Asili ya Madhehebu katika Uislamu

Page 1

Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page A

Asili ya Madhehebu katika Uislamu Kimeandikwa na: Isa Rwechungura


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

B

7/1/2011

12:18 PM

Page B


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

Haki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 88 - 1 Kimeandikwa na: Isa Rwechungura Kimehaririwa na: Ramadhani Kanju Shemahimbo Na Ustadh Abdallah Mohammed Kupangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab. Toleo la kwanza: Januari, 2010 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

C

12:18 PM

Page C


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page D

Š Haki ya kunakili imehifadhiwa Ni lazima ipatikane idhini ya maandishi kwa Taasisi yoyote ya Kiislamu au Mwislamu anayetaka kuchapisha kitabu hiki kwa shughuli ya Tabligh. Idhini ya kufasiri kitabu hiki katika lugha nyingine yaweza kutolewa pia kwa masharti ya kutuma nakala yake kwa mtungaji. Kitabu hiki kimekusudiwa kwa wasomaji wenye kuzama katika kutafakari mambo kwa undani, hali ya kuwa wako tayari kuiona haki na kuikubali, japo haki hiyo inatambuliwa na kukubalika na watu wachache. (Qur’ani: 6:116) Mwenye kupinga kila hoja kwa sababu ya ujinga wake, atabakia kipofu asiyeuona ukweli. - Mtume (s.a.w.w.) Saa moja ya kutafuta elimu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko ibada ya miaka sitini. - Mtume (s.a.w.w.) Usingizi wa mtu mmoja mwenye elimu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko ibada ya usiku mzima ya kundi la wajinga elfu moja. Mtume (s.a.w.w.) Tafuta elimu toka mberekoni hadi kaburini - Mtume (s.a.w.w.) Kusikiliza ukweli, sio kila sikio linafaa, kama vile chakula kwa kila ndege si kimoja na kilekile. - Mshairi wa Kihindi: Rumi

D


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page E

Yaliyomo Utangulizi ...................................................................................................3 Maelezo juu ya mwandishi wa kitabu hiki na historia fupi ya utafiti wake..........................................................................................................17 Asili ya Tofauti kati ya Suni na Shia Ithnashari.......................................22 Utukufu wa Bani Hashim..........................................................................32 Bwana Hashim.........................................................................................34 Utamaduni wa Maquraishi........................................................................35 Bwana Abdul Muttalib..............................................................................36 Kisima cha ZamZam.................................................................................38 Abraha ataka kuvunja Al-Kaaba..............................................................39 Je, Hao Ahlul Bayt wa Mtume Sa.w.w. ni Nani?....................................53 Maneno ya Mtume (s.a.w.w) juu ya Ahlul Bayt wake.............................53 Sifa za Ahlul - Bayt wa Mtume (s.a.w.w).................................................56 Imam Hasan na Imam Husein (a.s)...........................................................56 Bibi Fatma (a.s)................................................................................ .......57 Msaada wa Allah kwa Bibi Fatma (a.s) katika shida................................57 Ahlul - Bayt waletewa chakula toka Peponi...........................................58 Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alikuwa akimheshimu sana Bibi Fatma.........59 Kwa nini aliitwa Fatma Zahra?.................................................................60 Ahlul Bayt (a.s) katika tukio la Mubahilah .............................................60 Kisa cha Imam Hasan Al-Askari Imam wa 11 (a.s)................................63 Kisa cha Imam Muhamad Mahdi (A.s) Imam wa 12...............................66 Utoto na Ujana wa Imam Mahdi (a.s)......................................................70 E


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page F

Imam Mahdi (a.s) katika kasri (Ikulu) ya Khalifa Mu’tamid...................73 Asili ya elimu za kidunia na maendeleo ya Kisayansi.............................90 Jinsi Elimu za Kiislamu zilivyoleta maendelea ya Sayansi huko Ulaya..93 Uchanganyaji madawa (Pharamacology)..................................................93 Hospital.....................................................................................................93 Kemia (Chemistry)...................................................................................93 Barabara za kisasa (paved Roads)............................................................94 Hisabati (Mathematics).............................................................................94 Abdul -Wahid Muhammad Ibn kushd.....................................................100 Abu Husein ibn Al-Haitham ..................................................................101 Abu ali Al-Husein Ibn Abdullah Ibn Sina............................................ 102 Abu Adullah Al-Battani..........................................................................103 Jabor Ibn Hayyan ...................................................................................104 Abu Rahman Muhammad Al-Biruni...................................................... 105 Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abdallah Ibn Idrisi (1099-1166A.D).105 Kwa nini Hatusikii majina ya wanasayansi maarufu wa Kiislamu........106 Sifa za peke a Ahlul - Bayt wa Mtume (s.a.w.w)...................................106 Hotuba (wasia) kamili ya mtume (s.a.w.w) pale Ghadir Khum na ushahidi kamili wa tuko hilo ................................................................................108 Mwisho wa Khutba ................................................................................126 Kwa nini wasia wa Mtume (s.a.w.w) ulipuuzwa?..................................128 Hoja za Sunni kuhusu uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w)................................................................................................. 137 Jeshi la Usamah bin Zayd.......................................................................143 Alipokaribia kufariki Mtume (s.a.w.w) hadi kufa kwake..................... 145 Mkutano wa Saqifah ban Sa’idah ......................................................... 151 Demokrasia au Shura?........................................................................... 158 Bibi Fatima (a.s.) kunyang’anywa Urithi wake Fadak......................... .191 Kufutwa zaka ya Khums....................................................................... .193 F


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page G

Utawala wa Umar ibn al- Khattab .........................................................194 Kuhusu udhu wa Tayamam.....................................................................197 Taraweh kuswaliwa jamaa......................................................................197 Umar atoa hukumu bila ujuzi na hivyo akakosolwa na Imam Ali (a.s).200 Talaka tatu kwa mpigo...........................................................................202 Ndoa ya Muda Maalum (Mut’ah)...........................................................204 Faida ya unyago katika ndoa zetu...........................................................216 Wanawake wajane...................................................................................219 Kanuni za ndoa ya Mut’ah......................................................................223 Tamko la ndoa (ndoa zote) .................................................................. 223 Idhini ya Baba au Babu na mke (Ndoa zote)..........................................224 Mashahidi (kwandoa zote)..................................................................... 225 Utawala wa Uthman ibn Affan ..............................................................230 Waislamu wanamtaka Imam Ali ibn Abu Talib kuwa Khalifa. wao..... 242 Sababu za kuuwawa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s) ................................269 Ulul-amr ni Nani? Qur’an 4:59...............................................................275 Muawiyah Anyakua Ukhalifa.................................................................295 Muawiya amwachia urithi wa Ukhalifa mwanawe Yazid......................307 Je, ili Muislamu Suni inabidi kuamini Nini?..........................................320 Dini siyo nadharia popote Dogma bali ni Tauluma ..............................330 Deni siyo nadharia potofu ‘DOGMA’ bali ni Taaluma...........................336 Asili ya tofauti katika ibada kati ya Shia na Sunni.................................356


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page H

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako kinaitwa, Asili ya Madhehebu katika Uislamu, kilichoandikwa na Ndugu Isa Rwechungura kwa lugha ya Kiswahili. Maudhui kubwa katika kitabu hiki ni kuhusu madhehebu za Kiislamu. Suala la madhehebu limekuwa na bado halieleweki vizuri miongoni mwa Waislamu kiasi kwamba wakati mwingine hufikia kupigana na kuuana kutokana na kuzozana juu ya suala hili. Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW mwenyewe katika hadithi zake tukufu: “Mayahudi walikuwa madhehebu sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoni isipokuwa moja.� Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote hizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama, na sio kugombana kwa jambo ambalo lilikwishatabiriwa na Bwana Mtume mwenyewe - na hiki ndicho alichofanya mwandishi wa kitabu hiki. Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe.


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page I

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Shukurani zimuendee mwandishi wa kitabu hiki, tunamwomba Allah Mwenye uhai wa milele, amjaalie umri mrefu, amruzuku ilmu na fahamu ili aweze kufanya tafiti nyingine zaidi, Insha-Allah. Tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701, Dar-es-Salaam.


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page J

BISMILLAHIR-RAHMANIR-RAHIYM

LENGO KUU LA KUANDIKA KITABU HIKI Sababu kubwa ya kuandika kitabu hiki ni kuwaeleza Waislamu au mtu yeyote anayetaka kufahamu Uislamu asilia, kuhusu hotuba (Wasia) ndefu aliyotoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mnamo mwezi 18, Mfunguo Tatu, Mwaka 10 A.H. (632 A.D.), mahali paitwapo Ghadir-Khum wakati akitokea Hijja yake ya mwisho, miezi mitatu tu kabla hajafariki. Hotuba hiyo ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitoa mbele ya Masahaba wapatao 140,000, inaeleza wazi Uislamu ulivyotakiwa kuendeshwa baada yake, kinyume kabisa na hali halisi iliyofuatia mara tu alipofariki hadi wakati huu! Jambo la maana ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hotuba hiyo alituamrisha Waislamu kila atakayeisikia, ni wajibu kwake kumweleza asiyewahi kuisikia hadi Siku ya Kiyama. Kwa hiyo mimi nimetimiza wajibu wangu kwenu na nimeeleza pia historia juu ya sababu zilizosabibisha Wasia huo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kupuuzwa. Kimsingi naomba ieleweke kuwa mimi simlazimishi au kumshawishi Mwislamu yeyote aipokee hotuba hiyo tukufu. Ni juu ya kila mmoja wetu kuamua atakavyo baada ya kusoma kitabu hiki. Yaliyoelezwa katika kitabu hiki ni uchambuzi wa kisayansi na siyo ‘ung’ang’anizaji wa imani’. Hotuba kamili ipo ndani ya kitabu hiki – Sura ya 3.


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page K

JINSI YA KUTUMIA KITABU HIKI Ili uweze kupata haraka moja kwa moja somo unalotaka, fungua mwishoni - Sura ya 22 ambapo utakuta orodha ya masomo muhimu yaliyomo kitabuni na kurasa zake. Isa Rwechungura Mtungaji

MAPITIO Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Ee Allah! Mteremshie baraka zako Bwana wetu na Rasuli wetu Muhammad Mustafa na Dhuria wake uliowatoharisha na ukawateua kuwa viongozi wetu na ukatufaradhisha kuwapenda, kuwatii na kuufuata mwongozo wao. Alhamdulilahi nimekipata na kukisoma kitabu hiki: ASILI YA MADHEHEBU KATIKA UISLAMU. Namshukuru Allah (s.w.t.) kwa kumwezesha ndugu yetu Isa Hamisi Rwechungura kukiandika kitabu hiki, na kututanabaisha watu wa dini zote kwa ujumla kutokana na ukweli kwamba Mungu ni mmoja na kwa hiyo dini inapaswa kuwa moja tu. Kwa upande mwingine, Waislamu wa wakati huu, kwa kukosa elimu ya dini ya kutosha, tumeichukulia dini kimzaha tu, kwa misingi ya kurithi imani mbali mbali ambazo baadhi yake ni upotofu. Hata hivyo siku hizi wapo Waislamu wengine ambao wanaitumia dini kwa manufaa yao ya kiuchumi, kisiasa na kijamii. Ndugu zetu hao hatuna haja ya kuwaeleza kwa sababu wao wanaishi kwa ajili ya dunia tu, na hawaoni faida kubwa za kiroho ambazo wangezipata huko akhera. Ama kwa wale ambao, kwa nia njema kabisa, wanayo shauku ya kutaka K


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page L

kujua ukweli wa dini, kwa misingi ya mafunzo sahihi, lakini wanashindwa kuupata ukweli kutokana na wingi wa dini na madhehebu, na kila dini au madhehebu inadai ndiyo ya kweli, basi kitabu hiki kitawapa mwangaza mkubwa na kuwafikisha kwenye Uislamu wa kweli, ili mradi wazingatie hoja zilizomo na wasiwe na jazba au ushabiki, iwapo hoja hizi zitatofautiana na itikadi zao. Jambo la msingi ni kuufikia ukweli kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hayo ningependa kumshauri msomaji wa kitabu hiki, kabla ya kuanza kukisoma, azingatie yafuatayo ili aweze kupata faida iliyokusudiwa.

1. Kujua faida na umuhimu wa dini Ni lazima binadamu yeyote atambue kuwa ameumbwa na Mwenyezi Mungu, na kwamba anatakiwa kuishi duniani chini ya amri au mamlaka ya Muumba wake. Isitoshe ni lazima kila mtu afahamu kuwa kuna maisha ya duniani ambayo ni mafupi sana, na kisha kuna maisha ya akhera yasiyo na mwisho. Ubora wa maisha ya akhera utategemea utiifu kwa Mwenyezi Mungu hapa duniani. Kwa hiyo mtu yeyote ambaye anajenga imani potofu za dini na kuzitumikia uhai wake wote hapa duniani, hatapata chochote huko akhera ila kuangamia tu! Kwa maana hiyo, dini ya kweli lazima ijengeke juu ya hoja imara za kisayansi na siyo katika misingi ya kurithi toka kwa babu zetu, au kujenga imani tu isiyoweza kuthibitika kimantiki.

2. Jukumu la kuitafuta dini ya kweli ni la kila mtu peke yake. Ni jukumu la kila mtu kutafuta dini ya kweli ili aweze kutimiza wajibu wake wa kumtii Mwenyezi Mungu. Mbele ya Mwenyezi Mungu kila mtu atahukumiwa peke yake kwa sababu ya kupewa akili. Maana yake ni kwamba hakuna mtu atakayedai kuwa alipotezwa na wazazi wake au kiongozi wake wa dini au kundi fulani la watu. Nikifafanua zaidi ni kwamba binadamu tumepiga hatua kubwa katika L


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page M

sayansi na teknolojia kwa sababu ya kutumia akili. Tunatakiwa tutumie akili hiyo hiyo kutambua dini ya kweli, la sivyo tutahukumiwa. Lazima tutambue tofauti kati ya binadamu na mnyama, nayo ni akili. Huwezi kumpeleka ng’ombe mahakamani kwa kula mazao yako shambani kwani ng’ombe hana akili. Badala yake atashitakiwa yule mmiliki wa ng’ombe huyo. Kwa hiyo iwapo binadamu atatarajia msamaha kwa yeye kutotumia akili aliyopewa, atakuwa anajilinganisha na mnyama, na hilo halitakubalika mbele ya Mwenyezi Mungu. 3. Kujua kuwa Mungu ni mmoja na Uislamu ni mmoja tu Baada ya maelezo hayo juu ya umuhimu na ukweli wa dini kwa maisha ya duniani na akhera, ni muhimi kwa Mwislamu mwaminifu, kutambua kuwa kwa kadri ya mafunzo sahihi ya dini, Uislamu ni mmoja tu ingawa zipo madhehebu nyingi za kiislamu zinazotofautiana kimatendo (hukumu za dini). Kwa hiyo kwa msaada wa kitabu hiki tutaona kuwa Uislamu ni mmoja tu kwa manabii wote; na kwamba hivi sasa ingawa kuna madhehebu nyingi, ni madhehebu moja tu ya kweli mbele ya Mwenyezi Mungu. Ukweli huu unatokana na sababu zifuatazo: (a) Uislamu ni ukweli. Dini ya Uislamu ni ya kweli na ukweli wa jambo lolote lile hauwezi kuwa zaidi ya mmoja. Kitu kimoja hakiwezi kutofautiana. Uislamu ulifundishwa na mwenyewe Mtume (s.a.w.w) na kwa hiyo asingefundisha kitu kimoja kinachotofautiana kama ilivyo wakati huu katika Uislamu. Kwa hiyo lazima iwepo madhehebu moja tu sahihi miongoni mwa migawanyiko hii kama tutakavyoona mbele kwa ushahidi wa mafunzo ya dini, ya kutegemewa. Kibusara ni kwamba haiwezekani nchi moja ikawa na sheria tofauti kwa raia wake watokao mikoa mbalimbali ya nchi hiyo. (b) Kazi ya Mtume na vitabu ni kutuondolea mifarakano katika dini: Tunaposoma Qur’ani tukufu tunagundua kwamba hawa Mitume na vitabu vyao wameletwa ili kutuondolea sisi binadamu mifarakano, na iwapo tutaM


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page N

farakana tuweze kupambanua ukweli uko wapi. Hebu tuone Aya ifuatayo:

“Wanadamu wote walikuwa taifa moja (limwaminilo Allah tu lakini baadaye walihitilafiana), hivyo Allah akawapelekea manabii, kuwa wabashiri na waonyaji, na pamoja nao akateremsha Kitabu na ukweli ili kuhukumu baina ya wanadamu katika yale waliyohitilafiana......... (Qur’ani 2:213). Bila shaka tunaona wazi kwamba, kuwa na madhehebu mengi zinazotofautiana kiitikadi na kimatendo, kunaleta mifarakano, jambo ambalo ni kinyume na makusudio ya kuletwa Uislamu. Kwa hiyo wingi wa madhehebu sio Uislamu bali Uislamu ni madhehebu moja tu kama ushahidi zaidi utakavyobainisha ndani ya kitabu hiki. (c) Ushahidi wa Qur`ani juu ya Uislamu mmoja tu Tukisoma Qur`ani Tukufu tunazikuta Aya zionyeshazo wazi kuwa Uislamu ni mmoja tu.

“Na hakika hii ndiyo Njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni (hii tu) wala msizifuate njia nyingine na mkafarakana na njia yake (hii), Allah Anakuusieni haya ili mpate kuchelea (maovu).” (Qur’ani 6:153).

N


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page O

“Hakika wale walioigawa dini yao na wakawa makundi makundi (wewe Mtume wetu Muhammad) huna chochote kwao; hakika jambo lao liko kwa Allah (tu), kisha (siku ya Kiyama) Atawaambia waliyokuwa wakiyatenda........” (Qur’ani 6:159 ). Kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi ni Uislamu mmoja tu. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Umma wa Nabii Isa uligawanyika makundi 71 baada yake. Umma wa Nabii Musa uligawanyika makundi 72 baada yake. Umma wangu baada yangu utagawanyika makundi 73. Wote wataangamia (motoni) ila kundi moja tu.” - Rejea: Sahih Muslim, Juzuu ya 8 Ukurasa wa 7, Sahih Bukhari na Sahih Tirmidh. Kwa hiyo basi, kutokana na hoja zote hizi, si rahisi kwa Mwislamu yeyote mwaminifu kudai hivi hivi tu bila hoja thabiti, kwamba madhehebu yake ndiyo sahihi katika Uislamu. Kwa kuwa Uislamu wetu unategemea yale tuliyorithi kwa babu zetu bila kutumia akili zetu na kufanya utafiti, ina maana tungewakuta wazazi wetu ni Wakristo na sisi tungekuwa Wakristo. Kwa hiyo umuhimu wa kuchunguza imani zetu za kurithi bado upo. Hivyo basi kama tutazingatia yaliyoandikwa na ndugu yetu Isa H. Rwechungura na kuyafuata, tutafaidika na pia kuongoka - Inshaallah. Jambo la maana katika utafiti huu, ni muhimu tutumie sana akili bila kujali utetezi wa madhehebu uliyowakuta nayo wazazi wako, au madhehebu yenye wafuasi wengi zaidi, au madhehebu yenye watu mashuhuri, n.k. Hayo hayatatusaidia kuufikia uongofu unaotakiwa. Mwisho namwomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Amjaalie ndugu yetu Isa Rwechungura kheri, baraka, na amfungulie milango ya elimu ili azidi kutuelimisha. O


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:18 PM

Page P

Na sisi sote Mwenyezi Mungu atujaalie usikivu mwema wa kutuwezesha kuyaelewa mafunzo haya ya haki na kuyatumia kufikia ukweli wa dini ya Mwenyezi Mungu ambao ni Uislamu mmoja tu - Amin. Na Baraka za Allah zimshukie Mtume Wake (Muhammad) na Maimamu watukufu watokanao na Kizazi chake kitukufu na Awateremshie amani na utulivu kwa wingi. Dhikiri U.M.Kiondo Dar es salaam - T.I.C. (Mwenyekiti) 4th Jamadiul Awwal 1419 A.H. / 27th August 1998.

P


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

2

7/1/2011

12:18 PM

katika Uislamu

Page 2


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 3

katika Uislamu

UTANGULIZI Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Namwomba Mwenyezi Mungu amteremshie baraka njema za milele Bwana wetu Muhammad na watu wa Familia yake ambao walitoharishwa kikamilifu kwa kadri ya “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Qur’ani 33:33); pamoja na maswahaba waaminifu walioshikamana na mwendo wa Mtume (s.a.w.w) - Amin. Ndugu zangu, namshukuru Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kuniwezesha kukamilisha kazi hii ambayo ni wajibu kwa kila Mwislamu. Kama tulivyotangulia kusoma kuwa ni muhimu kila mmoja wetu achunguze upya imani na itikadi yake ya kidini, ili afikie dini moja ya kweli mbele ya Mwenyezi Mungu, kuliko kubakia kujivunia madhehebu mbali mbali. Kwa msingi huo nilijaaliwa kufanya utafiti kwa miaka 16 kwa kusoma vitabu mbalimbali hasa vile vya Historia sahihi ya Uislamu. Niliyoyakuta katika vitabu hivyo, yalinitia simanzi moyoni kwa muda mrefu, kwa kuona jinsi ambavyo Waislamu kwa miaka mingi tumekuwa tunaendeleza utamaduni wa kiislamu lakini Uislamu wenyewe upo mbali na sisi. Nasema hivi kwa sababu tumetangulia kuona kuwa sisi binadamu tunapaswa kuishi hapa duniani chini ya amri za Muumba wetu wakati wote. Pale tunapoachana na amri hizo au tunapoacha amri hizi na kuanza kuchagua tunayotaka, na kuacha tusiyoyataka, hiyo si dini tena. Hali hiyo ndiyo tuliyonayo wakati huu katika Uislamu wetu. Kwa sababu tutambue kuwa maana ya neno ‘Islam’ ni kujitoa nafsi yako yote kumtii Mwenyezi Mungu. Utiifu wa nusu nusu sio Uislamu unaotakiwa.

3


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 4

katika Uislamu

Isitoshe kama hivi leo Mtume (s.a.w.w.) angekuwa hai tunamwona, vipi angetuamrisha jambo lolote lile kisha tukatae kumtii? Lakini pamoja na kwamba hatuko naye tena, mafunzo yake na amri zake kwetu zipo na zimehifadhiwa katika vitabu vya Hadithi. Inasikitisha kuona Waislamu tunapuuzia amri muhimu za Mtume (s.a.w.w.) zilizo katika vitabu tunavyodai kuwa vinatuongoza! Kwa hiyo yale nitakayobainisha hapa siyo mageni kwa wale wenye ujuzi wa dini. Ningependa tutambue ukweli kwamba Uislamu ulianza karne kumi na nne zilizopita. Katika muda huo mrefu, ni matukio mengi yametokea. Mtu yeyote asiye na ujuzi wa matukio hayo, hana haki yoyote ya kupinga au kuunga mkono hoja zilizomo humu. Kama ambavyo mimi siwezi kuingia kwenye ndege kwa nia ya kujifanya rubani wakati sina ujuzi wa kazi hiyo. Kwa maana hiyo, nakaribisha mjadala kwa wasomaji wa kitabu hiki, ambao wana mawazo tofauti, mradi mawazo hayo yawe yametoka katika vitabu vinavyotegemewa. Kama zipo hoja za msingi zaidi ya hizi, nitakuwa tayari kuzijadili. Vinginevyo siko tayari kupoteza muda katika kujibu au kujadili hoja kinyume na msimamo huu; kwani itakuwa ni kukiuka misingi ya utafiti. Nina maana kwamba anayetaka tujadili hoja hizi au kunipinga, itabidi kwanza athibitishe elimu yake ya Historia sahihi ya Uislamu kama inamtosha kujadili hoja hizi. Sababu yake ni kwamba, imenichukua miaka 16 kufanya utafiti huu, kwa kusoma vitabu vingi sana, kuliko hivyo nilivyovitaja mwishoni mwa kitabu hiki. Isingekuwa busara katika ulimwengu wa wasomi, kutoa hoja au kupinga hoja bila ujuzi wowote wa kutosha. Kwa kuwa nimetaja vitabu ambamo zinapatikana habari hizi, ni bora anayetaka kutoa hoja atafute vitabu hivyo au awaulize wanaovifahamu, ili athibitishe hoja nilizotoa na ndipo naye atoe hoja zake. Elimu niliyotoa humu ni ya ngazi ya juu sana ukizingatia elimu ya chini sana tuliyonayo Waislamu tulio wengi. Nimejitahidi kuelezea hoja mbali mbali kwa lugha nyepesi, na kwa mtiririko bayana kuhusu matukio kadhaa yalivyofuatana, kuanzia miaka zaidi ya 500 kabla ya Uislamu wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) hadi mwan4


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 5

katika Uislamu

zo wake mpaka wakati huu. Elimu yote hiyo si rahisi kuipata katika muda mfupi hata kwa mtafiti mwenye bidii sana. Mimi nawaheshimu na kuwapongeza mashekhe wetu kwa kuendelea kutoa elimu ya dini katika mazingira duni yatokanayo na kukosa taasisi rasmi za kisasa za kutoa elimu bora ya dini. Uduni wa elimu ya dini siyo kosa la mashekhe bali ni mfumo mbaya wa kukosa chombo imara cha kuongoza Waislamu kwa jumla. Hebu tujadili mfano mmoja ambao ni rahisi kila mtu kuelewa. Tuchukulie kuwa hapa Dodoma mjini, mwaka 1995 kulikuwa na Waislamu laki moja na nusu tu, kati ya wakazi wapatao laki tatu hivi. Tuchukulie kuwa kila Mwislamu achange shilingi 100 kila mwezi. Ina maana tutapata shilingi milioni 15 kwa mwezi! Hata kama tutapata shilingi milioni saba tu kwa kila mmoja wetu kuchanga shilingi hamsini. Je, ndugu Waislamu hizo pesa hazitoshi kuwalipa mashekhe wetu mishahara ya heshima na wakaacha kupiga ramli? Je, pesa hizo hazitoshi kujenga misikiti mipya na kuifanyia matengenezo ile ya zamani? Je, pesa hizo hazitoshi kujenga mashule ya kisasa ya kutoa elimu zote za dini na dunia? Je, pesa hizo hazitoshi kuanzisha vituo vya ajira kwa vijana wetu wasio na kazi? Je, pesa hizo hazitoshi kuwasaidia mayatima na wajane na wazee wasiojiweza? Kwa hiyo Waislamu tukubali kuwa tunao uwezo wa kubadili hali zetu duni za kidini na kidunia iwapo tutapata viongozi waaminifu chini ya uongozi wa chombo chenye uadilifu. Nikirejea kwenye hoja ya msingi ni kwamba, kutokana na elimu duni ya dini tuliyonayo, ni vizuri tukubali ukweli huo kwa sababu kulitambua tatizo ni nusu ya kulitatua. Haina maana mtu kuitwa wakili wakati hajui sheria! Haina maana mtu kuitwa daktari wakati anawaua wagonjwa kwa matibabu yasiyofaa! Haina maana mtu kuitwa mwalimu wakati hana cho5


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 6

katika Uislamu

chote cha kuwafundisha wenzake! Kwa misingi hiyo hiyo, haina maana yoyote Mwislamu kuitwa Sheikh wakati ambapo hawezi kujibu hoja muhimu za dini. Kushika uongozi kama huo bila ujuzi wa kutosha, ni kujibebesha mzigo wa lawama za kuwapotosha watu, kesho huko akhera. Ujuzi wa dini ni taaluma sawa na taaluma nyingine za elimu. Hakuna taaluma bila elimu. Hata uchawi wa shetani una elimu zake. Kila mara tumewasikia viongozi mbali mbali wakiwataka Waislamu kupata elimu kwa sababu siyo siri tena kwamba Waislamu hatuna elimu! Kwa hiyo hatuna sababu ya kujifanya tunayo elimu! Jambo la maana ni kwamba tuanze kutafuta njia za kuondoa kasoro hii kwa sababu katika kitabu hiki, tutaona kuwa elimu zote tunazojivunia zilizoleta maendeleo makubwa zimeletwa na Uislamu. Baada ya utafiti katika historia sahihi ya dunia, hivi sasa hata wazungu wanakubaliana na ukweli huu! Kama Uislamu ndio ulioleta elimu duniani, kwa nini leo hii Waislamu tuwe nyuma? Matatizo yaliyotokea hadi tukadidimia kiasi hiki utayakuta humu. Inasikitisha kwamba, niliwahi kusikia Sheikh mmoja maarufu katika semina mojawapo ya kidini, akiwahutubia washiriki kwa kuwaogopesha kwamba elimu ya dini ni kubwa sana; na kwa hiyo si rahisi watu kuipata na kuhitimu! Hizi ni mbinu za baadhi ya viongozi wa dini kuficha upungufu wao wa elimu, au hata kuficha ukweli iwapo ukweli huo unahatarisha maslahi ya kidunia ya mtu binafsi. Nasema hivi kwa sababu madai ya kwamba elimu ya dini ni kubwa sana na ni vigumu kuipata, ni madai ya uongo! Mbona watu wamesoma miaka mingi hadi wakaweza kutengeneza vyombo vya kuwasafirisha na kutua mwezini? Namna gani watu wamepata uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia? Ni elimu gani kubwa kuliko elimu hizo? Upotofu ulioingia katika Uislamu ni suala la historia na si tatizo la hukumu za dini. Katika kitabu hiki kidogo tutaona vitabu vingi sana vya historia ya Uislamu sambamba na historia ya dunia. Je, vitabu hivyo ni vya bandia? Je, ni viongozi wetu wa dini wangapi walionavyo au wanaovifahamu? Je, 6


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 7

katika Uislamu

kutokijua kitu maana yake ni kwamba kitu hicho hakipo? Kwa kuwa Uislamu haukuanzia Afrika Mashariki lazima tusome na kuelewa asili yake hadi wakati huu. Katika ulimwengu wa leo, hakuna elimu iliyojificha labda iwe ni siri ya Mwenyezi Mungu. Elimu zipo wazi kwa wenye kuzitafuta. Elimu tunayoongelea hapa ni ile ya kutosha Mwislamu wa kawaida kufahamu misingi ya dini ili awe Mwislamu kamili anayeongozwa na itikadi sahihi za Uislamu. Natoa msimamo huu wa kutafuta elimu kutokana na ukweli kwamba, historia ya Uislamu ni sambamba na historia ya dunia. Na tunafahamu kuwa huwezi kuifahamu historia ya dunia bila kusoma katika shule za sekondari hadi Chuo Kikuu. Tatizo hili la madhehebu ni tatizo la kihistoria; na kwa hiyo ni lazima kutafiti katika historia, ili tuone chanzo chake ni nini. Lakini kama tujuavyo, mashekhe wetu tunaowategemea wakati huu, hawakupata elimu ngazi hiyo, kutokana na ukweli kwamba enzi zao walipata elimu yao kwa mashekhe wenzao mitaani bila kipimo chochote cha viwango. Tatizo hili ni la hapa Afrika Mashariki, lakini katika nchi nyingi za Waislamu zilizoendelea, elimu yote ya dini inatolewa kwa viwango kuanzia Shule za msingi hadi ngazi ya Chuo Kikuu. Nina maana kuwa kwa mfano, unapojifunza lugha ya kiarabu utaanzia ngazi ya shule ya msingi na ukihitimu unapewa cheti ngazi hiyo. Kisha utaingia ngazi ya elimu ya shule za sekondari darasa la kumi na mbili na ukihitimu unapewa cheti. Kisha unaingia ngazi ya darasa la kumi na nne na unahitimu na kupata cheti. Mwisho unaingia Chuo Kikuu kwa shahada ya kwanza na ya pili iwapo utahitimu masomo yako. Utaratibu huo wa masomo utamchukua mtu miaka isiyopungua 18 tangu shule ya misingi. Vinginevyo ukianza na elimu ya msingi peke yake, utahitaji vyuo maalumu vya lugha ya kiarabu, kwa masomo ya miaka isiyopungua mitano. Au kama utampata Sheikh mwenye ujuzi wa lugha ya kiarabu kwa viwango vya kimataifa, aweze kukufundisha binafsi. Mashekhe wenye ujuzi wa 7


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 8

katika Uislamu

viwango hivyo ni wachache sana hapa kwetu. Lakini hata hapa kwetu, lugha yetu ya kiswahili inafundishwa kwa utaratibu huo! Wala sidhani kuwa kiarabu ni rahisi kuliko kiswahili! Viwango katika elimu yoyote ile ni muhimu sana katika ulimwengu wa leo wa wasomi. Njia nyingine inayotegemewa hapa kama msingi wa kujifunza kiarabu, ni kutumia vitabu vya ‘Fiq-hi’ vya madhehebu ya Sunni kama: IrshadulMuslimiin, Safinat Najah, Risalatul-Jamaa na Durarul-Bahiyyah. Vitabu hivi si vya kufundishia lugha. Kwa hiyo kuvitumia, yaani kutumia lugha iliyomo, kama njia ya kujifunza kiarabu, ni sawa na mtu asiyejua kiswahili, akaamua kusoma magezeti mengi ya kiswahili kwa matumaini ya kuhitimu moja kwa moja na kufahamu kiswahili, bila kujifunza kwa undani, kanuni za lugha na viwango vyake hatua kwa hatua! Kwa kweli huwezi kutumia kiswahili cha darasa la nne kufahamu masomo ya Chuo Kikuu! Isitoshe kiarabu ni lugha ngumu yenye msamiati mpana sana, kiasi kwamba neno moja laweza kuwa na maana zaidi ya sita, lakini uamuzi sahihi wa matumizi yake, hutegemea kanuni nyingine nyingi, kufikia uamuzi kama neno litumike mahali hapo au lisitumike. Lugha ya kiarabu inajitosheleza hata katika lugha ya kisayansi kama tutakavyoona mbele katika kitabu hiki. Sisi Waislamu wa Afrika Mashariki, iwapo tunataka kupata elimu za juu za dini, hasa somo la historia, tunaweza kupata urahisi kwa kufaidika na vitabu vingi vya kiingereza, yaani tafsiri za kiingereza za vitabu maarufu vya Historia ya Uislamu. Vitabu hivyo vimefasiriwa na wajuzi wakuu wa lugha hizi mbili. Lakini kama tutajaribu kutumia kiarabu cha ngazi ya chini kufafanua elimu za juu, tutaishia kuwapotosha kabisa wale wanaotuona kama viongozi wao. Nasisitiza sana jambo hili ili Waislamu tulio wengi tutambue kuwa kuitwa ‘Sheikh’ ni rahisi sana hasa hapa kwetu, lakini kufahamu dini ni kitu kingine. Kuna kitabu kimoja maarufu kilichoandikwa na mwanachuoni mmoja maarufu sana huko Tunisia. Mwanachuoni huyo mwanzoni alikuwa Sunni Maalik, lakini alipofanya utafiti akaamua kuwa Ansari Sunna, akatafiti zaidi hatimaye akawa Shia na kwa hiyo akaandika kitabu hicho kueleza aliyoyagudua. Kwa bahati kitabu hicho 8


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 9

katika Uislamu

kimeshafasiriwa hadi lugha ya kiingereza na kiswahili. Kitabu hicho kiitwacho: HATIMAYE NIMEONGOKA, ni muhimu Waislamu wote kukisoma. Siku moja nikampa kitabu hicho Sheikh mmoja maarufu nikiwa katika ‘tabligh’ ili tujadili hoja zilizomo. Yeye alidai nimpe nakala ya kiarabu, nikampa. Mpaka leo hii ni zaidi ya miaka 5 hajanipa jibu wala kugusia suala hilo wakati ambapo hoja zilizomo ni nzito sana! Mwanzoni nilifikiri kuwa anataka kuficha ukweli, lakini siku moja akatutembelea mwanachuoni mmoja toka nchi za nje na ndiye aliyenipatia jibu. Mwanachuoni huyo aliwatembelea mashekhe mbali mbali kwa nia ya kuwasalimia. Mwisho wake karibu na kuondoka, alisikika akisema kuwa ni mashekhe wawili tu aliowaona wanafahamu kiarabu fasaha kwa kanuni za lugha! Bali sisi hatujui siri hiyo! Lakini sijapata kusoma popote pale katika mafunzo ya dini, kwamba Sheikh atabeba dhambi za wafuasi wake! Kwa hiyo Waislamu tujikomboe kwa kutafuta elimu. Tusiwe wafuasi vipofu. Kwa kweli hata hizo kanuni muhimu za lugha ya kiarabu, ni wachache wenye kuzifahamu zote. Matokeo yake utaona kuwa tafsiri za Qur’ani zinapotoshwa japo isiwe kwa makusudi. Kwa mfano katika tafsiri ya kiswahili ya Qur’ani ya Marehemu Saleh Farsy, aliifasiri Aya ya udhu (Qur’ani 5:6) kuonyesha kuwa ni wajibu kuosha miguu kwa maji! Tafsiri sahihi ya Aya hiyo tutaijadili kwa upana katika maelezo ya sura za mbele za kitabu hiki. Katika maelezo haya sina maana kuwa Mashekhe wetu hawajui kufundisha na kusoma Qur’ani! Usomaji wa Qur’ani una kanuni zake zinazofanana dunia nzima. Tatizo la hapa kwetu ni tafsiri ya Qur’ani. Kwa sababu Qur’ani haiwezi kufasiriwa kwa kutumia kanuni za lugha peke yake; bali pia sababu za kushuka Aya kihistoria, lazima zieleweke na zizingatiwe. Lakini kutokana na upungufu tulionao hapa kwetu katika somo la historia sahihi ya Uislamu, ndiyo maana kuna walakini katika baadhi ya tafsiri za Aya za Qur’ani. Nimetangulia kueleza kuwa itamchukua mtu 9


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 10

katika Uislamu

miaka kama 18 kujifunza lugha ya kiarabu mpaka ngazi ya Chuo Kikuu katika nchi za kiarabu, kwa mfumo wa kawaida wa elimu ya sekondari. Kama siyo hivyo, itabidi mtu huyo asome walau miaka mitano katika vyuo maalumu vya lugha na dini bila masomo mengine. Siyo rahisi mtu kuhitimu ngazi hiyo kwa kusoma mitaani bila viwango. Kumbukumbu za historia nitakazoeleza humu zinatoka katika vitabu ambavyo vimeandikwa na wanahistoria wa ngazi ya Chuo Kikuu kwa lugha ya ngazi hiyo. Ndiyo maana sitarajii kuwa itakuwa rahisi kwa mashekhe wetu walio wengi, kufahamu kwa ufasaha, yaliyomo katika vitabu vitakavyotajwa humu kama ushahidi wa kihistoria kuthibitisha kumbukumbu hizo. Pengine mashekhe wetu hapa kwetu hawatafurahia ukweli huu nilioeleza humu kuhusu ngazi za elimu ya viwango! Huenda wengine wakapinga ili wasionekane hawana elimu ya kutosha! Lakini suala la msingi ni kwamba, kama kuhitimu lugha ya kiarabu ni rahisi hivyo, kwa nini nchi hizo zilizoendelea zaidi ya sisi, wapoteze muda wao mrefu kusoma miaka yote hiyo tena kwa viwango maalumu? Au kama kusoma kwa viwango si lazima kwa nini vijengwe vyuo vya taaluma mbali mbali dunia nzima? Kwa nini watu wasihitimu urubani, unahodha, udaktari au uhandisi, mitaani bila kwenda kusoma katika vyuo maalumu? Je inaingia akilini? Maelezo haya nimeyatoa mapema kupinga madai ya baadhi mashekhe wengi, ambao hudai kuwa kitabu cha kufundisha dini lazima kiwe katika lugha ya kiarabu! Lakini Waislamu wengi wa kawaida hawafahamu kiarabu. Kwa hiyo Waislamu hao hawawezi kumkosoa Sheikh wao, iwapo kiongozi huyo ataongea kiarabu kibovu au kufasiri maneno ya kiarabu kwa makosa! Mfano wake ni sawa na mzungu mgeni, ambaye hawezi kutofautisha kati ya kiswahili cha mtoto mdogo wa darasa la kwanza, na kiswahili cha ngazi ya Chuo Kikuu! Lugha usiyoielewa utaiona sawa tu masikioni mwako hata kama inakosewa! Hata hivyo pamoja na kushabikia kiarabu, ukweli ni kwamba wengi wa hao viongozi wetu wa dini, ujuzi wao wa kiarabu bado ni wa chini. Mfano 10


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 11

katika Uislamu

mmoja wa kusikitisha ni kwamba, miaka kama ishirini hivi iliyopita, katika mji mmoja kwenye msikiti mmoja, alitembelea shekhe mmoja ambaye alitokea Misri. Wenyeji wake walibaini kuwa kiarabu anachoongea ni cha ngazi ya juu na hakieleweki. Baada ya majadiliano, ulitolewa ushauri kuwa apatikane mtu aliyesomea Misri ili asaidie ukalimani. Mtu huyo alipatikana na haraka akaletwa msikitini kuokoa jahazi. Baada ya siku mbili za mtu huyo kutoa msaada wake, iligundulika kwa masikitiko, kuwa mtu huyo alikuwa Mkristo na alipelekwa Misri zamani kusomea fani ya uhandisi katika taaluma fulani. Mafunzo yake huko Misri yaliendeshwa katika lugha ya kiarabu fasaha cha ngazi ya Chuo Kikuu, na ndiyo maana ujuzi wake wa lugha hiyo ni wa kiwango cha juu. Kwa tabia yetu ya kushabikia kiarabu, siku moja tutafikia kuswalishwa na Mkristo kwa sababu tu anaongea kiarabu! Ni muhimu tuelewe pia kwamba, lahaja za kiarabu za nchi mbali mbali za Arabuni zinatofautiana kama ambavyo kiswahili cha Mombasa, Zanzibar, Musoma, Mwanza, Mtwara, Tanga, Zaire na Uganda, kinavyotofautiana. Kwa kweli hata tukishabikia kiarabu, ukweli ni kuwa hata somo la ‘Elimu ya Kiislam’ katika shule zetu za sekondari halifundishwi, kwa kukosa walimu. Je, hizo taasisi za kiislamu za kutosha kufundisha kiarabu ngazi hiyo ziko wapi? Ni kwa njia gani Waislamu walio wengi watapata elimu ya dini? Tutangoja mpaka lini? Nimeeleza nyuma kuwa kuna mashekhe wanaojua ukweli lakini wanaficha ili kulinda maslahi yao. Lakini wakati naandika kitabu hiki, tayari teknolojia ya kompyuta imefikia hatua ambapo zimetengenezwa ‘Computer Programmes’ zenye uwezo wa kufasiri lugha kwenda lugha nyingine tena kwa ngazi ya lugha inayotakiwa! Kwa mfano ukiwa na hotuba ya maandishi ya kiingereza, ni kiasi cha kuingiza tu kwenye kompyuta ikakutolea tafsiri ya kifaransa muda huo huo! Je, zikipatikana taratibu ‘programmes’ za kufasiri kiarabu kwenda kiingereza au kiswahili, ni vipi tutaendelea kuficha hayo yaliyomo katika ‘Sahih Muslim, Sahih Bukhari’ n.k. Je, wakiyagundua hayo wasio Waislamu na wakayaweka wazi, tutalalamika 11


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 12

katika Uislamu

kuwa wanatukashifu? Lengo langu kuandika kitabu hiki, ni kuwaelimisha Waislamu wote waelewe Uislamu wetu, na wajenge hoja kwa ujuzi wa dini, kuliko tabia yetu ya miaka mingi ya kurithi badala ya kutumia akili na kuichambua dini. Mwislamu ambaye atahitaji ufafanuzi zaidi atajitokeza na atasaidiwa ili aweze kuelewa. Sidhani kama ni kosa kwa Daktari aliyepata ujuzi wake katika lugha ya kiingereza, kuandika kitabu kuelezea jinsi ya kuepuka magonjwa, katika lugha ya kiswahili kwa faida ya watu wote. Na sidhani kama kuna faida yoyote kwa daktari huyo, kuandika kitabu kama hicho, katika lugha ya kiingereza na kuwataka watu wenye kutaka ufafanuzi, kila mara waje kwake ili awafasirie maelezo yake! Hata hivyo natambua ukweli kwamba vitabu vingi vya mafunzo ya dini vimo katika lugha ya kiarabu, lakini bado Waislamu wengi wanaweza kufaidika kwa kusoma vitabu vingi vya kiingereza kama mimi. Isitoshe mimi nimeweza kujifunza kusoma Qur’ani kwa kutumia vitabu maalum vya lugha ya kiingereza vyenye maelezo bora zaidi ya hizi Juzu Amma tulizozizoea, ambazo humfanya mwanafunzi achukue zaidi ya miaka 8 kuhitimu kusoma Qur’ani! Mimi ilinichukua mwaka mmoja tu tena bila mwalimu! Elimu inazidi kuwa nyepesi! Katika masuala ya dini tusiwe wanafiki wa nafsi zetu. Wengi wetu elimu zetu ni za kurithi kwa mababu na mashekhe wetu na siyo elimu za msingi wowote wa utafiti! Kwa hiyo tusione uzito kuachana na baadhi ya elimu potofu tulizopoteza muda mrefu kuzipata, na leo tunagundua kuwa kwa hakika elimu hizo hazifai! Mfano mzuri tunaupata kwa wasomi wengi waliomiminika Urusi ya zamani kusoma Elimu ya Ukomunisti na Ujamaa. Wasomi hao walihitimu na kupewa shahada za juu. Walirejea kwetu na kupewa vyeo vikubwa vya uongozi. Walijaribu kutekeleza elimu yao hiyo kwa vitendo lakini baada ya miaka mingi sana, hao wasomi wakagundua kuwa elimu yao hiyo inafurahisha na kutia moyo ukiisoma katika vitabu, lakini kivitendo haiwezekani! Baadaye hata huko Urusi ikadhihirika kuwa Ukomunisti na Ujamaa ni nadharia potofu! Viongozi hao hao waliotetea Ukomunisti kwa miaka mingi, hivi 12


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 13

katika Uislamu

sasa wamefumbua macho na kukumbatia Ubepari! Elimu zao zote za Ukomunisti na Ujamaa hazina faida yoyote tena! Kwa hiyo sisi Waislamu tusione hasara kuachana na elimu za mazoea, iwapo kufanya hivyo kutatuelekeza kufaulu mbele ya Mwenyezi Mungu. Na hilo ndilo lengo la dini kimsingi. Hatufuati dini kutafuta umaarufu toka kwa binadamu wenzetu au kupata faida za kidunia. Uislamu ni kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.); lakini utiifu huo tutaufikia kwa njia ya elimu sahihi ya dini. Ni vizuri kuchunguza elimu zako kwa makini kwa sababu kwa miaka mingi tumefundishwa kuwa Uislamu ndio umeleta Utumwa (slavery); na kwamba, Uislamu ulienezwa kwa upanga! Baada ya miaka mingi ya imani hizo potofu, leo hii vinapatikana vitabu vinavyoeleza ukweli tofauti na tulivyoaminishwa miaka mingi iliyopita! Rejea: Slavery - From Islamic & Christian Perspective - cha S.S.A. Rizvi - Canada Uk. 105 -138. Faida gani tuendelee kukumbatia elimu potofu zilizopitwa na wakati? Katika dini zote kuna mafunzo mengi potofu yasiyo na ukweli wowote lakini binadamu na akili zetu tunaendelea kuyakumbatia! Hiyo ni dini au utamaduni? Katika kitabu hiki tutaona kuwa upotofu katika dini unasababishwa na ujinga tulionao ambao tumeurithi kwa mababu zetu kwa miaka mingi. Inashangaza kuwaona mashekhe wetu siku hizi wanakazania lugha ya kiarabu kama njia pekee ya kujifunza dini wakati ambapo Mtume (s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa: “Tafuteni elimu hata kama itabidi kuifuata mpaka China.� Tukitafakari maneno hayo tutaona kuwa siku hizo huko China, haikutumika wala kueleweka lugha ya kiarabu! Maana yake ni kwamba mwenye kwenda huko kutafuta elimu, ingemlazimu kujifunza lugha ya Kichina. Je, kuna shekhe yeyote ambaye anaweza kudai kuwa elimu yote niliyotoa humu anayo, ingawa kuna aliyonayo ambayo humu haimo? Je, niliyoeleza humu hayafai kwa kuwa sikuyaandika katika kiarabu? 13


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 14

katika Uislamu

Hakuna mtu mwenye ujuzi wa elimu zote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu. Mwenye ujuzi wa lugha ya kiarabu na elimu zake, na mjuzi wa lugha nyinginezo naye ana elimu zake kutegemea vitabu ambavyo kila mmoja amevitumia kupata elimu. Tabia ya Waislamu wa kawaida kutegemea tu maneno au uamuzi wa shekhe peke yake, ni makosa makubwa kwa sababu anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: “Saa moja ya kutafuta (kujifunza) elimu ni bora kuliko miaka sitini ya ibada.” Vile Vile anakaririwa akisema kuwa: “Usingizi wa mtu mmoja mwenye elimu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko ibada ya usiku mzima ya kundi la wajinga elfu moja.” Maana yake ni kwamba mwenye elimu ndiye mwenye hakika ya kila atendalo. Maneno haya yote yanaonyesha wazi umuhimu wa kila Mwislamu kujifunza elimu yoyote ile iliyo halali na yenye manufaa, mbali na elimu ya dini. Kwa mfano tutaona kuwa katika Qur’ani kuna elimu nyingi za sayansi. Kama shekhe amehitimu Qur’ani mpaka kufasiri, lakini hana elimu ya sayansi, ni vipi shekhe huyo ataweza kufasiri aya zinazohusiana na sayansi? Je, kuna shekhe mwenye kitabu cha sayansi cha kiarabu hapa kwetu? Upungufu huo ndio unaopelekea tafsiri potofu za Aya japo isiwe makusudi. Tukumbuke kuwa baadhi ya wanasayansi wazungu wanasilimu mara tu wakikuta “ukweli wa kisayansi” katika Qur’ani! Sababu yake ni kwamba wanatambua kuwa miaka iliyoshuka Qur’ani elimu hizo hazikuwepo duniani. Zaidi ya hayo tutambue kuwa, hivi sasa dunia nzima inaimba wimbo wa Sayansi na Teknolojia. Maana yake ni kwamba katika misingi hiyo, ni lazima tufahamu kuwa Sayansi na Teknolojia vimejengeka katika Ukweli. Njia pekee ya kupata ukweli ni kupata elimu sahihi ya jambo linalohusika. Katika karne hii hakuna nafasi tena ya kuamini vitu visivyo na ukweli wowote. Hii ni enzi ya uwazi na ukweli. Katika dunia nzima kuna imani nyingi za dini ambazo kimsingi hazina ukweli wowote. Kwa mfano imani za wenyeji wa Jamaica juu ya marehe14


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 15

katika Uislamu

mu Haile Selassie si za kweli. Ukichunguza historia ya Vita Kuu ya Pili ya dunia, utakuta maelezo ya wahusika wakuu mbali mbali; na hasara walizowatia maadui zao. Lakini ukirejea Encyclopedia of Second World War, utakuta maelezo yenye ukweli tu ambayo mara nyingine ni tofauti na imani za watu kuhusu matukio fulani ya kivita ya vita hivi. Mnamo tarehe 29 Septemba, 1999 saa kumi na mbili na robo asubuhi, Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujerumani ilitangaza mahojiano na bwana Mohamed Saidi wa Tanga mwandishi wa kitabu kipya: The Life and Times of Abdul Wahid Sykes, kuhusiana na waasisi 17 Waislamu waanzilishi wa chama cha TANU hapa Tanzania. Ni ajabu jinsi ambavyo hatusikii kabisa majina ya wazee hao mashuhuri kisiasa! Badala yake, historia tunayoisikia ni ile ya kuwasifu watu wengine, kinyume na ukweli kwamba Waislamu ndio viongozi wakuu wa harakati za uhuru Tanzania. Maelezo yote haya yanaonyesha kuwa, utafiti wa kielimu ndio pekee uwezao kumfikisha mtu kwenye ukweli, na siyo tu mazoea au imani za kufuata matakwa ya watu fulani kwa nyakati fulani. Ulimwengu wa leo, elimu yoyote ile haitegemei lugha maalumu. Kwa mfano Wajapani walipata ujuzi wao wa Sayansi na Teknolojia huko Amerika na Ulaya Magharibi katika lugha ya kiingereza. Hivi sasa Wajapani wanatengeneza gari zima kwa mafunzo ya lugha ya Kijapani kitupu hata jina la msumari! Je, hilo gari halifanyi kazi sawa sawa? Je, ubora wa bidhaa za Japan umepungua? Jambo la msingi ni kwamba lugha ni njia ya kuipata elimu yoyote ile, kwa hiyo lugha zote zitumike ili watu wapate elimu. Tusitumie kiarabu kuficha ukweli na kuifanya dini kuwa ngumu hata kwa mambo ya kawaida ya ibada za kila siku. Kwa mfano hapa kwetu kuna misikiti mingi ambayo mashekhe wake hawataki kutoa elimu ya kuosha na kukafini maiti kwa watu wote, ila watu fulani tu wa kudumu, kwa sababu kuna ushuru wa kuosha maiti! Utadhani kuosha maiti ni ajira! Lakini mashekhe hao hao wanatueleza kuwa akizikwa Mwislamu bila kuoshwa, Waislamu wote wa mahali hapo huandikiwa dhambi! Kama ni 15


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:18 PM

Page 16

katika Uislamu

wajibu kwa sote, basi ni lazima kila Mwislamu afahamu kufanya kazi hiyo! Nimetoa mfano huu kuonyesha kuwa kuna mambo kadhaa tunayofichwa waumini wa kawaida. Kimsingi hata huko kumwosha maiti Mwislamu mwenzetu kwa kulipwa ni haramu lakini Waislamu hatujui! Tusichukulie upungufu mkubwa tulionao hapa kwetu katika elimu ya dini tukadhani kuwa dunia nzima iko hivyo! Katika nchi za India, Pakistan, Bangladesh, Malaysia na Indonesia, utawakuta wasomi wengi wenye shahada (Degree) mpaka tatu au tano za dini! Je, wasomi kama hao watakuwa sawa na Mashekhe wetu wa mitaani? Ni lazima tutambue na kukubali kasoro hii na tufanye juhudi zote kuiondoa. Vinginevyo tunaweza kuaibika mbele ya wajuzi wa mambo ya dini yetu wasio Waislamu! Kwa hiyo msomaji wa kitabu hiki asishangae kwa nini hajawahi kuyasikia haya atakayoyakuta humu! Elimu ya dini ni kubwa mno kuliko tunavyoichukulia. Baadhi ya sababu za msingi ni hizo nilizozitaja kwa ufupi. Kama waumini wa kawaida wanafichwa jinsi ya kuosha na kukafini maiti, je, ukweli ambao unaweza kuwaunganisha Waislamu wote na kuwa kitu kimoja utapokelewa vipi? Ni viongozi wangapi (mashekhe) wako tayari kupoteza vyeo vyao ili Uislamu uwe mmoja? Naomba Mwenyezi Mungu aniepushe na kuwa miongoni mwa wale wafichao ukweli (Qur’ani 2:146) kwa unafiki. Jambo la maana sana katika kitabu hiki, tutachunguza sababu kwa nini sisi Ummat Muhammad (s.a.w.w.) tutagawanyika katika makundi 73 hadi kufikia Siku ya Kiyama, na makundi yote yataangamia motoni kasoro kundi moja tu! Leo hii Waislamu tunaongezeka na misikiti inajaa, lakini wengi wetu tutaangamia! Kwa nini? Endelea kusoma ufahamu. Rejea: Sahih Muslim, Jz. 8 uk.7 kuhusu Waislamu kugawanyika makundi 73. Isa Rwechungura DODOMA - TANZANIA. 27 DHUL QAA’DAH, 1418 A.H. 26 MACHI, 1998 A.D. 16


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 17

katika Uislamu

MAELEZO JUU YA MWANDISHI WA KITABU HIKI NA HISTORIA FUPI YA UTAFITI WAKE Mimi ni mzaliwa wa Mkoa wa Kagera, kutoka miongoni mwa Tarafa ambazo Waislamu wakazi ni kama asilimia mbili hivi kwa kukisia. Kwa uchache wetu huo, tulilazimika kusoma katika shule za Wamisionari wa kikristo na hivyo kufundishwa Ukristo kama sehemu ya masomo yetu. Hali hiyo ilinifanya kuwa mtafiti mapema sana kuhusu tofauti za Uislamu na Ukristo. Baadaye kidogo nilipofikia darasa la tatu, nilihamia shule ya Serikali za mitaa ambako kila mwanafunzi alikuwa huru kujifunza dini yake. Shuleni hapo kulikuwepo ‘Madrassa’ lakini kwa uchache wetu wanafunzi Waislamu, pamoja na uchumi duni wa wazazi wetu, mwalimu wetu hakulipwa mshahara wa uhakika na hivyo tukakosa masomo muhimu. Kwa hiyo elimu yangu ya dini sikuipata utotoni bali niliipata kwa kiasi kikubwa, kwa jitihada zangu ukubwani kwa kusoma vitabu mbali mbali. Lengo langu kueleza haya yote nataka kuonyesha kuwa mtu yeyote akiweka nia, anaweza kuitafuta na kuipata elimu ya dini bila kujali umri wake. Isitoshe Mtume (s.a.w.w.) alipotuamrisha kutafuta elimu hadi China alikusudia Waislamu wote. Hata hivyo natambua kuwa watakaosoma kitabu hiki watapata shauku ya kutaka kujua ni vipi nilipata elimu zote hizi iwapo sikupitia njia za kawaida yaani kuanzia Madrassa na kupitia mashekhe kadha wa kadha kwa miaka mingi kama tulivyozoea. Kwa kweli namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia kipaji cha lugha ya kiingereza tangu shule ya msingi. Bado ninaamini kuwa iwapo ningesoma dini kupitia mfumo duni tuliouzoea, nisingeweza kugundua yote haya. Pamoja na ukweli kwamba ujuzi wa lugha ya kiingereza umedidimia kwa miaka mingi sasa mashuleni, mimi nilijibidisha binafsi kutokana na 17


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 18

katika Uislamu

mazoea yangu ya kupenda kusoma vitabu mbali mbali. Kwa hiyo katika shule ya msingi nilikuwa miongoni mwa wanafunzi wanaoongoza kwa ujuzi wa lugha hiyo. Hiyo ni neema ya Mwenyezi Mungu. Nikiwa shule ya sekondari, nilishinda mashindano ya uandishi wa Insha katika lugha ya kiingereza. Nilipata nafasi ya kwanza miongoni mwa wanafunzi 245, walioshiriki mashindano hayo. Shule yetu ilikuwa ni sekondari ya Ufundi, ikipokea wastani wa wanafunzi kumi bora zaidi, toka kila mkoa. Siku hizo zilikuwepo shule mbili tu za aina hiyo nchi nzima. Baada ya kumaliza masomo na kuanza kazi, nilipata bahati ya kupelekwa Indonesia kwa masomo zaidi, mara mbili miaka ya themanini. Indonesia ndiyo nchi yenye Waislamu wengi kuliko zote duniani. Katika safari za kuelekea huko nilipata bahati pia kupitia India, Malaysia na Pakistan na kuwaona Waislamu wa huko wanavyoendesha ibada zao pamoja na mtazamo wao juu ya Uislamu. Niligundua kwamba Uislamu wa hapa kwetu ni tofauti na huko, kwa sababu kwa mfano, huko Pakistan masomo ya dini yanayofundishwa shule za msingi ni ya juu zaidi kuliko hata elimu ya mashekhe wetu walio wengi! Mfano mdogo ni kwamba utaona misikiti mingi hapa kwetu wanazuia mtu kuingiza mkono kwenye birika (reservoir) la maji, kwa madai kuwa maji yatatenguka udhu! Lakini hata ukirejea hukumu sahihi za Sunni, utakuta kuwa maji kama hayo hayawezi kutenguka udhu kwa sababu hiyo tu! Kiasi fulani cha maji hakiwezi kutenguka udhu kwa kuingia najisi seuze kuingiza mkono tu. Nikiwa huko Indonesia nilipata fursa ya kubadilishana mawazo na wenyeji wangu na kwa mara ya kwanza nikapata bahati ya kuona vitabu muhimu vinavyoongoza Uislamu kama Sahih Muslim, Sahih Bukhari, Sahih Tirmidh, Tarikh Tabari n.k. Kwa hakika Mwislamu yeyote asiyewahi kusoma vitabu hivyo, afahamu kuwa hajaujua Uislamu, kwa sababu yaliyomo humo ni mazito na ni tofauti na imani zetu za Kurithi tulizopokea toka kwa wazazi wetu au mashekhe wetu bila uchunguzi wowote wa kielimu!

18


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 19

katika Uislamu

Masomo yangu huko Indonesia yalinishirikisha na wafanyakazi ambao kwa mkataba ulionipeleka huko, wa serikali mbili, walitakiwa pia kuja Tanzania kusimamia utekelezaji wake. Walipofika huku kwetu na kutembelea misikiti yetu, walishangaa kwa mfano walipoona jinsi ambavyo watu hawazingatii kuswali kwa unyenyekevu. Halafu walishangaa utaratibu tunaotumia misikitini wa kumkuta mtu anasali ukampiga begani ili awe Imam wako! Waliuliza kwamba unapompiga mtu begani unajuaje kama anasali Swala ipi; yaani inawezekana analipa Swala fulani au anaswali Sunna fulani au ni mtu asiyefahamu kanuni za Swala! Walinieleza kwamba huko kwao kuna Chuo maalum cha kufundisha kanuni za Swala kwa mwaka mmoja! Sisi hapa tunaona Swala ni kitu kidogo na kwamba kila mtu anajua kuswali au kuswalisha. Kutokana na mwangaza huo, mnamo, mwaka 1982 nilijikuta na maswali mengi kichwani kuhusu asili ya madhehebu. Nilisoma vitabu vingi kutoka Bilal Muslim Mission-Dar es Salaam kwa miaka mitatu nikapata mwangaza mkubwa sana. Namshukuru sana Hujjatul Islam Seyyid Saeed Akhtar Rizvi kwa kujibu barua zangu zote na kufafanua mambo mengi ya dini yaliyonitatiza wakati huo. Alinialika rasmi kutembelea taasisi yake kwa wiki moja na akanipatia vitabu vingi zaidi. Lakini sikuishia hapo bali niliandika barua na kuzituma katika taasisi zaidi ya nane za kiislamu duniani, kuomba msaada wa vitabu zaidi hasa juu ya historia ya Uislamu. Nilipokea vitabu vingi na kuvisoma kwa makini. Mwisho niligundua ukweli kwamba kwa hakika kulitokea fitna kubwa katika Uislamu. Mnamo miaka ya tisini na moja, niliandika makala (pamphlet) na kuiwakilisha kama Mada katika semina ya kiislamu iliyofanyika Singida chini ya Bilal, ambayo ilijumuisha Waislamu toka karibu mikoa yote. Mada hiyo ilikuwa juu ya hatari za Waislamu kutofahamu madhehebu yao. Washiriki wa semina waliomba nakala zake wakapewa lakini hapakuwepo uwezo wa kumpa kila mmoja.

19


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 20

katika Uislamu

Baadaye nilirekodi hotuba hiyo katika kanda za kaseti na watu wengi waliomba wazipate lakini nilishindwa kutosheleza mahitaji yao. Hata hivyo kwa kadri nilivyozidi kupokea na kusoma vitabu zaidi, nilipata ushahidi muhimu sana kuhusiana na hoja mbali mbali. Mwisho nikaamua kuipanua hiyo ‘Pamphlet’ ili iwe kitabu kamili chenye hoja zote muhimu. Kazi hii nimeikamilisha baada ya miaka 16 ya utafiti! Nilitambua ugumu wa Waislamu walio wengi kuweza kupata na kusoma vitabu vyote nilivyopitia, kwa muda wote huo, ili kupata ukweli wote huu. Ndiyo maana nilifikia uamuzi wa kuandika kitabu hiki, ili kurahisisha kazi ya mtu yeyote atakayetaka kuchunguza ukweli huu. Napenda kusisitiza tena kwamba vitabu vingi vya lugha ya kiarabu, hata pale vinapofasiriwa katika kiingereza, utakuta kwamba kiingereza chake ni kigumu pia; kwa sababu kiarabu chake pia ni kigumu kama nilivyoeleza nyuma. Kitabu kama Nahjul Balaghah utakuta tafsiri yake ya kiingereza unaisoma na kamusi (Dictionary) pembeni, vinginevyo hutaambulia kitu. Ndiyo maana nasema kuwa namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kipaji cha kufahamu kiingereza kuliko ningefahamu kiarabu kwa ngazi ya hapa kwetu ambayo haitoshelezi kabisa kielimu. Mpaka hapa tumeona kuwa milango ya elimu ipo wazi kwa wenye kuitafuta kwa bidii. Sina maana kwamba mimi nimehitimu sana! Kwa kweli bado naendelea kupokea vitabu mbali mbali toka nje, na hapa nchini. Elimu ya dini ni kubwa mno, na mjuzi wa yote ni Mwenyezi Mungu. Jambo la maana ni kwamba kila Mwislamu ajitahidi kupata elimu ya msingi ya dini ili imani yake ikamilike. Elimu nyinginezo zaidi ya hapo zitategemea bidii ya mtu. Unapofariki, Malaika hukuuliza maswali ya kupima ukamilifu wa imani yako ya Uislamu. Hilo halina msamaha. Katika ulimwengu wa Shia, kielimu mimi ni mtu mdogo sana wala sina cheo chochote cha ujuzi wa dini! Nilichofanya hapa ni kuitikia mwito wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba “Enezeni mafunzo yangu japokuwa unaifahamu Aya moja tu.” Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri ngazi za ujuzi wa dini ni za juu sana kuliko kijitabu hiki kidogo. 20


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 21

katika Uislamu

Sababu kubwa ya kueleza ujuzi wangu wa lugha ya kiingereza siyo kujisifu bali nataka ieleweke wazi kuwa ujuzi wa lugha yoyote peke yake, hautoshi kumwezesha mtu kuandika kitabu. Mwandishi wa kitabu chochote kile ni muhimu awe na ujuzi wa uandishi au kipaji cha uandishi. Lazima kitabu kiwavutie waliokusudiwa kukisoma, na maelezo yake yawe na mtiririko unaofaa. Matukio yaelezwe kama yalivyofuatana n.k. Mara nyingi tunasikia wanafunzi wakilalamika kuwa mwalimu fulani ana elimu kubwa lakini hajui kufundisha. Njia za kueneza mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) zipo nyingi. Yawezekana mtu akawa na kipaji cha kutoa hotuba za kuwavuta wasikilizaji. Kwa hiyo ni vizuri anayetaka kufanya ‘tabligh’ kwanza aelewe kipaji chake na aendeleze kipaji hicho. Kwa kweli ujuzi wa lugha ni njia tu ya kupata elimu iliyokusudiwa. Kufikisha elimu hiyo kwa watu wengine, ni suala linalohitaji kipaji au ujuzi mwingine tofauti. ‘Tabligh’ ina misingi yake. Kwa upande mwingine kama sisi wazazi tunataka vijana wetu wawe na moyo wa kuipenda dini, ni muhimu sana sisi wenyewe tuonyeshe mfano wa kujali dini. Mimi baba yangu alifariki nikiwa na miaka miwili tu. Lakini marehemu mama ambaye hakujua kusoma wala kuandika, alikuwa tayari keshafundishwa kuswali Swala tano na marehemu baba! Sikuwahi kumuona mama akipitwa na kipindi cha Swala maisha yake yote! Leo hii sisi elimu tuliyonayo pamoja na urahisi wa kuipata elimu zaidi, bado hatusali! Je! hao watoto wetu vipi wataipenda dini?

21


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 22

katika Uislamu

ASILI YA TOFAUTI KATI YA SUNNI NA SHIA ITHNASHERI Waislamu wote tunakubaliana kuwa katika uhai wote wa Mtume (s.a.w.w.), Uislamu ulikuwa kitu kimoja kwa maana kwamba hayakuwepo madhehebu kama tunavyoyaona wakati huu. Wapo mashekhe wanaofundisha kwamba kuhitilafiana ni ‘Ijtihad’ na kwa hiyo ni katika njia ya Mwenyezi Mungu. Lakini ukichunguza tofauti hizo, utakuta mambo yanayopingana na Qur’ani na Sunna! Je, hayo nayo ni katika njia ya Mwenyezi Mungu? Maneno yanayodaiwa yalisemwa na Mtume (s.a.w.w.) kwamba: ‘Kuhitilifiana kwa maulamaa ni rehema.’ Kusudio la maneno hayo siyo hilo. Maana yake ni kwamba watakapohitilafiana maulamaa, itakuwa ni nafasi nzuri ya kukaa pamoja na kujadili tofauti zao na mwisho kuafikiana. Kuendelea kupingana kwa maulamaa siyo misingi ya Uislamu. Rehema iliyopo hapa ni kule kupanuana mawazo kielimu. Lakini iwapo atatokea ulamaa akafanya ijtihad yake akadai kuwa wakati huu wa sayansi na teknolojia, Waislamu hatuna muda wa kutosha kuswali Swala tano bali tuanze kuswali Swala tatu tu, je, itafaa tukubaliane naye? Pana rehma gani kuachana na Sunna sahihi na Qur’ani? Pengine tusingejali kuchunguza jambo hili iwapo lisingekuwa na madhara yoyote kwetu. Kwanza tunafahamu kuwa Waislamu wengi hawalipi uzito suala la madhehebu. Wengi wetu hatufahamu kwa nini tunaitwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni wafuasi wa hukumu za Imam Shafii! Maana yake ni kwamba tunaendeleza Uislamu wa kurithi! Kwa kawaida ni vigumu kumpata Mwislamu aliyechagua mwenyewe madhehebu yake kwa akili yake! Hata Wakristo ni hivyo hivyo. Dini ya mtu au madhehebu yake hutegemea walioleta dini mahali hapo kwa mara ya kwanza! Lakini kwa upande mwingine tutaona kuwa hizi imani za dini za kurithi, zinaambatan22


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 23

katika Uislamu

ishwa na mila potofu kama sehemu ya dini. Katika maisha ya makabila mbali mbali utakuta mila fulani zilizoungana na dini na kuwa sehemu ya dini! Kadri urithi huu utakavyopitia vizazi kadhaa, ndivyo itakuwa vigumu kutenganisha dini ya kweli, mbali na mila ambazo mara nyingi ni potofu. Na hiyo ndiyo sababu kubwa inayofanya Uislamu uonekane mgumu kutokana na Waislamu kulazimika kutekeleza yasiyohusiana na dini. Hali hii yadhihirisha kuwa Uislamu tulionao wakati huu ni mchaganyiko wa dini na utamaduni. Haya yote yaonyesha kuwa, katika kipindi kirefu cha karne 14 za Uislamu wetu huu, dini yetu imepitia mikononi mwa watawala wengi na tamaduni nyingi kiasi kwamba kuna kasoro nyingi zilizopenyeza katika mafunzo halisi ya dini na kubadili sura ya Uislamu kiasi kikubwa. Ukichunguza utaona kuwa hiyo ni sababu mojawapo iliyopelekea kutugawanya Waislamu kwa sababu tamaduni za mataifa na makabila mbali mbali zinatofautiana, na hivyo hivyo watu wanatofautiana matendo yao. Bali kama tulivyotangulia kuona, dini ni amri za Mwenyezi Mungu zisizobadilika na ndiyo maana hatustahili kabisa kurithi dini. Tunatakiwa kuelewa dini kwa kutumia elimu za kutegemewa. Qur’ani nayo inatukataza imani za dini za kurithi.

“Na wanapoambiwa ‘Njooni katika njia ya Mwenyezi Mungu na Mtume’ husema: ‘Yale tuliyowakuta nayo baba zetu yanatutosha’. Vipi! Hata kama baba zao hawakujua kitu na hawakufuata njia ya haki?” (Qur’ani 5:104). Qur’ani inawakemea wale ambao hung’ang’ania waliyorithi kwa wazazi wao bila kuyachunguza kujua asili yake ni nini. Aya hii inakubaliana na 23


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 24

katika Uislamu

ukweli kwamba ibada yoyote anayofanya mtu bila kuielewa binafsi, kwa mfano kuswali Swala tano kwa sababu ya kulinda heshima ya marehemu baba yako aliyekuwa anasali kila siku, ili na wewe uonekane mchamungu kama baba yako! Swala kama hiyo haipokelewi na Mwenyezi Mungu kwa sababu unatakiwa kuswali Swala tano kwa kutambua wajibu wako kwa Mwenyezi Mungu tu. Kwa hiyo mtu mwenye kutambua wajibu wake huo, siku zote atajitahidi kuswali kwa kufuata kanuni za Mwenyezi Mungu ili kumridhisha na kukubaliwa Swala zake. Na ili kuzifahamu kanuni za Mwenyezi Mungu, itambidi mhusika atafute elimu. Hebu tuone Qur’ani inasemaje:

“Vipi! yule mnyenyekevu wakati wa usiku wa manane, akisujudu na kurukuu, akijitayarisha kwa (safari) ya akhera na kutumaini msamaha wa Mola wake! Sema: Je, wale wenye elimu na wale wasio na elimu ni sawa? Ni wale wenye ujuzi ndio wenye kujali.” (Qur’ani 39:9). Aya hii yaonyesha kuwa hakuna nafasi ya ujinga katika dini. Kila unachokifanya ukifanye kwa ujuzi na yakini. Aya zifuatazo zinaonyesha kuwa kama mtu alipotezwa na watu wengine, hata hivyo asitegemee msamaha kwa sababu itakuwa kinyume na lengo la binadamu kupewa akili. Lazima binadamu awajibike kwa matumizi mabaya ya akili yake:

24


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 25

katika Uislamu

(a) “Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu (ili awalipe); Hapo wanyonge waliopotea kwa ajili ya kuwafuata wakubwa zao waliojivuna watawaambia: ‘Hakika tulikuwa wafuasi wenu, je mnaweza kutuondolea kitu kidogo hivi katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?’ Hao wakubwa zao watajibu kuwa, ‘Angalituongoza Mwenyezi Mungu bila shaka tungelikuongozeni. Lakini sasa ni mamoja kwetu tukitapatapa au tukisubiri hatuna pakukimbilia.” (Qur’ani 14:21).

(b) “Wakati wale waliofuatwa (viongozi) watakapowakana wafuasi (wao) huku wakiona adhabu yao (inayowasubiri); (hali ya kuwa) uhusiano wao (wa kidunia) umekatwa.” (Qur’ani 2:166).

(c) “Na wale wafuasi watasema: ‘Kama tungeweza kurejea (duniani), tungewakana kama walivyotukana.’ Hivyo Mwenyezi Mungu atawaonyesha matendo yao ambayo watayajutia majuto makuu, na hawataondolewa motoni.” (Qur’ani 2:167).

25


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 26

katika Uislamu

(d) “Atasema: Ingia motoni kati ya umma zilizopita kabla yenu miongoni mwa majini na binadamu; kila umma utakapoingia, utawalaani wa nyuma yake mpaka wote watakapoingia motoni; wa mwisho wao watasema kuwaambia waliotangulia: ‘Ee Mwenyezi Mungu! hawa (ndio) waliotupoteza kwa hiyo wape adhabu mara mbili motoni.’ Naye Atasema: Kila mmoja wenu atapata (adhabu) mara mbili ila hamfahamu.” (Qur’ani 7 : 38 ). Nimetangulia kueleza jinsi ambavyo Uislamu ulikuwa kitu kimoja pale mwanzoni katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Lakini tunaona leo hii Waislamu dunia nzima tumegawanyika makundi mawili kiitikadi nayo ni SHIA NA SUNNI. Duniani Waislamu wote jumla yetu ni bilioni moja. Kati ya idadi hiyo, Waislamu milioni 750 ni madhehebu ya SUNNI, na Waislamu milioni 250 ni madhehebu ya SHIA. Sasa tuchunguze kwa nini kulitokea mfarakano huu miongoni mwetu. Mara tu alipofariki Mtume (s.a.w.w.) kabla hata hajazikwa, kulitokea fitina kubwa miongoni mwa Waislamu wa wakati huo walioishi hapo Madina. Kulitokea kundi moja likadai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuacha wasia kuhusu uongozi wa Waislamu kwa hiyo Waislamu wachague kiongozi wa Umma wa Waislamu. Lakini kundi la pili la Waislamu walikataa na kusema kuwa Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake, na katika matukio kadhaa, alieleza wazi Uongozi wa Waislamu baada yake. Kwa ndugu zetu Sunni (au Ahlul Sunna Wal-Jamaa) wanadai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuacha wasia. Tuahirishe kidogo kujadili hoja zao na tuanze na madai ya Shia Ithnasheri ambao tunasisitiza kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia. Hata hivyo kabla ya kuzama katika mjadala huu, ni vizuri kwanza tupate mwangaza juu ya uhalali wa vitabu vinavyotambuliwa kuwa ni sahihi kwa upande wa madhehebu ya Sunni. Vitabu hivyo idadi yake ni sita ambavyo huitwa ‘Sitat Sihah’ navyo ni hivi vifuatavyo: Sahih Bukhari. Sahih Muslim. Sahih Tirmidhi. Sunan Ibn Majah. Sunan Abi Daud. 26


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 27

katika Uislamu

Sunan Nasai. Hivi ndivyo vitabu vinavyotegemewa sana na madhehebu ya Sunni baada ya Qur’ani. Ushahidi mwingi wa kuthibitisha maelezo yaliyomo humu, umetolewa katika vitabu hivyo kwa kiasi kikubwa. Lakini katika ulimwengu wa wasomi wa dini na historia ya dini, kuna vitabu vingi zaidi vya kutegemewa kama tutakavyoona mbele Inshallah. Historia ya Uislamu ni ndefu sana. Kwa Waislamu wenye ujuzi wa historia kidogo ya Nabii Musa (a.s.), Nabii Ibrahim (a.s.) na Nabii Isa (a.s.) wanafahamu kuwa Manabii wote hao waliacha warithi wao nyuma yao ili waendeleze dini katika misingi ile ile ingawa mazingira ya wakati huo hayakuwawezesha warithi hao kufanya kazi yao kwa ufanisi. Na kwa kuwa Manabii wote wanaongozwa na Mwenyezi Mungu, bila shaka uchaguzi huo wa warithi ni wa Mwenyezi Mungu. Qur’ani (38:26), (21:73), (3:30), (28:68), (28:5). Nabii Adam alimteua Shiith. Nabii Ibrahim alimteua Ismail. Nabii Ya’kub alimteua Yusuf. Nabii Musa alimteua Yusha bin Nuun. Nabii Isa alimteua Shamuun. Nabii Muhammad alimteua Imam Ali Ibn Abu Talib. Ilimradi sisi Waislamu tunachambua Biblia na kuwaeleza Wakristo kuwa dini ilikuwa ni moja kwa Manabii wote, itakuwaje Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w.) alifariki bila kuacha wasia juu ya nani awe kiongozi nyuma yake? Wakati ambapo Manabii waliomtangulia katika dini ile ile, waliacha warithi wao kwa amri ya Mwenyezi Mungu? Tukirejea kwenye Qur’ani tunaona kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha kuandika wasia (Qur’ani 2:180) na (Qur’ani 2:240). Kwa maana hiyo tutambue kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mstari wa mbele kutekeleza amri zote za Mwenyezi Mungu yaani Qur’ani. Ilipoteremka amri ya kuswali au kuhiji au kufunga Ramadhan, Mtume (s.a.w.w.) alitekeleza mara moja. Hakuna wakati ambapo Mtume (s.a.w.w.) alipuuza amri yoyote ya Mwenyezi Mungu hata iwe ndogo namna gani. Kwa misingi hiyo ni vipi Mtume (s.a.w.w.) angeacha kuandika wasia na hivyo kumuasi Mwenyezi Mungu! Tuchambue mambo kibusara. 27


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 28

katika Uislamu

Uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) umeelezwa pia katika Biblia Suala hili la uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni jambo zito sana kwa sababu ndilo limetugawanya Waislamu siku ile ile aliyofariki Mtume (s.a.w.w.). Ingawa matukio kadhaa ya kihistoria yanaonyesha kuwa njama za kuhujumu wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya suala hili, zilifanyika mapema kwa kificho kabla hajafariki. Kimsingi ni kwamba, makabila fulani ya Waarabu hayakufurahia kuona ukoo wa Mtume (s.a.w.w.) unapata Utume na kisha uongozi baada ya Mtume nao unaendelea kuwa katika ukoo wa Mtume (s.a.w.w.) wa Bani Hashim. Chuki za kijahiliya ndilo chimbuko la mgogoro huu wa uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.):

“Hakika dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu. Na waliopewa kitabu hawakuhitilafiana ila baada ya kuwajia elimu, kwa sababu ya hasadi tu baina yao. Na anayezikataa aya za Mwenyezi Mungu, basi haikia Mwenyezi Mungu ni Mwepesi wa kuhesabu.� (3:19);

28


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 29

katika Uislamu

“Watu walikuwa kundi moja, basi Mwenyezi Mungu akawapelekea manabii watoao habari njema na waonyao, na pamoja nao akateremsha Kitabu kwa haki, ili ahukumu baina ya watu katika yale waliyohitilafiana. Wala hawakuhitilafiana katika hicho (Kitabu) ila wale waliokipewa baada ya kuwafikia dalili zilizo wazi, kwa sababu ya uasi kati yao. Hapo Mwenyezi Mungu akawaongoza walioamini kwa yale waliyohitilafiana katika haki kwa idhini Yake, na Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka.” (2:213)

“Na hawakutengana ila baada ya kuwafikia elimu, kwa sababu ya uasi baina yao na kama isingelikuwa kauli iliyotangulia kutoka kwa Mola wako juu ya muda uliowekwa, lazima ingelihukumiwa (sasa hivi). Na kwa hakika wale waliorithishwa Kitabu baada yao wanakitilia shaka inayowahangaisha.” (42:14)

“Na tukawapa maelezo wazi ya amri, lakini hawakukhitilafiana ila baada ya kuwafikia elimu, kwa uasi tu baina yao, hakika Mola wako atahukumu kati yaoSiku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.” (45:17) Lakini kwa msimamo wetu Waislamu, kwamba dini ilikuwa moja ya Uislamu kwa manabii wote, hebu tuangalie katika Biblia tuone maelezo 29


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 30

katika Uislamu

kuanzia kwa Nabii Ibrahim (a.s.) hadi mpaka kwa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake (a.s.). Nabii Ibrahim (a.s.) aliwazaa watoto wawili yaani Nabii Is’haqa (a.s.) kwa upande wa Wayahudi, na Nabii Ismail (a.s.) kwa upande wa Waarabu. Baada ya Wayahudi kutowatii Mitume, Nabii Isa (a.s.) aliwaeleza kuwa ufalme wa Mungu utaondolewa kwao na kupelekwa kwa ndugu zao yaani Waarabu. Tazama (Kumbukumbu ya Torati. 18:15). Kutokana na kizazi cha Nabii Ismail (kwa kufupisha maelezo) ukapatikana ukoo mtukufu wa Bani Hashim kwa vizazi mbali mbali hadi kufikia kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo kwa kuzaliwa Mtume Muhammad, ikawa ahadi ya Mwenyezi Mungu kwa Nabii Ibrahim imetimia alipomwambia kuwa: “Ibrahimu akamwambia: Lau kwamba Ishmaeli angeishi mbele yako. Mungu akasema, sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake. (Bibila; Mwanzo: 17:18-19) Utabiri huu unaonyesha jinsi ambavyo Mwenyezi Mungu alitimiza ahadi ya kubariki kizazi cha Nabii Ibrahim (a.s.) kupitia kwa mwanae Nabii Isihaka (a.s.) kwa kuendeleza kizazi chake hadi kwa Nabii Isa (a.s.). Mwisho Nabii Isa (a.s.) anawaeleza Wayahudi kwamba utukufu wa kabila lao kuendelea kuwa na Manabii umekwisha na utahamia kwa ndugu zao waarabu yaani kizazi cha kaka yake (baba mmoja) Ismail (a.s.). “….. Na kwa habari za Ishmail nimekusikia, nimembarika, nitamzidisha, nami nitamuongeza sana sana. Atazaa maseyidi kumi na wawili, nitamfanya awe taifa kuu. (Biblia: Mwanzo: 17: 20).

30


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 31

katika Uislamu

Kisha inaelezwa katika Biblia kuwa viongozi kutoka kizazi cha kuanzia kwa Nabii Ismail (a.s.) hadi kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.), wataendelea kutoka kizazi hicho hata baada ya uhai wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.): “Kwani Bwana Mungu wako amemchagua katika kabila zako zote, asimame atumike kwa jina la Bwana, yeye na wanawe milele.” (Kumb. Torati 18:5). Nabii aliyechaguliwa kwa mataifa yote ni Mtume Muhammad (s.a.w.w.) lakini uongozi wake ni pamoja na wanawe, tena milele! Milele maana yake hadi Siku ya Kiyama. Hapa tutaona kuwa, kwa kadri ya maelezo ya mwenyewe Mtume (s.a.w.w.) katika Hadithi na Qur’ani, watoto wake ni AHLUL-BAYT wake waliokusudiwa katika (Qur’ani 33:33) kama tutakavyoona katika maelezo ya mbele kwa ushahidi kamili. Maana yake ni kwamba utume na ukhalifa vyote vilipangwa kutokana katika ukoo mtukufu wa Bani Hashimu. Hiyo, ni mipango ya Mwenyezi Mungu kwa sababu angependa angemleta Mtume toka kwa Waarabu tu bila kupitia ukoo maalumu unaotokana na Nabii Ismail (a.s.) moja kwa moja hadi kwa Nabii Ibrahim (a.s.). Ndiyo maana kabila la ‘Quraish’ (lenye maana ya wakusanyaji) ni kabila la kizazi cha Nabii Ismail (a.s.). Kabila hilo ndilo lilikuwa na hadhi kubwa miongoni mwa Waarabu kwa sababu ya kazi yao ya heshima ya kuwa walinzi wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu yaani Al-KAABA ambayo ilijengwa kwa mara ya kwanza na Nabii Ibrahim (a.s.) akisaidiana na mwanae (Nabii Ismail).

“Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuh na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu. Kizazi cha wao kwa wao, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (3:3334) 31


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 32

katika Uislamu

“Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu katika fadhila Zake? Basi bila shaka tuliwapa watoto wa Ibrahim Kitabu na hekima, na tukawapa mamlaka makubwa.” (4:54)

Utukufu wa Bani Hashim Katika masomo yatakayofuata baadaye, tutapata maelezo juu ya Waarabu wa makabila ya BANI UMAYYAH na BANI ABBAS, wakipinga kwa nini ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.) uendelee kuwa katika ukoo wa BANI HASHIM. Utukufu wa Bani Hashim unaanzia kabla hata ya Uislamu wa Mtume (s.a.w.w.). Kumbukumbu za historia zinatueleza kuwa: Baada ya Hajira mke wa Nabii Ibrahim (a.s.) kuachwa jangwani pamoja na mwanae Ismail kwa amri ya Mwenyezi Mungu, mahali hapo kwa miujiza kulitokea chemchem ya maji inayoitwa Zamzam. Kabila moja lililojulikana kama Jarham lilipoona kisima hicho kipya cha maji, liliomba ruhusa ya kuhamia hapo na likakubaliwa na Nabii Ibrahim (a.s.). Nabii Ismail (a.s.) alipofikia utu uzima akaoa katika kabila hilo na kupata watoto 12 ambao mkubwa kabisa akiitwa Cedar (kwa lugha ya Kiyunani). Wana wa Ismail waliogezeka sana. Baada ya kupita vizazi kadhaa alitokea mmojawapo katika kizazi hicho aliyeitwa Quraish. Wakati huo alikuwepo mtu toka katika kabila la Khuz’aa aliyeitwa Hulail. Huyu alikuwa na dhamana ya kutunza Al-Kaaba wakati huo. Ikawa Quraish amemwoa binti wa Hulail na huyo Hulail kabla ya kufariki aliusia kuwa dhamana yake ya kutunza Al-Kaaba amemrithisha Quraish. Quraish alianzisha taasisi nyingi mpya kama ‘Dar-un-Nadwa’ (nyumba ya kukutania), mahali ambapo majadiliano muhimu kama vita au amani yalifanyika. 32


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 33

katika Uislamu

Misafara ya biashara ilikutana hapo kabla ya kuanza safari zao. Quraish alianzisha utaratibu wa ‘Siqayah’ (kuwapatia maji mahujaji) na utaratibu wa ‘Rifada’ (kuwalisha mahujaji) siku hizo. Utaratibu huo kwa kadri ya Tarikh Tabari uliendelea kwa miaka 500 baada ya kufariki Quraish. Vile vile ni huyo Quraish aliyefanya matayarisho kuwawezesha mahujaji kulala usiku pale Mash-a’rul-Haram katika ibada ya Hijja. Alikuwa akimulika bonde hilo kwa taa (mioto) nyingi usiku ili mahujaji wasipate taabu. Ni huyo Quraish aliyejenga upya Al-Kaaba na kuchimba kisima cha kwanza cha maji hapo Makka kwa sababu wakati huo kisima cha Zamzam kilishafukiwa muda mrefu kisijulikane mahali kilipokuwa tena. Wanahistoria wanakiri kwamba huyo Quraish alikuwa Mkarimu, shujaa na mwenye huruma. Mawazo yake yalikuwa safi na tabia yake ya kuvutia. Neno lake liliheshimiwa na kutekelezwa kama dini hata alipokwishafariki. Watu walizoea baadaye kuzuru kaburi lake huko Hajun mahali ambapo leo panaitwa Jannatul-Maala. Quraish alikuwa kiongozi mkuu (chief) wa kabila lake ambalo liliitwa jina hilo hilo kwa heshima yake ya uongozi mwema. Alibeba majukumu yote yaliyoinua hadhi ya kabila hilo yaani dhamana ya Al-Kaaba (Hijaba), kunywesha na kulisha mahujaji yaani (Rifada na Siqaya). Alikuwa mshika bendera ya vita (Liwa) na alikuwa Amiri Jeshi Mkuu wakati wa vita (Qiyada). Hizi ndizo sifa kuu zilizowafanya kabila la Quraish kuheshimiwa na makabila mengi ya Waarabu. Huyu Quraish alipata watoto 6 wa kiume na mtoto mmoja wa kike. Katika watoto wa kiume Abdud-Dar alikuwa mkubwa zaidi akifuatiwa na Mughira (aliyejulikana kama Abd Munaf). Lakini Quraish alimpenda sana Abdud-Dar na hivyo alipokaribia kufariki alimkabidhi Abdud-Dar majukumu yote makuu sita ya kabila la Quraish yaliyotajwa hapo juu. Hata hivyo Abdud-Dar hakuwa mwenye uwezo wa kuongoza, wakati ambapo Abd Munaf alionekana mwenye sifa zote za uongozi na hivyo 33


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 34

katika Uislamu

watu walimtii kama kiongozi wao. Kwa hali hiyo ilibidi Abduddar ashirikiane majukumu hayo kwa pamoja na Abd Munaf. Mwisho Abd Munaf alitokea kuwa kiongozi mkuu wa kabila la Quraish. Abd Munaf alipata watoto wa kiume 6 nao ni Hashim, Muttalib, AbddusShams na Nawfil. Hakukuwepo mgogoro wowote katika uhai wa AbdudDar na Abd Munaf. Walipofariki ndipo mgogoro ukaanza miongoni mwa watoto hao kuhusiana na majukumu sita niliyoyataja chini ya dhamana ya kabila la Quraish. Ilikaribia kutokea vita katika mgogoro huo, lakini makubaliano yalifikiwa kwamba majukumu ya Siqaya, Rifada na Qiyada yatekelezwe na watoto wa Abd Munaf; na kwamba majukumu ya Liwa na Hijaba yabakie kwa watoto wa Abdud-Dar. Iliamuliwa pia kwamba uenyekiti wa Darun-Nadwa watashirikiana pande zote mbili. Na hapo ikawa mgogoro umekwisha.

Bwana Hashim Jina la bwana huyu ni maarufu na litaendelea kung’ara katika historia ya Arabuni na Uislamu. Si kwa sababu tu alikuwa babu mkubwa wa Mtume (s.a.w.w.) bali kutokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika uhai wake. Alikuwa mkarimu mno, mwenye hadhi kubwa ya kuheshimiwa na wote kama kiongozi wa Quraish. Alikuwa akiwalisha mahujaji katika kipindi cha Hijja kwa moyo mkunjufu. Lakini kigezo kikubwa cha heshima yake kuu ni jina hilo la Hashim. Wakati fulani kulitokea njaa kubwa sana Uarabuni. Bwana Hashim hakuvumilia kuona mateso kwa wakazi wa Makka. Alichukua utajiri wake wote akaenda Syria akanunua unga na mikate mikavu (mofa) akavileta. Kisha ikawa kila siku anachinja ngamia kadhaa kupika supu ya nyama, mikate na mofa na kuwalisha watu wote hadi njaa ikaisha. Ni kitendo hicho kilichomjengea heshima kubwa kwa watu na akawa ameitwa ‘Hashim’ yaani (anayevunja mikate) ingawa jina lake hasa lilikuwa Amr.

34


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 35

katika Uislamu

Bwana Hashim ndiye mwanzilishi wa misafara ya biashara ya Maquraishi. Aliingia mikataba ya amani na makabila yote yaliyo katika njia kuu ya misafara, kwa sababu siku hizo kulikuwepo na ujambazi na uporaji wa mali za wafanyabiashara. Aliingia pia katika mkataba na Mfalme wa dola ya Byzantine ili kusamehewa ushuru wa aina zote na kodi katika misafara ya biashara ya Maquraishi. Kwa hiyo Maquraishi walianza misafara ya biashara huko Yemen, Syria mpaka Ankara-Uturuki kwa amani. Kutokana na mafanikio aliyoyapata Hashim siku hizo, ndiyo maana katika Qur’ani Mwenyezi Mungu anaelezea tukio hilo kama neema kubwa ya Mwenyezi Mungu kwa Maquraishi: “Kwa ajili ya Maquraish kuzoea, kuzoea safari za Kusi na Kaskazi, basi wamuabudu Mola wa Nyumba hii, Anayewalisha wakati wa njaa na kuwapa amani wakati wa hofu.” (Suratul Quraish).

Utamaduni wa Maquraishi Kulikuwepo na mila ya kutokuwa na matumaini mema iliyoitwa ‘ihtifad.’ Mila hii ilitumika wakati wa shida ili kulinda heshima ya kabila lao. Iwapo familia fulani ilikuwa maskini sana na kushindwa kujipatia chakula, familia yote huondoka kwenda jangwani na kupiga hema na kukaa hadi kifo kiwamalize wote mmoja mmoja bila siri yao kujulikana kwa watu wengine; na hivyo kulinda heshima yao. Bwana Hashim ndiye aliyesimamisha mila hiyo ya kudhalilika na umaskini, na badala yake akaweka mikakati ya kuupiga vita umaskini. Alibuni utaratibu wa kumwunganisha maskini mmoja kwa tajiri mmoja ili mradi familia (wanaomtegemea huyo tajiri na wanaomtegemea maskini) zao ziwe sawa kwa idadi. Kazi ya maskini ni kumsaidia tajiri katika misafara ya biashara. Ziada inayopatikana juu ya mtaji wa tajiri, wagawane sawa; na hivyo umuhimu wa ‘ihtifad’ hautakuwepo tena. Mpango huo ulipokelewa na wote na sio tu uliondoa ufukara, bali pia ulizidisha udugu na mshikamano miongoni mwao. Matendo hayo yangehalalisha umri mrefu kwa Bwana Hashim, lakini ukweli ni kuwa alifariki akiwa mdogo kwa umri wa miaka 25 tu mnamo miaka kama 82 kabla ya kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.) 35


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 36

katika Uislamu

yaani mwaka (488 A.D). Bwana Hashim alikuwa kijana mwenye haiba nzuri na hivyo watawala na machifu mbali mbali walitaka aoe binti zao. Lakini alimwoa Salma binti wa Amr. (kutoka kabila la Adi Bani Najjar) huko Madina. Mke wake huyo ndiye mama yake Bwana Shaibatul-Hamd (aliyejulikana kama AbdulMuttalib). Huyu Bwana Abdul-Muttalib alikuwsa mtoto mchanga wakati Bwana Hashim alipofariki. Bwana Hashim alipata watoto 5 wa kiume lakini watatu hawakupata uzazi. Kati ya watoto hao, Asad alipata mtoto wa kike tu naye akiitwa Fatima Bint Asad - mama yake Imam Ali Ibn Abi Talib. Kwa hiyo ni kutoka kwa Bwana Abdul-Muttalib ambapo kizazi cha Hashim kiliendelea baada yake.

