Hadithi ya Thaqalaini katika vitabu vya Ahli Sunna

Page 1

Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

HADITHI YA THAQALAINI KATIKA VITABU VYA AHLI SUNNA

Kimeandikwa na: Dk. Sayyid Alaauddin al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini

Kimetarjumiwa na: Ustadh Amir Musa

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 48 - 5

Kimeandikwa na:

Dr. Sayyid Alaau-Deen al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwiini

Kimetarjumiwa na:

Ustadh Amir Musa Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: Januari, 2009 Nakala: 1000

Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

YALIYOMO Utangulizi..........................................................................................2 Mdahalo wetu na Ahmad bin Hajar Aal- Buutwamiy katika kitabu chake al-aqaidus- Salafiyyah...........................................................13 Ahlul-Bayt katika aya ya mapenzi kwa mujibu wa vitabu vya AhlulSunna...............................................................................................20 Kitabu Shawahidut-Tanzil cha Halam Haskaani.............................22 Ahlul-Bayt katika Aya ya utakaso kwa mujibu wa vitabu vya AhlulSunna...............................................................................................32 Mdahalo wetu na Ihsaan ilahi dhahiir na kitabu chake (Shia wa Ahlul-Bayt)......................................................................................39 Hitimisho kuhusu aya ya utakaso kama ilivyokuja katika vitabu vya Ahlul-Sunna....................................................................................95 Ufisadi wa Sanadi hadithi “Ninakuachieni kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu�...............................................................104 Muhammad Nassur - Diin al- albaani na hadithi Thaqalaini..........111 Al-Khaswais cha Nisaai Mmoja wa watunzi wa vitabu Sahihi Sita.................................................................................................125 Bibliografia....................................................................................150 Vitabu vya mtunzi .........................................................................155 Vitabu visivyochapishwa...............................................................155

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjumi ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Hadith ath-Thaqalayn kilichoandikwa na Dk. Sayyid Alaauddin al-Sayyid Amir Muhammad al-Qazwini. Sisi tumekiita, Hadithi ya Thaqalain. Kitabu hiki, Hadith ya Thaqalain ni hadithi maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu. Hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja hadithi hii, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimulizi wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kuitaja hadithi hii. Hadithi ya Thaqalain ni wasia ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.) alioutoa kwa Waislamu pale Ghadir Khum wakati anarudi kutoka kwenye Hija yake ya mwisho (maarufu kama Hijjatu ’l-Widaa). Qur’ani inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir Khum ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.) alitoa khutba ndefu ambayo kwayo alitoa kauli hii inayojulikana kama hadithi ya Thaqalain: “...Ninakuachieni vizito viwili (thaqalayn); Qur’ani Tukufu na Kizazi changu...” Baada ya tukio hili la Ghadir, aya ifuatayo iliteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.): “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema Yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...” (5:3) Baada ya kushuka aya hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.) alimwita Ali juu ya mimbari ambayo ilitengenezwa kwa matandiko ya ngamia, kisha akanyunyua mkono wake akasema: “Man kuntu mawlahu fahadha Aliyyun mawlahu.” (Yule ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake basi huyu Ali (naye) ni mwenye kutawalia mambo yake.” Kisha akaomba dua: D

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

“Ewe Allah! Msaidie mwenye kumsaidia (Ali) na mpige vita mwenye kumpiga vita (Ali).� (Rejea ya hadithi hii utaipata kwenye kitabu hiki kadiri unavyoendelea kusoma) Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huu, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili, ili kuongeza ujuzi wao katika masuala ya dini na ya kijamii. Tunamshukuru ndugu yetu, Ustadh Amir Musa kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania.

E

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

F

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

UTANGULIZI Sifa zote njema anastahili Mola Mlezi wa viumbe kisha rehema na amani zimfikie hitimisho la Mitume bwana wetu Muhammad (s.a.w.w.) na ndugu zake wema watoharifu (a.s.), pamoja na sahaba wake wema. Nimepata kitabu kidogo chenye anwani “Hadith Thaqalain na ufahamu”, mwandishi Dk.. Ali Ahmad Saaluus, mwalimu msaidizi katika kitivo cha sheria na kanuni katika chuo kikuu cha sheria – Chuo kikuu cha Qatar - na kimepigwa chapa na - Darul-Islah - Abudhabi mwaka 1986, anwani yake ilinivutia hapo nikapatwa na shauku ya kukiangalia ndani, nikaangalia kwa makini, nikidhani huenda nitakuta humo yale ambayo humtuliza mkereketwa na kuziba mwanya wa mwenye kujishughulisha, huku nikitamani wajitokeze wale wenye ujuzi wa kufanya uchunguzi na utafiti, aidha kuwa na maarifa juu ya misingi na vigezo vya ukosoaji, ili kuziba mwanya huo ambao umeathiri umma wa kiislamu na bado unaendelea, lakini dhana hiyo ilikwenda kombo na kupotea bure. Katika kitabu chake nimemkuta ni mtu asiye na upeo wa maoni na itikadi, bali mambo yote yaliyotajwa katika kitabu hicho huelezea maoni ya wale waliomtangulia hapo kabla kuhusiana na Hadith Thaqalain, nayo ni kutokana na kasumba na kufuata mambo kibubusa, kama nilivyowaona wengineo ambao hujituma ili kuifanya dhaifu Hadith Thaqalain, ambayo inapatikana katika vitabu vyote sahihi vya Ahlus-Sunna, hali kadhalika Musnad zao kwa lafudhi ya: “Hakika mimi nakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Na hadithi hiyo imethibiti katika pande zote mbili upande wa Sunni na Shia, na kwa upokezi sahihi hata kama sio mutawatiri, kama itakavyombainikia hivyo mpendwa msomaji. Dk.. Ali Ahmad Saaluus hakuishia tu 2

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kuifanya dhaifu Hadith Thaqalain bali aliwabebesha mzigo wa tuhuma Wanachuoni wakubwa wa Kishi’a kuwa wao pekee ndio walioipokea Hadith Thaqalain kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Iliyothibiti katika vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna, na hilo tutaliweka bayana kwa nguvu ya hoja na vithibitisho kedekede kutoka katika vitabu vya Wanachuoni waliotangulia wa Ahlus-Sunna na Mahafidh pia, ambao walipasisha usahihi wa hadithi hiyo. Bali walikiri kuwa ni Hadith Mutawatiri, kwa mantiki hiyo ndio maana wafuasi wa Ahlul-Bayt huiamini na kuukubali usahihi wa hadithi hiyo, na itikadi hiyo haikuwa makhsusi kwao pekee, bali hata wale ambao hutafautiana na Shi’a wamekiri na kutangaza bayana usahihi wa Hadith Thaqalain kwa tamko la “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”, kiasi kwamba hata Ibnu Taymiyyah pamoja na upinzani wake na ushabiki wake dhidi ya Shia lakini amekiri kuwa Hadith Thaqalain ni sahihi. Bila shaka kitendo cha Dk.. Saaluus na wapambe wake kuikadhibisha hadithi hiyo kinalazimu kumkadhibisha Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala), Mtume wake, Wanachuoni na Maimamu wa Ahlus-Sunna ambao wamepokea hadithi hiyo kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) na wakakiri usahihi wake ndani ya vyanzo na njia mbalimbali ambazo hazipungui thelathini au zaidi, vyote hivyo ni sahihi kwa mujibu wa kukiri kwa Wanachuoni wa Ahlus-Sunna waliokiri na kukubali hilo wao pamoja na Mahafidh wao. Kisha hakika ikiwa lengo la msingi la kuifanyia uchunguzi Hadith Thaqalain ni kuhakikisha kuwa tunafika kwenye ukweli halisia, usio na ubishi wala uzushi, hapana budi sisi kuambatana na kushikamana kikamilifu na hadithi hiyo pamoja na madhumuni yake ambayo hutambuliwa na makundi yote mawili. Kwani bila shaka uislamu humhukumu mzushi kuwa ni mtu muovu na kuahidiwa adhabu kali mno, hilo limewekwa bayana na Bwana Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote mwenye kunizulia mimi jambo basi ajichagulie makazi yake motoni.” Aidha amesema tena: “Mambo manne mojawapo likiwepo kwa mtu basi huyo ni mnafiki wa kweli hadi aachane nayo: Akiaminiwa hufanya hiyana, akizungumza husema uwongo, akiahidi hatekelezi na akigombana hufanya uovu.” 3

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Uchunguzi huu utatufichulia baadhi ya watafiti uchwara ambao wameinasibisha hadithi hiyo kuwa ni katika hadithi zilizozushwa, na kwamba haipo katika vitabu vinavyotegemewa na Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, eti hilo ni kutokana na dalili walizonazo kutoka kwenye vitabu ambavyo kwao huviona ni sahihi... Kwa hivyo Dk. Ali Ahmed Saaluus anaambiwa na aelewe kwamba Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” haikupokewa na Shi’a pekee bali imeelezwa katika vitabu mbalimbali vya Ahlus-Sunna na kwamba sehemu kubwa ya mlolongo wa wapokezi wake ni sahihi. Hivyo kama si mutawatiri, basi kitendo cha kuitia dosari na kuifanya dhaifu kitalazimu kuzifanya dhaifu hadithi zilizo nyingi za Bwana Mtume (s.a.w.w.). Na yatosha kuwa ushuhuda wa usahihi wa hadithi hiyo bali kuwa kwake Mutawatiri kwamba Imam Muslim ameeleza katika kitabu chake Sahih Muslim hadithi nne ambazo zote ni sahihi, aidha Tirmidhi katika kitabu chake Sunanut-Tirmidhi amezitaja kwa njia kadhaa wa kadhaa, ukiongezea aliyoyaeleza Imam Ahmad Imam wa madhehebu ya Hanbal katika Musnad yake, Nasaai ambaye ni mmoja wa waandishi wa vitabu sita sahih vya kisunni katika kitabu chake Khasais, na wengineo wasio kuwa hao kama atakavyofahamu mpendwa msomaji asiyekuwa na kasumba. Ili ajue kwamba Shi’a ni watu ambao wako mbali na uzushi na ukadhibishaji wa hadithi za Mtume (s.a.w.w), kwani wao wameshikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala na kizazi kitoharifu cha Bwana Mtume (s.a.w.w), kwani mwenye kushikamana navyo hatopotea kamwe, kama ilivyokuja katika hadithi ya Mtume (s.a.w.w.). Na uzushi na uongo ni katika upotovu, na mwenye kushikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wake ameepukana na upotovu, na kuanzia hapa unadhihiri upotoshaji wa yule ambaye anajaribu kuifanya dhaifu hadithi hiyo au kuikadhibisha.

4

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Huambiwa haya Dk. Saaluus na wengineo: Hakika miongoni mwa mifumo ya kielimu katika kujibu hoja ya mpinzani ni kwamba dalili inayotumika iwe katika dalili ambazo zinakuwa ni hoja juu ya mpinzani wake ili aweze kuikubali, sio atumie dalili au hadithi ambazo mpinzani wake hazijui, na kwa mfano huo Shi’a katika kuthibitisha yale wanayoyaamini wao hutumia dalili na nguvu ya hoja za hadithi sahihi ambazo zimeelezwa katika vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna, hivyo ni hoja thabiti kwa Dk. Saaluus, na kwa ajili hiyo itamlazimu kuzifanyia kazi hadithi hizo. Wala haipasi yeye awalazimishe Shi’a kuziamini hadithi wasizoziamini, hata kama zimeelezwa katika vitabu vyao, kwani hakuna vitabu vya Kishi’a vinavyoitwa Sahihi, bila shaka katika vitabu vya Kishi’a zimo hadithi sahihi kama vile pia zimo hadithi dhaifu na fasidi, bali zimo baadhi ya hadithi ambazo Shi’a hawaziamini. Na kwa ajili hiyo haifai wala sio haki mpinzani amlazimishe Shi’a kuzikubali isipokuwa hadithi hizo zikiwa zinategemewa na Wanachuoni wao ambao wanategemewa, na sio mtu yeyote yule kama alivyofanya Dk. Saaluus. Na hilo linapingana na kanuni na misingi ya kiislamu katika kujibu hoja, malumbano, mahojiano, mjadala na mdahalo, na kwa kuwa Dk. Saaluus ni mtu asiyejua misingi ya kujibu hoja, na mifumo ya ukosoaji, amejaribu kuifanya dhaifu Hadith Thaqalain ambayo imethibiti kwa waislamu wote. Lakini pindi lilipokuwa lengo la Dk. Saaluus ni kuwaponda Shi’a hata kama upondaji huo unaambatana na uzushi na kumkadhibisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) basi hayo yote yalikuwa mepesi kwake, kwa sababu lengo lake ni kuhalalisha na kujirahisishia njia ya kufikia lengo lake. Na kwa kuwa lengo lake ni kuwazulia Shi’a kwa njia yoyote ile inayowezekana, basi hakukuwa na kizuizi chochote kwake katika kuikanusha Hadith Thaqalain na hadithi zinginezo zilizopokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), kwani kuitikadi ukweli wa hadithi hiyo kutamlazimu kushikamana na kizazi kitoharifu Ahlul-Bayt (a.s.), Nao ni: Ali bin Abi Twalib, Fatimah Zahra na mabwana wa vijana wa peponi Maimamu wawili Hasan 5

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain na Husein (a.s.), na jambo hilo ni zito kwake asiloweza kulikubali kutokana na kutowakubali ndugu wa karibu wa Rasuul. Na tutalielezea hilo hapo baadaye kwa kutoa dalili kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna ili ukinai na kutosheka, hicho ni kilele cha hali ya juu cha ukarimu usio na mfanowe, pale tunapotoa dalili kuthibitisha jambo fulani juu ya mpinzani tunatumia hoja ambazo yeye huzikubali, pasi na kurejea na kutumia uzushi, uwongo au ubabaishaji kama tutakavyotoa baadhi ya mifano muda si mrefu. Hakika mbinu ya kuzifanya dhaifu hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ni mbinu walizozitumia Bani Umayya na Bani Abbas, ili wafiche fadhila na vyeo vya ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.), hiyo ni pale ziliposhindwa na kuwachosha mbinu zao za vitisho na mateso kwa Ahlul-Bayt (a.s.), kwa sababu hiyo walifanya chini juu kupotosha hadithi za Mtume kwa malengo ya kisiasa, kasumba, matamanio, chuki binafsi na akdi zao, katika kutokomeza kabisa fadhila za Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.). Hakika wasomi waajiriwa waliokuwa watiifu kwa tawala za wakati huo walichangia sana katika kubadilisha na kupotosha hadithi za Bwana Mtume (s.a.w.w.), na dalili zilizo wazi juu ya hilo ni kuwa Umma wa kiislamu, miongoni mwa Masunni hawajui lolote kuhusu Hadith Thaqalain iliyo kwa lafudhi ya: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” bali wapo baadhi yao wenye kukanusha mfano wa hadithi hiyo, na wanaamini kuwa ni katika hadithi iliyowekwa na Shi’a ili kuipinga hadithi inayosema: “Na Sunna yangu.” Wamefanya hivyo ili wawachanganye watu kuwa Shi’a ni miongoni mwa wabunifu wa hadithi, ambao hubadilisha maneno kutoka mahala pake, kwa chuki waliyonayo kwa ndugu zao masunni, au bughdha yao kwa sahaba wa Mtume (s.a.w.w.), japo inajulikana fika kwamba Shi’a ni watu wenye kushikamana zaidi na Sunna za Mtume (s.a.w.w.), kwa ajili hiyo wamefungua mlango wa kufutu mas’ala ili waweze kuchuja hadithi sahihi toka katika hadithi zisizo sahihi ambazo zinanasibishwa kwa Mtume (s.a.w.w.).

6

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Wapo wenye kujaribu kuponda vitabu vya Wanachuoni wa Kishi’a, kwa sababu tu hueleza baadhi ya hadithi ambazo huenda kinyume na akili, Qur’anii au Sunna, hufanya hivyo kwa lengo la kuwachanganya halaiki kwamba Shi’a huamini hadithi hizo, ilihali uhalisia ni kwamba Shi’a hawana vitabu vinavyoitwa sahihi kama ilivyo kwa Ahlus-Sunna, kwa hiyo kwa mujibu wa Shi’a wenyewe ni kuwa hadithi zinazoelezwa katika vitabu vyao zinastahili kukosolewa, kwani kama zilivyomo hadithi sahihi katika vitabu vyao hali kadhalika zimo dhaifu na zenye mapungufu, bali zimo hadithi zinazojulisha ghuluu1. Lakini lililothibiti kwa Shi’a wote ni kwamba maghulati wote wamepetuka mipaka na wametoka katika Uislamu, na riwaya hizi sio sahihi wala hazikubaliani na Shi’a bali wao wamezikadhibisha. Na wala kuwepo mtu mmoja au wawili wanaodai kuzingatia hadithi zote zilizomo katika vitabu hivi kuwa ni sahihi hakuwakilishi mtazamo wa Shi’a, bali hiyo ni rai na maoni ya mtu binafsi. kwa hivyo majaribio ya baadhi ya watu miongoni mwa Ahluls-Sunna kuziponda hadithi zote za Shi’a, hilo ni zoezi la kujaribu kupotosha ukweli na haki ambayo wanayo Shi’a, na mbinu hiyo ni mbinu ya wale waliotangulia miongoni mwa vibaraka wa Bani Umayya na Bani Abbas ili kuteketeza Ushi’a na wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) na kuwaweka watu mbali nao. Lau kama umma wa Kiislamu ungetaka ukweli na kufikia hakika na kupata maarifa ya hakika kama baadhi walivyoelewa, ingekuwa ni lazima kutafuta na kufanya utafiti kutoka katika vyanzo vya Wanachuoni wa Ahlus-Sunna pamoja na wapokezi wao wa hadithi, ili mtu mwenyewe ajionee yale yaliyopokelewa kutoka kwao miongoni mwa hadithi ambazo hufungamana na Ahlul-Bayt (a.s.), na mwenye kushuhudia baadhi ya hadithi hizo haangalii maana yake na madhumuni yake, bali wapo baadhi yao ambao hujitahidi kuzifanya dhaifu na kuzikadhibisha, na wengine hujaribu kuzieleza kulingana na matamanio yao, na hayo yamepitishwa na kutekelezwa na wale waliotangulia, na wakafuatiwa na waliokuja baada yao katika zama zetu hizi, zama za Sayansi na teknolojia na utafiti kuhusiana na haki, mfano Muhammad Nassur-diin Albaani, Dk. Aamir Najjar, Dk. Ali Ahmad Saaluus, Ihsan dhahir na wengineo wasiokuwa hao kati ya 7

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain wale ambao hujaribu kupotosha ukweli na kubadilisha maneno kutoka mahala pake kwa lengo la kuwatumikia maadui wa ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.) kama tutakapowadhihisha hilo katika kitabu hiki. Na kwa njia hiyo watu hawa wamejaribu kuifanya dhaifu Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” au hadithi kuitolea maelezo, kwani kushikamana na mfano wa hadithi hiyo na nyinginezo hubomoa nguzo ya msingi miongoni mwa nguzo za itikadi kwao, na kubatilisha taawili zote au utoaji maelezo wa aina yoyote ule ambao umetolewa kuhusiana na wale waliotangulia juu ya Maimamu wa Ahlul-Bayt (a.s.), hayo yote ni kutokana na muktadha wa kuwajibika kushikamana na Kitabu kitakatifu na kizazi kitoharifu, na hayo hayawaridhishi hao, kwa ajili hiyo wakajaribu kuiponda hadithi hiyo kwa upande mmoja na kuwakadhibisha wapokezi wake kwa upande mwingine, na wapo wengine wenye kuwatuhumu wapokezi wake, bila kujali kuwa wengi wao ni miongoni mwa watunzi wa vitabu sahihi na Musnad zao mbele ya Ahlus-Sunna kama vile sahihi Muslim, Tirmidhi, Ibn Maaja, Nasaai, Musnad ya Imam Ahmad bin Hambali ambaye ni Imamu wa madhehebu na wengineo ambao mpendwa msomaji utawatambua, wote hao wameipokea Hadith Thaqalain, kwa lafudhi ya: “Na kizazi changu AhlulBayt wangu” na kuieleza katika vitabu vyao, ilihali hao sio miongoni mwa Wanachuoni wa Kishi’a, hadi watuhumiwe kwa uzuaji, uzushaji na uwongo juu ya hadithi hiyo. Tunatoa mfano juu ya hilo, kwani kuna genge kubwa la wale ambao wanajidai na kujiita kuwa ni miongoni mwa Wanachuoni wa Ahlus-Sunna, ambao hujaribu kukadhibisha hadithi za Mtume na kusema riwaya hizo hazipo katika vitabu vya Ahlus-Sunna, na kwamba zenyewe ni uongo na uzushi wa Mashi’a. Lakini utafiti huu unatoa picha kamili ya watu hao, na kwa hivyo itambainikia mwislamu mwadilifu haki kutokana na batili, mkweli na muongo, hapo atagundua dhamira yao mbaya na litamthibitikia hilo kutokana na utafiti huo wa kielimu wenye kusimama juu ya uaminifu, na hadithi lukuki na sahihi za pande zote mbili. Mwenyezi Mungu swt. 8

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain anasema: “Halitamkwi neno lolote isipokuwa kwake Yeye liko katika uangalizi mkali.” Na kwa ajili ya siasa hiyo chafu ni siasa ya upotoshaji na ubadilishaji, ambayo ilitekelezwa na ukoo wa Amawiyya na Abbasiyya, baada ya kushindwa mazoezi yao ya kunyanyasa, kuadhibu na kuwaua Shi’a na Maimamu wao (a.s.), walibadilisha na kupotosha hadithi za Mtume (s.a.w.w.), kama walivyofanya hivyo katika Hadith Thaqalain, na hakika mbinu hiyo ilifuatwa na wale waliokuja baada yao, basi wakaweka kanuni maalum za kusihi hadithi na kutosihi kwake, na zile hadithi ambazo huelezea fadhila za Ahlul-Bayt (a.s.) wakasema:- Katika mlolongo wa wapokezi wake yupo Atwiya Aufi au Aamash hao watu hutuhumiwa kubuni hadithi, waliopotoka na watu wa bidaa, kwa sababu wao wamepokea hadithi inayohusiana na fadhila za Ahlul-Bayt (a.s.) hata kama walikuwa waaminifu na wa kweli, bali hata kama wakiwa miongoni mwa wapokezi wa Bukhari na Muslim katika sahihi zao ambazo hao wawili vitabu vyao ndio vitabu sahihi kuliko vyote baada ya Qur’anii kwa mujibu wa Ahlus-Sunna. Kwa mfano Atwiya bin Auf amepokea kutoka kwa Abu Saidi, Abu Huraira, Ibn Abbas, Ibn Umar, na Zayd bin Arqam, yeye ni miongoni mwa wapokezi wa Bukhari, naye pia ni kati ya wapokezi wa Abi Daud, na Tirmidhi amemueleza Atwiya Aufi katika kitabu chake ambacho huhesabiwa kati ya vitabu sahihi sita kwa Ahlus-Sunna, aidha ni miongoni mwa wapokezi wa Ibn Maaja, vilevile ni kati ya wapokezi wa Ahmad bin Hambali katika Musnad yake, na wasiokuwa hao kama alivyopokea hadithi inayoeleza fadhila za baadhi ya masahaba hata hivyo walimhukumu kwa ubunifu na upandikizaji wa hadithi kwa sababu amepokea Hadith Thaqalain kwa matamshi ya: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Pamoja na kuwa hadithi hiyo ilipokewa na watu lukuki achilia mbali Atwiya, Habib, na Aamashi, bila shaka imepokewa na wapokezi chungu nzima wote ni miongoni mwa watunzi wa vitabu sahihi na Musnad basi 9

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain virejewe hivyo ili ukweli wake ujulikane. Shahabi katika kitabu chake (Miizanul-iitidali Fi Naqdir-Rijaal) anasema katika wasifu wa Abaani bin Taaghlib Sheikh wa Shi’a: “Abaan bin Taghlub Kufiy ni shia lakini ni mkweli, sisi tunachukua ukweli wake na ni juu yake bidaa yake. Na amesifiwa kwa uadilifu na Ahmad bin Hambali, Ibn Mu’in na Abu Haatam, basi msemaji anaweza kusema: ‘Vipi imefaa kumsifia uaminifu mtu mwenye bidaa? Vipi mtu wa bidaa anakuwa mwaminifu?’ Na jawabu la maswali hayo ni kwamba bidaa imegawanyika katika sehemu mbili: Bidaa ndogo kama vile upotokaji wa Shi’a au Shi’a ambaye sio mpotokaji, na watu wa aina hiyo ni wengi miongoni mwa taabiina na waliowafuatia hao ambao wenye dini na wakweli, na lau zitakataliwa hadithi zilizopokewa na watu hao basi zitapotea na kutoweka hadithi kedekede za Mtume (s.a.w.w.) na huo ndiyo ufisadi wa bayana.”1 Na kauli hiyo ya kinagaubaga kutoka kwa Shahabii katika kitabu chake cha Mizanul-iitidali kuwa kuikataa hadithi ya Shi’a ni ufisadi mkubwa katika dini, na wengi miongoni mwa taabiina na waliokuja baada ya taabii walikuwa ni Shi’a, na walikuwa wakisifika kwa ukweli, uchamungu na uwanadini, na hizo ndizo sifa za wale wenye kushikamana na vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt (a.s.), na kwa ajili hii Dhahabi amemzungumzia Shariik bin Abdillah An-Nakhai akisema: “Amesema Ahmad bin Hambali: “Shariik ni kundi moja na Abi Is’haq ni madhubuti zaidi ya Zuheri.... na Abu Haatam amesema: Shariik ni mkweli ananipendeza sana kuliko Abu Ahwaswi na hakika Shariik ni Shi’a...”’ Dhahabii akasema: “Hakika Shariik alikuwa kati ya watu wenye elimu kubwa, amepokea kutoka kwake Is’haq al-Azraq hadithi elfu tisa na akasema Nasaai: “Hakuna ubaya kufanya hivyo.”’2 1 Mizanul-I’itidal fi naqdur-Rijal Juz. 1 Uk. 4 2 Mizanul-I’itidal fi naqdur-Rijal Juz. 1, uk. 271, 273, 274. 10

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na anasema Khatiibul-Baghdad katika tarjuma yake ya Muhammad bin Rashid mmoja wa wapokezi tisa wa Kishi’a: “Amesema Abdul-Razzaq: ‘Katika maisha yangu sijawahi kumuona yeyote mchamungu na mkweli katika mazungumzo zaidi yake,”’ yaani Muhammad bin Rashid. Abu Nadhri akasema: “Nilikuwa nazungumza na Shuuba, ghafla akajitokeza Muhammad bin Rashid, Shuuba akasema: ‘Sikuandika kutoka kwa huyu, ama yeye ni mkweli lakini ni Shi’a au Qadar?”’ Khatiibu-Baghdad anasema: “Ametupa habari Ibn Fadhili, ametuambia Ibn Darastuway ametupa habari Yakuub ibn Sufyani amesema: ‘Nilimuuliza Abdulrahman bin Ibrahim, nikamwambia: Muhammad bin Rashid? Akasema: Alikuwa akitajwa kwa Qadar ila yeye ni mkweli katika hadithi.”’3 “Wamepokea kutoka kwake Sufyan Thauri, Shuuba, Yahya bin Said AlQatwan, Abdul-Rahman bin Mahdi, Abunaiim, Abdul-Razzaq bin Hammam, Haytham bin Jamiil, Abu Nadhri Hashim bin Qasim na Ali bin Jaada. Ametuhadithia Abu Said Muhammad bin Mussa Aswarafi, ametueleza Abu Abbas Muhammad Ibn Yakuub al-Aswamu, ametuhadithia Abdullah bin Ahmad bin Hambal, amesema na nikamuuliza (yaani baba yake) kuhusu Muhammad bin Rashid anayesimulia kutoka kwa Makhuul akasema: “Ni mtu mwaminifu”. Aidha akasema Abdul-Razzaq: ‘Sijawahi kumuona mchamungu na mkweli katika mazungumzo kama vile yeye - yaani Muhammad bin Rashid.”’4 Nasema (Mtunzi): Pamoja na hayo yote na wapokezi wa Kishi’a kupewa sifa kemkem kama vile ucha Mungu, washika dini, wenye msimamo wa kweli na waaminifu katika upokeaji wa hadithi, pamoja na hayo tunakuta wababaishaji ambao lengo lao ni kuwatia doa na kuwapaka matope 3 Al-Khatibu Al-Baghdadiy: Juz. 5 uk 271 na 272. 4 Al-Khatibu Al-Baghdadiy: Juz. 5 uk 271. 11

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain wapokezi wa Kishi’a kwa kuwabambikizia sifa za hiyana, upotevu, uwongo na utapeli, ni baadhi ya wale ambao wanachuki binafsi na familia ya Bwana Mtume (s.a.w.w) na hata kama wakiwa ni miongoni mwa masheikh wa Bukhari katika kitabu chake Sahih Bukhari. Ibn Athiir anasema katika kitabu chake (Al-Kamil fi Ta’arikh) katika mambo yaliyotokea katika mwaka wa mia mbili na kumi na tatu (213): “Katika mwaka huo alifariki Abdullah bin Mussa Al-Abasi ambaye alikuwa faqiih na pia alikuwa Shi’a, naye ni miongoni mwa masheikh wa Bukhari ambao amewataja katika kitabu chake Sahih Bukhari”.5 Na Isma’il bin Abaan Al-Azdi Al-Kuufii Al-Waraqii ni Sheikh wa Bukhari aidha Yahya na Ahmad bin Hambali walipokea kutoka kwake na akasema Bukhari: Ni mkweli, na wengine walisema: Alikuwa Shi’a.”6 Anasema Dhahabi katika kitabu chake Miizan katika tarjuma ya Abdullah bin Umar bin Abdaan Al-Kuufii Mushkidana: “Abdallah bin Umar bin Abdan Al-Kurashii Al-Kuufii Mushkidana, ni mtu mkweli na mwenye kukubalika kwa hadithi... amesema Abu Haatam: Yeye ni mkweli, na ikawa yaeleweka kuwa ni Shia, amesema Bakr Ibn Muhammad AlSwayrafii na ambaye alimtaja Al-Hakim akasema: Ni msimulizi wa Khurasani katika zama zake, nilimsikia Swaleh bin Muhammad Juzrat anasema: Alikuwa Abdullah bin Umar bin Abaan akiwatahini wapokezi wa hadithi na mara nyingi walikuwa Shi’a.”7 Nasema kumwambia Uthman bin Muhammad al-Khamiis Nawiri: Muogope Mwenyezi Mungu na wala usiwe miongoni mwa wazushi katika maneno yako: “Basi utaona wale wapotovu (yaani Wanachuoni wa 5 Ibu Athir ndani ya Al-Kamil fit-Tarikh Juz. 5 uk .217. Pia tazama MizanulI’itidal Juz. 3 uk 16. 6 Mizanul-I’itidal Juz. 1 uk 212. 7 Mizanul-I’itidal Juz. 2 uk 466. 12

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Kishi’a) wanapotoshana, wanafanya hiyana bali wanasema uwongo, wanazusha na wanabadilisha ukweli na hizo ndizo bidhaa zao...!”8 Nasema: Tumeeleza mengi wanayosema Wanachuoni wa kisunni kwamba Shi’a wanasifika kwa ucha mungu, ukweli na uaminifu, na wenye sifa hizo hawawezi kuwa wazuaji, waongo na wageuzaji wa mambo, kwani ubadilishaji wa mambo sio sifa zao bali ni sifa za wale wasiokuwa wao kama utakavyoona katika maudhui hii, kwani matusi na shutuma si sifa za waumini achilia mbali wanazuoni. Na hoja huvunjwa kwa hoja na si kwa matusi na shutuma ambazo hazikubaliki na Waumini, na kama maneno hayo hayakukushangaza basi tumia nguvu ya hoja, usitumie matusi na kebehi kwani hiyo ni silaha ya mwenye kushindwa, kwani fikra hupambanishwa na fikra nyingine na kwa dalili ambayo inakuwa hoja kwa mpinzani wako. Ama kutukana kwenyewe ni sifa za wale wanaokwenda kinyume na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt Nabii (s.a.w.w.), kama tutakavyoona baadhi ya mifano hapo baadaye Mungu akipenda.

MDAHALO WETU NA AHMAD BIN HAJAR AALBUUTWAMIY KATIKA KITABU CHAKE - ALAQAIDUS-SALAFIYYAH Ahmad bin Hajar Aal Buutwamiy katika kitabu chake (al-AqaidusSalafiyah) anasema katika kuwajibu Wanachuoni wa Kishi’a kwa dalili za Qur’ani, hadithi na akili; haya ndio maneno yake: “Mwenyezi Mungu anasema: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Amepokea Ahmad bin Hambali katika kitabu chake Musnad kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Maswahaba wakasema: “Ewe Mjumbe wa 8 Kashful-Janiy uk. b. 13

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mwenyezi Mungu ni nani hao ndugu zako ambao ni wajibu wetu kuwapenda?” Akasema Mtume (s.a.w.w.): “Ali, Fatimah, na watoto wao”. Vivyo hivyo imekuja katika Tafsir Thaalabi, katika Sahih mbili (Bukhari na Muslim) na kadhalika”. Ibn Butwaamiy anasema: ‘Jawabu lina aina nyingi, moja wapo: Maombi ya kusihi hadithi na kauli yake: ‘Ahmad bin Hanbali amepokea hadithi hiyo katika Musnad yake’ ni uwongo wa bayana, na nakala za Musnad ya Ahmad mashaallah tunazo nyingi na hazina hadithi hiyo. Pili: Hakika hadithi hiyo ilizushwa na kupandikizwa, hilo ni kwa makubaliano ya wasomi na wataalamu wa hadithi, na kwa mantiki hiyo haipatikani hadithi hiyo katika kitabu rejea chochote.”’9 Nasema: Anajibiwa Ibn Aal Buutwamiy kama ifuatavyo: Mosi: Ama kauli yake: “Maombi ya kusihi hadithi hii...” huo ni uzushi juu ya Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao ambao waliipokea hadithi hiyo na wakaipasisha kuwa ni sahihi, nako ni kuwachanganya Ahlus-Sunna kwa kusema kwamba hadithi hiyo ni uzushi uliyopandikizwa, kwa makubaliano ya wasomi, ili kuwaweka mbali Waislamu kuhusiana na hadithi za Mtume (s.a.w.w.), na huo ni upotokaji wake wa bayana dhidi ya sunna za Mustafa (s.a.w.w.), na ni ubadilishaji wa maneno ulio wa dhahiri kabisa na huko ni kutangaza uadui wa wazi azi juu ya Ahlul-Bayt (a.s.). Pili: Ama kuhusu kauli yake: “Na kwa mantiki hiyo haipatikani hadithi hiyo katika kitabu rejea chochote ...” Tunasema kuwa, kafanya hivyo ama kutokana na ujinga wa kutoyajua yale yaliyomo katika vitabu vya Wanachuoni wa Ahlus-Sunna, kama methali isemavyo: “Udhuru wake ni ujinga wake.” Na ima ni kupitiwa na shetani hadi akasahau kumkumbuka Mwenyezi Mungu swt. na hatimaye akakanusha mfano wa hadithi hiyo 9 Al-Aqaidu As-Salfiyyah Juz. 2, uk. 332 - 333. 14

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ambayo imepokewa na kuthibitishwa na vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna na Masanid zao kama mpendwa msomaji atakavyofikia uhakika huo. Tatu: Sijui je ni itikadi ya waliopita hapo kabla kuzua na kumsingizia Mwenyezi Mungu swt. na Mtume wake (s.a.w.w.) na waumini pia, pamoja na kuwa watu waliotangulia walinukuu kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kuwa, aya ya Mawaddah (upendo) ambayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu swt. isemayo: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” iliteremshwa kuhusiana na Ali, Fatimah, na watoto wao wawili. Na hapana shaka kuwa watu waliotangulia ni wajuzi na wataalamu zaidi wa hadithi za Bwana Mtume (s.a.w.w.) kuliko Aal Ibn Butwaamiy. Nne: Inafaa kujua machache na ya msingi yaliyopokewa na kuelezwa katika vitabu vya Ahlus-Sunna kuhusiana na aya hiyo, ambayo mtu pekee aliyeikanusha kuwepo kwake ni Ibn Twaami, na akadiriki kusema kwamba Hadith Thaqalain imepandikizwa na ya uwongo kwa itifaki ya wataalam wa hadithi. Tuyajue hayo ili abainike mwongo na mkweli, wenye kushikamana na hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ni akina nani na wale ambao ndio wapinzani wa hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ni akina nani, tujue ni akina nani ambao daima hushikamana na sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w.) na ni akina nani wale ambao huacha na huenda kinyume na sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). 1: Anasema Al-Hakim Naysabuuri katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Maswahaba walisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao ambao imewajibika kwetu sisi kuwapenda?” Akasema Mtume (s.a.w.w.): “Ni Ali, Fatimah na watoto wao wawili,” na hadithi hiyo imepokewa kwa njia tofauti tofauti”.10 10 Shawahidul-Tanziil Juz. 2, uk. 130. 15

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 2: Na katika kitabu cha Jamiu-Ahkamul-Qur’ani cha Qurtubi: “Imepokewa kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi Mwenyezi Mungu alipoishusha aya hiyo, masahaba walisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao ambao tunalazimika kuwapenda?” Akasema (s.a.w.w.): ‘Ali, Fatimah na watoto wao.”’11 3: Na katika kitabu Anwarut-Tanziil cha Baydhawi: “Imepokewa kwamba pindi iliposhushwa aya hiyo iliulizwa: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao watu wako wa karibu?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ni Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’12 4: Na katika kitabu Al-Kashaaf cha Zamakhshari amesema: “Hakika pindi ilipoteremshwa aya hiyo iliulizwa: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao watu wako wa karibu ambao ni wajibu juu yetu kuwapenda?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ni Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’13 5: Katika Tafsir Gharaibul-Qur’ani ya Al-Allama Naysabuuri kutoka kwa Said bin Jubair, “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Masahaba walisema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! ni nani hao watu wako wa karibu ambao imewajibika kwetu kuwapenda?” Basi Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na wana wao wawili.”’14 6: Katika Tafsir Nasafii kwenye maelezo ya Tafsiril-Khaazin kwamba pindi ilipoteremshwa: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu, isipokuwa kuwapenda watu wa karibu yangu”, ikaulizwa: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao wa karibu yako ambao ni lazima juu yetu kuwapenda?” Basi akasema (s.a.w.w.): ‘Ali, Fatimah na wana wao waw11 Jaamiu Ahkamul-Qur’ani Juz. 16. uk. 21-22. 12 Anwarut-Tanziil uk. 642. 13 al-Kishaf, Juz. 3, uk. 402. 14 Tafsir Gharaibul-Qur’ani ya Naysabuuri Juz. 25, uk. 35 16

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ili:”’15 Wahusika wa aya hiyo ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) kama tutakavyoliashiria hilo kwa urefu muda mfupi ujao, wafasiri wote kuanzia Fakhru Raazi katika Tafsir yake, Twabari kutoka kwa Ali bin Husein, Ibn Kathiir, Suyuutwi katika kitabu chake Durru-Manthuur, Abi Suud na wengineo miongoni mwa wafasiri na Wanachuoni wakubwa wa AhlusSunna ambao Ibn Twaami katika kitabu chake alikanusha uwepo wa hadithi hiyo ndani ya vitabu vyao”, na hilo linajulisha ukanushaji wake wa hadithi sahihi za Mtume (s.a.ww.). Kwa hakika aliambatanisha na kuwabebesha Shi’a mzigo wa tuhuma kutokana chuki zake binafsi kwa Ahlul-Bayt (a.s.), kinyongo na akdi yake juu yao, kama walivyokuwa wale waliomtangulia kutoka Bani Umayyah. Hali kadhalika wanahifdhi wa Ahlus-Sunna waliinasibisha na kuihusisha aya hiyo na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) kama tutakavyolieleza hilo kwa kinaga ubaga hivi punde. 1: Ibnu Swabaan anasema katika kitabu chake kiitwacho Isa’afurRaaghibiina, mlango wa pili katika fadhila za Ahlul-Bayt ....., “Mwenyezi Mungu (s.w.t) anasema: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Amepokea Twabaraani, Ibn Abi Haatam, ibn Murdawayhi kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya hiyo masahaba wakasema: “Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nani hao akraba zako ambao aya hii imeshushwa kwao?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’16 2: Qunduuzi Al-Hanafii anasema: “Twabarani ameitaja hadithi hiyo katika kitabu chake Muujam Kabiir, Ibn Abi Hatam katika Tafsiri yake, Hakim katika kitabu chake Al-Wasiitwu, Abu Na’im Al-Haafidh katika kitabu 15 Tafsiri Nasfiibi Hamishi Tafsiri Khazin, Juz. 4, uk. 101 16 Is-aafur-Raaghibiina kwenye maelezo ya Nuurul-Abswaar uk. 113. 17

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain chake Hilyatul-Awliyaai, Thaalabi katika Tafsir yake, Al-Hamuwayni katika kitabu chake Faraidus-Simtwaini na wengi wengineo ambao wameeleza kuwa hadithi hiyo inawahusu watukufu hao watano.”17 3: Amesimulia Allama Hafidh Muhibbu Diin Twabari: Kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Watu wakasema: “Ewe mjumbe wa Allah ni nani hao akraba zako ambao ni wajibu wetu kuwapenda?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na wana wao wawili.”’ Ameeleza Ahmad katika kitabu chake Manaaqib kuwa, imepokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kuwa amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu amejaalia ujira wangu kutoka kwenu ni kuwapenda Ahlul-Bayt wangu, na mimi nitakuulizeni kesho akhera kuhusiana na hao.” Hali kadhalika amelieleza hilo Al-Malai katika kitabu chake cha siira.”18 4: Ametaja Ibn Maghazili Shafi’i: “Kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi iliposhushwa aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Masahaba wakasema: “Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuwapenda?” Akasema: ‘Ali, Fatimah na wanao wao wawili.”’19 Nasema: Hayo ni machache tu ambayo yameelezwa na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna pamoja na wafasiri wao ambao wameipokea Hadith Thaqalain ambayo aliukana uwepo wake mtunzi wa kitabu “AlAqaidus- Salafiyyah”, akiwa anafuata nyayo za wale wenye chuki na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.), na akaongeza kusema kuwa hadithi ya Aya ya mapenzi sio sahihi, aidha aliomba apewe maelezo juu ya usahihi 17 Yanabiiul-Muwaddah Juz. 1, uk. 105. 18 Dhakhairul-Uqba uk 25 - 26.

