Fatima al-Zahra

Page 1

Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page A

FATIMA Al-ZAHRA

Kimeandikwa na:

Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi

Kimetajumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui P.O. Box 19701, Dar es Salaam. Tanzania.


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page B

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 -21 -8 Kimeandikwa na:

Sayyid Muhammad al-Husaini al-Shirazi Kimetajumiwa na: Abdul Karim Juma Nkusui P.O. Box 19701, Dar es Salaam/Tanzania. Kimehaririwa na: Septemba,2008 Dr. M. S. Kanju Email: mokanju2000@yahoo.com P. O. Box 19701, Dar-es-Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab. Toleo la kwanza: Septemba,2008 Nakala:1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation P.O. Box 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu:+255 22 2110640 Fax: +255 22 211310


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page C

YALIOMO 1. Neno la mchapishaji………………………………................................2 2. Al-Hadith al–Qudsi………………………………….….........................5 3. Ushahidi wa kihistoria………………………………….......................15 4. Njama zaendelea........…………………………………………............16 5. Utukufu wa Zahra............................................………….…….............17 6. Zahra (a.s) ni Nuru ya Mwenyezi Mungu.............................................17 6. Bibi wa wanawake wa ulimwenguni………………………….............19 7. Kigezo na mfano mwema…………………………………..................20 8.Maisha ya ndoa.......................................................................................21 9. Ukarimu wake…………………………………………………............22 10. Miongoni mwa Ibada zake………………………………..................23 11. Katika elimu ya Az - Zahraa…..…………………………..................24 12. Hotuba yake Msikitini.........................................................................25 13. Shahada na uchungu...........................................................................25 14. Fatwa kuhusu Bi. Fatma-Zahra (a.s) ………………….......................29 15. Bibliografia..........................................................................................34


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page D

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Fatimah al-Zahra. Sisi pia tumekiita, Fatima al-Zahra. Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya marehemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehemu). Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha ya Bibi huyu mtukufu mwenye nuru. Cha kuzingatia ni kwamba kumjua mtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema: “Jueni kwamba mimi ni Fatima al-Zahra.� Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi Fatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul Muuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s). Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page E

Tunamshukuru ndugu yetu, Abdul Karim Juma Nkusui kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

F

Page F


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 1


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 2

Fatima al-Zahra

NENO LA MCHAPISHAJI (KIARABU) Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu “Lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu……” Hadithil-Qudusi tukufu…… kwayo zimetaabika akili na kupumbaa, na kwayo fahamu zimetahayari lakini nyoyo safi zimeipenda…… ikaathiri, ikaangaza na nuru yake ikawaangazia walio mbinguni kama nyota zinavyowaangazia walio ardhini. Amesema Al-Imam Swadiq (a.s): “Mwenyezi Mungu hafanyi mambo isipokuwa kwa kupitia sababu1 (zake)”. Kwa kanuni hii Mwenyezi Mungu ameumba ulimwengu, nayo ni kanuni ya ‘sababu na kisababishwa’ au ‘chanzo na matokeo’ (Al-I’lalu wal-Ma’aluulaat) kulingana na walivyosema wanafalsafa, na wote wanaafikiana kwamba chanzo kikuu au mwanzilishi wa vitu ni Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na Mwenyezi Mungu anasema: “Lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu…..”, anamwambia Mtume wake Mtukufu na kipenzi chake, Muhammad bin Abdullah (s.a.w.w), yaani Mwenyezi Mungu Mtukufu amemfanya Mtume (s.a.w.w) ndio sababu ya lengo la kuumba, kwa maana kwamba lau kama si Muhammad na kizazi chake, na wajibu wa kuwajua, kuwapenda na kuwatii (a.s) basi Mwenyezi Mungu asingeumba ulimwengu huu… Na katika Hadithi nyingine anasema (s.w.t): “Mja wangu nimeumba vitu kwa ajili yako na nimekuumba wewe kwa ajili yangu, nimekupa dunia kwa ihsani na nimekupa akhera kwa imani”2. Wa mwanzo kuambiwa na mkusudiwa ni Mtume wa wanadamu Muhammad (s.a.w.w) na Ahlul –bait wake (a.s). 1Baswairud-Darajaat uk: 6, na rejea Ghawaaliy liaaliy J: 3 uk: 286. 2 Kalmatullahi uk: 169 2


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 3

Fatima al-Zahra Hadithi hii na nyingine nyingi kati ya Hadithi tukufu za Qudsi, za Mtume na Maimam zilizopokelewa kuhusu jambo hili huenda kuna ugumu kwa baadhi kuzielewa au kuzistahamili, na ameshasema Imam Amirul’Muuminina Ali (a.s): “Jambo letu ni gumu mno halistahamili isipokuwa Malaika mkuruba au Nabii mursali au mja ambaye Mwenyezi Mungu ameujaza moyo wake imani”3. Jambo hili linahitaji moyo uliojaa imani na uchamungu na viwiliwili vinavyoenda mbio kwa kufanya ibada na kutii, usiku na mchana bila ya taabu, uchovu n.k. Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatma Zahra (a.s) ni kati ya mihadhara ya thamani ya Al-Imam Muhammad Al-Husein As-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehemu) - ambayo ameitoa kabla ya miaka 25, yaani 17 Jumadul-Ulaa 1400 A.H. ikawa imesambazwa na kupata umashuhuri tangu wakati huo kwa nguvu ya mvuto wake, uzuri wake, na kwa maana yake nzuri, hadi ikawa ndugu na jamaa wanapokezana kanda zake… kisha baadae ikatolewa katika njia ya maandishi, na hatimaye AlImam as-Shirazi akayarejea na akaongeza baadhi ya nukta muhimu na kutoa ufafanuzi uliohitajika…, ni kitabu kizuri kilioje, na ni haja ilioje kwa wakati huu ambao mazungumzo yamekuwa ni mengi kuhusu Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s), mijadala na midahalo imezidi juu ya shakhisiya yake tukufu na nafasi yake katika umma. Cha kuzingatia ni kwamba kumjua Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa waislamu kwani ameshasema (a.s): “Jueni kwamba mimi ni Fatma-Zahra.”4 Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini … yeye ni maasum wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha AmirulMuuminina Ali (a.s) na watoto wake maasumu (a.s).

3 Al-Khiswali uk. 624. 4 Kwa maelezo zaidi rejea (Min fiqihiz-Zahraa juz. 3, Khutba yake msikitini. 3


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 4

Fatima al-Zahra Na sisi katika taasisi yetu iitwayo Muasasatul-Kalmati litahqiyqi wanashir tumesimamia kuchapisha na kusambaza kijitabu hiki kwa kutaraji kuwa kutokana na nafasi yake tukufu awe ni kati ya waombezi wetu siku ya malipo. Amani na shukurani zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe vyote. Muasastul-Kalmat litahaqiyqi wanashir P.O Box 6080 – Shauran - Beirut – Lebanon.

4


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 5

Fatima al-Zahra

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, sala na salamu zimwendee Mtume Muhammad (s.a.w.w) na aali zake wema waliotoharika (a.s), na laana daima ziwashukie maadui zao hadi Siku ya Malipo.

AL–HADITH AL-QUDSI Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Al-Qudsi kumwambia Mtume wake Mtukufu (s.a.w.w): “Ewe Muhammad lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu, na lau kama si Ali basi nisingekuumba na lau si Fatmah basi nisingewaumba nyinyi.”5 Kuna tofauti gani baina ya Hadith Al-Qudsi na Aya za Qur’ani Tukufu? Tofauti baina yake ni katika mambo mengi, kati ya hayo ni: Changa moto: Kwani Qur’ani Tukufu ni muujiza kutoka kwa Mwenyezi Mungu, inabeba ndani yake mwongozo kamili kwa ajili ya maisha mema duniani na akhera na humo kuna muujiza na changamoto katika nyanja zote: Kielimu kifasihi kijamii kiuchumi kisiasa na katika mambo ya ghaibu 5 Rejea Kaashif liaaliy cha Al-Arandasi kama alivyonukuu As-Sayid Mir Jihaaniy katika Janatul-aswimah na Allamah Al-Mrandi katika Multaqaal Bahrain uk. 14 na Mustadraku Safinatil-Bihari Juz. 3, uk. 334 na ameinukuu Awaalimul-Ulumi uk. 26 kutoka katika Majmaun-Nurain na katika Fiqiuhiz -Zahraa Juz. 19. 5


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 6

Fatima al-Zahra Kisha changamoto haiko katika Qur’ani tu bali na kwa yule aliyeteremshiwa Qur’ani pia, naye ni Nabii Mtukufu (s.a.w.w). Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

“Sema kama watakusanyika wanadamu na majini ili walete mfano wa Qur’ani basi wasingeweza kuleta mfano wake hata kama watasaidiana baadhi yao kwa baadhi” (Sura Al-Israi: 88) Na katika Aya nyingine amesema (s.w.t):