Bwana Abdul-Muttalib Bwana Abdul-Muttalib alizaliwa Madina kwa babu yake mzaa mama. Kazi zote za Bwana Hashim zilirithiwa na Bwana Muttalib. Bwana Muttalib alikwenda Madina na kumleta bwana ‘Shaibatul-Hamd’ yaani mjomba wake. Waliporejea Makka, wakazi wa pale wakadhani kuwa Bwana Muttalib kamleta mtumwa wake (yaani huyo bwana Shaibatul-Hamd). Kwa hali hiyo ikawa Shaibatul-Hamd ameitwa Abdul-Muttalib kwa maana ya mtumwa wa Muttalib, ingawa Bwana Muttalib aliwaeleza wazi kuwa huyo ni mjomba wake! Hata hivyo likashika jina hilo la Abdul-Muttalib. Bwana Muttalib alimpenda sana Abdul-Muttalib lakini Abdus-Shams na Nawfil walimchukia. Alipofariki Bwana Muttalib, Abdul-Muttalib alirithishwa majukumu yake yaani kutoa huduma ya maji na chakula kwa mahujaji (Siqaya na Rifada). Pamoja na uadui wa wajomba zake wawili, matendo yake mema na sifa za uongozi mwema alizokuwa nazo zilimfanya kupata cheo cha Seyyidul-Bat’ha, yaani, Chifu wa Makka. Kuna baadhi ya mashekhe wanaojaribu kueleza kuwa wazazi wa Mtume (s.a.w.w.) hawakuwa Waislamu! Madai hayo si kweli kwa sababu ingawa Waarabu 36


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 37

katika Uislamu

walikuwa katika ujinga mkubwa wa kiroho wakati huo, ukoo wa Bani Hashim waliishi katika misingi ya maadili na sheria za kiislamu (Tawhiid) pamoja na kwamba hakuwepo mtume yeyote. Bila shaka Mwenyezi Mungu alipanga kuongoza ukoo huu katika usafi wa kiroho, akijua kuwa mwisho wake atazaliwa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) mahali hapo. Haiwezekani Mwenyezi Mungu apandikize mbegu bora kwenye shamba chafu! Tunafikia uamuzi huu kutokana na maelezo yafuatayo. Bwana Abdul-Muttalib aliwazuia watoto wake kunywa pombe. Alikuwa akiingia Pango la Hira Mfungo wa Ramadhan na kutumia muda wa mwezi mzima kumkumbuka Mwenyezi Mungu (dhikri) na kuwalisha maskini. Alikuwa pia anaendeleza kazi za baba yake na mjomba wake za kuwalisha mahujaji msimu wa Hijja. Hata wanyama na ndege walilishwa mwaka mzima toka kwake; na kwa hali hiyo aliitwa pia jina la Mutimut-tayr (Mlisha ndege). Baadhi ya hukumu za dini tunazozitumia wakati huu, zilianzia katika uhai wa Bwana Abdul-Muttalib. Kwa mfano alikuwa wa kwanza kuweka nadhiri kama tunavyoitumia leo hii na hukumu zake kidini. Alianzisha hukumu ya kutoa Khumsi (Qur’ani 8:41) katika njia ya Mwenyezi Mungu. Alizuia ndoa kati ya watu wasiostahili kuoana kama ilivyo sasa hivi. Mwizi alikatwa mkono. Uzinifu ulikatazwa katika kabila lake. Alizuia mila ya kuwaua watoto wa kike wanapozaliwa. Alizuia kutufu Al-Kaaba bila nguo yaani uchi. Alipanga kiwango cha fidia kwa mauaji yasiyo ya kukusudia, ngamia 100. Hukumu hizi ziliendelea kutumika mara Uislamu ulipoanza baadaye yaani baada yake. Ingekuwa hukumu hizi zote haziongozwi na Mwenyezi Mungu vipi ziendelee kutumika katika Uislamu? Watu wanaoongozwa na Mwenyezi Mungu hawawezi kuwa makafiri. Historia ya Bwana Abdul-Muttalib ni ndefu mno lakini nitaeleza machache jinsi alivyogundua upya Kisima cha Zamzam kilichojazwa takataka na kupotea muda mrefu kabla ya yeye kuzaliwa. Kisha nitaeleza jaribio la kuishambulia Al-Kaaba lililopangwa na Gavana wa Ethiopia bila mafanikio. 37


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 38

katika Uislamu

Kisima cha Zamzam: Kwa karne kadhaa, Kisima cha Zamzam kilijazwa na kupotea kabisa na hakuna aliyejua kiko wapi au nani alikijaza. Siku moja Bwana AbdulMuttalib alikuwa amelala katika Hatim Al-Kaaba katika ndoto aliagizwa achimbe Tayba apate maji. Aliuliza hiyo Tayba iko wapi lakini ndoto ikakatika bila jibu! Ndoto hiyo ilirudiwa mara tatu na kila mara jina linabadilishwa. Mara ya nne aliambiwa chimba Zamzam. Abdul-Muttalib aliuliza hiyo Zamzam iko wapi na alielezwa alama zake. Abdul-Muttalib akiwa na mwanae wa pekee (wakati huo) walichimba mahali hapo yaani pale pale ilipo Zamzam wakati huu! Siku ya nne ya uchimbaji, kuta za kisima zikaonekana! Kwa jitihada zaidi, maji yalifikiwa. Kwa mafanikio hayo Abdul-Muttalib alipiga ukele, ‘Allahu Akbar’ na kusema: ‘Hiki ni kisima cha Ismail’! Maquraishi walikusanyika na kuanza kubishana kwamba kwa kuwa kisima cha mwanzo kilikuwa cha Ismail, ugunduzi huu mpya ni mali ya kabila lote. Abdul-Muttalib alikataa madai hayo na kuwaeleza kuwa kisima hicho amepewa yeye na Allah. Quraysh walikuwa tayari kupigana na kujaza kisima hicho ili wachimbe upya wote. Mwisho waliafikiana kuwa wapeleke shauri lao kwa mama mmoja mwenye hekima huko Syria. Kila ukoo ulituma mjumbe mmoja mwakilishi. Abdul-Muttalib akiwa na mwanae na wafuasi wake wachache, alikuwa katika msafara huo. Katikati ya jangwa Abdul-Muttalib aliishiwa maji na watu wake. Kundi lake liliteseka kwa kiu kali. Viongozi wa makundi mengine walikataa kuwapa maji hadi wakakaribia kufa. AbdulMuttalib aliwashauri watu wake kuchimba makaburi ili kwamba kila atakayekufa, wenzake wamzike mpaka walau abakie mmoja tu asiyezikwa kuliko wote kutozikwa. Ikawa wamechimba makaburi yao huku viongozi wa vikundi vingine wakifurahia hali hiyo.

38


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 39

katika Uislamu

Siku ya pili Abdul-Muttalib aliwahutubia watu wake kuwa ni dalili ya woga kupokea kifo bila jitihada yoyote ya mwisho. Alipanda ngamia wake na ngamia akasimama. Kwa muujiza ikawa kumetokea chemchem pale mguu wa ngamia ulipogonga ardhi. Maji matamu ya baridi yakabubujika! Abdul-Muttalib alipiga ukelele ‘Allahu Akbar’ na wafuasi wake hivyo hivyo. Walikata kiu, wakajaza maji mikoba yao na ikawa Abdul-Muttalib amewakaribisha makundi ya watu wengine wa msafara nao wateke maji. Watu wake walipinga uamuzi huo kutokana na kitendo cha wenzao hao kuwanyima maji hadi wakakaribia kufa. Abdul-Muttalib aliwaeleza kuwa ‘Iwapo tutafanya kulipiza kisasi kwao tutakuwa sawa na wao’. Hivyo msafara wote ulikusanyika hapo na kuteka maji watakavyo. Kisha hao wapinzani wa Abdul-Muttalib wakasema ‘Ewe Abdul-Muttalib, kwa jina la Mungu, Mungu amehukumu baina yetu, amekupa ushindi juu yetu, hatutapingana tena na wewe kuhusu ‘Zamzam’, Allah ni yule yule aliyeumba chemchem hii hapa jangwani na ndiye aliyekupa hiyo Zamzam’. Baada ya hapo Zamzam ikawa mali ya Abdul-Muttalib. Alichimba kisima hicho kwenda chini zaidi na kukuta sanamu mbili za dhahabu, majambia na mavazi ya vita (deraya). Quraysh walipoona vitu hivyo walidai wapate sehemu yake lakini Abdul-Muttalib alikataa. Mwisho ilipigwa kura ambapo sanamu za dhahabu mfano wa paa ziliangukia kuwa mali ya AlKaaba, lakini majambia na mavazi ya vita vilimwendea Abdul-Muttalib, wakati ambapo Maquraishi hawakupata kitu. Ni wakati huo ambapo Abdul-Muttalib alitoa Khums ya thamani ya vitu hivyo alivyopata, kwa AlKaaba yaani kwa Mwenyezi Mungu.

Abraha ataka kuvunja Al-Kaaba: Tukio la mwisho muhimu lilitokea miaka 8 kabla hajafariki. Wakati huo alikuwa kiongozi wa kabila. Kulitokea Gavana wa Yemen aliyeitwa Abraha al-Ashram. Gavana huyu aliona wivu jinsi Waarabu walivyoienzi Al-Kaaba. Yeye alikuwa Mkristo mkereketwa kwa hiyo aliamua kujenga Kanisa kubwa (Cathedral) huko Sanaa (Mji mkuu wa Yemen) na aliamuru Waarabu waje pale kuhiji. Amri hiyo ilipuuzwa kabisa na si hivyo tu, bali 39


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 40

katika Uislamu

mtu mmoja aliingia ndani na kujisaidia choo humo kanisani! Hasira ya Abraha haikujua mipaka kwani aliamua kulipiza kisasi kwa kuvunja na kuidhalilisha Al-Kaaba. Alielekea Makka na jeshi kubwa. Jeshi lake lilikuwa na tembo (ndovu) wengi, na yeye alipanda tembo mkubwa. Kwa kuwa kabla ya hapo Waarabu hawakuwahi kuona tembo, ndiyo maana mwaka huo ukaitwa mwaka wa tembo, ‘Aamul-Fil’ na ikawa mwanzo wa kalenda ya Waarabu kuhesabu miaka kuanzia mwaka wa tukio hilo. Utaratibu huo wa kalenda uliendelea kutumika hadi katika utawala wa Umar ibn al-Khattab, wakati ambapo kwa ushauri wa Imam Ali Ibn Abu Talib, alianzisha kalenda mpya ya kuanzia pale Mtume (s.a.w.w.) alipohamia Madina yaani Hijra. Habari za Abraha kusonga mbele kuelekea Makka zilifika. Ikawa makabila yote ya Waarabu yaani Quraish, Kanana, Khuzaa na Hudhail walikusanyika kulinda Al-Kaaba. Abraha alituma jeshi dogo kwenda Makka kwanza ili kuteka ngamia na vijana. Mamia kadhaa ya mifugo yalitekwa miongoni mwake ngamia 200 wa Abdul-Muttalib. Alitumwa mjumbe kuwaeleza Maquraishi kwamba lengo la Abraha ni kuvunja Al-Kaaba na iwapo watazuia kazi hiyo watasagwasagwa. Watu walielezwa Jeshi la Abraha lilivyo na nguvu na vifaa vingi imara kuliko mkusanyiko wa Quraish wote. Abdul-Muttalib alijibu kuwa: “Kwa jina la Allah, hatutaki kumpiga vita, lakini hii Al-Kaaba ni nyumba ya Mwenyezi Mungu na ndiye atakayeinusuru au kuacha ivunjwe akipenda hakuna awezaye kuilinda zaidi yake.” Abdul-Muttalib akiongozana na viongozi wenzake maarufu alikwenda kumwona Abraha ambaye alishaarifiwa ugeni huo mapema. Abraha alijua hadhi na heshima aliyonayo Abdul-Muttalib kwa Waarabu-Quraish. Alimkaribisha kwa heshima zote na walipoanza maongezi, Abdul-Muttalib alimwomba Abraha kurejesha ngamia zake. Abraha alishangaa kuona Abdul-Muttalib hatetei Al-Kaaba! Na badala yake anasisitiza ngamia tu bila kujali heshima ya Al-Kaaba ambayo ndiyo kitovu cha dini yake na heshima kuu ya Waarabu! Abdul-Muttalib alijibu kuwa: “Mimi ninamiliki 40


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 41

katika Uislamu

ngamia na hivyo najitahidi kuwaokoa, lakini hiyo nyumba ina mwenyewe ambaye naamini atailinda.” Abraha alishangaa kusikia hivyo na akaamuru ngamia wa Abdul-Muttalib arejeshewe. Mara ya pili Abraha alimwita tena Abdul-Muttalib na kumwuliza kuhusu Al-Kaaba, naye alijibu hivyo hivyo. Ndipo AbdulMuttalib aliposhika mlango wa Al-Kaaba na kumuomba Allah kwamba: “Ewe Allah! Hakika mtu hulinda nyumba yake kwa hiyo Uilinde Nyumba Yako. Ewe Allah! Walinde watu wako dhidi ya balaa la watoto wa msalaba na waumini wake.” Baada ya Swala hiyo Abdul-Muttalib aliondoka na kwenda kilele cha mlima wa Abu Qubays. Abraha naye alisonga mbele kuelekea kwenye AlKaaba. Alipoona kuta za Al-Kaaba aliamuru jeshi lake lianze kuivunja. Mara jeshi lilipokaribia Al-Kaaba, ndipo jeshi la Mwenyezi Mungu likatokea kutoka Magharibi. Wingu zito la ndege wadogo waitwao ‘Ababil’ kwa kiarabu, walitanda juu ya jeshi la Abraha. Kila ndege alikuwa amebeba vijiwe vitatu,viwili miguuni na kimoja mdomoni. Kwa muujiza mvua ya vijiwe vya moto ilinyeshea Jeshi la Abraha kutoka ndege hao na ikawa jeshi lote limeangamia! Abraha alijeruhiwa vibaya na kufariki njiani akikimbia kuelekea Yemen. Tukio hili ndilo linatajwa katika (Qur’ani: Sura 105). Kisa hicho kilitokea mwaka 570 A.D. Mwaka huo ndio alizaliwa Mtume (s.a.w.w.). Mpaka hapa tumeona kuwa kuanzia kwa Nabii Ismail (a.s.), kizazi chake hadi kwa Mtume (s.a.w.w.) kilikuwa kizazi kilicholindwa na Mwenyezi Mungu na kuongozwa katika maadili ya kiislamu kufikia lengo maalum liliokusudiwa. Kama tutaamini kuwa Uislamu haukuwepo kabla ya Mtume (s.a.w.w.) mbona hiyo Al-Kaaba ilikuwepo miaka yote na watu wakifika hapo kumwabudu Mwenyezi Mungu? Isitoshe mara nyingi tunawaeleza Wakristo kuwa Manabii wote walileta Uislamu kabla ya Mtume wetu.

41


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 42

katika Uislamu

Hatukatai kwamba upotofu ulijipenyeza mpaka Waarabu wakaanza kuweka masanamu kwenye Al-Kaaba na kuyaabudu, huo ni upotofu ambao hata leo hii tunao miongoni mwetu kwani kuna baadhi ya matendo tunayotenda ambayo ni ya kikafiri ingawa Uislamu tunao siku nyingi. Tunachosisitiza ni kwamba kizazi kinachohusiana na Mtume (s.a.w.w.) kiliepushwa na ukafiri. Zaidi ya hayo ni aibu kwa Mtume (s.a.w.w.) Siku ya Kiyama iwapo wazazi wake watatupwa motoni kwa imani zao potofu za kikafiri. Ni jambo ambalo haliwezekani! Tumeona Bwana Abdul-Muttalib alivyomwomba Allah kulinda Al-Kaaba na kweli ikalindwa. Pia tumeona anaoteshwa siri ya chemchem ya Zamzam kuonyesha alivyo na uhusiano na Nabii Ismail kiroho. Zaidi ya hayo Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) alikaririwa akisema kuwa: “Nuru yangu ilikuwa inahamishwa toka uzao huu kwenda uzao mwingine, wote watu wasafi.” Nimeeleza wazi ibada zilizofanywa wakati wa vizazi mbali mbali vya Quraish na kisha zikaendelea kuwa sehemu ya Uislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) kupokea Utume. Itakuwaje Mwenyezi Mungu aunganishe ibada za kikafiri na Uislamu, au vipi makafiri wafanye ibada nyeti kama hizo? Huo utakuwa ukafiri gani? Vile Vile tumeona kuwa utukufu wa Quraish siyo kabila lote bali ni ule ukoo maalumu wa Mtume (s.a.w.w.) yaani Bani Hashim. Umuhimu wake tutauona baadaye katika maelezo ya mbele. Ndiyo maana hadi kuzaliwa Mtume (s.a.w.w.), wapo Quraish waliokuwa tayari wanaabudu sanamu. Imam Ali Ibn Abi Talib hakuwahi kusujudia sanamu kwa sababu anatoka katika ukoo wa Mtume (s.a.w.w.) wa Bani Hashim. Ukweli huu hauwekwi wazi kwa sababu kama tutakavyoona mbele, Bani Hashim walipigwa vita vikubwa na Bani Umayyah na Bani Abbas baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya maadui hao walidiriki kukufuru na kudai kuwa ‘Haukuwepo utume wowote ila ni ujanja wa Bani Hashim kutawala Waarabu wote milele’. Kauli kama hizi zilichochewa na tamaa ya Bani Umayyah na Bani Abbas kutaka kutawala dola kubwa ya Waislamu, ya wakati huo, na kujinufaisha kwa mali nyingi za Baitul-Maal zilizotokana na makusanyo ya Zaka.

42


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 43

katika Uislamu

Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) kuhusu uongozi nyuma yake: Baada ya maelezo hayo muhimu, sasa turejee nyuma kabisa tulikoishia kuhusu hoja zetu Shia Ithna’asheri kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia kuhusu uongozi wa Waislamu nyuma yake. Suala hili kimsingi halistahili kuwa na maelezo marefu iwapo Waislamu tungekuwa waaminifu. Nina maana kwamba katika vitabu vya kutegemewa nilivyovitaja nyuma kuna Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ambazo ni ‘mutawatir’ zinazoeleza suala hili. Kwa kawaida Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) zimegawanywa katika mafungu mbali mbali kuhusu kama ni za kutegemewa au zinafaa au zisizoaminika au zisizo na ubishi au zisizofaa kabisa. Huu ni utaratibu uliokubalika na wanavyuoni wote wa Shia Ithna’asheri na Sunni (Ahlul Sunna wal-Jamaa). Kwa hiyo iwapo Hadithi ni Mutawatir (isiyo na ubishani) maana yake ni kwamba itekelezwe kama ilivyo bila kusita. Hata hivyo ili kufupisha ubishi, naweza nikatoa Hadithi moja tu ‘Mutawatir’ kwa ushahidi. Lakini uzoefu unaonyesha kuwa binadamu tuna tabia ya kukwepa ukweli kama isemavyo (Qur’ani 75:31-32). Kutokana na ukweli huo nitalazimika kutoa karibu Hadithi zote muhimu pamoja na kwamba hata moja ingetosha! Tungekuwa waaminifu tungepokea maneno ya Mtume (s.a.w.w.) na kuyatekeleza japo iwe Hadithi moja tu mradi ni ya kweli. Je, angekuwa hai tungeacha kumtii? Mtiririko wa historia fupi ya utukufu wa Bani Hashim utaishia kwanza pale ambapo Mtume (s.a.w.w.) alipozaliwa mwaka 570 A.D. Nisingependa kuelezea kipindi kabla Mtume (s.a.w.w) hajaruhusiwa kutangaza Utume wake, kwa sababu kipindi hicho si muhimu sana kuhusiana na somo letu juu ya utukufu wa Bani Hashim.

Hadithi ya Kwanza: Mtume (s.a.w.w.) alipopata umri wa miaka 40 yaani mwaka 610 A.D. alik43


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 44

katika Uislamu

abidhiwa kazi ya kutangaza utume wake. Wafuasi wake waliongezeka kadri muda ulivyopita. Miaka mitatu baada ya kupokea Utume, ilishuka amri ya Mwenyezi Mungu ikimwamuru awakaribishe jamaa zake katika Uislamu: “Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.” (Qur’ani 26:214-216). Kutokana na amri hiyo, Mtume (s.a.w.w.) alitayarisha karamu na kuwakaribisha jamaa zake takriban 40. Kabla Mtume (s.a.w.w.) hajawaeleza ujumbe aliowaitia, kulitokea ami yake aliyeitwa Abu-Lahab alileta fujo na akamwonya Mtume (s.a.w.w.) aache kueneza dini yake mpya. Hali hiyo ilimfanya Mtume (s.a.w.w.) kuahirisha ujumbe huo na ikawa wageni wanaharakisha kuondoka. Baada ya siku kadhaa kupita, Mtume (s.a.w.w.) aliwakaribisha tena kwa karamu nyingine na waliporidhika aliwahutubia kuwa: “Enyi watoto wa Abdul-Muttalib, Mwenyezi Mungu amenituma kama mjumbe Wake kwa watu wote na hasa kwenu. Ameniamuru: ‘Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe’. Nawakaribisheni kupokea sentensi mbili fupi. Ni rahisi kuzitamka lakini kwa kipimo cha matendo ni nzito na ngumu sana. Kutokana na sentensi hizo, ninyi mtakuwa mabwana wa Waarabu na wasio Waarabu. Mataifa yatanyenyekea kwenu. Mtaingia Peponi na kuepushwa na Jahanam. Nazo ni ushuhuda kwamba: Hapana Mola ila Allah na kwamba mimi ni Mjumbe wa Allah. Atakayenijibu na kunisaidia katika jambo hili kulitekeleza atakuwa ndugu yangu, wasii na khalifa wangu.’” Wito huu ulirudiwa mara mbili na Mtume (s.a.w.w.) pasipo kujitokeza mtu yeyote zaidi ya Imam Ali Ibn Abi Talib. Katika mara zote mbili, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimwambia Imam Ali Ibn Abi Talib akae chini. Mara ya tatu ikawa pia amesimama Imam Ali akiwa tayari kuwa msaidizi wa Mtume (s.a.w.w.). Ndipo Mtume (s.a.w.w.) alipoweka mikono yake mabegani mwa Imam Ali Ibn Abi Talib na kusema: “Hakika huyu ni Ndugu yangu, Waziri wangu na Khalifa wangu kwenu, msikilizeni na mumtii.” 44


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 45

katika Uislamu

Katika tukio hilo, bwana Abu Talib alimwunga mkono Mtume (s.a.w.w.) kwa kumwambia: “Endeleza jukumu hilo ulilopewa. Kwa jina la Allah nitakulinda na kuzuia wanaotaka kukudhuru.” Wakati huo huo bwana Abu Lahab, kwa mara nyingine alimkemea na kumwonya Mtume (s.a.w.w.) asiendeleze kazi hiyo. Kutokana na imani ndogo waliyokuwa nayo kwa Mtume (s.a.w.w.), hao waalikwa waliobaki, walipokuwa wakinyanyuka kuondoka, walimdhihaki bwana Abu Talib wakisema: “Leo uwe na furaha kuingia dini ya mtoto wa kaka yako ambaye amemfanya mwanao (Ali Ibn Abi Talib) kuwa kiongozi wako!” Hadithi hii inajulikana kama: Hadith da’awat dhil a’shirah na inapatikana katika : Tarikh Abil-Fida, Jz. 1, Uk. 116 Katika kitabu cha Tarikh at-Tabari, toleo la ‘Leiden’ la mwaka 1879 A.D, tafsiri ya kiingereza, ukurasa 1173, yamenakiliwa maneno ya Mtume kuwa: ‘Ali ni Wasii na Khalifa Wangu.’ Lakini katika kitabu hicho hicho toleo la mwaka 1963 A.D, toleo la Cairo, maneno hayo muhimu yamefutwa na badala yake yakawekwa maneno ya: kadha wa kadha ili kuficha ukweli huu! Lakini ukweli haupotei kabisa na ndiyo maana tunakuta Uislamu katika vitabu vya dini nyingine. Kwa hiyo tumeona kuwa suala hili la uongozi wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) lilishawekwa wazi tangu mwanzo wa Uislamu. Busara ya Mwenyezi Mungu kufanya uchaguzi huo mapema, ni kwamba hata hapa duniani kila kiongozi mkuu huwa ana naibu wake. Iwapo huyo kiongozi wa nchi yoyote ile atafariki, mara moja anakuwepo mwingine. Au kama kiongozi mkuu hajiwezi kiafya atamwachia madaraka naibu wake. Itakuwa ajabu dini ya Mwenyezi Mungu iwe haina utaratibu mzuri wa uongozi lakini mambo yetu sisi viumbe wake yawe ndiyo yenye mipango mizuri!

45


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 46

katika Uislamu

Hadithi ya Pili: Hadithi hii tunaipata kwa mke wake Mtume (s.a.w.w.) aliyeitwa Ummu Salama. Mama huyu ni miogoni mwa Waislamu wa mwanzoni kabisa. Alikuwa mwenye hekima, na Mtume (s.a.w.w.) alimheshimu sana kutokana na sifa zake za uaminifu, uadilifu na uvumilivu wa mateso waliyopata Waislamu wa kwanza. Alikuwa mchamungu sana. Siku moja Mtume (s.a.w.w) alimwambia mama huyu kwamba: “Ewe Ummu Salma, mwili wa Ali umetokana na mwili wangu, na damu ya Ali imetokana na damu yangu, nafasi yake kwangu ni sawa na nafasi ya Harun kwa Musa ila tu kwamba hakuna nabii baada yangu.� Katika Hadithi hii, maneno mazito ni uhusiano wa Harun na Musa. Hebu tuone ni uhusiano upi huo. Historia ya Nabii Musa (a.s.) inaonyesha kuwa baada ya kuwaokoa Bani Israil kutoka kwa Firauni, Nabii Musa (a.s.) aliwaaga watu wake kwamba anakwenda mlimani kwa siku chache, lakini huko nyuma watabakia na Harun kama naibu wake. Aliwaamrisha kumtii Harun kama wanavyomtii yeye. Baada ya hapo akaelekea Mlima Sinai. Huko nyuma watu wa Nabii Musa (a.s.) wakamuasi Harun na kuanza kuabudu sanamu la dhahabu. Maelezo haya yanaonyesha kuwa Nabii Musa (a.s.) alimchagua Harun kuwa naibu wake. Kwa hiyo katika Hadithi ya kwanza tumeona jinsi Ali Ibn Abi Talib alivyochaguliwa na Mtume (s.a.w.w.) kwa wadhifa sawa na huo wa Harun kwa Nabii Musa (a.s.). Na hiyo ndiyo maana yake. Zaidi ya hayo historia yaonyesha kuwa pale Mtume (s.a.w.w.) alipohamia Madina alimwacha Ali Ibn Abi Talib nyuma na kumwamuru alale kitandani kwake (s.a.w.w.) na kurejesha dhamana za watu. Waliotaka kumuua Mtume (s.a.w.w.) iwapo wasingechunguza nani kalala kitandani kwake, wangemuua Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.). Inashangaza kuona sifa za ushujaa katika tukio hilo anapewa Abu Bakr Sidiq peke yake! Kumbukumbu za Hadithi hii ya mfano wa Nabii Musa (a.s.) na Harun zinapatikana katika vitabu vifuatavyo: 46


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 47

katika Uislamu

(a) Kanzul-’Ummal-Jz 4 Uk. 154 (b) Tarikhut-Tabari-Jz.2 Uk. 319

Hadithi ya tatu: Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: “Umma wa kiislamu utaongozwa na viongozi 12 mmoja baada ya mwingine, na kwamba wote hao watatokana na kizazi chake Mtume (s.a.w.w.) yaani Ahlul-Bayt katika ukoo wa Bani Hashim kabila la Quraish.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo:Sunan Abi Daud Jz. 2, Uk. 207, toleo la Cairo, 1348 A.H. Musnad al-Imam Ahmad ibn Hambal - Jz. 5, Uk. 92 Sahih Muslim - Kitabul Imamah Jz. 2, Uk. 79 Musnad al-Imam Ahmad ibn Hambal, Jz. 1, Uk. 398 & 406 Kanzul-Ummal, Jz. 6, uk. 160 Durr al-Manthur fi Tafsir bil - Ma’thur Mustadrak al-Hakim Sahih Bukhari, Kitabul-Ahkam, Baabul Umaraa - Jz. 4, Uk. 144 & 153

Hadithi ya nne: Hadithi hii inahusiana na kushuka kwa Aya ya Qur’ani ifuatayo:

“Enyi mlioamini, mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka juu yenu (Ulul Amr) walio katika nyie (Waislamu wenzenu).” (Qur’ani 4:59). Baada ya kushuka Aya hii, bwana mmoja Jabir Ibn Abdullah al-Answari alimwuliza Mtume (s.a.w.w.) kwamba: ‘Tunamfahamu Allah na wewe Mtume Wake, je ni nani hao waliopewa madaraka juu yetu?’ Mtume (s.a.w.w.) alijibu kuwa: “Hao ni Maimamu wakianzia na Ali Ibn Abi Talib, Hasan Ibn Ali, Husein Ibn Ali, Ali Ibn 47


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 48

katika Uislamu

Husein, Muhammad Ibn Ali, Jafar Ibn Muhammad, Musa Ibn Jafar, Ali Ibn Musa, Muhammad Ibn Ali, Ali Ibn Muhammad, Hasan Ibn Ali na mwisho Muhammad Mahdi Ibn Hasan.” Katika Hadithi hii tunagundua kwamba sio tu Mtume (s.a.w.w.) alimtaja kiongozi atakayefuata baada yake, bali pia aliwataja viongozi wote watakaofuata hadi Kiyama! Viongozi waliotajwa hapa ni 12 na ndiyo sababu sisi Shia tunaitwa Shia Ithna’asheri kwa maana ya wafuasi wa viongozi 12 toka kizazi cha Mtume (s.a.w.w.). Kwa kuwataja viongozi hawa, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiongozwa na Mwenyezi Mungu. Pengine wasomaji watataka kujua ni nani kiongozi wa wakati huu, iwapo kweli uongozi huu ulikusudiwa kuongoza hadi Siku ya Kiyama? Maelezo kuhusu swali hili yatatolewa mbele pamoja na kwamba huko nyuma, tumeshaona utabiri wa Biblia kuonyesha jinsi ambavyo watoto wa Mtume (s.a.w.w.) wataongoza Umma wa kiislamu hadi Kiyama. Hadithi hiyo imeandikwa na mwandishi maarufu wa madhehebu ya Sunni aitwaye Jamalud-Diin katika kitabu chake maarufu kiitwacho Raudhatul Ahbab. Hadithi hii bila shaka inakubaliana na Hadithi iliyotangulia kuhusu viongozi 12.

Hadithi ya tano: Hadithi hii hujulikana kama Hadith Ghadir-Khum. Inahusiana na kuteremka Aya ya Qur’ani:

“Ewe Mtume, Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako; na kama hutafanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi wanaokufuru.” (Qur’ani 5:67). 48


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 49

katika Uislamu

Aya hii ilishuka mnamo mwezi 18 Dhul Hajj (Mfunguo tatu) mwaka wa 10 A.H. wakati Mtume (s.a.w.w.) akitokea Hijja yake ya mwisho, miezi mitatu tu kabla hajafariki. Mtume (s.a.w.w.) akiwa katika safari hiyo, alijiwa na Malaika Jibril mara kadha, kumletea amri ya Mwenyezi Mungu kwamba, afikishe ujumbe muhimu ambao umuhimu wake, iwapo hataufikisha kwa watu, itakuwa kama kazi nzima ya Utume hakuitekeleza. Ndugu Waislamu, huo ndio uzito wa tukio hilo ambalo wengi wetu hatulijui kabisa. Kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) alipofika mahali hapo paitwapo Ghadir Khum, Malaika Jibril akamjia tena na kumtaka asipite zaidi ya hapo bila kutoa ujumbe huo. Mahali hapo ni jangwani katikati ya Makka na Madina. Ilimbidi Mtume (s.a.w.w.) kusimamisha msafara wa watu wote alioandamana nao. Aliamuru waliotangulia warejeshwe, na walio nyuma wahimizwe kufika hapo. Mahali hapo palisafishwa miiba na ikatengenezwa mimbari kwa kukusanya na kurundika matandiko ya ngamia. Ndipo Mtume (s.a.w.w.) akapanda hapo katika jua kali na kutoa hotuba ifuatayo mbele ya masahaba wapatao 140,000. Hotuba hiyo nimeifupisha kwa sababu ni ndefu sana. Hapa tunaeleza maneno muhimu sana kufuatana na somo letu - Hotuba kamili itaelezwa katika Sura ya 3. “Enyi watu, fahamuni kuwa Malaika Jibril amenijia mara nyingi akiniletea amri toka kwa Mwenyezi Mungu, Mkarimu, kwamba nisimame hapa nakuwaeleza watu wote kwamba Ali, mtoto wa Abu Talib ni ndugu yangu na wasii wangu, khalifa na Imam baada yangu. Nafasi yake kwangu ni sawa na ile ya Harun kwa Nabii Musa isipokuwa kwamba hapana nabii mwingine baada yangu. “Enyi watu, hakika Mwenyezi Mungu amemchagua awe Imam wenu na mtawala. Kumtii kwenu ni wajibu, muwe Ansari au Muhajirina, watumwa au waungwana, Waarabu au wengineo, weusi au weupe, wazee au vijana. Amri yake lazima itekelezwe. Neno lake lisipuuzwe na amri yake ni wajibu kwenu Waumini wote. Amelaaniwa yule asiyemtii Ali na ame49


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 50

katika Uislamu

barikiwa anayemtii Ali. Na anayemfuata Ali na kumwamini ni muumini wa kweli kweli. “Enyi watu, hii ni mara ya mwisho nimesimama katika hadhara hii kwa hiyo sikilizeni na muwe watiifu na mjitoe mhanga kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Allah ni Bwana wenu na Mungu wenu; kisha baada yake, Mtume wake Muhammad anayewahutubia ni bwana wenu. Kisha baada yangu Ali ni bwana wenu na Imam wenu kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Na baada yake Ali uongozi (Uimam) utaendelea kupitia kwa kizazi changu kwa Ali mpaka siku mtakapokutana na Allah na Mtume Wake. “Enyi watu, someni na kutafakari Qur’ani na mwelewe Aya zake. Fikirini juu ya Aya zake zilizo wazi na msijitahidi kuzitafsiri Aya zisizo wazi kwa sababu kwa jina la Mwenyezi Mungu,hapana atakayewaelezea maana yake isipokuwa huyu hapa ambaye ninainua mkono wake mbele yangu. Na ninawaeleza wazi kuwa yeyoye ambaye mimi nina mamlaka juu yake, Ali pia ana mamlaka juu yake. Huyu ni Ali mtoto wa Abu Talib. Ni ndugu yangu na Wasii wangu, na kumtii na kumpenda kumewajibishwa kwenu na Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu Aliyetukuka. Ee Allah mpende ampendaye Ali na uwe adui kwa adui wa Ali. Msaidie anayemsaidia Ali na umtupe asiyemsaidia Ali.” Mara tu baada ya hotuba hiyo, ikateremka Aya ya Qur’ani: “Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu..... (Qur’ani 5:3). Aya hiyo ilishuka baada ya Mtume (s.a.w.w.) kumtangaza Imam Ali (a.s.) kuwa kiongozi baada yake. Rejea: Tafsir Safi - Uk.128. Katika uwanja huo wa Ghadiir, tayari lilishajengwa hema ambapo Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) aliwekwa na Mtume (s.a.w.w.) ili watu waje kumpongeza na kutoa mkono wa Bay’ah (kiapo cha utii). Umar Ibn alKhattab alimpongeza Imam Ali (a.s.) kwa kusema: “Hongera kwako ewe 50


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 51

katika Uislamu

mwana wa Abu Talib kwani umekuwa bwana wangu na bwana wa kila muumini mwanamume na muumini mwanamke.” Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kureje Madina baada ya kumtangaza Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) kuwa mrithi wake, bwana mmoja Harith Ibn Nu’man alibishana na Mtume (s.a.w.w.) kuhusu uchaguzi huo na akajigamba kuwa kama kweli uchaguzi huo ni wa Mwenyezi Mungu, balaa limshukie (yeye Harith) kutoka mbinguni. Pale pale lilishuka jiwe kutoka juu likampiga kichwani kwake na kumuua mara moja! Rejea: Tafsir Thalaby, Jz. 12, maelezo ya Sura ya 70:1. Nimetangulia kueleza kuwa tukio hili lilitokea miezi mitatu kabla ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. Kilichotokea mara tu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki kabla hata hajazikwa, ni masikitiko makubwa kuona Waislamu wanautupilia mbali wasia huo wenye maagizo yote muhimu sana kwa Waislamu. Hayo tutayaona mbele. Hadithi hii ni katika zile Hadithi zinazoitwa Mutawatir kutokana na kusimuliwa kwake kwa wingi na masahaba waliokuwepo katika tukio hilo. Isitoshe kabla Mtume (s.a.w.w.) hajaenda kuhiji hiyo hija yake ya mwisho, watu wote walitangaziwa ili wanaotaka waongozane naye na kufanya naye ibada hiyo tukufu ya mwisho kwa Mtume (s.a.w.w.). Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo: Ghayatul-Maraam, uk. 336 ambapo Hadithi 6 za Sunni, na Hadithi 15 za Shia Ithna’asheri zinaelezea maana na lengo la tukio hili muhimu. Al-Bidayah wan-Nihayah, Jz. 5, uk. 208 na Jz. 7, uk. 346. Dhakhairul-Uqba, uk. 67 Al-Fusulul-Muhimmah, Jz. 2, uk. 23 Khasais, uk. 31 Katika vitabu vyote hivi kuna jumla ya Hadithi katika nyororo (asnad) 89 za madhehebu ya Sunni, na nyororo 43 za madhehebu ya Shia Ithna’asheri kuhusu tukio hili. Katika misingi ya uaminifu, yeyote atakayesoma Hadithi hii hana haja ya kwenda kwa Sheikh au kuuliza kitu kwa mtu yeyote yule 51


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 52

katika Uislamu

kwa sababu maneno yake yako wazi. Kinachotakiwa ni kuyatekeleza kwa sababu ni amri ya Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu. (Qur’ani 2:13). Aya hiyo inaonyesha jinsi watu walivyo tayari kukwepa ukweli kwa madai kwamba ni uongo! Kwa kifupi twaweza kusema kuwa mwongozo wote wa Uislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.) upo wazi katika hotuba hiyo, lakini hatuko tayari kupokea ukweli! Hata hivyo kutokana na umuhimu mkubwa wa wasia huo, Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru wote waliokuwepo hapo kwamba kila aliyesikia hotuba hiyo ni wajibu kwake kumweleza asiyewahi kuisikia mpaka Siku ya Kiyama. Sababu kubwa ni kwamba kama tulivyoona (Qur’ani 5:3) mapema, tangazo hilo ndilo lililokamilisha Uislamu kwa sababu ukifikiria utaona kuwa, dini iliyokusudiwa kuongoza binadamu hadi Siku ya Kiyama, haiwezi kuachwa wazi kwa kila mtu kuwa kiongozi bila uongozi maalumu wenye sifa tofauti na uongozi wa mambo ya kidunia. Nina maana kwamba uongozi wa Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa hauna kasoro kwa sababu anaongozwa na Mwenyezi Mungu. Lakini alipofariki iwapo Uislamu ungeachwa mikononi mwa watawala wa kawaida, bila shaka watawala hao wangelinda maslahi yao tu bila kujali sheria za Mwenyezi Mungu. Na huo ndio Uislamu tulio nao wakati huu; kwa sababu viongozi aliowachagua Mwenyezi Mungu walisukumwa pembeni kama tutakavyoona katika maelezo ya mbele. Mfumo huo wa mtu yeyote kuchukua ukhalifa, uliwawezesha madhalimu wakubwa kunyakua uongozi huo na kuipotosha dini ili kufanikisha malengo yao ya kidunia.

Je, hao Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ni nani? Tumeona utabiri wa Biblia kwamba Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ataongoza, akifuatiwa na kizazi chake hadi Siku ya Kiyama. Katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) tumeona kuwa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ndio watarithi uongozi huo. Sasa tupate ushahidi wa kutuweka sawa kuhusu ni nani hao watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.)? 52


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 53

katika Uislamu

Ushahidi wa kwanza ni Qur’ani:

“Hakika Allah anataka kukuondoleeni (kila aina ya) uchafu enyi Ahlal-Bayt (wa Mtume) na kukutoharisheni (kwa) tohara kamili.” (Qur’ani 33:33). Aya hii ilishuka wakati Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwa mke wake mchamungu sana mama Salama. Mara baada ya kushuka Aya hii, Mtume (s.a.w.w.) alimchukua binamu yake ambaye pia ni mkwe wake, Ali Ibn Abi Talib (a.s.), akamchukua binti yake, Bibi Fatima (a.s.), akawachukua wajukuu zake wawili, Imam Hasan (a.s.) na Imam Husein (a.s.). Wote hawa na yeye mwenyewe akawafunika shuka nyeusi na kusema: “Ee Allah, hawa ndio Ahlul-Bayt wangu, basi watoharishe na kila aina ya uchafu.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo: Jam’a Tirmidh Al-Isti’ab cha Abdul Barr Mustadrak al-Hakim, n.k. Hapa tunaona kwamba viongozi hawa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu aliwatoharisha na kasoro zote za kibinadamu. Maana yake ni kwamba wao wamelindwa na dhambi yaani ni ‘Maasum’ kama Mtume (s.a.w.w.). Tutapata maelezo zaidi katika Sura ya 17 kwa nini viongozi hao wawe na sifa ya kulindwa na dhambi yaani wawe tofauti na sisi binadamu wa kawaida.

Maneno ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Ahlul-Bayt wake: Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: “Mimi nimeitwa na Mwenyezi Mungu na nimeitikia mwito huo. Lakini nawaachia vitu viwili 53


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 54

katika Uislamu

vya thamani kubwa, navyo ni Qur’ani na kizazi changu (Ahlul-Bayt). Kwa kadri mtakavyovishikilia vitu viwili hivi hamtapotea kamwe..... Jihadharini na jinsi mtakavyojihusisha navyo.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo:Sahih Muslim (Kifungu cha Matendo mema ya Ali Ibn Abu Talib) Jz. 5, Uk. 122. Sahih Al-Tirmidhi, Jz. 5, Uk. 328 Mustadrak al-Hakim, Jz. 3, Uk. 148 Musnad Imam Ahmad ibn Hambal, Jz. 3, Uk. 17. “Mfano wa Ahlul-Bayt wangu ni sawa na Safina ya Nabii Nuh. Yeyote yule aingiaye humo, huokoka, na yeyote yule aiepukaye hupotea (hufa maji).” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo: (a) Al-Mustadrak al-Hakim, Jz. 3, Uk.151 (b) Yanabiul-Mawaddah, Uk. 30 & 370 (c) As-Sawaiqul-Muhriqah, cha Ibn Hajar Uk.184 & 234 (d) Musnad -Imam Ahmad ibn Hambal “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni Lango lake.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo: Mustadrak al-Hakim, Jz. 3, Uk. 127 Tarikh Ibn Kathir, Jz.7, Uk.358 “Ali anatokana na mimi. Na mimi ninatokana na Ali. Hakuna awezaye kufanya kazi yangu isipokuwa mimi au Ali.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo: Sunan Ibn Majah , Jz. 1, Uk. 44 Khasais al-Nisa’i, Uk. 20 Sahihl-Tirmidhi, Jz. 5, Uk. 300 Jami ‘ul-Usul, cha Ibn Kathir - Jz. 9, Uk. 471 54


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 55

katika Uislamu

Al-Jamius–Saghir, cha As-Suyuti Jz. 2, Uk. 56 Al-Riyadh al-Nadirah, Jz. 2, Uk. 229 “Huyu ni ndugu yangu Ali, wasii wangu na khalifa baada yangu. Kwa hiyo msikilizeni na muwe watiifu kwake.” Hadithi hii inapatikana katika vitabu vifuatavyo : (a) Tarikh-Tabari - Jz. 2, Uk. 319 (b) Tarikh Ibn al - Athir - Jz. 2, Uk. 62 (c) Al - Sirah al-Halabiyah - Jz. 1, Uk. 311 (d) Kanzul -Ummal - Jz. 15, Uk. 15 Kwa maelezo haya pamoja na ushahidi wake katika vitabu vya kutegemewa, vilivyoandikwa na Maulamaa, Wanahistoria na Wanahadithi wajuzi wa dini, sina shaka tunauona utukufu na nafasi ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya umma wa kiislamu. Sasa tujaribu kwa ufupi kuona sifa za Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.). Sifa ambazo zinawatofautisha na binadamu yeyote yule mbali na Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Sitataja sifa na miujiza ya kila mmoja katika wale viongozi (Makhalifa) 12 aliowataja, kwani hiyo ni historia ndefu ya miaka 244 yaani muda ambao waliishi; kabla ya kiongozi wa mwisho yaani wa 12 (a.s.) hajafichwa na Mwenyezi Mungu machoni pa watu, lakini yupo hai hapa duniani akisubiri kazi maalumu aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuifanya itakapowadia. Suala hili la kufichwa Imam wa 12 (a.s.) tusimwone ingawa yupo, linahitaji maelezo marefu, kitabu kizima cha peke yake, kwa ushahidi wa mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani. Lakini nitajitahidi kutoa maelezo muhimu ili kukamilisha picha ya wasia wa Mtume kwamba viongozi (Maimamu 12) aliowataja wataongoza umma wa kiislamu hadi Siku ya Kiyama. Tukumbuke kuwa hata kwenye Biblia utabiri wake ni huo huo yaani ni sawa na maneno ya Mtume (s.a.w.w.).

55


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 56

katika Uislamu

Sifa za Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.): Hapa nitaeleza kwa ufupi sana badhi ya mambo yaliyotokea katika maisha ya Ahlul-Bayt. Mambo hayo ni pamoja na miujiza mbalimbali inayodhihirisha kuwa wao hawakuwa binadamu wa kawaida kama sisi.

Imam Hasan na Imam Husein (a.s.): Kwa kadri ya Hadithi ya Mtume (s.a.w.w), Imam Hasan (a.s.) ni kiongozi wa pili, wakati ambapo Imam Husein (a.s.) ni kiongozi wa tatu katika mpangilio wa uhai wa hao viongozi 12 (a.s.). Siku moja katika uhai wao karibu na Sikukuu ya Idd, Hasan na Husein (a.s.) walimwendea mama yao, Bibi Fatima (a.s.) na kumwuliza: ‘Mpendwa mama, kesho ni Sikukuu, wapi nguo zetu mpya za Sikukuu?’ Mama yao alijua kuwa wakati huo hapakuwepo nguo wala uwezo wa kuzipata, kwani hata chakula kilikuwa cha taabu na nguo yake mwenyewe ilijaa viraka vya majani ya mtende. Zaidi ya hayo urithi wake alioachiwa na Mtume (s.a.w.w) yaani ‘Fadak’ ulikuwa umetaifishwa na watawala wa wakati huo (yaani khalifa Abubakr Sidiq). Kwa hiyo Bibi Fatima (a.s.) akawajibu wanawe kuwa wasubiri kesho yake fundi ushonaji atazileta nguo zao. Usiku huo walipokuwa wamelala watoto Hasan na Husein (a.s.), Bibi Fatima aliamka na kukaa kwenye mswala akaswali na kuomba: “Ee Allah, Fatima mtumishi wako anayetegemea neema zako ameahidi nguo mpya kwa watoto wake Hasan na Husein (a.s.). Bwana wangu, wakipata nguo hizo watafurahi na wewe utaridhika na kufurahi kwao. Ee Allah usiache ahadi ya Fatima iache kutimia na usiache watoto hawa wasikitike.” Mapema kesho yake asubuhi Siku ya Idd, watoto hao wakaamka na kitu cha kwanza wakauliza nguo mpya. Pale pale ikasikika sauti mlangoni mtu akitoa salamu na kusema, ‘Enyi Ahlul-Bayt wa Mtume, chukueni nguo hizo za Hasan na Husein.’ Nguo hizo zililetwa na Malaika toka Peponi. Walipovaa nguo hizo na kutoka mitaani. Watu walishangaa kuona mavazi hayo ya ajabu yasiyopatikana popote wakati huo! Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa: “Hasan na Husein (a.s.) ni viongozi 56


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 57

katika Uislamu

wa vijana wa Peponi.”

Bibi Fatima (a.s.): Mama yake Bibi Fatima (a.s.) yaani Bibi Khadija anaelezea kisa hiki kuhusu wakati wa kujifungua mimba ya mwanawe Fatima (a.s.): “Wakati wa kumzaa Fatima nilituma watu wakaniitie majirani zangu mabibi wa Kikuraishi ili wanipatie huduma za ukunga. Mabibi hao walikataa katakata wakidai kwamba nimewasaliti kwa kumuunga mkono Muhammad katika dai lake la utume. Kwa kitambo fulani nilipatwa na wasiwasi lakini mara nikapatwa na mshangao mkubwa kuwaona wanawake wanne nisiowafahamu, warefu na wenye duara za mwanga nyusoni mwao wakinitokea. Waliponikuta kwenye hali ya kukata tamaa, mmoja wao aliniambia: ‘Ewe Khadija, Mimi ni Sara mama yake Isihaka, na hawa mabibi watatu wengine ni Mariam mama yake Isa, Asia binti Muzahim (bibi huyu alikuwa muumini na mchamungu sana aliyekuwa mkewe kafiri mkuu Firauni enzi za Nabii Musa (a.s.)), na Ummu Kulthum, dada yake Nabii Musa. Tumeamrishwa na Allah tukupatie huduma kutokana na utaalamu wetu wa ukunga.’ Baada ya kusema hivyo, wote wanne walinizunguka wakanihudumia hadi nilipomzaa Fatima.”

Msaada wa Allah kwa Bibi Fatima (a.s.) katika shida: Hapo Madina waliishi Wayahudi matajiri sana. Binti mmoja toka katika hao Wayahudi alikuwa anatayarishwa kuolewa. Wayahudi hawa walisikia habari za ufukara wa Bibi Fatima (a.s.) na habari za mavazi yake makuukuu yasiyo na thamani aliyokuwa akiyavaa daima. Wayahudi hao waliona kuwa huo ndio wakati wa nafasi nzuri ya kumdhalilisha na kumfanya kichekesho Bibi Fatima (a.s.). Muda ulipowadia, walimtuma mjumbe kwa Mtume (s.a.w.w.) kumwomba amruhusu Bibi Fatima (a.s.) ahudhurie harusi hiyo.

57


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 58

katika Uislamu

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimshauri mjumbe huyo amwendee mume wake Bibi Fatima (a.s.) yaani Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.). Imam Ali (a.s.) alishangazwa na ombi hilo toka kwa watu kama hao! Hata hivyo alimwambia mjumbe huyo kuwa jibu litatoka baadaye kidogo. Imam Ali (a.s.) akaelekea kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa majadiliano kuhusu suala hilo na mwisho wakaafiki mwaliko huo. Bibi Fatima (a.s.) akajitayarisha kwenda harusini bila kujali mavazi yake yaliyochakaa. Lakini Mwenyezi Mungu akazifahamu njama za hao Wayahudi, na hakupenda kumwona Bibi Fatima (a.s.) akivunjiwa heshima na matajiri hao. Kwa hiyo Allah akamtuma Malaika Jibril kwenda kwa Bibi Fatima (a.s.) na sinia lenye nguo za kupendeza mno. Bibi Fatima (a.s.) akashangazwa sana na mavazi hayo ya kuvutia mno. Malaika Jibril akamwambia kuwa hayo ni mapenzi ya Allah kuwa ayavae mavazi hayo kisha ahudhurie harusi hiyo. Bibi Fatima (a.s.) akavaa nguo hizo zenye mapambo ya kumeremeta. Wayahudi walipomwona walipigwa na mshangao wakakosa la kufanya ila kumkodolea macho tu. Nguo hizo zilionekana ni muujiza kwa sababu zisingepatikana popote pale duniani. Na huo ukawa mwisho wa Wayahudi hao kuwakejeli wale wasiokuwa sawa nao kimaisha.

Ahlul-Bayt waletewa chakula toka Peponi: Siku moja ilitokea kwamba nyumbani mwa Bibi Fatima (a.s.) hamkuwa na chakula chochote. Bibi Fatima (a.s.) na familia yake hawakuwa na chochote cha kula kwa muda wa siku mbili na hazikuwepo pesa za kununulia chakula. Siku ya tatu Imam Ali alikopa sarafu ya fedha na akaenda haraka sokoni kununua chakula. Akiwa njiani alikutana na mmoja wa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akihangaika. Imam Ali (a.s.) akamwuliza sahaba huyo sababu iliyomfanya atoke nyumbani mwake wakati ule wa mchana. Kwanza yule sahaba alijaribu kukwepa swali la Imam Ali (a.s.), lakini Imam Ali (a.s.) aliposhikilia, yule sahaba akasema kuwa alitoka ili kutafuta njia ya kujipatia chochote kitakachoweza kuzima njaa ya watu wa familia yake. 58


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 59

katika Uislamu

Sahaba huyo alimweleza Imam Ali kisa kizima na alipomaliza kueleza, Imam Ali (a.s.) aliamua kuwa shida ya huyo sahaba ni kubwa kuliko ile yake. Hapo Imam Ali (a.s.) akamwambia kuwa ndiyo mara tu alitoka kukopa sarafu ya fedha na alikuwa akienda sokoni kununua chakula, lakini bora hiyo sarafu ampe yeye. Kwanza yule sahaba alikataa lakini mwisho akakubali. Baada ya hapo Imam Ali (a.s.) alikwenda msikitini na akabakia huko akiswali hadi kuchwa jua. Swala ya Isha ilipokwisha kuswaliwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda nyumbani kwa Imam Ali (a.s.) ambaye aliwaomba abakie hapo kwa chakula cha usiku; bila kujua ni vipi atamweleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa nyumbani hamna chakula. Wakati huo Bibi Fatima (a.s.) alikuwa akiswali pale nyumbani, lakini Imam Ali (a.s.) alishangaa kuona sinia pembeni lililojaa vyakula vitamu kwenye kitambaa cha chakula. Baada ya kuswali, Bibi Fatima (a.s.) aliandaa chakula hicho, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Imam Ali (a.s.) kuwa chakula hicho ni zawadi toka Peponi kutokana na Imam Ali (a.s.) kujinyima ile sarafu ya fedha na kumpa yule sahaba!

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akimheshimu sana Bibi Fatima (a.s.): Kila Bibi Fatima (a.s.) akimtembelea Mtume (s.a.w.w.), ilikuwa kawaida ya Mtume (s.a.w.w.) kusimama kwa heshima yake; na alikaa baada ya Bibi Fatima (a.s.) kukaa. Kwa kawaida mtu mzima hafanyi hivyo kwa kijana seuze mtu na binti yake! Kwa kuwa Mtume huongozwa na Mwenyezi Mungu wakati wote, bila shaka huu ni ushahidi kuwa alifanya hivyo japo ni kinyume na desturi za kawaida, kwa nia ya kuonyesha cheo cha mama huyo mbele ya Mwenyezi Mungu. Imepokelewa Hadithi kuwa bibi huyu kupewa jina la Fatima ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu, na kwamba jina hilo maana yake ni yule aliyeokolewa pamoja na wafuasi wake kutokana na moto wa Jahanamu. 59


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 60

katika Uislamu

Hadithi nyingine inasema kuwa Fatima ni kiongozi wa akina mama wa Peponi.

Kwa nini aliitwa Fatima Zahra?: Katika majina yake mengi matukufu, alijulikana sana kwa jina la Zahra (Nuru). Sababu yake ni kwamba kila alipokuwa anasali hutokea nuru kali iliyochomoza toka mbinguni hadi hapo nyumbani kwake anaposalia. Na hapo wakazi wa Madina hujua kuwa Bibi Fatima Zahra (a.s.) yumo katika Swala! Wakati wa Swala yake, shughuli zake za nyumbani hufanywa na Malaika kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Heshima yote hii kwake bila shaka ni pamoja na kwamba ndiye mama wa kizazi kitukufu cha viongozi (Maimamu) 11 (a.s.) aliowataja Mtume (s.a.w.w.) kuongoza Waislamu baada yake na baada ya Imam Ali Ibn Abi Talib (as) kufariki.

Ahlul-Bayt (a.s.) katika tukio la Mubahilah: Mnamo mwaka wa 9 A.H. makabila mbali mbali yalimjia Mtume (s.a.w.w.) na kusilimu baada ya habari kuenea kuwa ni Mtume wa kweli. Mtume (s.a.w.w.) aliwatuma wahubiri mbali mbali kuhubiri dini ya kiislamu na aliwaagiza wawe wapole, watumie hekima na wasiwakashifu watu. Ikawa Mtume (s.a.w.w.) amemtuma mjumbe kwenda huko Najran-Yemen kuwakaribisha kabila moja la Wakristo katika Uislamu. Watu hao walishauriana na wakachagua kamati ya watu 14 miongoni mwa kundi la watu 60. Kamati hiyo ilitumwa kuchunguza tabia na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w.) na walete taarifa. Katika kamati hiyo walikuwemo watu maarufu nao ni Abdul Masih kiongozi wa kisiasa, Al-Ayham mwangalizi wa masuala ya Makasisi, na Abu Hatam Ibn Alqama ambaye alikuwa kasisi (Bishop). Walipofika Madina walimfuata Mtume (s.a.w.w.) lakini Mtume aliwashauri wapumzike hadi kesho yake. Bila shaka Mtume (s.a.w.w.) alisubiri ‘wahyi’ juu ya suala hili kwani kesho yake iliteremka Aya ya Qur’ani:

60


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 61

katika Uislamu

“Bila shaka hali ya Isa kwa Mwenyezi Mungu ni kama hali ya Adam, alimuumba kwa udongo kisha akamwambia: ‘Kuwa’ basi akawa.” (Qur’ani 3:59).

“Watakaokuhoji (sasa) katika haya baada ya kukufikilia ilimu hii na kuwafikilia wao, waambie, ‘Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wa kwetu na wanawake wa kwenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Qur’ani 3:61). Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza ujumbe huu wa Qur’ani lakini hawakuridhika bali walisisitiza na kushikilia imani yao. Kwa hiyo waliomba muda wa siku moja ili wajishauri kama wakubaliane na mkutano wa kuomba laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo; au hapana. Kesho yake tarehe 24 Dhul-Hajj 9 A.H., mapema asubuhi walikubali mkutano huo na hivyo Mtume (s.a.w.w.) akawasili uwanjani hapo kwa maombi hayo, akiwa amembeba Husein mikononi, huku amemtanguliza Hasan kwa mkono, akifuatiwa nyuma na Bibi Fatima pamoja na Ali Ibn Abi Talib aliyebeba bendera ya Uislamu. Kabla sijaendelea, ningemwomba msomaji atambue kuwa kwa tafsiri ya (Qur’ani 3:61) iwapo mtu ataifasiri kwa misingi ya lugha tu, tutaona kuwa ingebidi Waislamu wote wake kwa waume na watoto wao, waje hapa 61


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 62

katika Uislamu

uwanjani kushiriki maombi hayo! Lakini tafsiri sahihi ni kwamba tunamwona Mtume (s.a.w.w.) anawaleta Ahlul-Bayt wake (Qur’ani 33:33) kwa maana kwamba ndio waliokusudiwa na Mwenyezi Mungu. Bila shaka kwa mara nyingine tunaona utukufu wao ulivyo mbele ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya masheke huitafsiri Aya hii kwa maana ya ‘kilugha’ bila kuzingatia historia ya tukio hilo, na bila kuzingatia Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) alipokaririwa akisema kuwa: “Qur’ani imeteremshwa ikiwa na maana ya wazi na maana iliyojificha na kwamba maana zote mbili anazijua Ali Ibn Abi Talib”. (Rejea Sahih Bukhari pamoja na Hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) pale Ghadir Khum niliyoieleza nyuma) Soma Sura ya 3. Nikirejea kwenye somo letu ni kwamba kiongozi wa Wakristo alipomwona Mtume (s.a.w.w.) kawaleta Ahlul-Bayt wake, alishtuka na kuwahutubia wenzake kuwa: ‘Msikubali maombi hayo ya kuapizana kwa sababu kwa utukufu wa hawa walio mbele yetu, hata wakiomba mlima usogee utasogea tu.’ Wakristo walikubali ushauri huo na wakaomba kwa Mtume (s.a.w.w.) waendelee na dini yao ya Ukristo, kwa mapendekezo kwamba wako tayari kuweka mkataba na Mtume (s.a.w.w.) ili Wakristo watoe kila mwaka mavazi elfu mbili kila moja thamani yake dirham 40, mikuki 40 pamoja na mavazi mengine 30 ya vita. Mkataba huo ulikuwa wa kawaida kwa wasio Waislamu iwapo wanataka ulinzi wa dola ya kiislamu kwa wao wenyewe na mali zao. Mtume (s.a.w.w.) alikubali maombi yao. Kwa mara nyingine tunaona mfano mzuri wa kufanya tabligh toka kwa Mtume (s.a.w.w.). Hakuna aliyekashifiwa au kulazimishwa kuwa Mwislamu. Tukio hili laonyesha jinsi ambavyo Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) ndio wawakilishi wa Waislamu, tukisherehesha Qur’ani 3:60-61: “Nafsi zetu na nafsi zenu” Mtume (s.a.w.w.) na Ali Ibn Abi Talib (a.s.)kama nafsi yake.

62


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 63

katika Uislamu

Wanawake zetu: Bibi Fatima (a.s.). Watoto wetu: Hasan (a.s.) na Husein (a.s.). Ni hao waliolindwa na dhambi ambao Mwenyezi Mungu alikuwa tayari kupokea maombi yao. Ndiyo maana Mtume (s.a.w.w) alitangulia kuwaeleza kuwa katika maombi hayo yeye ataomba na wao waitikie ‘Aamin.’ Sababu ya kushuka Aya (Qur’ani 3:58-61) ni kwa kuwakusudia AhlulBayt kama tunavyosoma katika vitabu vifuatavyo: Sahih Muslim, Juz. 1 Sahih Tirmidh Kama wangekusudiwa Waislamu wote, Mtume (s.a.w.w.) asingefanya kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu! Kwa upande mwingine tutaona kuwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) ni hao niliowataja na siyo wake zake Mtume (s.a.w.w.) kama wanavyodai baadhi ya mashekhe! Hata Ummu Salama ambaye alikuwa mchamungu sana siyo katika Ahlul-Bayt, kwa sababu iliposhuka Aya ya Ahlul-Bayt (Qur’ani 33:33) alikuwepo pale pale na alimwomba Mtume (s.a.w.w.) ili aingie katika lile shuka jeusi lakini Mtume (s.a.w.w.) alimjibu kuwa ‘Wewe ni mchamungu lakini kaa hapo ulipo.’

Kisa cha Imam Hasan Al-Askari - Imam wa 11 (a.s.): Imam Hasan Al-Askari (a.s.) aliishi kati ya mwaka 232 A.H. na 260 A.H. Wakati huo mtawala wa dola ya kiislamu alikuwa khalifa Al-Mu’tamad wa ukoo wa Bani Abbas. Mtawala huyo, kama waliomtangulia, alimweka kizuizini (gerezani) Imam Al-Askari (a.s.) kwa miaka mingi kutokana na chuki kubwa ya Bani Umayyah na Bani Abbbas dhidi ya Ahlul-Bayt (a.s.) kama tutakavyoona baadaye. Zaidi ya hayo, mtawala huyo alikuwa anafahamu sana Hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba Imam wa 11 ndiye atakayemzaa Imam wa mwisho yaani Imam Mahdi (a.s.); na kwamba Imam Mahdi ndiye 63


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 64

katika Uislamu

ataanzisha na kustawisha utawala wa dhuria ya Mtume (s.a.w.w.) ulimwenguni kote, na kuangamiza maadui wa Ahlul-Bayt (a.s.). Kwa hiyo khalifa Al-Mu’tamid aliona bora amfunge Imam Hasan Al-Askari (a.s.) ili Imam Mahdi (a.s.) asizaliwe! Hebu tuone Qur’ani inasemaje: Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani:

“Wao (maadui) wanapenda kuzima nuru yake (Mungu) kwa vinywa vyao, lakini Allah atakamilisha nuru yake, ijapokuwa wasioamini watakahirika.” (Qur’ani 9:32). Vile Vile katika Biblia tunaona kuwa Firauni alidai kuwa yeye ni Mungu. Wanajimu walimshauri kwamba kutokana na kizazi cha Bani Israil, atazaliwa mtoto atakayeangamiza ufalme wake kwa kumuua yeye Firauni na wafuasi wake. Kwa hiyo Firauni aliweka ulinzi mkali kwa wanawake wa Bani Israil na kumwua kila mtoto wa kiume anayezaliwa ili asizaliwe Nabii Musa (a.s.). Hata hivyo alivyotaka Mwenyezi Mungu ikatimia. Nabii Musa (a.s.) alizaliwa na kulelewa pale pale kwa Firauni, na yakatimia waliyotabiri wanajimu! Kwa hiyo tukirejea somo letu ni kwamba katika kipindi cha kufungwa gerezani Imam Hasan Al-Askari (a.s.) kulitokea ukame mkubwa hapso Samarra, Iraq. Kwa muda mrefu haikunyesha mvua. Waislamu waliswali Swala maalumu ya kuomba mvua inyeshe lakini bila mafanikio. Waislamu wote wakakusanyika nje ya Jiji la Samarra na ikawa Padri mmoja wa Kikristo akanyanyua mikono yake juu kuomba mvua kwa Mungu. Papo hapo mawingu yalikusanyika na mvua ikanyesha kidogo! Kuona hivyo Waislamu walibabaika. Wakaanza kupatwa na wasi wasi kwamba Uislamu umeshindwa! Khalifa Al-Mu’tamad akaitisha baraza lake na kupata ushauri wa viongozi wa Waislamu, mawaziri na maafisa 64


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 65

katika Uislamu

wake. Wote walipigwa na butwaa! Mmoja wa washauri wake akatoa wazo kuwa, yuko mwokozi mmoja tu ambaye anaweza kuwaokoa, naye ni Imam Hasan Al-Askari (a.s.) ambaye alifungwa gerezani. Khalifa alikuwa na hakika (yakini) juu ya elimu, ukweli, utukufu na uimamu wa Imam Hasan Al-Askari (a.s.); na haki yake Imam kuwa kiongozi (khalifa) wa dola ya kiislamu. Hivyo aliagiza aletwe hapo katika baraza la mfalme. Alipofika kwenye kasri (Ikulu) ya mfalme, ikawa khalifa amesimama kwa heshima zote akamkaribisha na kumkalisha karibu sana na kiti chake na kumweleza mambo yote. Imam alijibu kuwa asiwe na wasi wasi hilo ni jambo dogo: “Waamrishe Waislamu wote wakusanyike nje ya Jiji kesho ili waswali na kuomba mvua inyeshe. Na muda huo huo mwamuru huyo Padri wa kikristo afike.” Kesho yake Waislamu wote pamoja na yule Mkristo walikusanyika hapo. Imam akamwambia huyo Padri aombe mvua na papo hapo mawingu yakakusanyika. Imam akamwomba khalifa kumtuma mtu akalete kile kitu ambacho Padri huyo kakificha katikati ya vidole vyake! Khalifa aliamrisha afisa wake akamnyang’anye mfupa uliofichwa katikati ya vidole vya Padri, na akamkabidhi Imam Hasan Al-Askari (a.s.). Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akaufunika huo mfupa katika leso na kuiweka hiyo leso mfukoni mwake. Pale pale mawingu yaliyokusanyika yakatawanyika. Hapo Imam akamwambia huyo Padri amwombe Mungu tena ili inyeshe mvua. Padri huyo alijitahidi sana bila mafanikio. Hapo Imam akamjulisha khalifa kuwa ule mfupa ulikuwa wa Nabii mmojawapo wa zamani na wakati wowote mfupa huo unapowekwa chini ya mbingu, basi mawingu hukusanyika. Imam akiwaongoza Waislamu katika Swala, alinyanyua mikono yake mitakatifu. Papo hapo mawingu yalikusanyika pande zote. Imam aliwaamuru watu waende makwao na baadaye mvua kubwa ikanyesha. Imam na khalifa walirudi makazi ya mfalme na hilo lilikuwa jambo pekee lililokuwa likizungumzwa na kila mtu mjini hapo. 65


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 66

katika Uislamu

Khalifa alifurahi sana kwa kuunusuru Uislamu. Khalifa na watu wote waliamini manufaa ya Swala na ukweli wa utawala wa Imam. Baada ya muda Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akondoka hapo kwa mfalme, khalifa akamwuliza wapi anakoelekea? Imam akajibu: “Gerezani.” Kusikia hayo, khalifa akaona haya na akasema: “Ewe mjukuu wa Mtume, tafadhali rudi nyumbani kwako.” Na hapo ndipo Imam akarejea nyumbani kwake na kupokelewa na mke wake aliyeitwa Narjiskhatun kwa furaha. Maneno ya Mwenyezi Mungu: Mwenyezi Mungu hukamilisha nuru yake ijapokuwa makafiri wanakihirika. (Qur’ani 61:8) yakatimia. Ni katika wakati huo ndipo ilipotunga mimba ya Imam wa 12 (a.s.) yaani Imam Muhammad Mahdi (a.s.).

Kisa cha Imam Muhammad Mahdi (a.s.), Imam wa 12: Anakaririwa bwana Bashir bin Suleiman aliyekuwa sahaba wa Imam wa 10 (a.s.). Imam wa kumi ndiye baba yake Imam Hasan Al-Askari (a.s.) kwamba: “Niliitwa na Imam wa kumi (Imam Ali Naqi a.s.) ambaye alinieleza kwamba, ‘Wewe ni katika kizazi cha wasaidizi wetu na marafiki zetu. Nitakupa kazi muhimu kwa sababu mimi nina imani na wewe. Nenda Baghdad ufike kwenye ukingo wa mto utaona majahazi mengi na mateka wa kike wanauzwa. Nenda kwa mtu mmoja aitwaye Umar bin Yazid ambaye atakuwa na mateka mmoja wa kike aliyevaa nguo mbili za hariri. Yeye (huyo mateka wa kike) atakataa kuuzwa kwa yeyote na atakuwa anazungumza lugha ya kituruki. Mwuzaji atakubali kumuuza mateka huyo kwa bei ya Dinar 120 hivyo chukua pesa hizo na barua hii ukampe huyo mateka wa kike.’ “Nilikwenda Baghdad kama nilivyoagizwa na kwa alama nilizoelezwa na Imam Ali Naqi (a.s.) niliweza kumtambua huyo mateka na nikampa barua. Mara aliposoma barua hiyo, huyo bibi machozi yalimjaa machoni mwake na akamwambia mmiliki wake kuwa hatakubali kununuliwa na mtu yeyote ila mimi tu (Bashir Bin Suleiman). 66


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:19 PM

Page 67

katika Uislamu

“Nilirudi Baghdad na mateka huyo ambaye aliweka barua hiyo usoni na kulia sana. Nilimuuliza kwa nini anabusu hiyo barua na kulia wakati yeye ni mgeni kutoka Uturuki na hamjui mwandishi wa barua hiyo? Naye akanijibu kuwa: ‘Sikiliza, mimi ni mjukuu wa Kaizari Mfalme wa Uturuki na jina langu ni Malika. Jina la baba ni Yashua na la mama ni Shamunusafaa. Baba yangu aliandaa mipango niolewe na mpwa wake. Siku moja aliwaita mapadri wote, mawaziri, viongozi na wafuasi wake. Alimkalisha mpwa wake juu ya kiti cha enzi ambacho kilipambwa na almasi na kumwomba Padri afunge ndoa yetu. Padri alipoanza kufungua kitabu, masanamu yaliyotundikwa ukutani yaliporomoka na mwana wa mfalme (mpwa wa babu yangu) akazirai na kuanguka na kiti cha enzi kilivunjika vipande vipande. Mapadri walitetemeka na kumwomba msamaha baba yangu mfalme, kwa sababu hakukutarajiwa balaa hilo. Mfalme alihuzunika sana akaona ndoa hiyo ilikuwa na nuksi na hivyo aliagiza kiti kingine cha enzi na kutundika masanamu tena ukutani na kurudia kama mwanzo kutaka kufunga ndoa upya, lakini matokeo yakawa yale yale! Walioalikwa wote walishtuka sana na kuondoka mara moja, ikawa baba yangu amefedheheka sana na kukaa ndani siku nyingi bila kutoka hadharani. “Usiku huo huo nilimwona Nabii Isa katika ndoto, akiwa na masahaba wake waliokuwa wamehudhuria sherehe ya ndoa yangu. Kiti kirefu cha enzi kiliwekwa pahali palipowekwa kiti cha mwana wa mfalme (aliyetaka kunioa) na kilikuwa kimekaliwa na mtu mwenye cheo na mwenye uso uliojaa nuru. Muda mfupi niliwaona watu wenye nyuso za nuru, na hapo Nabii Isa alisimama kuwakaribisha na kuwapa nafasi karibu yake. Nilimwuiliza mtu mmoja anijulishe hao waliokuja walikuwa ni nani? Nikaarifiwa kuwa hao ni Mtume wa Uislamu na Maimamu (warithi) wake 12 wanaotokana na dhuria yake. “Ndipo Mtume Mtukufu akamwomba Nabii Isa kumchumbia Malika binti Shamunusafa, kwa mjukuu wake Imam Hasan Al-Askari ambaye uso wake uling’aa kwa nuru. (Ombi hilo lilifanywa kwa nabii Isa kwa sababu Malika alitokana na kizazi cha Hadhrat Shamoon mrithi wa Nabii Isa.) Nabii Isa 67


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 68

katika Uislamu

akamwomba Hadhrat Shamoon atoe kibali chake, na papo hapo Hadhrat Shamoon akakubali kwa kuona hiyo ni heshima kuu. Kwa hiyo ndoa yangu na Imam Hasan Al-Askari ikafungwa. “Macho yangu yalifunguka ghafla na mimi nikajawa na furaha. Nilikumbuka ndoto hiyo lakini niliogopa sana sikumhadithia mtu yeyote. Hapo baadaye nikaanza kuwa mgonjwa na kumkumbuka Imam Hasan AlAskari na hali yangu nikaanza kudhoofu. Safari ya pili katika ndoto nilimwona binti wa Mtume (s.a.w.w.) Mwana Fatima (a.s.). Katika ndoto hiyo mimi nilisimama kwa taadhima na nikamweleza hali yangu na kutomwona Imam Hasan Al-Askari (a.s.). Bibi Fatima (a.s.) aliniamrisha nisome Shahada na nikawa Mwislamu na baadaye kila usiku nilimwona Imam Hasan Al-Askari katika ndoto akinituliza. Mara moja Imam Hasan AlAskari (a.s.) aliniambia kuwa babu yangu atatuma jeshi kuivamia nchi ya Waislamu na mimi nibadilishe mavazi yangu niungane na jeshi kama mtumishi mmojawapo. Waislamu watashinda vita hiyo na mimi nitatekwa na kwa hiyo niungane na mateka wengine mpaka Baghdad.” Mimi (Bashir Bin Suleiman) niliposikia maelezo hayo nilijawa na furaha na nilimleta Bibi Narjiskhatun hadi Samara kwa Imam Ali Naqi (a.s.). Imam Ali Naqi (a.s.) alimkaribisha na akamkabidhi kwa dada yake (Halima Khatun). Baadaye Imam Ali Naqi (a.s.) alimuoz a Bibi Narjiskhatun kwa mwanawe Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akawabashiria kwamba watampata mwana ambaye atakuwa Hujjat (dalili) duniani wa kuthibitisha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu, wakati dunia itakapokuwa imezama katika ukandamizaji uovu, na ulaghai. Yeye (Imam Mahdi) atadhihiri na kutawala na kuleta uadilifu na usawa.”

Kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.): Imam Muhammad Mahdi (a.s.) alizaliwa Samarra - Iraq alfajiri ya tarehe 15 Shaaban 255 A.H., siku ya Ijumaa, nyumbani kwa baba yake mtukufu. Alizaliwa akiwa tohara (ametahiriwa) na uso wake ulijaa nuru ambayo ilipenya paa na kuchomoza mbinguni. Alipozaliwa tu, kwanza alisujudu na 68


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 69

katika Uislamu

kunyosha kidole chake cha shahada kuelekea mbinguni na kuthibitisha Upweke wa Alllah (Tawhid) na Unabii wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Uimamu wa Ali Ibn Abi Talib (a.s.) pamoja na warithi wake kumi (mbali ya yeye na Imam Ali) kuwa ni Maimamu wa kweli. Kisha alimwomba Allah atimize ahadi yake! Halima Khatun binti wa Imam wa tisa, Imam Muhammad Taqi (a.s.), shangazi yake Imam Hasan Al-Askari (a.s.), akamnyanyua mtoto aliyezaliwa na kumpa baba yake ambaye alimpakata. Imam Mahdi (a.s.) pale pale akamwamkia baba yake ambaye alimjibu na akamwambia aendelee kusema kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hapo tena Imam Mahdi (a.s.) akarudia kutoa Shahada na kusoma Qur’ani:

“Tumekusudia kuwaajalia jamala yetu wale ambao waliofikiriwa ni wanyonge duniani na kuwateua Maimamu na kuwafanya warithi duniani.” (Qur’ani 28:5). Baada ya hapo, Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akamrudisha huyo mwana kwa Bibi Halima Khatun ambaye naye alimrejesha kwa mama yake. Mwana huyo alimwamkia mama yake vile vile. Katika sherehe ya aqiqa, Imam Hasan Al-Askari (a.s.) alimwamrisha wakili wake Uthman Said Umri kuwagawia maskini nyama ya mbuzi 10,000 na mikate 10,000. Kabla sijaendelea na somo hili, natumaini wasomaji watapenda kupata ushahidi wa kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.) pamoja na kwamba nimetangulia kueleza Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) inayowataja Maimamu 12 kwa majina. Nafahamu kuwa mashekhe wengi wa Sunni wanamtambua Imam Mahdi (a.s.) lakini tatizo ni kwamba hawamtambui kama Imam wa 12, kwa sababu wakimtambua hivyo bila shaka watakuwa wameikubali itikadi ya Shia Ithna’asheri, na hivyo kuachana na madhehebu yao! Lakini his69


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 70

katika Uislamu

toria ya Maimamu 12 (a.s.) aliowataja Mtume (s.a.w.w.), inamfikia Imam Mahdi (a.s.) kama Imam wa mwisho (wa 12 ): Kwa mfano kitabu maarufu cha madhehebu ya Sunni kiitwacho: Yanabiul-mawaddah’ - yapo maelezo kuhusu ukweli wa madhehebu ya Shia Ithna’asheri kwamba: ‘Mwana wa Imam Hasan Al-Askari (a.s.) yu hai hapa duniani lakini kafichwa na Mwenyezi Mungu.’ Kitabu cha Jami’ul-Usul kinatumia ushuhuda uliomo kwenye Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Abi Daud, Sahih Tirmidh, wanamkariri Abu Hurayra akisema kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Miongoni mwa wafuasi wangu kikundi kimoja kitatangaza jihadi ya kushinda vita zote. Hapo Nabii Isa atateremka kutoka mbinguni na kiongozi wa kikundi hicho Imam Mahdi (a.s.) atamkaribisha Nabii Isa kuongoza Swala ya jamaa lakini Nabii Isa atajibu, ‘Wewe ndiye mwenye mamlaka (madaraka) juu ya viumbe wa Mungu na kutokana na dhuria ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.) Mwenyezi Mungu amekutunukia heshima na ubora kuliko waumini wote wa wakati huu.’

Utoto na ujana wa Imam Mahdi (a.s.): Mwenyezi Mungu alimjaalia Imam Mahdi (a.s.) hekima na ubora tangu kuzaliwa kwake. Alijaaliwa uwezo wa kuonyesha miujiza, kusema, kusoma Qur’ani, akiwa bado mtoto kwenye susu (kitanda cha mtoto) yake. Siku ya pili tangu kuzaliwa kwake Imam Mahdi (a.s.), mhudumu mmoja wa nyumbani hapo aliyeitwa Nasim Khatuun alipokaribia susu ya Imam Mahdi (a.s.), alipiga chafya. Imam (a.s.), kama ilivyo desturi ya kiislamu kulingana na Hadith ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akamwombea akasema: “Mungu akuteremshie rehma,” na akamweleza: “Mtu yeyote anayepiga chafya anahakikishiwa kwamba hatafariki kabla ya siku tatu kupita.” Mhudumu mwingine Masr alipokaribia hiyo susu, Imam Mahdi (a.s.) alimwomba amletee sandili nyekundu. Alipoleta hiyo sandili, Imam akamwuliza, “Unanijua mimi”? Mhudumu akajibu, ‘Wewe ni Sayyid 70


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 71

katika Uislamu

wangu na mwana wa tajiri wangu.’ Imam akasema, “Mimi sikuulizi hayo. Mimi ni Imam wa 12 na wa mwisho. Mwenyezi Mungu atajalia ushindi Dhuria ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) na kwa mkono wangu na wafuasi wangu tutakomesha dhulma na maafa duniani.” Siku arubaini baada ya kuzaliwa Imam (a.s.), Bibi Halima Khatuun alipokwenda kwa Imam Hasan Al-Askari (a.s.) alishangazwa kumwona Imam Mahdi (a.s.) amekua kama mwana wa miaka miwili! Imam Hasan AlAskari (a.s.) akamweleza kwamba watoto wa Imam hukua kwa haraka kuliko watoto wa watu wengineo. Siku moja Ahmad bin Is’haq bin Sadulashary anahadithia kwamba safari moja alikwenda kwa Imam Hasan Al-Askari (a.s.) kutaka kumwuliza nani atakuwa Imam baada yake. Kabla hajamaliza kuuliza swali hilo, Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akasema: “Ee Ahmad, Mungu haachi pengo la ‘Hujjat’ Wake duniani na Hujjat Wake atakuwepo mpaka siku ya Hukumu na kwa sababu ya kuwepo kwake ndiyo Mungu huteremsha rehma na kuepusha maafa.” Baada ya hapo akauliza swali. Hapo Imam Hasan Al-Askari (a.s.) akamleta mtoto mmoja wa sura ya miaka mitatu mwenye uso uliojaa nuru na akamwambia Ahmad: “Ewe Ahmad, wewe ni katika masahaba waaminifu na kwa hivyo ninakuonyesha mwana wangu; yeye ni ‘Hujjat’ wa Mungu, Imam baada yangu na mrithi wangu. Yeye ataeneza insafu na usawa duniani.” Ahmad aliposhangazwa na hayo akamsikia huyo mtoto akisema: “Ewe Ahmad, mimi ni mrithi wa mwisho wa Maimamu wa haki. Dunia itaendelea kwa sababu yangu. Mimi nitachukua kisasi na kuwaadhibu maadui wa Dini. Wakati dunia itakapoghilibiwa na ulaghai, dhuluma, ukandamizaji na uovu, mimi nitajitokeza kwa amri ya mwenyezi Mungu na nitatawala kwa insafu na usawa.”

71


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 72

katika Uislamu

Mnamo tarehe 8 Rabiul-Awwal 260 A.H. ikawa baba yake Imam Mahdi (a.s.) amefariki. Watu wote walikusanyika hapo kwa majonzi kutokana na umaarufu wake. Katika matayarisho ya mazishi, ndugu yake Imam Hasan Al-Askari; yaani Jaffar Tawwab, alijitokeza ili kuongoza Swala ya maiti. Alisimama karibu na jeneza na watu wote walishajipanga safu kuswali. Jaffar Tawwab alipotaka kuanza, alitokea mtoto mmoja mdogo (Imam Mahdi) uso wake uking’ara kama mbaramwezi, akaja na kumwambia Jaffar: “Ewe baba mdogo sogea kando, mimi ninastahiki zaidi kuongoza Swala hii ya baba yangu kuliko wewe mdogo wake.” Huyo Jaffar alikuwa hajawahi kumwona Imam Mahdi (a.s.) kwa sababu Imam Mahdi (a.s.) alikuwa amefichwa kwa kuhofia usalama wake kutokana na khalifa Mu’tamid alivyokuwa amemfunga Imam Hasan Al-Askari (a.s.) ili Imam Mahdi (a.s.) asizaliwe. Naye Jaffar alitaraji kuwa ndiye mrithi wa Imam (a.s.). Baada ya kuongoza Swala hiyo, Imam Mahdi (a.s.) alikwenda kuonana na mtumishi wa baba yake kwa jina la Adiyan na kumwuliza juu ya barua aliyopewa. Adiyan alimpa barua hiyo. Kilichotokea ni kwamba kabla ya kufariki, Imam Hasan Al-Askari (a.s.) alimtuma Adiyan kwenda Baghdad kupeleka barua na kumweleza kuwa atakaporudi na jibu, yeye (Imam Hasan Al-Askari (.a.s.) atakuwa amekwishafariki na kwa hiyo amkabidhi jibu mtu atakayeongoza Swala ya maiti na atakayedai barua hiyo kutoka kwake yeye Adiyan. Alimwambia kuwa mtu huyo ndiye atakuwa mrithi wake (Imam mpya). Kwa hiyo njama za Jaffar Tawwab za kutaka apate mali za kaka yake na Uimamu zikashindwa. Ndugu wasomaji, tufahamu kuwa pale ambapo Imam yeyote yule alipokuwa na watoto zaidi ya mmoja wa kiume, ilibidi ijulikane wazi ni nani atafuatia kuwa Imam baada ya Imam aliye hai mwenye mamlaka kufariki. Pamoja na kwamba Mtume (s.a.w.w.) alitangulia kuwataja Maimamu wote, lakini ilibidi kila Imam, kwa kuongozwa na Mungu, amtaje mrithi wake miongoni mwa watoto wake, kwa sababu mara nyingi wato72


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 73

katika Uislamu

to karibu wote walionyesha uchamungu wa hali ya juu, iwapo uchamungu ungekuwa ndicho kigezo pekee! Hata hivyo tutaona sifa nyingine zaidi za pekee, kwa mtu kuwa nazo na kustahili kuwa Imam. Kwa utaratibu huu, hapakuwa na uwezekano wowote wa mtu kujipenyeza na kuupata Uimamu kwa njia za ulaghai au kwa makosa.

Imam Mahdi (a.s.) katika kasri (Ikulu) ya khalifa Mu’tamid: Mmoja wa wahudumu wa Imam Hasan Al-Askari (a.s.), Ali bin Zamahiyar anasimulia kuwa kazi yake mojawapo ilikuwa kumleta Imam Mahdi (a.s.) kwa baba yake kutoka mafichoni yaliyokuwa kwenye ghorofa ya chini ya ardhi ambako Imam Mahdi (a.s.) akiishi na mama yake; na kisha kumrejesha huko chini (Sardab). Siku moja tarishi wa khalifa Mu’tamid, Abbas, alitumwa kwa Imam Hasan Al-Askari (a.s.), kumweleza kuwa khalifa kapata habari kuwa Imam Hasan Al-Askari kapata mtoto lakini hakumwalika kushiriki furaha ya kuzaliwa huyo mtoto. Kwa hiyo khalifa alikuwa anasubiri kwa hamu sana kumwona mtoto huyo. Imam Hasan Al-Askari, alimwamrisha Ali bin Zamahiyar kumleta huyo mtoto (Imam Mahdi a.s.) na kumpeleka kwa khalifa. Kusikia hivyo, Ali Zamahiyar alijawa na hofu kwamba lazima khalifa atamuuwa huyo mtoto (Imam Mahdi a.s.). Imam Hasan Al-Askari (a.s.) alipomwona Ali Zamahiyar ana hofu sana akamwambia asiogope kumpeleka huyo mtoto kwa khalifa kwa sababu Allah Mwenyewe atamlinda ‘Hujjat’ Wake. Ali Zamahiyar anasema: “Mimi nilikwenda ghorofa ya chini na nikaona nuru iliyoje ikinga’a usoni mwa Imam Mahdi (a.s.), nuru ambayo sikuwahi kuiona maishani mwangu! Kiwaa kwenye shavu la kulia kiking’ara kama nyota! Nilimbeba mabegani; na nilipotoka nje ya nyumba niliona uso wake unatoa nuru ambayo ilimulika Jiji lote la Samarra mpaka mbinguni! Wakazi wa mjini waliacha shughuli zao na kumtupia macho huyo mtoto (Imam Madhi a.s.). Wanawake na watoto walikuwa wakimchungulia huyo mtoto mwenye nuru, kupitia madirishani kutoka maghorofani. Punde si 73


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 74

katika Uislamu

punde barabara zilijazana watu na ilikuwa shida kwangu kupita nifike kwa mfalme. Tarishi wa mfalme ilimbidi aniongoze njia nzima. Nilipofika barazani niliona khalifa na washauri wake na walinzi wameaibika na ung’avu wa uso wa Imam Mahdi (a.s.). Mimi nikaenda moja kwa moja mpaka kwa mfalme na nikasimama upande wa kulia nikimbeba Imam Mahdi (a.s.) mabegani na kumwelekea mfalme. Baada ya muda mrefu, waziri aliyesimama karibu na mfalme akamnong’oneza mfalme. Mimi nilikuwa na hakika kwamba ilikuwa ni juu ya kumwua Imam Mahdi (a.s.) na hapo mwili ukanisisimka! mfalme papo hapo aliamrisha walinzi wake wamwue mtoto (Imam Mahdi (a.s.)! Walinzi hao walijaribu kuvuta panga zao kutoka katika ala zao lakini panga zilikataa kutoka! Mfalme akasema kuwa panga hizo zilikataa kutoka kwa mazingaombwe ya mwana wa Bani Hashim. Hivyo mfalme aliamrisha uletwe upanga kutoka ‘Baitul-maal’ ambao hautaathirika na uchawi. Upanga ukaletwa, lakini nao ukakwama katika ala! Mfalme na washauri wake walipigwa na butwaa! Ikawa katika kutapatapa mfalme akaamrisha waletwe simba watatu wakali kutoka kwenye matundu yao. Simba hao wakaletwa. Mimi (Ali Zamahiyar) niliamrishwa nimweke mtoto mbele ya simba hao. Nilitetemeka lakini nikafanya nilivyoamrishwa, baada ya Imam Mahdi (a.s.) kuninong’oneza na kusema kuwa nisiogope. Kwa mshangao niliona hao simba watatu wananyanyua mikono yao na kunisaidia kumpokea mtoto (Imam Mahdi (a.s.) na kumweka chini kwenye sakafu. Kisha simba hao wakasimama kwa taadhima mbele ya Imam (a.s.) huku wameinamisha vichwa vyao. Kati yao, simba mkongwe ghafla akaanza kusema katika kiarabu fasahi kuthibitisha Tawhid, Unabii wa Muhammad (s.a.w.w.), na kuwataja Maimamu 12, kisha kumwamkia Imam Mahdi (a.s.) na kuongeza: “Wewe ni ‘Hujjat’ wa Mungu duniani.” Yule simba mkongwe akamweleza Imam Mahdi (a.s.) kwamba: “Hawa simba wawili wenzangu ambao ni vijana kila mara wanavamia chakula 74


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 75

katika Uislamu

chote tunacholetewa na hivyo kuninyima fungu langu, na ninaendelea kubaki na njaa.” Mtoto (Imam Mahdi) akatamka adhabu kutokana na dhuluma hiyo na kusema kuwa hao simba vijana wageuke wakongwe, na huyo mkongwe awe kijana na afya ya ujana. Kabla hata Imam Mahdi hajamaliza kusema maneno hayo, simba wawili vijana wakazeeka na kudhoofu, kisha yule mkongwe akawa kijana na mwenye nguvu. Khalifa (mfalme) pamoja na wote waliokuwepo hapo na kushuhudia miujiza yote, kwa pamoja walipiga ‘Takbir’ - ALLAHU AKBAR! kwa mshangao mkubwa na msisimko. Mara moja mfalme aliamuru Mtoto (Imam Mahdi a.s.) arejeshwe kwao kwa wazazi wake. Hapo mimi (Ali Zamahiyar) nilimshukuru Mungu na nikambeba mtoto huyo na kumrejesha nyumbani. Njiani barabara zote zilijaa watu na wote walishangazwa na nuru ya Imam Mahdi (a.s.). Kufika nyumbani nilimhadithia baba yake (Imam Hasan Al-Askari (a.s.) ambaye alifurahi na kumshukuru Mungu pia.” Ndugu wasomaji, ni kwamba maelezo juu ya Imam Mahdi (a.s.) ni kitabu kizima cha kurasa 165. Hapa nimeeleza kidogo kwa kadri ya mipaka ya somo letu. Suala la Imam Mahdi (a.s.) kughibu, yaani kufichwa akiwa hai, linawatatiza watu wengi wasio Mashia ambao wanaona kwa nini kiongozi afichwe kwa wale anaostahili kuwaongoza? Baadaye tutaona kuwa wengi wa hao Maimamu 12 (a.s.) ni kwamba waliuawa kikatili pamoja na wafuasi wao nyakati mbali mbali za uhai wao. Viongozi hao watukufu, waliuawa kwa sababu ndio waliotakiwa kuongoza Umma wa kiislamu kwa ushahidi mwingi niliotoa humu mpaka hapa. Kwa hiyo iwapo wangeshika uongozi huo, bila shaka hao walionyang’anya Uongozi huo wasingefanikiwa. Na huo ndio msingi mkuu wa uhasama. Kwa hiyo, ili ahadi ya Mwenyezi Mungu itimie na makusudio yake, ndiyo sababu mojawapo ya Mwenyezi Mungu kumficha Imam Mahdi (a.s.) ili wakati ukiwadia kabla ya Kiyama, Imam Mahdi (a.s.) asimamishe uongozi wa dunia nzima katika misingi aliyokusudia Mwenyezi Mungu. Kazi nyingine ya Imam Mahdi (a.s.) ni kulipiza kisasi (kuwaadhibu madhalimu) 75


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 76

katika Uislamu

kwa wote waliotenda maovu makubwa hapa duniani. Imani ya kulipiza kisasi kwa madhalimu ni ya Waislamu wote kama tutazingatia maneno yanayosomwa na Sunni katika ‘talqin’ wakati wa mazishi. Wakati wa kulipiza kisasi hicho ni katika ‘Raj’aat’ yaani baadhi ya watu madhalimu kutoka kila Umma watafufuliwa na kuadhibiwa kabla ya Siku ya Kiyama. Watu wema nao watafufuliwa ili kushuhudia uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Rejea Qur`an:

“Na siku hiyo tutakusanya kutoka kila taifa baadhi yao ambao walikanusha maagizo yetu na watakusanywa katika makundi.” (Qur’ani - 27 : 83 )

“Na sisi tutawakusanya wote na hatutamwacha hata mmoja wao.” (Qur’ani- 18:47) Ukizingatia Aya hizo mbili utaona kuwa zinazungumzia matukio mawili tofauti, yaani Kiyama ndogo na Kiyama kubwa kama ilivyo katika Qur’ani:

“Wao watasema: ‘Bwana wetu umetufisha tuhuisha mara mbili.” ( Qur’ani 40 : 11 )

mara

mbili na ume-

Kama kuna wasomaji wanaoona kuwa haiwezekani watu kurejeshwa duniani kabla ya Siku ya Kiyama turejee maelezo kwamba Nabii Musa (a.s.) aliwachukua masahaba 70 wateule kumwomba Mungu na kusikia Maagizo ya Mungu. Walidai wanataka kumwona Mungu kwa macho yao! Hivyo 76


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 77

katika Uislamu

wote walikumbwa na kifo. Kwa dua ya Nabii Musa, Mungu aliwarudisha duniani upya. Hayo yamo katika Qur’ani. Vile vile kuna Aya nyingine ya wazi:

“Hamkuwafikiria wale ambao waliacha majumba yao kwa kuogopa kifo na walikuwa katika maelfu, tena Mungu akaamrisha wafe; wakapewa uhai wa pili na Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani 2: 243 ) Kuna Waislamu wengine ambao wanadai kuwa itakuwaje Imam Mahdi (a.s.) kama binadamu, aishi tangu mwaka 255 A.H.? Nimekwishaeleza kuwa Maimamu siyo binadamu wa kawaida kama sisi kwa ushahidi niliotoa nyuma. Hata hivyo suala la ‘kughibu’ halikuanzia kwake tu, bali lina historia ndefu katika Uislamu kwa ushahidi ufuatao: Mayahudi walishatabiriwa na Nabii Yusuf (a.s.) kuja kwa Nabii Musa (a.s.) pamoja na dalili za kumtambua atakapokuja. Mayahudi waliteseka miaka 400 chini ya utawala wa kikatili wa Firauni. Wakati wote huo Nabii Musa (a.s.) alishazaliwa na kufichwa na Mwenyezi Mungu. Miongoni mwa Mayahudi hao alikuwepo mwanazuoni mmoja mchamungu ambaye alizidi kuwapa moyo wawe na subira hadi siku moja, wakiwa msituni ambako aliishi mwanazuoni huyo akiogopa Waisraeli kupoteza subira kwa mateso ya Firauni, aliwatokea Nabii Musa (a.s.). Mwanazuoni huyo pamoja na wenzake walisujudu kumshukuru Mungu. Walibusu miguu ya Nabii Musa (a.s.) na kumweleza mateso ya Firauni. Hata hivyo Nabii Musa (a.s.) alijificha tena na Waisrael wakamwendea tena mwanazuoni wao ambaye aliwaeleza kuwa amefahamishwa na Mwenyezi Mungu kuwa Waisraeli watapata ushindi juu ya Firauni katika miaka 40. Waisraeli walimshukuru Mungu kwa yote hadi Mwenyezi Mungu akawaondolea subira ndefu na punde wakamwona Nabii Musa 77


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 78

katika Uislamu

(a.s.) ametokeza ghafla! Hapo hapo wakasujudu sajida ya shukrani kwa Mwenyezi Mungu, na wakaibusu miguu ya Nabii Musa (a.s.). Nabii Musa (a.s.) akawaeleza kuwa ameamrishwa na Mwenyezi Mungu kujitokeza na kumkabili Firauni. Yaliyofuatia hapo, Waislamu wengi wanayafahamu toka kwenye Qur’ani na Biblia ambapo Firauni alizamishwa baharini na ikawa Nabii Musa (a.s.) na watu wake wamevuka Salama. Mfano wa pili ni ule wa Nabii Suleiman (a.s.) aliyerithi ufalme toka kwa Nabii Dawood (a.s.). Nabii Suleiman (a.s.) kwa amri ya Mungu alijificha kutoka kwa wafuasi wake na katika kipindi hicho alipata taji la ufalme. Uamuzi wa Nabii Dawud (a.s.) kumteua Nabii Suleiman (a.s.) haukuwaridhisha Waisraeli eti kwa sababu Nabii Suleiman (a.s.) alikuwa mdogo mno kuliko nduguze wote. Lakini Nabii Dawuud (a.s.) alisisitiza kuwa amri ya Mwenyezi Mungu itekelezwe. Kisa hiki ni kirefu na siyo muhimu kukieleza chote kwani baadhi yetu tunaelewa kuwa Nabii Suleiman (a.s.) alipewa ufalme mkubwa juu ya viumbe wote na Majini pia. Mara Nabii Dawud (a.s.) alipofariki ikawa Nabii Suleiman (a.s.) amekwenda kujificha na hakuonekana hadi aliporejea akiwa tayari ameoa na amevaa pete ya Ufalme. Hoja ya kwamba Imam Mahdi (a.s.) hawezi kuwa hai tangu mwaka 255 A.H. haina msingi wowote kwa sababu zifuatazo: Nabii Nuhu (a.s.) aliishi miaka 2500 Hadhrat Lukman (a.s.) aliishi miaka 3800 Nabii Suleiman (a.s.) aliishi miaka 700 Nabii Hud (a.s.) aliishi miaka 464 Nabii Adam (a.s.) aliishi miaka 930 Nabii Shiis (a.s.) aliishi miaka 900 Bibi Hawa (a.s.) aliishi miaka 930

78


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 79

katika Uislamu

Kisha tunaona kuwa Ibilisi amepewa uhai mrefu usio na idadi ya miaka hadi Kiyama; na hatumwoni lakini anatupoteza kila dakika! Kwa hiyo tufahamu kuwa Mwenyezi Mungu ana uwezo wa lolote lile atakalo. Sababu za Mwenyezi Mungu kumweka hai na kumficha Imam Mahdi (a.s.) kipindi cha muda wote huo, ni siri yake Mwenyewe (swt). Ingekuwa miujiza ya Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu inamtosha binadamu kuamini, ulimwengu mzima tungekuwa Waislamu. Nasema hivi kwa sababu hapo Samarra alipozaliwa Imam Mahdi (a.s.) na kuishi hadi kufichwa kwake, bado muujiza wake Imam Mahdi (a.s.) unazidi kutokea mpaka leo! Imam huwa anakuja mji huo kuzuru makaburi ya baba na babu yake. Mara anapofika, Jiji zima hujaa nuru ya ajabu! Waarabu wakazi wa hapo hufurahia sana na wanawake hupanda maghorofani kufurahia kuja kwa Imam (a.s.). Hata katika usiku wa giza, Imam (a.s.) anapozuru Jiji hilo, lote hung’aa kwa nuru kiasi kwamba mtu akinyoosha kidole au akitoa ufunguo na kuuning’iniza, ufunguo huo huwaka kama mshumaa! Lakini Imam mwenyewe haonekani. Hata hivyo pamoja na hayo, utaona kuwa wakazi wa mji huo ni Waislamu wa madhehebu ya Sunni wala si wenye itikadi ya Shia Ithna’asheri! Nina maana kuwa hawana imani kuwa huyo Imam Mahdi (a.s.) ndiye Kiongozi wa 12 katika viongozi aliowataja Mtume (s.a.w.w.) kuongoza Waislamu baada yake! Takwimu zaonyesha kuwa wakazi wa mji huo ni Sunni kwa asilimia kati ya 90-95%! Kwa hiyo ndugu wasomaji ni kwamba kazi ya ‘tabligh’ ni sawa na kumfikisha ngamia mtoni, na siyo kumlazimisha kwa kumkandamiza shingo ili anywe maji! Ushahidi juu ya Imam Mahdi (a.s.) katika vitabu vya Sunni Sheikh Suleiman Hanafi Kanduuzi (Aliyefariki mwaka 1873 A.D (1294 A.H.) mtunzi wa kitabu maarufu cha Sunni kwa jina Yanabii-ul-Mawaddah ukarasa 369-71 (Tafsiri ya kiingereza) ameandika kuwa: Yahudi mmoja jina lake Naasal alimwendea Mtume (s.a.w.w.) akitaka maelezo ya kumuondoa shaka alizonazo juu ya Uislamu; na kwamba akipata maelezo ya kuridhisha ataingia Uislamu. 79


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 80

katika Uislamu

Naasal aliuliza juu ya upweke wa Allah, akajibiwa na kuridhika. Kisha aliuliza juu ya Urithi wa Mtume na Mitume waliopita na utangazaji wa warithi hao. Mtume (s.a.w.w.) alijibu kuwa: “Nabii Musa (a.s.) alimteua Yushaa bin Nun. Baada yangu mrtihi wangu ni Ali Ibn Abi Talib. Baada yake ni wajukuu zangu wawili Hasan na Husein. Baada ya hao watakuwa Maimam tisa ambao watatokana na kizazi cha Husein (a.s.); nao ni warithi wangu.” Kufikia hapo yule Yahudi akaomba majina ya hao Maimamu tisa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, “Baada ya Husein atafuata mwanae: Ali Ibn Husein, kisha Muhammad Ibn Ali (Baqir), kisha Jaffar Sadiq, kisha Musa Kadhim, kisha Ali Ridha, kisha Muhammad Taqi, kisha Ali Naqi, kisha Hasan Al-Askari, na mwisho Muhammad Mahdi.” Yule Yahudi aliomba aelezwe hao warithi watatu wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w.) watakufa namna gani? Mtume (s.a.w.w.) alijibu kuwa: “Hazrat Ali (a.s.) atauawa kwa upanga, Hasan atapewa sumu na Husein atauawa (kwa kuchinjwa) huku akiwa na njaa na kiu ya siku tatu.” Yule Myahudi akamwuliza Mtume (s.a.w.w.) kama hao Mashahidi watakuwa na Mtume (s.a.w.w.) huko peponi? Mtume akajibu: “Hao watakuwa na mimi peponi.” Hapo yule Myahudi akakiri na kutamka Shahada takatifu na akawa Mwislamu na akasema: “Ewe Mtume wa Allah, bila shaka hao uliowataja ni warithi wako. Hao wametajwa kwa kirefu katika vitabu vya Manabii waliopita na vile vile katika maagano ya Nabii Musa. Imeelezwa wazi humo kwamba atakuja Nabii katika kipindi cha mwisho akijulikana kwa majina ya Ahmad na Muhammad na ndiye wa mwisho wa Manabii na baada yake hatakuja Nabii mwingine. Nabii huyo atakuwa na warithi kumi na wawili; wa kwanza ni binamu yake na mkwewe; wa pili na wa tatu watakuwa ndugu. Mrithi wa kwanza atauawa kwa upanga, wa pili kwa sumu, na wa tatu atauawa jangwani pamoja na wanawe na masahaba wake wakiwa na njaa na kiu ya siku tatu. Watakabili misiba yote kwa subira na watapewa jazaa na Mungu na kutukuzwa na uwezo wa kuokoa (Shafaat) marafiki na wafuasi wao kuepuka kwenda motoni. Waliobaki tisa watatokana na kizazi chake (Husein) na kwa ujumla watakuwa kumi na wawili kama idadi ya ‘Asbat.’ 80


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 81

katika Uislamu

Mtume Mtukufu (s.a.w.w.) alimwuliza huyo myahudi kama anajua habari za Asbat. Myahudi alijibu; “Ndiyo, walikuwa Kumi na Wawili na katika hao Lawa bin Barkhya alighibu na kujitokeza tena na kupigana na mfalme wa Karastya na kumwua’. Mtukufu Mtume naye akaendelea kusema kuwa: “Kwa hakika yale yaliyowakabili Wayahudi, yatatokea pia kwa wafuasi wangu. Mrithi wangu wa Kumi na Mbili ataghibu. Katika siku hizo Uislamu utabakia jina tu. Qur’ani itasomwa kama kawaida ya dini lakini bila kufuatwa kwa vitendo. Wakati dhuluma (kufuru) itakapokuwa imetawala dunia, mrithi wangu wa Kumi na Mbili atajitokeza na kufufua Uislamu, kurejesha haki na insafu. Watakaobahatika ni wafuasi wale ambao watamtii Mahdi, na ghadhabu ya Allah itawasubiri watakaomuasi Mahdi.” Katika kitabu cha Jami-ul-Usul kinatoa ushahidi toka vitabu vya Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sunan Abudawood na Sahih Tirmidh; kwamba anakaririwa Abu Huraira akimkariri Mtume (s.a.w.w.) kuwa alisema: “Miongoni mwa wafuasi wangu, kikundi kimoja kitatangaza jihadi ya kushinda vita zote. Hapo Nabii Isa atateremka kutoka mbiguni, na kiongozi wa hicho kikundi. Imam Mahdi atamkaribisha Nabii Isa kuongoza swala ya jamaa lakini Nabii Isa atajibu, “Wewe ndiye mwenye mamlaka (madaraka) juu ya viumbe wa Mungu na watokana na dhuria ya Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu amekutunukia heshima na ubora kuliko waumini wote wa wakati huu’. Imam Ahmad Ibn Hanbal, mwandishi maarufu wa vitabu vya Kisunni ameridhia katika sehemu ya kwanza ya kitabu chake cha Musnad, ukurasa 99 kwamba imesimuliwa kuwa: Mwenyezi Mungu atamleta Mahdi (a.s.) aliyetokana na dhuria yangu kutoka mafichoni kabla ya Siku ya Kiyama, japokuwa ibakie hata siku moja kabla ya mwisho wa dunia, naye ataeneza haki, usawa na usalama duniani na kutokomeza dhulma na ukandamizaji.