19 al-Manaqib cha Ibn Mughaziliy uk. 191 - 192 18

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain wake. Kwa itikadi yake hadithi hiyo ni yenye kubuniwa kwa itifaki ya wasomi wa hadithi, kwani alikanusha katakata uwepo wake katika vitabu vya Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna. Na hapo baadaye zitakuja hadithi lukuki kutoka katika vitabu rejea vya Wanachuoni wa Ahlus-Sunna, wanahifadhi wao na wafasiri wao, zenye kujulisha kuwa mradi wa AhlulBayt (a.s.) sawa iwe inahusiana na Aya ya Mapenzi au Aya ya Utakaso, ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). Na ninachokiamini mimi kuwa mtunzi wa kitabu (Al-Aqaidus-Salafiyah) na kitabu (Kashful-Jaaniy) na visivyokuwa hivyo viwili miongoni mwa wale wanaofanya chini juu ili kuhakikisha wanapingana na kukanusha hadithi sahihi za Bwana Mtume (s.a.w.w.), na huku wanajidai kuwa wao ni miongoni mwa Ahlus-Sunna, je! hadithi hizo sio hadithi za Bwana Mtume (s.a.w.w.) ambaye ametuamrisha kushikamana nazo na tuzifuate? Au Mtume (s.a.w.w.) ametuamrisha tujiepushe na sunna zake? La hasha Bwana Mtume (s.a.w.w.) hawezi kutuamrisha hivyo, kwani Mwenyezi Mungu swt. anasema: “Na anachokupeni Mtume kichukueni...” Lakini wapo baadhi ya wale ambao hutumia muda wao mwingi ili kuhakikisha kwamba sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w.) wanaziangamiza kabisa kutokana na chuki zao binafsi, kasumba na ukereketwa wao wa kijahiliya, aidha kufuata matamanio yao pamoja na uadui wao hata kama kufanya kwao hivyo kunakwenda kinyume na maandiko ya kisheria, na bila shaka hilo tutaliweka bayana pindi tutakapotaja aya mbalimbali ambazo zimeshushwa kuhusiana na Ahlul-Bayt (a.s.). Ibn Mughazili as-Shafi’i anasema: “Yakuub bin Hamiid amesema katika shairi lake: ‘Naapa kwa baba yangu hakika watu watano wameepushwa na uchafu, wametukuka na wametoharishwa tohara ya kabisa kabisa. Nao ni Muhammad Mustafa, Fatima, Ali, Shubbar na Shubbir. Hakika mwenye kuwatawalisha hao atatawalishwa na mmiliki wa arshi, na 19

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain atakuwa na uso wa kumeremeta na mwenye furaha. Na wenye kuwachukia hao watalaaniwa na Mwenyezi Mungu, na mafikio yao ni moto uunguzao.’”20

AHLUL-BAYT KATIKA AYA YA MAPENZI KWA MUJIBU WA VITABU VYA AHLUS-SUNNA. Mwenyezi Mungu swt. katika Suratul-Shuura aya 23 anasema: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Walijaribu baadhi ya watu na bado wanaendelea kujaribu kama tulivyoashiria hapo kabla kuwatenga Ahlul-Bayt (a.s.) kuhusiana na aya hiyo tukufu nao ni Imamu Ali, Bi Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). Hivyo wakati mmoja huihusisha na wake za Mtume (s.a.w.w.), ndugu zake na watu wake wa karibu, na wakati mwingine pia huihusisha na kaumu yake (s.a.w.w.), na majaribio yote hayo hayawezi kuvunja dalili zilizothibiti juu ya jambo hilo, kwani aya inakataa kabisa maana hizo, wala haiwaelekei washirikina kama wanavyodai baadhi ya watu, haiwezekani Bwana Mtume (s.a.w.w.) awaombe washirikina wawapende watu wa karibu yake, kaumu yake na jamaa zake, kwani wao ni maadui wa tawhiid, kwa hivyo zoezi la kubadilisha ukweli wa neno la Qurba na kusema linawahusu Waislamu wote, halina msingi wowote, kwa mantiki hiyo hapana budi maelekezo hayo yawe yanawaelekea waislamu wote kuwapenda watu maalumu wanaotokana na ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.) ambao wana mafungamano makubwa na Bwana Mtume (s.a.w.w.), bila shaka zipo dalili lukuki kutoka katika vitabu vya Ahlus-Sunna na Mahafidh wao achilia mbali zilizomo katika vitabu vya Kishi’a zikithibitisha kuwa kwa hakika mradi wa “Qurba” yaani watu wa karibu waliyotajwa katika aya, ni wale watu wa kishamiya, nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). 20 - Manaaqib ibn Mughazili uk. 191.

20

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Hakuna mwingine anayekuwa nao pamoja, wala haingii asiyekuwemo, sio wake wa Mtume (s.a.w.w.) wala watu wengine wa karibu, sembuse kaumu yake, kama wanavyodai baadhi ya watu. Nasi hapa tutataja Wanachuoni chungu tele wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao ambao walisema: “Ahlulbayt wanaohusika pekee ni Imam Ali (a.s.), Swiddiqatu Twahirah Fatimah Zahra (a.s.), na mabwana wa vijana wa peponi Hasan na Husein (a.s.)”, ili ithibiti hivyo kwa nguvu ya hoja yenye kukinaisha, na iwe hoja juu ya yule mwenye kukanusha kwamba aya hiyo haiwahusu watu hao au anayepinga kuwepo hadithi hiyo katika vitabu vya Ahlus-Sunna, kama alivyosema Dk. Saaluus, Ihsanllahi Dhahiir, Dk. Aamir Najjar, Muhammad Nasur diini Albaani katika kitabu chake Silsilatul-Ahadithi As- Sahiha, na wasiokuwa hao. Bila shaka zoezi na jitihada zao ni kuutenga umma wa kiislamu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) Ahlul-Bayt zake, ili wawachanganye watu hatimaye waelewe kwamba makusudio ya Ahlul-Bayt katika Aya ya Mapenzi si kama wasemavyo Shi’a bali ni kinyume, bali wajue mradi wa Ahlul-Bayt ni wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) na jamaa zake, na hakika watu hawa wanne wameingizwa katika aya hiyo tukufu kupitia mlango wa kujuzisha na kuruhusu, kwani Ahlul-Bayt halisi ni wakeze Mtume (s.a.w.w.), wanasema hivyo ili kupotosha ukweli, na hivyo ndivyo watu hao wanavyoendesha zoezi hilo la kubadilisha sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w.), kumkadhibisha Mtume (s.a.w.w.), kuwasingizia wafasiri wa Qur’anii wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, kwa hivyo inakupasa ewe ndugu yangu msomaji uwe mtafiti juu ya haki na ukweli ili umridhishe Mola wako Mlezi. Na ufuatao ni mfano tu wa yale wanayoyasema wasomi wakubwa wa Ahlus-Sunna, naomba uyazingatie na kuyafanyia utafiti wa kina.

21

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

KITABU SHAWAHIDUT-TANZIIL CHA HAKIM HASKAANI: Hakim Naysaabuuri naye ni mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa AhlusSunna na mfasiri wao ameitaja Aya ya Mapenzi katika Tafsiir yake kwamba, aya hiyo iliteremshwa kwa ajili ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) na kwa ujumla yafuatayo ni katika aliyoeleza Al-Hakim: a) “Imepokewa hadithi kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Pindi iliposhushwa aya inayosema: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Wakasema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuwapenda?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na wana wao wawili.”’ b) “Na katika hadithi nyingine kama ilivyopokewa na Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu.” Masahaba wakasema: “Ni nani hao karaba zako ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kwetu kuwapenda?” Akasema (s.a.w.w.): ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’ Na katika hadithi nyingine maswahaba walisema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha kuwapenda?” Akasema (s.a.w.w.): “Fatimah, Ali na watoto wao wawili.” Na katika hadithi nyingine imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas aidha amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya: “Sema sitaki.....”. Masahaba wakasema: “Ni nani hao Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni lazima tuwapende.” Akasema (s.a.w.w.) ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’

22

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain c) “Kutoka kwa Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya iliyotangulia Masahaba wakasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ni nani hao ambao imewajibika juu yetu kuwapenda?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ali, Fatimah na wana wao wawili.” Na akasema Isma’il: “Na watoto wake (Yaani Fatimah)”. Aidha imepokewa kutoka kwake walisema Maansari kati yao: “Lau tungemkusanyia Mtume (s.a.w.w.) mali ya kutosha kiasi hawezi kumfikia yeyote,” na baadhi yao wakasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ukitaka tukupe mali sema tukulimbikizie mali,” basi Mwenyezi Mungu swt. akateremsha Aya hii: ‘Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu ila kuwapenda watu wangu wa karibu,”’21 na hadithi nyingi nyinginezo ambazo zimepokewa na Ibn Abbas ambazo zote zinathibitisha kwamba Ahlul-Bayt na karaba wa Mtume (s.a.w.w.) ndio ambao wamekusudiwa katika aya husika ambao ni wane, nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) na haingii yeyote katika ndugu zake wa karibu wasiokuwa hao. Ifahamike kwamba Ibn Abbas ni Ibn ammi yake Mtume (s.a.w.w.), naye hakudai hata mara moja kuwa ni miongoni mwa karaba wa Mtume (s.a.w.w.) ambao ilishushwa aya tukufu hiyo juu yao, naye ni wino wa umma na mjuzi miongoni mwa wajuzi wa Ahlus-Sunna, na hiyo inajulisha kuwa Ahlul-Bayt katika aya hiyo ni wanne, kuna watoto wengi wa Mtume (s.a.w.w.) na wote hao hawakudai na kujinasibisha na karaba wa Mtume (s.a.w.w.), na hiyo inavunja hoja inayosema karaba za Mtume (s.a.w.w.) ni watu wote au ndugu wote nao ni karaba wa Mtume (s.a.w.w.) ambao wameashiriwa katika Aya ya Mapenzi.

21 Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk. 130 - 132. 23

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 2). TAFSIRUL-KABIIR CHA FAKHRU RAAZI: Anasema Fakhru Raazi ambaye ni mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna katika tafsiri ya maneno ya Mwenyezi Mungu swt.: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu,” “Na mimi nasema hivi: Ndugu wa Muhammad (s.a.w.w.) ni wale ambao uzito wa mambo yao huelekezwa kwake, na kila ambao uzito wa mambo yao unamwelekea yeye zaidi na kwa ukamilifu wa hali ya juu, bila shaka watakuwa hao ni ndugu wa Rasuuli, na hakuna shaka kwamba wahusika wa aya hiyo ni Fatimah, Ali, Hasan na Husein, ambao mafungamano baina yao na mjumbe wa Mwenyezi Mungu yalikuwa makubwa zaidi, na hivyo ikawajibika wao ndio wawe aali Rasuul. Aidha watu wametofautiana kuhusu aali Rasuul, wapo waliosema kuwa ni wale karaba wa Mtume (s.a.w.w.), na imesemwa aali wake ni umma wake, na kama tutawachukulia karaba kuwa ndio aali Rasuul.... basi amepokea Mtunzi wa Kitabu Al-Kashaf kwamba ilipoteremshwa aya hiyo sahaba walimuuliza Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Mtume, ni nani hao karaba ambao imefaradhishwa kwetu kuwapenda?” Akasema: “Ali, Fatimah na watoto wao wawili.” Hivyo imethibitika kwamba watu hao wanne ndio hasa karaba wa Mtume (s.a.w.w.), na iwapo itathibiti hivyo itawajibika wawe makhsusi kwa utukufu wa ziada, na hayo yanathibitishwa na mielekeo ifuatayo: Mosi: Nassi: Maneno ya Mwenyezi Mungu swt.: “Isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu”, na katika kuthibitisha hilo, hoja yake ni kama ilivyokwishaelezwa hapo kabla. Pili: Hapana shaka kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anampenda Fatimah (a.s.), na amesema (s.a.w.w.): “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu, huniudhi mimi linalomuudhi yeye.” Imethibti kwa upokezi wa kimaandishi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anampenda Ali, Hasan na Husein, na iwapo hilo litathibiti basi itawajibika kwa umma wote wa Kiislamu kuwafuata kulingana na maneno ya Subhaanahu wa Ta’ala anasema: “Na wakamfuata ili wapate kuongoka.” 24

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Tatu: Hakika kuwaombea dua aali wa Mtume (s.a.w.w.) ni cheo adhimu sana, na kwa sababu hiyo ikafanywa ni dua ya kuhitimisha Swala katika kutoa Shahada na Salam pale inaposomwa: ????? ???? ???????? ????? ‘Allahumma Swalli ala Muhammad Wa aali Muhammad’ “Ewe Mola Wangu mpe rehema na amani Muhammad na ndugu wa Muhammad”, Kuadhimishwa huko na utukuzwaji huo hakupatikani kwa mtu yeyote isipokuwa kwa ndugu wa Mtume (s.a.w.w.), basi yote hayo na yanayofanana na hayo yanajulisha kuwa upendo na mapenzi kwa ndugu wa karibu wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) ni wajibu. Imam Shafi’i (r.a.) amesema katika shairi lake: ‘Ewe Mwenye kupenda simama mina mahala patulivu, ambapo watu hunong’ona kwa utulivu, na unadi kwa sauti ya mwamko. Usiku pindi mahujaji wakifurika sehemu ya mina, kwa hakika huwa mkusanyiko mkubwa kama vile mafuriko ya mto Furati. Ikiwa kuwapenda ndugu wa Muhammad ni usaliti na kutoka katika dini, basi vishuhudie vizito viwili hakika mimi ni msaliti.”’22 3). KITABU MANAQIBU CHA IBN MUGHAZILI SHAFI’I. Amepokea Said bin Jubair kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Sema sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu” Watu wakasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu ameamrisha kuwapenda?” Mtume Muhammad (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’23 22 Tafsirul-Kabiir Juz. 24 uk. 142 - 143. 23 Manaqib, uk. 191 – 192. 25

7/1/2011

4:05 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 4. KITABU YANABI’UL-MAWADDAH CHA AL-QUNDUZIY: Al-Qunduziy amesema: “Amepokea Ahmad bin Hambal katika Kitabu chake Musnad Ahmad kwa Sanadi yake kutoka kwa Said bin Jubeir kutoka kwa Ibn Abbas (r.a.) amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Sema sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu.” Sahaba wakasema: “Ewe Mtume, ni nani hao ambao imewajibika kwetu sisi kuwapenda?” Akasema:’Ali, Fatimah, Hasan na Husein.”’ Al-Qunduuziy anasema: “Twabaraani ameeleza hadithi hiyo katika kitabu chake Muujamul-Kabiir, Ibn Abi Hatam katika Tafsiir yake, Haakim katika kitabu chake Manaaqib, Wahidi katika kitabu chake Al-Waaswitwu, Abu Naim Al-Haafidh katika Kitabu chake Hilyatul-Awliyai, Thaalabi katika Tafsir yake, Al-Hamuwayni katika kitabu chake Faraidus-Samtwayn... na wasiokuwa hao ambao wote wameipokea hadithi hiyo kutoka kwa Wanachuoni wao”.24 5. KITABU AL-KASHAAF CHA ZAMAKHSHARI: Zamakhshari katika kitabu chake cha Tafsiri anasema: “Imepokewa kwamba pindi ilipoteremshwa aya hiyo sahaba wakasema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao karaba wako ambao imewajibika kwetu kuwapenda?” Akasema (s.a.w.w.): “Ali, Fatimah na watoto wao wawili.” Na hayo yanajulishwa na yale yaliyopokewa kutoka kwa Ali bin Abi Twalib (r.a.): “Nilishitaki kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na husda za watu kwangu akasema: ‘Ridhia kwani wewe utakuwa ni mmoja kati ya watu wanne wa mwanzo kuingia peponi, nao ni mimi, wewe, Hasan na Husein...”’25

24 Yanabiiul-Mawaddah Juz. 1, uk. 105. 25 Tafsirul-Zamakhshari Juz. 4, uk. 19 - 22. 26

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 6. KITABU ANWARUT-TANZIIL WAASRARUT-TAAWILI CHA BAYDHAWI: Baydhawi anasema katika Tafsiri yake: “Imepokewa kwamba pindi iliposhushwa Aya hiyo sahaba wakasema: ‘“Ewe Mtume, ni nani hao ndugu zako wa karibu?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘ Ali, Fatimah na wana wao wawili....”’26 7. KITABU JAAMIU AHKAMUL-QUR’ANI CHA QURTUBI: Qurtubi katika kutafsiri aya hiyo anasema: “Watu waliuliza: “Ewe Mtume, ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao wameelezwa katika aya hii: Sema, sihitaji malipo yoyote isipokuwa...” Akasema: “Sikuombeni ujira wowote isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu Ahlul-Bayt wangu.” Kama vile alivyoamrisha watukuzwe na kuheshimiwa ndugu zake wa karibu, na hayo ni maneno ya Ali bin Husein, Amru bin Shuaib na Sandai. Ama katika riwaya ya Said bin Jubeir amepokea kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi Mwenyezi Mungu aliposhusha aya hii: “Sema sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu”, ikaulizwa: “Ewe Mtume, ni nani hao tuwapende”” Akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’27 8. TAFSIR RUUHUL-MAANIY YA SHEIKH ISMA’IL BURUSAWIY: Burusawiy katika Tafsir yake anasema: “Ama maana ya “isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu,” ni upendo uliyothibiti na wenye kupatikana kwao, imepokewa kwamba ilipoteremshwa aya hiyo sahaba waliuliza: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao ni wajibu wetu kuwapenda?” Akasema: “Ali, Fatimah na watoto wao” yaani Hasan na Husein (r.a.) na hilo linajulishwa na yale yaliyoelezwa na Ali bin Abi Twalib (r.a.) aliposema: “Nilishitaki kwa 26 Anwarut-Tanziil cha Baydhawi Juz. 25 uk. 642. 27 Jamiul-Ahkamul-Qur’ani Juz. 16, uk. 21-22. 27

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na husda za watu kwangu basi (s.a.w.w.) akasema: ‘Ridhia kwani wewe ni mmoja kati ya wanne ambao watakuwa wa mwanzo kuingia peponi...”’28 9. TAFSIRUL-QUR’ANI YA IMAM AN-NASAFII: An-Nasafii amepokea katika Tafsir yake kwamba: “Iliposhushwa aya iliyokwishatangulia, ikaulizwa: “Ewe Mtume ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao ni lazima tuwapende” Akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’29 10. KITABU JAAMIUL-BAYAAN FIT-TAAWIILIL-QUR’ANI CHA TWABARI: Imepokewa kutoka kwa Abu Daylami amesema: “Pindi Ali bin Husein alipoletwa mateka na kusimamishwa katika mnara wa Damascus, akasimama mtu miongoni mwa watu wa Sham akasema: “Sifa zote njema anastahiki Mola Mweza ambaye amekuuweni, kukufanyeni mateka na kukata mzizi wa fitina,” akasema Ali bin Husein (r.a.) na kumwambia: “Je! umesoma Qur’anii?” Akajibu: “Ndio.” Akasema: “Je! umesoma ndugu wa Haamiim?” Akajibu: “Nimesoma Qur’anii wala sijasoma ndugu wa Haamiim,” Akasema: “Je! hujasoma aya inayosema: “Muwapende ndugu zangu wa karibu?” Akasema: Kwani hao ndio nyinyi?” Akasema: ‘Ndio.”’30 11. KITABU DHAKHAIRUL-UQBA CHA MUHIBBU TWABARI: Ameeleza Hafidh Muhibbu diin Twabari kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Pindi iliposhushwa aya inayosema: “Sema; sihitaji malipo yoyote kuto28Tafsirur-Ruuhul-Maani Juz. 8, uk. 311. 29 Tafsirul-Qur’ani ya Imam An-Nasafii Juz. 3, uk. 293. 30 Jaamiul-Bayani fit-Taawilil-Qur’ani Juz. 25, uk. 25. 28

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ka kwenu...” Walisema: “Ewe Mtume ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao imefaradhishwa kwetu kuwapenda?” Akasema: “Ali, Fatimah na watoto wao wawili,” aidha ameeleza Ahmad katika kitabu chake Manaqib, imepokewa kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Mwenyezi Mungu amefanya ujira wangu kutoka kwenu ni kuwapenda Ahlul-Bayt wangu, na mimi nitawauliza kesho akhera kuhusiana na hao.” Muula amesema hayo yapo katika kitabu chake cha Siira.”31 12. KITABU IS’AAFUR-RAGHIBIINA CHA IBN SWAABAN: Imekuja kutoka kwa Swaaban: Mlango wa pili katika Fadhila za AhlulBayt... Mwenyezi Mungu swt. anasema: ‘“Sema; Sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu.’ Aidha amepokea Twabaraani, Ibn Abu Hatam na Ibn Murdawayhi kutoka kwa Ibn Abbas kwamba ilipoteremshwa aya hiyo wakasema: “Ewe Mtume ni nani ndugu zako wa karibu ambao aya hii imeshushwa kwa ajili yao? Akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’32 13. KITABU NUURUL-ABSWAAR CHA SHABALANJI: Anasema Shabalanji: Amepokea Imam Abu Hasan Al-Baghawi katika Tafsir yake, kwa Sanad yake inayokwenda hadi kwa Ibn Abbas (r.a.) ambaye amesema: “Pindi ilipoteremshwa aya hii: “Sema sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu,” wakasema: “Ewe Mtume, ni nani hao ambao Mwenyezi Mungu ametuamrisha tuwapende” Akasema: “Ali, Fatimah na watoto wao wawili,” na katika kitabu Musamarati cha Sheikh Akbar ni kuwa Abdallah bin Abbas amesema hayo katika kuunga mkono maneno ya Mwenyezi Mungu anayosema: ‘Wanatekeleza nadhiri.”’33 31 - Jaamiul-Bayani fit-Taawilil-Qur’ani Juz. 25, uk. 25. 32 Dhakhairul-Uqba uk. 26. 33 Is’aafur-Raghibiina uk. 113. 29

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

14. TAFSIRUL-BAHRUL-MUHIIT YA ABU HAYYAN ANDALUSI: Na jambo ambalo linajulisha kwamba Aya ya Mapenzi (Mawaddah) imeteremshwa kuhusiana na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) ni maneno ya Abu Hayyan Andalusi, na akaongeza kusema kuhusiana na aya hiyo, yaani maana ya aya hiyo kwamba imeteremshwa ikiwa makhsusi kwa watu hao wanne: “Ali bin Husein bin Ali bin Abi Twalib alitoa ushahidi kwa kutaja aya hiyo pindi alipochukuliwa mateka hadi Sham, nayo ndio kauli ya Ibn Jubeir, Saday na Amru bin Shuaib, na kwa Taawiili hiyo Ibn Abbas amesema: Ilipoulizwa “Ewe Mtume ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao Mola Manani ametuamrisha tuwapende?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’34 15. TAFSIRUD-DURRUL-MANTHURU YA SUYUUTWI: Ameeleza Said bin Mansuur amepokea kutoka kwa Said bin Jubeir: “Isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu” akasema: Ni ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.), na amepokea Ibn Jariir kutoka kwa Abu Daylami amesema: “Pindi alipoletwa Ali bin Husein (r.a.) mateka walisimamishwa katika mnara wa Damascus, akasimama mtu mmoja miongoni mwa watu wa Sham akasema: “Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amekuuweni na kukufanyeni mateka”, hapo akasema Ali bin Husein (r.a.) na kumwambia: “Je! Umesoma Qur’anii?” Akasema: “Ndio,” akasema: “Je, Umesoma ndugu wa Haamiim?” Akajibu: “Hapana. Akasema: “Hujasoma aya hii? “Sema sihitaji malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu.” Akasema: “Kwani nyinyi ndio hao?” Akasema: ‘Ndio”’.35

34 Tafsirul-Bahrul-Muhiit Juz. Uk. 516. 35 Tafsirud-Durrul-Manthuur Juz. 5 Uk. 701.

30

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 16. TAFSIR GHARAIBUL-QUR’ANI YA AL-QUMMIY ANNAYSABUURI: Na katika Tafsir Gharaibul-Qur’ani ya Allama Al-Qummiy AnNaysabuuri katika mstari wa pambizo wa Jaamiul-Bayaan ya Twabari kutoka kwa Said bin Jubeir pindi ilipoteremshwa aya hii: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwa penda ndugu zangu wa karibu”, wakasema: “Ewe Mtume ni nani hao ndugu zako wa karibu ambao ni lazima sisi kuwapenda?” Akasema: ‘Ali, Fatimah na watoto wao wawili.”’ Nasema hayo ni machache tu kati ya yale ambayo yamo katika vitabu vya Ahlus-Sunna, kuwa Aya ya Mapenzi iliteremshwa ikiwa makhsusi kwa Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), kwa kiwango hicho tumetosheka na kuelewa kwamba Aya hiyo inawahusu watu hao wanne, kwa hivyo Dk. Aamir Najjar, Ust. Muhammad bin Nassur Diin Abaani, Dk. Ali Ahmad Saaluus na wengineo ambao wana fikra kama zao, yawapasa kufahamu kuwa Shi’a hawaamini hivihivi tu wala kuitikadi jambo lolote lile kibubusa isipokuwa hutegemea hadithi ambazo Waislamu wote wamekubaliana usahihi wake, ili iwe dalili na hoja kwamba wanayoitikadi ni sahihi na yaliyosimamia nguvu ya hoja, na iwapo hadithi hizo zote zitakuwa ni miongoni mwa hadithi zilizopandikizwa basi zitakuwa zimepandikizwa na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, na hilo halisemwi na yeyote kwa sababu kusema hivyo itapelekea na kusababisha kuwatuhumu viongozi na Maimamu wao kwa upandikizaji wa hadithi, kwa mantiki hiyo hapana budu kutangaza, kukubali na kusalimu amri kwa dalili za hadithi hizo, na bila shaka itawajibika kwetu kuwakubali na kuwafuata wale ambao Mwenyezi Mungu swt. amefanya wajibu kuwapenda hao, na hayo ni kwa mujibu wa hoja ifuatayo: Hakika kuwapenda Ahlul-Bayt (a.s.) ni faradhi kulingana na aya tukufu iliyokwisha tangulia hapo kabla, na kila yule ambaye imefaradhishwa juu yake kupendwa ni dhahiri shahiri ni wajibu kumtii kwa muktadha wa 31

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain maneno ya Mwenyezi Mungu swt. anasema: “Ikiwa mwampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni.” Na kwa munasaba huo nasema: Utakapothibiti wajibu wa upendo aidha huthibiti wajibu wa utiifu, na yule ambaye imewajibika kutiiwa vile vile huwajibika kufanywa kiongozi au imamu, kwa hivyo basi mbele yetu tuna nguvu ya hoja, nayo ni mfumo wa nguvu ya hoja wa kimantiki katika aina ya awali: Yeyote mwenye kuwajibika kupendwa ni wajibu kutiiwa. Na kila mwenye kuwajibika kutiiwa ni wajibu kufanywa kiongozi. Hatimaye tija ni: Yeyote mwenye kuwajibika kupendwa ni wajibu kufanywa kiongozi. Ama hoja mwambata ni maneno matukufu ya Subhaanahu wa Ta’ala: “Sema Sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda ndugu zangu wa karibu.”

AHLUL-BAYT KATIKA AYA YA UTAKASO KWA MUJIBU WA VITABU VYA AHLUS-SUNNA Mwenyezi Mungu swt. katika Suratul-Ahzab aya 33 anasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na kukutakaseni tohara ya kabisa kabisa.” Mosi: Dk. AAMIR NAJJAR NA AYA YA UTAKASO: Waislamu wote kwa ujumla wameafikiana kuhusiana na Aya ya Utakaso kwamba iliteremshwa juu ya Imam Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna ambao ni Wafasiri wa Qur’ani na Mahafidh wao wameifasiri Aya husika kwa kuwahusisha watu hao wanne (a.s.), kama waaminifu miongoni mwao walivyoielezea hiyo katika vitabu vyao sahihi na Musnad zao, kati yao ni Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim ambacho kwa mujibu wa Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna ndio kitabu sahihi mno baada ya Qur’anii, na pia kama vile 32

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Tirmidhi katika kitabu chake Sunanu Tirmidhi, Imam Ahmad bin Hambali katika kitabu chake Musnad Ahmad, Nasaai naye ni mmoja kati ya watunzi wa vitabu Sahih sita katika kitabu chake Khasais na wengineo wengi ambao wamo Mahafidh wa hadithi miongoni mwa Ahlus-Sunna, kama tutakavyoashiria hilo hapo baadaye Inshaallah. Na wapo wale ambao wanajaribu kukadhibisha na kuikanusha hadithi hiyo na kuiona siyo chochote, hata kama imepokewa na kuwemo katika vitabu vyao sahihi, ili kubadilisha maneno ya Mwenyezi Mungu pamoja na chuki zao binafsi kwa watu wa nyumba ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), na miongoni mwao ni Dk. Amir Najjar katika kitabu chake alichokiita “Shia wa Imamatu Ali” amejaribu katika kitabu hicho kupotosha yale yaliyosemwa kwamba Aya hiyo inawahusu watu hao wanne, na akalikanusha hilo na kusema kuwa hizo ni hadithi za Shi’a, aidha akakanusha kwamba Wanachuoni wa Ahlus-Sunna hawakuihusisha na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). Bila shaka ana lake jambo na hatofautiani na wale waliomtangulia miongoni mwa wale ambao hawakuona taabu kumzulia Mwenyezi Mungu swt. na kukadhibisha hadithi za Mtume (s.a.w.w.), na hiyo ndiyo sifa ya wale ambao wameacha kushikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume kitoharifu, na hilo linadhihirisha uzoefu wao mkubwa wa uwongo, kwa mantiki hiyo hatushangai kumuona Dk. Aamir Najjar akikanusha kwamba Aya ya Utakaso imeteremshwa ikiwahusu watu hao wanne, ukiachilia mbali hayo, yapo yaliyopokewa na kuelezwa na Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim. Dk. Aamir Najjar hakutosheka kwa hilo bali alijasirika kuwabebesha tuhuma nzito Shi’a katika kitabu chake, amesema: “Bali miongoni mwao yaani Wanachuoni wa Kishi’a - wamefikia kiwango cha kusema: ‘Aya ya Utakaso haina uhusiano wowote ule wa hapo kabla, na wala baada yake katika baadhi ya Aya, na hiyo imewekwa ili kuleta mvurugano, mfarakano na mtafaruku baina yake, ama kwa amri ya Mtume (s.a.w.w.) au utungaji 33

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain na uzushaji wa hadithi baada ya kufariki kwake.”’ Aidha anasema: “Na pindi ilipokuwemo Aya ya Utakaso katikati ya Aya ambazo zinawazungumzia wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) na wala haichukuliwi juu ya taawili yoyote, kwa hakika vibaraka na mamluki wa Abdullah bin Sa’bah ambaye ni Yahudi, hawakupata mwanya na hila za kupotosha ukweli ila kutumia hadithi ambazo kwazo watapata nafasi ya kulipotosha na kuligeuza neno toka sehemu yake na kuziepusha Aya na makusudio yake. Nasema kuhusiana na Dk. Aamir Najjar: “Sijui ni chuo kikuu gani katika vyuo vikuu vya ulimwenguni ambacho amehitimu na kukabidhiwa shahada ya udaktari, ni shahada gani ambayo inatolewa kwa mtu ambaye hajasoma hata chembe ndogo ya tabia na maadili mema ya Wanachuoni! Je! Hujawahi kuona maneno ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema: “Miongoni mwa sifa za mnafiki anapozungumza husema uwongo na anapozozana hufanya uovu.” Na sisi twajiweka mbali ili tusifikie katika kiwango hicho, hatutakabiliana kwa tuhuma za matusi, kwa sababu sisi tumeshikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt Rasuul, aidha tumejifunza kutoka katika vyuo vyetu kwamba fikra haijibiwi ila kwa fikra na hoja haivunjwi isipokuwa kwa hoja ambayo ni ngangari zaidi, sio kwa ubabaishaji na kubwabwaja hovyo, na ulipokuwa Dk. Saaluus miongoni mwa wasaliti wa vizito viwili, ndio maana tukakuona unachokijua na kukimiliki ni shutuma na matusi, pasina kutumia silaha ya kitaalam, maarifa na nguvu ya hoja, na sisi tunatumia silaha ya elimu, maarifa na nguvu ya hoja kutoka katika madrasa ya Ahlul-Bayt wa Nabii (s.a.w.w.) ambao ni kitivo cha elimu na maarifa, kwa hivyo basi sisi tunakabiliana na matusi na shutuma zako kwa hoja kutoka katika vitabu ambavyo unavitegemea wewe na wale ambao wana chuki binafsi kwa wafuasi wa ndugu wa karibu wa Muhammad (s.a.w.w.) ili ikupambanukie mpendwa msomaji tofauti kubwa iliyopo kati ya mwenye kushikamana na kizazi kitoharifu cha Mtume (s.a.w.w.) na wale wasioshikamana nao.