“Au wanasema ameizua, sema leteni Sura kumi mfano wa Qur’ani zilizozuliwa kama nyinyi ni wakweli”. (Sura Hud: 13) Na katika Aya ya tatu anasema (s.w.t):

“Kama nyinyi mnashaka kwa yale tuliyoyateremsha kwa mja wetu basi leteni Sura moja mfano wa Qur’ani na waiteni mashahidi wenu wasiokuwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi ni wakweli.” (Sura AlBaqarah: 23) Hapa unadhihiri muujiza wa Qur’ani na changamoto ya Qur’ani Tukufu ambapo tangu iliposhuka hadi leo hii watu wameshindwa kuleta hata sura 6


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 7

Fatima al-Zahra moja angalau mfano wa Suratul–Kauthar. Qur’ani Tukufu inaendelea kuwa na sifa hii hadi siku ya Kiyama, na changamoto hii ipo na itaendelea kubaki milele. Na Hadith Al-Qudsi ni ile ambayo imetoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu lakini sio mahsusi kwa Mtume Muhamad tu, bali inawahusu Manabii wengine wa Mwenyezi Mungu na wala haina sifa ya changamoto na muujiza. Baadhi ya maulamaa wamekusanya kiasi kikubwa cha Hadithi Al- Qudsi katika vitabu vyao mfano:Al–Allammah Al–Majlisiy (r.a) katika kitabu chake Al-Biharul-Anwaar na katika baadhi ya vitabu vyake vingine Ndugu yangu As-Shahdi6 katika kitabu chake Kalmatu llahi. Ama neno Qudsi- lina maana ya tukufu - yaani isiyo na dosari au upungufu. Al-Hadithi Al-Qudsi ni Hadithi tukufu ambayo imeepukana na kasoro na upungufu. Hadithi Al-Qudsi ziko aina mbili: 1. Zenye njia imara ya upokezi - yaani zilizopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Maimamu (a.s) kwa sanadi sahihi na ambazo wamezipokea kutoka kwao wapokezi waaminifu. 2. Mursal sanad – yaani sanadi zake hazikuungana na mursal yake inakuwa ni dhaifu. Hivyo ambayo iko katika aina ya kwanza ndio yenye kukubaliwa na kutegemewa na Maulamaa. Ama aina ya pili, kama humo kutakuwa na 6 Ayatullah As-Shahidi As-Sayyid Hasani As-Shiraz mwasisi wa HauzatuzZainabiyah –Syria. 7


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 8

Fatima al-Zahra hekima, mawaidha na mwongozo ambao una manufaa kwa mwanadamu au hukumu isiyo ya lazima, basi itakuwa inaingia katika kanuni ya “tasaamuhu” katika hoja za Sunnah7 nk… hivyo inakubaliwa pia. Tukiongezea ni kwamba nyingi kati yake maulamaa mashuhuri wamezikubali, kuzikubali kwao na kuzifanyia kazi kunalazimu kuzitumia. Kama ilivyobainishwa katika Usul, hususan inapokuwa haizalishi hukumu ya kisheria, ambapo Hadith Al-Qudsi aghalabu zinakuja katika upande wa maadili, adabu, hekima, desturi za kijamii na mwongozo katika baadhi ya maslahi na kuhadharisha baadhi ya ufisadi wa kilimwengu, kijamii, kitabia n.k. Tukirejea mwanzo, hakika Hadithi ambayo tumeitungia kijitabu ni dalili iliyo wazi juu ya utukufu wa Ahlul–bait (a.s) na daraja zao, hususan asili ya mti wao mtukufu naye ni Fatma, baba yake, mume wake na watoto wake (a.s).

MAANA YA HADITHI Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu anamhutubia Mtume wake mtukufu (s.a.w.w) kwa kumwambia: “Ewe Muhammad lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu”. Hivyo yeye ndio lengo la kuumba. Na “Lau kama si Ali basi nisingekuumba wewe”, na “Lau kama si Fatmah Zahra basi nisingewaumba nyinyi.” Katika sharti hili la mwisho inadhihirika kwetu thamani ya Fatma Zahra (a.s) na utukufu wake kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwa Mtume wake na kwa Maimamu (a.s), fadhila kubwa aliyonayo na athari ya kisheria na kimaumbile katika kuumbwa ulimwengu na viumbe wote… 7 Rejea kitabu Risaalatu Tasaamuh fiy adilatis–Sunnah (cha mtunzi huyu) ndani ya kitabu al-Waswaailu ilaa rasaaili J: 6 cha Imam As-Shirazi. 8


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 9

Fatima al-Zahra Tumezungumzia Hadithi hii ya Al-Qudsi hasa kwa ajili ya kupata utukufu wa kutaja baadhi ya fadhila za Bibi huyu mtukufu ambaye Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema juu yake: “Binti yangu Fatma Zahra ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni.” 8 Huenda yatakuja maswali mawili katika akili za baadhi ya watu: Swali la kwanza: Je, Mwenyezi Mungu ni bakhili - Mungu atulinde na hilo – kiasi kwamba lau si Mtume (s.a.w.w) asingeumba ulimwengu, sayari, jua, mwezi na nyota? Kama si hivyo basi nini maana ya “Lau si wewe nisingeumba ulimwengu?” Katika swali hili tunauliza: Kwanza: Je, Mwenyezi Mungu ana madhumuni na lengo katika kuumba ulimwengu au hana? Jawabu: Ndio, anayo madhumuni na lengo. Pili: Lengo hilo ni lipi? Jawabu: Ni kumfikisha mwanadamu kwenye ukamilifu wa kiroho wa hali ya juu kama anavyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: “Sikuwaumba majini na watu isipokuwa waniabudu.”3 Tatu: Je ukamilifu ni jambo linalofahamika wazi kwa watu wote? Yaani katika hisia za dhahiri au zilizofichikana? Jawabu: Hakika hauko wazi kwa watu wote. Nne: Je, kuna uwezekano wa kuufikia ukweli huu au hapana? Jawabu: Kwa kawaida hakuna uwezekano wa mwanadamu kuufikia ila kwa wasila wa dalili na kiongozi. Tano: Dalili ni ipi na kiongozi ni nani? Jawabu: Dalili ni Qur’ani Tukufu na kiongozi ni Nabii (s.a.w.w), Fatma Zahra na Maimamu (a.s). 8 Amaalis-Suduqu uk. 298 Majlis No. 49 Hadith ya 12. 9


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 10

Fatima al-Zahra Kama hivyo ndivyo basi mwenye kukamilisha lengo la kuumbwa ni Mtume, Fatmah na Maimamu (a.s), hivyo kama sio wao kungekuwa na upungufu katika kuumba ulimwengu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu haumbi kiumbe chenye upungufu, kwa ajili hiyo amesema (s.w.t): “Lau si wewe nisingeumba ulimwengu…” Ama ikiwa Mwenyezi Mungu anamuumba mwanadamu bila ya kuumba dalili pamoja naye basi lengo la kuumba kwake halitatimia, na hiyo itamaanisha upungufu wa Muumbaji na kushindwa kwake – tunajilinda kwa Mwenyezi Mungu kwa hayo – na kuumbwa mwandamu kutakuwa ni upuuzi, na Mwenyezi Mungu ametakasika kutokana na upuuzi.9 Kwa msingi huu, kuumbwa Nabii Mtukufu kunakuwa ndio sababu ya kuumbwa ulimwengu huu, na kwamba cha mwanzo alichoumba Mwenyezi Mungu ni nuru ya Nabii (s.a.w.w) na Ahlul Bait wake (a.s)10 na kisha akaumba ulimwengu huu wote kutokana na nuru yao. Hivyo wao ndio sababu ya lengo la kimaumbile kama wanavyosema watu wa falsafa. Na katika Hadithil-Kisaa: “Hakika Mimi sikuumba mbingu na ardhi wala mwezi na jua, sayari hazizunguki, bahari haiendi wala meli hazitembei isipokuwa kwa ajili ya mapenzi ya hawa watano.”11 8 Amaalis-Suduqu uk. 298 Majlis No. 49 Hadith ya 12. 9 Kwa ufafanuzi rejea Qaulu sadid fiy sharhit tajiriyd katika kusudio la nne katika unabii na uimamu cha mtunzi wa kitabu hiki. 10 Yanabiul Mawadah Juz. 1 uk. 118, Shawahidut-Tanzil Juz. 1 uk. 414, Nahjul Haq cha Allamah al-Hilliy uk. 190, Tafsir Burhan cha Baharan Juz. 3 uk. 170, Nurul-Abswar, Tafsir Tha’alab katika tafsiri ya Aya ya 54 Suratul Furqan. Yanabiul Mawadah Juz. 1 Babul Awal uk. 14 pia Juz. 1 10-11, Tadhkiratul Khawaas cha Ibn Jawzi uk. 46, Kashiful Ghumah Juz. 2 uk. 84, DalailunNubuwah Juz. 2 uk. 148 nk. 11 Duau waziyarah: Hadithul kisaa pia tazama mujaladi wa 1 (min fiqihizZahraa). 10