Elimu ya kuzaliwa ya Imam Muhammad At-Taqi (a.s.) Imam wa Tisa: Imam Muhammad At-Taki (a.s.) aliishi kati ya mwaka 195 A.H-220 A.H. 81


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 82

katika Uislamu

Baba yake waliishi wote miaka mitano tu na baada ya hapo hawakuonana tena kwa sababu baba yake alifariki huko Khurasan Iran miaka mitatu tangu waachane. Wakati huo alikuwa anatawala mfalme Maamun. Tukianzia utawala wa bwana Abubakr Sidiq, tutaona kuwa huyu Maamun anashika nafasi ya 30 tangu kufariki Mtume (s.a.w.w.). Mfalme huyu alitambua sana utukufu wa Ahlul-Bayt (a.s.) na wa Mtume (s.a.w.w.) na nafasi yao. Aliona kuwa njia ya kumdhibiti Imam Taqi (a.s.) ni kumwoza binti yake ili awe karibu naye zaidi. Mfalme huyo aliona pia atangaze kuwa Imam Ali Ridha (Baba Yake Imam Muhammad Taqi) ndiye atakuwa mrithi wake kwa matumaini ya kuungwa mkono na kiongozi huyo wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo ikawa Imam Ali Ridha (a.s.) ameuawa kwa sumu kwa njama za mfalme Maamun kwa sababu mfalme huyo alimwona Imam Ali Ridha (a.s.) akifufua Uislamu wa kweli ambao ungehatarisha utawala wake (mfalme) usiojali dini. Pamoja na uamuzi huo, mfalme Maamun aliona kuwa lengo lake la kutaka kuungwa mkono na kiongozi wa dini bado ni muhimu. Kwa hiyo aliona kuwa mtoto wa Imam Ali Ridha (a.s.), yaani Imam Muhammad Taqi (a.s.), kwa vile ni mdogo wa miaka 8 tu, hatakuwa mpinzani wa utawala wake, na mbinu ya kwanza ikawa amemwozesha binti yake, kama alivyomwozesha dada yake kwa Imam Ali Ridha (a.s.). Kwa hiyo watu mashuhuri walio karibu na mfalme Maamun hawakuridhika na uamuzi wa mfalme wa kumfanya Imam Muhammad Taqi (a.s.) kuwa kiongozi mkuu wa dini. Watu hao walipendelea mfalme achague kati ya wanachuoni watu wazima kujaza nafasi hiyo. Lakini mfalme aliwaeleza kuwa ingawa Imam Muhammad Taqi (a.s.) ni mdogo, ana elimu kubwa mno kuliko wanachuoni wote maarufu. Ikawa mfalme amemwita Imam Muhammad Taqi (a.s.) na kuwaalika wanachuoni na watu wote waje wafanye majadiliano naye kuhusu elimu ya dini. Viliwekwa viti 900 kwa ajili ya wanachuoni tu, mbali na watu wengine wengi. Mwanachuoni mmoja maarufu aliyeitwa Yahya alichaguliwa kuhojiana na Imam (a.s.). Yahya alimwuliza Imam Muhammad Taqi (a.s.) kwamba: “Iwapo mtu aki82


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 83

katika Uislamu

winda hali ya kuwa yumo katika Hijjah, Kafara yake ni nini?” Swali hili lilionyesha jinsi Yahya alivyokuwa hajui ukubwa elimu aliyokuwanayo Imam Muhammad Taqi (a.s.)! Katika kumjibu Yahya, Imam (a.s.) alisahihisha swali hilo na kusema kuwa, “Swali lako halieleweki. Ungelisema kama kitendo hicho kilitendwa ndani ya mipaka mitakatifu ya Al-Kaaba au nje yake, kama huyo mtu alifanya hivyo akifahamu vema sheria za tendo hilo au la, kama alimwua mnyama huyo makusudi au kwa bahati mbaya, kama mtu yule alikuwa mwungwana au mtumwa, mtu huyo ni mtu mzima au mtoto, kama ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya hivyo au vipi; kama alimuuwa ndege au, kama alifanya kitendo hicho usiku; au kwa siri au mchana, na kama alikuwa anakwenda ‘Hajj’ au ‘Umra’. Haiwezekani kutoa jibu kamili kwa swali lako mpaka hayo yote yamewekwa wazi kwa sababu kafara ya kila kosa kati ya hayo itakuwa tofauti!” Yahya alipigwa na mshangao pamoja na wenzake na watu wote waliohudhuria hapo, kuona mtoto mdogo wa miaka 8 anafafanua sheria za dini kwa ujuzi mkubwa kama huo! Yahya alimwomba Imam (a.s.) aeleze hukumu za kosa hilo katika mazingira yote hayo. Imam (a.s.) alifafanua kila kitu kwa utaratibu mzuri na utaalamu wa hali ya juu, kiasi ambacho kila mtu aliridhika kwamba Imam Muhammad Taqi (a.s.) alikuwa mrithi wa kweli wa baba yake na alikuwa na elimu zaidi ya wanavyuoni wote. Yote haya yalitokea wakati ambapo Imam Muhammad Taqi (a.s.) hakuwahi kufundishwa na mtu yeyote yule katika shule yoyote ile! Hata baba yake walitengana akiwa na umri mdogo wa miaka mitano tu! Umri huo pia haumwezeshi kusomeshwa shuleni na kuhitimu kiasi hicho! Huo ndio ukweli wa hali ya Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.). Sio binadamu wa kawaida kama sisi! Elimu ya kuzaliwa nayo Imam Jafar Sadiq (a.s.), Imam wa Sita: Imam Jafar Sadiq (a.s.) alikuwa maarufu sana kutokana na elimu yake kubwa sana ya dini. Kama tutakavyoona katika maelezo ya mbele, ni 83


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 84

katika Uislamu

kwamba yeye ndiye mwalimu mkuu wa viongozi wakuu wa Sunni wa kwanza yaani bwana Abu Hanifa na bwana Maliki. Hata mabwana Shafii na Hambal yaani kukamilisha viongozi wakuu wanne wa madhehebu ya Sunni, nao pia walipata msingi mkuu wa elimu ya dini iliyotokana na Imam Ja’far Sadiq (a.s.) ambaye aliishi kati ya mwaka 83 A.H. na 148 A.H. Wakati huo alitawala mfalme Mansur ad-Dawaniqi wa ukoo wa Bani Abbas. Huyu mfalme Mansur alikuwa mtawala wa 24 kuanzia kwa bwana Abubakr Sidiq. Tukirejea kwa Imam Ja’far Sadiq (a.s.) ni kwamba siku moja alifika kwa mfalme Mansur, akamkuta daktari mmoja Mhindi anasoma kwa sauti habari za udaktari toka kwenye kitabu chake. Ikawa Imam Ja’far Sadiq (a.s.) naye anasikiliza. Baada ya huyo daktari kumaliza kusoma, alimwuliza Imam iwapo ana lolote la kuuliza. Imam akamwambia kuwa elimu aliyo nayo ni bora zaidi, hivyo hana cha kuuliza. Yule daktari akauliza ‘Ni elimu gani uliyonayo’. Imam (a.s.) akaanza kumwuliza maswali yafuatayo: Imam: Kwa nini mifupa ya kichwa ni mingi na imeunganishwa badala ya kuwa mfupa mmoja uliofunika kichwa chote? Daktari: Sijui nieleze bwana. Imam: Kuna viungo vya kuunganisha mifupa katika kichwa kwa sababu kichwa kiko wazi kwa ndani. Kama ungekuwa mfupa mmoja bila viungio ingekuwa rahisi kuumwa kichwa mara kwa mara. Imam: Kwa nini utosi hauna nywele? Daktari: Sijui labda unieleze. Imam: Nywele zimeoteshwa juu ya kichwa ili zisaidie kuingiza mafuta kwenye ubongo na kusaidia hewa (gases) ndani ya ubongo kutoka nje na kulinda kichwa dhidi ya joto la nje. Imam:

Kwa nini nyusi zimeota juu ya macho?

84


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 85

katika Uislamu

Daktari: Sijui bwana nieleze. Imam:

Imam:

Nyusi zimeoteshwa juu ya macho ili ziweze kuzuia mwanga mkali na kuruhusu mwanga kiasi kinachostahiki tu kwa sababu utaona mwanga ukizidi mtu hukinga kiganja usoni kuzuia mwanga. Kwa nini pua imewekwa katikati ya macho?

Daktari: Kwa kweli sijui, labda unieleze Imam:

Pua imewekwa katikati ya macho ili igawe mwanga kwenye macho kwa usawa kila jicho.

unaoingia

Imam:

Kwa nini midomo na masharubu vimewekwa juu ya kinywa?

Daktari: Sielewi. Imam:

Vimewekwa hapo ili kuzuia uchafu utokao kwenye ubongo usiingie kinywani; na pia kuzuia kinywaji na chakula cha mtu kisichafuke na uchafu huo.

Imam : Kwa nini kucha na nywele havina uhai? Daktari: Sifahamu bwana, nieleze. Imam:

Nywele na kucha vinapokua huchukiza na ni muhimu kuvikata. Kwa hiyo iwapo vingekuwa na uhai, kuvikata ingekuwa maumivu makali sana kwa mtu.

Imam: Kwa nini magoti hujikunja kwa nyuma? Daktari:Kwa kweli sifahamu, nieleze. Imam: Magoti hujikunja kwa nyuma kwa sababu mtu husonga mbele anapotembea, kwa hiyo umbo la magoti lilivyo, husawazisha miondoko ya mtu. Vinginevyo ingebidi mtu aanguke akitaka kutembea.

85


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu Imam:

7/1/2011

12:20 PM

Page 86

katika Uislamu

Kwa nini unyayo umeacha nafasi chini ?

Daktari: Sifahamu. Imam:

Nafasi imeachwa ili kwamba kama isingeachwa, mguu ungekuwa mzito sawa na jiwe la kusaga nafaka. Iwapo jiwe hilo litalalia chini (sehemu ya juu yenye bonde katikati) hata mtoto anaweza kulisogeza. Lakini likikalia makalio yake hata mtu mzima atashindwa kulisogeza.

Daktari huyo aliposhindwa kujibu maswali yote hayo, alimwuliza Imam (a.s.) ni wapi kapata elimu yote hiyo? Imam (a.s.) alijibu kuwa ameipata kupitia kwa babu zake hadi kwa Mtume (s.a.w.w.) na Malaika Jibril (a.s.) hadi kwa Mwenyezi Mungu Mwenye uwezo usio na mipaka, Mwumba wa viumbe na roho. Daktari alikiri ukweli huo kwa Shahada. Ndugu wasomaji bila shaka tumeona kuwa majibu aliyotoa Imam Ja’far Sadiq (a.s.) yanadhihirisha elimu kubwa mno aliyokuwa nayo. Siku hizo za karne ya pili ya kalenda ya Kiislamu, yaani wakati wa uhai wa Imam Ja’far Sadiq (a.s.), ni miaka zaidi ya 1,200 iliyopita! Wakati huo elimu kama hiyo usingeweza kuipata shule yoyote ile. Hata wakati huu tulionao, si rahisi kumpata daktari au mtaalamu ambaye anaweza kutoa majibu sahihi kwa maswali hayo! Kwa hiyo tunaposema kuwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) wanaongozwa na Mwenyezi Mungu, hatusemi hivyo kwa mapenzi yetu tu au ushabiki; bali ni ukweli wa wazi kwa watu wenye kufikiri. Kutokana na elimu kubwa ya Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.), Imam Ja`far as-Sadiq (a.s.) aliwaeleza kundi la baadhi ya watu kutoka Kufa, Iraq kwamba: “Ajabu iliyoje watu wanasema kuwa wamepata elimu yote kutoka kwa Mtume wa Allah, (s.a.w.w.) na wanatenda kwa mujibu wake na wameongozwa nayo, lakini wakati huo huo watu hao wanafikiri kuwa sisi, watu wa nyumba yake hatukupata elimu yoyote kutoka kwake, wala kuongozwa sawa sawa katika njia iliyonyoka, ambapo sisi ni watu wake na 86


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 87

katika Uislamu

kizazi chake! Ilikuwa ni katika nyumba yetu ufunuo (Qur’ani) uliletwa kwake na kutokana na nafasi zetu, elimu iligawanywa kwa watu. Unafikiri kwamba walipata elimu na waliongozwa wakati sisi tukabakia wajinga na tukapotea? Kwa hakika hayo hayawezekani.” Rejea: Bihaarul-Anwar, Jz. 26, Uk. 158. Zaidi ya hayo ukizingatia historia ya dunia utaona kuwa maendeleo makubwa ya kisayansi, asili yake yameanzia kwa Waislamu na baadaye kuendelezwa na Wazungu baada ya mfumo wa elimu wa dola ya kiislamu kuporomoka. Tunao ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukweli huu wa maendeleo makubwa ya fani mbali mbali kuletwa na Uislamu. Kwa mfano Sayansi ya tiba, Sayansi ya uchanganyaji madawa, ujenzi wa hospitali maalumu, elimu ya kemia (Chemistry), viwanda, hisabati, jiografia, sanaa, fizikia, takwimu n.k. Wakati huo wa maendeleo makubwa ya elimu katika dola ya kiislamu ya wakati huo, huko Ulaya ulikuwa ni wakati wa giza nene la ujinga, mpaka Uislamu ulipofika huko na kubadili kabisa maisha ya watu wa huko. Wanasayansi dunia nzima hadi wakati huu, wanaendelea kuvumbua mambo mapya kwa binadamu. Ukichunguza uvumbuzi wao huo utaona kuwa mengi ya yale wanayodai kuyavumbua, yalishatajwa katika Qur’ani miaka 1400 iliyopita! Kwa mfano mwanasayansi maarufu sana duniani bwana Newton alivumbua nguvu ya uvutano (gravity) ambayo huvuta vitu viangukie duniani na hutawala (huongoza) mzunguko wa sayari. Kwa wajuzi wa tafsiri sahihi ya “Mwenyezi Mungu ndiye aliyeziinua mbingu bila nguzo mnazoziona..” (Qur’ani 13:2) kwa mtazamo wa kisayansi, tutaona kuwa nguvu hiyo (gravity) ilishatajwa katika Qur’ani na jinsi inavyoongoza mwenendo mzima wa sayari zisitokee kugongana au kuacha njia zake maalumu na kuanguka! Hapa inabidi tuzingatie ukweli kwamba alimradi Siku ya Kiyama haijafika, bado katika Qur’ani kuna elimu nyingi ambazo uwezo wa binadamu wa kisayansi haujafika kuzigundua na kuzithibitisha katika Qur’ani tukufu. 87


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 88

katika Uislamu

Kwa hiyo Waislamu tuache tabia ya baadhi yetu kujidai tunaweza kuifasiri Qur’ani yote na kuisherehesha kwa usahihi na kufahamu kila maana yake! Yawezekana tukawa na ujuzi wa kuighani Qur’ani, lakini siyo kuifasiri kwa usahihi wote. Ukitaka kuthibitisha ukweli huu jaribu kusoma maelezo ya uvumbuzi wa elimu mbali mbali za kisayansi ambazo hata hivyo si ngazi ya watu wasio wasomi huwa na uwezo wa kuzielewe japo zimo katika Qur’ani! Sasa ni vipi utafasiri na kufafanua suala ambalo huna elimu nalo kisayansi? Kimsingi ni kwamba wakati huu baadhi ya watu maarufu huko Ulaya na Marekani wanakiri wazi wazi, ukweli kwamba Uislamu ndio chanzo (pioneer) cha elimu nyingi za kisasa tunazojivunia; na ambazo zimeibadili sura ya dunia - (Rejea: Sura ya 23 kwa ushahidi wa kauli hizo) au soma kitabu: Bible, Qur’ani and Science, cha Maurice Bucaille au kitabu: The seal of the Prophets and his Message, cha Sayyid Mujtaba Musavi Lari - Iran. Tutakumbuka kuwa mwanasayansi maarufu bwana Galilei ndiye wa kwanza kuwakilisha kwetu binadamu, nadharia juu ya kwamba dunia huzunguka milele. Ugunduzi wake huo ulipokelewa kwa wimbi la upinzani kwamba ni mwongo. Lakini katika Qur’ani, ukweli huu ulishaelezwa wazi miaka 1400 iliyopita pamoja na kazi ya milima tunayoona duniani:

“Je, hatukuifanya dunia kama kiti (cradle) na milima kama mambo (vigingi)” (Qur’ani78: 6-7)

“(Mwenyezi Mungu) ameiweka milima duniani, kuzuia isiwayumbishe ovyo (bila utulivu)” (Qur’ani 31:10 )

“Yeye ndiye aliyefanya ardhi laini kwa ajili yenu, basi nendeni katika pande zake na kuleni katika riziki zake.” (Qur’ani 67:15 ) 88


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 89

katika Uislamu

Hapa tunaona kuwa Qur’ani imeeleza ardhi kama kiti (cradle) cha kupumzikia bila usumbufu (discomfort) japo dunia imo katika kuzunguka daima! Na huo ndio ukweli kwa sababu dunia huzunguka kwa mwendo wa kilomita ishirini na saba kwa dakika bila sisi kutikisika! Leo hii tunasikia kwamba maendeleo yameanzia Ulaya lakini asili ya maendeleo hayo siyo Ulaya! Na tunapothibitisha kwamba Uislamu ndio msingi mkuu wa elimu zote hizi, ni vizuri tujiulize kwa nini leo hii Waislamu tumerudi nyuma wakati ambapo Qur’ani tunayo na Sunna za Mtume (s.a.w.w.) tunazo; na wakati huu ni rahisi kupata elimu ya dini kutokana na uvumbuzi wa vifaa vya kisasa tulivyonavyo? Lakini badala yake leo hii tunasikia kilio cha Waislamu kuwa tumedidimia kielimu, hali ya kuwa elimu ilianzia katika Uislamu! Siri yake ni kwamba enzi hizo, kama tulivyoona nyuma, ulikuwa ni wakati wa uhai wa hao Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) ambao japo walikuwa wakiishi katika mazingira magumu ya wafalme waovu, walitoa elimu yao kubwa kwa wafuasi wao, na ukawa mwanzo wa elimu bora kama hiyo kuenea ulimwenguni. Vinginevyo si rahisi kuamini kuwa enzi hizo kulikuwepo na taasisi za elimu kama wakati huu! Na elimu kubwa kama hiyo haiwezi kuwafikia watu hivi hivi bila chanzo maalumu. Hakuna elimu ya miujiza. Tunafikia uamuzi huu kutokana na ukweli kwamba Uislamu ni dini iliyokusudiwa kuongoza maisha yote ya Mwislamu katika kila ngazi ya maisha yaani kiroho, kijamii, kiuchumi, kisiasa n.k. Kwa msingi huo, ni kwamba Mwenyezi Mungu, kupitia kwa wawakilishi wake halali, alikusudia kumwendeleza binadamu kiroho na kidunia na hivyo kumpa elimu ya kufikia azma hiyo. Binadamu siyo sawa na mnyama. Lakini kwa kuwa binadamu hakuuchukulia Uislamu kama mfumo kamili wa maisha, yaani binadamu ameamua kuchagua hili na kuacha lile katika dini, baraka ya Uislamu imeondoka na kutuacha kama tulivyo sasa. Hatuna wa kumlaumu ila sisi wenyewe. Ilimradi historia ya dunia inathibitisha kuwa maendeleo 89


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 90

katika Uislamu

na elimu vilianzia kwetu, hakuna sababu kwa nini vituponyoke wakati Uislamuu ni ule ule haujabadilika mbele ya Mwenyezi Mungu! Nimetangulia kueleza kuwa sitaweza kutoa historia ya maisha ya kila Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu ni matukio mengi mno. Sasa nitaelezea sifa za jumla na za pekee kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wote wa Mtume (s.a.w.w.). Sifa za Imam Ali Ibn Abu Talib (.a.s.) zitaelezwa peke yake katika Sura ya 10. Lakini kabla ya kueleza hayo yote, ingefaa nieleze kwanza ni vipi msingi mkuu wa elimu zote muhimu unatokana na Uislamu. Maelezo zaidi ni muhimu.

Asili ya elimu za kidunia na maendeleo ya kisayansi: Tunaposoma kuwa chanzo au misingi ya maendeleo ya kielimu huko Ulaya ni Uislamu, siyo kama ni uongo bali ni ukweli wa kihistoria. Mnamo miaka ya 476 A.D. huko Ulaya Kanisa lilichukua madaraka zaidi juu ya jamii, mbali na uongozi wa kiroho. Kanisa lilitawala fikra na maisha ya watu kiasi kwamba hakuna mwanasayansi aliyeruhusiwa kutoa mawazo yanayotofautiana na msimamo au imani ya kidini. Wakati huo (zama za kati) Ulaya ilikuwa katika giza nene la ujinga wa kuvamiana, umwagaji damu na migongano ya kitaifa na kikabila. Kwa msimamo huo wa Kanisa dhidi ya wanasayansi, Kanisa lilimshutumu bwana Galileo kwa hatua yake ya kisayansi ya kuthibitisha nadharia ya Copernicus kwamba dunia milele inazunguka jua! Kanisa lilimwandama Galileo na kumlazimisha kukanusha ugunduzi huo wa kisayansi! Galileo alitubu kwa maneno yafuatayo: “Mimi Galileo katika umri wangu wa miaka 70 (mnamo mwaka wa (1633 A.D.) nikiwa nimepiga magoti mbele ya Mtakatifu Papa na Waadhama Maaskofu, na vitabu vitakatifu, vikiwa mbele yangu, ninavishika mikononi na kuvibusu, huku nikitubu na kukanusha madai ya kijinga kwamba dunia huzunguka jua, na ninachukulia madai hayo kuwa ni uzushi wa kuchukiza.� Wakati Kanisa limejenga msimamo huo huko Ulaya, ni ajabu kwamba miaka 500 nyuma ya hapo, mwanasayansi Mwislamu (mtaalamu wa elimu 90


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 91

katika Uislamu

ya nyota) mashuhuri na mwanahisabati pia, aliyeitwa Umar Khayyam wa huko Nishapur; India, (wakati William the Bastard akiiteka England), alikuwa amewapa Iran kalenda (Jalali Calendar) ambayo hadi hivi leo ndiyo inayotuwezesha kuanza mwaka mpya kwa usahihi wa saa, dakika na sekunde na siyo kwa kufuata siku tu! Hayo ni mahesabu aliyoyafanya mwanasayansi huyo enzi hizo zisizo na vifaa vya kisasa lakini kwa usahihi wa hali ya juu unaokamilisha mzunguko mmoja (orbit) kuzunguka jua. Mifano ya wanasayansi waliozuiwa na Kanisa kutoa uvumbuzi wao, ipo kadhaa wa kadhaa lakini nafasi haitoshi kueleza yote. Kwa upande wa nchi za kiislamu za wakati huo, mnamo miaka ya 794 A.D. chini ya utawala wa Bani Abbas, khalifa Ma’amun alizindua ‘Nyumba ya Maarifa’ huko Baghdad kama kituo cha sayansi. Aliweka humo vyombo vya uchunguzi wa anga, maktaba ya wazi (public library), ambapo alitumia Dinari 200,000 (dola million saba). Aliwakusanya hapo wasomi maarufu wajuzi wa lugha za nje na taaluma tofauti. Khalifa huyo alitenga pesa nyingi za kuwezesha kuwatuma nchi mbali mbali kukusanya vitabu juu ya sayansi, tiba, hekima, hisabati na ujuzi wa lugha mbali mbali. Wakusanyaji hao wa vitabu walituma huko mzigo wa vitabu uliobebwa na ngamia 100! Miaka hiyo Ulaya yote haikuwa na chuo kikuu hata kimoja. Katika kitabu chake kiitwacho: History of Islamic and Arab Civilisation, Dr. Gustave Le Bon anaandika, katika uk. 329, juzuu ya tatu, kwamba: “Siku hizo wakati vitabu na maktaba havikuwa na maana yoyote Ulaya, nchi nyingi za kiislamu zilikuwa na vitabu na maktaba kwa wingi. Huko Baghdad katika ‘Nyumba ya Maarifa’ kulikuwa na vitabu milioni nne; na huko Cairo katika Maktaba ya Mfalme, vitabu milioni moja, na huko katika maktaba ya Syria, vitabu milioni tatu. Huko Spain wakati wa utawala wa Waislamu, kulikuwa na uchapishaji (publication) wa vitabu kati ya elfu 70 hadi 80 kila mwaka.” Mnamo mwaka wa 1300 A.D. mwanzoni, bwana ‘G.L. Estrange katika kitabu chake: ‘The Legacy of Islam’ ukurasa 230 anaeleza kuwa ‘Chuo 91


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 92

katika Uislamu

Kikuu cha Mustansariya kiliwekewa vifaa vingi na kilijengwa katika eneo kubwa (campus) kwa majengo ya kupendeza, vitengo (Vitivo) vinne vya sheria kila kimoja wanafunzi 75 na mkufunzi (Professor) aliyefundisha wanafunzi bila kuwatoza ada, na akilipwa mshahara. Sarafu moja ya dhahabu alipewa kila mwanafunzi kila mwezi kama masurufu. Jiko la Chuo lilihudumia wanafunzi 300 kwa chakula. Maktaba ilikuwa na vitabu vingi vya taaluma mbali mbali kwa wanafunzi wote, na vifaa vya kuandikia pia vilitolewa. Madaktari waliwapitia wanafunzi kila siku na kuchunguza afya zao na madawa yalihifadhiwa ya kutosha kuhudumia wanachuo wote. Maendeleo yote hayo ni miaka 700 iliyopita hadi leo (1998 A.D.)!’ Dr. Gustave Le Bon katika kitabu chake hicho hicho cha “Islamic and Arab Civilisation” uk. 557 - 558 ameandika kuwa “Waislamu walisoma elimu na kuzitumia kikamilifu. Kila mji walioutawala, kitu cha kwanza walijenga msikiti na kufuatia chuo (college). Hali hii iliwezesha kujengwa taasisi za elimu za hadhi kubwa katika miji mingi. Benjamin Toole (aliyefariki mwaka 1173 A.D.) alisema kuwa huko Alexandria alikuta vyuo 20 vikifanya kazi, wakati miji ya Baghdad, Cairo, Cordova n.k., ilikuwa na vyuo vikuu vyenye maabara, vyombo vya uchunguzi wa anga, maktaba kubwa na huduma za kutatua matatizo ya kitaaluma. Huko Alexandria (Andalusia) kulikuwa na maktaba za umma 70. Maktaba ya Al-Hakeem the II huko Cordova ilikuwa na vitabu 600,000 na ilichukua vitabu 44 kuhakiki (cataloging) hazina ya vitabu vyote vya maktaba hiyo’. Katika kitabu chake hicho, uk. 562 anaongeza kuwa, ‘Waislamu walianzisha sayansi kwa mtazamo sahihi wa kuona mbele na uvumbuzi kwa njia ya kisayansi (hypothesis) huku wakiandika vitabu vilivyoeneza uwezo wao kitaaluma dunia yote. Kwa njia hiyo waliifungulia Ulaya milango ya kuelekea kwenye barabara ya ufufuaji wa elimu (Renaissance). Ni kwa njia hiyo ambapo sayansi za zamani za Ugiriki na Roma zilivumbuliwa upya na kurejeshwa tena Ulaya pale ambapo Ulaya ilikuwa inafufuka toka kipindi cha giza (Dark Ages.)’

92


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 93

katika Uislamu

JINSI ELIMU ZA KIISLAM ZILIVYOLETA MAENDELEO YA SAYANSI HUKO ULAYA. Uchanganyaji Madawa (Pharamacology): Waislamu walivumbua ujuzi wa kuchanganya madawa ya kemikali katika vidonge na dawa za maji ambazo nyingi zake bado zinatumika hadi leo, ingawa baadhi ya dawa hizo zinadaiwa kuwa ni uvumbuzi mpya wakati siyo kweli! Mji wa Baghdad ulikuwa na maduka (Chemist) ya dawa hizo yapatayo 60. Asili ya majina ya Alcohol, Alkali, Alkaner, Apricot, Arsenic ni Uarabuni, India na Uajemi katika nchi za Waislamu.

Hospitali: Baada ya miaka 200 kufariki Mtume (s.a.w.w.), huko Makka, Madina na miji mikubwa ya kiislamu, ilikuwa na hospitali. Miaka 300 baada ya Hijra, gavana Adhud-ud-Dowleh Deylamy alizindua ‘Adhud Hospital’ iliyokuwa na mabingwa 24 wa fani mbali mbali. Tiba ilitolewa kwa wote bila kujali dini zao au kabila au rangi zao. Wagonjwa wa maradhi mbali mbali walitenganishwa, na hospitali hizo zilitumika kufundishia tiba kwa wanafunzi ambao walifundishwa nadharia na vitendo. Sultan Mahmoud alSeljuk alikuwa na hospitali inayotembea, ‘Mobile Hospital’ ambayo ilihitaji ngamia 40 kusafirisha vifaa vyake!

Kemia (Chemistry): Sahaba mmoja wa Imam Ja`far Sadiq (a.s.) Jabir Ibn Haiyan ni bingwa maarufu duniani na anaitwa Baba wa Kemia (Father of Chemistry) pamoja na fani ya kubadili chuma kuwa dhahabu yaani ‘Alchemy’. Vitabu vyake zaidi ya 500 vimechapishwa na kuhifadhiwa katika hazina za Maktaba za Taifa huko Paris, Ufaransa na Berlin, Ujerumani. Wasomi wakuu wa Ulaya wanamwita bwana huyu: ‘Profesa wa Hekima’ na wanamhusisha kuwa mvumbuzi wa ‘element’ 19 na uzito wake (density) kila moja! Hiyo ni miaka ya 720 A.D! Ni ajabu kubwa! 93


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 94

katika Uislamu

Kusafisha madini na chuma, kutengeneza chuma, kutia rangi na kutengeneza rangi ni baadhi tu ya fani ambazo Waislamu walikuwa viongozi mapema. Walitengeneza kemikali za Nitric Acid, Sulphuric Acid, Nitro Glycerine, Hydrochloric Acid, Potassium, Aqua Ammonia, Swalamoniac, Silver Nitrate, Sulphuric Chloride, Potassium Nitrate, Alcohol na Alkali. Yote haya bado yanajulikana kwa majina yao ya kiarabu! Kwa mfano ‘Borax’ inatokana na neno la kiarabu ‘Buuraq.’ Ujuzi wa mvuke (distilling), kuchemsha (evaporation), kuchujua na matumizi ya Sodium Carbon, Potassium Carbonate, Chloride na Ammonia, yalikuwa ni kitu cha kawaida chini ya utawala wa Bani Abbas miaka hiyo ya 730 A.D. (148 A.H)!

Barabara za kisasa (Paved Roads): Bwana Philip Hitti anaandika katika kitabu chake cha ‘History of the Arabs’ kwamba katika nchi za kiarabu kama Cordova zilikuwa na barabara ndefu za kisasa zilizoangazwa na taa pande zake zote mbili kutoka majumba yanayopakana nazo ili watu watembee kwa usalama usiku. Wakati huo huko London na Paris mtu aliyejaribu kutembea barabarani usiku wa mvua, alilazimika kutumbukia katika matope hadi magotini, tena kwa karne saba ambapo Cordova ilikuwa na barabara za kisasa! Wakati huo pia watu wa Oxford - Uingereza walichukulia kitendo cha kuoga mwili kuwa ni cha kuabudu masanamu wakati ambapo wanafunzi huko Cordova walifaidika na kuoga katika bafu za jumuia (Public Hammams)!

Hisabati (Mathematics): Bwana Baron Carra de Vaux mwandishi wa makala ‘Astronomy’ and Mathematics’ katika ‘The legacy of Islam’ uk. 376-398, anaeleza kuwa neno ‘Algebra’ ni neno la Kilatini ambalo asili yake ni neno la kiarabu: ‘AlJabr’ neno lenye maana ya ‘kupunguza’ ambapo linahusiana na kuzichanganua hesabu ngumu na kuziweka katika lugha au maana nyepesi ya alama (symbols). Kwa uvumbuzi huo muhimu sana, dunia inalo deni kubwa kwa Waarabu (Uislamu). Zaidi ya hayo tarakimu tunazotumia sasa hivi kila siku, asili yake ni za kiarabu (Kiislam) kihistoria. Vile vile uvumbuzi wa ‘zero’ ndio msingi mkuu wa teknolojia ya kompyuta. Lakini neno 94


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 95

katika Uislamu

hilo ‘zero’ asili yake ni neno la kiarabu la ‘sefr.’ Neno ‘cipher’ ni mfano mwingine wa jitihada ya kuliweka neno ‘sefr’ katika lugha ya Ulaya! kiswahili tunaita sifuri. Kwa maelezo hayo yote na yaliyotangulia, bado tunazidi kuona kuwa, kwa kadri ya nyakati hizo za maendeleo ya elimu kwa Waislamu, yaani miaka ya 730 A.D, ni wakati ambapo Ulaya ilikuwa katika giza la ujinga (Dark Ages). Isitoshe tutaona kuwa Waarabu kabla ya Uislamu walikuwa pia katika giza nene la ujinga wa kiroho (spiritual ignorance) na ujinga wa kidunia. Ni baada ya Waarabu kuwa Waislamu ndipo walipopata elimu zote nilizozitaja. Kihistoria tutaona kuwa elimu hizo hazikuwepo katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Lakini tutaona maelezo mengi humu ambapo Mtume (s.a.w.w.) anasema kuwa yeye na Ahlul-Bayt (a.s.) wake ni kitu kimoja. Anakaririwa Imam Ja`far Sadiq (a.s.) akisema kuwa: “Awwaluna Muhammad. Awsatuna Muhammad. Aakhiruna Muhammad. Kulluna Muhammad.” Maana yake ni kwamba - Wa kwanza wetu ni Muhammad. Wa kati wetu ni Muhammad. Wa mwisho wetu ni Muhammad. Kila mmoja wetu ni Muhammad. Maana yake inahusu Maimamu 12 (a.s.) kwamba wote, pamoja na Mtume (s.a.w.w.) ni kitu kimoja kasoro tu kwamba baada ya Mtume (s.a.w.w.) hakuna tena Mtume wala ‘Wahyi.’ Nikifafanua zaidi ni kwamba elimu yote ya Mtume (s.a.w.w.) walibakia nayo Ahlul-Bayt (a.s.) wake, na ndio walioitoa kwa wafuasi wao kuanzia mwaka wa 11 A.H. hadi mwaka 255 A.H (834 A.D). Ushahidi wa ukweli huu nimeueleza katika sifa za Maimamu nilizozitoa nyuma na nitakazozitoa mbele. Kila elimu ina chanzo chake. Haiwezekani watu wakaipata elimu hivi hivi bila kuwepo wafundishaji wa elimu hiyo, tena enzi hizo za ujinga! Uvumbuzi wa teknolojia yoyote ile, unategemea sana elimu za awali za kuwezesha kutatua matatizo ya msingi, ili teknolojia hiyo iwe yenye kufaa na isiyo na matatizo. Kwa mfano nguvu za nyuklia zina manufaa kwa 95


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 96

katika Uislamu

binadamu lakini kuvumbua nyuklia bila kuwa na elimu ya kujikinga na miozi yake ya hatari, kusingewezesha binadamu kunufaika na nguvu za nyuklia. Nataka kuonyesha kuwa elimu mbali mbali za kisayansi ndizo zinazowezesha uvumbuzi wa teknolojia inayotakiwa. Utengenezaji wa ndege umepitia hatua nyingi za kisayansi kuwezesha ndege kuruka kwa usalama. Kama ndege ingeundwa hivi hivi bila kuzingatia elimu hizo, bila shaka isingeweza hata kuruka! Vile vile tufahamu kuwa utengenezaji wa ndege au gari hutumia vyuma na vifaa vyenye sifa mbali mbali, kwa mfano chuma kisichosagika upesi au chuma kisichopata joto upesi au chuma imara lakini chepesi au chuma kisichopata kutu. Vyote hivyo inabidi vivumbuliwe na kupimwa (kujaribiwa) kwanza, kabla havijatumika kutengeneza teknolojia inayotakiwa. Kwa hiyo ninaposema kuwa Uislamu ndio ulioleta maendeleo ya sayansi na teknolojia huko Ulaya, sina maana kuwa Waislamu siku hizo walikuwa na elimu ya kutengeneza magari, ndege na manowari au gari moshi. Maana yangu ni kwamba elimu hizo za kisayansi ziliendelezwa hadi kuwawezesha wazungu kufikia hapa walipo. Sababu kubwa iliyowafanya Waislamu kutoendeleza elimu hizo ni kuacha dini na kujali dunia tu; wakati ambapo Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa: “Itumikie dunia kama vile utaishi milele, na itumikie dini kama vile utakufa kesho.” Kama tutakavyoona katika kitabu hiki sura za mbele, baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.) uongozi halali wa Waislamu ulisukumwa pembeni na badala yake wakatawala watu wasiojali dini kabisa. Hali hiyo ni sawa na mifano mingi katika Qur’ani ambapo watu waliopita zamani, walivuka mipaka ya Mwenyezi Mungu na wakaangamizwa au wakateremshiwa adhabu mbalimbali. Adhabu waliyoteremshiwa Waislamu wa nyakati hizo, ni kwamba Uislamu ulishaenea sehemu kubwa ya Ulaya kwa maana ya ‘Dola ya kiislamu.’ Natumia maneno ya ‘Dola ya kiislamu’ kwa maana kwamba kilichoenea Ulaya siyo dini ya kweli ya Uislamu bali ni Himaya ya Kiarabu (Arab Empire) iliyojengwa kwa utamaduni wa kiislamu. Kwa kawaida utawala wa Himaya huzingatia maslahi ya kidunia na ndiyo 96


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 97

katika Uislamu

maana elimu za kiislamu (za kidunia) zilistawi sana. Kama tutakavyoona katika sura zifuatazo, Uislamu aliouleta Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ulitelekezwa pale alipofariki, na badala yake ukaanzishwa Uislamu usiozingatia misingi muhimu ya Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo Mwenyezi Mungu aliondoa baraka ya Uislamu na ndipo Vita vya Msalaba (miaka ya 1095 hadi 1270 A.D) vilipowaangamiza Waislamu kwa mamilioni. Vita hivyo vilivyojulikana kama ‘ The Crusades’ ambavyo kimsingi vilikuwa ni vita vya kuangamiza Uislamu, ambavyo vilianzishwa na kiongozi mkuu wa Ukristo na viongozi wenzake, viliwaua na kuwang’oa Waislamu kutoka Ulaya hadi Jerusalem. Historia ya vita vya msalaba na mauaji ya kikatili waliyofanyiwa Waislamu, ni ndefu sana na siyo lengo langu kueleza kirefu hapa. Matokeo yake ni kwamba wakati huo Wazungu walishafaidika na elimu za Waislamu na hivyo kutambua umuhimu wake kidunia. Waliendeleza elimu hizo kwa nguvu hadi baadaye zikawawezesha kupata maendeleo waliyonayo wakati huu. Kwa kuwa Wazungu hadi hivi leo wameweka mkazo zaidi kwenye maendeleo na starehe za dunia, Qur’ani inasema kuwa:

“Mwenye kupenda jaza ya akhera, tutamzidishia katika jaza hiyo; na mwenye kutaka jaza ya dunia tutampa, lakini huko akhera hatakuwa na sehemu (mapato) yoyote.” (Qur’ani 42:20). Kwa hiyo tutaona kuwa sisi tunaojiita Waislamu, tumewekwa hapa duniani siyo hasa kuifaidi dunia, bali kumwabudu Mwenyezi Mungu, (Qur’ani 51:56). Iwapo tutaweka mkazo kwenye dunia peke yake, ni makosa makubwa na siyo lengo kuu la Mwenyezi Mungu kutuumba na kutuweka duniani. Vitu vyote tunavyovitumia duniani katika kuboresha na kuende97


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 98

katika Uislamu

sha maisha yetu, vimekusudiwa na Mwenyezi Mungu kutusaidia kumwabudu ipasavyo, na siyo tuvitumie kumuasi au kuvifanya kuwa ndilo lengo kubwa la sisi kuwekwa duniani. Kwa kadri ya (Qur’ani 42:20) tofauti yetu na wazungu ni kwamba, sisi tunajiita Waislamu lakini tunashika dini nusu na tunaikumbatia dunia! Matokeo yake tunavikosa vyote! Sina maana kuwa tuiache dunia kabisa! Nina maana kuwa dunia inatufanya tushindwe kumwabudu Mwenyezi Mungu kikamilifu. Lakini wenzetu wazungu, moja kwa moja wamechagua dunia kwa hiyo Mwenyezi Mungu amesema kuwa atawapa kikamilifu! Sisi tunakosa baraka kamili ya Uislamu kwa sababu tumeshika dini nusu tu au tumeitelekeza yote hali ya kuwa bado tunapenda kujitambulisha kuwa ni Waislamu! Ndiyo maana tunaikosa dunia na pia tunakosa baraka za Uislamu. Maana yake ni kwamba hatutafaidi dunia kama wazungu na wala hatutaifaidi akhera, bali tutapata hasara kotekote. Ukichunguza historia ya Uislamu utaona kuwa kila Waislamu walipomwabudu na kumtegemea Mwenyezi Mungu kikamilifu bila unafiki, katika vita vya jihadi, walipata ushindi hata kama maadui zao walikuwa wengi kiasi gani! Kwa maana hiyo ni kwamba kama tungemwabudu Mwenyezi Mungu ipasavyo, hata hivyo Vita vya Msalaba visingefanikiwa kuwaangamiza Waislamu ingawa inasadikiwa jeshi hilo la Crusades lilikuwa na askari milioni moja! Katika kitabu hiki tutaona kuwa, haitoshi sisi kujiita Waislamu bila kudumisha Uislamu wa kweli mbele ya Mwenyezi Mungu. Tunaweza kujiita Waislamu hali ya kuwa Mwenyezi Mungu alikwishafuta majina yetu katika daftari la Waislamu! Imam Ja`far Sadiq (a.s.) alikaririwa akisema kuwa: “Kiwango cha chini sana cha dhambi ya Shirk (ambayo haina msamaha) ni kuanzisha tendo potofu la dini na kuwapenda wanaolifanya na kuwachukia wasiolifanya.� Tukirejea kwenye somo letu la msingi ni kwamba baada ya Himaya ya Waarabu kuanguka, Waislamu walipoteza karibu taasisi zote za elimu. Kuanzia hapo (1270 A.D) wazungu wakaendeleza elimu hizo ambazo 98


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 99

katika Uislamu

zilibadili kabisa sura ya Ulaya. Waislamu waliobakia katika nchi za Waislamu, waligawanywa na wakoloni katika nchi ndogo ndogo kama zilivyo wakati huu. Hali hiyo ilidhoofisha kabisa Waislamu kidini na kielimu mpaka leo. Hiyo ni siasa ya “wagawanye uwatawale.” Mnamo miaka ya 1800 hadi 1919 A.D Wazungu walikuwa wameshapiga hatua kubwa kielimu na hivyo kuvumbua teknolojia nyingi mpya zilizoubadili ulimwengu: (1) Injini ya mvuke (Fulton’s first steam boat) mwaka 1803 A.D (1224 A.H). (2) Uchapishaji vitabu (Power Printing Press) mwaka 1811 A.D (1232 A.H). (3) Gari moshi (Steam Train) 1825 A.D (1246 A.H). (4) Mashine za kuvunia (Mower & Reaper) 1831 A.D (1252 A.H) (5) Simu ya waya ( Electric Telegraph) 1836 A.D. (1257 A.H) (6) Upigaji picha (Photography) 1839 A.D (1260 A.H) (7) Cherehani (Sewing Machine) 1846 A.D (1267 A.H) (8) Chuma (Bessemer Steel) 1856 A.D- (1277 A.H) (9) Typewriter 1864 A.D (1285 A.H) (10) Simu (Telephone) 1876 A.D - (1297 A.H) (11) Reli ya Umeme - 1879 AD- (1300 A.H (12) Injini ya Gari - 1883 A.D - (1304 A.H) (13) Gari - 1892 A.D - (1313 A.H) (14) Sinema - 1893 A.D - (1314 A.H) (15) X- Ray - 1895 A.D - (1316 A.H) (16) Wireless Telephone - 1902 A.D - (1323 A.H) (17) Ndege yenye rubani - 1903 A.D - (1324 A.H) (18) Radio - 1920 A.D - (1341 A.H) (19) Televisheni - 1936 A.D - (1357 A.H) (20) Chanjo ya Polio - 1953 A.D. - (1374 A.H) (21) Binadamu kutua mwezini - 1961 A.D. Hata hivyo tutambue kwamba siyo uvumbuzi wote umetokana na elimu 99


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 100

katika Uislamu

peke yake! Baadhi ya uvumbuzi (inventions) ni baraka ya Mwenyezi Mungu kwa binadamu, kwa mfano: Simu ya upepo (Telegraph) - Ilivumbuliwa na mchora picha (Portraits Painter) ambaye hakuwa na elimu yoyote inayohusiana na uvumbuzi huo! Jina la mvumbuzi huyo ni Morse! Boti ya Mvuke - Ilivumbuliwa na Fulton ambaye alikuwa mchora picha za jumla na hakuwa na ujuzi wowote wa kisayansi! Mtambo wa kuchambua pamba - Ulivumbuliwa na mwalimu wa kawaida wa shule ambaye hakuwa na ujuzi wa fani hiyo! Mota za umeme (Electromagnet) - Ilivumbuliwa na Thomas Davenport ambaye alikuwa fundi chuma (blacksmith) asiye na ujuzi wowote wa umeme au sayansi yoyote! Ushahidi zaidi kwamba sayansi na tekinolojia vimeletwa na Waislamu: Tumeona kuwa huko Ulaya uvumbuzi mkubwa wa Sayansi na teknolojia za kisasa ulianzia miaka ya 1800 A.D. Lakini kumbukumbu za historia zinaonyesha kuwa Wanasayansi wa kiislamu walikwishavumbua elimu nyingi mapema zaidi kabla ya hapo kama ifuatavyo:

(1) Abdul-Walid Muhammad Ibn Rushd Huyu anajulikana kama Averroes huko Ulaya. Aliishi miaka – ya 1198 A.D na anajulikana kama Mshereheshaji (Commentator) Mkuu wa ‘Falsafa ya Aristotle.’ Anachukuliwa kuwa mmoja wa Wanafalsafa wakuu wa karne ya 12 ambao walitawala mawazo ya watu wa Ulaya mpaka karne ya 16. Katika falsafa aliandika sharh (commentaries) tatu juu ya Aristotle, ambazo ziliathiri falsafa ya Wakristo na Wayahudi wa miaka ya 1100-1400 A.D. Katika elimu ya dini alilinganisha imani na mantiki (logic) na alikuwa na athari kubwa kwa St. Thomas Aquinas - mmoja wa wanafalsafa 100


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 101

katika Uislamu

wakuu wa Kikristo. Katika tiba, kitabu chake maarufu ni Was-al-Kulliyyat fit Tibb ambacho kilielezea juu ya dawa mbali mbali, kutambua magonjwa, tiba na kinga.

(2) Abu Husein Ibn Al-Haitham Huyu aliishi miaka ya 1040 A.D na alijulikana kama Alhazen huko Ulaya. Alikuwa mhandisi na mwanasayansi. Katika safari yake huko Misri kujifunza juu ya mto Nile, alipendekeza kujengwa bwawa pale Aswan ili kuhifadhi maji ya mafuriko yatumike baadaye wakati wa ukame. Pendekezo hilo lilifanikishwa karne ya 20! Mwanasayansi huyu alifanya majaribio mengi kuhusu kusafiri (propagation) kwa mwanga na rangi. Vile vile alichunguza miali katika mazingira tofauti. Alifanya majaribio ya kwanza ya kutawanya mwanga ili kutenganisha na kubainisha rangi zake tofauti. Alitofautiana na nadharia ya awali ya Plotemy na Euclid juu ya jinsi macho yanavyoona vitu. Nadharia yao hawa wanasayansi wawili, waliamini kuwa macho hutoa miali ya mwanga. Lakini yeye, Alhazen, alithibitisha kwa usahihi kwamba, miali ya mwanga hutoka katika vitu vinavyotazamwa kwa macho. Kwa hiyo huyu Alhazen anajulikana kama baba wa taaluma ya macho na mwanga (optics). Katika maandishi yake utaona jinsi alivyobainisha taratibu za kisayansi za uchambuzi wa mambo, taratibu ambazo ziliendelezwa na kutumiwa na wanasayansi wa kiislamu. Utaratibu huu ulikuwa ni changamoto katika taratibu za kisayansi ambazo zimejengeka juu ya uchunguzi wa jambo au wazo kwa kadri ya ukweli uliopo wa kisayansi (hypothesis), na mwisho kuthibitisha hoja inayohusika.

(3) Thabit Ibn Qurrah Huyu aliishi mnamo miaka ya 901 A.D na alijulikana kwa jina la Thebit huko Ulaya. Katika fani ya Hisabati alivumbua ‘Aljebra ya jiometri’ ambayo iliwezesha uendelezaji wa ‘jiometria kinyume na ile ya Euclid’, 101


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 102

katika Uislamu

‘trigonometria ya duara’ ‘kalklas rejeo’ na ‘namba halisi’. Katika fani ya ‘mechanics’ ambayo inahusiana na uchunguzi wa mwendo wa vitu na jinsi vitu hivyo vinavyoendesheka kwa misukumo. Anatambuliwa kama baba wa ‘statics’ ambayo ni fani ya makaniki ya mlingano wa vitu visivyosogea, mihimili na nyenzo (Equilibrium mechanics of stationery bodies, beams and levers). Fani hii ni muhimu sana kwa teknolojia ya ujenzi wa nyumba za aina zote hasa maghorofa na madaraja. Katika fani ya ‘Falaki’ alikosoa mawazo au maoni ya Ptolemy. Alitafakari matatizo kadhaa juu ya mwendo wa jua na mwezi. Kwenye uso wa mwezi kuna tambarare ya mviringo yenye kipenyo (diameter) cha maili 30, ambayo imepewa jina lake kwa mchango wake wa kisayansi. Alifasiri katika kiarabu elimu (maandishi) za Kigiriki kama zile za Plotemy: ‘AlMagest’ na za Euclid: ‘Elements of Geometry’ na baadhi ya kazi za Archimedes.

(4) Abu Ali Al-Husein Ibn Abdullah Ibn Sina Huyu aliishi miaka ya 1037 AD na alijulikana kwa jina la Avicenna huko Ulaya. Alikuwa mjuzi sana katika tiba (medicine), Sayansi, Falaki, Sheria, Muziki, Ushairi, Falsafa na Saikolojia. Alibobea katika Hisabati ambayo alijifunza chini ya Al-Khawarizmi. Kitabu chake cha rejea cha tiba, AlQanun fiyt Tibb (The Canon in Medicine) kilikuwa kikubwa kuliko vyote katika fani ya tiba, kikiwa na zaidi ya maneno millioni moja na kilibakia kikiongoza duniani katika fani hiyo mpaka karne ya 19! Siyo tu katika ulimwengu wa kiislamu, bali pia kilisomwa katika vyuo vikuu vya Ulaya. Ibn Sina alitambua (diagnosed) kansa na alitumia upasuaji (surgical operations) na kuiondoa kutoka kwa wagonjwa. Alihusisha vidonda vya tumbo kusababishwa na athari za mawazo (psychological effects) kama wasiwasi na majonzi pamoja na matatizo yenye madhara tumboni. Alihusisha maradhi na vijidudu vilivyosambazwa hewani na wagonjwa, yaani ‘bakte-

102


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 103

katika Uislamu

ria’. Elimu hiyo ilipelekea matumizi ya karantini ili kudhibiti ueneaji wa magonjwa ya kuambukiza. Kazi yake nyingine ilikuwa ni kitabu chake maarufu: Kitabu-Shifaa (The Book of Healing) ambacho kilikuwa ensaiklopidia ya kifalsafa. Kwa Ibn Sina, Falsafa ilikuwa ni msingi wake mkuu na njia sahihi ya kumwelewa Mwenyezi Mungu na Maumbile.

(5) Abu Abdullah Al-Battani Huyu aliishi miaka ya 929 A.D na anajulikana huko Ulaya kama AlBategnius. Anasifiwa kuwa bingwa wa enzi zake katika fani ya Falaki, yaani elimu ya nyota. Mchango wake katika fani hii ni pamoja na hesabu zake sahihi za njia (orbits) za mwezi na sayari nyinginezo. Kwa uwezo wake alibuni kwa ustadi sana njia za kuwezesha kuonekana mwezi mpya wa kiislamu. Alithibitisha uwezekano wa kupatwa mwezi hali ya kuwa mwanga wa jua umezunguka mwezi kama pete (annular solar eclipse) pamoja na kupatwa kabisa kwa mwezi au jua (total eclipse). Alifanya ukokotoaji wa hesabu sahihi ya urefu wa mwaka (solar year) kuwa ni siku 365, saa 5, dakika 48 na sekunde 24! Katika uso wa mwezi kuna tambarare yenye kipenyo (diameter) cha maili 80, ambayo imepewa jina lake. Aliandika vitabu vingi juu ya ‘Trigonometria’ ambayo ni tawi la Hisabati. Matumizi ya mwanzo ya fani hii yalikuwa ni katika unahodha wa meli baharini, upimaji (surveying) na Falaki, hasa katika upimaji urefu ambao hauwezi kupimwa moja kwa moja na futi kamba. Waislamu walitumia elimu hii ili kupata mwelekeo wa Kibla yaani huko Makka kwenye AlKaaba tunakopaswa kuelekea wakati wa kuswali.

(6) Abbas Ibn Firnas Simulizi za kale zimejaa kumbukumbu za majaribio ya usafiri angani. Wanafalsafa waliamini kuwa suala hili linawezekana kwa kuigiza mwenendo wa mabawa ya ndege anayeruka angani; au kwa kutumia moshi au kitu chepesi kuliko hewa. Historia imeweka kumbukumbu kwamba katika mwaka 861 A.D Abbas Ibn Firnas, mwanasayansi wa kiarabu, alifanya 103


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 104

katika Uislamu

majaribio juu ya suala hili. Alifika Cordoba kufundisha muziki, kisha nadharia ya tawi mojawapo la Hisabati. Muda si mrefu alipata shauku katika mbinu (mechanics) ya kupaa angani. Alijenga jozi moja ya mabawa kwa kutumia manyoya ya ndege kwenye fremu ya mbao, na akajaribu kuruka akimuigiza ‘Leonardo da Vinci’ miaka 600 iliyopita. Kwa bahati Abbas alinusurika. Katika sayansi ya uvumbuzi wa vitu, msingi wa kwanza ni kuleta wazo ambalo hufanyiwa kazi kwa kadri ya taarifa sahihi za kisayansi zilizopo. Kwa hiyo wazo la kuruka angani liliendelezwa kupitia hatua ngumu mbali mbali kwa miaka mingi iliyofuatia baada ya Abbas Ibn Firnas kufariki mwaka 888 A.D.

(7) Jabir Ibn Hayyan Huyu alikuwa mchangayaji dawa za tiba (Pharmacist) na madawa ya kemikali (Chemist). Anajulikana Ulaya kama Geber. Aliandika zaidi ya vitabu 200 kukiwemo vitabu 80 juu ya Kemia. Tafsiri za kazi zake zilikuwa maarufu huko Ulaya kwa karne nyingi na hivyo kuathiri kemia ya kisasa. Msamiati wa maneno ya kemia yaliyoletwa na Jabir kama ‘alkali’, yanapatikana katika lugha kadhaa za Ulaya na ni sehemu ya msamiati wa kisayansi. Alipendekeza kujengwa maabara ya kemikali mbali na makazi ya binadamu ili kuepusha watu na madhara ya athari za uchafu wa kemikali. Alikuwa baba wa kemia ya molekuli na alitambua kwa usahihi jinsi ‘elementi’ zinavyoungana katika ngazi ya ‘molekuli’ ili kuunda ‘kompaundi’ mpya bila kupoteza umbile (structure) lao halisi! Kulipita karne 10 kabla ya John Dalton ‘kuvumbua’ kitu kile kile! Alikuwa bingwa mwanzilishi (pioneer) wa matumizi ya mfanyiko tendani wa kemikali ‘applied chemical processes’, taaluma ambayo ilipelekea katika kuendeleza: (a) Chuma (steel) (b) Aina tofauti za chuma (c) Kuzuia kutu (d) Kuandika herufi za dhahabu (e) Kutumika manganese dioxide katika kutengeneza kioo. (f) Kutia rangi nguo (dyeing) (g) Turubai (Varnishing zisizo ingia maji.) (h) 104


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 105

katika Uislamu

Aina za rangi na ‘grisi’.

(8) Abu Rahman Muhammad Al-Biruni Huyu ni mmoja wa wanachuoni maarufu wa kiislamu, wa nyakati za ustawi wa sanaa (Golden Age) za sayansi za kiislamu. Kwa elimu yake amechangia katika fani ya elimu ya nyota (falaki), Fizikia, Hisabati na elimu ya Jeologia. Katika Falaki alielezea njia saba tofauti za kupata Kaskazini na Kusini. Alivumbua vifaa vichache vya falaki. Alifanya hesabu sahihi za ‘longitudo’ na ‘latitudo’. Alieleza jinsi ambavyo kasi ya mwanga ni zaidi ya mwendo wa sauti na kwamba anga ya sayari ina mkusanyiko wa vipande vya nyota visivyo na hesabu. Alitumia mizani na kupata uzito wa ‘elementi’ na ‘kompaundi’ 18. Katika Hisabati alianzisha elimu ya pembe, pembe tatu na mitambuko ya duara, ‘chords of circles’ na alijadili tarakimu za Kihindi. Katika elimu ya miamba na madini (Jiologia) alichunguza milipuko ya volkano, sayansi ya kupata na kuchanganya madini ya chuma (metallurgy) na elimu ya kuunganisha mikondo ya chemchem za asili na visima virefu vya maji.

(9) Muhammad Ibn Muhammad Ibn Abdallah Ibn Idrisi (1099 1166 AD) Anajulikana kama mwana jiografia mkuu wa Zama za Kati. Jina lake maarufu huko Ulaya ni Dreses. Alisafiri sehemu nyingi za mbali pamoja na Ulaya ili kukusanya kumbukumbu (data) muhimu. Wanasayansi wa kiislamu katika fani hii walishafanya vipimo sahihi vya sura ya uso wa dunia na ramani za dunia. Nyakati ambazo jitihada za Ulaya za kutengeneza ramani zilishasimama, Muhammad alikaribishwa na mfalme wa Sicily, Roger wa Pili, kutengeneza ramani mpya ya ulimwengu. Idrisi alitengeneza ‘Tufe la fedha la kilo 400’ na kurekodi hapo makontinenti saba pamoja na njia za biashara, maziwa, mito, miji mikubwa, tambare, milima pamoja na urefu wa mwendo, na urefu wa muinuko toka usawa wa bahari (altitudo). Tafsiri ya kazi zake katika lugha ya Kilatini ilikuwa ni rejea maarufu na ‘ensaiklopedia’ kwa karne nyingi huko Ulaya pamoja na ramani aliyotu105


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 106

katika Uislamu

mia Christopher Columbus.

Kwa nini Hatusikii Majina ya Wanasayansi Maarufu wa Kiislamu?: Nimetangulia kueleza katika somo hili kwamba Vita vya Msalaba (Crusades) vililenga kung’oa Uislamu huko Ulaya na vilifanikiwa. Baada ya hapo zilifanyika jitihada za kufuta kila alama ya Uislamu iliyobakia ili Uislamu usionekane kama dini inayokubalika kwa watu. Majina halisi ya wanasayansi wa kiislamu tumeona yalivyobadilishwa yawe kama ya kizungu ili yasiambatanishwe na Uislamu. Lakini historia haipotei! Rejea: Muslim Scientists - The Fathers of Modern Technology - Hijr Calendar, 1420 A.H. (1999 A.D.) by: Tabligh Sub Committee, K.S.I. Jamaat, Dar es salaam, Tanzania. Hadi hapa tumeona kuwa elimu kubwa waliyokuwa nayo Waislamu ilitokana na Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) na wala haikuja kwa miujiza. Sasa tuone sifa za peke yake walizokuwanazo Ahlul-Bayt (a.s.), mbali na uwezo wao mkubwa wa elimu. Tukumbuke kuwa hata ‘Masharifu’ wasio Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) bado mpaka leo wanaonyesha karama (miujiza) zao!

Sifa za Pekee za Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.): Lazima awe na elimu ya kuzaliwa nayo na awe mjuzi kuliko watu wa kawaida wa wakati wake. Awe kiongozi na mwamuzi wa watu wote iwapo ni Imam. Awe mwenye subira kuliko watu wote wa wakati wake. Awe mcha Mungu zaidi kuliko watu wote wa wakati wake. Awe shujaa kuliko watu wote. Awe mkarimu kuliko wote. Akizaliwa awe tayari katahiriwa kama ni mwanaume. Huwa ana uwezo wa kuona nyuma yake kama anavyoona mbele yake wakati huo huo bila kugeuka. 106


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 107

katika Uislamu

Mwili wake hauna kivuli (kama Mtume). Akizaliwa hapo hapo huweka mikono yake (viganja) ardhini (sakafuni) na kutoa Shahada. Hapati ndoto chafu Hata akiwa amelala huwa macho kifahamu. Malaika huja kumwamkia na kuzungumza naye. Deraya ya Mtume (s.a.w.w.) humtosha sawa sawa kama ni Imam. Mkojo au kinyesi chake hakionekani na mtu yeyote. Humezwa na ardhi na hakuna harufu mbaya bali hutoa harufu ya ambari na maski. Hudhibiti maisha ya watu kwa hukumu za dini. Huwa na huruma kwa watu kuliko wazazi wao. Huwa mnyenyekevu mno katika Swala zake na ibada za Mwenyezi Mungu. Dua zake zote hukubaliwa na Mwenyezi Mungu mara moja (papo hapo). Huwa ni mwenye kumiliki deraya ya Mtume (s.a.w.w.) na upanga wake (Dhulfikar). Huwa na daftari ya orodha ya wafuasi wake wote pamoja na watakaozal wa hadi Siku ya Kiyama. Huwa na kitabu cha orodha ya maadui zake wote. Huwa na ‘Jamiah’ yenye urefu wa yadi 70 ambamo kuna maelezo kamili kuhusu mambo ya dunia. Huwa na nyaraka kubwa iitwayo Jafar kuu, na nyaraka ndogo iitwayo Jafar Ndogo, ambazo zinaeleza kanuni zote za kidini hata jambo dogo sana kama vile hukumu ya mtu aliyemchoma mwenzie kwa ukucha. Huwa na Kitabu alichorithishwa toka kwa Bibi Fatima (a.s.) Binti yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa kadri ya Itikadi ya Shia Ithna’asheri, mtu hawezi kuwa Imam bila kuwa na sifa hizo. Kwa hakika sifa kama hizo aweza kuwa nazo mtu yule 107


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 108

katika Uislamu

tu anayeongozwa na Mwenyezi Mungu wakati wote (Qur’ani 33:33). Umuhimu wake ni kwamba Kiongozi asiyeongozwa na Mwenyezi Mungu anaweza kuvuka mipaka na kufanya vitendo vinavyopingana na uadilifu na matakwa ya Mwenyezi Mungu. Vitendo hivyo nitavieleza wazi zaidi katika Sura za mbele. Mpaka hapa tumejadili kwa kirefu hoja ya Shia Ithna’asheri kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia ulio wazi, tena katika matukio mbali mbali, kuhusu uongozi wa Waislamu nyuma yake. Kutokana na uzito wa hotuba hiyo ya Mtume (s.a.w.w.), nimeona ni muhimu sana niitoe yote hapa pamoja na idadi (asnad) ya masahaba walioipokea, ili Waislamu waifuate au waikatae. Narudia kusisitiza kwamba kama Waislamu tungeamua kuwa waaminifu na tukaifuata kikamilifu, tusingekuwa na migawanyiko na mifarakano ya madhehebu, bali tungekuwa kitu kimoja tukiongozwa na itikadi sahihi za Uislamu.

HOTUBA (WASIA) KAMILI YA MTUME (s.a.w.w.) PALE GHADIR KHUM NA USHAHIDI KAMILI WA TUKIO HILO Iwapo Waislamu wangepokea wasia huu, pasingekuwepo haja ya kuandika kitabu hiki. Maelezo mengi yaliyomo katika kitabu hiki, ni ushahidi wa kuonyesha jinsi ambavyo Waislamu walio wengi walivyokataa kutii wasia huo wa Mtume (s.a.w.w.) kwa makusudi! Mwislamu yeyote mwaminifu baada ya kusoma wasia huu, hana haja ya kutafuta ushahidi mwingine zaidi. Na iwapo Mwislamu yeyote akipokea wasia huu, moja kwa moja atakuwa mfuasi wa Imam Ali (a.s.)! Na bila shaka huo ndio Uislamu aliotuachia Mtume (s.a.w.w.). Kwa nini Waislamu tunakuwa wazito kutambua ukweli huu? Hotuba hiyo ifuatayo imetolewa kutoka kitabu Ihtijaji Tabrasi, na imefasiriwa na bwana Abeid Kingazi wa huko Tanga: “Kwa jina la Allah, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Shukrani zote zamstahiki Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika umoja wake Aliye karibu na Upweke Wake, na akatakasika katika Uongozi Wake. Ametukuka kwa 108


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 109

katika Uislamu

kila jambo kwa kujua kila kitu, naye yuko kwenye heshima Yake. Akavitawala viumbe vyote kwa uwezo Wake mkuu na kwa karipio lake lenye nguvu. Daima Ametukuka kwa sifa zisizobadilika, Muumbaji wa mbingu, Mkunjuaji (riziki) wa watoaji, Mshindi ardhini na mbinguni, Mwenye kusifiwa, kutukuzwa, Mola wa Malaika na Ruh (Jibril). “Mbora wa wote wenye kumtakasia, ni wa milele kwa kila alichokiumba. Huona kila jicho la kiumbe, lakini wao hawamwoni, ni Mkarimu, Mpole na mwenye subira. Ameeneza rehema Zake juu ya kila kitu, kisha akawaneemesha kwa neema Zake, haharakishi kuwaadhibu na wala hawashtukizi kwa adhabu zake wanazostahiki, kwani anajua yale ya siri na pia ya dhahiri (nia) yaliyostiriwa, hakanganywi na mambo, na ni mjuzi. “Amekizingira na kukitawala kila kitu, Naye hafananishwi na chochote, kwa sababu ni Muumbaji wa ambavyo havikuwepo, ni wa milele kwa uadilifu, Hapana Mola wa haki isipokuwa Yeye Mtukufu, Mwenye hekima, Aliyetakasika kiasi cha kutodirikiwa na macho, Lakini Yeye huyadiriki, ni Mpole na Mjuzi, hasifiwi yeyote kwa sifa zake kwa kuwepo Kwake, na wala hakuna anayejua mambo Yake ya siri na ya dhahiri isipokuwa kwa yale (baadhi) aliyojulisha Mwenyewe. “Na ninakiri kwamba ni Yeye tu ndiye aliyezijaza dahari (zama) Utukufu Wake, na ni Yeye ambaye nuru Yake imeenea daima. Hupitisha uamuzi Wake bila ya Ushauri wa mshauri; kwani hana mshirika katika kupanga, wala hakuna tofauti katika mfumo alioumba viumbe bila ya mfano (wao), kisha akaumba alivyoumba bila ya kuhitaji msaada wa yeyote, bila ya taabu, wala mbinu za kuanzia ili viwe. Akaviumba navyo vikaumbika. “Basi Huyo ndiye Allah ambaye hapana wa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, Hakimu wa ulimwengu, Msanii wa kuumba, Mwadilifu asiyedhulumu, Mkarimu ambaye Kwake tu ndiyo marejeo ya mambo. “Nakiri kwamba Yeye ndiye ambaye vitu vyote vimenyenyekea uwezo Wake, na vikakiri kwa heshima Yake, Mmilikaji wa sayari, na akavitiisha 109


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 110

katika Uislamu

jua na mwezi, vikawa vinapishana kwa muda maalumu, huufunika usiku juu ya mchana na akaufunika mchana juu ya usiku, hufuatilia kwa haraka! Ni mshindi kwa kila jabari (mwenye kiburi) na mkaidi, Mwangamizaji wa kila mfuata shetani muasi. Hana pingamizi wala mwenzi, yuko peke yake, anayetegemewa kwa kila kitu, hakuzaa wala hakuzaliwa, wala hafanani na chochote. “Ni Mungu mmoja na Mlezi, Mtukufu kwa atakalo na kulitekeleza, anajua na kudhibiti, anafisha na kuhuisha, hufukarisha na kutajirisha, hufurahisha na kuhuzunisha, hujongeza na kusogeza, hunyima na kutoa - kwani ni Wake Ufalme na sifa. Heri zote zatoka Kwake, naye ni Muweza juu ya kila kitu. Huufunika usiku juu ya mchana na mchana juu ya usiku. Hapana Mola isipokuwa Yeye, Aliyetukuka, Mwingi wa kusamehe, anayejibu maombi, Mwingi wa kutoa, Huzidhibiti nafsi (baada ya mauti), naye ni Bwana wa majini na watu. Hatingwi na chochote wala hakerwi na vilio vya wenye kutaabika na msisitizo wa waombaji. Ni mhifadhi wa watu wema, na Mlinganifu wa wenye kufuzu, Bwana wa walimwengu, anayestahiki shukrani toka kwa kila kiumbe chake, katika fanaka au matatizo, katika shida na raha. “Namwamini Yeye pamoja na Malaika Zake, vitabu Vyake na Mitume Yake. Ninazisikiliza na kuzitii amri Zake, ninaharakisha kila linalomridhisha. Na ninasalimu amri kutokana na makadirio Yake huku nikiridhia kumtii, na pia nikichelea kamio Lake; kwani Yeye ni Allah ambaye hazishindwi hila Zake, wala ujabari Wake haukabiliwi na tishio! Hivyo najiangusha Kwake kwa nafsi yangu nikiwa ni mja wake, nikiukiri Uungu Wake na kutekeleza kwa yale aliyonifunulia; kwa tahadhari nisije nikateleza hadi nikatengwa naye kwa masafa kwamba hatapatikana yeyote wa kuniokoa zitakaposhadidi hila Zake. “Hapana Mola wa haki ila Yeye, kwani amenifunulia kwamba nisipofikisha yale niliyoteremshiwa, basi sikufikisha ujumbe Wake. Kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amenichukulia dhamana ya ulinzi , Amenifunulia akisema: 110


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 111

katika Uislamu

“Kwa Jina la Allah Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu, Ewe Mtume, fikisha uliyoteremshiwa toka kwa Mola wako. (yaani kuhusu ukhalifa wa Ali bin Abu Talib) Na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda na watu...............” (Qur’ani 5:67). “Enyi watu! Sikupunguza katika kufikisha niliyoteremshiwa, nami ninawabainishieni sababu ya Aya hii, kwamba Jibril alinijia mara tatu, akiniamrisha kutokana na ujumbe wa Mola wangu (Qur’ani 5:67): nao ni ujumbe wa kuufikisha mahali hapa. Hivyo ninamfahamisha kila mweupe na kila mweusi; kwamba (huyu) Ali Ibn Abi Talib ni ndugu yangu, wasii wangu, khalifa (mshika makamu) wangu na Imam (kiongozi) baada yangu, na kwamba cheo chake baada yangu ni sawa na kile cha Harun kwa Musa isipokuwa tofauti ni kwamba hakuna Nabii baada yangu. “Naye ni kiongozi wenu baada ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, kwani kwa hayo nimeteremshiwa Aya na Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwenye kitabu chake:

“Hakika Kiongozi wenu ni Allah na Mtume wake na waliomini ambao husimamisha swala, na hutoa Zaka na hali ya kuwa wamerukuu.” (Qur’ani 5:55). “Na Ali Ibn Abi Talib alisimamisha Swala, akatoa Zaka huku akiwa amerukuu, akimkusudia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) katika hali zote. “Nami nimemwomba Jibril anisamehe nisiwafikishieni hilo enyi watu kwa kujua kwangu uchache wa wacha Mungu (kati yenu), wingi wa wanafiki, khiana za waovu pamoja na njama za wadanganyifu katika Uislamu, wote aliowataja Mwenyezi Mungu kwenye kitabu chake. Kwamba wao wanasema tu yaliyomo kwenye ndimi zao, na hayamo nyoyoni mwao, na wakid111


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 112

katika Uislamu

hani hayo kuwa ni madogo lakini ni makubwa kwa Mwenyezi Mungu. “Na pia waliponiudhi si mara moja, hadi ikafikia kuniita Sikio, wakidai niko hivyo. Kwa ajili ya kutangamana naye na kumwelekea sana, hadi Mwenyezi Mungu akateremsha Aya kwenye Qur’ani:

“Na miongoni mwao wako (wanafiki) wanaomuudhi Mtume na kusema: Yeye ni sikio tu. Sema; Sikio la heri kwenu” (Qur’ani 9:61). “Lau ningalitaka kuwaita (kwa majina ya kukebehi) ningelifanya hivyo au kuwaonyesha wajionee wenyewe; au kuwajulisha kwa watu, basi ningefanya lakini Wallah, kwa mambo yao hayo nimefanya staha, na yote hayo Mwenyezi Mungu hapendi niyafanye ila tu nifikishe lile aliloniamrisha. Kisha baada ya hapo (Jibril) akanisomea Aya:

“Ewe Mtume, fikisha uliyoteremshiwa toka kwa Mola wako, na kama hutafanya basi hukufikisha ujumbe Wake. Na Allah atakulinda na watu .” (Qur’ani 5:67). “Jueni enyi watu! Mwenyezi Mungu amemhusisha (Ali) kwenu awe kiongozi na Imam; akalazimisha atiiwe na Muhajirina na Ansari pamoja na wale wote, waliowafuatia wao kwa wema, na pia (akalazimisha) kwa walio mbali na waliopo hapa, Waarabu na wasio Waarabu, waungwana na watwana, wadogo na wakubwa, weupe na weusi. “Na ni juu ya kila mcha Mungu kutekeleza hukumu yake na kupitisha usemi wake. Basi amelaanika yule atakayempinga, atarehemewa kila atakayemfuata, na atakuwa Muumin yule atakayemsadikisha, Mwenyezi Mungu amsamehe huyo na kila mwenye kumsikia na kumtii. “Enyi watu! Hakika hii ni fursa ya mwisho kuipata mahali hapa, hivyo sik112


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 113

katika Uislamu

ilizeni, tiini na mzingatie amri ya Mola wenu, kwani Yeye ndiye Mlezi wenu, Kiongozi wenu, (wa haki), kisha baada ya yeye ni Mtume wake Muhammad, kiongozi wenu mliye naye sasa akiwahutubia, kisha baada yangu mtakuwa naye Ali, Kiongozi na Imam wenu kwa amri ya Mola wenu, kisha baada yake watakuwepo Maimamu (viongozi) kutokana na kizazi (Ahlul-Bayt) changu katika uzao wake (Ali) hadi siku ya Kiyama, hapo mtamkabili Mwenyezi Mungu na Mtume Wake. “Hakuna halali isipokuwa ile aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu, na hakuna haramu isipokuwa ile aliyoharamisha; kwani ameshanifahamisha ya halali na ya haramu, nami natangaza hayo na yale aliyonifundisha Mola wangu kwenye Kitabu Chake, na kutokana na ya halali na ya haramu Kwake. “Enyi watu! Kila elimu Mwenyezi Mungu ameidhibiti kwangu, na kila elimu niliyopewa, basi nimemnukulia Ali, kiongozi wa wacha Mungu na hakuna elimu ila nimekwisha mfundisha, naye ni kiongozi anayepambanua kati ya haki na batili. “Enyi watu! Msijitenge naye wala msimtoroke, na wala msiwe wapinzani kwa uongozi wake; kwani ndiye aongozaye kuielekea haki na huku akiitekeleza, anayeondoa batili na kuikataza, kwani kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, haimuathiri lawama ya mwenye kumlaumu, kisha yeye ni wa mwanzo kumwamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake kwa sababu hakuna yeyote miongoni mwa wanaume aliyemwabudu Mwenyezi Mungu akiwa pamoja na Mtume Wake isipokuwa yeye Ali. Enyi watu! Mtukuzeni na kumkubali; kwani Mwenyezi Mungu amemchagua. “Enyi watu! Hakika yeye ni kiongozi aliyeteuliwa na Mwenyezi Mungu na kamwe Mwenyezi Mungu hatakubalia toba ya yeyote anayekanusha uongozi wake; na wala hatasamehewa!

113


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 114

katika Uislamu

“Ni juu ya Mwenyezi Mungu kufanya hivyo kwa yeyote atakayekhalifu agizo lake linalomhusu Ali. Na kwamba atamwadhibu adhabu kali iumizayo daima milele, na atakaa (humo) milele. Hivyo jihadharini msije mkamwasi, matokeo ya kuingia moto ambao kuni zake ni watu na mawe; wameandaliwa makafiri. “Enyi watu! Wallah wamenitolea habari zangu manabii na Mitume (Mursali) wa mwanzo, nami ni mwisho wao, na hoja kwa viumbe wote wa mbinguni na ardhini. Yeyote anayetia shaka kwa agizo hili, huyu ni kafiri tena ukafiri wa ujahiliya wa mwanzo! Na anayeshuku juu ya usemi wangu huu, basi huyo anayashuku yote kutoka Kwake (Mwenyezi Mungu), na huyo ataingia motoni. “Enyi watu! Mwenyezi Mungu amenipendelea kwa fadhila hii ikiwa kama neema na ihsani toka Kwake. Na hapana Mungu mwabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye, shukrani zote ni Zake daima milele katika hali zote. “Enyi watu! Mtukuzeni Ali, kwa wanawake na wanaume, kwani yeye ni mbora wa watu baada yangu, na ni kwa ajili yetu Mwenyezi Mungu huruzuku (viumbe) na watu watabakia katika hali ya uasi, kulaaniwa, kughadhabikiwa na kukhasirika, iwapo tu watakana kauli yangu hii, japo wasikubaliane nayo. Isipokuwa ni kwamba, Jibril amenifahamisha hayo toka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akisema: ‘Mwenye kumfanyia uadui Ali, kisha asimfanye kuwa kiongozi wake, basi huyo atapata laana Yangu.’ Na kila mtu aangalie anayoyatanguliza (miongoni mwa amali) kwa ajili ya kesho, na mcheni Mwenyezi Mungu msije mkamkhalifu, miguu yenu ikateleza baada ya kwamba ilikuwa imethibiti, kwani hakika ya Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yale mnayoyafanya. “Enyi watu! Kwa hakika ni upande (haki) wa Mwenyezi Mungu alioutaja kwenye kitabu chake, aliposema: Isije ikasema nafsi ee majuto yangu kwa yale niliyopunguza upande wa Allah..... (Qur’ani 39:56)

114


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 115

katika Uislamu

“Enyi watu! Izingatieni Qur’ani na zifahamuni Aya zake, na zingatieni zile Aya zake zilizowazi (hukumu yake) na kamwe msifuate zile (Aya) zinazogongana (maana) kwani Wallah hakuna mtu wa kuwabainishia makatazo yake (Qur’ani) wala hakuna wa kuwawekeeni wazi tafsiri yake isipokuwa huyu (Ali) ambaye nimeshika mkono wake, na ambaye nimemsimamisha mbele yangu, na ambaye ni mkufunzi wenu. Ambaye mimi ni kiongozi wake, basi na huyu Ali ni kiongozi wake, naye ni Ali bin Abu Talib; ndugu yangu, walii wangu, na kwamba uongozi wake ni amri niliyoteremshiwa toka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) “Enyi watu! Kwa hakika Ali pamoja na wabora wanatokana na uzao wangu (Ahlul-Bayt), wao ni kizito kidogo, na Qur’ani ni kizito kikubwa basi vyote viwili viko pamoja, kila kimojawapo kikieleza (kukifafanua) kingine na kukiunga. Kwani vyote havipingani hadi hapo vitakaponifikia peponi katika kisima cha Kawthar. “Wao ni wadhamini (waaminifu) wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake, na ni waongozi wake duniani. Jueni kwa hakika nimetekeleza, na kwa kweli nimefikisha nami nikafahamisha na kufafanua. Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amesema, nami nikasema kwa niaba Yake, Yeye Aliyetukuka. Je, kwa kweli si huyu Amirul Muuminin (Ali) na ndugu yangu? Na baada yangu hautasihi uongozi wa yeyote kwa Waislamu isipokuwa yeye. (Alipofika hapa, Mtume (s.a.w.w.) akawa anampigapiga mabega Ali, akamwinua Ali hadi miguu ya Ali ikalingana na magoti ya Mtume. Kisha Mtume Akaendelea): Enyi watu! Huyu hapa Ali ni ndugu yangu, walii wangu, mrithi wa elimu yangu na mshika hatamu, khalifa wa umma wangu, mfasiri wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, mlinganiaji kwake, mtekelezaji wa yale yanayomridhisha, mpinzani wa maadui zake Allah akiambatanisha na utiifu wake, mkatazaji uasi juu ya Mwenyezi Mungu, khalifa wa mjumbe wa Mwenyezi 115


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 116

katika Uislamu

Mungu, kiongozi wa Waislamu, Imam mwongozi, shujaa wa wakorofi, wakaidi na wahaini wa hukumu za Mwenyezi Mungu. “Nami nasema: Hakuna neno tunalobadilishiwa kwetu, ila ni kwa amri ya Mwenyezi Mungu, Mola wangu. Nasema: Ewe Mola, mwongoe atakayemfanya Ali kuwa ni kiongozi, mfanyie uadui anayemfanyia uadui, mlaani mwenye kumkanusha, na mghadhibikie mwenye kuikataa haki yake! Ee Mola, kwani Wewe umeniamrisha kwamba Uimamu ni wa Ali, walii wako katika kunieleza hilo, na kumchagua kwangu yeye kwa ulilowakamilishia waja wako miongoni mwa mambo ya dini yao na ikatimia neema yako kwa kuwaridhia wao kuwa Uislamu ndio dini; Uliposema: “Na anayefuata dini isiyokuwa ya kiislamu, basi haitakubaliwa kwake (amali). Naye akhera yu miongoni mwa wenye khasara.” (Qur’ani 3:85). Ee Mola nakuhakikishia kuwa nimefikisha. “Enyi watu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amekamilisha dini yenu kwa Uimamu wake Ali. Yeyote yule ambaye hatamfanya mwongozi, pamoja na Ahlul-Bayt watokao kizazi chake, watakaoshika uongozi huu baada yake hadi Siku ya Kiyama, basi hao ndio zimeporomoka amali zao, na wataingia motoni milele, hawatapunguziwa adhabu na Mwenyezi Mungu, na wala hatawaangalia kwa wema. “Enyi watu! Huyu Ali ni mnusuru wenu kwangu, mbora wenu zaidi wa haki kwangu, wa karibu zaidi kwangu na mtukufu zaidi kwangu kati yenu. Mimi na Mwenyezi Mungu tuko radhi naye na haikuteremka Aya ya kuridhiwa isipokuwa kwa ajili yake. Na Mwenyezi Mungu hakuwatangazia wale waliomwamini isipokuwa ni kwa heshima yake na wala haikuteremka Aya ya kusifu isipokuwa ni kwa ajili yake na wala Mwenyezi Mungu hakuwashuhudia pepo wale watu waliotajwa katika Suratu-Dahar isipokuwa ni kwa ajili yake, na hakuiteremsha kwa ajili ya mwingine, na hakumsifu mwingine.