34

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Kisha tunasema kumwambia Dk. Aamir Najjar kwamba Aya ya Utakaso imeteremshwa kwa ajili ya watu wa Kishamiya nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) wala haiwahusu wakeze (s.a.w.w.), na hilo wamekubaliana Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao. Kwa mfano Imam Muslim katika Sahih yake, Tirmidhi katika kitabu chake Sunanut-Tirmidhi, Imam Ahmad bin Hambali katika kitabu chake Khasais ambacho ni kimoja kati ya vitabu sahihi na vinavyotegemewa kwa Ahlus-Sunna, bali hata Imam wa Hadithi Ibn Taymiyya amehukumu na kukubali kwamba ni sahihi kuwa Aya ya Utakaso iliteremshwa kuhusiana na hao wanne (a.s.), basi ni jambo la lazima Dk.. anasibishe na kuhusisha upotoaji na ubadilishaji wa maneno juu ya wale ambao wamesema na kukiri kwamba Aya hiyo tukufu imeteremshwa makhsusi juu ya hao wanne (a.s.) pasi na kuwasingizia Wanachuoni wa Kishi’a na kuwatuhumu kuwa wao ni vibaraka na mamluki wa Abdallah bin Sabah ambaye ni Yahudi, na hiyo sio sifa ya Wanachuoni bali ni miongoni mwa sifa za majahili au mambumbumbu na mazumbukuku wenye kueneza kasumba na propaganda mbaya katika itikadi ya Shi’a, aidha wanapotosha haki na ukweli, kwa ajili ya vitu visivyo na thamani au kwa lengo la kujilimbikizia mali zaidi, kwa kitu fulani au maslahi ya muda mfupi. Na sisi tunaelekeza baadhi ya yale yaliyoelezwa na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna kuhusiana na Aya ya Utakaso, ili afahamu Dk.. na wenzake kwamba Shi’a wanashikamana zaidi na tafiti za kielimu na nguvu za hoja ambazo husimama juu ya ukweli na uaminifu katika nukulu, rejea na vithibitisho, bila ya kuwepo msukumo au maslahi duni ya kidunia, na utaelewa mengi na kwa kirefu muda si mrefu Inshallah. Anasema Ibn Taymiyya katika kitabu chake (???? ?? ????? ??? ?????? yaani ‘Haki za Ahlu-Bayt baina ya Sunna na Bidaa’, naye ni Imam na Sheikh wa Dk. Aamir Najjar, haya hapa maneno yake: “Kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hiyo Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika kishamiya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ndio Ahlul-Bayt wangu waondolee 35

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain uchafu na watoharishe tohara kabisa kabisa.”’36 Namwambia Dk. Aamir Najjar: Wewe unamjua Ibn Taymiya na upinzani wake juu ya Mashi’a, hata hivyo ameifasiri Aya hiyo tukufu juu ya watu hao wanne (a.s.), kwa mantiki hiyo kulingana na rai ya Aamir bin Najjar yeye (Ibnu Taymiyya) ni miongoni mwa wale wapingaji na wapotoshaji wa hadithi za Mtume (s.a.w.w.). Ifahamike kwamba Ibn Taymiya sio Shi’a na wala si kati ya Wanachuoni wao, bali ni katika wale wenye chuki na usongo juu yao. Na ambalo linajulisha kuwa Dk. Aamir Najjar amekosa uaminifu katika kitabu chake “Shia wa Imamatu Ali”, na amepotosha maneno ya Mwenyezi Mungu swt. ili msomaji achanganyikiwe kwamba tafsiri ya Aya hiyo imebuniwa na kuzushwa na Shi’a, na kuwa wafasiri wa Ahlus-Sunna hawafahamu lolote mfano wa tafsiri hiyo, ni yale maneno ya Qurtubi ambaye ni mmoja wa maulamaa wakubwa wa Ahlus-Sunna na mfasiri kati ya wafasiri wao aliyoyasema ndani ya tafsiri yake Jaamiu’l-Ahkamiil-Qur’ani katika kuifasiri Aya hiyo “...... Na jambo hilo limejiri katika habari mbalimbali kwamba Mtume (s.a.w.w.) pindi ilipoteremshwa Aya hiyo aliwaita Ali, Fatimah, Hasan na Husein, hapo Mtume (s.a.w.w.) akachukua kishamiya na akawafunika, kisha akainua mkono wake na kuuelekeza mbinguni na akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ni Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na uwatakase kabisa kabisa.”’37 Nasema kumwambia Dk. Aamir Najjar: Hakika zoezi lako la kukanusha mfano wa hadithi hizo ni kuwa unakanusha kuwepo jua mchana peupe, hakika maneno ya Qurtubi katika tafsiri yake, naye sio katika Shi’a, na kutafsiri Aya hiyo tukufu kuwa imeteremshwa kuhusiana na watu hao wanne inawekwa bayana na hadithi zilizo mutawatiri kama iliyokwishatangulia habari zake, kwa hivyo ukanushaji wako ni kuzikanusha 36 Huquuq Ahli-Bait cha Ibn Taymiya, chapa 1981 Uk 10. 37 Jaamiu liahkamil-Qur’ani cha Qurtubi Juz. 14 uk 184. 36

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain hadithi sahihi na mutawatiri za Bwana Mtume (s.a.w.w.). Na ikiwa hadithi hizo sahihi, mutawatiri na muttafaku unajaribu kuzikadhibisha, na kuzipotosha na hata kuzinasibisha hizo kwa Shi’a na mayahudi, na dhahiri hadithi hiyo chanzo chake ni wahyi kutoka mbinguni basi utakuwaje kuhusu hadithi lukuki ambazo si mutawatiri. Baydhaawi ambaye ni mmoja wa wafasiri wakubwa wa Ahlus-Sunna katika kitabu chake anasema: “...Shi’a kuwafanya Ahlul-Bayt ni makhususi kwa Fatimah, Ali na watoto wao (Mwenyezi Mungu awawie radhi) ni kutokana na yale yaliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) pindi alipojitokeza siku moja hali akiwa....”38 hadi mwisho wa hadithi. Kwa mantiki hiyo Ibn Hajar Al-Haythami katika kitabu chake Sawa’qulMuhriqah naye ni katika wale ambao hawakubali ndugu wa karibu wa Mtume (s.a.w.w.) na haya ndio maneno yake: “Kwa hakika wafasiri wengi wamefasiri Aya hiyo kuwa imeteremshwa kuhusiana na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.).”39 Na tutaeleza hapo baadaye idadi kubwa ya wafasiri wa Qur’anii na vitabu vyao vya tafsiri, vilevile Mahafidh wao ambao hutilia mkazo kwamba Aya hiyo kuwa imeteremshwa juu ya watu hao wanne (a.s.), na kwamba wake za Mtume (s.a.w.w.) hawahusiki kabisa katika Aya hiyo, bali wao wapo nje kuhusiana na maudhui ya Aya hiyo tukufu. Ama analodai Aamir Najjar katika kukadhibisha hadithi hiyo ambayo imethibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), eti hadithi hiyo imepokewa kwa matamshi mbalimbali na mahala tofauti, na kuwa ikhtilafu hiyo ni dalili ya kutokuwa Sahih, hilo ni kutokana na uovu wake dhidi yao, bali bila shaka hiyo ni dalili tosha inayothibitisha usahihi wake na kuwa kwake mutawatiri, hivyo Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akitilia mkazo hilo katika kila mnasaba na kila mahala ili iwabainikie watu wake wote, na hiyo inaonyesha usafi wa nyoyo hizo na jinsi zilivyo tohara, si wengine bali ni kizazi 38 Anwaarut-Tanziil uk. 557. 39 Sawa’qul-Muhriqah uk. 141. 37

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayt wake, ambao wametolewa ishara na Aya tukufu kwa lengo la kuweka maandalizi na matayarisho katika mchakato mzima wa kushika uongozi wa Kiislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.). Na ambalo linajulisha ukweli na usahihi wa yale tuliyoyasema sikiliza anayoyasema Sheikhul-Islam Ibn Taymiya katika kitabu chake ‘Huquuqu Ahlul-Bayt’ “Na pindi alipobainisha Subhanahu Wataala kwamba anataka awaondolee uchafu Ahlul-Bayt wake Mtume (s.a.w.w.) na awatoharishe tohara ya kabisa kabisa, Mtume (s.a.w.w.) aliwaita watu wake wa karibu Ahlul-Bayt akawatukuza hao ili kuwafanya makhsusi kwake, nao ni Ali, Fatimah (r.a.) na mabwana wa vijana wa peponi, akawakusanya hao na Mwenyezi Mungu swt. akawatoharisha tohara ya kabisa kabisa baada ya kukamilika dua ya Mtume (s.a.w.w.), kwa hakika tukio hilo lilikuwa ni dalili na hoja tosha kuwa kutoharishwa kwao ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu”.40 Na wewe msomaji unamwona Ibn Taymiya hakuwataja wake wa Mtume (s.a.w.w.) na wasiokuwa hao miongoni mwa Ahlul-Bayt na Karaba wa Bwana Mtume (s.a.w.w.), kwa ujumla, kilafudhi Aya ni jumuishi inawajumuisha watu wote hao kama baadhi wanavyodai, lakini (s.a.w.w.) aliihusisha Aya hiyo na hao wanne pekee bila kuwaingiza wakeze (s.a.w.w.), na hilo tutalielezea Inshaallah. Kwa hivyo imekuja katika Sahih Muslim kwamba pindi alipoulizwa Zayd bin Arqam: “Tukasema kwamba miongoni mwa Ahlul-Bayt wa Mtume ni pamoja na wakeze?” Akasema: “Hapana, ole wenu kwa Mwenyezi Mungu, mwanamke hawi na mwanaume muda wote, unafika wakati anaachwa na anarudi kwao kwa baba na mama yake. Ahlul-Bayt wake ni katika damu yake ambao wameharamishiwa sadaka baada yake.”41 Na ufafanuzi huo si wa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) bali ni kutoka kwa Zayd bin Arqam. 40 - Huquuqu Aalil-Bayt Uk. 12. 41 - Sahih Muslim Juz. 4 Uk. 1874. 38

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Hakika kuifanya dhaifu hadithi ya kishamiya na kuiegemeza kwa Shi’a, sio kasumba ya Dk. Aamir Najjar peke yake, bali wamemtangulia katika hilo walimu wake katika ubabaishaji na upotoshaji, na hawa wafuatao ni baadhi tu ya vinara wao, mfano Ihsaan Ilahi Dhahiir katika kitabu chake ‘Shia wa Ahlul-Bayt,’ Muhammad Nasrudiini Albaani katika kitabu chake ‘Silsilatul-Ahadiithi Swahiihah,’ Dk. Ali Ahmad Saaluus katika kitabu chake ‘Hadiithut-Thaqalaini wa Fiqhuhu’ na wengineo ambao ni wapinzani na waasi wa hadithi ya vizito viwilii, ambavyo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.).

MDAHALO WETU NA IHSAAN ILAHI DHAHIIR NA KITABU CHAKE (SHIA WA AHLUL-BAYT): Anaandika katika kitabu chake alichokiita (Shia na Ahlul-Bayt) hivi: “Basi tunalojifunza ni kwamba mradi wa Ahlul-Bayt wa Mtume kiasili na kwa hakika ni wakeze (s.a.w.w.), na wanaingia katika (Ahlu) watoto, baba wadogo pamoja na watoto wao na kuendelea, kama vile ilivyopokewa kwamba Bwana Mtume (s.a.w.w.) aliwaingiza katika kishamiya chake Fatimah, Ali, Hasan na Husein, na akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndiyo hasa Ahlul-Bayt wangu.” ili wawe wahusika maalum wa maneno ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na kukutakaseni kabisa kabisa,” kama vile alivyomwingiza Ami yake Abbas na watoto wake katika nguo nyeusi ili tu wawe miongoni mwa wahusika wa Aya hiyo. Na zipo baadhi ya hadithi ambazo zimeeleza kuwa watu wa ukoo wa Bani Hashim wote wanahusika katika Aya hiyo, na hao ndio Ahlul-Bayt Nabii (s.a.w.w.), ama Shi’a wao wamesema kinyume na hivyo na wakawahusisha Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) kuwa watu hao ni wanne, nao ni Ali, Fatimah kisha Hasan na Husein, na wakawatoa wote wasiokuwa hao....42 42 - Shia wa Ahlul-Bayt uk. 19. 39

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nasema: Inatosha katika kujibu dhana za Ihsaan Ilahi Dhahiir ukiongezea yale yaliyokwishatangulia na yatakayofuata kutoka katika vitabu vya Ahlus-Sunna kuwa, Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote atayesema lolote katika Qur’anii pasi na kuwa na elimu nalo basi ajichagulie makao yake motoni.” Vile vile (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote atakayemsingizia yeye lolote basi ajichagulie makazi yake motoni.” Na ni dhahiri shahiri kwamba Ihsaan ilahi Dhahiir ameandika hivyo katika kitabu chake, achilia mbali upotoshaji wake wa maneno ya Mwenyezi Mungu swt., naye ameifasiri Qur’anii bila ya elimu kama wenzake, wale wenye kuifasiri Qur’anii bila elimu na kufuata matamanio yao na wakafanya dhihaka na kusema kuwa hayo ni ya Shi’a, na hilo sio la ajabu kwa Ihsani Ilahi Dhahiir kuikumbatia njia ya upotoshaji na kugeuza maneno ya Mwenyezi Mungu swt. kisha kuyanasibisha hayo kwa Shi’a, bila shaka kugeuza maneno kutoka mahala pale ni mtindo wa wale ambao wanakhalifu kizazi kitoharifu cha Mtume (s.a.w.w.), kama walivyofanya wale wa kabla yao miongoni mwa vibaraka wa Bani Umayya na Bani Abbas, ili kuziteketeza hadithi za Mtume (s.a.w.w.), hayo yote ni kutokana na uadui wao, chuki zao, kasumba na ushabiki wao, kwani kuamini mfano wa hadithi hizo itawalazimu kushikamana nazo, kwa hivyo itawawajibisha kushikamana na kizazi kitakatifu, na hatimaye kuchukua mambo na mafunzo mbalimbali yanayofungamana na dini na dunia, kwa ajili hiyo wakafanya chini juu mara kuzihusisha kwa Shi’a na kwa Abdallah bin Saba’ Mzayuni, na wakati mwingine kuzifanya hadithi hizo ni dhaifu na kuzikadhibisha hata kama zitadhibiti kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.). PILI: MUHAMMAD NASSURUDIIN ALBAANI NA AYA YA UTAKASO: Kabla hatujaeleza makusudio ya Aya hiyo tukufu, na yale yaliyoelezwa kutoka kwa Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na wafasiri wao, tutadokeza kidogo yale aliyoyasema Ustadh (Muhammad Nassurudiin Albaani) katika kitabu chake ambacho alikiita ‘Silsilatul-Ahaadithi Swahihah,’ naye huhesabiwa katika wakosoaji wakubwa wa hadithi, anasema hivi: “Ama Shi’a 40

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kuwahusisha Ahlul-Bayt katika Aya hiyo kuwa ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) bila kuwahusisha wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni kutokana na upotoshaji wa Aya za Mwenyezi Mungu swt. ili kutetea na kufuata matamanio yao binafsi... Vilevile hadithi ya Kishamiya na zenye maana yake, lengo kuu ni kupanua wigo na kupambanua hoja ya Aya hiyo ili kupata mwanya wa kumuingiza Ali na familia yake, kama vile alivyobainisha Haafidh Ibn Kathiir na wengineo, vivyo hivyo hadithi ya kizazi cha Mtume”.43 Nasema: Inajibiwa kama ifuatavyo: 1. Shi’a sio wao pekee ambao wamewahusisha Ahlul-Bayt katika Aya hiyo kuwa ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na hakuna shaka kuwa hata Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao wamehusisha walengwa katika Aya hiyo kuwa ni watu hao wanne (a.s.), hayo yamesemwa na wao, kama vile: Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim, Tirmidhi katika kitabu chake Sunanu Tirmidhi, Imam Ahmad, Sheikhul-Islam Ibn Taymiya katika kitabu chake Huquuqu Aali Bayt baina Sunna wal-bidaa, Qurtubi katika tafsiri yake, Ibn Kathiir katika tafsiri ya Qur’aniil-Adhiim na wengineo miongoni mwa wafasiri na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao kama tutakavyoeleza hilo Inshallah. 2. Ama kuhusu maneno yake: “Kutokana na upotushaji wao wa Aya za Mwenyezi Mungu...”, hakika tumeshatangulia kusema hapo kabla kwamba Shi’a siyo sifa yao kupotosha maneno ya Mwenyezi Mungu swt. bali hizo ni miongoni mwa sifa za wasiokuwa wao, kama itakapodhihiri hapo baadaye na kama tulivyosema kabla na ninarudia kusema kuwa Shi’a wanasifika kwa ukweli, kushikamana na dini, ucha Mungu na uaminifu, na tumeyanukuu hayo kutoka kwa Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna, 43 Silsilatul-Ahadith As-Sahih cha Muhammad Nasrud-Din Al-Baniy Juz. 4, uk. 359 – 360. 41

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain bila shaka kuwatuhumu wao kwa upotoshaji ni dhahiri mheshimiwa Ustaadhi Muhammad Nassir diin Albaani, amepotoka na inalazimu atubie makosa yake juu ya tuhuma zake kwa Shi’a, anakabiliwa na changamoto ya kukabiliana na Ahlul-Bayt na ajiandae jawabu la kuwajibu hao (a.s.). 3. Na ama maneno yake: “Vilevile hadithi ya Kishamiya na zenye maana yake, lengo kuu ni kupanua wigo na kupambanua hoja ya Aya hiyo ili kupata mwanya wa kumuingiza Ali na familia yake, kama vile alivyobainisha Haafidh Ibn Kathiir na wengineo.....,” huo ni uzushi na kumzulia uongo Ibn Kathiir na wengineo miongoni mwa Wanachuoni wa AhlusSunna. Huyu hapa Ibn Kathiir anasema katika tafsiri yake Al-Qur’aniul-‘Adhiim akitafsiri maneno ya Subhannahu Wataala: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara kabisa kabisa.” “Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik (r.a.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa anapita mbele ya mlango wa Bi Fatimah (r.a.) kwa muda wa miezi sita akitoka kwenda msikitini kwa ajili ya Swala ya asubuhi akisema: ‘Swalaa ya Ahlul-Bayt, hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.”’44 Na Ibn Kathiir hakutaja katika tafsiri yake kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya mlango wa wakeze au wanawake wake (s.a.w.w.) na kufanya hivyo, na hilo linajulisha bali ni dalili tosha kwamba hata maulamaa wa Ahlus-Sunna na wafasiri wao ambao bila ajizi wameihusisha Aya hiyo na watu hao wanne (a.s.) tu, na sio wakeze (s.a.w.w.), na ushahidi wa hilo ni maneno anayoyasema Ibn Hajar Al-Haythami katika kitabu chake kinachoitwa Sawa’qul-Muhriqah: “Hakika wafasiri wengi wamekiri kwamba Aya hiyo iliteremshwa kuhusiana na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.)”. 44 Tafsirul-Qur’an Adhiim cha Ibn Kathiir Juz. 3, uk. 483 - 485. 42

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Aidha Wahiidi anaandika katika kitabu chake cha tafsiri kinachoitwa Asbabun-Nuzuul, “Kutoka kwa Abi Said Al-Khudri: “Hakika anataka Mwenyezi Mungu kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt...” Iliteremshwa kwa watu watano; Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.)”45 Tunarudia kutaja yale aliyoyasema Ibn Kathiir ili imbainikie na umdhihirikie mpendwa msomaji ukweli na kuwatambua watu hao ambao hawaoni ubaya wowote katika kuongopa na kupandikiza mambo, Ibn Kathiir amepokea katika tafsiri yake kutoka kwa Ummul-Muuminina Aisha (r.a.) alimwambia Ibn ammi yake pindi alipomuuliza kuhusu Ali (a.s.), akajibu: “Umeniuliza kuhusu mtu ambaye anapendwa mno mbele ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), na binti yake alikuwa chini yake, na ndiye ampendaye mno. Hakika nilimwona mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) akawafunika guo lake jeusi (Kishamiya) akasema (s.a.w.w.): “Ewe Mola Wangu hawa ni Ahlul-Bayt wangu basi uwaondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.” Akasema Aisha: “Nikasogea karibu yao na nikasema: “Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mimi ni katika Ahlul-Bayt wako?” Akasema (s.a.w.w.): ‘Kaa kando (huhusiki) hakika wewe upo katika kheri”’46 Nasema: Hayo ni ambayo ameyaeleza Ibn Kathiir katika tafsiri yake ya Qur’ani kutoka kwa Ummul-Muuminina Aisha, naye kama tunavyoona amewahusisha Ahlul-Bayt kuwa ni hao watu wanne nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na ameeleza Ummul-Muuminina yakwamba hahusiki wala haimjumuishi Aya hiyo, na hilo tunalikuta katika maneno yake (r.a.): “Na mimi ni miongoni mwa Ahlul-Bayt wako?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kaa kando hauhusiki, hakika wewe umo katika kheri.” Na hiyo ni dalili tosha ya kuonyesha kuwa wanawake wa Bwana 45 Asbabun-Nuzuul ya Wahiid Naysabuuri uk. 239. 46 Tafsirul-Qura’n Adhiim cha Ibn Kathiir Juz. 3, uk 485-486. 43

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mtume (sa.w.w) haiwashamili wala kuwahusu Aya hiyo tukufu, kwa hivyo basi madai ya Ustadh Muhammad Nassurdiin Albaani na wenziwe kwamba Aya hiyo imeteremshwa juu ya wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) ni uzushi na kumsingizia Mwenyezi Mungu swt. - hilo la kwanza. Pili - kulinasibisha hilo na Ibn Kathiir kunakhalifu na kwenda kinyume na yale tuliyonukuu kutoka kwa Ibn Kathiir yeye mwenyewe. Hivyo ndivyo ustadh Albaani anavyojaribu kupotosha na kubadilisha maneno, kuinasibisha na kuuelekeza upotofu kwa Shi’a au wafuasi wa Amirul Muuminina Ali bin Abi Twalib (a.s.). 4. Na ama maneno ya Ustadh Albaani: “Ama Shi’a kuwahusisha AhlulBayt katika Aya hiyo kuwa ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) bila kuwahusisha wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni kutokana na upotoshaji wa Aya za Mwenyezi Mungu swt. ili kutetea na kufuata matamanio yao binafsi...” huo ni uelewaji wake mbaya, na upotoshaji wa Aya za Mwenyezi Mungu na yale yaliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kama ilivyokwisha tangulia. Na hiyo ni dalili na hoja mwafaka ya ndugu Albaani kutokuwa mwaminifu katika kunukuu hadithi sahihi kwa ajili tu ya kufuata matamanio ya nafsi yake, bali huo ni ukadhibisho wa wazi juu ya yale yaliyoelezwa na maulamaa wakubwa wa Ahlus-Sunna na waaminifu wao na kuwatuhumu na kuwaelekezea tuhuma nzito za kumzulia Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kama vile tulivyoona namna alivyomzulia Ibn Kathiir. Na kama si hivyo basi, vipi alijuzisha kuinasibisha Aya hiyo juu ya wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) ilhali anakhalifu yale yaliyoelezwa na kuthibitishwa na wafasiri, maulamaa wakubwa wa Alhus-Sunna na Mahafidh wao, kuwa Aya hiyo iko bayana ikieleza kuondolewa uchafu Ahlul-Bayt. Na muradi wa uchafu ni dhambi, hivyo kulingana na maneno ya Albaani kwamba Aya imeteremshwa kuhusiana na wanawake wa Mtume (s.a.w.w.), inalazimu wanawake hao wawe wameondolewa uchafu (dhambi) na kutofanya maasi, kwa mantiki hiyo haisihi kuambiwa na 44

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mwenyezi Mungu swt.: “Enyi wanawake wa Mtume ninyi sio kama wanawake wengine iwapo mtafanya ucha Mungu ...” (Sura 33 : 32), hilo la kwanza. La pili: Lau ungekuwa muradi au makusudio ya Aya tukufu ni wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba Mwenyezi Mungu alitaka awaondolee dhambi zao, basi lisingekuwa ni jambo la busara kwa Mwenyezi Mungu Subhaana wa Ta’ala kuwaeleza kwa kusema: “Enyi wanawake wa Mtume yeyote atakayefanya uovu wa dhahiri ataongezewa adhabu mara dufu na jambo hilo kwa Mwenyezi Mungu ni jepesi.” Tatu: Na ambalo linajulisha juu ya upotoaji wa maneno na kupotoka kwa watu hao ni yale maelezo aliyoeleza Imam Bukhari katika kitabu chake Sahih Bukhari kuhusiana na mafungamano yalivyokuwa kati ya Mtume (s.a.w.w.) na wakeze, aidha namna maudhi yao yalivyokuwa kwa Mtume (s.a.w.w.), na hilo haliambatani hata kidogo wala kukusanyika pamoja na utakaso na tohara ya kabisa kabisa, na kwa ajili hiyo imekuja katika Sahih Bukhari: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) aliwahama Aisha na Hafsa kwa muda wa mwezi na sababu ya hii ilitokana na Hafsa kutoa siri ambayo ilikuwa kati yake na Mtume (s.a.w.w.) naye akamweleza Aisha, Aisha akasema kumwambia Mtume (s.a.w.w.): “Wewe uliapa hatokuja kwetu kwa muda wa mwezi...”. Na katika riwaya ya Anas bin Malik kama ilivyoelezwa katika Sahih Bukhari anasema: “(Mtume) aliwahama wakeze kwa muda wa mwezi, unyayo wake ulipasuka akakaa katika kigoda chake punde akaja Umar na akasema: “Je! Umewataliki wakezo?” Akasema: ‘Hapana, lakini nimewahama kwa mwezi.”’47 Namwambia Ustadhi Albani: Je inawezekana kujumuisha pamoja hayo na maneno ya Mwenyezi Mungu swt.: “Hakika anataka Mwenyezi Mungu kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa”, aidha amesema: “Au nyoyo zao zina kufuli”. Hali kad47 Sahih Bukhari Juz. 3 uk 34. 45

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain halika kama Aya hiyo inawahusu wake wa Mtume (s.a.w.w.) kama inavyodaiwa, basi inalazimu kiwakilishi (dhamiri) katika Aya ya Utakaso kiwe kama kilivyo eneo jingine pale walipozungumzwa wanawake wa Mtume (s.a.w.w.), badala ya neno (Ankum) ingekuwa (Ankunna), na katika kitenzi Yutwahirakum ingekuwa Yutwahirakunna, kulingana na fuo la Aya zilizoitangulia Aya hiyo na zile zilizoifuatia. Na yakutosha kuwa dalili juu ya upotofu wa Ustadh Albaan na mfanowe, Bukhari amesimulia katika kitabu chake Sahih Bukhari kutoka kwa Ibn Abbas, na hiyo ni dalili tosha ya kuwaweka mbali wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) na Aya ya Utakaso, Ibn Abbas amesema: “Nilikuwa na hamu ya kumuuliza Umar bin Khattab kuhusiana na wanawake wawili miongoni mwa wakeze Mtume (s.a.w.w.) ambao Mwenyezi Mungu swt. anasema: “Iwapo mtatubu kwa Mwenyezi Mungu atakusameheni,” mpaka alipokwenda Hijja nami nikahiji naye. Aliendelea hadi aliposema: “Nikasema: Ni akina nani hawa ambao Mwenyezi Mungu amewaambia: “Iwapo mtatubu kwa Mwenyezi Mungu atakusameheni”? Akasema: ‘Kwa kweli ni jambo ambalo litakufanya ushangae na kustaajabu ewe Ibn Abbas, na hao ni Aisha na Hafsa...” Aliendelea hadi aliposema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu hakika wakeze Mtume humrejea (s.a.w.w.) lakini mmoja wao akamhama Mtume kuanzia asubuhi hadi usiku, basi hilo likanifadhaisha sana, nikasema: Kwa hakika amepata hasara aliyefanya hivyo miongoni mwao, kisha nikaweka nguo zangu vizuri nikaingia kwa Hafsa nikamuuliza: “Ewe Hafsa, anadiriki mmoja wenu kumuudhi Mtume (s.a.w.w.) kuanzia asubuhi hadi usiku?” Akasema: “Ndiyo”. Nikasema: ‘Hakika ameharibikiwa na amepata hasara, je hujui mwenye kumchukiza Mtume (s.a.w.w.) amemchukiza Mwenyezi Mungu na hakika ameangamia.’”48 48 Sahih Bukhari Juz. 3, uk 135. 46

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na tumsikie Bukhari kwa mara nyingine alivyotupa picha ya waziwazi ya msimamo wa wakeze Mtume (s.a.w.w.) na kiwango na upeo wa heshima zao kwake (s.a.w.w.), ili ashushuke Ustaadh Albaani na wapambe wake kwa madai yao kwamba Aya ya Utakaso iliteremshwa kuhusiana na wake wa Mtume (s.a.w.w.), ili tu awadhulumu waziwazi Ahlul-Bayt (a.s.). Bukhari ameeleza katika kitabu chake Sahih Bukhari katika mlango wa mwenye kutoa zawadi kwa Swahiba wake na akawaacha huru baadhi ya wakeze na kutowaacha baadhi, katika hadithi ndefu iliyopokewa kutoka kwa Ummul Muuminuna Bibi Aisha amesema: “Basi wakamtuma Zainab binti Jahsh akamjia Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakika wake zako wanakuombea kwa Mwenyezi Mungu uadilfu juu ya binti wa Abi Quhafah”, basi (Zainab) akanyanyua sauti yake hadi kufikia kutoa maneno makali na kutoa matusi dhidi ya Aisha, ilihali (Aisha) akiwa ameketi chini, aliendelea kumtukana (Aisha) huku Mtume (s.a.w.w.) akimwangalia Aisha je, atazungumza chochote. Amesema: Ndipo Aisha akazungumza na kumjibu Zainab hadi akamnyamazisha.” 49 Namwambia Ustaadhi mwandishi wa kitabu ‘Silsilatul- Ahadithi Swahihah’: Je! Huoni hadithi hizo na hali wewe ungali unatafiti hadithi Sahih na ukiwa huo ndiyo msimamo wa wake wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) kumuelekea yeye, wanamhama siku nzima, siku mbili na hata mwezi, wanagombana mbele yake bali wanatoleana matusi, kushutumiana na kupashana mbele yake (s.a.w.w.), hayo na yanayofanana na hayo yanafanywa na wao hadi zikateremshwa waziwazi Aya kadhaa wa kadhaa kuhusiana na wao huku zikitofautiana na yale anayodai Ustadh Albaani na wale wenye kufuata nyayo zake kwamba: Aya ya Utakaso imeteremshwa juu yao. Na hayo ni kwa mujibu wa maneno ya Subhaanahu wa Ta’ala pale aliposema: “Huenda Mola wako akikupeni talaka ambadilishie yeye wake bora kuliko nyinyi waislam safi, waumini, wanyenyevu na wachamungu...” (Surat Tahrim: 5). 49 - Sahih Bukhari Juz. 7 uk 28-29. Na Juz. 3 uk 133. 47

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Si hilo tu bali limefichika kwa Ustaadhi Ali Albaani, Aamir Najjar, Ihsaani Ilahi Dhahiir na Dk. Saaluus kwamba mwenye kumuudhi Mtume (s.a.w.w.) kwa hakika amemuudhi Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu amemuahidi mtu huyo adhabu kali, hiyo ni kutokana na maneno ya Subhaanahu wa Ta’ala.” Hakika wale wenye kumuudhi Mwenyezi Mungu na Mtume wake Mwenyezi Mungu amewalaani duniani na akhera na amewaahidi wao adhabu ya kunyongesha” (Surat Tawbah: 61). Kwa kuongezea zaidi yaone yaliyopo kwa Imam wa hadithi kwenda kwa Ustadhi Albaani na yeye si mwingine bali ni Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim, pindi alipoulizwa Zayd bin Arqam: “Ni nani AhlulBayt wake? Ni wakeze?” Akasema: “Hapana, Ole wako, hakika mwanamke huwa pamoja na mwanamume kwa muda fulani, kisha anamtaliki na anarudi kwa wazazi wake, Ahlul-Bayt wake ni watu wanaotokana na damu yake ambao wameharamishiwa sadaka baada yake.”50 Kutokana na hayo unadhihiri ufisadi wa maneno na fikra za Ustadh Albaani kutokana na kuihusisha Aya ya Utakaso kwamba imeteremshwa juu ya wanawake wa Mtume (s.a.w.w.), na baadaye zitafuata hadithi Sahih ambazo zimo katika vitabu Sahih na Musnad za Ahlul Sunna zenye kujulisha na kuwatambulisha hasa Ahlul-Bayt katika Aya ya Utakaso kuwa wao ni wale watu wa kishamiya, nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na watu hao wametajwa na maulamaa wa Ahlus-Sunna na waaminifu wao. Na sio miongoni mwa Shi’a hata watuhumiwe kwa ubunifu, uzushi, ukadhibishaji na upotoshaji.

50 Sahih Muslim Juz. 4, uk 1874. 48

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

TATU: AYA YA UTAKASO KATIKA VITABU VYA AHLUS-SUNNA Tulidokeza hapo kabla kwamba makusudio ya Ahlul-Bayt ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) kwa ibara nyingine wao ni watu wa Kishamiya ambao Mwenyezi Mungu swt. amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa kabisa, ni wao tu wala haingii yeyote miongoni mwa wake wa Bwana Mtume (s.a.w.w.) wala yeyote katika ndugu zake na hilo limebainishwa na hadithi sahihi za Mtume (s.a.w.w.) kutoka katika vitabu Sahih vya Ahlus-Sunna na Musnad zao zilizoelezea kinaga ubaga. Imebakia kwetu kazi moja tu ya kudokeza na kutoa vidokezo kadhaa hadithi na maelezo mbalimbali ili udhihirike ufisadi wa yale yanayodaiwa kwamba hadithi hizo ni miongoni mwa hadithi ambazo zimebuniwa na Shi’a kutokana na uzushi wao upotoaji wa Aya za Mwenyezi Mungu swt. na kufuata matakwa yao, ili impambanukie muumini safi ambaye anataka kupata ridhaa ya Mola wake na maisha mazuri peponi, kwamba ni nani anayemsingizia Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) na anajaribu kupotoa Aya za Mwenyezi Mungu swt. ili kufuata matamanio yake binafsi na kwa malengo na maslahi duni. Ukiachilia mbali hadithi zilizokwishatangulia ambazo zimetafsiri Aya ya Utakaso katika kauli yake swt.: “Sema, sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu,” ambapo Wanachuoni wa Ahlus-Sunna wameitafsiri Aya hiyo kwamba imeteremshwa juu ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), kadhalika lililobakia ni kudokeza yale yaliyoelezwa na kuandikwa katika vitabu Sahih vya AhlusSunna na Musnad zao kwamba makusudio ya Ahlul-Bayt katika Aya ya Utakaso ni watukufu hao wanne.

49

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 1. SAHIH MUSLIM: Amepokea Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim nacho ni kitabu Sahih zaidi baada ya Qur’ani tukufu kwa mujibu wa Ahlus-Sunna, amepokea kwamba Aya ya Utakaso na zile zenye maana kama Aya hiyo miongoni mwa Aya kadhaa zimeteremshwa mahsusi kwa ajili ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). “Kutoka kwa Ummul Muuminiina Aisha (r.a.) amesema: “Siku moja alitoka Mtume (s.a.w.w.) akiwa na nguo nyeusi, punde akaja Hasan bin Ali akamwingiza, kisha akaja Husein akamwingiza, kisha akaja Fatimah akamwingiza na hatimaye akaja Ali akamwingiza, kisha akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu enyi Ahlul-Bayt na akutakaseni utakaso wa kabisa kabisa.”’51 Na katika hadithi nyingine imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam kama ilivyo Hadith Thaqalain: “...Tukasema miongoni mwa Ahlul-Bayt ni wakeze. Akasema Zayd bin Arqam: ‘Hapana ole wako, hakika mwanamke anakuwa pamoja na mwanamume kwa muda fulani kisha anamtaliki anarudi kwa baba na mama yake, Ahlul-Bayt wake ni wenye kutokana na yeye na wa damu yake ambao wameharamishiwa sadaka baada yake.”’52 Nasema: Na wewe unaona kuwa tafsiri ya Ahlul-Bayt imepokewa na wapokezi wengi na katika riwaya hii imekanusha kwa kutumia kiapo kuwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) sio miongoni mwa Ahlul-Bayt, na kuwaingiza wakeze (s.a.w.w.) katika hao ni kutafsiri kwa kutumia maoni ya mtu binafsi na bila dalili, bali dalili iliyopo inasema kinyume na hivyo, na kwamba makusuido ya Ahlul-Bayt ni wale watu wa kishamiya (a.s.), hilo ni kwa muktadha wa yale yaliyoelezwa katika Hadithi ya Kishamiya ambayo imepokewa na Ummul- Muuminina Aisha (r.a.), hilo ni kwanza. 51 Sahih Muslim Juz. 4, uk. 1883. 52 Sahih Muslim Juz. 4, uk. 1874. 50

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain La pili: Hakika kutafsiri Aya ya Utakaso kuwa inawahusu wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni kutafsiri Qur’ani bila ya elimu....na kumsingizia Mwenyezi Mungu na Mtume, yeye (s.a.w.w.) amesema: “Mwenye kusema lolote katika Qur’ani bila ya kuwa na elimu basi ajichagulie makazi motoni”. Aidha imekuja katika kitabu cha Sahih Muslim cha Imam Muslim “Kutoka kwa Amar bin Said bin Abi Waqaas kutoka kwa baba yake anasema: “Muawiya bin Abi Sufyan alimwamrisha Said akamwambia: “Ni kipi kinachokuzuia kumtukana baba wa udongo (yaani Ali), akasema: “... pindi ilipoteremshwa aya hii: “Basi sema njoeni tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo watu wangu.”’53 Nasema: Hiyo ni dalili juu ya kuwafanya watu hao wanne kuwa wahusika makhusus wa tamko Ahlul-Bayt (a.s.), na hilo anaambiwa na kupashwa yule ambaye anawatuhumu Shi’a kwa kuzusha hadithi hiyo, na kuwa sifa za Shi’a ni kupotosha maneno, na kubadilisha na kupandikiza hadithi. Anaambiwa: Unasemaje juu ya Imam Muslim ambaye ni Imam wa hadithi, je! hajazieleza hadithi hizo katika kitabu chake Sahih Muslim? Au Imam Muslim ni miongoni mwa wazuaji, wabunifu na wakadhibisha ambao hadithi walizozipokea hazikubaliki au ni katika Shi’a? Atajibu nini siku ya Kiyama mbele ya Hakimu Mwadilifu? Watakwepea wapi Dk. Aamir Najjar, Muhammad Nassur diin Albaani, Ihsaani Ilahi Dhahiir, Dk. Ali Ahmad Saaluus na Uthman Aali Khamiis Naswiry kutoka katika mzani?

2. SHEIKHUL-ISLAM IBN TAYMIYA: Ibn Taymiya anasema katika kitabu chake ‘Huquuq Ahlul-Bayti baynasSunnat Wal-Bidaa,’ pamoja na uadui wake wa enzi na enzi juu ya Shi’a, lakini ni haya hapa maneno yake: “Na pindi Mwenyezi Mungu alipobainisha kwamba anataka kuwaondolea uchafu Ahlul-Bayt na kuwatoharisha 53 - Sahih Muslim Juz. 4, uk. 1871. 51

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain tohara ya kabisa kabisa, Mtume (s.a.w.w.) aliwaita ndugu zake wa karibu na akawatukuza ili wawe makhsusi kwake, nao ni Ali, Fatimah (radhiyallahu anhum) na mabwana wa vijana wa peponi, Mola aliwatoharisha hao baada ya kukusanyika na du’a ya Mtume (s.a.w.w.) kukamilika, na hilo lajulisha kuwa kuondolewa uchafu na kutakaswa ni neema kutoka kwa Mwenyezi Mungu swt.”54 Vile vile anasema Ibn Taymiya: “Kutoka kwa Ummu Salama: ‘Hakika Aya hiyo ilipoteremshwa Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika Kishamiya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’55 Anasema Ahmad Muhmuud Subhi Ustadhi wa falsafa naye ni katika Masunni, katika kitabu chake ‘Nadhariyyatul-Imamah’ akiweka pambizo kwenye Aya ya Utakaso: “Na tafsiri hii inafaidisha kwamba Ahlulbayt ni wale ambao wamekusudiwa katika lafudhi ya Qurba katika Aya, na hata Ibn Taymiya pamoja na upinzani wake juu ya tafsiri za Kishi’a lakini amesarenda, kwani imepokewa katika vitabu Sahih kwamba Mtume (s.a.w.w.) alihutubia siku ya Ghadiir-Khum akasema: “Ninawakumbusha kuhusiana na Ahlul-Bayt wangu, aliyasema hayo mara tatu”.56 Na la kuchunguza na kuzingatia hapa ni kwamba hakuwataja wake wa Mtume (s.a.w.w.) na hakusema Aya ya Utakaso imeteremshwa kwao, wala haikuwajumuisha wake wa Mtume (s.a.w.w.) na hiyo ni dalili tosha kwamba Aya hiyo imeshushwa juu ya watu hao wane (a.s.) kutokana na kukiri hivyo Wanachuoni wa Ahlus-Sunna. 54 Hukuuk Aali-Bayt cha Ibn Taymiya uk. 12. 55 Hukuuk Aali-Bayt cha Ibn Taymiya uk. 10. 56 Nadhariyatul-Imamah uk. 184.

52

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 3. KITABU KHASA’IS CHA NASAAI: Na katika kitabu Khasais cha Nasaai katika hadithi Sahih kutoka kwa Saad bin Abi Waqaas amesema: “Mu’awiya alimwamrisha Saad amtukane Ali akamwambia: “Ni kipi kinakuzuia kumtukana baba wa mchanga? - yaani Ali,” – akasema: “Ama nikiyakumbuka maneno ambayo Mtume (s.a.w.w.) aliyasema kumwambia yeye siwezi kumtukana... hakika pindi ilipoteremshwa Aya “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa”, Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio ndugu zangu wa karibu.”’57 Na katika riwaya iliyopokewa kutoka kwa Ibn Abbas nayo ni Sahih amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alichukua nguo yake kisha akawafunika Ali, Fatimah, Hasan na Husein hapo akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...”’58 Na katika riwaya Sahih nyingine ambayo ameitaja Nasaai kutoka kwa Bakiir bin Mismaar amesema: “Nilimsikia Amr bin Saad akisema: Muawiya alimwambia Saad bin Abi Waqaas: “Kipi kinakuzuia kumtukana Ibn Abi Twalib?” Akasema: “Siwezi kumtukana kwani nikikumbuka mambo matatu ambayo Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia yeye, iwapo ningekuwa nayo mimi lau jambo moja lingekuwa bonge la neema, siwezi kumtukana nikikumbuka pindi ulipoteremshwa wahyi kwa Mtume (s.a.w.w.) akamchukua Ali, Fatimah na watoto wao wawili akawaingiza katika nguo yake kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo AhlulBayt wangu na ndugu zangu.”’59

57 Khasais cha Nasaai uk. 24. 58 Khasais cha Nasaai uk. 34-35. 59 Khasais cha Nasaai uk. 56. 53

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nasema: Ikiwa hiyo ndiyo hali ya Muawiya bin Abi Sufyani mwandishi wa wahyi kama baadhi wanavyodai, anamtaka mtu amtukane AmirulMuuminiina, Ibn ammi Rasuulillah, mume wa binti yake Bibi mbora wa Wanawake wa mwanzo na wa mwisho, baba na mzazi wa Hasan na Husein ambao ni mabwana wa vijana wa watu wa peponi, na ambaye Mtume Muhammad (s.a.w.w.) amesema kuhusu yeye: “Yeyote mwenye kukutukana wewe amenitukana mimi na mwenye kunitukana mimi amemtukana Mwenyezi Mungu,” na vipi hali ya Dk. Aamir Najjar, Ustadh Muhammad Nassur diin Albani, Ihsaani Dhahiir, Dk. Ali Ahmad Saaluus na Uthman bin Muhammad Aali Khamiis. Ikiwa kuna baadhi ya wale ambao wanaitwa sahaba wa Mtume (s.a.w.w.) anawalingania na kuwaomba watu bali anaanzisha Sunna mbaya ya kumtukana Imam Ali (a.s.) juu ya mimbari, na ikawa ni Sunna iliyofuatwa kwa muda wa miaka themanini, unasemaje juu ya watu hao na wale wanaofanana na hao ambao wamefanya ni Sunna kwao kukanusha hadithi Sahih za Bwana Mtume (s.a.w.w.), kuzinasibisha na kuzituhumu kuwa ni za kubuniwa ilihali zimepokewa ndani ya vitabu ambavyo kwa imani yao wao ndio vitabu sahihi mno baada ya Qur’ani. Hivyo sio jambo la ajabu kwani wao kukanusha hadithi Sahih ni katika kufuata sunna ya kiongozi wao Muawiya bin Abi Sufyaani.