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 11

Fatima al-Zahra Na amesema Al-Imamu Al–Mahdi (a.s): “Sisi tumeumbwa kwa ajili ya Mola wetu na viumbe wameumbwa kwa ajili yetu.”12 Na imekuja katika Biharul-Anwar ya Allammah Al–Majilisi amenukuu kutoka kwenye kitabu Al-Hidayah cha Sheikh Tusiy amesema: “Ni wajibu tuitakidi kuwa unabii ni wa kweli kama ambavyo tunaitakidi kuwa tawhid ni ya kweli na kwamba manabii ambao amewatuma Mwenyezi Mungu ni 124,000, wamekuja kwa haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu na kwamba kauli yao ni kauli ya Mwenyezi Mungu na jambo lao ni jambo la Mwenyezi Mungu na kuwatii wao ni kumtii Mwenyezi Mungu na kuwaasi wao ni kumwasi Mwenyezi Mungu; na kwamba wao hawakutamka isipokuwa yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kutoka katika wahyi wake na kwamba mabwana wa Manabii ni watano na wao ndio bora zaidi, wao ndio walipewa sheria na wao ni ulul-azmi nao ni: Nuhu, Ibrahim, Musa, Isa na Muhammad (a.s). Na kwamba Muhammad ndio Bwana wao na mbora wao na kwamba alikuja kwa haki na ameisadikisha Mitume, na kwamba wale ambao wamemwamini wakamwadhimisha, wakamnusuru na wakafuata ile nuru iliyoteremshwa pamoja naye hao ndio wenye kufaulu, na ni wajibu tuitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hakuumba kiumbe bora na kitukufu zaidi Kwake kuliko Muhammad (s.a.w.w), na baada yake ni Maimamu (a.s.), na wao ndio viumbe vipenzi zaidi kwa Mwenyezi Mungu na wa mwanzo wao kumkubali Mwenyezi Mungu, pale Mwenyezi Mungu alipochukua ahadi kwa Manabii katika ulimwengu wa kiroho na akawashuhudisha juu ya nafsi zao kwa kuwauliza: Je, yeye si ndio Mola wao? Wakasema: Ndio wewe ni Mola wetu. Na kwamba Mwenyezi Mungu alimtuma Nabii wake (s.a.w.w) kwa Manabii katika ulimwengu wa kiroho; na kwamba Mwenyezi Mungu alimpa kila Nabii aliyompa kwa kadri ya kumjua kwake Nabii wetu 12 Al-ghaibatu cha Tuusiy uk. 285 Hadith ya 7 na al-Ihtijaaj uk. 467. 11


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 12

Fatima al-Zahra (s.a.w.w) na kwa kutangulia kwake katika kumkubali. Na tunaitakidi kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu ameumba vitu vyote kwa ajili yake na Ahlul–Bait wake, na kwamba lau kama si wao basi Mwenyezi Mungu asingeumba mbingu, ardhi, Pepo na Moto wala Adam, Hawa, Malaika wala chochote katika vilivyoumbwa”13 mwisho wa kunukuu. Maneno haya yaliyonukuliwa kutoka kwa As-Suduq ni muhtasari wa Hadithi na riwayah nyingi zilizokuja kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s) zinazotueleza kwamba wao ndio msingi wa kuumbwa ulimwengu, na Mwenyezi Mungu amewajaalia kuwa ni wasila wa kuumbwa ulimwengu na sababu ya lengo lake, kama ambavyo wao (a.s) ndio sababu ya huruma ya Mwenyezi Mungu na rehema yake kwa ulimwengu na wao ndio sababu ya kuendelea kuwepo kwa ulimwengu… Na zinaeleza hayo wazi dalili mbali mbali… kama sio wao basi ardhi ingedidimia.14

SWALI LA PILI: Nini maana ya ‘Lau kama si Ali basi nisingekuumba?’ Wakati Mtume (s.a.w.w) ana shakhsiya tukufu zaidi, kwa nini kuumbwa kwake kuambatane na kuumbwa kwa Ali Amirul-Muuminina (a.s) na nini uhusiano uliopo baina yao? Jawabu la hilo ni kwamba: Uimamu ambao unapatikana kwa Amirul–muuminina ni mwendelezo wa kawaida wa kazi ya unabii, na kwamba mnyororo wa uhusiano baina ya unabii na uimamu umemfanya Amirul-Muuminina (a.s) awe ndio mwenye kukamilisha lengo la kuumbwa Mtume (s.a.w.w) kwa sababu Nabii (s.a.w.w) alikuja ili kuongaza watu na kuwafikisha katika ukamilifu unaotakikana. Lakini umri wa Nabii (s.a.w.w) ni mfupi na hakuna budi apatikane baada yake atakayeendelea kuongoza njia, tukiongezea kwamba watu wengi hawafikii kwenye 13 Biharul Anwar Juz. 16, uk. 372 Fadhail Nabii (s.a.w.w) wakhaswaiswihi. 14 Rejea al-Kaafiy Juz. 1, uk. 179, Hadith ya 10. 12


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 13

Fatima al-Zahra ukamilifu mara moja bali hatua kwa hatua. Hivyo ilikuwa hakuna budi ya kupatikana mtu mwingine kwa ajili ya kukamilisha na kuendeleza baada ya kufariki Nabii (s.a.w.w) ambaye ndio wasii wa Mtume na Imamu baada yake Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (a.s). Tukiongezea kwamba watu walifanya njama katika dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na wakapotosha Uislamu, na kama si Ali (a.s) basi isingebainika haki na batili….. kwa sababu hiyo Mwenyezi Mungu alimuumba Ali (a.s) ili asimame dhidi ya upotovu, mfarakano na ikhitilafu ambazo zitapatikana katika umma baada ya kuondoka Mtume Mtukufu (s.a.w.w). Kama sio kuwepo Amirul-Muuminina (a.s) basi juhudi yote aliyoifanya Mtume katika kueneza ujumbe wa Uislam ingepotea na watu wangerudi kwenye ujahili wa kikafiri kwa mara nyingine, na huenda upotovu na itikadi zilizo kama vile Mungu kuwa na kiwiliwili, kutezwa nguvu, taf’widh n.k, zingeenea katika ulimwengu wa Kiislamu, fikra ambazo alikujanazo Muawiya na mfano wake baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) ili kubomoa juhudi na kazi ya Nabii (s.a.w.w) ya kueneza dini tukufu ya Kiislamu, na badala yake kufuata nyendo za Muawiya na kutekeleza misingi yake, hiyo ni sawa iwe katika hukumu za kisheria au za kuamiliana pamoja na watu wengine, serikali na wananchi… hivyo isingepatikana faida inayotakikana ya kuwepo dini ya Kiislamu, na kutumwa kwa Nabii ambako hakujafikia lengo kamili, na hapo kusingekuwa na faida yeyote. Hapa inadhihirika dharura ya kuwepo Imam Ali (a.s) ambapo ilishuka Aya ya kukamilika dini kwa ajili yake siku ya Ghadir pale Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomtawaza Ali (a.s) kuwa Khalifa baada yake kwa amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu akisema (s.w.t):

“Leo nimewakamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema yangu na nimekuridhirieni Uislam kuwa dini yenu.” (Sura Al-Maidah: 3) 13


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 14

Fatima al-Zahra Imam Ali alikuwa amesimama msimamo sambamba na neno la ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuuhami na kuulinda kutokana na hila za wanafiki… Amesema (s.w.t):

“Na hakuwa Muhammad isipokuwa Mtume walishapita kabla yake Mitume, je akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu.” (Sura Ali Imran: 144) Mwenyezi Mungu kwa Aya hii tukufu amekusudia kuwa haijuzu kuacha mambo ya dini ya Mwenyezi Mungu kwa watu bila ya kiongozi, sawa awe Mtume yupo au hayupo.15 Kweli Imam Ali Amirul –muuminina (a.s) alikuwa na jukumu kubwa na la msingi katika kusimama dhidi ya nia za wanafiki, makafiri na wapotoshaji, na kuuhifadhi Uislamu kutokana na upotovu na uovu. Imepokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kwamba amesema: “Mimi nimeng’oa mzizi wa fitina na hakuthubutu yeyote asiyekuwa mimi kufanya hivyo.” 16 Na kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Nilimwona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) siku ya Fatih Makka amegandamana na pazia la AlKa’aba naye anasema: “Ee Mwenyezi Mungu niletee msaidizi miongoni mwa watoto wa ami yangu atakayeniongezea nguvu.” Jibrilu akateremka kwake akasema: “Ewe Muhammad je, Mwenyezi Mungu hajakuunga mkono kwa upanga kati ya panga za Mwenyezi Mungu ulioelekezwa kwa maadui wa Mwenyezi Mungu? Anamkusudia kwa hilo Ali bin Abu Twalib.”17 15 Rejea Majmaul Bayan cha Tabarisi Juz. 1, uk. 512-514. 16 Nahjul Balagha Khutba na. 93. 17 Biharul Anwar Juz. 1, uk. 61 mlango wa Babu 106 Hadith ya 1. 14


