemwa: “Endapo ukitaka kujua hilo basi angalia athari yake (Wasilu).” 7. Dhuhal’islamu,uk267-268. 8. 8.fadh'lul'I'itizal uk234 16


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kama hivyo wamesema kumhusu Amri bin Ubaidu kuwa naye amechukuwa kutoka kwa Abiy Hashimu p, na kadhi (Abduljabbar) amesema: “Ama Abu Hashimu Abdullah bin Muhammad bin Ali, lau elimu yake na ubora wake visingedhihiri isipokuwa kwa kiwango kile kilichodhihiri kutoka kwa Waasilu bin Atwaa ingetosha, na alikuwa anachukuwa elimu kutoka kwa baba yake, na Wasilu alikuwa kama kitabu alichokiweka Abu Hashimu, hivyo hivyo ndugu yake Ghiylanu bin Atwaa inasemekana kuwa yeye amechukuwa elimu kutoka kwa al-Hassan bin Muhammad bin alHanafiyah nduguye Abiy Hashimu.9 Na al-Jahidhu amesema: “Basi nani mfano wa Muhammad bin alHanafiyah na mwanawe Abu Hashim ambaye amesoma elimu ya Tawhid na uadilifu kiasi kwamba Muutazila wanasema: ‘Tumewashinda watu wote kwa sababu ya Abu Hashimu wa kwanza.” Ibn Abiy al-Hadid amesema: “Kwa hakika elimu iliyo bora ni elimu ya kiungu, kwa sababu ubora wa elimu watokana na ubora wa kijulikanwa chenyewe na kijulikanwa chake ni bora wa viwa, kwa mujibu huo imekuwa bora.” Na kutokana na maneno ya Ali (a.s.) amedondowa na kutoka kwake amenakili, ameanzia kutoka kwake na kwake ameishia. Kwa sababu Muutazila ambao wao ndio asili ya Tawhidu na uadilifu na mabingwa wa utafiti, kutoka kwao watu wamejifundisha fani hii. Muutazila ni wanafunzi wake, na swahaba wake, kwa kuwa mkubwa wao Waasilu bin Atwaa ni mwanafunzi wa Abiy Hashimu Abdullah bin Muhammad AlHanafiya na Abu Hashimu mwanafunzi wa baba yake na baba yake ni mwanafunzi wake . Ama Ashaira, wao wanahusiana na Abul, Hassan Ali bin Is’mail bin Abiy bashar al-Ash’ariy, naye ni mwanafunzi wa Abiy Ali Al-juba’iy, na Abu Aliy ni mmoja wa masheikh wa Muutazila, hivyo basi maashaira mwishowe wananasibika na ustadhi wa Muutazila na mwalimu wao naye 9. Fadhlul-Iitizal, uk 226 17


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ni Ali bin Abi Twalibi”.10 Na Bw. Murtadha amesema ndani ya Aamali yake: “Juwa kuwa asili ya Tawhidu na uadilifu vimechukuliwa kutoka kwenye maneno ya Kiongozi wa waumimini (a.s.) na hotuba zake, kwani hizo ndani yake kuna yasiyokuwa na ziyada wala lengo jingine nyuma yake. Na mwenye kuzingatia maneno yake yaliyopokewa kuhusu hilo , atajua kuwa yote waliyokithirisha wana theiolojia baada yake katika kuyahariri na kuyakusanya sio lingine bali ni ufafanuzi wa jumla na sherehe za misingi ile. Na imeelezwa kutoka kwa maimamu miongoni mwa watoto wake (a.s.) kuhusu hilo yasiyowezwa kuzingirwa kwa wingi. Apendaye kuelewa hayo na kuyatafuta kwenye madhanio yake atayapata mengi mno, ambayo baadhi yake ni ponyo kwa vifuwa vigonjwa na ni zalisho kwa akili tasa.11 Na allama Sayyed Mah’diy Ar-Ruhaniy amesema katika maoni yake kuhusiana na nadharia ya Ahmad Amin: “Kwa kweli Ahmad Amin amebabaisha maelekezo hayo na jibu hilo , ili ayakinishe uhusiano wa I’itizali na Muutazila mbali kwa Amirulmuuminin, wala hatujapata kumuona yeyote miongoni mwa Shia amesema kuwa Wasilu amesoma kwa Imam Swadiq kiasi kwamba akanushwe kuwa As-Swadiq alikuwa anamshikia ngamia mwanafunzi wa Wasilu, ambaye ni Zaidu, kwa hiyo kusoma kwa Swadiqu ni jambo lililo mbali.. Bali jinsi ya mawasiliano ya al-Mu’utazila na kiongozi wa waumini ni ile walioitaja wenyewe kulingana na nijuavyo, na kule tu kushika kwa Imamu As-Sadiq ngamia wa ami yake Zaidu hakujulishi kuwa As-Sadiq amesoma kwa ammi yake Zaidu. Ahmad Amin amefanya hivyo kwa msukumo wa utashi wa nafsi yake ambao ni maarufu kumhusu, na ulio dhahiri katika vitabu vyake, nao ni kumpokonya Ali (a.s.) yawezayo kuhusishwa naye miongoni mwa fadhila kwa kadiri iwezekanavyo. 10.Sherhi Ibn abiyl'Hadiid j.1-uk27 11. Udhdulfawaidi wa dawrulqalaidi, au Amaliy Al-murtadhwa, Juz.1,uk148 18


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Lakini kwa sura ya uhakiki wa kielimu, amefanya hayo ili kuwapambia watu, na hilo limefanyika baada ya kujitokeza sifa na semi zenye kuwapa hadhi Muutazila kutoka kwa wamoroko kuwa wao ni wanafikra huru. Nafsi ya Ahmad Amin hairuhusu watu kama hao wawe wanaungana na Ali katika misingi ya madh’habi yao na fikra yao, kwa ajili hiyo akababaisha maelekezo hayo kwa kukanusha na kughafilisha. Kama ambavyo amekanusha bila ya dalili kuhusika elimu ya Nahau na yeye, hali ikiwa Ibnu Nadiim amesema ndani ya al-faha’rist: “Wanachuoni wengi wanasema kuwa Nahau ameichukuwa Abul’aswadi kutoka kwa Kongozi wa waumini (a.s.).”12

Kurejea mwanzo Hebu turejee kwenye somo la kuwepo kwa asili ya ismah ya Nabii kwenye maneno ya Ali (a.s.) alipomsifu Nabii katika hotuba ijulikanayo kuwa ni hotuba ya al-Qaswi’ah, kwa kauli yake: “Kwa kweli Mwenyezi Mungu amemkutanisha- Nabii(s.a.w) - na Malaika mtukufu mno toka alipo acha ziwa anapita naye njia ya mwennendo bora, na tabia nzuri za ulimwengu usiku wake na mchana wake.”13 Na ishara iliyo kwenye hotuba hii ni ya hali ya juu kabisa na ya wazi ikiashiria kwenye ismah ya Nabii (s.a.w.) katika kauli na matendo na kuwa hasemi wala hatendi kosa na kwenda kombo, kwa kuwa aliyelelewa na Malaika mtukufu mno miongoni mwa Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) toka alipoacha ziwa, mpaka mwisho wa uhai wake mtukukufu, haachani na uhifadhi wa kutopotoka na kutotenda kosa, basi ataachana vipi na uhifadhi hali Malaika huyu yupo ambaye anapita naye njia ya mwenendo bora, na anamlea katika misingi ya tabia njema ya ulimwengu usiku wake na mchana wake!

12. Buhuthu Maa Ahlis-Sunnah Walsalfiyyah, Uk 108. 13. Nah,julbalaghah chapa ya Abduh Hotuba 187. 19


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na maasi sio kitu kingine ila ni kupita njia za dhambi na za tabia mbaya, na apitaye njia ya kwanza huwa ni mwenye kujiepusha kuipata njia ya pili. Kwa hakika Imamu Kiongozi wa waumini katika hotuba hii hamuelezei khususan Nabii, bali pia anaelezea kuwahusu ahali wa Nabii(s.a.w.) kwa kauli yake: “Wao ndio maisha ya elimu na umauti wa ujinga upole wao unakuhabarisheni elimu yao na dhahiri yao inakuhabarisheni hali yao ya ndani ukimya wao unakuhabarisheni hikma ya matamshi yao, hawa khalifu haki wala hawatofautiani ndanimwe. Wao ni nguzo za Uislamu na mapitio ya mshikamano. Kwa wao haki imerudi kwenye kiwango chake na batili imetoweka kutoka mahali pake na ulimi wake umekatika kwenye maoteo yake. Wameitia akilini dini utiyaji akilini wa kuelewa na kuieleza sio utiaji akilini wa kusikia na kuieleza.”14 Hebu chunguza maneno haya, na yazingatiye kwa makini je wapata neno ambalo ni wazi zaidi katika kujulisha kuhifadhika kwao mbali na dhambi na kuzuilika kwao kutenda makosa kuliko kauli yake: “Hawaendi kombo mbali na haki, wala hawatofautiani humo.”kwa kauli wala kwa kitendo, kama ambavyo wengine wana tofautiana humo miongoni mwa vikundi, na wanamadh’habu. Miongoni mwao kuna ambao ana kuwa na kauli mbiliau zaidi katika suala moja , na miongoni mwao kuna asemaye kauli baadae ana ikana, na miongoni mwao kuna ambaye ana kuwa na rai katika usulu dini baadaye huikanusha na kuitupilia mbali. Imamu ana waeleza Ahali wa Nabii kwa kauli yake: “Wameitia akilini dini, na wameujua utambuzi wa aliye fahamu kitu kiusahihi.” Yaani wameielewa dini na wameihifadhi, wameizingira, sio kama wanavyoitia akilini watu wengine kwa kusikia na kuieleza. Kwa jumla usemi wake (a.s.) “Hawaendi kombo mbali na haki.” ni dalili ya ismah ya kutotenda maasi. Na usemi wake “Wameitia akilini dini utiya14.Nahjul,balaghah chapa ya Abduh-Al-khutbah: 187. 20


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ji akilini wa kuelewa na kuieleza.” ni dalili ya kuhifadhika kwao kwa maana ya kutotenda makosa na salama ya kuifahamu kwao dini na kuielewa kwao. Na Imamu hatosheki katika kubainisha ismah ya kizazi cha Mtukufu Mtume kwa maneno haya mawili, bali anaelezea kuhusu waja wapendwa mno wa Mwenyezi Mungu kwake kwa ibara na jumla zinazoafikiana na ismah na zalingana nayo, asema: “Mwenyezi Mungu amemsaidia binafsi, ameijua huzuni, na ameivaa hofu, kwa hiyo taa ya uongofu ikaangaza moyoni mwake, na akaandaa masurufu kwa ajili ya siku atakayofika huko, amejisogezea binafsi la mbali, amemleta mshari karibu kwa kuzingatia akaona, alikumbusha na alikithirisha, alipoza kiu kwa maji baridi ambayo upatikanaji wake ulimuia rahisi akanywa na kukata kiu, alipita njia mpya, ameyavua mavazi ya matamanio, na amejiweka kando na wasiwasi ila wasiwasi mmoja tu amekuwa nao peke yake. Kwa hiyo ametoka nje ya sifa ya upofu, na kushirikiana na watu wanaofuata utashi wa nafsi na amekuwa miongoni mwa funguo za milango ya uongofu, na vifungio vya milango ya maangamio, ameiona njia yake na ameshika njia yake na amejua alama zake, ….ameshikamana na kishiko kilicho madhubuti mno, na kamba ilio imara zaidi, kwa hiyo yu katika yakini mfano wa mwanga wa jua amejiweka binafsi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika mambo ya hali ya juu sana, miongoni mwa subira ya kila limfikalo, na kulirejesha kila tawi kwenye asili yake. Yeye ni taa ya giza, muondoaji wa upofu mfumbuzi wa yaliyojifumba, mzuiaji wa utata kiongozi wa jangwani, anasema na kufahamika, ananya maza na abaki salama, amekuwa mukh’lisu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu akamuengua, kwa hiyo yeye ni mahali pa dini yake, na ni vigingi vya ardhi yake, amejilazimisha binafsi uadilifu, kwa hiyo ukawa uadilifu wake wa kwanza kujiondolea tamaa ya binafsi, anaieleza haki na kuitendea kazi…, 21


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

wala dhana ila aikusudia, amekidhibiti kitabu hatamu yake kwa hiyo yeye ni kiongozi wake na Imamu wake…, na huteremkia mahali pake.”15 Sioni, yeyote atakayeizingatia hotuba hii na kuzichunguza ibara zake na jumla zake, ila atakuwa na yakini kuwa msifika wa sifa hizi yuko kilele cha juu cha ismah. Je wadhania nafsini mwako asiyekuwa na lolote limshughulishalo isipokuwa moja tu nalo ni kusimama kwenye mipaka ya kisheria, na ambaye binafsi amejilazimisha uadilifu, na kujiondolea hawaa nafsini mwake, asiwe maasumu kwa kutotenda dhambi, na kuzuilika na upotovu, na vipi – asiwe hivyo—hali akiwa ameidhibiti Qur’an hatamu yake, yeye ni kiongozi wake na Imamu wake, anahalalisha ilipohalalisha na aiteremsha ilipoteremkia. Ibn Abil’hadidi amesema: “Kwa kweli kutoka ndani ya maneno haya maswahaba wake wamechukuwa elimu ya twariqa na ukweli, nayo ni kuiweka wazi hali ya Aarifu, na nafasi yake kwa Mwenyezi Mungu, na Ir’fani ni daraja ya heshima ya hali ya juu kabisa, heshima yake yalingana na unabii, na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humuambatisha nayo yule inayemkurubisha kwake katika viumbe wake. Amesema pia: “Hakika ya sifa hizi na sharti na madaha alizozitaja katika kufafanuwa hali ya Aarif anajikusudia binafsi, nayo ni miongoni mwa maneno yenye dhahiri na batini, kwa hiyo dhahiri yake anafafanuwa hali ya Aarifu kwa jumla, na batini yake anafafanuwa hali ya Aarifu maalumu naye ni yeye mwenyewe (a.s.).” Kisha Ibn Abiy Al-hadid amezitafsiri sifa hizi na sharti moja baada ya 15. Nahjul,balaghah chapa ya Abduh-Al-khutbah: 83.

22


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

nyingine, mpaka ameifikia sharti ya kumi na sita,16 na atakayekuelewa malengo ya hotuba hii na airejelee na nyingine miongoni mwa sherehe. Hii ndio misingi ya suala hili katika Kitabu na Sunnah, ndiyo kwa hakika wanatheiolojia ndio ambao wameliwekea anuwani suala la ismah na kuliweka katikati ya Uislamu, kwa hiyo Shia na Muutazila wanaitikadi ismah kwa kufuata kauli kadhaa na ufafanuzi mbalimbali kwa mujibu wa vikundi vyao, huku kila kikundi kikitoa dalili kuthibitisha madai yake. Haiwezekani kukanusha kuwa mjadala uliojiri kati ya Imamu Ali bin Musa Ar-ridhaa (a.s.) na watu wenye makala miongoni mwa vikundi vya Kiislamu umeipa suala hili nafasi makhsusi, na jeraha kubwa, Imamu Aridhaa (a.s.) amebatilisha hoja za wapinzani na dalili zao walizozitoa ili kukanusha ismah ya manabii wote kwa ujumla wao na Nabii mtukufu (s.a.w.). Na kama si kuhofia kurefusha tungeleta baadhi ya mijadala hiyo iliyojiri kati ya Imamu (a.s.) na wanasemi hizo miongoni mwa vikundi vya Kiislamu, na endapo utataka kujua zaidi hilo basi rejea Biharul-anwari.17 Na mwishowe tutarejea kwenye tafsiri ya baadhi ya Aya ambazo wapinzani wanazitumia kukanusha ismah ya manabii (a.s.).

Nini hasa ukweli wa ismah ? Ismah imetambulishwa na wanatheiolojia kwa jumla kuwa ni nguvu imzuiayo mtu kufanya maasi na kuingia makosani.18 Al-Fadhilu al-Miq’dadu ameitambulisha kwa kauli yake: “Ismah ni jamala, Mwenyezi Mungu humfanyia mukalafu kiasi kwamba baada ya hivyo hatokuwa na sababu ya kuacha utii wala kutenda maasi hali akiwa na uwezo wa kufanya 16. Sharhu Ibnu Abil Hadid, Juz 6, Uk 367 - 380. 17.Buharulanwar, Juz.11,uk72-85. 18.Al-miizanu, juz.2, uk142 chapa ya Teheran. 23


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

hivyo, na hupatikana utaratibu wa jamala hii kwa kupata kipaji kinachomzuia kuyaendea maovu na kuasi, zaidi ya hapo ni elimu juu ya thawabu za utii na kuhifadhika dhidi ya adhabu, huku akioogopa malipizi ya kuacha yaliyo bora...”19 Na amesema katika shar’hul’mawaqifi ndani ya kududio la sita kuhusu ukweli wa ismah : “Nayo kwetu kulingana na inavyolazimiana na misingi yetu ni kuviegemeza vitu vyote kwa mtendaji mwenye hiyari toka mwanzo.20 Kisha alisema: “ Nayo (kwa wenye hekima) kulingana na kauli waliyofikia kuwa ni kuwajibika na kuzingatiya utayarifu kwa ajili ya uwezo (kipaji kinachozuwia uovu na hupatikana). Sifa hii ya nafsini kuanzia (elimu ya kemeo la maasi na sifa nzuri za utii) yenyewe hukemea dhidi ya maasi na hushawishi utii...”21 Na ninasema: Tafsiyri hii ya ismah kutoka kwa Ashaira ni ya ajabu kulingana na misingi yao, baada ya hivyo je inafaa ismah ihesabike kuwa ni heshima na kuacha dhambi kuwe ni ubora! Na Maana ya Tawhidu katika kuumba sio kuondoa taathira kutoka kwenye sababu zingine, na tumefafanuwa hali hii katika juzuu ya kwanza ndani ya kitabu (Mafahimul Quran) kwenye utafiti wa sehemu hii ya tawhiid chunguza. Kisha amesema ndani ya Sharhul’muwafiq: (na kaumu wamesema) “Ismah huwa ni jambo makhsusi ndani ya nafsi ya mtu au mwili wake kwa ajili yake huziwilika kupatikana dhambi kwake. Yamkosowa (yaani kauli hii) kwa kuwa lau ingekuwa kupatikana kwa dhambi kama hivyo (yaani kwazuilika) basi hangestahiki sifa njema kwa tendo hilo - (yaani kwa kuacha dhambi) kwa kuwa hapana sifa njema wala thawabu kwa kuacha 19. Irshadu Twalibiina ila nahjilmustarshidiina,uk301-302 20. Biharul’anwar.Jalada.11.uk.72.-85. 21. Ibtalu nahjul’baatili nukuu ya Dalailu swidqi.J.1:uk.370-371. 24


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ambalo haliwezekani kwa kuwa halipo chini ya hiyari.�22 Nasema: Ikiwa ukweli wa ismah maana yake ni nguvu inayozuia kutenda maasi na kuingia katika makosa, kama walivyo arifisha wanatheiolojia kwa hiyo maneno hapa yanajitokeza katika aina mbili: Ya kwanza: Ismah dhidi ya maasi. Ya pilii: Ismah dhidi ya makosa. Na ili kuweka wazi hali ya nafasi mbili hizi kwa kutolea dalili na uthibitisho ni wajibu ujadiliwe ukweli wa ismah kabla ya kitu chochote. Ukweli wa ismah wa kutotenda maasi warejea kwenye mojawapo ya mambo matatu bila ziada japokuwa haizuiliki kujumuika pamoja.

1-Ismah ni daraja ya upeo wa mbali kabisa wa takwa Marejeo ya ismah ni takwa bali ni daraja yake ya juu kabisa. Ipatikanapo takwa na kujulikana hutambulika na kusifika ismah.Wala hapana shaka kuwa takwa ni hali ya nafsani inayomuhifadhi mtu asitende mambo mengi miongoni mwa maovu na maasi. Hali hiyo ikifikia upeo wake yamuhifadhi mtu kabisa kutenda matendo yote maovu, na matendo yote ya lawama, zaidi ya hayo humuhifadhi mtu kwa kiasi hata cha kutofikiri kufanya maasi, kwa hiyo mtu ambaye ni maasumu sio yule asiyetenda maasi tu bali ni yule ambaye fikra yake haizungukii hata chembe kwenye kutenda uovu. Kwa hakika ismah ni nguvu ya kiroho iliyojikita nafsini ina athari yake makhsusi kama zilivyo nguvu zingine za kiroho kama vile, ushujaa, utawa, ukarimu, hivyo mtu akiwa shujaa na jasiri, mtoaji, mpaji, msafi maishani 22. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 281. 25


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

mwake, hupenda kutenda mambo matukufu, hujiepusha na yale ya upuuzi. Anakuwa makini kwa yote hayo, hafanyi kinyume na athari ya vipaji hivyo kama vile kuwa mwoga, kutokuwa shujaa, kuwa bakhili, mchoyo, mbaya, mwovu, na wala haitoonekana athari ya hayo maishani mwake. Hali ni hiyo hiyo kuhusu ismah, endapo mtu ataifikia daraja ya mbali ya takwa, hali hiyo ikachukuwa nafasi nafsini mwake na hapo maishani mwake mtu hufikia kiwango ambacho haionwi athari ya maasi, ukiukaji na kuthubutu kuasi‌ na uwanja wake huwa safi bila ya maasi. Ama mtu ataifikiaje daraja hii na sababu zipi zitamuwezesha hali hii, hilo ni shauri lingine tutalirejelea kwenye mijadala ya hapo baadaye. Na ikiwa ismah ni aina ya takwa na ni daraja yake ya juu, basi waweza kuigawa ismah sehemu mbili: Ismah ya moja kwa moja na ismah kwa kiwango fulani. Kwa hiyo ismah ya moja kwa moja ingawaje yahusika na tabaka makhsusi la watu lakini Ismah ya kiwango fulani inawaenea watu wengi bila tofauti kati ya mawalii wa Mwenyezi Mungu na wengine. Kwa sababu mtu mtukufu ambaye kuwepo kwake si kuchache kati yetu, hata akiwa anatenda baadhi ya maasi lakini yuajiepusha na baadhi yake ujiepushaji kamili kiasi kwamba haimjii fikirani mwake sembuse kuyatenda, kwa mfano mtu aheshimiwaye hatembei utupu wazi mitaani na njiani hata kama atashawishiwa vipi na watu wengine, kama ambavyo watu wengi hawaibi wala kunyanganya kitu chochote sawa kiwe miongoni mwa vitu rahisi au ghali. Kama ambavyo hawathubutu kuwaua watu wasio na hatia au kujiuwa wao wenyewe binafsi japo wapewe malipo ya mali kiwango kikubwa, wala haipo nafsini mwao misukumo na hima ya kutenda matendo kama haya maovu. Kwa sababu misukumo kama hiyo na chombezo hizo huwa zinarudishwa nyuma na takwa walizojipamba nazo watu hao, kwa ajili hiyo wamekuwa kando na mbali na matendo hayo mabaya kiasi kwamba hawayafikirii wala hayagongi nafsi zao kabisa. 26


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na ismah kwa kiwango fulani tuliyo itambuwa inaikaribia ismah ya moja kwa moja ndani ya fahamu zetu, na endapo hali hiyo ya nafsini-inayo zuiamtu itafikia ukali wa kiwango cha juu na daraja yake ya nguvu kiasi cha kumziwia kutenda maovu yote, atakuwa maasumu wa moja kwa moja kama ambavyo mtu katika sehemu ile ya kwanza huwa ma’asumu wa kiwango fulani. Kwa jumla: Endapo misukumo ya ukiukaji na ya maasi na sababu zimpelekazo mtu kuhalifu zitadhibitiwa na mtu na zikafungwa na zikawa zinamchukiza kwa sababu tu ya hali hiyo kukita basi hapo mtu huwa maasumu kamili mwenye kutakasika dhidi ya kila aibu na dosari.

2-Ismah hutokana na elimu ya uhakika juu ya matokeo ya maasi Umetambuwa nadharia ya kwanza kuhusu ukweli wa ismah na kwamba nayo ni: Daraja ya juu ya takwa, ila tu kuna nadharia nyingine kuhusu ukweli wake, ambao haupingani na nadharia ya kwanza, na yaweza ikahesabika kuwa miongoni mwa sababu ya kuthibiti kwa daraja ya juu ya takwa ambayo kwayo tumeijua ismah na sababu ya kuundika kwake nafsini. Ukweli wa nadharia hii maana yake ni: (kuwepo kwa elimu ya mkato yenye uyakini wa matokeo mabaya ya maasi na madhambi) elimu ya mkato haiyumbi, wala haiingiwi na shaka wala haipatwi na wasiwasi. Nayo ni elimu ya mtu kufikia daraja ambayo kwayo anaweza katika maumbile haya kugusa matokeo ya lazima ya matendo na athari zake katika ulimwengu mwingine na malipizi yake huko, na anakuwa katika kiwango cha kudiriki bali kuona daraja za watu wa peponi na tabaka za watu wa motoni. Na elimu hii ya mkato ndiyo iondoayo pazia iliopo kati ya mtu na matokeo ya matendo, na hapo mtu huwa kielelezo cha kauli yake (s.w.t.) “Lahasha lau mungejua ujuzi wa yakini mungeiona jahiim.� (Atakathur-5-6). 27


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na mwenye elimu hii ndiye yule ambaye Imamu Ali (a.s.) anamueleza kwa kauli yake: “Wao na Pepo ni kama ambaye ameiona, wao humo ni wenye kuneemeka. Na wao na moto ni sawa na ambaye ameuona,wao humo ni wenye kuadhibiwa.”23 Basi elimu ifikiapo daraja hii ya kufichuwa yamzuia mtu kuthubutu kutenda maasi na kufanya madhambi, si hivyo tu bali fikra yake haiyazungukii. Amesema ndani ya shar’hul’muwafiq, kuhusu ukweli wa ismah: “Hupatikana sifa hii ndani ya nafsi kuanzia (elimu ya kujua) aibu ya maasi na (kutambua) mema ya utii) kwani hiyo ni mkaripiaji wa maasi na muwitaji wa kwenye utii (na inathibiti), na sifa hii huimarika katika kwao kwa kuufatilia wahyi (kwa amri) inayopelekea kwenye yapasayo kufanywa na kwa makatazo yenye kukemea yasiyopaswa.”24 Na ili kuweka wazi taathira ya elimu hii katika kumfanya mtu awe maasumu wa kutotenda dhambi twaleta mfano: Bila shaka mtu akiafiki kuwa ndani ya nyaya za umeme kuna nguvu iwezayo kuuwa mtu, endapo ataugusa bila ya kiziwizi kiasi inakuwa kugusa na umauti hakuna kizuizi. Mtu atajizuia nafsi yake kugusa nyaya hizo, na kuzisogelea karibu bila ya kizuizi. Huu ni mfano wa tabibu mjuzi wa matokeo mabaya ya maradhi na athari ya virusi, kwani yeye akijua kuwa maji ameoga humo aliyepatwa na ukoma au mbalanga au kifua kikuu, hangekunywa na kuoga humo na kuyagusa hata awe na haja ya kiwango kipi juu ya maji hayo, hiyo ni kwa sababu ya kujua kwake 23.Nahjulbalaghah,chapa ya Abduh,Jalada.2,hotuba N0-188.uk187. 24. Sharhulmuwafiq, Juz.8,Uk 281.