116


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 117

katika Uislamu

“Enyi watu! Yeye Ali ni mnusuru wa dini ya Mwenyezi Mungu, na mtoaji hoja (dalili) juu ya Mtume, naye ni mchaji, mtakasifu na kiongozi mwokozi. Mtume wenu ni Mtume bora, na wasii wenu ni wasii bora kwani ameteuliwa na mbora wa Manabii. Enyi watu, kizazi cha kila Nabii kinatokana na uzao wake, na kizazi changu kinatokana na Ali. “Enyi watu! Hakika Ibilisi alimtoa Adam peponi kutokana na husuda, hivyo msimfanyie (Ali) husuda, zikawa tupu amali zenu, na ikateleza miguu yenu, kwani Adam aliteremshwa ardhini kwa ajili ya kosa moja tu, pamoja na hayo alikuwa mnyofu kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) sasa hali hiyo itakuwaje kwenu nanyi kati yenu wamo maadui wa Mwenyezi Mungu? “Naam! Kwa hakika hambughudhi Ali isipokuwa mwovu, hamwongozi Ali isipokuwa mchaji, na wala hamkubali Ali isipokuwa yule Mwislamu wa kweli (Muumin), kwani Wallah kwa ajili ya Ali imeshuka Surat al-Asr. “Enyi watu! Mcheni Mwenyezi Mungu kwa upeo wa uchaji wake, nanyi msife ila baada ya kuwa mmesilimu. Enyi watu! Mwaminini Mungu na Mtume Wake na nuru tuliyoiteremsha kabla hatujazigeuza nyuso tukazipeleka kisogoni. “Enyi watu! Hiyo nuru toka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ni njia kwangu, kisha kwa Ali, kisha katika uzao wake hadi kwa Al-Mahd (Imam wa Zama) ambaye atawakilisha (kuongoza) kwa haki ya Mwenyezi Mungu na kwa kila haki ambayo inatuhusu Ahlul-Bayt, kwani Mwenyezi Mungu (s.w.t.) ametufanya tuwe ni hoja (dalili) kwa wazembe, wakaidi, wahaini, waovu na madhalimu miongoni mwa wanadamu wote. “Enyi watu! Hakika ninawaonyeni, kwani mimi ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwenu. Kwa hakika wameshapita Mitume wengi kabla yangu. Nikifa au kuuawa je, mtarudi nyuma kwa visigino vyenu (kwenye ukafiri)? Na mwenye kurudi nyuma hatamdhuru Mwenyezi Mungu chochote, na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaomshukuru. Jueni! Kwamba Ali anasifi117


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 118

katika Uislamu

wa kwa subira na shukrani, kisha baada yake ni watoto wangu wanaotokana na (mgongo) uzao wake (Ahlul-Bayt). “Enyi Watu msimtangazie Mwenyezi Mungu Uislamu wenu akawaghadhibikieni ikawapata adhabu Yake, kwani Yeye ni mrakibu (wa mambo na amali). Enyi watu! Baada yangu watakuwepo Maimamu (viongozi) watakaowalingania watu kwenye moto, nao Siku ya Kiyama hawatapata mtu wa kuwanusuru. “Enyi watu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu na mimi tuko mbali nao. Enyi watu! Hakika wao pamoja na vibaraka wao na wafuasi wao watakuwa katika tabaka ya chini kabisa motoni, na hayo yatakuwa ni makazi mabaya kwa wafanyao kiburi. “Je, hawaoni kuwa wao ni watu wa nyaraka (za kuandikiwa amali)? Basi achunguze kila mmoja wenu waraka (wake), wasije wakasema: Wakawakasirikia watu, ila kikundi kidogo miongoni mwao waliozidhibiti nyaraka zao. “Enyi watu! Mimi naliacha suala hili la Uimamu na urithi kwa vijukuu vyangu hadi Siku ya Kiyama, kwani kwa kufanya hivyo nitakuwa nimefikisha lile nililoamrishwa kulifikisha, ili iwe ni hoja kwa kila aliyehudhuria, na aliye mbali. Basi ni jukumu la kila mmoja miongoni mwa walioshuhudia na wasiokuwepo, waliozaliwa, au kizazi kijacho. Hivyo waliohudhria wawafikishie habari wasiokuwepo, mzazi amfikishie mwanawe hadi Siku ya Kiyama.Watalifanya jambo hili (Ukhalifa) kuwa ni ufalme, kwa kunyang’anyana. Ole wao hao! Mwenyezi Mungu awalaani wanyang’anyi na vibaraka wao. Na wakati huo itasemwa: “Tutakukusudieni enyi majeshi mawilli (watu na majini) Mtaletewa miali ya moto na shaba na hapo hamtaweza kujilinda.” (Qur’ani 55: 31, 35). “Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu (s.w.t.) hakupendelea kuwaacheni kama mlivyo mpaka apambanue wabaya na wema na wala haiwi kwa 118


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 119

katika Uislamu

Mwenyezi Mungu kuwajulisheni mambo ya ughaibuni. “Enyi watu! Hakuna kijiji chochote ila Mwenyezi Mungu alikiangamiza kutokana na uasi wao. Hivyo hivyo ataviangamiza vijiji vikibakia katika uovu, kama alivyokwisha sema Mweyezi Mungu (s.w.t.). “Na huyu hapa Ali, Imam na kiongozi wenu, na hii ni ahadi ya Mwenyezi Mungu ambaye huthibitisha kwa aliloliahidi. Enyi watu! Kwa hakika walipotoka wengi wa mwanzoni kabla yenu, na Mwenyezi Mungu aliwaangamiza watu hao na pia ndiye atakayewaangamiza wengine, kama alivyosema:

“Je, hatukuwaangamiza wa mwanzo? Kisha tukawaandamizia wengine? Basi hivi ndivyo tutakavyowafanyia waovu. .” (Qur’ani 77: 16 - 19). “Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ameniamrisha na kunionya, nami nikamwamrisha na kumkataza Ali, hivyo akayajua hayo kutokana na amri ya Mola wake Mtukufu. Basi zisikilizeni amri zake, mnyenyekeeni na kumtii yeye ili mpate kuongoka, jizuieni kutokana na anayowakatazeni ili mpate kunyookewa, na fuateni nyayo zake na kamwe msitolewe kwenye njia (uongozi) yake, nami ndiyo njia ya Mwenyezi Mungu aliyowaamrisha kwayo kuifuata, na kisha kumfuata Ali baada yangu, na mwisho kizazi changu kinachotokana na Ahlul-Bayt wangu, kutoka kwake (Ali). Hao ni Maimamu ambao wanaongoza kwenye haki, na kwayo wanaitekeleza. (Mtume alipofika hapa akasoma Surat Fatiha yote na ndipo akaendelea): “Sura hii imeteremshwa kwa ajili yangu na kwa ajili yao (Maimamu) au Ahlul-Bayt wangu na inawahusu wao tu. Wao ni mawalii (wafuasi) wa Mwenyezi Mungu wasiokuwa na hofu wala huzuni juu yao. 119


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 120

katika Uislamu

“Jueni! kwamba wafuasi wa Mwenyezi Mungu ndio wenye kufaulu. Ole wao! Maadui wa Ali ni watu wa mashakani, wanafiki, waasi, na hao ndio wafanyao uadui. Ni kundi la shetani (mataghuti), ambao baadhi yao wanawafunulia wenzao maneno ya kupamba ili kuwadanganya. “Jueni! kwamba wafuasi wao Maimamu ndio Waislamu wa kweli, ambao Mwenyezi Mungu amewataja katika kitabu chake aliposema: “Hupati (kuwaona) watu wanaomwamini Allah na Siku ya Kiyama, kuwa wanawapenda wale wanaompinga Allah na Mtume wake. ............” (Qur’ani 58:22) “Na ni wafuasi wao hao hao aliowasifu Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliposema: “Wale walioamini, hawakuchanganya imani yao na ushirikina; kuwa hao ndio watakaopata amani nao ndio walioongoka.” (Qur’ani 6:82) “Mwenyezi Mungu (s.w.t.) akawasifu kwa kuwaambia kuwa hao ndio watakaoingia peponi kwa amani, na watawakuta Malaika kwa utii, wakisema kwamba furahini na ingieni humo mkae milele. “Naam! Hakika wafuasi wao ndio aliowazungumzia Mwenyezi Mungu (s.w.t.) kwamba: Wataingia peponi bila hesabu (bila kuhojiwa amali zao). Ole wao maadui wa Ahlul-Bayt ambao wataunguzwa katika moto uwakao. “Maadui hao watausikia moto wa jahanamu ukivuma na kufoka na kutoa sauti (ya kutisha). Hao ndio maadui ambao Mwenyezi Mungu alisema kwamba: “Kila utakapoingia humo umma, utawalaani wenzao...........” (Qur’ani 7:38). Vile vile akasema: “Kila mara litakapotupwa humo kundi la waovu, walinzi wake watawauliza: Je, hakukufikieni mwonyaji? Watasema: Kwa nini, Alitujia, lakini tulikadhibisha, na tulisema Allah hakuteremsha chochote, ninyi hampo ila katika upotofu mkubwa.” (Qur’ani 67 : 8-9). Akasema tena: “Ambao wanamwogopa Mola wao (hata) wanapokuwa faraghani, watapata msamaha na ujira mkuu.” (Qur’ani 67:12). 120


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 121

katika Uislamu

“Enyi watu! Wapi na wapi baina ya moto (Jahannam) na pepo? Atakuwa adui yetu yule aliyeshutumiwa na kulaaniwa na Mwenyezi Mungu, na kipenzi chetu ni yule aliyependwa na Mwenyezi Mungu na akasifiwa. “Enyi watu! Jueni, kwamba mimi ni mwonyaji na Ali ni mwongozi. Enyi watu! Mimi ni Mtume, na Ali ni wasii, na kwamba mwisho wa Maimamu kutokana nasi ni Al-Mahdi ambaye ataidhihirisha dini, kwani yeye atalipiza kisasi kwa madhalimu. Kwa yakini ataziteka ngome (za maadui) na kuzibomoa, atawapiga vita kila kabila la washirikina, na kwamba yeye atapambana na kila mpinzani wa mawalii (viongozi) wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.). “Jueni! Kuwa yeye ni mwokoaji ndani ya kina cha bahari. Kwa hakika atawatambua wabora kutokana na ubora wao, na wajinga kwa ujahili wao. Kwa hakika yeye amechaguliwa na Mwenyezi Mungu, na ni mteule Wake, ni mrithi wa kila elimu ambayo imemzunguka. “Yeye ni mtoaji habari kwa ajili ya Mola Wake Mtukufu, mzinduzi kwa amri ya imani yake, ni kiongozi mpigania haki, kwani anaitetea. Jueni kwamba yeye amebashiriwa na waliomtangulia kwenye utawala wake. Yeye atabakia awe ni hoja, na hapo hakutakuwa tena na udhuru baada ya kuwepo kwake, na hakuna haki (ukweli) isipokuwa iko pamoja naye, wala nuru isipokuwa iko kwake, kwani hana wa kumshinda nguvu wala hakuna (mwovu) atakayejinasua toka kwake. Hakika yeye ni walii wa Mwenyezi Mungu duniani, kiongozi Wake kwa viumbe Wake, mdhamini (mwaminifu) wa mambo Yake ya siri na yale ya dhahiri. “Enyi watu! Hakika nimewabainishieni na kuwafahamisheni, na kwamba huyu Ali ataendelea kuwafahamisheni baada yangu. Jueni kwamba mara tu baada ya kumalizika kwa khotuba yangu hii, nawaombeni mjumuike pamoja nami katika kumuunga mkono (bai’a) na kumkubali yeye, kisha muendelee kumuunga mkono baada yangu. Tambueni kwamba mimi nimekiri kwa Mwenyezi Mungu, na Ali amenikubali mimi. Nami 121


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

7/1/2011

12:20 PM

Page 122

nawahimizeni kumuunga mkono (kumkubali) yeye kwa amri ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.). “Basi avunjaye ahadi (hizi) anavunja kwa kuidhuru nafsi yake .....” (Qur’ani 48:10). “Enyi watu! Hakika ya Hijja na Umra Swafa na Mar’wa (majabali mawili) ni miongoni mwa alama za kuadhimisha dini ya Mwenyezi Mungu. Basi anayehiji au kufanya Umra si kosa kwake kuyazunguka (hayo majabali). Enyi watu! Fanyeni Hijja kwenye nyumba hiyo kwani Ahlul-Bayt wangu hawakuizuru nyumba isipokuwa walivuna. Nanyi msiiache, kwani mkifanya hivyo mtafakirika. “Enyi watu! Mwislamu wa kweli (Muumin) hawi na msimamo thabiti isipokuwa Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yake, yaliyopita na anayofanya. Kwani (mwanadamu) zinapokoma harakati zake, basi amali (vitendo) zake huendelea kubaki. “Enyi watu! Wanaohiji huvuna, na masurufu yao yamehifadhiwa (kwa Mwenyezi Mungu) kwani Yeye hapotezi ujira wa watu wema. Enyi watu! Fanyeni Hijja kwenye hiyo nyumba kwa ajili ya ukamilifu wa dini pamoja na kujifunza, wala msiondoke kwenye sehemu tukufu za Hijja isipokuwa muwe mmekwisha tubia na kusamehewa. “Enyi watu! Simamisheni swala na toeni Zaka, kama mlivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (s.w.t.). Pindi muda ukawa mrefu, nanyi mkazembea au kusahau, basi Ali ni kiongozi wenu wa kuwabainishia yale ambayo Mwenyezi Mungu (s.w.t.) amemhusisha baada yangu. “Na mwenye kufanywa khalifa na Mwenyezi Mungu na mimi pia, huyo atawafahamisheni kwa yale mtakayomwuliza, na atawabainishieni yale msiyoyajua. “Jueni kuwa maswala ya halali na haramu ni mengi kwamba ninayadhibiti na kuyafahamisha. Kwa sababu anayeamrisha mambo ya halali na anayekataza haramu wako daraja moja, hivyo nimeamrishwa nipokee 122


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 123

katika Uislamu

kiapo cha utii toka kwenu, pamoja na kushikamana nanyi kwa kukiri kwa yale niliyoyaleta toka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) yale yanayomhusu Ali -Amirul Muuminin pamoja na Maimamu watakaofuatia baada yake; ambao wao wanatokana nami. Na kutokana naye wamo watu waliotengenea. Miongoni mwao ni Al-Mahdi ambaye atabaki hadi Siku ya Kiyama, naye atahukumu kwa haki. “Enyi watu! Kila jambo la halali nililowajulisheni, au la haramu nililowakatazeni, basi mimi kamwe sirudii hilo na wala sibadilishi. Jueni na muyakumbuke na kuyahifadhi na mshikamane nayo bila ya kuyabadilisha wala kuyageuza. “Jueni! Kwani mimi tu ndiye ninayebadilisha kauli. Simamisheni Swala, toeni Zaka, amrisheni mema na katazeni maovu. Jueni kwamba msingi wa kuamrisha mema ni kufanya hivyo kwa mujibu wa maneno yangu, na kumfikishia asiyekuwepo na kumwamrisha ayakubali, na kumhadharisha asiyapinge, kwani hiyo ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (s.w.t.) na kwangu pia. Na ni lazima katika suala la kuamrisha mema na kukataza maovu apatikane Imam ‘maasum’ (aliyelindwa na madhambi). “Enyi watu! Qur’ani itawafahamisheni kwamba Maimamu baada yake Ali watatokana na uzao wake, na niliwafahamisheni kwamba yeye Ali anatoka na nami, nami natoka na naye. Ndipo aliposema Mwenyezi Mungu katika Kitabu Chake: “Na akalifanya neno hili (Uislamu) ni lenye kubakia katika kizazi chake ili warejee.” (Qur’ani 43:28) “Na ninasema: Kamwe hamtapotea ikiwa mtashikamana navyo (Qur’ani na Ahlul-Bayt). Enyi watu! Mcheni Mungu! Mcheni Mungu! Jihadharini na Siku ya Kiyama, kama alivyosema Mwenyezi Mungu (s.w.t.): “Hakika mtetemeko wa Kiyama ni jambo kubwa.” (Qur’ani; 22:1). Kumbukeni kifo, hesabu, amali na kuhesabiwa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w.t.) Mola wa walimwengu. Pia kumbukeni kuwa kuna thawabu na adhabu. Atakayefanya jema atalipwa thawabu, na atakayefanya uovu huyo hana fungu peponi. 123


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 124

katika Uislamu

“Enyi watu! Hakika nyie hasa mniunge mkono barabara, kwani Mwenyezi Mungu ameniamrisha nipate uthibitisho kwa kauli zenu, kuyakiri haya niliyoyafungamanisha kwa Ali kuhusu suala la uongozi wa Waislamu, pamoja na wengine watakaofuatia baada yake miongoni mwa Maimamu wanaotokana nami na yeye kwa yale niliyokwisha wajulisheni; kwamba kizazi changu kinatokana na uzao wake. Basi nyote semeni: Tumesikia, tunatii na kuridhia - kwa kuthibitisha haya niliyofikisha, toka kwa Mola wetu na Mola wako kuhusu suala la Ali na watoto wa uzao wake miongoni mwa Maimamu, kwamba tunakuunga mkono kwa hilo; kwa nyoyo zetu, nafsi zetu, ndimi zetu na kwa hali zetu. Na juu ya hayo tutapata uhai, kufa na kufufuliwa na kamwe hatugeuzi, wala kubadilisha, wala kuwa na shaka, wala kunungunika, wala kuisaliti ahadi wala kuvunja kiapo! “Nasi tutamtii Mwenyezi Mungu pamoja na kukutii wewe na Ali AmirulMuuminin, na kuwatii watoto wake, Maimamu ambao umewataja, wanaotokana na kizazi chake kwenye uzao wake, baada ya Hasan na Husein, ambao nimekufahamisheni vyeo vyao kwangu, pamoja na daraja zao kwa Mola Wao Mtukufu.’ Yote hayo nimetekeleza kwenu, kwani wao Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi, na kwamba wao watakuwa Maimamu baada ya baba yao Ali, nami ni babu yao kabla yake Ali. “Basi semeni: ‘Tumemtii Mwenyezi Mungu kwa hilo, tumekutii wewe, Ali, Hasan, Husein pamoja na Maimamu uliowataja, pia tumeitii ahadi na kiapo kilichochukuliwa kwa Amirul Muuminin, katika nyoyo zetu, nafsi zetu na ndimi zetu pamoja na kuwaunga mkono kwa ulimi wake kila atakayewakaribia, kwani hatukatai hiyo badili, na wala kamwe hatuoni nyoyoni mwetu kuliacha hilo. Tunamthibitishia Mwenyezi Mungu, naye anatosha kuwa shahidi nawe kwake ni shahidi upande wetu, na kwa kila aliyetii miongoni mwa waliojitokeza, na wale wasiokuwapo, Malaika wa Mwenyezi Mungu pamoja na jeshi lake, watumishi wake (pia nao ni mashahidi). Na Mwenyezi Mungu ni mkubwa juu ya kila shahidi.’

124


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:20 PM

Page 125

katika Uislamu

“Enyi watu! Kwa kila msemalo, basi Mwenyezi Mungu anajua kila sauti na undani wa kila nafsi. Hivyo atakayeongoka, basi huyo amejiongoa na atakayepotea, huyo amepata khasara. Na mwenye kufungamana nawe, huwa amefungamana na Mwenyezi Mungu, na nusura ya Mwenyezi Mungu iko juu ya mikono yao. Enyi watu! Mcheni Mungu na muungeni Ali Amirul Muuminin, Hasan, Husein na Maimamu ambao ni neno (kizazi) zuri lenye kubaki (kudumu). Mwenyezi Mungu humwangamiza mwenye kuhini, na humrehemu anayetekeleza: “........ Na avunjaye ahadi, anavunja kwa kuidhuru nafsi yake.........” (Qur’ani 48:10). “Enyi watu! Yatangazeni hayo niliyowaambieni, na nyenyekeeni (kwa utii) kwa Ali juu ya uongozi wa Uislamu. Semeni basi: ‘Tumesikia na kutii, msamaha ni wako ewe Mola wetu,na Kwako tu ndiyo marejeo’. Na kisha semeni pia ...... “Sifa njema ni za Allah aliyetuongoza kwa hili (la Uislamu) na kamwe tusingeongoka lau si Allah kutuongoza......” (Qur’ani 7:43). “Enyi watu! Fadhila za Ali Ibn Abu Talib mbele ya Mwenyezi Mungu, ni nyingi. Kwani nimefahamishwa hayo zaidi ndani ya Qur’ani kiasi kwamba siwezi kudhibiti mahali hapa, basi atakayewafahamisha kwazo msadikisheni. “Enyi watu! Mwenye kumtii Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, Ali pamoja na Maimamu niliowataja, basi huyo atapata ushindi mkubwa. Enyi watu! Wale wa mwanzo kufungamana naye Ali katika kumuunga mkono, na kuukiri uongozi wake kwa Waislamu, basi hao ndio watakaofuzu kwenye pepo yenye neema. “Enyi watu! Semeni yanayomridhisha Mwenyezi Mungu kwenu miongoni mwa maneno, kwani hata kama mkikufuru nyie pamoja na wote waliomo ardhini, basi hilo halimdhuru Mwenyezi Mungu chochote. “Ee Mola, waghufirie Waislamu, wake kwa waume, na waghadhabikie makafiri, wake kwa waume, na sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu” 125


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 126

katika Uislamu

MWISHO WA KHUTBA Ndugu wasomaji hiyo ndiyo hotuba (wasia) kamili ya Mtume (s.a.w.w.). Katika Sura ya Pili chini ya - Hadithi ya Tano: nimeeleza historia yake ilivyotokea. Nitakachoongeza hapa ni ushahidi wa masahaba walioipokea, kama ifutavyo. Hakuna Hadithi iliyopokelewa na masahaba wengi sana kama hiyo! Katika hotuba hiyo Mtume (s.a.w.w.) kasema wazi kwamba katika mkutano huo kulikuwepo na wanafiki wengi wapinzani ambao angeweza kuwataja kama Mwenyezi Mungu angemruhusu! Kwa hiyo sisi Shia Ithna’asheri tunaposema kuwa kulikuwepo na masahaba wengi wanafiki wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), ushahidi wetu mmojawapo ni huo. Kama siyo unafiki uliokithiri, ilikuwaje masahaba 140,000 wasikilize hotuba kama hiyo kwa masikio yao halafu miezi mitatu baadaye masahaba hao hao wakapuuzia wasia huo pale Mtume (s.a.w.w.) alipofariki! Aliyoyaeleza Mtume (s.a.w.w.) katika hotuba hiyo, yalitokea kweli kwa ushahidi wa kumbukumbu za historia sahihi ya Uislamu. Migogoro yote aliyotabiri Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na kupinga na kuzuia uongozi wa Imam Ali (a.s.), ilitokea kweli. Maelezo yanayofuatia katika Sura za mbele yanaeleza migogoro hiyo kwa ushahidi kamili. Hata kama ingekuwa historia niliyoeleza humu yote ni ya uongo, bado kila Mwislamu mwaminifu ataona kuwa kihistoria, hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w) ilipuuzwa kabisa! Kitendo hicho hakikubaliki hata kidogo! Wafuatao ndio baadhi ya masahaba waliopokea Hadithi hiyo toka kwa Mtume (s.a.w.w) moja kwa moja: Abu Huraira (Taarikh Baghdad , Jz. 8 uk. 290) Abu Laila Ansari - Manaaqibi Khwarzimi, uk. 35 Abu Zainab Bin Auf Ansari - Asadul Ghaabah, Jz. 3, uk. Abu Fudhaala Ansari - Asadul Ghaabah, Jz. 3 uk. 307 Abu Qudaama Ansari - Asadul Ghaabah, Jz. 3 uk. 276 126

307


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 127

katika Uislamu

Abu Umrah Bin Amru bin Muhsin Ansari - Asaadul Ghaabah, Jz. 3 uk. 307 Abul Haitham Bin Nabhaan - Maqtal Khwarzimi, uk. 47 Abu Raafi Qibti (Mtumwa wa Mtume) - Hadithi Wilayat -Al-Ghadir, Jz.1, uk. 16 Abu Zuwait Khuwallid - Khilafaat Uthman, cha Khwarzimi Abubakar bin Abi Quahafa, cha Abu Ju’abi - kitabu: Nakhb. Ummi Salma Twaahira (mke wa Mtume), cha ibn Uqda kupitia kwa Amru ibn Said kitabu : Yanabil’Mawaddah. Umme Hani bint Abu Talib, kitabu: Yanabiul’Mawaddah - uk. 40 Abu Hamza Anas bin Malik Ansari Khazraji (Mtumwa wa Mtume) kitabu: Khatibi Baghdadi, Jz. 7, uk. 377. Burra Ibn Aazib Ansari Uweisi kitabu: Musnad Ahmad, Jz. 4, uk. 281. Yazid Ibn Khasib Abu Sahl Aslami- kitabu: Mustadrak al Hakim, Jz. 3, uk. 110 Abu Said Thabit Bin Wadii’ah Ansari Khazraji Madani -kitabu: Asadul Ghaabah - Jz. 3, uk. 307 Jaabir Ibn Samra Ibn Junaada - kitabu: Kanzul Ummal, Jz. 3, uk. 398. Jabir Ibn Abdullah al-Answari- kitabu: Al-Isti’ab, cha Abdul Baar Jz.2 uk. 476. Jabla Ibn Amru Ansari - kitabu: Hadithi Wilayat. Jabir Ibn Mut’am Ibn Abdi Qarashi Naufali - kitabu: Qadhi Bahlul Bahjat, uk. 68. Abu Dharr Jundub Ibn Junada Ghiffari - kitabu: Hadithi Wilayat. Abu Janidah Jundu Ibn Amru Ibn Maazin Ansari - kitabu: Asadul Ghaabah, Jz.1 uk. 308 . Jund Ibn Jawin Abu Kudaama Arabi Bijli - kitabu: Asadul Ghaabah, Jz.1, uk. 367. 127


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 128

katika Uislamu

Habashi Ibn Junada Saluuli - kitabu: Asadul Ghaabah, Jz. 3, uk. 67. Habibu Ibn Badeel Ibn Darqa - kitabu: Khuzaai, Jz. 1, uk. 304. Hudhaifa Ibn Aasiid Abu Sariiha Ghaffari - kitabu: Yanaabil’ Mawaddah, uk. 38. Hudhaifa Ibn Yamaani - kitabu: Taqrib, uk. 82. Aisha bint Abubakar Ibn Abu Quhafa - kitabu: Hadithi Wilayat. Abu Abdillah Salman Farsi - kitabu: Shafii, cha Ibn Uqda, Juabi na Hamwini. Ummar Ibn al-Khattab - kitabu: Manaaqib na kitabu: Riyadhun Nadharah, Jz. 2, uk. 161 Idadi ya masahaba walioandikwa kwa majina kuhusiana na kuielezea Hadithi hii, inafikia 110 lakini nafasi haitoshi kuwaandika wote. Hata hivyo ninaamini kuwa Mwislam yeyote mwaminifu hatahitaji ushahidi zaidi ya hapa, au kwenda kwa shekhe kuuliza la kufanya, ili kufikia uamuzi wa haki kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia ambao ulipuuzwa na Waislamu wa wakati huo. Na kwamba sisi Waislamu wa wakati huu tunaendeleza upotofu huo bila kujitambua! Waislamu tujiulize ni Uislamu gani tunaokwenda nao wakati huu? Ni Uislamu au utamaduni wa mababu zetu?

KWA NINI WASIA WA MTUME (S.A.W.W.) ULIPUUZWA? Iwapo ushahidi niliotoa kuhusu uongozi wa Waislamu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni maneno ya Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu, kwa nini hayakutekelezwa? Kwanza tujiulize ni nani waliotakiwa kuyatekeleza? Waliotakiwa kuyatekeleza ni Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Huko nyuma niliuliza swali kwamba, Iwapo Mtume (s.a.w.w) angekuwa hai wakati huu, vipi tungeacha kutii amri yake hata moja tu iwapo kweli tunajiita Waislamu, kwa kuzingatia maana ya neno ‘Islam’ niliyoeleza nyuma? 128


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 129

katika Uislamu

Kwa hiyo tunaanza kuona kuwa Masahaba walikiuka makusudi huo wasia wa Mtume (s.a.w.w.)! Hebu tuone Qur’ani inatueleza nini juu ya Mtume (s.a.w.w.) “Na hatukuleta Mtume yeyote ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu................”. (Qur’ani 4: 64). “Wala hasemi kwa matamanio yake (ya nafsi yake) ila ni wahyi …..” (Qur’ani 53:3). “Hayakuwa haya (anayosema) ila ni Wahyi (ufunuo) uliofunuliwa (kwake)” (Qur’ani 53 : 4 ). Vile vile zipo Aya nyingi za Qur’ani zinazotuamrisha kumtii Mtume (s.a.w.w.) - (47:33), (3:32), (5: 92), (8:1), (24: 54), (58:13), (64:12) n.k. Masahaba waadilifu na wanafiki: Itikadi ya Sunni ni kwamba Masahaba wote ni waadilifu. Suala hili limeleta malumabano mengi kati ya Sunni na Shia Ithna’asheri. Hebu tuone Qur’ani inasemaje: (a) “Na katika Mabedui wanaokaa pembezoni mwenu katika vitongoji vya karibu yenu hapo Madina kuna wanafiki. Na katika wenyeji wa Madina pia kuna wanafiki. Wamezama katika unafiki hata huwajui kuwa ni wanafiki. Sisi tunawajua..............” (Qur’ani 9 : 10 ). (b) “Mwenyezi Mungu amekusamehe. Kwa nini umewapa ruhusa? (Ungengoja) mpaka wale wanaosema kweli wakupambanukie na uwajue waongo” (Qur’ani 9:43). Aya hizi mbili zinawazungumzia masahaba kwa hiyo hapana haja ya maelezo marefu kwani aya zinaeleweka. Hatuoni hapa madai ya kwamba masahaba wote ni waadilifu! 129


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 130

katika Uislamu

Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) nayo inathibitisha ukweli wa Qur’ani: “Watu miongoni mwa sahaba zangu watanijia peponi katika kisima cha Kawthar, nitakapowaona wakiletwa kwangu watazuiliwa wasinifikie. Kisha nitasema hawa ni sahaba zangu, lakini nitaambiwa wewe hujui walizua nini nyuma yako.” Hadithi hii inapatikana katika Sahih Muslim, Kitabul Fadhail, mlango wa Haudhu Nabiyyina (s.a.w.w.). Kwa ushahidi zaidi katika Qur’ani soma Aya zifuatazo: (9:97), (9:74), (9:77), (2:10), (48:11), (47:30), (47:16), (63:3), (4:62), (4:142), (63:4), (33:19). Katika Sura ya 9 na Sura ya 63 kuna Aya zaidi ya 150 za Qur’ani juu ya masahaba wanafiki! Je Huo uadilifu wa jumla uko wapi? Waislamu tujenge hoja kisayansi. Pengine ingefaa tuchambue kwanza baadhi ya matendo ya masahaba wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Ni muhimu tufanye utafiti wa matendo ya masahaba tuone kama walikuwa watiifu kwa Mtume (s.a.w.w.) au hapana? (a) Anakaririwa Ibn Abi Mulayka akisema, “Nilikutana na Masahaba 30 wa Mtume (s.a.w.w.) na kila mmoja wao alihofia kuwa ni mnafiki kwa sababu hakuna aliyekuwa na Imani juu ya kuwepo kwa Malaika Jibril au Malaika Mikail! - Sahih al-Bukhar Jz. 1 uk. 97. Nikisherehesha zaidi ni kwamba hawa Masahaba ambao hawakuamini kuwepo kwa hao Malaika wawili, ina maana hawakuamini Utume wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.) kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) aliletewa ‘Wahyi’ na Malaika Jibril toka kwa Mwenyezi Mungu! Isitoshe Imani ya Waislamu wote ya kuamini Malaika na vitabu vya Mwenyezi Mungu iko wapi kwa hao masahaba? Je, hao nao ni waadilifu? Na Uislamu wao ukoje? (b) Katika Sahih al-Bukhari chini ya kifungu cha ‘Maneno ya Mwenyezi Mungu’ katika Qur’ani 63:6 kuhusu sababu ya kushuka kwa Aya hiyo:.... 130


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 131

katika Uislamu

“Ni mamoja ukiwaombea msamaha au ukiacha. Mwenyezi Mungu hatawasamehe; kwani hawaongozi wapotofu” - (Qur’ani; 63:6). Bukhari anasema kuwa kilichotokea kuhusiana na kushuka Aya hiyo ni kwamba ‘Mtu mmoja kutoka Muhajirun alimpiga Ansari mmoja.’ Ansari akasema, ‘Enyi Ansari nisaidieni.’ Naye Muhajirin akasema ‘Enyi Muhajirun nisaidieni.’ Mtume (s.a.w.w.) aliyasikia hayo na kusema, “Ni mabishano gani hayo yenye hisia za enzi za ujinga (jahiliya)?” Masahaba wakasema ‘Ewe mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Muhajirin kampiga Ansari.’ Mtume akasema, “Acha kitendo hicho kinachukiza.” Ikawa Abdullah bin Ubayy amesikia hayo na kusema, ‘Wamefanya hayo? Tukirejea Madina wale wenye nguvu watawafukuza wanyonge’! Maneno hayo yakamfikia Mtume (s.a.w.w.) na ikawa Umar Ibn al-Khattab amenyanyuka na kusema: ‘Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu niruhusu nikate kichwa cha mnafiki huyu.’ Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mwacheni ili watu wasijesema kuwa Muhammad anawaua sahaba zake.” - Sahih alBukhari, Jz. 6, uk. 65. Kwa maelezo zaidi ni kwamba Hadithi hii yaonyesha wazi kuwa sahaba hao walikuwa wanafiki kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) alikubaliana na Umar kwamba sahaba huyo Muhajirin alikuwa mnafiki, lakini alizuia asiuawe ili kuepusha picha mbaya kwa watu. Pengine Mtume (s.a.w.w.) alijua kuwa iwapo kila mnafiki angeuawa huenda pasingebakia masahaba wengi! Tunachokiona hapa ni hao masahaba kuendelea kujitambulisha kama Muhajirun na Ansari badala ya kujiona ndugu moja, kama Waislamu tunavyotakiwa kufuta ukabila na utaifa na kujiona taifa na kabila moja dunia nzima. (c) Katika Sahih al-Bukhar, anakaririwa Mama Aisha akisema, ‘Mtume (s.a.w.w.) alifanya jambo fulani na kuliruhusu lakini baadhi ya watu walikataa kulifanya. Habari zilimfikia Mtume (s.a.w.w.) ambaye alitoa hotuba baada ya kumsifu Mwenyezi Mungu na akasema: “Inakuwaje kundi la watu miongoni mwenu hukataa kufanya ninalofanya! Kwa jina la 131


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 132

katika Uislamu

Allah mimi ni mwenye elimu zaidi ya wote kuhusu kumjua Mwenyezi Mungu na ninamwogopa zaidi.’ - Sahih al-Bukhari, Jz. 7, uk. 96. Hapa tunaona masahaba wanafikiri kwamba wameweza kumkosoa Mtume (s.a.w.w.) kwa kukataa kufuata mwendo wake! Mafunzo yote ya Qur’ani yanayowaamrisha kumtii Mtume (s.a.w.w.) mbona hayaonekani katika vitendo vyao? Je, huo nao ni uadilifu? (d) Katika Sahih al-Bukhari, anakaririwa Ibn Abbas akisema kuwa, “Katika siku ya nne ya Dhu’l-Hijja, Mtume (s.a.w.w.) alifika akiwa tayari keshaweka nia ya Hijja na si lolote linginelo. Alipotokeza alituamuru tufanye Umra na kisha twende kukutana na wake zetu. Watu walisema maneno mengi kupinga amri hiyo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): ‘Ata akasema: ‘Jabir alisema kuwa iwapo mmoja wetu akienda Mina atakuwa bado anachuruzika mabaki ya uchafu wa kukutana na mkewe.’ Maneno hayo yalimfikia Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliwahutubia watu akisema, ‘Nimepata taarifa kuwa watu wanasema hivi na vile. Kwa jina la Allah mimi ni mcha Mungu zaidi yenu na ni mwingi wa kumwogopa Mwenyezi Mungu.” - Sahih al-Bukhari Jz. 2, uk. 114. Hapa ni ajabu kuona kuwa, wakati tunategemea Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutuongoza katika matendo ya dini, tunaona hapa masahaba wanapinga alivyowaelekeza Mtume (s.a.w.w.)! Je, huo ni uadilifu? Ina maana masahaba hao hawakufahamu kuwa baada ya kukutana kimwili hufuatia kuoga na hivyo kutoharika? Vipi wangeenda Mina katika hali ya uchafu? Na ni uchafu gani huo ambao Mtume (s.a.w.w.) hakuufahamu! (e) Katika Sahih al-Bukhari katika kitabu cha Swala ya Ijumaa, anakaririwa Jabir bin Abdullah akisema kuwa, ‘Msafara wa biashara uliwasili toka Syria ukiwa umebeba vyakula. Tulikuwa tukisali Swala ya Ijumaa tukiongozwa na Mtume (s.a.w.w.). Watu wote waliacha Swala isipokuwa walibaki watu 12 tu! Na hapo ndipo ikashuka Qur’ani: “Na wanapoona biashara na mambo ya upuuzi, hufanya haraka kuondoka na 132


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 133

katika Uislamu

kukuacha umesimama.’.......” (Qur’ani 62:11). Hapa tunawaona masahaba wanadiriki kukatisha Swala inayoongozwa na Mtume (s.a.w.w.) kukimbilia misafara ya biashara! Ndugu wasomaji nawauliza tena kwamba kama Mtume (s.a.w.w.) angekuwa hai, vipi sisi Waislamu wa leo pamoja na upotofu wetu, tungediriki kumwacha Mtume (s.a.w.w.) anaongoza Swala, tukakimbilia sokoni kupakua shehena za biashara zilizoingia? Au ni Waislamu wangapi leo hii ambao hukatisha Swala ya Ijumaa kabla haijaisha na kukimbilia shughuli za kidunia? Hiyo ndiyo sura ya masahaba tunaowatukuza kijumla bila kuchunguza historia zao! Uadilifu uko wapi? (f) Kuna tukio lingine maarufu sana lililotokea wakati Mtume (s.a.w.w.) akitokea katika vita vya kujihami dhidi ya watu wa kabila la Bani Mustaliq mnamo mwaka wa 5 A.H, ambapo Mtume (s.a.w.w.) na msafara wake walipiga kambi sehemu fulani usiku ulipoingia. Mama Aisha aliondoka kambini hapo usiku huo na akaelekea porini kwenda haja. Akiwa huko alipoteza mkufu wake wa shingoni na akawa anautafuta. Alipoupata mkufu, ikawa huko kambini hawana habari kuwa Mama Aisha alitoka kambini na hivyo wakaanza safari kuondoka hapo. Kwa kuwa ngamia wa mama Aisha alijengewa kibanda juu yake cha kumhifadhi na kwamba kibanda hicho kimefunikwa kabisa na ni gizani, hakuna aliyehisi kuwa mama Aisha hayumo kibandani humo. Mama Aisha aliporejea kambini alikuta watu wote wameondoka na hivyo akakaa chini kusubiri kama atatokea mtu kumfuata. Akiwa hapo usiku huo alishikwa na usingizi akalala. Kesho yake asubuhi, sahaba mmoja, Safwan bin Hantala aliyeachwa nyuma na jeshi la Waislamu, ili kuangalia kama kuna chochote kilichoachwa nyuma gizani, alimkuta mama Aisha. Alimpandisha mama Aisha kwenye ngamia na ikawa yeye anatembea kwa miguu hadi walipokuta msafara wa Mtume (s.a.w.w.).

133


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 134

katika Uislamu

Tukio hilo liliwafanya masahaba wanafiki kumwudhi Mtume (s.a.w.w.) kwa kueneza uvumi wa uongo kumsingizia tendo la uzinifu mama Aisha! Kiongozi wa unafiki huo alikuwa Abdulla bin Ubay - kiongozi wa wanafiki wa Madina. Miongoni mwa waenezaji wa uvumi huo alikuwemo Mistah ambaye alikuwa mtoto wa mjomba wake Abu Bakr. Mtume (s.a.w.w.) alimwita Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) na Ibn Zayd na kuwaeleza uvumi huo potofu ulioenezwa na wanafiki. Zayd alisema kuwa maneno ya wanafiki yapuuzwe. Imam Ali (a.s.) alishauri kuwa Burairah mtumishi wa mama Aisha aitwe na kutoa ushahidi kuhusu tabia ya mama Aisha. Yule mtumishi aliitwa na akasema kuwa hajaona dalili zozote za yeye kuamini uvumi huo. Uvumi huo ulipuuzwa na ndipo ikashuka Aya, (Qur’ani : 24:11). Katika Aya hiyo maneno ya mwisho ya: “......... Yule aliyebeba sehemu kubwa ya kueneza uvumi huo atapata adhabu kali.” Maneno hayo yanamhusu Abdullah bin Ubay kwa kuongoza kueneza uvumi huo. Na huo ndio umuhimu wa kutafuta sababu za kushuka Aya, na siyo kufasiri maneno tu kwa kanuni za lugha peke yake. Lengo la kueleza kisa hiki ni kuonyesha kuwa kundi la hao masahaba waliueneza uvumi huo kinyume na mafunzo au amri ya Qur’ani inayoamuru kuwa tuhuma ya uzinifu ithibitishwe kwa ushahidi wa watu wanne. Je, masahaba hao, nao ni waadilifu? Hao wanaodai kuwa masahaba wote ni waadilifu, ni kwa ushahidi gani? (g) Katika historia ya vita vya Uhud tunaelezwa kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliondoka Madina na Jeshi la watu (sahaba) elfu moja. Lakini huko njiani Abdullah bin Ubay Salul alimkimbia Mtume (s.a.w.w.) akarejea Madina na wenzake 300! Sitawataja majina yao lakini jambo la msingi ni kwamba walikuwa masahaba! Je, Qur’ani inasemaje juu ya watu kama hao:

134


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 135

katika Uislamu

“Enyi mlioamini, Mnapokutana vitani na wale waliokufuru, basi msiwageuzie migongo. Yeyote atakaye wageuzia mgongo wake siku hiyo, isipokuwa kama amegeuka ili kushambulia, au amegeuka ili kuungana na sehemu nyingine (ya jeshi lake), basi huyo anastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makazi yake ni Jahannam napo ni marejeo mabaya” (Qur’ani 8:15-16 ). Maelezo ya Aya hii yanajitosheleza kuhusu hukumu ya mtu anayekimbia vitani, katika vile vita vya kujitetea vya Jihad, wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Je, masahaba kama hao waliolaaniwa na Mwenyezi Mungu na kuhukumiwa kwenda Jahannam, nao bado tunawaita waadilifu? Ndugu Waislamu tuwe waangalifu na imani potofu tulizopandikiziwa ambazo zinapingana na maneno ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.). Kwani tunapata faida gani kuwatukuza watu waliomuasi Mtume (s.a.w.w.)? Mwanzoni mwa somo hili niliuliza swali: “Kwa nini wasia wa Mtume (s.a.w.w.) ulipuuzwa?” Nadhani kutokana na maelezo juu ya tabia za masahaba, bila shaka tunaweza kwa uaminifu, kusema kuwa ilikuwa ni kawaida kwa baadhi ya masahaba kumuasi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na hivyo ndivyo tutakavyozidi kuona katika somo lifuatalo. Jambo linalotusikitisha sisi Shia Ithna’asheri ni kuona wanatukuzwa masahaba ambao kihistoria hawakuwa na sifa yoyote ya kustahili kutukuzwa! Wakati huo huo masahaba waongofu na wacha Mungu kupindukia hawatajwi kabisa! Hebu tujadili masahaba wafuatao, ambao walikuwa waadilifu: Salman Farsi (Mwajemi – Mwiran):

135


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 136

katika Uislamu

Kuhusu sahaba huyu, Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Salman minna Ahl al Bait” – ‘’Salman ni katika sisi Ahlul-Bayt.’’ Hiki ni cheo kikubwa ambacho hakupewa sahaba yeyote wa kawaida. Kutokana na ahadi ya Mtume (s.a.w.w.) kwa Salman Farsi, sisi Shia tunapata ushahidi wa matukio yote yanayomkuta mtu kuanzia anapokaribia kufariki hadi kuzikwa; pamoja na maswali (Talqin) sahihi anayoulizwa mtu kaburini. Katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.) alimwahidi bwana Salman Farsi kwamba, ‘Ewe Salman kabla tu ya kufariki kwako utapata fursa ya kuongea na watu wa makaburini.’ Utabiri huo ulitimia na kwa hiyo maongezi hayo yakawa ushahidi wa wazi wa ‘Talqin’, (hasa kwa wale wanaodai kwamba kumsomea maiti ni bid’a, eti kwa vile maiti hasikii). Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa Imani ina daraja 10, na Salman yupo daraja la kumi, la juu kabisa, na kwamba ukiondoa Ahlul-Bayt hakuna sahaba aliyekuwa na hadhi kubwa kwa Mtume (s.a.w.w.) kama Salman, Abu Dharr na Miqdad. Rejea: (a) al-Majlisi, katika Bihar, Jz. 20 u.k. 189 & 198, na (b) katika Jz. 22 uk. 348. Salman, Miqdad na Abu Dharr: Imam Musa Kadhim (a.s.) alisema, “Siku ya Kiyama sauti itaita kwa niaba ya Mwenyezi Mungu kwamba: ‘Wako wapi ‘hawariyun’ na ‘Muuminin’ wa Muhammad bin Abdullah, waliosimama imara katika njia ya haki waliyoonyeshwa na Muhammad na hawakuvunja agano kwake?’ Kisha Salman Miqdad na Abu Dharr watasimama.’” Rejea: al-Majlisi katika Bihar, Jz. 22, uk. 342. Vile vile anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, “Mwenyezi Mungu ameniamuru kuwapenda masahaba zangu wanne ambao ni Ali Ibn Abi Talib, Salman, Miqdad na Abu Dharr.” Rejea: al-Majlisi katika Bihar, Jz. 22, uk. 321 & 325. Historia ya bwana Salman Farsi ni ndefu sana na ni kitabu kizima kinachoeleza mateso ya kutisha aliyoyapata akiutafuta Uislamu. Na hawa 136


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 137

katika Uislamu

mabwana Abu Dharr na Miqdad habari zao zimeelezwa humu katika sura zinazohusika. Bwana Ammar bin Yassir alitabiriwa na Mtume (s.a.w.w.) kuwa atauawa na kundi la waasi. Utabiri huo ulitimia alipouawa katika vita vya Siffin akiwa na umri wa miaka 90. Rejea: Sahihi al-Bukhari, Jz. 8 (Toleo la Misri) uk. 185-186. Sahih al-Tirmidh, Jz. 5, uk. 669 (Toleo la Misri). Hao ni baadhi tu, ya masahaba waongofu ambao hawatajwi sana.

HOJA ZA SUNNI KUHUSU UONGOZI WA WAISLAM BAADA YA MTUME (S.A.W.W.) Ndugu zetu Sunni wanaodai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hakuacha wasia, wanakubaliana na utaratibu wa Waislamu kuchagua kiongozi wamtakaye kuongoza Umma wa kiislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.). Hiyo ndiyo tofauti kubwa ya kiitikadi kati ya Shia Ithna’asheri na Sunni (Ahlul Sunna wal-Jamaa). Mara nyingi nimewasikia baadhi ya viongozi wa Sunni wakieleza kwamba wale viongozi wanne wa kwanza baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), wanaoitwa ‘Al-Khulafaau Rashidun’ walichaguliwa katika misingi ya Demokrasia ya kiislamu kuongoza Umma! Kuhusu viongozi wengine wa Sunni wanadai kuwa ulitumika utaratibu wa Shura kuchagua viongozi hao! Sababu kubwa ya Sunni kupendelea mfumo huo wa uongozi ni kwamba wao Sunni wanaona kuwa eti dini siyo kama ufalme1 kwa hiyo si lazima ukoo wa Mtume (s.a.w.w.) wa Bani Hashim uendelee kushika Ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. Kwa hiyo katika somo hili tutajadili hoja hizi tuone kama zinakubaliana na Qur’ani na Sunna au hapana; na kama zilitumika kweli kihistoria? Demokrasia ya kiislamu (Islamic Democracy): Matumizi ya neno ‘Democracy’ katika Uislamu siyo sahihi kwa sababu 1 Lakini Masuni hao hao wameutawalisha ukhalifa wa kifalme wa Bani Umayyahh na Bani Abbas, mara baada ya Al-Khulafaau Rashidun! 137


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 138

katika Uislamu

neno hilo kihistoria lilitafsiriwa na bwana Abraham Lincoln wa huko Marekani miaka 160 tu iliyopita kwamba ni: “Serikali ya watu, inayotokana na watu, kwa ajili ya watu.” Kabla ya enzi za Abraham Lincoln, neno hili halikutumika sana. Lakini Uislamu una miaka zaidi ya 1400 iliyopita! Sasa itakuwaje tuseme kuwa Makhalifa wanne wa kwanza walichaguliwa katika misingi ya demokrasia kushika Ukhalifa miaka 1400 iliyopita! Lakini hata kama neno hilo lingekuwa linatumika, ukweli ni kuwa: “Uislamu ni Serikali ya Mwenyezi Mungu, Inatokana na Mwenyezi Mungu, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu” - kama Qur’ani inavyotufundisha: (a) “Haiwi kwa muumini mwanamume au muumini mwanamke kuwa na khiari katika jambo, wakati Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao...” (Qur’ani 33:36). (b) “Sikuwaumba majini na binadamu ila waniabudu” (Qur’ani 51:56). Katika Aya hizi tutaona kuwa tunatakiwa kutii amri yoyote ya Mtume (s.a.w.w.) bila kusita iwapo kweli sisi tunajiita Waislamu (waumini). Niliyotangulia kueleza nyuma kuhusu wasia wa Mtume (s.a.w.w.) hayakutekelezwa! Katika Uislamu hakuna nafasi ya waumini kuamua watakayo kinyume na yaliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kwa hiyo kuingiza siasa za demokrasia katika dini ni sawa na kuwapa watu uhuru wa kumuasi Mwenyezi Mungu! Katika mfumo wa demokrasia kisiasa, watu wanaweza kuandamana kupinga serikali yao. Lakini binadamu hatuna uhuru wa kujadili amri yoyote ya Mwenyezi Mungu bali wajibu wetu ni utiifu Kwake na kwa wawakilishi Wake halali. Aya ya (51:56) inatutaka tumwabudu Mwenyezi Mungu. Kumwabudu Mwenyezi Mungu maana yake ni kumtii na kumtumikia kwa sababu ibada zote zinalenga katika kutekeleza amri za Mwenyezi Mungu. Aya ifuatayo ya Qur’ani inazidi kutufundisha kuwa hatuna madaraka yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu: (c) “Na Mola wako Huumba Alitakalo na Huchagua Alitakalo; wao viumbe hawana hiari ......”(Qur’ani 28:68). 138


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 139

katika Uislamu

Kwa hiyo mpaka hapa tumoeona kuwa demokrasia haina uhusiano wowote na dini. Isitoshe huko mbele tutaona kuwa hata kama tungehalalisha matumizi yake katika dini, ukweli ni kwamba hao Al-Khulafaau Rashidun hawakuchaguliwa na watu isipokuwa Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) peke yake! Jinsi walivyopata Ukhalifa mabwana Abubakr Sidiq, Umar Ibn alKhattab na Uthman Ibn Affan tutaona mbele. Kwa hiyo tunabakia na hoja ya matumizi ya utaratibu wa Mtume (s.a.w.w.) wa Shura. Kwa kifupi Shura maana yake ni utaratibu aliotumia Mtume (s.a.w.w.) kushirikisha watu katika kujadili mambo yanayohusu maisha ya kila siku ya watu, nayo uamuzi wa mwisho ulikuwa ni wa Mtume. Nina maana kwamba suala linalohusu maendeleo ya watu lilijadiliwa kwa kujumuisha wawakilishi wa watu wanaohusika, ili kufikia uamuzi muafaka. Lakini kama imeshuka Aya ya Qur’ani inawaamrisha watu labda kuswali Swala tano, hapo hakuna ‘shura’ yoyote ya kujadili kama watu waswali au wasiswali! Nina maana kuwa matumizi ya Shura siyo kujadili amri za Mtume (s.a.w.w.) au Mwenyezi Mungu! Kwa hiyo tumekwishaona huko nyuma kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliacha wasia juu ya Uongozi huo muhimu na kwa hiyo hakuna Shura yoyote iliyostahili kutumika! Zaidi ya hayo kumbukumbu za historia hazionyeshi kuwa ulitumika utaratibu wa Shura kuwapata viongozi hao! Sasa ndugu wasomaji turejee nyuma tuone kulitokea nini baada ya Mtume (s.a.w.w.) kurejea Madina toka Hijja yake ya mwisho, miezi mitatu tu kabla hajafariki. Lakini tutaanzia nyuma kidogo kuanzia pale mji wa Makka ulipotekwa na Waislamu, ili tuone mwenendo mzima wa baadhi ya masahaba waovu. Unafiki uliojificha: Hapa nataka kuonyesha kwamba pamoja na kupita muda mrefu wa miaka minane ya Uislamu hadi kutekwa Makka, bado masahaba kadhaa walikuwa hawajauamini Utume wa Nabii Muhammad (s.a.w.w.); bali walimwona kama mfalme mwenye nguvu! Uislamu katika kipindi cha baada ya kutekwa kwa mji wa Makka ni tofauti na kabla ya hapo. Kabla ya kutek139


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 140

katika Uislamu

wa Makka watu waliosilimu walivutiwa na ukweli wa Uislamu. Lakini baada ya kutekwa kwa mji wa Makka wengi wa watu walisilimu kunusuru mali zao na uhai wao baada ya kushindwa nguvu na Uislamu. Kwa hiyo wakalazimika kusilimu bila kuwa na imani katika Uislamu! Na huo ndio unafiki. Kwa mfano kila mara alisikika Abu Sufyan akisema kuwa hakuna Utume wowote wa Muhammad (s.a.w.w.) ila ni ufalme! Maneno hayo aliyasema tena wakati Makka ilipotekwa, pale ambapo Abu Sufyan alitoka Makka kuja kupeleleza nguvu ya jeshi la Mtume (s.a.w.w.). Ikawa Abbas amemwona akamkamata na kumpeleka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumshauri Mtume (s.a.w.w.) kuwa Abu Sufyan apewe kinga na heshima ili aingie Uislamu. Abbas akampeleka Abu Sufyan kukagua jeshi la Waislamu; na kuonyeshwa viongozi maarufu walio katika jeshi hilo waliotoka katika koo mbali mbali. Punde si punde akapita Mtume (s.a.w.w.) na kundi lake lililovalia sare za kijani. Pale pale Abu Sufyan akapiga ukelele akisema ‘Ewe Abbas, hakika ami yako (Mtume s.a.w.w.) amepata ufalme mkubwa!’ Abbas akajibu: ‘Aibu iwe juu yako! Huu siyo ufalme bali ni Utume!’ Huyu Abu Sufyan hakubadilisha msimamo wake kwani siku zilizofuata wakati Uthman Ibn Affan alipoupata ukhalifa, Abu Sufyan alimwendea na kumshauri, ‘Enyi Bani Umayyah, sasa ufalme umekuja kwenu (mmeupata). Uchezeeni kama watoto wachezeavyo mpira, na mpasiane (mpeane) mmoja baada ya mwingine katika ukoo wenu!’ Ndugu wasomaji hayo ndiyo maneno ya sahaba aliyejidai amesilimu miaka kumi nyuma! Kumbukumbu hizi tunazipata katika vitabu vifuatavyo: Sahih al-Bukhari - Jz. 5 uk. 191 Al-Bidayah wa’n-Nihayah - Ibn Kathir Jz. 5, uk. 40 Al- Mukhtasar - Abu’l Fida - Jz. 1, uk. 143 Tarikh Ya’qubi - Jz. 2, uk. 59 Kutokana na maelezo hayo, tutaona kuwa maadui wa Uislamu waliposhindwa kuupiga vita Uislamu wazi wazi, waliamua kujifanya wamesil140


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 141

katika Uislamu

imu ili wajiimarishe kichinichini, wakisubiri fursa ya kufanikisha azma yao. Kwa upande mwingine, wanafiki wa Madina ni wale ambao hawakuwa na imani na Utume, na badala yake waliona wamelazimika kuacha ibada zao za masanamu, na kupoteza maslahi yao ya kidunia ambayo Uislamu umeyazuia (umeyakataza). Wanafiki hao waliona kuwa uwezekano wa kufanikiwa kwao, ni pale ambapo Mtume (s.a.w.w.) atakapofariki. Kifo cha Mtume (s.a.w.w.) kilisubiriwa kwa hamu sana! Kumbukumbu za historia zinaonyesha kuwa baadhi ya masahaba wanafiki waliongozana na Mtume (s.a.w.w.) vitani ili wamuue huko! Kisa chenyewe ni kwamba safari moja wakirejea toka vitani, wanafiki walijaribu kujificha vichakani karibu na jabali mbele ya Mtume (s.a.w.w.) ili Mtume (s.a.w.w.) akifika mahali hapo, wamshitue ngamia wake atumbukie na Mtume (s.a.w.w.) katika genge la kina kirefu mahali paitwapo ‘Aqaba Dhil-Fitaq.’ Lakini njama hiyo haikufaulu kwa sababu Mwenyezi Mungu aliwahi kumfahamisha Mtume (s.a.w.w.) na hivyo kumwepusha ngamia wake kuelekea hapo! Aya ya Qur’ani niliyotangulia kuandika nyuma, yaani (Qur’ani 9:101) ilishuka kuhusiana na wanafiki hao waliodhani wanaweza kumwua Mtume (s.a.w.w.). Ni Jambo la kusikitisha kuona kuwa sahaba mmoja anayeheshimiwa sana na ndugu zetu Sunni alikuwemo katika kundi la hao waliopanga kumwua Mtume (s.a.w.w.)! Kumbukumbu hizi zinapatikana katika vitabu vifuatavyo: Maghaz - cha bwana Waqid Jz. 3, uk. 1042/1043 (b) Sirat al-Halabiya - cha Ali Ibn Halabi - Jz. 3, uk. 162 Njama za kuwang’oa Ahlul-Bayt (a.s.) mapema!: Hata hivyo wanafiki hao walifahamu fika, wasia wa Mtume (s.a.w.w.) pale Ghadiir Khum pamoja na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Watakuwepo Makhalifa 12 kutoka Bani Hashim baada yangu kuongoza 141


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 142

katika Uislamu

Umma wa Waislamu.” Kwa hiyo wanafiki hao waliona kuwa ni muhimu kuwang’oa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) kabla hawajaota mizizi imara katika Uongozi wa Umma wa Waislamu. Wanafiki hao walitambua kuwa wasipowang’oa Ahlul-Bayt (a.s.) mapema, kutatokea matatizo kwa sababu Waislamu waaminifu kwa Mtume (s.a.w.w.) hawatalipokea hilo kwa urahisi. Kwa hiyo walipanga mapinduzi hayo yafanywe na masahaba maarufu wenye heshima kuu mbele ya macho ya umma, ili kuyapa mapinduzi hayo sura nzuri. Lengo la wanafiki lilikuwa ni kuiteka na kuimiliki dola kubwa ya kiislamu kwa manufaa yao, kama tutakavyoona katika maelezo ya mbele. Matayarisho ya kwenda Tabuk: Mnamo mwezi wa Rajab mwaka wa 9 A.H. (630 A.D) Mtume (s.a.w.w.) alipata taarifa kuwa Warumi walikuwa wanakusanya majeshi yao kuvamia sehemu ya kaskazini ya Dola ya kiislamu inayopakana na dola ya Warumi ya wakati huo. Sehemu hiyo ilikuwa ni Ghuba ya Arabuni (Arabian Peninsula). Mtume (s.a.w.w.) aliamuru liundwe jeshi la kiislamu hapo Madina na maeneo ya jirani. Waislamu wengi walijiunga lakini wanafiki kadhaa walijitenga na kukataa kujiunga na jeshi, kwa visingizio kwamba ni mwendo mrefu na joto kali sana kufika huko. Ndipo ikashuka Qur’ani: “...Wakasema: ‘Msiende kwenye joto (kali).’ Waeleze: Moto wa jahannamu ni mkali zaidi kwa joto iwapo wangejua.” (Qur’ani 9:81). Wanafiki hao walibakia nyuma ili kuleta mapinduzi au ghasia mjini Madina baada ya kuondoka Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo Mtume aliarifiwa na Mwenyezi Mungu kuhusu njama hizo za wanafiki, kwa hiyo akamchagua Ali Ibn Abi Talib (a.s.) kubakia nyuma na kuihami Madina. Wanafiki hao walipojitokeza na kumkuta Imam Ali (a.s.) wakashindwa kutekeleza lengo lao. Habari hizi zinapatikana katika vitabu vifuatavyo: (a) Tarikh al-Tabari (b) Tarikh Abu al-Fida. 142


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 143

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) alitamani kushiriki jeshi hilo lakini Mtume (s.a.w.w.) alimwambia kuwa abakie Madina na kuongeza: “Huridhiki wewe kuwa ndugu yangu na kushika wadhifa kama ule wa Harun kwa Musa, isipokuwa kwamba hakuna Mtume baada yangu?” Kwa mara nyingine tunaona kuwa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa tayari ametajwa kuwa mrithi wa Mtume (s.a.w.w.) iwapo utazingatia uhusiano wa Harun na Musa ulivyokuwa kama nilivyouelezea huko nyuma. Katika tukio hilo la Tabuk vita havikupigwa kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) na jeshi lake walipofika huko wakakuta Warumi wamekwisharejea kwao kwa woga wa jeshi la Waislamu. Ndipo Mtume (s.a.w.w.) aliamua kutoingia kwao na hivyo kurejea Madina. Hapo ndipo iliposhuka Sura atTawbah. Na ndipo Mtume (s.a.w.w.) alipochoma moto msikiti wa Dhirar uliokuwa umejengwa na wanafiki wakiutumia kama kichaka cha kuficha njama zao za uovu. Kikundi kilichoutumia msikiti huo kilikuwa cha hao wanafiki waliokuwa na lengo la kudhoofisha Taifa la kiislamu.

Jeshi la Usamah bin Zayd: Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kutoa hotuba (wasia) yake ndefu pale Ghadiir Khum alirejea Madina na kukaa hapo hadi mwaka wa 10 A.H (631 A.D) ukaisha. Mwaka wa 11 A.H Mtume (s.a.w.w.) aliugua na ikawa wake zake wamemruhusu akae kwa mama Aisha. (Haya tunayapata katika Tarikh Abu al-Fida). Wakati Mtume (s.a.w.w.) anaendelea kuugua, aliamrisha liundwe jeshi likiongozwa na bwana Usamah Ibn Zayd; na kwamba jeshi hilo liende kupigana kuanzia Ubna kulipiza kisasi cha kuuawa pale kwa bwana Zayd Ibn Harithah katika vita vya Mau’tah. Aliamuru jeshi liondoke upesi na kushambulia kwanza watu wa Ubna kwa kuwasili pale mapema asubuhi kuliko ilivyotegemewa. Lakini baadhi ya masahaba hawakutii amri ya Mtume (s.a.w.w.) ya kuwataka kujiunga na jeshi chini ya bwana Usamah; kama walivyowahi 143


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 144

katika Uislamu

kupinga amri nyingine kama hiyo huko nyuma, ambapo waliamrishwa kuongozwa na bwana Zayd Ibn Haritha (baba yake Usamah). Masahaba hao wakorofi walimkashifu Usamah Ibn Zayd ingawa walishuhudia Mtume (s.a.w.w.) akimteua kuwa kiongozi wao! Vilevile walimshuhudia Mtume (s.a.w.w.) akiifunga bendera ya amiri jeshi kwenye nguzo kwa mikono yake ingawaje alikuwa anaumwa ana homa kali. Kisha Mtume (s.a.w.w.) akampa bendera hiyo bwana Usamah, lakini bado masahaba hao waliendelea kugoma! Ubishi huo uliongezeka na kumlazimisha Mtume (s.a.w.w.), akiwa amefunga kichwa na amejifunika shuka kutokana na homa kali, kutoka nyumbani kwake na kuingia msikitini. Siku hiyo ilikuwa ni Rabi’ul’Awwal tarehe 10, 11 A.H yaani siku mbili tu kabla hajafariki. Alipanda mimbari akamsifu Mwenyezi Mungu na kutoa hotuba ifuatayo: “Enyi watu wangu, nimesikia kwamba baadhi yenu mnapinga uchaguzi wangu wa Usamah kuwa kiongozi wenu amiri jeshi, kama mlivyowahi kupinga nilipomchagua baba yake kwa nafasi kama hii katika vita ya Mau’tah. Kwa jina la Mwenyezi Mungu, baba yake alikuwa anafaa kwa cheo hicho, na baada yake mtoto wake huyu vile vile anafaa kwa cheo hiki.” Mtume (s.a.w.w.) alizidi kuwahimiza masahaba kujiunga upesi na kuelekea Jarf kambini. Hata hivyo masahaba hao wakorofi waliendelea kugoma. Mwisho wake ikawa Mtume (s.a.w.w.) amemwomba Mwenyezi Mungu amlaani kila sahaba atakayeacha kutii amri hiyo ya Mtume (s.a.w.w.) ya kuwataka kujiunga na jeshi chini ya Usamah bin Zayd. Wakati wote huo Mtume (s.a.w.w.) alikwishamuamuru Imam Ali (a.s.) abakie naye pale pale Madina, wakati akiendelea kuugua. Mtume (s.a.w.w.) aliamuru jeshi hilo liondoke Madina kama njia ya kuwaondoa masahaba wakorofi ambao alishaona lengo lao la kuhakikisha kuwa Imam Ali (a.s.) hashiki uongozi huo baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. 144


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 145

katika Uislamu

Huko nyuma nimeeleza jinsi ambavyo ni lazima kumtii Mtume (s.a.w.w.) kwa ushahidi wa Qur’ani. Sasa hapa tunawaona hata masahaba wakuu wanakataa kumtii Mtume (s.a.w.w.)! Sababu walizotoa ni kwamba eti Usamah ni mtoto wa mtumwa aliyeachwa huru, kwa maana kwamba hao masahaba ni watu wa heshima kubwa ambao hawawezi kuongozwa na mtoto wa mtumwa aliyeachwa huru! Ndugu wasomaji hapa tunajiuliza kwamba, ina maana masahaba hao hawakufahamu (Qur’ani 49:13) maneno ya Mwenyezi Mungu kwamba wabora mbele Yake ni wale watimizao wajibu wao kwa Mwenyezi Mungu? Na kwamba kutimiza wajibu mbele ya Mwenyezi Mungu ni Kumtii Yeye na Mtume Wake? Zaidi ya hayo wakati huo Uislamu ulikuwa na miaka kumi na mmoja, na katika miaka hiyo Mtume (s.a.w.w.) alikwishafundisha mengi kuvunja ukabila na tabia za watu fulani kujiona watukufu kuliko wenzao. Lakini masahaba hao bado wanajitukuza na kumuasi Mtume (s.a.w.w.). Yote hayo ya kumuasi Mtume (s.a.w.w.) yalikuwa na lengo maalumu tutakaloliona katika matukio yafuatayo: Rejea: Sharh Nahj al-Balagha cha Ibn Abi alHadid Jz. 1, uk. 53 Toleo la Cairo 1329 A.H.

ALIPOKARIBIA KUFARIKI MTUME (S.A.W.W.) HADI KUFA KWAKE Wakati Mtume (s.a.w.w.) akiendelea kuugua, hali yake ilizidi kuwa mbaya na ikawa ameamuru aletewe vifaa vya kuandika wasia wa kuwaongoza Waislamu wasipotee au kupotezwa nyuma yake. Alisema: “Nileteeni karatasi na kalamu niwaandikie jambo ambalo kwalo hamtapotea kamwe baada yangu” Lakini Umar Ibn al-Khattab aliingilia kati na kukataza visiletwe na kusema, “Kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu, maradhi yamemzidi Mtume (s.a.w.w.) anasema maneno ya upuuzi.”1 Sahih Bukhari Jz.1, mlango - Kitaabul-Ilm na vingine vingi. 1 Wala hasemi kwa tamaa ya nafsi yake. Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa ...... (Qur’ani; 52: 3-4). Je! Ni kweli kwamba Aya hizi Umar na wenzie walikuwa hawazijui? 145


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 146

katika Uislamu

Hapo yalizuka mabishano makali miongoni mwa masahaba wanaotaka Mtume (s.a.w.w.) aletewe vifaa vya kuandika, na wale ambao wanakubaliana na maneno ya Umar Ibn Al-Khattab. Tumeona Umar na Abubakar walivyokataa kujiunga na jeshi chini ya Usamah bin Zayd hadi Mtume (s.a.w.w.) akawalaani! Sasa tunamwona Umar anakataza Mtume (s.a.w.w.) asiletewe vifaa vya kuandika wasia! Na yote haya yalitendeka katika siku zisizozidi tatu yaani karibu muda ule ule! Pana lengo gani hapa? Kabla sijaendelea ningeomba wasomaji tujiulize kwamba inawezekanaje Umar akadai kuwa Mtume (s.a.w.w.) anasema upuuzi? Hiyo ndiyo heshima ya sahaba mkuu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Isitoshe nimetangulia kueleza Qur’ani inasemaje juu ya kumtii Mtume (s.a.w.w.): “Na hatukumleta Mtume yeyote ila atiiwe kwa amri ya Mwenyezi Mungu...........” (Qur’ani 4:64). Inasikitisha pia kuona kuwa baadhi ya waandishi wa Hadithi (Muhadithun) kwa kulinda heshima ya Umar waliandika kuwa Umar alisema kuwa, ‘Mtume (s.a.w.w.) anaweweseka’. Ukweli ni kwamba Umar alitumia neno ‘Yah-jur’ ambalo maana yake ni upuuzi. Tutaona baadaye sababu za kuwatukuza baadhi ya masahaba na kuficha maovu yao. Kwa hiyo mabishano hayo yalipozidi na kelele zikapanda, ndipo Mtume (s.a.w.w.) alipowafukuza wote na kuamuru waondoke. Wakati huo Imam Ali (a.s.) alikuwa ametumwa, hakuwepo. Ndugu wasomaji hebu tuone tena Qur’ani inasemaje juu ya kitendo cha kupiga kelele wakati wa kuongea na Mtume (s.a.w.w.) au watu wanapokuwa mbele ya Mtume (s.a.w.w.):

146


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 147

katika Uislamu

“Enyi mlioamini msipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume wala msiseme naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi, visije vitendo vyenu vikakosa thawabu na hali hamtambui.” (Qur’ani 49:2). Iwapo kupiga kelele mbele ya Mtume (s.a.w.w.) kumekatazwa je, kumwambia Mtume (s.a.w.w.) kuwa anasema upuuzi? Jibu nawaachia wasomaji! Wewe msomaji hata kama huna elimu ya dini mwulize shekhe yeyote iwapo vitabu vyenye habari hizo vipo kweli na tunavitegemea? Pia mwulize iwapo hiyo aya niliyotaja hapo juu ipo kwenye Qur’ani? Kisha hapo na wewe utaamua mwenyewe. Haya tunayapata katika vitabu:(a) Sahih Bukhari - Jz. 3 (b) Sahih Muslim - Jz. 5 (c) Tarikh al-Tabari - Jz. 2 - uk. 436 Kwa maneno yake Umar hapo juu, alisema kuwa Qur’ani inatosha kwa maana kwamba aliyotaka kuandika Mtume (s.a.w.w.) si muhimu, Qur’ani inatosha. Sasa tutaona huko mbele kama kweli alitekeleza hukumu za Qur’ani kwa usahihi na uaminifu? Mara alipofariki Mtume (s.a.w.w.) ikawa watu wa familia yake wanatayarisha mazishi. Waislamu walikusanyika hapo kwa majonzi makubwa. Umar alisimama na kupiga ukelele kuwa, ‘Mtume hajafariki, atakayetamka kuwa kafariki atauawa kwa upanga!’ Umar aliendelea kudai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hatakufa mpaka dini yake ivunje dini zote na kwamba atarudi kuwakata mikono na miguu wale waliotangaza kuwa kafariki, yaani mfano wa tukio la wakati wa Nabii Musa (a.s.)! Ukitafakari matendo haya ya Umar yanavyofuatana, itabidi uwe na wasiwasi juu ya lengo lake kama tutakavyozidi kuona mbele. Kabla sijaendelea ningependa kusahihisha imani ya baadhi ya Waislamu kwamba eti Mtume (s.a.w.w.) alifia mikononi mwa mama Aisha! Kwa kadri ya vitabu sahihi vya historia ni kwamba, Mtume (s.a.w.w.) 147


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 148

katika Uislamu

alipokaribia kufariki, alimwambia binti yake, Bibi Fatima (a.s.) kwamba amletee wajukuu zake. Bibi Fatima (a.s.) aliwaleta Hasan (a.s.) na Husein (a.s.). Ndipo hao wajukuu zake wakamwamkia na wakaanza kulia kwa nguvu hadi na watu waliokuwepo wakaanza kulia. Ndipo Mtume (s.a.w.w.) akasema ‘Niitie ndugu yangu mpendwa Ali.’ Wakati huo Ali (a.s.) alikuwa bado hajarudi. Mtume (s.a.w.w.) alirudia hivyo mpaka mara ya tatu ndipo Ali (a.s.) akatokea na kukaa karibu yake upande wa kichwani. Mtume (s.a.w.w.) aliponyanyua kichwa kuangalia, Ali (a.s.) akashikilia kichwa na kukituliza kwenye paja lake. Mtume (s.a.w.w.) akaanza kumweleza kuhusu pesa alizochukua toka kwa Mayahudi fulani fulani kwa ajili ya jeshi la Usamah, na kwamba zirejeshwe. Kisha Mtume (s.a.w.w) akamweleza Ali (a.s.): “Ewe Ali utakuwa mtu wa kwanza kukutana na mimi Kawthar peponi na utapata matatizo makubwa baada ya kufariki kwangu. Itakubidi uwe mvumilivu na uwe na subira, na utakapowaona watu wanachagua tamaa ya dunia, wewe chagua akhera.” Kumbukumbu zinaonyesha kuwa masahaba walioshuhudia tukio hilo wanasema kuwa wakati Mtume (s.a.w.w.) akiwa katika maongezi marefu ya faragha na Ali (a.s.), wao waliondoka hapo chumbani na kuwaacha wawili. Baadaye masahaba walimwuliza Imam Ali (a.s.) ni kitu gani waliongea muda mrefu na Mtume (s.a.w.w.)? Imam Ali (a.s.) aliwajibu kuwa, ‘Mtume alinifundisha milango 1,000 ya elimu, na kila mlango ulinifungulia milango 1,000 ya elimu! Natumaini ndugu wasomaji Waislamu mnakumbuka Hadithi maarufu ya Mtume (s.a.w.w.) isemayo kwamba: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Lakini tujiulize swali tena, ‘Iwapo kuipata elimu ya Mtume (s.a.w.w.) inatubidi tupitie kwa Imam Ali (a.s.), mbona hakupewa nafasi ya kutuongoza mpaka baada ya kumdhalilisha kwa miaka 25 na hata hivyo pia akauawa kwa upanga wa sumu?’ Ni kitu gani kilichotokea hadi tukaacha kutekeleza wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Haya tunayapata katika vitabu vifuatavyo: (a) Kanz al -Ummal - Jz. 6, uk. 392 na Jz. 6, uk. 399 148


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 149

katika Uislamu

(b) Mustadrakul-Hakim. Kwa hiyo historia sahihi ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alifariki akiwa mikononi mwa Imam Ali (a.s.) na siyo mikononi mwa Mama Aisha. Tukirejea somo letu ni kwamba, baada ya Umar Ibn al-Khattab kuzuia mtu yeyote asitamke kuwa Mtume (s.a.w.w.) kafariki, watu wa familia ya Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wakishughulikia mipango ya mazishi! Kwa kadri ya maagizo ya Mtume (s.a.w.w.), alimweleza Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) kwamba, wote watakaoshiriki kumwosha, wafungwe vitambaa usoni isipokuwa Imam Ali (a.s.) peke yake. Kwa hiyo wakati wa kumwosha, masahaba waliokuwa wakipindua mwili wa Mtume (s.a.w.w.) ni mabwana Abbas, Fadhil, na Qasim. Waliomwagilia maji ni Usamah na Shaqran. Mwoshaji alikuwa ni Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) ambaye ndiye pekee aliyekuwa hakufunga kitambaa usoni. Mila ya Waarabu ya kiapo cha utii (Bay’at) Kabla sijaendelea na maelezo ya mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ningependa kwanza kuelezea mila ya siku nyingi ya Waarabu ya kiapo cha utii kwa mtu anayekusudiwa kuwa kiongozi wa ukoo au kabila. Ndiyo maana baada ya hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) pale Ghadiir Khum, watu walimwendea Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) na kumpa Baya’t baada ya Mtume (s.a.w.w) kumtangaza kuwa kiongozi wa kwanza baada yake. Ansari walishapata taarifa za Muhajirun, kutaka kuvunja kiapo cha utii kwa Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.), katika tukio la Ghadiir Khum, na hivyo kumnyang’anya Ukhalifa! Waliona kuwa iwapo Muhajirun ambao ndio waliokaribu na Mtume (s.a.w.w.) kwa ukoo, wameamua hivyo, basi ni bora huo ukhalifa wauchukue Ansar kwa sababu wao ndio waliopigana zaidi kulinda Uislamu. Ansar hao waliona kuwa kama si wao kutumia mali zao na nyumba zao kuwapokea Muhajirun walipofukuzwa Makka, 149


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 150

katika Uislamu

kusingekuwepo na sifa yoyote ya Muhajirun katika Uislamu. Ndugu wasomaji huko nyuma nimeelezea unafiki uliojificha, sasa tunaona unafiki unaanza kufichuka! Hakuna anayetetea wasia wa Mtume (s.a.w.w.)! Kwa hiyo viongozi na masahaba maarufu wa Ansari waliposikia habari za kifo cha Mtume (s.a.w.w.), walitoka na kukusanyika katika makao yao mahali palipoitwa Saqifah Bani Sa’ida ili wamchague khalifa na kumpa kiapo cha utii kabla ya ‘Muhajirun’ hawajapata nafasi hiyo! Kwa kawaida ya mila hiyo ya kiapo cha utii, ni kwamba hata kama watu wachache maarufu watampa mtu kiapo cha utii, itabidi waliobaki wote wamkubali na kutoa viapo vyao kwake kama kiongozi wao! Mila hii iliheshimiwa sana na Waarabu hata baada ya kuja Uislamu! Katika mkutano huo wa Saqifah, maili mbili tatu toka Madina, majadiliano yaliendelea. Wakati huo watu wengi pamoja na masahaba kama mabwana Ammar na Salman Farsi walikuwa katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) wakiomboleza. Kwa kawaida pale Saqifah hapakuwa mahali pa kujadili masuala ya Waislamu au masuala ya dini. Masuala ya dini yalijadiliwa kwenye msikiti wa Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo kikao hicho cha Saqifah kujadili suala la ukhalifa hakikuwa halali pamoja na ukweli kwamba kikao hicho hakikuwaalika masahaba wengineo maarufu kuhudhuria! Kuwasili kwa Bwana Abu Bakar Sidiq Kwenye Msikiti wa Mtume (s.a.w.w.). Muda wote tangu kufariki Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr Sidiq alikuwa nyumbani kwake huko Sanha, umbali wa kilomita sita toka Madina! Baadaye Abu Bakr akafika na kumnyamazisha Umar akisema kwa kukariri Qur’ani: “.......... Muhammad ni mjumbe wa (Mwenyezi Mungu); na wajumbe (mbali mbali) walipita kabla yake; je, akifa au akiuawa, mtarejea nyuma kwa visigino vyenu (katika ukafiri)?” (Qur’ani 3:144). Hapo ndipo watu walipoanza kusoma Aya hiyo, na ikawa Umar anapiga 150


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 151

katika Uislamu

mguu chini kama ishara ya mshagao wa ukweli wa Aya hiyo ya Qur’ani! Kwa hiyo Umar akatulia na kuacha madai ya kutaka kumuua atakayesema kuwa Mtume (s.a.w.w.) kafariki! Ndugu wasomaji ni vigumu kuamini kuwa sahaba mkuu kama Umar hakuwa mwenye kufahamu maneno hayo ya Qur’ani tukufu! – Ingawa alitamka kwamba ‘kinatutosha kitabu cha Allah’ hapo kabla. Baadhi ya wanahistoria wasio waaminifu, walijaribu kuhalalisha kitendo hicho cha Umar kuwazuia watu kusema kuwa Mtume (s.a.w.w.) kafariki, kwa madai kuwa Umar alikuwa na mapenzi makubwa kwa Mtume (s.a.w.w.) kwa hiyo alichaganyikiwa! Lakini matendo ya Umar katika siku tatu za mwisho za uhai wa Mtume (s.a.w.w.) na baada ya hapo, hayaonyeshi dalili yoyote ya kuchanganyikiwa! Katika maelezo ya mbele nitaleta ushahidi wa maneno yake mwenyewe kuhusu lengo lake kwa vitendo hivyo.

MKUTANO WA SAQIFAHH BANI SA’IDAH Masahaba waliokuwa katika mkutano wa Saqifah waliendelea na majadiliano. Ansari hao walimleta kiongozi wao bwana Sa’d Ibn Ubadah ambaye alikuwa anaumwa, akiwa amefunikwa nguo nzito anatetemeka kwa homa. Alikalishwa kwenye kiti cha enzi ili apendekezwe kuwa khalifa! Bwana Sa’d alitoa hotuba na kusema kuwa anatambua matendo mema waliyotenda Ansari na kwa hiyo ni bora wauchukue ukhalifa kabla yeyote hajauchukua! Ansari hao walikubali na wakamtaka yeye (Sa’d Ibn Ubadah) awe khalifa. Lakini wakatokea Ansari miongoni mwao wakajiuliza kwamba watawapa hoja gani Makureshi Muhajirun iwapo nao watadai ukhalifa? Mmoja wao akashauri kuwa kiongozi mmoja awe Ansari na mwingine awe Muhajirin! Bwana Sa’d Ibn Ubadah akasema: ‘Hiyo ni dalili ya kwanza ya kuonyesha udhaifu ambayo mmeionyesha.’ Kabla sijaendelea na maelezo ya mkutano wa Saqifah, kwanza turejee Madina katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.). Matayarisho ya mazishi ya Mtume (s.a.w.w.) yaliendelea na watu walizidi kumiminika kwa majonzi 151


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 152

katika Uislamu

kuomboleza msiba huo. Lengo la Umar kuzuia watu wasiseme kuwa Mtume (s.a.w.w.) amefariki, lilikuwa ni kuzuia watu wasijadili suala la wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya uongozi nyuma yake, ili mipango ya kunyakua uongozi huo ikamilike! Zaidi ya hayo, miezi mitatu nyuma ya hapo, Mtume (s.a.w.w.) alieleza wazi pale Ghadiir Khum kwamba hiyo ilikuwa ni Hijja yake ya mwisho na anakaribia kufariki. Hata kabla msafara wa Hijja hiyo haujaanza kuelekea Makka toka Madina, Mtume (s.a.w.w.) alitangaza wazi kuwa anakaribia kuodoka duniani na ndiyo maana watu wengi walitoka kuongozana na Mtume (s.a.w.w.) katika Hijja hiyo ya mwisho. Kwa hiyo hakuna sababu yoyote ya msingi kwa Umar kudai kuwa Mtume (s.a.w.w.) hajafariki! Kitendo cha Umar kuzuia Mtume (s.a.w.w.) asiweke wasia katika maandishi yake binafsi ni kwamba Umar na wenzake waliona kuwa kuwepo kwa maandishi ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya suala hilo kungeleta ugumu fulani kufanikisha mapinduzi hayo! Upo ushahidi wa kutosha kuthibitisha ukweli huu katika maelezo ya mbele kama tutakavyoona - Insha Allah. Tuwe na subira. Umar na Abu Bakr hawakushiriki mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Wakati Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) akiongoza matayarisho ya mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), macho ya Muhajirun yalikuwa makali kuchunguza kwa makini nyendo za Ansari. Sahaba mmoja (mtumwa aliyeachwa huru na bwana Abu Hudhayfa) jina lake Salim ndiye aliyekwenda mbio kumweleza Abu Bakr, Umar na Abu Ubayda kuhusu mkutano huo wa siri huko Saqifah. Baada ya kupata taarifa hiyo ya upelelezi, Abu Bakr, Umar na Abu Ubayda waliondoka haraka msikitini hapo bila kuwaarifu masahaba wenzao maarufu, na kuelekea Saqifah ili kuvuruga mipango na maamuzi ya Ansari, na kuwadhihirishia kuwa walikuwa wanafahamu kinachoendelea hapo 152


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 153

katika Uislamu

Saqifah Bani Sa’idah. Ndugu wasomaji hapa tena tunaona maajabu mengine! Abu Bakr na Umar walikuwa wanataka kuitwa masahaba wakuu na pia walikuwa wakwe zake Mtume (s.a.w.w.), kwa sababu Bibi Aisha ni binti yake bwana Abubakr Sidiq, na Bibi Hafsa ni binti yake Umar Ibn al-Khattab. Jambo la ajabu ni kuwaona wanaondoka msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) bila kushiriki mazishi wala mipango ya mazishi (ya mkwe wao)! Iwapo mabwana hawa waliona ndio wanaostahili uongozi baada ya Mtume (s.a.w.w.), kwa nini wasifanye heshima ya kushiriki mazishi ya Kiongozi wao mkuu? Au kwa nini wasishiriki mazishi ya mkwe wao? Picha kama hii inaonyesha sura gani kwa watu? Pana njama gani hapa? Kwani hata katika wakati wetu huu, hatujapata kusikia kuwa mfalme fulani kafariki, lakini mawaziri wake fulani ndio kwanza wanaondoka kwenda safari kikazi au kibinafsi, bila kwanza kuhudhuria mazishi ya Kiongozi wao mkuu! Kwa kweli hata sisi wakazi wa mijini, haiwezekani jirani yako akafariki na wewe ukaacha makusudi kushiriki mazishi yake! Lakini hata kwa Mwislamu yeyote mwaminifu wa kawaida, ni lazima atambue utukufu mkubwa wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya Waislamu, na kwa hiyo asingetegemewa kufanya vitendo kama hivyo! Punde si punde mara Abu Bakr na Umar wakawasili Saqifah wakakaa kwenye viti. Bwana Thabit Ibn Qays alisimama na kuanza kutaja sifa za Ansari na kusisitiza kuwa ni muhimu ukhalifa uchukuliwe na Ansari. Umar alitaka asimame kutoa hoja lakini Abu Bakr akamuashiria kukaa chini na kunyamaza. Kisha Abu Bakr alisimama na kuhutubia mkutano kuwa: ‘Enyi Ansari tunakubaliana na sifa zenu nzuri na matendo yenu mema. Wala hatujasahau harakati zenu za kujitoa mhanga kusimamisha Uislamu. Lakini hadhi waliyo nayo Quraish miongoni mwa Waarabu ni kubwa kuliko makabila yote ya kiarabu na Waarabu wote ni lazima wawe watiifu kwa Quraish.’ Haya yanapatikana katika vitabu vifuatavyo: As-Sirah – cha al-Halabi Jz. 3, uk. 357 Tarikh at-Tabari - Jz. 3, uk. 208 153


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 154

katika Uislamu

Baada ya hotuba hiyo ya Abu Bakr, kulizuka mabishano makali, ambapo Umar alipiga ukelele na kusema, ‘Kwa jina la Allah nitamwua yeyote atakayetupinga mimi na Abu Bakr.’ Sahaba mmoja Ansari ukoo wa Khazraj jina lake al-Hubab Ibn al-Mundhir Ibn Zayd alisimama na kumpinga Abu Bakr akisema, ‘Kwa jina la Allah hatutamwachia yeyote kutawala kama khalifa; bali ni lazima kiongozi mmoja atoke kwetu na mwingine atoke kwenu washirikiane katika ukhalifa.’ Hapo Abu Bakr akajibu, ‘Hapana, haiwezekani; ni haki yetu kutawala, na ninyi muwe mawaziri.’ Bwana al-Hubab akasema, ‘Enyi Ansari, msikubali wanayodai hawa, kuweni imara; kwa jina la Allah kama mmoja wenu atanipinga, sasa hivi nitafyeka pua yake kwa jambia langu.’ Ndipo Umar akajibu kuwa, ‘Kwa jina la Allah haiwezekani kushirikiana Ukhalifa watu wawili. Hawawezi kuwepo wafalme wawili katika nchi moja! Na Waarabu hawatakubali uongozi wenu kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) hakutoka katika kabila lenu.’ Katika Tarikh al-Tabari na Tarikh al-Kamil cha Ibn al-Athir, wanaeleza kuwa kulikuwepo mabishano marefu hadi Umar akamlaani Al-Hubab kwa kusema ‘Mola akuulie mbali.’ Naye Al-Hubab akamjibu hivyo hivyo. Ndipo Umar akasogea na kusimama kwa bwana Sa’d Ibn Ubadah na kumwambia, ‘Tunataka tukuvunjevunje kila kiungo chako.’ Akiwa amekasirika kwa maneno hayo ya Umar, bwana Sa’d Ibn Ubadah alinyanyuka huku anaumwa, na akavuta ndevu za bwana Umar! Umar alikasirika na kusema, ‘Ukingo’a japo udevu mmoja utanitambua leo.’ Lakini Abu Bakr alimsihi Umar kuwa mtulivu. Ndipo Sa’d akajibu, ‘Kama ningekuwa na nguvu leo japo ya kusimama tu, wewe Umar ungewasikia simba wakinguruma kila pembe ya Madina na ungetamani kujificha kwenye shimo!’ Haya tunayapata katika historia katika kitabu Al-Imamah was-Siyasah cha bwana Ibn Qutaybah, Jz. 1.

154


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 155

katika Uislamu

Kwa kadri ya maelezo ya Ibn Qutaybah ni kwamba kufikia hapo, bwana Bashir Ibn Sa’d, chifu wa Ansari ukoo wa Aws alipoona Ansari wanaungana kwa mshikamano chini ya chifu wao Sa’d Ibn Ubadah wa ukoo wa Khazraj, aliona wivu sana kwamba huenda wakafanikiwa kunyakua Ukhalifa. Kwa hiyo Bashir Ibn Sa’d aliamua avunje mshikamano wa Ansari kwa kuwaunga mkono Muhajirun. Kuhusu uhasama kati ya koo mbili za Ansari yaani Aws na Khazraj ni kwamba ni wa siku nyingi. Wakati fulani katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.), koo hizi mbili zilidumisha uadui, kiasi kwamba waliwahi kukusanya majeshi yao, ili wapigane mbele ya Mtume (s.a.w.w.) lakini aliingilia kati na kuwazuia. Haya tunayasoma katika Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 16 na Jz. 3, uk. 34. Na hiyo ndiyo sababu ya kushuka Aya (Qur’ani 49:9) kihistoria. Baada ya Umar kuwaona Ansari wamegawanyika kwa njia ya kuchochea uhasama wao wa asili, Umar alisimama na kumwambia Abu Bakr: ‘Nyosha mkono wako nikupe kiapo cha utii (Bay’at)! Abu Bakr akasema ‘Hapana nyosha wewe nikupe Bay’at kwa sababu wewe ni mwenye nguvu kunizidi na inafaa uwe khalifa.’ Umar alichukua mkono wa Abu Bakr na kumpa Bay’at akisema, ‘Nguvu zangu hazina thamani yoyote ukilinganisha na matendo yako mema pamoja na kunizidi cheo. Na kama nguvu zangu zina thamani, zikiongezwa juu ya sifa zako, kwa pamoja tutafanikisha ukhalifa wako.’ Wakati huo huo kiongozi (chifu) wa kabila la Aws bwana Bashir Ibn Sa’d aliamka na kutoa Bay’at kwa Abu Bakr. Lakini ukoo wa Khazraj walimlalamikia Bashir Ibn Sa’d kwamba amefanya hivyo kwa kumwonea wivu Sa’d Ibn Ubadah asipate ukhalifa. Ukoo wa Aws walishauriana kwamba iwapo Sa’d Ibn Ubadah angepata ukhalifa, ukoo wa Khazraj wangejivuna sana na kujiona bora kwa Aws na hapana Aws ambaye angepata hadhi hiyo. Kwa hiyo Aws wakaona bora wampe Bay’at Abu Bakr. Mtu mmoja kutoka Khazraj alichomoa jambia lake lakini akazidiwa nguvu. 155


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 156

katika Uislamu

Wakati migogoro yote hii inaendelea hapo Saqifah, matayarisho ya mazishi ya Mtume (s.a.w.w.) yalikamilika na ikawa amezikwa. Mara tu baada ya mazishi ya Mtume (s.a.w.w.), ghafla watu walisikia Takbira kwa sauti kubwa katika kundi kubwa la watu waliomzunguka Abu Bakr wanampa mikono ya Bay’at kama khalifa! Ndugu wasomaji hivyo ndivyo bwana Abu Bakr alivyopata ukhalifa! Baadhi ya Waislamu hudai kuwa kama Abu Bakr hakuwa na haki ya ukhalifa, kwa nini Waislamu wengi walimwunga mkono? Hoja hii inatupatia mwangaza kudhihirisha kuwa ni kweli masahaba wengi sana walikuwa wanafiki! Kwa sababu tumeona huko nyuma katika hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) hapo Ghadiir Khum, ameeleza kuwa alikuwa amesita kuwaeleza watu amri hiyo ya Mwenyezi Mungu kwa sababu kulikuwepo na wanafiki na wapinzani wengi ambao hawakutaka kusikia Imam Ali (a.s.) anashika uongozi huo! Wapinzani hao walikuwa watu waovu sana kiasi kwamba Mwenyezi Mungu alimhakikishia ulinzi Mtume (s.a.w.w.), (Qur’ani 5:67). Rejea: Sura ya 2 chini ya Hadithi ya Tano. Maana yake ni kwamba hata pale pale Ghadiir Khum kulikuwepo na wanafiki wengi. Zaidi ya hayo tukirejea Sura ya 2 chini ya Masahaba waadilifu na wanafiki tunakuta maelezo na ushahidi mwingi wa masahaba wengi wanafiki. Kwa hiyo sioni ajabu pale alipofariki Mtume (s.a.w.w.), kuwaona wanafiki wote wanajitokeza wazi kupinga Imam Ali (a.s.) asiwe khalifa! Pana ugumu gani kuelewa suala hili? Mtu mmoja alimwuliza Mtume (s.a.w.w) kuhusu uwiano kati ya watu wa motoni na watu wa peponi, ambapo Mtume (s.a.w.w.) alijibu kuwa, ‘Mfano wake ni sawa na ng’ombe mmoja mnene mweusi mwenye unyoya mmoja mweupe.’ Kwa maana kuwa manyoya meusi ndio watu wa motoni, na unyoya mmoja mweupe ndio watu wa peponi! Sidhani kuwa kuna mtaalamu yeyote enzi hizi za teknolojia ya kompyuta, ambaye anaweza kuhesabu manyoya ya ng’ombe mmoja!

156


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 157

katika Uislamu

Mfano huo unaonyesha wazi kuwa binadamu tunakabiliwa na balaa kubwa kama tusiposahihisha itikadi zetu potofu. Mfano huo hautofautiani na maneno mengine ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuwa, “Umma wangu baada yangu utagawanyika katika makundi 73 hadi Siku ya Kiyama, na makundi yote yataangamia motoni isipokuwa kundi moja tu ndilo litakalonusurika (likiwa katika haki).” Wingi si hoja katika dini. Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) na ukoo wa Bani Hashim walipigwa na mshangao mkubwa kuona Waislamu wanakiuka wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya ukhalifa! Wakati huo Umar Ibn al-Khattab alikuwa mbele ya umati wa watu akiwahimiza wamtambue Abu Bakr na kumpa Bay’at kama khalifa, huku akizungusha fimbo yake mikononi. Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) na masahaba wachache waaminifu wafuasi wake, walishuhudia mapinduzi hayo ya kusikitisha! Haya tunayasoma katika: Tarikh at-Tabari - chini ya Kifungu cha Saqifah. Ningependa kufafanua kwamba asili ya wafuasi wa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) kuitwa Shia ni pale ambapo Jabir Ibn Abdullah al-Answar anamkariri Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba huyu Ali na wafuasi wake (Shia) wataokolewa Siku ya Kiyama, na Mwenyezi Mungu ataridhika nao.” Lakini mwanzo kabisa wa ‘Shia’ ni pale ambapo Mtume (s.a.w.w.) alipowataja Ahlul-Bayt (a.s.) wake kuwa viongozi wa Waislamu nyuma yake. Hapo ndipo masahaba na Waislamu wote waaminifu walipoanza kuwafuata Ahlul-Bayt (a.s.) na kuwategemea kama Viongozi wa Umma wa kiislamu. Tumeona pale Ghadiir Khum Umar anatoa Bay’at kwa Imam Ali (a.s.), lakini Umar huyo huyo anavunja kiapo hicho na kumsimika Abu Bakr kuwa khalifa pale Saqifah! Kwa hiyo tutaona kuwa pale alipofariki Mtume (s.a.w.w.), Waislamu wengi waliangukia kumkubali Abu Bakr kama khalifa. Waislamu wachache sana walibakia waaminifu kwa Imam Ali (a.s.) na hao ndio Shia wa kweli wa mwanzo, na inakadiriwa kuwa hawakuzidi asilimia kumi ya Waislamu wote wa wakati huo! Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) 157


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 158

katika Uislamu

niliyotaja hapa juu kuhusu wafuasi wa Imam Ali (a.s.), inapatikana katika vitabu vya:Al-Durr al-Manthur fiy al-Tafsir bi-al Ma’thur, cha as-Suyuti, toleo la Cairo, mwaka 1313 A.H. Jz. 6, uk. 379 pia kitabu cha Ghayat al-Maram, uk. 326.

DEMOKRASIA AU SHURA? Huko nyuma nimetangulia kueleza msimamo wa Sunni kuhusu mfumo uliotumika kumchagua khalifa wa kwanza, wa pili na wa tatu. Tumeona kuwa baadhi ya mashekhe wanadai kuwa ilitumika Shura. Wengine wanadai kuwa ilitumika Demokrasia ya kiislamu! Hoja zote mbili nimezikataa kwa ushahidi wa Qur’ani na historia sahihi ya Uislamu. Zaidi ya hayo katika Sura ya saba nimeelezea jinsi Abu Bakr alivyopata ukhalifa pale Saqifah Bani Sa’idah. Hata kama tungekubaliana na matumizi ya ‘Demokrasia ya kiislamu’ katika dini, sidhani kama kuna demokrasia iliyotumika pale Saqifah kwa sababu watu wengi sana au tuseme Waislamu wote na sahaba wengi sana maarufu, walikuwa kwenye msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) wakisubiri mazishi ya kiongozi wao mpendwa. Demokrasia katika misingi ya kisiasa, hushirikisha watu wote na hutegemea maamuzi ya walio wengi. Lakini hapo Saqifah hatuoni ushirikishwaji wa watu wengi! Tukijadili hoja ya Shura hatuoni ushahidi wowote wa kujumuika kwa wawakilishi wa Waislamu kutoka sehemu mbali mbali za taifa kubwa la kiislamu la wakati huo! Kwa kweli hata masahaba maarufu kama Ali Ibn Abi Talib, Abbas, Usama bin Zayd, Az-Zubair, Salman Farsi, Abu Dharr al-Ghifari, Miqdad Ibn al-Aswad, Ammar Ibn Yasir, Hudhaifa Ibn alYaman, Khuzayma Ibn Thabit, Abu Burayd al-Aslami, Al-Buraa Ibn Azib, Abu Kaab, Sahl Ibn Hanif, Qays Ibn Saad, Abu Ayyub al-Ansari, Jabir Ibn Saad, Khalid Ibn Saad n.k. Hawa wote pamoja na umaarufu wao hawakuwepo Saqifah! Sasa hayo matokeo ya Saqifah yatachukuliwaje kuwa katika misingi ya Shura?

158


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 159

katika Uislamu

Kuna hoja nyingine ya ndugu zetu Sunni kwamba Abu Bakr Sidiq alichaguliwa na Mtume (s.a.w.w.) kuongoza Swala badala ya Mtume (s.a.w.w.); usiku wa kuamkia kufariki kwake, kwa hiyo uchaguzi huo wa kuongoza Swala unamhalalisha kuwa khalifa! Ukweli ni kwamba Abu Bakr alitaka kuswalisha Swala hiyo usiku huo, kutokana na Mama Aisha kupotosha agizo sahihi la Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliagiza Imam Ali (a.s.) aswalishe Swala hiyo. Lakini kutokana na chuki ya muda mrefu ya Mama Aisha dhidi ya Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.), aliamua kumwita baba yake badala ya Imam Ali (a.s.)! Hata hivyo kabla Swala hiyo haijafika popote, Mtume (s.a.w.w.) alipata habari za Abu Bakr kuongoza Swala hiyo, akakasirika na kuamka na maumivu yake, akakatisha Swala hiyo na kumkemea kwa kusema, ‘Wewe Aisha ni sawa na wale wanawake waliomdanganya Nabii Yusuf.’ Tukirejea niliyoyaeleza nyuma ni kwamba huo wakati unaodaiwa Abu Bakr kuongoza Swala, ni wakati bwana yeye alitakiwa kuwa katika jeshi chini ya Usamah kwa amri ya Mtume (s.a.w.w.). Na kama tulivyokwishaona, bwana Abu Bakr alikataa kujiunga na jeshi hilo na ikawa Mtume (s.a.w.w.) amewalaani wote waliokataa kujiunga na jeshi! Kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) asingemwita Abu Bakr ambaye hata hivyo alishakiuka amri ya Mtume (s.a.w.w.) bila sababu za msingi. Habari hizi tunazipata katika: Kanzul - Ummal - Jz. 5, - uk. 312 Sahih Bukhari - Jz. 1, - uk. 7 Sahih Muslim - Chini ya Uimamu Sharh Ibn Abi al-Hadid - Jz. 1, uk. 53, chapa ya Cairo mwaka 1329 A.H

Sababu za kumpindua Imam Ali (a.s.) zatajwa: Sahaba mmoja bwana Ibn Abbas alipinga vikali kitendo cha kukiukwa wasia wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imam Ali (a.s.). Sahaba huyo alimwuliza Umar kwa nini walimzuia Imam Ali (a.s.) kushika uongozi huo? Umar alijibu kuwa, ‘Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu kwamba Ali (a.s.) alistahiki kabisa kuwa kiongozi lakini tulimsukuma pembeni kwa sababu nne’: 159


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 160

katika Uislamu

Alikuwa kijana mno (alikuwa na umri wa miaka 33 alipofariki Mtume (s.a.w.w.) Ni kizazi cha Abdul-Muttalib ( Bani Hashim) Waarabu hawakupenda kuona Utume na Ukhalifa unatoka Bani Hashim peke yake!1 Naapa kwamba Ali (a.s.) angestahiki uongozi huu lakini Quraysh wasingevumilia utawala wake kwa sababu angewalazimisha watu kufuata ukweli mtupu na njia iliyonyooka. Chini ya uongozi wake, watu wasingeweza kuvuka mipaka ya haki na kwa hiyo wangejiunga na kuanzisha vita vya kumpinga! Haya tunayapata katika vitabu vifuatavyo: (a) Sharkh Ibn Abil-Hadid Jz.1 uk. 134 , (b) Tarikh Yaqubi - Jz. 2 uk. 137. Ndugu Waislamu, sababu hizo 4 alizotoa Umar ni maneno yake binafsi na siyo maneno ya Mtume (s.a.w.w.) wala siyo Qur’ani. Maneno ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Uongozi huu yapo. Sasa kwa nini tufuate maneno ya Umar na kuyaacha yale ya Mtume (s.a.w.w.)? Zaidi ya hayo tunaelewa kuwa maneno ya Mtume (s.a.w.w.) ni maneno ya Mwenyezi Mungu. Maneno ya Mtume (s.a.w.w.) na maneno ya Mwenyezi Mungu hayawezi kujadiliwa na watu ila kuyatekeleza tu (Qur’ani: 4:64, 33:36 ). Sababu hizo alizotoa Umar zinaonyesha wazi kuwa masahaba wengi walikuwa wanafiki; kwa sababu Umar anaeleza kuwa Quraysh hawakutaka kutawaliwa na hukumu za Mwenyezi Mungu, bali walitaka kujitawala na kuvuka mipaka! Na kwamba walikuwa tayari kumpiga vita Imam Ali (a.s.), ili asiuongoze umma katika misingi ya haki! Wote hao ni masahaba! Je, tuwaweke kundi gani hao wanaojiita Waislamu lakini hawataki kuongozwa na sheria za Mwenyezi Mungu? Waislamu tusidumishe kuwatukuza masahaba kinyume na kauli zao wenyewe! Kauli zao hizo zinapatikana katika historia ya Uislamu. 1 Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kutoka na fadhila Zake? Hakika tumewapa kizazi cha Ibrahim Kitabu, na hekima na tukawapa mamlaka makubwa! (Qur’ani; 4:54) – Je! Sababu hizi, 2 na 3, hazipingani na Aya hii? Au Aali Muhammad sio Aali Ibrahim?! 160


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 161

katika Uislamu

Isitoshe tukijadili hoja hizi tutaona kuwa hazina maana yoyote kwa sababu madai ya kuwa Imam Ali (a.s.) alikuwa mdogo (miaka 33) hayana uzito kwani tunaona hata hivi leo kisiasa hapa duniani, kijana wa umri huo au chini ya hapo, anaweza kuwa kiongozi kama mbunge mradi achaguliwe kwa kura za kutosha. Wakati huo huo historia za vita vya ‘Jihad’ zinaonyesha kuwa hapakuwepo shujaa mkubwa kama Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) kwa kadri ya maelezo yanayofuata kuhusu vita hivyo. Kwa hiyo hata katika historia za ufalme tutaona kuwa ushujaa ulikuwa ni sifa mojawapo ya kutosha kumpa mtu ufalme. Sababu nyingine alizotoa Umar ni za misingi ya ukabila ambao ni kinyume kabisa na mafunzo ya Uislamu. Mbali na Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) nilizozitaja nyuma juu ya Imam Ali (a.s.), ningependa kuongeza maelezo muhimu juu ya ushujaa wa Imam Ali (a.s.) katika vita vya Jihadi. Katika vita hivyo hakuna sahaba aliyeonyesha ushujaa kama Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.). Ushujaa ni sifa kuu ya kiongozi.