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 15

Fatima al-Zahra

USHAHIDI WA KIHISTORIA Muawiya bin Abu Sufian alikusanya pembezoni mwake kundi kati ya wale ambao hawamchi Mwenyezi Mungu na walikuwa ni wapenda dunia‌ basi akatengeneza kwao Uislamu mahsusi na mfumo mbaya zaidi kuliko wa kijahilia, kutokana na Uislam huu wa ki-Banii Umayyah watu wakawa wanauwana baadhi yao kwa baadhi kwa jina la dini, na katika aliyoyafanya Muawiya ni kwamba alichoma moto Waislamu arobaini elfu huko Yemeni kwa jina la dini. Na kama sio kusimama kidete Amirul-Muumina mbele ya Muawiya basi dini ya Kiislamu ingekuwa ni wasila wa kufanyia dhulma, ufedhuli, udikteta na kupora haki za wengine. Hakika akili na mantiki inaunga mkono Hadithi hii ya Al-Qudusi iliyotangulia ambapo kama sio kuja kwa Amirul- muumina na Maimam maasum (a.s) baada ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w) watu wasingejua Uislamu wa kweli, na wangedhani kuwa Uislamu ndio ule upotovu wa Banu Umayya, kiasi kwamba Bani Umayya waliufanya Uislamu kuwa ni wasila wakutumikia maslahi yao ya kidunia na kushibisha matamanio yao na shahawa zao. Na kama sio Ahlul-Bait (a.s) basi mafunzo sahihi ya dini yangefutwa na kuzimika nuru yake na zingetawala katika jamii ya Kiislamu itikadi ambazo zinamaanisha kuwa dini ndio hii dhulma ujeuri na upotovu wa kiBani Umayya, hiyo ni kwa sababu watu walioishi katika utawala wa Bani Umayya hawakuona mwendo mzuri alioufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika kujenga jamii ya Kiislamu. Je, uovu wa Muawiya na mfano wake ulikuwa ni mwendo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu? Hapana. Hakika wao walikuwa wanatangaza ufisadi na upotovu na kuwa mbali na hukumu za dini, walikuwa wanakunywa pombe, wanauwa watu wema bila ya hatia, wanavunja heshima za watu, yote hayo kwa jina la ukhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na 15


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 16

Fatima al-Zahra hawakutosheka na hilo bali walikuwa wanadai kuwa wao ni wawakilishi wa Mwenyezi Mungu duniani na kwamba vitendo vyao vyote ni sahihi na vinafuata sheria… imenukuliwa kutoka kwa Muawiya kwamba siku moja alimwambia Mughira bin Shuubah: “Humru wamezidi na nimefikiria kuuwa theluthi yao.”18

NJAMA ZAENDELEA Lakini Imam Amirul-Muuminina (a.s) alisimama imara dhidi ya mbinu ya Muawiya na kuuhifadhi Uislamu kutokana na upotovu. Ama baada ya Amirul-Muuminina kufa shahidi, ni nani atakayesimama kwa muda wote wa historia dhidi ya watawala ambao wanachezea mali za umma kwa jina la Uislamu mfano wa Bani Umayya na Bani Abbas? Kwa sababu hii kulikuwa na haja sana kuwepo Maimamu watukufu Maasum (a.s) na kama sio wao dini yote ingefutwa na kazi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) na Amirul-Muuminina ingepotea kabisa… Hapa linabainika kwetu jukumu la Fatma Zahra (a.s) kuwa ni ukweli mkuu na ni dharura mno katika hekima ya Mwenyezi Mungu katika kuumba, nayo ni ambayo inafasiriwa na kipande cha tatu katika Hadithi Al–Qudsi: “Na lau kama sio Fatma basi nisingewaumba nyinyi.” Hii ni pamoja na kuongezea kwamba Az-Zahra (a.s) alikuwa na jukumu la msingi katika kuwafedhehesha wale waliotawala kwa jina la Uislamu, na kama sio msimamo wake imara basi waislamu wa kawaida wangechanganyikiwa… hivyo yeye alikuwa kati ya waliohifadhi dini ya Mtume wa Mwenyezi Mungu punde tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). 18 Humru –Yaani Humraau: Hao ni walioingia katika Uislamu baada ya kutekwa, na katika kamusi imeandikwa: al-Mawaaliy na al-Humrau ni yeyote asiye kuwa Mwarabu. 16


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:27 PM

Page 17

Fatima al-Zahra

UTUKUFU WA ZAHRA (AS) Fatmatuz-Zahraa (a.s) ana jukumu kubwa katika kujenga na kuipa nguvu misingi ya dini ya Kiislamu na kuimarisha nguzo zake, ambapo anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Al–Qudsi: “Na lau kama si Fatma nisingewaumba nyinyi”, hivyo Fatma Zahra ni zawadi ya Mwenyezi Mungu na tuzo la uchamungu kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.w)19 na neema nyingi, naye ndio siri ya Uimamu na kitovu cha kuumbwa Maimamu maasum (a.s) ambapo yeye ndio ameupa uhai, nuru na amesimamisha dini ya haki kupitia kwa watoto wake na misimamo yake ya kihistoria… hadi leo hii unaona Uislamu umehifadhika kwa fadhila za kupatikana kwake na kwa kuwepo Imam Al-Mahdi (a.s), yeye ni baraka katika baraka za Fatma (a.s). Kuna Hadithi nyingi mutawatir zinazoelezea nafasi ya Zahra (a.s) na zimepokewa na pande mbili katika vitabu vyao mbalimbali. Kama ambavyo kutukuza cheo chake Zahra (a.s) ni kutukuza hadhi ya unabii na dini ambayo ameiteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu.

ZAHRA (A.S) NI NURU YA MWENYEZI MUNGU Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): “Mwenyezi Mungu aliumba nuru ya Fatma (a.s) kabla ya kuumba mbingu na ardhi” (Maelezo yake yameshepita hapo juu). Baadhi ya watu wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, je yeye si 19 Hii nikuashiria kauli yake (s.w.t): “Hakika sisi tumekupa kheri nyingi” Suratul Kauthar:1. 17


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 18

Fatima al-Zahra mwanadamu?” Akasema: “Fatma ni Hurul’aini wa kibinadamu.” Wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, vipi yeye ni Hurul’aini wa kibinadamu?” Akasema: “Mwenyezi Mungu amemuumba kutokana na nuru yake kabla ya kumuumba Adam ambapo alikuwa ni roho, Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam akamuonyesha kwake.” Wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu Fatima alikuwa wapi?” Akasema: “Alikuwa chini ya Arshi.” Wakasema: “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu, chakula chake kilikuwa nini?” Akasema: “Tasibihi, tahalili na tahamid, Mwenyezi Mungu alipomuumba Adam na akanitoa katika mgongo wake Mwenyezi Mungu akapendelea kumtoa yeye katika mgongo wangu, akamjaalia kuwa tufaha katika pepo, na Jibrilu (a.s) aliniletea akaniambia: ‘As-salam alaika warahmatullahi wabarakatuhu ewe Muhammad.’ Nikasema, waalaika salamu warahmatullahi wabarakatuhu ewe kipenzi changu Jibril. Akasema: ‘Ewe Muhammad hakika Mola wako anakusalimia.’ Nikasema: Amani inatoka kwake na kwake inarejea. Akasema: ‘Mwenyezi Mungu amekupa zawadi ya tunda hili kutoka peponi.’ Nikalichukua na nikalikumbatia kifuani mwangu. Akasema: ‘Ewe Muhammad, Mwenyezi Mungu anasema ulile. Basi nikalipasua nikaona nuru angavu nikaogopa kwayo. Akasema: ‘Ewe Muhammad una nini mbona huli? Lile na wala usiogope kwani hiyo ni nuru ya Mansurah mbinguni, na katika ardhi ni Fatmah.’ Nikasema kipenzi changu Jibril kwa nini ameitwa Mansurah mbinguni na ardhini akaitwa Fatma? Akasema: ‘Ameitwa Fatma ardhini kwa sababu wafuasi wake wataepushwa na moto, na maadui zake wamenyimwa mapenzi yake. Na katika mbingu ni Mansurah nayo ni kauli yake (s.w.t):

“Katika miaka michache. Amri ya Mwenyezi Mungu kabla yake na 18


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 19

Fatima al-Zahra baada yake. Na siku hiyo watafurahi waumini kwa nusura ya Mwenyezi Mungu, anamnusuru amtakaye naye ni mwenye nguvu, mwingi wa rehema” (Sura Rum: 4 -5) Yaani nusura ya Fatma kwa wanaompenda.’”20 Na marehemu baba yangu21 alitunga kaswida nzuri na ndefu katika uzao wake mtukufu na hizi ni baadhi ya beti zake: Johari imechomoza kwa uzuri wa nuru yake, Dunia ikaangaza kwa nuru yake, Ulimwengu umeangaza kwa nuru ya miali yake, Kwa nuru ya miali yake imeangaza sehemu zake, Mwanga mzuri ulioje, ukatoa nuru na nuru yake, Imeongoa wanadamu kwa uongofu wake.