28


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

yatakayomtokea miongoni mwa hatari kwa kunywa kwake, kuoga au kuyagusa. Na mtu kamili akiwa anatambuwa yaliyo nyuma ya maumbile haya na akajua matokeo ya matendo yatakavyokuwa na kwa macho akaziona che chem za barzakh zabadilisha hazina zilizowekwa miongoni mwa dhahabu na fedha na kuwa moto uliookwa, na kwazo zinachomwa paji za nyuso za waliozihodhi, mbavu zao na migongo yao, bila shaka atajiziwia kuhodhi mali na kutozitumia katika njia ya Mwenyezi Mungu. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:

“Siku ambayo zitapashwa moto-ndani ya Jahannam-kisha zitabandikwa juu ya vipaji vya nyuso zao na pande za miili yao na migongo yao–huku wakiambiwa-: hizi ni zile- dhahabu - mulikuwa mukizihodhi, kwa ajili yenu, hebu onjeni mulizokuwa mukizi hodhi” Atawbah-35-36). Maana iliyo dhahiri ya kauli yake (s.w.t.): “Hizi ni zile- dhahabu mulikuwa mukizihodhi, kwa ajili yenu” ni kwamba moto ambao vitachomwa nao vipaji vyao vya uso vya waliohodhi mali hapa duniani kwa ajili yao tu binafsi, pande zao za miili na migongo yao, si moto mwingine ni ile ile dhahabu, na fedha, lakini katika hali ya kuwepo kwake katika sura ya Akhera kwa kuwa dhahabu na fedha zina sura mbili tofauti ya kuwepo kwake katika limwengu mbili, duniani na akhera, hivyo basi hii miili ya kimadini, hudhihiri katika ulimwengu wa dunia, katika sura ya dhahabu na fedha, na katika ulimwengu wa akhera katika sura ya moto uliokolezwa kwa waliozitumia kwa uovu.

29


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kwa hiyo mtu wa kawaida anapoyagusa haya madini yaliyohodhiwajapokuwa hawezi kuhisi joto lake wala hauoni moto humo wala muwako wake, hiyo ni kwa sababu anapougusa anakosa hisia zinazowiana na kuudiriki moto wa ulimwengu wa Akhera na joto lake, kwa mfano mtu aliye kamili atamiliki hisia hizi pamoja na hisia zingine za kawaida zilizobaki na akadiriki kwa aina makhsusi sura nyingine ya hizi dhahabu, nayo ni ile sura yake ya moto na ya mwako wake basi angejiepusha nazo, kama anavyojiepusha na moto wa kidunia, hangethubutu kuzikusanya na kuzihodhi.

Na maelezo haya yana maanisha kuwa elimu ina daraja yenye nguvu imara yamzuia mtu asiingie katika maasi na dhambi na wala hashindwi na matamanio na silika. Jamaludini al—Miqdadu bin Abdillahi al—Asadiy al—Suriy al—, Hilliy amesema ndani ya kitabu chake cha maana (Lawamiul’Ilahiyah): Na baadhi yao wana maneno mazuri yenye kujumuisha hapa wamesema: “Ismah ni udhibiti wa nafsi wamzuia mwenye kusifika nao kutenda ya ovyo hali akiwa na uwezo wa kuyatenda (ya ovyo), na udhibiti huu wasimama juu ya elimu juu ya ubaya wa maasi na ubora wa utii. Kwa sababu utawa upatikanapo ndani ya nafsi hasa, ukiongezewa elimu iliyo kamili ya yaliyo ndani ya maasi miongoni mwa mahangaiko, na ile hali njema iliyomo ndani ya utii. Basi hapo elimu hiyo huwa sababu ya kuimarika Ismah ndani ya nafsi na huwa kipajidhibiti.”25 Na anasema Al-Allamah Atab tabaiy katika wazo hili: “Kwa kweli nguvu inayoitwa kuwa ni nguvu ya ismah ni sababu ya utambuzi wa kielimu usioshindwa kamwe, lau 25. Lawamiul’Ilahiyah.uk.170. 30


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ingekuwa mfano wa ambao tuutambuao miongoni mwa aina za utambuzi na idraki, ingeingiliwa na uhalifu, na kwa taathira yake mtu angeyumba baadhi ya nyakati, hivyo basi elimu hii si katika aina ya elimu zingine na idiraki zitambulikanazo, ambazo huchumwa na kufundishika. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameishiria ndani ya maagizo yake ambayo aliyafanya mahsusi kwa Nabii wake kwa kauli yake:

“Na amekuteremshia kitabu na hekima na amekufundisha ambayo ulikuwa huyajui.� (Nisaa:113). Na huu ni usemi mahsusi hatuufahamu fahamu ya uhakika; kwa kuwa hatuna onjo lake katika uwanja huu.26 Naye (Q.s) ana ishiriria jinsi mahsusi ya elimu na utambuzi ambao tumeufafanuwa ilipokuja kuhusu hazina na athari zake. 3- Kutambua utukufu wa Mola, ukamilifu wake na uzuri wake Kwa hakia hapa kuna nadharia ya tatu katika kubainisha ukweli wa ismah kiini chake charejea kwenye ukweli wa mja kuutambuwa utukufu wa muumba na kumpenda na juhudi yake kubwa ya kumtambua na kumpenda kwake sana kutamzuia kufanya ambayo yanakwenda kinyume na ridhaa yake (s.w.t.). Nadharia hii ni kama nadharia ya pili haipingani na nadharia ya kwanza ambayo tuliifasiri kuwa ismah: Ni daraja ya juu kabisa ya takwa, ile hali ya mja kuhisi utukufu wa Muumba, kumpenda sana na kumjua kwa kina 26. Al-Mizan, Juz 5, Uk 81.

31


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

cha mwisho kabisa, huwa ni moja ya sababu za kufikia kiwango hicho cha takwa. Aina hii ya utambuzi haipatikani isipokuwa kwa walio kamili katika maarifa ya kiungu waliofikia vilele vyake vya juu kabisa. Mwanadamu akimjua Muumba wake ujuzi kamili uliyo mwepesi, na akatambuwa mahali pa ukamilifu wa kweli, uzuri wake na utukufu wake, atajikuta nafsini mwake ana mvuto kuelekea ukweli, na kujiangika kwa namna makhsusi kiasi kwamba hawezi badilisha ridhaa yake na chochote, hivyo basi, ukamilifu huu wa kweli aufikiapo mtu mjuzi basi huchochea nafsini mwake moto wa shauku na mahaba, na humsukuma asitakekingine, wala huwa hapendi isipokuwa utii wa amri yake na kutekeleza kama alivyokataza, na huwa achukia kila linalokwenda kinyume na amri yake na radhi zake na huwa ni jambo baya na lakuchukiza sana kwa mtizamo wake na hapo mtu huwa amehifadhika dhidi ya kutenda kinyume, huwa mbali na maasi, kiasi kwamba haingizi katika utii wa Mola wake kitu, na hilo ndilo analoliashiria Imamu Ali bin Abi Twalib (a.s.) kwa kauli yake: “Sijakuabudu kwa kuogopa moto wako wala kwa tamaa ya pepo yako, bali nimekukuta mstahiki wa ibada.�27 Nadharia hizi tatu au hii nadharia moja iliyo tofauti katika ubainisho na kukiri yadhihirisha kuwa ismah ni nguvu ndani ya nafsi ina muhifadhi mtu asiingiye ndani ya maasi, na ismah sio jambo liko nje ya dhati ya mtu aliye kamili na utambulisho wake wa nje. Ndiyo aina tatu hizi za uchambuzi wa ukweli wa ismah, zote zarejea kwenye ismah ya kuhifadhika dhidi ya maasi na ukiukaji, hilo liko wazi kwa mwenye kuizingatia. Ama ismah ya kuhifadhika wakati wa kuupokea wahyi na ya kuhifadhika wakati wa kuufikisha kwa watu, au ismah ya kuhifadhika dhidi ya makosa katika mambo ya maisha ya mtu binafsi au maisha ya kijamii, Ismah ya namna hiyo hapana budi itazamwe kwa sura nyingine mbali na sura hizi tatu kama ambavyo ubainifu wake utakuijia pindi utakapofanywa mjadala wa ngazi ya pili, yaani wa ismah ya kuhi27. Hadithi maarufu. 32


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

fadhika dhidi ya kukosea na kuchanganyikiwa. Muhimu ni kujadili kuhusu ngazi ya kwanza na kwa ajili hiyo ndio maana tulitanguliza maneno kuihusu. Naam, kuna riwaya nyingi zinabainisha wazi kuwa, kuna (Roho) anaye wahifadhi manabii na Mitume wasitumbukiye kwenye maangamizi, na makosa, ubainifu wake wakuujia:

Roho ambaye huwa weka sawa mawalii Imiilezwa Abu Baswiru amesema: “Nilimuuliza Aba Abdillahi (a.s.):kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu tabaraka wa ta’ala :

“Kama hivi kwa amri yetu tumekuletea ufununuo haukuwa unajua kitabu ni nini wala imani.” (Ashura-52.) Akasema: “Ni Kiumbe miongoni mwa viumbe wa Mwenyezi Mungu mtukufu ni mkubwa mno kuliko Jibril na Mikail alikwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu akimpa habari na kumuweka sawa naye yu pamoja na maimamu wa baada yake.”28 Na riwaya hii japokuwa dhahiri yake haina mafungamano na Aya hii kwa kuwa wahyi huwa unaambatana na mafuhumu na matamko, sio na viini na miili, kwa hiyo Malaika ambaye mkubwa kuliko Jibrilu na Mikailu wahyi hauwezi kuambatana naye awe yeye ndiye anayefunuliwa, yeye huambatana na kutumwa na mfano wake, hana mafungamano na mlango wa maasi bali yeye hurejea kwenye uwekaji sawa katika kuupokea wahyi na kuufikisha kwa watu, na kuwahifadhi wasikosee kwa sura ya moja kwa moja. 28. Al-kaafii, Juz 1. Uk 272, mlango wa Roho awapaye nguvu Maimam 33


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na ya kuwa kuna riwaya zinajulisha kuwa Roho hizi ambazozinawaongezea nguvu manabii haziko nje ya dhati yao. Huyu hapa Jaabiru Al-Jaafiy anaeleza kutoka kwa Imamu Swadiq katika kuitafsiiri kauli yake Mwenyezi Mungu: “Na nyinyi mtakuwa namna tatu. Basi watu wenye heri, watakuwa namna gani wenye heri. Na watu wenye shari, watakuwa namna gani wenye shari. Waliotangulia ndio waliotangulia. Hao ndio watakaokaribishwa.” (Al-waqiah-6-11) Kwa hiyo Waliotangulia wao ni Mitume wa Mwenyezi Mungu, na watu mahsusi katika viumbe wake. Amewafanyia Roho watano. Amewaongezea nguvu kwa Roho mtakatifu, kwake wamevitambuwa vitu. Amewaongezea nguvu kwa roho ya imani, kwake wamemwogopa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Amewaongezea nguvu kwa roho ya nguvu, kwake wameweza kumtii Mwenyezi Mungu. Amewaongezea nguvu kwa roho ya matamanio, kwake wametamani utii wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na wakachukia kumuasi yeye. Na akawawekea roho ya uwanda ambao kupitia kwake watu waenda na waja.29 Wala haifichiki kuwa Roho hawa wanne hawako nje ya dhati zao, wala si mbali hata huyu wa tano ambaye ni Roho mtakatifu kutokuwa nje ya dhati zao. Hivyo makusudio yake ni kuwa: Nafsi zao ziko katika ukamilifu wa kiwango ambacho wanavijua vitu kwa hakika yake kama vilivyo. Sheikh Swaleh Al—Mazandaraniy katika kuwatafsiri hawa Roho watano amesema: “Mwenyezi Mwenyezi Mungu kwa hekima ya hali ya juu na maslahi kamili amejaalia ndani ya Mitume na watu mahsusi, Roho wa tano ili kuwalinda wasifanye makosa na kuwafanya wawe kamili kwa elimu na matendo ili kauli yao iwe ya kweli, na thabiti, na kuwafuata wao ni uon29.Al-kaafii, Jalada.1,uk262. Babu(ar ruhu latiy yusadidu bihal’aimata). 34


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

gofu na yakini, ili wengine wasiwe na hoja mbele ya Mwenyezi Mungu siku ya Kiyama, na yawezekana makusudio ya roho hapa ni nafsi.30 Kadiri itakavyokuwa riwaya hizi ambazo zinashuhudia kuwawekwa sawa manabii kwa njia ya Roho, aidha zaweza kuwa zinarejea kwenye kuwaweka sawa wakati wa kuupokea wahyi, au yarejea kwenye kuwaweka sawa wasikosee katika ahkami na maudhui, na hayo yote yapo nje ya wigo wa mjadala huu, bali maneno yapo katika kuwahifadhi wasifanye maasi.

Hivi Ismah ni kipaji cha kiungu au ni jambo la kujichumia? Umekwishajua ukweli wa (ismah) na sababu ambazo hulazimu mtu kuhihadhika dhidi ya kuangukia ndani ya mtego wa maasi, na maangamizi ya ukaidi na ukiukaji, ila tu hapa kuna swali muhimu, ambalo ni wajibu lijibiwe nalo ni: Ismah bila kujali tafsiri yake kuwa ni daraja ya juu ya takwa, au kuwa ni elimu ya kata shauri juu ya matokeo mabaya ya dhambi na maasi, au kuwa ni utambuzi wa utukufu wa Mola, uzuri wake na enzi yake, kadiri vyovyote vile itakavyotafsiriwa bado yenyewe ni ukamilifu wa nafsi ulio na athari makhsusi. Hapo ndipo yapaswa iulizwe kuwa je! Ukamilifu huu ni kipaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa waja wake walio na ikhlasi, au ni jambo mtu hulipata kwa kulichuma? Ambalo ni dhahiri katika maneno ya wanatheiolojia ni kuwa: Yenyewe ni kipaji miongoni mwa vipaji vya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) huwafadhili awatakao katika waja wake baada ya kuwepo kwa ardhi nzuri inayo ruhusu na ustahiki uhalalilishao kupewa. Shekh al—Mufiidu amesema: “Ismah ni ufadhili kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa amjuaye kuwa atashikamana na Ismah yake.”31 Na ibara hii 30. Pambizoni mwa Usulul Kafiy, Uk 136, chapa ya zamani. 31.Sharhu Aqaidu As-Suduqu, Uk. 16. 35


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

inajulisha kuwa ufadhili wa Ismah kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni jambo liko nje ya wigo wa hiari, ila tu kuitendea kazi na kufaidika nayo kupo upande wa mja na ndani ya wigo wa utashi wake, kwa hiyo ana hiari kujiambatanisha nayo na abaki maasumu mbali na maasi, kama ambavyo ana hiari pia ya kutojiambatanisha na Ismah hiyo.” Pia amesema: “Na ismah kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni Tawfiki ambayo kwayo mja husalimika na anayoyachukia pindi akitenda utii.”32 Na Bw. Murtadha amesema ndani ya kitabu chake: al-Aamalu, kuwa: “Ismah, ni tawfiki ya Mwenyezi Mungu ambayo aifanyayo, na hapo mja huchagua kujizuwia dhidi ya kutenda uovu.” Allama Hilliy amenukuu kutoka kwa baadhi ya wanatheiolojia wa kiislamu kuwa wameifasiri ismah kuwa ni fadhila isegezayo kwenye utii, ambayo Mwenyezi Mungu humtendea mja, ambayo hujua fika akiwa nayo hatotenda maasi. Kwa sharti tu fadhila hiyo isimpelekee kukosa hiari. Na imenukuliwa kutoka kwa baadhi yao kuwa: Ismah ni fadhila ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humfanyia mwenye nayo kiasi kwamba hato kuwa na msukumo wa kuacha utii na kufanya maasi. Baada ya hapo amefasiri sababu za fadhila hii kuwa ni mambo manne.33 Na amesema Bw. Jamaludiini Mikdadi bin Abdillahi ambaye ni mashuhuri kwa al—Fadhlu as-Suyuriy al-Hilliy, aliye kufa mwaka 826 A.H. katika kitabu chake cha maana (al-Awamiu al-Ilahiyah fil’mabahithil’kalamiyah) “Wamesema watu wetu na walioafikiana nao miongoni mwa al-Adliyah kuwa: Ismah ni fadhila aifanyayo kwa mukallafu kwa kiwango ambacho kwake maasi yanazuwilika kutokea kwa kukosekana msukumo wake, na kuwepo kwa kinacho zuia japokuwa uwezo wake upo.” 32. Awailul-Maqalati, Uk 11. 33.Kashful-Muradi, Uk 228, chapa ya Swida. 36


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Baadaye amenukuu kutoka kwa Ashairah kuwa yenyewe ni(yaani ismah): Uwezo wa kufanya utii na kuto kuwa na uwezo wa kufanya maasi, amesema ndani ya Sharhulmawaqifi: (Kundi lime sema): Ismah ni jambo mahsusi ndani ya nafsi ya mtu au mwilini mwake, kutokana na jambo hilo inazuwilika kutenda dhambi.” Na kauli hii yampinga, (kwa kuwa lauingekuwa kutokea kwa dhambi kunazuilika, basi mtu asingestahiki sifa kwa kule kuacha kutenda dhambi) kwa sababu hakuna sifa wala thawabu kwa ajili ya kuacha kisichowezekana kwa kuwa hakiko chini ya hiari ya mtu mwenyewe.34 Itakufikia kuwa Ismah haipingani na uwezo, na lengo la kunakili kauli ya Ashaira hapa ni kuthibitisha kule kuafikiana kwa wasemao kuwa ismah ni kipaji. Kama alivyo nukuu al-Fadhlu al-Mikdadi as-Suyuriy- kutoka kwa baadhi ya wanafalsafa kuwa mtu maasumu Mwenyezi Mungu amemuumba umbo safi, na udongo ulio safi na hali inayokubali na akamtnuku akili yenye nguvu na fikra iliyo sawa, na akamzidishia uwezo wa ziada, kwa hiyo yeye ni mwenye nguvu kwa kule kumfanya wa pekee kwa kutekeleza wajibu na kujiweka kando na mabaya, na kwa kuzielekea malakuti za mbinguni, na kuupa kisogo ulimwengu wenye pande kwa hiyo nafsi iamrishayo mabaya imetekwa na imeshindishwa chini ya uwezo wa nafsi yenye akili.35. Na Allama Tabatabaiy amesema ndani ya tafsiri yake kauli yake (s.w.t.):

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu watu wa nyumba na kukutakaseni kabisa.” (Al—ahzab-33). 34. Sharhul-Mawaqif, Juz 8. Uk 281. 35.Al-Lawamiu Al-Ilahiyah, Uk 169. 37


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Kwa kweli Mwenyezi Mungu utashi wake waendelea anakufanyieni kipaji cha pekee cha ismah kwa kuwaondolea ninyi Ahlul-bayt itikadi batili na athari ya matendo maovu, na kuleta lile liondoalo athari ya hayo kwenu, nalo ni Ismah.”36 Na maneno mengine mbali na hayo ambayo yanabainisha wazi kuwa Ismah ni kipaji chake (s.w.t.) kwa waja wake walio na ikhlasi. Katika Aya za Qur’an kuna ishara zinazojulisha hayo mfano wa kauli yake (s.w.t.)

“Wakumbuke waja wetu Ibrahim na Ishaqah na Yaqubu wenye nguvu na uoni kwa hakika tumewachaguwa kwa jambo makhsusi (ambalo ni) kupiga mbiu ya siku ya mwisho. Hakika wao kwetu ni wateuliwa wema. Na mkumbuke Ismail na Al—yasaa na Dhul-kiflu wote miongoni mwa watu wema.” (Swad,45-48). Na kauli yake (s.w.t.) kuwahusu Baniy Israil na wakusudiwa ni manabii wao na Mitume wao:

“Na hakika tuliwachaguwa kwa ujuzi kuliko walimwengu. Na tukawapa katika mambo ambayo ndani yake mna neema zilizo dhahiri.” (Adukhan 32-33).

36.Al-Mizanu, Juz 16, Uk 331. 38


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kauli yake: “Hakika wao kwetu ni wateuliwa wema” na kauli yake “Na hakika tuliwachaguwa kwa ujuzi kuliko walimwengu” yajulisha kuwa unabii, Ismah, na upaji wa Aya kwa wahusika ni miongoni mwa vipaji vya Mwenyezi Mungu( (s.w.t.) kwa manabii, na kwa wale wanaoshika nafasi zao miongoni mwa mawasii. Basi maadamu ismah ni suala la kiungu na ni kipaji miongoni mwa vipaji vyake (s.w.t.) basi hapo hoja mbili zajitokeza amabazo ni lazima zijibiwe nazo ni: 1. Kama ismah itakuwa kipaji kutoka kwa Mwenyezi Mungu ambacho ni fadhila yake mwenyewe na kuwafikia Mitume wake na mawasii wake basi hauwi ni ukamilifu na jambo la kujifaharisha kwa ambaye ni maasumu kiasi kwamba awe anastahiki kutukuzwa na kuhimidiwa. Kwani sifa yoyote iliyo nje ya hiari ya mtu mfano wa usafi wa lulu, haistahili kuhimidiwa na kutukuzwa kwa sababu himidi na sifa njema huwa sahihi kwa ajili ya kitendo cha hiari, ama ambacho kiko nje ya wigo wa hiari haitokuwa sahihi asifiwe mwenye nayo. Kwa sababu yeye na mtu mwingine hatofautiani naye, katika nyanja hizi wako sawa, kwa kuwa lau ukamilifu ule unge pewa mtu mwingine angekuwa mfano wake. 2. Na kama ismah inamuhifadhi mtu asiwe maasini basi mtu ambaye ni maasumu hawezi kutenda maasi na kujihusisha na madhambi, na hatimaye katika hali hiyo hawezi kustahiki himidi yeyote kwa kutotenda maasi wala thawabu kwa kuwa hana hiari. Tofauti iliyopo kati ya hoja mbili hizi iko wazi kabisa, kwa kuwa hoja ya kwanza yarejea kwenye ile hali ya kitendo cha kupewa ismah chenyewe binafsi kuwa fahari miongoni mwa fahari za maasumu, kwa kuwa ikiwa ni kipaji cha kiungu haingekuwa sahihi izingatiwe kuwa ni ukamilifu kwa maasumu. Kinyume na hoja ya pili, kwani hii ya pili ina mwelekeo wa kuizingatia kuwa ismah inamwondolea maasumu uwezo wa kutenda maasi, hivyo basi kuacha kwake kutenda maasi hakuhesabiki kuwa ni 39


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ukamilifu wala hakuwi sababu ya kustahiki thawabu. Hoja hizi mbili ndio nzito mno katika mlango wa ismah. Lifuatalo ni jibu la hoja zote mbili.

Ismah ya kutunukiwa ni ukamilifu kwa aliyetunukiwa Kwa kweli ismah ya kiungu haikabidhiwi kwa mtu ila baada ya kuwepo utayarifu mzuri unaofaa kwa huyu maasumu mwenyewe ambaye yabidi apewe kipaji hicho. Ama swali kuwa: Je, ni utayarifu upi mzuri unaofaa ambao inapasa awe nao ili apewe? Hili liko nje ya mjadala huu, lakini twasema kwa sura ya jumla: Utayarifu huo upo katika aina mbili: Aina moja iko nje ya hiari ya mtu na aina ya pili iko ndani ya wigo wa hiari ya mtu na utashi wake mwenyewe. Ama aina ya kwanza, ni ile hali ya utayarifu na ardhi nzuri inayohamishiwa kwa Nabii kutoka kwa baba zake na babu zake kwa njia ya kurithi, kwani watoto kama vile wanavyorithi mali ya mababa na utajiri wao, pia wanarithi sifa zao za dhahiri na za ndani, kwa mujibu huo utona mtoto anafanana na baba au ammi yake, au mama au mjomba, na imekuja katika methai, : “Mtoto wa halali hufanana na ammi yake au mama, au mjomba.� Kwa hali hiyo roho njema au mbaya zinahamia kwa watoto kwa njia ya kurithi, ndio utaona mtoto wa shujaa hutokea kuwa shujaa, na mtoto wa mwoga huwa mwoga na nyinginezo miongoni mwa sifa za kimwili na kiroho. Hivyo basi manabii kama inavyotuonyesha historia walikuwa wanazaliwa kutoka kwenye nyumba zenye maadili mema zenye asili ya matukufu na makamilifu, kwa hiyo huendelea kuhamia yale makamilifu na matukufu ya kiroho, kizazi mpaka kizazi na huendelea kukamilika mpaka sifa zile zichukuwe nafasi yake ya kimwili ndani ya nafsi ya Nabii na yeye azaliwe na roho njema yenye utayarifu mkubwa tayari kwa kupata vipaji vya kiun40


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

gu. Naam, kurithi sio sababu pekee ya kupatikana utayarifu huo, kuna sababu zingine zawajibisha kuwepo utayarifu huo ndani ya nafsi za manabii, nayo ni sababu za malezi, kwa hiyo ukamilifu na ubora upatikanao kwenye mazingira yao uhamia kwa njia ya malezi kwa watoto. Kwa hiyo chini ya vipengele hivi viwili “kurithi na cha malezi” tuna waona wengi miongoni mwa wana wa nyumba hizo huwa wenye imani, uaminifu, werevu, uelewa, na si kwa lingine ila ni kwa sababu wanaoishi ndani ya mazingira hayo na kuinukia humo hupata kiasi kikubwa cha ukamilifu huo kwa njia hizi mbili, kwa mujibu huo, huu ukamilfu wa kiroho una mazingira mazuri yanayopelekea vipaji hivi vya kiungu kutunukiwa mahali panapolingana navyo. Miongoni mwa vipaji hivyo ni ismah na unabii. Ndiyo kuna sababu zingine za kujipatia hali muwafaka, nayo ipo kwenye uwezo wa mwanadamu na iko chini ya uchaguzi wake na uwezo wake. Ifuatayo ni baadhi ya mifano yake: 1. Kwa kweli maisha ya manabii toka kuzaliwa kwao mpaka wakati wa kutumwa kwao yamejaa mapambano ya mtu na nafsi yake mwenyewe na ya kijamii, walikuwa wanapambana na nafsi iamrishayo uovu mapambano makali, na walikuwa wanajiadabisha wenyewe na jamii yao maadabisho mema. Huyu hapa Yusufu mkweli (a.s) aliipiga mweleka nafsi yake na akapambana nayo na hatimaye akaifunga hatamu huku akiithabiti kabisa pindi aliposhawishiwa na mwanamke ambaye Yusufu alikuwa nyumbani mwake: “Alifunga milango na akasema: Njoo basi” akajibu kwa kukataa na kujiweka mbali na tendo hilo kwa kusema:

“Mwenyezi Mungu apishe mbali kwa kweli bwana wangu ambaye ndiye aliyeyafanya makazi yangu yawe muwafaka kwa kweli wadhal41


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

imu hawatofaulu.”(12:22:Yusuf) Na huyu hapa Musa yeye ni Kalimullah alipokwenda kwenye nchii ya Madiyan aliwakuta wanawake wawili wamebaki nyuma hawanyweshi wanyama wao huku wakiwa wamesimama mbali na kisima ambacho hutumika kunyweshea wanyama, basi akawaendea na kuwauliza: Vipi? Wakasema: Hatuwezi kunywesha mpaka watoke wachungaji na baba yetu ni mzee sana. Hapo aliharakisha kuwaondolea shida yao, na wala fikra zake hazikwenda kwenye wazo lolote lingine, aliwanyweshea kisha aka elekea kivulini huku akisema:

“Oh! Mola wangu kwa kweli mimi kheri yeyote uniteremshiayo nina haja nayo sana”.Al-Qaswas:28-24 Hivyo hivyo katika kisa kingine cha Nabii wa Mwenyezi Mungu Musa (a.s.) alipomuhami mwisraeli dhidi ya mkibti mchokozi katika kauli yake:

“Oh! Mola wangu kwa vile ulinineemesha sitokuwa msaidizi wa waovu.”(Al-qaswas:17) Kuna ushahidi mwingi wa kihistoria kuhusu mapambano ya manabii na kutekeleza kwao wajibu wao wakati wa ujana wao mpaka zama za kutumwa kwao ambako kumeelezwa na vitabu vya mbinguni na kunakiliwa na vitabu vya visa vya manabii na historia ya mwanadamu. Hivyo basi sababu hizi, ambazo baadhi yake zaingia chini ya utashi wa mtu na baadhi ziko nje ya wigo wa uwezo wa mtu na hiari yake, zime fanya ipatikane hali muwafaka, ardhi nzuri, na utayarifu mwema wa wao kutunukiwa sifa ya ismah na kuchaguliwa kwa tunu hiyo tukufu. Kwa hali hiyo ismah inakuwa ni fahari kwa Nabii na ya faa kumtukuza nayo huyu 42


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Nabii na kumuheshimu na kumsifu. Na ukipenda utasema: Kwa kweli Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliziangalia dhamira zao na niya zao na hali yao ya baadaye, na vilevile hali yao itakavyokuwa, na akawajua kuwa wao ni dhati takatifu, lau watapewa kipaji hicho watajisaidia kwacho katika kutekeleza utii na kuacha maasi kwa uhuru na kwa hiari. Elimu hii yatosha kurekibishia tunu hili juu yao kinyume na ajulikanaye kuwa hali yake ni kinyume na hivyo. Allamah Tabatabai anasema: “Kwa hakika Allah mtukufu amewaumba baadhi ya waja wake kwa unyoofu wa kimaumbile, na umbo la wastani, kwa hiyo waliinukia mwanzo kabisa wakiwa na akili, uongofu, udiriki uliyo sahihi, nafsi safi, na nyoyo salama, kwa hiyo kwa neema ya ikhlaswi wakapata waliyoyapata wengine kwa sababu tu ya usafi wa kimaumbile na usalama wa nafsi kwa njia ya juhudi binafsi na ya kuchuma. Bali wakapata hali ya juu sana kuliko hiyo kwa sababu ya usafi wa dhati zao na kuto chafuka na uchafu wenye kuzuia kuipata daraja ya juu na nafsi ya juu. Na dhahiri ni kuwa hao ndio wale wenyekutakaswa kwa ajli ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa istilahi ya Qur’an, nao ni manabii na maimamu. Na Qur’an imetamka kuwa Mwenyezi Mungu amewachaguwa, yaani ame wakusanya kwa ajili yake na kuwatakasa kwa ajili yake wawe karibu naye. Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

“Na tuliwachaguwa na tuliwaongoza kwenye njia iliyonyooka”. (AlAnaam:87) Na amesema:

43


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Yeye ndiye aliye kuchaguweni, wala haku wafanyieni taabu ndani ya dini.”(Al-hajj:78)”37 Ibara hii kutoka kwa Allamah Tabatabai yaashiria sehemu ya pili nayo ni hali muwafaka iliyo nje ya hiari ya manabii isipokuwa tu kuna mambo yaliyo ndani ya uwanja wa hiari yao kama ulivyokwishajua. Hivyo yote yanatoa ufaaji wa kutunukiwa tunu hii ya kimungu ndani ya nafsi hizo takatifu.