Nasaba yake: Uhusiano wake na Mtume (s.a.w.w.) ni babu yao mzaa baba yaani bwana Mtukufu Abdul Muttalib bin Hashim.

Kuzaliwa kwake: Alizaliwa ndani ya Al-Kaaba tarehe 13 Rajab mwaka 600 A.D (Kabla ya Hijriya). Nimewasikia mashekhe kadhaa wasio na elimu ya historia sahihi, wakikanusha ukweli na utukufu wa Imam Ali (a.s.) kuzaliwa ndani ya AlKaabah!

Jina lake: Wakati anazaliwa Imam Ali (a.s.), Mtume (s.a.w.w.) hakuwepo Makka, na aliporudi akakuta Imam Ali (a.s.) ameshazaliwa na kupewa majina ya Asad na Haydar na mama yake. Baba yake Mzee Imran (Abu Talib) naye alishampa jina la Zayd. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa kaamrishwa na Allah kumpa jina la Ali ambalo lina maana ya 161


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 162

katika Uislamu

‘Aliyetukuka zaidi’. Soma Sherkhe Sahih al-Bukhari ya Imam Nuudi, pamoja na kitabu cha Tadhkrat-ul-Khawas cha Ibn Jawzii.

Sifa zake: Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Wako watu watatu walioitikia miito ya Mitume watatu bila kusitasita, na watu hao hawakuwahi kumwabudu yeyote asiyekuwa Allah japo kwa muda mdogo kama kupepesa kope ya jicho nao ni: Yusha bin Nun aliyemwamini Nabii Musa (a.s.), Sahib Yasin aliyemwamini Nabii Isa (a.s.) na Ali Ibn Abi Talib aliyemwamini Mtume Muhammad. Watu hawa wameandikwa huko mbinguni kuwa ni Sidiq na miongoni mwao Ali yu wa juu zaidi’. (Habari hizi zinapatikana katika kitabu cha Tafsir Tha’laby).

Malezi yake: Alilelewa, akalishwa na kukogeshwa na Mtume (s.a.w.w.). Pia akimvisha nguo na kwenda naye Mlima Hira kufanya ibada. Uliposhuka ufunuo (wahyi) wa kwanza, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na Ali (a.s.) humo pangoni (Soma Nahjul-Balaghah) na alikuwa mwanamume wa kwanza kupokea Uislamu. Kabla ya hapo, ni sahaba pekee ambaye hakuwahi kusujudia sanamu wala kunywa pombe na ndiyo maana anapotajwa jina lake tunasema,. Karramallahu Wajhahu ‘Uso wake Allah umeutukuza’.

Tabia zake: Ukweli, ukarimu, ushujaa, uaminifu, huruma, uchamungu, ni baadhi tu ya sifa zake njema.

Ali (a.s.) katika vita vya Badr: Hivi ni vita vya kwanza vya Jihad vilivyopigwa mnamo tarehe 17 Ramadhan mwaka wa 2 A.H (624 A.D). Katika vita hivi Mwenyezi Mungu aliteremsha Malaika kuwasaidia Waislamu kwa sababu maadui wa Waislamu walikuwa wengi (Qur’ani 8:9) Mwenyezi Mungu aliwapa ushindi Waislamu. Katika vita hivyo waliuawa makafiri 70 kati ya hao 36 waliuawa na Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) peke yake! Huu ni muujiza kwa mtu mmoja kuwa na ushujaa wa namna hii. Imam Ali (a.s.) hakuwa sawa 162


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 163

katika Uislamu

na sisi binadamu wa kawaida kama nilivyoeleza nyuma sifa za Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) (Qur’ani 33:33). Ali (a.s.) katika Vita vya Uhud: Katika makafiri 70 waliouawa katika vita vya Badr, wengi wao walikuwa machifu wakuu wa Quraish. Kwa hiyo katika vita vya Uhud, Quraish wakiongozwa na chifu wao mpya Abu Sufyan bin Harb walitaka kulipiza kisasi. Vita hivi vilikuwa Madina tarehe 11 Shawwal mwaka wa 3 A.H (625 A.D.). Katika vita hivi wapiganaji halisi wa kiislamu walikuwa 700 kwa sababu wanafiki 300 walijiengua wakiongozwa na Abdullah bin Ubayy bin Salul. Makafiri wapiganaji walikuwa 3000. Katika vita hivi Mtume (s.a.w.w.) alichagua kundi fulani la askari wake na kuwaweka mahali fulani mlimani ili makafiri wasije wakawazunguka na kuwashambulia kwa nyuma. Lakini askari hao wakakiuka amri hiyo kwa tamaa ya ngawira ambazo wenzao walikuwa katika nafasi bora zaidi ya kuzipata. Kwa hiyo wakaondoka hapo kinyume na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matokeo yake makafiri wakajipenyeza hapo hapo na kushambulia kwa nyuma. Waislamu wakakimbia na kumwacha Mtume (s.a.w.w.) ambaye alishambuliwa akiwa na askari wachache kama Imam Ali (a.s.), ammi yake (Hamza) na Mus’ab bin Umair. Mtume (s.a.w.w.) alilengwa na jiwe likampiga na kumchana mdomo na kuvunja meno mawili, kisha akapigwa mshale wa chuma ukakwama usoni na akatoka damu nyingi. Katika vita hivyo, baadhi ya masahaba wakuu walikimbia vita baada ya makafiri kupenya ngome ya Waislamu. Uvumi ulizagaa kuwa Mtume (s.a.w.w.) ameuawa ndiyo maana masahaba fulani wakaona bora waondoke vitani kama kwamba Dini nayo imekufa! Ukweli ni kuwa Mtume (s.a.w.w.) alizidiwa akazimia kutokana na majeraha. Bwana Hamza Ibn Abdul-Muttalib aliuawa na mtu aliyeitwa Wahshi mtumwa wa Abu Sufyan. Rejea: Tarikh Tabari na Tarikh Khamis.

163


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 164

katika Uislamu

Wakati huo, Hind mke wa Abu Sufyan alikuwa akiwahimiza makafiri kushambulia Waislamu kwa kuwaimbia nyimbo za kuwatia hamasa. Mama huyu katili, aliamuru tumbo la bwana Hamza lipasuliwe na akakata maini na kuanza kuyatafuna! Kisha alikata pua na masikio na kuyavaa shingoni kama mkufu lakini alitapika maini hayo. Baadaye baadhi ya Waislamu waliokimbia vita walirejea na kujiunga tena huku Imam Ali (a.s.) akipigana kwa ushujaa kumlinda Mtume (s.a.w.w.) wakati wote. Siku iliyofuata Mtume (s.a.w.w.) alimpa Imam Ali (a.s.) bendera ya Uislamu na kuamuru Waislamu na majeraha yao wawafuate makafiri. Lakini Waislamu walipofika Hamraul-Asad walikuta Abu Sufyan na jeshi lake wamesharejea Makka. Hivyo nao wakarejea Madina na Mtume (s.a.w.w.). Katika vita hivyo waliuawa mashuja wa kikafiri 103 na kati yao, 28 waliuawa na Imam Ali (a.s.) peke yake.

Ali (a.s.) katika vita vya Khandaq: Vita vya Uhud havikuwapa ushindi makafiri na kwa hiyo wakatayarisha vita vingine vya Khandaq ambavyo vilipikuwa Madina mnamo tarehe 23 Dhul-Qaad mwaka wa 5 A.H (627 A.D). Asili ya vita hivi ni pale ambapo wayahudi walitaka kuungana na makafiri kumpiga vita Mtume (s.a.w.w.). Ndipo ikashuka Aya ya Qur’ani 4:51. Wayahudi walifanikiwa kuwapata makabila ya Bani Fazarah, Ashja, Murrah, Salim, Bani As’ad n.k. Chini ya uongozi wa Abu Sufyan bin Harb al-Amawi, makafiri 10,000 walikusanyika na kuelekea Madina. Lakini Mtume (s.a.w.w.) aliamua kubakia Madina na kuihami. Mashariki na Magharibi mwa Madina, nyumba zilijengwa karibu karibu kama ngome. Kusini mashariki ya mji, waliishi wayahudi wa Bani Quraidha ambao walikuwa na mkataba wa amani na Mtume (s.a.w.w.) hivyo wasingeshiriki vita. Kwa hiyo ni kaskazini tu mwa mji ambako maadui wangeweza kupenya. Mtume (s.a.w.w.) alishauriana na masahaba wake na ikawa sahaba mmoja bwana ‘Salman Farsi’, alijitokeza na kushauri kuwa huko kwao walikuwa 164


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 165

katika Uislamu

na kawaida ya kuchimba mtaro kama kinga walipozingirwa na maadui. Ushauri huo ulikubalika na uchimbaji ukaanza kaskazini mwa mji kwa siku sita. Mtume (s.a.w.w.) aliweka tayari jeshi lake la watu 3,000 imara ambao walipiga kambi nyuma ya huo mtaro. Makafiri nao walisonga mbele na kushangaa kuona huo mtaro ambao ulikuwa ni mbinu mpya ya kivita! Makafiri walizidi kukata tamaa na kutaka kurejea Makka kutokana na kukaa katika baridi kali na upepo. Kiongozi wao mmoja aliwasihi wasikate tamaa na kwamba angewashawishi Bani Quraidha wavunje mkataba wa amani na Mtume (s.a.w.w.) ili wajiunge pamoja na kujipenyeza Madina kutokea kusini mashariki. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mtume (s.a.w.w.) alipopata habari hizo alituma ujumbe kwao lakini wakawa jeuri. Waislamu waliogopa sana kushambuliwa pande mbili kama Qur’ani tukufu inavyolielezea tukio hilo (Qur’ani; 33:10-13). Madina ilizingirwa mwezi mzima na ikawa makafiri wamekusanya jeshi kubwa. Handaki lilipunguza kasi ya maadui lakini tishio lilibakia kubwa kwa Waislamu. Wanafiki walianza kuwakebehi Waislamu kwamba wamedanganyika na matumaini ya uongo ya Mtume (s.a.w.w.) lakini baadaye Mwenyezi Mungu alipindua imani hiyo ya wanafiki. Kwa woga wa nguvu za jeshi kubwa la makafiri, Waislamu wanafiki walianza kusambaza uvumi wa uongo wakidai kuwa Waislamu watashindwa. Vile vile wanafiki hao walijiondoa kijanja jeshini kwa madai kuwa wanarudi kulinda nyumba zao na familia zao. Hali hiyo ilipelekea shujaa wa kikafiri wa Quraish aliyejulikana kama Amr Ibn Abd Wud al-Amiri, na ambaye kwa nguvu zake za ajabu na umbo lake la kutisha, alikadiriwa kuwa na nguvu za askari elfu moja! kujaribu kufanya shambulizi. Amr Ibn Abd-Wud aliongozana na mashujaa wengineo wa kikafiri kama Nawfal Ibn Abdullah Ibn Mughira, Dhirar Ibn Khattab, Hubaira bin Abi Wahab, Ikrima bin Abi Jahl na Mirdas Fahr.

165


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 166

katika Uislamu

Amr Ibn Abd-Wudi alifaulu kujipenyeza kupita njia nyembamba na kujitupa mbele ya Waislamu na kuwataka ajitokeze wa kupigana naye. Waislamu kwa kujua umaarufu na nguvu za Amr na ujuzi wake mkubwa wa vita; pamoja na tukio mojawapo ambapo Amr akiwa katika vita, aliwahi kumshika ngamia mdogo kama ngao yake kwa mkono mmoja na kupigana na kundi la maharamia 1000 ambao aliwashinda vibaya, wakaogopa kujitokeza! Mtume (s.a.w.w.) aliwageukia masahaba na kuwauliza, “Ni nani kati yenu ambaye kwa niaba ya Mwenyezi Mungu na Uislamu atajitokeza kupambana na kafiri huyo tishio?” Wote waligeuka mabubu na wakainama kuangalia chini ili pengine, wasichaguliwe kupambana na Amr! Lakini Imam Ali (a.s.) alijitokeza haraka na kusema kuwa yuko tayari kwa kazi hiyo. Mtume (s.a.w.w.) alirudia wito wake huo mara tatu lakini aliyekuwa akijitokeza kila mara ni Imam Ali (a.s.) peke yake! Katika tukio hilo walikuwepo masahaba wote maarufu kama Abu Bakr, Umar na Uthman na wengineo lakini hakuna aliyethubutu kuitikia mwito huo. Sahaba mmoja alimweleza Mtume (s.a.w.w.) kuwa “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, unatutaka kukabiliana na yule ambaye ukimkabili matokeo yake ni kifo tu; kwani tumemwona akikabiliana peke yake na kundi la maharamia elfu moja na kuwashinda, huku akishikilia ngamia mdogo kama ngao yake!’ Maneno hayo yalikuwa sawa na kumtukuza adui na hivyo kumpa kichwa cha kujigamba kwa Waislamu. Mwisho ikawa Mtume (s.a.w.w.) amemwita Imam Ali (a.s.) akamvalisha kilemba chake na kumkabidhi upanga wake kisha kumwombea ushindi juu ya adui. Imam Ali (a.s.) alijitokeza kumkabili adui na ndipo Mtume (s.a.w.w.) aliposema: “Uislamu (imani) wote unakabiliana na ukafiri wote.” Mtume (s.a.w.w.) aliomba kwa Mwenyezi Mungu: “Ewe, Mola, huyu ni ndugu yangu na binamu yangu. Usiniache peke yangu. Wewe ni mbora wa kurithisha.” Wakati huo Imam Ali (a.s.) alikuwa kijana mdogo, urefu wa wastani na umbo la kati. Adui yake alikuwa na umbo kubwa la kutisha na ni mzoefu wa vita. Amr alikuwa kapanda farasi wakati ambapo Imam Ali (a.s.) alikuwa chini bila kipando. 166


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 167

katika Uislamu

Amr alipomwona kijana mdogo akijitokeza miongoni mwa watu wazima alijigamba na kusema: Amr: Ewe Muhammad hakuna mtu kati yenu wa kupigana na mimi ila kijana mdogo huyu? Siwezi kupigana na kijana mdogo. Imam Ali: Kama hutaki kukutana na mimi, mimi nataka kukutana na wewe kwa niaba ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.) Wake. Kwa hiyo kutana na kijana huyu wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu! Bila shaka itatosheleza matakwa yako. Amr: (Akapiga ukelele na kusema): Ewe ami, safari moja niliwahi kuwa mgeni wa baba yako Abu Talib na kula meza moja. Sipendi kumwua mtoto wa mtu aliyewahi kuwa mwenyeji wangu na ambaye alikuwa rafiki yangu. Imam Ali: Haiwezekani kuwepo urafiki wowote wa kweli kati ya muumini Abu Talib na kafiri Amr Ibn Abd Wud. Amr:

Hata hivyo sitaki kupigana na mtoto kama wewe.

Imam Ali: Kwa kuwa umejitokeza kumpinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na pia hutaki kupigana na mimi, basi mimi nimekuja kupigana na wewe ili kulinda njia ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na dini Yake. Amr: (Alitafakari majibu hayo ya busara. Hata hivyo Amr huko nyuma akiwa Makkah, aliweka nadhiri ya siri kwa sanamu (mungu wake) ndani ya Al-Kaabah na hakuna aliyejua siri hiyo). Imam Ali: Ewe Amr nimepata habari kuwa umeweka nadhiri ya siri kwa sanamu lako kwamba yeyote katika maadui zako akikutaka uchague kati ya mapendekezo matatu, utapokea japo moja tu. 167


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 168

katika Uislamu

Amr: (Akishangaa vipi siri hiyo alivyoijua Imam Ali) alijibu kwa majivuno kuwa : Ndiyo! Imam Ali: Sikiliza Amr, kwanza nataka uingie Uislamu. Amr: Hilo lawezekanaje wakati nimekuja hapa kuufuta Uislamu? Imam Ali: Basi rejea nyumbani kwako na usijihusishe na Mtume na Uislamu na Waislamu. Amr: Ningeweza kufanya hivyo lakini hata wanawake wa kwetu wataimba nyimbo za kusifu woga wangu na watasema kuwa nimeogopa kijana mdogo kama wewe na nimeshindwa kupigana baada ya kuchokoza. Imam Ali: Basi teremka chini ili tukutane kwa pambano la usawa. Amr: Wewe ni mtenda haki. Hapo Amr akateremka chini na hapo hapo akamkata farasi wake miguu kikatili (akamlemaza) na hapo Imam Ali akasema: Hiyo ni ishara mbaya kwako ewe dhalimu usiye na huruma. Amr: (Akiwa amepandisha mori) alimwambia Ali: Basi anza wewe kushambulia. Imam Ali: Sisi Ahlul-Bayt hatuanzishi vita au ugomvi, isipokuwa sisi hujibu mashambulizi. Basi anza wewe uliyeanzisha na utajibiwa. Ghafla, Amr alimshambulia Imam Ali (a.s.) kwa dharuba kali, lakini chenga za haraka za Imam Ali (a.s.) zilisababisha wingu la vumbi zito lililotanda na kuwafunika kabisa kiasi kwamba haikujulikana kilichokuwa kinaendelea mbele ya watazamaji! Zilisikika sauti kali za mapanga yakigongana. Watu walipigwa butwaa huku macho yao yakiwa yamekazia kwenye pam168


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 169

katika Uislamu

bano hilo la kishujaa. Punde si punde ilisikika sauti ya Takbir (Allahu Akbar) toka katika wingu la vumbi! Katika kambi ya Waislamu alisikika Mtume (s.a.w.w.) akisema kwa ufahari: “Namshukuru Mwenyezi Mungu! Ali amepata ushindi.” Vumbi lilitoweka na akatokeza Imam Ali (a.s.) akiwa amebeba mkononi kichwa cha Amr Ibn Abd Wud, akimwendea Mtume (s.a.w.w.). Imam Ali (a.s.) alitupa kichwa cha Amr miguuni kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia, ‘Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hicho ni kichwa cha adui wa Mwenyezi Mungu na adui yako.’ Na hapo ndipo Mtume (s.a.w.w.) alipomkumbatia Imam Ali (a.s.) na kusema, “Dharuba moja la upanga wa Ali siku ya vita vya Khandaq ni bora kuliko maombi (Swala) ya dunia yote na akhera kwa pamoja.” Maneno hayo ya Mtume (s.a.w.w.) ni kweli kwa sababu kama siyo ushindi huo siku hiyo, Uislamu ungefutika na Waislamu wangeuawa kikatili baada ya wanafiki miongoni mwa Waislamu kurejea ukafiri na kujiunga na maadui! Baadhi ya wanahistoria wameandika kwamba katika pambano hilo, Imam Ali (a.s.) alipata jeraha baya la kichwani. Mara baada ya kuuawa Amr Ibn Abd Wud, makafiri walipata kiwewe na kukimbia ovyo isipokuwa shujaa wao mmoja aliyeitwa Nawfal ambaye hata hivyo naye pia aliuawa na Imam Ali (a.s.). Kulitokea mfarakano miongoni mwa jeshi la makafiri. Wakati huo kulitokea baridi kali isiyo ya kawaida. Mvua kubwa iliyoandamana na kimbunga ilinyesha, na upepo ulitangulia kutimua vumbi nene ambalo liliwaingia machoni. Kimbunga kilikuwa na nguvu, kikang’oa mahema na kupindua vyombo vyao vya kupikia na kuwatimua ngamia na farasi wao wasiweze kushikika tena. Kwa hayo yote, makafiri walipiga kelele kuwa yamesababishwa na uchawi wa Muhammad! Makafiri waliingiwa na woga wa kushambuliwa na Waislamu na hivyo wakasambaratika na kuacha nyuma kila kitu.

169


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 170

katika Uislamu

Ukweli ni kwamba mkasa huo uliowapata makafiri unatokana na maombi maalumu ya Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikwenda mahali ulipo msikiti wa Masjid-ul-Fat’h na kumwomba Mwenyezi Mungu aepushe balaa la hao makafiri. Katika mkasa huo wa makafiri, wanyama wao walikufa kwa wingi na chakula kiliwaishia. Qur’ani 33:9-11, inaeleza neema ya Mwenyezi Mungu kwa Waislamu katika tishio hilo kubwa. Pamoja na matayarisho makubwa ya makafiri, Waislamu hawakuwa na sababu ya kutoamini ukweli wa utabiri wa Mtume (s.a.w.w.) aliotangulia kutoa mwanzoni kwamba Waislamu watashinda vita hivyo pamoja na ushindi zaidi huko Syria na Yemen. Mwanzoni mwa matayarisho ya vita hivyo, Waislamu wakichimba mtaro (Khandaq) ambao ulikuwa na futi 15 upana, na kipimo hicho hicho kwa kina chake, walikutana na mwamba ambao usigeweza kuvunjwa. Ikawa Mtume (s.a.w.w.) ameitwa kwa ushauri. Walimkuta Mtume (s.a.w.w.) amelala msikitini huku akiwa amefunga jiwe tumboni kukandamiza tumbo kutokana na njaa kali kwa kuwa katika vita hivyo Waislamu pia walikuwa na uhaba mkubwa wa chakula. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa pia amefunika uso wake kwa kitambaa. Alipoelezwa tatizo hilo la mwamba, siyo kwamba hakushiriki kuchimba ila wakati huo alikuwa kapumzika msikitini. Mtume (s.a.w.w.) aliagiza aletewe maji, akatia udhu, akachukua maji toka kinywani akatema maji hayo juu ya mwamba na akagonga huo mwamba kwa shoka ambapo kulitokea cheche kama radi na katika mwanga huo, watu waliona sura ya mji wa Syria. Mtume (s.a.w.w.) aligonga mara ya pili na watu wakaona sura ya mji wa Madina. Mara ya tatu watu waliona sura ya mji wa Yemen. Hapo ndipo Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuwa ‘Punde Mwenyezi Mungu atatupa ushindi juu ya miji yote hiyo.’ Kwa hiyo hao wanafiki ambao hawakuwa na imani na maneno au uwezo wa Mtume (s.a.w.w.), ndio walioeneza maneno ya kuwatia woga Waislamu eti maneno ya Mtume (s.a.w.w.) ni ya uongo anajaribu kueleza ushindi wa Yemen na Syria wakati amezingirwa Madina! 170


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 171

katika Uislamu

Baada ya muujiza huo, Mtume (s.a.w.w.) alivunja mwamba huo kwa mikono mitupu katika vipande vidogo vidogo. Siku za shida ziliendelea huku Mtume (s.a.w.w.) akiwa bado kafunga jiwe tumboni kwa njaa na uchimbaji mtaro ukiendelea. Mwisho ikawa Jabir Ibn Abdulla al-Answari ameomba ruhusa ya Mtume (s.a.w.w.) kumtengenezea chakula Mtume (s.a.w.w.). Jabir alipoulizwa ni chakula gani anacho akasema kuwa ana kondoo mmoja na nafaka kidogo. Baada ya Jabir kutengeneza chakula hicho, Mtume (s.a.w.w.) aliwakaribisha Waislamu wote wapatao elfu moja kwa niaba ya Jabir. Mtume (s.a.w.w.) aliagiza chakula hicho kibakie kwenye vyungu na watu wote wale kwa zamu ya watu kumi kumi tu. Kwa muujiza chakula hicho kilitosha watu wote na kikabaki! Lakini utakuta bado wanafiki kadhaa hawakuwa na imani katika uwezo wa pekee wa Mtume (s.a.w.w.)! Baada ya hapo ndipo lilifuata pambano la Amr Ibn Abd Wud na Imam Ali. Ali (a.s.) katika vita vya Khaybar: Vita hivi vilipiganwa dhidi ya makafiri wa Kiyahudi walioishi Khaybar, kilomita 128 Kaskazini mwa Madina mnamo nusu ya pili ya kumalizia mwezi wa Muharram mwaka wa 7 A.H (629 A.D). Wayahudi hao waliishi hapo Khaybar baada ya kuhamia hapo kutoka Madina kutokana na uadui wao kwa Waislamu. Khaybar maana yake ni ngome madhubuti. Wayahudi hao katika kujihami pindi ikitokea vita, walijenga ngome saba nazo ni Naa’im, Katiba, Shiqu, Natat, Watih, Sulalim, na imara kuliko zote ilikuwa Qamus. Mayahudi hao wa Khaybar walijenga uhasama wa kudumu kwa Waislamu, na walikuwa kila mara wakishawishi makabila mengine wajiunge nao kuleta uchokozi kwa Waislamu. Pamoja na kushindwa kwao katika vita vya Ahzab hawakutulia. Chifu wao Usir bin Razam alikusanya makabila yote ya Wayahudi na kupata msaada wa Ghaftah. Kuonyesha nguvu yao, Ghaftah alituma askari wachache ambao waliteka ngamia 20 wa Mtume (s.a.w.w.) baada ya kumwua mchungaji na kuteka mke wake. Habari za 171


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 172

katika Uislamu

matukio hayo ziliendelea kufika Madina na mwisho Mtume (s.a.w.w.) akaamua kuwashambulia kabla hawajawadhuru Waislamu. Kwa hiyo katika mwezi wa Muharram, 7 A.H Mtume (s.a.w.w.) alielekea Khaybar na jeshi lake la askari 1,400. Siku hizo Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akisumbuliwa kuumwa kichwa mara kadhaa. Siku aliyofika Khaybar ikawa pia anaumwa kichwa. Kwa hiyo ikawa Mtume (s.a.w.w.) anawatuma masahaba mbali mbali kuongoza mashambulizi, hadi zilipotekwa ngome sita zenye askari 20,000. Ngome hizo zilitekwa kirahisi. Lakini ngome ya Qamus ilishindikana kwa sababu ilikuwa ngome imara sana yenye kulindwa na mashujaa wa Kiyahudi. Wakati huo Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) alikuwa kaachwa Madina anaugua macho. Kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) akawa anachagua sahaba mmoja mmoja kuongoza mashambulizi ya ngome hiyo ya Qamus. Kwanza alichaguliwa bwana Abu Bakr Sidiq na kupewa bendera. Bwana Abu Bakr alihamasisha Waislamu na kupigana kwa nguvu zote lakini hakufanikiwa kuiteka Qamus. Kisha Umar Ibn al-Khattab naye akapewa bendera na akaongoza mapigano makali zaidi lakini bila mafanikio. Kutokana na hali hiyo Mtume (s.a.w.w.) alisema, “Kwa jina la Allah kesho nitampa bendera ya vita mtu yule mwenye kumpenda Allah na Mtume Wake na ambaye Allah na Mtume wake wanampenda, ambaye daima hushambulia na wala hakimbii (vitani) bali husonga mbele, na Mwenyezi Mungu keshapima moyo wake kwa imani.” Tunayakuta haya katika Sahih Muslim chini ya kifungu cha, Matendo ya Imam Ali (a.s.). Masahaba wote walilala na shauku ya kuona ni nani huyo mwenye sifa hizo. Kesho yake Mtume (s.a.w.w.) akauliza, ‘Yuko wapi Ali?’ Masahaba wakajibu kuwa anaumwa macho. Mtume (s.a.w.w.) akaagiza aletwe mbele yake. Mara ikawa Ali Ibn Abi Talib (a.s.) amefika. Mtume (s.a.w.w.) akachukua mate yake akampaka machoni Imam Ali (a.s.) na ikawa macho yamepona! Mtume (s.a.w.w.) alimpa Imam Ali (a.s.) bendera. Imam Ali (a.s.) akaishika na ikawa masahaba wote wametambua aliyekusudiwa kwa 172


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 173

katika Uislamu

maneno ya Mtume (s.a.w.w.) niliyotaja hapo juu. Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) aliondoka na kuelekea ngome ya Qamus. Alisimika bendera kwenye mwamba chini ya ngome hiyo madhubuti. Kiongozi wa Wayahudi wa kidini (Rabbi) aliyekuwa akiangalia akiwa juu ya ngome hiyo, aliuliza, ‘Ewe mshika bendera, wewe ni nani?’ Imam akajibu ‘Mimi ni Ali mtoto wa Abu Talib.’ Kiongozi huyo ‘Rabbi’ aliwageukia watu wake na kuwaeleza, ‘Kwa haki ya Taurati mtashindwa; huyu mtu hatarejea kwao bila kushinda vita kwanza.’ Bila shaka huyo ‘Rabbi’ alisoma utabiri juu ya Imam Ali (a.s.) katika Taurati kama nilivyoelezea mwanzoni kabisa mwa kitabu hiki kwamba Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) walitabiriwa katika Biblia, kama alivyotabiriwa Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe ambaye naye yumo katika hao Ahlul-Bayt (a.s.) waliokusudiwa (Qur’ani 33:33). Kwa upande wa Wayahudi, waliongozwa na Jemadari wao aliyeitwa Marhab ambaye alikuwa na mdogo wake aliyeitwa Haris Judah. Haris Judah alitangulizwa apambane kwanza. Alitokeza kukabiliana na Imam Ali (a.s.), akiwa amebeba mkuki mzito na kumwua Mwislamu mmoja. Ndipo Imam Ali (a.s.) alipomshambulia na kumwua hapo hapo. Marhab alipelekewa habari za kuuawa mdogo wake (Haris Judah). Alitoka nje ya ngome akiwa pamoja na askari hodari sana, ili kulipiza kisasi. Marhab alikuwa mrefu sana, mwenye nguvu nyingi na mkali sana miongoni mwa askari Wayahudi wa Khaybar. Hakuwepo shujaa kama yeye kwa upande wake. Siku hiyo alibeba silaha zaidi na kuvaa mavazi ya kinga ya mwili mara mbili pamoja na kubeba majambia mawili. Alisonga mbele vitani akiimba nyimbo za kujisifu. Hakuna Mwislamu aliyethubutu kupigana naye vitani. Imam Ali (a.s.) alisonga mbele huku akitoa maneno ya kumjibu Marhab. Marhab alitangulia kushambulia kwa jambia, lakini Imam Ali (a.s.) alikwepa na hapo hapo akamtupia dharuba moja ya upanga (Dhulfiqar) ambao 173


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 174

katika Uislamu

ulikata kinga (kofia ya chuma) ya kichwa na shingo na kumgawanya mara mbili, na ukawa ndio mwisho wake. Imam Ali (a.s.) aliwaamuru Waislamu kuanza kushambulia Wayahudi. Katika Majemadari wakuu wa Kiyahudi, Imam Ali (a.s.) aliwaua saba kati yao, na hali hiyo ilisababisha askari wa Kiyahudi kukimbia ovyo. Imam Ali (a.s.) aliwafukuza lakini Yahudi mmoja akampiga mkono Imam Ali (a.s.) na ikawa ngao yake (Imam) imedondoka chini. Askari mmoja wa Kiyahudi akaiokota na kujipatia ngawira. Imam Ali (a.s.) alikasirika na alipata nguvu za ajabu za kiroho kiasi kwamba aliruka mtaro wa kinga ya maadui (moat) na kutua kwenye lango la ngome (la chuma) na kuling’oa kisha likawa ndilo ngao yake na akaendelea kupigana. Baada ya mapigano hayo alilitupa hilo lango ambalo kwa uzito wake, watu wanane wasingeliweza kuligeuza! Haya yote yanaonyesha uwezo wa ajabu wa Imam Ali (a.s.) akiongozwa na Mwenyezi Mungu. Maelezo haya yamo katika: (a) Siirat Ibn Hisham (b) Tariikhul Kamil (c) Tarikh Abi al-Fida. H i v y o ndivyo uliyopatikana ushindi wa vita vya Khaybar. Ushujaa wa Imam Ali (a.s.) unaonekana wazi. Madhumuni mengine ya kushuka Aya 4 za Sura ya An-Najm Washereheshaji wa Qur’ani wa Shia na Sunni wanaeleza Hadithi mbili kuhusu sababu za kushuka Aya nne za kwanza za Sura An-Najm kwamba: Nyumba za Muhajirun kutoka Makkah zilijengwa kuzunguka, na milango yake kufungukia msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) wa Madina. Mara ikawa Uislamu umeenea na idadi ya Waislamu ikaongezeka, na ndipo Mtume (s.a.w.w.) alipopokea amri ya Mwenyezi Mungu kwamba milango yote inayofungukia msikitini ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Imam Ali (a.s.) ndio ubakie hivyo. Mara iliposhuka amri hiyo, mtu wa kwanza kutaka kutekeleza amri hiyo alikuwa Imam Ali (a.s.) lakini Mtume (s.a.w.w.) akasema, ‘Ewe Ali, amri hiyo haikuhusu wewe kwani wewe ni mimi na mimi ni wewe.’ Baadhi ya 174


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 175

katika Uislamu

masahaba walielezea kutoridhika kwao kwa madai kuwa mapenzi ya Mtume (s.a.w.w.) kwa Imam Ali (a.s.) yamezidi na amepoteza fahamu na kuacha njia ya haki. Hapo ndipo ziliposhuka Aya hizo nne za kwanza za Sura hiyo. Hadithi ya pili inaeleza kuwa anakaririwa Ibn Abbas akisema kuwa, “Tuliswali Swala ya Isha na Mtume (s.a.w.w.) ambaye baada ya Swala hiyo alitugeukia na kusema, ‘Asubuhi nyota itateremka kutoka angani na itatua juu ya nyumba ya mtu ambaye atakuwa mrithi wangu, khalifa wangu na Imam nyuma yangu.’ Masahaba wote walikaa wakisubiri nyota hiyo. Abbas ammi yake Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na matumaini makubwa kuwa ni yeye ambaye nyota hiyo itatua juu ya nyumba yake. Hata hivyo nyota hiyo ilitua juu ya nyumba ya Imam Ali (a.s.)!’” Mtume (s.a.w.w.) alimweleza Ali (a.s.) kuwa ‘Ewe Ali, kwa jina la Yule aliyenifanya Mtume Wake, nasema kuwa umeteuliwa na Allah kuwa mrithi na khalifa na Imam.’ Wanafiki ambao hawakupenda kusikia hivyo, walisema kuwa Mtume amevuka mipaka ya kumpenda Ali na amepoteza fahamu (busara) na ameacha njia ya haki (amepotoka)! Na hapo ndipo zikashuka Aya hizo kuwakosoa wanafiki hao. Maelezo yote haya yanaonyesha jinsi ambavyo suala hili la uongozi wa Waislamu lilishawekwa wazi na Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe mapema kabisa. Lakini mara tu alipofariki Mtume (s.a.w.w.) ikawa Waislamu wamempa mgomgo Imam Ali (a.s.)! Ukweli upo wazi kwa wale wanaoupenda. Tukio hilo linaongeza ushahidi kwamba mrithi halali wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w.) ni Imam Ali (a.s.) na alichaguliwa na Mwenyezi Mungu na kwamba uchaguzi huo hauwezi kufanywa na watu. Lakini pamoja na muujiza huo, utaona kuwa katika vita vya Siffin kulitokea askari wa Imam Ali (a.s.) waliokataa kumtii kwa ubishi; na matokeo yake ikawa Muawiyah amenusurikia kwa kutumia ulaghai wa kuwagawanya askari wa Imam Ali 175


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 176

katika Uislamu

(a.s.), ingawa hata hivyo askari wengi mno wa Muawiyah waliangamizwa. Waislamu ni muhimu tuwe waaminifu kama kweli tunataka baraka za Mwenyezi Mungu. La sivyo tuyapuuzie haya lakini kesho akhera tutalia na kusaga meno na mwisho kuangamia milele. Tusiichukulie dini kama kwamba ni utamaduni au mshikamano wa kufa na kuzikana. Muujiza kuelekea vita vya Siffin: Nimetangulia kueleza mwanzoni mwa kitabu hiki kwamba Ahlul-Bayt wa Mtume Muhammad (s.a.w.w.) wametajwa katika ‘Injiil’ ya Nabii Isa (a.s.) kama alivyotabiriwa humo yeye mwenyewe Mtume (s.a.w.w.). Katika uongozi wa Imam Ali (a.s.) wakati akiongozana na jeshi lake kuelekea vita vya Siffin (Sura ya 13 chini ya vita vya Siffin), yeye na jeshi lake wakiwa njiani walilazimika kupiga kambi sehemu ambayo hapakuwepo maji kabisa. Wanyama wao na askari wote walishikwa na kiu kali, wakati ambapo maji yasingeweza kupatikana popote eneo hilo. Mara akatokea Kasisi mtawa (monk) kutoka katika Parokia (monastery) akasema kuwa maji yaweza kupatikana umbali wa maili tano toka hapo. Lakini jeshi hilo lilikuwa linakaribia kufa kwa kiu na ilikuwa vigumu kwao na wanyama kutembea zaidi ya hapo. Imam Ali (a.s.) alimwomba Mwenyezi Mungu na kisha akanyoosha kidole akiashiria sehemu fulani ardhini hapo, ambapo aliamuru pachimbwe. Baada ya kuchimbwa kidogo, ulionekana mwamba mkubwa. Watu wote walijiunga na kujaribu kuinua mwamba huo wakashindwa. Imam Ali (a.s.) aliteremka toka juu ya farasi wake na akaingiza mikono chini ya mwamba huo na akauinua na kuutupa pembeni. Hapo hapo yakaonekana maji masafi ya ladha nzuri. Wakati huo huyo kasisi mtawa alitokeza tena na kumwuliza Imam Ali (a.s.); ‘Je, wewe ni Nabii?’ Imam Ali akajibu ‘Hapana.’ Kisha Kasisi akauliza tena; ‘Je, wewe ni Malaika?’ Imam Ali akajibu ‘Hapana ila mimi ni mrithi wa Mtukufu Mtume.’ Pale 176


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 177

katika Uislamu

pale yule Kasisi aliingia Uislamu mbele ya Imam Ali (a.s.) na akasema kuwa yapo maandishi katika vitabu vya zamani kwamba kuna kisima kilichofichika maeneo hayo, na ni Mtume wa Mwenyezi Mungu au mrithi wake aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu, ndio pekee wawezao kukigundua kilipo. Kasisi huyo aliongozana na Imam Ali (a.s.) katika vita vya Siffin na akauawa huko kishahidi. Tutaona kuwa yule Kasisi alipotambua wadhifa wa Imam Ali (a.s.) alisilimu hapo hapo. Lakini leo hii tunapotoa ushahidi mzito wa cheo na utukufu wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya umma wa Kiislamu, bado utaona Waislamu walio wengi hawaoni bado umuhimu mkubwa wa kuwa wafuasi wa hao warithi halali wa Mtume (s.a.w.w.) Baada ya kuteka maji katika kisima hicho na kutosheleza mahitaji ya jeshi lake, Imam Ali (a.s.) alifunika tena kisima hicho na kurejea kambini kwake. Baada ya muda Imam Ali (a.s.) aliwataka wale alioongozana nao kisimani hapo, warejee tena waone kama watagundua sehemu hiyo tena. Watu hao walijibu kuwa isingekuwa vigumu kwao kugundua sehemu hiyo kwa kuwa ilikuwa karibu na Parokia. Kwa hiyo waliondoka na kuelekea huko lakini hawakuweza kamwe kugundua sehemu hiyo! Imam Ali (a.s.) aliwaelezea kuwa hadi Kiyama kisima hicho kitabakia kimefichika. Rejea: Early History of Islam – cha S.S. Husein, toleo la mwaka 1933. Kwa hiyo tumeona kuwa katika historia za vita vya Jihadi, ushujaa wa Imam Ali (a.s.) pamoja na elimu yake iliyotajwa na Mtume (s.a.w.w.) kuwa Ali ni lango la elimu ya Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, bila shaka hata kusingekuwepo na wasia wa Mtume (s.a.w.w.), Imam Ali (a.s.) alistahiki kuwa kiongozi hata kwa sifa za kawaida za kidunia. Madai yote ya Umar kumzuia Imam Ali (a.s.) asipate uongozi huo muhimu hayana msingi wowote kwa Waislamu waaminifu. Zaidi ya hayo ushahidi niliotoa mapema juu ya Abu Bakr alivyopata ukhalifa pale Saqifah, ni wazi kwamba njia zilizotumika si za kidini wala si za kisiasa. Ndiyo maana Umar anakaririwa akisema kuwa njia iliyotumika kumchagua Abu Bakr ni makosa na ili177


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 178

katika Uislamu

fanyika bila kufikiri na isirudiwe tena. Rejea: Sahih al-Bukhari, Jz. 8, uk. 21 Tarikh Tabari, Jz. 1, uk. 1822 As-Sirah an-Nabawiyyah, Ibn Hisham Jz. 4, uk. 308/309 Tarikh al-Kamil, Ibn al-Athir Jz. 2, uk. 327 Tarikh Ibn Kathir, Jz. 5, uk. 245/246 Al-Ansab al-Baladhuri, Jz. 5, uk. 15 Sharh Ibn Abi al-Hadiid, Jz. 2, uk. 23 Kwa hiyo sisi Shia tunaposisitiza kuwa hatukubaliani na mfumo huo wa ukhalifa tunaungwa mkono na Umar Ibn al-Khattab kwa ushahidi wa vitabu hivyo vya ndugu zetu Sunni! Kabla sijaendelea kuelezea jinsi Umar na Uthman walivyopata ukhalifa na walivyokiri kubatilisha baadhi ya hukumu za Qur’ani na Sunna, ni muhimu kwanza tufahamu historia sahihi ya Bibi Aisha, kwa sababu karibu Hadithi zote za kumsifu bwana Abu Bakr zinakaririwa toka kwa Mama Aisha peke yake, kama tulivyoona madai ya kuwa Abu Bakr aliamrishwa aswalishe watu usiku wa kuamkia kufariki Mtume (s.a.w.w.)!

BIBI AISHA Wengi wetu tunasikia Bibi Aisha akisifiwa kwa sifa nyingi za kupindukia kuliko hata wake wengineo wa Mtume (s.a.w.w.) waliokuwa wacha Mungu kama Bibi Khadija na Mama Salma. Kwa kuwa madhumuni ya utafiti huu ni kuchunguza matukio muhimu katika Uislamu, hatuna budi kuwataja wahusika wakuu kwa nia ya kuweka wazi ukweli wa mambo. Jambo la maana ni kuthibitisha maelezo hayo kutoka katika vitabu vya kutegemewa. Isitoshe katika ulimwengu wa leo, historia siyo siri ya Waislamu bali ni elimu iliyotapakaa katika vitabu vingi duniani! Iwapo sisi Waislamu tutashindwa kujifunza historia yetu, watatokea watu wasio Waislamu wenye ujuzi wa dini yetu kuliko sisi, na hiyo itakuwa ni aibu kwetu.

178


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 179

katika Uislamu

Vile vile ni muhimu tutambue kuwa wake zake wote Mtume (s.a.w.w.) tunawaita mama zetu, kutokana na wasia wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba wake zake wote hawataolewa na mtu baada ya yeye kufariki. Kwa hiyo kuwa mke wa Mtume (s.a.w.w.) siyo cheo bali ni heshima kubwa tu. Hata kwenye Qur’ani tunakuta kwamba wake zao Mitume si wote walikuwa waadilifu! Wengine walikufuru! Yafuatayo ni maelezo juu ya Bibi Aisha kwa Hadithi za Mtume (s.a.w.w.): Maelezo mengine juu yake tutayakuta Sura ya 12. Hadithi ya Kwanza: Katika kitabu cha Sahih al-Bukhari, akisherehesha, chini ya Surat at-Tahrim, akielezea Hadithi zinazotokana na Umar Ibn alKhattab, anamkariri Umar akisema kuwa, ‘Wanawake wawili katika wakeze Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wanamdhalilisha Mtume na kumfanyia majivuno, nao ni bibi Aisha na bibi Hafsa. Maelezo haya yamo katika: Sahih al–Bukhari, Jz. 3, uk. 136 Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 68 Sahih al-Muslim, Jz. 2, uk. 14 Hadithi ya Pili: Wakati Mtume (s.a.w.w.) akiugua, mwisho wa uhai wake, mbele ya bibi Aisha, alimtaja Imam Ali (a.s.) kuwa kiongozi baada yake, lakini bibi Aisha akaficha habari hizo! Rejea vitabu vifuatavyo: Sahih al-Bukhari chini ya sura ya Al-Wasaya Jz. 3, uk. 68 Tarikh al-Tabari Tarikh Ibn al-Athir Sahih Muslim Jz. 1, uk. 61 Sahih at-Tirmidhi Jz. 5, uk. 306 An-Nasai Jz. 8, uk. 116 Kanz- al-Ummal Jz. 15, uk. 105 Sababu ya bibi Aisha kuficha habari hizo ni chuki yake kubwa kwa Imam Ali (a.s.) kama tutakavyoona katika maelezo ya mbele. Katika vitabu nilivyovitaja hapo juu, kuna Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: 179


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 180

katika Uislamu

“Kumpenda Ali ndio uumini wa kweli kweli, na kumchukia ni unafiki.” Huko nyuma tumekwishaona bibi Aisha alivyomwita baba yake kuswalisha Swala badala ya Imam Ali (a.s.) kinyume na amri ya Mtume! Hadithi ya Tatu: Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anahutubia kisha akaashiria nyumba ya bibi Aisha na kusema “Kuna balaa, kuna balaa, kuna balaa ...... litalotokea katika nyumba hii. Pembe za kichwa cha shetani zitaibuka nyumba hii.” Habari hizi zinapatikana katika Sahih al-Bukhari Jz. 4, uk. 61 Na Jz. 12, uk. 68. Utabiri huu wa Mtume (s.a.w.w.) ulidhihirika pale bibi Aisha alipohamasisha Waislamu kujiunga na kumpiga vita Imam Ali (a.s.) katika vita vya Jamal ndogo na Jamal kubwa. Vita hivyo vilisababisha Waislamu wengi kupoteza maisha kuliko vita vyote vya Jihad (katika uhai wa Mtume)! Habari hizo tutazikuta kwa ufasaha katika maelezo ya mbele - Sura ya 12. Hadithi ya Nne: Siku moja, mbele ya baba yake (Abu Bakr Sidiq), bibi Aisha alianzisha ugomvi na Mtume (s.a.w.w.), na kumwambia, ‘Uwe Mwadilifu!’ Abu Bakr alikasirika na kumpiga bibi Aisha kibao cha usoni kwa nguvu mpaka bibi Aisha akawa anavuja damu nyingi usoni. Haya yamo katika vitabu vifuatavyo: (a) Kanz al-Ummal, Hadithi ya 1020 Jz. 7, uk. 116. (b) Adab al-Nikah katika kitabu Ihya’al-’Ulum, Jz. 2, uk. 35 (c) Makashifah al-Qulub - Sura ya 94 uk. 238, na (d) Ihya’al-’Ulum - Sura ya 3. Hadithi ya Tano: Mke wake Mtume (s.a.w.w.) aliyeitwa bibi Zainab bint Jahsh, siku moja alitengeneza kinywaji cha asali kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w.). Baada ya Mtume kunywa kinywaji hicho alikwenda kwa bibi Aisha ambako aliambiwa eti ananuka ‘maghafir’ ambayo ni aina ya maua pori ya mti fulani, yenye harufu mbaya sana! Kisha baada ya hapo alikwenda kwa bibi Hafsa ambaye naye alisema maneno hayo hayo! Lengo la uongo huo lilikuwa kumfanya Mtume (s.a.w.w.) amchukie Mama Zainab bint Jahsh na asiende kwake tena! Mbinu hiyo ilikuwa imepangwa kuonye180


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 181

katika Uislamu

sha kuwa asali iliyotengeza kinywaji hicho, iliingiwa na nyuki waliotoka kwenye maua ya mti wa maghafir kabla ya kupakuliwa huko porini. Kutokana na tukio hilo, Mtume (s.a.w.w.) aliapa kuwa hatakula asali tena. Lakini zikashuka Aya mbili kubatilisha uamuzi huo:“Ewe Mtume! Kwa nini unaharamisha kile ambacho Mwenyezi Mungu amekuhalalishia; unatafuta radhi ya wake zako; Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamahe, Mwenye kurehemu.” (Qur’ani 66

“Hakika Mwenyezi Mungu amekufaridhishieni kafara ya kufungua viapo vyenu na Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wenu, naye ni Mjuzi, Mwenye hekima.” (Qur’ani 66:2) Haya tunayapata katika Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 136. Kwa sifa nyingi nzuri tunazosikia akisifiwa bibi Aisha, tusingetegemea afanye fitina kama hiyo kwa mke mwenzake! Maelezo mengine juu ya bibi Aisha yatafuata mbele katika matukio yanayohusika. Kabla ya kuelezea jinsi Umar alivyopata ukhalifa, nitaeleza tukio jingine juu ya tabia ya bibi Aisha na Hafsa. Tukio jingine katika historia tunalipata katika sababu za kushuka Aya ya Qur’ani (33:28):

“Ewe Mtume! Waambie wake zako; ikiwa mnapenda maisha ya dunia hii na mapambo yake, basi njooni, nitakupeni kitokaunyumba na kukuacheni muachano mwema.” ( Qur’ani 33:28). Washereheshaji wa Qur’ani wanaeleza kuwa, mara Mtume (s.a.w.w.) aliporejea toka vita vya Khaybar, wake zake walimtaka awagawie ngawira. 181


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 182

katika Uislamu

Aliwajibu kuwa amezigawa kama alivyoamriwa na Allah (swt). Wake zake walizidi kumhoji kuwa, ‘Unafahamu kuwa baada yako hatutaolewa na mtu yeyote?’ Mtume hakuwajibu bali aliwatenga kwa mwezi mmoja ambapo ikashuka Aya hii na ndipo Mtume (s.a.w.w.) aliwaita wake zake wote akawaeleza maneno hayo ya Mwenyezi Mungu juu yao, ili wachague ama kupokea mahari zao na zawadi nono kisha wapewe talaka milele, au waishi kwa amani na Mtume (s.a.w.w.) na waridhike na maisha hayo. Hapo hapo alinyanyuka bibi Salma na kusema, ‘Namchagua Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.’ Hapo ndipo ilifuatia kushuka Aya ya pili yake yaani:

“Na kama mnampenda Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na maisha ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia watendao mema miongoni mwenu, malipo makubwa.” (Qur’ani 33:29). Katika historia tunaona kuwa bibi Aisha na bibi Hafsa walikuwa na kawaida ya kujiona bora zaidi ya wake wenzao, na hivyo wakimdai Mtume (s.a.w.w.) awapendelee, lakini kila mara akiwakatalia. Siku moja bibi Aisha alidai apewe ngawira toka vita mojawapo ya Jihad. Madai hayo ya bibi Aisha yalikuwa ni kukiuka kanuni za haki za kugawa ngawira lakini bibi Aisha alizidi kugan’gania apewe, hata ikawa Mtume (s.a.w.w) alisikitika kwa majivuno ya bibi Aisha na madai yake batili. Imam Ali (a.s.) alikuwepo na akajaribu kumtuliza bibi Aisha bila mafanikio na badala yake bibi Aisha akamkemea Imam Ali (a.s.). Mtume alisononeka sana hapo alipokemewa Imam Ali (a.s.). Rejea (1) Rawazatul Ahbab (2) Habib Siyar (3) Asimi Kufi (4) Manaqib Murtazawi.

182


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 183

katika Uislamu

Ushahidi mwingine wa ukorofi wa bibi Aisha unapatikana katika Aya ifuatayo:

“Iwapo ninyi wawili mtatubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwishaelekea upande. Na iwapo mtasaidiana dhidi yake, basi Mwenyezi Mungu ndiye Mlinzi wake, na Jibril na waumini wema, na zaidi ya hayo, Malaika pia ni wasaidizi wake pia.” (Qur’ani 66:4). Aya hii ilishuka kuwakemea bibi Aisha na bibi Hafsa na kuwataka watubu maovu yao kwa Mtume (s.a.w.w.)! Kama kuna Mwislamu mwenye shaka na sababu za kushuka Aya hii, rejea Hadithi ya kwanza ya mtiririko huu, kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) aliusia kuwa tuikatae Hadithi yoyote inayopingana na Qur’ani. Rejea: The Right Path, cha Abd al-Husayn Sharaf-alDin-al-Musawi, uk. 353, toleo la kiingereza - Iran.

SURA YA UTAWALA WA ABU BAKR SIDIQ Tumekwishaona jinsi Abu Bakr Sidiq alivyopata ukhalifa pale Saqifah. Sasa tuone alivyoendesha utawala wake akiwa kiongozi mkuu wa Dola ya kiislamu. Nimetangulia kueleza mila ya Waarabu ya kiapo cha utii (Bay’at). Baada ya uamuzi wa Saqifah, Waislamu wa Madina walilazimika kumtii Abu Bakr ingawa ni kinyume na wasia wa Mtume (s.a.w.w.)! Kulikuwa na Waislamu waliotaka kumpa Bay’at Imam Ali (a.s.) kwa kutii wasia wa Mtume (s.a.w.w.), lakini Imam Ali (a.s.) alikataa na kusema kuwa ukhalifa ulikuwa ni haki yake ya moja kwa moja isiyohitaji majadiliano. 183


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:21 PM

Page 184

katika Uislamu

Isitoshe miezi mitatu nyuma ya hapo, Waislamu hao hao walishampa Bay’at pale Ghadiir Khum, mara tu alipotangazwa na Mtume (s.a.w.w.) kuwa khalifa baada ya Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo Waislamu wale wale ndio wanampa Bay’at Abu Bakr! Kwa hiyo Imam Ali (a.s.) alijua kuwa ukhalifa sio ufalme na kwa hiyo haoni vipi watu wapewe uwezo wa kuamua nani awe khalifa. Imam Ali (a.s.) hakutaka aupate ukhalifa kwa matakwa ya watu, bali aliona ni wajibu wa watu kutii amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume (s.aw.w.). Imam Ali (a.s.) aliona kuwa kama watu watamfuata kwa kutii amri ya Mtume (s.a.w.w.), ni sawa, na ni kwa faida yao. Iwapo hawataki ni kwa hasara yao kesho Akhera mbele ya Mwenyezi Mungu. Sura ya kwanza ya utawala wa bwana Abu Bakr anaitoa Umar Ibn alKhattab alipokaririwa akisema kuwa, ‘Nimesikia kuwa kuna mtu amesema kwamba Umar akifariki nitampa Bay’at fulani. Asitokee mtu akajidanganya namna hii, akifikiri kuwa ingawa Bay’at kwa Abu Bakr ilikuwa ya ghafla, hata hivyo ilifanikiwa. Ni kweli ilikuwa ya ghafla lakini Mwenyezi Mungu alitunusuru kutokana na uovu wake (bay’at). Kama kuna anayetaka kuigiza hivyo, nitamkata shingo yake.’ Kauli hiyo ya Umar inapatikana katika Sahih al-Bukhari - Kitabul Muharibin, toleo la Cairo, Jz. 8, uk. 210 na kitabu cha Tarikh at-Tabari, Jz. 4, uk. 1821 na Kanz al-Ummal, Jz. 3, Hadithi Na. 2323. Kwa maneno hayo ya bwana Umar, inashangaza kuona anawazuia watu kutumia njia ile ile iliyomfanya rafiki yake mkuu, Abu Bakr kupata ukhalifa! Vile vile Umar anakiri kuwa njia hiyo iliyotumika kumchagua Abu Bakr ilikuwa ya uovu lakini Mwenyezi Mungu ameepusha shari yake! Bwana Abu Bakr apewa Bay’at: Amri ya kwanza ilikuwa ni kuwataka Waislamu wote watoe Bay’at kwa bwana Abu Bakr Sidiq. Umar Ibn al-Khattab ndiye aliyesimamia binafsi utekelezaji wa amri hiyo. Imam Ali (a.s.) alikataa kutoa Bay’at kwa sababu 184


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 185

katika Uislamu

nilizotangulia kueleza. Baada ya Imam Ali (a.s.) kukataa kutoa Bay’at kwa Abu Bakr, bwana Abu Bakr alimwamuru Umar kuwataka Imam Ali (a.s.) na bibi Fatima (a.s.) watoe Bay’at. Pamoja na msimamo wa Imam Ali (a.s.) kujifungia ndani na kutotaka kushiriki katika siasa za ugomvi wa madaraka, hawakumwacha akae kwa amani na familia yake. Umar Ibn Al-Khattab na wafuasi wake, kwa amri ya bwana Abu Bakr, walipoona Imam Ali (a.s.) hataki kutoa Bay’at, walivamia nyumba yake na kuichoma moto ghafla, huku Imam Ali (a.s.) na familia yake wakiwa ndani! Kulitokea mtafaruku ndani ya nyumba, huku watoto Hasan na Husein wakikabwa na moshi mzito na kulia. Katika tukio hilo, wakati bibi Fatima (a.s.) akiwa mlangoni, pengine akitaka kutoka nje, mlango ulivunjwa kwa nguvu kutoka nje na ukampiga bibi Fatima (a.s.) ukamvunja mbavu na mkono. Matokeo yake ikawa bibi Fatima (a.s.) aliendelea kuugua na mwisho mimba aliyokuwa nayo ikaporomoka na kisha yeye akafariki tarehe 14 Jamad-ul-Awaal 11 A.H, miezi sita tu baada ya kufariki Mtume, (tarehe 28, Safar 11 A.H). Mlango huo uliomjeruhi bibi Fatima (a.s.) ulivunjwa toka nje na ndipo wakaingia walioingia, wakamkamata Imam Ali (a.s.) na kumburuza hadi kwa Abu Bakr ili atoe kiapo cha utii ambacho hata hivyo hakukitoa. Rejea:Tarikh Tabari, Jz. 3, uk. 198 Aqdul Farid Ibn Abd-e-Rubbabo, Jz. 2, uk. 179 - Misri Tarikh Abu al-Fida, Jz. 1 uk. 156 - Misri Kitabul al-Imama wa Siyyasah, Allama Ibn Qutaybah, Jz. 1, uk. 20 Misri (Kitabu hiki kinaeleza bayana zaidi) Muruuj ad-Dhahab, uk. 159 Milal wa Nihal, Shahrastani - Jz.1, uk. 25 - Bombay Nahjul Balaghah - Ibn Abi al-Hadiid Kabla ya kufariki Bibi Fatima (a.s.): Kitendo cha Abu Bakr kuchukua ukhalifa na kutaifisha mali za bibi Fatima (a.s.) alizorithishwa na baba yake, kulimkasirisha bibi Fatima (a.s.) kiasi 185


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 186

katika Uislamu

kwamba hakutaka kabisa kuonana au kuongea au kusalimiana na Abu Bakr au Umar. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, ‘Fatima ni sehemu ya mwili wangu, anayemuudhi Fatima kaniudhi mimi.’ Tunasoma pia kwamba kutokana na vitendo viovu alivyotendewa bibi Fatima (a.s.), alimwambia Abu Bakr kuwa, ‘Kwa jina la Allah, nitakulaani katika kila Swala yangu.’ Naye bwana Abubakar alianza kulia na kusema, ‘Naomba Mwenyezi Mungu aninusuru na hasira ya bibi Fatima.’ Hasira ya bibi Fatima (a.s.) ni pamoja na kuchomwa moto nyumba yake wakati yeye na mumewe na watoto walipokataa kutoa Bay’at kwa bwana Abu Bakr. Urithi wa bibi Fatima (a.s.) uliotaifishwa ni shamba kubwa lenye rutuba lililoitwa ‘Fadak’ ambalo Wayahudi walilitoa kwa Mtume (s.a.w.w.) baada ya vita vya Khaybar. Katika vitabu vifuatavyo anakaririwa bibi Fatima (a.s.) akiwaeleza Abu Bakr na Umar kuwa, “Nakiri mbele ya Allah na Malaika kuwa ninyi wawili mmeniudhi na nitakapokutana na Mtume (s.a.w.w.) nitawakilisha kwake malalamiko yangu.” Zaidi ya hayo bibi Fatima (a.s.) aliusia kuwa mabwana Abu Bakr na Umar wasihudhurie mazishi yake, na kwamba azikwe usiku kwa siri. Hadi leo haijulikani nafasi maalumu ya kaburi lake! Bila shaka bibi Fatima (a.s.) aliusia azikwe usiku kwa siri ili pengine vizazi vijavyo wajiulize na kufanya utafiti juu ya migogoro iliyosababisha hali hiyo! Hata kama kuna mtu anayekataa kuwa haya hayakutokea, au hayawezi kufanywa na masahaba wakuu, itabidi ajiulize kwa nini leo hii kaburi la binti pekee wa Mtume (s.a.w.w.) lisionekane? Hata kaburi la Uthman Ibn Affan hapo lilipo sasa hivi inashangaza kwa kadri ya kipindi alichofariki, lakini hayo tutayakuta mbele. Maelezo yote haya (juu ya bibi Fatima) rejea vitabu vifuatavyo: Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 39 Tarikh al-Khulafa, Ibn Qutaybah, Jz. 1, uk. 20 Al-Imamah wal-Siyasah, Ibn Qutaybah, Jz.1, uk. 20 Tarikh al-Tabari 186


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 187

katika Uislamu

Kanz al-Ummal Minhaj al-Sunnah, Jz. 3, uk. 120 Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 206 Uandishi na usimuliaji Hadithi wakatazwa: Katika Sura ya nane, nimeeleza sababu nne ambazo Umar alizitoa kama kisingizio cha kumpindua Imam Ali (a.s.). Sababu mojawapo ni kwamba chini ya uongozi wa Imam Ali (a.s.) angeamrisha haki tupu na watu wasingepata mwanya wa kuvuka mipaka ya haki, na kwa hiyo wangeungana na kumpiga vita! Maana yake ni kwamba angeongoza katika nyayo za Mtume (s.a.w.w.) lakini watu hawataki hivyo! Kwa hiyo, ili kuepukana na amri za Mtume (s.a.w.w.) ilibidi kwanza kumwondoa Imam Ali (a.s.) katika uongozi, na hatua ya pili ni kuzuia watu kuelezea na kuandika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.). Rejea:Al-Ghadir al-Amini, Jz. 7, uk. 74-236 An-Nass wa’l Ijtihaad, cha Sharafu’d-Din uk. 76-154 Muqaddamah Mir’aatu’l-uquul, cha al-Askari, Jz. 1 & 2 Huko nyuma tumeona kuwa Umar alizuia visiletwe vifaa vya kuandikia wasia kwa Mtume (s.a.w.w.), akasema kuwa, ‘Qur’ani inatosha, ugonjwa umemzidi Mtume anasema upuuzi.’ Kwa hiyo hatushangai hapa kuona Umar na Abu Bakr wanakataza maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yasielezwe na yasiandikwe! Kwa maana nyingine, wao walichotaka ni kutawala na siyo kulinda dini. Na hapo ndipo Taifa lililokuwa la Serikali ya kiislamu wakati wa Mtume (s.a.w.w.), ghafla likageuka kuwa ‘Dola ya kiarabu’ baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. Isitoshe kuendelea kueleza na kuandika maneno ya Mtume (s.a.w.w.), kungesababisha wao (watawala) waonekane wanatenda kinyume na Uislamu na hivyo kuleta manung’uniko kama tutakavyoona mbele. Rejea: Sahih Bukhari, Jz. 6, uk. 98. Vitendo vya watawala (makhalifa) kuzuia simulizi na uandishi wa Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) vilidumu muda mrefu hadi mwaka 190 A.H, karibu miaka 179 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.)! Wanahistoria wote wanakubaliana na ukweli huu kutokana na maneno ya khalifa pekee mwadilifu wa Bani Umayyah “Umar Ibn Abd al-’Aziz (R)” aliyekaririwa 187


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 188

katika Uislamu

akimwandikia Abu Bakr Ibn Hazm kuwa, ‘Angalia kama kuna Hadithi zozote zilizobaki za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na uziandike, kwani ninaogopea ni vipi mafunzo yataendeshwa wakati wanazuoni wameshapita. Kisipokelewe chochote ila Hadithi za Mtume (s.a.w.w.). Hivyo waache wajuzi wa dini waeneze elimu na wakae pamoja ili yule asiye na elimu ajifunze kwani elimu hupotea mara tu inapofanywa siri.’ Maneno haya ya hekima yanapatikana katika Sahih al-Bukhari chini ya kifungu cha ‘Kitabu cha Elimu.’ Hata hivyo kama tutakavyoona baadaye, inashangaza kuona mabwana Abu Bakr na Umar wanatoa hoja zinazopingana kabisa na dini, kwa sababu pale Umar aliposema kuwa ‘Qur’ani inatutosha’ ni maajabu!1 Hukumu nyingi za dini zinapatikana kwa ufasaha katika Hadithi na siyo katika Qur’ani! Mwenendo huo umeendelea hadi leo, ambapo baadhi ya Waislamu wanakwepa ukweli katika vitabu vya Sunna, na badala yake wanapindisha tafsiri ya Qur’ani kuhalalisha upotofu wao. Tumeona katika wasia wa Mtume (s.a.w.w.) pale Ghadiir Khum akituonya tusijaribu kufasiri Qur’ani kwa matakwa yetu bali tukitaka kuelewa maana ya Aya zake, turejee kwa Imam Ali (a.s.) na Ahlul-Bayt wake (a.s.) wenye ujuzi wa maana iliyowazi na maana iliyojificha. Kwa hiyo tusije tukadhani kuwa kila mtu anaweza kufasiri Qur’ani kwa misingi ya ujuzi na kanuni za lugha ya kiarabu peke yake! Kutokana na wasia huo wa Mtume (s.a.w.w.) ni lazima tukubali kwamba tafsiri sahihi ya Qur’ani baada ya Mtume (s.a.w.w.) ni ile inayotokana na mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.). Tutapata maelezo zaidi juu ya suala hili, katika sura za mbele - Sura ya 14 - Insha Allah. 1 Ni maajabu kweli kwa sababu Umar huyu huyu mara nyingi amekosea katika kutoa hukumu, na alikuwa akisahihishwa na Imam Ali (a.s.) huyu huyu aliyetaka kuandikwa kwenye wasia alioukataza yeye – mathalan rejea: Sawa’iq Muhriqa uk. 8; Yanabiul-Mawadda Sura ya 14; Tarikh Khulafa’ uk. 66; Usudul-Ghaba Jz. 4, uk. 22 na vingine vingi. Pia amebatilisha hukumu za Qur’ani na kuweka maoni yake; mathalan suala la ‘Talaqa Tatu kwa mpigo, kuharamisha Mut’a mbili na adhabu za kifo zinazohitilafiana na sheria. (Mhariri) 188


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 189

katika Uislamu

Kuchoma moto Hadithi zilizoandikwa!: Anakaririwa mama Aisha akieleza kuwa, ‘Katika utawala wa baba yangu (Abu Bakr) alikusanya Hadithi 500. Siku moja nilimwona akiwa hana raha usiku wote mpaka asubuhi ambapo aliniambia nimletee Hadithi hizo 500 na akazichoma moto.’ Rejea: Kanz al-Ummal - cha Alau al-Din Muttaqi, Toleo la Hyderbad mwaka 1364 A.H - 1375 A.H Jz. 5, uk. 237; na Musnad al-Sadiq cha Ibn Kathir. Kuwaua waliokataa kutoa Zaka!: Anakaririwa bwana Abu Hurayra akisema kuwa, ‘Baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki na Abu Bakr kupata ukhalifa kuna baadhi ya Waarabu waliokufuru. Umar alisema, ‘Ewe Abu Bakr! Unawezaje kupiga watu vita wakati Mtume (s.a.w.w.) alisema: Niliamrishwa kuwapiga watu vita mpaka watamke: “Hapana Mola ila Allah.” Na anayetamka hivyo huwa amesalimika na mali yake isipokuwa kwa hukumu ya ‘shariah’ na kwa hiyo malipo yake yapo kwa Mwenyezi Mungu.’ Abubakar akajibu, ‘Kwa jina la Allah! Nitampiga vita kila atakayetenganisha Swala na Zaka kwani Zaka ni halali itolewe kutokana na mali. Kwa jina la Allah! Iwapo watazuia japo mnyama mmoja ambaye walizoea kumtoa kwa Mtume (s.a.w.w.), nitawapiga kwa kitendo hicho.’ Ndipo Umar akasema, ‘Kwa jina la Allah niliona kuwa Allah ameufungua moyo wa Abu Bakr kupigana, na ndipo nikaona kuwa ni sahihi.’ Haya yanapatikana katika vitabu vifuatavyo: (1) Sahih al-Bukhari - Katika Kitabu cha: Kuwaita waliokufuru kutubia, katika kifungu cha: Kuwaua wale wanaokataa kupokea Sheria za wajibu na wale wanaohusiana na kukufuru. (2) Sahih Muslim - Katika kitabu cha Imani, somo la amri ya kuwapiga vita watu. Katika uamuzi huo wa Abu Bakr, alimtuma Khalid Ibn al-Walid ambaye aliwachoma moto watu wa kabila la Bani Sulaym. Kisha alitumwa huko alYamama kwa Bani Tamim kuwaua kikatili baada ya kuwafunga na kamba 189


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 190

katika Uislamu

kisha kuwakata vichwa! Katika mauaji hayo aliuawa sahaba wa heshima bwana Malik Ibn Nuwayra, aliyekuwa mwaminifu mweka hazina wa pesa za sadaka za watu wake. Baada ya kumwua, huyo Khalid Ibn al-Walid usiku huo huo alimchukua mke wa marehemu Malik na kulala naye! Watoto na wake za marehemu walifanywa mateka. Marehemu Malik na watu wake hawakuwa na kosa lolote ila tu walipata habari za matokeo ya Saqifah baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.). Vilevile walipata habari za kumsukuma pembeni Imam Ali (a.s.) na kutaifishwa kwa urithi wa Bibi Fatima (a.s.). Kisha walipata habari kuwa Sad Ibn Ubadah chifu wa Ansari naye kavunja kiapo chake cha utii kwa Imam Ali (a.s.). Walipata habari zingine miongoni mwa makabila ya jangwani, kuhusu wasiwasi wao juu ya uhalali wa kumtii Abu Bakr Sidiq. Kutokana na hayo yote, bwana Malik Ibn Nuwayra na watu wake walisita kutoa Zaka. Ndipo Abu Bakr akiwa khalifa aliamuru wauawe kwa kutotoa Zaka! Abu Bakr alihofia huenda makabila yote ya mbali na Madina yakamgomea na hivyo kuponyokwa na Ukhalifa. Jambo la kusikitisha ni kuona baadhi ya Wanahistoria wasio waaminifu wanahalalisha kitendo hicho kwa sababu tu ya kulinda heshima ya Abu bakr, wakati Abu Bakr mwenyewe anakiri uovu huo, na alilazimika kulipa fidia ya kifo cha bwana Malik kwa kaka yake marehemu, na akasema kuwa Khalid alitafsiri vibaya agizo lake! Fidia ilitoka Baitul Maal! Maneno ya Umar kumuunga mkono Abu Bakr kwa kitendo hicho, kama nilivyotangulia kueleza, hayaonyeshi kuwa Umar alisema hivyo kwa uaminifu. Kwa sababu katika tukio hilo, Umar alikasirika kwa kitendo cha Khalid Ibn alWalid kumwua Malik na kuchukua mke wake siku hiyo hiyo! Umar alimwambia Khalid, ‘Ewe adui wa Mwenyezi Mungu, ulimwua Mwislamu na kuchukua mke wake ............. Wallahi nitakupiga mawe (mpaka ufe). Lakini Abu Bakr alimtetea Khalid na kusema, ‘Ewe Umar, msamehe alikosea lakini usimkaripie!’ Haya tunayapata katika:

190


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 191

katika Uislamu

Tarikhut-Tabari, Jz. 3, uk. 280 Tarikh Abul-Fida, Jz. 1, uk. 158 Tarikh al-Ya’qubi, Jz. 2, uk. 110 Al- Isabah fi Ma’rifati-Sahabah, Jz. 3, uk. 336 Kukokana na kitendo hicho cha Abu Bakr kuamuru mauaji hayo, tutaona kuwa ni kinyume kabisa na Sunna ya Mtume (s.a.w.w.), kwa sababu katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.) kulitokea tatizo kama hilo katika kisa cha Tha’labah - ambaye aliomba Mtume (s.a.w.w.) amwombee dua ili atajirike, lakini alipotajirika akakataa kutoa Zaka ya mifugo yake na akiita hiyo Zaka kuwa ni sawa na kodi waliyotozwa wasio Waislamu katika Taifa la kiislamu yaani ‘Jiziyah’. Pamoja na msimamo huo wa Tha’labah, Mtume (s.a.w.w.) hakuamuru auawe au apigwe, na ilishuka Aya ya Qur’ani; 9:75-77 kuhusu kisa hicho. Kwa hiyo Abu Bakr alipingana na Qur’ani pia! Ingawa tumeona nyuma jinsi yeye na Umar walivyodai kuwa ‘Qur’ani inatosha!’ Baada ya kushuka Aya hizo, Tha’labah alikuja mbio kwa Mtume (s.a.w.w.) akilia na kumwomba apokee Zaka yake lakini Mtume (s.a.w.w.) alikataa. Bibi Fatima (a.s.) kunyang’anywa urithi wake wa Fadak: Katika Sura hii huko nyuma nimetangulia kueleza jinsi Abu Bakr alivyotaifisha urithi (shamba la Fadak) wa Bibi Fatima (a.s.) na ikawa Bibi Fatima (a.s.) amefariki hali ya kuwa amewakasirikia Umar na Abu Bakr. Msimamo huo wa Abu Bakr unatokana na madai yake kwamba alimsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa: “Mitume hawarithiwi na mtu ila mali wanazoacha ni sadaka!” Kisa chenyewe, kwa kadri ya maelezo ya Wanahistoria wengi, ni kwamba mara Abu Bakr alipochukua Ukhalifa, Bibi Fatima (a.s.) alipeleka ujumbe kwake kudai urithi wake aliopewa na baba yake (Mtume s.a.w.w.). Abu Bakr alikataa na kutoa jibu hilo hapo juu. Lakini Bibi Fatima (a.s.) alipinga madai hayo kwa ushahidi wa Qur’ani kuonyesha kuwa madai ya Abu Bakr siyo kweli: 191


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 192

katika Uislamu

“Mwenyezi Mungu anawausia kuhusu watoto wenu. Mtoto wa kiume atapata sawa na fungu la (watoto) wawili wa kike.” (Qur’ani 4:11) “Na Suleiman alikuwa mrithi wa Dawuud.” ( Qur’ani 27:16) “.........basi nipatie mrithi toka kwako, ambaye atanirithi na pia awarithi watoto wa Ya’qub, na mfanye, Ewe Mola Wangu, ni mwenye kuridhisha.” (Qur’ani 19:5-6) Katika Qur’ani 4:11, Aya hiyo inawahusu watu wote, Mitume na wasio Mitume. Na Qur’ani 27:16, waliotajwa humo wote ni Manabii! Wakati ambapo:Qur’ani 19:5-6, inajieleza wazi juu ya suala hili la urithi kwa watoto. Ingekuwa ni kweli kwamba Abu Bakr anafuata Qur’ani tu, basi angetimiza madai ya haki ya urithi ya Bibi Fatima (a.s.)! Isitoshe iwapo ilikuwepo Hadithi ya kwamba Mitume hawaachi urithi, mbona baadaye wake zake Mtume (s.a.w.w.) nao walidai urithi? Kwa nini wasijue Hadithi hiyo? Rejea: Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 16. Lakini tunaelezwa kuwa Abu Bakr na Umar walishirikiana katika utawala wa Abu Bakr. Ajabu ni kwamba baada ya Abu Bakr kufariki, Umar aliwagawia urithi, wake zake Mtume (s.a.w.w.)! Rejea: Sahih al-Bukhari, Kitabu cha Unaibu (Deputyship), Sura ya Mgawanyo wa Mapato. Al-Bukhari anaeleza kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliwekeana mkataba na watu wa Khaybar kutumia ardhi ya huko (baada ya vita) kwa masharti kuwa nusu ya mazao itakuwa yao. Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na kawaida ya kuwapa wake zake mgao wa mazao hayo kwa kiasi cha wasaq 100 kila mmoja, ‘wasaq’ 80 za tende na ‘wasaq’ 20 za shairi. Mara Umar alipopata Ukhalifa aliwapa wake zake Mtume (s.a.w.w.) hiari ya kuchagua kumiliki ardhi na maji kama mgao wao au kuendelea na 192


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 193

katika Uislamu

utaratibu wa Mtume (s.a.w.w.). Je, kama Mitume hawarithiwi mbona Umar alitofautiana na Abu Bakr!? Bibi Aisha alichagua kumiliki ardhi! Kama Mitume hawaaachi urithi, mbona bibi Aisha mke wa Mtume (s.a.w.w.) alipata urithi lakini binti yake Mtume (s.a.w.w.) akanyimwa! Haki iko wapi enyi watu wenye kutafakari? Zaidi ya hayo ieleweke kuwa ilikuwa ni amri ya Mwenyezi Mungu kwamba bibi Fatima (a.s.) apewe urithi huo wa Fadak: “Na umpe jamaa yako wa karibu haki yake....” (Qur’ani 17:26). Kusudio la kushuka Aya hiyo ni hiyo Fadak. Mabwana Bazaar, Abu Yala na Ibn al-Hatim wameipokea Hadithi kutoka kwa bwana Sa’id Khudri kwamba, iliposhuka Aya hiyo hapo juu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa bibi Fatima (a.s.) shamba hilo ambalo lilitekwa bila vita (mali ambayo kwa mujibu wa Amri ya Mwenyezi Mungu huwa ni mali ya Mtume ) mwaka wa 7 A.H kama tulivyoona nyuma. Vipi Abu Bakr apinge amri ya Mwenyezi Mungu? Yeye kapata wapi uwezo huo? Rejea: Ad-Durul-Manthur, cha Imam Suyutwii.

Kufutwa Zaka ya Khums: Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), Zaka hii ilikuwa inatolewa kwa amri ya Mwenyezi Mungu katika Qur’ani; 8:41. Sehemu ya Zaka hii ilikuwa ni kwa matumizi ya Mtume (s.a.w.w.) na Bani Hashim (Saadaat) pamoja na maskini, wasafiri walioharibikiwa, mayatima na wenye dhiki. Mara Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, Abu Bakr akaizuia Zaka hii ili kuwadhoofisha Ahlul-Bayt (a.s.) kiuchumi na hivyo kuwafanya wasiwe na hadhi yoyote mbele ya Umma wa kiislamu. Ukizingatia na kitendo cha Bibi Fatima (a.s.) kudhulumiwa urithi wake wa shamba la Fadak ambalo lilikuwa likitoa mapato mazuri, utaona kuwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) walibakia bila msaada wowote kiasi kwamba Imam Ali (a.s.) alilazimika kubeba na kuuza maji kwa watu ili apate mahitaji yake na familia yake! Bibi Fatima (a.s.) alidhalilika kiasi cha kuvaa nguo za viraka kwa sababu Bani Hashim hawaruhusiwi kupokea sadaka. Kwa upande wa madhehebu ya Shia Ithna’asheri, Zaka hii 193


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 194

katika Uislamu

(Qur’ani 8:41) inaendelea kutolewa na kuwakilishwa kwa Mujtahid ambaye ndiye mwakilishi (au mrithi) wa Imam - baada ya kughibu Imam wa 12 (a.s.). Ufafanuzi zaidi utatolewa mbele. Hapa tutaona kuwa iwapo Sunni wangeamua kutekeleza amri hii ya Qur’ani, sijui Zaka hii wangempa nani tukizingatia kuwa tangu zamani Sunni hawakujiambatanisha na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.). Kuwepo kwa Zaka hii ya Khums milele, ni ushahidi mwingine kuonyesha kuwa uongozi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ulikusudiwa na Mwenyezi Mungu kuongoza Waislamu milele hadi Kiyama.

UTAWALA WA UMAR IBN AL-KHATTAB Abu Bakr Sidiq alikuwa khalifa kuanzia mwaka 11 A.H (632 A.D) hadi alipofariki mwaka 12 A.H (633 A.D). Bwana Abu Bakr alipokaribia kufariki alimwita Uthman Ibn Affan aandike wasia wake (Abu Bakr) kama ifuatavyo: “Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa rehema, Mwenye kurehemu. Hii ni amri ya Abu Bakr kwa Waislamu ambapo........... (Kufikia hapo akazimia). Lakini Uthman akaongeza: ‘Namchagua Umar Ibn al-Khattab kuwa mrithi wangu kati yenu.’” Abu Bakr aliporejewa na fahamu alimwamuru Uthman kusoma yaliyoandikwa. Uthman akasoma. Abu Bakr akasema: Allahu akbar (Mungu Mkubwa), na akafurahi sana na kuongeza, ‘Nadhani uliogopa kwamba watu hawataafikiana miongoni mwao iwapo ningefariki bila kukamilisha wasia.’2 Uthman akajibu, ‘Ndiyo.’ Abu Bakr akasema, 2 Je, hushangai ewe Muislam! Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka karatasi na kalamu ili kuandika wasia wake, yeye aligomewa na ikatamkwa “Kinatutosha Kitabu cha Mwenyezi Mungu,” lakini Abu Bakr anakubaliwa kuacha wasia, ili wasije wakahitilafiana Waislam baada yake! (Mhariri) 194


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 195

katika Uislamu

‘Mungu akuzawadie kwa niaba ya Uislamu na Waislamu.’ Rejea: (a) Tarikh Tabari, uk. 2138-2139 (b) al-Imama was-Siyasah, chini ya kichwa cha habari: Abu Bakr kumchagua Umar. Kwa hiyo kwa mara nyingine tunaona jinsi Abu Bakr alivyompa ukhalifa mwenzake yaani bwana Umar. Hatuoni matumizi ya Shura au hiyo inayoitwa ‘Demokrasia ya kiislamu’. Huu ulikuwa ni uamuzi wa mtu mmoja kama vile mfalme anavyoamua kumrithisha ufalme mtoto wake. Tukirejea matukio yote kuelekea kufariki Mtume (s.a.w.w.) na baada yake, hatutashangaa kuona Abu Bakr anampa ukhalifa Umar moja kwa moja! Kwa kweli hata katika utawala wa Abu Bakr utaona kuwa kuna mambo mengi ambayo Umar alionekana wazi kumpinga Abu Bakr! Kwa maana kwamba walishirikiana ukhalifa! Kwa mfano katika historia tunasoma kuwa ilikuwa kawaida ya Mtume (s.a.w.w.) kutenga fungu la ‘sadaqa’ kwa ajili ya wale watu wanaoelekea kukubali Uislamu na wengineo, kwa kadri ya Qur’ani:-

“Sadaqa ni kwa ajili ya masikini na wenye dhiki na walioajiriwa kuikusanya, na wale ambao nyoyo zao zinaelekea (kukubali Uislamu) na kuwakomboa mateka wa vita, na wale wenye madeni, na katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri; hii ni amri ya Mwenyezi Mungu; Naye ni Mjuzi wa yote, Mwenye hekima.’’ (Qur’ani 9:60). Sasa, katika utawala wa Abu Bakr Sidiq, walikwenda watu kwake kuomba msaada huo. Abu Bakr aliwapa kibali waende kwa Umar awape haki yao. Hao watu walikuwa ni wale ambao wanaelekea kuukubali Uislamu. 195


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 196

katika Uislamu

Walipomwendea Umar na kumpa kibali chao, Umar alichukua kibali hicho na kukichana na kuwaeleza kuwa, ‘Hatuna haja na ninyi, Mwenyezi Mungu ameshaimarisha Uisalmu ambao hauwahitaji ninyi. Mkitaka kusilimu, sawa, kama hamtaki, upanga utahukumu kati yetu.’ Baada ya hapo watu hao wakarejea kwa Abu Bakr kulalamika kwamba,’ Wewe ndiye khalifa au Umar? Akajibu ‘Naona ni Umar, Mwenyezi Mungu akipenda!’ Kwa hiyo Abu Bakr alikubaliana na upinzani wa Umar kinyume na amri ya Qur’ani! Kuna wanavyuoni wanaomtetea Umar kwa tendo hilo eti alifanya ‘ij’tihad’ kulingana na wakati! Hoja hii haina msingi kwa sababu amri za Qur’ani zitadumu hadi Kiyama bila kuathirika na mabadiliko ya kisayansi au kijamii. Qur’ani ilikusudiwa kuongoza watu hadi Kiyama. Ni juu yetu kujirekebisha tulingane na matakwa ya Qur’ani, tuzifuate aya zinakotupeleka na siyo tuirekebishe Qur’ani ifuate matakwa yetu! Ndiyo maana hukumu ya kufupisha Swala inaendelea bila kujali maendeleo makubwa ya sasa hivi ya vyombo vya usafiri, ukilinganisha na usafiri wa ngamia na farasi wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.)! Rejea: Al-Jawhari al- Nayyira fiy fiqh al-Hanafi, Jz. 1 uk. 164. Kitendo hicho cha Umar ni kukiuka maneno ya Qur’ani:-

“Na wanaposomewa Aya zetu zilizo wazi, wale wasio na matumaini ya kukutana Nasi husema: Lete Qur’ani nyingine isiyokuwa hii. Waambie: Siwezi kuibadili kwa hiari ya nafsi yangu; sifuati ila yanayoteremshwa kama wahyi kwangu. Mimi naogopa kama nikimuasi Mola Wangu, adhabu ya siku iliyo kuu (Siku ya Kiyama).” (Qur’ani 10:15). 196


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 197

katika Uislamu

Kwa upande wa Sunna tunasoma kuwa, ‘Alichohalalisha Muhammad ni halali hadi Siku ya Kiyama. Na kile alichokiharamisha ni haramu hadi Siku ya Kiyama’. Hadithi hii ni maarufu sana miongoni mwa Waislamu waaminifu wenye ujuzi wa dini. Haina haja ya rejea. Katika Ibada ya Hijja: Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) aliswali rakaa mbili hapo Mina katika ibada ya Hijja. Katika utawala wa Abu Bakr naye alifanya hivyo. Lakini katika utawala wa Umar na Uthman wao waliswali rakaa 4 hapo Mina katika ibada zao za Hijjah. Rejea: (1) Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 154 (2) Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 260. Kuhusu Udhu wa Tayamam: Qur’ani 5:6 imeamrisha matumizi ya Tayamam na kanuni zake. Lakini katika utawala wake Umar aliipinga Qur’ani na Sunna - Rejea: Sahih alBukhari, Jz. 1, uk. 88. Mtu mmoja alimwendea Umar siku hizo na kumwambia, ‘Nimechafuka na siwezi kupata maji ya kujisafisha.’ Umar alimjibu kuwa, ‘Basi usiswali’. Lakini bwana Ammar akamwambia, ‘Hukumbuki ewe kiongozi wa waumini, wakati mimi na wewe tulipokuwa tunasafiri, mimi na wewe tukachafuka. Wewe hukuswali wakati mimi nilijiviringisha kwenye vumbi nikaswali. Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ingetosha wewe kupiga viganja kwenye ardhi na kupuliza viganja kisha kujipaka na mikono.” Umar akasema: ‘Mwogope Mwenyezi Mungu ewe Ammar!’ Ammar naye akasema, ‘Kama hutaki watu wayasikie sitayaelezea.’ Ushahidi huo wa wazi ulitolewa na sahaba kuhusu Mtume (s.a.w.w.) alivyoamrisha Tayamam lakini Umar alitumia ‘ijtihad’ yake na kuamuru kuwa, ‘Kama hakuna maji acha kuswali ili siku ya baridi watu wasije wakapata kisingizio cha kutotumia maji!’ Rejea: (1) Sahih al-Bukhari, Jz. 1, uk. 91 (2) Sahih al- Bukhari, Jz. 1, uk. 52 & 54. Taraweh kuswaliwa Jamaa: Katika utawala wake bwana Umar, siku moja mwezi wa Ramadhan, aliku197


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 198

katika Uislamu

ta watu wanaswali Taraweh msikitini kila mtu peke yake kama ilivyokuwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.). Umar akiwa kiongozi mkuu, aliamuru kuwa Swala hiyo ianze kuswaliwa jamaa kama wafanyavyo leo madhehebu ya Sunni! Kesho yake alipokuta Swala hiyo inaswaliwa jamaa akasema, ‘Hii ni bidaa nzuri sana!’ Rejea: (1) Sahih al-Bukhari Jz. 3, uk. 126127, tafsiri ya kiingereza. Umar anywa pombe kwa visingizio: Mwanzoni mwa kitabu hiki tumeona kuwa pombe haikuwa haramu kwa watu wote kabla ya Uislamu wa Nabii wetu Muhammad (s.a.w.w.). Hata hivyo nimeeleza kuwa kizazi cha moja kwa moja cha mababu zake Mtume (s.a.w.w.) hawakutumia pombe. Lakini mwanzoni mwa Uislamu ilishuka Aya ya kukemea matumizi ya pombe: “Wanakuuliza juu ya ulevi na michezo ya kamari. Sema: Katika hayo kuna dhambi kubwa na faida kwa watu, na dhambi yake ni kubwa kuliko faida yake...................” (Qur’ani 2:219). Baada ya kushuka Aya hiyo wengi wa masahaba waliacha pombe na kamari lakini wengine hawakuridhika kuacha mazoea yao mpaka iliposhuka Aya nyingine: “Enyi mlioamini msikurubie Swala mkiwa mmelewa mpaka muwe mnaelewa (vyema) mnayoyasema (katika Swala) ...........................” (Qur’ani 4:43) Hata baada ya kushuka aya hizi za wazi, bado kuna masahaba wengine ambao hawakuridhika kwa sababu wanahistoria mashuhuri wameweka kumbukumbu za masahaba maarufu wapatao kumi ambao walikusanyika katika nyumba ya Abu Talha ambapo sahaba Anas bin Malik aliyekuwa mdogo kuliko wote (miaka 18) alikuwa kama mhudumu akiwazungushia pombe huku wanakunywa! Walipolewa wakaanza kuomboleza vifo vya babu zao makafiri waliokufa katika vita vya Badri. Mara ikawa habari hizo 198


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 199

katika Uislamu

zimemfikia Mtume (s.a.w.w.) ambaye aliwaita na kusoma Aya hiyo (Qur’ani 4:43). Hapo ndipo Umar Ibn al-Khattab alisikika akisema ‘Intahaina! Intahaina! Yaa Rasuulullah’ (Tumeacha, tumeacha ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu). Ingawa baada ya hapo waliacha ulevi lakini katika hukumu za dini (fiqh) za madhehebu yote; imeelezwa wazi kuwa, mbali na kulewa, hata tone la pombe ni haramu. Anakaririwa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) akisema kuwa iwapo bwawa la maji litamwagwa pombe kisha likakauka, mahali hapo hawezi kupanda mboga za majani na kuzila. Anaongeza kuwa ngazi ya chini kabisa ya uharamu wa pombe ni mtu kufanya kazi ya ulinzi wa shamba ambalo zabibu zake hutengeneza mvinyo. Tukirejea katika kipindi cha utawala wa Umar tunamwona bwana huyo anawaeleza watu kuwa hakuna madhara kunywa kinywaji chenye asilimia ndogo sana ya ulevi (alcohol) ndani yake! Vilevile alihalalisha pombe kali kuwekwa maji (kuizimua) ili mtu asilewe! Anakaririwa mwandishi wa kitabu Iqdul Farid akisema kuwa hata baada ya pombe kuharamishwa kabisa, Umar aliendelea kunywa ‘Nabiidh’ kwa madai kuwa asipoinywa hiyo anapata taabu ya tumbo lake kusaga nyama ya ngamia! Hiyo ‘Nabiidh’ ni kinywaji kinachotokana na tende zilizovumbikwa kwenye maji. Uhalali wa kunywa ‘Nabiidh’ haupo ingawa baadhi ya ulamaa wa Sunni wanatoa hukumu za kuhalalisha unywaji wake, bila shaka kwa kuwa Umar alihalalisha! Ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa ziliposhuka Aya (Qur’ani 5:90-91), alipita mpiga mbiu mjini Madina akisoma Aya hizo kwa sauti ya juu na ndipo watu wakawa wanachukua hiyo ‘Nabiidh’ waliyo nayo majumbani na kuimwaga barabarani mitaani. Je, huyo Umar hakuwepo siku hizo? Au hakupata habari? Pombe ni haramu kwa kila hali. Katika utawala wa bwana Umar, mtu mmoja alimwendea na kunywa toka katika chombo (jagi) cha maji cha bwana Umar, akiamini kuwa ni maji! Lakini mtu huyo alilewa na aliporejewa na fahamu, Umar alimpiga viboko. Yule mtu aliomba msamaha akisema kuwa, ‘Nilikunywa kutoka kwenye 199


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 200

katika Uislamu

chombo chako.’ Umar akasema, ‘Ndiyo, lakini ulipaswa kuchanganya (kuzimua) na maji kwanza! Rejea: The Holy Qur’ani (Full Commentary) Mir Ahmad Ali - M.A. B.O.L, B.T. Juz. 1, India. Leo hii hata Waislamu walio wengi huamini kuwa nguruwe ni haramu sana kuliko pombe! Ndiyo maana siku hizi utaona baadhi ya harusi za Waislamu wameweka chupa za ‘bia’ mezani kwa bwana na bibi harusi wanakunywa! Lakini sijaona mezani kwa bwana na bibi harusi kumewekwa ‘ndafu’ ya nguruwe! Sijui Waislamu tunaelekea wapi kwa kuigiza mila za kikafiri kama hizo, pamoja na bibi harusi kuacha kuvaa hijabu na badala yake kuvaa mashela eti kwenda na wakati! Tunaukoka moto na tutauingia kesho akhera. Umar atoa hukumu bila ujuzi na hivyo akakosolewa na Imam Ali (a.s.): Wanaohalalisha Umar Ibn al-Khattab kuwa kiongozi mkuu wa Taifa la kiislamu hawazingatii suala la sifa muhimu za cheo hicho. Yeyote aliyeshika cheo hicho alitakiwa pia kutoa hukumu mbali mbali kwa waumini kwa mujibu wa Sharia. Iwapo aliyeshika cheo hicho hakuwa na ujuzi huo ina maana haki isingetendeka kwa raia. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa katika utawala wa makhalifa watatu wa kwanza. Ni wajibu wangu kufichua ukweli. Tukio mojawapo ni pale siku moja katika utawala wa Umar ambapo waliitwa kwake watu sita kwa tuhuma za uzinifu. Umar alitoa hukumu ya viboko mia moja kwa kila mmoja wao! Imam Ali (a.s.) akamwambia Umar kuwa siyo haki kutoa hukumu moja kwa wote. Umar alimpa nafasi Imam Ali (a.s.) kutoa hukumu anavyoona sawa. Imam Ali (a.s.) alitoa hukumu zifuatazo: Mtu wa kwanza alikuwa kafiri (Dhimmi) chini ya utawala (ulinzi) wa Taifa la kiislamu. Mtu huyo alizini na mwanamke wa kiislamu. Kwa hukumu sahihi ni kwamba kafiri huyo kwa tendo hilo anapoteza haki ya kuitwa ‘Dhimmi’ na hivyo hukumu yake auawe kwa upanga. 200


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 201

katika Uislamu

Mtu wa pili alikuwa mume mwenye ndoa na hivyo hukumu yake apigwe mawe hadi afe. Mtu wa tatu alikuwa kapera – hajaoa - kwa hiyo apigwe viboko mia moja. Wa nne alikuwa mtumwa kwa hiyo adhabu yake viboko 50. Wa tano alikuwa kijana mdogo – hajafikia baleghe, hivyo apewe onyo kali. Wa sita alikuwa kichaa hivyo aachwe huru. Rejea: The Holy Qur’ani (Full Commentary) ya S.V. Mir Ahmad Ali- M.A., B.O.L B.T - India - (chini ya maelezo ya Aya ya 2 ya Surat an-Nur). Tukio lingine ni pale ambapo siku moja katika utawala wa Umar mama mmoja alijifungua mimba ya miezi sita. Umar aliamua mama huyo kuuawa kwa kupigwa mawe, kwa madai kuwa mama huyo alistahili aonekane na mimba kwa miezi tisa au zaidi. Imam Ali (a.s.) alimwuliza Umar kwamba, kama huyo mama atamshitaki Umar kwa hukumu ya Qur’ani; je, Umar atakuwa na hoja gani ya kujitetea? Imam Ali (a.s.) aliitaja Qur’ani 46:15 isemayo kuwa muda wa mimba na kunyonyesha ni miezi thalathini. Kisha akataja Qur’ani 2:233 isemayo kuwa kunyonyesha mtoto inapaswa kuwa miaka miwili kwa maana kwamba ukiondoa miaka miwili katika miezi thalathini, unabakiwa na miezi 6 ambayo ni muda wa chini kabisa wa kudhihirika mimba! Kwa hiyo yule mama akawa ameachwa huru na kufutiwa mashitaka ya uzinifu. Rejea: The Holy Qur’ani - Full Commentary, Juz.1, Uk. 892, ya S.V. Mir Ahmad Ali. Kuna mifano mingi ya namna hii lakini hiyo miwili inatosha kuonyesha jinsi ambavyo hata hao tuliowaita al-Khulafaau Rashidun walivyokuwa ukimuondoa Imam Ali (a.s.) peke yake, ambaye ndiye mrithi halali wa kwanza wa Mtume (s.a.w.w.). Bila shaka upungufu huo ndio uliomfanya Umar kusikika kila mara akisema kuwa, “Kama si kuwepo Ali Ibn Abi Talib, Umar angeangamia.” Vile vile anakaririwa Umar akisema pia kwamba “Mwenyezi Mungu anilinde na tatizo ambalo kulitatua kwake 201


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 202

katika Uislamu

kunahitaji awepo Abul Hasan (Imam Ali).� Huo ni ushahidi mwingine wa kuonyesha jinsi ambavyo Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ndio pekee waliokuwa na ujuzi wa kuifasiri Qur’ani kwa usahihi na kuelewa matumizi sahihi ya hukumu za dini. Leo hii Uislamu unatukanwa kutokana na watawala wa kiislamu ambao hupotosha hukumu za dini ama kwa ujinga wao au ubinafsi wao. Sheria ya uzinifu huko nchini Pakistan imepindishwa kinyume na kanuni za dini, hadi kuwadhalilisha akina mama kwa kuwahukumu vifungo batili vinavyotokana na tuhuma bandia za uzinifu. Yote haya ni matokeo ya kuachana na msingi wa uongozi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.).