4. KITABU JAAMIUS-SIHAAH CHA TIRMIDHI: Amepokea Tirmidhi katika kitabu chake Sahih Tirmidhi Hadithi ya Kishamiya ikiwa makhsusi kwa ajili ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). “Imepokewa kutoka kwa Shahar bin Hawshab kutoka kwa ummu Salama kuwa hakika Mtume (s.a.w.w.) alimtukuza Ali, Fatimah, Hasan na Husein akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa,” Ummu Salama akasema: “Na mimi ni pamoja nanyi, ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Mtume Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’ Tirmidhi akasema: “Hadithi hii ni hasan, nayo ni nzuri sana katika mlolongo huo imepokewa kutoka kwa Umar bin Abi Salama, Anas bin Malik, 54

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Abu Hamrai, Maakil bin Yassar na Aisha”.60 Nasema: Na wewe mwenyewe unaona kwamba Mtume (s.a.w.w.) hajamuingiza Ummu Salama (r.a.) japokuwa naye ni miongoni mwa wake zake (s.a.w.w.), na hii ni dalili tosha kuwa Ahlul-Bayt wanaohusishwa katika Aya hiyo sio wakeze (s.a.w.w.) bali ni hao watukufu wanne. Mwenyezi Mungu swt. anasema:

“Hakika macho hayawi pofu lakini nyoyo ambazo ziko katika vifua huwa pofu.” (Surat Hajji: 46). Aidha amepokea Tirmidhi katika kitabu chake Sahih Tirmidhi kutoka kwa Umar bin Salama mtoto wa kufikia wa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Aya hii iliteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...” katika nyumba ya Ummu Salama, Mtume (s.a.w.w.) alimwita Fatimah, Hasan, Husein na Ali akawafunika Kishamiya kisha akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa ndio AhlulBayt wangu basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa,” Ummu Salama akasema: “Na mimi ni pamoja nao ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ‘Wewe una sehemu yako na wewe uko katika kheri.”’ Tirmidhi amesema: “Na katika mlango huu kuna kutoka kwa Ummu Salama, Maakil bin Yasaar, Abu Harmrai na Aisha”.61 Amepokea Tirmidhi katika kitabu chake Sahih Tirmidhi kutoka kwa AAmr ibn Saad bin Abi Waqaas kutoka kwa Babu yake amesema: “Muawiya bin Abu Sufyani alimwamrisha Saad...” Aliendelea hadi kauli yake: “.......na ilipoteremshwa Aya hii: “Basi sema njoeni tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwaita Ali, Fatimah, 60 Jaamiu-Swihahi cha Tirmidhi Juz. 5 uk. 656-657, hadithi namba 3871. 61 - Jaamiu-Swihahi cha Tirmidhi Juz. 5 uk 621-622. 55

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Hasan na Husein na akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo ndugu zangu.”’ Abu Salama amesema: “Hadithi hiyo ni Hasan na Sahih.”62

5. KITABU MUSNAD CHA IMAM AHMAD BIN HANBALI: Amepokea Imam Ahmad katika Kitabu chake Musnad Ahmad kutoka kwa Ummu Salama: “Hakika siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekaa ndani ya nyumba yake (Ummu Salama) punde akamjia Fatimah, ndipo Mtume (s.a.w.w.) akamwambia kamwite mumeo na watoto wako, akaenda kuwaita akaja Ali, Hasan na Husein wakaingia kwake... basi hapo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.” Akasema Ummu Salama: hapo akachukua Kishamiya chake, akawafunika kisha akatoa mkono wake akauelekeza mbinguni na akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa ndiyo hasa Ahlul-bat wangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.” Basi nikasema: Na mimi ni pamoja nanyi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ‘Wewe upo katika kheri.”’ Abdul-Malik amesema: “Abulaila amenihadithia kutoka kwa Ummu Salama mfano wa hadithi ya Atwai hakuna mapungufu, Abdul-Malik amesema: ‘Amenihadithia Daudi bin Abi Auf Al-Jahafi kutoka kwa Hawshab kutoka kwa Ummu Salama vivyo hivyo wala hakuna tofauti.”63 b) Vile vile amepokea Imam Ahmad bin Hambali katika kitabu chake Musnad: “Kutoka kwa Shahar bin Hawshab amesema: “Nilimsikia Ummu Salama mke wa Mtume (s.a.w.w.) pindi zilipokuja habari za kifo cha Imam Husein bin Ali, aliwalaani watu wa Iraq, akasema: Wamemuuwa, basi Mwenyezi Mungu awauwe…hakika nilimwona mjumbe wa Mwenyezi Mungu wakati alipojiwa na Fatimah......” Akaendelea hadi aliposema: 62 Jaamiu-Swihahi cha Tirmidhi Juz. 5, uk. 596. 63 Al-Musnad Juz. 6, uk. 292. 56

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain “Ewe Mola Wangu hawa ndiyo ndugu zangu wa karibu basi waondolee uchafu na watoharishe kabisa kabisa.” Nikasema: Ewe Mtume Je! mimi sio katika Ahli wako? Akasema: “Bila shaka” akaniingiza katika Kishamiya baada ya kukamilika dua yake juu ya Ibn ammi yake ambaye ni Ali, watoto wake na binti yake Fatimah (r.a.)”.64 Nasema: Mwishoni mwa hadithi hiyo mwajulisha kwamba Aya hiyo iliteremshwa makhsusi kuhusiana na hao wanne, na haya ni katika maneno yake: “Pindi ilipokwisha dua yake kwa Ibn ammi yake Ali, wanawe na binti yake Fatimah” . Na ama kuhusiana na maneno yake: “Nikasema: Je! mimi sio katika Ahli wako? Akasema: “Bila shaka ni hivyo, basi ingia katika Kishamiya,” yenyewe yanakwenda kinyume na hadithi zilizokwishatangulia hapo kabla, nazo ni chungu nzima na wapokezi lukuki, aidha dalili tosha juu ya hilo ni zile alizopokea Imam Ahmad bin Hambali katika kitabu chake Musnad, ikiwemo ifuatayo. c) “Imepokewa kutoka kwa Shahar bin Hawshab kutoka kwa Ummu Salama kuwa Mtume (s.a.w.w.) alimtukuza Ali, Hasan, Husein na Fatimah kwa kuwafunika katika Kishamiya kisha akasema: “Ewe Mola Wangu hawa hasahasa ndiyo Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa,” Ummu Salama akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mimi ni pamoja nao? Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’65 d) Aidha amepokea Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake kutoka kwa Bakiir bin Mismaar bin AAmr ibn Saad kutoka kwa baba yake amesema: “Nilimsikia Mtume (s.a.w.w.) anasema: “…….”, Aliendelea hadi aliposema: “Na ilipoteremshwa Aya hii: “Basi sema njoeni tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mtume (s.a.w.w.) aliwaita Ali, Fatimah, Hasan 64 Al-Musnad Juz. 6, uk 298. 65 Al-Musnad Juz. 6, uk. 340. 57

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain na Husein (radhi ya Mwenyezi Mungu iwe juu yao) akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo Ahli wangu.”’66 e) Amepokea Imam Ahmad bin Hanbali katika Musnad yake kutoka kwa Amru bin Maymuuna katika hadithi ndefu kutoka kwa Ibn Abbas: “......akasema: “Mtume akachukua nguo yake akawafunika Ali, Fatima, Hasan na Husein hapo akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa”’.67 f) Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Ali bin Zayd kutoka kwa Anas bin Malik kuwa, “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anapita mbele ya mlango wa Fatimah kwa muda wa miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali swala ya asubuhi akisema: ‘Swala! Swala! Enyi Ahlul-Bayt, hakika Mwenyezi Mungu anataka akuondosheeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.”’68 Nasema: Hadithi hii ya Anas bin Malik, haikueleza kwamba Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya nyumba ya wakeze au nyumba ya ndugu zake isiyokuwa nyumba ya binti yake Fatimah, na hilo linajulisha kinagaubaga kuwa Aya ya Utakaso imeteremshwa ikiwa mahsusi hasa juu ya hao (a.s.) na sio wakeze wala ndugu zake wengine.

6. KITABU HASKAANI:

SHAWAHIDUT-TANZIL

CHA

HAAKIM

Zifuatazo ni miongoni mwa hadithi ambazo amezieleza Haakim Haskaani Al-Hanafii katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil na zote zinatoa ishara kuwa Ahlul-Bayt ambao ndio walengwa wa Aya ya Utakaso ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). 66 Al-Musnad Juz. 1, uk. 185. 67 Al-Musnad Juz. 1, uk. 330 - 331. 68 Al-Musnad Juz. 3, uk 259. 58

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain a) Amepokea AAmr ibn Saad kutoka kwa baba yake amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Basi sema tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Bwana Mtume akawaita Ali, Fatimah, Hasan na Husein hapo akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio ahli wangu.”69 “Amepokea Abdallah bin Hasan kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake amesema: Amesema Abu Hamrai mtumishi wa Mtume (s.a.w.w.): “Pindi iliposhushwa Aya hii: “Na waamrishe ahli zako Swala.....”, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya nyumba ya Fatimah na Ali kila kipindi cha Swala huku akisema: ‘Swala! Swala! Mwenyezi Mungu akurehemuni: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na kukutakaseni tohara ya kabisa kabisa.”’70 “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Hakim Haskaani amesema: “Hakika zimekithiri hadithi kuhusiana na hilo, na kati ya hizo ni hadithi iliyopokewa na Anas bin Malik Al-Answary... kuwa hakika mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa akipita mbele ya mlango wa Fatimah kwa muda wa miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali akisema: ‘Swala! Enyi Ahlul-Bayt hakika Mwenyezi Mungu anataka akuondoleeni uchafu.....”’ Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kwa muda wa miezi sita akipita mbele ya mlango wa Fatimah wakati akienda kuswali akisema: ‘Swala! Enyi Ahlul-Bayt mara tatu, hakika Mwenyezi Mungu anataka kuondoeeni uchafu...”’71 Na kwa njia nyingine kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Alikuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu akipita mbele ya nyumba ya Fatimah kwa 69 Shawahidut-Tanziil Juz. 1, uk. 124. 70 Shawahidut-Tanziil Juz. 1, uk 381. 71 Shawahidut-Tanziil Juz. 2, uk. 10 -12. 59

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain muda wa miezi sita pindi anakwenda kuswali swala ya alfajiri akisema: ‘Swala! Enyi Ahlul-Bayt...’” na njia nyinginezo nyingi ambazo hadithi hizo zinapokewa kutoka kwa Anas bin Malik. Miongoni mwa hadithi hizo imepokewa na Baran bin Azib, naye ana njia lukuki, tunataja baadhi ya hizo, imepokelewa kutoka kwa Muhammad bin Umar kutoka kwa Is’haqa bin Swawaid bin Baran bin Azib amesema: “Alikuja Ali, Fatimah, Hasan na Husein katika mlango wa Mtume (s.a.w.w.) wakabisha hodi akasema katika kuwaitikia: ‘Ewe Mola Wangu hiki ndicho kizazi changu.’” Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Is’haqa bin Zayd Al-Answary kutoka kwa Barau bin Azib amesema: “Alikuja Ali bin Abi Twalib mbele ya mlango wa Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Fatimah, Hasan na Husein, akatoka Mtume huku akitokwa na jasho, akawakaribisha kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo Ahli zangu.”’73 e) Na kati ya hizo amepokea Jabir bin Abdillah Answaary: “Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, watoto wake wawili na Fatimah akawafunika nguo yake kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahli zangu”’.74 f) Na miongoni mwa hizo imepokewa hadithi kutoka kwa Hasan bin Batuul (a.s.) amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya ya Utakaso Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwakusanya katika nguo yake katika nyumba ya Bi Ummu Salama Khaybary kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu na kizazi changu basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’75

72 Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 16. 73 Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 16. 74 Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 17. 60

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain g) Na Miongoni mwa hadithi hizo ni hadithi iliyopokewa na Saad bin Abi Waqaas Az-Zahry kuwa alisema kumwambia Muawiya huko Madina: “Hakika nimeshuhudia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na Ali mambo matatu....” Aliendelea hadi aliposema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu basi waondolee uchafu.”’ Na hadithi nyingine kutoka kwa AAmr ibn Saad kutoka kwa baba yake amesema: “Muawiya alipita kwa Saad akasema: ‘Ni kitu gani kinachokuzuia kumtukana Abu Turab (baba wa Mchanga)...”’75 h) Na kati ya hizo ni hadithi iliyopokelewa na Abu Said Al-Khudry na ameiandika hadithi hiyo Haakim Haskaani Naysabury kwa njia mbalimbali.76 i) Na kati ya hizo ni hadithi kutoka kwa Abdallah bin Abdul Mutwalib Hashimi (a.s.).77 j) Na kati ya hizo ni hadithi kutoka kwa Amirul-Muuminiina Ali bin Abitwalib (a.s.).78 k) Kati ya hadithi hizo ni hadithi iliyopokewa na Ummul Muuminiina Aisha, kutoka kwa Sofia binti Shaybaha amesema: “Amesema Aisha: “Mtume (s.a.w.w.) alitoka akiwa na nguo yake akaja Hasan bin Ali akamwingiza, kisha akaja Husein akamwingiza, kisha akaja Fatimah akaingia na hatimaye akaja Ali akamwingiza kisha akasema: ‘Hakika anataka Mwenyezi Mungu kukuondoleeni uchafu na kuwatoharisheni tohara ya kabisa kabisa”’.79 75 76 77 78 79

Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 21-22. Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 22-23. Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 29-30. Shawahidut-Tanziil Juz. 2 uk 31-33. Shawahidut-Tanziil Juz. 2. uk 33. 61

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Katika hadithi nyingine imepokewa kutoka kwa Aisha... “Basi nikasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi sio katika ahali zako? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri” wala hakuniingiza pamoja nao”. Na hadithi nyinginezo ambazo Haakim amezipokea kutoka kwa Aisha.80 Nasema: Na kukiri huko kutoka kwa Ummul Muuminiina Aisha kwamba yeye sio katika watu ambao inawahusu Aya hiyo ni kutokana na maneno yake aliposema: “Na wala hakuniingiza pamoja nao”. Bila shaka anayedai kuwa Aya ya Utakaso imeteremshwa juu ya wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni ubadilishaji wa maneno kutoka sehemu yake, na kumsingizia Mwenyezi Mungu swt. na Mtume wake (s.a.w.w.). l) Kati ya hadithi hizo ni hadithi iliyopokewa na Wathlatu bin Rabii Laythi na wengineo miongoni mwa sahaba ambao wamesema: “Aya ya Utakaso imeteremshwa kuhusiana na Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) nao ndiyo Ahlul-Bayt khaswa na wala si wengineo”.81 m) Na ambalo linajumuisha tuliyoyasema, ni hadithi iliyopokewa na Ummu Salama amesema: “Ilipoteremshwa Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Aliendelea hadi aliposema: “Nikainua kishamiya niingie pamoja nao, ndipo akakivuta toka mikononi mwangu na akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’82 Na kutoka kwa Majmaa amesema: “Niliingia pamoja na mama yangu kwa Aisha, mama yangu akamuuliza kwa kusema: “Je uliona umeruhusiwa kutoka siku ya vita vya Jamali?” Akasema: “Hakika ilikuwa ni kadari kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” Kisha akamuuliza kuhusiana na Ali, akasema: “Unaniuliza mtu apendwaye zaidi na Mtume wa Mwenyezi Mungu, 80 Shawahidut-Tanziil Juz. 2. uk 33 na baada yake. 81 Shawahidut-Tanziil Juz. 2. uk 39-54. 82 Shawahidut-Tanziil Juz. 2. uk 76. 62

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain aliyekuwa mume wa kipenzi cha Mtume (s.a.w.w.), hakika nilimuona Mtume (s.a.w.w.) akiwakusanya na kuwaingiza katika nguo yake Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu na wapendwa wangu basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Basi nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi ni katika Ahali zako? Akasema: ‘Sogea kaa kando hakika wewe uko katika kheri.”’ Na katika hadithi nyingine nikasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi sio katika Ahali Zako? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri,” na wala hakuniingiza pamoja nao”.83 Ya kuzingatia katika hadithi hiyo iliyopokewa na Ummul-Muuminiina Aisha ni yafuatayo: Mosi: Kukiri kwake kwa dhambi yake katika kupambana na Imam Ali (a.s.) ili kupigana naye siku ya Jamal, lakini yeye ameegemezea hilo kwenye kadari, yaani kwa Mwenyezi Mungu, ili tu ahalalishe msimamo wake juu ya Imam Ali (a.s.) na kupigana naye. Pili: Amekiri kuwa yeye si muhusika wa Aya hiyo kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) hakumwingiza pamoja nao, na hiyo ni dalili tosha ya kuwa Aya hiyo haiwahusu wanawake au wake wa Mtume (s.a.w.w.). Aidha nasema: Hizo ni baadhi tu ya hadithi zilizopokewa kutoka kwa Haakim Haskaani Al-Hanafiy, naye ni miongoni mwa wanachuo wa Ahlus-Sunna na mfasiri wao, ya kwamba Aya ya Utakaso inawahusu watu hao wanne (a.s.) na wala haiwajumuishi wake wa Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo ujanja wa Aamir Najjar, Muhammad Nassur Al-albaani, Ihsani Dhahiir, Ali Ahmad Saalus na wengineo katika tafsiri ya Aya hiyo kuwa inawahusu wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni upotoshaji na ubadilishaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu swt., na kama pia unavyodhihiri uzushi wake juu ya Shi’a katika maneno 83 Shawahidut-Tanziil Juz. 2. uk 38. 63

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain yao kama ilivyokwisha tangulia waliposema: “Na Shi’a kuwahusisha Ahlul-Bayt ambao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) bila ya wakeze (s.a.w.w.) ni katika upotoshaji wao wa Aya za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kufuata matamanio yao...”. Na kutokana na tuliyoeleza hapo kabla, imedhihiri wazi kati yetu na wao ni nani anayemsingizia Mwenyezi Mungu swt. ili kufuata matamanio ya nafsi yake. Na utafuata mlolongo mkubwa wa vitabu vya tafsiri lukuki kutoka kwa Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, ambao wameifasiri Aya hiyo juu ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.).

7. KITABU TWABARY:

JAAMIUL -BAYAAN

CHA IBN

JARIIR

Ibn Jariir Twabary ameileza Aya hiyo juu ya Ali, Fatimah , Hasan na Husein (a.s.), naye ni mmoja wa Wanachuoni na wafasiri wakubwa wa Ahlus-Sunna, wote kwa njia mbalimbali wameeleza Aya hiyo kuwa imeteremshwa kuwahusu watu hao wanne (a.s.) tu, tunataja baadhi ya hizo ili iwe dalili na kuthibitisha yale wanayoyasema na kuitikadi Shi’a: a) Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudry amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Aya hii imeteremshwa kwa watu watano: Kwangu mimi, Ali, Hasan, Husein na Fatimah (a.s.), hakika Mwenyezi Mungu ametaka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharishieni tohara ya kabisa kabisa.’” b) Imepokewa kutoka kwa Sofia bin Sheibah amesema: “Amesema Aisha: ‘Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka akiwa na nguo nyeusi, punde akaja Hasan akamuiingiza... kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...”’. c) Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik: “Alikuwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) akipita mbele ya nyumba ya Fatimah kwa muda wa miezi sita kila alipokuwa anakwenda kuswali akisema: ‘Swala! Enyi Ahlulbayt, haki64

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ka Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’ d) Imepokewa kutoka kwa Shahar bin Hawshab kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w.) kwangu na Ali, Fatimah, Hasan na Husein... akawafunika nguo nyeusi au kishamiya, akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ni Ahlul-Bayt wangu, waondolee hawa uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’ Imepokewa kutoka kwa Abu Hamrau amesema: “Nilikuwa Madina kwa miezi saba katika zama za Mtume (s.a.w.w.)”. Akasema: “Nilimuona Mtume (s.a.w.w.) kila ikichomoza Alfajiri, akienda katika mlango wa Ali na Fatimah na akisema: “Swala! Swala! Hakika anataka Mwenyezi Mungu...”. Anasema Twabary: “Ameniambia Abdul-Aala bin Waswil akasema: ‘Alituhadithia Fadhili bin Dakiin akasema: ‘Alituhadithia Yunus bin Abi Is-haqa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na mfanowe.”’ f) Imepokelewa kutoka kwa Abu Amar akasema: “Nilikuwa nimekaa kwa Wathilah bin Askaa walipomtaja Ali (r.a.) na kumshutumu, basi waliposimama akasema: “Kaa hadi nikupe habari juu ya huyu ambaye wamemtukana, nilikuwa mimi mbele ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) pindi alipoingia Ali, Fatimah Hasan na Husein akawafunika kishamiya chake kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ni Ahali zangu, Ewe Mola Wangu waondolee hawa uchafu na watoharishe tohara...”’ g) Imepokewa kutoka kwa Abu Said Al-Khudry kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Hakika anataka Mwenyezi Mungu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein akawafunika kishamiya chake cha Khaybar, kisha akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa Ahli zangu “Ewe Mola Wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema: “Je! Mimi si katika wao?” Akasema: ‘Wewe upo katika kheri.”’ 65

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain h) Imepokewa kutoka kwa Muhammad bin Siyriin kutoka kwa Abu Huraira kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Fatimah akaja kwa Mtume (s.a.w.w.)….” Aliendelea hadi aliposema: “Alipowaona wakija alinyoosha mkono wake katika Kishamiya akawafunika na akanyoosha mkono wake mbinguni akasema: ‘Hawa ni ahali zangu watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’ i) Na imepokewa kutoka wa Abu Said kutoka kwa Ummu Salama mke wa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Aya hii iliteremshwa katika nyumba yake: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi si katika AhlulBayt? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri, wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume (s.a.w.w.).” Akasema: ‘Hakika ndani ya nyumba ya Mtume (s.a.w.w.) alikuwamo Ali, Fatimah, Hasan na Husein.” j) Imepokewa kutoka kwa Hashim bin Hashimi bin Utbah bin Abi Waqas kutoka kwa Abdallah bin Wahab bin Zamuat amesema: “Amenisumulia Ummu Salama...”. k) Na kutoka kwa Umar bin Abi Salama amesema: “Aya hii imeteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.) naye akiwa katika nyumba ya Ummu Salama: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” akamwita Ali, Hasan, Husein, Fatimah, kisha akasema: ‘Hawa ni ahali zangu basi waondolee uchafu...”’ l) Ali bin Husein alimwambia mtu mmoja katika watu wa Sham: “Je! hujasoma katika Qur’ani: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...?” Akasema: “Ndiyo nyinyi?” Akasema: ‘Ndiyo.”’ m) Na kutoka kwa Bakiir bin Mismar amesema: “Nilimsikia Amr ibn Saad amesema: “Saad amesema: “Pindi Mtume (s.a.w.w.) ulipoteremshwa wahyi kwake aliwakusanya Ali, watoto wake wawili na binti yake Fatimah akawafunika katika nguo yake kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa 66

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ndiyo ahali zangu.”’ n) Kutoka kwa Hakim bin Saad amesema: “Tulimkumbuka Ali bin Abi Twalib (r.a.) tukiwa kwa Ummu Salama, akasema: “Kuhusiana na yeye imeteremshwa Aya: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt ...’”84 8. TAFSIRUL-KABIIR YA IMAM FAKHRU DIIN AR-RAAZI: Amesema Fakhru Raazi katika kitabu chake cha Tafsiri kuhusiana na maneno ya Mola Muweza: “Basi sema njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu na wanawake wetu na wanawake wenu na nafsi zetu na nafsi zenu...” Haya hapa maneno yake: “... na Mtume (s.a.w.w.) akatoka na nguo yake nyeusi na alikuwa amemweka begani Husein, akamshika mkono Hasan, Fatimah akitembea nyuma yake na Ali (r.a.) nyuma yao wawili huku akisema: “Nikiomba dua semeni Amiin,” hapo akasema Askofu wa Najran: “Enyi wanaswara, mimi naona nyuso hizi lau watamuomba Mwenyezi Mungu ahamishe jabali kutoka mahala pake basi atalihamisha, kwa hivyo msiapizane naye mtaangamia na hatobaki ardhini mkristo yeyote mpaka siku ya Kiyama, hadi aliposema - yaani Ibn Kathiir - na imepokewa kwamba Mtume (s.a.w.w.) pindi alipotoka na nguo yake nyeusi alijiwa na Hasan (r.a.) akamwingiza, akaja Husein (r.a.) akamwingiza, akaja Fatimah kisha Ali (r.a.), hapo akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu ...”’ Jua kwamba hadithi hiyo imekubalika juu ya usahihi wake kwa wafasiri wakubwa na wanahadithi.85 Na anasema Fakhru Raazi katika tafsiri yake kutoka Suratu Twaha aya ya 132: “Na waamrishe ahali zako swala...”: “Na alikuwa Mtume (s.a.w.w.) 84 Jamiul-Bayan fi Taawilil-Qur’ani cha At-Tabariy, Jalada la kumi, Juz. 22, uk 296 na kuendelea. 85 At-Tafsirul-Kabir ya Fakhrur-Raziy, Jalada la nne Juz. 8 uk 71. 67

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain baada ya kuteremshwa Aya hiyo akienda kwa Fatimah na Ali (a.s.) kila asubuhi akisema: “Swala! Swala!” Alifanya hivyo mwezi mzima”.

9. TAFSIRUL-QUR’AN ADHIIM YA IBN KATHIIR: a) Anasema Ibn Kathiir: “Ametuhadithia Imam Ahmad ametusimulia Hamad ametupa habari Ali bin Zayd kutoka kwa Anas bin Malik (r.a.) amesema: “Alikuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akipita mbele ya mlango wa Fatimah (r.a.) kwa muda wa miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali Swala ya alfajiri akisema: “Swala! Swala! Enyi AhlulBayt hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa”. Na amepokea Tirmidhi kutoka kwa Abdu Ibn Hamiid bin Afaani hadithi hiyo akasema ni Hasan na ya kushangaza.”86 b) Aidha akasema Imam Ahmad: “Ametuhadithia Muhammad bin Musab ametuambia Al-Auzai ametusimulia Shidaad Ibn Ammar amesema: “Niliingia kwa Waathilat bin Askar (r.a.) akiwa na halaiki ya watu, basi wakamtaja Ali (r.a.) na wakamtukana, nami nikamtukana pamoja nao. Basi walipoinuka akaniambia umemtukana mtu huyu? Nikasema, walimtukana nami nilimtukana pamoja nao. Akasema: “Je! Nikupe habari ya yale niliyoyaona kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.)?” Nikasema: Ndio. Akasema: “Nilikwenda kwa Fatimah (r.a.) kumuuliza kuhusiana na Ali (r.a.) akasema: “Kaelekea kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.),” basi nikakaa ninamsubiri hadi alipokuja Mtume (s.a.w.w.) nikamuona pamoja naye Ali, Hasan na Husein (r.a.) akiwa amemkamata kila mmoja mkono wake mpaka alipoingia. Kisha akawasogeza Ali na Fatimah (r.a.) akawakalisha mbele yake, na akawakalisha Hasan na Husein (r.a.) kila mmoja juu ya paja lake, hapo akawafunika kishamiya chake, kisha akasoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu.” Na akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa Ahlul-Bayt wangu.”’ 86 Tafsirul-Qur’ani Adhiim ya Ibn Kathiir Juz. 3 Uk. 492. 68

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na ameipokea hadithi hiyo Abu Jafaar bin Jariir kutoka kwa Abdul-Karim bin Abi Umair Al-Quzai kwa Sanadi hiyo hiyo.” c) Na katika hadithi kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Basi akaja Ali, Hasan na Husein... Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu...” Kisha akasema (s.a.w.w.): “Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na watoharishe kisawa sawa”. Akasema: “Nikaingiza kichwa changu ndani ya nyumba na kusema: “Na Mimi ni pamoja nanyi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’ d) Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Abu Huraira naye amepokea kutoka kwa Ummu Salama... hadithi hiyo na nyinginezo kutoka kwa Said amesema: “Tulimtaja Ali bin Abi Twalib (r.a.) mbele ya Ummu Salama...” Aliendelea hadi aliposema: Nikasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mimi? Naapa kwa Mwenyezi Mungu neema ilioje” akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.”’ e) Imepokewa kutoka kwa Ummul Muuminiina Aisha alisema kumwambia mtoto wa ami yake pindi alipomuuliza kuhusiana na Ali (r.a.) akasema: “Unaniuliza juu ya mtu anayependwa mno na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na binti yake aliye kipenzi kwake alikuwa chini yake (mkewe). Hakika nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa amemwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) akawafunika nguo yake na akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa ndio Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Nilisogelea kwao nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi si katika ahali zako?” Akasema (s.a.w.w.): ‘Kaa kando hakika uko katika kheri.”’87

.87 Tafsirul-Qur’ani Al-Adhiim Juz. 3, uk 483 na kuendelea.

69

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nasema: Ama maneno ya Ummul-Muuminina Aisha aliposema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi sio katika Ahlul-Bayt wako?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kaa kando hakika uko katika kheri.” Hiyo ni dalili ya dhahiri kwamba wakeze (s.a.w.w.) hawahusiani kabisa na Aya hiyo ambayo ni Aya ya Utakaso, na hilo amelikiri Ummul Muuminiina Aisha, kwa hivyo tuwaeleweje wale wasiofahamu hilo. 10. AD-DURRUL-MANTHUR CHA JALALU DIIN SUYUUTWI: Na ama Suyuutwi ameieleza Aya ya Utakaso katika tafsiri yake ambayo ni muhimu sana kwa Ahlus-Sunna juu ya Imamu Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na hivyo inajulisha uzushi wa yule ambaye anadhani kuwa Shi’a wao ndio ambao pekee wameihusisha Aya hiyo na hao watukufu wanne (a.s.), ili tu kufuata matamanio yao binafsi, japokuwa wote tuliowataja ni Wanachuoni wakubwa wa Ahli Sunna na wapokezi wao waaminifu ambao wanategemewa zaidi kwao. Amepokea na kuelezea Suyuutwi katika Tafsiir yake ya maneno ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...” zipo hadithi lukuki baadhi ya hizo ni: a) Ameeleza Ibn Munzil Ibn Ali Haatawi, Twabaraan na Ibn Murdawayh kutoka kwa Ummu Salama (r.a.) mke wa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na zamu nyumbani kwake aliletewa kishamiya cha Khaibar na Fatimah (r.a.)....” Aliendelea hadi aliposema: “Kisha akatoa mkono wake kutoka katika kishamiya na akauelekeza mbinguni hapo akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndiyo hasa Ahlulbayt wangu, waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa,” alisema hayo mara tatu, Ummu Salama (r.a.) alisema: “Nikaingiza kichwa changu katika sitara nikasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nami niko pamoja nanyi, akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.”’ b) Amepokea Twabarani kutoka kwa Ummu Salama (r.a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Fatimah (a.s.) niitie mumeo na watoto 70

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain wako, basi akaja nao, Mtume (s.a.w.w.) akawafunika kishamiya chake, kisha akaweka mkono wake juu yao akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wa Muhammad, na katika lafudhi nyingine “Aali Muhammad”, basi jaalia rehema zako na baraka zako juu ya Aali Muhammad kama ulivyojaalia juu ya Aali Ibrahim hakika wewe ni Mwenye kuhimidiwa na uliyetukuka.” Ummu Salama akasema: “Nikainua kishamiya ili niingie pamoja nao, basi akausogeza mkono wangu na akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’ c) Na ameeleza Ibn Murdawayh kutoka kwa Ummu Salama akasema: “Hakika Aya hii imeteremshwa kwenye nyumba yangu: “Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” nyumbani wakiwa Saba, Jibril, Mikail (a.s.) Ali, Fatimah Hasan na Husein na Mimi nikiwa mlangoni, nikasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi sio katika Ahali zako?” Akasema: “Hakika wewe uko katika kheri, na hakika wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume (s.a.w.w.)”. d) Na ameeleza Ibn Murdawayhi na Al-Khatiib kutoka kwa Abu Said AlKhudri (r.a.) amesema: “Ilikuwa siku ya Ummul Muuminina Ummu Salama (r.a.) ndipo nyumbani kwake akateremka Jibril (a.s.) kwa Mtume (s.a.w.w.) akiwa na Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...”. Akasema: Mtume (s.a.w.w.) alimwita Hasan, Husein, Ali, na Fatimah akawa nao pamoja akawafunika nguo yake huku Ummu Salama akiwekewa sitara, kisha akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema: “Nami ni pamoja nao, ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Wewe unasehemu yako, hakika uko kwenye kheri.”’ e) Ameeleza Tirmidhi na amesema ni sahih, Ibn Jariir, Ibn Munzil na Haakim huku naye akisema ni sahih, na Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika kitabu chake cha Sunna kupitia kwa wapokezi wengi kutoka kwa Ummu Salama (r.a.), amesema: “Nyumbani kwangu ilishushwa Aya hii: 71

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu AhlulBayt...” ndani wakiwemo Fatimah, Ali, Hasan, na Husein, basi Mtume (s.a.w.w.) akawafunika kwa kishamiya ambacho alikuwanacho kisha akasema: ‘Hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe kabisa kabisa.”’ f) Na ameeleza Ibn Jariir, Ibn Abu Haatam na Twabaraani kutoka kwa Abu Said Al-Khudri (r.a.) amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: ‘Aya hii imeteremshwa juu ya watu watano, kwangu, kwa Ali, Fatimah Hasan na Husein: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na kuwatoharisheni tohara ya kabisa kabisa.”’ g) Ameeleza Ibn Jariir, Hakiim na Ibn Murdawayh kutoka kwa Saad amesema: “Uliteremshwa wahyi kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) basi akamwingiza Ali, Fatimah na watoto wao wawili katika nguo yake kisha akasema: ‘Hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu.”’ h) Na ameeleza Ibn Abi Shaybah, Ahmad, Ibn Jariir, Ibn Munziil, Ibn Haatam, Twabaraani na Hakim huku akisema kuwa ni sahih, na Bayhaqi katika kitabu chake Sunnan, kutoka kwa Waathilal Al-Aska’u (r.a.) amesema: “Alikuja Mtume (s.a.w.w.) kwa Fatimah akiwa pamoja na Hasan, Husein na Ali hadi walipoingia ndani akawajongeza Ali na Fatimah akawakalisha mbele yake na Hasan na Husein akawapakata kisha akawafunika nguo yake... kisha akasoma Aya hii: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt....’” i) Ameeleza Ibn Abi Shaybah, Ahmad Tirmidhi akaikubali kuwa ni hadithi Hasan, Ibn Jariir, Ibn Munzil, Twabaraani, Hakim naye akaikubali kuwa ni Sahih, na Ibn Murdawayh kutoka kwa Anas (r.a.) amesema: “Mtume wa Mwanyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa anapita mbele ya mlango wa Fatimah (r.a.) alipokuwa anakwenda katika Swala ya alfajiri akisema: ‘Swala! Swala! Enyi Ahlul-Bayt: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’ 72

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain j) Ameeleza Ibn Murdawayhi kutoka kwa Anas (r.a.) amesema: “Tulimshuhudia Mtume (s.a.w.w.) kwa muda wa miezi tisa akienda kwenye mlango wa Ali bin Abi Twalib (r.a.) kila siku mara tano wakati wa kila Swala akisema: ‘Assalaamu alaykum warahmatullahi wabarakatuhu Ahlal-Bayt. Hakika mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt Swala! Swala! Mwenyezi Mungu akurehemuni.”’ k) Ameeleza Twabaraani kutoka kwa Abu Hamran (r.a.) anasema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa muda wa miezi sita akija mbele ya mlango wa Ali na Fatimah akisema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.”’89 Nasema: Hayo ndiyo ambayo anayaeleza Allamah Suyuutwi katika Tafsiir yake, naye ni mmoja kati ya Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na wafasiri wao, kwamba Aya ya Utakaso imeteremshwa makhususi kwa watu hao wanne ambao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) wakiwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.), basi yaliyosemwa na yatakayosemwa kuwa Shi’a ndio ambao wameihusisha Aya hiyo kwa watu hao wanne (a.s.) ili kufuata matamanio yao binafsi, sio kweli bali huo ni uzushi wa dhahiri, ni kumwongopea Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) na ni upotoshaji wa maneno ya Mwenyezi Mungu, na huko ni kutafsiri Qur’ani kwa rai na kufuata matamanio, ambako Bwana Mtume (s.a.w.w.) amekataza katika kauli yake pale aliposema: “Yeyote atakayesema kuhusiana na Qur’ani pasi na kuwa na elimu, basi ajichangulie makao yake motoni.” 11. AL-JAAMI’U L-AHKAMIL-QUR’ANI CHA QURTUBI: Anasema Qurtubi katika Tafsiir yake kuhusiana na Aya ya Utakaso: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt ...”. Jambo hilo limeelezwa katika habari mbalimbali kwamba Mtume 88 Ad-Durul-Manthur Juz. 5, uk 376 – 377. 73

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain (s.a.w.w.) pindi iliposhushwa kwake Aya hiyo, alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein, akawafunika kishamiya chake, kisha akainua mkono wake na kuelekeza mbinguni akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’89

12. TAFSIRUL-KHAZIN: Imekuja katika Tafsirul-Khazin katika kutafsiri Aya ya Utakaso, kutoka kwa Aisha Ummul-Muuminina amesema: “Siku moja alitoka Mtume (s.a.w.w.) huku akiwa na nguo nyeusi….” Hadi mwisho wa hadithi. Na imepokewa kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Aya hii iliteremshwa katika nyumba yake: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...”90 Na kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kwa muda wa miezi sita akipita mbele ya mlango wa Fatimah alipokuwa anakwenda katika Swala ya alfajiri akisema: ‘Swala! Swala! Enyi AhlulBayt...”’91

13. TAFSIRIUL-BAGHAWY: Anasema Baghawy katika kutafsiri Aya ya Utakaso: “Na akaenda Abu Said Al-Khudry na kikosi kikubwa cha taabiina miongoni mwao Mujahid, Qitaada na wasiokuwa hao kwamba, hao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein”. Imepokewa kutoka kwa Sofia binti Shaybah kutoka kwa Aisha Ummul-Muuminiina amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alitoka...” Hadi mwisho wa hadithi. 89 Jami’ul-Ahkamil-Qur’ani Juz. 14, uk 184. 90 Tafsirul-Khazin Juz. 3, uk 499. 91 Tafsirul-Khazin Juz. 3, uk 499. 74

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Nyumbani kwangu iliteremshwa Aya: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”.

14. TAFSIRUT-THAALABY: Amesema Ummu Salama: “Iliteremshwa Aya hii katika nyumba yangu, Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha Mtume (s.a.w.w.) akaingia pamoja nao ndani ya Kishamiya cha Khaybary, akasema: ‘Hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu.....”’

15. AHKAAMUL-QUR’ANI CHA IBNUL ARABI: Imepokewa kutoka kwa Umar bin Abi Salama amesema: “Ilipoteremka Aya hii kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” katika nyumba ya Ummu Salama, Mtume (s.a.w.w.) alimwita Fatimah, Hasan na Husein na Ali alimweka nyuma ya mgongo... kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu...”’.

16. AL-ITIQAAN FI ULUUMUL-QUR’ANI CHA SUYUUTWI: Mtume (s.a.w.w.) amesema Ahlul-Bayt ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein. Ameeleza Tirmidhi na wengineo kutoka kwa Amru bin Abi Salama, Ibn Jariir na wasiyekuwa hao kutoka kwa Ummu Salama, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alimuita Fatimah, Ali, Hasan na Husein pindi iliposhushwa Aya hii: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’92

17. TAFRIRUL-MARAAGHI: Imekuja kutoka kwa Maraaghi katika tafsiri ya Aya ya Utakaso, kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “Nilimshuhudia Mtume (s.a.w.w.) kwa muda wa 92 Al-Itiqaani Fi Uluumil-Quran Juz. 2, uk. 148-149. 75

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain miezi tisa kila siku akienda mbele ya mlango wa Ali bin Abi Twalib kila wakati wa Swala akisema: “Assalaamu Alaykum Warahmatullah, hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu... Swala! Swala! Akarehemuni Mwenyezi Mungu” kila siku mara tano”.