Maneno ya Sayyid Murtaza Kwa hakika Sayyid Murtaza ana maneno katika kujibu swali hili, hapa tunaleta tamko lenyewe: “Endapo itasemwa ikiwa tafsiri ya ismah ni hiyo muliyoisema, basi kwa nini Mwenyezi Mungu asingewahifadhi mukalafina wote, na wakafanya kwa mujibu wake wayachaguwayo kwake kujizuia na maovu? Tungesema: Kila ambaye Mwenyezi Mungu anamjua kuwa ana wema ambaye atachaguwa kujizuia dhidi ya mabaya, hapana budi atamfanyia wema japokuwa si Nabii wala si Imamu, kwa sababu taklifu hupelekea kufanya fadhila kama sehemu nyingi zinavyoonyesha hilo, isipokuwa ni kuwa haizuiliki kuwepo Mukallafu ambaye hajulikani kama endapo atafanya kitu atachaguwa kujizuwia dhidi ya baya. Hivyo mukallafu huyu anakuwa hana ismah ijulikanayo wala fadhila. Kumkalifisha asiyekuwa na fadhila ni uzuri wala si ubaya, kwani ubaya ni kule kuzuia fadhila kwa yule mwenye fadhila huku taklifi ikithibiti kwake.”38. Lipatikanalo katika maelezo yake ni: Kigezo cha kutunukiwa kipaji hiki ni ile elimu yake (s.w.t.) ya hali ya mtu mmoja mmoja kuhusu hali yake ya baadaye, hivyo basi kila ambaye (s.w.t.) ajua lau angetunukiwa sifa ya 37. Al-Mizan, Juz 11, Uk 177. 38. Amaliy Al-Murtadha, Juz 2, Uk 347 - 348, uhakiki wa Abul Fadhli Ibrahim. 44


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ismah angechaguwa kujizuia dhidi ya mabaya, basi hutunukiwa ismah, japo asiwe Nabii au Imamu. Na ambaye anamjua kuwa hata kama atatunukiwa kipaji hicho hatochaguwa kujizuia dhidi ya maovu, basi hatunukiwi ismah kwa kuwa hana sifa ya kufaa kutunukiwa na yeye si mahali pa Ismah. Kwa minajili hiyo sifa ya ismah ni kipaji cha kiungu hutunukiwa mtu ambaye hali yake inajulikana kuwa atanufaika nayo kwa kuacha mabaya kwa uhuru na hiari. Kwa ajili hiyo yahesabika kuwa ni fahari inayofaa kupongezwa na kuheshimiwa, na si lazima maasumu awe Nabii au Imamu, bali kila ambaye atanufaika nayo katika njia ya kupata radhi zake (s.w.t.) hutunukiwa. Mpaka hapa jibu la swali la kwanza limetimia na limebaki jibu la swali la pili. Lifuatalo ni jibu lake.

Je, hivi Ismah yapokonya hiari? Huenda ikadhaniwa kuwa mtu maasumu hawezi kutenda maasi na kufanya madhambi kwa hiyo Ismah inapokonya uwezo na hiari kutoka kwa mwenye nayo, kwa mujibu huo kuacha kuasi hakuhesabiwi kuwa ni utukufu, na kwa ajili hii Sayyid Murtadha anasema: “Nini ukweli wa ismah ambayo yaaminiwa ni lazima iwepo kwa manabii na maimamu (a.s.)? Je, ni maana ilazimishayo utii na kuzuia uasi, au ni maana ifananayo na hiari. Endapo itakuwa ni maana ilazimishayo utii na ikatazayo maasi basi vipi yafaa mtendaji wake kuhimidiwa na kulaumiwa? Na ikiwa ni maana ifananayo na hiari basi semeni, na onyesheni jinsi inavyoafikiana nayo kwa usahihi.�39 39. Amalil-Murtadha, Juz 2. Uk 347.

45


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Jibu: Ukweli ni kwamba ismah haipokonyi hiari kutoka kwa mtu kwa maana yoyote itakayofasiriwa, sawa endapo tutasema kuwa ismah ni daraja ya juu ya takwa, au ni matokeo ya elimu ya katashauri ya matokeo mabaya ya madhambi na maasi, au ni athari ya kutambuwa utukufu wa Mola na upendo kwa Allah (s.w.t.), kadiri itakavyokuwa ni kuwa mtu maasumu ni mwenye hiari katika matendo yake, muweza wa pande mbili za kadhia kati ya kufanya na kuacha. Tunalifafanua hilo kwa mfano ujao: Kwa kweli mtu mwenye akili akijua kuwepo kwa nguvu za umeme kwenye nyaya zilizo wazi zisizofunikwa na kizuwizi chochote, hatothubutu kuzigusa huku zikiwa katika hali hii. Kama ambavyo daktari hali makombo ya chakula kilichobakishwa na waliopatwa na ukoma au kifua kikuu kwa sababu tu ya kujua kwao matokeo mabaya ya matendo haya mawili, huku kila mmoja wao anajikuta anao uwezo wa kufanya tendo lile, kiasi kwamba lau mmoja wao akikiuka taratibu za maisha yake na akajiandaa kuhatarisha maisha yake atajiingiza kwenye tendo hili la kuhilikisha kwa kugusa nyaya za umeme na kula chakula kilichosalia kutoka mlo wa waliopatwa na maradhi ya hatari ya kuambukiza, ila wao hawato thubutu kufanya hivyo kwasababu tu wangali wanapenda kuishi kwa salama na kuwa mbali na hatari. Ukitaka utasema: Kwa kweli kazi ambayo imetangulia kutajwa ina wezekana ikafanywa na mwenye akili kwa dhati na kwa asili hata na daktari, lakini yazuilika kufanywa kwa sababu tu ya sababu iwezayo kujitokeza - kama vile kupenda kuishi na kupenda usalama - na kwa sababu ya kawida inayotawala, nayo ni kuwa mwenye akili hathubutu kutenda mambo kama haya. Na sio kama kutokea kwake ni muhali kiasili na kiakili. Kuna tofauti kubwa kati ya jambo lililo muhali kiada na lile lililo muhali kiakili. Kwa hiyo katika hali ya muhali wa kiada, kitendo kiasili huwezekana kutokea, isipokuwa tu moja ya pande zake mbili ndio inayotiliwa uzito kuliko nyingine kwa kigezo maalumu kinachopelekea kuacha kitendo kinacho 46


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

dhuru. Hali hiyo ni kinyume na muhali wa kiakili, kwa kuwa kitendo hapo huwa chazuilika kiasili, kwa hiyo hakitokei kwa sababu ya kutowezekana kiasili. Na kwa ibara ya wazi zaidi ni kuwa: Kwa kweli muhali wa kiakili hauwezi kupatikana kwa kuwa kupatikana kwake ni kinyume na gezi ya kuwa ni muhali na yenye kuzuwilika. Ukitaka zingatia kutokea ubaya kwa (s.w.t.), kwani kutokea ubaya upande wake ni jambo liwezekanalo kiasili na limo ndani ya wigo wa uwezo wake, hivyo basi anaweza kumuingiza mtiifu moto wa Jahannam na muasi amwingize kwenye neema za Pepo, lakini halitokei hilo kwake kwa kuwa ni kinyume na hekima na lapingana na alivyowaahidi watiifu kuwa atawalipa malipo mema na alivyowakamia waasi kuwa atawaadhibu, kwa msingi huo kuzuilika kutokea kitendo kutoka kwa mtu kwa sababu ya kuhifadhi malengo yake na matarajio yake, haiwi dalili ya kupokonywa hiari na uwezo. Hivyo basi Nabii maasumu anao uwezo wa kutenda maasi na kufanya makosa kulingana na uwezo na uhuru aliopewa lakini ili aifikiye daraja ya juu ya takwa na kwa sababu ni mwenye elimu ya katashauri ya kuzielewa athari za maasi na madhambi, na kwa kuutambua utukufu wa Mola na muumba, yeye hujiepusha kutenda dhambi na kufanya maasi, wala haiwezekani yatokee kwake maovu kama haya japokuwa ni muweza wa kufanya hivyo. Mfano wa manabii katika kujiepusha kwao binafsi kufanya maovu na kutojiingiza katika madhambi, ni sawa na mzazi mwenye huruma ambaye hathubutu kumuuwa mwanawe hata kama atapewa mali nyingi, hazina ilio hodhi mali na cheo cha juu, japokuwa ana uwezo wa kumuuwa kwa silaha ya aina yeyote ile na kwa njia yeyote. Na kwa lengo hili anasema Allamah Tabatabai: “Kwa kweli elimu hii 47


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

nakusudia sifa hii pambanuzi ya Ismah haibadilishi tabia ya mtu teule katika matendo yake yafanyikayo kwa utashi na wala haimpeleki kwenye hali ya kukosa hiari. Itawezekanaje akose hiari ilihali elimu ni miongoni mwa misingi ya hiari. Nguvu ya elimu peke yake haiwajibishi ila nguvu ya utashi, kama mpenda salama atakuwa na yakini kuwa kimiminika fulani ni sumu iuwayo, basi hapo hapo bila shaka atajizuwia kwa hiari yake kunywa kabisa. Ila mtendaji atadharurika na kukosa hiari pale tu mlazimishaji ataondoa moja ya pande mbili za hali ya kutenda na kutotenda, kutoka kwenye uwezekano mpaka kwenye muhali. Hilo linathibitishwa kwa ushahidi wa kauli yake:

“Tuli wachaguwa na tuliwaongoza njia iliyo nyooka huo ni mwongozo wa Mwenyezi Mungu ambao kwao huwaongoza awapendao miongoni mwa waja wake lau wange fanya ushirikina ange yabatilisha ambayo walikuwa wakiyatenda.�(Al—Anam:87-88). Aya yamaanisha kuwa wao wanao uwezo wa kumshirikisha Mwenyezi Mungu japokuwa uchaguzi na mwongozo wa Mwenyezi Mungu wazuia hilo. Na kauli yake:

48


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Oh! Ewe Mtume, fikisha ulicho teremshiwa kutoka kwa Mola wako endapo hauto fanya utakuwa hauja ufikisha ujumbe wake.� (AlMaida:67). Na Aya nyinginezo kama hizo, kwa hiyo mtu ambaye ni maasumu huacha kutenda maasi mwenyewe na kwa hiari yake na utashi wake, na uhusiano wa kuielekea Ismah yake (s.w.t.) ni sawa na uhusiano wa kitendo cha asiye kuwa maasumu kuyaacha maasi na kuielekea tawfiki yake (s.w.t.). Wala hilo pia halipingani na lile linaloashiriwa na maneno yake (s.w.t.) na kuelezwa wazi wazi na habari, nalo ni kuwa manabii na maimamu huwekwa sawa kupitia Roho mtakatifu, kwani uhusiano wa kuwekwa sawa na Roho mtakatifu ni sawa na uhusiano wa kumuweka sawa muumini kupitia roho ya imani, na uhusiano wa upotovu na shetani, kwani hali hiyo haifanyi kitendo kutokuwa ni kitendo kilichotoka kwa mtendaji wake chenye kutegemea hiari yake na utashi wake. Naam, kuna watu wanadhania kuwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) humwondowa mtu mbali na maasi kwa njia isiyokuwa ya hiari yake na utashi wake bali kwa njia ya mkinzano wa sababu na taathira zake kwa kuumba utashi au kumtuma Malaika ambaye atakinza utashi wa mtu na kuuzuwia usi athiri au kubadilisha njia yake, na kuiepusha mbali na tabia ya kusudio la mtu, kama mtu mwenye nguvu amzuiavyo mtu dhaifu dhidi ya atakalo kulitenda kwa utashi wake. Japo baadhi ya watu hawa Mujabirah lakini asili ya shirikishi ambayo ndio msingi wa nadharia yao hii na mfano wake ni kuwa: Wao wanaona kuwa vitu humuhitajia muumba wa haki wakati wa kutokea tu, lakini vikishakuwepo havimuhitajii tena Muumba ili viendelee kubaki, kwa hiyo yeye (s.w.t.) ni sababu katika kudhihirisha sababu nyingine, ila tu kwa sababau yeye ni mwenye uwezo zaidi na nguvu zaidi kuliko kila kitu ndio maana huamiliana na vitu apendavyo katika hali ile ya uhai. Hivyo akitaka kwa nguvu huvizuia au huviacha, huvipa uhai au huvifisha, huvipa siha 49


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

au huvipa maradhi, huvipa wasaa au huvibana, na mengineyo kama hayo, yote hayo kwa shinikizo. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) apendapo kumwondowa mtu kwenye shari kwa mfano, humtumia Malaika amabaye humkinza ndani kwa ndani na kubadilisha mapito ya utashi wake kutoka shari na kwenda kwenye kheri, au akitaka kumpoteza mja kwa kustahiki kwake hivyo, atamchombezea ibilisi amgeuze kutoka kwenye kheri na kumwelekeza kwenye shari, ingawaje si kwa kadiri inayowajibisha kumkomwondoa hiari. Nadharia hii, inapingwa na tuyashuhudiayo wenyewe nafsini mwetu katika matendo ya kheri na ya shari ushuhuda wa bayana kuwa, hakuna sababu nyingine itubadilishayo na kutukinza na kutushinda nguvu mbali na nafsi zetu ambazo zinafanya kazi yake huku tukiwa tunazitambuwa na utashi ulio kwenye mpango tunaousimamia. Lile ambalo lathibitishwa kwa kusikia na kwa akili nyuma ya nafsi zetu miongoni mwa sababu nyingine kama vile Malaika na shetani ni sababu kwa kirefu si kwa upana. Zaidi ya hayo ni kuwa maarifa ya Qur’an kuanzia Tawhid na matokeo yake yanaipinga kauli hii.� 40

Daraja za ismah na dalili zake Umeshajua ukweli wa ismah na utafiti unaorejea humo miongoni mwa mijadala mingine iliyo nje ya mada, hivyo kwa sasa yapasa kuzijua daraja zake, kwani kulingana na hali ya kidaraja zagawnyika kwenye daraja zi fuatazo: 1- Ismah wakati wa kupokea wahyi, kuulinda na kuufikisha kwa watu. 2-Ismah dhidi ya maasi na kutenda dhambi kwa istilahi iliyopo. 40- Al-mizan, Juz 11. Uk 179-180. 50


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

3-Ismah dhidi ya makosa katika mambo ya mtu binafsi na ya kijamii. Hizi ndio daraja za Ismah, na yawezekana kuzibainisha daraja hizo kwa njia nyigine nayo ni: Kwa kweli kiambatanacho na Ismah na uhifadhi hakiwezi kuwa nje ya moja ya mambo haya: Aidha kumkufuru Mwenyezi Mungu au kumuasi na kumkhalifu. La pili haliachi kuwa aidha maasi makubwa, au madogo. Na madogo yapo katika sehemu mbili: Yale yanayoonyesha uduni wa mtendaji na uchafu wa nafsi yake, mfano wa kuiba tonge moja au vinginevyo. Vyovyote itakavyokuwa ni kuwa kutokea kwa maasi kwaweza kuwa kwa makusudio au kwa kusahau, inaweza kuwa ni kabla ya kukabidhiwa unabii au baada yake. Kadhi Abdul-jabbari sheikh wa Muutazila katika zama zake amefafanua madhhabu ya Muutazila katika ismah na hatimaye akapitisha maamuzi kuwa Nabii ni lazima awe amesafika na kuwa mbali na ambayo yamfanyayo awajibike kutoka nje ya upenzi wa Mwenyezi Mungu mtukufu na kuwa miongoni mwa maadui zake kabla ya unabii na baada yake ili awe ametakasika dhidi ya uongo au kuficha au kusahau na menginayo yasiyokuwa hayo. Na anapasa asifanye litakalopelekea kutokukubalika au linalomwondolea uaminifu au linalopelekea kuichunguza elimu yake, kama vile uongo kwa hali zake zote, tawria na hadaa katika ayatendayo, na kutenda madogo yanayoshusha hadhi.”41 Na amesema Bw. Taftazaniy ndani ya sherehe ya al—Aqaidun-Nasfiyah: “Hakika wao ni maasumu walio mbali na kufuru kabla ya wahyi na baada yake kwa ijmai. Pia kwa rai ya jumhuri ni maasumu dhidi ya kufanya maasi makubwa kwa makusudio, kinyume na Hashawiy. Ama katika hali ya kusahau walio wengi wanasema kuwa yawezekana. Ama maasi madogo kwa rai ya jumhuri wanaweza kuyafanya kwa makusudio, kinyume na 41 -Al--mughniy, Juz 15, Uk 279. 51


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

rai ya al-Jubaiy na wafuasi wake. Na wote wnaafikiana kuwa yawezekana kwa kusahau isipokuwa kwa lile tu linaloonyesha uduni.42 Na katika kitabu hiki Shia wamenasibishwa na kauli ya kuwa inafaa kudhihirisha ukafiri kwa Taqiyah, na wao wako mbali na nasibisho hili.” Al—fadhwilu Al—qawshajiy amesema: “Ama yale yanayodhaniwa kuwa ni maasi kutoka kwa manabii, kwanaza ima yatakuwa yanapingana na hali halisi ya muujiza, kama vile uongo katika mambo yanayohusu uhubiri. Pili ima yatakuwa ni ukafiri au kuasi. Hali hiyo ima iwe ni dhambi kubwa kama vile kuuwa na kuzini, au liwe ni dogo duni kama vile kuiba tonge au lkupunguza punje kwenye mizani au lingile lichukizalo kama vile uongo na kashfa, hayo yote ni maasi ima yatakuwa ni kwa makusudi au kwa kusahau, ima itakuwa ni baada ya kukabidhiwa unabii au kabla.43 Hivyo basi twasema: Kuhusu la kwanza: Nakusudia kutokea kufuru kwa mtu ambaye ni maasumu, hilo halijasemwa na yeyote kuwa lafaa, na kauli ambayo huenda ikanasibishwa na baadhi ya vikundi kama vile (AlAzaariqah) kuwa kufuru yawezekana kwa manabii, basi linalokusudiwa kwenye maana ya neno kufuru ni maasi kulingana na istilahi ya Waislamu, wao wameuita uasi kuwa ni kufuru kwa sababu ya kuitikadi kwao kuwa kila maasi ni kufuru.” Al—fadhwilu Al—qawshajiy amesema: “Al—Azaariqah, kundi miongoni mwa ma Khawariji wame ijuzisha kufuru kutokana na kujuzisha kwao dhambi huku wakisema kuwa kila maasi ni kufuru.”44 Na amesema ndani ya Sharhul-muwafiq: “Ama madhambi mengine - (Anakusudia yasiyo kuwa uongo katika uhubiri) hayo Aidha ni ukafiri au mengine (maasi) 42. Al-Maana. Juz 15, Uk 289. 43. Al-Aqaidu An-Nasfiyyah, Uk 171. 44. Sharhu Al--tajridi lilfadhili Al--qawshajiy, Uk 464. 52


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ama kuhusu ukafiri ni kuwa umma umeafikiana kuhusu kuhifadhika kwao nao (kabla ya unabii na baada yake wala hakuna tofauti kwa yoyote miongoni mwao katika hilo) isipokuwa Al-Azariqah miongoni mwa Khawariji wao wamejuzisha dhambi kwa manabii, na kila dhambi kwa makhawariji ni ukafiri. (Basi ikawalazimu kujuzisha ukafiri, na yaelezwa habari kutoka kwao kuwa wamesema yafaa kutumwa Nabii ambaye Mwenyezi Mungu Mtukufu alikuwa anajua tangu mwanzo kuwa atakufuru baada ya unabii wake.”45 Na Al—fakhrur Raziy amesema katika tafsiri yake: “Ama itiKadi yao ukafiri na upotovu hakika hilo si jaizi kwa walio wengi katika umma huu. Na Al-fadhiliyatu miongoni mwa makhawariji wamesema kuwa: Dhambi nyingi zimetokea kwao. Na dhambi kwa makhawariji ni ukafiri na ushrikina, hivyo si mbaya kama wataamini kutokea ukafri kwao” 46 Al—fadhilu Al—mikdad amesema: “Wameafikana juu ya kauli moja nayo ni kuwa haiwezekani kufuru kwao -manabii- isipokuwa Al—fadhiliyah miongoni mwa makhawariji wao wamejuzisha kutokea dhambi kwao, na kila dhambi kwao ni ukafiri, kwa hiyo imewalazimu wajuzishe ukafiri juu yao. Na kundi la watu lilijuzisha ukafiri juu yao kwa Taqiyah na woga, na wakauzuia dhahiri, kwani wakati bora wa Taqiyah ni mwanzo wa uhubiri kwa sababu ya kukithiri wapinzani 45. Sharhul muwafiqi. Juz 8.Uk 264. 46 - Tafsirul Ar-Razi, Juz 1, Uk 318.

53


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

wake wakati huo, lakini hiyo itasababisha kufichi dini kabisa.”47 Je! Baada ya maneno ya Al—Fadhilu Al—Mikdad - (ya kukanusha usemi wa kuwa inawezekana ukafiri kwa manabii kwa Taqiyah) - je yanasihi waliyoyahusisha baadhi yao kwa Shia kuwa wanaruhusu ukafiri kwa manabii kwa Taqiyah? kama alivyodai Al-qawshajiy ndani ya sherehe ya Altajridiu! pale aliposema: “Shia wameruhusu kuudhihirisha kwa Taqiyah na kuihifadhi nafsi isiingiye ndani ya maangamizi.”48 Kadhalika al-Adhdiy katika Sharhul-mawaqif: “Shia wameruhusu kuudhihrisha” yaani kuudhihrisha ukafiri kwa Taqiyah pindi wanapohofia kuangamia, kwa sababu kuudhihirisha Uislamu wakati huo ni kuiingiza nafsi katika maangamizi.”49 Na amewafuata katika uhusisho huu batili AlFakhru Raziy katika tafsiri yake. Amesema: “Imamia wameruhusu kwao kudhihirisha ukafiri kwa Taqiyah.”50 Walilolisema jamaa hawa kuwanasibisha Shia ni usemi batili, kwa kuwa hajapata kusema usemi kama huu mtu yeyote miongoni mwa Shia wala kamwe hajawahi itikadia hilo yeyote miongoni mwao. Kwa hiyo kudhania kuwa inafaa kudhihirisha ukafiri kwa Nabii kwa ajili ya taqiyah ni batili, kwa kuwa taqiyah ina sharti zake mahsusi na hivyo taqiyah huruhusiwa endapo tu sharti hizo zitathibiti, na mahali hapo palipoelezwa hazipo sharti hizo. Na kwa kulingana na hayo kadhi Abdul-Jabbar Al-hamdaniy Al-Asadiy Abadiy amesema: “Endapo atasema: Mwaruhusu taqiyah juu ya Mtume katika yale ayatekelezayo? Ataambiwa: Hairuhusiwi kwake katika yale 47 - Al-Lawamiu Ilahiyyah. 48. Sharhut-Tajridi Al-Qawshajiy, Uk 464. 49. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 264. 50. Tafsiri Raziy, Juz 1, Uk 318. 54


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

yanayomlazimu kuyatekeleza, kwani ingekuwa inaruhusiwa basi daraja ya unabii haingetukuzwa, kwani daraja hiyo hutukuzwa kwa kuwa yeye anadhamana ya kuitekeleza risala, na kuvuta subira kwa kila litakalojitokeza-.” Akaendelea mpaka akasema: “Lau akiogopa kuuwawa iwapo atatekeleza sharia yake, hukumu yake nini katika hilo? Ataambiwa: Yamlazimu aitekeleze na ajuwe kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu atamuepushia hilo.”51 Al—Fakhru dini Raziy amesema ndani ya kitabu (Ismatul-anbiyai): “Umma (wa Kiislamu) umeafikiana kuwa manabii ni maasumu dhidi ya ukafiri na hawafanyi bidaa, isipokuwa alFadhliyah miongoni mwa Khawariji, wao wanasema manabii (a.s.) wanaweza kukufuru, hivyo ni kwa sababu wao-Alfadhliyah kwa mtazamo wao wanaona yawezekana kutokea dhambi upande wao, na kila dhambi kwa mtizamo wao ni ukafiri, kwa njia hii wameruhusu kutokea ukafiri kwao (manabii). Rawafidhu kwa kweli wao wanasema inafaa kwa manabii kudhihirisha neno la ukafiri kwa njia ya taqiya.”52 Na pambizoni mwa kitabu ukurasa wa kumi na nane imenakilwa kutoka kwa Ibn Hazmi ndani ya Al-milalu-wan-nihal kuwa: Yeye amewacharukia Al-karamiya nao ni kundi miongoni mwa Murjiah na Ibnil-Baqlaniy ambaye yeye ni miongoni mwa Al-ashariyah kuwa wao wanasema: “Kwa hakika Mitume wanamuasi Mwenyezi Mungu katika madhambi makubwa yote na madogo kwa makusudio ukiondoa uongo katika uhubiri tu.” Na akasema: “Na hiyo ni kauli ya Mayahudi na manaswara, na nimemsikia anayeelezea kutoka kwa baadhi ya Alkaramiyah kuwa, wao wanaruhusu uongo kwa manabii kati51. Al-Mughniy, Juz 15, Uk 284. 52. Ismatul-Anbiya, Uk 18. Chapa ya Jedah.