Talaka tatu kwa mpigo!: Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) mwanamke alipewa talaka moja kwa wakati mmoja na kufuatiwa na eda ya talaka, ya miezi mitatu. Ina maana kwamba katika muda wa eda hiyo mwanamke alipaswa kuishi kwa mume na kupewa mahitaji yake yote hadi eda iishe. Iwapo katika muda huo wa eda, mume ataamua kumsamehe mkewe, au iwapo atamwingilia kabla eda haijaisha, ina maana kwamba amemsamehe na talaka imefutika (imebatilika). Lakini iwapo muda wa eda utaisha, basi itahesabika talaka moja ambayo hata hivyo haiwazuii wahusika kurudiana. Na kama mwanamke atapatikana na kosa la pili siku nyingine, na ikabidi apewe talaka, itakuwa talaka ya pili. Iwapo talaka hiyo ya pili itafuata utaratibu huo huo na kukamilika, basi itahesabiwa ni talaka ya pili. Kama mwanamke huyo atapewa talaka ya tatu siku zifuatazo katika ndoa yake, na iwapo talaka hiyo itakamilika, basi hapo mke na mume watalazimika kutengana kabisa baada ya eda ya talaka hiyo. Iwapo watataka kurudiana, itabidi mke aolewe na mume mwingine kwanza na aachike kihalali na mume huyo, ndipo anaweza kumrudia mume wake wa zamani tena kwa kufunga ndoa upya. Hata hivyo haikatazwi mume kumwacha kabisa mke wake kwa talaka ya kwanza au ya pili. Kinachokatazwa ni kumpa talaka tatu kwa mpigo! Hiyo 202


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 203

katika Uislamu

ni haramu. Rejea: Sahih Muslim, Jz. 2, uk. 404, chini ya Kitab at-Talaq (Toleo la kiingereza). Matendo haya ya hao Makhalifa waliochukua madaraka ya kutawala, yanatukanisha Uislamu kwa wasio Waislamu. Kwa sababu utasikia watu wanasema kuwa ndoa za kiislamu ni rahisi kuvunjika, ambapo hiyo siyo kweli iwapo tungefuata alivyoamrisha mwenyewe Mtume (s.a.w.w.)! Tutaona kuwa iwapo utaratibu nilioeleza hapa utatumika, talaka nyingi zitafutika katika muda wa eda kwa sababu utaona kuwa kama mke kamkosea mumewe na wakakaa pamoja miezi mitatu ya eda, bila shaka hasira zitaisha na watasameheana au mume atamwingilia mke wake na hivyo kubatilisha hiyo talaka! Au katika muda huo labda mume atakuwa amepeleleza na kugundua kuwa mke wake hakutenda kosa analotuhumiwa nalo na hivyo kubatilisha talaka! Je, Waislamu wangefuata mwenendo huo wa Mtume (s.a.w.w.) vipi ingekuwa rahisi ndoa za kiislamu kuvunjika? Tukirejea historia ni kwamba aliyeamrisha talaka tatu kwa mpigo ni Umar ibn al-Khattab kwa mara ya kwanza. Wakati wa utawala wa Abu Bakr hazikutolewa talaka tatu kwa mpigo. Madhara yake ni kwamba hivi sasa ni karne 14 tunatumia amri ya Umar badala ya alivyoamrisha Mtume (s.a.w.w.)! Je, ni wanawake wangapi wamedhulumiwa kwa kuachika bila haki? Hiyo ‘ijtihad’ ya Umar imeleta manufaa gani katika Uislamu? Labda tujikumbushe maneno ya Qur’ani :

(a) “Na anachokupeni Mtume kipokeeni na anachokukatazeni jiepushe nacho, na mcheni Mwenyezi Mungu.” (Qur’ani 59:7)

“Haiwi kwa muumini mwanamume au muumini mwanamke kuwa na 203


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 204

katika Uislamu

uchaguzi katika mambo yao wakati Mwenyezi Mungu na Mtume wake wameshakata shauri.” (Qur’ani 33:36). Hatuoni mahali popote katika Qur’ani au Sunna ambapo bwana Umar, Abu Bakr, Uthman au sahaba yeyote yule aliyeruhusiwa kupinga amri ya Mtume (s.a.w.w.) au Qur’ani. Kama angekuwepo sahaba anayestahiki kumkosoa Mtume (s.a.w.w.) ni Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa, “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Vile vile Mtume (s.a.w.w.) alisema, “Hakuna amjuaye Allah ila mimi na Ali, na hakuna anijuaye mimi isipokuwa Allah na Ali, na hakuna amjuaye Ali isipokuwa Allah na mimi.” Lakini pamoja na uzito wa maneno hayo ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Ali (a.s.), hatuoni popote katika historia ambapo Imam Ali (a.s.) alikwenda kinyume na mwenendo wa Mtume (s.a.w.w.) au Qur’ani! Rejea: (Kuhusu Umar na Talaka) (1) Al-Ghadir, cha al-Amini, Jz. 6, uk. 83-325 (2) An-Nass wa’l-ij’tihad, cha Sharafu’dDin uk. 155-276. Ndoa ya Muda Maalumu (Mut’ah): Ndoa hii ilitumika wakati wa uhai wote wa Mtume (s.a.w.w.) na pia muda wote wa utawala wa Abu Bakr Sidiq. Umar ibn Al-Khattab alipochukua Ukhalifa, ndoa hii ilitumika muda mfupi wa utawala wake kisha akaipiga marufuku kwa pamoja na ‘Mutatul Hajj.’ Aina hii ya ndoa ilitumika kumwoza binti yake Abu Bakr Sidiq yaani Asma, kwa bwana Zubair-al-Sahab, na kwa ndoa hiyo wakazaliwa watoto halali: Abdallah Ibn Zubair na Urwah Ibn Zubair. Na hiyo Mutatul Hajj au Umra kwa bahati hakufanikiwa kabisa kuifuta ingawa aliitamka kuifuta, kwani bado inatumika hadi leo! Hata hivyo aliamuru kuwa atakayefunga ndoa ya Mut’ah auawe na ikawa baadhi ya watu wameacha. Ingawa hivi leo baadhi ya Sunni wachache hutumia ndoa hii, na walio wengi wanaipinga na kuiita haramu, Shia Ithna’asheri bado wanaendelea kuitumia. Nitatoa maelezo zaidi hapa kama ushahidi wa uhalali wa ndoa hii kutoka katika Sunna na Qur’ani. Tuanze na (Qur’ani 4:24): 204


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 205

katika Uislamu

“Na (pia mmeharamishiwa) wanawake wenye waume isipokuwa wale wanaomilikiwa na mikono yenu ya kulia. Hii ni sheria ya Mwenyezi Mungu juu yenu, pia mmehalalishiwa wasiokuwa hao, ili muwatafute kwa mali zenu pasi na kuzini nao. Na wale ambao mmestarehe nao katika hao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu. Wala si vibaya kwenu (kuwapa kiasi zaidi) katika yale mliyokubaliana, hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi, Mwenye hekima.” ( Qur’ani 4:24 ). Ukichunguza Aya hii utaona kuwa inawazungumzia wanawake wa aina tatu kama ifuatavyo: Wanaomilikiwa na mikono yenu ya kulia: Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri, tafsiri yake ni wanawake watumwa waliotekwa katika vita halali vya Jihadi au kununuliwa. Lakini vita hivyo viwe vimeamrishwa na Mtume (s.a.w.w.) au na mmojawapo kati ya Maimamu 12 (a.s.) au kwa wakati huu amri itoke kwa Mujitahid anayeongoza Waislamu katika misingi ya Taqlid. Vita vilivyoamrishwa na kiongozi yeyote wa nchi yoyote kwa misingi ya kidunia, haviwezi kuitwa Jihadi labda kama ni vita vya kuwahami Waislamu dhidi ya maadui wa nje bila uchokozi kuanzia kwa Waislamu wanaojihami. Na pia mmehalalishiwa wanawake wengine wasiokuwa hao, ili muwatafute kwa mali zenu: Hapa tafsiri yake ni wanawake katika ndoa za kawaida tulizozoea yaani ndoa za ‘kudumu’. 205


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 206

katika Uislamu

Na wale ambao mmestarehe nao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu: Hili ni kundi la tatu la wanawake ambao kwa kadri ya Shia Ithna’asheri, ndio wanaohusika na ndoa ya muda maalumu yaani Mut’ah. Katika Aya hii maelezo yamewagawa wanawake sehemu tatu. Ingekuwa Aya hii inaongelea ndoa ya aina moja tu, isingetenganisha maelezo. Isitoshe kwa wajuzi wa lugha ya Qur’ani, maneno haya: Na wale ambao mmestarehe nao katika hao, ndiyo maneno yanayohusiana na ndoa ya Mut’ah kwa sababu tutaona baadaye kuwa aya hii ilishuka kwa ajili ya ndoa hiyo. Wakati Umar anaipiga marufuku ndoa hii alisema kuwa, “Kuna Mut’ah mbili ambazo zilitumika wakati wa Mtume (s.a.w.w.) na Abu Bakr ambazo nimezipiga marufuku na nitawaadhibu watakaokiuka amri hii.” Rejea: Musnad ya Imam Ahmad Ibn Hambal. Katika Sahih Muslim, anakaririwa sahaba mmoja bwana Abdullah bin Masu’di akielezea juu ya madai kuwa ndoa hii ya Mut’ah ni haramu, alijibu kuwa katika vita ya kuiteka Makka, masahaba waliomba wahasiwe ili wasizini kwa sababu hawakuongozana na wake zao. Mtume (s.a.w.w.) aliwakatalia na badala yake aliwaamuru wafunge ndoa ya Mut’ah kwa muda maalumu utakaokubalika kati ya wahusika, lakini watoe nguo moja kuwapa wanawake kama mahari. Katika Sahih al-Bukhari, Juzuu ya sita ukurasa 37 tafsiri ya kiingereza ya Dr. Muhammad Muhsin Khan wa Chuo Kikuu Cha kiislamu hapo Madina, tunasoma kuwa siyo tu kama Mtume (s.a.w.w.) karuhusu, bali pia aliwahimiza masahaba kufunga ndoa hii. Masahaba wawili mabwana Jabir bin Abdulla Al-Answari na Salama bin Al-Akwa wanasema kuwa Mtume alituma ujumbe kwa sahaba zake jeshini akiwaeleza kuwa, “Mmeruhusiwa kufunga ndoa ya Mut’ah, hivyo ifanyeni.’ Kisha aliwaeleza jinsi ya kufunga kwa kusema kuwa, ‘Iwapo mume na mke watakubaliana, isipungue muda wa siku tatu lakini wakitaka kuongeza 206


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 207

katika Uislamu

muda wanaruhusiwa; na wakiamua kuachana pia wanaruhusiwa.’” Maelezo haya yamo katika Hadithi namba 52. Zaidi ya hayo wakati huo, tayari ilishashuka Qur’ani 23:6 kukataza uzinifu. Kwa hiyo kama madai ya kuwa ndoa ya Mut’ah ni uzinifu, vipi Mtume (s.a.w.w.) angeamrisha masahaba zake kuzini? Wale wanaodai kuwa hakuna Aya ya ndoa ya Mut’ah sio waaminifu kwa sababu kwa kadri ya masahaba wa karibu sana na Mtume (s.a.w.w.) kama Abdullah bin Abbas, Abdullah bin Mas’ud na Ubayy bin Ka’b, aliyekuwa mwandishi wa wahyi mmojawapo, wanasema kuwa maneno ya Qur’ani 4:24; FAMASTAM-TA’TUM BIHI MINHUNNA yana maana ya, wale mnaotaka kustarehe nao katika ndoa ya mut’ah. Tafsiri hii inakubaliwa na ‘mufasiriina’ wote, hata wale wanaodai kuwa eti Aya hiyo ya Mut’ah ilibatilishwa! Kwenye Hadithi, maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yako hivi: “Innahu qad udh’na lakum an tastamti’u fastamti’u” maneno ambayo yana maana kuwa: Mmeruhusiwa kufanya ndoa ya Mut’ah hivyo ifanyeni. Na siyo tafsiri potofu ya kuwa: Mmeruhusiwa kuburudika hivyo burudikeni! Kwenye Sahih Muslim anakaririwa sahaba maarufu bwana Jabir Ibn Abdullah Al-Answari akijibu madai kuwa Mtume (s.a.w.w.) alizuia ndoa hiyo. Sahaba huyo anasema kuwa, ‘Tulizoea kufunga ndoa hiyo kwa kutoa tende au unga kama mahari wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) na wakati wa utawala wa Abu Bakr, mpaka utawala wa Umar alipozuia katika utawala wake. Hiyo ni Hadithi ya 3249 - Sahih Muslim, Juzuu ya pili. Kwa kweli masahaba wa karibu na Mtume (s.a.w.w.) walikiri kuwa amri ya Umar ilikiuka mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani. Kwa mfano bwana Abdullah bin Umar (mtoto wa Umar) alipoulizwa juu ya uhalali wa amri hiyo ya baba yake alijibu, ‘Hatuwezi kufuata maneno ya baba yangu na kuacha Sunna ya Mtume (s.a.w.w.)!’ Sahaba mwingine bwana Imran bin His’win akizungumzia amri hii ya 207


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 208

katika Uislamu

Umar alisema kuwa, ‘Aya ya Mut’ah iliteremka katika Qur’ani kwa hiyo tukaifanya tukiwa na Mtume (s.a.w.w.) na hakuna Aya yoyote iliyoteremka tena kuharamisha ndoa hiyo wala Mtume (s.a.w.w.) kuiharamisha hadi alipofariki, lakini Umar aliikataza kwa matakwa yake binafsi. Rejea: Sahih al–Bukhari, Juzuu ya 6 Hadithi Na. 43, Tafsiri ya kiingereza ya Dr. Muhammad Muhsin Khan-Chuo kikuu Madina. Wale wanodai kubatilishwa kwa Aya hiyo (Qur’ani 4:24), baadhi ya Aya wanazodai zilibatilisha Aya hiyo, zilishuka Makka kabla hata Aya hiyo (4:24) ya Mut’ah haijashuka Madina! Vipi Aya itabatilishwa kabla hata haijashuka na kutumiwa? Wapinzani wengine wanamsingizia Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) eti aliwaambia kuwa ndoa hiyo ilikatazwa katika vita vya Khaybar mwaka wa 7 A.H! Masahaba wote hata wapinzani wa ndoa hii, wanaafikiana kuwa ndoa hii iliamrishwa na Mtume (s.a.w.w.) katika vita vya kuiteka Makkah toka kwa makafiri mwaka 8 A.H! Sasa ni vipi ndoa hii ingebatilishwa kabla ya kutumika! Upinzani wa ndoa hii hauna uzito wala ushahidi wa kutegemewa katika mafunzo ya dini. Ndoa ya Mut’ah ni halali. Faida za ndoa ya Mut’ah kwa jamii: Msimamo wa Shia Ithna’asheri ni kwamba kila aliloamrisha Mwenyezi Mungu lina faida na hekima kubwa hata kama kwa akili zetu ndogo hatufahamu faida na hekima zake. Leo hii uzinifu umeongezeka sana duniani kwa sababu mbali mbali. Kwanza mfumo wa ndoa ya mke mmoja, unasababisha kubaki kwa idadi kubwa ya wanawake wasio na ndoa kwa sababu wanawake ni wengi kuliko wanaume katika nchi nyingi duniani. Takwimu zinaonyesha kuwa mnamo Septemba, 1939 kulikuwa na wanawake millioni 3 zaidi ya wanaume huko Uingereza. Baada ya vita kuu ya kwanza, wanaume millioni tatu walipoteza maisha na hivyo kuongeza pengo. Maelfu ya wanaume zaidi walibakia vilema wasioweza kuoa. Iwapo wakati huo kila mwanamume alioa mke mmoja, basi walibakia wanawake millioni 4 wasio na ndoa! 208


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 209

katika Uislamu

Huko Marekani (U.S.A.) takwimu zilionyesha kuwa mnamo mwaka 1970 kulikuwa na wanaume millioni 9 wasio na ndoa, dhidi ya wanawake millioni 12 wasio na ndoa. Takwimu za mwaka 1995 zinaonyesha kuwa huko Marekani kulikuwa na wanawake millioni nane wasioolewa, zaidi ya wanaume wasio na ndoa! Huko Guinea kulikuwa na wanawake 122 wasioolewa, kwa kila wanaume 100 wasio na ndoa. Hapa Tanzania kuna wanawake 100 kwa kila wanaume 95. Sababu za kulazimisha ndoa za mume mmoja kwa mke mmoja huko Ulaya, ni tofauti na hali halisi hapa Afrika. Imani ya huko Ulaya kwamba ndoa ya wake wengi humdhalilisha mwanamke, haikubaliki hapa kwetu kwa sababu wapo wanawake wengi ambao wangependa kuolewa ndoa ya wake wengi, mradi tu mume anayehusika anawajibika kikamilifu kwa wake zake; kuliko ndoa ya mume mmoja na mke mmoja, ambapo mume hawajibiki ipasavyo kwa familia yake. Rejea:- (1) Women in Islam Versus The Judeo-Christain Tradition -Myth and Reality cha Sharif Muhammad, kilichochapishwa na: Institute of Islamic Studies - U.K. 1995. (2) Islam - An Introduction - cha Begum Aisha Bawany Wakf - Karachi Pakistan. Kwa nyongeza hebu tujadili hoja zaidi za kuunga mkono ndoa za wake wengi kutoka kwa wasomi, waandishi na wana taaluma mbali mbali toka huko Ulaya kama ifuatavyo:Dr. Mc Farlane katika kitabu chake chenye kuelimisha kiitwacho, The Case For Poligamy, anaandika kuwa: ‘Bila kujali kama suala hili litajadiliwa kidini au kijamii, ni wazi kimaisha kwamba ndoa ya wake wengi haipingani na kiwango cha juu cha ustaarabu. Ndoa hii inatoa changamoto ya jinsi ya kutatua tatizo la hapa Ulaya la wanawake wapweke wasiotakiwa. Vinginevyo ni kuongezeka kwa umalaya, uvimada na ubikira wa kukarahisha usio na tumaini.’

209


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 210

katika Uislamu

Bwana George Ryley Scott, mtaalamu wa masuala ya jinsia, katika kitabu chake: History of Prostitution, anaandika kuwa: Asili ya mwanamume ni kutamani wake wengi, na kwa hiyo maendeleo ya ustaarabu yanaongeza hisia hiyo katika mwanamume. Bwana Havelock Ellis, akieleza juu ya suala hili katika kitabu chake: The Psychology of Sex – Juz. 4, uk. 495, anasema kuwa: “Kama tutatafsiri kwamba mwanamume asili yake ni mnyama mwenye matamanio ya asili ya kupenda kubadili wanawake, basi kuna ushahidi mkubwa wa kuunga mkono ukweli huu.” Mtaalamu (Mfaransa) wa Jinsia Dr. Le Bon alitabiri kuwa mwisho wa yote mabunge ya Ulaya yatatambua umuhimu wa ndoa ya wake wengi na kuihalalisha. Anaongeza kuwa: Kurejea ndoa hii ambayo ni ya asili (natural) kutatatua maovu mengi kama ukahaba, maradhi ya zinaa, utoaji mimba na madhara yake ya watoto haramu, mateso kwa mamillioni ya wanawake wasioolewa kutokana na uwiano mbaya kati ya wanaume na wanawake kwa idadi. Hoja itolewayo na baadhi ya watu wa Ulaya ni kwamba ndoa hii ni kinyume na ustaarabu na kwamba haikubaliani na matakwa ya nyakati hizi. Lakini historia imejaa ushahidi kuwa nyakati zote za ustaarabu wa binadamu, ndoa ya wake wengi iliendelea kuwepo mpaka leo kwa umuhimu wake. Ushahidi huu unapatikana katika Encyclopaedia Britannica, toleo la 14, Juzuu ya 14 ukarasa 949. Bwana Max Nordan anaandika katika kitabu chake: Conventional Lies of Our Civilization - uk. 301, kwamba: Mwanamume huishi katika hali ya kutamani wake wengi katika nchi zilizostaarabika, ingawa hali ya mume mmoja na mke mmoja imewekwa katika sheria za nchi husika. Kati ya wanaume laki moja ni vigumu kupata mmoja ambaye anaweza kula kiapo katika kitanda chake cha mauti kuwa maisha yake alishiriki mke mmoja tu! Maelezo yote haya ni kuonyesha kuwa hata huko Ulaya au hapa kwetu 210


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 211

katika Uislamu

ambapo dini fulani fulani zinakataa ndoa ya wake wengi, wafuasi wake wanaishi tofauti na amri hiyo ya mke mmoja! Maana yake ni kwamba hulka ya binadamu yeyote yule, huwezi kuiondoa au kuizuia (suppress) mwilini mwake bali kuiongoza kwa kanuni zenye busara. Rejea:- Islam An Introduction – cha Begum Aisha Bawany Wakf - Karachi - Pakistan uk. 139 -142. Kiongozi mkuu wa Wakristo duniani mara kwa mara amesikika akilaani vitendo vya sheria mbali mbali za nchi kadhaa duniani, kuwaruhusu wanawake kutoa mimba. Lakini mnamo tarehe 29/1/98 Radio Sauti ya Ujerumani ilisikika ikitangaza mnamo saa saba na nusu mchana, katika moja ya vipindi vyake kwamba, katika Bara la Ulaya, Uingereza inaongoza kwa wasichana wasio na ndoa wapatao 58,000 kupata mimba kila mwaka! Bila shaka matokeo ya mimba kama hizi ni kuzaliwa watoto nje ya ndoa au wasichana kutoa mimba hizo. Yote haya ni matatizo makubwa katika jamii yoyote ile. Iwapo wasichana hao wangekuwa Waislamu na wakatumia japo ndoa ya Mut’ah, badala ya kuzini ovyo, kusingetokea tatizo la utoaji mimba au kuzaliwa watoto haramu wasiotakiwa. Kwa hiyo tutaona kuwa uhuru wa binadamu usio na mipaka kwa kisingizio cha haki za binadamu, si jambo lenye manufaa yoyote kwa jamii yoyote ile. Shariah ya kiislamu inapaswa kuongoza kila hatua ya maisha ya Mwislamu. Hivyo basi kwanza kabisa tutaona kuwa mfumo wa mke mmoja mume mmoja haujatatua mahitaji ya wanawake kuolewa wote. Hata hivyo mfumo huo siyo amri ya Mungu ingawa unatumika katika dini. Kwa upande wa Shia Ithna’asheri, ndoa hii inamsaidia mwanamume kutowajibika na matendo ya dhambi za mke wake. Nina maana kwamba, utaona katika baadhi ya ndoa, wanaume wanatawaliwa na wake zao. Matokeo yake ni kwamba wanaume hao, hawana sauti tena ya kuwaamrisha wake zao kutimiza sheria za dini kama vile kuswali Swala tano au kuvaa hijab n.k. 211


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 212

katika Uislamu

Katika ndoa ya kudumu, mwanamume anaandikiwa dhambi kwa kushindwa kumdhibiti mke wake. Maana yake ni kwamba kwa mfano, mume asipomwamuru mkewe kuvaa hijabu, yeye na mkewe wote wanaandikiwa dhambi! Madai ya baadhi ya wanaume kuwa wake zao wamewashinda, ni madai yasiyo na msingi kwa sababu kwa mfano, mwanamume ana haki ya kumpa talaka mke wake anayekataa kuswali Swala tano. Hata mke ana haki ya kumwacha mume iwapo mume huyo anamzuia kuvaa hijabu au kuswali Swala tano n.k. Lakini katika ndoa ya kudumu, mume anawajibika zaidi kwa sababu yeye ndiye kiongozi wa familia mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo mume asiyemdhibiti mkewe, ina maana anabeba dhambi za mkewe pia, katika ndoa ya kudumu! Kutokana na hali ya sasa hivi ya baadhi ya wanawake kutotaka kudhibitiwa, itakuwa busara kwa wanaume kutojiingiza mikataba ya ndoa za kudumu, na badala yake kufunga ndoa za Mut’ah kwa sababu katika ndoa za Muda Maalumu, hukumu zake ni kwamba mke anawajibika binafsi kwa matendo yake. Kinyume na hivyo, wanaume wengi wataendelea kubeba mizigo ya dhambi za wake zao, kwa sababu kimila, ndoa nyingi hazizingatii hatari hiyo na ndiyo maana kila ndoa ni ya kudumu! Kwa kweli hata wanawake katika ndoa za kudumu, wanaokubali kwa mfano, kuacha kuvaa hijabu, kwa kukatazwa na waume zao kwamba mavazi hayo ni ya kizee, na hayaonyeshi uzuri wa asili wa mwanamke wa kisasa; wanawake hao waelewe kuwa wameangamia - hapa duniani na kesho akhera. Ndoa ni ibada sawa na Swala tano. Hakuna Swala ambayo inasaliwa na watu watakavyo bila kufuata kanuni zilizowekwa. Kila ibada ni kumtii Mwenyezi Mungu tu; na ndiyo maana hatuwezi kuoana kwa misingi tutakayo bila kuzingatia matakwa ya Mwenyezi Mungu. Suala la msingi hapa ni kwamba, katika ndoa ni lazima mume na mke wote wamtii Mwenyezi Mungu, kwa kila mmoja kutambua kanuni za ndoa. Maana yake ni kwamba mke amtii mume katika mipaka ya Mwenyezi Mungu, na mume amwongoze mkewe katika mipaka hiyo hiyo. Kusiwepo na 212


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 213

katika Uislamu

mwelekeo wa mke kumwabudu mume au mume kumwabudu mke eti kwa kisingizio cha kupendana sana. Mungu hawezi kuamrisha mateso kwa watu. Yote haya yana faida kwetu japo hatujui. Mbele ya Mwenyezi Mungu, ndoa imewekwa kuzuia uzinifu na kulinda vizazi visichanganyike ovyo kwa mfano mtu kuzaa na mtu ambaye ni haramu, kama vile mtu kubeba mimba ya kaka yake au mjomba wake au kuzaa ovyo bila ndoa na ikawa mtoto akizaliwa hajulikani baba yake. Hivyo basi Mwenyezi Mungu alikusudia kila mtu aoe au kuolewa kwa sababu tendo la ndoa ni la asili (natural) katika miili ya binadamu wote, hata mtu awe taahira au kichaa. Kila binadamu atafikia wakati atahitaji huduma hiyo. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu hana upendeleo au uonevu, ina maana kila mtu anastahiki kuoa au kuolewa, lakini uzinifu umekatazwa. Kila Mwislamu mwaminifu na mjuzi wa dini, lazima afahamu kuwa Uislamu (Qur’ani na Sunna) unaongoza maisha ya binadamu hadi siku ya Kiyama na ndiyo maana Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa, ‘Alilohalalisha Muhammad ni halali hadi Siku ya Kiyama na aliloliharamisha ni haramu hadi Kiyama.’ Ina maana kuwa kanuni zote za kuongoza maisha ya binadamu zilishapangwa na Mwenyezi Mungu hata kama kwa ujinga wetu hatuzijui au hatuzitaki. Vile vile Mwenyezi Mungu alijua kuwa hapa duniani wanawake watawazidi wanaume kwa idadi na wala siyo bahati mbaya! Kwa hiyo lazima Mwenyezi Mungu alishaweka njia ya kuhakikisha kuwa kila binadamu ataoa na kuolewa kwa sababu kinyume na hivyo Mwenyezi Mungu atakuwa na sifa ya uonevu kutokana na ukweli kuwa amekataza kuzini lakini anawalazimisha watu kuzini (kimaumbile) na kasha aje kuwaadhibu Siku ya Kiyama! Na hiyo ndiyo busara ya Mwenyezi Mungu kuweka ndoa hii mbali na ndoa za kawaida tulizozoea kidini na kimila. Ndoa hii ya Mut’ah imekusudiwa kuleta manufaa yafuatayo, katika jamii: 213


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 214

katika Uislamu

(1) Wanaume wasioweza kumudu gharama za kuoa na kutunza familia: Hili ni kundi la kwanza la wanaume ambao ni wazima kimaumbile na wanataka kutimiza haja zao za mwili lakini hawana uwezo wa kiuchumi wa kuoa kwa ndoa za kawaida. Katika kundi hili twaweza pia kuunganisha wanawake ambao wanataka kukutana na wanaume lakini hawajapata nafasi ya kuolewa ndoa ya kudumu. Watu hawa wote wanaruhusiwa kufunga ndoa hii ya Mut’ah ili wasizini. Kwa masharti ya ndoa hii, iwapo watazaliwa watoto watakuwa halali kwa sababu masharti ya ndoa hii ni sawa na yale ya ndoa ya kudumu, kasoro tu unafuu wa mume kutowajibika ki-shariah kumtunza mke kwa sababu si lazima mwenye kuhitaji ndoa hii awe mume tu! Bali hata mke anawajibika kutafuta mume wa halali amwoe ili asizini. Kwa hiyo yawezekana pia ikawa huyo mama ana uwezo kiuchumi kuliko mwanamume! Hata hivyo kabla ndoa hiyo haijafungwa, ni lazima mke aridhike kuwa hatamtegemea mume kimaisha. Vinginevyo asiporidhika itabidi mume awajibike kumtunza au vinginevyo wasioane. Faida yake ni kwamba mume asiye na uwezo kiuchumi anaweza akaoa mke na kutimiza haja zake bila kuzini, kwa sababu kuzini ni dhambi kubwa kwa kadri ya adhabu ya mzinifu kwa hukumu za Mwenyezi Mungu. Mtoto anayezaliwa katika ndoa hii lazima atunzwe na mume. Leo hii tunawaona, kwa mfano, wanawake wasioolewa maisha yao yote, na wanaume wasiooa maisha yao yote, lakini wanazini na kuzaa ovyo nje ya ndoa. Iwapo wangetumia ndoa hii bila shaka wasingeingia dhambi ya kuzini kwa wale wanaotaka kumtii Mwenyezi Mungu. Zaidi ya hayo kwa matumizi ya ndoa hii, kusingetokea migogoro ya watoto haramu wasio na baba zao. Kwa vyovyote vile kwa ndoa hii, kila mwanamke angepata mume wa kukidhi haja zake bila kuzini hata kama hataolewa ndoa ya kudumu. Isitoshe hakuna muda maalumu (wa kiwango cha juu) wa ndoa hii bali ni maelewano kati ya wahusika. Lakini mke lazima awe na mume 214


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 215

katika Uislamu

mmoja tu kama kawaida ya ndoa zote. Bali mume anaruhusiwa kuwa na idadi yoyote ya wanawake kwa kadri ya uwezo na mahitaji yake. Busara yake ni kwamba wanawake ni wengi kuliko wanaume. Maelezo zaidi yatafuata mbele. (2) Wanaume waliooa na kuishi mbali; pia vijana waliokomaa tayari kwa ndoa: Wanaume waliooa na kwa namna moja au nyingine wakalazimika kuishi mbali na wake zao wana uwezekano wa kupatwa na dharura ya kuhitaji jimai, hivyo ni njia hii tu ya ndoa ya Mut’a ndio ufumbuzi wa halali wa dharura hiyo. Na kwa vijana, hawa ni vijana ambao umri wao tayari wanasikia haja ya kushiriki vitendo vya ndoa kwa sababu siyo hiari yao ni sawa na usingizi au njaa. Yawezekana vijana hawa bado wanasoma vyuoni kwa muda mrefu na wana uwezo wa kuzini lakini kuzini kumekatazwa. Vijana hawa wanaweza kufunga ndoa hizi na pengine wakazuia kuzaa hadi baadaye. Uzazi wa Mpango: Tufahamu kuwa kwa kadri ya sheria za kiislamu zilizo sahihi, Uislamu haujazuia kutumia njia za kuzuia mwanamke asibebe mimba. Kinachokatazwa ni kutoa mimba au kufunga kizazi bila sababu za kiafya kwa maoni ya daktari. Tunasoma katika Hadithi sahihi jinsi ambavyo Mtume (s.a.w.w.) aliwafundisha masahaba namna ya kuzuia mimba kwa kadri ya mbinu za wakati huo yaani tukizingatia kwamba hazikuwepo njia kama hizi tunazotumia wakati huu. Jambo la maana ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwafundisha masahaba jinsi ya kuzuia mimba kwa namna ambayo sitaieleza hapa. Hata hivyo Qur’ani inawataka baba na mama kuhakikisha kuwa mtoto wanayemzaa ananyonyeshwa miaka miwili (Qur’ani 2:233). Kibusara ni kwamba lazima iwepo njia ya kuzuia mwanamke asibebe mimba katika muda huo, na wala haina maana kuwa uhusiano wa kawaida 215


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 216

katika Uislamu

wa mume na mke unakoma kuwepo katika hiyo kwa miaka miwili! Kwa mantiki hiyo tutaona kuwa iwapo hakuna njia ya kuzuia mimba, itabidi mwanamke ashindwe kutii amri ya Qur’ani ya kunyonyesha miaka miwili, kwa sababu atabeba mimba na maziwa ya mtoto yataharibika! Ndiyo maana wale Waislamu wanaopinga uzazi wa mpango inabidi wafikirie upya! Maelezo zaidi juu ya mwongozo kamili wa ndoa ya kiislamu kuhusiana na kanuni na maadili, yanapatikana katika kitabu changu kingine ambacho kinatayarishwa kwa kuchapishwa Insha’Allah, kwa jina la

FAIDA YA UNYAGO KATIKA NDOA ZOTE. Huenda wengi wetu tusiafikiane na suala la vijana kujihusisha na vitendo vya ndoa lakini hali halisi ni kwamba karibu vijana wote siku hizi wanashiriki uzinifu. Mara nyingine wasichana wa shule wanabeba mimba na utaona wazazi wao wanagharimia kutoa mimba hizo kwa siri! Kwa hiyo tunaogopa mtoto asipoteze masomo lakini hatuogopi dhambi ya uzinifu! Tunaijali dunia na hatumuogopi Mwenyezi Mungu na amri Zake! Uislamu ni kujitoa nafsi yako yote kumtii Mwenyezi Mungu hata kama utapoteza kila ulichonacho! Katika kundi hili tunaunganisha pia watu wazima wanaokwenda nchi za mbali kusoma au kwa biashara kwa muda mrefu. Kwa kadri ya hukumu za madhehebu ya Sunni ni kwamba kwa mfano ukienda kusoma Ulaya kwa miaka mitano, kwa vyovyote itabidi uzini au ufunge ndoa ya udanganyifu! Nina maana kuwa Sunni walio wengi hawatambui ndoa ya Mut’ah. Kwa hiyo Sunni aliyeacha mke wake hapa na akaenda kusoma nje ya nchi au mbali na mkewe, hawezi kuoa huko mke wa pili kwa ndoa ya kudumu. Atakachofanya ili asizini, itabidi apate mwanamke, amdanganye, kuwa wanafunga ndoa ya kudumu! Kisha baada ya masomo yake, amtelekeze mama huyo huko! Kwanza ndoa kama hiyo ni batili kwa sababu ya udanganyifu! Pili, hata mwanamke huyo akipewa talaka si halali kwa sababu hana kosa! Lakini kwa upande mwingine haiwezekani mtu akae Ulaya miaka mitano ya 216


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 217

katika Uislamu

masomo bila kushiriki tendo hilo! Kwa hiyo tutaona kuwa ndoa tuliyozoea haitoshelezi mahitaji yote ya binadamu kwa nyakati zote! Hapa tena tunaona umuhimu wa ndoa ya Mut’ah iwapo inabidi tubakie ndani ya mipaka ya Mwenyezi Mungu, pale tunapolazimika kuwa mbali na maskani yetu ya kudumu. Nimetangulia kueleza kuwa Mwenyezi Mungu ametuacha huru kula, kunywa, kusinzia n.k.; bila kizuizi mradi tusivuke mipaka. Kwa hiyo si busara kumwambia mtu akiwa katika mazingira fulani aache kula kabisa! Madhali njaa siyo hiari ya mtu, lazima uhuru wa kula uwepo. Iwapo ‘Shari’ah’ ya kiislamu inatakiwa au imekusudiwa kutuongoza hadi siku ya Kiyama, lazima itatue kila tatizo la kijamii nyakati zote, mradi Waislamu wawe na ujuzi wa kutambua na kutumia kanuni zinazohusika ili kutatua tatizo litakalojitokeza. Nina maana kuwa kanuni au sheria zipo, lakini ujuzi wa dini tulionao ni kidogo sana, au hatuna uaminifu wala nia ya kumtii Mwenyezi Mungu. Mpaka hapa tumeona hekima ya ndoa hii hata kwa wanaume wenye ndoa zao, pamoja na wanafunzi watu wazima. Mbali na wanaume wanaolazimika kuwa mbali na wake zao wa ndoa za kudumu kwa masomo au biashara, hebu tuone wale wanaume walio nyumbani mwao na ndoa zao za kudumu kama nao wanahitaji kutumia ndoa hii ya Mut’ah? Tufahamu kuwa katika ndoa ya kudumu inawezekana mwanamke akawa ana kasoro za kiafya zinazomfanya asimtosheleze mumewe. Suala hili ni siri katika ndoa za watu. Lakini yawezekana mwanamume hataki kumwacha mke huyo labda wametoka naye mbali kimaisha. Hata hivyo huyo mume atahitaji apate mke mwingine japo kwa ndoa ya Mut’ah ili kukidhi haja zake iwapo hataki kuzini. Yawezekana pia ikawa mume huyo hana uwezo tena wa kuoa mke wa pili kwa ndoa ya kudumu. Kwa vyovyote kuzini ni rahisi mno kwa mtu asiyetaka kuishi katika mipaka ya dini! Haya yote tunajadili watu wanaotaka kuwa Waislamu waaminifu kwa Mwenyezi Mungu.

217


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 218

katika Uislamu

Mnamo tarehe 19/10/1999, shirika la habari la BBC katika kipindi chake cha ‘Ulimwengu wa Watoto’, Idhaa ya kiingereza, saa kumi na moja na nusu (11:30) jioni, lilitangaza kuwa, ‘Karibu nusu ya ndoa zote nchini Uingereza huishia kupeana talaka.’ Yaani ndoa hizo huvunjika. Tunatambua kuwa mara nyingi talaka kama hizo huwaathiri zaidi wanawake ambao sio wote wawezao kuolewa tena kwa urahisi. Je, wanawake kama hao wafanyeje ili watimize haja zao? Nina maana kwamba iwapo Uingereza ni nchi ya Kikristo, wanawake hao watalaka hawawezi kuolewa (kidini) hadi waume zao wafariki. Wanaume nao ni hivyo hivyo. Uwezekano wa watu hao kuoa au kuolewa unabakia kwa njia ya kisheria tu na siyo kidini. Kwa hiyo Ukristo haujatatua tatizo hili kwa manufaa ya wahusika. Katika ndoa nyingine, utakuta wanaume fulani wana nguvu nyingi katika tendo la ndoa, na kwa hiyo hawatosheki na mke mmoja wa ndoa ya kudumu! Na wakawa hawana uwezo wa kuoa wa pili wa kudumu! Wanaume kama hawa wakilazimika kutegemea mke mmoja, wanaweza kudhuru afya za wake zao, au kwa upande mwingine wanaweza kulazimika kuzini! Kwa hiyo hawa nao watahitaji ndoa ya Mut’ah ili kukidhi haja zao. Hali hii nayo ni siri katika ndoa za watu. Mara nyingi wanaume kama hawa hulaumiwa eti wana tamaa sana ya wanawake! Lawama kama hizo siyo halali kwa sababu tendo hilo ni sawa na njaa na hatusikii watu wenye njaa wakilaumiwa kwa kula milo mitano au sita kwa siku! Hayo hutegemea maumbile ya mtu. Vile vile tunawaona baadhi yetu mtu anakula chakula cha kutosha watu watatu wa kawaida, bila kulaumiwa kwa ulafi! Kwa hiyo asiyetosheka na mke mmoja kwa misingi hiyo tu, ni lazima Sharia ya kiislamu impe nafasi na uhalali wa kutimiza haja zake. Mwanamke naye ana haki ya kumwacha mwanamume asiyemtosheleza haja zake katika ndoa, kwa sababu wapo pia wanawake wasiotosheka kirahisi kimaumbile; au wenye wanaume wabovu kiafya au kimaumbile.

218


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 219

katika Uislamu

Yote haya ni masuala nyeti, yaani siyo mambo yanayoonekana au ambayo watu wanaweza kuyaeleza wazi wazi kwa wenzao! Kwa hiyo si busara kuyapuuzia au kuwalaumu wahusika. Jambo la maana ni kwamba Sharia ya kiislamu haipo kuwabana watu au kuwapa uhuru wa kuvuka mipaka, bali kuwaongoza na kuwapa uhuru ndani ya mipaka maalumu, kwa kuzingatia hata mahitaji ya mtu mmoja katika jamii. (3) Wanawake Wajane: Hapa tunajadili wanawake ambao walikuwa na ndoa zao lakini ghafla waume zao wakafariki. Hawa walizoea kutimiza haja zao kwa waume zao, sasa wafanyeje? Kutokana na familia zao, si rahisi wakaolewa tena ndoa za kudumu. Kwa vyovyote itafaa watumie ndoa ya Mut’ah ili wasizini. Kwa maelezo yote haya tumeona kuwa Mwenyezi Mungu alipoamrisha ndoa hii kupitia kwa Mtume (s.a.w.w.), alikusudia kutatua matatizo makubwa ya kijamii yanayotokana na uzinifu. Iwapo Mwenyezi Mungu anajua kuwa wanawake au wanaume fulani hawataoa au kuolewa ndoa za kudumu, basi angewaondolea haja ya tendo hilo, wakazaliwa na kuwa watu wazima bila kuhitaji tendo hilo, kwani siyo hiari yao bali ni maumbile (silika). Tatizo ni kwamba sisi binadamu hatutaki kuishi katika mipaka ya dini, na ndiyo maana siku hizi utasikia watu katika semina mbali mbali, wanadai kuwa eti ndoa za wake zaidi ya mmoja zinaeneza ukimwi! Tunasahau kuwa kinachoeneza ukimwi ni kukosa uaminifu katika ndoa zetu kwa sababu iwapo mume ana wake watatu ambao wote wanamtegemea mume wao mmoja kwa uaminifu wote, na mume huyo akawa anawategemea wake zake kwa uaminifu wote; huo ukimwi utatoka wapi? Lakini ndoa ya mume mmoja kwa mke mmoja ina usalama gani iwapo wahusika si waminifu, wanazini ovyo? Au mwanamume asiyetimiziwa haja zake na mke wake mmoja kutokana na sababu mbali mbali afanyeje kama siyo kuzini? Tukirejea kumtii Mwenyezi Mungu tutatatua matatizo yetu yote. Yeye ndiye aliyetuumba na kutumbaua vilivyo, hivyo akatuelekeza njia. 219


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 220

katika Uislamu

Lakini tunapokiuka maelekezo Yake ni kufanya maovu, na hakuna sheria za Bungeni zitakazotusaidia kumaliza matatizo yetu, ni kelele za mmilikiwa kupingana na Mmiliki Wake! Leo hii kutokana na balaa la Ukimwi, wengi wetu wanaamini kuwa ni adhabu ya Mwenyezi Mungu kutokana na binadamu kukithiri katika vitendo vya uzinifu. Siku hizi heshima ya ubinadamu tumeivunja na tumekuwa kama wanyama wasiojua watendalo. Pamoja na balaa hili la kutisha, utaona kuwa, bado uhuru wa kuzini unachukuliwa kama sehemu ya ustaarabu. Kwa hakika uzinifu unaongezeka kwa kasi sana duniani kote. Mnamo tarehe 23/9/1999, saa saba na nusu mchana, Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujeremani, katika kipindi chake cha ‘Afya ya Jamii’, ilitangaza kuhusu Mkutano Juu ya Ukimwi, uliofanyika nchini Zambia mwezi wa nane 1999, kwamba: ‘Huko Ivory Coast, mwalimu mmoja anafariki kila siku ya kazi kutokana na ukimwi! Takwimu za nchini Zambia zilionyesha kuwa kila kijana wa umri wa miaka 15 yuko hatarini kufa kwa ukimwi kwa asilimia 60! Mnamo tarehe 1/10/99, saa kumi jioni, Radio Tanzania Dar es Salaam ilitangaza kuwa watu 100 huambukizwa ukimwi kila dakika duniani kote kwa ujumla. Tarehe 21/10/99 Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujerumani ilitangaza juu ya Ukimwi katika kipindi cha ‘Afya yako’, kuhusiana na mkutano uliofanyika nchini Namibia tarehe 11-13 Oktoba, 1999 juu ya Ukimwi kwamba: “Bara la Afrika lina wakazi asilimia kumi tu ya watu wa dunia nzima, lakini lina wagonjwa wa ukimwi asilimia 70 ya dunia nzima; na kwamba Afrika ya Kusini peke yake, watu 1,600 huambukizwa ukimwi kila siku.” Nchini Zimbabwe, robo ya raia wake wote wana virusi vya Ukimwi. Kwa hiyo tutaona kuwa kuoa wake wengi siyo sababu ya kuenea ukimwi. Mnamo tarehe 20/11/99, saa nane na nusu mchana, Idhaa ya kiingereza ya BBC katika kipindi chake cha ‘African Perspective’, yalielezwa mambo yanayosababisha kuenea haraka kwa Ukimwi katika kabila la Waluo nchini Kenya. Ilielezwa kuwa takwimu za wakati huo, zilionyesha kwamba 220


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 221

katika Uislamu

katika kila watu watatu, mmoja ana virusi vya ukimwi. Sababu kubwa za hali hiyo zilielezwa kuwa ni mila potofu ya kurithi wajane, pamoja na mila ya kujamiana, kama sehemu ya kimila ya kuanza kutayarisha mashamba kwa upandaji mbegu na pia kusherehekea mavuno ya kwanza toka shambani! Yote hayo ni kinyume na mafunzo ya Uislamu. Ndoa ya kiislamu hairuhusu vitendo vya namna hii, na wala haimlazimishi mwananamke kuolewa na mume asiyemtaka. Maana yake ni kwamba iwapo katika ndoa ya kiislamu, mume ataishi na wake zake wengi katika mipaka ya dini, suala la ukimwi halitakuwepo kabisa. Uislamu ni mfumo kamili na sahihi wa maisha ya mwanadamu, laiti binadamu wangejua. Idhaa ya kiswahili ya Sauti ya Ujerumani ilitangaza katika kipindi chake cha ‘Afya ya Jamii’, tarehe 9/12/99, saa saba na nusu mchana kwamba nchini Kenya kwa ujumla, wanafariki watu 500 kila siku kutokana na ugonjwa wa ukimwi. Habari nyingine za kuaminika zilitangulia kueleza kuwa katika Chuo Kikuu cha Nairobi, hufariki mwanafunzi mmoja kila wiki kwa ukimwi. Mifano yote hii ya maafa haihusiani na kanuni za ndoa ya kiislamu. Je ndugu wasomaji, maafa hayo yanatokana na ndoa za wake wengi? Maisha katika mipaka ya ndoa ya mke mmoja au wake wengi ndilo jawabu la kujikinga na matatizo kama haya. Suala la msingi siyo kutafuta dawa ya ukimwi kama njia pekee ya kuondokana na balaa hili. Kwanza tufahamu kuwa, Mwenyezi Mungu akitaka anaweza kuleta balaa lingine la aina kama hii. Isitoshe, wataalamu wanatueleza kuwa, virusi vya ukimwi siyo vya aina moja kwa watu wote walioathirika! Maana yake ni kwamba hata ikipatikana dawa ya chanjo, itakuwa ni ya aina mojawapo tu ya virusi! Hatua ya kufikia kuvumbua chanjo ya kudhibiti aina zote za virusi vya ukimwi, bado ni ndefu sana. Bila shaka ndiyo maana watu wengi wanatambua kuwa ni adhabu ya Mwenyezi Mungu! Historia ya dunia haina mfano wake. Iwapo ndiyo hivyo, ni muhimu sisi Waislamu turejee katika mipaka ya kanuni za dini yetu kwa sababu kwa mfano, balaa la ukimwi siyo tishio katika nchi zinazotawaliwa na sheria za kiislamu kama Uarabuni na Iran; 221


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 222

katika Uislamu

ambako vyombo vya dola hudhibiti hata dalili tu za uzinifu. Lakini huku kwetu ambako tunadhani kuwa ‘Haki za Binadamu’ ni pamoja na uhuru wa binadamu usio na mipaka, bila shaka tutaangamizwa na uhuru huo huo! (Qur’ani 33:36). Mwisho nataka kuwajibu wale wanaodai kuwa Uislamu umeweka umri mdogo mno kwa mtoto wa kike kuweza kuolewa. Yawezekana umri wa miaka tisa ukaonekana mdogo mbele ya jamii, lakini jambo la maana hapa ni kwamba, Shariah ya kiislamu haishughulikii matakwa ya watu fulani tu bali inatawala maisha ya jamii ya dunia nzima. Nina maana kuwa, itatokea mahali fulani duniani, utamkuta msichana wa umri huo mwenye mwili uliokomaa kuliko umri wake! Msichana huyo huenda akashawishiwa kujihusisha na vitendo vya zinaa, au yeye binafsi akashiriki, kutegemea na anavyojisikia mwilini mwake. Iwapo ‘Sharia’ itamchukulia kuwa ni mtoto, wakati ambapo anashiriki tendo la zinaa kwa hiari yake, na ana uwezo wa kuzaa mtoto haramu, ina maana msichana huyo atakwepa kuwajibika kidini bila sababu za msingi. Hata hivyo ni sheria hiyo tu ya ndoa (kiislamu), ambayo imemwajibisha msichana katika umri wa chini sana, ili msichana huyo ama aolewe, au awajibike kwa kuzini. Lakini ukiangalia kwa mfano, sheria ya kutoza kodi raia wasio Waislamu katika taifa la kiislamu (ili kuwalinda wao na mali zao), utaona kuwa mtozwa kodi lazima awe na umri wa zaidi ya miaka ishirini. Busara yake ni kwamba kwa umri huo, mtu anaweza kufanya kazi ya kulipwa na hivyo kuwa na kipato. Kwa hiyo sheria za kibusara lazima zizingatie madhara yanayoweza kuletwa na wahusika, na hivyo kuwadhibiti. Haina maana kwa mfano kumwacha huru jambazi mwenye umri wa miaka 15 eti ni mtoto, wakati anao uwezo wa kuua watu na kuwanyanganya mali zao. Kwa hiyo umri huo haukuwekwa kama sheria kwamba lazima msichana aolewe umri huo, bali ni tahadhari ya kudhibiti vitendo viovu. Iwapo msichana huyo atajisikia haja hiyo, lazima aolewe au vinginevyo asubiri afikie utu uzima ndipo ashiriki mambo hayo. Kwa 222


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 223

katika Uislamu

vyovyote kwa kawaida, hakuna mwanamume mwenye haja ya kuoa mtoto mdogo namna hiyo, labda pale ambapo msichana huyo ni mkubwa kwa maumbile yaani anavyoonekana! Hata hivyo wajibu wa Mwislamu ni kutekeleza amri zote za dini bila kujali kama anaelewa hekima yake au hapana. Zaidi ya hayo ukichunguza mwenendo mzima wa watoto wa kike siku hizi, utaona kuwa kwa hiari zao, na mara nyingine bila kurubuniwa, wanajiingiza katika vitendo vya uzinifu katika umri mdogo mno kuliko zamani za miaka ya sitini kurudi nyuma! Je, ni bora mabinti hao waolewe ndoa halali au waendeleze umalaya na uzinifu na mwisho wapate hasara ya kudumu hapa duniani na kesho akhera? Lakini wataolewa vipi iwapo tunatunga sheria za kidunia kuzuia wasichana wasiolewe umri huo? Vile vile tunafahamu kuwa hatuwezi kutunga sheria imara za kufanikisha kuzuia kabisa wasichana hao wasizini! Ni kweli kwamba umri huo ni tatizo iwapo msichana atabeba mimba, lakini ni bora waolewe na wazuie mimba kwanza, kuliko kukaa bila kuolewa na kutumbukia katika maasi na maradhi mabaya. Maneno ya Qur’ani kwamba Mwenyezi Mungu alikusudia Uislamu kuwa dini nyepesi ni ya kweli, lakini sisi wenyewe ndio tumeifanya dini kuwa ngumu kwa kuachana na mafunzo sahihi na pia kutokuwa waaminifu kwa Mwenyezi Mungu. (Qur’ani 2:176). Kwa hiyo kitendo cha Umar kuzuia ndoa ya Mut’ah kimesababisha wanawake wengi kudhulumiwa kwa kutoolewa na mwisho kujiingiza katika vitendo vya zinaa pamoja na kuzaa nje ya ndoa. Je hiyo nayo ni ‘Ijtihad’? Kanuni za Ndoa ya Mut’ah: Mwisho ningependa kueleza kanuni muhimu za kufunga ndoa hii, ili ieleweke wazi kuwa siyo nyepesi kama baadhi yetu wanavyofikiria. Hakuna urahisi wa kuitumia vibaya:

223


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 224

katika Uislamu

(1) Tamko la Ndoa. (Kwa ndoa zote): Tamko rasmi lazima litamkwe na wahusika kwa kauli zao au kwa kuwakilishwa na mawakili wao.

(2) Idhini ya baba au babu wa mke (Ndoa zote): Msichana bikira aliyefikia umri wa kuolewa lazima apate idhini ya baba yake au babu yake. Mwanamke aliyepoteza bikira kwa uzinifu au ndoa iliyotangulia, hahitaji idhini hiyo kuolewa.

(3) Muda wa ndoa utajwe na kiasi cha mahari: Tamko la Ndoa litataja muda wa ndoa na kiasi cha mahari. Mwenye haki ya kupanga mahari ni mwolewaji (mwanamke) katika aina zote za ndoa. Wazazi hawana haki ya kupanga kiasi cha mahari. Na kile kiwango cha pesa ambacho hupangwa na wazazi mfano kama shilingi laki tatu au moja, siyo mahari kidini, bali hiyo ni mila. Kwa hiyo ndoa haiwezi kuzuiwa isifungwe eti kwa mume kushindwa kulipa hizo pesa. Mwanamke awe huru kupanga mahari atakayo, hata kama ni shilingi elfu tano kutegemea hali ya mume na makubaliano kati yao. Na mahari hiyo ni mali ya huyo mke. Masharti mengineyo ya kimila, hayo yanaweza kutekelezwa baadaye lakini yasiingilie kanuni za ndoa za dini ambazo ni muhimu ili ndoa iswihi. Ndoa ni rahisi bali mila ndizo zinakatisha tamaa wanaume na wanawake. (4) Mashahidi (Kwa ndoa zote): Mashahidi si muhimu, kwa sababu ndoa ni ibada sawa na kufunga Swala. Unapofunga Swala huwaiti mashahidi waone ulivyofunga Swala! Au unapochinja kuku huwaiti watu washuhudie kuwa hujala kibudu! Au unapofunga saumu huweki shahidi wa kushuhudia kuwa umefunga kweli! Mashahidi katika ndoa, umuhimu wao ni sharti la serikali kwa ajili ya vyeti vya ndoa basi. Kwa sababu tuelewe kuwa nia ya wewe kuoa au kuolewa imo moyoni mwako. Mashahidi hawajui nia yako kama kweli una nia ya kuoa au huyo mke utamwacha kesho! Sawa na mtu kushinda anatema mate 224


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 225

katika Uislamu

ili aonekane kafunga saumu wakati pengine moyoni mwake hajaweka nia ya kufunga! Nia yako anaijua Mwenyezi Mungu! Isipokuwa mwanamume anapotoa talaka lazima alete mashahidi ili atakapotengana na mkewe, na huyo mke akaolewa na mume mwingine, huyo mume asidai kuwa huyo mama bado ni mke wake. Zaidi ya hayo ni jambo la kawaida kuwaona mwanamume na mwanamke wameishi miaka mingi kama mtu na mkewe bila kufunga ndoa rasmi. Maana yake ni kwamba walichukuana bila shahidi yeyote na wanaishi kwa nia yao ya kuwa pamoja. Mashahidi hawasaidii kitu kama nia ya wahusika kudumisha ndoa haipo. (5) Cheti cha Ndoa (Ndoa zote): Cheti cha ndoa ni sharti la serikali na siyo kanuni ya dini. Kwa hiyo pale ambapo hakuna vyeti haina maana kuwa watu wasioane! Kwa maisha ya wakati huu, vyeti vinaweza kutatua migogoro ya mirathi pale mume anapofariki. Kwa ndoa ya Mut’ah hata hivyo cheti si muhimu kwa sababu inawezekana ikawa ni ndoa ya muda mfupi kutegemea mahitaji ya wahusika! Ushahidi wa ndoa hii siyo cheti bali ni uaminifu wa wahusika mbele ya Mwenyezi Mungu. (6) Urithi: Ndoa hii haina sharti la wahusika kurithiana pindi mmojawao akifariki. Lakini wakitaka kurithiana itawabidi wakubaliane hivyo na waweke ushahidi tangu mwanzo wa ndoa yao. (7) Eda ya Talaka au Kifo: Mwanamke lazima aingie eda iwapo ndoa itavunjika au muda wa ndoa ukiisha au mume akifariki. (8) Mke awe hana mume mwingine: Katika ndoa hii ni lazima mke awe na mume mmoja tu kama ndoa ya kudumu. Kwa upande wa mwanamume katika ndoa ya Mut’ah, ameruhusiwa 225


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 226

katika Uislamu

kuwa na idadi yoyote ya wanawake. Isipokuwa katika ndoa ya kudumu, mwanamume haruhusiwi kuoa zaidi ya wanawake wanne. Sababu yake mojawapo ni kwamba ndoa ya Mut’ah faida yake mojawapo imekusudia kusaidia idadi kubwa ya wanawake kupata wanaume kwa hiyo wanaume wawe huru kuoa wanawake hao. Lakini katika ndoa ya kudumu, ni lazima mume awape mahitaji yao yote wake zake na asiwategemee jasho lao, ni haramu! Kwa hiyo si rahisi wanaume kuwatunza wanawake zaidi ya wanne katika ndoa ya kudumu na ndiyo maana ikawekwa mipaka. Mpaka hapa tumeona kuwa ndoa hii ina kanuni ambazo wengi wetu si rahisi kuzitimiza. Maana yake ni kwamba haiwezekani Mwislamu yeyote akaitumia ndoa hii kama njia nyepesi ya kuzini ovyo, iwapo kanuni zote zitatimia! Nini maana ya mtoto wa haramu?: Kwa muda mrefu sasa, wapo Waislamu ambao wamekuwa wanazaa nje ya ndoa, na kisha utawasikia hasa wanaume, wanawaita baadhi ya Mashekhe wenye upungufu wa elimu sahihi ya dini, eti kuhalalisha watoto waliozaliwa nje ya ndoa! Tendo hili la kujidai kuhalalisha haramu ni la kustaajabisha na kusikitisha kwa sababu kwa nini tusihalalishe maovu mengine chungu nzima isipokuwa uzinifu peke yake? Huo uwezo tumeupata wapi? Mtoto wa haramu hawezi kugeuka kuwa halali, kwa sababu asili yake ni uzinifu ambao ni haramu. Huwezi kuuza pombe ukapata pesa eti ukajenga msikiti kwa pesa hizo na ukadai kuwa msikiti huo ni halali. Vile vile huwezi kufanya ibada ya Hijja kwa pesa za haramu. Kwa hiyo tutaona kuwa haramu haiwezi kuzaa halali. Tendo zima la eti kuhalalisha mtoto haramu, linaweza kuchukua muda zaidi kuliko ibada fupi ya kufunga ndoa yoyote kati ya hizi mbili yaani ya kudumu au ya muda maalumu! Kwa hiyo hakuna sababu ya msingi ya Mwislamu yeyote kuzini. Tukirejea hukumu sahihi kuhusu mtoto haramu, ni kwamba mtoto huyo ni mali ya mama yake. Mwanamume hana haki na mtoto huyo kidini labda kwa sheria za nchi. Kwa hiyo wanaume Waislamu wanaodai kumiliki 226


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 227

katika Uislamu

watoto wa haramu ni makosa. Maana yake ni kwamba iwapo mtoto haramu atazaliwa, atafuata dini ya mama yake. Na pindi mtoto huyo akifariki, atazikwa na mama yake hata kama sura ya mtoto huyo inafanana na huyo mume aliyezaa na mama yake. Waislamu tujiepushe na kugang’ania mambo yanayopingana na dini eti kwa sababu tu ya kufurahisha nafsi zetu. Tufahamu kuwa kuzaliwa mtoto haramu hakutokani tu na mume Mwislamu kuzaa na Mkristo. Hata kama mwanaume na mwanamke wote ni Waislamu, uharamu upo pale pale! Hata kama mwanamume na mwanamke wameishi miaka mingi na kuzaa watoto wengi, mradi hawakufunga ndoa, basi watoto wote ni haramu! Hata wazinifu hao wakifunga ndoa, bado watoto waliotangulia kuzaliwa kabla ya ndoa, ni haramu hadi Siku ya Kiyama! Isitoshe tufahamu kuwa, maisha ya mke na mume wasio na ndoa, ni maisha ya uzinifu. Kwa kadri ya hukumu za Shia Ithnasheri na baadhi ya madhehebu ya Sunni, tendo moja la uzinifu, japo wa dakika tatu, humfanya mhusika kuwa najisi kwa siku arobaini hata akioga mara kumi! Maana yake ni kwamba watu wanaoishi na wenzao bila ndoa, siku zote miili yao ni najisi na kwa maana hiyo ibada zao zote ni batili. Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri ndiyo maana mtu mzinifu haruhusiwi kuongoza Swala ya jamaa. Kwa hiyo tutaona kuwa uzinifu ni dhambi kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu ingawa duniani kote watu wanazini ovyo. Tumeona katika Sura za nyuma kwamba kuongezeka uzinifu duniani, ni mojawapo ya dalili za kukaribia Kiyama na kwamba Mwenyezi Mungu ataleta maradhi ya uzinifu yasiyo na dawa na yasiyopata kuonekana kabla yake, kama adhabu ya uovu huo. Hayo ndiyo tunayoyaona wakati huu. Bila shaka ndiyo maana Mwenyezi Mungu akatuwekea urahisi wa kuoana ili tuepukane na uovu wa zinaa iwapo tutazingatia mafunzo sahihi ya dini. Uislamu unaheshimu ndoa kiasi kwamba iwapo mke na mume walifunga 227


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 228

katika Uislamu

ndoa ya Kikristo wakiwa Wakristo, kisha wakasilimu, basi ndoa yao itaendelea hiyo hiyo. Hawatafunga upya ndoa yao, kwa sababu madhumuni ya ndoa ni yale yale kidini. Kubadili maneno ya Adhana: Kwa kawaida kiongozi wa juu (khalifa) katika taifa la kiislamu ndiye alikuwa akiongoza Swala pale anapoishi. Siku moja katika utawala wa Umar alichelewa kuamka asubuhi ikawa ‘muadhin’ ameongeza maneno, ‘As Swalaatu khairum -minan-nawm’ kwa maana kwamba - Swala ni bora kuliko usingizi. Umar akiwa njiani aliyasikia maneno hayo na alipofika msikitini akaamuru maneno hayo mapya yawekwe kwenye adhana, na yale ya Hayya ‘Alaa Khayril ‘Amal (yaliyowekwa na Mtume (s.a.w.w.) katika tukio la Ghadiir Khum) kwa maana ya: Harakisheni kuja kwenye tendo bora kuliko yote - yaliondolewa yaani hayakutumika tena; lakini bado yanatumika katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri. Kwa kauli ya Umar anakaririwa akisema kuwa hayo maneno yaliyoondolewa ni kuzuia watu wasithamini Swala kuliko vita vya Jihad! Kwa maana kwamba watu wangeona Swala ni bora kuliko vita vya Jihad. Siku hizo vita vya Jihad vilikuwa vinapewa uzito sana, kwa sababu ya mapato makubwa ya ngawira, ili kutunisha Hazina (Baitul-Maal) kama tutakavyoona mbele. Umar achoma moto Hadithi na kuwaweka kizuizini wanaohadithia Hadithi za Mtume (s.a.w.w.)! Tunasoma katika Sahih Muslim - Kitabu cha Tabia, Somo la Kuomba Ruhusa, kwamba Umar alitishia kumpiga Abu Musa al-Ash’ari, kutokana na bwana huyo kuelezea watu Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.)! Bwana Abu Saidi al-Khudri anasema kuwa, “Tulikuwa tumekaa na Ubay bin Ka’b wakati Abu Musa al’Ash’ari alipofika akiwa ameudhika na kutueleza, `Je, hamkuwahi kumsikia Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa unapobisha hodi nyumbani kwa mtu ufanye hivyo mara tatu, ukikubaliwa ingia na usipokubaliwa urudi?’ Ubay akasema, ‘Kwani kuna nini?’ Abu Musa akasema, ‘Jana nilifanya hivyo kwa Umar na hakuitikia kwa hiyo nikaon228


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 229

katika Uislamu

doka. Leo nimemwendea na nilipomwona nikamweleza nilivyofanya jana, na ndipo Umar akasema, ‘Tulikusikia lakini tulikuwa na shughuli nyingi kwa hiyo ungeendelea kubisha mpaka uruhusiwe!’ Abu Musa akasema: mimi nikamjibu, ‘Nilibisha hodi kwa kadri ya mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.).’ Lakini Umar akaniambia, ‘Kwa jina la Allah, nitakucharaza mgongo na tumbo mpaka ukamlete mtu mwingine wa kushuhudia maneno yako.’ Abu Said alikwenda kwa Umar na kukiri maneno hayo ya Mtume (s.a.w.w.).” Ndugu wasomaji, tukirejea nyuma kabisa wakati Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, Umar alikataa Mtume (s.a.w.w.) asiandike wasia kwa madai kuwa Qur’ani inatosha kwa maana kwamba maneno ya Mtume (s.a.w.w.) siyo muhimu! Kwa hiyo hatushangai kuona Umar akikataza masahaba kuelezea maneno ya Mtume (s.a.w.w.)! Rejea:- (a) Al-Dhahabi, Tadhkira, Jz. 1, uk. 3-4. (b) Sahih alBukhari - Kitabu cha kuomba Ruhusa - somo la: Salamu na Kuomba Ruhusa Mara Tatu. Baada ya Umar kuzuia maelezo juu ya Hadithi za Mtume (s.a.w.w.), na kutishia kuwapiga viboko watakaovunja amri hiyo, alianza kuchoma moto Hadithi zote ambazo zilikuwa tayari zimekusanywa na masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Umar alihutubia watu kuwa, ‘Enyi watu, nimepata habari kuwa kuna vitabu mlivyonavyo (vya Hadithi). Ningependa, kwa jina la Allah, kwamba nivisahihishe vitabu hivyo na kuvibadili. Asibakie mtu yeyote miongoni mwenu mwenye kitabu, bali kila mmoja akilete kwangu nikikague.’ Watu walidhani kuwa Umar anakusanya vitabu hivyo ili kuhakikisha kuwa havina makosa, kwa hiyo wakampelekea vitabu vyao vyote na akavichoma moto! Rejea:- (a) Tabaqat al-Kubra cha Ibn Sa’d, Jz. 5 uk.188 toleo la Baghdad - Iraq. Umar hakuridhika na amri zake hizo kwani alisikia kuwa baadhi ya masahaba waliendelea kueleza waliyoyasikia kwa Mtume (s.a.w.w.), kila walipokutana katika safari zao nje ya Madina. Kwa hiyo Umar aliamua kuwazuilia wasitoke Madina, na hata kuwazuilia wasitoke majumbani mwao! Anakaririwa bwana Ibn Is’haq, naye akimkariri Abdur-Rahman bin 229


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 230

katika Uislamu

Awf akisema kuwa, ‘Kabla Umar hajamaliza uhai wake, alikwishawaita kwake masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) kutoka kila pembe kama Abdullah bin Hudhaifa, Abu Darda, Abu Dharr al-Ghifari na Uqba bin Amir; na kuwaambia, ‘Ni Hadithi gani mlizoelezea katika maeneo yanayozunguka Madina?’ Wakamwuliza, ‘Kwani unakataza tusifanye hivyo?’ Akawajibu, ‘Hapana! Lakini kwa jina la Allah hamtaondoka hapo kwangu nikiwa hai!’ Rejea: Musnad Ahmad Ibn Hambal, Jz. 1, uk. 363.

UTAWALA WA UTHMAN IBN AFFAN Mnamo mwaka 23 A.H. (643 A.D) Umar aliuawa. Kifo chake kilisababishwa na jeraha kubwa la upanga aliopigwa na Abu Lu’lu’ah (mtumwa wa Kiajemi). Kabla hajafariki, aliacha ameweka masharti jinsi ya kumpata khalifa nyuma yake. Kwa mara nyingine hatuoni Shura wala demokrasia iliyotumika! Masharti yenyewe ni kwamba, Umar aliacha amechagua kamati ya watu 6 na kuwataka wamchague mmoja kati yao, kwa masharti kwamba iwapo kati yao, watu wanne wakikubali na wawili wakikataa basi wawili wauawe! Na kama wakipingana watatu kwa watatu, upande wa Abdur-Rahman Ibn Awf ndio upewe uzito wa kuamua, kwa kura ya turufu,(veto)! Na kama zikipita siku tatu bila maelewano kati yao, basi wote wauawe! Maelezo yake ni marefu lakini kwa kifupi ni kwamba Abdul Rahman Ibn Awf alimchagua Imam Ali kwa masharti kuwa Imam Ali aongoze Waislamu kwa misingi ya Qur’ani na Sunna na maongozi ya Abu Bakr na Umar! Imam Ali alikataa kuongoza kwa misingi ya Abu Bakr na Umar, isipokuwa alikubali kuongoza kwa misingi ya Qur’ani na Sunna sahihi ya Bwana Mtume (s.a.w.w.). Kwa msimamo huo, Imam Ali (a.s.) aliukosa ukhalifa kwa kutokubaliana na masharti hayo. Uthman Ibn Affan alikubali masharti hayo na hivyo akaupata ukhalifa! Waislamu wengine wote hawakushirikishwa katika suala hili! Ujanja huo alioupanga Umar Ibn alKhattab, ni kwamba alikusudia kuwa, kwa kadri ya hao wanakamati 230


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 231

katika Uislamu

wanavyohusiana kindugu, lazima atakayepata ukhalifa ni Uthman Ibn Affan! Imam Ali (a.s.) kwa kutambua ujanja huo alimwambia ndugu yake Abbas kwamba, ‘Ukhalifa hatutaupata.’ Bwana Abbas akauliza, ‘Umejuaje?’ Imam Ali (a.s.) akasema, ‘Kwa sababu Umar aliweka sharti kuwa upande wa walio wengi ndio uamue suala hili, kwa maana kwamba, kwa vyovyote hata tukipingana sawa kwa sawa, itabidi msuluhishi rasmi Abdullah Ibn Umar (mtoto wake Umar) aamue upande gani uwe na uwezo wa kuchagua khalifa. Kwa hali yoyote Sa’d atamwunga mkono Abdur-Rahman Ibn Awf, ambaye ni mtoto wa mjomba wake na ni shemeji yake pia! Na iwapo sisi tutapinga upande wa Abdur-Rahman Ibn Awf, maana yake ni kwamba tuuawe mara moja kwa kupinga uamuzi huo wa walio wengi kwa kadri ya masharti ya Umar!’ Kikao hicho kilifanyika nyumbani kwa mama Aisha tarehe 1 Muharram, 25 A.H (644 A.D); huku bwana Abu Talhah al-Ansari akiwa tayari mlangoni na watu wake hamsini wenye panga mikononi wakisubiri kuwaua wale watakaokiuka matakwa hayo (wasia) ya Umar Ibn al-Khattab! Je, hiyo ndiyo Shura? Abu Talha alifungua kikao kwa kumpa kura Uthman Ibn Affan na kuwajulisha wanakamati wote uamuzi wake huo. Hali hiyo ilimfanya az-Zubair kujali udugu na hivyo akamchagua Imam Ali (a.s.). Ndipo Sa’d Ibn Abi Waqqas akamchagua Abdur-Rahman Ibn Awf. Hali hiyo iliwabakiza wajumbe watatu wa kamati. Hata hivyo Abdur-Rahman kwa hiari yake akabuni siasa nyingine ya ujanja kwa kujidai kusamehe kura yake ya turufu (veto), kwa masharti kuwa Uthman na Imam Ali (a.s.) wampe uwezo wa kuchagua kati yao nani awe khalifa, au mmoja wao ajiuzulu kwa hiari. Hii ilikuwa siasa yenye ujanja wa hali ya juu kwa sababu ilimbana Imam Ali (a.s.) pande zote mbili asipate pa kupumulia! Imam Ali (a.s.) alibakia hana uchaguzi isipokuwa, ama ajiuzulu au amwachie Abdur-Rahman kufanya atakavyo! 231


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 232

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) hakuona uhalali wa kujiuzulu. Wala hakuona uhalali wa kumchagua Uthman au Abdur-Rahman. Imam Ali (a.s.) aliamua kutojiuzulu. Hata hivyo Abdur-Rahman akajifanya kuleta usawa na kujidai kusamehe ‘veto’ yake kwa kupendekeza kuwa: ‘Namchagua Ali kwa masharti kwamba ataongoza Umma kwa mwongozo wa Qur’ani, Sunna ya Mtume na kufuata nyayo za Abu Bakr Sidiq na Umar Ibn al-Khattab!’ Imam Ali (a.s.) alikubali kuongoza kwa misingi ya Qur’ani na Sunna lakini akakataa kufuata nyayo za bwana Abu Bakr na bwana Umar. Kwa msimamo huo ikawa Imam Ali (a.s.) ameukosa ukhalifa! Uthman alikubaliana na masharti hayo na akaupata ukhalifa! Mara baada ya Uthman kupewa kiapo cha utii yaani ‘Bay’at’ kwa ushindi wake huo, Imam Ali (a.s.) aliwaeleza Uthman na Abdur-Rahman kuwa, ‘Naomba Mwenyezi Mungu ajenge uadui kati yenu wawili.’ Kama ilivyo ni kwamba dua ya Ahlul-Bayt lazima ipokelewe. Watu hao wawili hawakuongea tena kati yao hadi kufariki kwa Uthman! Hapa tunaona maajabu matupu kwa sababu sharti alilowekewa Imam Ali (a.s.) la kufuata nyayo za Umar na Abu Bakr; mbona Umar hakufuata nyayo za Abu Bakr katika suala hili la ukhalifa? Haya yote yanadhihirisha kuwa ni siasa za kawaida tu zilizotumika tangu pale Saqifah Bani Sa’idah na hakuna misingi yoyote ya dini iliyotumika! Imam Ali (a.s.) hata hivyo alishiriki kamati hiyo, siyo kwa kutafuta haki bali kulinda Waislamu wasigawanyike, na wasitokee wanafiki wakadai kuwa hawakupata nafasi kumchagua kwa sababu hakushiriki katika kamati hiyo ya ulaghai! Rejea:Tarikh Tabari, Jz.1, uk. 2725 - 2780 Tarikh Ibn al-Athir, Jz. 3, uk. 67 Tarikh Tabari, Jz.1, uk. 2779 - 2780 Tarikh Ibn Athir, Jz. 3, uk. 51 & 67 Tarikh Tabari, Jz. 5, uk. 35 - 38 Tarikh Tabari, Jz. 16, uk. 590 232


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 233

katika Uislamu

Tarikh Abu al-Fida, uk. 34 Raudhatul Safa, Jz. 2 uk. 98 Uthman afuata nyayo za Abu Bakr na Umar kuhusu Hadithi: Baada ya kupata Ukhalifa, Uthman alipanda mimbari na kuhutubia, ‘Hairuhusiwi mtu yeyote kusimulia Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) ambayo haikusikika wakati wa uhai wa Abu Bakr na Umar.’ Rejea: Musnad Ahmad Ibn Hambal – Jz. 1, uk. 363. Ukichunguza amri hiyo utaona kuwa, wakati wa Abu Bakr na Umar, tayari Hadithi zilishakatazwa, na kuchomwa moto! Sasa ni Hadithi gani tena zilizosikika wakati huo ambapo zilikwishapigwa marufuku?’ Adhana mbili Swala ya Ijumaa! Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), ilikuwepo adhana moja tu. Na pie katika vipindi vya makhalifa wawili. Katika utawala wa Uthman, yeye akaamrisha ziwepo adhana mbili! Rejea: Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 17 Tafsiri ya kiingereza. Uthman akiuka maadili ya ukhalifa: Mara kadhaa tunasikia Uthman akisifiwa kwa sifa njema kwamba hata Malaika walimwonea haya! Tukichunguza historia tunasoma kwamba wakati habari za kufariki sahaba mwadilifu sana bwana Abu Dharr Ghiffari zilipomfikia Uthman, yeye alisema, ‘Mungu amsamehe.’ Hapo hapo sahaba mwingine mwadilifu sana bwana Ammar bin Yasir akasema, “Ndiyo; Mwenyezi Mungu amemsamehe kutokana na sisi kumchoka.” Hapo Uthman akamwambia Ammar, ‘Unadhani ninasikitika kumfukuza hapa (hadi akafia porini) ewe mwenye (....... tusi) ya baba yako!’ Pale pale Uthman aliamuru huyo Ammar akamatwe na kuwekwa rumande na kusema, ‘Na wewe nenda huko huko (uhamishoni) alikofia Abu Dharr Ghiffari.’ Walipokuwa tayari kuondoka kumpeleka Ammar, watu wa ukoo wa Makhzum walimwendea Imam Ali kumtaka aingilie kati kuzuia tendo hilo. 233


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 234

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) akamwambia Uthman, “Mwogope Mwenyezi Mungu, ulimfukuza Mwislamu mwongofu na akafia porini, na sasa unataka kumfanya hivyo mwingine kama yeye?” Walijibizana maneno mpaka Uthman akamwambia Imam Ali, ‘Wewe unastahiki kufukuzwa kuliko hata Ammar.’ Imam Ali (a.s.) akamjibu, “Fanya hivyo kama unaweza.” Ndugu wasomaji ni kwamba bwana Abu Dharr Ghiffari alifukuzwa Madina na Uthman, kutokana na upinzani wake kwa utawala wa Uthman. Rejea: Ansab al –Ashraf, cha Al- Baladhuri - Jz. 5, uk. 54 Katika tukio hilo, Muhajirun walimwendea Uthman na kumlalamikia kuwa: “Haistahiki hata kidogo kwamba kila atakayeongea unamfukuza mjini.” Na hapo Uthman akamwachilia Ammar Ibn Yassir, lakini akaamuru akamatwe na kutandazwa ardhini kisha akampiga mateke sehemu za siri na kumhasi! Ammar alikuwa mzee na mnyonge wakati huo na hivyo alipoteza fahamu! Maelezo haya ni maarufu sana miongoni mwa wanahistoria mashuhuri. Rejea:Ansab al-Ashraf, Jz. 5, uk. 49 Al-Istiab, Jz. 2, uk. 422 Al-Imama was Siyyasa, cha Ibn Qutayba, Jz. 1, uk. 29 Sharkh Nahjul-Balagha, cha Ibn Abil-Hadid, Jz. 1, uk. 239 Al-’Aqd al-Farid, cha Ibn ‘Abd al-Rabbih, Jz. 2, uk. 272 Hizi rejea ni vitabu vya historia na siyo vile vitabu vya Hadithi. Vitabu vya historia ni vingi mno duniani kama nilivyoeleza huko nyuma. Uthman abadili hukumu ya Swala ya Msafiri: Katika Sahih Muslim - Somo la Swala ya Msafiri na Kufupisha Swala Mina, anakaririwa Salim Bin ‘Abdullah ambaye alipokea toka kwa baba yake kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliswali Swala ya msafiri (Qasri) pale Mina na mahali penginepo (akiwa safarini) rakaa mbili; na kwamba Abu Bakr na Umar walifanya vivyo hivyo pia. Uthman alifanya hivyo pia mwanzoni mwa utawala wake, kisha baadaye akabadili na kuswali rakaa nne! Je, hiyo nayo ni Ijtihad? 234


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 235

katika Uislamu

Inaelezwa pia katika Sahih Muslim kwamba az-Zuhri alisema, “Nilimwambia Urwah: ‘Kwa nini mama Aisha anaswali rakaa nne akiwa safarini?’ Akajibu: ‘Aisha alifanya Ijitihad yake na kuelewa hivyo!’” Katika Sahih al-Bukhari - Somo la ‘Kitabu cha Hijja’ chini ya at-Tamattu na Iqran,’ anakaririwa Marwan bin al-Hakam akisema, “Niliwaona Uthman na Ali. Uthman alizoea kukataza watu wasifanye Hijja ya Tamattu na Hijja al-Qiran (Umra) pamoja! Ali alipoona hivyo alivaa ‘Ihram’ kwa ajili ya Hijja zote mbili na kufanya ibada zake akisema kuwa hawezi kuacha Sunna ya Mtume (s.a.w.w.) kwa maneno ya mtu yeyote.” Msimamo wetu Shia ni kwamba hatukubaliani na mtu yeyote kutengua Sunna sahihi ya Mtume (s.a.w.w.) kwa ijtihadi yake, kwa sababu katika karne 14 za Uislamu, dini yetu imevurugwa na amri za watawala. Isitoshe baadhi ya amri binafsi za makhalifa Abu Bakr, Umar na Uthman, ambazo ziligeuka na kupewa uzito wa Sunna; baadhi ya amri hizo zilikataliwa na Waislamu. Kwa mfano amri ya Uthman ya kuamuru msafiri aswali Swala kamili bila kupunguza rakaa; na amri ya Umar ya kukataza Hijja ya Umra. Yote haya ni kinyume na Sunna sahihi ya Mtume (s.a.w.w.) na Waislamu walikataa mabadiliko hayo, ingawa kuna baadhi ya wachache wasiopunguza Swala ya safari – Qasri. Sasa tujiulize kuwa, kama ni wajibu kwetu tukubaliane na amri zao hizo pamoja na nyinginezo, kwa nini tusiwatii amri zao zote halafu tuone kama tutabakiwa na Uislamu? Matokeo yake ni kwamba amri zao hizo zilichanganyika na Sunna sahihi na hivyo kuvuruga Uislamu. Na kama tuna uwezo wa kupangua na kukataa yale yasiyo ya Mtume (s.a.w.w.), kwa nini tuyakubali baadhi ya yale ambayo ushahidi wa kihistoria unaonyesha kuwa si ya Mtume (s.a.w.w.)? Maana ya Mwenyezi Mungu kukamilisha Uislamu (Qur’ani 5:3) ina faida gani iwapo baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), watawala wanaongeza na kupunguza watakavyo katika dini? Kuhusu Uthman, Rejea:

235


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 236

katika Uislamu

Al-Ghadiir al –Amini, Jz. 8, uk. 98 An -Nass wa’l ijtihad, Sharafu’dDin, Uk. 284-289 (c) Muqqaddamah mir’aatu’l-uquul al-’Al-Askari, Jz.1 & 2. Uthman akiri makosa ya Abu Bakr juu ya urithi wa Bibi Fatima (a.s.): Katika utawala wa Uthman, Mama Aisha na Mama Hafsa walimwendea Uthman kudai urithi wao kwa Mtume (s.a.w.w.). Uthman alikuwa amenyoosha miguu kwenye kochi lake, akaamka na kumweleza mama Aisha, “Wewe na mwenzako mlimleta mwanamume fulani aliyeoga uchafu wake na kushuhudia kuwa Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa Mitume hawaachi urithi. Kama kweli Mtume hakuacha urithi kwa nini mnaulizia urithi? Na kama aliacha urithi kwa nini mlimnyima Fatimah haki yake?” Baada ya hapo bibi Aisha aliondoka akiwa amekasirika na kusema, ‘Mwueni Na’thal (kizee mjinga) amegeuka kuwa kafiri’. Rejea: Sharh Nahjul Balaghah, cha Ibn Abi al-Hadid, Jz. 16, uk. 220-223 Tarikh Tabari (3) Tarikh al-Kamil Yaliyopelekea kuuawa Uthman Ibn Affan: Utawala wa Uthman Ibn Affan ulijaa ukabila, dhulma na uonevu kwa raia wa kawaida. Magavana wake katika sehemu mbali mbali waliwaonea na kuwakandamiza raia.Kutokana na hali hiyo, kundi la Waislamu toka huko Misri walimuasi Uthman. Yeye Uthman aliona kuwa uasi huo ni wa hatari na kwa hiyo akamwendea Imam Ali (a.s.) kutaka ushauri, akiwa mwenye kuonyesha masikitiko kwa matendo yake hayo kwa raia. Imam Ali (a.s.) aliwaambia Wamisri kuwa, “Mmefanya uasi ili kuleta haki na ukweli katika maisha. Uthman ametubu maovu yake kwenu na amesema kuwa atabadili mwenendo wake katika siku tatu na kutekeleza matakwa yenu kwa kuwafukuza kazi viongozi waovu.” Imam Ali (a.s.) aliandika mkata236


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 237

katika Uislamu

ba kwa niaba ya Uthman na ndipo wakaondoka kurejea makwao Misri. Wakiwa njiani walimwona mtumwa wa Uthman amepanda ngamia akielekea Misri pia. Walimtilia shaka na kumpekua na kumkuta na barua toka kwa Uthman kwenda kwa gavana wa Misri. Barua hiyo ilikuwa na maagizo kuwa, ‘Abdur-Rahman Ibn Addis akija kwako mpige viboko 100, mnyoe kichwa na ndevu na mhukumu kifungo kirefu. Fanya hivyo hivyo kwa Amr Ibn al-Hamq, Suda Ibn Hamran na Urwah Ibn Niba.’ Wamisri hao walisikitika sana na walipeleka barua hiyo na kurejea kwa Uthman kumhoji kuhusu ukweli wake! Walimkuta na kumshambulia kwa maneno: “Umetusaliti!” Uthman alikanusha barua hiyo. Wakamwambia, “Mtumwa wako alikuwa na barua hii.” Akajibu, “Amekuwa nayo bila idhini yangu.” Wakasema, “Alipanda ngamia wako.” Akajibu, “Ngamia wangu aliibiwa!” Wakasema, “Barua hii ni mwandiko wa katibu wako.” Akajibu, “Hayo yamefanyika bila idhini wala taarifa yangu.” Wakasema, “Kwa hali yoyote huna uwezo wa kuwa khalifa na kwa hiyo ujiuzulu, kwa sababu; kwa barua yako hii, inaonyesha wazi kuwa wewe ni msaliti, kwa maana kwamba; iwapo haya yote yanafanyika bila wewe kufahamu au bila ruhusa yako, basi huo ndio udhaifu wako. Kwa hali yoyote bora ujiuzulu au uwafukuze kazi viongozi wako waovu mara moja.” Uthman aliwajibu, “Iwapo nitafanya kazi kwa matakwa yenu ina maana ninyi ndio watawala? Sasa kazi yangu mimi ni ipi?” Basi ikawa Wamisri hao wamesimama na kuondoka kwa hasira. Rejea:(1) Tarikh Tabari, Jz. 3, uk. 402-409. (2) Tarikh Ya’qubi, Jz. 2, uk. 150-151 Uthman awatajirisha jamaa na rafiki zake kwa Hazina ya Baitul Maal!: Alimpa mkwe wake Dirham 300,000 kutoka Baitul Maal. Rejea: Kitab alAnsab cha Baladhuri Jz. 5, uk. 58. Vile vile alimpa ngamia wote walioletwa kama Zaka toka kwa raia! Rejea: Kitab al-Ansab, Jz. 5, uk. 28. 237


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 238

katika Uislamu

Zubair Ibn Awam alitajirishwa sana kwa kuchotewa Zaka na Uthman kiasi kwamba alipofariki huyo Zubair aliacha nyumba 11 Madina, nyumba 2 Basra, nyumba moja Qufa-Iraq na nyumba moja Misri. Alikuwa na wake zake wanne ambao walirithi moja ya nane ya mali zake, na kila mmoja alipata Dirham milioni moja na laki mbili! Jumla ya utajiri huo ulikuwa ni Dirham milioni 59 na laki nane. Ndugu wasomaji huo ni utajiri mkubwa usio na mfano kulingana na wakati huo miaka 1400 iliyopita! Rejea:Sahih al-Bukhari, Jz. 5, uk. 21 na Tarikh Ibn Kathir. Mali zake hizo alizomiliki peke yake, ni pamoja na farasi elfu moja, watumwa elfu moja na makasri kadhaa. Rejea:- Muruuj-Dhahab (Tarikh al-Masudi) Jz. 1, uk. 34. Talha Ibn Ubaidullah alipofariki aliacha ngozi za maksai (mifuko) 300 imejaa dhahabu! Uzito wa dhahabu hiyo ungebebwa na ngamia mia tatu! Ndugu wasomaji huo ni utajiri ambao hata hivi leo hatuna! Utajiri wote huo walipewa na Uthman toka hazina ya serikali bila uhalali kwa sababu hapo hapo watu wa kawaida yaani raia, walikuwa wanaishi maisha ya dhiki kupindukia, hali ya kuwa hayo makusanyo ya Zaka yalitakiwa kihalali wapewe raia wanaostahiki yaani wenye dhiki. Rejea:- at-Tabaqat, cha Ibn Saa’d Jz. 3, Uk. 158 na Muruj al-Dhahab, Jz. 1, uk. 444 na Aqd alFarid Jz. 2, uk. 275. Uthman alimwoza binti yake kwa Abdullah Ibn Khalid na kuamuru kuwa huyo Abdullah apewe Dirham 600,000. Alimwamuru Mweka Hazina wa Baitul Maal kutoa pesa hizo huko Basra-Iraq. Rejea: Tarikh Ya’aqubi, Jz. 2, uk. 145. Na mengine mengi nafasi hapa haitoshi kuyaelezea. Uthman akiuka Swala ya Msafiri na kubadili Swala za Idul Fitri – Hajj: Mtume (s.a.w.w.) alionyesha kwa vitendo kupunguza rakaa za Swala akiwa safarini, lakini Uthman na hata Mama Aisha waliswali rakaa zote! Vile vile Uthman aliongeza adhana moja katika Swala ya Ijumaa, na kuamuru Hotuba za Swala za sikukuu za Iddi kutangulia Swala! 238


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 239

katika Uislamu

Masuala kama haya hayana haja ya malumbano na ubishi kuhusu Mtume (s.a.w.w.) alifanya nini au aliacha nini. Masahaba wa Mtume (s.a.w.w.) ni wengi mno na waliishi naye muda mrefu kiasi ambacho madai ya kujidai kusahau Sunna sahihi hayawezi kupokelewa. Ndiyo maana tunachambua vitabu vya historia ili tujue upotofu ulianzia wapi. Hatuwezi kuendesha Uislamu kwa matakwa ya watawala wa dola ya kiarabu, badala ya kuongozwa na Qur’ani na Sunna Sahihi. Rejea:(1) Al-Ghadiir al-Amini, Jz. 8, uk. 98 (2) An-Nass wa’l Ijtihaad, cha Sharafu-d-Din, uk. 284-289 (3) Muqaddamah mir’aatu’l- uquul al ‘AlAskari, Jz. 1&2 Uthman amrejesha sahaba aliyelaaniwa na kuhamishwa na Mtume (s.a.w.w.)!: Alikuwepo sahaba mmoja mwovu sana akiitwa Hakam Ibn Aas, ambaye alikuwa adui mkubwa wa Mtume (s.a.w.w.) kabla na baada ya Uislamu. Baada ya kutekwa Makka mwaka wa 8 Hijiria sahaba huyu alihamia Madina ingawa hapana uhakika wa kusilimu kwake kihistoria. Mtu huyo alikuwa na tabia ya kumbeza Mtume (s.a.w.w.) kwa kumfuata nyuma akimfanyia ishara za kumdhalilisha kwa kubinua midomo au ishara za vidole. Sahaba huyo alilaanika na ikawa midomo yake imelemaa hivyo hivyo milele hadi kufa kwake. Siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa kwa mke wake mmojawapo na ikawa sahaba huyo amekwenda nyumba hiyo na kumchungulia Mtume (s.a.w.w.) kwenye tundu! Mtume (s.a.w.w.) alimtambua na akatoka nje na kusema, “Huyu Hakam Ibn Aas na kizazi chake hawataishi mahali ninapoishi mimi.” Kwa hiyo Mtume (s.a.w.w.) alimfukuza Madina na kumhamishia karibu na Taif. Mara Mtume (s.a.w.w.) alipofariki ikawa Uthman amemwendea Abu Bakr kuomba eti Hakam aruhusiwe kurejea! Abu Bakr alikataa na kusema kuwa 239


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 240

katika Uislamu

hawezi kumrejesha aliyefukuzwa na Mtume (s.a.w.w.). Mara Umar alipopata ukhalifa ikawa Uthman amemwendea kuomba eti Hakam aruhusiwe kurudi! Umar naye akakataa kumrudiasha kwa misingi ile ile. Sasa, mara tu, Uthman alipopata ukhalifa alimrejesha Hakam Ibn Aas na kuwaeleza Waislamu kuwa eti alishapendekeza kwa Mtume (s.a.w.w.) kuwa Hakam na familia yake warejee Madina, na Mtume (s.a.w.w.) akaahidi kutoa ruhusa hiyo lakini akafariki kabla ya kutekeleza! Rejea: Kitab al-Ansab, Jz. 5, uk. 27. Siyo tu kwamba Uthman alimrejesha Hakam Ibn Aas bali alimfanya mshauri wake mkuu na kumpa mali zote zilizokusanywa kama Zaka, kutoka kwa kabila la Bani Qaza’a! Katika mambo yaliyowaudhi Waislamu ni Uthman kumrejesha huyo dhalimu na kumpa mali na madaraka ya kukusanya Zaka toka ukoo wa Bani Qaza’a. Zaka hiyo ilifikia Dirham 300,000! Rejea: Tarikh al-Ansab, cha Baladhuri, Jz. 5 uk. 28. Waislamu waanza kumgomea Uthman Ibn Affan na kumuasi pia: Kutokana na matendo ya Uthman pamoja na maofisa wake katika sehemu mbali mbali, Waislamu walichukizwa na uonevu huo uliofanywa na watawala hao. Watu wa Madina waliandika barua na kuzituma miji mingine wakiwataka Waislamu waje kufanya Jihad kusafisha dini ya Muhammad (s.a.w.w.) iliyochafuliwa na watawala. Tatizo kubwa la Uthman lilikuwa katibu na mshauri wake mkuu yaani Marwan Ibn Hakam. Huyu Marwan alikuwa na madaraka kuliko hata Uthman mwenyewe! Marwan hakutaka kusikia pendekezo lolote la kuwatendea haki raia. Mnamo mwaka 35 A.H (655 A.D) Waislamu walibadilishana barua kuelezana umuhimu wa kuwang’oa Bani Umayyah na Uthman katika madaraka. Habari hizi zilimfikia Uthman ambaye alijaribu pia 240


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 241

katika Uislamu

kuandika barua miji yote kuleta suluhu lakini bila kuchukua hatua ya kuwadhibiti maofisa wake waovu au kuyabadili yale yanayowakera raia. Katika hali hiyo, watu wachache kutoka Misri walimletea malalamiko Uthman kuhusu gavana wa huko, Ibn Abi Sarah. Uthman aliwasikiliza kwa makini na kumkaripia Abi Sarah huku akiahidi kuchukua hatua. Uthman alimwandikia barua Abi Sarah na kumtaka ajirekebishe, la sivyo angemwadhibu. Marwan Ibn Hakam hakutaka msimamo huo wa Uthman. Mara watu hao walipotoka kwa Uthman ikawa Marwan ametoka na kuwakaripia na kusisitiza kuwa Uthman asitimize ahadi alizotoa za kumdhibiti Abi Sarah. Wamisri walimpelekea Abi Sarah hiyo barua toka kwa Uthman. Alipoisoma alikasirika na hakujali amri ya Uthman ya kumtaka ajirekebishe! Badala yake alimuua kiongozi wa ujumbe huo! Dharau hiyo ya Abi Sarah inatokana na uhusiano wake na Uthman wa undugu (kaka wa kunyonya) na ndiyo sifa pekee ya kumpa ugavana huo wa Misri. Wamisri walichukizwa na tabia hiyo ya Abi Sarah na waliamua kumtumia Uthman ujumbe mwingine wa watu 1,000. Watu hao walifikia katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.). Viongozi wao walikutana na masahaba maarufu wa Mtume (s.a.w.w.) ili kuwaeleza maovu ya Abi Sarah. Masahaba hao walikutana na Uthman kumweleza hali hiyo ya Misri. Vile vile watu wengine wakiongozwa na Imam Ali (a.s.) walikutana na Uthman na kumshauri achukue hatua upesi. Uthman aliapa mbele ya watu na kuwahakikishia kuwa atajitahidi kurekebisha hali hiyo. Aliwataka pia wapendekeze jina la gavana mpya wa Misri, nao walipendekeza mtoto wa Abu Bakr yaani Muhammad bin Abu Bakr. Uthman alimteua kuwa gavana wa Misri na pia kuteua kamati ya Ansar na Muhajirun kuchunguza maovu ya Abi Sarah. Muhammad bin Abu Bakr na watu wake wakaondoka kuelekea Misri. Katika siku ya tatu ya safari yao wakiwa njiani, walimwona mtumwa mwenye asili ya Ethiopia akiendesha ngamia kwa kasi kuelekea Misri. Walishangaa na kumtilia shaka kisha kumsimamisha na kumwuliza 241


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 242

katika Uislamu

anakwenda wapi. Alibabaika kujieleza na mwisho wakagundua kuwa ni mtumwa wa Marwan au Uthman. Alisema ametumwa kwa gavana wa Misri. Wakamwambia kuwa mbona gavana ni huyu hapa? Akasema kuwa siye huyu. Wakamwuliza kama ana barua, akakataa. Ndipo walipompekua na kumkuta na barua iliyoonyesha kuwa inatoka kwa Uthman kwenda kwa Ibn Abi Sarah. Barua ikafunguliwa mbele ya masahaba wa msafara huo, nayo inasema hivi:“Mara Muhammad Ibn Abu Bakr na wenzake watakapofika huko Misri, waue kwa visingizio vyovyote. Barua atakayoleta Muhammad Ibn Abu Bakr usiitilie maanani imebatilishwa na uendelee na madaraka yako. Mfunge yeyote atakayekujia na malalamiko.� Barua hiyo iliwashangaza na ikawa wote wamenyamaza wasipate la kusema. Hakuna aliyetegemea kuwa khalifa anaweza kuwa dhalimu kiasi hicho kwa kupanga njama kama hiyo! Bwana Muhammad Ibn Abu Bakr alifunga barua hiyo na wote wakarejea Madina na kuonyesha barua hiyo kwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Barua hiyo iliposomwa, watu wote walisikitika na kupanda hasira hasa ukizingatia maovu ya nyuma waliyotendewa Abu Dharr Ghiffari, Ammar Ibn Yasir n.k. kama nilivyoelezea huko nyuma. Ujumbe wa Waislamu ukiongozwa na Imam Ali (a.s.) ulimwendea Uthman na kumwonyesha barua hiyo na wakaanza kuhojiana: Imam Ali: Huyu ni mtumwa wako? Uthman: Ndiyo. Imam Ali: Ngamia huyu ni wako? Uthman: Ndiyo. Imam Ali: Je, nembo iliyofungia barua hii ni yako? Uthman: Ndiyo. 242


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 243

katika Uislamu

Imam Ali: Kwa hiyo barua hii uliituma wewe? Uthman: Hapana, Naapa kwa jina la Allah kuwa sikuandika wala kumwamuru mtu kuandika, wala sijamtuma huyo mtumwa. Masahaba waliamini maelezo ya Uthman lakini uchunguzi ulionyesha wazi kuwa mhusika mkuu alikuwa ni Marwan Ibn Hakam! Kwa hiyo walimtaka Uthman amtoe Marwan ili ahojiwe. Uthman alikataa! Hali hiyo iliongeza ghadhabu na uasi dhidi ya Uthman. Uthman Ibn Affan aliona uasi unaongezeka na hivyo akapata wazo kuwa aombe msaada toka Syria kwa Muawiyah ili kuzima uasi huo. Muawiya aliumezea mate ukhalifa na aliona kuwa huenda Uthman akiuawa, yeye Muawiyah anaweza akafanikiwa kuutwaa. Hata hivyo Muawiyah hakutaka kuonyesha nia hiyo wazi wazi; na kwa hiyo alitayarisha jeshi la askari 12,000 na kupiga kambi karibu na Damascus. Muawiyah alimwendea Uthman na kumweleza kuwa jeshi liko tayari, badala ya kuja na jeshi hilo! Uthman alitambua ujanja huo; na akamwambia Muawiyah kuwa, “Umeacha jeshi nyuma ili niuawe na kisha uanzishe vita ya kulipiza kisasi cha damu yangu.” Baada ya Uthman kuuawa, utabiri wake huu ulitimia! Rejea :- (1) Tarikh Tabari, Jz. 3, uk. 403. (2) Muruj al-Dhahab, Jz. 2 uk. 415 (3) Muruj al –Dhahab, Jz. 3, uk. 403 Imam Ali (a.s.) alijaribu sana kumshauri Uthman na kumweleza kuwa uasi umeenea nchi nzima lakini haikusaidia kitu. Mwisho alimshauri walau atoke nje atoe hotuba kwa watu kuwatuliza. Uthman alitoka na kuwahutubia watu msikitini, akieleza masikitiko yake na kujutia maovu yaliyopita, na kuwa hayatarudiwa tena. Aliahidi kutekeleza matakwa yao pamoja na kumwondoa Marwan Ibn Hakam madarakani. Hotuba hiyo iliwagusa watu walipomwona Uthman akitokwa na machozi! Baada ya hotuba hiyo Uthman alitoka msikitini akarejea kwake. Alipofika nyumbani alikutana na Marwan pamoja na Bani Umayyah wa karibu naye ambao wote hawakuhudhuria hotuba ya yake. Uthman alipokaa chini, Marwan akamwuliza, “Ewe bwana wangu waniruhusu niseme kitu au ninyamaze?” Uthman akajibu, “Sema utakalo.” Marwan 243


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:22 PM

Page 244

katika Uislamu

akasema, “Umehamasisha watu kukuasi na wala si vinginevyo.” Uthman akajibu, ‘Nimesema niliyosema na siwezi kuyameza.’ Marwan akasema, ‘Watu wamejazana kwenye lango kama mlima. Iwapo mmoja wao atalalamikia uonevu na mwingine utamsikia eti anadai kuwa gavana fulani aondolewe kazini; umehatarisha ukhalifa wako.’ Uthman akasema, ‘Naona aibu kumeza maneno yangu, labda wewe uende ukaongee nao.’ Marwan alitoka nje na kuwaendea watu na kuwauliza, “Mkusanyiko huu ni wa nini? Inaelekea mmekuja kuhujumu nyumba hii? Nyuso zenu na zigeuke nyeusi. Mmekuja kunyakua serikali toka kwetu! Kama mna mawazo hayo tutawashughulikia kwa njia ambayo hamtaisahau. Rudini makwenu, hatutavumilia kuingiliwa madaraka yetu na mtu yeyote.” Watu waliondoka kwa kukata tamaa huku wakiwatishia watawala. Kwa mara nyingine Marwan alivuruga usuluhishi bila Uthman kuchukua hatua yoyote! Kwa hiyo waasi walikuja juu wakitaka ahadi zote alizotoa Uthman zitekelezwe na kwamba Marwan akabidhiwe kwao walipize kisasi. Lakini Uthman alikataa kumtoa Marwan. Waasi waliizingira nyumba ya Uthman. Hata hivyo waasi hao hawakuwa na nia ya kumdhuru Uthman ila walitaka ajiuzulu ukhalifa. Sahaba mmoja wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa mstari wa mbele wa waasi alipiga ukelele kumwambia Uthman: “Inabidi ujiuzulu na wala hutadhurika.” Sahaba huyo aliitwa Nayyar bin Ayaz. Lakini alikuwepo Kathir Bin Salat Kandi ambaye alimwunga mkono Uthman na alikuwa nyumbani kwa Uthman wakati huo. Huyo Kathir alichukua upinde na kumpiga mshale Nayyar Bin Ayaz na kumwua! Waasi walipiga kelele, ‘Kabidhi huyo mwuaji kwetu.’ Uthman alikataa na kusema kuwa hawezi kukabidhi mtetezi wake! Waasi walishambulia lango kuu na ikawa lango hilo limefungwa. Waasi walichoma moto lango hilo, na wapiga mishale walianza kurusha mishale kwenye kasri ya Uthman. Wakati mapambano yanaendelea, Muhammad Ibn Abu Bakr na wenzake wawili walifanikiwa kuingia kwa Uthman kupitia pembeni kwenye nyumba ya Muhammad Abi Khurram Ansari. Walimkuta Uthman akiwa na mkewe Naa’ila. Wale watu wawili walioongozana na bwana Muhammad Ibn Abu Bakr, walimshambulia kwa silaha yenye ncha kali na kumwua 244


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 245

katika Uislamu

kisha walitoroka kupitia njia hiyo hiyo. Alisikika Naa’ila akilia, “Wamemwua khalifa kiongozi wa waumini!” Waliokuwa mstari wa mbele katika mauaji hayo ni pamoja na hawa wafuatao:(1) Talha Ibn Ubaidullah. Alizingira nyumba ya Uthman na kuzuia maji yasiingizwe ndani. Aliamuru kundi lililokusudia kumwua Uthman, na ndiyo maana Marwan Ibn Hakam (katibu wa Uthman) alimwua Talha katika vita vya Jamal Kubwa. Rejea:- (a) Tarikh Tabari, Jz. 6, uk. 154 (b) Tarikh Kamil, ya Ibn Athir, Jz. 4, uk. 70. Lengo lake kuongoza mauaji hayo alitarajia uwezekano wa yeye kuwa khalifa. (2) Zubair Ibn Awam. Huyu alikuwa adui mkubwa wa Uthman, rejea: Mustadrak, Imam Hakim, Jz. 3, uk. 118, Al-Imamah was-Siyyasah, Jz. 6, uk. 58; Muruuju-Dhahab, Jz. 11, uk. 11. Lengo lake lilikuwa sawa na hilo la rafiki yake yaani Talha. Habari za unafiki wao zitaelezwa katika maelezo ya vita vya Jamal ndogo na Jamal kubwa katika sura za mbele. (3) Amr Ibn Aas. Katika Tarikh Tabari, huyu Amr alimchukia sana Uthman kwa sababu alimwondoa kwenye cheo cha ugavana wa Misri. Huyu alifikia kumtukana Uthman msikitini. Lakini kwa unafiki wa Amr, alijiunga na Muawiyah huko Syria eti kulipiza kisasi cha mauaji ya Uthman! Madai ya wapotoshaji wa historia kwamba Imam Ali (a.s.) alihusika na mauaji hayo na alikuwepo Madina siyo kweli. Wakati huo Imam Ali (a.s.) alikuwa nje ya Madina kwa sababu aliamriwa na Uthman aondoke Madina ili watu wasije wakampa kiapo cha utii na kumchagua kuwa khalifa katika migogoro hiyo iliyokuwa inaendelea! Imam Ali (a.s.) alikuwa akiamriwa mara kwa mara na Uthman kuondoka mjini Madina na kwenda shambani kwake Yanb’a kisha kuitwa tena Madina kutatua migogoro inapomzidia Uthman! Rejea:- Majma’uz-Zawaid, Jz. 7, uk. 63 na Ansab al-Ashraf cha Al-Baladhuri. Lakini tunasoma kuwa Bibi Aisha aliwataka watu wamwue Uthman kwa kusema, “Mwueni Na’thal (mzee mjinga) kwani amegeuka kuwa kafiri.” 245


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 246

katika Uislamu

Mama Aisha alisema maneno hayo pale Uthman alipokataa kuwapa urithi toka kwa Mtume (s.a.w.w.) Rejea: Sahih al-Bukhari, Jz. 3, uk. 39. Masahaba maarufu waliokuwa mstari wa mbele kwenye mauaji hayo ni Talha Ibn Ubaidullah, Zubair Ibn al-Awam na Muhammad Ibn Abu Bakr na wengineo wengi kama nilivyoeleza na wala siyo Imam Ali (a.s.). Baada ya kuuawa Uthman, watu wenye hasira walizuia asizikwe kwa muda wa siku tatu! Mwisho walimzika bila kumkafini wala kumwosha, na kwamba alizikwa eneo la Hashsh Kawkab ambalo lilikuwa eneo la kuwazika makafiri wa Kiyahudi! Ukweli huu wa kuzikwa Uthman katika hali hiyo ni kweli kabisa na hauhitaji vitabu vya historia kwa ushahidi! Leo hii ukifika Madina utaona kuwa kaburi la Uthman lipo mwisho kabisa mwa Janatul Baqi. Janatul Baqi ni eneo la makaburi ya Waislamu tangu wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) na ndiko walikozikwa watu wote mashuhuri. Wakati huo wa kufariki Uthman Ibn Affan, hiyo Janatul Baqi ilikuwa haijajaa makaburi! Kwa hiyo hakuna sababu kwa nini Uthman asizikwe hapo wakati ambapo alikuwa Kiongozi wa Taifa la Waislamu! Badala yake akazikwa kwenye eneo la makafiri kwa kadri ya maelezo yafuatayo! Kwa hiyo hakuna sababu, na haingii akilini kabisa, kwa nini kaburi la Uthman liwe mwishoni mwa makaburi, ukitilia maanani muda aliofariki! Ukweli ni kuwa, ni kweli Uthman alizikwa katika eneo la makaburi ya makafiri wa Kiyahudi kwa sababu hapo lilipo kaburi lake, haikuwa sehemu ya kuzika Waislamu wakati huo! Kilichotokea ni kwamba wakati wa utawala wa Muawiya, aliweka mkazo mkubwa kuwatukuza Bani Umayyah na kuwadhalilisha Bani Hashim. Kwa hiyo katika kuinua heshima ya Uthman, Muawiyyah alinunua eneo hilo la Wayahudi makafiri, na kuliunganisha na Janatul Baqi kwa sababu maeneo hayo yalipakana! Vinginevyo mpaka leo ushahidi huo ungebakia wazi na watu wangekuwa wanajiuliza ilikuwaje ‘Kiongozi wa Waumini’ akazikwa kwa makafiri? Ni mgogoro gani ulikuwepo? Hiyo ndiyo namna ya kufanya utafiti kisayansi.