18. ANWAARUT-TANZIIL CHA BAYDHAAWY: Anasema Baydhaawy katika Tafsiir yake: “Shi’a kuwahusisha Ahlul-Bayt pekee kuwa ni Fatimah, Ali na watoto wao (r.a.) ni kutokana na yale yaliyopokewa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w.) pale alipotoka na nguo yake nyeusi...”93

19. AL-KASHAAF CHA ZAMAKHSHARY: Amepokea Zamakhshary katika kitabu chake Al-Kashaafu kutoka kwa Aisha (r.a.): “Siku moja alitoka Mtume (s.a.w.w.) akiwa na nguo nyeusi, akaja Hasan akamuingiza akaja Husein akamwingiza, akaja Fatimah na Ali akawaingiza, kisha akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuendoleeni uchafu Ahlul-Bayt...”’94

20. AL-MUSTADRAK ALAS-SAHIHAIN CHA HAAKIM: a) Katika kitabu Mustadrak ipo hadithi sahihi kutoka kwa Ibn Abbas, amesema: “Mtume (s.a.w.w.) akachukua nguo yake akawafunika Ali, Fatimah, Hasan na Husein akasema: “Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlulbayt...” hadithi hii ni Sahih Sanad na wala mashekhe wawili (Bukhary na Muslim) hawakuileza Dhahabiy anasema katika kitabu chake Talkhiiswu ala Mustadrak: “... na Mtume (s.a.w.w.) akachukua nguo yake akawafunika Ali, Fatimah, Hasan na Husein... ni hadithi sahih.” 95 93 Anwaarut-Tanzill Juz. 22, uk 577. 94 Al-Kashaf Juz. 1, uk 193, tafsiri ya Aya ya Sura Aali Imran: 61. 95 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk. 132-133. 76

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain b) Na kutoka kwa Atwai bin Yassar kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Nyumbani kwangu iliteremshwa Aya: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni....” Akasema: Mtume (s.a.w.w.) akaagiza waje Ali, Fatimah, Hasan na Husein, walipokuja akasema: “Hawa ndiyo AhlulBayt wangu” hadithi hii ni Sahih kwa sharti LA Masheikh wawili japo hawajaiandika, na Dhahabi alikiri usahihi wake katika kitabu chake Talkhiiswu.”96 c) Na kutoka kwa Waathilah bin Askaan amesema: “Nilikwenda kwa Ali sikumkuta, Fatimah akaniambia amekwenda kwa Mtume (s.a.w.w.)... kisha akasema (s.a.w.w.): “Hawa ni Ahlul-Bayt wangu, ewe Mwenyezi Mungu Ahlul-Bayt wangu ndio wenye haki zaidi.” hadithi hii ni sahih kwa sharti la masheikh wawili Bukhari na Muslim japo hawajaiandika, na Dhahabi ameikubali katika kitabu chake Talkhiiswu.”97 d) Na kutoka kwa Sophia bint Shaybah amesema: “Amenihadithia Ummul Muuminiina Aisha (r.a.) amesema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka akiwa na nguo nyeusi akaja Hasan na Husein akawaingiza pamoja naye, punde akaja Fatimah akamuingiza, mara akaja Ali akaingia pamoja nao, kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Hadithi hii ni Sahih kwa sharti la masheikh wawili japo hawajaiandika, na Dhahabi ameikubali katika kitabu chake Talkhiiswu”.98 e) Kutoka kwa Amr ibn Saad amesema: “Uliteremka wahyi kwa Mtume (s.a.w.w.) basi akamuingiza Ali, Fatimah na watoto wao ndani ya nguo yake kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ni Ahli wangu, na ndiyo Ahlul-Bayt wangu.”’99 96 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 146. 97 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 147. 98 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 147. 99 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 147. 77

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain f) Kutoka kwa Isma’il bin Abdillah bin Jaafar bin Abi Twalib kutoka kwa baba yake amesema: “Pindi Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaangalia rehema ikishuka akasema: “Niitieni” Sofia akasema: “Nani ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Ahlul-Bayt wangu Ali, Fatimah, Hasan na Husein”, wakaitwa na walipokuja akawafunika nguo kishamiya chake kisha akainua mkono wake na kuelekeza juu hapo akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ni Ahali wangu basi mpe amani Muhammad na Aali Muhammad”, na Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...” Hadithi hii ina sanad sahih japo Bukhari na Muslim hawakuiandika.” 100 g) Kutoka kwa Bakiir bin Mismaar kutoka kwa Amr ibn Saad kutoka kwa baba yake amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii “Basi tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu, nafsi zetu na nafsi zenu,” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein (r.a.) akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ni Ahli wangu”, hadithi hii ni Sahih kwa sharti la masheikh wawili japo hawajaiandika.” 101 h) Kutoka kwa Anas bin Malik (r.a.) amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya mlango wa Fatimah (r.a.) kwa muda wa miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali swala ya Alfajiri akisema: “Swala! Swala! Enyi Ahlul-Bayt: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu.....”, hadithi hii ni Sahii kwa sharti la Muslim.” 102 i) Kutoka kwa Atwai bin Yassar kutoka kwa Ummu Salama (r.a.) amesema: “Nyumbani kwangu iliteremshwa Aya hii “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt ...” akasema: Mtume (s.a.w.w.) akawaita na kuwakusanya pamoja Ali, Fatimah, Hasan na Husein (ridhaa ya Allah iwe juu yao) basi akasema: “Hawa ndiyo Ahlul100 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 148. 101 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 150. 102 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 3, uk 158 78

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Bayt wangu,” Ummu Salama akasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nami ni katika Ahlul-Bayt?” Akasema: “Hakika wewe uko katika kheri, na hawa ndio hasa Ahlul-Bayt wangu, ewe Mwenyezi Mungu AhlulBayt wangu ndio wenye haki zaidi.” Hadithi hiyo ni Sahih kwa sharti la masheikh wawili, na ameikubali Al-Haafidh katika kitabu chake Talkhiiswu.” 103 Nasema: Mazingatio yanayopatikana katika hadithi hizo ni: Mosi: Ahlul-Bayt katika Aya ya Utakaso ni watu maalum nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). Pili: Hadithi hizo zote ni sahihi, aidha Dhahabi amekiri katika kitabu chake Talkhiiswu kuwa hizo ni sahihi. Tatu: Na jambo ambalo linajulisha usahihi wa hadithi hizo, ni kuwapo ushuhuda sahihi lukuki ambao umepokewa na Sahih Muslim, Sunan Tirmidhi, Musnad Imam Ahmad na nyinginezo miongoni mwa hadithi Sahih. Na yote hayo yanathibitisha usahihi na ukweli wa hadithi hizo ambazo Haakim amezieleza katika kitabu chake Mustadrak Alas-Sahihaini na Al-Haafidhi Ad-Dhahabiy amezikubali. Zaidi ya hapo ni kuwa, iwapo hadithi yenyewe binafsi haitakuwa sahihi, kisha zikapatikana hadithi sahihi zinazoshuhudia usahihi wa maana yake, basi hadithi hiyo itakuwa hoja na dalili ya kufuatwa. Na tayari zimeshashuhudia hadithi za Muslim, Imam Ahmad na Tirmidhi kuwa yaliyoelezwa katika kitabu Mustadrak miongoni mwa hadithi zinazohusu Aya ya Utakaso ni sahihi. Nne: Ikhitilafu ya baadhi ya hadithi ambazo zimepokewa kuhusiana na mpito wa Mtume (s.a.w.w.) mbele ya mlango wa Ali na Fatimah (a.s.) ni kulingana na mazingatio ya mpokezi, baadhi yao wameishi na Mtume (s.a.w.w.) kwa muda wa miezi sita, nacho ni kipindi ambacho alichomuona akipita mbele ya mlango wa Ali na Fatimah, na baadhi yao walikuwa Madina mathalan kwa muda wa miezi tisa na wakamwona Mtume 103 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 2, uk 416. 79

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain (s.a.w.w.) akipita mbele ya mlango wa Fatimah (a.s.) akisema: “Swala! Swala!”. Hivyo ndivyo hadithi hutofautitiana kulingana na hali ya mpokezi wa hadithi ambayo ameishi na tukio husika, na hiyo ni dalili ya kuwepo njia nyingi za hadithi na usahihi wake.

21. DHAKHAIRUL-UQBA CHA MUHIBBU DIIN TWABARI: Muhibbu Diin Twabari ambaye ni mmoja wa wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna anasema: “Mlango wa kubainisha kuwa Fatimah, Ali, Hasan, na Husein hao ni Ahlul-Bayt ambao wameashiriwa na maneno ya Mwenyezi Mungu “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlulbayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.” a) Kutoka kwa Umar bin Abi Salama mtoto wa kufikia wa Mtume (s.a.w.w.): “Aya hii ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...’” ilimteremkia Mtume (s.a.w.w.) katika nyumba ya Ummu Salama (r.a.), hapo Mtume (s.a.w.w.) alimuita......, na Ummu Salama akasema: “Na mimi niko pamoja nao ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Wewe una sehemu yako na wewe uko katika kheri.” Na katika hadithi nyingine: ‘Hakika wewe uko katika kheri, wewe ni katika wake wa Mtume (s.a.w.w.)”’104 b) Kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika kishamiya chake Hasan, Husein, Fatimah na Ali, hapo akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watakase utakaso wa sawa sawa.” Ummu Salama akasema: “Nami ni pamoja nao, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.”’105 c) Kutoka kwa Aisha amesema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka na nguo yake nyeusi...” Aliendelea hadi aliposema: “Kisha akasema 104 Dhakhairul-Uqba uk. 21. 105 Dhakhairul-Uqba uk. 21-22. 80

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Ameieleza hiyo Muslim, naye Ahmad ametaja maana yake kutoka kwa Waathilah, na mwishowe akaongeza: “Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa hasa Ahlul-Bayt wangu na Ahlul-Bayt wangu ndio wenye haki zaidi.”106 d) “Kutoka kwa Abu Said Al-Khudri katika maneno ya Subhaanahu wa Ta’ala: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Akasema: “Iliteremshwa kwa watu watano, kwangu mimi Mtume (s.a.w.w.) kwa Ali, Fatimah, Hasan na Husein.” Ameieleza Ahmad katika kitabu Manaaqibu na ameieleza hiyo Twabarani.” 107 e) Kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa anapita mbele ya mlango wa Fatimah kwa muda wa miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali swala ya alfajiri akisema: “Swala! Swala! enyi Ahlul-Bayt...” Ameieleza hiyo Ahmad, na kutoka kwa Abuhamrau amesema: “Nilisuhubiana na Mtume (s.a.w.w.) kwa miezi tisa, alikuwa akiamka anakwenda mbele ya mlango wa Ali na Fatimah akisema: ‘Mwenyezi Mungu akurehemuni: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’108 Anasema Muhibbu Twabary: “Pindi iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu swt.: “Basi sema tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanaweke wetu na....,” Mtume (s.a.w.w.) aliwaita watu hawa wanne, imepokewa kutoka kwa Abu Said (r.a) kuwa pindi ilipoteremshwa Aya hii kwa Mtume (s.a.w.w.): “Basi sema tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein na akasema: “Hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu.” Ameieleza Muslim na Tirmidhi.” 109

106 Dhakhairul-Uqba uk. 24. 107 Dhakhairul-Uqba uk. 24. 108 Dhakhairul-Uqba uk. 24-25. 109 Dhakhairul-Uqba uk. 24-25. 81

7/1/2011

4:06 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 22. AR-RIYAADHU AN-NADHRAT FI MANAAQIBIL-ASHRA CHA MUHIBBU TWABARY. Amepokea Muhibbu Din Twabary kutoka kwa Saidi amesema: “Muawiya alimwamrisha Saad amtukane Abu Turaab (Imam Ali), akasema: “Ama nikikumbuka mambo matatu aliyoyasema Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana naye kamwe siwezi kumtukana... na pindi ilipoteremshwa: “Basi sema tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita, Ali, Fatimah, Hasan na Husein akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa ndio Ahli wangu.” Amepokea Muslim na Tirmidhi”.110 Na kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika Hasan, Husein, Ali na Fatimah kishamiya, akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa hasa hasa Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Ameipokea Tirmidhi na akasema ni hadithi hasana na Sahih”. Na kutoka kwa Said bin Amru kutoka kwa Saidi bin Aswi amesema: “.......Na yalipoteremshwa maneno ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Hakika Mwenyezi Mungu anatoka kukuondoleeni uchafu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Fatimah, Ali, Hasan na Husein katika nyumba ya Ummu Salama akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ndiyo Ahlul-Bayt wangu hasa, basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’111 Na kutoka kwa Ibn Abbas amesema: “.....Mtume (s.a.w.w.) akachukua nguo yake akawafunika Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha akasema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na awatoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’112 110 Riyadhun- Nadhra fi Manaqibil- Ashra Juz. 3, uk 134-135. 111 Riyadhun- Nadhra fi Manaqibil- Ashra Juz. 3, uk 134-135. 112 - Riyadhun- Nadhra fi Manaqibil- Ashra Juz. 3, uk 154. 82

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 23. AL-MANAAQIB CHA IBN MAGHAZILY SHAAFII: Ameeleza Ibn Maghazily Shaafii katika kitabu chake Al-Manaqib hadithi lukuki zinazojulisha juu ya Aya ya Utakaso kwamba iliteremshwa maalum kwa ajili ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.) na baadhi ya hizo ni:Imepokewa kutoka kwa Ali bin Abi Twalib (a.s.) siku ya kongamano la kutoa na kusoma tenzi akasema: “Mwenyezi Mungu akupeni jazaa njema Je! Yupo kati yenu ambaye imeteremshwa juu yake Aya ya Utakaso kama inavyosema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...” asiyekuwa mimi? Wakasema: “Kwa kweli hapana”.113 Imepokewa kutoka kwa Ummu Salama amesema Aya hii: “‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt....’ iliteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatimah, Hasan na Husein”.114 Imepokewa kutoka kwa Abu Yakdhaan kutoka kwa Zadaayn kutoka kwa Hasan Bin Ali amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya ya Utakaso Mtume (s.a.w.w.) alitukusanya katika kishamiya cha Ummu Salama cha Khaybar kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu, hawa ndio Ahlul-Bayt wangu na kizazi changu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”115 Kutoka kwa Shaharu bin Hawshab amesema: “Nilimsikia Ummu Salama anasema: ‘Wakati Mtume (s.a.w.w.) amekaa na mimi akaagiza waitwe Hasan, Husein, Fatimah na Ali, rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao, akachukuwa kishamiya chini yangu akawafunika akasema: “Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa”, mara kadhaa. Akasema: “Na mimi ni pamoja nao?” Akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.’”116 113 Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 91. 114 Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 188. 115 Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 188-189. 116 Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 189. 83

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na katika hadithi nyingine imepokewa kutoka kwa Fatimah (Rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) Amesema: “Basi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akasema: Mwite mumeo na wanao Hasan na Husein, nikawaita na wakati wao wakila ikateremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.) Aya: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” hapo Mtume (s.a.w.w.) akachukua kishamiya chake na akawafunika kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu, basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”’117 Na kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: “Aya hii “Hakika Mwenyezi Mungu anataka.....” iliteremshwa kuhusiana na Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatimah, Hasan na Husein.” Akasema: “Ummu Salama akiwa mlangoni alisema: “Ewe Mtume na mimi?” Akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri”’118

24. IS’AAFUR-RAGHIBIINA CHA IBN SWABAAN: Anasema Ibn Swabaan katika kitabu chake Is’aafur-Raghiibina, naye ni miongoni mwa wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna: “Imepokea kwa wapokezi mbalimbali kuwa, Mtume (s.a.w.w.) alikuja na Ali, Fatimah, Hasan na Husein huku akiwa kamshika kila mmoja mkono mpaka alipoingia, kisha akamsogeza Ali na Fatimah na kuwakalisha mbele yake na akawakalisha Hasan na Husein kila mmoja kwenye paja lake, kisha akawafunika kishamia na kusoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutakaseni kabisa.” Kisha akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa, ndio Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na uwatakase kabisa.”’ 119

117 Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 189-190. 118 - Manaqib Ibn Maghazil Shafii uk. 190. 119 Is’aafur-Raghiibina uk. 115. 84

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na katika hadithi iliyopokewa na Ummu Salama amesema: “Nikainua kishamiya ili niingie pamoja nao akausogeza mkono wangu, nikasema mimi ni pamoja na nyinyi ewe Mjumbe wa Mungu? Akasema: ‘Hakika wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) uko katika kheri.”’ Na katika hadithi nyingine aliyoipokea Ummu Salamah amesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa katika nyumba yake punde akaja Fatimah... Hadi mwisho wa hadithi.120 Na amepokea Ahmad na Twabaraani kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Aya hiyo ilitereremshwa juu ya watu watano, kwangu mimi, kwa Ali, Hasan, Husein na kwa Fatimah.” Na amepokea hadithi hiyo Ibn Abu Sheyban, Ahmad, Tirmidhi na kuikubali kuwa ni sahihi, aidha Ibn Jariiri, Ibn Mundhir, Twabarani na Hakim nao wameikubali”. Na kutoka kwa Anas amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya nyumba ya Fatimah pindi alipokuwa anakwenda kuswali swala ya alfajiri anasema: ‘Swala! Enyi Ahlul-Bayt. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’ Na katika hadithi iliyopokewa na Ibn Murdawayhi kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema kwamba Mtume (s.a.w.w.) alipita siku arobaini mbele ya mlango wa Fatimah akisema: “Assalaam Alaykum Ahlul-Bayt Warahmatullahi Wabarakatuhu, Swala Mwenyezi Mungu akurehemuni. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”. Na katika hadithi iliyopokewa na Ibn Abbas alifanya hivyo kwa muda wa miezi saba na amepokea Muslim na Nasaai kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alisimama na akahutubia akasema: ‘Ninawakumbusha kuhusiana na Ahlul-bat wangu.”’121 120 Is’aafur-Raghiibina uk. 115. 121 Is’aafur-Raghiibina uk. 116-117. 85

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 25. JAAMIUL-USUUL MIN AHADITHIR-RASUUL CHA IBN ATHIIR: Hadithi nambari 6689, kutoka kwa Ummu Salama (r.a.) amesema: “Aya ifuatayo iliteremshwa nyumbani kwangu nayo ni: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutakaseni utakaso wa kabisa kabisa.” Akasema: Na mimi nimekaa mlangoni nikasema: “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je! Mimi sio katika Ahli wako?” Akasema: “Hakika wewe uko katika kheri na wewe ni miongoni mwa wake wa Mtume (s.a.w.w.)”. Wakati huo ndani alikuwemo Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatimah, Hasan na Husein basi akawafunika kwa kishamiya chake, hapo akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu...” Na katika hadithi nyingine: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika Hasan, Husein Ali na Fatimah, kisha akasema: “Ewe Mola Wangu hawa hasa ndio Ahlul-Bayt wangu...” Ummu Salama akasema: “Na mimi ni pamoja nao ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Hakika wewe uko katika kheri.”’ Na kutoka kwa Umar bin Abu Salama (r.a.) amesema: “Aya hii iliteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.) “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...” katika nyumba ya Ummu Salama, akasema Ummu Salama: “Mimi ni pamoja nao ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Wewe una mahala pako, na wewe uko katika kheri.”’122 Na kutoka kwa Anas bin Malik (r.a.) amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hiyo hakika Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya mlango wa Fatimah pindi alipokuwa anakwenda kuswali.”123 122 Jamiul-Usuul, hadithi namba 6690. 123 Jamiul-Usuul, hadithi namba 6691. 86

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na kutoka kwa Aisha (r.a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alitoka akiwa na nguo yake nyeusi, punde akamjia Hasan akamwingiza akamjia Husein akamwingiza, kisha akamjia Fatimah akamwingiza, hatimaye akaja Ali akamwingiza hapo akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka...” hadithi hiyo imeelezwa na Muslim.”124 26. AL-ISTIAAB FIMAARIFATIL-AS’HAAB CHA IBN ABDULBARR: Katika kitabu Istiaab cha Ibn Abdul-Barr amesema: “Pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlulbayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Fatimah, Ali, Hasan na Husein (r.a.) katika nyumba ya Ummu Salama na akasema: ‘Ewe Mola Wangu hakika hawa ndio AhlulBayt wangu waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’ 27. USUDUL-GHAABA FIMAARIFATIS-SWAHABAH CHA IBN ATHIIR: a) Kutoka kwa Umar bin Abi Salama rabibu wa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Aya hii imeteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”, katika nyumba ya Ummu Salama, basi Mtume (s.a.w.w.) akamwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein akawafunika kishamiya chake kisha akasema: “Ewe Mola Wangu, hawa ndio Ahlul-Bayt wangu basi waondolee uchafu...”, Ummu Salama akasema: “Nami ni pamoja nao ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Wewe una mahala pako na wewe upo katika kheri.”’125 b) Amepokea Al-Auza’i kutoka kwa Shidadi bin Abdullah amesema: “Nimemsikia Waathilat bin Asqaa, wakati kilipoletwa kichwa cha Husein, 124 Jamiul-Usuul, hadithi namba 6692. 125 Usudul-Ghabah Juz. 2, uk. 12. 87

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain mtu wa Sham akamlaani (Husein) na akamlaani baba yake (Ali), Wathilat akasema: “Naapa kwa Mwenyezi Mungu nitaendelea kumpenda Ali, Hasan, Husein na Fatimah kwa hakika nilimsikia mjumbe wa Mwenyezi Mungu akiwaambiwa aliyowaambia, kwani hakika nilimuona siku moja nilipokwenda kwake akiwa katika nyumba ya Ummu Salama, punde sipunde akaja Hasan akamkalisha katika paja lake la kulia kisha akambusu kisha akaja Husein akamkalisha katika paja lake la kushoto na akambusu kisha akaja Fatimah akamkalisha mbele yake hatimaye akamwita Ali hapo akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Nikamuuliza Wathilat: “Nini uchafu?” Akasema: ‘Shaka kwa Mwenyezi Mungu Azza Wajalla.”’126 c) Na kutoka kwa Amari bin Saad bi Abu Waqaas kutoka kwa baba yake amesema: “Muawiya alimwamrisha Saad akamwambia: “Kipi kinachokuzuia kumtukana baba wa mchanga-yaani Ali –?” Akasema: “Ama nikikumbuka mambo matatu ambayo Mtume (s.a.w.w.) alimwambia yeye siwezi kumtukana..... na iliteremshwa Aya hii “Basi sema njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu wanawake wetu na wanawake wenu na nafsi zetu na nafsi zenu”. Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein na akasema: ‘Hawa ndio Ahlul-Bayt wangu.”’127 d) Na kutoka kwa Shahar bin Hawshab kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika kishamiya chake Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha akasema: “Ewe Mola Wangu hawa hasa hasa ndio AhlulBayt wangu basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema. “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nami ni pamoja nao?” Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri”’128

126 Usudul-Ghabah Juz. 2, uk. 21. 127 Usudul-Ghabah Juz. 4, uk. 25-26. 128 Usudul-Ghabah Juz. 4, uk 29. 88

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 28. MUSHKILUL-ATHAAR CHA ABU JAFAR AL-TWAHAAWY: Amepokea Twahawy kwa Sanadi yake kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Aya hii iliteremshwa kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatimah, Hasan na Husein ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...”’129 Na amepokea Twahawy kwa Sanadi yake kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Aya hii iliteremshwa nyumbani kwangu: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka...” ikiwahusu watu saba, Jibril, Mikail, Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatimah, Hasan na Husein”.130 Aidha amepokea kwa Sanadi yake kutoka kwa Amraatu Al-Hamadaani amesema: “.....” Aliendelea hadi aliposema: “Nikasema “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi ni katika Ahlul-Bayt?” Basi akasema: “Hakika una kheri mbele ya Mwenyezi Mungu.” Nilipendelea aseme ni miongoni mwao, ingekuwa ni bora zaidi kwangu kuliko kilichochomozewa na kuzama jua.”131 Vile vile amepokea Twahawy kwa Sanadi yake kutoka kwa Abu Hamraani amesema: “Nilimsuhubu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu miezi tisa, alikuwa akiamka na kwenda mbele ya mlango wa Fatimah akisema: ‘Assalam Alaykum ya Ahlul-Bayt. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’132 29. MAJMAUZ-ZAWAID CHA HAYTHAMY: Kutoka kwa Abu Saidi Al-Khudri amesema: “Hakika Bwana Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita asubuhi mbele ya mlango wa Ali siku arobaini 129 Mushkilul-Athaar Juz. 1, uk 332. 130 Mushkilul-Athaar Juz. 1, uk 336. 131 Mushkilul-Athaar Juz. 1, uk 336. 132 Mushkilul-Athaar Juz. 1, uk 338. 89

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain akisema: “Assalaamu Alaykum Ahlul-Bayt Warahmatullahi Wabarakatuhu. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...”. Akasema: Ameipokea Twabarany katika kitabu Awsat”. Aidha imepokewa kutoka kwa Hamraan amesema: “Nilimuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akienda mbele ya mlango wa Ali na Fatimah kwa muda wa miezi sita akisema: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’ Vilevile amepokea Abu Barzah amesema: “Niliswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) miezi saba, alikuwa akitoka nyumbani kwake akipita mbele ya mlango wa Fatimah akisema: ‘Assalaamu alaykum. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...”’ Hadi mwisho wa alivyoeleza Haythamy katika Majmauz-Zawaid. 30. ASBABUN-NUZUUL CHA WAAHIDY NAYSABUURY: Katika kauli yake Subhanahu Wataala: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” amesema Wahidy Naysabuury: “Kutoka kwa Abu Said amesema: ‘Aya hiyo iliteremshwa juu ya watu watano, kwa Mtume (s.a.w.w.), Ali, Fatimah, Hasan na Husein.”’133 Kutoka kwa Atwai bin Abu Riyah amesema: “Amenieleza ambaye alimsikia Ummu Salama akitaja...” Aliendelea hadi aliposema: “Kisha akatoa mikono yake na akailekeza mbinguni hapo akasema: “Ewe Mola Wangu hawa hasa ndio Ahlul-Bayt wangu, basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Akasema: “Nikaingiza kichwa changu ndani nikasema: Nami ni pamoja nao ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Hakika upo katika kheri.”’134

133 Asbabun-Nuzuul uk. 295. 134 Asbabun-Nuzuul uk. 296. 90

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 31. NUURUL-ABSWAR CHA SHABLANJI: Kutoka kwa Aisha (r.a.) amesema: “Hakika Mtume (s.a.w.w.) alitoka siku moja akiwa na nguo nyeusi akaja Hasan....” Hadi mwisho wa hadithi.135 Shablanji amesema: “Imepokewa katika njia nyingi zilizo sahihi kuwa, Mtume (s.a.w.w.) alikuja akiwa na Ali, Fatimah, Hasan na Husein kisha akachukua nguo yake nyeusi na kuwafunika kisha akasoma Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”, na akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahlul-Bayt wangu basi watoharishe na watakase kabisa kabisa.’” Na katika hadithi nyingine: “Ewe Mola Wangu hawa ndio ndugu wa Muhammad, basi jaalia rehema na baraka zako juu ya Aali Muhammad kama ulivyojaalia juu ya ndugu wa Ibrahim hakika Wewe ni mwenye kuhimidiwa na kusifiwa.”136 Na katika hadithi ya Ummu Salama amesema: “Nikaingia katika kishamiya ili niingie pamoja nao, akausogeza mkono wangu, nikasema: “Na mimi ni pamoja na nyinyi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Hakika wewe ni miongoni mwa wake za Mtume upo katika kheri”’.137 Katika hadithi ya Ahmad na Twabaraani kutoka kwa Abu Said Al-Khudri amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Aya hiyo imeteremshwa juu ya watu watano kwangu mimi, Ali, Fatimah, Hasan na Husein.’” Na amepokea Ibn Abi Shayba, Ahmad na Tirmidhi, naye amesema ni hadithi Hasan. Na Ibn Jariir, Ibn Mundhiri, Tabaraani, na Haakim naye amesema ni hadithi Sahih. Kutoka kwa Anas amesema: “Baada ya 135 Nurul-Absar uk. 123. 136 Nurul-Absar uk. 123. 137 - Nurul-Absar uk. 123. 91

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kuteremshwa Aya hiyo, kama ilivyokuja katika hadithi ya Tirmidhi: Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya nyumba ya Fatimah pindi alipokuwa akienda katika Swala ya alfajiri akisema: ‘Swala enyi AhlulBayt...”’ Na katika hadithi ya Ibn Murdawayh kutoka kwa Abu Saidi Al-Khudri amesema kwamba, Mtume (s.a.w.w.) alipita siku arobaini asubuhi mbele ya nyumba ya Fatimah...138

32. ANSBABUL-ASHRAAF CHA BALADHURI: Kutoka kwa Anas bin Malik amesema: “Alikuwa Mtume (s.a.w.w.) akipita mbele ya nyumba ya Fatimah (a.s.) miezi sita pindi alipokuwa anakwenda kuswali Swala ya asubuhi anasema: ‘Swala yaa Ahlul-Bayt. Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kuwatoharisha tohara ya kabisa kabisa.”’139

33. SAWAIQUL-MUHRIQAH CHA IBN HAJAR AL-HAYTHAMI: Ameandika Ibn Hajar katika kitabu chake Sawaiqul-Muhriqah: “Ni sahihi Mtume (s.a.w.w.) aliwaingiza watu hao katika kishamiya na akasema: “Ewe Mola Wangu hawa hasa ndio Ahlul-Bayt wangu basi waondolee uchafu na watoharishe tohara ya kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema: “Na mimi ni pamoja nao?” Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri.”’ Aidha anasema: “Wafasiri wengi wameeleza kwamba Aya ya Utakaso imeteremshwa kwa ajili ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein”. Vilevile ameandika: “Ameeleza Ahmad kutoka kwa Abu Said Al-Khudri kwamba Aya hiyo iliteremshwa juu ya hao watano, kwa Mtume (s.a.w.w.), 138 Nurul-Absar uk. 124. 139 Ansabul-Ashraf uk. 104. 92

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Ali, Fatimah, Hasan na Husein, na ameeleza hivyo Ibn Jariir kwa lafdhi: “Aya hiyo imeteremshwa juu ya watano, kwangu mimi, Ali, Hasan, Husein na Fatimah.” Na hali kadhalika ameeleza hadithi hiyo Twabaraani, na Muslim amesema: ‘Mtume (s.a.w.w.) aliwaingiza hao katika kishamiya alichokuwa nacho na akasoma Aya hii: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu....”’140 34. FAT’HUL-QADIIR CHA SHAWKANI: Shawkani anasema: “Ameeleza Tirmidhi na kuikubali hadithi hiyo kuwa ni Sahih, Ibn Murdawayh na Bayhaqi katika kitabu chake Sunnan kwa njia kadhaa kutoka kwa Ummu Salama amesema: “Nyumbani kwangu imeteremshwa Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...” na nyumbani wakiwa Fatimah, Ali, Hasan na Husein basi Mtume (s.a.w.w.) akawafunika kwa kishamiya alichokuwa nacho kisha akasema: ‘Hawa ndio Ahlul-Bayt wangu, basi waondolee uchafu na uwatoharishe tohara ya kabisa kabisa.”’ Ameeleza Ibn Jariir, Ibn Mundhir, Ibn Abi Haatam, Twabarani na Ibn Murdawayhi kutoka kwa Ummu Salama, aidha amesema Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwake akiwa na kishamiya cha Khaybari, akaja Fatimah Mtume (s.a.w.w.) akamwambia: “Niitie mumeo na wanao Hasan na Husein” akawaita, wakiwa wanakula ikateremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.) Aya hii: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlulbayt...” hapo Mtume (s.a.w.w.) akachukua kishamiya chake na kuwafunika, kisha akatoa mkono wake na kuuelekeza mbinguni akasema “Ewe Mola Wangu hawa ndio hasa hasa Ahlul-Bayt wangu basi waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa”. Aliyasema hayo mara tatu, Ummu Salama akasema: “Nikaingiza kichwa changu katika sitara nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na mimi ni pamoja nanyi?” Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri.” Mara mbili. 140 Sawaiqul-Muhriqah uk. 141-143.

93

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Shawkani anasema: “Hakika ametaja Ibn Kathiir katika Tafsiir yake hadithi ya Ummu Salama kwa njia mbalimbali kwa sanadi ya Ahmad na wengineo, na ameeleza Ibn Murdawayh na Khatiib kuhusiana na hadithi ya Abu Saidi Al-Khudri na wengineo, aidha ameeleza Tirmidhi, Ibn Jariir, Twabaraani na Ibn Murdawayh kutoka kwa Umar bin Abu Salama rabibu wa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Pindi Aya hii ilipoteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’ Akaieleza hadithi ya Ummu Salamah. Shawkaani anasema: “Ameeleza Ibn Abi Shayba Ahmad, Muslim, Ibn Jariir, Ibn Abi Haatam na Hakimu kutoka kwa Aisha amesema: ‘Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alitoka akiwa na nguo yake nyeusi, punde si punde akaja Hasan na Husein akawaingiza katika nguo yake punde akaja Fatimah akamwingiza katika nguo yake, kisha akaja Ali akamwingiza hapo akasema: Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlulbayti na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.’” Na ameeleza Ibn Abu Shayba, Ahmad, Ibn Jariir, Ibn Mundhir, Ibn Abi Haytaam, Twabaraani na kusema ni sahihi, Haakim na Bayhaqi katika kitabu chake Sunnan, kutoka kwa Wathilah bin Asqa’u amesema: “Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuja kwa Fatimah akiwa pamoja na Ali, Hasan, na Husein hadi alipoingia, akawasogeza Ali na Fatimah na kuwakalisha mbele yake, na Hasan na Husein kila mmoja katika paja lake, kisha akawafunika nguo yake na akasoma Aya hii... “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt...” na akasema: ‘Ewe Mola Wangu hawa hasahasa ndio Ahlul-Bayt wangu, waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”’ Ameeleza Ibn Abi Shayba na Ahmad akaikubali kuwa ni hadithi sahih, Ibn Jariir, Ibn Mundhir, Twabarani, Hakim wakaikubali kuwa ni hadithi sahih, na Ibn Murdawayh kutoka kwa Anas amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akipita mbele ya mlango wa Fatimah alipokuwa anakwenda kuswali Swala ya Alfajiri akisema: ‘Swala.. Ahlul-Bayt. Hakika Mwenyezi Mungu 94

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa.”’ Amesema Ibn Jariir na Ibn Murdawayh kutoka kwa Abu Hamraan amesema: “Nilikaa Madina kwa muda wa miezi saba katika zama za Mtume (s.a.w.w.), akasema: Nilimuona Mtume (s.a.w.w.) inapochomoza alfajiri akienda mbele ya mlango wa Ali na Fatimah na akisema: ‘Swala! Swala! Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...”’141 Na katika mlango huu kuna hadithi na athari nyngi, na tumezitaja hizo tu ikiwa ni zile zinazofaa kushikamana nazo na kuziacha zile zisizofaa.

HITIMISHO KUHUSU AYA YA UTAKASO KAMA ILIVYOKUJA KATIKA VITABU VYA AHLUS-SUNNA: Nasema: Tunatosheka na kiwango hicho kutokana na dalili zilizopatikana kwa njia mbalimbali katika vitabu vya Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na wafasiri wao, na kuna vitabu vingi sana miongoni mwa vitabu vya AhlusSunna ambavyo vimefasiri Aya ya Utakaso kwa ajili ya watu hao wanne (a.s.) nasi tumevitaja kwa mukhtasari.

MAMBO KADHAA YA KUZINGATIA: Mosi: Ahlus-Sunna wametaja katika vitabu vyao kwamba Ahlul-Bayt waliotajwa katika Aya ya Utakaso ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na baadhi ya vitabu hivyo vinaitwa Sahih na Musnad, kama vile Sahih ya Imam Muslim, Sunanu Tirmidhi, Khasais Nasaai, Musnad Ahmad na wengineo ambao tumewataja hapo kabla, na hii ni hoja mwafaka ambayo yampasa Dk. Aamir Najjar, Ust. Albaani, Saaluus na Uthman Aal-Khamiis wazichukue na washikamane nazo iwapo watataka kujua ukweli na haki. 141 Fat’hul-Qadiir, jalada la nne, Juz. 4, uk 279-280. 95

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Pili: Aya tukufu haiwahusu wake wa Mtume (s.a.w.w.) kwa kukiri hilo Ummul-Muuminiina Aisha na Ummu Salama kama ilivyokwishatangulia hapo kabla, zipo dalili tosha na za wazi ambazo zinawatoa wake wa Mtume (s.a.w.w.) katika Aya ya Utakaso, na hao sio katika Ahlul-Bayt ambao Mwenyezi Mungu swt. amewaondolea uchafu na kuwatakasa kabisa kama alivyosema Mtume (s.a.w.w.) kumwambia Aisha: “Sogea kaa kando hakika wewe upo katika kheri, au wewe ni katika wake wa Mtume (s.a.w.w.)” na hiyo ni dalili tosha kwamba mke sio katika Ahlul-Bayt mpaka iwahusu Aya ya Utakaso. Ama wale ambao wanadai kwamba Aya hiyo inawahusu wake wa Mtume (s.a.w.w.) kama ilivyokuja kutokana na maneno ya mke wa Nabii Ibrahim (a.s.), huo ni uthibitisho batili, kwa sababu mke wa Nabii Ibrahim (a.s) alikuwa miongoni mwa Ahali wake kwa sababu ya mafungamano ya ukaraba wa nasaba, na hii ni kinyume na wake wa Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo Aya hiyo imewahusisha hao wanne tu, na hilo amelieleza kinaga ubaga Bwana Mtume (s.a.w.w.), naye hatamki kwa matamanio yake isipokuwa kwa kupewa ufunuo ambao anaofunuliwa. Tatu: Hilo limedhihiri kwetu kutokana na kutaja idadi kubwa ya Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna miongoni mwa wale ambao wameifasiri Aya ya Utakaso juu ya hao wanne nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na hilo linaonyesha uzushi wa yule ambaye anadai kwamba: “Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna hawajui lolote kuhusiana na hadithi hizo, na kwamba hadithi hizo hazipo katika vitabu vya AhlusSunna, na hizo ni katika hadithi zilizozushwa na kubuniwa na Shi’a, na upotoshaji huo ni kwa ajili ya kufuata matamanio yao kwa lengo la kuwababaisha watu, aidha ili watu wawaone wako katika haki na kwa ajili hiyo wateke nyoyo zao kuwaelekea Shi’a na hayo yote ni katika kutumikia maadui wa Uislamu na kupanda mbegu za fitina na utengano baina ya Waislamu.”