55


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ka uhubiri. Na Abiy Jaafari Asimnaniy mwenzi wa Al— Baqlaniy amehusishwa na kitendo cha kuruhusu ukafiri kwao (manabii). Ama kuhusu dhambi isiyokuwa ukafiri, maelezo ya madhehebu nyingi ni kwamba Shia wameafikiana kuwa manabii ni maasumu hawatendi maasi, sawa yawe makubwa au madogo, iwe kwa kusahau au makusudio, kabla ya unabii au baada yake, kabla ya kutumwa au baada yake.” Naam kulingana na rai ya sheikh Al—Mufidu inaonekana anaruhusu baadhi ya maasi madogo kwa manabii bila ya kukusudia kabla ya utume, amesema: “Kwa kweli manabii wote wa Mwenyezi Mungu (s.w.t) wamehifadhika na madhambi makubwa kabla ya unabii na baada yake, na yale madhambi madogo yote ambayo hudharauliwa mtendaji wake. Ama madogo ambayo hadharauliwi mtendaji wake, yanaruhusiwa kutokea kwao kabla ya unabii na katika hali isiyo ya kukusudia, na huzuilika kwao baada ya unabii kwa hali yoyote ile.” Kisha akasema: “Na haya ndio madhehebu ya kundi kubwa la Imamiyah. 53 Na hilo linadhihiri kwa mtafiti Al—Ardabiliy katika maoni yake juu ya kitabu Sharhut-Tajridi cha Al-Fadhilu al-Qaushajiy pale mtafiti Tusi alipotoa dalili kuhusu ismah kuwa: “Kwa kuwa kama si ismah basi kauli za manabii zisingeaminika.” Mfafanuzi akaeleza: “Kutokea dhambi hasa ndogo kwa kusahau hakuondoi uaminifu.” Al-Ardabili akaongeza kwa kauli yake: “Hasa ikiwa kabla ya kukabidhiwa unabii.” 54 Na kuhusu wasiokuwa Shia tayari umekwishayajua maoni ya (Al-iitizalu) isipokuwa Al-fadhlu Al-qawshajiy anapambanuwa kwa kusema: “Kundi kubwa lawajibisha ismah kwao dhidi ya yale madhambi yanayopingana na hali ya muujiza, lakini Al—Qadhi ameruhusu katika hali ya kusahau, 53. Awailul- Maqalaat, Uk 29 na 30. 54. Taaliquhu al--Ardabili ala sharhi tajridi, Uk 464.

56


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

akidai kuwa hayatii dosari katika kusadiki linalokusudiwa na muujiza. Pia wamewajibisha dhidi ya madhambi makubwa kwa kukusudia baada ya kukabidhiwa unabii, lakini Al-hashawiyyah wameruhusu. Pia wamewajibisha dhidi ya madogo yanayochukiza, kwa sababu ya kutia dosari wito wa kufuatwa. Na kwa sababu hii Muutazilah wengi wamekanusha kutenda madhambi makubwa kabla ya kukabidhiwa unabii. Chaguo la wahakiki wa Ashaira ni kuzuwia madhambi makubwa na madogo kabisa yaliyo duni baada ya kukabidhiwa unabii, na madogo yasiyo duni kwa kukusudia na si kwa kusahau. Imamu wa Haramayni miongoni mwa Ashairah na Abu Hashimi miongoni mwa Muutazilah wameruhusu madhambi madogo kwa kukusudia.”55 Na amesema katika Sharhul-mawaqifi: “Ama madhambi ambayo si ukafiri ima yatakuwa makubwa au madogo na kila moja kati ya hayo, ima yatakuwa yanatokea kwa makusudi au kwa kusahau. Hivyo vigawanyo ni vinne, na kila kimoja kati ya hivyo ima kiwe kabla ya kutumwa au baada yake. Ama kuhusu madhambi makubwa, kundi kubwa limezuwia (kutokea hilo miongoni mwa wahakiki na maimamu, wala hakuna aliyekwenda kinyume na hilo isipokuwa Al-hashawiyyah). Na walio wengi (miongoni mwa wanaozuia) wanazuia kwa hoja ya kusikia. (Al—Qadhii na wahakiki miongoni mwa Ashairah wamesema kuwa, kwa kweli ismah nje ya uhubiri si wajibu kiakili kwani hakuna dalili ya muujiza juu yake. Hivyo kuzuilika kwa madhambi makubwa kwao kwa makusudi kumetokana na hoja ya kusikia na ijmai ya umma kabla ya kudhihiri wapinzani wa hilo.) Na Muutazila wamesema kulingana na kanuni zao (mbaya katika uzuri na ubaya wa kiakili na kanuni ya ulazima wa kuchunga kati ya kinachofaa 55. Sharhut-Tajridi cha Al-Fadhilu Al-Qushujiy 464. 57


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

na kinachofaa zaidi kuwa) hilo lazuilika kiakili (kwa sababu kutenda kwao madhambi makubwa makusudi kwawajibisha haiba yao kuporomoka kutoka mioyoni na daraja yao kupunguwa machoni mwa watu na hatimaye kutasababisha kutopendwa na kutotiiwa, na hilo lapelekea viumbe kuharibika na kutosuluhika, na hilo ni kinyume na muktadha wa akili na hekima). Ama (kutokea hayo madhambi kwao) kwa kusahau (au kwa makosa katika taawili) walio wengi wameliruhusu hilo, (na teule ni kinyume chake.)”56 Hizi ndizo kauli maarufu kati ya wanatheiolojia na muda si mrefu utatambuwa jinsi zote hizo zilivyo mbali na Kitabu na Sunnah na hukumu ya akili, isipokuwa kauli ya kwanza tu, nayo ni kauli ya Shia. Al-Fakhru Razi amesema kuhusu Ismah ya manabii. “Pili: Inayoambatana na sharia zote na hukumu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), wameafikiana wote kuwa hairuhusiwi kwao kupotosha na khiyana katika mlango huu, si kwa kusudi wala kusahau, kwa sababu kama si hivyo basi hakitobakia chochote cha kutegemewa katika sharia. Nne: Yanayoambatana na matendo yao na hali zao. Wametofautiana katika hilo hadi kufikia kauli tano…Na ambalo tusemalo sisi ni kuwa: Kwa kweli manabii (a.s.) ni maasumu dhidi ya madhambi makubwa na madogo kwa makusudio katika zama za unabii. Ama kwa kusahau wanaweza kutenda.”57 Hivyo twasema: Maneno yatakuwa katika hatua zifuatazo: Hatua ya kwanza: Ismah ya manabii katika kuifikisha Risala: Madhehbu ya waliowengi kati ya Sunni na Shia wote wanasema kuwa, manabii ni maasumu katika hatua hiyo, ila tu kuna kauli imehusishwa na Al-baqlaniy kuwa yeye aruhusu kukosea katika kuifikisha risala kwa kusa56. Sharhul- Mawaqif, Jalada la 8, Uk 264 - 265. 57. Ismatul-Anbiyai, Fakhrudini Raziy uk19,-chapa ya Jeddah chapa ya kwanza 1406 A.D. 58


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

hau na kughafilika, si kwa kusudi. Abul-Hassan Abdul-Jabbar ambaye ni maarufu kwa jina la al-Qaadwiy, yeye ni raisi wa Iitizali katika zama zake, aliye fariki mwaka (415) amesema: “Haiwezekani kuwepo uongo katika lile alitekelezalo Nabii kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu, kwa kuwa yeye mtukufu ana hekima, na lengo lake katika kutuma ni kuyatambulisha yaliyo bora, hivyo lau angelijua kuwa (Mtume) atachaguwa kusema uongo katika lile alitekelezalo basi asingelimtuma, kwa sababu hilo lapingana na hekima. Na kwa sababu hii haruhusiwi kuacha kutekeleza ujumbe aliopewa, au kuuficha au kuficha baadhi yake.” Akaendelea mpaka akasema: “Sisi hatujuzishi kwake kusahau na kukosea katika lile alitekelezalo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ajili ya sababu iliyotangulia kutajwa, kwa sababu hapana tofauti katika kutoka kwake nje ya utekelezaji ikiwa atasahau, au atakosea au atachanganya au ataficha au atasema uongo, hali ya hayo yote ni moja wala hakuna tofauti. Linalowezekana tu ni kusahau katika kitendo ambacho tayari alikwishakibainisha hapo kabla na akawa tayari alikwishatekeleza yanayolazimu kuhusiana na kitendo hicho, hivyo akifanya kwa maslahi yake haizuwiliki kutokea usahaulifu na ukoseaji, hapo haitomchanganya yeyote kuwa lililo mtokea katika utekelezaji wa mara ya pili ni usahaulifu, pia lililomtokea katika habari ya Dhilyadayni na mengine yasiyokuwa hayo.”58 Kuhusu aliyoyasema kuwa inawezekana Nabii akasahau katika kitendo ambacho hukumu yake tayari ameshaibainisha, usemi wetu utakuja baadaye kuhusiana na hilo. Wahakiki miongoni mwa wanatheiolojia wamethibitisha ismah yao katika hatua hiyo kwa kutumia baadhi ya dalili ambazo mtafiti Tusi amezigusia ndani ya kitabu chake (Atajridu) kwa kusema: “Ili upatikane uaminifu wa 58. Al-mughniy Juz 15, Uk 281. 59


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

matendo yake na kauli zake, na lipatikane lengo la kutumwa, nalo ni kufuatwa na wale aliyetumwa kwao katika amri zake na makatazo yake.”59 Dalili mbili alizozitaja japokuwa sio mahsusi kwa hatua hii bali zajumuisha hatua nyingine, lakini ni dalili kamili zinazotegemea akili na dhamira katika suala la Isma ya manabii katika nyanja ya ufukishaji wa risala. Ufafanuzi wake ni kama ifuatavyo: Kwa hakika lengo la hali ya juu na la upeo wa mbali la kuwapeleka manabii na kuwatuma Mitume, ni kuwaongoza watu kwenye mafunzo ya kiungu na sheria za Mwenyezi Mungu zilizotakasika. Lengo hilo halitotimia isipokuwa kwa imani ya watu na itikadi yao kwa kuwaamini hao walio tumiwa na kuwa na yakini kuwa hao ni wajumbe kutoka kwake (s.w.t), na kwamba maneno yao na kauli zao ni maneno yake na kauli zake (s.w.t.). Imani hii na yakini ile havipatikani isipokuwa kwa kukiri na kuamini kuwa hawa manabii wamehifadhika dhidi ya makosa katika ngazi tatu: Katika ngazi ya kuifikisha risala, nako ni kuhifadhika katika kuupokea wahyi. Kuhifadhika katika kuuhifadhi wahyi huo. Na kuhifadhika katika kuufikisha na kuubainisha. Mfano wa mambo kama hayo hayawezi kupatikana isipokuwa kwa kumuhifadhi Nabii dhidi ya utelezaji na makosa kwa makusudio na kwa kusahau. Kadhi Abul-Hasan Abdul-jabbar amesema: “Kwa hakika nafsi hazitulii na kukubali neno kutoka kwa ambaye vitendo vyake vinapingana na kauli zake, utulivu ule unaopatikana kutoka kwa yule aliyetakasika dhidi ya hali hiyo. Hivyo inabidi kwa manabii (a.s.) isiwezekane ila ile hali tuisemayo, ya kuwa wao wametakasika dhidi ya yale yawajibishayo adhabu na kushushwa hadhi na kutoka nje ya upenzi wa Mwenyezi Mungu mtukufu na kuwa miongoni mwa maadui zake.” 59. Sharhut-Tajridi cha Al-Fadhil Al-Qushijiy, Uk 463. Kashful-Muradi, Uk 217, chapa ya Swida. 60


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Hilo labainisha kuwa ikiwa wao wametumwa ili kuziwia dhambi kubwa na maasi kwa kuziwia na kukinza na kuhofisha basi haiwezekani wao wenyewe watenda mfano wa hayo, kwani ni maarufu kuwa mwenye kutenda kitu hakubaliki iwapo atamzuwia mtu mwingine hilo kwa kumkataza na kumkaripia, na kuwa hali kama hii haiathiri ikitoka kwake…...... lau muwaidhi akisimama na kumuhofisha dhidi ya kutenda maasi mtu ambaye humshuhudia muwaidhi huyo akitenda mfano wa maasi yake, kwa kweli mtu huyo atampuuza na kupuuza mawaidha yake.”60 Na amesema mahali pengine: “Kwa kweli mtoa mawaidha na mkumbushaji japo itazidi dhana yetu kuhusu hali yake kuwa ameacha maovu, ametubu kwa anavyoonyesha kwa alama za toba na majuto, lakini kwa vile kabla ya hapo tuliitambua hali yake ya kuzama katika kunywa na uovu, waadhi wake hautuathiri kwa kiwango kile cha taathira ya waadhi wa ambaye ni msafi na mtakasifu katika hali zake zote kwa muda wote.”61 Na aliyoyasema mwishoni yazingatiwa kuwa ni dalili ya kuwa Ismah ni wajibu hata kabla ya kukabidhiwa unabii . Na uthibitisho huu ukikubaliwa kwa sura kamili utakuwa ni uthibtisho tosha katika hatua zote za Ismah ambazo tutabainisha katika mijadala ijayo. Al-Fakhru Raziy amesema ndani ya (Ismatul-Anbiyai) pindi alipobainisha zile sura na dalili kuhusu Ismah ya manabii katika hatua ya kufikisha: “Hoja ya sita: Kwa kweli wao walikuwa wanaamrisha utii na kuacha maasi hivyo laiti wangeliacha utii na wakatenda maasi basi wangeingia ndani ya kauli yake Mtukufu:

60. Al-mughniy, Juz 15, Uk 303. 61. Ismatul-Anbiya cha Al-Fakhri Raziy, Uk 21, chapa mpya mwanzoni mwa 1406, A.H. 61


Umaasumu wa Mitume “Oh! Ninyi mlioamini, hamuyafanyi?”(Aswaf: 2.)

Sehemu ya kwanza kwa

nini

mnasema

ambayo

Na chini ya kauli yake Mtukufu:

“Mnawaamurisha watu kutenda-mema na mnajisahau ninyi wenyewe” (44:Al-Baqrah.) Ni wazi kuwa Nabii kuwa katika hali kama hii ni mbaya mno, na pia Mwenyezi Mungu Mtukufu ameelezea habari ya mjumbe wake Shuaibu (a.s.) kuwa yeye aliitakasa nafsi yake na kuwa mbali na hali kama hiyo aliposema: “Wala sitaki ni waende kinyume na ambayo na wakatazeni.”62 Hii ndiyo mantiki ya kiakili, ama mantiki ya Wahyi yatilia mkazo juu ya kuhifadhika Nabii katika kuifikisha risala kwenye nyanja tatu zilizotangulia. Ufuatao ni ufafanuzi wa hilo:

Quran yazungumia Ismah ya Nabii katika hatua ya kukabidhiwa wahyi Kuna Aya kadhaa zinazotoa dalili juu ya Ismah katika uwanja huo, tutazitaja moja baada ya nyingine: Aya ya kwanza:

“Ni mjuzi wa yaliyo ghibu wala hamdhihirishii ghibu yake mmoja yeyote . Isipokuwa Mtume anayemridhia kisha yeye humfayia kundi 62. Al-Mughniy, Uk 305. 62


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

la walinzi wanamfuatilia mbele yake na nyuma yake.”(Al-jinnu:26-27)

“Ili ajuwe kama wamefikisha ujumbe wa Mola wao, na yu akizunguka kila walichonacho na yu adhibiti idadi ya kila kitu.”(Al-jinn:28). Kwa kweli ili ikamilike dalili za Aya hizi juu ya kuhifadhika kwa mitume na manabii kwenye nyanja za kukabidhiwa wahyi inategemea ufafanuzi juu ya baadhi ya misamiati ya Aya hizi. 1-Kauli yake: “Wala hadhihirishi” mfano wa kauli yake (s.w.t.)

yamaanisha kuonyesha kujulisha,

“Mwenyezi Mungu alimjulisha, alimtambulisha baadhi na kuacha baadhi. (Atahrim; 66:3). 2-Tamko (min) katika kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu (min rasulin) min katika hii Aya ni ya kubainisha kuwa ni nani aliyeridhiwa na Mwenyezi Mungu, basi huyu Mtume ndiye mridhiwa ambaye Mwenyezi Mungu amemchaguwa ili amtambulishe habari fulani ya ghaibu. 3-Nomino (innahu) katika usemi wake: (innahu yasluku) inarerjea kwa Mwenyezi Mungu, kama ambavyo nomino inayoishiria mtendaji katika kauli yake (yasluku) pia yarejea kwake (s.w.t.) na ina maana sawa na kitenzi anajalia. 4-Nomino katika maneno ( yadayhi na khalfahu) inamrejelea Mtume. 5-Na (Arrasdu) ni kulinda na kuhifadhi. 63


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

6-Na makusudio ya (bayna yadayhi) ni mbele ya Mtume, yaani kaiti ya Mtume wake na watu waliotumiwa. Kama ambavyo makusudio ya (min khalfihim) ni kati ya Mtume na chimbuko la wahyi ambalo ni Mwenyezi Mungu. Kwa minajili hiyo Nabii anakuwa ni mwenye kuhifadhika katika nyanja za kuupokea wahyi pande zote mbili. Katika taabiri hii limechukuliwa lile linalofahamika toka kwenye maana ya risala, nalo ni kuwa risala ni kipaji kilichoungana kutoka kwa mtumaji ambaye ni Mwenyezi Mungu (s.w.t) na kumwendea Mtume. Aya inaelezea njia ya kufika ghaibu kwa Mitume, na kuwa Mtume ni mwenye kuzingirwa na uangalizi na walinzi mbele na nyuma, wala hapatwi na jambo limwekalo kando na wahyi na wala kwenda kinyume na lile aliloliteremsha Mwenyezi Mungu mtukufu. Na maana ya Aya ni: Kwa hakika Mwenyezi Mungu anaweka watazamaji na walinzi miongoni mwa Malaika kati ya Mtume na waliotumiwa, na kati ya Mtume na chimbuko la wahyi, na lengo la uwekaji huu mbele ya Mtume na nyuma yake ni kuuhifadhi wahyi dhidi ya aina yoyote ya ziyada au nuksani au mchanganyiko wowote ule ndani yake, kama kutanguliza au kuchelewesha, au mchanganyiko ujao kutoka kwa shetani moja kwa moja au kuptia kitu kingine. Kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ameeleza sababu ya kuweka walinzi mbele na nyuma ya Mtume kwa kusema: “…ili ajuwe kama wamefikisha risala ya Mola wao.” Na makusudio ya elimu hapa ni elimu ya kivitendo maana yake ni kukitimiza kitu nje kivitendo, yaani ili ufikishaji wa risala nje kivitendo utimie, hiyo ni sawa na kauli yake:

“Mwenyezi Mungu atawajua ambao ni wa kweli na atawajua waongo.” (3:Al-Ankabuti).

64


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Yaani ufikishaji wa risala ya Mola wao utimie kama ilivyoteremshwa bila ya kubadilishwa au kupindishwa, bila ya nyongeza au upungufu. 7- Kauli yake: “Amevizunguka walivyokuwanavyo” ni kifungu kamilishi cha ulinzi uliopatikana kutoka kauli yake (raswadan)”. Kwa sura ya jumla ni kuwa ibara hizi tatu zilizokuja katika Aya zinabainisha na kudhihirisha upeo wa utiliaji manani wa muumba (swt) kwa kutoa ulinzi na uhifadhi kwa wahyi mpaka umfikiye aliyetumiwa huku ukiwa katika hali yake halisi bila ya mabadiliko yoyote au kuingiliwa na mikono ya shetani. Hilo linatokana na vifungu: a- Mbele yake (min bayni yadayhi) b- Nyuma yake (wamin khalfihi) c- Amevizunguka walivyokuwanavyo (wa ahaatwa bima ladayhim.) Kifungu cha kwanza kinaashiria kuwepo walinzi kati ya Mtume na watu. Kifungu cha pili kinaashiria kuwepo walinzi na wajifadhi kati yake na chimbuko la wahyi. Na kifungu cha tatu chaonyesha kuwa kuna wahifadhi ndani ya dhati ya Mtume, hivyo matokeo yake ni kuwa wahyi upo katika amani na usalama hauwezi kuingiliwa na upotoshi kuanzia pale ulipoidhinishwa na chimbuko la wahyi na kuingia ndani ya nafsi ya Mtume mpaka uwafikiapo watu waliotumiwa. 8- Kauli yake: “Na adhibiti idadi ya kila kitu” imeletwa ili kujulisha elimu yake ya kila kitu na kuvizunguka kwake vitu vyote ukiwemo ule wahyi uliopelekwa kwa Mtume na mambo mengine. Allama Tabatabaiy anasema: Hakika ya kauli yake Mtukufu: Wanamfuatilia mbele yake na nyuma yake” mpaka mwisho wa Aya mbili yajulisha kuwa wahyi wa kiungu umehifadhiwa toka mwanzo pale ulipotoka kwenye chimbuko la wahyi mpaka ulipowafikia watu, umehifadhiwa ulipokuwa wateremka mpaka ulipomfikia aliyekusudiwa umshukiye. Ama kuhifadhiwa kwake toka ulipotoka kwenye chimbuko lake mpaka 65


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ulipoishia kwa Mtume kwatosha kuthibitishwa kwa kauli Yake “Nyuma yake”. Ama kuhifadhiwa kwake toka Mtume alipouchukuwa kutoka kwa Malaika wa wahyi huku akiutambuwa bila kuuchukua kimakosa, na kuhifadhika kwake katika kuuhifadhi huku akiwa anauelewa kama alivyofunuliwa bila ya kuusahau au kuubadilisha. Ama kuhifadhika kwake katika kuufikisha kwa watu bila shetani kujiingiza humo, dalili yake ni kauli Yake: “…ili ajuwe kama wamefikisha risala ya Mola wao.” inajulisha kuwa lengo la kiungu la kuwaingiza waangalizi ni ili ajuwe ufikishaji wao wa risala ya Mola wao, yaani ili utimie kivitendo ufikishaji wa wahyi kwa watu, na matokeo yake ya lazima ni kuwafikia, na lau si kuhifadhika kwa mitume katika hatua hizo zote tatu zilizotajwa basi lengo la Mwenyezi Mungu halingeli timia, na hilo liko dhahiri. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuitaja njia nyingine mbali na ile ya kuwaingiza waangalizi ili kulifikia lengo hili, basi hilo limejulisha kuwa wahyi unalindwa na malaika uwapo kwa Mtume, kama ambavyo hulindwa na malaika hao uwapo njiani kumweleka Mtume mpaka umfikiapo, hilo linasisitizwa na kauli yake: “Amevizunguka walivyokuwanavyo”. Na kuhifadhika kwake katika safari yake ya kutoka kwa Mtume mpaka kuwafikia watu, yatosha kuthibitsha hilo kwa kauli Yake: “Na mbele yake” kwa maana ile iliyotangulia. Zaidi ya dalili hiyo ni kauli Yake: “…ili ajuwe kama wamefikisha risala ya Mola wao.” kwa ufafanuzi wake uliotangulia katika kuikurubisha dalili. Kutokana na ufafanuzi huu yazalika maelezo yafuatayo: Mtume huongezewa nguvu ya ismah katika kuuchukuwa wahyi toka kwa Mola wake na katika kuuhifadhi na kuufikisha kwa watu, amehifadhiwa dhidi ya makosa katika pande zote tatu kwa mujibu wa dalili zilizotangulia, kwa kuwa aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ndani ya dini yake kwa watu kwa njia ya wahyi yamehifadhiwa katika hatua zake zote mpaka yawafikie watu. Na miongoni mwa hatua zake ni hatua ya Mtume kuchukuwa wahyi, kuuhifadhi na kuufikisha kwa watu. Ufikishaji wajumuisha kauli na kitendo, kwa sababu katika kitendo kuna ufikishaji kama vile ulivyo katika kauli, 66


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kwa hiyo Mtume ni maasumu hatendi maasi kwa kufanya mambo yaliyo haramishwa na kuacha kutekeleza wajibu wa kidini kwani katika hilo kuna ufikishaji unaopingana na dini. Hivyo yeye ni maasumu hatendi maasi kama ambavyo ni maasumu hakosei katika kuchukuwa wahyi, kuuhifadhi na kuufikisha kwa kauli.63. Raziy amesema ndani ya tafsiri yake: “Watu wametofautiana kuhusu Ismah ya manabii (a.s.), na kauli iliyo madhubuti katika suala hili isemwe hivi: Tofauti katika mlango huu yarejea kwenye sehemu nne....... Ama aina ya pili: Nayo ni ile inayohusiana na kufikisha, umma umeafikiana kuwa wao ni maasumu hawasemi uongo wala kupotosha linalohusu ufikishaji, vinginevyo uaminifu katika utekelezaji ungetoweka. Na wameafikana kuwa kama ambavyo haiwezekani kutokea hilo kwa makusudio pia haiwezekani kwa kusahau. Lakini miongoni mwa watu kuna wanaoruhusu hilo kwa kusahau, wamesema kwa sababu kujihfadhi dhidi ya hilo haiwezekani.�64 Usemi unaoruhusu wao kusahau katika hatua ya ufikishaji ubatili wake uko wazi dhahiri shahiri.

Aya ya pili. Kauli Yake (s.w.t.):

63. Al-mizaan, Juz 2, Uk 123. 64. Tafsir Al-Fakhru Raziy Juz 1, Uk 318.

67


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Watu walikuwa umma mmoja Mwenyezi Mungu aliwapeleka manabii wabashiri miongoni mwao na waonyaji na aliteremsha pamoja nao Kitabu kwa ukweli ili kuhukumu kati ya watu katika mambo ambayo wametofautiana, lakini watu wa Kitabu, baada ya kujiwa na dalili zilizo wazi, hawakutofautiana kati yao, ila kwa sababu ya uovu kati yao, Mwenyezi Mungu kwa rehema zake aliwaongoza waumini kwenye ukweli, kwa yale waliyohitilafiana, kwa kuwa Mwenyezi Mungu huwaongoza awatakao kwenye njia iliyonyooka.” (AlBaqara:213) Aya hizi zabainisha kuwa lengo la kuwatuma manabii ni kuhukumu kati ya watu waliohitilafiana, na makusudio ya hukumu sio nyingine ila ni kuhukumu kwa haki, nako ni sehemu ya ufikaji wa ukweli kwa kadhi bila mabadiliko wala upotoshi. Kisha faida ya hukumu ni kuwaongoza watu kwenye ukweli kwa idhini yake kama lilivyoonyeshwa wazi hilo kwa tamko lake: “Mwenyezi Mungu kwa rehema zake aliwaongoza waumini kwenye ukweli, kwa yale waliyohitilafiana”. Ingawaje anayeongoza kwa ukweli hasa ni Mwenyezi Mungu (s.w.t.) lakini hidaya hutimia kwa njia ya Nabii, na kupitia kwake, na kuthibiti kwa hidaya kwa njia yake kunatokana na yeye mwenyewe kuwa katika haki na mjuzi wake bila upotoshaji. Yote hayo yanalazimu kupatikana ismah ya Nabii wakati wa kupokea wahyi, kuuhifadhi na kuufikisha kwa watu. Kwa jumla Aya yajulisha kuwa Nabii huhukumu kwa ukweli kati ya watu na huwaongoza waumini kwenye haki, na hayo yote, kuhukumu kwa ukweli, na kuwaongoza waumini, kunalazimu yeye mwenyewe awe ni mwenye kuelewa ukweli kama ulivyo, na makusudio ya ukweli hapa si mengine ila ni ule wahyi uliyofunuliwa kwake.