246


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 247

katika Uislamu

WAISLAM WAMTAKA IMAM ALI IBN ABI TALIB KUWA KHALIFA WAO Siku tano baada kuuawa Uthman Ibn Affan, Waislamu walikusanyika kwa wingi katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) na kutafakari jinsi Uislamu unavyodidimia. Mwisho waliamua na kusisitiza kuwa lazima Imam Ali (a.s.) awe khalifa wao. Walimwendea nyumbani kwake na kumweleza kuwa hawataondoka hapo mpaka awe amekubali kuwa khalifa. Imam Ali (a.s.) kwa kuona jinsi Uislamu ulivyovurugika kwa kipindi cha miaka 25 iliyopita, alikataa cheo hicho kwa sababu watu walishaachana na kutawaliwa na Shariah ya kiislamu kwa kiasi kikubwa, ila tu kwa baadhi ya mambo fulani fulani. Mwisho Imam Ali (a.s.) alikubali kushika uongozi huo kwa masharti kuwa watu wawe tayari awaongoze kwa misingi ya Qur’ani na Sunna kama Mtume (s.a.w.w.) na kwamba waahidi kumtii wakati wa amani na wa vita. Imam Ali (a.s.) alifika msikitini na kuagiza Talha Ibn Ubaidullah pamoja na Zubair Ibn al-Awam wafike, kwa sababu walikuwa watu mashuhuri hapo Madina. Walipofika wakataka kutoa ‘Bay’at’ kwa Imam Ali (a.s.) lakini Imam Ali (a.s.) alisita kwanza na kuwaeleza kuwa watoe ‘Bay’at’ kwa moyo mweupe kama ambavyo yeye angefanya kwa mmoja wao. Walikiri kuwa wanafanya hivyo kwa moyo safi. Wa kwanza kutoa mkono alikuwa Talha Ibn Ubaidullah ambaye mkono wake ulikatika katika vita vya Uhud na hivyo akawa anaunyosha kwa shida, na kuwafanya waliokusanyika hapo kuona kuwa hiyo ni ishara mbaya kwa zoezi hilo. Kisha walifuata wengineo wakatoa bay’at zao kwa Imam Ali (a.s.). Katika tukio hilo tarehe 24 Dhul-Hajj, 34 A.H, walikuwepo wawakilishi kutoka Basra, Kufa, Misri na Hijaz. Wote walishiriki kumwendea na kumsisitizia Imam Ali (a.s.) awe khalifa wao.

247


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 248

katika Uislamu

Hiyo ilikuwa mara ya kwanza tangu kufariki Mtume (s.a.w.w.), Waislamu kumchagua khalifa kwa ridhaa ya walio wengi! Quraishi wa Bani Umayyah na wafuasi wa Uthman hawakufika hapo kutoa bay’at. Mabwana Sa’d Ibn Waqqas, Maslama Ibn Khalid, Mughira Ibn Shu’ba, Abdallah Ibn Salam, Husein Ibn Thabit na Ka’ab Ibn Malik hawakutoa bay’at kwa Imam Ali (a.s.). Kazi ya kwanza ya Imam Ali (a.s.): Kwanza kabisa aliwang’oa madarakani viongozi waovu wote. Magavana waovu waliondolewa isipokuwa Muawiyah Ibn Abu Sufyan aliyekuwa gavana wa Syria tangu enzi za utawala wa Abu Bakr Sidiq. Kwa jinsi Muawiyah alivyojijenga kijeshi kwa miaka mingi kwa kutumia vibaya ‘Baitul Maal’, iwapo Imam Ali (a.s.) angejaribu kumwondoa madarakani, kungetokea vita kubwa na watu wengi kupoteza maisha yao. Baadhi ya Magavana walioondolewa madarakani ni kama Yala aliyekuwa gavana wa Yemen na Ibn Amir aliyekuwa gavana wa Basra. Mara baada ya kuvuliwa madaraka, magavana hawa walitoroka na mali nyingi kutoka ‘Baitul Maal’ na kumpelekea Bibi Aisha. Kwa mfano bwana Yala alimpelekea bibi Aisha pesa, Dinari 60,000 na ngamia 600. Miongoni mwa ngamia hao alikuwepo ngamia mmoja mwenye sifa za pekee ambaye thamani yake ilikuwa sawa na vipande 200 vya dhahabu. Ngamia huyo ndiye aliyetumiwa na bibi Aisha katika vita vya Jamal (vita vya ngamia) na ndiyo sababu ya vita hivyo kuitwa vita vya Jamal. Vita hivyo vilipigwa mahali paitwapo Khoreiba - Iraq. Magavana wapya wafuatao walichaguliwa kushika nafasi za uongozi kama ifuatavyo :Ubaidullah Ibn Abbas - Yemen Qais Ibn Saad Bin Ubada - Misri Qutham Ibn Abbas - Makkah Samaha Ibn Abbas - Tihama Uthman Ibn Hunaif - Basra Ammara Ibn Shahab - Kufa - Iraq Saidi Ibn Abbas - Bahrain 248


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 249

katika Uislamu

Vita vya Jamal Kubwa na Jamal Ndogo: Machifu wawili maarufu mabwana Talha Ibn Ubaidullah na Zubair Ibn alAwam walitarajia kuwa kwa kutoa bay’at zao kwa Imam Ali (a.s.), wangepewa vyeo fulani vya uongozi kama ugavana. Walipoona kimya walimwendea Imam Ali (a.s.) na kudai kuwa mauaji ya Uthman yalipiziwe kisasi na kwamba wako tayari kwa kazi hiyo! Imam Ali (a.s.) alishangaa kwa sababu ni watu hao hao walioshiriki kwa njia moja au nyingine katika mauaji hayo! Imam Ali (a.s.) alitambua kuwa hiyo ni njama yao ya kuleta ghasia kwa kuchochea machafuko na kuzua maadui bandia. Aliwajibu kuwa mauaji ya Uthman sababu zake ziko wazi kutokana na utawala wake wa ukabila, ubadhilifu na uonevu kwa raia. Aliwaasa kuwa huo haukuwa wakati wa kuanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Machifu hao walipoona kuwa uovu wao umebainika, walinyamaza wakaondoka kupanga ujanja mwingine kwa siri. Huko Syria Muawiyah alishatayarisha jeshi la askari 60,000 eti kulipiza kisasi cha kuuawa Uthman Ibn Affan! Madai ya Muawiyah yalikuwa eti Imam Ali (a.s.) ndiye kamwua Uthman! Muawiyah alitumia mbinu ya kutundika kanzu ya marehemu Uthman msikitini huko Syria siku za Ijumaa. Kanzu hilo likiwa na madoa ya damu, lilitumika kuwadanganya watu wahamasike kushiriki vita vya kulipiza kisasi bandia, bila kuelewa kuwa kilichomwua Uthman ni maovu ya utawala wake. Imam Ali (a.s.) aliposikia hayo alikasirika na kupiga ukelele kuwa, “Mpatanishi kati yangu na Muawiyah ni upanga.” Tangu mwanzo, Muawiyah alitambua kuwa kikwazo chake kikubwa kupata ukhalifa ni Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.). Hapo hapo alitambua umaarufu wa machifu wawili hapo Madina yaani Talha Ibn Ubaidullah pamoja na Zubair Ibn al- Awam. Kwa hiyo kwa ujanja wake, alimwandikia barua Zubair na kumweleza kuwa yeye Muawiyah amepokea viapo vya utii kwa ajili ya Zubair, na kwamba Talha atakuwa mrithi wa Zubair. Alimweleza kuwa Syria yote ipo tayari kumwunga mkono kumwondoa madarakani 249


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 250

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) ili waende Syria wapokee huo ukhalifa. (Rejea: Hotuba No:12 ya Nahjul Balaghah). Lengo la Muawiyah lilikuwa ni kuwarubuni hawa wazee wawili ili waanzishe uasi kwa Imam Ali (a.s.); na hivyo katika migogoro hiyo, Muawiyah apate muda wa kujiimarisha zaidi katika madaraka huko Syria. Lakini kama tutakavyoona katika maelezo ya vita vya Jamal, uasi wa mabwana hawa ni kwamba wote waliuawa; na hivyo kumnufaisha Muawiyah bila wao kufaidi uhaini wao dhidi ya Imam Ali (a.s.). Baada ya hapo ikawa Muawiyah amewatafuta wanafiki wengine kama Mughira Ibn Shu’ba, Marwan Ibn Hakam, Walid Ibn Aquaba, Abdullah Ibn Amr, Abu Hurayra na Amr Ibn Aas. Kati ya hawa wote, Amr Ibn Aas alitokea kuwa wa manufaa makubwa kwa Muawiyah. Hata hivyo ilimbidi Muawiyah ampatie hongo kubwa Amr ili kununua utiifu wake kwake. Baadaye kama tutakavyoona katika matukio yafuatayo, Amr Ibn Aas alimsaidia sana Muawiyah Ibn Abu Sufyan. Vile vile Muawiyah alichunguza na kuthibitisha kuwa Zayd Ibn Abihay alikuwa mtoto haramu wa Abu Sufyan na siyo mtoto wa Obeid. Muawiyah alitangaza mabadiliko hayo ya aibu na kumfanya Zayd kuwa kaka yake rasmi! Huyu Zayd alikuwa dhalimu asiyejali dini na asiyejali haki za binadamu, na hivyo akatokea kuwa mtu muhimu sana kwa Muawiyah ukiondoa Amr Ibn Aas. Muawiyah akisaidiwa na vibaraka wake hao, alipata nguvu ya kuanzisha uasi kwa Imam Ali (a.s.). Rejea: Tarikh Tabari Raudhatul Safa A’asum Kaafi Muruuju - Dhahab Tarikh Abul-Fida Tarikh Kamil - Ibn Athir Maelezo juu ya uasi huo uliopelekea vita vya Siffin, yatafuatia baada ya maelezo ya vita vya Jamal. Tuanze na maelezo kuelekea vita vya Jamal. 250


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 251

katika Uislamu

Wanafiki wawili Talha Ibn Ubaidullah na Zubair Ibn al-Awam walibuni njia nyingine ya kuwawezesha kuondoka Madina bila kutiliwa shaka. Walimwendea tena Imam Ali (a.s.) wakiomba waende Makkah kwenye Hijjah ya Umra! Imam Ali (a.s.) alitambua ujanja wao na kuwakumbusha kiapo cha utii kwake walichotoa kwa hiari zao. Aliwakumbusha kuwa aliwataka watoe bay’at kwa hiari zao hadharani hapo mwanzo, kwa sababu alifahamu kuwa si waaminifu. Imam Ali (a.s.) aliwaachia waende. Wakati huo Mama Aisha alikuwa anarejea toka Makkah kwenye Hijja. Akiwa njiani alipata habari za kuuawa Uthman, akawa amefurahi, kama nilivyoelezea huko nyuma, juu ya kauli yake baada ya Uthman kuwanyima urithi. Lakini hapo hapo, akapata habari za kuchaguliwa Imam Ali (a.s.) kuwa khalifa. Kusikia hivyo alikasirika sana na kusema, “Natamani mbingu zingeporomoka kabla Ali (a.s.) hajawa khalifa!” Pale pale aliamuru arejeshwe Makkah. Kutoka Makkah alielekea Basra akiwahamasisha watu njia nzima kujiunga na jeshi la uasi dhidi ya Imam Ali (a.s.)! Aliondoka Makkah na wapanda ngamia 600, wapanda farasi 400, na aliwashawishi watu 3,000 kuwa askari hadi kufikia askari 30,000. Kati ya Makkah na Basra maelfu ya Waislamu wanaomwunga mkono Imam Ali (a.s.) waliuawa kwa amri ya Bibi Aisha! Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imam Ali (a.s.): Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, ‘Utawatambua wanafiki kwa chuki yao dhidi ya Ali Ibn Abi Talib’. Rejea: 1. Sahih Muslim, Jz. 1, uk. 61 2. Sahih-Tirmidh, Jz. 5, uk. 306 3. An-Nasai al-Kafiya, Jz. 8, uk. 116 4. Kanzul-Ummal, Jz. 15, uk. 105 Mama Aisha akiuka amri ya kukaandani akiwa mke wa Mtume (s.a.w.w.): Wake za Mtume (s.a.w.w.) waliamriwa na Mwenyezi Mungu kukaa ndani majumbani mwao milele - (Qur’ani 33:33). Lakini tunamwona hapa 251


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 252

katika Uislamu

Mama Aisha anapanda ngamia na kupita mijini anahamasisha watu kwenda kwenye maovu, kwani Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kumpenda Ali ndio ucha Mungu (uumini) wa kweli kweli na kumchukia Ali ni unafiki.” Rejea:- Tarikh Tabari na Tarikh Ibn al-Athir. Hadithi nyingine ya Mtume (s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa: “Kisha muda si mrefu baadaye, mbwa wa Hawab watambwekea mmoja wa wake zangu atakayekuwa katika kundi la uasi (uhaini).” Rejea:- (a) Muir’s Annals of History, uk. 353. (b) Tarikh Tabari. Utabiri huo wa Mtume (s.a.w.w.) ulitimia wakati Mama Aisha akiwa njiani toka Makkah kwenda Basra akiongoza jeshi lake dhidi ya Imam Ali! Rejea: (a) Tarikh Tabari, Jz. 5, uk. 178. (b) Muir’s Annals of History. Kuhusu Mama Aisha kuwaamuru Waislamu kama kiongozi wao, Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa: “Jamii ya watu ambayo mambo yake yataongozwa na mwanamke haitafanikiwa.” Rejea:- Sahih alBukhari, Jz. 8, uk. 97. Hadithi nyingine inatuonya kuhusu Mama Aisha: Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa (wakati akitoka ndani ya nyumba ya Mama Aisha): Chimbuko (nguzo) la ukafiri ni hapa ambapo pembe za kichwa cha shetani zitachomoza. Rejea: Sahih Muslim, Jz. 8, uk. 181. Vita vya Jamal Ndogo: Kabla ya maelezo juu ya vita hivi vilivyotokea hapo Basra-Iraq, turejee Makka kabla ya safari ya mama Aisha kuelekea Basra. Wakati mama Aisha akihamasisha watu kujiunga na jeshi lake na wenzake; Talha Ibn Ubaidullah na Zubair Ibn al-Awam, alimwendea pia mke mwingine wa Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa kaja hapo Makka kwa ibada ya Hijja, naye ni mama Umm Salama. Alimtaka mama Salama ajiunge na kampeni yake dhidi ya Imam Ali (a.s.)! 252


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 253

katika Uislamu

Umm Salama alimwambia mama Aisha kuwa: “Unakumbuka maneno ya mume wetu, Mtume (s.a.w.w.) kwamba: ‘Ali ni mrithi wangu katika uhai wangu na baada ya kufa kwangu na atakayemuasi kaniasi mimi?’” Mama Aisha alijibu kuwa ni kweli. Mama Salama akamwuliza mama Aisha tena, “Je, unakumbuka maneno ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuwa mke wake mmoja kati yetu atabwakiwa na mbwa katika bonde la Haw’ab, akiwa katika kundi la waasi?” Mama Aisha akakubali. Hapo Mama Salama akamwambia, “Ewe Humaira (Aisha) uwe makini usije ukawa ni wewe.” Mama Aisha aliyakumbuka vizuri maneno hayo ya Mtume (s.a.w.w.) na akaogopa! Mama Aisha alirejea maskani kwake kwa nia ya kujiondoa katika janga hilo, lakini akakutana na mtoto wake wa kupanga, Abdallah Ibn Zubair, ambaye alimshawishi asijiondoe. Mama Hafsa, mke mwingine wa Mtume (s.a.w.w.) alikatazwa kutoshiriki, na kaka yake. Mama Hafsa ni mtoto wa Umar Ibn al-Khattab. Mama Aisha alikuwa kajengewa kibanda juu ya ngamia wake, ambamo alijisetiri katika safari hiyo ya uasi dhidi ya Imam Ali (a.s.)! H u k o njiani walikutana na sahaba mmoja Muhajirin, bwana Saidi ambaye alitilia shaka lengo la Talha na Zubair na kuwauliza: “Je, mkishinda vita nani kati yenu atakuwa khalifa?” Wakamjibu, “Mmoja kati yetu atakayechaguliwa na watu.” Akawauliza tena, “Kama vita hivi ni vya kulipiza mauaji ya Uthman kwa nini msifuate kawaida kwa kumpa ukhalifa mtoto wake Uthman, ambaye hata hivyo mnaye hapa! Au mnatafuta kisingizio cha kupigana kwa manufaa yenu binafsi?” Kufikia hapo sahaba huyo bwana Saidi pamoja na mwenzake, bwana Mughira Ibn Shu’ba wakajitoa katika jeshi hilo la uasi. Bwana Mughira Ibn Shu’ba alikuwa gavana katika utawala wa Uthman Ibn Affan. Katika kujitoa kwao walisikika wakipiga ukelele kuwa, ‘Waueni wauaji wa Uthman ambao ni viongozi wenu hao watatu wa jeshi lenu hilo (yaani Talha, Zubair na mama Aisha) kisha mrejee makwenu msipoteze muda wenu!’

253


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 254

katika Uislamu

Jeshi la mama Aisha likiwa njiani lilipata habari kuwa Imam Ali (a.s.) katuma jeshi lake linawafuata kuwazuia wasifike Basra. Hivyo mama Aisha aliamuru waache njia kuu watumie njia ya pembeni ili wafike Basra bila upinzani. Mtu mmoja mjuzi wa njia, alipitisha usiku akiimba na kutangaza majina ya vijiji wanavyopitia. Wakiwa njiani usiku mmoja, kiongozi huyo wa njia alitangaza, ‘Hili ni bonde la Haw’ab’ Rejea:Successors of Muhammad - cha Bwana W. Irving, Uk. 172. Mama Aisha kusikia neno ‘Haw’ab’ alisisimka mwili na hapo hapo mbwa wa pale kijijini wakafika na kumzunguka ngamia wa Mama Aisha na kuanza kubweka! Mama Aisha aliuliza tena, “Hapa ni wapi?” Yule kiongozi akajibu, “Hili ni bonde la Haw’ab.” Mama Aisha alisikika akipiga ukulele, kwani utabiri wa Mtume (s.a.w.w.) ulitimia kama nilivyoeleza hapo nyuma! Lakini Talha na Zubair walikula kiapo cha uongo na wakawanunua (wakawahonga) wenyeji 50 kula kiapo cha uongo na kudai kuwa mahali pale siyo Haw’ab na kwamba kiongozi kakosea! Hapo ndipo mama Aisha aliamuru wapige kambi hapo kwa kutoridhika na uongo huo. Lakini Talha na Zubair wakabuni ujanja na kupiga kelele ghafla kuwa jeshi la Imam Ali (a.s.) tayari linawafukuzia! Ndipo mama Aisha akanyanyuka upesi na kupanda ngamia wakaondoka haraka na mwisho kufika pembezoni mwa mji wa Basra mahali paitwapo Khoreiba wakapiga kambi hapo. Mama Aisha alituma ujumbe kwa gavana wa Basra Uthman Ibn Hunaif akimtaka kujiunga naye. Gavana aliondoka na wafuasi wake wengi kumsikiliza mama Aisha na akakuta jeshi la waasi limetapakaa. Talha na Zubair wakahutubia kisha mama Aisha naye akahutubia akiwa juu ya ngamia wake. Ikawa kumezuka kutoelewana. Mtu mmoja mkazi wa Basra akasema, “Ewe mama wa waumini! Kumuua khalifa ni kosa lingine, lakini wewe kusahau heshima yako na amri juu yako ya kukaa ndani (Qur’ani 33:33) na badala yake kuja hapa bila hijabu tena ukiwa juu ya ngamia ni vipi uzito wake?” Mtu mwingine akawageukia Talha na Zubair akasema, “Nyie mmemleta mama yetu Aisha mbona wake zenu hamkuwaleta pia?”

254


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 255

katika Uislamu

Talha na Zubair walitaka kumkamata gavana wa Basra, Uthman Ibn Hunaif kwa kujidai kumkaribisha kambini kwao lakini gavana alitambua njama hizo za kutaka kumwua na hivyo akakataa. Rejea:- (1) Sahih alBukhari, Jz.12, uk. 68 (Kuhusu Mama Aisha) (2) Tarikh Tabari. Usiku mmoja wa giza, waasi hao walichagua kundi la askari na kuvamia nyumba ya gavana na kumkamata baada ya kufanikiwa kuwaua walinzi wake 40. Jitihada za kumwokoa zilishindwa na mama Aisha akapoteza askari 70 kabla ya kuichukua Basra. Mama Aisha aliulizwa ni adhabu gani apewe gavana huyo, akaamuru auawe, lakini mama mmoja mwenyeji maarufu akaomba hukumu hiyo isitishwe. Ikawa hukumu hiyo imetenguliwa lakini gavana huyo aliteswa sana kwa kung’olewa nyusi na ndevu moja moja na mwisho akawatoroka. Vita vya Jamal Ndogo vilipigwa mnamo tarehe 25 Rabi al-Thani, 36 A.H sawa na 656 A.D. Wafuasi 40 wa Imam Ali (a.s.) waliuawa kwa amri ya mama Aisha, katika msikiti wa Basrah, na wengine 70 sehemu nyinginezo. Bwana Hakim Ibn Jablah aliyekuwa chifu wa ukoo wa Abd al-Qays, na mwenye hekima na elimu, akiwa pia ameikariri Qur’ani yote, alijitokeza na watu wake wakisaidiwa na watu wachache wa ukoo wa Rabiah, wakashambulia jeshi la mama Aisha kwa ushujaa lakini walizidiwa na kuuawa wote. Baada ya hapo likafika jeshi la Imam Ali (a.s.) na Vita vya Jamal Kubwa vikaanza. Vita vya Jamal Kubwa: Huko Madina Imam Ali (a.s.) alipata taarifa za uasi huo wa Talha, Zubair na mama Aisha. Aliingia msikitini na kuwahutubia Waislamu akiwataka wabebe silaha lakini watu walionekana wazito, na baadhi yao waliona labda si sahihi kuingia vita dhidi ya mama Aisha, ingawa Hadithi za Mtume (s.a.w.w.) ziko wazi. Hata hivyo mwisho wake watu walijitokeza kujiunga na jeshi hilo la Imam Ali (a.s.). 255


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 256

katika Uislamu

Huko Kufa-Iraq kulitokea kutoelewana baada ya baadhi ya viongozi kupotosha ukweli wa mambo kuhusu mgogoro huo. Imam Ali (a.s.) alimtuma mwanae Husein (a.s.) pamoja na sahaba mmoja mwadilifu bwana Ammar Ibn Yassir kupeleka ujumbe kwa watu wa Kufa na kuwaeleza ukweli juu ya mgogoro huo. Imam Husein alitoa hotuba ndefu na kukariri maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuwa: “Ali siku zote atakuwa upande wa haki.” Watu 9,000 walijiunga na jeshi na hivyo kufikia askari 20,000 wengi wao wakiwa sahaba wa Mtume (s.a.w.w.). Jeshi la mama Aisha lilikuwa na askari 30,000 wengi wao wakiwa wanafunzi wa vita. Imam Ali (a.s.) alipowasili na jeshi lake pale Khoreiba, mama Aisha, Talha na Zubair waliogopa kumwona amevalia tayari kwa vita. Imam Ali (a.s.) alipeleka ujumbe kujaribu kuleta suluhu. Talha na Zubair walimtaka aende kwenye kikao. Majadiliano marefu yaliendelea kwa muda mrefu kati yao, huku wakizunguka huku na huko bila muafaka, hali ya kuwa Imam Ali (a.s.) anawakumbusha Talha na Zubair maneno muhimu ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya migogoro kama hiyo na matokeo mabaya yanayowasubiri akhera. Zubair Ibn al-Awam aliogopa na kukaribia kujitoa, lakini aliporejea kwa mama Aisha na kumweleza majadiliano hayo, mama Aisha alimkasirikia sana na kumbadili mawazo. Hivyo alibakia. Imam Ali (a.s.) alifanya suluhu ya mwisho kwa kutaka Qur’ani iwe mpatanishi. Mtu mmoja jina lake Muslim alijitolea kuitundika Qur’ani kwenye mti na kuiinua juu ili jeshi la mama Aisha waache uasi na umwagaji damu lakini askari mmoja wa mama Aisha alijitokeza na kumkata mkono ulioinua hiyo Qur’ani na kisha kumwua! Baada ya mazishi ya mwenzao, askari wa Imam Ali (a.s.) hawakuvumilia tena uovu huo, na hivyo walijitokeza uwanjani na vita vikaanza kwa nguvu. Talha aliuawa na mshale uliotupwa na msaidizi wake, wakati Talha akihimiza mapigano! Sababu ni kwamba huyo msadizi wake alifahamu wazi kuwa vita hivyo si halali kwani yeye Talha alishiriki kumwua 256


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 257

katika Uislamu

Uthman! Zubeir alipigana shingo upande alipokumbuka maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuwa sahaba mmoja Ammar Yasir siku zote atakuwa upande wa haki na atauawa na waasi. Utabiri huo ulitimia katika vita hivyo! Kwa hiyo Zubeir alijiondoa katika vita hivyo na kutoroka. Akiwa njiani alikutana na kikundi cha walinzi wa bwana Ahnaf Ibn Qais wakisubiri matokeo ya vita. Huyo bwana akaamuru mlinzi mmoja amfuate Zubeir. Yule mlinzi akamfuata lakini alipomkaribia ikawa Zubeir ameshtuka, hata hivyo wakasalimiana na baadaye kuswali pamoja. Zubeir akiwa amesujudu, mwenzake akachukua panga na kumkata kichwa na kukipeleka kwa Imam Ali (a.s.) ambaye pamoja na uovu wa Zubeir, alikasirishwa na kitendo hicho na kumfukuza kwa sababu hairuhusiwi kumwua mtu aliyekimbia vita. Yule mlinzi aliyeleta kichwa hicho cha Zubeir alitarajia zawadi nono lakini hakupata, hivyo naye akajiua kwa hasira! Jeshi la bibi Aisha baada ya kupoteza viongozi wao muhimu lilianza kusambaratika huku bibi Aisha akipiga kelele kuwahimiza wasife moyo hadi yeye mwenyewe akakosa ulinzi wa kutosha na ikawa ngamia wake wa ajabu amekatwa miguu na kuanguka. Askari wa bibi Aisha wakakimbia na kutawanyika. Marwan Ibn Hakam alikamatwa na kuletwa kwa Imam Ali (a.s.) akitarajia kusamehewa na ikawa hivyo. Matokeo ya vita hivyo ni kwamba askari 17,000 wa bibi Aisha walipoteza maisha wakati Imam Ali (a.s.) alipoteza askari 1,070. Hakuna vita vilivyoua watu wengi kama hivyo, uhai wote wa Mtume (s.a.w.w.) hadi wakati huo! Kwa hiyo maneno ya Mtume (s.a.w.w.) yalikamilika juu ya bibi Aisha! Rejea:Tarikh Abul-Fida, uk. 518-520 Tarikh Tabari, Jz. 4, uk. 548-565 Tarikh Ibn Athir Historians History of the World, Jz. 8, uk. 170

257


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 258

katika Uislamu

Baada ya bibi Aisha kupoteza vita hivyo alitekwa, lakini alimwomba Imam Ali (a.s.) amsamehe mateka wake. Imam Ali (a.s.) alikubali kumsamehe na kumtendea kila wema na uadilifu. Imam Ali (a.s.) aliwasamehe pia viongozi wengineo wa jeshi la uasi kama Abdullah Ibn Zubair na Marwan Ibn Hakam. Marwan Ibn Hakam aliwaomba Imam Hasan (a.s.) na Imam Husein (a.s.) kumwombea msamaha huo. Lakini huko baadaye miaka iliyofuata, huyo Marwan ndiye alifanya kitendo kiovu kwa kuongoza kundi la wapiga mishale kupiga mishale jeneza la mwili wa Imam Hasan (a.s.) alipouawa kwa sumu na Muawiyah Ibn Abu Sufiyan. Na ni Marwan huyo huyo aliyemwomba gavana wa Madina kumwua haraka Imam Husein (a.s.) kama hatoi kiapo cha utii kwa Yazid Ibn Muawiyah! Rejea:- MuruujuDhahabi, uk. 28. Imam Ali (a.s.) alifanya matayarisho ya kumrejesha bibi Aisha Madina kwa heshima zote chini ya uangalizi wa kaka yake bibi Aisha yaani Muhammad Ibn Abu Bakr. Mateka wote na waasi wote walisamehewa. Rejea:Tarikh Tabari, Jz. 4, uk. 548 Raudhatul sw-Swafa Jz. 11 Tarikh Abul-Fida, uk. 518-520 Kutokana na sababu ambazo hazieleweki, bibi Aisha ametukuzwa sana kwa sifa nyingi sana ambazo zinapingana na historia sahihi kama nilivyoitoa kwa ushahidi. Lakini Qur’ani ndiyo inatueleza ukweli kwamba mwanamke kuwa mke wa Mtume, isichukuliwe kuwa ni lazima awe na sifa za uchamungu! Vile vile bibi Aisha kuitwa mama wa waumini ni kwa sababu Mtume (s.a.w.w.) aliusia kuwa hakuna mke wake yeyote aliyeruhusiwa kuolewa na mume yeyote baada ya yeye kufariki. Kwa hiyo wake zake wote Mtume (s.a.w.w.) ni mama zetu ingawa mwelekeo wa wengi wetu ni kumpa cheo hicho bibi Aisha peke yake! Hebu tuone Qur’ani inasemaje juu ya wake za Mitume:

258


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 259

katika Uislamu

“Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa wale waliokufuru, kwa mke wa Nuhu na mke wa Lut, wawili hawa walikuwa chini ya waja wetu wema wawili kati ya waja wetu, basi (wanawake hao) wakawafanyia khiana, (lakini waume zao) hawakuwasaidia chochote mbele ya Mwenyezi Mungu; na ikasemwa: Ingieni motoni pamoja na waingiao.” (Qur’ani 66:10) Kwa hiyo hapa tunaona kuwa mke wa Nabii Nuhu (a.s.) na mke wa Nabii Luti (a.s.) walikufa makafiri kwa vitendo vyao, na kwamba walitupwa motoni! Hivyo basi sisi tunamheshimu bibi Aisha kama mke wa Mtume (s.a.w.w.) lakini hatuna sababu za kufumbia macho matendo yake. Imani yetu ni kwamba hukumu yake ipo kwa Mwenyezi Mungu. Siyo juu yetu kuamua. Vita vya Siffin: Baada ya vita vya Jamal, bwana Muawiyah aliunda jeshi imara la askari 120,000 kwa nia ya kumwondoa madarakani Imam Ali (a.s.). Imam Ali (a.s.) aliunda jeshi la askari 90,000. Baada ya Muawiyah kukataa suluhu, Imam Ali (a.s.) alilazimika kupigana vita hivyo vya Siffin kwa siku 10 tangu tarehe 11 Safar, 37 A.H. Nimetangulia kueleza kuwa Muawiyah alikuwa gavana wa Sham (Syria) tangu enzi za utawala wa bwana Abu Bakr Siddiq. Syria ilikuwa na raslimali nyingi, na Bani Umayyah wengi walihamia huko na hivyo kumfanya Muawiyah kuwa imara kijeshi. Muawiyah alishuhudia kwa masikitiko jeshi lake likiangamizwa na askari hodari wa Imam Ali (a.s.), huku Imam Ali (a.s.) mwenyewe akionyesha 259


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 260

katika Uislamu

ushujaa mkubwa. Muawiyah aliamuru aletewe farasi wake ili atoroke baada ya kuzidiwa! Lakini askari wake mmoja mjanja aitwaye Amr Ibn Aas alimwita Muawiyah na kumwambia, “Usikate tamaa, nimeshabuni ujanja wa kusimamisha askari wa Ali waache mapigano.” Amr Ibn Aas akamwambia Muawiyah: ‘Waite maadui kwa kutundika Qur’ani juu ya mikuki na kuwataka suluhu ipatikane kwa Kitabu kitukufu. Iwapo watakubali, tutakuwa tumeokoka na wasipokubali hata hivyo, tutakuwa tumevunja umoja wao na kuwadhoofisha.” Muawiyah akafanya hivyo na ikawa askari wa Imam Ali (a.s.) wamegawanyika kati ya wanaokubaliana na hiyo suluhu ya ulaghai, na wale wanaokubaliana na Imam Ali (a.s.) kuendelea na vita mpaka kumwangamiza Muawiyah Ibn Abu Sufyan. Wafuasi wa Muawiyah waliogopa walipomwona sahaba maarufu Ammar Ibn Yasir ameuawa akiwa upande wa Imam Ali (a.s.), kutokana na Hadithi ya Mtume (s.aw.w.) kwamba Ammar atauawa na kundi la waasi. Walipomwuliza Muawiyah suala hilo alisema ‘Aliyemwua Ammar ni Ali (a.s.) aliyemleta vitani!’ Imam Ali (a.s.) alijibu kuwa, “Kama ni hivyo basi tuseme kuwa Mtume alimwua ammi yake Hamza kwa kumwamuru kupigana na makafiri katika vita vya Uhud! Rejea:Tarikh Tabari, Jz. 1, uk. 3316-3322; Jz. 3 uk. 2314-2319. Tarikh Ibn Kathir, Jz. 7, uk. 267-272. Sharkh Nahjul Balaghah, Jz. 5, uk. 252-258 Baada ya Imam Ali (a.s.) kuona askari wake wamemwasi, aliamuru Amiri jeshi wake - Malik Ashtar aliyekuwa anapambana kishujaa kwamba, “Kutafuta ushindi kuna faida gani wakati uhaini umezuka kambini kwetu? Rudi upesi kabla askari wetu hawajaniua kwa uasi wao kwani hawataki kuendeleza mapigano.” Kwa hiyo ilimbidi bwana Malik Ashtar kusimamisha vita na kurejea akiwa na askari wachache watiifu. Rejea:Raudhatu sw-Swafa, cha Ibn Khaldun.

260


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 261

katika Uislamu

Ujanja huo wa kusitisha mapigano, uliendelezwa na Muawiyah kwa mbinu mbali mbali za ulaghai, kwa kisingizio cha suluhu bandia kupitia mikutano na vikao vya unafiki ili kupata suluhu bandia za ulaghai wakati anajiimarisha kijeshi. Matokeo ya kutisha ya vita vya Siffin ni kwamba Muawiyah alipoteza askari 45,000 wakati ambapo Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) alipoteza watu 25,000. Vita hivi, kama vita vya Jamal, vilikuwa ni vya Waislamu wenyewe kwa wenyewe! Hakuna vita vyovyote vile katika historia ya Uislamu, viliyopoteza maisha ya Waislamu wengi namna hiyo! Rejea:Mustadrak al-Hakim, Jz. 3, uk. 104 Al-Isti’ab, Jz. 3, uk. 1138 Tarikh Ya’qubi, Jz. 2, uk. 188 Tarikh Ibn Kathir, Jz. 7, uk. 275 Tarikh Ibn Abi’l-Hadid, Jz. 10 uk. 104 Tarikh Abu’l - Fida’ Jz. 1, uk. 175 Kwa hiyo wale Waislamu wasiotaka kusikia kuwa kulikuwa na migogoro mikubwa baada ya Mtume (s.a.w.w.), wajiulize kwa nini vita moja tu vya Siffin vilipoteza roho za Waislamu 70,000? Kwa nini katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.) vita vya jihad kwa pamoja havikupoteza Waislamu wote hao? Baada ya Uislamu kukamilishwa na Mtume (s.a.w.w.), hayo mauaji makubwa namna hiyo yalisababishwa na migogoro gani halali miongoni mwa Waislamu; miaka 26 tu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.)! Hatuwezi kupuuzia matukio kama hayo iwapo tunataka kuchunguza historia sahihi ya Uislamu ili kujua asili ya upotofu! Upotofu na unafiki uliosababisha vita hivyo, ndio ulioendelea kupotosha Uislamu miaka iliyofuatia mpaka leo hii. Uislamu tulionao leo siyo sawa na ule aliouacha Mtume (s.a.w.w.). Maelezo yafuatayo yatafafanua zaidi.

261


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 262

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) alipoona upinzani huo wa watu wake, alijitoa kabisa katika maamuzi yote na ndipo bwana Ash’athi Ibn Kais Kindi akajitokeza kuwakilisha upande wa Imam Ali (a.s.) katika suluhu hizo bandia. Upande wa Muawiyah uliwakilishwa na Amr Ibn Aas. Kutokana na makubaliano ya kikao hicho, walichaguliwa wawakilishi wa kudumu na ikaamuliwa kuwa hao ndio watatoa maamuzi ya mwisho yatakayoheshimiwa na pande zote mbili. Rejea:- S. Ockley’s History of the Saracens - uk. 317. Kwa hiyo akachaguliwa Abu Musa kwa upande wa Imam Ali (a.s.) na Amr Ibn Aas kwa upande wa Muawiyah. Miezi sita baada ya vita, kulifanyika kikao cha mwisho kilichotawaliwa na udanganyifu. Amr Ibn Aas alikuwa mwanasiasa mjanja na mnafiki kiasi kwamba alimdanganya Abu Musa na ikawa Abu Musa amefanikisha malengo ya Amr Ibn Aas bila kujitambua! Kilichotokea ni kwamba kikao cha mwisho kilipangwa kufanyika Duma. Abu Musa aliwasili hapo na kupokelewa kwa heshima kubwa ya kiunafiki. Maongezi ya faragha yalifanyika kati yao katika kibanda maalumu kilichojengwa kwa madhumuni hayo. Amr Ibn Aas alikuwa anafahamu udhaifu wa Abu Musa. Amr Ibn Aas alimlaghai Abu Musa na kumvuta kumtumia atakavyo. Amr Ibn Aas alimfanya Abu Musa kukiri madai potofu kwamba Uthman Ibn Affan aliuawa bila haki na kwa hiyo apatikane mtu wa damu yake (Uthman) apewe ukhalifa. Abu Musa alikataa pendekezo hilo. Ndipo Amr Ibn Aas alipendekeza kuwa Imam Ali (a.s.) na Muawiyah wote wakataliwe kuwa khalifa na Waislamu wachague mtu mwingine. Abu Musa alikubali pendekezo hilo. Kwa hiyo walikubaliana watoke nje watangaze uamuzi huo. Abu Musa alitaka Amr Ibn Aas aende kutangaza kwanza, lakini Amr Ibn Aas alitoa sababu kumtaka Abu Musa aanze kutangaza. Abu Musa alitokeza na kutangaza kuwa, ili kurejesha amani na utulivu, imeamuliwa kuwa Imam Ali (a.s.) na Muawiyah waachie madaraka ili watu wachague kiongozi mwingine. Kwa hiyo alisema kuwa anavua pete toka kwenye kidole kuashiria kuondolewa madarakani Imam Ali (a.s.) na Muawiyah. Ndipo akateremka chini ya jukwaa. 262


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 263

katika Uislamu

Hapo hapo Amr Ibn Aas alipanda na kusema kuwa, ‘Abu Musa amemvua madaraka kiongozi wake Ali (a.s.) lakini mimi ninamvua madaraka Ali (a.s.) na kumvisha madaraka kiongozi wangu Muawiyah na kumfanya khalifa kama ninavyovaa pete kwenye kidole!’ Ulaghai huo ulifanyika mwezi wa Ramadhani 37 A.H hapo Duma. Abu Musa baada ya kunaswa katika ulaghai huo, alikimbilia Makkah na hakusikika tena hadi alipofariki miaka ya 42 au 52 A.H! Waislamu maarufu kama mtoto wa Umar Ibn Al-Khattab na mtoto wa Abu Bakr walikasirika sana kwa tukio hilo. Abu Musa alirejea Madina, na Muawiyah Ibn Abu Sufyan alipokelewa kama khalifa huko Syria. Kwa hiyo Muawiyah akawa imara tena! Abu Musa tangu mwanzo wa ulaghai huo, alishaahidiwa donge nono la rushwa ya Dirham 100,000. Baada ya hapo Abu Musa alistaafu huko Madina na kupewa pensheni maalum toka kwa Muawiyah kila mwaka. Rejea:Tarikh Tabari Tarikh Abul-Fida Raudhatu-Swafa Muruuju-Dhahab Tarikh Kamil - cha Ibn Athir The Short History of the Saracens Baada ya suluhu batili ya Siffin huko Duma, iliyokamilika tarehe 13 Safar, 37 A.H, askari 12,000 walijitenga kutoka Jeshi la Imam Ali (a.s.) na walijulikana kama ‘Khawarij’ (yaani wapinzani wa misingi halisi ya dini). Askari hao walipiga kambi Harora karibu na mji wa Kufa na wakashabikia itikadi yao mpya ya ‘La Hukmu illa Lillah’ kwa maana kuwa ‘Hapana hukumu ila kwa Mwenyezi Mungu tu.’ Itikadi yao hiyo ilikuwa na maana kuwa hawatambui amri yoyote ya kiongozi yeyote yule ila Mwenyezi Mungu tu! Itikadi yao hiyo ikapindukia mipaka na kuwafanya ‘mashabiki’ yaani wanaoshikilia jambo bila mantiki. Kwa itikadi yao hiyo wakawa hawamtambui Imam Ali (a.s.) kuwa khalifa, na hawataki kula kiapo cha utii kwake au kwa yeyote yule, ila wao na Mwenyezi Mungu tu! 263


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 264

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) aliwakosoa msimamo wao huo usio na misingi yoyote ya dini ndani yake. Baada ya hapo, hao waasi walikiri makosa yao na wakawa tayari kutubia lakini kwa sharti kwamba Imam Ali (a.s.) naye atubie! Imam Ali (a.s.) hakuona lolote la yeye kutubia na kwa hiyo akakataa. Waasi nao wakarudia na kusisitiza msimamo wao wa mwanzo tena. Baada ya suluhu batili ya Duma, Imam Ali (a.s.) alifuatilia taarifa za upelelezi kuhusu mwenendo wa Muawiyah ambaye alikuwa tayari anakusanya ushuru toka kwa raia wa Syria ili kuanzisha tena vita. Vile vile alipata habari juu ya askari wake waliojitenga yaani ‘Khawariji’. Imam Ali (a.s.) aliwataka askari hao wajiunge naye ili kumpiga vita Muawiyah lakini askari hao walikataa na wakaanzisha uasi na mauaji ya wale wasiokubaliana na itikadi yao mpya. Kutokana na tishio hilo kwa usalama wa raia, ilimbidi Imam Ali (a.s.) kuwatumia mjumbe askari hao kuwahoji juu ya uhalali wa vitendo vyao viovu. Lakini mjumbe huyo akauawa. Imam Ali (a.s.) alisimamisha bendera yake ya vita karibu na kambi yake na kuwatangazia hao waasi kuwa wanaotaka kujisalimisha wajikusanye hapo au warejee makwao. Askari hao waasi walianza kutawanyika lakini wengineo 1800 wakakatalia hapo na kushikilia itikadi yao hiyo. Hao waliobakia hapo wakiongozwa na kiongozi wao Abdallah Ibn Wahab, walikabiliana na jeshi la Imam Ali (a.s.) kwa mapigano na wakauawa, isipokuwa askari tisa ndio walionusurika katika vita hivyo vya ‘Nahrawan’ viliyopigwa mwaka huo huo wa 37 A.H. Askari hao 9 walionusurika hapo, ndio walioendeleza itikadi hiyo potofu na ndiyo asili ya madhehebu moja ya kiislamu ambayo hata hivyo inakanusha ukweli huo wa kihistoria. Baada ya vita hivyo, jeshi la Imam Ali (a.s.) likiongozwa na yeye mwenyewe lilivuka mto Tigris kuelekea Syria, lakini viongozi wa jeshi walimwomba awaruhusu askari warejee nyuma wapumzike kwa matayarisho ya kusonga mbele. Kwa hiyo wakarudi nyuma na kupiga kambi 264


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 265

katika Uislamu

mahali paitwapo Nokheila karibu na mji wa Kufa na ikawa askari wametawanyika kwa makubalino kuwa warudi kesho yake. Askari hao hawakurejea tena kambini mpaka ikabidi Imam Ali (a.s.) awafuate mjini bila mafanikio, na mwisho wake safari hiyo ikavunjika kabisa. Vitendo hivyo vya uasi wa mfululizo, vilimvunja moyo Imam Ali (a.s.) na havikumpa muda wa kutoa elimu yake kubwa kwa umma wa kiislamu, umma ambao ulishadidimia kiroho kiasi cha kutojali maagizo ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imam Ali (a.s.). Kwa hiyo Syria ikabakia mikononi mwa dhalimu Muawiyah Ibn Abu Sufyan. Kutokana na uaminifu na ucha Mungu wa mtoto wa bwana Abu Bakr Siddiq yaani Muhammad Ibn Abu Bakr, Imam Ali (a.s.) alimchagua kuwa gavana wa Misri. Bwana Muhammad Ibn Abu Bakr alikuwa hodari wa vita na pia mwadilifu. Akiwa huko Misri, bwana Muhammad alifanya kazi yake vizuri lakini Muawiyah alianza uchokozi na kumlazimisha waingie vitani. Kwa hiyo bwana Muhammad akaomba msaada kwa Imam Ali (a.s.) ambaye alimtuma bwana Malik al-Ashtar huko Misri. Lakini bwana Malik aliuawa kwa sumu akiwa njiani na kibaraka wa Muawiyah. Rejea:Tarikh Tabari, Jz. 4, uk. 521. Kwa hiyo bwana Muhammad Ibn Abu Bakr akalazimika kupambana peke yake na kibaraka mkubwa wa Muawiyah yaani Amr Ibn Aas. Bwana Muhammad Ibn Abu Bakar alizidiwa nguvu na hivyo akauawa. Muawiyah aliamuru mwili wa marehemu uchomwe moto badala ya kuzikwa! Rejea: Tarikh Tabari - Jz. 4 uk. 592 Wakati Imam Ali (a.s.) anapanga kutuma afisa mzoefu huko Misri, Muawiyah alitayarisha makundi ya wapiganaji wa kuvizia wa misituni na kuwatuma wapore, waue, wachome moto nyumba na kubaka wanawake huko katika majimbo ya Hijaz, Basra, Raay, Mosul na Hirat. Imam Ali (a.s.) alichukua hatua ya kuweka ulinzi katika majimbo hayo na ikawa njama hizo zimevunjwa.

265


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 266

katika Uislamu

Uongozi wa Imam Ali (a.s.) kwa vitendo, ulikuwa ni uongozi wa uadilifu wa hali ya juu na ucha Mungu. Pamoja na Imam Ali (a.s.) kushika uongozi huo mkuu, aliishi maisha ya chini sana katika kibanda chake cha udongo sawa na raia wa chini kabisa. Hazina kubwa ya ‘Baitul Maal’ aliiona ni mali ya taifa na alijigawia kiasi kidogo sawa na thamani ya mahitaji ya raia wa chini kabisa. Aliwadhibiti viongozi wa chini yake wasishiriki vitendo vya ubadhilifu, anasa na majivuno kwa raia. Uadilifu wa Imam Ali (a.s.): Tukichunguza kumbukumbu za historia zinaonyesha kuwa katika uongozi wake, Imam Ali (a.s.) alimwandikia barua gavana wa Basra kwamba: “Ewe Ibn Hunaif, nimepokea taarifa kuwa kijana mmoja tajiri wa hapo Basra amekukaribisha katika harusi yake ya kifahari na kwamba ulipokea mwaliko huo na uliandaliwa vyakula vitamu vya kitajiri. Sikutegemea kuwa unaweza kupokea mwaliko wa watu ambao huwatenga masikini mbali kabisa na meza zao za chakula, na kuwaalika matajiri tu. Kumbuka kuwa waumini waaminifu wanahitaji kufuata mifano mizuri ya kiongozi wao (Imam) na wewe ni mwakilishi wangu huko. Ukumbuke kuwa katika maisha ya kidunia, Imam wako (Hadhrat Ali) amepunguza matumizi yake kiasi kwamba kwa mavazi hahitaji zaidi ya kanzu mbili chakavu, na kwa chakula hahitaji zaidi ya mikate miwili. Ni kweli kwamba wewe huwezi kujinyima kiasi hicho, lakini bado unaweza, kiasi cha kutosha, kunisaidia, kwa wewe kuwa mcha Mungu kwa vitendo na kuwa mwaminifu na mwongofu. Ningependa kuendekeza nafsi yangu kula na kuishi kwa anasa, ningeweza lakini itanifaa nini wakati nafahamu kuwa kuna watu wengi Hijaz na Yemen ambao hawana uwezo wa kupata japo kipande tu cha mkate. Vipi nifurahie kuitwa ‘Kiongozi wa Waumini’ wakati sishiriki matatizo ya wanaoniita hivyo.” Barua hiyo ya Imam Ali (a.s.) kwa gavana wake wa Basra ni sehemu ndogo tu ya ushahidi wa uadilifu katika uongozi wa Imam Ali (a.s.). Tunasoma pia kwamba Imam Ali (a.s.) alikuwa kiongozi mwadilifu na maarufu hata 266


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 267

katika Uislamu

kwa wasio Waislamu, kiasi kwamba alipouawa, Wakristo, Wayahudi na Wamajusi (Zorastrians) katika mji wa Kufa, na hasa akina mama na watoto ambao Imam Ali (a.s.) aliwajibika kuwahudumia binafsi, kwa mujibu wa kanuni za uongozi katika taifa halisi la kiislamu, wote hao walimlilia sana na kuomboleza kana kwamba ni baba yao! Msiba huo uliombolezwa hata huko Jerusalem ambako Lord Bishop naye alishindwa kujizuia kutokwa na machozi. Rejea: Professor M.G. Reynold’s Book on Islam - Sura ya Tatu. Mfano mwingine wa uadilifu wa Imam Ali (a.s.) unaelezwa na Ibn Abi Rafi’ ambaye alikuwa mwendeshaji msimamizi wa Hazina (Baitul Maal) na pia Katibu wa Imam Ali (a.s.) katika kipindi cha ukhalifa wake. Bwana Ibn Abi Rafi’ anaeleza kuwa: “Nilipokea mkufu wa vito toka Basra, pamoja na mali nyinginezo kwa ajili ya Hazina. Binti wa Imam Ali (a.s.) alinitumia ujumbe: ‘Nafahamu kuwa kuna mkufu wa vito humo katika hiyo Hazina ya Baitul Maal iliyo chini ya uangalizi wako, nitumie huo mkufu kwa kuazima ili niuvae sikukuu ya Idd Kubwa. Baada ya hapo nitaurejesha kwako.’” Bwana Ibn Abi Rafi’ anaendelea kueleza kuwa, alimtumia mkufu huo kwa masharti kuwa atawajibika kuutunza usipotee au kuharibika na kwamba ataurejesha mnamo siku ya tatu. Binti yule alikubaliana na masharti hayo. Kwa bahati Imam Ali (a.s.) alitokea kuona na kutambua mkufu huo na kupata maelezo jinsi binti yake alivyoupata. Imam alimhoji Ibn Abi Rafi’, “Unadhani ni halali kwako kuvunja dhamana ya Waislamu?” Abi Rafi’ alijibu: “Mwenyezi Mungu aniepushe na uovu huo.” “Kama ni hivyo kwa nini hukupata idhini yangu au idhini ya Waislamu, kumwazima binti yangu mkufu toka Baitul Maal?” Abi Rafi’ alijibu: “Ewe Kiongozi wa Waumini, huyo ni binti yako. Aliazima ili kujipamba na kisha kurejesha:” Imam Alimkaripia Abi Rafi’ na kusema: “Rejesha mkufu huo leo hii na usirudie siku zijazo vinginevyo nitakuadhibu.” 267


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 268

katika Uislamu

Binti yake alipopata taarifa hiyo alimwendea baba yake na kumwambia, “Ewe baba, mimi ni kipenzi binti yako, ni nani mwingine anayestahili kuvaa mkufu huo zaidi yangu?” Imam alijibu, “Ewe mtoto wa Abu Talib, usiache njia ya haki. Unaweza kunieleza ni wanawake wangapi Ansari na Muhajirun wanaojipamba kwa mikufu kama hiyo?” Kisa kingine ni pale ambapo Imam Ali (a.s.) aligundua kuwa ngao yake ya vazi la vita alikuwa anayo raia mmoja Mkristo. Alimpeleka mahakamani kwa hakimu aliyeitwa Shurayh. Imam alimweleza hakimu kuwa vazi hilo la kinga ni lake na hajaliuza au kulitoa zawadi kwa yeyote. Hakimu alimwuliza huyo mtu: “Je unasemaje?” Yule mtu akajibu: “Vazi hili ni langu ingawa sidhani kuwa Kiongozi wa Waumini ni mwongo.” Hakimu akamwuliza Imam kama ana shahidi yeyote. Imam alijibu kuwa hana. Kwa hiyo Hakimu alihukumu kuwa mshindi ni huyo Mkristo ambaye baada ya hapo alibeba hilo vazi na kuondoka. Imam Ali (a.s.) alimfuata nyuma huyo mtu na akawa anamtaza tu anavyokwenda. Baada ya hatua chache yule Mkristo aligeuka na kumuona Imam anamtazama, alirudi na kumweleza Imam Ali (a.s.): “Kwa kweli nakiri kwamba hukumu hiyo ni sawa na Manabii kwa sababu Kiongozi wa Waumini amesimamishwa mahakamani na mtu wa chini kama mimi, wakati ambapo hakimu yuko chini yake, na kisha hakimu akatoa hukumu dhidi yake!” Yule Mkristo aliongeza kuwa, “Ewe Kiongozi wa Waumini, vazi hili la vita ni la kwako na madai yangu yachukuliwe kuwa batili.” Ndugu Muislamu, huo ndio uadilifu unaotakiwa kwa Kiongozi Mkuu katika Taifa la kweli la kiislamu. Lakini tukirejea Sura ya 11 chini ya: Uthman awatajirisha jamaa na rafiki zake kwa Baitul Maal; tutaona jinsi Uthman alivyofuja Baitul Maal kama mali yake binafsi! Hivyo hivyo na makhalifa wenzake wengi waliofuatia baadaye kwa karne nyingi. Migogoro ya kugombea ukhalifa ilikuwa ni tamaa ya kufaidi Baitul Maal kinyume na matumizi yake ya halali. Rejea: (The Voice of Human Justice, cha George Jordac - Lebanon Syria) – au tarjuma ya Kiswahili - Sauti ya Uadilifu wa Binadamu. 268


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 269

katika Uislamu

SABABU ZA KUUAWA IMAM ALI IBN ABI TALIB (a.s.) Pamoja na uadilifu wa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.), Khawarij hawakuridhika. Kwa kweli hawakuridhika pia na maamuzi yaliyowatenganisha Muawiyah na Imam Ali (a.s.). Waliona kuwa serikali yoyote imara juu yao, itakomesha uporaji walioufanya wao mara kwa mara na kujipatia mali nyingi mno na ngawira. Katika misingi ya itikadi yao potofu niliyotangulia kueleza, baadhi yao walijiona wachamungu zaidi na kwa hiyo walidai kuwa lazima watawaliwe na ufalme wa Mwenyezi Mungu moja kwa moja hapa duniani. Lakini hapo hapo waliamini kuwa lengo hilo haliwezi kufanikiwa mpaka kwanza Imam Ali (as.) na Muawiyah waondolewe madarakani, kwa imani kuwa viongozi hao wawili wamepata madaraka kinyume na msimamo au itikadi ya La Hukmu Illa Lillah (Hakuna hukumu isipokuwa ya Mwenyezi Mungu). Wale Khawarij walionusurika katika vita vya Nahrawan walikimbilia Makka kupata kinga ya ‘haram’ ili wasishambuliwe. Wakiwa hapo walifanya mikutano kadhaa na kuweka mikakati pamoja na kula njama ya kulipiza kisasi cha ndugu zao waliouawa katika vita vya Nahrawan kama nilivyoelezea huko nyuma. Katika vikao hivyo waliamua kuwaua Imam Ali (a.s.) na Muawiyah. Vile vile waliamua kumwua pia kibaraka mkuu wa Muawiyah yaani Amr Ibn Aas ili atakapokufa Muawiyah, huyo kibaraka wake asije kudai kulipiza kisasi cha damu ya Muawiyah kama kisingizio cha kunyakua ukhalifa! Kwa hiyo walijitolea Khawarji watatu shupavu kufanya kazi hiyo ya mauaji hayo eti kuusafisha ulimwengu na madhalimu! Wauaji hao walikuwa ni Abdur Rahman Ibn Muljim, Burk Ibn Abdullah na Amr bin Bakr. Njama hiyo ilipangwa itekelezwe siku ya Ijumaa tarehe 19, Ramadhan 40 A.H sawa na 660 A.D. 269


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 270

katika Uislamu

Mauaji yatekelezwa: Burk Ibn Abdullah alifika Damascus Syria, kisha akachanganyika na waumini katika Swala ya Asubuhi na ndipo akapata nafasi ya kumchoma kisu Muawiyah lakini kisu kiliteleza na kumjeruhi Muawiyah kwapani. Burk alikamatwa na akajigamba kwamba muda ule ule Abdulrahman Ibn Muljim atakuwa tayari ameshamuua Imam Ali (a.s.) huko mjini Kufa Iraq. Muawiyah aliamuru watu wake kumkata miguu na ulimi na kumtesa hadi afe. Huko Misri, Amr bin Bakr alienda msikitini asubuhi. Siku hiyo Amr Ibn Aas aliyekusudiwa kuuawa hakufika msikitini kwani alikuwa anaumwa tumbo. Badala yake siku hiyo aliswalisha naibu wake yaani Kharja bin Huzafa. Huyo muuaji kwa kutojua nani anaswalisha, alinyanyua jambia na kumpiga dharuba moja na kumuua. Punde si punde ikawa Amr Ibn Aas amefika. Baada ya kumhoji Amr bin Bakr kwa nini kafanya hivyo alijibu kuwa, “Wewe Amr Ibn Aas ndiye uliyekusudiwa.� Hapo hapo Amr bin Bakr akauawa. Abdul Rahman Ibn Muljim alifika mjini Kufa na kufanya mipango ya siri. Kwa bahati yake alikutana na mwanamke mmoja mrembo kupindukia aitwaye Qutaum na ikawa amempenda. Mwanamke huyo alimchukia sana Imam Ali (a.s.) kwa sababu mume wake na mjomba wake waliuawa katika vita vya Nahrawan. Kwa hiyo Abdul Rahman Ibn Muljim alipomwendea kumposa mama huyo, alikubali kwa masharti matatu: 1. Apewe Dirham 3000 taslim. 2. Apewe watumwa wawili - wa kike na wa kiume. 3. Aletewe kichwa cha Imam Ali (a.s.). Sharti la tatu halikuwa gumu kwa sababu ndiyo kazi iliyomleta Abdul Rahman hapo Kufa. Mwanamke huyo alimwambia mchumba wake kuwa, ili aweze kumuua Imam Ali (a.s.) ni muhimu amshambulie wakati Imam Ali (a.s.) akiwa amesujudu katika Swala na akiwa haoni kinachofanyika. 270


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 271

katika Uislamu

Siku ilipowadia, Abdul Rahman aliwahi msikitini mapema. Imam Ali (a.s.) naye alifika kuswalisha kama kawaida. Muuaji alisimama nyuma ya Imam Ali (a.s.) na ndipo Imam Ali (a.s.) alipoinama kusujudu na hapo hapo akapigwa upanga mkali uliopakwa sumu. Hapo hapo Imam Ali (a.s.) akasema, “Kwa hakika nimefuzu! Ee Mungu nakushukuru kwa kunituza kifo cha kishahidi, ukarimu wako na upendo wako ni mkubwa.” Imam Ali (a.s.) alimwona muuaji wake amekamatwa na amefungwa kamba zimemkata mpaka kwenye nyama, aliwasihi walegeze kamba hizo na wamtendee wema kama binadamu! Muuaji huyo kusikia hivyo alisikitika na kutokwa machozi. Kisha Imam Ali (a.s.) alibebwa na kupelekwa nyumbani kwake. Aliwaagiza wanawe Hasan na Husein (a.s.) kwamba; “Huyu ni mfungwa wenu, mlisheni na kumnywesha kama ninyi wenyewe. Kama nitapona nitamuadhibu mwenyewe adui yangu huyu, lakini kama nitafariki, nawausia muamue mtakavyo; mkiamua kumuua basi mpigeni dhuruba moja tu, wala msimkatekate.” Aliishi na kufariki dunia tarehe 21 Ramadhan 40 A.H sawa na 661 A.D akiwa na umri wa miaka 63. Kabla hajafariki, aliwaita watoto wake Hasan (a.s.) na Husein (a.s.) na kuwaeleza kuwa jeneza lake libebwe kwa nyuma tu, bali sehemu ya mbele itaelea yenyewe na asiwepo mtu mbele kwa sababu jeneza lenyewe litajiongoza hadi litakaposimama watakuta kaburi tayari limechimbwa! Aliwaeleza watoto wake hao kuwa azikwe kwa siri kwa kuhofia maadui kulichimbua kaburi lake. Jeneza hilo lilisimama sehemu iitwayo Najaf kiasi cha maili 4 toka mjini Kufa. Sehemu hiyo aliyozikwa Imam Ali (a.s.) iliendelea kuwa siri kwa miaka mingi hadi utawala wa khalifa Harun Rashid. Katika kipindi chote cha utawala wa Bani Umayyah, sehemu hiyo ilibakia siri bila kufahamika. Lakini wakati wa utawala wa Bani Abbas chini ya kiongozi (khalifa) wao mmoja bwana Harun al-Rashid mwaka 175 A.H, sawa na (791 A.D.), alipokuwa anawinda sehemu hiyo akawa anawafukuza paa. Wanyama hao wakafika sehemu iliyoinuka kidogo wakasimama hapo. 271


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 272

katika Uislamu

Harun Rashid aliwaamuru mbwa wake wawakamate hao wanyama lakini wakakataa hata kusogelea hapo! Harun akamwelekeza farasi wake kusogelea hapo lakini naye akakataa! Kwa mshangao aliwauliza wenyeji wa hapo kuna nini mahali pale? Mzee mmoja mwenyeji kwa taabu sana akamweleza siri ya hapo kuwa hapo pana kaburi la Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.)! Harun al-Rashid aliamuru kilima hicho kichimbuliwe taratibu mpaka wakaiona alama ya kaburi. Harun ar-Rashid akaamuru sehemu hiyo ijengewe vizuri kwa mara ya kwanza kwa Quba la mawe. Ndipo watu wakaanza kuhamia hapo na kupanua makazi yao hadi ukawa mji mkubwa sana mpaka leo. Rejea: The Shiite Religion - The Shrine of Imam Ali at Najaf - cha Dwight Donaldson; na vilevile Mikesha ya Peshawar - cha Sultanul-Waidhin Shirazi. Je, Imam Ali (a.s.) alikubaliana na ukhalifa wa Abu Bakr, Umar na Uthman? Kuna baadhi ya Waislamu wanaodai kuwa, kwa nini Imam Ali (a.s.) hakuunda jeshi na kupigana ili aupate ukhalifa kwa kadri ya wasia wa mtume (s.a.w.w)? Watu hao wanadai kuwa Imam Ali (a.s.) aliwaunga mkono hao watatu kwa kukaa kwake kimya! Ukweli ni kwamba Imam Ali (a.s.) ambaye ni mmojawapo wa Ahlul-Bayt wa Mtume (Qur’ani 33:33) alishaelezwa yote yatakayotokea, na mwenyewe Mtume (s.a..w.w.). Kwa hiyo kwa kadri ya wasia huo, Imam Ali (a.s.) alitambua kuwa iwapo angeunda jeshi la namna hiyo, kungetokea umwagaji mkubwa wa damu na kudhoofisha au kubomoa kabisa kazi yote aliyoikamilisha Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo Imam Ali (a.s.) pamoja na kwamba alikuwa na wafuasi wake imara, aliamua kuukosa ukhalifa na kuimarisha kazi kubwa ya kujenga Uislamu, aliyoiacha Mtume (s.a.w.w). Na hata kama Imam Ali (a.s.) angeafikiana na uongozi huo, angekuwa anakiuka wasia wa Mtume (s.a.w.w) kwa kadri ya ushahidi niliotangulia 272


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 273

katika Uislamu

kutoa nyuma katika Hadithi za Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo Imam Ali (a.s.) hakutoa kiapo cha utii kwa bwana Abubakar ila baada ya miezi 6 kupita. Imam Ali (a.s.) aliona afanye hivyo baada ya kufariki Bibi Fatima (a.s.) na ilipokuwa watu wamemtenga kabisa Imam Ali (a.s.) ambaye hakutaka mgawanyiko wa Waislamu katika makundi mawili, moja linalomwunga mkono na lingine la wafuasi wa Abu Bakr. Zaidi ya hayo tumeona kuwa njia zilizotumika kuwapa ukhalifa akina Abu Bakr, Umar na Uthman hazikubaliki hata hivi leo katika masuala ya siasa za kidunia, tukiachilia mbali misingi ya Uislamu. Imam Ali (a.s.) ambaye ni lango la elimu ya Mtume (s.a.w.w) asingeonyesha msimamo kama huo wa kuunga mkono uovu, na kwa ushahidi ni kwamba yeye alikuwa mara kwa mara akikumbusha kwamba nafasi hiyo ilikuwa ni yake ambapo Abu Bakr alikuwa ameipora. Abu Bakr Sidiqi na Umar Ibn al-Khattab walijuta pale walipokaribia kufariki!: Tunasoma kwamba bwana, Umar Ibn al-Khattab alipopigwa upanga kabla hajafariki, alijuta na kusema kuwa ‘Ningemiliki dhahabu yote ya dunia, ningeitumia kujikomboa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu kabla sijamwendea!’ Rejea: Sahih al- Bukhari, Jz. 2, uk. 20! Mara nyingine Umar alisikika akijuta kwamba, ‘Afadhali ningekuwa kondoo nikaliwa na watu wa familia yangu. Kabla sijaliwa wangeninenepesha sana na pale watembelewapo na marafiki, wangenichinja na kunibanika na kunila na mwisho wangeenda choo. Bora ningekuwa hivyo kuliko kuwa binadamu ‘ Rejea: (i) Minhajus-Sunnah, cha Ibn Taymiah - Jz. 3, uk .131 (ii) Hil’yat al-Awliya, cha Ibn Abi Nuaym - Jz. 1, uk. 52. Kwa upande wa Abu Bakr tunakuta katika historia kwamba, siku moja alimwangalia ndege aliyekuwa kwenye mti na kusema: “Hongera ewe 273


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 274

katika Uislamu

ndege, unakula matunda na unasimama kwenye miti wala huwajibiki kwa lolote lile au kwa yeyote yule, wala huwezi kuadhibiwa. Natamani ningekuwa mti pembeni mwa njia na ikawa ngamia amepita na kunitafuna kisha akaenda choo. Bora ningekuwa hivyo kuliko kuwa binadamu.” Rejea: (i) Tarikhut-Tabari, uk. 41 (ii) Al-Riyadhun- Nadhira, Jz. 1, uk. 134 (iii) Kanzul-Ummal, Uk. 361 (iv) Minhajus- Sunnah, cha Ibn Tay-miah, Jz. 3, uk. 120 Rejea: Qur’ani 10:62-64, Qur’ani 41: 30 -32 Qur’ani 10:54 na Qur’ani 39:47-48. Aya hizo za Qur’ani zinaongeza mwanga juu ya malipo ya uongofu na upotofu huko Akhera. Abu Bakr Siddiq muda mfupi kabla hajafariki anakaririwa tena akijutia mambo matatu kwa kusema: i. “Afadhali nisingeigusa nyumba ya Ali hata kama Ali na Fatima wangenipiga vita.” ii. “Afadhali siku ya Saqifah Banu Saida ningetoa Bay’at kwa Abu Ubayda au Umar akawa kiongozi na mimi nikawa waziri.” iii. “Ni bora nilipokutana na Dhial-Faja’a as-Sulami akiwa mfungwa wa vita, ningemchinja au kumsamehe badala ya kumchoma moto.” Rejea: Tarikhut- Tabari, Jz. 4, uk. 52; Al- ‘Aqd-al-Farid, Jz. 2, uk. 254; Muruj adh-Dhahabi, Jz. 1, uk. 414. Kwa hiyo tumeona kuwa mabwana Abu Bakr na Umar, walijuta kwa kitendo chao cha kunyakua ukhalifa kinyume na wasia wa Mtume (s.a.w.w) pamoja na vitendo vyao vilivyofuatia hapo. Sasa ni vipi Imam Ali (a.s.) ambaye ni Ma’asum (amelindwa na madhambi) angewaunga mkono na kuwahalalisha! Tutapata maelezo na ushahidi zaidi, kwa nini hatutakiwi kumtii yeyote mtenda madhambi yaani asiyelindwa kutokana na kutenda madhambi. Maelezo hayo yanafuata hapa - Sura ya 15. 274


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 275

katika Uislamu

ULUL AMR NI NANI? (QUR’ANI 4:59) Sasa tukamilishe maelezo juu ya umuhimu wa kuwategemea Viongozi 12 (a.s.) peke yake baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Maelezo haya yanahusiana na Qur’ani:

“Enyi Mlioamini, Mtiini Mwenyezi Mungu na mtiini Mtume na wenye mamlaka katika ninyi (Ulul Amr). Na kama mkihitilafiana juu ya jambo lolote basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume ikiwa mnamwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hilo bora zaidi na lenye mwisho bora zaidi.” (4:59). Nimetangulia kueleza kwamba tafsiri yoyote ya Qur’ani isiyotokana na misingi ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w) siyo sahihi kwa sababu katika hotuba ya Mtume (s.a.w.w) ya Ghadiir Khum, ambayo nimeielezea nyuma, Mtume (s.a.w.w) alituonya juu ya kujaribu kuifasiri Qur’ani bila kumwendea Imam Ali (a.s.) na kupata maana iliyo sahihi, kutokana na ukweli kwamba Qur’ani ina maana iliyo wazi na maana iliyojificha. Hata ile maana ya Aya fulani ambayo inaonekana kuwa wazi, ni lazima tafsiri yake isipingane na Aya nyingine ndani ya Qur’ani. Kwa hiyo anayetaka kufasiri Qur’ani lazima awe na ujuzi wa Aya zote za Qur’ani, mbali na kanuni nyinginezo nilizokwishaelezea; ili kuondoa uwezekano wa tafsiri zinazogongana yaani tafsiri potofu. Nimeeleza pia kwamba kuifasiri Qur’ani kwa misingi ya kanuni za lugha peke yake siyo 275


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 276

katika Uislamu

sahihi ukizingatia kwa mfano Aya ifuatayo:

“Na kila aliye kipofu katika dunia hii, basi atakuwa kipofu (pia) katika akhera; na atakuwa aliyepotea zaidi katika njia (ya haki).” (Qur’ani 17:72). Iwapo aya hiyo itachukuliwa kwa maneno yake yalivyo, hatuwezi kudai kuwa hiyo ndiyo maana yake, hata kama haikushuka kwa sababu maalum! Lakini kwa tafsiri ya kanuni za lugha ya kiarabu, maneno yake yako hivyo! Bali kuhusu maana ya Qur’ani iliyojificha kabisa kama alivyosema Mtume (s.a.w.w.), hiyo tunaipata kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wake tu. Upofu uliotajwa katika Aya hiyo hapo juu sio upofu wa macho, bali ni upofu wa ujinga wa elimu ya dini. Tunapokuta maneno kama ‘Alif Laam-Miiim’ au ‘Yaasin’ n.k ambayo kwa upande wa Sunni hayana tafsiri, haina maana kuwa Mwenyezi Mungu aliweka maneno yasiyokuwa na maana yoyote! Tafsiri yake inapatikana kwa Ahlul-Bayt (a.s.). Natumaini hoja zifuatazo zitafafanua zaidi suala hili la kufasiri Qur’ani. Kwa kuwa tangu mwanzo alipofariki Mtume (s.a.w.w), Imam Ali (a.s.) hakupata uongozi wa Waislamu, ina maana hakuna aliyemwendea kutaka ushauri huo wa tafsiri sahihi isipokuwa wafuasi wake wachache kwa wakati huo. Tatizo lingine katika kufasiri Qur’ani ni kutokuwa na elimu ya historia sahihi ya Uislamu ili kuweza kufahamu sababu za kushuka Aya mbalimbali za Qur’ani katika muda wa miaka 23 ya kushuka Qur’ani. Matokeo yake utakuta baadhi ya mashekhe wanafasiri Qur’ani kwa misingi ya kanuni za lugha ya kiarabu peke yake, bila kuzingatia matukio yanayohusika, pamoja na kuwategemea Ahlul-Bayt kufafanua maana iliyojificha! Kwa hiyo tabia ya Waislamu wengi kubishana kwa kutumia Aya za 276


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 277

katika Uislamu

Qur’ani bila ujuzi huo muhimu, ni jambo la hatari katika dini yetu. Turekebishe kasoro hizi. Tukirejea Aya hiyo ya (Qur’ani 4:59) tunaamrishwa kuwatii Ulul-Amr walio miongoni mwetu. Ndugu zetu mashekhe wa Sunni walio wengi, wanaifasiri Aya hiyo kwa maana ya kumtii kila kiongozi mradi ni Mwislamu! Wengine wanaifasiri kwamba tunatakiwa kuitii serikali yoyote hata kama ni ya kidhalimu! Lakini ipo Aya nyingine inayotuonya tusiwatii madhalimu na watenda madhambi! “Basi ngojea hukumu ya Mola wako wala usimtii miongoni mwao mwenye kufanya madhambi au mwenye kukufuru.” (Qur’ani 76:24) Kwa hiyo Aya ya Ulul-Amr haituamrishi kuwatii watenda madhambi au madhalimu. Kiongozi mmoja mashuhuri (sasa ni marehemu) hapa Afrika Mashariki na mtetezi wa haki za binadamu, aliwahi kualikwa katika sherehe ya Waislamu, ambapo shekhe mmoja maarufu wa Sunni alikuwa anahutubia kwa kufasiri Aya hiyo, kwa maana kwamba ni wajibu kwa Waislamu kuwatii viongozi walio miongoni mwao! Lakini kiongozi huyo mwanasiasa katika kujibu hotuba hiyo, aliuliza kama ni wajibu pia kuwatii hata viongozi madhalimu mradi tu wapo madarakani? Hakuna jibu lolote lililotolewa hapo, kwa sababu hayo ni matokeo ya tafsiri potofu ya Qur’ani! Sababu kubwa ya Mtume (s.a.w.w) kutuamrisha sisi tuwategemee AhlulBayt ni kwamba hao Ahlul-Bayt wamelindwa na dhambi na makosa katika kila watendalo au wasemalo. Msingi mwingine wa kufasiri Aya hiyo ya Qur’ani kwa usahihi ni kuhakikisha kuwa tafsiri yako haipingani na Aya hizi mbili (Qur’ani 4:59) na (Qur’ani 76:24) Ukisoma na kufasiri Aya ya kwanza peke yake utakosea mpaka usome na hiyo Aya ya pili! Sasa turejee kwenye somo letu. Tuanzie kwa Mtume (s.a.w.w.) ambaye tunafahamu kuwa kalindwa na dhambi na makosa. Kama Mtume (s.a.w.w) asingelindwa na dhambi na makosa, sisi waumini tungepata matatizo makubwa, kwa sababu iwapo Mtume angetuamrisha makosa na wakati huo huo Mwenyezi Mungu anat277


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 278

katika Uislamu

uamrisha kumtii Mtume (Qur’ani 4:64), lakini anatukataza pia kuwatii wenye kutenda madhambi, tungejikuta tunamtii ama Mtume au Mwenyezi Mungu na hapo hapo tunamuasi mmoja wao! Na hilo haliwezekani kwa sababu Mwenyezi Mungu na Mtume ni kitu kimoja! (Qur’ani; 53:2-18, Qur’ani 59:7). Kwa hiyo tuna uhakika na amri ya mtu aliyelindwa na dhambi na makosa, yaani ‘Ma’asum’ kwa sababu mtu huyo hawezi kutuamrisha yale ya kumuasi Mwenyezi Mungu. Vinginevyo tukimuasi Mwenyezi Mungu tutakuwa tumeangamia. Bila shaka Mwenyezi Mungu hawezi kutuacha katika utatanishi wa namna hii! Kwa maneno ya Aya hiyo, tunaona kuwa tumeamrishwa kumtii Mtume (s.a.w.w) na waliopewa madaraka. Hao waliopewa madaraka ni wale waliolindwa na dhambi kama Mtume mwenyewe, kwa sababu uongozi wa dini unaendelea hadi Kiyama na haukukusudiwa kuishia pale alipofariki Mtume (s.a.w.w)! Na hiyo ndiyo sababu sisi Shia Ithna’asheri tunawategemea hao viongozi 12 aliowataja Mtume (s.a.w.w) kwa majina kama nilivyoeleza nyuma katika Sura ya Pili. Kwa nyongeza fuatilia mpangilio wa aya hizi na zinavyotafsiriana: “Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuhu na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu. Kizazi cha wao kwa wao, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.” (3:3334); na “Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Mwenyezi Mungu kutokana na fadhila Zake? Basi bila shaka tuliwapa kizazi cha Ibrahim Kitabu na hekima na tukawapa mamlaka makubwa.” (4:54) Waislam wote tunakubaliana kwa pamoja kwamba Muhammad (s.a.w.w.) ni kizazi cha Ibrahim; hivyo kizazi cha Muhammad nacho hata kwa desturi ya kawaida ni kizazi cha Ibrahim, ndio waliopewa Kitabu na mamlaka makubwa! Na katika Tashahudi Sunni wenyewe wanasema: “Ewe Mola mpe rehema na amani Muhammad na kizazi cha Muhammad, kama ulivyompa rehema na amani Ibrahim na kizazi cha Ibrahim. Mbariki Muhammad na kizazi cha Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na kizazi cha Ibrahim juu ya walimwengu, hakika Wewe ndiye mwenye kuhimidiwa!” Sasa rehema na baraka hizi Mtume ameomba kama du’a na 278


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 279

katika Uislamu

kutukumbusha yaliyo kwenye aya hizo, na kutaja Maimam watokanao na kizazi chake mmoja kutokana na mwingine; je, du’a ya Habiba’llah Muhammad (s.a.w.w.) haikukubaliwa mpaka sisi tutilie shaka na kukiepuka kizazi chake na kuona kwamba sio Ulul-Amri halisi? (Mhariri) Waislamu tuwe makini sana tunapojifunza dini kwa sababu wajuzi wa Qur’ani wanatueleza kuwa katika Qur’ani kuna Aya 835 zinazomhimiza binadamu kufikiri na kutafakari. Tusiishie kujidanganya kwamba ‘Jalalain’ inatosheleza kuifahamu Qur’ani na makusudio yake. Mwaka 1998 kulitokea mgogoro wa kidini hapa Tanzania ambapo tuliwasikia mashekhe maarufu wakitoa tafsiri zinazotofautiana kuhusu Aya ya UlulAmr (Qur’ani 4:59)! Kama ‘Jalalain’ inatosha, hao mashekhe kwa nini watofautiane? Au walifanya hivyo kwa makusudi? Utiifu unaoelezewa katika Aya hiyo ni utiifu usiopingana na sheria za Mwenyezi Mungu. Kwa vyovyote mtu asiye Ma’asum, yaani asiyelindwa na dhambi na makosa, hata kama ni mchamungu kiasi gani, hawezi kuhukumu kwa haki kutokana na kutoongozwa na Allah.1 Nitaeleza kisa kimoja ambacho kitatupanua mawazo zaidi. Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchagua bwana Walid Ibn Aqbah kwenda kwa Bani Mustalaq kukusanya Zaka. Watu hao kabla ya kuingia Uislamu walikuwa na uhasama na huyo Walid Ibn Aqbah. Lakini baada ya bwana huyo kuingia Uislamu walimwona kuwa ni ndugu yao. Kwa hiyo siku hiyo alipofika kwao walitoka kumpokea lakini yeye aliwatilia shaka akihofia uhasama wa zamani kati yake na wao. Hivyo bila kuwepo uchokozi wowote aliamua kurejea kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumdanganya kuwa watu hao (kabila hilo) wameritadi (wamerejea katika ukafiri)! Huko 1 Kuna tofauti kati ya Wenye mamlaka na waliopewa mamlaka. Viongozi wetu wa kidunia tunawapa sisi wenyewe mamlaka kwa kura zetu, na tunaweza kuwauzulu kwa kutoridhika nao. Wale Wenye mamlaka hatuna uwezo wa madaraka juu yao, kwani wameteuliwa na kuongozwa na Mola Mwenyewe, na mtu hatawaona na kasoro, ila mwenye kukufuru. 279


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 280

katika Uislamu

Madina, Mtume (s.a.w.w), akiongozwa na Mwenyezi Mungu alitambua kuwa madai hayo ni ya uongo na ni kashifa dhidi ya watu hao. Hapo ndipo ikashuka Qur’ani 49:6:

“Enyi mlioamini! Pindi anapowajieni fasiki na habari yoyote ile, basi ichunguzeni kwa makini, msije mkawadhuru watu katika (hali ya) ujinga, na kisha mkajijutia kwa mliyoyatenda.” (Qur’ani 49:6). Huyo Walid Ibn Aqbah alikuwa mtu mwenye vitendo vya kumtilia shaka katika tabia yake kwa sababu kitendo chake hicho kiovu kingesababisha Mtume (s.a.w.w) kuwachukulia hatua kali watu hao ki-Shariah, iwapo Mtume (s.a.w.w) angekuwa haongozwi na Mwenyezi Mungu. Nina maana kwamba sifa za uongozi kama wa Mtume (s.a.w.w) zilitakiwa awe nazo mrithi wake ili haki iendelee kuwepo katika kuwaongoza Waislamu hadi Kiyama. Tukiendelea na maelezo juu ya Walid Ibn Aqbah ni kwamba baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), katika utawala wa Uthman Ibn Affan, Uthman alimchagua huyo Walid kuwa gavana wa Kufa huko Iraq. Hapo ndipo Walid alipoonyesha unafiki na uovu wake. Siku moja huyo Walid akiwa ndiye kiongozi mkuu wa juu hapo mjini Kufa, alikuwa pia moja kwa moja ndiye ‘Imam’ wa Swala. Siku moja ilipoingia swala ya asubuhi alifika msikitini akiwa amelewa pombe na kuswalisha Swala ya Subhi kwa rakaa nne badala ya rakaa mbili! Na hapo alipomaliza kuswalisha aliwageukia watu na kuwauliza, “Je, mnataka niwaongeze zaidi?” Habari hizo zilimfikia Uthman ambaye alimtaka Imam Ali (a.s.) atoe ushauri juu ya tatizo hilo na ikawa Walid ameondolewa madarakani. Je, vipi mtu kama huyo awe kiongozi wa waumini? Na kwa nini Uthman atafute ushauri kutoka kwa Imam Ali (a.s.)?