96

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nne: Hakika kuitafsiri Aya kwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) ni jambo lisilokubalika kwa sababu linakwenda kinyume na yale yaliyothibiti yaliyo wazi na sahihi, kwamba wake wa Mtume (s.a.w.w.) sio katika Ahlul-Bayt ambao wameelezwa katika Aya ya Utakaso, bila shaka huo ni upotoshaji wa Dk. Aamiir Najjar, Ustadhi Muhammad Nassuro Diin Albaani, Dk. Saaluus, Ihsaan Dhahiir, Uthman na Khamiis na wasiokuwa hao miongoni mwa wale ambao hujaribu kupotosha maneno ya Mwenyezi Mungu swt., Sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.), kama ilivyodhihiri kwamba Shi’a ni watu wakweli zaidi, wachamungu na wenye kushikamana na dini, aidha ni watu ambao wameepukana na uzushi, uongo na upaotoshaji, na sifa hizo za uongo na upotoaji ni alama za wale walioacha vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt kama tulivyoashiria hapo kabla. HADITH THAQALAIN KATIKA VITABU VYA AHLUS-SUNNA: Mosi: Mjadala juu ya hadithi inayosema: “Na Sunna yangu” na yenyewe ni hadithi iliyozushwa. Kabla hatujaielezea Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya: “Na kizazi changu, Ahlul-Bayti wangu,” tunapenda kuashiria kwamba hadithi hiyo ipo katika vitabu vya Ahlus-Sunna katika riwaya mbili: Kwanza: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu.” Pili: “Nimekuachieni ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.), au na Sunna yangu.” Na kabla hatujaonesha udhaifu wa hadithi inayosema: “Na sunna yangu” kwani hiyo ni miongoni mwa hadithi zilizobuniwa, ni kuwa Imam Muslim hajaipokea hadithi hiyo katika kitabu chake Sahih Muslim, na hiyo ni dalili dhahiri Shahir ya kuonyesha udhaifu wa hadhithi hiyo. Kinyume na hadithi inayosema: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu,” ambayo ameipokea 97

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Imam Muslim katika Sahih yake kwa riwaya nne. Na lililo bayana ni kwamba kuichukua hadithi inayosema “Na sunna yangu” kuwa ni maneno pekee kutoka kwa Nabii (s.a.w.w.), na kuacha hadithi inayosema “Na kizazi changu”, kunawatengenezea Ahlus-Sunna baadhi ya juhudi zenye lengo la kuepuka na kutupilia mbali natija itokanayo na kitendo cha kushikamana na hadithi hii kwa lafudhi ya “Na kizazi changu.” Kwa sababu kuichukua hadithi hii kwa lafudhi ya “Na kizazi changu” kunavunja nguzo ya msingi ya itikadi kwao wao, hiyo ni kwa kuwa lafudhi hiyo inawajibisha kushikamana na Ahlul-Bayti (a.s.), na hatimaye kushikamana huko kunapelekea kubatilika kisheria ukhalifa wa wale waliochukua ukhalifa miongoni mwa makhalifa wao, na hapo linabomoka kila lile walilolijenga kwa kutegemea lafudhi ya “Na sunna yangu”, kuanzia akida mpaka hukumu za kifiqhi. Kwa hali hiyo walifanya chini juu Dk. Aamir Najjar, Ustadhi Muhammad Nassur Diin Albaani, Dk. Ali Ahmad Saaluus na wengineo ima kufasiri neno “Ahlul-Bayt” katika hadithi kwa maana ya wake wa Mtume (s.a.w.w.), kama alivyofanya Albaani na Najjar. Au kuifanya dhaifu hadithi: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” kama alivyofanya Saaluus. Lakini yanayovunja na kuharibu mtazamo huo ni ule uzito uliyopo kwenye hadithi inayosema: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Kama zilivyopokewa hadithi nyingi ambazo zinaeleza muradi wa Ahlul-Bayt ni Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.). Ama aliyoyaaeleza Dk. Ali Ahmad Saaluus na wengineo juu ya hadithi inayosema: “Nimekuachieni ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.)” sio sahihi, kwa sababu ni katika hadithi zilizobuniwa, nayo ni hadithi iliyopokewa na mtu mmoja kwa hivyo haifai kuzingatiwa wala kufanyiwa kazi, na kwa mantiki hiyo haiwezi kuikabili na kuipinga hadithi iliyothibiti ukweli na usahihi wake na iliyo mutawatiri kwa Waislamu wote, kwa hakika hadithi Thaqalain (vizito viwili) yenye lafud98

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain hi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” imepokewa katika vitabu Sahih vya Ahlus-Sunna na Musnad zao zaidi ya Sahih ishirini na tano kama anavyosema Ibn Hajar Al-Haythami, ama kauli nyingine inasema vipo vitabu Sahih thelathini na tano. Anasema Ibn Hajar Al-Haythami katika katibu chake Sawa’qul-Muhriqah, wakati alipotaja hadithi ya Swala ya Abubakr (r.a.): “Najua kwamba hadithi hiyo ni mutawatiri.”142 Kisha akasema wapokezi walikuwa wanane, akadai kuwa ni hadithi mutawatiri, kwa sababu tu imepokewa katika njia nane kama alivyodhani Ibn Hajar, pamoja na kuwa mpokezi wa Hadithi hiyo ni mtu mmoja kwa mujibu wa Ahlus-Sunna, na haikuwa yenye kukubalika baina ya Waislamu, na hali hiyo inatofautiana na Hadith Thaqalain yenye lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Hivyo ukiachilia mbali yale makubaliano ya waislamu juu ya hadithi hiyo kwa kuiandika katika vitabu vyao na Sahih zao, pia imepokewa na sahaba ishirini na tano, hivyo idadi hiyo ni mara dufu zaidi ya ile ya wapokezi wa hadithi ya swala ya Abubakr ambayo Ibnu Hajar amedai ni mutawatiri ilihali wapokezi wake kwa madai yake ni wanane tu. Kuanzia hapa inathibiti Hadith Thaqalain kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” kuwa ni mutawatiri, na hiyo ni kinyume na hadithi yenye lafudhi inayosema: “Na sunna yangu” au “Sunna ya Nabii wake (s.a.w.w.w),” kwa sababu ni katika hadithi ambazo hawajulikani wapokezi wake, hilo la kwanza. La pili: Ni miongoni mwa hadithi zilizobuniwa na Bani Umayya ili kukabiliana na hadithi inayosema: “Na kizazi changu.” Tatu: Hadithi hiyo haijatajwa katika vitabu Sahih, hakuitaja Bukhari wala Muslim katika Sahih zao na wasiokuwa hao katika sahihi zao, na hiyo inatofautiana na Hadith Thaqalain kwa lafudhi “Na kizazi changu,” 142 As-Sawa’iqul-Muhriqah uk. 21. 99

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain yenyewe imepokewa katika Sahih Muslim hadithi nne, kama ilivyotajwa katika vitabu vingine, vitabu Sahih na Musnad mbalimbali ambavyo hutegemewa, na vyote hivyo ni Sahih, bali ni mutawatiri kama tutakavyoashiria Mungu akipenda. Na hata tukikubali kuwepo hadithi hii “Nimekuachieni ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.), au na Sunna yangu” wala hakuna utata kati yake na hadithi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”, kwani Sunna ni kama vile Qur’ani inahitaji mwenye kuihifadhi na kuzuia kuchezewa na watu mfano wa akina Dk. Ali Ahmad Saaluus, na kwa ajili hiyo hapana budi wawepo watakaoihifadhi dhidi ya ziada na upungufu, na wabainishaji wa hayo ni wale ambao Mtume (s.a.w.w.) aliwaambatanisha na Qur’ani, nao ni Ahlul-Bayt wake ambao ni Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.). Kwa kuongezea hayo ni kuwa, vipi itawezekana Waislamu wote wawe walengwa wa maneno yake (s.a.w.w.): “Kenu nyinyi,” washikamane na Kitabu na Sunna, pamoja na kuwa Sunna haikuwa imeandikwa wakati yanapozungumzwa maneno hayo, bali iliandikwa baadaye. Na la kushangaza ni kuwa hata baadhi yao walizuia kuandikwa Sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ili isichanganyike na Qur’ani! Sasa vipi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) awahutubie waislamu kushikamana na kitu ambacho hakijakusanywa wala kuandikwa, bali wenye kumzushia walikuwa wengi mno mpaka akasema (s.a.w.w.): “Yeyote atakayenizushia uongo mimi basi ajichagulie mahala pake motoni.” Kwa hakika ulikuwepo upotoaji, ubadilishaji na uzuwaji katika Sunna za Mtume (s.a.w.w.), na hii ni tofauti na kitu ambacho Mwenyezi Mungu amekihifadhi dhidi ya ubadilishaji, ugeuzaji, uongezaji na upunguzaji, hivyo hayo yote yanajulisha kutosihi kwa hadithi inayosema: “Na sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.)” au “Na Sunna yangu”.

100

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Anasema Sayyid Muhammad Taqii Hakiim: “Hadithi ya kushikamana na vizito viwili kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” ni hadithi mutawatiri katika tabaka zote za wapokezi, aidha kuna vitabu lukuki ambavyo vimefurika hadithi hiyo wala havina idadi, na njia za sahaba chungu nzima, vilevile wapokezi wake ni wengi sana, halikadhalika zipo hadithi nyingi sahihi kama alivyoshuhudia hilo Al-Hakiim na wengineo. Filhali tunaona hadithi nyingine inasema: “Na Sunna yangu” ambayo imepokewa na watu wachache mno, pamoja na hivyo hushirikiana pamoja katika riwaya ya hadithi zote mbili isipokuwa Malik, yeye ameishia kuitaja moja tu, na kuiachilia mbali hadithi nyingine katika kitabu kiitwacho Muwatai, kwa hiyo yaonekana kwamba ni hadithi iliyobuniwa. Na inatosha kuthibitisha udhaifu wake kuwa, ni hadithi ambayo mlolongo wa wapokezi wake haujulikani na wala hakuna kitabu kilichoutaja, na hivyo haikosi kuwa ni hadithi ya wapokezi wachache ambayo haiwezi kusimama na kukabiliana na Hadith Thaqalain yenye tamko “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”, ambayo wapokezi wake wamekithiri katika vitabu vya Ahlus-Sunna na kukubalika wapokezi wake kuwa ni Sahih”.143 Na hayo tutayaeleza pindi tutakapotaja wale waliopokea hadithi hii kwa lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” kutoka katika vitabu sahihi vya Ahlus-Sunna na Musnad zao, ili zibainike mbinu za wale wenye kujaribu kuifanya hadithi hii kuwa ni dhaifu au kugeuza na kuwahusisha wake wa Mtume (s.a.w.w.). Baada ya kutaja hadithi “Na Sunna yangu”, huku akiwa anategemea alivyopokea Imam Malik katika kitabu chake Muwatai bila ya kueleza wapokezi na namna inavyopokelewa, pale alipopokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Nimekuachieni mambo mawili, mkishikamana nayo hamtapotea kamwe baada yangu, kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna ya Mtume wake (s.a.w.w.)” Dk. Saaluus anasema: “Hadithi hiyo tukufu haina mlolongo wa wapokeaji, isipokuwa Ibn Abdu-Barri kaiunga 143 As-Swiyaghah Al-Mantiqiyyah cha Hasan Abbas Hasan, uk 340 - 341.

101

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kwenye hadithi ya kutoka kwa Kathiir bin Abdullah bin Amru bin Auf kutoka kwa baba yake, kutoka kwa babu yake.”144 Nasema: Na ambaye anaangalia kwa makini maneno ya hadithi anayakuta yako ovyo ovyo hayana mpangilio, tena yaliyo duni, kwa hivyo haiwezekani yakawa yametoka kwa Mtume (s.a.w.w.), zaidi ya hapo ni ule udhaifu wa njia ya upokezi wake. Kwa hakika Wanachuoni wa AhlusSunna na wataalamu wao wa hadithi wameuponda mlolongo wa upokezi wake na kusema kuwa ni dhaifu, kwa hivyo husema Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya “Na Sunna yangu” ni uzushi na ni kumkadhibisha bayana Mtume (s.a.w.w.), hilo la kwanza. Pili: Lau ingekuwa hadithi hiyo ipo na imetoka kwa Mtume (s.a.w.w.), basi ingetajwa kwa njia nyingine kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) pasi na kukomea na kutajwa katika kitabu Muwaatai tu cha Imam Malik, kwa hivyo tunamkuta Dk. Saaluus alipoishiwa na hila akawa hana njia ila kuthibitisha usahihi wa hadithi “Na Sunna yangu” kwa kutegemea dalili ambazo hata mwanafunzi wa chekechea katika fani ya hadithi hawezi kuzikubali. Mara tunamwona anashikamana na yale yaliyoelezwa na Bukhari katika maneno yake, pale Bukhari aliposema katika: “Kitabu cha kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna”, na mara nyingine tunamkuta anategemea yale yaliyotoka kwa Daarimi, kama vile katika maneno yake: “Na tunakuta katika vielelezo hivi kumi usia wa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu pasi na kuitaja Sunna, hivyo ndiyo ilivyokuja katika Sunani Daarimi.”145 Nasema: Ikiwa Dk. Saaluus anaitakidi kwamba vielelezo kumi vinausia kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu pekee na halipo neno “Na Sunna yangu”, kwa nini amefanya vielelezo hivyo kuwa ndio dalili ya kusihi hadithi hiyo yenye lafudhi ya “Na Sunna yangu”? Na kwa nini 144 Hadith-Thaqalayn uk. 9.

145 Hadith-Thaqalayn uk. 10. 102

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain amepuuzia hadithi yenye lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” kama ilivyokuja katika Sunanu Daarimi Juzuu ya 2, uk. 431 na 432. Yafuatayo ni matamshi ya hadithi kama yalivyo ndani ya kitabu Sunanu Daarimi, japo Dk.. Saaluus kama ilivyo ada yake hakuitaja hadithi hiyo kwa chuki binafsi aliyonayo kwa Ahlul-Bayt (a.s.): “Ametuhadithia Jafar bin Aun: Alitueleza Abu Hayyan kutoka kwa Zayd bin Hayyan, kutoka kwa Zayd bin Arqam, amesema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alisimama na kuhutubia akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamsifu kisha akasema: “Enyi watu hakika mimi ni mtu si muda mrefu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu nami nitamuitikia na hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina uongofu na ni nuru kwenu basi shikamaneni na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na chukueni mafundisho kutoka katika hicho.” Na akaasa na kuhimiza kushikamana nacho, kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt wangu” - Mara tatu.”146 Anaambiwa Dk.. Saaluus: Hakika hadithi ambayo umeitaja kutoka kwa Imam Malik katika Muwatai, haina lafudhi ya neno “Thaqalaini” kwa hiyo haina mnasaba wowote na Mtume (s.a.w.w.) katika maneno yake (s.a.w.w.): “Ninakuachieni mambo mawili”, na wala katika hadithi hiyo hakusema (s.a.w.w.): “Ninakuachieni vizito viwili”. Hali hiyo inatofautiana na hadithi “Na kizazi changu”, kwani inajumuisha neno “Thaqalain”, bila shaka hiyo ni dalili ya dhahiri inayojulisha kwamba hadithi inayosema “Na Sunna yangu” ni hadithi iliyowekwa na Bani Umayya kisha Bani Abbas wakaisambaza ili kuikabili au kuzipinga hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zenye kuhimiza kushikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi na kizazi chake kitukufu. Na Dk.. Saaluus Mwalimu wa hadithi akazidi kujichanganya kwa kusema: “Katika kitabu cha Sunani Nasaai kuna riwaya nyingine kuhusiana na hadithi hiyo, na anasema Suyuutwi katika kitabu chake Sharh: ‘Aliusia 146 Sunan ad-Darmi Juz. 2, uk 431- 432. 103

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Kitabu cha Mwenyezi Mungu, yaani dini yake au mfano wake ili kiijumuishe Sunna.”’147 Nasema: Je huo sio ujinga wa Dk. Saaluus na ubadilishaji wa maneno kutoka mahala pake, pamoja na kuwa Suyuutwi katika kitabu chake Jaamiu Swaghiir ameitaja hadithi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” katika orodha ya hadithi Sahih kama tutakavyoligusia ishara hilo Mungu akipenda. UFISADI WA SANADI YA HADITHI “NINAKUACHIENI KITABU CHA MWENYEZI MUNGU NA SUNNA YANGU”: Imekuja katika kitabu Muwata cha Imam Malik bin Anas, Imam wa madhehebu, “Ilimfikia habari kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) amesema: ‘Ninakuachieni mambo mawili mtakaposhikamana nayo hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Nabii wake.”’148 Na riwaya hiyo kama unavyoiona haina mlolongo wa wapokezi wa hadithi, na hadithi ambayo haina mlolongo wa wapokezi wa hadithi si hoja kabisa, na hilo ni kutokana na kutokuwepo mlolongo wa wapokezi hadi tuweze tuchunguze ukweli wa wapokezi wake. Amesema Al-Hakim Niysabuuri katika kitabu chake Mustadrak: “Ametuhadithia Abu Bakr Ahmad bin Is’haaq Al-Faqiih, ameeleza Abbas bin Fadhili Isqaatwi. Ametuhadithia Isma’il bin Abi Awiis, amenieleza Isma’il bin Muhammad bin Fadhl Shaarani, amenieleza babu yangu, amenieleza Ibn Awiis, amenieleza baba yangu kutoka kwa Thauru bin Zayd Dayli, kutoka kwa Akrama, kutoka kwa Ibn Abbas kuwa: Hakika Mtume (s.a.w.w.) aliwahutubia watu katika Hija ya mwisho akasema: ‘...Enyi watu 147 Hadith-Thaqalayn uk. 10 - 25. 148 Al-Muwatau Juz. 2, uk 899. 104

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain hakika mimi ninakuachieni ambayo mtakaposhikamana nayo kamwe hamtapotea, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya nabii wake.”’149 Hadithi hiyo ni dhaifu kwa upande wa upokezi, kwa sababu ndani yake yumo Ismail bin Awiis, naye ni katika wapandikizaji wa hadithi. Anasema Ibn Hajar Al-Askalani katika kitabu chake Tahdhib: “Isma’il bin Abdullah bin Abdullah bin Awiis bin Malik... Muawiya bin Swalehe amesema kuhusu yeye: “Yeye na baba yake ni watu dhaifu...” Na akasema Ibrahim Jariil kuhusu Yahya: “Mchanganyaji, huongopa, naye sio chochote...” Na Nasaai akasema: “Ni dhaifu.” Na akasema katika mahala pengine: “Sio mkweli...”. Na Ibn Uday akasema: “Amepokea kutoka kwa mjomba wake hadithi za kiajabuajabu ambazo mwenye akili timamu hawezi kuzikubali..” Na akasema Ibn Hazam katika Muhla: “Abul Fatha Alazad amesema: ‘Amenihadithia Seif bin Muhammad kwamba Ibn Abu Awiis alikuwa akipachika hadithi...”’150 Dhahabi amemzungumzia katika Al-Miizan: “..... Ni msimulizi naye ni mbabaishaji sana.....” Nasaai amesema: “Ni mtu dhaifu”. Na akasema Daaru Qutni: “Yeye sio katika watu safi...” Akasema Ibn Uday: “Kasema Ahmad bin Abi Yahya: Nilimsikia Ibn Muiinu akisema: Yeye na baba yake ni wezi wa hadithi”. Na kasema Daulabi katika kuwazungumzia madhaifu: “Nilimsikia Nadhra bin Salamah Al-Mutuuzi akisema: Ni mwongo alikuwa akimhadithia Ibn Wahab mas’ala mbalimbali kutoka kwa Malik”. Na Aqiil akasema: “Amenihadithia Usama Daqaq, nilimsikia Yahya bin Muiinu akisema: ‘Isma’il Bin Abi Awiis hafai hata kidogo.”’150 Aidha amesema Hakim: “Ametupa habari Abubakri bin Is’haaq Al-Faqiih, amempa habari Muhammad bin Isa Ibn Sakan Al-Waasitwi, ametuhadithia Daudi bin Amru Dhabii, ametuhadithia Swalehe bin Mussa Al-Twauni 149 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 1, uk. 93. 150 Tahdhibut-Tahdhib Juz. 1, uk. 197 – 198. 151 Mizanul-Itidal Juz. 1, uk. 222 – 223. 105

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kutoka kwa Abdul-Azizi bin Rafii, kutoka kwa Abi Swaleh, kutoka kwa Abu Huraira (r.a.), amesema: “Amesema Mtume (s.a.w.w.): ‘Hakika mimi ninakuachieni vitu viwili kamwe hamtapotea baada ya hivyo: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna yangu na havitatengana mpaka virudi kwangu katika hodhi.”’152 Na hadithi hiyo vilevile ni dhaifu, kwani katika mlolongo wa wapokezi wake yupo Swalehe bin Mussa Al-Twalhi, naye ni katika waongo, anasema Ibn Hajar Al-Asqalaani: “....Kasema Ibn Muiinu: “Si chochote”. Aidha amesema tena: “Swaleh na Is’haaqa ni watoto wa Musa wote si chochote na wala haukubaliwi upokezi wao wa hadithi”. Hashim Ibn Murthad amepokea kutoka kwa Ibn Muiin amesema: “Sio mkweli”. Na Nasaai akasema: “Hadithi yake haiandikwi ni dhaifu...” Na Aqiil akasema: “Hakizingatiwi chochote katika hadithi yake...” Na Abu Nua’imu akasema: ‘Ni mwenye kuachwa na kupuuzwa kwani hueleza uzushi.”’153 Na Dhahabi amemzungumzia katika Al-Miizani: “.....Kuufiyu ni dhaifu .....” Yahya amesema: “Si chochote wala hadithi yake haiandikwi”. Na akasema Bukhari: “Hakubaliwi hadithi.” Na akasema Nasaai: “Ni mwenye kutelekezwa, kasema Abu Is’haaqa Al-Jauzu Jaani: “Ni dhaifu wa hadithi…..” Na akasema Abu Haatam. “Ni dhaifu wa hadithi...” Na amesema Ibn Uday: ‘Watu wote hawapokei chochote kutoka kwake wala hakubaliwi na yeyote.”’154 Vilevile amesema hadithi hiyo Ibn Abdubari Al-Qurtubi katika kitabu chake At-Tamhiid Limafi Muwata Minal-Maani Wal-Asaniid: “Isipokuwa katika mlolongo wa wapokezi wake yumo Kathiir bin Abdillah, naye ni miongoni mwa wabunifu wa hadithi. Dhahabi amesema: “Kathiir bin Abdillah bin Amr bin Auf...” amesema Ibn Muiinu: “Sio chochote” na amesema Shaafi’i na Abu Daudi: “Ni nguzo katika nguzo za uongo”, na 152 Al-Mustadrak Alas-Sahihayn Juz. 1, uk. 93. 153 Tahdhibut-Tahdhib Juz. 2, uk 540. 154 Mizanul-Itidal Juz. 2, uk. 302. 106

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Ahmad akaikataa hadithi, na akasema Daarul-Qutni na wengneo: “Ni mwenye kupuuzwa”. Akasema Abu Haatam: “Sio mwenye kutegemewa” na Nasaai akasema: “Sio mkweli”, na akasema Ibn Haban: “Amepokea kutoka kwa Baba yake na kutoka kwa babu yake hadithi za uongo..”. Na Ibn Uday kasema: ‘Watu wote hawapokei kutoka kwake wala hakubaliwi na yeyote.”’155 Na amesema Ibn Hajar katika wasifu wa Kathiir bin Abdillah: “.. Kasema Abu Twalib kutoka kwa Ahmed: “Babaishaji la hadithi hana maana, na akasema Abdullah bin Ahmed: Baba yangu aliitupilia mbali hadithi iliyopokewa na Kathiir bin Abdillah katika mlolongo wa wapokezi... na akasema Daarimi kutoka kwa Ibn Muiina: Hana maana. Al-Ajir amesema: Abu Daud aliulizwa kuhusu yeye, akasema: “Alikuwa ni mmoja wa waongo...” Na kasema Ibn Abi haatam: “Nilimuuliza Abu Zaraa kuhusu yeye akasema: Ni mpotoshaji wa hadithi”. Na akasema Abi Naiimu: “Ali bin Madini alimdhoofisha”. Na akasema Ibn Abdu Barri: “Kwa ujumla 156 wamekubaliana kuwa ni dhaifu...” Aidha Qadhi Ayyadhi amenukuu habari hii katika kitabu chake Al-Ilmaau Fidhabti Riwaya Wataqiyiidis-Simau ila tu kwenye mlolongo wa wapokezi wake kuna zaidi ya mmoja miongoni mwa watu ambao haukubaliki upokezi wao, kwa mfano Seif bin Umar At-Tamimu, ambaye Ibn Hajar amemwelezea katika kitabu Tahdhiib akisema: “...amesema Ibn Muiinu: “Ni mpokezi dhaifu wa hadithi,” na akasema Muurra: “Fulais ni bora kuliko yeye.” Abu Haatam amesema: “Ni mtu ambaye hakubaliki na ni mpokezi dhaifu wa hadithi....” Abu Daudi amesema: “Hana maana,” Nasaai na Daaru-Qutni wamesema: “Ni mtu dhaifu...” na Ibn Haban amesema: “Ni mpokezi wa hadithi zilizopandikizwa kwa majina ya walio madhubuti...”. Na Hakim amesema: ‘Alituhumiwa kwa upotokaji naye hazingatiwi katika upokezi wa hadithi”’157 155 Mizanul-Itidal Juz. 3, uk 406 na 407. 156 Tahdhibut-Tahdhib Juz. 4, uk 583 - 584. 157 Tahdhibut-Tahdhib Juz. 2, uk. 470. 107

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na imekuja hadithi hii katika Siiratu lbn Hisham 158 ndani ya hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) ya kuaga, na humo tunachambua mambo mawili: La kwanza: Hakika hadithi hiyo haina wapokezi, kwa hiyo hatuwezi kuukubali usahihi wake kwa kukosekana mlolongo wa wapokezi ambao huchunguzwa ukweli na uaminifu wao. La pili: Hakika Ibn Hisham ameitaja hadithi hiyo huku miongoni mwa wapokezi wake akiwemo Muhammad bin Is’haaq’ naye ni mtuhumiwa katika vitabu vya wapokezi wa hadithi kutoka kwa wataalamu wa kukosoa na kuwatambua wabunifu wa hadithi, na kuhusu yeye Dhahabi katika kitabu chake Al-Miizani amesema: “Muhammad bin Is’haaqa bin Yasar...Nasaai na wengineo wamesema: “Sio lolote ni dhaifu,” na DaaruQutni amesema: “Hachukuliwi kuwa ni hoja...” na Abu Daudi amesema: “Ni mtu wa Qadari na Muutazili,” na akasema Sulaiman Taymi: “Ni muongo,” na akasema Wahiiba: “Nilimsikia Hisham bin Arwat anasema: “Ni muongo” na akasema Wahiib: “Nilimuuliza Malik kuhusu Ibn Is’haaqa akamtuhumu”. Na akasema Abdur-Rahman bin Mahadi: “Alikuwa Yahya bin Saidi Al-Answari na Malik wakimtia kasoro Ibn Is’haaka ...” Yahya amesema: “Na la ajabu kwa Ibn Is’haaqa ni kuwa anasimulia kutoka kwa a watu wa Kitabu...” Ahmed kasema: “Yeye ni mbunifu mkubwa wa hadithi tena sana...” Yahya Qatwani amesema: “Nashuhudia kwamba Muhammad bin Is’haq ni mwongo”. Na amesema Abu Daud At-Twayalas: “Ametuhadithia rafiki yangu akasema: “Nimemsikia Ibn Is’haaqa akisema: “Ameihadithia mwaminifu”, akaulizwa ni nani? Akasema: Yakuub Myahudi...”159 Al-Uqayliy amesema katika kitabu chake katika wasifu wa Muhammad bin Is’haaqa: “Ametuhadithia Husein bin Urwat amesema: Nilimsikia Anas bin Malik akisema: “Muhammad bin Is’haaka ni mwongo...” Ametusimulia AbduIlah bin Idris amesema: “Nilikuwa kwa Malik bin 158 As-Siratun-Nabawiyyah Juz. 4, uk. 251. 159 Mizanul-Itidal Juz. 3, uk 468 - 471. 108

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Anas mtu mmoja akamwambia. Hakika Muhammad bin Is’haaqa anasema: “Nielezeni elimu ya Malik hakika mimi ni zaidi yake”, Malik akasema: ‘Mwangalieni mpotokaji miongoni mwa wapotokaji anasema: Nielezeni elimu ya Malik”’. Ametusimulia Ali, amesema: “Nilimsikia Yahya akisema: Mtu mmoja amesema kumwambia Aamashi: “Hakika Ibn Is’haaqa ametueleza kutoka kwa Ibn As’waad kutoka kwa baba yake kadha wa kadha”, basi akasema: Ibn Is’haaqa amedanganya na Ibn As’wad ameongopa...” Yahya amesema: ‘Usiamini lolote atakalokuhadithia Ibn Is’haaqa, yeye ni dhaifu na alikuwa anatuhumiwa kwa Qadar.....’ Ametuhadithia Abdul-Malik amesema: ‘Nilimsikia Yahya bin Muiinu akisema: Muhammad bin Is’haaqa ni mtu dhaifu...’160 Na hadithi hii imepokewa na Wanachuoni wengine wa Ahlus-Sunna, kama vile Bayhaqi katika As-Sunanul-Kubra, Suyuutwi katika Al-JaamiulKabiir na Muttaqil-Hindi katika Kanzul-Ummal, isipokuwa yaliyotajwa ima yawe hayana mlolongo wa wapokezi, na hivyo sio hoja, au wapokezi wake ni watu dhaifu ambao tumeshaeleza ufisadi wao. Kama vile tutakapoangalia kwa makini hadithi hiyo tunaikuta haipo katika Sahih mbili ya Bukhari na Muslim, wala haipo katika vitabu maarufu vya Ahlus-Sunna kwa mfano Sunanu Ibn Maaja, Tirmidhi, Abu Daudi na Nasaai, na wala katika Musnad Imam Ahmad, nayo ni habari ambayo wameafikiana watunzi wa vitabu Sahih, Sunan na Musnad juu ya kaiacha na kuipuuzia. Mpaka hapa imedhihiri kwetu kuwa hadithi “Na Sunna yangu” ni miongoni mwa hadithi zilizobuniwa na alizosingiziwa Bwana Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo unadhihiri ufisadi wa kila yule ambaye amejaribu kushikamana na hadithi hiyo na kuacha ile iliyothibiti usahihi wake kwa Waislamu wote.

160 Adh-Dhuafau al-Kabiir Juz. 4, uk. 24 -28.

109

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

PILI: HADITHI “NA KIZAZI CHANGU AHLUL-BAYT WANGU” KATIKA VITABU VYA AHLUS-SUNNA: Kabla hatujaziweka hadharani hadithi ambazo zimepokelewa na Wanachuoni wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, tutaashiria baadhi ya maneno ya wanachuoni wa Ahlus-Sunna ili ibainike kwamba Hadith Thaqalain kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” ni miongoni mwa hadithi sahihi Mutawatiri baina ya Waislamu. Ama majaribio na mbinu za Dk.. Ali Ahmad Saaluus katika kuifanya dhaifu hadithi hiyo, ni majaribio yaleyale ya waliomtangulia kabla yake, yaani Bani Umayya na Bani Abbasi. Ndugu yangu msomaji mpendwa! Ni juu yako kuyazingatia waliyoyasema Wanachuoni wa Ahlus-Sunna kuhusiana na Hadith Thaqalain na wala hakuna shaka kwamba watu hao wanazijua zaidi hadithi ambazo zimepokewa na Dk. Saaluus. Mmoja wa Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna Mahmuud Shukri AlAaluus anasema: “Hii hapa faida kubwa inanasibiana na maudhui hii, nayo ni kuwa, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) amesema: “Hakika mimi ninakuacheini vizito viwili, mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, kimoja ni kitukufu kuliko kingine Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu.....” Na hadithi hii imethibiti katika makundi yote mawili AhlusSunna na Shi’a, na imejulikana toka ndani ya hadithi hii kwamba, Mtume (s.a.w.w.) ameamrisha katika mambo yenye kipaumbele katika dini na hukumu za kisheria ni kushikamana na hivyo viwili vitukufu na kuvirejea katika kila jambo, basi yeyote yule atakayekwenda kinyume na hivyo katika mambo ya kisheria, itikadi na matendo huyo ni mpotevu…..”161 161Mukhtasarut-Tuhfah uk. 52. 110

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Ibn Hajar Al-Haythami katika kitabu chake Sawa’iqul-Muhriqah anasema: “Na katika hadithi sahih ni: “Hakika mimi ninakuachieni mambo mawili kamwe hamtapotea mtakapoyafuata; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu.” Twabarani ameongezea: ‘Hakika mimi nitawauliza juu ya hivyo viwili, msivitangulie mtaangamia wala msiviache mtahiliki na wala msivifundishe kwani ni vijuzi zaidi kuliko nyinyi.”’162 Hapana shaka Ibn Hajar na Aluusi ni wataalam zaidi wa kujua ukweli na usahihi wa hadithi kuliko Dk. Saaluus, hasahasa hadithi hii iliyopokewa na kuwepo katika vitabu Sahih, nacho ni kitabu cha Imam Muslim kiitwacho Sahih Muslim, kama itakavyompambanukia mpendwa msomaji hivi punde.

MUHAMMAD NASSUR-DIIN AL-ALBAANI NA HADITH THAQALAIN: Al-Albaani ameeleza Hadith Thaqalain katika kitabu chake alichokiita Silsilatul-Ahadiithi Swahihi, ameieleza chini ya namba 1761: “Enyi watu hakika mimi nakuachieni ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu.” Al-Albaani anasema: “Nilisema: Lakini hadithi ni sahihi, hakika ina ushuhuda kutoka kwenye hadithi ya Zayd bin Araam aliposema: Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alisimama mbele yetu na kuhutubia kwenye bonde la maji linaloitwa Khum, kati ya Makka na Madina, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, akawaidhi na kukumbusha, kisha akasema: “Ama baada ya hayo! Enyi watu hakika mimi ni binadamu, sio muda mrefu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu kuniita nitamuitikia, na mimi ninakuachieni vizuto viwili, kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kina uongofu wa nuru, yeyote atakayeshikamana nacho na kuchukua 162 As-Sawa’iqul-Muhriqah uk. 150. 111

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain mwongozo wake atakuwa katika uongofu. Na atakayekiacha atapotea, basi chukueni katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho,” na akaasa kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt wangu, ninawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya Ahlul-Bayt wangu, ninawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya ahali zangu, ninawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya Ahlul-Bayt wangu.” Muslim ameieleza katika Juz. 7, uk. 122 - 123, Twahaawi katika Mushkilul-Aathar Juz. 4 uk. 368, Ahmad Juz. 4 uk. 366 – 367, Ibn Abu Aswim katika kitabu As-Sunnah uk. 1550 - 1551 na Twabaraani uk. 5026 kupitia njia ya Yazid bin Hayyah Al-Tamiimiy. Kisha ameiandika Ahmad bin Hanbali Juz. 4, uk. 371, Twabaraani uk. 541, na Twahawi kwa njia ya Ali bin Rabiia, amesema: “Nilikutana na Zayd bin Arqam akiingia au kutoka kwa Mukhtar nikamwambia: Je umemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Kizazi changu?” Akasema: ‘Ndio.”’ Na mlolongo wa wapokezi wa hadithi hii ni sahihi na wapokezi wake ni watu wakweli, vilevile ina njia kadhaa wa kadhaa...” Albanii ameendelea hadi aliposema. “Kisha nikapata ushuhuda mkubwa kutoka kwenye hadithi ambayo Ali kaipokea. Ameiandika Twahaawi katika kitabu Muishkilul-Aathar Juz. uk. 307 kupatia njia ya Abi Amar AlAqdi: “Alieleza Yazid bin Kathiir kutoka kwa Muhammad bin Umar bin Ali kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ali kwa lafudhi: ‘Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho kipo mikononi mwenu na Ahlulbayt wangu...”’ Mpaka mwisho wa aliyoyasema Muhammad Nassur Diin Al-Albaani miongoni mwa ushuhuda mbalimbali kuhusiana na usahihi wa hadithi.

112

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na Albaani baada ya hayo akaongeza kusema: “Jua mpendwa msomaji ni maarufu kwamba ni miongoni mwa hadithi ambazo wanazitolea hoja Shi’a, na mara nyingi wanaitolea lahaja kadhaa wa kadhaa hata kuwafanya baadhi ya Ahlus-Sunna wadhani kuwa wao Shi’a wamepatia, ilihali wao kwa ujumla wamekosea, na ubainifu wake uko katika namna mbili: Kwanza: Hakika muradi wa hadithi katika maneno ya Mtume (s.a.w.w.): “Na kizazi changu” zaidi hutakwa na Shi’a na wala Ahlus-Sunna hawalikatai hilo, bali wao wameshikamana nalo, isipokuwa kizazi kilichotajwa hapo ni Ahlul-Bayt wake (s.a.w.w.), na kuna hadithi zimekuja katika baadhi ya njia zake kuwadhihisha hilo, kama vile hadithi iliyotarajumu na kufasiri: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”. Na katika asili Ahlul-Baiti wake ni wakeze (s.a.w.w.) akiwemo bibi Aisha aliye mkweli, kama ilivyoelezwa bayana na maneno ya Subhaanahu wa Ta’ala katika Suratul Ahzab: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na kukutoharisheni tohara ya kabisa kabisa...’” Aliendelea hadi aliposema: “Na Shi’a kuwahusisha Ahlul-Bayt katika Aya hiyo kuwa ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (radhi ya Mungu iwe juu yao) bila kuwahusisha wakeze (s.a.w.w.) ni katika upotoshaji na ubadilishaji wao wa Aya za Mwenyezi Mungu aliyetukuka ili kutetea matamanio yao kama inavyoeleweka katika upandikizaji huo. Namna ya pili: Hakika Makusudio ya “Ahlul-Bayt” si wengineo bali ni Wanachuoni wema miongoni mwao na wale wenye kushikamana na kitabu na Sunna...”163 Aliendelea hadi mwisho wa maneno yake. Nasema: Na tunayachunguza maneno ya Al-Albaani katika vipengele vifuatavyo: Mosi: Al-Albaani amekiri kusihi kwa Hadith Thaqalain kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” na kwamba ni miongoni mwa hadithi sahihi haina ihtilafu wala mzozo. 163 Silsilatul-Ahadiithi Swahihi, Mjalada wa nne uk. 355. 113

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Pili: Hakika tafsiri ya Aya za Qur’ani hapana budi ichukuliwe kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) sio kutokana na matamanio na utashi wa nafsi, chuki na ushabiki binafsi, na linalodhihiri kutoka kwa Ustadhi Muhammad Nassur Diin Al-Albaani ni miongoni mwa wale ambao wanaifasiri Qur’ani kwa utashi na kwa chuki binafsi waliyonayo kwa Shi’a, na sio kumridhisha Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala na wala sio kwa dhamira ya dini yake, kwa hakika vizazi vitakavyokuja vitamhukumu kwa upotoshaji wa maneno ya Subhaanah kutoka mahala pake, kama tulivyoashiria hayo katika mjadala wa “Ahlul-Bayt katika Aya ya Utakaso”. Huko tulithibitisha kwa dalili na nguvu ya hoja kupitia njia za Wanachuoni wa Ahlus-Sunna kuwa, na hakika Ahlul-Bayt katika Aya ya Utakaso ndio hao hao wahusika katika Aya ya Mapenzi, nao ni watu maalumu walio makhsusi, Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), basi rejea hayo katika baadhi ya utafiti huu ili ujue uzushi na upotoshaji wa Al-Albaani juu ya maneno ya Mwenyezi Mungu aliyetukuka na Sunna ya Mtume wake. Inamtosha kuwa dalili juu ya hilo yale aliyoyaeleza Imamu wa hadithi kwa Ahlus-Sunna, naye si mwingine ni Imam Muslim katika kitabu chake Sahih Muslim, pindi alipoulizwa Zayd bin Arqam: “Katika Ahlul-Bayt wake ni wakeze?” Akasema: “Hapana, Ole wako, hakika mwanamke anakuwa pamoja na mwanaume kwa muda fulani kisha anapewa talaka, anarudi kwa baba yake na walezi wake...” basi rejea hilo. Tatu: Ustaadhi Al-Albaani anaambiwa hivi: Mwenye kuzingatia maneno ya Mtume (s.a.w.w.) atajua kwamba kauachia umma wake Kitabu na Ahlulbayt na hayo yanawaelekea waislamu wote waliokuwapo wakati wa zama yaliposemwa hayo na waliofuata, inawahusu waliohudhuria na wasiokuwepo muda huo, na wala haingii akilini sisi katika zama hizi tushikamane na wake wa Mtume (s.a.w.w.) kama vile tunavyoshikamana na Qur’ani, na hilo hawezi kulisema yule mwenye akili timamu, muelewa na mwenye kutafakari, na Ustaadhi Albaani anajaribu kupotosha umma wa kiislamu kwa uzushi na upotoshaji huo ili kuwaridhisha Bani Umayya, na chuki binafsi aliyonayo kwa ndugu wa Mtume (s.a.w.w.). 114

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nne: Na ama kuhusu maneno ya Albaani aliyosema “Na Ahlul Bayt wake kwa asili ni wakeze, kama ilivyo sahihi katika maneno yake Subhaanahu wa Ta’ala katika Surat-Ahzab: ‘Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni...’” bila shaka tayari tumeshaijadili hapo kabla na tumebainisha ufisadi na uovu wa maoni yake kwa dalili kutoka katika vitabu vya Ahlu- Sunna, basi rejea. Kisha tafsri ya Ustaadhi Albaani ya Aya ya Utakaso mara kuwa ni wake wa Mtume (s.a.w.w.), na mara nyingine ni Ahlul-Bayt, ni dalili ya kutokuwa makini katika kufasiri kwake, na kwamba yeye anatafsiri kutokana na maoni yake, matamanio na matakwa yake binafsi, na ikiwa muradi wa Ahlul-Bayt katika Hadith Thaqalain ni Wanachuoni wa Ahlul-Bayti kama anavyodai basi ni kwa nini hashikamani nao, achukue maelekezo kutoka kwao, na awarejee wao katika itikadi zake na hukumu zake? Je! Imam Ali sio miongoni mwa maulamaa wa Ahlul-Bayt (a.s.), vivyo hivyo Imam Hasan, Imam Husein, Imam Ali bin Husein, Imam Muhammad Al-Baqir, Imam Swadiq na wengineo waliobakia katika Wanachuoni wa Ahlul-Bayt kama anavyodai. Je hawa sio ndio Wanachuoni wa Ahlul-Bayt, au Wanachuoni wa Ahlul-Bayt ni Abu Hanifa, Shafii, Maliki na Ahmad bin Hanbali? Basi kitu gani anajibu Ustaadhi Albaani, na kwa nini tunamuona amechukua kutoka kwa watu hao wanne na kuacha kushikamana na Wanachuoni wa Ahlul-Bayt (a.s.), au hao tuliowataja sio katika Wanachuoni wa Ahlul-Bayt kwa maoni ya Ustadhi Albaani, na Mtume (s.a.w.w.) amesema katika haki ya Maimam wawili Hasan na Husein (a.s.): “Hawa ni maimamu wawili wakiwa wamesimama au wamekaa,” hivyo ndivyo tunavyomkuta Ustaadh Albaani anabadilisha maneno kutoka mahala pake. Baada ya mahojiano hayo na Albaani tunataja kundi la Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao ambao wameeleza Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”, na kuwa makusudio ya “Ahlul-Bayt” ni Ali, Fatimah, Hasan, na Husein (a.s.).