68


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Aya ya tatu Nayo ni kauli Yake (s.w.t.):

“Hatamki kwa utashi wake, huo si kingine bali ni wahyi wafunuliwa.” (An najmu:3-4) Aya hii yaeleza wazi kuwa Nabii hatamki kwa utashi, yaani haongei kwa msukumo wa utashi binafsi. Kwa hiyo makusudio yanaweza kuwa ni yote yatokayo kwake miongoni mwa kauli katika nyanja za maisha kama ulivyo muktadha wa tamko jumuishi. Au yaweza kuwa inahusu yale aongeayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Vyovyote vile itakavyokuwa ni kuwa Aya yajulisha kuhifadhiwa kwake na Ismah yake katika hatua tatu zilizotangulia kutajwa kwenye nyanja za ufikishaji wa risala. Qurtubiy amesema ndani ya tafsiri yake “Hakupotea swahibu wenu wala hakufeli.”

kuhusu kauli yake (s.w.t.):

Imesemwa: Yaani hakupata kuongea maneno ya batili… Kisha yawezekana ikawa huu ni upashaji wa habari kuhusu hali ya baada ya wahyi, na yawezekana ikawa ni utambulisho wa hali yake kwa sura ya jumla...” Na katika kauli yake (s.w.t.): “Hatamki kwa utashi wake, huo si kingine bali ni wahyi wafunuliwa.” Amesema: Kuna maswala mawili: La kwanza: “Hatamki kwa utashi wake” Qutadah amesema: Haitamki Qur’ani kulingana na utashi wake. Na imesemwa: “Kwa utashi wake” yaani kwa matamanio, hilo kalisema Abu Ubeida An nahasu. Kauli ya Qutadah ni bora, na hii (kwa) inakuwa kwenye mlango wake, yaani tamko lake halitokani na rai yake, bali hilo (tamko) ni kwa wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuwa baada yake kumekuja kifungu: “Huo si kingine bali ni wahyi wafunuliwa”.

69


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

La pili: Humo mna dalili inayojulisha kuwa sunna ni kama wahyi ulio teremshwa katika utendaji.65 Na kwa kuwa ismah ya manabii katika hatua hiyo ni miongoni mwa mambo yanayokubaliwa na wahakiki wa wanamadhehebu na itikadi bila upinzani, basi tuelekeze hatamu ya mjadala kwenye mgongano wa rai za wanatheiolojia, japokuwa Shia wana kauli moja tu kuhusu hilo, nayo ni umaasumu wao dhidi ya maasi na uhalifu wa amri zake na makatazo yake.

Hatua ya pili: Ismah ya manabii dhidi ya maasi Umefahamu dalili za ismah ya manabii wakati wa kuupokea wahy, sasa umewadia wakati wa kujadili Ismay yao dhidi ya maasi, na katika hilo tutajadili kwa mitizamo miwili: Akili na wa Qur’an.

Akili inavyoeleza ismah ya manabii: Kwa kweli Qur’an Tukufu inasema waziwazi kuwa lengo la kuwapeleka manabii ni kuzitakasa nafsi za watu na kuzichuja ziwe mbali dhidi ya yale yenye kudharaulisha, na ili mtu apate matukufu humo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawa amenukuu ombi la Ibrahim kwake (s.w.t.):

“Ewe Mola wetu watumiye kati yao mjumbe kutokana na wao ili awasomee Aya zako na awafundishe kitabu na hekima na awatakase, kwa hakika wewe ni mwenye enzi ya juu mwenye hekima.”(AlBaqarah:129). Na akasema (s.w.t.): 65.Tafsiri ya al-Qurtubiy, Jalada.9, Juz 17,Uk 84 - 85.

70


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Mwenyezi Mungu amewaneemesha waumini alipomtuma kati yao Mtume kutokana na wao wenyewe ili awasomee Aya zake na awatakase na awaelimishe kitabu (yaani Qur’an) na hekima japokuwa hapo kabla walikuwa katika upotovu wa wazi”.(al-Imranu:164). Na makusudio ya utakaso ni kuzisafisha nyoyo ziwe mbali na machafu yaaibishayo huku zikiyakuza matukufu, na hii ndiyo inayoitwa “malezi” katika elimu ya maadili. Na hapana shaka kuwa taathira ya malezi ndani ya nafsi yategemea utambuzi wa akusudiwaye kupatiwa malezi kwa kumsadikisha mlezi na kuamini mafunzo yake. Hali hii ya kusadikisha na kumwamini hupatikana kupitia utendaji wa mlezi kwa msaada wa yale ayasemayo na ayatendayo. Hivyo endapo kutakuwa na utengano kati ya kauli na matendo, basi uaminifu kuhusu ukweli wa kauli yake utatoweka na litakalofuata ni malezi kukosa taathira yake, na hapo lengo la kutumwa (manabii) halitotimia. Ukitaka unaweza kusema: Kwa kweli uwiano kati ya kauli ya mlezi na vitendo vyake, ndiyo sababu pekee ya kuvuna uaminifu wa wengine kwa mafunzo ya msuluhishi na mlezi, na lau hakutakuwa na uwiano wala mwafikiano kati ya mawili hayo (kauli na matendo) basi watu watatawanyika na kumkimbia huku wakisema: Lau angekuwa anaamini usahihi wa wito wake mwenyewe basi kauli yake haingekuwa tofauti na matendo yake mwenyewe.

71


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Hoja na jibu: Naam, yawezekana ikasemwa: Ili kumwamini Nabii yatosha kuhifadhika kwake dhidi ya tendo moja tu la maasi, nalo ni uongo, kwani uthibitisho uliotajwa hapo nyuma kwa ukamilifu wake hauthibitishi isipokuwa uhifadhikaji wake dhidi ya uongo tu na si dhidi ya maasi yote. Nasema: Kujibu hoja hii ni rahisi kwa sababu kutenganisha kati ya maasi ni gezi tupu haufai uwe ndio msingi wa malezi kwa sura ya jumla kwa sababu ya ishikali zilizomo ndani ya hoja hiyo. Kwanza: Kwa kuhifadhika dhidi ya maasi ni matokeo ya sababu mbili ambazo tayari tulikwishaziashiria tulipokuwa kukizungumzia ukweli wa ismah, hivyo basi endapo sababu hizo zote zitakuwepo au zikawepo baadhi yake basi uhifadhikaji usio na mipaka utapatikana kwa mtu fulani, na kama si hivyo basi haiwezekani kutenganisha kati ya uongo na maasi mengine, eti mtu ajiepushe na uongo umri wake wote lakini huku akitenda maasi mengine, kwani sababu zinazomsukuma mtu kuyatenda maasi hayo ndio hizohizo zitamsukuma kusema uongo na kujiingiza katika tuhuma. Pili: Kama ingefaa kutenganisha kati ya uongo na aina nyingine ya maasi katika ulimwengu wa uthibiti basi usemi huu “Mlinganiaji hasemi uongo asilani japokuwa anatenda aina nyingine za maasi� hauwezekani kuthibitishwa kwa mlinganiaji na mdai unabii. Itawezekanaje mtu amkanushiye uongo mdai unabii ilihali ajua fika kuwa huyu mdai unabii hutenda maasi mengine yaliyobaki na pia hutenda dhambi mbalimbali. Hata pale atakapodharurika kusema uwongo kwa kigezo kuwa kufanya hivyo kuna manufaa, bado hili litawajibisha kutiliwa mashaka na wasiwasi kwenye maneno, hali hiyo ni hata kama yeye mwenyewe mdai unabii ataeleza waziwazi kuwa kuna mtengano huu. Na kwa jumla ni kuwa: Kwa kweli lengo la kuwatuma Mitume na kuteremsha vitabu ni kuwaita watu kwenye mwongozo wa kiungu ambao 72


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

husimamiwa na manabii na mitume, na lengo hilo halitokamilika ila baada ya watu kumwamini mbebaji wa wito huo, yule aliyetumwa kwa ajili ya hidaya. Kutenda maasi, kujiingiza kwenye dhambi na kwenda kinyume na yatakiwayo na misingi ya tabia njema, huondoa uaminifu nyoyoni na hu ondoa kule kutegemewa. Kwa ufafanuzi huo lajitokeza jawabu la hoja ambayo upotovu wake hautofautiani hata kidogo na hoja iliyotangulia. Huenda ikasemwa, mkanganyo hasa uliyopo kwenye dalili hii ni ile hali ya Nabii kulazimika kuwa msafi wakutojiingiza katika maasi katika jamii. Hali hii hailazimu yeye kutokuasi na kutojiingiza kwenye maasi awapo faraghani, kwani huenda akawa jasiri wa kuhalifu awapo faraghani peke yake. Hivyo kiasi hiki cha usafi katika jamii chatosha kuvuta uaminifu wa watu kwake. Jibu la hoja hii liko wazi kabisa, kwani mfano wa taswira kama hii kumuhusu Nabii kuwa, hutenda maasi faraghani na si hadharani, yamuharibia Nabii uaminifu wake kwa watu, kwa sababu katika hali hiyo ni kitu gani kimzuwiacho kusema uongo hata ajisitiri na kuuficha uongo wake, (ilihali watu wajua fika kuwa yeye husema uongo faraghani), na kwa hilo uaminifu wake utatoweka kwa kila asemalo na atendalo. Zaidi ya hilo ni kuwa anaweza kuwahadaa watu kwa mapambo ya nje kwa kipindi cha muda mfupi lakini si mrefu, kwa sababu hautopita muda mrefu ila yaliyojificha yatadhihiri na siri itafichuka na ukweli utajitokeza, na hatimaye aibu yake itafichuka. Mpaka hapa imedhihiri kuwa imani ya watu kwa manabii hutegemea imani yao na yakini yao juu ya usahihi wa usemi wao na unyoofu wa matendo yao, na hili hutokana na wao kuwa maasumu dhidi ya kutenda kinyume na kuasi barazani na faraghani, kwa siri na kwa uwazi, bila kutofautisha kati ya maasi haya na yale.

73


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kwa sababu ya kutoitia akilini nukta hii ambayo tuliifafanua hapo kabla ndio maana baadhi ya wanavyuoni wa theiolojia wametenganisha na kutofautisha kati ya uongo na maasi mengine katika yale yanayohus tablighi, na kati ya kusudi na kusahau. Kwa mujibu huo amesema ndani ya sherehe ya Al-mawaqif: “Watu wa madhehebu na sheria zote wamekongamana kuwa ismah yao ni wajibu dhidi ya kukusudia katika lile ambalo muujiza umethibitisha ukweli wao humo, kama vile madai ya utume na yale wayafikishayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (kuwaendea viumbe kwani laiti ingeruhusiwa wao kusema ya kwao66 na kuzuwa lolote basi hilo kiakili lingelisababisha kubatilisha dalili ya muujiza, na hilo ni muhali). Na katika kuruhusu kutokea (uongo) kwao (kama walivyosema) kwa njia ya kusahau na kupitiwa, katika hilo kuna tofauti, ustadhi (Abu Is’haqah) na wengi miongoni mwa maimamu wamezuia, kwa sababu muujiza umethibitisha ukweli wao (katika kuzifikisha hukmu, hivyo laiti ingeruhusiwa kinyume katika hilo, basi hali hiyo ingekuwa ni kubatilisha dalili ya muujiza, na hilo haliwezekani. Kadhi (Abubakri) ameruhusu huku aking’ang’ania kuwa halina uhusiano wowote na usadikishaji wa kila kinachothibitishwa na muujiza (kwani muujiza umethibitisha ukweli wake pale awapo na kumbukumbu tena mwenye makusudia. Ama awapo katika hali ya kusahau na utelezaji wa ulimi hapo hapana dalili ithibitishayo ukweli, na wala uongo wa hapo haulazimu kuipinga dalili ya muujiza.)”67 Al-Qaushajiy amesema ndani ya Sharhut-Tajriidi: “Kwa kweli yadhaniwayo kuwa ni maasi kutoka kwa manabii, ima yayatakuwa ni yale yanayopingana na muktadha wa muujiza kama uongo katika yale yanayohusu 66. Sharhul’mawaqif, Juz 8, Uk 263. 67. Sharhul’mawaqif cha Adhdiy Jalada la 8, Uk 264. 74


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

tabliighi au huenda yasiwe hayo‌ Na walio wengi wanashikamana na kauli ya ulazima wa Ismah yao katika yale yanayopingana na muujiza. Kadhi ameyaruhusu katika hali ya kusahau akidai kuwa hilo halitii dosari katika kusadikisha lile linalokusudiwa na muujiza.�68 Tayari huko mwanzo tumeshagusia kauli ya Ar-Razi ndani ya kitabu chake Ismatul-anbiya na madai yake kuwa kuna ijmai kuwa, hairuhusiwi kwao (manabii) kupotosha na kufanya khiyana katika mlango huu, si kwa makusudio wala si kwa kusahau, kwani kama si hivyo basi hapangelibakia chochote cha kutegemewa katika sharia.69

Uthibitisho wa Murtadha Kwa kweli Sayyid Al-murtadha amethibitisha dalili hii kwa ubainisho mwingine nao ni: Sayyid (Q.S) kwa kifupi amesema haya: Kwa kweli kujuzisha dhambi kubwa kunatia dosari lengo la kutumwa Mitume nalo ni kuikubali kauli yao na kutekeleza amri zao, wala nafsi zetu haziwezi kutulia kwa kuikubali kauli yake au kusikiliza waadhi wake kwa utulivu uleule upatikanao kwa ambaye haijuzu kwake chochote miongoni mwa hayo, na hii ndio maana ya kauli yetu: Kwa kweli kutokea kwa dhambi kubwa kwachukiza kukubali. Na rejea ya kuitambua dhambi inayochukiza na isiyochukiza ni ada na kuzingatia lipasalo, hilo si miongoni mwa yaenguliwayo kwa dalili na vipimo, na arejeaye kwenye ada hutambua tuliyoyasema. Kwa kweli hayo ni miongoni mwa yaliyo na nguvu mno yanayochukiza kuikubali kauli, kwani ikiwa hadhi ya madhambi makubwa ndani ya mlango huu haitoizidi hadhi ya upumbavu na kutokuwa na haya na utovu wa nidhamu basi si chini ya hapo. 68. Sharhut-Tajrid cha Al-Qaushajiy, Uk 464. 69. Ismatul-Anbiya cha Al-Fakhru Raziy, Uk 18, chapa ya Jidah. .

75


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Endapo itasemwa: Si tayari watu wengi wamejuzisha madhambi makubwa kwa manabii (a.s.) na hali ikiwa wao hawaoni vibaya kuzikubali kauli zao na kuyatendea kazi waliyoyafanya sheria miongoni mwa sheria, na hilo labatilisha usemi wenu kuwa: Madhambi makubwa yachukiza! Twasema: Swali hili ni la ambaye hakufahamu tuliyoyaeleza, kwa kuwa sisi hatukukusudia kuchukiza kuwa ni kutoweka usadikishaji na yakuwa amri haitotekelezwa kwa sura ya jumla, isipokuwa tulikusudia lile tulilolifasiri, nalo ni: Utulivu wa nafsi kukubali kutoka kwa awezaye kutenda hayo hauwi kwa kiwango kile cha utulivu utokao kwa asiyeweza tenda hayo. Kwa hakika sisi tunakuwa mbali sana kuikubali kauli yake ikiwa anaweza kutenda madhambi makubwa. Kama ambavyo akiwa hawezi kutenda madhambi makubwa tunakuwa karibu mno kukubali kauli yake. Asiyeweza kupata kitu huenda akawa karibu na kitu, kama ajiwekavyo mbali na kisichoweza kuwa mbali naye. Je huoni kukunja uso kwa mualikaji watu kwenye chakula chake na kuto wavumilia kwake kiada kwachukiza kuhudhuria mwaliko wake na kula chakula chake. Na uhudhuriaji na uliwaji chakula vyaweza vikapatikana pamoja na hali tuliyoitaja, na wala hakumtoi katika hali ya kuchukia. Hali ni hivyo hivyo kuhusu ukunjufu wa uso wake na kuonyesha kwake furaha na tabasamu yake, kwakurubisha kuhudhuria mwaliko wake na kula chakula chake. Pamoja na tuliyo yataja mahudhurio yanaweza kukosekana, na wala hayatomfanya asiwe mkaribishaji. Basi hilo lajulisha kuwa lizingatiwalo kwenye mlango wa liwekalo mbali na liletalo karibu ni lile tulilotaja bila kujali kutokea kitendo kinachochukiza au kutotokea kwake. Je ikisemwa: Hii yalazimu madhambi makubwa kutopatikana kutoka kwao katika hali ya unabii tu, ni vipi iwe hayawezi kupatikana kwao kabla ya unabii, ilihali hukumu yake hutoweka kwa unabii ambao watupilia mbali mateso na lawama na hatimaye kutobakia sura inayolazimu kuchukiza! 76


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Twasema: Njia katika mambo hayo mawili ni moja, kwa kuwa sisi tunajua kuwa ambaye ukafiri na madhambi makubwa kwake ni jaizi katika hali fulani japo awe ametubia kutokana nayo na ameepukana na kigezo cha kustahiki mateso, utulivu wa kuikubali kauli yake haupatikani kwa kiwango kile cha utulivu wetu kwa ambaye haijuzu kwake hayo kwa hali yeyote wala kwa sura yoyote miongni mwa sura zake. Na kwa sababu hii hali ya muwaidhi ambaye ni mfanya wito kwetu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ilihali tukiwa twamjua kuwa alikuwa mwenye kutenda dhambi kubwa mtendaji wa mazito miongoni mwa dhambi japo awe ameachana na yote hayo na ametubia kwetu na nafsini mwetu, yenyewe haiwi sawa na hali ya ambaye hatukumzoea ila akiwa msafi wa matendo. Tofauti iliyopo kati ya wawili hawa ni ya dharura (isiohitaji dalili) kabisa kuhusiana na yanayolazimu utulivu na kuchukiza, na kwa ajili hiyo mara nyingi watu waliyemzoea katika hali ya kutenda mabaya hapo nyuma humuaibisha kupitia mabaya hayo japokuwa awe ametubia, na wanajaalia hilo kuwa ni aibu na upungufu utiao dosari yenye kuathiri. Na si kuwa kujuzisha madhambi makubwa kabla ya unabii kwapunguza kuliko kuyajuzisha katika hali ya unabii, na wala si kuwa kwapunguza daraja yake katika mlango wa kuchukiza, na kwa ajili hiyo imekuwa wajibu kusiwe na kitu chochote kinachochukiza, kwa kuwa vitu viwili huenda vikashirikiana katika kuchukiza japokuwa kimoja kina nguvu zaidi kuliko chenzake. Huoni kuwa kukithirisha upuuzi, na kutokuwa na haya na kuendelea hivyo na kukazana katika hilo, bila shaka ni jambo linalochukiza , na uchache wa upuuzi ambao hautokei isipokuwa katika baadhi ya nyakati zenye mwanya mkubwa ni jambo lakuchukiza pia, japo latofautiana na la kwanza katika nguvu za kuchukiza, wala upungufu wake haujaliweka mbali na la kwanza katika mlango huu, bali limeendelea lenyewe binafsi kuchukiza. 77


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na endapo itasemwa: Basi ni vipi mumesema dhambi ndogo haijuzu itokee kwa manabii (a.s.) katika hali ya unabii na kabla yake? Twasema: Njia ya kukanusha madogo katika hali mbili ni njia ile ile ya kukanusha makubwa katika hali mbili ikizingatiwa, kwa kuwa sisi kama tujuavyo aliyetenda makubwa hapo kabla na akawa ametubu na ameyaacha, na ikawa hakuna kigezo kilichobakia pamoja naye anachostahiki kwacho mateso na kulaumiwa, utulivu wetu kwake hautakuwa kama utulivu wetu kwa ambaye hawezi kutenda hayo. Hivyo hivyo tunajua kuwa ambaye anaweza kutenda madhambi madogo miongoni mwa manabii (a.s.) akawa mtenda maovu na mfanya maasi katika hali ya unabii wake au kabla yake, japo yawe yamefanyiwa kafara, bado utulivu wetu kwake hautokuwa kama utulivu wetu kwa ambaye tuna imani naye kuwa yuko mbali na kila machafu na wala hawezi kutenda chochote katika hayo. 70

KUJIBU SWALI LINGINE Huenda ikasemwa: Kwa kweli wenye akili wanatosheka katika kuifikisha mipango yao ya ufundishaji na ya malezi kwa kigezo cha ukweli wake kuwa zaidi kuliko uongo wake, na katika hilo yatosha Mtume awe mtu mkweli mwadilifu, na mwenye kujulikana kuwa ni mkweli muadilifu asiyekuwa maasumu, asiyekuwa mkweli mia kwa mia, asiyekuwa katika upeo wa ukamilifu, na kwa minajili hiyo hapana kimziwiacho Allah (s.w.t.) asitosheke na baadhi ya walio wema ambao mema yao yanayashinda mabaya yao na uthabiti wao unashinda utelezaji wao. Hili ndio swali, ama jibu:

70. Tanzihul-Anbiyai, Uk 4 - 6.

78


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kwa kweli kutosheka kwa wenye akili na kiwango hiki cha wema na uthabiti ni kwa ajili ya sababu mbili: Ima ni kwa kutoweza kwao kuwapata walio kamili miongoni mwa wanajamii, au ni kwa kutosheka kwao kuyafikia malengo yao kwa kiwango mahsusi cha ukweli uliopo. Na hayo yote mawili hayalingani na heshima yake (s.w.t.) kwa kuwa Mola (s.w.t.) anao uwezo wa kuwatuma watu walio na ismah na kuthibitisha malengo yake kwa sura kamilifu. Allama Tabatabai anasema kuhusiana na lengo hili: “Kwa kweli watu wanapitia katika aina ya tablighi zao. Yaani ufikishaji wao na malengo yao ya kijamii kwa kufikisha kwa njia isiyoepukana na upungufu na uzembe katika tablighi, lakini hilo kwao hutokana na mojawapo kati ya mambo mawili ambayo hayafai katika hili tunalozungumzia. Hilo huwa kwa sababu ya msamaha wao ili kufikia malengo, kwa kuwa makusudio yao ni kuyafikia yaliyo mepesi miongoni mwa yatakiwayo, na kuyapata yaliyo rahisi na kuyafumbia macho yaliyo mengi. Na hilo halilingani na heshima Yake (s.w.t.).”71. Kwa ajili ya mitizamo hii ya kiakili twaiona Quran Tukufu inabainisha wazi wazi ismah ya manabii wakati mwingine, na pengine huwa ina ishiria kwa kuwasifu kuwa wao ni waja walioongoka hawatopotoka kamwe. Zifuatazo ni Aya hizo ambazo zahesabika kuwa ni miongoni mwa shuhuda za Qur’ani zilizo wazi mno kuhusiana na ismah ya manabii.

Qur’an yazungumzia Ismah ya manabii dhidi ya maasi Kwa kweli yeye (s.w.t.) ndani ya Kitabu chake Kitukufu anazungumzia sifa hii ya ismah kwa manabii, hilo linathibitishwa na kundi la Aya: 71. Al-mizan, Juz 2, Uk 141. 79


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Aya ya kwanza: “Na tulimpa yeye (yaani Ibrahim kizazi) Is-haqah na Yakubu, wote tuliwaongoza, na Nuhu tulimwongoza hapo kabla, na miongoni mwa dhuria yake Daud, Suleiman, na Ayub, na Yusuf, na Musa na Haruni, ni kama hivi twa walipa watendao mema. * Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema. * Na Ismail na al-Yasaa na Yunus na Lut na wote tuliwaboresha juu ya walimwengu. * Na miongoni mwa baba zao, dhuria zao na ndugu zao, na tuliwachaguwa na tuliwaongoza kwenye njia iliyonyooka” (Al-An’am: 84 - 87.) Kisha awasifu hawa waja wake wateule kwa kusema:

“Hawa ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza hivyo basi kwa mwongozo wao’ongoka. Sema: Sikuombeni ujira (kwa hii-kazi) huu sio, ila ni ujumbe kwa walimwengu.” (Al-An’ aam 90) Aya hii inaeleza kuwa manabii wameongozwa kwa mwongozo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa namna ambayo inawafanya wao kuwa mwongozo na kigezo. Hii ni kwa upande mmoja, na kwa upande mwingine twaona kuwa Allah (s.w.t.) anasema waziwazi kuwa mwenyekuwa ndani ya mwongozo wa kiungu hakuna wa kumpotosha anasema:

“Na ambaye Mwenyezi Mungu amempoteza hakuna awezaye kumuongoza na ambaye Mwenyezi Mungu amemuongoza hakuna awezaye kumpoteza”.(Azumar 36-37). Na katika Aya ya tatu asema wazi kuwa uhalisia wa uasi ni kupotoka kwa 80


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kuwa mbali na msitari wa kati, bali ndio upotovu wenyewe, akasema:

“Je! Sikuwaagiza oh! Ninyi wana wa Adam (kwamba) musimwabudu shetani hakika yeye kwenu ni adui aliye bayana* Na (kwamba) muniabudu mimi, hii ndiyo njia iliyonyooka.* Na kwa kweli amewapoteza kati yenu kundi kubwa je hamkuwa mnatumia akili!” ( Ya syn:60-61). Kwa kuzingatia kundi hili la Aya tatu ismah ya manabii ya dhihiri wazi, na ili kuliweka hilo wazi twasema: Kwa kweli Allah (s.w.t.) katika kundi la kwanza la Aya anaeleza kuwa manabii wao ni viongozi na vigezo na waongofu katika umma, kama ambavyo anaeleza wazi katika kundi la pili la Aya kuwa ambaye ameingizwa ndani ya hidaya ya kiungu hapotei wala hakuna cha kumpoteza. Kama ambavyo (s.w.t.) anaweka wazi katika kundi la tatu la Aya kuwa uasi ndio upotovu wenyewe au ni mwenzi wake wasioachana, akasema: “Na hakika amewapoteza miongoni mwenu”. Upotovu wao haukuwa ila ni kwa sababu ya kuasi kwao na kufanya kwao kinyume na amri na makatazo yake. Ikiwa manabii ni waongofu kwa mwogozo wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na kwa upande mwingine upotovu hauna njia kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amemwongoza, na kwa upande mwingine kila maasi ni upotovu basi faida inapatikana kuwa ambaye hapatwi na upotovu maasi hayamfiki. Na endapo utataka kuhitmisha linalomaanishwa na Aya hizi kwa sura ya kimantiki utasema: Nabii ni mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemwongoza. Na kila aliyeongozwa na Mwenyezi Mungu hakuna cha kumpoteza. Hivyo basi Nabii hana cha kumpoteza.