BIBI MBORA WA WANAWAKE WA ULIMWENGUNI Zahra (a.s) katika mwanzo wa kujenga jamii ya Kislamu Madina alikuwa ni mdogo kwa umri, bado hajafikia miaka minane ila alikuwa na fahamu na utambuzi wa elimu ya kiuchamungu, ya kidini na umaasumu kamili, kiasi kwamba alitekeleza jukumu muhimu katika ukuaji wa jamii mpya ya Kiislamu, alisifika kwa ikhilasi yake, kufuatilia kwake matukio na uelewa wake wa ujumbe wa mbinguni, pamoja na kuwepo wanawake wengine katika nyumba ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w), lakini yeye alipata cheo cha juu kitukufu kwa Mwenyezi Mungu na katika jamii ya Kiislamu. Hiyo ni kutokana na kuteuliwa kwake na Mwenyezi Mungu, ikhilasi yake, ibada yake, ukarimu wake, jihadi yake, zuhudi yake, subira yake na uvumilivu wake katika njia ya Mwenyezi Mungu. 20 Ma’anil –Akhibar uk. 396 na 397. 21 Ni Ayatullahi Al-Udhnaa Mirzaa Mahdi As-Shirazi. 19


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 20

Fatima al-Zahra Alitekeleza majukumu aliyokuwa nayo kwa njia nzuri mno, hivyo akastahiki kuwa ni Bibi mbora wa wanawake wa ulimwengu kwa wa mwanzo na wa mwisho. Katika Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Fadhili alisema: Nilimwambia Abu Abdillahi (a.s) nieleze juu ya kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) kuwa yeye ni Bibi mbora wa wanawake, je ni wa ulimwengu wake tu? Akasema: “Huyo ni Mariam, yeye alikuwa ni Bibi mbora wa wanawake wa ulimwengu wake tu. Lakini Fatma ni bibi mbora wa wanawake wa ulimwengu kwa waliotangulia na wajao.”.22 Hivyo Fatma Zahra (a.s) amestahiki kuwa kuwepo kwake ni sharti la kupatikana Mtume (s.a.w.w) na Amirul-Muuminina Ali (a.s) kama ilivyokuja katika Hadithi Al–Qudsi, ambapo yeye alikuwa na jukumu la kukamilisha na kutimiza katika kujenga jamii ya Kiislamu, na kutimiza lengo la kuumbwa wanadamu na Mtume Mtukufu, ambapo lau si Fatma Maimamu wasingeumbwa kutoka katika kizazi cha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika ulimwengu huu. Na kukosekana Maimamu ina maana ya kubatilika kuwepo kwa Nabii, na kubatilika kuwepo kwa Uislamu kwa pamoja, na haya mawili kwa umuhimu wake yanasababisha kubatilika kuwepo wanadamu vile vile… hivyo basi kama sio Fatma (a.s) kusingepatikana mwendelezo wa (kazi) ya Nabii na kuifanya idumu, hivyo yeye (a.s) ndio siri ya Uimamu tukiongezea yaliyotangulia katika kusimama kwake dhidi ya njama ambazo zilitokea baada ya Nabii (s.a.w.w).

KIGEZO NA MFANO MWEMA Hakika anayefuatilia maisha ya Bibi Fatma Zahra (a.s) anakuta kuwa yeye ni chuo kamili katika nyanja mbalimbali za maisha… hivyo anapasa kuwa ni kigezo chema kwa wanawake wote, bali hata kwa wanaume pia. Yeye ndiye aliyesimama pamoja na baba yake katika kutangaza Uislamu, amevumilia adha za washirikina wa kikuraishi pamoja na kundi dogo la wau22 Ma’anil- Akhibar uk. 107. 20


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 21

Fatima al-Zahra mini katika shi’ab (bonde) la Abu–Talib, amevumilia mateso ya kuhama toka Makka kwenda Madina… pia amesimama kidete pamoja na Amirul– Muuminina (a.s) ambaye aliimarisha misingi ya Uislamu… hivyo alikuwa ni kati ya waliohama na kupigana jihadi. Vilevile amevumilia uchungu na ugumu wa nyakati ngumu kwa kuipa kwake kisogo dunia na kuchagua akhera, kama ambavyo aliolewa na Amirul–Muuminina ili kushirikiana naye katika kuimarisha ujumbe pamoja na Uimamu, kuimarisha nguzo za jamii ya Kiislamu na kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu sambamba na baba yake na mume wake ambaye alitoa nafsi yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu… na huu ni mfano mwema watakaouiga wanawake wa ulimwenguni.

MAISHA YA NDOA Yeye pia aligawana majukumu ya maisha ya ndoa na Imam Ali (a.s), majukumu ya ndani ya nyumba yalikuwa ni juu yake na ya nje yalikuwa juu ya mume wake. Kutoka kwa Abu Jaafar (a.s) amesema: “Hakika Fatma alichukua dhamana kwa Ali ya kazi za nyumbani, kukanda unga, kuoka mikate na kusafisha nyumba, na Ali akachukua dhamana kwake kwa yaliyo nje ya nyumba kuleta kuni na chakula. Siku moja Ali alimwambia: “Ewe Fatma je, unachochote?” Akasema: “Hapana… naapa kwa aliye tukuza haki yako hatukuwa na chochote tangu siku tatu tunachoweza kukukirimu kwacho.” Akasema: “Kwa nini hukuniambia?” Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alinikataza kukuomba chochote. Aliniambia usimuulize mtoto wa ami yangu chochote, akikuletea chochote pokea vinginevyo usimuulize.”’

21


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 22

Fatima al-Zahra Abu Jaafar (a.s) akasema: Imam Alitoka akakutana na mtu akamkopa dinari kisha akarejea nayo na wakati wa jioni umeshaingia, akakutana na Miqdad bin al-Aswad akamwambia Miqidad: “Nini kimekutoa katika wakati huu? Akasema: “Njaa, naapa kwa aliye tukuza haki yako ewe Amirul-muuminina.” Mpokezi amesema: “Nilimuuliza Abu Jaafar Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa hai?” Akasema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa hai. Imam Ali akamwambia Miqdad: “Mimi pia njaa imenitoa nimekopa dinari na nitakupa, akampa akarejea akamkuta Mtume wa Mwenyezi Mungu amekaa na Fatma (a.s) anaswali na baina yao kuna kitu kimefunikwa, alipomaliza akaleta kile kitu wakakuta vipande vya mikate na nyama. Akasema: “Ewe Fatma hivi umevitoa wapi?” Akasema: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu anamruzuku amtakaye bila ya hisabu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akamwambia nikueleze aliye mfano wako na aliye mfano wake?” Akasema: Nieleze. Akasema: Mfano wako ni mfano wa Zakaria alipoingia kwa Mariam katika mihrabu akamkuta ana chakula, akasema: “Ewe Mariam umekitoa wapi? Akasema: ‘Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu hakika Mwenyezi Mungu anamruzuku amtakaye bila ya hisabu. 23 Wakala (chakula hicho) kwa muda wa mwezi mmoja, nacho ni chakula anachokula Al-Mahdi (a.s) nacho kipo kwetu.24

UKARIMU WAKE Kati ya sifa zingine alizokuwanazo Fatma Zahra (a.s) na ambazo zinapasa ziwe ni funzo katika jamii na umma wowote unaotaka kuendelea ni zuhudi, ukarimu, kutoa kwa wingi, subira na tabia nzuri iliyotukuka. Kisa cha kulisha chakula ambacho kimepokewa katika Qur’ani tukufu katika Suratud-Dahri ni ushahidi mzuri juu ya hilo ambapo walitoa chakula chao pekee na ambacho ni vipande vya mikate tu kwa watu watatu, kwa muda 23 Hii ni ishara ya kauli yake (s.w.t) katika Suratul Al-Imran: 37. 24 Tafsirul Ayashi Juz. 171 na 172. 22


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 23

Fatima al-Zahra wa siku tatu mfululizo wakabaki na njaa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu na hiyo ni baada ya kuweka nadhiri ya kufunga kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wakipona Hasan na Husein (a.s) kutokana na maradhi waliyougua, walipokaa tayari kwa kufuturu mlango uligongwa na maskini, wakatoa vipande vya mikate yao kwa maskini na wakalala njaa, vivyo hivyo walifanya siku ya pili kumfanyia yatima na katika siku ya tatu mambo yalijirudia kwa mateka. Hivyo Mwenyezi Mungu aliteremsha sura kamili kwa ajili yao nayo ni Suratud–Dahri, na miongoni mwayo ni Aya hizi:

“Na wanawalisha chakula maskini, yatima na mateka hali ya kuwa wao wanakihitaji.” (Surat Insaan: 8.) Na kisa hiki kimepokelewa pia na Masuni.25

MIONGONI MWA IBADA ZAKE Vilevile Fatma Zahra alikuwa anamcha Mwenyezi Mungu kwa ikhilasi na imani ya juu ambapo moyo wake ulikuwa ni chemchemu yenye kububujika kwa kumjua Mwenyezi Mungu na kufungamana Naye. Amesema Imam Hasan (a.s): “Nilimuona mama yangu hali akiwa amesimama kwenye mswala wake usiku wa Ijumaa basi aliendelea kurukuu na kusujudu hadi yakakaribia mapambazuko ya asubuhi, na nilimsikia anawaombea waumini kwa kuwataja majina yao na kuwaombea dua kwa wingi na wala haiombei nafsi yake chochote…Nikamwambia: “Ewe mama yangu kwa nini huiombei nafsi yako kama unavyowaombea wengine?” Akasema: “Ewe mwanangu jirani kwanza kisha nyumbani.” 26 25 Rejea Fatumatuz-Zahraa (a.s) fiyl Qur’an uk. 313 kwa kunukuliwa kutoka katika tafsirur Ruhulmaan Juz. 92 na uk. 157. 26 I’lalus-Sharau uk, 181. 23


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 24

Fatima al-Zahra

KATIKA ELIMU YA ZAHRA (AS) Na kati ya sifa zingine alizojipamba nazo Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ambazo ni wajibu kwa waislamu waume kwa wake wachukue kigezo kwake, nayo ni elimu… Ambapo alikuwa ni mjuzi, kwani alikuwa anapata elimu kutoka katika mji wa elimu naye ni Mtume (s.a.w.w) na kutoka katika mlango wa mji wa elimu naye ni Ali (a.s).27 Hivyo yeye anamjua Mwenyezi Mungu na anajua uhakika wa ulimwengu na falsafa ya maisha kama ambavyo kuwa kwake karibu na msikiti wa Nabii kulimpa fursa ya kufuatilia sheria za Mwenyezi Mungu na kusoma Aya zake Tukufu, hii ni pamoja na kwamba yeye alikuwa na elimu ya tabia njema. Nafasi yake tukufu na elimu yake nyingi imemuwezesha kulea, kufundisha na kuelekeza wanawake wa ulimwengu katika kila mji na kila zama, hususan wanawake wa ulimwengu wake ambao walikuwa wakikusanyika kwake na kuchukua elimu ya Kiislamu na walikuwa wanamuuliza kila kitu. Zahra alikuwa mwalimu na mlezi hata kwa wanaume kwa kupitia kwa wanawake. Kutoka kwa Imamu Hasan Al-Askari (a.s) amesema: “Mwanaume alimwambia mke wake: “Nenda kwa Fatma Binti Rasulillah muulize juu yangu, kuwa mimi ni katika wafuasi wao au sio katika wafuasi wao?” Akamuuliza. Akasema (a.s): “Mwambie kama anafanya tuliyomwamuru na anaacha tuliyomkataza basi yeye ni katika wafuasi wetu vinginevyo hapana.” Akarejea na akampa habari. Akasema: “Ole wangu nani ataniokoa kutokana na dhambi na makosa? Hivyo mimi nitakaa motoni milele, kwani asiyekuwa katika wafuasi wao atakaa motoni milele.” Mke wake akarejea na akamwambia aliyoyasema mume wake. Fatma (a.s) akasema: 27 Ni kuashiria Hadith isemayo “Mimi ni mji wa elimu na Ali ni mlango wake anayetaka elimu basi aeindee kupitia katika mlango wake.” Uyunul-Akhbar uk: 233. 24


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 25

Fatima al-Zahra “Mwambie sivyo, wafuasi wetu ni kati ya watu bora mno peponi na kila anayetupenda na mwenye kuwapenda wanaotupenda na mwenye kuwachukia maadui zetu na mwenye kujisalimisha kwa moyo wake na ulimi wake kwetu sio katika wafuasi wetu kama watakhalifu maamrisho yetu na makatazo yetu katika madhambi mengine, wao pamoja na hayo lakini wataingia peponi, lakini ni baada ya kutakaswa kutokana na madhambi yao kwa balaa na misiba au kwa adhabu ya Kiyama kwa aina za mateso yake, au katika tabaka la juu la moto wa Jahannam na adhabu zake, hadi tutakapowaokoa kwa mapenzi yetu kutoka kwayo na kuwaleta kwetu.�

HOTUBA YAKE MSIKITINI Kati ya mambo muhimu yaliyobakia kwetu kutoka kwa Bibi Fatma Zahra (a.s) ni hotuba yake aliyoitoa msikitini ambayo ni mchanganyiko wa elimu mbalimbali na maarifa mengi, na hotuba hiyo inahitaji mijaladi mingi ili kuielezea. Kama ambavyo kupitia hotuba yake na misimamo yake alitoa mwongozo sahihi kwa vizazi vijavyo hadi Siku ya Kiyama.

SHAHADA NA UCHUNGU Baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) Fatma alikuwa anaishi pamoja na mume wake Imam Amirul -Muuminina Ali (a.s) katika daraja la juu kabisa la jihadi kwa ajili ya kuhifadhi dini ya Kiislamu na ujumbe wa Mwenyezi Mungu, ambao Mtume wa mwisho na Mbora wa viumbe, ameutangaza na kuimarisha misingi yake, hivyo majukumu yao ni makubwa zaidi na muhimu baada ya kuondoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). Fatma hakutazama matukio kama ni kitu cha kupita tu, bali alikuwa anasimama dhidi ya udikteta na ukandamizaji, na alikuwa anazingatia msimamo wa watu kuwa ni hatua au mwanzo wa kurudi nyuma na kuuhesabu kuwa ni kuzima maendeleo ya Kiislamu yenye 25


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 26

Fatima al-Zahra kukua, msimamo wake huu ulikuwa ndio mwanzo wa jihadi na kufa shahidi ambao uliendelea hadi kwa watoto wake na kizazi chake, jihadi ya Imam Husein Bwana wa Mashahidi (a.s) kule Karbala na kufa kwake shahidi ni mlolongo wa msimamo wa Fatma wenye kuendelea dhidi ya kupotosha Uislamu. Misimamo hii ya kishujaa iliathiri sana afya yake hadi alipata majeraha mengi baada ya maadui kuvamia nyumba yake na kilichofuatia baada ya hapo ni kuvunjwa ubavu wake na kuharibika kwa mimba ya Muhsin Shahidi. Hiyo ilikuwa ndio sababu ya kufa kwake shahidi naye akiwa na umri wa miaka kumi na nane. Imekuja katika riwaya kuwa, Fatma–Zahraa aliugua sana kwa muda wa siku arobaini hadi alipofariki (a.s). Alipohisi dalili ya kufa kwake alimwita Ummu Amina na Asma binti Umais na akamtuma kwa Ali na akamleta, akasema (a.s): “Ewe mtoto wa ami yangu, hakika mimi naona dalili za kuondoka na mimi sioni kwa niliyonayo isipokuwa ni mwenye kumfuata baba yangu baada ya punde kidogo, na mimi nakuusia mambo ambayo yapo katika moyo wangu…”28 Imam baada ya kusikiliza wosia wake na miongoni mwayo ni kumuoa Umaamah baada yake, na amtengenezee jeneza, na asishuhudie yeyote jeneza lake ambaye amemdhulumu na kupora haki yake, azikwe usiku na kwa siri… Naye akamwambia, kama ilivyo katika riwaya; “Ewe binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, umeitoa wapi habari hii na wahyi umeshakatika kwetu?” Akasema: “Ewe Abul-Hassan nilikuwa nimelilala, mara nikamuona kipenzi changu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) katika kasri ya durr nyeupe, aliponiona akasema: “Njoo kwangu ewe binti yangu kwani mimi ninahamu kukutana na wewe.” Nikasema: “Wallahi mimi ninahamu ya kukutana na wewe zaidi kuliko wewe. “Akasema wewe utakuwa kwangu usiku wa leo, naye ni mkweli kwa aliyoyaahidi na ni 28 Tafsirul-Imam Hasan al-Askari (a.s) uk. 308. 26