115

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 1. SAHIHI MUSLIM Ama Imam Muslim ametaja hadithi nne zinazohusiana na hadithi hii tukufu, nasi tunaithibitisha kama ilivyokuja katika Sahih yake katika mlango wa fadhila za Imam Ali bin Abi Twalib, ili aone yule ambaye anajaribu kukanusha mfano wa hadithi hizi ambazo zipo katika vitabu vya AhlusSunna, na hadithi zenyewe ni hizi: Hadithi ya kwanza: Kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Siku moja Mjumbe wa Mungu (s.a.w.w.) alisimama na kuhutubia sehemu inayoitwa Khum baina ya Makka na Madina; basi akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu akatoa mawaidha kukumbusha kisha akasema: “Ama baada, Enyi watu hakika mimi ni mwanadamu karibu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu kuniita na nitaitikia, na mimi ninakuachieni vizito viwili, kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna nuru na uongofu, basi mshikamane nacho” akawaasa kushikamana nacho kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt, ninawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya Ahlulbayt wangu,” Haswiin akamuuliza: “Ni nani hao Ahlul-Bayt wake?” Akasema: “Wanawake ni miongoni mwa Ahlul-Bayt wake lakini Ahlul-Bayt wake ni wale ambao wameharamishiwa sadaka baada yake”, akasema: “Ni nani hao?” Akasema: “Familia ya Ali, Familia ya Aqiil, Familia ya Jaafar na familia ya Abbas”, akasema: ‘Wote hao wameharamishiwa sadaka...”’164 Hadithi ya pili: Kutoka kwa Zayd bin Arqam amepokea kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Na hakika mimi ninakuachieni vizito viwili kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza wajalla, nayo ni kamba ya Mwenyezi Mungu, mwenye kukifuata atakuwa katika uongofu na mwenye kukiacha atakuwa katika upotevu...” basi tukasema: “Je! wakeze ni katika Ahlul-Bayt wake?” Akasema ‘La hasha, hakika mwanamke anakuwa pamoja na mwanaume muda fulani katika zama kisha anapewa talaka basi anarejea kwa baba yake na watu wake, Ahlul-Bayt wake ni wale 164 Sahih Muslim Juz. 4, uk. 1873. 116

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain asili yake na wa damu yake ambao wameharamishiwa sadaka baada yake.”’ 165 Aidha amepokea Imam Muslim katika Sahih yake kutoka kwa Amr bin Saad bin Abi Waqqas kutoka kwa babu yake amesema: “Muawiya bin Abi Sufyan alimwamrisha Saad kwa kusema: “Kipi kinakuzuia kumtukana baba wa mchanga - yaani Ali” akasema: “Ama nikikumbuka mambo matatu aliyoambiwa na Mtume (s.a.w.w.) siwezi kumtukana ....” Aliendelea hadi aliposema: “Na pindi ilipoteremshwa Aya hii: “Basi sema njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu...” Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatimah, Hasan na Husein na akasema ‘Ewe Mola Wangu hawa ndio Ahli zangu”’.166 Nasema: Na yakuzingatia juu ya hilo ni: 1. Tafsiri ya Ahlul-Bayt haikuwa ya Mtume (s.a.w.w.) bali ni nyongeza ya mpokezi wa hadithi, na katika hadithi ya pili amekanusha tena kwa kuapa kuwa wake wa Mtume (s.a.w.w.) sio katika Ahlul-Bayt, na katika hadithi ya kwanza kuna mkorogo katika maana ya Ahlul-Bayt, na kitendo cha kuwaingiza wake wa Mtume (s.a.w.w.) katika wao “Ahlul-Bayt” ni kutafsiri Qur’ani kwa maoni binafsi bila ya dalili, bali ukweli ni kinyume na hivyo, kwani makusudio ya Ahlul-Bayt ni wale watu waliofunikwa kishamiya, na humo hakuingia pamoja nao muingiaji yeyote, na hivyo ni kufuatana na yale yaliyopokewa na kuwepo katika Sahih Muslim, katika maneno ya Bwana Mtume (s.a.w.w.) kwamba Ahlul-Bayt ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). 2. Hakika Hadith Thaqalain yenye lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” imethibiti katika pande zote mbili Sunni na Shi’a, na kwa hivyo yaliyopo katika vitabu vya Ahlus-Sunna kati ya hadithi zinazofungamana na hadithi “Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt” zinatilia mkazo 165 Sahih Muslim Juz. 4 uk. 1874. 166 Sahih Muslim Juz. 4 uk. 1871. 117

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain usahihi wake na hata ikiwa zimepokewa kwa lafudhi mbalimbali, kwani hadithi hata kama ikiwa dhaifu katika dhati yake, lakini hadithi sahih zikashuhudia usahihi wa maana yake, basi huwa ni hoja yenye kufuatwa. Na tayari kwa hakika kabisa hadithi sahihi zimetoa ushuhuda juu ya usahihi wa Hadith Thaqalain, basi unathibiti usahihi wake kutokana na hadithi zilizopokewa katika vitabu vinginevyo miongoni mwa vitabu vya AhlusSunna na hata kama ikiwa ni dhaifu katika dhati yake. Hiyo ni ili iwe hoja juu ya yule ambaye anakanusha mfano wa hadithi hizo na kusema kwamba hazipo katika vitabu vya Ahlus-Sunna. 2. MUSNAD CHA IMAM AHMAD BIN HANBALI: Imam Ahmad ametaja hadithi nyingi katika Musnad yake za Hadithi Thaqaalaini kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlulbayt wangu”, nayo inaafikiana na yale aliyoyapokea Imam Muslim katika Sahih yake. Miongoni mwa hayo ni: i) Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Siku moja Bwana Mtume (s.a.w.w.) alisimama mbele yetu na kuhutubia mahala palipo na maji panapoitwa Khum kati ya Makka na Madina, akamhimidi Mwenyezi Mungu swt. na akamsifu kwa sifa zake, akatoa mawaidha na... akakumbusha, kisha akasema: “Ama baada: Enyi watu hakika mimi ni binadamu si muda mrefu nitajiwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Subhaanahu kuniita nami nitaitikia; hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu aliyetukuka, ndani yake kuna uongofu na nuru, basi chukueni mafunzo katika Kitabu cha Mungu Mtukufu na mshikamane nacho,” na akaasa juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisha akasema: “Na Kizazi changu Ahlul-Bayt wangu ninawakumbusheni Mwenyezi Mungu Ahlul-Bayt wangu ninawakumbusha Mwenyezi Mungu Ahlul-Bayt wangu.” Haswin akamuuliza ni nani hao Ahlul-Bayt wake ewe Zayd, Je! wanawake wake ni miongoni mwa Ahlul-Bayt wake? Akasema: “Hakika wanawake wake ni Ahlul-Bayt wake, lakini Ahlul-Bayt wake hasa ni wale walioharamishiwa sadaka baada yake” akasema: “Ni nani hao?” 118

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Akasema: “Ni familia ya Ali, Familia ya Aqiil, familia ya Jaffar na familia ya Abbas.”’167 ii) Na imepokewa kutoka kwa Abi Said Al-Khudri kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika nitaitwa si muda mrefu nami nitaitikia, na hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza wajalla, na kizazi changu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, Mwenyezi Mungu Mwenye utukufu na Mwenye habari amenipa habari kuwa havitaachana kamwe mpaka vije kwangu katika hodhi, basi angalieni mtanifuataje katika hivyo.”168 iii) Imepokewa kutoka kwa Abuu Said amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili kimoja ni kikubwa zaidi kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu na hivyo viwili havitaachana kamwe hadi virudi kwangu katika hodhi.”’169 iv) Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Thabit amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili kimoja ni kikubwa zaidi ya kingine Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza-wajalla ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu kwa hakika hivyo viwili havitaachana hadi virudi kwangu katika hodhi.”’170 v) Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Thabit amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nakuachieni makhalifa wawili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ni kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi au kati 167 Musnad Ahmad Juz.4, uk. 366 - 367. 168 Musnad Ahmad Juz. 2, uk. 17. 169 Musnad Ahmad Juz. 3, uk. 14. 170 Musnad Ahmad Juz. 3, uk. 26. 119

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain ya mbingu na ardhi, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, na hivyo viwili havitaachana kamwe hadi virudi kwangu katika hodhi.”’171 vi) Kwa njia nyingine imepokelewa kutoka kwa Zayd bin Thabit amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nakuachieni makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu na hivyo viwili havitaachana kamwe hadi virudi vyote kwangu katika hodhi.”’172 vii) Na imepokewa kutoka kwa Ali bin Rabiya amesema: “Nilikutana na Zayd bin Arqam akiingia au akitoka kwa Mukhtar, nikamwambia: “Je! Umemsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema: Hakika mimi nawachia vizito viwili?” Akasema: ‘Ndio.”’173 JALIZO: Dk. Ali Ahmad Saaluus anasema: “Hadith Thaqalain ambazo zimepokewa na maimam wawili Muslim na Ahmad kutoka kwa Zayd bin Arqam, zinajulisha juu ya wajibu wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni Qur’ani Tukufu ambayo imetuamrisha tuchukue Sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w.), basi hadithi hizo bila shaka zinaafikiana na hadithi ambazo zinatutaka tushikamane na Kitabu na Sunna”. UPEMBUZI YAKINIFU JUU YA HAYO: 1. Hakika Dk.. Ali Ahmad Saaluus anajaribu kuwachanganya wasomaji kuhusu uzushi huu juu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.), na hilo ni katika maneno yake: “...nazo zinajulisha juu ya wajibu wa kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu aliyetukuka,” ilihali ukweli ni kuwa hadithi za Imamu Muslim na Imamu Ahmad zinatuasa na kutuhimiza juu ya kushikamana na vizito viwili “Kitabu cha Mwenyezi Mungu na 171 Musnad Ahmad Juz. uk. 181 -182. 172 Musnad Ahmad Juz. 5, uk.179-190. 173 Musnad Ahmad Juz. 4, uk. 371.

120

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Ahlulbayt”. Lakini yeye Dk.. Ali Ahmad Saaluus amewaweka kando Ahlul-Bayt kutokana na hadithi hiyo, akakomea kutaja Kitabu cha Mwenyezi Mungu tu ili ailiwadhe nafsi yake dhidi ya uchovu, mashaka na chuki aliyonayo kwa Ahlul-Bayt (a.s.), kwa sababu hawezi kusema: Kushikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kushikanana na wake wa Mtume (s.a.w.w.), hivyo akawaondoa Ahlulbayt kutoka kwenye hadithi, ili aiepushe nafsi yake na mushkeli, kwani katika dhati ya nafsi yake anaitikadi kuwa Ahlul-Bayt ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.). 2. Ama maneno yake: “Wamepokea maimam wawili Muslim na Ahmad kutoka kwa Zayd bin Arqam” na huo pia ni ubalilishaji wa maneno kutoka katika mahala pake, kwani Imam Ahmad amepokea Hadith Thaqalain katika Musnad yake mara kutoka kwa Zayd bin Arqam na mara nyingine kutoka kwa Abu Said Khudri, aidha kutoka kwa Zayd bin Thabit, basi hivyo ndivyo anavyojaribu Saaluus kupotosha Sunna ya Mtume (s.a.w.w.). 3. Na ama maneno yake: “Hadithi hizo zinaafikiana pamoja na hadithi ambayo inatuita na kututaka kushikamana na Kitabu na Sunna”, huo ni uzushi kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w.) na upotoshaji wa Sunna ya Nabii (s.a.w.w.), basi hadithi ambazo zimepokewa na maimam wawili Muslim na Ahmad zote hizo zinatuhimiza kushikamana na vizito viwili, Kitabu na Ahlul-Bayt, na haipo harufu hata kidogo ya neno “Sunna”. Hivyo ndivyo wanavyojaribu watu hao kupotosha maneno ya Mwenyezi Mungu ili kuwachanganya waislamu, na kuwaweka mbali na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.). AL-JAAMIUS-SWIHAH CHA TIRMIDHI: Amepokea Tirmidhi katika kitabu chake Jamius-Swihaah, katika fadhila za Ahlul-Bayt kutoka kwa Jaabir bin Abdillah amesema: “Nilimuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wakati wa hija siku ya Arafa juu ya kikalio cha ngamia akihutubia, basi nilimsikia akisema: ‘Enyi watu! Hakika mimi nakuachieni ambavyo mtakaposhikamana navyo hamtapotea kamwe, 121

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu’ Amesema: Na katika mlango mwingine kuna hadithi kutoka kwa Abu Dharr, Abu Said Zayd bin Arqam na Hudhaif bin Asiid...”174 Aidha imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika nakuachieni ambavyo mtakaposhikama navyo hamtapotea kamwe baada yangu kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni mpaka ardhini na kizazi changu Ahlulbayt wangu, na havitatengana mpaka virudi kwangu katika hodhi, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo.”’175 4. AL-JAAMIUS-SWAGHIIR CHA HAFIDH SUYUUTWI: Na imekuja katika Jaamius-Swaghiir katika hadithi sahihi nayo ni hadithi nambari 1608: “Ama baada ya hayo, enyi watu, hakika mimi ni binadamu anakaribia kuja mjumbe wa Mola Wangu kuniita nami nitaitikia, kwa hakika nawaachia vizito viwili, kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna nuru na uongofu, yeyote atakayeshikamana nacho na kukitendea kazi atakuwa katika uongofu na mwenye kukiacha atapotea, basi kifanyieni kazi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtakatifu, na mshikamane nacho, na Ahlul-Bayt wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Bayt wangu.”176 Aidha katika Jaamiul-Swaghiir cha Suyuutwi hadithi nambari 2631 amesema (s.a.w.w.): “Hakika mimi nawaachia vitu viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, na hivyo havitatengana mpaka virudi kwangu katika hodhi.”177 174 Al-Jamius-Sihah, Juz. 5, uk. 621. 175 Al-Jamius-Sihah, Juz. 5, uk. 622. 176 Al-Jaamius-Swaghiir Juz. 2, uk. 174 – 175.

177 Al-Jaamius-Swaghiir Juz. 3, uk. 14. 122

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain FAIDHUL-QADIIR CHA ALLAMA AL-MUNAWI: Anasema Allama Munawi: “Katika sifa na daraja kupita wote, kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: Mtume (s.a.w.w.) alisimama akahutubia sehemu ya maji inayoitwa Khum baina ya Makka na Madina, akamhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumsifu, akatoa waadhi na kukumbusha, kisha akasema: ‘Ama baada..”’ akaitaja Hadithi. Kisha akasema: Na imeelezwa na Muslim kwa njia tofauti, moja ya lafudhi yake ni: “Zayd aliambiwa: “Je! wanawake na wake sio miongoni mwa Ahlul-Bayt wake?” Akasema: ‘Wanawake sio katika Ahlul-Bayt wake, lakini Ahlul-Bayt wake ni wale ambao wameharamishiwa sadaka baada yake”’. Na katika hadithi nyingine: “Hakika mwanamke anakuwa pamoja na mwanamme muda fulani, kisha anapewa talaka basi hurudi kwa baba yake na watu wake, Ahlul-Bayt wake kwa hakika ni wale wanahusiana naye na katika damu yake ambao wameharamishiwa sadaka”.178 Nasema: Hayo yote ni dalili ya wazi katika kuonyesha ufisadi na uovu wa yule anayedhani kuwa wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) ni katika AhlulBayt wake (s.a.w.w.), kama asemavyo Ustaadh Muhammad Nassur Diin Albaani: “Na Ahlul-Bayt wake kwa hakika ni wakeze (s.a.w.w.) na kati yao ni Aisha (r.a.) aliye mkweli” na huko ni kumzushia Mtume (s.a.w.w.) kama ilivyoelezwa hapo kabla na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna. Aidha anasema Allama Munawi: ‘“Hakika mimi ninakuachieni baada kifo changu mambo mawili” na akaongeza katika hadithi, “kimoja kikubwa zaidi kuliko kingine,” na katika hadithi nyingine badala mambo mawili “vizito viwili”.179 Ameviita kwa jina hilo kutokana

ya ni ya na

178 Faydhul-Qadiir Juz. 2, uk. 175. 179 Nasema: Kauli yake “Makhalifa wawili” iliyopo kwenye baadhi ya riwaya inafasiri makusudio ya Ahlul-baiti, kwa sababu haiwezekani mwanamke au mke wa Mtume (s.a.w.w.) kuwa Khalifa juu ya waisilamu baada ya kifo chake (s.a.w.w.). Na hii pia ni dalili tosha kuthibitisha kuwa muradi wa Ahlul-baiti si wakeze Mtume (s.a.w.w.). Na ukishataja wake za Mtume, ya nini tena kusema, “akiwemo Aisha?” – Mhariri. 123

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain uzito wa utukufu wake, “Kitabu” ni Qur’ani “Kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi”...... “Na kizazi changu” ni mwenza wake, na “AhlulBayt” ni upambanuzi baada ya kutokuwa imeshachanganuliwa kinagaubaga na kibayana, nao ni watu wa kishamiya ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatoharisha tohara ya kabisa kabisa, na inasemekana kuwa ni wale ambao wameharamishiwa Zaka. Yaani mkifuata amri za kitabu chake na kukatazika makatazo yake mtaongoka kwa uongofu wa kizazi changu na uongofu wa nyendo zao hamtapotea. Qurtubi amesema: “Usia huu na msisitizo mkubwa huo unapelekea wajibu wa kuwaheshimu ndugu zake... na hilo linakwenda pamoja na kujua mambo makhsusi waliyonayo kwa Mtume (s.a.w.w.), na kwamba wao ni kiungo kutokana naye, nao ni msingi ambao ameuanzisha na matawi yake yakapatikana kutokana na yeye, kama alivyosema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu”, pamoja na hivyo Bani Umayya wakapinga - na miongoni mwao ni Aamir Najjar, Muhammad Nassor bin Albaani, Ali Ahmad Saaluus, Ihsaan Dhahiir na wengineo - haki hizo kubwa kwa kuziacha na kuzivunja, basi wakamwaga damu za Ahlul-Bayt, wakawapora wanawake wao, wakawatesa watoto wao, wakawatoa majumbani mwao, wakakanusha utukufu wao na fadhila zao, wakahalalisha kuwatukana na kuwalaani, basi wakamkhalifu Mtume (s.a.w.w.) katika wasia wake, wakakabiliana na kukusudia kuupotosha ukweli, fedheha iliyoje watakaposimamishwa mbele yake. “Na hivyo viwili”.... Na katika hadithi nyingine: ‘Hakika Mwenyezi Mungu mwenye lutfi amenipa habari kuwa hivyo viwili “havitatengana kamwe”, yaani Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi chake, yaani vitaendelea kuwa pamoja ‘hadi virudi kwangu katika hodhi”’. Allama Munawi anasema katika tanbihi: “Amesema Shariif: “Habari hizo zinafahamisha kuwepo kwa yule ambaye inastahiki kushikamana naye miongoni mwa Ahlul-Bayt na kizazi kitakatifu, katika kila zama mpaka Kiyama kitakaposimama, ndio maana msisitizo huu uliotajwa ukaelekeza kushikamana naye kama vile ilivyo kwa Qur’ani, kwa hivyo walikuwa ni 124

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain amana kwa watu wa ardhini, watakapotoweka wao basi watatoweka watu wa ardhini.” Haythami amesema: “Wapokezi wake ni waaminifu, aidha ameipokea hiyo Abu Yaali kwa mlolongo wa wapokezi, hakuna taabu juu ya hilo. Na Hafidh bin Abdul-Azizi bin Akhdhar ameongeza kuwa, hakika yeye alisema hayo katika Hijja ya kuaga. Na akadhania yule aliyedhania kuwa imezushwa kama vile Ibn Jauzi, amesema Samuhudi: ‘Katika mlango kuna hadithi zinazozidi ishirini kutoka kwa sahaba.”’180 Nasema: Haistaajabishi kusema kuwepo uzushi kwenye kila ambalo linalofungamana na watu wa kishamia, Ali, Fatima, Hasan na Husein katika hadithi, kwani ni kwa namna hiyo amejaribu Ibn Jauzi na wengineo miongoni mwa Bani Umayya na Bani Abbas kuzifanya dhaifu hadithi hizo, kwa malengo ya chuki binafsi, matamanio ya kijahili na itikadi yao.

AL-KHASWAIS CHA NISAAI, MMOJA WA WATUNZI WA VITABU SAHIH SITA: Na katika hadithi Sahih iliyopokewa na Zayd bin Arqam Amesema: “Pindi alipomaliza Mtume (s.a.w.w.) Hijja ya kuaga alifika Ghadiir-Khum, aliamrisha watengeneze jukwaa, baada ya kutengenezwa akasema: “Kana kwamba nitaitwa na nitaitikia wito, hakika mimi nawaachia vizito viwili, kimoja ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, basi angalieni mtanifuataje katika hivyo, hakika hivyo havitatengana kamwe hadi virudi kwangu katika hodhi.” Kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu ni msimamizi wa mambo yangu na mimi ni msimamizi wa kila muumini,” kisha akakamata mkono wa Ali (r.a.) hapo akasema: “Yeyote yule ambaye mimi nilikuwa mtawalia wa mambo yake, basi na huyu ni kiongozi wake, ewe Mola Wangu mtawalishe mwenye kumtawalisha yeye na mfanye adui anayemfanyia uadui yeye.” 180 Faydhul-Qadiir, Juz. 3, uk. 14 - 15. 125

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Nikasema kumwambia Zayd: “Ulimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema hayo?” Akasema: ‘Ndio, hakika yeye alisimama juu ya vikalio vya ngamia alionekana na kusikika na kila mmoja”’.181 Nasema: Na hiyo ni katika dalili za wazi kuthibitisha kuwa makusudio ya Ahlul-Bayt katika Hadith Thaqalain ni watu wa kishamiya (a.s.). 7. AL-MANAAQIB CHA IBN MAGHAZILI SHAFII: 1. Imekuja katika hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) siku ya Ghadiir-Khum kama alivyoipokea Ibn Maghazili, maneno ya Mtume (s.a.w.w.): “...Hakika mimi nitatangulia nanyi mtanifuata, mtakaporejea kwangu katika hodhi, nitakuulizeni kuhusiana na vizito viwili vipi mlinifuata katika hivyo,” Akasema: “Chungeni sana juu ya vizito viwili,” hapo akasimama mtu mmoja miongoni mwa Muhajiriina akasema: “Kwa haki ya baba na mama yangu, ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu ni vipi hivyo vizito viwili?” Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kikubwa zaidi ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ncha moja iko mikonini mwa Mwenyezi Mungu na ncha nyingine iko mikononi mwenu, basi mshikamane nacho wala hamtapotea, na kidogo kati ya hivyo ni kizazi changu, yeyote mwenye kuelekea kibla changu akaitikia mwito wangu msiwauwe, msiwatweze, wala msiwaache, hakika mimi nimemwomba hao Mwenyezi Mungu Mpole, Mwenye habari na akanipa, mwenye kuwanusuru nitamnusuru, mwenye kuwadhalilisha hao amenidhalilisha mimi, mwenye kuwatawalisha hao amenitawalisha mimi, mwenye kuwafanyia uadui amenifanyia mimi...” Kisha akakamata mkono wa Ali bin Abi Twalib (a.s.) akaunyanyua juu kisha akasema: “Yeyote yule ambaye mimi ni mtawalia wa mambo yake basi na huyu ni mtawalia wa mambo yake, na ambaye mimi nilikuwa walii wake basi na huyu ni walii wake. Ewe Mola Wangu mpende mwenye kumpenda huyu, na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui yeye,” alisema hayo mara tatu”.182 181 Al-Khaswais, uk. 70. 182 al-Manaqib, uk. 30 – 31. 126

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 2. Ameeleza Ibn Maghazili kutoka kwa Amirul Muuminiina siku ya maapizo kutokana na maneno yake (a.s.): “... akasema: Nakuapizeni kwa Mwenyezi Mungu na nakukumbusheni Mwenyezi Mungu Je! M n a j u a kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehma na amani ziwe juu yake) amesema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, kamwe havitaachana mpaka virudi kwangu katika hodhi? ” Wakasema: “Ndio.” Akasema: “Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu Je! Yupo mmoja kati yenu ameshushiwa na Mwenyezi Mungu Aya ya Utakaso ikamuhusu, kama anavyosema: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu Ahlul-Bayt na awatoharishe tohara ya kabisa kabisa” asiyekuwa mimi?” Wakasema: “Allahumma la hasha isipokuwa wewe.”183 3. Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu na hivyo viwili havitatengana mpaka virudi kwangu katika hodhi.”’184 4. Imepokewa kutoka kwa Abu Said Khudri amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Karibu nitaitwa nami nitaitikia, na hakika mimi ninawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azzawajalla na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, basi angalieni mtanifuataje katika hivyo.”’185 5. Kutoka kwa Abu Said Khudri kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi nitaitwa muda sio mrefu nami nitaitikia, na mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini na kizazi changu AhlulBayt, na Mwenyezi Mungu mwenye habari amenipa habari kwamba hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi, basi 183 al-Manaqib, uk. 91.

184 al-Manaqib, uk. 156. 185 al-Manaqib, uk. 156. 127

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain angalieni vipi mtanifuata katika hivyo.”186 6. Kutoka kwa Yazid bin Hayyan amesema: “Nilimsikia Zayd bin Arqam anasema: Siku moja Bwana Mtume (s.a.w.w.) alisimama mbele yetu na akahutubia akasema: “Ama baada ya hayo, Enyi watu, mimi ni binadamu hivi karibuni nitaitwa nami nitaitikia, hakika mimi nawaachia vizito viwili, navyo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna uongofu na nuru basi chukueni yaliyomo katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nayo,” na akaasa na kuhimiza juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt wangu nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Bayt wangu,” aliyesema hayo mara tatu”.187

DHAKHAIRUL-UQBA CHA HAFIDH MUHIBBUDIIN AT-TWABARI: Hafidh Muhibbu Diin Twabari anasema: “Mlango wa Fadhila za AhlulBayt na msisitizo wa kushikamana nao pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza-Wajalla, imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi ninawachieni vizito viwili, mkishikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu, kimoja ni kitukufu zaidi ya kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza-Wajalla, nayo ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi Ardhini, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, kamwe havitatengana mpaka virudi kwangu kwenye hodhi, basi angalieni mtanifuataje katika hivyo.”’188

9. SUNANUD-DAARMI: Amepokea Daarmi katika Sunan yake kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alisimama na kuhutubia, akamhimidi 186 Al-Manaqib, uk. 154. 187 Al-Manaqib, uk. 157. 188. Dhakhairul-Uqba, uk. 16. 128

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mwenyezi Mungu na kumsifu kisha akasema: “Enyi watu mimi ni binadamu, muda sio mrefu nitaitwa na mjumbe wa Mola Wangu nami nitamwitikia, na hakika mimi ninawaachia vizito viwili kimoja ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kina uongofu na nuru, basi shikamaneni na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mkitendee kazi,” akasisitiza na kuhamasisha kukifuata kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt wangu nawakumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya Ahlul-Bayt wangu.” alisema hayo mara tatu”.189 Nasema: Na ambalo linajulisha kuwa Hadith Thaqalain ni mutawatiri kwa lafudhi “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” ni kuwa hata Daarmi ameiandika katika Sunan yake, kwani ni mashuhuri kwamba Daarmi huwa haandiki wala hapokei fadhila za Ahlul-Bayt (a.s.), lakini hata hivyo ameieleza na kuiandika Hadith Thaqalain katika Sunan yake, na hilo linajulisha kuwa ni mutawatiri isiyowezekana kukanushwa.

10. IS’AAFUR-RAAGHIBIIN CHA IBN SWABAAN: Kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alisimama na kuhutubia, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu kisha akasema: “Enyi watu, hakika mimi ni binadamu mfano wenu, muda sio mrefu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu Azza Wajalla, yaani mauti, nami nitaitikia na hakika mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho kina uongofu na nuru basi shikamaneni na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza Wajalla na kitendeeni kazi, na Ahlul-Bayt wangu ...” Na katika hadithi nyingine: ‘Hakika mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.”’190 Na katika hadithi ya Imam Ahmad bin Hanbali amesema: “Hakika mimi muda sio mrefu nitaitwa nami nitaitikia, hakika mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nayo ni kamba iliyonyooka kutoka ardhini hadi mbinguni, na kizazi changu Ahlul-bat wangu, hakika 189. Sunanid-Darmiy Juz. 2, uk. 431- 432. 190. Is'afur-Raghibiin, uk. 119. 129

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain mwenyezi Mungu mpole mwenye habari amenihabarisha kuwa hivyo viwili havitatengana kamwe mpaka virudi kwangu kwenye hodhi siku ya Kiyama, basi angalieni mtanifuataje katika hivyo.” Na katika hadithi nyingine: ‘Hodhi yangu kati ya Basra na Swanaa idadi ya vyombo vyake ni idadi ya nyota, hakika Mwenyezi Mungu atakuulizeni namna gani mlinifuata Katika kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu.”’191

11. ANSAABUL-ASHRAAF CHA BALADHURI: Amepokea Baladhuri kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.w.) katika Hija ya muago, na pindi tulipofika Ghadir-Khum akaamrisha litengenezwe jukwaa kutokana na matandiko ya juu ya ngamia, ilipokamilika akasimama na kusema: “Kana kwamba nimeitwa nami nimeitikia, na hakika Mwenyezi Mungu ni mtawaliwa wa mambo yangu nami ni mtawalia wa kila muumini, na mimi ninawaachia ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi,” kisha akaukamata mkono wa Ali, akasema: ‘Ambaye nilikuwa mimi ni mtawalia wa mambo yake basi na huyu ni mtawalia wa mambo yake, ewe Mola Wangu, mtawalishe mwenye kumtawalisha yeye na mfanye adui mwenye kumfanyia uadui.”’192 12. SHARHUT-TWAHAAWIYAH FIL-AQIIDATIS-SALAFIYAH CHA IBN ABDUL-AZZI: Anasema Ibn Abdul-Azzi katika sherehe yake ya Twahawiya Fil-AqiidatisSalafiyah: “Na katika Sahih Muslim kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: Mtume (s.a.w.w.) alisimama mbele yetu akahutubia sehemu ya maji inayoitwa Khum baina ya Makka na Madina akasema: “Amma baada ya 191 Is'afur-Raghibiin, uk. 119 192. Ansabul-Ashraf, uk. 110 - 111. 130

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain hayo, Enyi watu, hakika mimi ni binadamu, muda sio mrefu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu kuniita nami nitamwitikia Mola Wangu, na hakika mimi nawachia vizito viwili, kimoja wapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kina uongofu na nuru ndani yake, basi kitendeeni kazi Kitabu cha Mwenyezi Mungu na mshikamane nacho.” Basi akasisitiza na kuasa juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu ili kufanya watu wakipende, kisha akasema: “Na Ahlul-Bayt wangu, nawakumbusha Mwenyezi Mungu katika AhlulBayt wangu.” Na ameeleza Bukhari kutoka kwa Abu Bakr (r.a.) amesema: ‘Mfuateni kwa makini Muhammad katika Ahlul-Bayt wake.”’193 Ibn Abdul-Izza anasema katika Sherehe ya Twahaawiya Fil-AqiidatisSalafiyyah: “Pindi Aya hii ilipoteremshwa: “Basi sema njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu nafsi zetu na nafsi zenu.” Mtume (s.a.w.w.) aliwaita Ali, Fatimah, Hasan na Husein akasema: ‘Hawa ndio Ahli zangu.”’194 13. HILYATUL-AWLIYAAI CHA ABI NA’IM ISFAHAAN: Amepokea Abu Na’im katika Hilyatul-Awliyaai kutoka kwa Abu Tufa’l Aamir bin Waathilah kutoka kwa Huzaifah bin Asiid Ghaffar amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Enyi watu mimi nitawatangulia na hakika mtakuja kwangu kwenye hodhi, na bila shaka nitawauliza mtakapokuja kwangu kuhusiana na vizito viwili, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo, kizito kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, ncha moja iko mikononi mwake na ncha nyingine iko mikononi mwenu, basi shikamaneni nacho msipotee wala msibadilike, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika mwenye upole na mwenye habari ameniambia kuwa hivyo viwili havitaachana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.”’195

193. Sharhut-Twahaawiyah Fil-Aqiidatis-Salafiyyah, uk. 332. 194 Sharhut-Twahaawiyah Fil-Aqiidatis-Salafiyyah uk 328. 195 Hilyatul-Awliyaai, Juz. 1, uk. 355. 131

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na amepokea Abu Na’im kutoka kwa Imam Shafii amesema: “Ametupa habari Abdullah bin Jafar... akasema: Ametusimulia Ahmad bin Yunus Dhabii, ametusimulia Ammar bin Nasurri, ametusimulia Ibrahim bin Yasia Malki, ametusimulia Jafar bin Muhammad amesema kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake kutoka kwa Ali amesema: “Alihutubia Bwana Mtume (s.a.w.w.) sehemu inayoitwa Juhfah akasema: ‘... Na nitakuulizeni kuhusu vitu viwili, kuhusu Qur’ani na kizazi changu.”’ 14 AD-DURRUL-MANTHUUR FIY TAFSIIRIL-MAATHUUR CHA SUYUUTWI: Ametaja Jalalu-Diin Suyuutwi katika tafsiri yake hadithi nyingi kuhusiana na Hadith Thaqalain kwa lafudhi ya “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu.” Hapa tunataja baadhi ya hizo: Mosi: Katika tafsiri ya maneno yake Subhaanah Wataala katika SuratulImraan Aya ya 103, na katika tafsiri ya kauli ya Subhaanahu wa Ta’ala: “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu .....” Na ameeleza Ahmad kutoka kwa Zayd bin Thabit amesema: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi nawaachia vitu viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kamba iliyonyooka kati ya mbingu na ardhi na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwenye hodhi.” Pili: Na ameeleza Twabaraani kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi nitakutangulieni na nyinyi mtakuja kwangu kwenye hodhi, basi angalieni vizuri vipi mtanifuata katika vizito viwili,” ikaulizwa: “Ni vipi hivyo vizito viwili, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: ‘Kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza Wajalla, ni kamba iliyonyooka toka mbinguni hadi ardhini, upande mmoja uko katika mikono ya Mwenyezi Mungu na upande mwingine uko katika mikono yenu, basi mshikamane nacho, hamtateleza wala ham132

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain tapotea, na kidogo ni kizazi changu hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi, nimemuomba Mola Wangu, hivyo msivitangulie mtaangamia, wala msivifundishe kwani ni vijuzi zaidi kuliko nyinyi.”’ Tatu: Ameeleza Ibn Saad, Ahmad na Twabaraani kutoka kwa Abu Said Khudri amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Enyi watu, hakika mimi nawaachia vitu viwili ambavyo mtakaposhikamana navyo hamtapotea baada yangu, kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka kati ya mbingu na ardhi, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.”’196 Na imekuja katika tafsiri ya maneno ya Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Ta’ala: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda karaba zangu.” Anasema Suyuutwi: Ameieleza Tirmidhi na akaipasisha kuwa ni hadithi hasan, na amesema Ibn Abbas katika Maswahif kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.): Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nawaachia ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini na kizazi changu AhlulBayt wangu, na kamwe havitatengana hadi virudi kwangu kwenye hodhi, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo.”’197 Nasema: Hayo ndiyo ambayo yameelezwa na Suyuutwi katika tafsiri ya maneno ya Subhanahu wataala: “Nashikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu” na katika tafsiri ya Aya hiyo hakusema: “Kushikamana na Sunna”. Na hilo lajulisha upotofu wa mwenye kuitikadi kuwa Mtume (s.a.w.w.) ameusia Kitabu na Sunna.