81


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Aya ya pili Ni kuwa yeye (s.w.t.) anawahesabu watiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume kuwa wao watakusanywa (siku ya Kiyama) pamoja na manabii, wasema kweli, mashahidi na watu wema ambao Mwenyezi Mungu ame waneemesha akasema:

“Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, hao watakuwa pamoja na ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha miongoni mwa manabii watu wakweli, mashahidi, watu wema, (oh) uzuri ulioje wa wenzi hao!” (69:An-nisaa). Kulingana na inavyoonesha maana ya Aya hii, bila ya shaka yoyote manabii ni miongoni mwa watu ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha. Kisha Mwenyezi Mungu analisifu kundi hili lililoneemeshwa na Mwenyezi Mungu kwa kusema:

“Wasio ghadhibikiwa wala si wapotovu” (Al-fatiha-7). Endapo tutaiambatanisha Aya ya kwanza inayoelezea kuneemeshwa kwa manabii, na Aya hii ambayo inawaelezea kuwa wao ni “Wasio ghadhibikiwa wala si wapotovu” tunapata jibu la wazi kwamba manabii ni maasumu wamehifadhika, kwa sababu mtu mwasi ni yule anayeingia kwenye ghadhabu za Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na huwa mpotovu kulingana na kiwango cha maasi yake na uhalifu wake. Kwa sura ya jumla: Asiyekuwa miongoni mwa walioghadhibikiwa na wala si miongoni mwa wapotovu, huyu hamkhalifu Mola wake wala haasi amri 82


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

yake, kwani kuasi kunaleta ghadhabu ya Mola, na kwasababisha kupotoka na kuwa mbali na njia iliyonyooka kwa kadiri ya maasi ya muasi. Aya ya tatu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaelezea kundi la manabii, asema kumuhusu Ibrahim, Ishaqa, Yakub, Musa, Harun, Ismail, na Idirisa:

“Hao ni ambao Mwenyezi Mungu amewaneemesha katika manabii miongoni mwa watoto wa Adam na miongoni mwa tulio wa beba pamoja na Nuhu (ndani ya jahazi) na miongoni mwa dhuria wa Ibrahim na Israeli na ambao tumewaongoza na tumewateuwa wasomewapo Aya ya Arrahmani-mwingi wa rehema- wanaporomoka kusujudu wakilia”.Mariam; 19:58 Aya hii inataja sifa nne za kundi hili la wateule: i. Mwenyezi Mungu amewaneemesha, ii. Tumewaongoza, iii. Tumewateuwa iv. Wameporomoka kusujudu wakilia. Kisha Mwenyezi Mungu anawaelezea watoto wao na vizazi vyao katika Aya inayofuata kwa sifa zinazopingana na sifa zilizotangulia, Anasema:

“Baada yao waliacha kizazi kilichoacha Swala na wakafuata mata83


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

manio ya nafsi watakuja kupata malipo ya upotevu wao.” Maryam 1959 Twashuhudia hapa kuwa Mtukufu anawasifu watoto wao kwa sifa tatu zinazopingana na sifa za baba zao, nazo ni: i. Wameacha Swala, ii. Wamefuata matamanio, iii. Wataingia kwenye adhabu ya upotevu. Na kwa mujibu wa hukumu ya kupambanisha kati ya sifa basi manabii wanakuwa si miongoni mwa walioacha swala, na wala hawakufuata matamanio ya nafsi, kwa hiyo matokeo yatakuwa: Wao hawatopata adhabu ya upotevu. Na kila ambaye huwa hali yake ni hiyo basi huyo ni maasumumwenye kuhifadhika dhidi ya ufanyaji kinyume, na amehifadhika dhidi ya kutenda maasi, kwa sababu kimsukumacho kuasi mpaka aingiye kwenye maasi ni kufuata matamanio ya nafsi, na ndipo huipata athari ya upotevu wake. Aya ya nne: Kwa kweli Qur’an Tukufu yawataka Waislamu kufuata athari za Nabii kwa ibara na maneno aina kwa aina asema (s.w.t.):

“Sema; Mkiwa mnampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni mimi Mwenyezi Mungu atawapendeni na atakughufirieni dhambi zenu na Mwenyezi Mungu ni mwenye kughufiria sana na mwenye huruma. * Sema, mumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, wakigeuka hakika 84


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Mwenyezi Mungu hawapendi makafiri.”(Al-Imran:31-32). Na pia asema :

“Ambaye yuamtii Mtume kwa kweli atakuwa amemtii Mwenyezi Mungu”. (An-nisaa:80). Na asema katika Aya ya tatu:

“Na mwenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akamwogopa Mwenyezi Mungu na kutenda takwa, basi hao ndio walio fuzu.” (An-nur :52). Kama ambavyo (s.w.t.) anawalaumu wale wanaodhani kuwa ni wajibu juu ya Nabii afuate rai ya walio wengi na aitii, akasema:

“Juweni kuwa kati yenu kuna mjumbe wa Mwenyezi Mungu, lau angekutiini katika mambo mengi mungeangamia.”(Al-hashr:7) Matokeo yanayopatikana kwa mchujo wa maneno ni: Aya hizi zinaagiza kumtii Nabii na kumfuata bila mipaka wala sharti, na ambaye utii wake umekuwa wajibu kwa sura isiyo na mipaka yaani bila ya kubagua au sharti, ni wajibu awe maasumu hafanyi maasi na amehifadhika dhidi ya makosa na utelezaji. Ufafanuzi wa hilo ni kwamba: Daawa wa Nabii hutimia kwa mojawapo ya mambo mawili: Kwa tamko au tendo. Na daawa ya kuandika yarejea 85


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kwenye moja ya hayo mawili, hivyo lau Nabii atakuwa mkweli kwenye kila analolingania kwa ulimi wake, mdomo wake na kalamu yake, na yakawa hayo yanaafikiana na ukweli wa mambo huku hayawi kinyume hata chembe, basi amri ya kumfuata itakuwa sahihi na kumtii itakuwa ni kumtii Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kama alivyo sema:

“Na anayemtii Mtume kwa kweli amemtii Mwenyezi Mungu.� (Annisaa; 4:80) Ama akiwa baadhi ya anayolingania kwa tamko na kwa kitendo na kwa maandiko yako kinyume na uhalisia wa mambo na yapo kinyume na anavyoridhiya Mwenyezi Mungu (s.w.t.), katika hali kama hiyo inabidi wito wa kumtii Nabii uambatane na mipaka au sharti, vitakachoondoa sura hii na kiwango kile ambacho humo uhalifu huu unapatikana, kwa hiyo hukumu ya kumfuata bila mipaka yaweka wazi kuwa daawa yake na amri zake kwa kauli na vitendo ni mwenzi wa uhalisia na havitofautiani hata chembe, hakuna tofauti kati ya daawa ya kauli au ya kitendo. Kwa kuwa daawa kwa njia ya kauli na vitendo ni miongoni mwa sababu zenye taathira kubwa katika malezi na mafunzo na ni miongoni mwa sababu zenye kuchukuwa nafasi imara zaidi ndani ya nafsi, kwa hiyo kila kazi itokayo kwa Mitume watu huikubali kwa hamu kubwa na kuharakia kuitekeleza na kufuata athari yake katika nyanja hizi. Na vikiwa vitendo vya Nabii na kauli zake maisha yake yote vyaafikiana na radhi zake na vyaafikiana na hukumu yake, amri ya kumfuata katika matendo na kauli ni sahihi. Ama zikiwa kauli zake na vitendo vyake haviafikiani na uhalisia katika baadhi ya nyakati, na vina ishara ya makosa na maasi, basi amri ya kumfuata na kuchukuwa mwongozo wake bila mipaka haingekuwa sahihi. Vipi iwezekane kupatikana uhalifu kwake ilihali Mwenyezi Mungu amemsifu kuwa yeye ni kigezo chema kwa kusema: 86


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Kwa kweli mmekuwa na kiigizo chema katika Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa ambaye anataraji kwa Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akawa amkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi�.(Alahzabu:33: 21) Hivyo basi yeye kuwa ni kigezo chema katika nyanja zote haito kubalika ila akiwa maasumu aliyehifadhika katika nyanja zote, kinyume na anaye kuwa maasumu kaitika baadhi ya nyanja na si kigezo chema katika nyanja zingine. Kwa mujibu huo yeye ni maasumu mwenye kuhifadhika dhidi ya uhalifu, uasi, ukoseaji na utelezaji. Ukipenda utasema: Lau ukiwa watokea uasi na uhalifukwa Nabii: Kwa upande mmoja ni wajibu juu yetu kumfuata na kumtii na kufuata nyayo zake, na kwa kuwa jambo lililotendwa au kusemwa na yeye ni ovu inakuwa haramu kumfuata na ni wajibu kuwa kinyume naye, hapo italazimu kutoa amri juu ya mambo mawili yanayo pingana. Kauli isemayo kuwa ni wajibu kumfuata khususan katika yale ambayo umethibiti uafikiano wake na sheria au katika yale ambayo haijajulikana kuwa katika hayo kahalifu sheria, hii ni kinyume na amri za Aya zinazo amrisha kumfuata bila mipaka na bila ya tofauti kati ya kitendo hiki na kitendo kile, na wakati huu na wakati ule. Na maeneo haya ni miogoni mwa maeneo ambayo hali ya maudhui na ukubwa wake hufichuka na kuwa inaoana na hukumu kwa kule kuifanya hukumu kuwa pana bila mipaka, na hali hiyo yapatikana katika maeneo mengi katika hukumu za kifiqhi. Wanazuoni wa usululfiqhi wameizungumzia tafiti hii katika tafiti za Aamu (ujumuishi) na Khaasu (uhusishi) na hivyo kutokana na hukumu kutokuwa na mipaka wanatam87


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

bua na kufichua kuwa maudhui ni pana, kama mfano wa kauli: “Mwenyezi Mungu awalaani banii Umayyah wote”, hivyo kupitia ile hali ya kutokuwepo mipaka kwenye kauli hiyo huthibitishwa kuwa maudhui ya laana ni pana na yajulisha kuwa hakuna muumini kati yao, kwani kama si hivyo basi hukumu ya bila mipaka haingefaa hapa. Raziy amesema ndani ya kitabu chake (Ismatul-anbiya): “Hoja ya nne lau ufasiki ungetokea kwa Muhammad (s.a.w.) tungekuwa tumeamrishwa kumfuata katika amri hii, na hilo haliruhusiwi. Au tuwe hatuamuriwi kumfuata, hili pia ni batili kulingana na kauli yake (s.w.t.):

“Sema: Ikiwa nyinyi mnampenda Mwenyeezi Mungu, basi nifuateni Mwenyeezi Mungu atawapenda na atawasamehe madhambi yenu, na Mwenyeezi Mungu ni Mwingi wa msamaha, Mwenye kurehemu. (AlImrani:31) na kulingana na kauli yake Mtukufu: “Mfuateni” na maadamu kutokea ufasiki kuna ababisha haya mawili ambayo ni batili imebidi kutokea ufasiki kwake kuwe muhali.”72 Aya ya tano Mwenyezi Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anaongelea kuhusu Shetani aliyefukuzwa kuwa amesema: “Naapa kwa uwezo wako nitawapotosha wote isipokuwa waja wako wateule wenye ikhlaswi miongoni mwao .” (Swad: 83 - 84.) Na anasema pia: 72. Ismatul-Anbiyai cha Fakhru Raziy. Uk 20.

88


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Oh Mola wangu kwa kuwa umenipotosha nitawapambia ardhini na nitawapotosha wote.* Isipokuwa waja wako walio na ikhlaswi miongoni mwao.” (Al-Hajar: 39-40). Kwa hiyo Aya hizi zote na zilizo mfano wa hizi zinaongelea usafi wa alMukhlaswina kuwa hawapotoshwi na shetani na kuwa hawakokoti kwenye njia za giza. Ufafanuzi wake: Neno ghayu mara hutumika kwa maana ya kinyume na mwongozo na kulitia jambo giza. Na pengine humika kwa maana ya kuharibika kitu. Ibnu Farisi amesema: Kwanza al-Ghayyu ni kinyume na mwongozo, na kutojua jambo, na kuingia sana katika batili. Husemwa: ghawa yaani amepotoka yaghwi anapotoka, ghayyan upotovu. au kujiingiza sana katika batili. Mshairi amesema:

(Fa man yulqi khairan yahmadunnasu amrahu. Waman yaghwi la ya adam alalghayyi laaiman) “Mwenye kuleta kheri watu watalihimidi jambo lake. Na mwenye kupotoka hakosekani wa kuulaumu upotovu.” Na hilo neno kwetu latokana na neno: Ghiyayah, ambayo ni ukungu na giza linalofunika kitu na giza linalogubika katika hali hiyo, kama kwamba mtu mpotovu amegubikwa na kisichoweza kumfanya aone njia ya ukweli. Na maana ya pili ni kama wasemavyo: Ghawiyalfaswilu: “Ameharibika mtoto wa mnyama”, endapo atakithirisha kunywa maziwa na kuharibika 89


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

tumbo lake. Na chimbuko la neno ni-: Alghawa.73 Kwa hiyo ni sawa neno ghiwayatu katika Aya hizi mbili likifasiriwa kwa maana ile ya kwanza kama ilivyo karibu mno au kwa maana ya pili, badohao waja ambao ni mukhlaswiin, watakuwa ni maasumu wametakaswa hawajagubikwa na hali ya ukungu na giza maishani mwao, pia hawatendi jambo la ufisadi. Kukanusha mawili yote kwalazimu ismah, kwa sababu mwasi hufunikwa na ukungu wa ujinga na giza la batili, kama ambavyo elimu yake uharibika kwa kuhalifu. Ndiyo kuthibitisha ghiwaya -giza au ukungu- hakulazimu kuthibitisha maasi, kwa sababu kuhalifu amri za mwongozo ambazo hazijengeki isipokuwa kwa lengo la nasaha na mwogozo, ingawaje kwalazimu kufunikwa na ukungu maishani na kuharibika kwa amali, lakini hakulazimu kuasi na kuvuka mipaka, hali ambazo ni mambo mawili ambayo ndiyo msingi wa kuthibiti maasi. Kwa kadiri itakavyokuwa ni kuwa, yaliyokuja katika kundi la Aya hizi yapo katika daraja ya udhibiti usio na mipaka katika hali ya hawa mukhlaswiina. Kwani ile hali ya wao kutakasika dhidi ya ghiwaya- giza au ukungu- yalazimu utakasifu wao dhidi ya maasi. Na kuna Aya zingine zinaleta majina ya mukhlaswina na kuwasifu zikisema:

“Wakumbuke waja wetu Ibrahim Is-haqah na Yakub wenye nguvu na busara.*Kwa hakika sisi tumewachaguwa kwa (lengo maalumu nalo ni) kupiga mbiu ujumbe (wa nyumba ya akhera).*Na kwa hakika wao kwetu ni miongoni mwa wateuliwa wema.*Na mkumbuke Ismaili na 73. Maqayisul-Lughah, Juz 4, Uk 399 - 400. 90


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

al-Yasaa na Dhilkifli wote ni miongoni mwa watu wema.” (Swad: 45 48). Kwa hiyo kauli yake (s.w.t.): “Kwa hakika sisi tumewachaguwa kwa (lengo maalumu nalo ni) kupiga mbiu ujumbe (wa nyumba ya akhera)” ni dalili bora ya kuwa watajwa ndani ya Aya hizi kuanzia Ibrahim na kizazi chake, wote ni miongoni mwa mukhlaswiina ambao Aya zimewatolea ushuhuda kuhusu usafi wao wakiwa mbali na potosho la Shetani, ushuhuda ambao walazimu kuwaepusha na uasi na uhalifu. Ndiyo kundi hili la Aya halijulishi ismah ya manabii na Mitume wote isipokuwa pale tu tusipotenganisha, kwani wanavyuoni wanaafikiana katika mojawapo, ima ismah au kutokuwa na ismah, wala hakuna anayetenganisha kati ya Nabii na Nabii mwingine, kwa maana aithibitishe ismah kwa baadhi ya manabii na aikanushe kwa baadhi ya wengine. Haya ni baadhi tu ya yale yanayoweza kuwa dalili kuhusu ismah ya manabii, na bado zimebaki Aya kadhaa nyingine ambazo yawezekana kuzitumia kama dalili kuhusu ismah, mfano kauli Yake (s.w.t.):

“Na baadhi ya baba zao, vizazi vyao na ndugu zao na tumewachaguwa na tumewaongoza kwenye njia iliyonyooka.” (Al—Anaam:87). Kwa sababu makusudio ya kuchaguwa ni kuchaguwa kwa ismah, ingawa yawezekana ikawa kwa ajili ya unabii. Na maongezi hapa ni katika kuchaguwa sio kuongoza. Na mfano kama huo ni kauli Yake (s.w.t.):

91


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Hao ndio aliowaneemesha Mwenyeezi Mungu, miongoni mwa Manabii, katika kizasi cha Adamu, na katika kizazi cha wale tuliowachukua pamoja na Nuhu, na katika kizazi cha Ibrahimu na Israeli, na katika wale tuliowaongoza na kuwachagua. Wanaposomewa Aya za Rahman huanguka wakasujudu na kulia.� (Maryam:58)

HOJA YA WAPINGAO ISMAH Umezitambua Aya zinazothibitisha ismah ya manabii katika nyanja zifuatazo: i. Kuupokea wahyi, ii. Kuuhifadhi iii. Kuufikisha kwa watu, iv. Kuutekeleza kivitendo. Lakini kuna Aya huenda zikamchanganya mtu kwa mtizamo wa mwanzo kuwa hali ni kinyume na zilivyoonyesha waziwazi Aya za mwanzo. Baadhi ya vikundi vya kiislamu vinavyojuzisha maasi kwa manabii katika sura zake tofauti wamezitumia kwa kuzifanya kisingizio na kushikamana nazo. Aya hizi ziko katika makundi: La kwanza: Ambazo maana yake ya dhahiri inagusa ismah ya manabii wote. La pili: Ambazo zinagusa ismah ya baadhi yao mfano wa Adam na Yunusi. La tatu: Zinazoelezea kuwa Nabii mtukufu (s.a.w.w.) sio maasumu. Hivyo basi ni juu yetu kuzifanyia darasa Aya za aina hii mpaka ukweli ujitokeze kwa mandhari yake ya wazi kabisa.

92


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Kundi la kwanza: Katika kundi hili kuna kauli yake (s.w.t.):

“Hatujapata kutuma kabla yako isipokuwa-tuliwatuma - wanaume twawafunulia miongoni mwa watu wa miji, je hawajatembea ardhini ili waone mwisho wa waliokuwa kabla yao, na nyumba ya Akhera ni bora kwa waliofanya uchaji, je hamzingatii.* Mpaka Mitume walipokosa matumaini (na watu wao) na walidhania kuwa wamefanywa kuwa waongo hapo msaada wetu uliwafikia wakaokolewa tuwapendao, na adhabu yetu haitoepushwa mbali na watu waovu.” (Yusuf: 109 - 110) Wanaosema manabii hawana ismah wamejenga hoja kwa maana ya dhahiri ya Aya wakisema kuwa nomino tatu katika kauli yake: “Na walidhania kuwa wamefanywa kuwa waongo” zinarejea kwenye nomino Mitume, hivyo linalojulishwa na Aya ni: Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na manabii wake walikuwa wanawaonya watu wao, na watu walikuwa wana wapinga kwa upinzani mkali kabisa, na Mitume walikuwa wanawaahidi waumini msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ushindi dhidi ya makafiri, na walikuwa wana waahidi makafiri kuwa watahiliki, na kuangamia, lakini usaidizi ulioahidiwa ulipochelewa, huku makafiri waki93


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

wa hawajaadhibiwa ndipo Mitume wakadhania kuwa wamedanganywa walichoahidiwa kutoka kwa Mwenyezi Mungu, nacho ni kuwa atawasaidia Waislamu na kuwahilikisha makafiri. Inavyojulikana ni kwamba dhana hii ni dhana batili sawa iwe kwa namna ya kutambua na uyakini au kwa namna ya kutazamia tu na kwa mwelemeo wa kinafsi, yenyewe ni itikadi batili haiendani na ismah. Na endapo wataka kuitafsiri Aya basi yakupasa uainishe marejeo ya nomino, yakubidi useme: Tulipochelewesha adhabu kwa umma uliopita, Mitume walidhania kuwa wao wamedanganywa (kwa kitenzi ambacho hakutajwa mtendaji wake) ahadi walio ahidiwa, ya usaidizi kwa waumini na maangamizi kwa makafiri. Kwa ajili hii jibu lolote kutoka kwa Shia wasemao kuwa Mitume ni maasumu litakalokuwa kinyume na dhahiri hii litakuwa si zito, bali ni lazima jibu lioane na dhahiri hii. Yafuatayo ni majibu yaliyotajwa ndani ya tafsiri mbalimbali La kwanza: Kwa kweli hizo nomino tatu zarejea kwa Mitume ila tu ahadi ambayo Mitume walidhani kuwa wamedanganywa ni kule kujionyesha kwa wengi miongoni mwa waumini kuwa wao ni waumini wa kweli na kujigamba kwao kuwa wana moyo wa dhati kwao, hapo Mitume walifanya taswira kuwa kujionyesha kwa hawa kuwa wana imani kulikuwa ni uongo na batili. Kama kwamba wao walifanya taswira kuwa watu wao ambao waliwaahidi kuwaamini imani waliwaenda kinyume na ahadi walidanganya kwa kujionyesha kuwa wana imani.74 Sura hii ya jibu ameitaja Al-Fakhru Raziy katika tafsiri yake na aliiona kuwa ni nzuri na aliijengea jinsi ya kuisoma hivi: (kudh dhibuu) kwa tashdidi. Akasema: “Ama usomaji wa tashdidi una sura mbili: Ya kwanza: neno dhwanu kwa maana ya yakini yaani wameyakinisha 74. Majmaul-Bayani Jalada 3. Uk 271. 94


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kuwa uma umewadanganya uongo ambao imani haitopatikana kwao baada ya hapo, basi ndipo walipowaombea vibaya. Mara nyingi ndani ya Qur’an dhana huja kwa maana ya elimu. Ya pili : Dhana huwa kwa maana ya kukisia au kuchukulia, mpaka walipo kata tamaa Mitume dhidi ya kuamini kwa watu wao ndipo wakadhania kuwa wale waliokuwa wamewaamini wamewadanganya. Taawili hii imenakiliwa kutoka kwa umul’Muminina Aisha, nayo ni miongoni mwa sura nzuri zilizopata kutajwa katika Aya hii. Ameeleza Ibnu Abiy Mulaika amenakili kutoka kwa Ibnu Abbasi (r.a) kuwa amesema: “Mitume walidhania kuwa wamefanywa waongo kwa kuwa wao ni wanadamu, huoni kauli yake: Mpaka aseme Mtume na ambao waliamini pamoja nae lini itakuja nusura ya Mwenyezi Mungu.” Akasema: Nilimwambia hilo Aisha naye alikanusha na akasema: “Mwenyezi Mungu hakupata kumuahidi Muhammadi (s.a.w.) kitu ila alikuwa anajua kuwa atamtekelezea, lakini majaribu yalikuwa yakiendelea kwa manabii mpaka wakahofia kufanywa waongo na wale waliokuwa wamewaamini.” Taawili hii na kanusho hili kutoka kwa Aisha viko katika upeo wa uzuri .”75 Al-Qurtubiy amesema katika kuitafsiri Aya hii: “Maana yake ni: Hatukuwatuma kabla yako ewe Muhammad isipokuwa watu wanaume kisha hatukuziadhibu umma zao kwa adhabu mpaka mitume walipokata tamaa, yaani walitokwa na matumaini ya kuamini kwa watu wao na walidhania kuwa watu wao wamewafanya kuwa waongo, yaani waliyakinisha kuwa watu wao wamewafanya kuwa waongo. Na imesemwa maana yake ni kuwa: Walidhania kuwa waliowaamini katika umma wao wamewadanganya.76 75. Tafsiiru Al-Fakhru-Raaziy, Juz.5, Uk 179. 76. Tafsiirul-Qurtubi, Juz.9,Uk. 275 . 95


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na katika tafsiri Addurul-manthur: Ametoa Abu Ubaida na Annajariy, Annasaiy, Ibnu Jariri, Ibnul-Mundhir, Ibnu Abiy Hatim, Abu Sheikh, na Ibnu Mardawayhi kwa njia ya Urwa kuwa yeye alimuuliza bibi Aisha kuhusu kauli yake: “Mpaka Mitume walipokosa matumaini” Akasema: Sema walidanganyika au walidanganywa! Bibi Aisha akasema: “Walidanganywa..…” Nikasema huenda walifanywa waongo, Akasema: “Najikinga kwa Mwenyezi Mungu, Mitume hawakuwa wakimdhania hivyo Mola wao…”.77 Jibu hili japo kuwa ni jibu lenye nguvu, kwa kuwa humo hamna mtengano kati nomino kama ilivyo ndani ya baadhi ya majibu yajayo lakini kinacholipinga jibu hili ni ule umbali wake dhidi ya maana dhahiri ya Aya, kwani ndani ya Aya hiyo hakuna athari ya imani ya lile kundi dogo hata iwe yaambatana na udanganywaji katika kauli yake (s.w.t.): (qad kudhibu). Na ukitaka utasema: Mwanzoni mwa Aya wala katikati yake hakuna kinachoonyesha kuwa idadi ndogo iliwaamini Mitume na walijionesha imani na kukapatikana kutoka kwao kitu kilichowafanya manabii wadhani kuwa wamedanganywa hata isihi kusemwa: Linacho ambatana na ukadanganywa ni hiki (kitendo cha kundi dogo kuamini). Bali lililosemwa mwanzoni mwa Aya na katika jumla ya maneno yake ni kule kufanya kinyume kwa kikundi kilichopetuka miongoni mwa kaumu za manabii, ukaidi wao na kung’ang’ania kwao ubishi mbele ya manabii wa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwani Mwenyezi Mungu anasema:

“Na hatukupeleka (Mtume ) kabla yako isipokuwa wanaume tuliowa77. Tafsiiru Adurul-Manthur, Juz. 4, Uk 40

96


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

funulia Wahyi miongoni mwa watu wa mijini. Je hawakutembea katika ardhi wakaona jinsi ulivyokuwa mwisho wa wale waliokuwa kabla yao? Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wamchao, Je, hamfahamu?(Yusuf:109 ). Na kauli Yake hii “Na nyumba ya Akhera ni bora kwa wale wamchao” peke yake haitoshi kuifanya imani yao iwe imeambatana na udanganyifu, kwa kuwa hapo itabidi Aya igusiye imani ya kile kikundi na igusie utokeaji wa ambalo linawajibisha manabii wawadhanie kinyume na walilolidhihrisha ili isihi kusema kuwa Mitume walidhania kuwa wale waliojionyesha kwa imani walifanya udanganyifu kwa kudai kwao kuwa wao ni waumini wa Mitume. Zaidi ya hapo ni kuwa: Jibu hili halisahihishi ismah isiyo na mipaka kwa manabii, kwani kutokana na jibu hili dhana ya manabii kuwa kikundi hicho kidogo hakina imani inakuwa ni ya makosa, na madai ya kundi hilo kuwa wana imani yanakuwa ni ya kweli. Na hili kwa upande fulani laondoa heshima ya manabii, kwa kuwa wao wanawaza kinyume na hali halisi, na wanamdhania Mwislamu kuwa ni kafiri. Na pia jibu lile halina uwiano na mwisho wa jumla kwa kuwa Yeye (s.w.t.) anasema baada ya jumla ile: “Hapo msaada wetu uliwafikia wakaokolewa tuwapendao” ilihali uwiano wa jibu hili ni kusema: “Lakini umewabainikia Mitume ukweli wa madai ya waumini kwa hiyo aliokolewa tumpendaye wala ukali wa adhabu yetu hauepushwi mbali na waovu.”. La pili: Kwa hakika maana ya Aya ni: Umma ulidhania kuwa Mitume wamedanganya habari walizozitoa kuwa Mwenyezi Mungu atawasaidia wao na atawahilikisha maadui zao. Sura hii ndiyo iliyoelezwa kutoka kwa Said bin Jubairi, na Allama Tabatabaiy akaichagua, kwa hiyo Aya inalenga kuwa Mitume wanapotokwa na matumaini ya watu hao kuamini, hili ni kwa upande mmoja na kwa upande mwingine, kwa sababu ya kuchelewa 97


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

adhabu watu walidhania kuwa Mitume wamedanganya, yaani wametoa habari ya uongo kuhusu kusaidiwa waumini na kuadhibiwa kwa makafiri, kisha baadaye msaada wetu ulikuja na kwa huo tunawaokoa tuwapendao nao ni waumini wala ukali wa adhabu yetu hauepushwi mbali na waovu. Al-Fakhru Ar-Razi amesema ndani ya tafsiri yake kulingana na usomaji wa kudhibu kwa tahfifu –bila shada -: “Na maana ya takhfifu ni kwa sura mbili: Moja ya hizo ni: Dhana imetokea kwa kaumu hiyo ya watu, yaani mpaka Mitume walipotokwa na matumaini ya kuamini kwa kaumu hiyo, ndipo kaumu ikadhania kuwa Mitume wamesema uongo katika ahadi za msaada na ushindi walizozitoa ).78. Na Aya zimejulisha kuwa umma zilizopita zilikuwa zinawanasibisha manabii na uongo, Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema katika kisa cha Nabii Nuh (a.s.) akielezea kauli ya kaumu yake:

“Basi tunakuoneni kuwa ni waongo” (Hud:27) Hivyo hivyo katika kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu Hud na Nabii Swaleh (a.s.). Na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema katika kisa cha Nabii Musa (a.s.):