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 27

Fatima al-Zahra mwenye kutekeleza aliyoyaahidi.”29 Fatma Zahra alikufa shahidi usiku wa Jumapili hali akiwa kadhulumiwa, baada ya kupita siku tatu za Jamadil-Aakhar mwaka wa kumi na moja hijiria akiwa na umri wa miaka kumi na nane na miezi saba, yaani baada ya kufariki baba yake kwa miezi mitatu… hivi ndivyo ilivyokuja katika baadhi ya riwaya… na katika riwaya zingine ni kwamba alifariki tarehe 13 Jamadil-Awwal. Pamoja na kwamba alifariki dunia katika umri mdogo lakini amebakia hadi leo hii kuwa ni chuo kwa vizazi vijavyo na taa yenye nuru, anaangaza upotovu, udikteta na anang’oa madiketa dhalimu na anasimama dhidi ya kila anayetaka kuzima mafunzo ya dini hii tukufu. Umma unapata somo na mazingatio kutokana na misimamo yake na ushujaa wake kama ambavyo unajifunza somo na mazingatio kutokana na misimamo ya watoto wake ma’asum, kwa ushujaa wao na kubeba kwao majukumu ya Uislamu ambapo wameutetea kwa upeo bora wa kuutetea. Na wanadamu bado wangali wanangojea kudhihiri kwa Swahib Zaman AlImam Al-Mahdi (a.s) ili kuwaokoa kutoka katika makucha ya wakandamizaji na madikteta, udhalimu na uadui ili aeneze uadilifu wa Kiislamu pembe zote za ulimwengu na kukamilisha lengo ambalo kwa ajili yake ameumbwa Nabii (s.a.w.w), Amirul-Muumina (a.s) kwa kueneza uadilifu, amani na uongofu katika sehemu zote za ardhi. Na katika yaliyotangulia zinadhihiri baadhi ya dalili za kauli za Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Hadithi Al–Qudsi: “Ewe Ahmad lau kama si wewe basi nisingeumba ulimwengu na lau kama si Ali basi nisingekuumba wewe na lau kama si Fatma basi nisingewaumba nyinyi.” Kama sio Fatma basi asingepatikana Al-Hujjah (Al-Imam Al-Mahdi) na Maimamu wengine (a.s)… na kama sio wao basi kusingekuwa na uadilifu, 29 Rejea Min fiqihiz Zahraa Juz. 2 na Juz. 3 na Juz. 4, katika hotuba ya Zahraa (a.s). 27


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 28

Fatima al-Zahra amani wala dini. Rehema na amani ziwe juu yako ewe Fatma; na ziwe juu ya baba yako, mume wako na watoto wako wema. Amani iwe juu yako ewe Bibi wa wanawake wa ulimwenguni. Amani iwe juu yako ewe mama wa Maimam wa watu wote. Amani iwe juu yako ewe uliyedhulumiwa haki yako. Ewe Mwenyezi Mungu mrehemu mja wako binti wa Nabii wako. Mke wa wasii wa Nabii wako, amani itakayomnyanyua daraja, Daraja juu ya daraja ya waja wako wema, Miongoni mwa watu wa duniani na mbinguni.�30

Huu ndio mwisho wa tuliyokusudia kuyabainisha katika kitabu hiki, tunamuomba Mwenyezi Mungu ayakubali kwani yeye ni mwenye kusikia maombi. Ametakasika Mola wako, Mola Mwenye enzi na yale wanayomsifu, rehema na amani iwashukie Mitume, na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, na rehema na amani zimshukie Muhammad na aali zake wema.31 Qum tukufu Muhammad As- Shirazi.

30 Biharul Anwar Juz. 43, Uk. 191 hadith ya 20 chapa ya Beiruti. 31 Biharul Anwar Juz. 43, Uk. 179 hadith ya 15, chapa ya Beiruti.

28


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 29

Fatima al-Zahra

FATWA KUHUSU FATMA ZAHRA (AS) Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu. Kwa Ayatullahi Al-Udhuma As-Sayid Muhammad Al–Husein As-Shirazi Assalam alaikum. Tafadhali tunaomba utupe fatwa ya mas’ala yafuatayo ambayo huwa yanaulizwa sana siku hizi katika baadhi ya jamii na Mwenyezi Mungu awape malipo mema. Swali la 1: Je Nabii (s.a.w.w), binti yake Fatma Zahra (as ) na Maimamu kumi na wawili (a.s) ni ma’asum? Je, uma’asumu wao ni upi? Ni kwa maasi tu, au hata katika kukosea na kusahau, au ni kwa hayo pamoja na kulala usingizi mzito unaoshinda usikivu hadi kupitwa na Swala? Jawabu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Assalamu alaikum warahamatullah wabarakatuh Nabii Mtukufu, binti yake Fatma Zahra, Amirul-Muumina na Maimamu kumi na moja wanaotokana na kizazi chake wote ni ma’asum wamehifadhiwa kutokana na maasi ya aina zote, kusahau na kutokana na usingizi unaoshinda usikivu hadi wakati wa Swala upite. 32 Bali wao ni ma’asum hata katika kuacha mambo ambayo sio wajibu lakini yana fadhila, na tumezungumza katika dalili za kiakili na za kunukuu kuhusu uma’asum huu katika sehemu mbalimbali za vitabu vyetu katika misingi ya akida na fiqih. 32 Mafatihul jinaan na ziara ya Zahraa. 29


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 30

Fatima al-Zahra Swali la 2: Daraja ya uma’asum kwa ma’asumu kumi na nne ni sawa au inatofautiana? Jawabu:

Daraja ya uma’asumu wao ni moja na inalingana.

Swali la 3: Mmetaja katika kitabu chenu Min fiqihiz-Zahraa zaidi ya mara moja kwamba Zahra ana daraja kubwa je, ni upi mpaka wa daraja lake, je linapita daraja la Maimam wote au baadhi yao au ni Maimam wanaompita kwa daraja? Jawabu:

Ndio Fatma ana daraja la juu lakini liko chini ya daraja la baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu na linalingana na daraja la mume wake Amirul-Muuminina Ali (a.s) na liko juu ya daraja la watoto wake kumi na moja (a.s).

Swali la 4: Vile vile mmetaja katika kitabu chenu baadhi ya matukio ambayo yalitokea baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w) je, ni upi mtazamo wenu humo? Jawabu:

Qur’ani Tukufu imeeleza hayo ambapo imesema: “Je, akifa au akiuliwa mtarejea nyuma kwa visigino vyenu?” (Surat Aali Imran: 144).

Swali la 5: Je, Fatma Zahraa (a.s) ni shahidi? Kwani mmetaja katika kitabu chenu kuwa alikufa shahidi. Jawabu:

Ndio yamepokewa hayo katika riwaya sahihi na pia imetajwa katika vitabu vya historia.

Swali la 6: Je, yeye alikuwa ni Swidiqah? Kama Qur’ani ilivyosema juu ya Mariam binti Imran kwamba yeye alikuwa Swidiqah, Jawabu: Ndio imepokewa katika athari zinazozingatiwa kwamba yeye alikuwa Swidiqah na ndio maana alioshwa na 30


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 31

Fatima al-Zahra Amirul–muuminina Ali ibn Abu Talib ambaye anafanana naye katika daraja licha ya kuwepo mwanamke ambaye angeweza kumuosha, kwani As-Swidiqah hawezi kuoshwa isipokuwa na As –Swidiq, na yeye ni bora kuliko Mariam kama zilivyoeleza wazi hayo riwayah ambazo ni mutawatiri. Swali la 7: Nini maoni yenu katika historia zilizotaja kupigwa kwa Fatma Zahraa, kuporwa Fadak yake, kubanwa kwake baina ya mlango na ukuta na kuharibiwa mimba ya Muhsin n.k ? Jawabu:

Hayo yote yamethibiti na ni sahihi.

Swali la 8: Nini mtazamo wenu juu ya uongozi wa kimaumbile na kisheria wa ma’asum kumi na nne kwa ujumla, na hususan kwa Fatma Zahra, na mmeshaeleza hayo katika kitabu chenu Min fiqihz- Zahraa (a.s) ? Jawabu:

Dalili nyingi zinazozingatiwa zimeunga mkono hayo kwamba Fatma Zahra na ma’asum wengine wote (a.s) wana uongozi wa kimaumbile na kisheria, na imekuja katika ziara ya Imam Al-Husein (a.s) ambayo amesema kwayo Sheikh AsSuduq kwamba ni ziara sahihi zaidi katika mapokezi yafuatayo: “Matakwa ya Mola katika makadirio ya mambo yake yanateremka kwenu na yanatoka katika nyumba zenu na ni yenye kutokana na yale yaliyohukumiwa kwa waja.”

Swali la 9: Nini mtazamo wenu kuhusu Raja’ah, asili yake, nasaba yake na ni kwa nani kati ya ma’asum? Jawabu:

Raja’ah imethibiti kwa dalili zinazozingatiwa na asili yake ni katika Qur’ani Tukufu na nasaba yake ni kwa Ma’asum wote kumi na nne (a.s), na itaanza baada ya kudhihiri Imam wa kumi na mbili Al-Mahdi (a.s). 31


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 32

Fatima al-Zahra Swali la 10: Je, dalili juu ya Imam Mahdi inatofautiana na dalili ya Maimam wengine? Jawabu:

Hapana … haitofautiani, kuna dalili zinazofanana katika Uimam wa Maimam kumi na mbili (a.s), nazo ni makumi ya Aya za Qur’ani ambazo zimefanyiwa taawili kulingana na riwaya mutawatir, dalili za kiakili kuhusu Maimam kumi na mbili, na kuna dalili mahususi za kunukuu juu ya uimamu wa kila mmoja kati ya Maimam kumi na wawili (a.s), na vilevile Imam Mahdi kwani zimepokewa riwaya maelfu katika mamia ya vitabu, zaidi ya hapo ni dalili za kiakili juu ya uimam wake.