196 Ad-Durul-Manthur Juz. 2, uk. 107. 197 Ad-Durul-Manthur Juz. 5, uk. 702. 133

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 15. TAFSIRUL-QUR’ANI ADHIIM YA IBN KATHIIR: Ibn Kathiir anasema katika tafsiri yake: “Na imethibiti katika hadithi sahihi kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema katika hotuba yake ya GhadiirKhum: ‘Hakika mimi nawaachia vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, na hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.”’198 Na hadithi iliyopokewa na Zayd bin Arqam: “.....Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alisimama akihutubia kati yetu sehemu ya maji panapoitwa Ghadir-Khum, akasema: “Na hakika mimi ninakuachieni vizito viwili kimoja wapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu, kina uongofu na nuru, basi chukueni Kitabu cha Mwenyhezi Mungu na shikamaneni nacho,” akaasa juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kuhamasisha, na akasema (s.a.w.w.): “Na Ahlul-Bayt wangu nawakumbusha kwa Mwenyezi Mungu katika Ahlul-Bayt,” Haswiin akamwambia: “Ni nani hao Ahlul-Bayt wake, ewe Zayd? Je! wanawake ni katika Ahlul-Bayt wake?” Akasema: ‘Hakika wakeze sio miongoni mwa Ahlul-Bayt wake...”’199 Nasema: Na kauli hiyo ni ya kinaga ubaga kutoka kwa Zayd bin Arqam kuwa wanawake wa Mtume (s.a.w.w.) sio katika Ahlul-Bayt, na hilo ndio lililo muktadha katika hadithi zote zilizotangulia katika tafsiri ya Aya ya Mapenzi, Aya ya Utakaso na Aya ya Maapizano, basi rejea huko. Na katika hadithi nyingine kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi nawaachia ambavyo mtakaposhikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kitukufu kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba inyookayo kutoka mbinguni hadi ardhini, na kingine ni kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, na 198 Tafsirul-Qur’ani Al-Adhiim Juz. 4, uk 122 199 Tafsirul-Qur’ani Al-Adhiim Juz. 4, uk 122. 134

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain kamwe havitatengana mpaka virudi kwangu kwenye hodhi, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo...” Aidha Tirmidhiy amesema: Kutoka kwa Jaabir bin Abdillah (r.a.) amesema: Nilimuona Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Rehema na amani ziwe juu yake na ndugu zake) wakati akiwa Hijja sehemu ya Arafa naye akiwa juu ya ngamia wake Qaswaai, akihutubia, nilimsikia akisema: “Enyi watu hakika mimi nakuachieni vitu ambavyo mtakaposhikamana navyo kamwe hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlulbayt wangu.” Ibn Kathiir amesema: “Ameipokea yeye pekee.” Aidha akasema tena: “Ni hadithi nzuri yenye kushangaza.” Na katika mlango mwingine kuna hadithi kutoka kwa Abu Dharr, Abu Said, Zayd bin Arqam na Hudhaifa (Mwenyezi Mungu awe radhi nao).”200 16. AL-MUSTADRAK ALAS-SWAHIHAIN CHA HAKIM, PAMOJA NA KITABU TALKHIISW CHA DHAHABI Hadithi ya kwanza: Hakimu anasema: “Amenipa habari Muhammad bin Ali Shaybaani Kufii, amesema Ahmad bin Hazim Ghaffar, ameeleza Abu Na’im, ameeleza Kamil Abu Allaai, amesema: “Nilimsikia Habiib bin Abu Thabiti akieleza habari kutoka kwa Yahya Ibn Juudah kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: “Tulitoka pamoja na Mtume (s.a.w.w.) hadi tulipofika Ghadiir-Khum.............“Na hakika mimi nakaribia kuitwa nami nitaitikia, na hakika mimi nawaachia ambavyo mtakaposhikamana navyo hamtapotea baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Azza Wajalla,” kisha akakamata mkono wa Ali (r.a.) akasema: “Enyi watu ni nani bora zaidi kuliko nafsi zenu?” Wakasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume ni wajuzi zaidi.” Akasema: “Yeyote niliyekuwa mimi ni kiongozi wake basi na huyu ni kiongozi wake.” Hadithi hii ni Sahih katika upokezi wake hata kama Bukhari na Muslim hawajaipokea.” 200 Tafsirul-Qur’ani Al-Adhiim Juz. 4, uk. 122 – 123. 135

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Al-Hafidh Dhahabi akasema katika Kitabu chake Talkhiis Alal-Mustadrak: “Amesema Abu Na’im: Ameeleza Kamil Abu Alaai: “Nilimsikia Habiib bin Abu Thabit kutoka kwa Yahya bin Juudah kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: “Tulitoka pamoja na Bwana Mtume (s.a.w.w.) hadi tulipofika Ghadiir-Khum....” Ni hadithi sahihi.”201 Hadithi ya pili: Kutoka kwa Abu Tufa’il kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: “Pindi Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anarejea kutoka katika Hijja yake ya kuaga alifikia Ghadiir-Khum... akasema: “Mimi nawachieni vizito viwili kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo viwili, hakika hivyo havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.” Kisha akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu Azza Wajalla ni kiongozi wangu, na mimi ni kiongozi wa kila muumini”, kisha akaushika mkono wa Ali (r.a.) akasema: ‘Yeyote ambaye mimi ni kiongozi wake basi na huyu ni kiongozi wake, ewe Mola Wangu, mtawalishe mwenye kumtawalisha yeye na mfanye adui mwenye kumfanyia uadui yeye.”’ Hadithi hiyo ni sahihi kwa mujibu wa sharti za Bukhari na Muslimu japokuwa hawakuiandika, na hakika Hafidh Dhahabi ameipitisha na kuikubali hadithi hiyo katika kitabu chake Talkhiis. 202 Hadithi ya tatu: Anasema Hakim (ameshuhudia) hadithi ya Salama bint Kahiil kutoka kwa Abu Tufa’il aidha ameipasisha na ni sahihi kwa sharti la Bukhari na Muslim….. kisha akasema: “Enyi watu, hakika mimi nakuachieni mambo mawili... Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu kizazi changu...” Na hadithi ya Buraidah Aslamah ni Sahih kwa Sharti la mashekhe wawili.203

201. Talkhiis Alal-Mustadrak Juz. 3, uk. 533. 202. Talkhiis Alal-Mustadrak Juz. 3, uk. 109 203. Al-Mustadrak Juz. 3, uk. 10 -11. 136

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Hadithi ya nne: Anasema Hakim: “Ametuhadithia Bakr Muhammad bin Husein bin Muslimul-Faqiih..... kutoka kwa Muslim bin Swabiih kutoka kwa Zayd bin Arqam (r.a.) amesema: Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na AhlulBayt wangu, na hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.” Hadithi hii ni hadithi Sahih katika upokezi wake kwa sharti la masheikh wawili japo hawajaipokea.” Na Dhahabi amekiri na ameikubali hiyo katika kitabu chake Talkhiis.204 17. TAFSIRUL-BAGHAWIY Anasema Baghawi katika Tafsiir yake: “Tumepokea kutoka kwa Yazid bin Hayyan kutoka kwa Zayd bin Arqam kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nawachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlul-Bayt wangu.”’ 205 18. AL-FUTUHAATUL-ILAHIYYAH FI TAWDHIIH TAFSIRUL JALALAINI CHA SULAIMAN SHAAFII: Na katika kitabu Futuhaatul-Ilahiyyah: “Na wametofautiana katika ndugu zake wa karibu na (s.a.w.w.), ikasemwa ni Fatimah, Ali na watoto wao, na kwao imeteremshwa Aya: “Hakika Mwenyezi Mungu anataka kukuondoleeni uchafu...” Amepokea Zayd bin Arqam kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Hakika mimi nakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlul-Bayt wangu.”’206

204Talkhiis Alal-Mustadrak Juz. 3, uk. 148. 205 Tafsirul-Baghawiy Juz. 4, uk. 125. 206 - Futuhaatul-Ilahiyyah Juz. 4, uk. 61 137

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 19. TAFSIRUL-KHAZIN: Imekuja katika Tafsirul-Khazin katika tafsiri ya kauli ya Subhaanahu wa Ta’ala: “Sema sitaki malipo yoyote kutoka kwenu isipokuwa kuwapenda watu wangu wa karibu.” Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam hakika Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi ninawaachia vizito viwili kimoja wapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna uongofu na nuru, chukueni katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu na shikamaneni nacho.” Akaasa juu ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu kisha akasema: ‘Na Ahlul-Bayt wangu nawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya AhlulBayt wangu, nawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya Ahlul-Bayt.”’207 20. KANZUL-UMMAL FIY SUNANIL-AQWAAL WAL-AF’AAL CHA AL-MUTTAQIY AL-HINDIY: 1. Hadithi namba 871: “Enyi watu hakika mimi nawaachia ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlulbayt.” (Ni kutoka kwa Jaabir). 208 2. Hadithi namba 872: “Enyi watu hakika ninakuachieni ambavyo mkishikamana navyo kamwe hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” (Ni kutoka kwa Jaabir) 209 3. Hadithi namba 873. “Hakika mimi nawaachia vitu viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka kati ya mbingu na ardhi na kizazi changu Ahlulbayt wangu, hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.” (Ni kutoka kwa Zayd bin Thabit)210

207 Tafsirul-Khazin, Juz. 4, uk. 101. 208 Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 153. 209 Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 153 - 154. 210 Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 154. 138

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 4. Hadithi namba 874. “Hakika mimi nakuachieni ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kikubwa kuliko kingine Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyonyooka kutoka mbinguni hadi ardhini, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, kamwe havitatengana mpaka virudi kwangu kwenye hodhi, basi angalieni vipi mtanifuata katika hiyo.” (Ni kutoka kwa Zayd bin Arqam)211 5. Hadithi namba 899: “Ama baada, enyi watu hakika mimi ni binadamu nitajiwa na mjumbe wa Mola Wangu kuniita nami nitamwitikia, mimi nawaachia vizito viwili kimojawapo ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ndani yake kuna uongofu na nuru, mwenye kushikamana nacho atakuwa katika uongofu na mwenye kukiacha atapotea, basi kitendeeni kazi Kitabu cha Mwenyezi Mungu Subhannahu wataala na shikamaneni nacho, na Ahlul-Bayt wangu, nawakumbusha Mwenyezi Mungu juu ya Ahlul-Bayt wangu.” ( Ni kutoka kwa Abdul bin Hamiid kutoka kwa Zayd bin Arqam)212 6. Hadithi namba 944. “Hakika mimi nawaachia ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu upande mmoja uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na upande mwingine uko mikononi mwenu, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika hivyo viwili havitatengana kamwe mpaka virudi kwangu kwenye hodhi.” (Ni kutoka kwa Abu Said)213 7. Hadithi namba 945: “Hakika mimi karibu nitaitwa nami nitaitikia, na hakika mimi nakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooka kutoka mbinguni mpaka ardhini, na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika mwenyezi Mungu Mtukufu na Mwenye habari amenieleza kuwa hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi, basi 211. Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 154. 212. Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 159. 213 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 165. 139

7/1/2011

4:07 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain angalieni mtanifuataje katika hivyo.” (Ni kutoka kwa Abu Said)214 8. Hadithi namba 946: “Hakika mimi nawaachia ambavyo mkishikamana navyo baada yangu hamtapotea kamwe: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, na hivyo viwili havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi.” (Ni kutoka kwa Abdul bin Hamid na Ibn Ambari kutoka kwa Zaid bin Thabit)215 9. Hadithi namba 947: “Hakika mimi nitatangulia nanyi mtakuja kwangu kwenye hodhi... basi angalieni vipi mtanifuata katika vizito viwili,” akaulizwa, ni vipi hivyo vizito viwili ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu ncha moja iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na ncha nyingine iko mikononi mwenu, basi shikamaneni nacho kamwe hamtapotea, na kidogo ni kizazi changu, hakika hivyo viwili kamwe havitaachana hadi virudi kwangu kwenye hodhi, na nilimuomba hivyo Mola Wangu, basi msivitangulie mtaangamia wala msivifundishe hakika hivyo ni vijuzi zaidi yenu.” ( Ni kutoka kwa Zayd bin Thabit)216 10. Hadithi namba 948: Hakika hadithi ni kutoka kwa Zayd bin Thabit na kutoka kwa Zayd bin Arqam.217 11. Hadithi namba 950: Katika hadithi nyingine ni kutoka kwa Abu Said.218 12. Hadithi namba 901: “Enyi watu hakika mimi ninakuachieni vizito viwili kamwe hamtapotea iwapo mtavifuata hivyo: Kitabu cha Mwenyezi 214 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 165 - 166. 215 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 166. 216 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 166. 217 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 166. 218 - Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 166 - 167. 140

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Mungu na Ahlul-Bayt wangu kizazi changu, mnajua mimi ni bora kwa waumini kuliko nafsi zao, basi yeyote ambaye mimi ni kiongozi wake basi Ali ni kiongozi wake.” (Ni kutoka kwa Zaid bin Arqam)219 13. Hadithi namba 954: “Kana kwamba nimeitwa nimeitikia, hakika mimi nawaachia vizito viwili kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo, hakika hivyo havitatengana kamwe hadi virudi kwangu kwenye hodhi, hakika Mwenyezi Mungu ni kiongozi wangu, na mimi ni kiongozi wa kila muumini, na ambaye mimi ni kiongozi wake basi pia Ali ni kiongozi wake, ewe Mola Wangu mtawalishe mwenye kumtawalisha yeye na mfanyie uadui mwenye kumfanyia uadui yeye.” (Ni kutoka kwa Abu Tufa’il kutoka kwa Zayd bin Arqam)220 14. Hadithi namba 959: “Katika hadithi ya Twabaraani kutoka kwa Abu Tufa’il kutoka kwa Hudhaifah bin Asiid: ‘Na hakika mimi nitawauliza mtakapokuja kwangu kutokana na vizito viwili, basi angalieni vipi mtanifuata katika hivyo, kizito kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu... na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, kwa hakika amenipa habari Latifu Mwenye habari kuwa, hakika hivyo viwili kamwe havitapoteana hadi virudi kwangu kwenye hodhi.” ( Ni kutoka kwa Hakiim kutoka kwa Hudhaifah bin Asiid) 221 21. LISAANUL-ARAB CHA IBN MANDHUUR AL-MISRII: Katika Lisaanul-Arab Juz. 4 uk. 538 kwenye neno Itra, amesema: “Na wengi hudhani hasa ni mtoto wa mtu. Ama Itra wa Mtume (s.a.w.w.) ni kizazi cha Fatimah (r.a.), kauli hii ni ya Ibn Sayyidah. Na Al-Azhariy amesema: Katika hadithi ya Zayd bin Thabit amesema: Mtume (s.a.w.w.) ame219 Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 167. 220 Kanzul-Ummal, Juz. 1, uk. 167. 221 Kanzul Ummal, Juz. 1, uk. 169. 141

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain sema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili baada yangu Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu, hakika hivyo viwili havitatengana kamwe mpaka virudi kwangu kwenye hodhi”, akasema: Amesema Muhammad bin Is’haaq kuwa hadithi hiyo ni sahih, na ameipokea nyingine mfano wa hiyo Zayd bin Arqam na Abu Said Khudri. Na katika baadhi ya hadithi hizo kuna: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt, basi hapo akawafanya Itra “kizazi” kuwa ndio Ahlul-Bayt...” 22. YANAABIIUL-MAWADDAH CHA AL-QUNDUUZIY: Ameeleza Sheikh Sulaiman bin Sheikh Ibrahim Balkhi Al-Qunduuziy Hadithi Thaaqalaini kwa njia nyingi tunazitaja baadhi ya hizo: Qunduzi anasema: “Katika kitabu Manaaqib kutoka kwa Ahmad bin Salam kutoka kwa Hudhaifah bin Yamani (r.a.) amesema: ‘...Na hakika mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu...”’ Kutoka kwa Atwai bin Saaibu kutoka kwa Abu Yahya kutoka kwa Ibn Abbas (r.a.) amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alihutubia.....hakika Ahlul-Bayt wangu na kizazi changu hawa ndio hasa wanaonihusu na wa karibu yangu, na hakika ninyi mtaulizwa kutokana na vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” Kutoka kwa Abu Dharr (r.a.) amesema: “Ali (a.s.) amesema kumwambia Twalhah, Abdul-rahman bin Auf na Said bin Abu Waqaas: Je! mnajua kuwa Mtume (s.a.w.) amesema: ‘Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu...”’ Al-Qunduuzi anasema: “Imepokewa Hadith Thaqalain na AmiirulMuumina Ali, Hasan bin Ali (a.s.) Jabir bin Abdillah Answari, Ibn Abbas, Zayd bin Arqam Abu Said Al-Khudri, Abu Dharr, Zayd bin Thabiti, Hudhaifah bin Yamani, Hudhaifah bin Asiid, Jabair bin Matwaan na 142

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Salman Al-Farsi (r.a.).222 Na ameeleza Twabaraani katika kitabu Al-Kabiir kuwa watu waliopokea ni waaminifu na lafudhi yake ni: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Ahlul-Bayt wangu...” Hadi mwisho wa aliyoyaeleza Al-Qunduuzi kuhusu Hadith Thaqalain katika kitabu Yanaabiul-Mawaddah kutoka kwa wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna na Mahafidh wao katika njia tofauti, basi rejea huko.223 23. TADHKIRATUL-KHAWAIS CHA SIBTWU IBNUL JAUZI Katika Tadhkiratul-Khawais mlango wa 12 uk. 322 amesema Ahmad katika fadhila: “Ametuhadithia Aswad bin Aamir, ametuhadithia Israail kutoka kwa Uthman bin Mughiirah kutoka kwa Ali bin Rabiia amesema: “Nilikutana na Zayd bin Arqam nikamwambia; Je! Umemsikia Mtume (s.a.w.w.), anasema: “Nimekuachieni vizito viwili kimoja ni kikubwa kuliko kingine?” Akasema: Nilimsikia akisema: ‘Ninakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu, kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu...”’ 24. AN-NIHAAYAAH FI GHARIIB HADITHI WAL-ATHAR CHA IBN ATHIIR Na katika Kitabu An-Nihaayah cha Ibn Athiir: “Hakika nakuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” Ameviita vizito viwili kwa sababu kuvichukua hivyo kuna uzito.

222 Yanabiul-Mawaddah, uk. 33 – 34. 223 Yanabiul-Mawaddah, uk. 35 na kuendelea.

143

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Na katika Juzuu ya tatu ya An-Nihaayah: “Nimekuachieni vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu.” Kizazi cha mtu hasa ni wale ndugu zake wa karibu sana, na kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) ni watoto wa Abdul-Mutwalib, na ikasemwa ni Ahlul-Bayt wake wa karibu, nao ni watoto wake, Ali na watoto wake.” Hapa pia Ibn Athiir hajawataja wanawake na wakeze (s.a.w.w.) kuwa ni miongoni mwa Ahlul-Bayt wake. Mpaka hapa tumetosheka na kutosheleza ubainishaji huo kuhusiana na Hadith Thaqalain kwa lafudhi: “Na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu” kutoka kwenye vitabu vya Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, ili ifahamike hadithi hiyo ni miongoni mwa hadithi mutawatiri kwa waislamu wote. Kilichobakia juu yetu ni kutaja yale aliyoyasema muhakiki wa kitabu Khasais cha Nasaai kuhusu Hadith Thaqalain: “Na hadithi hiyo ameieleza Bazzar Juz.3 uk. 183 - 190 katika kitabu Kashful-Astaar, Twabaraani katika Al-Kabiir Juz. 5, uk 185 - 186, na katika kitabu Awsat Juz. 2, uk. 106, na Hakim Juz. 3, uk. 109, na Khawarzami katika kitabu Al-Manaqib uk. 93 kwa njia kadhaa kutoka kwa Habib bin Abu Thabit na Hakim kaikubali kuwa ni sahihi kwa sharti la masheikh wawili na Dhahabi amekiri usahihi wake... na ameieleza hiyo Ahmad bin Hanbali katika Musnad Juz. 4, uk 370. Na katika Al-Fadha’il uk. 1167, na Ibn Habaan katika Mawarudud-Dham’an uk. 2205, na Ibn Asaakir Juz. 12 uk.111, kupitia njia ya Fitru bin Khalifa, kutoka kwa Abu Tufa’il kutoka kwa Zayd bin Arqam. Na wapokezi wa Ahmad na Ibn Habaan ni waaminifu isipokuwa Fatru yeye ni mkweli lakini alisingiziwa kuwa ni Shi’a, na kwa njia hiyo inapata nguvu njia ya Habib bin Abu Thabit na hivyo imekuwa ni sahih. Na ameieleza Tirmidhi Juz. 5, uk. 297, Ahmad katika Al-Fadha’il uk. 959, Twabaraani katika Al-Kabiir Juz. 3 uk. 199 na Ibn Assakir Juz. 12, uk. 113, kupitia njia ya Shuubah kutoka kwa Salamah bin Kuheli kutoka kwa Abu Tufa’il kutoka kwa Zayd bin Arqam au Huzziyah bin Asiid.... na wapokezi wake ni waaminifu. Tirmidhi amesema: ‘Ni 144

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain hadithi hasan sahih,” na katika toleo lingine: ‘Ni ghariibu.”’ MAFUNZO YA HADIITH: Tutataja mafunzo ya hadithi hivi punde, kwa hakika Hadith Thaqalain dalili yake iko bayana kuhusiana na kushikamana na vizito viwili, na Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiusisitizia umma wake kushikamana navyo, na akaeleza mtafikwa na upotevu kwa kwenda kinyume navyo, navyo ni kizito kikubwa ambacho ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, na kizito kidogo ni Ahlul-Bayt wake (s.a.w.w.), nao ni Ali, Fatimah, Hasan na Husein (a.s.), na kwamba hivyo viwili kamwe havitatengana mpaka virudi kwake (s.a.w.w.) kwenye hodhi, na hilo limethibititishwa na hadithi lukuki zilizoeleza kinagaubaga kupitia njia za Ahlus-Sunna na Mahafidh wao, kwa hivyo hadithi hiyo inajulisha juu ya: Kwanza: Wajibu wa kushikamana na vizito viwili, Kitabu kitukufu na kizazi chake, kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) alikifanya kizazi kuwa ni moja ya vizito viwili, na akahukumu kuwa hivyo abadan havitatengana mpaka virudi kwake (s.a.w.w.) kwenye hodhi, na hiyo ni dalili tosha juu ya uimamu wao na umaasumu wao, na mtu maasum anastahili zaidi kufuatwa kuliko mwingine, na hii ndiyo faida ya kikomo ya kuwajibika kushikamana na Kitabu, ambacho ni kizito kikubwa, na kizazi chake kizito kidogo, kwa mantiki hiyo kushikamana navyo ni kujiwekea dhamana ya milele ya kutopotea. Na ama dalili ya uma’asumu wa kizito kikubwa na kidogo nayo ni kwamba pindi Mtume (s.a.w.w.) alipoamrisha kushikamana na vizito viwili moja kwa moja pasi na kizuizi inatujulisha sisi kuwa hivyo viwili ni maasumu, kwani hivyo viwili lau kama visingekuwa maasumu asingefaradhisha kushikamana navyo na kuvifuata bila ya mipaka, kwani kila kilichoainishwa kufuatwa na kushikamana nacho ni lazima kiwe maasumu ili isilazimu kwenda kinyume na tamko la wazi la Mtume (s.a.w.w.) waziwazi kwa kutovifuata, kwa hivyo natija inayopatikana hapa ni wajibu wa uongozi 145

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain wao juu ya umma kulingana na nguvu ya hoja ifuatayo: Yeyote ineyewajibika kushikamana naye imewajibika kumtii. Na kila ambaye imewajibika kumtii inawajibika kumfanya kiongozi. Natija: Yeyote inayewajibika kushimana naye imewajibika kumfanya kiongozi. Ama dalili au nguvu ndogo ya hoja ni Hadith Thaqalain, hadithi hii inathibitisha Uimamu wa Amiirul-Muuminina Ali bin Abi Twalib (a.s.). Pili: Hakika Hadith Thaqalain ni hadithi ambayo imeeleza kuwa haiwezekani nyumba ya Utume (s.a.w.w.) kuwa tupu pasi kuwepo mtu wa nyumba hiyo katika kila zama, na hilo limeashiriwa na wanachuoni chungu tele miongoni mwa Wanachuoni wa Ahlus-Sunna, Ibn Hajar anasema katika kitabu chake Sawa’iqul Muhriqah uk. 149: “Ninazo hadithi nyingi zinazohimiza juu ya kushikamana na Ahlul-Bayt nayo ni ishara ya kutokuwa na kikomo katika kushikamana nao hadi siku ya Kiyama, vivyo hivyo Kitabu kitukufu”. Na hilo linathibitisha upotofu wa maneno ya wale ambao wanaodai kuwa makusudio ya Ahlul-Bayt katika hadithi ni wakeze (s.a.w.w.). Allama Munaawi anasema: “Amesema Shariifu habari hii inafahamisha kuwepo kwa mhusika wa kushikamana naye katika kila zama miongoni mwa Ahlul-Bayt na kizazi kitoharifu mpaka siku ya Kiyama, hata iende sambamba na msisitizo uliotajwa wa kushikamana nao kama ilivyokuwa Kitabu (Qur’ani), kwa hivyo walikuwa amani kwa watu wa ardhini, iwapo watatoweka wao aidha watoweka watu wa ardhini”.224 Tatu: Hadithi imejulisha kuwa yule mwenye kuviacha vizito viwili amepotea, na yule ambaye madhehebu yake hayaafikiani na madhehebu ya Ahlul-Bayt (a.s.) atakuwa ni mwenye kupotea, na hilo limeelezwa kina224 Faydhul-Qadiir Juz. 3, uk 14 – 15. 146

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain gaubaga na Wanachuoni wakubwa wa Ahlus-Sunna, anasema Mahmuud Shukri Aluusi: “Na hapa kuna faida kubwa ambayo inanasibiana na mchakato huu, kuwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika mimi ninakuachieni vizito viwili, mtakaposhikamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, kimoja ni kikubwa kuliko kingine, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu Ahlul-Bayt wangu”, na hadithi hii imethibiti pande zote kwa Ahlus-Sunna na Shi’a, na imejulikana kuwa Mtume (s.a.w.w.) ametuamrisha sisi katika vipaumbele vya kidini na hukumu za kisheria kwa kushikamana na vitukufu hivyo viwili na kuvirejea katika kila jambo, basi yeyote yule ambaye madhehebu yake yatakuwa yametofautiana na hivyo viwili katika nyanja mbalimbali zikiwemo za kisheria, itikadi, matendo basi atakuwa ni mwenye kupotea”. Nne: Hakika Nabii (s.a.w.w.) alibainisha kwamba upotevu unatokana na kuviacha hivyo viwili, na uongofu unapatikana kwa kuvifuata hivyo pamoja, kwa mantiki hiyo kushikamana na kimojawapo haitoshelezi chochote, bali hapana budi kushikamana navyo na kuvifuata kwa pamoja bila kubagua, hiyo ni kulingana na kauli yake “havitatengena kamwe” kama vile mwenye kuiacha Qur’ani atafikwa na upotevu na hasara, vivyo hivyo mwenye kwenda kinyume na kizazi cha Rasuuli atafikwa na hali hiyo. Tano: Hadithi imejulisha kule kutotambuliwa ukhalifa wa wale ambao walimtangulia Amiirul-Muuminiina Ali bin Abi Twalib (a.s.), na hilo ni kwa muktadha wa kuwajibika kwao hao makhalifa watatu waliomtangulia Imam Ali (a.s.) kushikamana na kumfuata Ali na Maimamu waliomfuata yeye (a.s.), na dalili hiyo iko wazi kabisa kutoka kwenye Hadith Thaqalain, na zinginezo miongoni mwa hadithi zinazokubalika.

147

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

HITIMISHO Na mwisho nasema: Kwa hakika hilo ndilo ambalo tulitaka kulibainisha kutoka kwenye Hadith Thaqalain, ili kuwatetea Maimam wetu (Alayhim, Salaam), Maimamu waongofu, taa ing’arayo gizani na kunusuru kundi la haki ambalo limeshikamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Subhaanah na Ahlul-Bayt rasuul (a.s.). Napenda kusema: Wapo ambao wametutuhumu katika vipeperushi, na kusema: Katika baadhi ya vitabu vyetu tumechepuka pembeni na kuiacha haki na kulitendea kundu fulani ubaya, tukawaponda Maulamaa wetu na tukawapinga, na sisi ni waharibifu na wababaishaji na hiyo ndio desturi yetu, na sisi tumewatuhumu baadhi ya Shi’a kwa upotokaji, na tukanasibisha kwa Wanachuoni wetu maneno wasiyoyasema na wala hatufahamu maneno yao, na kwa hakika sisi tumeziingiza nafsi zetu katika bahari ambayo hatuwezi kuogelea, aidha hatukuwaachia mambo wahusika wenyewe, bali tumesimama kidete na kuzikataa hadithi sahihi za AhlulBayt (a.s.), kisha tukaangukia kwenye hasara zake, na kwamba baadhi ya vitabu vyetu vinakusanya ngano za kale lukuki na upotofu ambao unapelekea kukanushwa vikali ili zisitue kwenye akili ya vizazi na vijana waumini, na hizo hazina thamani yoyote ile kiasi cha kiwango cha elimu, na hakika sisi tulikuwa tunafanya siri kuponda itikadi sahihi kwa jina la upondaji wa makundi potovu, na kuwa eti hakika sisi ni wafuasi wa Imamu mkubwa katika upotevu katika zama hizi. Kwa kweli wamesema mengi na yasiyokuwa hayo katika tuhuma za kidhuluma. Kwa kuwa inajulikana wazi kwamba lengo kubwa la kila kitabu kinachoandikwa na sisi ni kuwahami Maimamu Ahlul-Bayt (a.s.) ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatoharisha tohara ya kabisa kabisa, na pia kuhami madhehebu yao matukufu yaliyo safi huku tukibainisha fadhila, elimu na daraja zao mbele ya Mwenyezi Mungu 148

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain Subhaanahu wa Ta’ala, basi hayo yote hayatatuepusha sisi mbele ya yule anayetushambulia, kuponda mafundisho ya dini yetu, uadilifu wetu na kututoa kutoka katika watu wenye imani huku akitutuhumu kwa tuhuma nzito nzito. Na katika yote ninayoyasema Mwenyezi Mungu anitosha, na neema iliyoje kumtegemea Yeye tu, tuna makutano na ahadi siku ambayo sote tutasimama mbele ya Mwenyezi Mungu Azza Wajalla, Mtume wake (s.a.w.w.), Maimamu wangu watoharifu na Bibi Fatimah Zahraa (a.s.) Al-Batuul, AlMadhluumah ili wafanye insaafu na uadilifu kati yangu na aliyenidhulumu. Na dunia ijue kuwa mimi nimesimama ilihali nimekunyata mikono yangu bali nitadumu katika njia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na ndugu zake wote watoharifu (a.s.), nitaendelea katika njia hii na kamwe sitohofu kwa Mwenyezi Mungu lawama za mwenye kulaumu, nitabainisha haki vyovyote vile itakavyonikalifu thamani yoyote, katu sitozembea katika kadhihirisha itikadi sahihi. “Ewe Mola Wetu tusamehe na mwenye kutunanga, tuafu sisi na yule aliyetukosea. Ewe Mola wetu tusamehe na ndugu ambao wametutangulia katika imani wala usijaalie katika nyoyo zetu chuki kwa wale walioamini. Ewe Mola wetu hakika wewe ni Mpole na mwenye huruma. Mwisho namuomba Mwenyezi Mungu swt. atuwafikishe ili tulipwekeshe neno la Tawhiid la haki, na kufuata haki popote itakapokuwa, atujaalie tuwe miongoni mwa wale wenye kushikamana na vizito viwili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bayt Nabii (s.a.w.w.), hakika Yeye ni Msikivu wa dua, na mwisho wa maombi yetu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu Mola wa ulimwengu, rehema na amani zimfikie mbora wa viumbe Mtume Muhammad na ndugu zake watakatifu. 12 Mfunguo tano 1420 A.H. 149

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

BIBLIOGRAFIA 1. QUR’ANI KARIIM 2. AL-ITIQAN-FI ULUUMIL-QUR’ANI: JALALUD DIIN SUYUUTWI 3. AHKAMUL-QUR’ANI: IBNUL ARABI 4. ASBAABUN-NUZUUL: AL-WAAHID 5. AL-ISTIIAB FI MAARIFF’ATIL-AS-HAAB: IBNU ABDUL-BARRI ANDULUSI 6. USUDUL-GHAABA FI MAARIFATIS-SWAHAB: IBN ATHIIR 7. ISTIIAFUL-RAAGHIBIINA: MUHAMMAD BIN ALI SWABAAN 8. ANSAABUL-ASHRAAF: AHMAD BIN YAHYA AL-BALADHURI 9. AN-NUAARUT TANZIIL WA ASRAAR TAAWIIL: BAYDHAWI 10. TAARIKH BAGHDADI: KHATIBU BAGHDAD 11. TAFSIIRUL-BAHRUL-MUHIIT: ABU HAYYANIL ANDULUSI 12. TADHKIRATUL-KHAWA’IS: SIBTWI IBNUL JAUZI 13. TAFSIIRUL-KHAZINU: ALAU DIIN BAGHDAD 14. TAFSIIRUL-RUUHUL-BAYAANI: ISMA’IL HAKI BURUSUWI 15. TAFSIIRUL-QURANIL ADHIIM: IBN KATHIIR DAMASQUS 150

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 16. AT-TAFSIIRUL-KABIIR: FAKHRU DIIN RAAZI 17. TALKHISWUL- MUSTADRAK ALA SWAHIHAIN: DHAHABI 18. TAHDHIIBUT-TAHDHIIB: IBN HAJARIL ASQALAANI 19. JAAMI’UL-USUUL-MIN AHADITH RASUUL: IBNUL ATHIIR 20. JAAMI’UL-BAYAAN FI TAAWIILIL-QUR’ANIl MUHAMMAD BIN JARIIR TWABARI 21. JAAMI’US-SIHAHI:TIRMIDHI 22. JAAMI’US-SWAGHIIR: JALAL DIIN SUYUUTI 23. AL-JAAMI’UL-AHKAMUL-QUR’ANI: QURTUBI 24. HADIITHU THAQALAINI WA FIQHUHU: ALI AHAMAD SAALUUS 25. HUQUUQ AALI BAYT MA BAYNA SUNNA WAL BIDAA: IBN TAYMIYA 26. KHASA’IS AMIRUL-MUUMUNIINA ALI BIN ABI-TALIBNASAAI 27. DURRUL-MANTHUUR FI TAFSIIRU MAATHUUR: JALALUDIIN SUYUUTI 28. DHAKHAIRUL-UQBA FI MUHIBBUD DIIN TABARY

MANAAQIB

DHAWIL-QURBA:

29. RIYADHU NADHARAT WA MANAAQIBIL-ASHRA: MUHIBBUD 151

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain DIIN TABARY 30. SILSILATUL-AHADIITHI SAHIHA: MUHAMMAD NASUR-DIIN ALBAANI 31. SHARHU TWAHAAWI FI AQIIDAT SALAFIYYAH: ALI BIN ALI BIN ABIL-IZZA 32. SHAWAHIDU TANZIIL LIQAWAIDU TAHWIIL: HAAKIM HASKAANI HANAFI 33. SHIIATU WA IMAMAT ALI: AAMIR NAJJAR 34. SHIIATU WA AHLUL-BAYT: IHSAANU ILAHI DHARIIR 35. SAHIHI BUKHARI: MUHAMMAD BIN ISMA’IL 36. SAHIHI MUSLIM: MUSLIM BIN HAJJAJ 37. SAWA’IQUL-MUHRIQAH: AHMAD BIN HAJAR HAYTHAM 38. SWIYAGHAT MATFWIQIYYAH LIFIKRI SIYASAL-ISLAM: HASSAN ABBAS HASSAN 39. AL-DHUAFAUL-KABIIR: ABU JAAFAR MUHAMMAD BIN AMRU AQIIL. 40. AL-AQAIDUS-SALFIYA BIADILLAT NAQLIYA WAL-AQILIYA: AHMAD BIN HAJAR AALI ABU TWAANI BAGHALI 41. GHARAIBUL-QUR’ANI WARAGHAIR FURQAAN: AHMAD MUSTAFA MARAAGHI 42. FAT’HUL-GHADIIR: MUHAMMAD BIN ALI SHAWKAANI 152

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 43. FUTUHAATUL-ILAHIYYAH: SULEIMAN BIN OMAR AJALI 44. FAIDHUL-QADIIR FISHARH JAAMIUL-SWAGHIIR: ABDUL RAUF MUNAWI 45. AL-KAMIL FI TAARIKH: IBN ATHIIR 46. AL-KASHAF AN ZAMAKHSHARI

HAQAIQU

47. KASHFUL-JAAN MUHAMMAD MOHAMMAD AALI KHAMIIS

GHAWAMIDHU

TIJAANI:

TANZIIL:

OTHAM

BIN

48. KANZUL-UMMAL: AL MUTTAQI HINDI 49. LISAANUUL-ARAB: IBN MANTHUR 50. MUHTASAR TUHFAH ITHNA ASHARIA: MAHMUUD SHUKRI ALUUSI 51. MADARIKU TANZIIL WA HAQAIQU TAAWIL: ABDULLAH NASAFI 52. AL-MUSTADRAKU ALA SAHIHAIN: HAAKIM NAYSABUURI 53. AL-MUSNAD: AHMAD BIN HANBALI 54. MUSHKILUL-ATHAAR: ABU SAAFARI TWAHAAWI 55. MAALIMUL-TANZIIL: AL-BAGHAWI 56. MANAAQIBU AMIIRUL-MUUMINIINA ALI BIN ABI TALIB: IBN MAGHAZIL SHAAFII 153

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

57. AL-MUWATA: MALIK BIN ANAS 58. MIIZANUL-ITIDALI FINAQDI RIJAAL: MUHAMMAD BIN UTHMAN DHAHABI 59. NADHARIATUL-IMAMAT LADA SHIIA ITHNA ASHARIA: DK. AHMAD MAHMUUD SUBHI 60. AN-NIHAYAH FI GHARIIBIL-HADIITH WAL-ATHAR: IBN ATHIIR 61. NUURUL-ABSWAAR: SHABLANJI 62. YANAABIUL-MAWADDA: AL-QUNDUUZI HANAFI

154

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

VITABU VYA MTUNZI VITABU VILIVYOCHAPISHWA: 1. FIKRUTARBAWI INDA SHIIA IMAMIYYAH 2. SHIIA IMAMIYYA WA NASHAAT ULUUMI ISLAMIA 3. THAQALAINI - KITABULLAH WA AHLUL-BAYUT FI SUNNA NABAWIYYA 4. MAADR. MUSSA WA FIKITABIHI SHIIA 5. ZIWAJUL-MUT’AA FI KUTUBI AHLI SUNNA 6. SHIIA-NASHAATUHUM WA SUNNA FI USUULID DIIN 7. AQIIDU SHIIA WA AHLUS-SUNNA FI USUULID DIIN 8. SHIIA - NASHAATUHUM WA USULUUHUM AQAIDIYYAH 9.MASAIL AQAIDIYYAH: FI GHULUWI WA TAFWIIDH ALKHALQUWA RIZQU, AL-ILMU BIL-GHAIB WA HAQIQATULMUHAMMADA 10. WILAYATU TAKWIINIYYA WA TASHRIIYA - FIDHAU KITABU WA SUNNA WA AWAALUL-ULAMAAI 11. HADITHU THAQALAINI FI KUTBI AHLI SUNNA

VITABU VISIVYOCHAPISHWA: 1. NAQDH SHUBUHAAAT HAULA SHIIA MIN KUTUB AHLI SUNNA 2. AL-IMAMU ALI-FALSAFATUHU WAARAAU FITARBI YAT WATAALIM 3. TAASISI SHIIA LILFALSAFAT ISLAMIYYAH WAL-MINHAJ TAJRUUBI 4. ITHIBATU KHILAF IMAM ALI MIN KUTUBI AHLI SUNNA 5. AL-MUUTAZILA-FALSAFATUHUM WAARAAUHUM FI TARBIYAT WATAALIIM

155

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na mbili Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 156

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54.

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm 157

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82.

Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza Nahjul Balagha Sehemu ya Pili Ujumbe sehemu ya kwanza Ujumbe sehemu ya Pili 158

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

Hadithi Thaqalain 83 84. 85. 86. 87. 88. 89. 90. 91. 92.

Ujumbe sehemu ya Tatu Sunani-Nabii Hadithi Thaqalain Ukweli wa Shia Tabaruku Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu Amali za Ramadhani Al-Mahdi katika Sunna Swala ya Maiti Fatma zahra

159

7/1/2011

4:08 PM

P


Hadith_ya_ThaqalainEdited23-6-08- by Lubumba - PROOFREAD SHEMAHIMBO final D.Kanju.qxd

BACK COVER Hadith ya Thaqalain (Vizito Viwili) ni Hadith maarufu sana katika ulimwengu wa Kiislamu, hakuna madhehebu ya Kiislamu hata moja ambayo haikutaja hadith hii, ingawa kuna tofauti kidogo ya mapokezi kati ya wasimuliaji wake. Pamoja na hayo, ukweli unabakia palepale kwamba haitakamilika historia ya Uislamu bila ya kuitaja Hadithi hii. Hadith Thaqalain ni wosia ambao mtukufu Mtume (saw) aliutoa kwa Waislamu pale Ghadir Khum wakati anarudi kutoka kwenye Hija yake ya mwisho (maarufu kama Hijatu’l-widaa). Qur’an inatuthibitishia kwamba Uislamu ulikamilika baada ya tukio hili la Ghadir ambapo mtukufu Mtume (saw) alitoa khutba ndefu ambayo kwayo alitoa kauli hii ambayo hujulikana kama Hadith Thaqalain: “...Ninakuachieni vizito viwili; Qur’an Tukufu na Kizazi changu...” Baada ya tukio hili la Ghadir Aya ifuatayo iliteremshwa kwa mtukufu Mtume (saw): “...Leo nimekukamilishieni dini yenu, na kuwatimizieni neema yangu, na nimewapendeleeni Uislamu uwe dini yenu...” (5:3) Baada ya kushuka Aya hii mtukufu Mtume (saw) alimuita Ali (as) juu ya mimbari ambayo imetengenezwa kwa matandiko ya ngamia, kisha akanyunyua mkono wake akasema: “Man kuntu mawlahu fahadha Aliy mawlahu.” (Yule ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake basi huyu Ali (naye) ni mwenye kutawalia mambo yake”. kisha akaomba dua: “Ee Allah! Msaidie mwenye kumsaidia (Ali) na mpige vita mwenye kumpiga vita (Ali).” Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555

Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info 160

7/1/2011

4:08 PM

P


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.