“Firauni alimwambia Musa: Ewe Musa mimi nina yakini kuwa wewe umerogwa” (Al-Israa :101).79 Na Qurtubiy amesema katika tafsiri yake: “Imesemwa maana yake ni: Nyumati zinadhani kuwa Mitume wamedanganya katika ahadi zao kuwa watanusuriwa…”80. 78. Tafsiirul-Fakhru Raaziy, Juz.5,Uk.179. 79. Al-Mizan, Juz 11, Uk 307. 80. Tafsiirul-Qurtubi, Juz.9, Uk 275. 98


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Wala mushkeli haukujificha katika jibu hili, kwa kuwa inaonyesha wazi kuwa nomino iliyoko kwenye neno ‘dhwannu’ inarejea kwa ‘Mitume’ ambalo ni neno lililoitangulia, na kuirejesha kwenye neno ‘Watu’ ni kinyume na dhahiri na ni kinyume na balagha, wala katika Aya yenyewe hakuna usemi uhusuo tamko hili (Watu) ili liwe marejeo ya nomino iliyopo katika kitenzi ‘dhwannu’. Zaidi ya hayo ni kuwa, ushahidi aliotumia ambao ni yale yaliyokuja katika kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu, Nuh (a.s.) hayafungamani na aliyodai, kwani maana ya:“Basi tunakuoneni kuwa ni waongo” ni kuwa watu waliwadhania Mitume wenyewe ndiyo waongo na kwamba waoMitume walikusudia kuongea yaliyo kinyume na ukweli. Na kilichotajwa katika Aya inayojadiliwa sio kuwa Mitume waongo bali kuwa wao wamedanganywa yaani wameahidiwa uongo na wameambiwa kauli isiyo ya kweli, japokuwa wao wenyewe walijiona wakweli kuhusiana na walisemalo. Umbali ulioje kati ya maana hizi mbili!. Ar-Razi ameisema ishkali hii katika tafsiri yake kuwa watumiwa ujumbe hawakutajwa, basi vipi itakuwa sahihi nomino irejee kwao? Akasema: “Kama itasemwa: Katika ibara zilizotangulia watumiwa ujumbe hawajatajwa, basi vipi itafaa nomino hii irejee kwao? Tutasema: Kumtaja aliye tumwa kwajulisha waliotumiwa, na ukitaka utasema: Kwa kweli utajo wao umefanyika katika kauli yake: “Je hawakutembea katika ardhi....”, kwa hiyo nomino inarejea kwa wale waliokuwa kabla yao waliowafanya Mitume waongo, na dhana hapa ina maana ya taswira na kukisia”.81 Lakini jibu hili la kanusho kutoka kwa Bw. Raziy ni kinyume na dhahiri na ni kinyume na kanuni ikubaliwayo ya kuirudisha nomino au kiwakilishi kwenye jina la karibu mno, ilihali si kwamba nomino ameirejesha mbali tu bali zaidi ya hapo ameirejesha kwenye kitu kisichotajwa waziwazi isipokuwa kimeashiriwa kwa umbali usiyokuwa na mahusiao na nomino. 81.Tafsiiru ya Al—Fakhrur Raziy Jalada.5, Uk. 179. 99


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

La tatu: Riwaya iliyonukuliwa kutoka kwa Ibnu Abbas kuwa Mitume walipodhoofika na kushindwa walidhania kuwa wamefanyiwa kinyume na ambalo Mwenyezi Mungu aliwaahidi nalo ni ushindi. Akasema walikuwa wanadamu kisha akasoma kauli yake: “Walitikiswa mpaka akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu.” Al-Fakhru Ar-Razi amesema katika tafsiri yake: “Ameeleza Ibnu abiy Mulaika akimnakili Ibnu Abbas (r.a.) kuwa yeye amesema: Mitume walidhania kuwa wamedanganywa kwa sababu wao ni binadamu, huoni usemi wake: “Mpaka akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Lini nusura ya Mwenyezi Mungu....” Lakini yeye ameona dhana hii iko mbali akasema: “Isipokuwa dhana hiiiko mbali kwa kuwa muuminu haimfai amdhaniye Mwenyezi Mungu uongo bali kwa dhana hiyo anatoka nje ya imani basi itakuwaje hali kama hii kwa Mitume!” 82 Kadhalika Bw. al-Qurtubiy ameipokea dhana hii ndani ya tafsiri yake, amesema: “Na katika riwaya ya Ibnu Abbas: “Mitume walidhania kuwa Mwenyezi Mungu amekwenda kinyume na aliyowaahidi. Na imesemwa: Riwaya hii haikusihi, kwa kuwa Mitume hawadhanii dhana kama hii, na mwenye kudhani dhana hii hawezi kustahiki nusura, basi itakuwaje aseme: “Hapo msaada wetu uliwafikia”83. Mwandishi wa kitabu Al-Kashaf amesema kuhusu Aya hii: “Endapo riwaya hii itakuwa sahihi kutoka kwa Ibnu Abbas dhana anayokusudia itakuwa ni mawazo yanayoingia akilini na kugusa moyoni, yafanana na wasiwasi na maneno ya ndani ya nafsi kama walivyo wanadamu, ama dhana ambayo ni kuupa uzito upande mmoja kati ya pande mbili hali hiyo hairuhusiwi kwa yeyote katika Waislamu sembuse manabii wa Mwenyezi Mungu ambao ndio wamtambuao Mola wao zaidi kuliko watu wengine, na 82. Tafsiirul-Fakhru Raaziy, Jalada.5,Uk179. 83. Tafsiirul-Qurtubi Juz.9 Uk 275. 100


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kwamba Yeye (s.w.t.) ameepukana sana na kitendo cha kuweza kwenda kinyume na ahadi, ametakasika dhidi ya aina zote za ubaya.”84 Na pia ameinakili Al-Qurtubiy kutoka kwa Al-Qashiziy Abiy Naswiriy: “Endapo riwaya hii itakuwa sahihi basi haiwi mbali kuwa makusudio ni wazo kuingia ndani ya nyoyo za Mitume bila ya kulitimiza nafsini mwao… na yawezekana ikasemwa: Wamekurubia dhana hiyo, kama usemavyo: Nimefika nyumbani, yaani nimekuwa karibu na kufika.”85 Ar-Raziy ameinasibisha taawili hii na bibi Aisha kuwa dhana maana yake ni kuwaza na kukisia.86 Na tafsiri hii pamoja na maelekezo aliyoyasema Az-zamakhshari japokuwa ni katika tafsiri iingiayo sana moyoni lakini pia hailingani na heshima ya manabii ambao Roho mtakarifu huwaweka sawa na kuwahifadhi wasiteleze na kukosea katika kufikiri na utendaji, na wazo kama hilo ingawaje liko katika sura ya semesho la nafsi na lashabihiyana na wasiwasi lakini haliendani na ismah isiyo na mipaka inayotazamiwa kwa manabii.

La nne, nalo ndilo teule: Kwa kweli mtoa dalili amedai kuwa dhana iliyotajwa katika Aya ni jambo la kimoyo, limezikabili nyoyo za Mitume, na wameidiriki kwa hisia zao na akili zao mfano wa dhana zingine ambazo zazunguka akili za wanadamu na kukolea humo. Ilihali makusudio si hayo, bali makusudio ni kuwa hali ya mambo yaliyowazunguka Mitume ilifikia ugumu na shida kiasi kwamba wakawa wakitamka kwa ulimi wa kimaumbile kuwa ahadi ya msaada tulioahidiwa si ahadi ya kweli. Wala si kwa maana ya kuwa dhana ilikuwa inashawishi roho za Mitume na mioyo yao. Kuna tofauti kubwa kati ya wao kudhania kuwa msaada walioahidiwa na Mola ni ahadi ya uongo, na kati ya hali ya mambo na mazingira yaliyo 84. Al-Kashaafu, Juz. 2, Uk.175. 85. Tafsiirul-Qurtubi, Juz.9, Uk 275. 86. Tafsir Ar-Raziy, Juz 5, Uk 179. 101


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

wazunguka ya kimateso na shida kuwa kama kwamba yaonyesha kwa mtizamo wa awali wa juu juu kuwa ahadi yake (s.w.t.) ni habari isiyo na athari. Hivyo basi kitendo cha mazingira na hali ya mambo iliyokuwa imewazunguka kuonyesha kuwa ahadi si ya kweli ni suala lingine, na kitendo cha manabii kuwa mateka wa dhana isiyokuwa njema ni suala baki. Na ambalo lapingana na ismah ni hili la pili, si lile la kwanza, na mifano kama hii ni mingi katika Qur’an. Miongoni mwa mifano hiyo ni kauli Yake (s.w.t.):

“Na Dhan Nun (Yunusu) alipoondoka hali ameghadhibika na akadhani kuwa hatutakuwa na uwezo juu yake, basi alinadi katika giza kwamba: Hakuna aabudiwaye isipokuwa wewe tu, umetakasika, hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”(al-Anbiyau :87) Kwa kweli Yunus bin Matta ni Nabii aliyekuwa ametumwa kwa watu wa Ninawa. Aliwaita kwenye dini ya Mwenyezi Mungu hawakuamini hapo akamwomba Mwenyezi Mungu awaadhibu, lakini adhabu ilipokuwa karibu nao walifanya toba na waliamini, hapo Mwenyezi Mungu (s.w.t.). aliwaondolea adhabu. Yunus aliwaacha na kuondoka kabla ya kuteremka adhabu akiwa amewakasirikia watu wake akidhania kuwa (s.w.t.) hato mdhiki na kuwa atamponyoka kwa kujiweka mbali naye, hivyo hawezi kumchunga na kumuadabisha kwa ajili ya kule kujitenga na watu wake, huku wakiwa wanaweza kurejea kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kumwamini na kutubia vitendo vyao. Ni dhana ipi hii ambayo (s.w.t.) anaihusisha na Yunus, ilikuwa dhana ya hisia zake? Sisi tunamtukuza na twaitukuza heshima ya manabii wote haiwezekani wahusike na dhana kama hii, ambayo haigongi katika fahamu ya mtu wa kawaida ambaye si Nabii, sembuse kwa manabii!! Bali makusu102


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

dio ni kuwa kitendo chake hiki (yaani kuondoka kwake na kujitenga mbali na watu wake) kilikuwa kinawakilisha taswira kuwa anadhani kwamba Mola wake hatomdhiki, naye atamponyoka kwa kule kuwa mbali naye, hivyo hatokuwa na uwezo wa kumchunga. Kuna tofauti kubwa kati ya kupatikana dhana hii kwenye hisia za Yunusu na kati ya kitendo chake hiki kuonyesha na kuelezea dhana hii kwa kila aliyemtazama na kumshuhudia. Hivyo linalopingana na ismah ni swala la kwanza wala si suala la pili. Na miongoni mwa mifano hiyo ni kauli Yake (s.w.t.) katika Surati alHashr akielezea kuhusu Baniy An-nadhwiri moja ya makundi matatu ya kiyahudi yaliyokuwa yakiishi Madina, na walikuwa na makubaliano na Nabii kuwa wasifanye hiyana na washirikiane katika ustawi wa jamii. Lakini wao waliwasaliti Waislamu na waliwauwa baadhi ya waumini mbele ya macho ya watu na masikio yao. Hivyo Nabii aliwabana, ndipo wakakimbilia kwenye ngome zao, kuhusu hilo anasema (s.w.t.):

“Yeye ndiye ambaye aliwatoa waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu kutoka majumbani mwao mwanzoni mwa mkusanyo hamkudhania kuwa watatoka, nao walidhani kuwa ngome zao zitawakinga dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu aliwajia kwa namna ambayo hawakuiwazia…”( al-Hashr:2) Basi ni dhana gani hii ambayo Mwenyezi Mungu anainasibisha na kikundi hicho! Je walikuwa wanadhania kwa nyoyo zao kuwa ngome zao zitawakinga dhidi ya Mwenyezi Mungu, wazo hilo liko mbali sana kwa sababu wao walikuwa watu wenye imani ya tawhiid na wenye kutambua uwezo wake (s.w.t.), lakini matendo yao na kukimbilia kwao kwenye ngome zao kwa kukabiliana kwao na Nabii ambaye kwao ukweli wa unabii 103


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

wake umewabainikia kulikuwa kunabainisha kuwa wao ndiyo chimbuko la dhana hii na wenye nayo. Na mifano kama hii ni mingi katika mazungumzo ya kawaida kwani sisi tunawasema wanaoangamia duniani na waliozama katika mapambo yake, na wale wanaojenga ngome ndefu na majengo marefu ya pembe za ndovu kuwa, wao wanaamini wataishi milele na maisha ya kudumu, kama kwamba umauti wameandikiwa watu wengine. Hapana shaka kuwa uhusisho huu ni uhusisho unaosadikika lakini tu kwa maana uliyokwishaijua, yaani dhana hii hutokana na matendo yao, nayo ndio chimbuko la uhusisho huu. Kutokana na hali hiyo Aya inalenga kuwa balaa na shida zilikuwa zimewazunguka manabii ndani ya maisha yao yote huku matatizo na majonzi vikiwazidi kutoka kwa wapinzani na wale waliokuwa wakipambana dhidi ya daawa yao, kwa hiyo walikuwa wanaishi kati ya kaumu ya maadui wao. Na waliokuwa wanawaamini manabii walikuwa wachache, kwa hiyo maisha yao yalikuwa yamejaa balaa, misiba, umasikini na madhara kwa hiyo akaleta taswira - sawa awe Nabii au mtu mwingine- kuwa waliyo ahidiwa ni ahadi isiyo sadikika. Lakini hali haikubakia hivi ilivyo, ghafla waumini wakasitukizwa na msaada wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), na wapinzani wakahilikishwa. Hilo tulilolitaja ladokezwa na kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Au mnadhani kwamba mtaingia Peponi na hali bado hamjafikiwa na mfano (kama) wa wale waliopita kabla yenu? Yaliwashika mashaka na madhara na wakasukwa sukwa hata akasema Mtume na walioamini pamoja naye: Msaada wa Mwenyeezi Mungu (utafika) lini? sikilizeni bila shaka msaada wa Mwenyeezi Mungu uko karibu.� 104


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

(Al-Baqara; 2: 214). Kwa hiyo makusudio ya Mtume, siyo Nabii mtukufu, bali ni miongoni mwa Mitume waliotangulia, pindi ilipokuwa shida na madhara yamzunguka Mtume mwenyewe na waumini, na matatizo yalikuwa yanawatikisa hawa waumini kiasi kwamba kama yanabana pumzi zao, ndipoo zile pumzi zilizosongwa na maumivu yanayomtia mtu mweleka yakakaribia katika aina ya unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, basi Mtume na waliomwamini wakasema: “Lini itakuja nusura ya Mwenyezi Mungu”, hivyo neno: “Lini itakuja nusura ya Mwenyezi Mungu” limeambatana na unyenyekevu na uombaji. Hivyo maumbile yakaleta taswira ya wao kutawaliwa na hali ya kukatishwa tamaa, lakini si kwa maana ya kuwepo kwa hali hizi ndani ya roho na nyoyo zao bali ni kwa maana ambayo umeshaijua, nayo ni ile itokanayo na dhahiri ya hali zao, na si kutoka katika kauli zao. Hali ya mambo ikabaki hivyo mpaka ukashuka msaada na mawingu ya kukatishwa kwao tamaa (iliyo sababishwa na hali ile ya mbinyo) yakatawanyika. Hapa ndipo tulipofikia katika tafsiri ya Aya, na huenda msomaji anaweza kupata tafsiri inayokubalika sana ndani ya nafsi kuliko tuliyoitaja.

Aya ya pili:

105


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Wala hatukupata kumtuma kabla yako Mtume yeyote wala Nabii ila akitamani, shetani huingiza katika matamanio yake. Lakini Mwenyezi Mungu huondoa anachokiingiza shetani, kisha Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, mwenye hekima. *Ili aufanye ushauri uingizwao na shetani uwe mtihani kwa ambao ndani ya nyoyo zao kuna maradhi na ambao nyoyo zao ni ngumu, na kwa kweli wadhalimu wapo kwenye mfarakano wa mbali. * Na ili waliotunukiwa elimu wajuwe kwamba (Quran) ni kweli kutoka kwa Mola wako na ili waiamini, na nyoyo zao ziwe nyeyekevu kwayo, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mwongozi wa walioamini kwenye njia iliyonyooka. ” (Al-hajj:52 - 54). Aya hizi ni dalili zenye nguvu sana kwa mtizamo wa asemaye kuwa manabii sio maasumu, na wanahistoria wataalamu wa mambo ya nchi za mashariki - orientalists- wamezitumia ili kuutilia shaka wahyi ulioteremka kwa Nabii kwa sura ambayo ubainifu wake utakujia kikamilifu Mwenye kuzitolea dalili Aya hizi analifasiri neno ‘kuingiza shetani ndani ya matamanio ya Mtume au Nabii’ kwa maana ya kuingilia kati katika wahyi ulioteremshwa kwake, kwa hiyo anaubadilisha kwa maana ambayo sio ile iliyoteremshwa. Kisha Yeye (s.w.t.) huyaondoa yanayoingizwa na shetani na kuyasahihisha aliyoyateremsha kwa Mtume wake miongoni mwa Aya. Ikiwa hii ndiyo maana inayofahamishwa na Aya basi yenyewe ni dalili ya manabii kutokuwa na ismah katika uwanja wa kuuhifadhi wahyi au kuufikisha. Lakini lililoafikiwa na semi za wanachuoni wa theiolojia ni kuwa wao wamehifadhiwa katika uwanja huu. Na huenda tafsiri hii ikapewa nguvu na maelezo aliyoyapokea At-Tabariy na wengine kuhusu sababu ya kushuka kwa Aya hii, baadae tamko lake litakufikia kikamilifu na ishkali zake zilizopo utaziona. Na ambalo ni bora ni kuizungumzia Aya kwa utafiti na kuitafsiri ili ibainike kuwa Aya inalenga upande usiokuwa ule aliokwenda mtoa dalili na kuutolea tafsiri, hivyo basi twasema: Ni lazima kubainisha nukta kadhaa katika Aya hizi. 106


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Ya kwanza: Nini maana ya neno umniyyatu kwa mujibu wa kiarabu? Na inalenga nini kauli Yake (s.w.t.): “Akitamani”. Pili: Nini maana ya kujiingiza kwa shetani ndani ya umniyya ya Nabii inayoelezwa na kauli Yake Mwenyezi Mungu. (s.w.t.): “Shetani aingiza katika umniyya yake? Tatu: Mwenyezi Mungu anakusudia nini kwa kauli Yake: “Kisha Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake” Je makusudio ya Aya ni za Qur’an? Nne: Vipi akiingizacho shetani kinakuwa ni fitna kwa wagonjwa wa nyoyo na kwa wenye nyoyo ngumu? Na vipi kinakuwa ni sababu ya imani ya waumini na kunyenyekea kwa nyoyo zao kwake. Tukibainisha nukta hizi nne na kutafsiri madhumuni yake ndipo utatoweka mkanganyiko uliyofumwa na dhana kuhusu Aya, hivyo basi twasema: Ama kuhusu neno Al-umniyyatu, Ibnu Farisi amesema: “Latokana na neno Al-mana likimaanisha kukadiria kitu na kukipitishia maamuzi, miongoni mwa mifano yake ni usemi wa warabu: “maniya lahul’maaniy” yaani ame kadiria mkadiriaji. Na Al-mana: Ni kadirio, na maji ya mtu ni: Maniy: Yaani humo hukadiriwa umbo lake. Na Al-maniyatu: Ni umauti kwa sababu ni wenye kukadiriwa katika hali zote, Na tamanna al’insan: Yaani matarajio anayokadiria. Na Mina ya Makka: Kaumu wamesema : Imeitwa hivyo kwa vile kuchinja kumekadiriwa hapo, kutokana na kauli yako manahu llahu.”87 Kwa hiyo ni juu yetu kuelewa utashi na matarajio ya Mitume na manabii kupitia Kitabu kitukufu, na mwenye kuupima undani wa Kitabu kitukufu 87.

Al-maqaayisu Juz. 5, Uk. 276. 107


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

hana shaka kuwa Mitume na manabii hawakuwa na utashi na matarajio mengine ila kueneza mwongozo wa kiungu kati ya kaumu zao na kuwapa mwongozo kwenye njia ya kheri na maisha ya furaha, na walikuwa wanadumisha, na kufanya juhudi binafsi ili kutimiza kusudi hili la maana, na lengo la hali ya juu, wala kwa hilo hawaachi juhudi yoyote, na walikuwa wanaratibu mipango kwa ajili ya jambo hili na walikuwa wanafikiria ni jinsi gani watalifanikisha kwa njia zinazofaa na walikuwa wanafanya maandalizi kwa ajili yake kadiri ya uwezo wao. Hilo lajulishwa na jumla ya Aya kadhaa, tutakomea kutaja baadhi yake: Mwenyezi Mungu anasema kumuhusu Nabii mtukufu: “Watu wengi si wenye kuamini japo ufanye pupa” ( Yusuf:103). Pia anasema:

“Isiangamiye nafsi yako kwa huzuni na majonzi kwa sababu hawakuamini Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni mjuzi wa wanayo tendahayawezi kumchanganya mambo.”(Fatir:8). Pia anasema

“Japo ufanye pupa kwa ajili ya uongofu wao haitowafaa pupa yako kwa kuwa wao hawawezi ongoka,Mwenyezi Mungu hawaongozi wanaopoteza wala wao hawana wa kuwanusuru” (An-nahl:37) Na asema Mwenyezi Mungu :

“Kwa hakika huwezi kuwaongoza uwapendao lakini Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye.” (56: Al-Qasasu).

108


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na anasema Mwenyezi Mungu:

“Kumbusha wewe ni mkumbushaji tu sio mlazimishaji juu yao.” (Alghashiyah :21-22) Hayo yote ni kuhusu hali halisi ya Nabii-Muhammad - (s.a.w.). Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anasema akielezea msimamo ulionyooka wa Nabii Nuhu (a.s.), katika njia ya daawa yake:

“Na kila mara nilipowaita uwasamehe, waliziba masikio yao kwa vidole vyao, na walijifunika nguo zao na walizidi kuendelea na kufru na wakafanya kiburi kingine. Tena niliwaita kwa sauti kubwa. “Kisha nikawatangazia na nikasema nao kwa siri.” (Nuh :7-9) Na asema (s.w.t.) baada ya Aya kadhaa:

109


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Nuhu alisema: Oh! Mola wangu! Kwa hakika wao wameniasi na wamemfuata ambaye mali yake na watoto wake hawamzidishii ila hasara na wamefanya vitimbi vikubwa. Na wakasema: Musiwaache miungu wenu, wala musiwaache (miungu akina): Wadan wala Suwaan wala Yaghutha na Yauqa na Nasra. Na wamepotosha sana wala usi wazidishiye madhalimu ila upotovu.�(Nuh :21-24). Kwa hiyo Aya hizi na zilizo mfano wake kwa wazi kabisa zinatoa habari kuwa matamanio pekee ya manabii maishani mwao na njia yao ya daawa ni kuwaongoza watu kwa Mwenyezi Mungu, na kupanuwa wigo wa daawa ili ufike mbali zaidi iwezekanavyo, na wao wanafanya juhudi kwa ajili ya hilo kwa azma iliyojikita na matumaini thabiti na walikuwa wakienda kulielekea lengo hili kwa nyayo zilizojizatiti japo wakabiliwe na vikwazo katika njia ya kulitimiza hilo na mbele yao kuwe na pingamizi. Mpaka hapa jibu limekuwa bayana kuhusu swali la kwanza, hivyo basi sasa njoo pamoja na mimi kwenye jibu la swali la pili, nakusudia: Nini maana ya kujiingiza kwa shetani ndani ya umniyya ya mitume: Na swali hili ndiyo nukta nyeti katika dalili ya wapinzani wa ismah ya manabii, tukilijibu kwa dalili itadhihirika maana, na ili kutoa dalili kwa wazi twasema: Kwa kweli kuingiza Shetani katika matamanio ya manabii huwa kwa sura moja wapo kati ya sura mbili: 1. Atiye wasiwasi katika nyoyo za manabii na azidhoofishe zile azma zao zilizo thabiti na ajaribu kuwakinaisha kuwa daawa yao na miongozo yao haina umuhimu wowote na kuwa umma huu sio umma uwezao kuongozeka, kutokana na hilo mawingu ya kukata tamaa yaanze kujitokeza nyoyoni mwao, na waache kuwaongoza watu na kutupilia mbali mwongozo wao.