Swali la 11: Hadithi tukufu iliyopokewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Maimam baada yangu ni kumi na wawili” ni mutawatiri kwenu? Je, kuna shaka yeyote juu ya kuzaliwa Imam wa kumi na mbili ambaye ni Imam Al–Mahdi (a.s)? Jawabu:

Hadith hii ni mutawatir na wala hakuna shaka katika kuzaliwa kwa Imam wa kumi na mbili, na dalili juu ya hilo ni nyingi kwani kama sio kuwepo kwa Al-Hujjah basi ardhi ingeteketea pamoja na watu wake na kwamba kama kungekuwa na watu wawili wanaoishi ardhini basi mmoja wao angekuwa ndio Al-Hujjah kulingana na ilivyopokewa juu ya hilo riwaya mbalimbali ambazo ni mutawatir.

Swali la 12: Mmetaja katika kitabu chenu Min fiqihz-Zahraa kuwa Fatmatuz-Zahraa (a.s) alijali sana na kutetea uongozi wa mume wake, Imam Amirul-Muuminina Ali (a.s) na watoto wake kumi na mmoja, je ni upi mpaka wa hilo? Je, hayo ni wajibu kwetu katika wakati huu? Jawabu: Fatma Zahra (a.s) alikuwa mtetezi wa mwanzo baada ya 32


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 33

Fatima al-Zahra baba yake Nabii (s.a.w.w) wa Uimam wa Amirul-muuminina Ali bin Abi Talib (a.s) na katika njia hii amejitolea yeye binafsi pamoja na mwanae Muhsin na hakuacha fursa yeyote ambayo kwayo angeweza kunusuru uimamu wa AmirulMuuminina na kuthibitisha haki yake isipokuwa aliitumia, na ni wajibu kwa waumini kuiga mfano kwake (a.s) na hiyo ni kulingana na zama na sehemu na kulingana na masharti yaliyotajwa katika vitabu vya fiqihi, kwani kila kitendo, kauli na ridhaa yake ni hoja ya kisheria. Swali la 13: Mmetaja katika kitabu chenu kuwa ni Sunna kusimulia hotuba yake ya Fadak kutokana na kupokelewa kwake kwa wingi katika riwaya za Ma’asum (as ), je ni Sunna kutaja kila kinachohusiana na Fatma Zahra (a.s) kati ya yaliyotokea juu yake baada ya baba yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)? Jawabu:

Ndio yote hayo ni Sunna, na hayaepukani ima kuwa ni kauli yake au kitendo chake au ridhaa yake, na yote ni hoja kama tulivyotaja, na ambayo yako nje na hayo ambayo yanaambatana na fadhila zake na sifa zake (a.s), basi hakuna mushikeli katika Sunna kwa kuyataja, kuyanukuu na kuyaeneza bali inaweza kuwa ni wajibu kama yatakuwa yanahusiana na wajibu katika kuamrisha mema, kulingania kheri na kueneza dini tukufu.

Swali la 12: Mmetaja katika juzuu ya kwanza ya Min fiqihiz–Zahra kwamba yeye ni kati ya ambao Mwenyezi Mungu amefaradhisha kutiiwa na viumbe wote, na mmetoa ushahidi wa baadhi ya riwaya, je hizi riwaya kwa mtazamo wenu ni zenye kuzingatiwa? Kwa ihsani yenu tunaomba majibu na Allah swt. awalipe kila la kheri. Jawabu: Ndio hakika hizi riwaya zinazingatiwa na tumetia mkazo kati33


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 34

Fatima al-Zahra ka kuzingatiwa kwake katika kitabu kilichotajwa, na vilevile tumetaja dalili zingine kama ambavyo tumeeleza ufafanuzi wa baadhi ya yaliyotajwa katika kitabu chetu Fiqihul–Ba’iu) na katika vitabu vyetu vingine vingi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu atujalie kuwa ni katika kundi linaloshikamana na Fatma Zahra, baba yake, mume wake na watoto wake (a.s), na tuwe kati ya waliojitenga na maadui zao, na atujaalie kuwa kati ya wanaotaja fadhila zao, kueneza Sunna zao na kutangaza hazina ya elimu yao, na tuwe ni wenye kufaulu kwa kuwapenda wao duniani na akhera hakika Mwenyezi Mungu yuko karibu na ni Mwenye kujibu maombi. Wasalaam alaikum warahmatu-llahi wabarakatuh. Muhammad As-Shirazi.

34


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 35

Fatima al-Zahra

BIBLIOGRAFIA Al – Qur’ani. Nahjul-Balagha. Al-aamaal cha Sheikh As Suduq. Al-Ihtijaaj cha Twabarsi. Al-Jannatul asim cha Mir Jihaan. Al-Khisal cha Sheikh Suduq. Ad Duau wa Ziyaarah cha Imam As-Shirazi. Al–Ghaibah cha Sheikh Suduq. Al-Qaulu Sadid fiy sharh At Tajirid cha Imam As Shirazi. Al–Kaafi cha Sheikh Kulain. Al–Wasail ilaa Rasail cha Imam Shirazi. Biharul–Anwar cha Allammah Al – Majilsi. Baswairu Darajaat cha Safarul-Qummi. Tafsirul - Imam Al–Hasan Al -Askari. Tafsirul–Ayyashi cha Ayyashi. Risaalatut Tasamuh fiy Adilati s Sunan cha Imam As Shirazi. Ilalus Sharaiu cha Sheikh Suduq. Awalimul – Ulumi cha Bahran. Uyunul–Akhbar Ar–Ridhaa (as ) cha Sheikh As Suduq. Ghawali layali cha Ibn Jamhur Al–Ahsai. Fatmatuz-Zahraa (a.s) fiyl–Qur’ani cha Ayatullah Al-Udhmaa As Sayyid As-Swadiq As Shirazi. Kashful –Alii cha Al-Arandasi. Kalmatullah cha Ayatullah As Shahid As Sayid Hasan As Shirazi. Lisanul–Arab cha Ibn Mandhur. Majma’ul–Bayan cha Twabrsi. Majmau Nurain cha Sabzawari. Mustadrakus-Safinatul-Bihar cha Namaazi. Ma’anil – Akhbar cha Sheikh As Suduq. Mafatihul Jinan cha Al–Muhadith Al–Qummi Multaqaal–Bahrain cha Al – Marandi Min fiqihiz–Zahra cha Imam As Shirazi 35


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 36

Fatima al-Zahra

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL - ITRAH FOUNDATION: 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Ishirini na Moja Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi 36


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 37

Fatima al-Zahra 25. 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53.

Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto 37


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 38

Fatima al-Zahra 54. 55. 56. 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81.

as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliy onyooka Shia asema haya, Sunni asema haya, Wewe wasemaje? Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza Nahjul Balagha Sehemu ya Pili. Amali za Ramadhani 38


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 39

Fatima al-Zahra 82. 83. 84.

Mariam, Yesu na Ukristo kwa Mtazamo wa Kiislamu Ujumbe sehemu ya kwanza Ujumbe sehemu ya pili

39


Fatma Zahra Final D.Kanju.qxd

7/1/2011

3:28 PM

Page 40

Fatima al-Zahra

BACK COVER Kijitabu hiki ambacho kimepambwa kwa jina la Fatima Zahra (a.s), binti wa Mtume Muhammad (s.a.w.), ni kati ya mihadhara ya thamani ya marehemu Imam Muhammad al-Husaini al-Shirazi (Mwenyezi Mungu amrehemu). Ni kitabu cha aina yake katika lugha ya Kiswahili kinachoelezea maisha ya Bibi huyu mtukufu mwenye nuru. Ni kitabu kizuri kilioje, na ni haja ilioje kwa wakati huu ambao mazungumzo yamekuwa ni mengi kuhusu Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s), mijadala na midahalo imezidi juu ya shakhsia yake tukufu na nafasi yake katika Umma. Cha kuzingatia ni kwamba kumjua mtukufu huyu ambaye ni Bibi wa wanawake wa ulimwenguni (a.s) ni wajibu kwa Waislamu wote, kwani ameshasema (a.s): “Jueni kwamba mimi ni Fatima al-Zahra.” Yaani kunijua mimi ni wajibu kwa kila muumini. Bibi Fatima (a.s.) ni maasumu wa pekee katika jinsia yake, kumpenda kwake na kumtawalisha kwake ni sawa na kumpenda na kumtawalisha Amirul Muuminina Ali (a.s) na watoto wake walio maasumu (a.s). Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. – 19701, Daressalaam. Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info 40


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.