110


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Ar-Razi amesema ndani ya kitabu chake (Ismatul-anbiya): “Miongoni mwa wanatafsiri kuna aliyeibebesha Aya hii maana ya ‘matamanio ya moyo’. Na maana yake ni kuwa Nabii (s.a.w.) anapotamani awezalo kulitamani miongoni mwa mambo, shetani anamtia wasiwasi kwa jambo la batili na anamuita kwenye jambo lisilostahiki…” 88 Na katika Tafsiri ya At-Tibiyanu: “Wamesema baadhi ya wafasiri: Hakika ya makusudio ya kutamani katika Aya ni kutamani kwa moyo, na maana yake ni: Hapana Nabii wala Mtume isipokuwa anatamani kwa moyo wake ambacho kitakachomkurubisha kwa Mwenyezi Mungu miongoni mwa utii wake, na kuwa shetani huingiza wasiwasi wake na chombezo zake katika tamaaa yake kinyume na vile alivyokuwa anakusudia (Nabii au Mtume)”89 Na amesema ndani ya kitabu Sharhul-mawaqif: ( au Al-Muradi): “Kwa makadirio ya kuifanya tamanniy ni tamaa ya moyo na fikra zake (yaani anayotamani kwa wasiwasi wa shetani) maana itakuwa ni: ‘Nabii anapotamani kitu shetani humtia wasiwasi na humwita kwenye lisilofaa…”90 Bila shaka maana hii hailingani na heshima ya manabii kwa mujibu wa tamko la Qur’an Tukufu kwa kuwa italazimu shetani awe na sultani, yaani uwezo juu ya mioyo ya manabii na dhamira zao ili adhoofishe azma zao na awasimamishe wasiendelee na njia za daawa na mwongozo. Na hali Qur’an Tukufu inakanusha uwezekano wa shetani kuingilia dhamiri za watu mukhlaswiina ambao ndio manabii na wale ambao wapo chini yao, Mwenyezi Mungu anasema (s.w.t.):

“Kwa kweli waja wangu huna mamlaka juu yao isipokuwa atakaye kufuata miongoni mwa wapotovu.” (Hijri:42 na Israi: 65). 88. Ismatul-Anbiya cha Alfakhru Raziy, Uk 85. 89. Tafsiriul-Bayani cha Sheikh At-Tusiy Juz 7, Uk 331. 90. Sharhul-Mawaqif, Juz.8, Uk. 277. 111


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na anasema pia akimnukuu shetani mwenyewe:

“Naapa kwa uwezo wako nitawapoteza wote isipokuwa waja wako miongoni mwao waliotakaswa na wenye ikhlaswi.” (Swad: 82 - 83). Na hapana uingizaji wa udhaifu ndani ya azma za manabii kupitia shetani isipokuwa ni kwa njia ya ushawishi wake kwao, ushawishi ambao umekanushwa na tamko la Aya za Qur’an. 2. Iwe makusudio ya Shetani kuingiza katika matamanio ya Nabii ( s.a.w.) ni kuwapotosha watu na kuwaita kwake waende kinyume na manabii na kusimama mbele yao ili kuzuwiya mafunzo ya kiungu yasienee na ili mipango ya manabii isiwe na matunda na wala faida yeyote. Na maana hii ndiyo iliyo dhahiri ndani ya Qur,an Tukufu, kwani yatunukulia katika maeneo mengi kuwa shetani alikuwa anawahimiza kaumu za manabii waende kinyume nao, na alikuwa anawaahidi wayatamaniayo ili waende kinyume na manabii. Amesema (s.w.t.): “(Shetani) anawaahidi na kuwatia tamaa, na shetani hawaahidi ila udanganyifu.”(An-nisaa :120). Na amesema Mwenyezi Mungu:

“Na atasema shetani itakapopitishwa hukumu: Hakika Mwenyezi Mungu alikuahidini ahadi ya kweli na nilikuahidini na nimekuwa kinyume na nilivyokuahidini sikuwa na uwezo juu yenu isipokuwa 112


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

nilikuiteni tu na mukaniitikia hivyo basi musinilaumu mujilaumu binafsi.” (Ibrahim:22). Na Aya hizi na zilizo mfano wake kwa wazi kabisa zashuhudia kuwa shetani na jeshi lake walikuwa wanafanya juhudi kwa nguvu zote ili kuwatumbukiza watu katika uhalifu wa kwenda kinyume dhidi ya manabii na Mitume, na walikuwa wanawahadaa kwa ahadi na kuwapa matumaini. Hapo ndipo yanabainika madhumuni ya Aya: “Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala Nabii anapotamani....”. yaani endapo atafikiri katika kuongoza umma wake, na akaandaa mipango kwa ajili hiyo, na akaandaa maandalizi ya mwanzo, hapo shetani ataingiza tamaa yake kwa kuwahimiza watu wakatae na wakanushe daawa hii, na wapambane nayo waizuiye mpaka juhudi hizi zote ziwe hazina matunda. Tatu: Nini maana ya Mwenyezi Mungu hufuta kinachoingizwa na Shetani: Ikiwa umetambuwa kipande hiki cha Aya basi yapasa tuangaliye madhumuni ya kipande kingine cha Aya nacho ni ile kauli yake Mwenyezi Mungu: “Hivyo Mwenyezi Mungu hufuta akiingizacho shetani” Nini maana ya ufutaji huu? Makusudio ya ufutaji ni ile ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyowaahidi Mitume wake kuwa atawanusuru, kuwasaidia na kuwafanikishia, amesema Mwenyezi Mungu:

“Mwenyezi Mungu amepitisha kuwa nitashinda mimi na Mitume wangu, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni mwewye nguvu, mwenye uwezo.” (Al-mujadilah: 21). 113


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na amesema Mwenyezi Mungu:

‘Bali tunaivurumisha haki kwenye batili na inaivunja (batili) hivyo yenyewe hutoweka.” (al’Anbiyau: 18) Na amesema Mwenyezi Mungu:

“Na neno letu limepita- maamuzi yame pitishwa yasiyo kubali kinyume chake - kwa ajili ya waja wetu wenye kutumwa kuwa wao ndio wenye kusaidiwa na kwamba kundi letu ndilo lenye ushindi.”(Aswafat :171-173 ). Na amesema kumuhusu Nabii mtukufu (s.a.w.w.):

“Yeye ndiye ambaye amemtuma mjumbe wake na mwongozo na dini ya kweli ili ampe ushindi juu ya dini zote japo washirikina wachukiye.” (Atawba:33). Na pia amesema Mwenyezi Mungu:

114


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Na hakika tuliandika katika Zaburi baada ya ukumbusho kuwa: Ardhi (hii) watairithi waja wangu walio wema.” ( Al—Anbiyaa:105). Na Aya nyingine miongoni mwa Aya zinazotoa mwanga zinazoongelea kuwa ushindi ni wa haki iliyoko kwenye risala za kiungu katika mapambano yake dhidi ya batili na wafuasi wake. Nne: Nini maana ya Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake: Endapo maana ya kufuta kwa Mwenyezi Mungu yale anayoyaingiza Shetani imebainika basi yatabainika makusudio ya kauli yake Mwenyezi Mungu: “Kisha Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake”. Kwa hiyo makusudio ya Aya ni dalili zilizo wazi zenye kutoa mwongozo kuelekea kwa Mwenyezi Mungu na kwenye maridhawa yake na sheria zake. Na ukipenda utasema: Akifuta anayoyaingiza shetani, analeta mbadala hivyo mahali pake panachukuliwa na kinachoingizwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa manabii wake miongoni mwa dalili na Aya ambazo zina ongoza kwenye utii wa Mwenyezi Mungu kwanza, na maisha ya furaha kwa watu pili. Na miongoni mwa kauli duni mno ni kauli isemayo kuwa: “Makusudio ya Aya, ni Aya za Quran ambazo zimeteremshwa kwa Nabii mtukufu, hiyo ni kwa sababu maudhui ya mjadala humo sio makhsusi kwa Nabii mtukufu bali ni Mitume na manabii kwa sura isiyo na mipaka. Zaidi ya hapo ni kuwa sio kila Nabii ana kitabu na Aya, basi vipi yawezekana awe na Qur,an pia! Matokeo: Kwa kweli kwenye medani ya mapambano kati ya watetezi wa ukweli, na askari wa batili ushindi na kupata nusra na mafanikio huwa kwa watetezi wa ukweli, na kushindwa huwa kwa wasaidizi wa batili, kwa hiyo mipango ya kishetani hunyauka, na mkia wake -yaani wafuasi walio mfano wa mkia - hushindwa kwa utashi wa Mwenyezi Mungu. Na mahali pake huwekwa wazi ratiba ya kimaisha ya kiungu na Aya zilizo wazi, na ukweli 115


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

huchukua nafasi na huthibiti, na batili hutoweka na kukanushwa. Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema:

“Sema, Ukweli umekuja na batili imetoweka kwa hakika batili ni yenye kutoweka.” (Al’Israa: 81). Tano: Nini faida ya mapambano haya: Umeshajua kuwa Aya zimetoa sababu ya mapambano haya kuwa, kile kinachoingizwa na shetani huyafitini makundi matatu: i. Ambao nyoyoni mwao kuna maradhi ii. Wenye nyoyo ngumu. iii. Ambao wamepewa elimu. Kwa kweli faida ya mapambano haya ni kuwajaribu watu na kuwapa mtihani, ili kidhihirisha kilichojificha nyoyoni mwao na kilicho ndani ya dhamira ya nafsi zao, ikiwa ni ukafiri na unafiki, au unyofu na imani. Kwani nafsi zenye maradhi ambazo hazikupata utakaso na malezi ya kiungu, na nyoyo ngumu zilizotekwa na matamanio na zilizopofuliwa na mazuri ya maisha ya dunia, huvutwa na wito wa shetani ili zimfuate na hatimaye hujitokeza kilichozingirwa na vifua vyao miongoni mwa kufuru na ufasiki. Kwa hiyo unafiki wake huthibiti na ukafiri wake hujitokeza. Ama nafsi zenye imani zilizokiri kuwa alichokileta Mtume ni kweli kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) huzidi imani na uthabiti, uongofu na kuimarika upande wa ukweli. Na faida hii ipo katika majaribio yote ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwa waja wake, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hamjaribu mtu ili ajuwe ukweli wa nafsi na nafasi yake, kwani kwa hakika yeye anajua yaliyo ndani ya nafsi hizi kabla hajazijaribu, Mwenyezi Mungu asema (swt):

116


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Asijuwe aliyeumba na yeye ni mtambuzi wa siri mwenye habarikamili.” (Al-Mulku:14). Lengo katika majaribio si jingine isipokuwa kuzitoa shari hizo na nguvu ya batili iliyojificha ndani ya nafsi, zilizoota nyoyoni na kuzifikisha kwenye ulimwengu wa uhakiki na wa kivitendo na hatimaye kufuatiwa na utayarifu wa kudhihiri na kuwepo. Kutokana na hayo anasema Amirul-muminin (a.s.) kuhusu maana ya mtihani wa mali na watoto uliokuja ndani ya kauli yake (s.w.t.): “Juweni kuwa mali zenu na watoto wenu ni fitna.” “Ili abainike mwenye kuikasirikia rizki yake, na mwenye kuuridhiya mgao wake, japokuwa (s.w.t.) anawajua mno kuliko wanavyojijua wao wenyewe, lakini ili vitendo ambavyo kwa ajili yake wanastahiki thawabu na adhabu vidhihiri”91 Nilipomaliza kuhariri maneno haya niliyafahamu maneno ya Sheikh Muhammad Jawadi Al-Balaghiy (Q.s.) nayo yanakaribiana na tuliyoyasema. Alisema: “Makusudio ya umniyyah ni kitu kilichotamaniwa kama ilivyo katika matumizi yaliyoenea katika mashairi na tenzi, kama ilivyo dhahiri ya tamanniy iliyonasibishwa kwa Mitume na Nabii inayothibitishwa na mtiririko wa hizi Aya, ni ile inayolingana na wadhifa wake na si vingine, nayo ni kutamani mwongozo ushinde kati ya watu, upotovu ufutike, sheria ya haki iungwe mkono , na mfano wa hayo. Kwa hiyo Shetani anaingiza upotovu wake wenye kushawishi kati ya watu ndani ya huyu mtu mwema mwenye kutamani, na hatimaye inakuwa fitna kwa ambao nyoyoni mwao mna maradhi. Kama alivyoingiza upotovu na hali ya kuto fanikwa kati ya umma wa Musa. Na aliingiza kati ya wafuasi wa Sayyid al-Masihi ambalo lilisababisha walio wengi miogoni mwao kuritadi na 91.

Nahjul-balagha, sehemu ya hekima. Na.93. 117


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kutoka nje ya dini. Na akawaingizia shaka wale watu mahususi na hatimaye wakayumba katika mafunzo na hukumu za kisheria baada yake. Na aliingiza katika kaumu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu jambo ambalo liliwachochea wamkadhibishe na kumpiga vita, na aliingiza kati ya umma wake jambo ambalo lilisababisha tofauti na kujitokeza kwa bidaa. Lakini Mwenyezi Mungu kwa nuru ya mwonngozo hufuta upotovu na giza la Shetani, kwa hiyo asubuhi ya ukweli huchomoza katika akili zilizo salama, kisha Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake na kuwapa nguvu Hoja wake kwa kuwatuma Mitume, au kuweka sawa umoja wa neno la dini iliyonyooka. 92 Aliyoyasema (Q.S.) hayana vumbi na tayari tumeshaimarisha nguzo zake hapo kabla. Mpaka hapa zimebainika kwa wazi kabisa maana za milango yote na vipande vya Aya, na maneno yamebaki katika tafsiri isiyofaa ambayo wamejiambatanisha nayo baadhi ya makasisi wanaoukebehi Uislamu, na wale wafuatao nyayo zao miongoni mwa wanyonge.

Tafsiri batili za Aya: Baadhi ya makasisi waliokusudia kuukebehi Uislamu na kuipunguzia hadhi na heshima Qur,an na kuidunisha thamani yake, wameshikamana na Aya hizi na wakasema: “Makusudio ya Aya ni: “Hapana Mtume wala Nabii ila akitamani na akisoma Aya zilizoteremka juu yake shetani hujiingiza katika kisomo chake na kuingiza yasiyo yenyewe.” Walijitahidi kuitolea ushahidi tafsiri hiyo kwa kutumia maelezo yaliyoelezwa na Tabariy kutoka kwa Muhammad bin Kaaby Al-Qardhiyu na Muhammad bin Qaysi, wamesema:

92.

Al-huda ila dinil-Mustapha, Juz.1 Uk 134. 118


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

“Mtume wa Mwenyezi Mungu aliketi katika mojawapo ya kilabu miongoni mwa vilabu vya makuraishi ambayo watu wake walikuwa wengi, siku ile alitamani kisimjiye kitu chochote kutoka kwa Mwenyezi Mungu kitakachowafanya wamchukiye, hapo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akamteremshia: “Naapa kwa nyota inapoanguka. * Kwamba mtu wenu hakupotea wala hakukosea.” basi (s.a.w.w.) aliendelea kusoma mpaka alipofika “Je, mmewaona Lata na Uzza? * Na Manata mwingine wa tatu?” hapo shetani akamnong’oneza matamko mawili: “Hao ni waungu watukufu, na kwamba maombezi yao bila shaka yatarajiwa.” akayatamka kisha akaendelea akasoma Sura yote. Mwisho wa sura akasujudu na ile kaumu ya watu yote ikasujudu pamoja naye. Al-Waliydu bin Al-Mughira yeye alikuwa mzee kikongwe hawezi kusujudu hivyo alinyanyua udongo mpaka paji lake la uso na akasujudu juu yake. Hapo wakaridhika na aliyoyasema, wakasema tumetambuwa kuwa: Mwenyezi Mungu anahuisha na kufisha naye ndiye anayeumba na kuruzuku, lakini miungu yetu hii inatuombea kwake kwa kuwa umeiwekea hisa, hivyo sisi tuko pamoja na wewe.” Hao wawili walisema: “Ilipofika mchana Jibril (a.s.) alimjia akamwonyesha Sura, alipoyafikia yale matamko mawili ambayo aliyaingiza Shetani kwake Jibril akasema: “Sijakuletea haya mawili.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akasema: “Nimemzulia Mwenyezi Mungu na nimesema kumuhusu Mwenyezi Mungu asiyoyasema.” Ndipo Mwenyezi Mungu akamteremshia wahyi: “Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyokufunulia ili upate kutuzulia mengineyo, na hapo bila shaka wangelikufanya rafiki.” (Al-Israu:73) mpaka kauli yake (s.w.t.): “Kisha usingepata msaidizi juu yetu.” (AlIsrai: 75.) Basi Mtume alibakia na huzuni mwenye majonzi mpaka iliposhuka kwake: “Wala hatukupata kumtuma kabla yako Mtume yeyote wala Nabii ila akitamani, shetani huingiza katika matamanio yake. Lakini Mwenyezi Mungu huondoa anachokiingiza shetani, kisha Mwenyezi Mungu huimarisha Aya zake na Mwenyezi Mungu ni 119


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Mjuzi, mwenye hekima” (Al-Haji: 52). Tabariy akasema: Muhajirina waliokuwa katika ardhi ya Uhabeshi wakasikia kuwa watu wa Makka wote wamesilimu, basi wakarejea kwa jamaa zao na wakasema: Wao ni wapenzi mno kwetu, lakini wakawakuta wamerudi walivyokuwa pindi tu Mwenyezi Mungu alipofuta aliyoingiza shetani”93Yaliyo katika tafsiri hii na sababu ya uteremkaji wake hayajifichiki kuwa yana ishkali ambazo zautupilia mbali usahihi wa njia yake ya upokezi. Kwanza: Msingi wa tafsri hii ni kuwa kitenzi (tamanna) kimetafsiriwa kwa maana ya “akisoma” na tamko (umniyyatahu) likatafsiriwa kwa maana ya “usomaji wake”. Al-Qurtubiy katika kuitafsiri Aya hii amesema: “(Tamanna)yaani akisoma, (Umniyyatahu) yaani usomaji wake”.94 Na amesema ndani ya juzu ya pili Jalada la kwanza, ndani ya Tafsiri yake ukurasa wa sitini na moja: “ (Amaniy) ni wingi wa (umniyatu) nalo humaanisha kusoma. ..................hivyo akisoma shetani huingiza katika usomaji wake”95 Lakini matumizi haya hayakuzoeleka katika lugha ya Qur’an na Hadithi na endapo yatakuwa sahihi basi ni matumizi yaliyo kinyume na matumizi ya walio wengi na si maarufu, kwa hiyo yapasa kuiepusha Qur’an mbali na matumizi kama hayo. Matumizi yenyewe. Ndiyo kuna baadhi wameitolea dalili kauli ya Hassan kuhusu matumizi ya aina hiyo: “Tamannaa kitaba llahi akhira laylati. Tamannaa Daudu zZabura ala rusulin.” Hapo neno tamannaa likiwa na maana ya: Amesoma. yaani tamanna kita93.Tafsyiru ya Tabariy Jalada 17. Uk. 131, Suyut ameinakili katika kitabu Durul- Manthur katika tafsiri ya Aya hii. 94. Tafsyirul -Qurtubiy, Jalada 6. Juz 12, Uk 79. 95. Tafsyirul -Qurtubiy, Jalada 1. Juz 2, Uk 61.

120


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ba llahi, amesoma kitabu cha Mungu. Na tamanna Daudu Zabura Daudi amesoma Zaburi. Na hizi beti mbili hata kama sanadi yake inayokomea kwa mwarabu safi kama Hassan itakuwa sahihi- wala haitokuwa sahihi - lakini haipendezi kuichukua Qur’an katika lugha isiyo maarufu. Zaidi ya hayo ni kuwa beti zilizotolewa ushahidi hazipo katika diwani ya Hassan, bali zimenakiliwa na wafasiri ndani ya tafsiri zao, na amezinakili Abu Hayani ndani ya Tafsiri yake, Jalada. 6, Uk. 382. Na amezitolea ushahidi mwandishi wa kitabu alMaqayisu, Jalada. 5, Uk. 277. Ndiyo Qurtubi katika Tafsiri yake ameleta ubeti wenye kukusanya maana ya beti mbili hizi tulizozitaja na amezinasibisha na Kaab bin Malik, amesema: Kaab bin Malik amesema: “Tamannaa kitaballahi akhira laylihi wa’akhirihi laqa hamamal’maqadiri”96 Na kwa muhtasari ni kuwa kwa mfano endapo dalili itakuwa sahihi, basi itakuwa katika tamko la kwanza si tamko la umniyyatu kwa sababu ya kutokuwapo tamko hilo kakika ubeti uliotajwa. Pili: Kwa hakika riwaya hii haiwezekani kuitolea hoja kwa sababu nyingi, kwa uchache wake ni kwamba njia zake haziwavuki Tabiina na walio chini yao isipokuwa Ibnu Abbasi tu, ilihali yeye hakuwa amezaliwa wakati kisa hiki kilipowekwa. Zaidi ya hayo ni ule mbabaiko uliyopo ndani ya matini yake, kimenukuliwa katika sura tofauti zafikia sura ishirini na nne, Allama Al-Balaghiy amezikusanya sura hizo tofauti katika kitabu chake Al-Atharun-nafiysu fatilia humo.97 Tatu: Kwa kweli kisa hiki kinajikosoa chenyewe kwa sababu ndani yake kuna: Eti Nabii baada ya kuziingiza jumla mbili ambazo ni za ziyada katikati ya Aya mbili, aliendelea kuisoma sehemu iliyobaki ya sura mpaka mwisho, kisha Nabii alisujudu na washirikina waliokuwepo walisujudu pamoja naye wakiwa na furaha na yaliyokuja ndani ya jumla mbili hizo 96. Tafsirul’Qurtubiy. Jalada 1. Juz.2,Uk.61.

97. Al-huda iladinil-Mustafa Juz.1, Uk 130. 121


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

kwa ajili ya sifa kwa miungu yao. Lakini Aya ambazo zilifuata baada ya jumla hizi mbili ambazo Nabii aliendelea kuzisoma zinaeleza kuwa: “Huo tena ni mgawanyo mbaya.* Hayakuwa haya ila ni majina mliyowapa nyinyi na baba zenu, Mwenyezi Mungu hakuteremsha dalili juu yao...” mpaka mwisho wa Aya. (Najmu: 22 - 23). mpaka mwisho wa Aya. Hapo lajitokeza swali hili, nalo ni: Vipi nafsi za waarabu ziliridhia sifa chache kama hizi kuwahusu miungu wao kutoka kwa Nabii na zikaghafilika dhidi ya Aya zilizofuatia ambazo zailaumu miungu yao kwa ukali mno na zawahesabu kuwa ni waabudiwa wa uzushi hawamiliki sifa za uungu bali ni majina na anuwani tu? Ilihali walikuwepo wanamantiki wao, wanahekima wao na washairi wao kama vile: Al- Walidu bin al-Mughira. Hivi huoni kuwa hiyo ni dalili ya kuwa muweka kisa hiki ni miongoni mwa waweka visa au Hadithi za uzushi na waongo, ambaye amezuwa kisa akiwa ameghafilika kuwa si mahali pake. Wahenga wasema: Muongo hana kumbukumbu. Na la ajabu ni lile la baadhi ya waandishi ambao wanaleta baadhi ya mitazamo katika kuitafsiri riwaya hii bila ya dalili wala ushahidi. Raziy baada ya kumthibitikia kuwa makusudio ya kitenzi Atamaniy ni usomajii, akasema katika kitabu chake kuwa: “Wametofautiana wanaoamini taawili hii na kufikia mitizamo sita: Wa sita ni kuwa maana ya neno al-Gharaniqu (Miungu) ni Malaika, na matamko hayo yalikuwa ni Quran iliyoteremshwa kuwasifu Malaika, lakini washirikina walipodhania kuwa wanakusudiwa miungu wao Mwenyezi Mungu alifuta usomwaji wake.”98 Mtu mwenye insafu hawezi kuleta mtizamo huu. Na amesema katika kitabu Sharhul-Mawaqif: “Huenda ikawa (ibara zilizotajwa) ni Qur’an na hao Gharaniqu ikawa inaashiria (Malaika na ndipo usomaji wake ukafutwa) kwa ajili ya utatanishi (yaani usiwafanye washirikina wadhanie kuwa wakusudiwao ni miungu yao).”99 98.Ismatul-Anbiyai, Uk 85 - 88.

99. Sharhul-Mawaqif, Juz 8, Uk 277. 122


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Na ilipasa kwake na kwa mwingine wasikitaje kisa hiki kabisa achia mbali kule kuleta mitazamo kwa hila ya kutaja uwezekano wa kukifanyia taawili. Nne: Kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) anamsifu mwanzoni mwa Sura Nabii wake mtukufu kwa kauli yake:

“Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.” ( Najmu:3 -4) kutokana na hali hiyo vipi itasihi kwake (s.w.t.) amsifu Nabii wake mwanzoni mwa Sura kwa sifa kama hii, kisha litokee kwa Nabii wake linalokuwa kinyume na sifa hii kabisa, hali ya kuwa anaweza kumhifadhi Nabii wake asiteleze kwenye mtelezo hatari kama huu. Tano: Kwa kweli jumla mbili za ziyada zilizoambatanishwa na Aya, zinakosolewa na Aya zingine zinazojulisha kulindwa kwa Nabii mtukufu wakati wa kuupokea wahyi na kuhifadhika kwake wakati wa kuufikisha kama ilivyotangulia katika tafsiri ya kauli yake (s.w.t.):

“Isipokuwa Mtume aliye mridhia, basi hakika yeye humuwekea walinzi mbele yake na nyuma yake. (Al-Jinnu:27). Na kauli yake (s.w.t.):

“Na kama angelizua juu yetu baadhi ya maneno. *Lazima tungelimshika kwa mkono wa kulia. *Kisha kwa hakika tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo.” (Al-haqah:44-46). 123


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Sita: Kwa kweli wanazuoni wa Kiislamu, na watu wenye elimu na utambuzi miongoni mwa Waislamu wameikabili hikaya hii kwa kuikanusha, AlMurtadhwa ameielezea kuwa ni uzushi walioutunga.100 Nasafiy amesema: “Kwa kweli kukiongelea kisa hiki hakuridhishi”. Al-Khazinu ndani ya tafsiri yake amesema: “Kwa kweli wanazuoni hawakutilia manani asili ya kisa hiki, na hajakipokea yeyote miongoni mwa watu sahihi, wala muaminifu yeyote hakukileta katika njia iliyo sahihi au iliyo salama yenye kuungana, bali wamekipokea wanatafsiri na wana historia wanaoshabikia kila jambo la kustaajabisha, wanaonakili kila kitu kutoka magazetini sawa kiwe sahihi au kiwe si sahihi. Na ambalo lajulisha udhaifu wa kisa hiki ni kule kubabaika kwa waelezeaji wake, na njia zake kutoshikana na kutofautiana kwa matamko yake.”101 Amesema katika Sharhul-Mawaqif (au Al-muradi): “Endapo itachukuliwa maana ya Atamanniy kuwa ni kutamani kwa moyo na kufikiri kwake (lile analolitamani kwa wasiwasi wa shetani) hapo basi maana itakuwa ni: Nabii akitamani kitu shetani humtia wasiwasi na kumwita kwenye lisilopaswa, kisha Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hufuta hayo na kumwongoza kuacha kuelekea kwenye wasiwasi wake. Kwa minajili hiyo riwaya iliyotajwa inakuwa miongoni mwa uzushi wa makafiri. 102 Al-Fakhru Raziy amesema ndani ya tafsiri yake baada ya kunakili kisa hiki: “Riwaya hii ni ya wafasiri wote wa mambo ya dhahiri, ama wahakiki wao wamesema kuwa riwaya hii ni riwaya batili ya uzushi na walitoa hoja kutumia Qur’an na Sunnah na akili. Ama Sunnah ni ile iliyoelezwa na Muhammad bin Is’haqah bin Khuzaymah kuwa aliulizwa kuhusu kisa hiki akasema: Haya ni miongoni mwa yaliyowekwa na mazindiki. Na alitunga kitabu kuhusu hilo. Ama kwa upande wa dalili za kiakili miongoni mwazo ni......... 100. Tanzihul-Anbiyai Uk. 109. 101. Al-hudaa ila dinil-Mustafa ,Juz.1,Uk 130. 102. Sharhul-Mawaqif, Jalada. 8 Uk 277. 124


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

Ya nne: Ni kauli yake: Mungu hufuta aingizacho Shetani.... mpaka mwisho wake. Hiyo ni kwa sababu kuziimarisha Aya kwa kumuondolea Mtume anayoyaingiza shetani kuna nguvu zaidi kuliko kuyafuta kwa Aya hizi ambazo mkanganyiko bado huendelea kubaki pamoja nazo. Mwenyezi Mungu akipenda kuziimarisha Aya ili isidhanie isiyokuwa Qur’an kuwa ni Qur’an basi ni bora amzuie Shetani asifanye hivyo kabisa tangu mwanzo.”103 Na pia riwaya hii imepingwa na asiyekuwa Ar-Raziy mfano wa AlQurtubiy ndani ya tafsiri yake na mwingine, basi rejea huko.104 Hizi ndizo ishkali muhimu zinazokikabili kisa hiki na kukiweka kwenye hadhara ya ubatili. Wahakiki wametaja mengi katika kukijibu kisa hiki, na baadhi yake tumeyataja katika kitabu chetu Furughu abadiyati.105 Wala haturefushi hapa kwa kutaja zaidi ya kiasi hiki. Mpaka hapa tumemaliza utafiti kuhusu kundi la kwanza la Aya, sasa umefika wakati wa kuzungumzia kundi la pili la Aya ambazo zimekuwa kisingizio mkononi mwa wakosowaji ambao wanakanusha ismah kwa baadhi ya manabii maalumu.

103. Tafsirul-Qurtubiy, Jalada la 6. Juz 12. Uk 79 104. Tafsyirul-Qurtabiy Jalada 6. Juz.12. Uk.79, na ya baada yake. 105. Aliandika kitabu hiki ili kubainisha maisha yote ya Mtume (s.a.w.w.).

125


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26. 27. 28. 29.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Tisa Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 126


Umaasumu wa Mitume 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63

Sehemu ya kwanza

Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Maulidi Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza swala safarini Kufungua safarini Kuzuru makaburi Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto Tujifunze misingi ya dini Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza Nahjul Balagha Sehemu ya Pili Dua Kumayl Uadilifu wa masahaba Asalaatu Khayrunminaumi Sauti ya uadilifu wa binadamu Umaasumu wa Mitume Sehemu ya kwanza Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya kwanza 127


Umaasumu wa Mitume

Sehemu ya kwanza

BACK COVER Suala la ismah ya Manabii ni nukta ambayo imezua mjadala mkubwa miongoni mwa wanachuoni na miongoni mwa madhehebu. Upande mmoja unasema Manabii ni binadamu ambao wamehifadhiwa kutokana na dhambi na makosa ya aina yoyote. Upande mwingine unasema hapana, Manabii wanaweza kukosea na kufanya dhambi. Upi ni ukweli; mwandishi ya kitabu hiki ambaye ni mwanachuoni mkubwa wa Kiislamu analifafanua suala hili kwa urefu kwa kutumia dalili za kielimu, Qur’an na Sunna na kuhitimisha pasina shaka yoyote juu ya Umaasum wa Mitme. Kimetolewa na kuchapishwa na:

Al-Itrah Foundation P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Fax: +255 22 2127555 Email: alitrah@raha.com Website: www.alitrah.org Online: www.alitrah.info

128


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.