280


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 281

katika Uislamu

Kutokana na tukio hilo tutaona kuwa, kama Uthman angekuwa anaongozwa na Mwenyezi Mungu, yaani kama angekuwa Ma’asum, asingempa ugavana huyo dhalimu Walid Ibn Aqbah. Katika kipindi cha uongozi wa Imam Ali (a.s.) kihistoria, hapakuwepo gavana yeyote aliyelalamikiwa na raia kwa matendo ya uovu. Huwezi kutenganisha Uislamu na haki na uadilifu. Pale ambapo Uislamu hauambatani na haki, basi ina maana kwamba viongozi wake sio waadilifu na huo sio Uislamu bali ni utawala tu wa kidunia usiozingatia kanuni za Mwenyezi Mungu. Tukio hilo ni fundisho lingine kwetu kwamba siyo kila sahaba alikuwa mwadilifu. Huyo Walid alikuwa sahaba wa Mtume (s.a.w.w) kama tulivyoona. Lakini pamoja na usahaba wake huo, Qur’ani 49:6 inamtaja kuwa mtu mwovu, fasiki. Tunataka ushahidi gani zaidi, enyi Waislamu wenye kufikiri! Kuna tukio lingine kuhusu umuhimu wa Waislamu kuongozwa na viongozi ambao wamelindwa na dhambi na wanaoongozwa na Mwenyezi Mungu. Siku moja mtu mmoja alimzawadia Mtume (s.a.w.w) sarafu 300 za dhahabu. Mtume alikabidhi sarafu hizo kwa Imam Ali (a.s.) kama zawadi. Imam Ali naye aliamua kuzitoa zawadi katika mafungu matatu ya sarafu 100 kila moja. Siku ya kwanza, mara Imam Ali (a.s.) alipomaliza Swala yake ya jioni akielekea nyumbani, alikutana na kahaba mmoja na akampa sarafu 100 za kwanza! Siku iliyofuata, mji mzima watu walikuwa wanamsengenya na kumlalamikia Imam Ali (a.s.) kwa nini alichezea sadaka hiyo kumpa mwanamke mwovu! Usiku wa pili, akiwa njiani kuelekea nyumbani, Imam Ali (a.s.) alikutana na mtu ambaye ni mwizi na akampa sarafu 100 za dhahabu! Kesho yake watu wakazidi kulalamika kwa nini apewe pesa hizo mtu asiye na faida yoyote. Usiku wa tatu, Imam Ali (a.s.) akiwa njiani toka msikitini, alikutana na tajiri mmoja na akampa sarafu 100 za mwisho! Kesho yake mji mzima, watu walisikika wakilaumu kwa nini Imam Ali (a.s.) amepoteza pesa kumpa huyo tajiri bakhili. 281


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 282

katika Uislamu

Imam Ali (a.s.) alimwendea Mtume (s.a.w.w) na kumwelezea yote yaliyotokea. Mtume (s.a.w.w) alimwambia Imam Ali (a.s.) kwamba: “Malaika Jibril ameniletea habari kwamba Mwenyezi Mungu ameridhika na jinsi alivyotumia sarafu hizo kwa sababu yule kahaba alipopata sarafu hizo aliacha ukahaba na kuanza kuendesha maisha ya heshima. Yule mwizi ameacha wizi na kuanza biashara halali. Yule tajiri bakhili ameona aibu kwamba alipokea sadaka toka kwa mtu fukara kama wewe, na kwa hiyo ameamua kuacha kuhodhi utajiri na ametoa kila alichonacho kwa mafakiri!” Kwa hiyo hapa tunaona kuwa watu hawakuridhika na matukio hayo ya Imam Ali (a.s.) lakini Mwenyezi Mungu ndiye aliyemwongoza kufanya hivyo bila hata yeye kujua! Huko ndiko kuongozwa na Mwenyezi Mungu tunakosisitiza. Zaidi ya hayo, tunaelezwa katika historia jinsi ambavyo Imam Ali (a.s.) alivyoishi maisha ya ufukara japo alikuwa na uwezo wa kutumia chochote atakavyo toka Hazina (Baitul Maal). Alisikika akihutubia watu kuwa: “Mtu akifa utasikia nduguze wanauliza kaacha nini wakati ambapo Malaika huangalia alitoa nini katika sadaka au njia ya Mwenyezi Mungu.” Hata alipokuwa khalifa, alichukia ufahari na majivuno kiasi kwamba alionekana akifagia nyumba yake ya kibanda cha udongo. Alipasua kuni, alichota maji, alishona viatu vyake, alifua nguo zake, alikamua mbuzi wake na alionekana akitembea bila viatu. Mke wake naye aliishi hivyo hivyo akisaga nafaka, kuoka mikate, kuosha vyombo na kuwatunza watoto. Imam Ali (a.s.) alijisikia vibaya alipopanda farasi na kuona raia wanamfuata nyuma. Alikuwa anawauliza wanataka nini? Nao hujibu kuwa wanafurahi kuongozana naye. Kisha huwaambia warejee kwenye shughuli zao kwa sababu kutembea nyuma ya mpanda farasi ni kumtia majivuno, na wao kujiona dhalili kwake. Hapa tumeona kuwa uadilifu unaotokana na kuongozwa na Mwenyezi Mungu, ni wa hali ya juu sana na ndio unaotaki282


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 283

katika Uislamu

wa katika sifa za kiongozi katika Uislamu asilia. Rejea: Sautu’l Adalati’l Insaniyah (The Voice of Human Justice) Toleo la kiingereza la George Jordac - Lebanon – Syria, kilichotafsiriwa kwa Kiswahili kwa jina la ‘Sauti ya Uadilifu wa Mwanadamu’. Kwa hiyo ndugu Waislamu tusiweke mapenzi yetu mbele, lakini maneno ya Mtume na Mwenyezi Mungu tukayaweka nyuma. Na wala tusijiambatanishe na matendo yasiyo na msingi wowote wa kidini kwa sababu tu eti tuliyarithi kwa wazee wetu au yanatendwa na walio wengi kwa miaka mingi! Dini ya kiislamu siyo utamaduni, bali ni mwongozo wa kudumu wa Mwenyezi Mungu, na kwa kweli mwongozo huo haubadiliki kamwe. Mabadiliko ni kazi yetu binadamu. Na hiyo ndiyo sababu Mtume (s.a.w.w) alisema kuwa: “Mimi nimeitwa na Mwenyezi Mungu na nimeitika mwito huo. Nawaachia vitu viwili vya thamani navyo ni Qur’ani na kizazi (AhlulBayt) changu kutokana na familia yangu. Vitu hivi viwili havitaachana mpaka vinifikie katika kisima cha Kawthar peponi.” Rejea: Ghayat al-Maram, uk 336. Hadihti 6 za Sunni na Hadithi 15 za Shia zimetajwa humo. Al- Bidaya wan– Nihaya, Jz. 5, uk. 208 na Jz. 7 uk 346. Dhakhair al-Uqba, uk. 67 Al-Fusul al-Muhimmah, Jz. 2, uk. 23 Khasais, uk. 31. Mfano mwingine wa kufasiri vibaya Qur’ani: Mfano mwingine wa kufasiri vibaya Qur’ani ni kuhusiana na Qur’ani 17:71, ambapo tunafundishwa kuwa:

“Siku tutakapowaita kila watu pamoja na Imam wao; na kila atakayepewa kitabu chake kwa mkono wa kulia, hao watasoma vitabu vyao wala hawatadhulimiwa hata kidogo.” (Qur’ani 17:71). 283


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 284

katika Uislamu

Tukiunganisha Aya hiyo na maswali anayoulizwa mtu kaburini ‘Talqin’ tutaona kuwa maswali hayo ni pamoja na: Ni nani Imam wako? Baadhi ya mashekhe wa Sunni wanafundisha kuwa jibu la swali hilo ni: “Imam wangu ni Qur’ani!” Wengineo hudai kuwa Imam wako ni yule anayekuongoza msikitini katika Swala ya jamaa! Iwapo jibu sahihi ni Qur’ani ni jambo ambalo haliwezekani kwa sababu kwenye Talqin kuna swali lingine la: Ni kipi kitabu chako? Swali hilo jibu lake sahihi ni Qur’ani. Jibu la kwamba: Imam ni kiongozi wa Swala, haliwezi kuwa sahihi kwa sababu Waislamu wengine hawajawahi kuingia msikitini kuswali hadi kufariki kwao! Hata hivyo zipo Aya nyingine zinazofafanua kwamba kuna Imam anayeongoza watu kwenda motoni (Qur’ani 28:41) na Imam anayeongoza watu kwenda Peponi (Qur’ani 32:24). Iliposhuka Aya hiyo, (Qur’ani 17:71) watu walimwuliza Mtume (s.a.w.w) kama yeye si ndiye Imam wa watu wote? Aliwajibu kuwa, “Ndiyo, mimi ni Imam mpaka mwisho wa uhai wangu duniani, na baada ya hapo Imam atakuwa Ali akifuatiwa na kizazi chake (Maimamu 11). Watu watakaojiambatanisha na viongozi hao watapata wokovu Siku ya Kiyama. Na wale watakaojitenga nao, wataangamia.” Kwa hiyo kwa kuwa lengo la Talqin ni kupima imani ya mtu kama ni sahihi, jibu sahihi ni kutaja mmojawapo wa Maimam 12 (as.) kwa kadri ya Imam wa wakati wa uhai wake mtu. Kama utamtaja kiongozi aliyekupoteza, kuwa ndiye Imam wako, haitakusaidia kitu kwa sababu anakaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa: “Atakayefariki bila kutambua Imam wa zama zake, atakuwa amekufa kifo cha kijinga (Jahiliyyah) yaani kifo cha kikafiri.” Rejea: (i) Musnad at-Tayalis - uk. 259 (ii) Sahih Muslim - Jz. 6, uk. 22 (iii) Musnad Ahmad Ibn Hambal, Jz. 4, Uk. 96 (iv) Sunan al-Kubra al-Bayhaqi, Jz. 8, uk. 156 (v) Tafsir Ibn Kathir, Jz. 1, uk. 517. (vi) Majma’uz – Zawaaid, Jz. 5, uk. 218, 224/5 284


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 285

katika Uislamu

Kwa maelezo zaidi juu ya Imam aliyekusudiwa katika maelezo yote haya, rejea pia Sura ya 2 chini ya: ‘Imam Mahdi (a.s.) katika kasri ya khalifa Mutamid.’ Kwa hiyo ndugu Mwislamu, kama utazingatia mafunzo yaliyomo katika maelezo niliyotoa kuhusu somo hili, utaona kuwa suala la Waislamu kuongozwa na Maimamu (as.) wanaotokana na kizazi cha Mtume (s.a.w.w) baada ya yeye Mtume (s.a.w.w) kufariki, ni itikadi sahihi. Ni juu yetu kuwapokea au kuwakataa kama walivyokataliwa na hao waliotutangulia, kwa tamaa na ufahari wa dunia. Suala la sisi Shia Ithna’asheri kuwategemea Maimamu kama viongozi wetu halali katika dini, lina ushahidi wa kutosha kielimu na siyo itikadi zilizojengeka katika mapenzi ya nafsi au imani za kinadharia potofu. Waislamu wenye kufikiri wanakubaliana na hoja hizo nilizotoa lakini wanauliza kwamba mbona leo hii hao Maimamu 12 (a.s.) hawapo tena? Sisi Waislamu wa wakati huu tutamtaja nani kama Imamu wetu? Tukirejea Sura ya pili nyuma kabisa mwa kitabu hiki, chini ya ‘Utoto na Ujana wa Imam Mahdi (a.s.)’, tutakuta maelezo ya kutosha juu ya suala hili. Kwa hiyo Imam wetu wa sasa hivi hadi Siku ya Kiyama ni Imam Mahdi (a.s.) ambaye amefichwa na Mwenyezi Mungu machoni pa watu lakini yupo hai hapa hapa duniani na kuna matukio kadhaa ambapo watu fulani walipata bahati ya kumwona kama muujiza! Hata hivyo mojawapo ya dalili za kukaribia Siku ya Kiyama ni kudhihirika Imam Mahdi (a.s.) wazi wazi. Jambo la maana ni kwamba kazi ya Imam Mahdi (a.s.) ni kuilinda dini ya Mwenyezi Mungu isifutike kabisa hata kama upotofu zaidi utaongozeka. Matukio yafuatayo yatasaidia kudhihirisha kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.). Kwamba ingawa hatumwoni, lakini anatusaidia katika shida:

285


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 286

katika Uislamu

Tukio la kwanza: Imam Ali (a.s.) alizikwa mji wa Najaf, kama nilivyoeleza kabla. Kiasi cha maili 100 kutoka hapo, pana kituo muhimu sana cha elimu cha Shia. Zamani hizo alikuwepo Mujtahid (kiongozi wa juu kabisa na mjuzi sana katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri) ambaye aliishi hapo jina lake Allama Hilli. Siku moja watu walimwendea kumwuliza juu ya mazishi ya mwanamke mja mzito aliyefariki dunia akiwa na mimba ya mtoto aliye hai tumboni. Watu walitaka kujua kama wamzike na mimba yake au wampasue wamtoe mtoto? Huyo Mujitahidi aliwashauri wamzike hivyo bila kumpasua. Baada ya kumwosha na kumkafini maiti, walibeba jeneza kuelekea mazikoni. Njiani wakamkuta mtu mmoja aliyepanda farasi akawazuia na kuwaeleza kuwa huyo Mujitahid wao amebadilisha uamuzi wake na kwa hiyo ameagiza huyo marehemu apasuliwe na mtoto atolewe kwanza ndipo wamzike. Kisha huyo mpanda farasi akatoweka. Baada ya kupita miaka miwili au mitatu hivi, huyo Mujitahid alitembelewa na mtu mmoja akiongozana na mtoto mdogo (yule aliyetolewa tumboni mwa marehemu). Huyo mtu alimwuliza Mujitahid, ‘Je unamjua huyu mtoto? Huyu ni mtoto ambaye uliamuru atolewe tumboni mwa marehemu mama yake. Wewe kwanza ulishauri kwamba mama yake azikwe vilevile lakini baadaye ukamtuma mtu kubadili uamuzi wako. Mujitahid alishangaa kusikia hayo na uso wake ukageuka alipokumbuka kuwa hakuwahi kabisa kutuma mtu yeyote kubadili uamuzi wake! Moja kwa moja alitambua kuwa Imam Mahdi (a.s.) ndiye aliyemwokoa mtoto huyo, vinginevyo alijiona kuwa angekabiliwa na kosa kubwa la kuamuru kumzika mtu hai! Kuanzia siku hiyo akaamua kujifungia ndani kwake na kutotoa tena ‘fatwa’ za kidini, asije akarudia makosa! Baada ya muda mfupi alipokea barua toka kwa Imam Mahdi (a.s.) akimweleza kwamba asijali mambo yaliyopita na aendelee kuwaongoza waumini, na iwapo atakosea, Imam anaelewa yote yanayotokea na atakuja kumsaidia 286


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 287

katika Uislamu

kwa sababu huwasaidia wafuasi wake (Shia) wanapohitaji msaada wake. Rejea: Imam Zaman Hadhrat Mahdi (a.s.) - cha Mulla Muhammad Jaffer Sherif Dewji. Bilal Muslim Mission, Dar es salaam. 1991 A.D. Tukio la pili: Imenakiliwa katika kitabu cha Biharul Anwar kwamba katika enzi za utawala wa kiingereza, watu wote wa Bahrain walikuwa Waislamu. Ingawa wakati huo Waislamu walio wengi walikuwa Shia, alichaguliwa gavana wa madhehebu ya Sunni kuwa kiongozi wa nchi hiyo. Gavana huyo na waziri wake walikuwa na uadui kwa Shia. Siku moja waziri alimzawadia matunda ya komamanga ambayo yaliandikwa majina ya Makhalifa wanne (Al-Khulafau Rashidun) wa kiislamu, na ikadaiwa kuwa huo ni muujiza wa kuonyesha kuwa madhehebu sahihi ni Sunni. Waziri huyo alimshawishi gavana kuwaita wanazuoni wa Kishia kuthibitisha muujiza huo, ili waache madhehebu ya Shia na itikadi zake, wawe Sunni! Waziri huyo akasisitiza kuwa Shia wasipokubali muujiza huo wauawe au watozwe kodi (Jiziya) kama makafiri! Gavana aligeuza hilo tunda na kuona maandishi ya, ‘Laillaha Illa Allah, Muhammadun Rasulu’llah, Abubakar, Umar, Uthman, Ali Khulafau Rasulu’llah.’ Gavana huyo aliamini na kukubaliana na ushauri wa waziri wake. Kwa hiyo aliwaita wanazuoni wa Kishia akawaonyesha tunda hilo na kuwapa hiari tatu kama alivyoshauriwa na waziri wake. Wanazuoni hao wa Kishia walistaajabu sana lakini wakaomba muda wa siku tatu kwa gavana. Gavana alikubali na ikawa wameondoka. Wanazuoni hao wa Kishia waliamua kuomba msaada kwa Imam Mahdi (a.s.). Walichaguliwa wanazuoni wacha-Mungu watatu na ikaamuliwa kila mmoja wao kila siku atoke nje ya jiji na kwenda kumwomba msaada Imam Mahdi (a.s.). Siku mbili za kwanza wanazuoni wawili wakakesha kuswali na kumwomba Mungu awapatie msaada wa Imam lakini bila mafanikio. Usiku wa tatu mwanazuoni wa tatu akatoka nje ya mji kuomba kwa bidii 287


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 288

katika Uislamu

mno ili apate msaada wa Imam Mahdi (a.s.). Mnamo alfajiri, mwanazuoni huyo alimwona mtu mwenye haiba ambaye alijitambulisha kwamba ni Imam wake! Huyo mtu akamwuliza mwanachuoni shida yake. Mwanachuoni akajibu kuwa, iwapo kweli huyo mtu ndiye Imam wake, basi bila shaka anaelewa tatizo linalomkabili. Imam Mahdi (a.s.) akajibu kuwa ana habari kamili kuhusu balaa lililowapata wafuasi wake lakini wasikate tamaa bali wafuate maagizo yake. Imam akamwambia huyo mwanazuoni kwamba, “Kesho asubuhi wewe na mwenzako mwende kwenye kasri (ikulu) ya gavana na mkamwambie kuwa mtampatia jibu nyumbani kwa waziri. Waziri atakataa jibu hilo lakini lazima msisitize hivyo na mhakikishe kwamba waziri hafiki nyumbani kabla ya ninyi kufika. Mwende nyumbani kwa waziri mkifuatana pamoja naye. Waziri atababaika sana na atajitahidi kutangulia lakini ninyi mkamzuie kutangulia au kufika kabla hamjafika kwake. Huko ghorofani kwake mtaona mfuko katika kishubaka ukutani. Fungueni huo mfuko na mumwonyeshe gavana vitu vilivyomo. Humo ndani mtakuta ‘kalibu’ ambayo juu yake mtaona maandishi yaliyotokeza juu ya komamanga. Hizo ni kalibu zilizovishwa na waziri juu ya makomamanga yalipoanza kuota, na yalipokomaa, maandishi hayo yalizidi kuimarika. Gavana akiona hayo atakubali kuwa jambo hilo lilikuwa ni ulaghai wa waziri na halina ukweli wowote! Kisha mumwambie gavana kwamba kuna ushahidi mwingine kuhusu ulaghai huo. Mwombeni gavana amwamrishe huyo waziri wake avunje hilo tunda mbele yenu.” Asubuhi iliyofuata, huyo mwanazuoni (Muhammad Ibn Ali) akaenda kwa gavana akiwa na wenzake. Walimwomba wafuatane naye hadi nyumbani kwa waziri pamoja naye waziri mwenyewe. Mwisho wa yote gavana akamwamuru waziri avunje hilo tunda. Alipovunja ikawa vumbi jeusi limetoka na kuingia machoni na kwenye ndevu za huyo waziri. Hapo kila mtu akacheka! Gavana aliridhika kuwa suala zima lilikuwa ni ulaghai mtupu na akaamuru waziri huyo auawe! Wanazuoni wa Kishia wakaondoka hapo kwa heshima zote na ushindi. Rejea ni ile ile ya nyuma. 288


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 289

katika Uislamu

Na hiyo mifano ni baadhi tu ya ukweli kwamba Imam Mahdi (as.) haonekani lakini anaongoza na kulinda Dini ya Mwenyezi Mungu, na yuko hai hapa hapa duniani mpaka atakapodhihiri kwa amri ya Allah. Kama nilivyoeleza huko nyuma chini ya “Utoto na Ujana wa Imam Mahdi (a.s.)”, ni kwamba Imam Mahdi (a.s.) yuko hai na mpaka leo hii bado inatokea miujiza mingi hapo Samarra mahali alipozaliwa! Wakazi wengi wa Sammara ni Masunni na wanaamini kuwepo hai kwa Imam Mahdi (a.s.) na wala siyo Imani ya Shia peke yetu. Kughibu kwa Imam Mahdi (a.s.): Mnamo tarehe 10 Shawwal, 260 A.H, (sawa na 881 A.D), Imam Mahdi (a.s.) alighibu ghaibat ndogo, kwa maana kwamba walikuwepo wawakilishi wake maalum, ambao kazi yao ilikuwa ni kuleta au kupeleka ujumbe kwa waumini, badala ya waumini kumwona Imam moja kwa moja. Baada ya hapo Imam Mahdi (a.s.) alifichwa na Mwenyezi Mungu moja kwa moja mpaka leo. Pamoja na mifano niliyoeleza hapo juu, kuhusu jinsi Imam Mahdi (a.s.) anavyosaidia na kuongoza waumini wafuasi wake, napenda kuongeza kuwa si lazima tuwe tunamwona Imam Mahdi (a.s.) ndio tupate msaada wake. Kuna vitu vingi tusivyoviona lakini vinatusaidia hata uhai wetu kama vile hewa ya ‘Oksijeni’ hatuioni lakini tunaitegemea sana ili tuishi! Inawezekana jua likafunikwa na mawingu kutwa nzima, lakini mimea inanufaika na hali ya usanidimwanga (Photosynthesis), na pia mwanga wake upo unatusaidia bila jua kuonekana! Bakteria na virusi hawaonekani lakini wanatuletea maradhi. Tunamlilia na kumwomba msaada Mwenyezi Mungu, naye haonekani bali yupo na tunamtegemea na anatusaidia lakini hatumwoni! Upepo upo lakini hatuuoni! Dunia daima inazunguka kilomita ishirini na saba kwa dakika lakini hatuioni kuyumba. Lakini kwa upande mwingine hatutegemei Imam wa wakati huu (Imam Mahdi a.s) kutatua matatizo ya kila siku ya waumini. Kwa hiyo kabla ya Imam Mahdi (a.s.) kughibu (kufichwa) ghaibat kubwa, aliwafahamisha 289


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 290

katika Uislamu

wawakilishi wake kwamba kuanzia wakati huo (tarehe 10 Shawwal 329 A.H, sawa na 1050A.D), wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.), watamchagua mmoja wao mwenye elimu kubwa, ucha-Mungu na ujuzi wa misingi yote ya dini, awe kiongozi wao na wamtegemee kutoa fatwa na wazifuate hukumu hizo. Ndiyo maana sisi Shia Ithna’asheri tunamtegemea kiongozi mmoja wa juu aitwaye Mujitahid. Elimu peke yake ya Mujitahid ni kubwa mno kiasi kwamba huwezi kuipima kwa Stashahada (Diploma), Shahada (Digrii) au Shahada ya juu (PhD). Na wala elimu siyo kigezo pekee cha kumchagua Mujitahid! Ni lazima awe na tabia (akhlaq) njema na uadilifu wa hali ya juu. Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri, ni lazima kwa chini kabisa, Mujitahid awe na elimu zifuatazo: Ilmul Adab - Elimu ya fasihi Ilmul Lughah - Elimu ya lugha Ilmun-Nahw - Elimu ya Nahau (Syntax) Ilmul M’ani - Elimu ya utambuzi Ilmul Akhlaq - Elimu ya maadili Ilmul Faraidh - Sheria za mirathi Ilmul fiqh - Elimu ya Shari’ah (Fiqihi) Ilmul Ahadith - Elimu ya Hadithi Ilmur- Rijaal - Utambuzi wa wasifu wa wapokezi wa Hadithi lmul Usul - Misingi ya Shari’ah ya kiislamu Ilmul Qiraa - Elimu ya visomo vya Qur’ani Ilmul Kalaam - Elimu ya Theolojia Ilmul Ilahiyat - Elimu ya Theolojia Ilmul Mantiq - Elimu ya Mantiki Ilmut-Tawarikh - Elimu ya Historia (Taarikh) Ilmus- Sarf - Elimu ya Sarufi Ilmut- Tafsir- Elimu ya Tafsir ya Qur’ani Tukufu.

290


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 291

katika Uislamu

Zaidi ya hayo kila Mujitahid, hata kama hajachaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa mataifa au taifa, ni lazima awe na kitabu chake cha uchambuzi wa hukumu zote za dini kuhusu maeneo yote ya maisha ya Mwislamu. Lazima awe ameandika hukumu zote za ibada, biashara, mikataba n.k. Hata hukumu ya jirani yako aliyepanda mti ikawa mizizi ya mti huo imeingia kwako na kuleta madhara, utaikuta! Kwa kawaida, kutokana na ujuzi wao mkubwa, Mujitahid wote hukumu zao hazitofautiani katika mambo ya ‘Wajib’ Isipokuwa linapotokea tatizo jipya miongoni mwa Waislamu, ndipo kuna uwezekano mdogo kutokea tofauti. Hata hivyo hakujawahi kutokea tofauti kiasi cha Shia kugawanyika kama Sunni au kufarakana. Umuhimu wa Mujitahid kuwa na ujuzi wa ‘Shariah’ zote, ni kwamba yeye ndiye mwenye jukumu la kuhukumu kesi zote za waumini badala ya kwenda mahakama za kidunia. Zaidi ya hayo, itikadi ya Shia ni kwamba hata baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w), Uislamu unaendelea kuwaongoza Waislamu kwa misingi ya haki na uadilifu, chini ya viongozi wajuzi ili kuzuia uwezekano wa dhuluma na uonevu. Iwapo hukumu (Shariah) zitasimamiwa (zitatolewa) na watu wasio na ujuzi muhimu wa kutosha, haki haiwezi kutendeka. Katika hali hiyo, maana halisi ya uongozi wa kiislamu haitakuwepo. Zaidi ya hayo tusichukulie dini kwamba kila mtu anao uwezo wa kuielewa na kujitegemea katika kufikia maamuzi mbalimbali ya kumtii Mwenyezi Mungu. Tutambue kuwa hapa duniani kuna wajuzi mbalimbali tunaowategemea katika maisha yetu ya kila siku kutatua matatizo yetu. Kwa mfano kama nilivyotangulia kuelezea katika ‘Dibaji’ yangu kwamba, tukiugua tunamwendea daktari na tunapopewa dawa tunalazimika kutii masharti ya matumizi yake. Hivyo hivyo tunawaendea wanasheria au wanasiasa au wahandisi ili watusaidie kutatua yale tusiyokuwa na ujuzi nayo. Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri tunayo itikadi inayomtaka kila muumini kuhakikisha kuwa ameweka nia ya kumfuata Mujitahid fulani katika hukumu zote za dini. Mujitahid huyo lazima awe hai. Kinyume na 291


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 292

katika Uislamu

hivyo inachukuliwa kuwa Uislamu wa mtu haujakamilika kwa sababu ni sawa na mtu asiyejua sheria, kujaribu kujitegemea mahakamani bila ujuzi wowote na matokeo yake ni uwezekano mkubwa wa mtu huyo kushindwa kesi. Iwapo mimi si daktari wa upasuaji vipi nitamfanyia upasuaji mtoto wangu anayeumwa tumbo? Nitajuaje kama tatizo lake ni la upasuaji bila msaada wa daktari? Kwa makusudio ya Mwenyezi Mungu kwamba Uislamu uongoze binadamu hadi Kiyama, Mujitahid ni naibu wa Imam wa 12 (a.s.) kama nilivyoeleza nyuma, ili kuhakikisha kuwa uongozi huo muhimu uliokusudiwa, unaendelea hadi Kiyama kwa sisi Shia wafuasi wa AhlulBayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.). Kitendo cha kumfuata Mujitahid kinaitwa ‘Taqlid’ na ni wajibu. Kwa hiyo tutaona kuwa tabia ya viongozi mbalimbali wasio na ujuzi muhimu wa dini, kutoa ‘Fatwa’ mbalimbali za kidini ni jambo la hatari kwao na kwa Waislamu. Dini siyo tu kuamini kuwa Mungu yupo, kuswali Swala tano n.k, bali kuna mambo mengi zaidi ya kuzingatia. Namalizia hoja hii nikisisitiza kuwa: Dini ni taaluma na siyo kufuata bila mantiki na hoja - Dogma. Taaluma zote duniani zinaongozwa na wasomi waliothibitishwa ujuzi wao katika fani mbalimbali. Kitendo cha kila Mwislamu kujidai anaielewa dini na kujitolea hukumu zake au kujiamulia msimamo wake kidini siyo sahihi. Mwenyezi Mungu aliyeumba vitu vyote kwa hekima kubwa kama tuonavyo katika ugunduzi wa kisayansi, hawezi kutuletea dini isiyokuwa na kanuni maalumu kwa waumini wote wanaomtambua Muumba wao! Yeyote anayeichukulia dini kijuujuu bila kuzama na kutafakari, yampasa arekebishe mtazamo wake huo. Lazima dini iongozwe na viongozi halali wenye ujuzi uliothibitika; na siyo baadhi yetu kujipachika vyeo vikubwa vya dini bila ujuzi wala uadilifu au kuchaguliwa na watu kwa kura za kawaida.

292


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 293

katika Uislamu

Dalili za kujitokeza Imam Mahdi (a.s.): Dalili za kujitokeza Imam Mahdi (a.s.) zilishaelezwa miaka 1400 iliyopita kama ifuatavyo: (Baadhi yake): 1. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa, “Masikitiko juu ya vijana wenye manywele marefu wa Magharibi, ambao watapata riziki zao kwa kucheza muziki na kuimba na kuwaathiri watu wenye maadili mabovu wa Mashariki na Magharibi.” Katika Hadithi hii, Mtume (s.a.w.w.) alitabiri vijana ambao sasa hivi si wengine bali ni wacheza muziki wa ‘Reagae’ na marasta yao, na wa HiPop. Na athari zao zinaonekana! Rejea: Rabi-ul-Abrar, cha Allama Zamakhshari. 2. Imam Musa Ibn Jafar (Imam wa 7) (a.s.) anakaririwa akisema kuwa, mojawapo ya dalili za kudhihiri Imam Mahdi (a.s.) ni wakati ambapo watu watabeba mifukoni vyombo vya miziki na kwamba uchezaji wa muziki utajipenyeza Makkah na Madina! Wakati Imam huyo wa 7 akiwa hai, ni miaka ya 800 A.D muda ambao hata wazo la redio lilikuwa ni ndoto ya mbali sana! Leo hii ndiyo tunaona watu wakibeba mifukoni vyombo kama hivyo vilivyotabiriwa zaidi ya miaka 1100 iliyopita! Kuhusu muziki kujipenyeza Makkah na Madina maana yake ni miziki inayosikilizwa toka vituo vya redio na televisheni vilivyoenea nchi za kiarabu. Rejea: Biharul-Anwar 3. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa, “Mojawapo ya dalili za kudhihiri Imam Mahdi (a.s.) ni uvumbuzi wa vyombo vyenye uwezo wa kufanya kazi badala ya binadamu.” Bila shaka utabiri huo una maana ya Kompyuta na roboti na mashine nyingi zinazotumika dunia nzima katika fani mbali mbali! Rejea: Rabi-ul-Abrar, cha Zamakhshari 4. lango la elimu ya Mtume (s.a.w.w) yaani Imam Ali (a.s.) akisema kuwa, 293


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 294

katika Uislamu

“Mojawapo ya dalili za kujitokeza Imam Mahdi (a.s.) ni kwamba India itadhurika kwa ajili ya Tibet na Tibet nayo itadhurika na China.” Imam Ali (a.s.) aliishi miaka ya 661 A.D yaani miaka 1337 iliyopita. Utabiri huo umekamilika! Rejea: Manaqib - ya Ibn Shehr Ashob (aliyefariki 1309 A.D). Kwa hiyo tutaona kuwa baadhi ya utabiri huo, ulitolewa karne 14 zilizopita, wakati ambapo waandishi wa vitabu nilivyovitaja waliishi miaka zaidi ya 600 iliyopita wakati ambapo haya yote yaliyotajwa hayakuwepo! Kwa hiyo asiyeamini kuwepo kwa Imam Mahdi (a.s.) sijui tumpe hoja gani zaidi? Na hadith hizi ni mifano michache tu, nafasi haitoshi kuonyesha tabiri zote. Tukirejea swali la Ulul Amr ni nani, swali ambalo limeulizwa mwanzoni mwa sura hii, jibu lake sahihi ni: Mwenyewe Mtume (s.a.w.w) na kizazi chake kitukufu (Ahlul-Bayt ) wote 13 (a.s.). Tukirejea nyuma Sura ya Pili chini ya ‘Utoto na ujana wa Imam Mahdi (a.s.)’, tunakuta maelezo mafupi juu ya Kiyama Ndogo (Qiyamat Sughra). Nimeeleza pia kuwa kazi kubwa ya Imam Mahdi wakati huo ni kusimamisha (kuweka) utawala wa haki na dini moja ya haki na kuvunja dhuluma kwa kuwaadhibu madhalimu toka umma mbalimbali. Madhalimu wengi waliishi kwa anasa hadi kufariki kwao bila kuwajibika. Kwa upande mwingine watu wema waliishi chini ya udhalimu hadi wakafariki bila faraja yoyote ya kuwalipizia kisasi. Kwa hiyo kipindi hicho cha ‘Raj’at’ kimewekwa na Mwenyezi Mungu kuwaadhibu (kulipiza kisasi) watu waovu, huku watu wema kabisa wakishuhudia na kufarijika na uadilifu wa Mwenyezi Mungu. Yote haya yanatokana na ukweli kwamba uhai wa binadamu ni mfupi sana kiasi kwamba watu waovu hawawezi kuadhibiwa vya kutosha, na watu wema hawawezi kulipwa hapa hapa duniani kiasi cha kutosha. Rejea: Sura ya 2, chini ya ‘Utoto na Ujana wa Imam Mahdi (as).’

294


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 295

katika Uislamu

Vile vile tukirejea mafunzo ya Qur’ani; 9:32-33 tunaelezwa kuwa makafiri wanatamani kuzima nuru (Islam) ya Allah kwa vinywa vyao lakini Mwenyezi Mungu hataruhusu hali hiyo, na badala yake ataimarisha nuru hiyo. Katika Aya hizo inaelezwa pia kwamba Uislamu utashinda dini zote. Utabiri huo bado haujatimia kwa sababu hali halisi kidini hapa duniani, bado Uislamu unapigwa vita. Kwa kadri ya mafunzo sahihi ya dini, ni kwamba utabiri huo utatimia kipindi cha utawala dhahiri wa Imam Mahdi (a.s.). Haiwezekani maneno ya Qur’ani yasitimie, bali tu muda wake bado haujafika. Msomaji baada ya kusoma kitabu hiki utaona kuwa wakati huu hapa duniani, Uislamu umejazwa kasoro nyingi kwa karne nyingi. Huo sio Uislamu uliokusudiwa kushinda dini zote! Uislamu usio na kasoro utafufuliwa na kuongozwa na kiongozi halali toka kizazi cha Mtume (s.a.w.w) akiongozwa na Mwenyezi Mungu, naye ni Imam Mahdi (a.s.).

MUAWIYAH ANYAKUA UKHALIFA Kwa kadri ya wasia wa Imam Ali (a.s.) aliusia kuwa ukhalifa ushikwe na mtoto wake, Imam Hasan (a.s.) kwa kulingana na wasia wa Mtume (s.a.w.w) juu ya viongozi (Maimam) 12 baada yake. Nimeeleza kwa kirefu kuhusu uhasama wa Muawiyah kwa Imam Ali (a.s.) na Ahlul-Bayt (a.s.) kwa ujumla. Kwa hiyo baada ya Imam Hasan (a.s.) kushika uongozi huo, Muawiyah aliona kuwa ndio wakati unaofaa kwake kunyakua ukhalifa. Huko nyuma tumeona Muawiyah alivyojaribu kumpiga vita Imam Ali (a.s.) bila mafanikio ya kumwondoa madarakani. Waislamu wengi walipoteza maisha bila sababu za msingi. Muawiyah alitayarisha jeshi lake kwa kutumia ‘Baitul Maal’ kugharimia silaha na vifaa muhimu. Aliongoza jeshi lake hadi Iraq - makao makuu ya ukhalifa wakati huo. Katika vita hivyo Muawiyah aliwarubuni askari wa 295


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 296

katika Uislamu

Imam Hasan (a.s.) kwa pesa nyingi hadi wakamsaliti Imam Hasan (a.s.). Imam Hasan (a.s.) baada ya kugundua kwamba askari wake wamemsaliti, alilazimika kuingia mkataba wa amani na Muawiyah kwa makubaliano kwamba, ukhalifa uchukuliwe na Muawiyah lakini atakapofariki arejeshe ukhalifa kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w); na kwamba familia ya Imam Hasan (a.s.) na wafuasi wake walindwe. Na hivyo ndivyo Muawiyah alivyopata ukhalifa. Rejea: (i) Irshad, uk. 172 (ii) Al-Fusul al-Muhimmah, uk.144 (iii) Al-Imamah wa-Siyyasah - cha Ibn Qutaybah chapa ya Cairo, 1327 A.H - 1331 A.H- Jz. 1, uk. 163. Baada ya Muawiyah Ibn Abu Sufyan kunyakua ukhalifa, alifanikisha azma yake ya siku nyingi ya kutawala dola yote ya kiislamu. Aliingia Iraq na kuhutubia watu kwamba, “Sikupigana vita hivi kwa ajili ya kuamrisha Swala tano au kufunga Ramadhan. Hayo mnaweza kuyafanya wenyewe. Lengo langu lilikuwa ni kutawala na nimefanikiwa kwa hilo. Mkataba nilioweka na Hasan nimeuvunja na kuukanyaga, siutambui tena. Sitatetea maslahi ya dini wala kanuni zake na nitalinda madaraka yangu kwa gharama yoyote.” Rejea: (i) Tarikh Yakubi, Jz. 2, uk.193 & 207 (ii) An-Nasaih al-Kafiyah cha Muhammad al-’Alawi, chapa ya Baghdad mwaka 1368 A.H. Jz. 2, uk. 161. Muawiyah aliendelea kuhutubia kuwa, “Sitaruhusu Ahlul-Bayt (a.s.) na wafuasi wao kuishi kwa amani na kuendeleza harakati zao kama zamani. Raia yeyote atakayeelezea Hadithi ya kusifia matendo mema ya AhlulBayt hatakuwa na usalama wa roho yake na mali yake. Na atakayeleta Hadithi ya kuwasifia Makhalifa wengine wasio Ahlul-Bayt atazawadiwa maridhawa. Kuanzia leo ni lazima kumlaani Ali Ibn Abi Talib katika misik296


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 297

katika Uislamu

iti yote katika Swala za Ijumaa na Idd!” Rejea : (i) An-Nasaih al-Kafiyah, uk. 72-73 (ii) An-Nasaih al-Kafiyah, uk. 58, 64, 77-78. Amri hiyo ya Muawiyah ya kumlaani Imam Ali (a.s.), ilidumu takriban miaka 40 yaani hadi miaka 20 baada ya kufariki Muawiyah! Amri hiyo ya kidhalimu ilisimamishwa (ilisitishwa) na khalifa mwadilifu pekee wa Bani Umayyah – Umar Ibn Abdul Aziz, aliyekuwa khalifa tangu 99-101 A.H, na aliuawa kwa sababu ya msimamo wake wa haki. Kuanzia hapo Muawiyah aliwasaka na kuwaua wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) na kuwakata vichwa, kuvitundika kwenye mikuki na kuvichezea shere kuzungukia miji ya Iraq. Kuhusu amri ya kumlaani Imam Ali (a.s.) katika Swala za Ijumaa, watu wengi wakifahamu utukufu wa Imam Ali (a.s.) walikuwa wakikwepa kitendo hicho kwa kuondoka haraka msikitini mara baada ya Swala. Lakini Muawiyah alipoona hivyo alitoa amri mpya kwamba laana hiyo itolewe kwenye hotuba za mwanzoni mwa Swala hiyo! Rejea: (i) Tarikh Abul’ Fida, Jz. 1, uk. 186 (ii) Muruju- Dhahab, Jz. 3, uk. 33 & 35 (iii) Sahih Muslim Chini ya sifa za Ali Ibn Abi Talib (a.s.). Pamoja na Muawiya kuamuru magavana watekeleze amri hiyo na ipewe uzito wa Sunna, baadhi ya masahaba maarufu wa Mtume (s.a.w.w) walipinga vikali amri hiyo na ndipo Muawiyah akaamuru wauawe na kuchomwa moto. Waliouawa ni kama bwana Hijr Ibn Adi al-Kindi, na wafuasi wake wengine walizikwa wakiwa hai! Kwa hiyo basi inashangaza kuona baadhi ya vitabu vya ndugu zetu Sunni, vinamtukuza Muawiyah na hata kumwita mwandishi wa wahyi wa Mtume! Kwa maana kwamba alikuwa akiandika aya ziliposhuka kwa 297


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 298

katika Uislamu

Mtume (s.a.w.w)! Uongo kama huo unapingana na historia kwa sababu Mtume (s.a.w.w) aliishi Madina wakati ambao Muawiyah alipojidai kusilimu kwa unafiki hata hivyo hakuishi Madina bali aliishi Makkah. Hata pale ilipotekwa Makkah, Mtume (s.a.w.w) hakuishi Makkah. Kwa ukweli huo vipi Muawiyah awe mwandishi wa wahyi? Nimeeleza jinsi Muawiyah alivyokaribisha watu walete Hadithi za uongo za kuwasifia Bani Umayyah na kuwadhalilisha Bani Hashim na kuahidi zawadi nono kwa kazi hiyo! Kwa hiyo Waislamu tusishangae kuona sifa nyingi walizosifiwa baadhi ya masahaba, sifa ambazo hazikubaliani na kumbukumbu sahihi za historia! Waislamu tutambue kuwa kitendo cha Muawiyah kukaribisha na kuwalipa watu waovu waandike Hadithi za uongo, ni balaa kubwa mpaka leo hii katika Uislamu. Utawala wake wa miaka ishirini ulipandikiza upotofu mkubwa katika dini kiasi ambacho ni vigumu kutenganisha uongo na ukweli, mpaka upitie vitabu vingi vya historia na kulinganisha matukio yanayohusika. Hata hivyo mchunguzi yeyote mwaminifu ataupata ukweli wote kwa sababu Mwenyezi Mungu alishaahidi kuulinda ukweli wa dini usipotee (Qur’ani 15:9). Imam Ali (a.s.) anamkariri Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa: “Enyi Waislamu, pindi mkimwona Muawiyah amesimama mimbarini muueni mara moja.” Rejea: (i) Kitaab Siffin, uk. 243 - 248 (ii) Sharkh Nahajul Balaghah, cha Ibn Abi’l-Hadiid, Jz. 1, uk. 348 (iii) Tarikh Baghdad - Jz. 12 uk. 181 (iv) Mizaan al-I’tidaal - Jz. 2, uk. 128 (v) Tah’dhib at-Tah’dhib, Jz. 2, uk. 428 & Jz. 5, uk. 110 & Jz. 7, uk. 324. Bila shaka Mtume (s.a.w.w) akiongozwa na Mwenyezi Mungu, alijua madhara makubwa ya Muawiyah katika Uislamu. Lakini badala yake Waislamu wakapokea upotofu wake na kuufanya sehemu ya dini mpaka leo hii! Kama tutayapuuzia haya na kuendeleza Uislamu wa kurithi, tufahamu kuwa tunaelekea gizani, na tutajuta kesho akhera.

298


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 299

katika Uislamu

Kwa kweli hata ndugu zetu Sunni kuitwa Ahl al-Sunna wal-Jamaa, kihistoria ni maneno yaliyoanza kutumika mwaka 40 A.H baada ya Muawiyah kunyakua ukhalifa kama nilivyoeleza. Utumiaji wa maneno hayo unaonyesha kuwa Muawiyah aliwataka Waislamu wajitambulishe kuwa wafuasi wa sunna zake badala ya Sunna sahihi za Mtume (s.a.w.w)! Kwa mfano nimeeleza alivyoamuru kulaaniwa Imam Ali (a.s.) na amri hiyo ikadumu kama Sunna kwa miaka 40! Waislamu waliotekeleza amri hiyo kwa muda wote huo walitekeleza hivyo kama sehemu ya Swala ya Ijumaa, wakati siyo sunna ya Mtume (s.a.w.w)! Na khatib akikosa kutaja laana hiyo watu walimkemea “Umesahau Sunna.” Ndiyo maana ninasema kwa ushahidi kwamba Sunna nyingi za Muawiyah ziliingizwa katika Uislamu na kuwa sehemu ya Dini. Na hicho ndicho chanzo cha itikadi potofu na Hadithi potofu, zinazotatanisha kwa Mwislamu mchunguzi wa mambo, mwenye nia ya kupambanua kati ya ukweli na uongo. Kwa hiyo maneno haya, Ahl al-sunna wal-Jamaa yalikusudiwa hasa kuwatambulisha wafuasi wa sunna za Muawiyah, kwa sababu kauli na vitendo vya Muawiyah, havionyeshi kuwa alikuwa na ujuzi wa dini au uadilifu na uhalali wa kuwa kiongozi mwaminifu wa Waislamu. Lakini utawala wake mrefu wa miaka 20 ulipandikiza upotofu katika dini, upotofu ambao madhara yake tunayaona hadi hivi leo mpaka siku ya Kiyama! – Rejea maelezo zaidi juu ya Hadithi za uongo - Sura ya 16 chini ya: ‘Hadihti zilivyokusanywa na kuchujwa.’ Je, ni kweli masahaba waovu wamesamehewa? Tunapochunguza katika historia na kugundua matendo maovu waliyoyafanya masahaba, tunasikia ndugu zetu Sunni wanadai kuwa tusiwachunguze wamesamehewa kwa mujibu wa Qur’ani 9:100. Lakini ukichunguza Aya hiyo kwa uaminifu, utaona inaeleza kuwa Mwenyezi Mungu ameridhika na matendo mazuri (yaliyopita) ya masahaba na siyo yale matendo maovu waliyoyatenda baadaye! Binadamu yeyote anaandikiwa thawabu au dhambi kwa yale tu aliyoyatenda na siyo kwa matendo ya siku zijazo! 299


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 300

katika Uislamu

Hata kama tutang’ang’ania kuwa Aya hiyo (Qur’ani 9:100) iliwasamehe masahaba, itakuwa ni makosa. Nimetangulia kueleza kuwa tafsiri ya Aya yoyote ile ni muhimu isigongane na tafsiri ya Aya nyingine kwenye msahafu. Hebu basi tutupie macho Qur’ani 63:6, (Sura hii ni juu ya Wanafiki). Tutaona kuwa: “Ni mamoja kwao ukiwaombea msamaha au usipowaombea; Mwenyezi Mungu hatawasamehe; hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi wavukao mipaka.” (Qur’ani 63:6) Aya hii yaonyesha kuwa hakuna suala la kusamehewa masahaba moja kwa moja! Hao waliotajwa katika Aya hiyo ni masahaba! Kwa hiyo tusijenge hoja zisizo na msingi kwa kusingizia Qur’ani. Aya nyingine juu ya masahaba wanafiki ni (Qur’ani 9:73): “Ewe Mtume! Pigana na makafiri na wanafiki na uwe mgumu kwao, na makazi yao ni Jahannam, na hayo ni marejeo mabaya.” (Qur’ani 9:73). Aya hii ilimwamuru Mtume (s.a.w.w) kufanya Jihad dhidi ya makafiri na wanafiki. Lakini pamoja na madhara makubwa ya unafiki kama tulivyoyaona nyuma, hatuoni popote katika historia ambapo Mtume aliwapiga vita wanafiki! Labda kutokana na wingi wao, Mtume (s.a.w.w) aliona Jihad hiyo ingeleta hofu kubwa kwa wale ambao walikuwa bado kusilimu kama wangeona Mtume (s.a.w.w) anaamuru wauawe wale ambao tayari wanajiita Waislamu hali ya kuwa undani wao ni maadui wakubwa! Amri hiyo ya kuwapiga vita makafiri na wanafiki, kihistoria ilitekelezwa na Imam Ali (a.s.) baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Jambo hilo si ajabu tukizingatia maneno ya Mtume (s.a.w.w) kuwa, “Ana wa Ali min Nuurin Waahid” - (Mimi na Ali tunatokana na nuru moja). Vile vile Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa ‘Ali yu pamoja na Qur’ani, na Qur’ani ipo pamoja na Ali’. Kuhusiana na Qur’ani 9:73, Mtume (s.a.w.w) alisema akimwambia Imam Ali, ‘Ewe Ali baada yangu utawapiga vita wakiukaji wa Qur’ani (Nakisiin), wapinzani (Qasitiin) na wapotofu (Mariqiin). Utabiri huo ulikamilika pale Imam Ali (a.s.) alipopigana katika vita vya Jamal, Siffin na Nahrawan kama nilivyoeleza nyuma kwa kirefu. Isitoshe 300


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 301

katika Uislamu

tutambue kuwa iwapo masahaba wangesamehewa kwa kiwango hicho, na daraja ya wote ni kama nyota wa kufuatwa wanayowapa, dini isingekuwa na maana yoyote, na kuwepo Mtume (s.a.w.w) kusingekuwa na maana yoyote. Nasema hivi kwa sababu Mtume (s.a.w.w) anaongozwa na Mwenyezi Mungu katika yote anayotuamrisha. Iwapo akitokea sahaba akafuta amri ya Mtume (s.a.w.w), kwa mfano iwapo sahaba ataamuru watu waswali Swala tatu tu kwa siku badala ya tano! Je, ingefaa Waislamu wamfuate sahaba? Na kama wangemfuata sahaba, Mtume (s.a.w.w) angekuwa na kazi gani? Au kama tutaendekeza kufuata amri za masahaba kiasi hicho, dini itakuwa na hukumu ngapi katika karne 14 za Uislamu; kila mtawala anaongeza amri zake au kupunguza atakavyo, kwa sababu hatutaki kuchunguza na kutenganisha ukweli na upotofu. Nataka kusisitiza kuwa hata kama sahaba wangesamehewa, wasingesamehewa kwa kuyabomoa aliyojenga Mtume (s.a.w.w)! Kwa hiyo imani ya kwamba masahaba walikuwa na uhuru wa kufanya watakavyo siyo sahihi. Imani hiyo ilipandikizwa katika dini ili kuhalalisha maovu ya hao waliokwenda kinyume na mwongozo wa Mtume (s.a.w.w) kwa makusudi, na kwa faida zao binafsi. Tatizo la Hadithi za uongo katika Uislamu ni la kusikitisha sana iwapo utachunguza vitabu vya Hadithi. Ukiongeza na tatizo la tafsiri potofu ya Qur’ani utaona kuwa huo ndio msingi mkuu wa upotofu. Na waliopandikiza upotofu huo ni masahaba hao hao! Sasa tuwatii masahaba au tumtii Mtume (s.a.w.w)? Ni vipi masahaba wasamehewe uovu huo? Waislamu ni muhimu tuwe waaminifu kwa sababu mara nyingi nawasikia viongozi wa tabligh wanawaeleza Wakristo kwamba, aliyepotosha Ukristo ni Paulo, kwa maana kwamba mafunzo ya Nabii Isa (Yesu) ni sahihi lakini Paulo ndiye aliyeyapotosha. Sisi Waislamu tunawatetea masahaba kwa nguvu zote! Kwa hiyo Wakristo wanayo haki ya kumtetea Paulo kwa sababu Paulo alikuwa sahaba! Mtazamo kama huo hauwezi kutuongoza kufikia ukweli wa mambo. 301


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 302

katika Uislamu

Lakini suala la Hadithi za uongo halikuanzia kwa Muawiyah tu; bali pia katika uhai wa Mtume (s.a.w.w), kuna sahaba waliomsingizia Mtume uongo! Abu Hurayra bingwa wa Hadithi? Mfano mmoja wa Hadithi za uongo, unamhusu sahaba mmoja bwana Abu Hurayra ambaye ni maarufu kwa kutajwa kama mpokezi wa Hadithi nyingi. Bwana huyu alisilimu mwishoni mwa uhai wa Mtume (s.a.w.w), na usahaba wake ni miaka mitatu ya mwisho ya uhai wa Mtume (s.a.w.w). Hata hiyo miaka mitatu haina maana kuwa alikuwa anaishi au anakaa na Mtume (s.a.w.w) muda wote. Katika muda huo mfupi, sahaba huyo anadai kuwa alisikia Hadithi 5374 kwa Mtume (s.a.w.w)! Wakati ambapo makhalifa wanne (al-Khulafau Rashidun) na wake zake Mtume, jumla ya Hadithi walizopokea ni 1411 tu na walikuwa karibu sana na Mtume (s.a.w.w) kwa miaka mingi! Uchunguzi huo ulifanywa na mabingwa wa Hadithi yaani ‘Muhadithun’. Je, pana ukweli katika madai haya ya kumsifia Abu Hurayra? Hadithi zilivyokusanywa na kuchujwa: Kuanzia wakati huo wa Muawiyah na kuendelea, ukaanza utamaduni mpya wa kubuni (kughushi) Hadithi za uongo za kuwatukuza watawala. Hadithi kama hizo ziliingizwa katika vitabu vya Hadithi kwa karne nyingi zilizofuata. Ushahidi wa ukweli huu ni kwamba mkusanyaji maarufu wa Hadihti bwana Bukhari alikusanya Hadithi 600,000 lakini alipozichambua alizichuja na akaamua kubakia na Hadithi 2,761 tu! Hizo ndizo zilizomo katika kitabu chake maarufu sana tunachokitegemea kiitwacho Sahih alBukhari. Hata hizo Hadithi 2761 baadaye zilichunguzwa upya na ‘Muhadithun’ kuhakikisha ubora wake na zikapangwa upya katika mafungu ya ubora (daraja) wake kama tutakavyoona katika maelezo haya. Kwa hiyo ndugu 302


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 303

katika Uislamu

Waislamu tukitaka kuzielewa Hadithi inatubidi tusome sana somo la historia ili tufahamu sifa na vitendo vya wanaohusika, tuone kama sifa wanazopewa ni za halali. Rejea: (i) Tarikh Baghdad, Jz. 2, uk. 8 (ii) Al-Irshad as-Sari, Jz. 1, uk. 28 (iii) Sifatu’s Safwah, Jz. 4, uk. 143 Mkusanyaji mwingine maarufu ni bwana Muslim ambaye alichagua Hadithi 4,000 tu toka katika Hadithi 300,000 alizokusanya! Rejea: (i) Tarikh Baghdad, Jz. 13, uk. 101 (ii) Al-Muntzam, Jz. 5, uk. 32. Kwa upande mwingine ukipitia vitabu maarufu vya Hadithi utakuta kuna Hadithi nyingi zinazowatukuza makhalifa watatu wa kwanza, kwa sifa nyingi ambazo zinapingana kabisa na matendo waliyoyatenda niliyoyaeleza nyuma kwa ushahidi. Hiyo ni kasoro ya kwanza kwa mtafiti mwaminifu ambaye itamlazimu ajiulize kwa nini? Jibu lake ni kwamba mara Muawiyah aliponyakua ukhalifa, kutokana na chuki yake ya wazi kwa Ahlul-Bayt kama nilivyoeleza nyuma, aliamuru ziandikwe Hadithi za uongo za kuinua hadhi ya hao makhalifa watatu wa kwanza pamoja na masahaba wa ukoo wa Bani Umayyah. Muawiyah alitoa zawadi nono za nguo, pesa ardhi na mali nyinginezo kwa waandishi hao waovu. ‘Muhadithun’ na mwanahistoria maarufu mmojawapo, bwana Ibn Abi’lHadiid anamkariri mwandishi mwenzake Abu’l-Hasan al-Madaaini akiwa ameandika katika kitabu chake kuwa, ‘Muawiyah aliwaandikia maofisa wake kuwa; “Muwajali sana wale waliokuwa wafuasi watiifu wa khalifa Uthman. Watakaoleta Hadithi za kumtukuza, Hadithi zao hizo ziletwe kwangu na majina yao, ya baba zao na ukoo wao.” Watu waovu, kutokana na mwito huo, walianza kubuni Hadithi za uongo na kuziwakilisha. Hadithi hizo zililenga kuwatukuza Bani Umayyah na zikawa zimeingia 303


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:23 PM

Page 304

katika Uislamu

katika vitabu vya Hadithi! Rejea: (i) Kitab al-ah’daath - Abu’l-Hasan al- Madaaini (ii) Sharkh Nahjul Balaghah, Jz. 11, uk. 43-47. (iii) Tabaqat al-Huffadh, Jz. 2, uk. 151 & 157 (iv) Wafayaat al-A’yaan - Jz. 5, uk. 194. Mkusanyaji mwingine maarufu, bwana Abuu Daud alichagua Hadithi 4,800 tu, kati ya Hadithi 500,000 alizokusanya! Rejea: (i) Tarikh Baghdad, Jz. 9, uk. 57 (ii) Tabaqaat al-Huffaz, Jz. 2, uk. 154 (iii) Al- Muntazam, Jz. 5, uk. 97. (iv) Wafayat al-A’yaan, Jz. 2, uk. 404 Mkusanyaji mwingine maarufu, bwana Ahmad Ibn Hambal alichagua Hadithi 30,000 kutoka katika Hadithi karibu ya milioni moja alizokusanya! Rejea: (i) Tarikh Baghdad, Jz. 4, uk. 419-420 (ii) Tabaqat al-Huffaz, Jz. 2, uk. 17 (iii) Wafayaat al-A’yaan, Jz. 1, uk . 64 (iv) Tahdhib at-Tahdhib, Jz. 1, uk. 74 Katika maelezo haya tutaona kuwa wakusanyaji niliowataja hapa ni baadhi tu ya ‘Muhadithun’ lakini vitabu vyao ni maarufu sana navyo ni: Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Sahih Abuu Daud na Musnad al-Imam Ahmad Ibn Hambal. Tumeona jinsi ambavyo wakusanyaji hawa walivyotupilia mbali Hadithi nyingi mno za uongo, kuliko chache walizobaki nazo ambazo waliona zinafaa. Lakini kwa kuwa Hadithi nyingi za uongo zilichanganyika na zile za kweli kwa karne nyingi, hatuwezi kusema kwa uhakika kuwa hizi zilizobakia kwenye vitabu zote ni za kweli! Nasema hivi kwa sababu, kuna wakati ambapo palikuwepo na baadhi ya madhehebu za zamani hizo, waliojenga imani yao kwamba, kuzusha Hadithi kwa ajili ya kuzuia utendaji wa dhambi, au kwa nia ya kuwavuta watu kutenda mema, ni halali! Lakini msimamo wa Mwislamu mwaminifu ni kuipokea Hadithi ya kweli 304


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 305

katika Uislamu

ya Mtume (s.a.w.w.) na kuikataa yoyote ile hata kama inaamrisha mema, alimradi siyo Hadithi ya kweli. Rejea: Nahajul Balaghah. Kwa upande mwingine tutaona kuwa bado kuna Hadithi katika vitabu ambazo zinamdhalilisha hata Mtume (s.a.w.w) na Ahlul-Bayt wake. Kwa mfano katika Sahih al-Bukhari na Sahih Muslim. Katika Sahih al-Bukhari - kifungu cha: ‘Kitabu cha Swala’ somo la: ‘Uharamu wa Kuswali Uchi. Sahih al- Bukhari, inamkariri bwana Jabir bin Abdullah akisema kuwa, “Mtume (s.a.w.w) alikuwa anabeba mawe ya kujenga Al-Kaabah akiwa amevaa msuli (saruni) (Izar) ikawa ami yake (Abbas) akamwambia: “Ewe Mtume! Ni bora uvue huo msuli uweke begani (ukunje) ubebee mawe, na Mtume akavua msuli akaweka begani lakini akaanguka na kuzimia na hakuonekana tena akiwa uchi ila siku hiyo tu!” Sidhani kama kuna Mwislamu mpumbavu awezaye kukubaliana na Hadithi ya kipuuzi kama hii ya kumfanya Mtume (s.a.w.w) aonekane dhalili kama kichaa (Mungu apishe mbali)! Hadithi kama hizo zipo nyingi katika Sahih Muslim na Sahih al-Bukhari na vitabu vingine. Tufahamu kuwa kuna Wakristo katika nchi zenye Waarabu Wakristo kama Lebanon na huko Syria. Waarabu hao ni wajuzi wa lugha ya kiarabu kiasi kwamba wanaposoma Hadithi hizo katika vitabu vyetu Waislamu, wao wanapoteza imani kabisa katika Uislamu! Upotofu mwingine katika Hadithi unatokana na kutofahamu baadhi ya Hadithi zilizobatilisha Hadithi nyingine. Hali hiyo inasababisha kutumiwa Hadithi zilizobatilika! Kwa mfano alipojeruhiwa Umar kabla hajafariki, Suhayb alimwendea akiwa anamlilia. Bwana Umar akasema kuwa: ‘Ewe Suhayb unanililia wakati Mtume alisema kuwa marehemu huadhibiwa iwapo jamaa zake watamlilia’. Baada ya kufariki Umar ikawa habari hizo zimemfikia mama Aisha ambaye alisema, ‘Mwenyezi Mungu amsamehe Umar, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakusema hivyo ila alisema kuwa kafiri huadhibiwa iwapo jamaa zake watamlilia!’

305


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 306

katika Uislamu

Lakini tutaona kuwa hadi hivi leo utawasikia Waislamu wengi sana katika misiba yao, wanakataza watu wasilie kwa madai kuwa marehemu ataadhibiwa! Rejea: Sahih al-Bukhari, Jz. 2, uk. 100 – 102 Ndiyo maana katika vitabu maarufu vya Hadithi, utakuta Hadithi zimepangwa katika mafungu ya Sahih (za kweli), Hasan (nzuri), Muwath’thaqu (imara), Dhaif (dhaifu) na Mutawatir (zisizo na shaka). Vinginevyo tukizipokea Hadithi zote bila uchambuzi, tutakuwa na Uislamu wa kuchekesha, kwa sababu hata huyo Salman Rushdie aliyeandika kitabu cha kumkashifu Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alitumia baadhi ya Hadithi hizo zinazomdhalilisha Mtume (s.a.w.w) na Uislamu kwa ujumla! Hadithi hizo zimo katika vitabu vyetu vya Hadithi! Njia nyingine ya kuzipima Hadithi ni kuhakikisha kuwa hazipingani na tafsiri sahihi ya Qur’ani, kwa sababu haiwezekani Mtume (s.a.w.w) akaamrisha kitu kinachopingana na Qur’ani! Na wala hatuwezi kusema kuwa tutegemee Qur’ani peke yake na tuachane na sunna. Tukifanya hivyo tutakuwa hatuna Uislamu tena kwa sababu matendo mengi ya ibada zetu za kila siku, yamefafanuliwa katika sunna ingawa yameamrishwa katika Qur’ani kama Swala, Zaka, Hijja, kufunga na mengineyo mengi. Kwa hiyo tumeona jinsi ambavyo baadhi ya masahaba wakuu walivyoshiriki vitendo viovu vya kumsingizia Mtume (s.a.w.w) maneno ya uongo! Matokeo yake ikawa dini imepotoshwa. Msimamo wa Shia Ithna’asheri ni kwamba hatuamini kuwa masahaba wanaweza kusamehewa vitendo vya kuvunja kazi yenyewe aliyoletewa Mtume (s.a.w.w) kuifanya!

306


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 307

katika Uislamu

MUAWIYAH AMWACHIA URITHI WA UKHALIFA MWANAWE – YAZID Muawiyah alipokaribia kufariki aliwaita matajiri wa hapo mjini Kufa na kuwahonga pesa nyingi na ardhi ili wampe kiapo cha utii mtoto wake Yazid awe khalifa mara tu Muawiyah atakapofariki. Maofisa wa jeshi nao walihongwa pesa nyingi kwa nia hiyo hiyo. Waliokataa hongo hizo waliuawa. Muawiyah alifariki mwaka 60 A.H Kutokana na njama hiyo, mara Muawiyah alipofariki ikawa Yazid amechukua ukhalifa! Yazid Ibn Muawiyah alikuwa dhalimu, fasiki, mlevi kupindukia. Udhalimu wake ulizidi hata huo wa baba yake Muawiyah Ibn Abu Sufyan. Jambo la kusikitisha ni kwamba Yazid alitamka waziwazi kuwa hana imani yoyote na Uislamu kuwa ni dini ya Mwenyezi Mungu. Hakumwamini Mtume wala Siku ya Kiyama. Alisikika akisema kuwa imani ya kuwepo Kiyama ni upuuzi wa kuwahadaa watu waache starehe zao za dunia!

Tafrija zake za usiku za mara kwa mara, zilitawaliwa na muziki na mvinyo. Alikuwa na mbwa na nyani ambao walikaa karibu yake saa zote kwa kujifurahisha. Nyani wake aliitwa Abu Qays na alimvalisha vazi maridadi na kuwa naye katika tafrija zake. Mara nyingine nyani huyo alipandishwa kwenye farasi na kushirikishwa katika mashindano ya mbio za farasi. Rejea: (i) Tarikh Ya’qubi, Jz. 2, uk. 196 (ii) Murujudh-Dhahab, Jz. 3, uk. 77 Alidharau Swala tano kama vile hazina uzito wowote! Alicheza michezo haramu kama kamari na alikunywa pombe muda wote. Alikuwa mzinifu 307


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 308

katika Uislamu

hadi kuwalazimisha mama zake wa kambo na shangazi zake kuzini nao! Aliwavalisha mbwa wake mavazi ya viongozi wa dini kama ishara ya dharau. Hizo ndizo sifa za Kiongozi wa Waumini! Cheo cha juu kabisa katika Umma wa kiislamu, kinachukuliwa na mtu kama huyo asiye na imani na Uislamu wenyewe! Miaka 50 tu baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w), Uislamu unadidimia kiasi hicho kutokana na Waislamu kutotekeleza wasia wa Mtume (s.a.w.w) juu ya uongozi wa Waislamu baada yake! Mara tu baada ya kupata ukhalifa, aliruhusu askari wake kufanya watakavyo kwa raia wa mji wa Kufa kwa siku tatu! Alianza kuchota pesa za Zaka na kutumia ovyo kwa kuwavalisha na kuwapamba mbwa wake kwa vikuku vya dhahabu, lulu na nguo za hariri wakati raia waliotozwa hizo Zaka walikuwa wanakufa kwa njaa na mateso ya ufukara. Alichota pesa na kuwapa washirika wake na watumwa wa kike, waimbaji n.k. Alimpeleka nyani wake hadi kwenye mimbari! Katika mwaka wa pili wa ufalme wake, alituma jeshi lake kwenda Madina na kuhujumu raia wa hapo bila kujali utukufu wa mji huo. Yazid aliamuru jeshi lake kushambulia Makkah na Madina ambapo watu wapatao 11,000 waliuawa wakiwemo sahaba 700 waliokuwa wasomaji, wahifadhi maarufu wa Qur’ani tukufu. Wanawake zaidi ya 1,000 walibakwa! Msikiti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) uligeuzwa zizi la ngamia! Wakazi wa Madina walilazimishwa kula kiapo kwamba wao ni watumwa wa Yazid na ni juu yake kuwauza sokoni au kuwaacha huru. Rejea: (i) Tarikh Ya’qubi, Jz. 2, uk. 216 (ii) Tarikh Abul-Fida, Jz. 1, uk. 190 (iii) Muruuju-Dhahab, Jz. 3, uk. 64 (iv) Voice of Human Justice, uk. 300. (v) Sauti ya Uadilifu wa Mwanadamu, uk.224 Kwa kutumia chombo (silaha) kama mzinga, cha kurushia mawe mazito kwa masafa marefu, jeshi la Yazid lilirusha mapande makubwa ya magogo 308


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 309

katika Uislamu

ya moto hadi kwenye Al-Kaabah na kuharibu kis’wah (yaani paa la dungu) yake. Yazid amuua mjukuu wa Mtume (s.a.w.w) - Imam Husein (a.s.): Yazid hakutosheka na maovu hayo bali alimwamuru gavana wake wa Madina (Walid Ibn Utbah) kwamba achukue kiapo cha utii kwa Imam Husein kwa Yazid la sivyo Imam Husein (a.s.) akatwe kichwa kipelekwe kwa Yazid! Gavana huyo alimwita Imam Husein (a.s.) wakati wa usiku na kumweleza uamuzi huo. Imam Husein (a.s.) alitumia uwerevu akaomba atoe kiapo hicho akiwa na watu wengineo wa hapo Madina saa za mchana. Lakini mshauri wa gavana, Marwan ibn Hakam alishauri kuwa kiapo kitolewe pale pale au Imam Husein (a.s.) akatwe kichwa pale pale, na kwamba akimwachia hapo hatampata tena. Hata hivyo gavana aliamua kukubaliana na ombi la Imam Husein (a.s.) kwa sababu hakutaka kuhusika na udhalimu huo wa kumwua mjukuu wa Mtume (s.a.w.w). Sababu ya Yazid kuamuru hivyo, ni kwamba alijua kuwa Imam Husein (a.s.) ndiye kiongozi halali baada ya kuuawa Imam Hasan (a.s.). Kwa hiyo Yazid alitaka atambuliwe na kiongozi halali mwenye hadhi ili Waislamu wote wamkubali Yazid kama kiongozi halali, akijua kwamba bila ya hivyo mambo yanaweza yakamuwia magumu katika kukubalika kwake kama kiongozi. Kwa hiyo usiku wa tarehe 27 Rajab, 60 A.H (sawa na 681 A.D) Imam Husein (a.s.) na familia yake walitoroka na kuelekea ngome tukufu Makkah, ambako aliwasili tarehe 3 Shaaban, 60 A.H. Alikaa hapo takriban kwa miezi 4 na katika muda huo alipokea barua kama 150 toka kwa watu wa Kufa huko Iraq wakimwomba ahamie huko wampe kiapo cha utii awe kiongozi wao, afufue Uislamu uliokuwa unadidimizwa na Yazid Ibn Muawiyah. Imam Husein (a.s.) alimtuma mjumbe wake huko Iraq kuthibitisha taarifa hizo na kama ni za kweli apokee viapo vya utii vya watu hao. Mjumbe huyo, ambaye ni binamu yake, bwana Muslim Ibn Aqiil alifika mjini Kufa na kupokea viapo vya watu takriban 18,000. 309


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 310

katika Uislamu

Imam Husein (a.s.) akiwa Makkah alipata taarifa kuwa Yazid kawatuma wauaji 30 ili wamwue hata kama yuko katika ibada ya Hijjah. Wauaji hao waliamriwa wavae kama mahujaji na kuchanganyika humo ili wapate fursa ya kumuua Imam Husein (a.s.). Wakati huo huo Imam Husein (a.s.) alipokea barua ya mjumbe wake huko Iraq kumtaka aende huko. Imam Husein (a.s.) alibadili mavazi ya Hijjah. Mnamo tarehe 8 Dhul Hajj 60 A.H Imam Husein (a.s.) aliondoka Makkah na kukatisha Hijjah yake akaelekea Kufa - Iraq. Akiwa njiani pamoja na watu wake, Imam Husein (a.s.) alizingirwa na jeshi la Yazid la askari 1000 waliokuwa jangwani karibu na mji wa Kufa. Kwa ushauri wa kiongozi wa jeshi hilo Hurr Ibn Yaziid, Imam Husein (a.s.) aliacha njia ya Kufa na kuelekea porini kwa sababu njia zote za kuelekea Kufa zilifungwa. Akiwa njiani alifika sehemu moja tambarare ambapo farasi wake alikataa kabisa kwenda mbele! Imam Husein (a.s.) alibadili farasi sita lakini wote wakakataa kuondoka hapo! Imam Husein (a.s.) ilimbidi awaendee wenyeji kuwauliza mahali hapo ni wapi. Baada ya kutajwa majina kadhaa, mzee mmoja alisema kuwa alisikia kwa babu zake kuwa hapo ni Karbala. Kusikia hivyo Imam Husein (a.s.) aliamuru watu wake wasimame na kupiga kambi hapo, kwa sababu tukio hilo lilishatabiriwa mara nyingi na Mtume (s.a.w.w) pamoja na matokeo yake. Uzito wa tukio la Karbala katika Uislamu ni kwamba Mtume (s.a.w.w) alielezwa na Malaika Jibril kuwa siku hizo Uislamu utakuwa katika migogoro mikubwa sana karibu kufutika, lakini kunusurika Uislamu kutatokana na kafara kuu ya damu ya Imam Husein (a.s.) huko Karbala. Vilevile anakaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa adhabu ya muuaji wa Imam Husein (a.s.) itakuwa sawa na nusu ya adhabu zote za watenda madhambi wa dunia nzima! Tukio hilo la kikatili lilitokea jangwani Karbala ambapo Imam Husein (a.s.) na wafuasi wake waaminifu 72, waliuawa kikatili tarehe 10 mwezi wa Muharram mwaka 61 A.H, na kukatwa vichwa vyao, vikatundikwa 310


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 311

katika Uislamu

kwenye mikuki na kuvichezea kwa sherehe na ulevi kumpelekea Yazid Ibn Muawiyah huko Damascus – Syria. Siku hiyo ya mwezi wa Muharram tarehe 10, huitwa Ashura na huadhimishwa kila mwaka kwa hotuba juu ya tukio hilo pamoja na maombolezo. Maadhimisho hayo yanatokana na Sunna ya Mtume (s.a.w.w) ambaye mara kwa mara alijiwa na Malaika Jibril na kuelezwa kisa kizima cha tukio hilo la Karbala. Kila mara Mtume (s.a.w.w) alipoelezwa tukio hilo, alilia sana na kuomboleza; na kusema kuwa mkasa huo utaadhimishwa kwa maombolezo na kundi la wafuasi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w) kila mwaka na kila karne. Siku hiyo ya Ashura ilinyesha mvua ya damu na mbingu zilibakia nyekundu kwa siku arobaini! Baada ya mauaji hayo, watu wa familia ya Imam Husein (a.s.) waliobakia walitekwa na kufanywa wafungwa na kutembezwa njia ndefu kuelekea Syria kwa Yazid, huku wakiwa wamevalishwa mavazi yasiyo ya heshima, na kupitishwa mitaa ya watu wengi mijini. Tukio hilo la Ashura maelezo yake ni kitabu kizima na kwa hiyo nafasi haitoshi hapa kuelezea mambo yote. Mateka wa familia tukufu ya Imam Husein (a.s.), walipofikishwa kwa Yazid, walihukumiwa kifungo cha muda mrefu na adhabu nyingi za mateso, kabla ya kuachiwa na kurejea kuishi Madina. Jambo la kuzingatia katika tukio la Ashura ni kwamba kwa upande wa madhehebu ya Shia Ithna’asheri, mwezi wa Muharram ni mwezi wa maombolezo lakini kwa upande wa madhehebu ya Sunni, siku hizi baadhi yao wameanza mfumo mpya wa kusherehekea mwezi huo wa mwaka mpya wa kiislamu. Labda sherehe hizo ni za kuigiza Wakristo wanaposherehekea Noeli na mwaka mpya wa Masihiya? Waislamu hawakatazwi kusherehekea mwaka mpya ‘Solar year’ bali pia ni vizuri tuzingatie kalenda yetu ‘Lunar Calender’ ya kiislamu ambayo inatukumbusha matukio ya kihistoria ambayo baadhi yake ni ibada kuyaadhimisha. Isitoshe iwapo kuna Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) inayoonyesha kuwa ni bora katika mwezi huo kuomboleza, kwa nini tusherehekee?

311


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 312

katika Uislamu

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Husein anatokana na mimi, na mimi ninatokana na Husein.” Rejea Musnad Ahmad, Jz. 4, uk.172, Fara’id Simtain, Mlango wa 30, Tabaqatul-Kubra, Jz. 8, Yanabiul-Mawadda na vinginevyo.Hadith hii ina maana, mbali na nasaba ya damu, kwamba Mtume (s.a.w.w.) ndiye aliyeleta Uislamu, kwa juhudi kubwa kabisa Bani Umayyah wamejitahidi kuufuta Uislamu kiasi kwamba wakati huo wa Imam Husein Uislam ulikuwa unafutika kwa kuingizwa mambo chungu nzima yasiyo ya kiislamu kwa maslahi ya utawala wa kifalme. Kwa kafara ya damu ya Imam Husein (a.s.) ndipo Waislam wakazinduka na kuuona ubaya wa Yazid na wakaanza baadhi yao kumuasi. Ndipo Uislamu ukasalimika, na bila ya kutoka Husein (a.s.) tusingekuwa na Uislamu huu. Imam Husein (a.s.) akiwa Karbala alisema: “Kama dini ya babu yangu haiwezi kusimama ila kwa damu yangu, basi enyi panga njooni mnichukue.” Hivyo Muharram ni mwezi wa msiba, na wakati huo huo wa kushukuru kubakia kwa dini ya Mwenyezi Mungu. (Mhariri) Maelezo haya si kama ninaondoka katika somo letu, bali nimekusudia kuonyesha kuwa mara nyingi tunaona viongozi wa Sunni wanapoeleza historia ya Uislamu, huishia kwa al-Khulafau Rashidun, wakati ambapo Uislamu una historia ndefu ya karne 14 hadi hivi sasa. Labda hali hiyo inasababishwa na ukweli kwamba mfumo uliotumika Saqifah Bani Sa’idah kumpata khalifa wa kwanza, ndio uliowawezesha madhalimu kama Muawiyah na Yazid kupata Ukhalifa! Nina maana kwamba, kama tulivyoona nyuma, hakuna Shura wala Demokrasia iliyotumika kuwachagua mabwana Abu Bakr, Umar, Uthman, Muawiyah na Yazid! Aliyechaguliwa kwa ridhaa ya watu ni Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) peke yake. Huo ndio ukweli kwa kadri ya kumbukumbu sahihi za historia ya Uislamu. Kwa hiyo iwapo kwa mfano, wangetokea Waislamu wakati huo, wakahoji uhalali wa Yazid au Muawiyah kuwa khalifa, na ikawa Muawiyah au Yazid amepelekwa mahakamani, ni vipi hakimu angetofautisha mbinu za 312


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 313

katika Uislamu

hawa mabwana watano kuchukua ukhalifa? Hapa tunajadili hoja katika misingi ya utafiti. Daktari anapochunguza tatizo la mgonjwa ni lazima awe mwaminifu katika matokeo ya vipimo. Vinginevyo mgonjwa hawezi kupona. Kama vipimo vya mgonjwa vinaonyesha kuwa tatizo ni malaria, haiwezekani daktari mwaminifu akadai kuwa ni kichocho! Kwa hiyo iwapo Waislamu tunataka kuupata uhakika wa dini yetu, tuwe tayari kukubali ukweli japo unauma. Ni muhimu pia tuwe waaminifu. Yazid Ibn Muawiyah afariki: Mnamo mwaka 64 A.H (sawa na 681 A.D) Yazid alifariki kwa ajali ya farasi. Ajali hiyo ilitokea wakati Yazid akiwa katika starehe zake zisizokatika. Siku hiyo Yazid alikuwa amepanda farasi wake akijaribu kumfukuza nyani wake ili kumshinda mbio, ndipo akaanguka toka juu ya farasi wake na akafariki papo hapo. Rejea: Voice of Human Justice - uk. 299 - Tafsiri ya kiingereza ya Kitabu: Sautul ‘Adalatil’ Insaniya, na tafsiri ya Kiswahili – ‘Sauti ya Uadilifu wa Mwanadamu’ uk. 223 Utawala wa dola ya Kiislamu baada ya kufariki Yazid: Mpaka hapa tumefahamu migogoro mikubwa iliyotokea katika Uislamu katika kipindi cha miaka 53 tangu alipofariki Mtume (s.a.w.w). Ni maelezo marefu sana kueleza historia ya makhalifa wote waliofuatia hapo hadi kuishia mwaka 1923 A.D (mwisho wa utawala wa makhalifa duniani) huko Uturuki. Rejea: Crescent International News Magazine Jz, 25 – Na. 20 January 1-15-1997. Utawala huo wa cheo cha khalifa ulitumika nchini humo kwa mara ya mwisho mwaka huo, na ulifutwa na mwanamageuzi Mustafa Kerman At-Tartuk ambaye alianzisha Jamhuri ya Uturuki kwa siasa za kukandamiza Uislamu hadi leo. Kwa hiyo kueleza historia ndefu ya makhalifa wa Bani Abbas na Bani Umayyahh, kunahitajia kitabu kizima. Kufikia huo mwaka wa 1923 A.D, idadi ya makhalifa inafikia 103, kama nilivyoichanganua hapa chini. Kuandika historia ndefu ya makhalifa wote hao, ni kazi kubwa sana inayohitaji rejea za maelfu ya vitabu vya historia vilivyotawanyika ulimwen313


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 314

katika Uislamu

guni kote! Kwa hiyo kuanzia pale alipofariki Mtume (s.a.w.w) hadi mwaka 1923 A.D, idadi ya makhalifa ni kama ifuatavyo: (i) Al – Khulafau Rashidun 4 (ii) Bani Umayyah 14 (iii) Bani Abbas 37 (iv) Bani Abbas na Wamisri 18 (v) Waturuki 30 Jumla. 103 Ukiondoa baadhi ya makhalifa wa al-Khulafaau Rashidun pamoja na khalifa Umar Ibn Abdul Aziz (99 -101 A.H), makhalifa waliobaki, wengi wao walikuwa madhalimu, na hawakutawala kwa uadilifu wala ucha Mungu; kama tutakavyoona katika maelezo yafuatayo: Makhalifa wa Bani Umayyah na Bani Abbas: Historia inaonyesha kuwa makhalifa hao waliendeleza mfumo wa kutumia njia zozote na gharama yoyote, kuupata na kuulinda ukhalifa na kisha kuugeuza kuwa ufalme, ili kuurithisha kwa wanaowataka kila inapowezekana. Ukhalifa ulipaswa kuwa uongozi wa Waislamu katika mipaka yote ya amri za Mwenyezi Mungu lakini haikuwa hivyo. Badala yake tunaona kuwa viongozi hao walionyakua ukhalifa, walichota mali nyingi katika hazina kubwa ya Baitul Maal. Mali hizo zilitokana na ngawira na malipo ya Zaka, lakini viongozi hao pia waliwatoza raia kodi zaidi zisizo halali kidini, na ngawira nyingine zisizokuwa halali, ili kutunisha hazina hiyo, na kuwawezesha watawala hao kugharimia anasa zao za kupindukia mipaka. Magavana wa khalifa Hisham Ibn Abdul Malik walikuwa na kawaida ya kuchota mamilioni ya Dirham, kila mwaka kugharamia starehe zao. Wakati huo huo raia walidhalilishwa na kutishiwa uhai wao, ili wasilete upinzani na watawaliwe kirahisi.

314


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 315

katika Uislamu

Kwa mfano khalifa Abdul Malik aliamuru visima vya maji na chemchem zote za mji wa Bahrain zijazwe vumbi na uchafu ili raia wapate shida na waweze kuwa watiifu kwake! Vipi kiongozi wa waumini awatendee raia uovu kama huo? Hizo siyo sifa za khalifa, kiongozi wa juu wa Taifa la kiislamu! Kwa upande wa makhalifa wa Bani Abbas tunasoma kuwa walimiliki binafsi hadi watumwa 10,000 wa kike na pia watumwa wengi wa kiume waliohasiwa makusudi! Makhalifa hao wa Bani Abbas walijifaharisha kwa kujenga majumba makubwa yaani kasri (ikulu) zenye anasa na mapambo ambayo hata hivi leo si rahisi kuyapata kwa sababu kwa thamani ya wakati huo yaligharimu hadi Dirham milioni mia tatu! Kiasi hicho cha pesa kwa wakati huo, yaani miaka kama elfu moja na zaidi iliyopita, ni kiasi cha kutisha! Khalifa Ibn Mu’tiz alijenga Ikulu ambayo mapaa yake yalifunikwa kwa matofali ya dhahabu tupu! Majengo hayo yalinakishiwa kwa ufundi mkubwa kiasi kwamba ungedhani ni kazi ya majini na siyo mikono ya binadamu! Waliwekwa humo watumwa wa kiume 11,000 waliohasiwa, na pia maelfu ya watumwa wa kike kutoka Roma, Ethiopia na Sicily. Katika jengo hilo la ajabu lenye vyumba vingi sana, kulijengwa mti wa lulu tupu wenye uzito sawa na Dirham 500,000. Kisha ndege wengi wa lulu tupu walipachikwa katika matawi ya mti huo wa lulu, na kila upepo ukipitia hapo, ndege hao hutoa sauti za kupendeza. Katika jumba hilo kulikuwa na ghala yenye vito vingi vya thamani kubwa vya kupambia. Idadi ya mapazia yaliyofunika kuta zote yalifikia 38,000, na yalikuwa ya thamani kubwa kwa sababu yalikuwa ni ya hariri maalumu. Kulikuwepo na nyumba ya wanyama wakiwemo farasi 1000 wenye kupambwa kikamilifu, wakihudumiwa na watumishi waliovaa rasmi mavazi ya gharama. Ilikuwepo sehemu ya wanyama pori mbalimbali wakiwemo tembo wanne waliovalishwa nguo za hariri, na kuhudumiwa na 315


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 316

katika Uislamu

watumishi wengi. Kiti cha kifalme cha khalifa kilikuwa pembezoni mwa mto kikiwa kimepambwa kwa gharama kubwa sana. Kiti hicho kilielekea mandhari ya mto ili kumstarehesha khalifa wakati wa mapumziko yake! Mawaziri wa khalifa walikuwa na mali nyingi walizopewa kwa wadhifa wao. Mali hizo walizopewa, ni kama pesa nyingi kutoka Hazina ya Umma, pamoja na kumiliki ardhi nzuri wakati ambapo raia wa kawaida waliteseka kupindukia, kwa maisha ya dhiki. Hayo yote ni kinyume na wajibu wa serikali kwa raia katika Taifa la kiislamu, kama inavyoonyesha historia wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w). Rejea: Tafsiri ya kiingereza ya: Sautul Adalatil-Insaniya (The Voice of Human Justice), uk. 258, chapa ya June, 1990, cha George Jordac Lebanon – Syria, Tafsiri ya Kiswahili ‘Sauti ya Uadilifu wa Mwanadamu’ uk. 192. Uovu wa makhalifa maarufu; Al-Walid na Harun Rashid: Al-Walid Ibn Yazid: Alikuwa khalifa wa ukoo wa Bani Umayyah. Alikuwa mlevi mwenye tabia chafu sana kama za Yazid Ibn Muawiyah. Siku moja alikuwa kwa kimada wake wakiwa wote wamelewa. Mara wakasikia ‘Muadhin’ kwa ajili ya Swala ya Subhi. Khalifa huyo akiwa katika hali hiyo ya ulevi, aliapa kwamba siku hiyo lazima kimada wake aongoze Swala! Ndugu wasomaji tufahamu kuwa siku hizo za makhalifa ilikuwa lazima khalifa aongoze Swala pale anapoishi. Sasa tunaona kuwa huyu Al-Walid Ibn Yazid kwa kudharau misingi yote ya dini, anaamua kimada wake mwanamke aongoze Swala! Kwa hiyo mwanamke huyo alivalishwa vazi rasmi la khalifa na kuongoza Swala hiyo akiwa katika hali ile ile ya ulevi! Na wala si halali mwanamke kuongoza Swala ya wanaume! Rejea: (i) Tarikhu’ l-Khamis, Jz. 2, uk. 320 (ii) Musnad Ahmad, uk. 328 (iii) Fawatu’l Wafayat, Jz. 4, uk. 256 (iv) Tarikhu’l Khulafa’, uk. 291 Tunapozisoma kumbukumbu za kihistoria kama hizi, tunajiuliza kwamba, iwapo kama Shura na Demokrasia vilitumika kuchagua khalifa, ni vipi 316


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 317

katika Uislamu

Waislamu wangechagua madhalimu na makafiri kama hao kushika cheo cha khalifa? Ndugu wasomaji inabidi tufahamu kuwa, Dola ya kiislamu ya wakati huo, ilikuwa imekusanya nchi nyingi, ambazo siku hizi zimegawanyika kutokana na wakoloni kuzigawanya kwa maslahi yao. Bila shaka inaonyesha jinsi ambavyo raia hawakuwa na sauti yoyote juu ya nani anafaa kuwa khalifa! Kwa kweli hata katika siasa zetu za kidunia za wakati huu, haiwezekani watu wakamchagua japo diwani mwenye tabia kama hizo, wachilia mbali kiongozi mkuu wa nchi! Harun ar–Rashid: Alikuwa khalifa maarufu sana kama anavyohadithiwa katika kitabu maarufu cha Alfu lela Ulela (siku elfu moja na moja). Bwana huyu aliishi mnamo miaka ya 800 A.D sawa na 184 A.H huko Iraq. Siku moja alitaka kulala na mmojawapo wa vimada wa marehemu baba yake! Yule mama alikataa na kumwambia kuwa yeye ni sawa na mama yake kidini. Harun ar-Rashid hakuridhika bali aliamua kumwita Kadhi Mkuu ili amsaidie kupindisha Sharia ili Harun ar-Rashid ampate mama huyo! Kadhi huyo Abu Yusufu alitoa ‘fatwa’ kwamba mama huyo alikuwa mtumwa kwa hiyo hakuna tatizo kwa Harun ar-Rashid kumchukua! Kwa hiyo Harun ar-Rashid akamchukua mama huyo! Rejea: Kitabu maarufu cha historia kiitwacho Ibid. Inasemekana kuwa Harun ar-Rashid alilaanika na kufa kipofu kutokana na tabia yake chafu ya kujistarehesha kwa kuangalia ngoma za wanawake wanaocheza uchi wa mnyama! Kwa hakika hiyo ni aibu katika historia ya Uislamu. Labda ndiyo maana ndugu zetu Sunni wanapoelezea historia ya makhalifa, huishia kwa al-Khulafau’ Rashidun kana kwamba Uislamu haukuendelea baada ya hapo! Waislamu kama tunakubaliana na zile mbinu zilizotumika Saqifah Bani Sa’idah, hatuna haki ya kuwalaumu makhalifa wote waliofuatia hadi mwaka 1923 A.D huko Uturuki! Tukitaka haki turejee wasia wa Mtume (s.a.w.w) na ndipo tuone nani waliutekeleza na ni akina nani walikwenda kinyume chake.

317


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 318

katika Uislamu

Vinginevyo tutaaibika pale ambapo siri yetu hii wataijua na kutusuta, wale tunaowavuta wawe Waislamu, kwa njia ya mihadhara. Jambo la maana ni kwamba kama tungefuata wasia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w) kwa uaminifu na utiifu, haya yote yasingetokea, na Uislamu ungekuwa tayari umeitawala dunia yote kama alivyokusudia Mwenyezi Mungu. Watu wote wangevutiwa kuingia Uislamu. Nimeeleza jinsi ambavyo khalifa Harun ar-Rashid alivyomwamuru Kadhi Mkuu kuhalalisha haramu kwa kutoa fatwa inayomruhusu khalifa huyo kuzini! Fatwa hiyo ni kinyume cha Qur’ani 4:24. Rejea maelezo chini ya kifungu cha ‘Ndoa ya muda maalumu’ huko nyuma - Sura ya 10. Huo ni mfano wa khalifa mmoja miongoni mwa makhalifa wengi waliopindisha sheria mbalimbali za dini, kwa manufaa yao ya kidunia. Baadhi ya fatwa potofu walizotoa katika uhai wao, ziliendelea kutumika kama sheria za dini, kama tulivyoona nyuma mabadiliko ambayo ni kinyume na mafunzo ya Mtume (s.a.w.w) alivyofanya au alivyoamrisha. Kwa hiyo leo hii tufahamu kuwa baadhi ya mambo ambayo tunayaita Uislamu, kimsingi siyo ya Kiislam. Kwa mfano, kama tulivyoona hapo nyuma kwamba, kumpa mwanamke talaka tatu kwa mpigo siyo Uislamu! Yapo mengi ambayo siyo Uislamu iwapo utafanya utafiti kati ya yale aliyoamrisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w) na yale tunayoyatenda sasa hivi. Kwa mfano mara nyingi tumesikia katika semina mbalimbali za wasio Waislamu, wakiwakilisha mada zinazodai kuwa kuna sheria za kiislamu zinazokandamiza mwanamke wa kiislamu! Mtazamo huo ni upotofu mkubwa sana kwa sababu ukichunguza haki alizopewa mwanamke wa kiislamu, utaona kuwa hata hao wanaojiita watetezi wa haki za mwanamke, wangezifahamu haki za kweli za mwanamke wa kiislamu, kwa kadri ya mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.w), wangeshauri wanawake wote wawe Waislamu! Soma kitabu changu kingine cha “FAIDA YA UNYAGO WA KISASA KATIKA NDOA ZOTE”, juu ya madai ya kudhalilishwa wanawake wa Kiislam.

318


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 319

katika Uislamu

Kwa mfano mwanamke wa kiislamu anapoolewa siyo wajibu kwake kidini kupika, kufua nguo pamoja na kazi zote za ndani! Hayo yote akifanya anapata thawabu za sunna. Kwa kweli mwanamke wa kiislamu kishari’ah anayo haki ya kudai ujira wa kunyonyesha mtoto aliyemzaa katika ndoa, toka kwa mumewe! Bali kuna kitu kimoja tu ambacho mwanamke wa kiislamu ni lazima (wajibu) amtimizie mumewe nacho ni unyumba (tendo la ndoa) basi! Kama mwanamke akikataa, ataandikiwa dhambi na kulaaniwa na Malaika hadi amridhie mumewe kwa hilo tu. Isipokuwa katika ndoa ya muda maalumu mwanamke ana haki, wakati wa kufunga ndoa hiyo, kuweka sharti kwamba hatashiriki unyumba na huyo mume! Lakini iwapo katika ndoa yao hiyo, ikitokea siku moja huyo mama akakubali tendo hilo na mumewe huyo, basi kuanzia siku hiyo hatakuwa na haki ya kukataa tena! Labda wasomaji watajiuliza kuwa itakuwaje ifungwe ndoa bila unyumba wa moja kwa moja? Jibu ni kwamba mwanamume haruhusiwi hata kumgusa mwanamke asiye mkewe. Hata kitendo cha mwanamke na mwanamume kukumbatiana (romance) bila hata unyumba, au kuchezeana, au kubusiana, yote hayo hayaruhusiwi bila kuwepo ndoa kati ya wahusika. Kwa hiyo ndoa inaweza ikawa inawahalalisha kuchezeana (romance) bila unyumba iwapo mwanamke alitaka hivyo tangu mwanzo katika ndoa ya muda maalumu tu. Yote haya yanaonyesha haki ya mwanamke na uhuru alionao kisharia’h kwa Waislamu waaminifu na wajuzi wa dini. Ujinga katika misingi sahihi ya dini ndilo tatizo kubwa. Tabia iliyoenea miongoni Waislamu wa makabila mbalimbali hasa vijijini, ya kuwakatia mashamba wake zao walime na kisha mazao yakiuzwa pesa anachukua mwanamume au pesa hizo anapewa huyo mwanamke wa ndoa azitumie kujitegemea sio sahihi! Hayo yote ni haramu katika Uislamu. Mwanamke aliyeolewa katika ndoa ya kudumu ni lazima atimiziwe mahitaji yake yote na mumewe. Labda mume huyo awe hajiwezi kiafya; na hata hivyo mke ana haki ya kuchagua kumsaidia mumewe au kuachana 319


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 320

katika Uislamu

naye, yaani kumpa talaka. Kwa kifupi ni kwamba katika ndoa ya kudumu ni haramu mume kula jasho la mkewe! Iwapo mume hana uwezo wa kumtunza mkewe na kumtimizia mahitaji yake yote basi asimwoe, na kama amemwoa amwache - ampe talaka. Ndiyo maana kuna ndoa ya muda maalumu kama nilivyoeleza nyuma. Katika ndoa hii, mwanamume hawajibiki kumtunza mke labda kama mke akiweka sharti kuwa atunzwe na mume. Vile vile si haramu mume kula jasho la mke katika ndoa ya muda maalumu kwa sababu inawezekana kuwa mwenye kuhitaji ndoa hii ni mwanamke mwenye uwezo wa kiuchumi na hahitaji kutunzwa na mume, ila tu hataki kuzini. Rejea Sura ya 10 kwa maelezo zaidi chini ya ‘Ndoa ya Muda Maalumu’. Kwa hiyo, japo tunawaona wanawake wakiteseka kwa kazi ngumu hasa vijijini, hali ya kuwa ni Waislamu, tusichukulie kuwa hiyo ni haki, bali huo ni utamaduni tu, ndio unaowatesa. Na ndiyo maana Mtume (s.a.w.w) akasema kuwa ‘Achana na mila yoyote ile inayopingana na dini na endeleza mila inayokubaliana na dini.’ Napenda kusisitiza kwamba UTAMADUNI NA MILA YA MWISLAM NI UISLAM BASI. Nimeeleza huko nyuma maana ya Uislamu kwamba ni kujitoa nafsi yako yote kumtii Mwenyezi Mungu. Huwezi kuwa Mwislamu na hapo hapo ukaendelea kukumbatia mila zinazopingana na Uislamu!

JE, ILI MWISLAM AWE SUNNI INABIDI KUAMINI NINI? Maelezo yote yaliyotangulia hapa, yamejengeka katika mtazamo wa madhehebu ya Shia Ithna’asheri. Sasa tuchunguze asili ya madhehebu ya Sunni pamoja na itikadi zake, kwa kadri ya kumbukumbu sahihi za historia ya Uislamu, Sunna sahihi na Qur’ani.

320


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 321

katika Uislamu

Napenda tukumbuke kuwa umuhimu wa kuchunguza madhehebu unatokana na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) kwamba baada yake, Umma wake utagawanyika katika makundi 73 hadi Siku ya Kiyama, na kwamba makundi yote hayo yataangamia isipokuwa ni kundi moja tu litakalonusurika! Hatuwezi kujua ni madhehebu gani itanusurika bila kuchunguza kwanza ni madhehebu gani ambayo kwa uhakika inatekeleza mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.w). Sasa turejee kwenye somo letu hapo juu. Kutokana na wingi wa wafuasi wa madhehebu ya Sunni hapa Afrika Mashariki, wengi wetu tumetokea kuamini kuwa labda ni Mtume (s.a.w.w) aliyewaita hivyo au labda ni wao tu wafuatao mafunzo ya Mtume (s.a.w.w) kwa ukamilifu; au labda Mtume (s.a.w.w) naye alikuwa Sunni! Madhehebu ya Sunni kihistoria yalianzishwa takriban miaka 100 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), lakini ilikamilika miaka 140 baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati Abul Hasan al-Ashari alipobainisha itikadi za kisunni ambazo viongozi wenzake wanne waliomtangulia hawakuziweka; bali walifundisha “Fiqhi� peke yake! Dini haikamiliki bila ya itikadi. Ukweli ni kwamba Sunni ni wale ambao katika masuala ya Shariah, hufuata maoni (fatwa) ya mmoja wapo kati ya viongozi wao wakuu wanne yaani Abu Hanifa, Malik, Shafiii na Hambal. Na katika masuala ya itikadi hufuata maoni ya Abul Hasan al-Ashari. Inakubalika pia iwapo Sunni atakuwa ni mwenye kuwafuata wanafunzi wa viongozi hao wakuu niliowataja, ili mradi maoni ya mwanafunzi huyo yasipingane na hao viongozi wakuu wa Sunni. Kwa hiyo iwapo mtu hakubaliani na mfumo huo hawezi kuitwa Sunni. Sasa turejee katika historia tuone Usunni ulianza lini. Katika uchunguzi huu ni muhimu tufahamu ni nyakati gani hasa ambazo viongozi hawa wal321


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 322

katika Uislamu

izaliwa, kupata elimu, kuwa viongozi wa dini na mwisho kufariki. Bwana Abu Hanifah: Huyu alitokea Uajemi lakini babu yake alitokea Kabul - Afghanistan. Abu Hanifah alizaliwa mwaka 80 A.H (sawa na 701 A.D) mjini Kufa - Iraq yaani miaka 69 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Alifariki huko Baghdad - Iraq mwaka 150 A.H (sawa na 871 A.D) na kuzikwa karibu na mto Tigris. Miongoni mwa walimu wake wakuu ni Imam Jafar as- Sadiq (a.s.). Kwa kauli yake Abu Hanifah, anasema kuwa kama siyo miaka miwili aliyosoma kwa Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) angeangamia kielimu. Imam Jafar asSadiq (a.s.) ni Imam wa sita wa Shia Ithna’asheri katika wale viongozi 12 (a.s.) aliowataja Mtume (s.a.w.w) kuongoza Waislamu baada yake kama nilivyoeleza kirefu nyuma. Katika ‘Ijtihaad’ yake, Abu Hanifa alitegemea zaidi maoni yake binafsi na kutumia akili yake badala ya kutegemea Qur’ani na Sunna! Maulamaa wenzake wa wakati huo walikemea na kukanusha mfumo wake huo wa ‘Ijtihaad’ na walimtaka ategemee Qur’ani na Sunna peke yake. Madhehebu yake ilienea nchini Iraq wakati huo, na nchi nyinginezo za kiislamu. Aliishi miaka 52 chini ya utawala wa Bani Umayyahh lakini hakuwaunga mkono kwa sababu aliamini kuwa ukhalifa ulistahiki kupewa watoto wa Imam Ali (a.s.), na akatoa fatwa kuunga mkono wafuasi wa Imam Ali (a.s.) wapewe Zaka ili waimarishe harakati zao. Watawala wa Bani Umayyah walimtaka Abu Hanifa awe Kadhi mkuu lakini alikataa. Walimkamata na kumfunga na kumpiga viboko kwa siku kadhaa hadi alipokaribia kufariki. Hata hivyo mlinzi wa gereza alimsaidia kutoroka. Abu Hanifa alielekea Makka na Madina akiishi miji hiyo nyakati tofauti. Kipindi hicho ndipo alipokutana na Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) na kusoma kwake miaka miwili. Tufahamu kuwa elimu yake ya kwanza 322


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 323

katika Uislamu

kabisa aliipata mjini Kufa - Iraq ambapo alianza akiwa mfanyabiashara lakini muda si mrefu akaamua kutafuta elimu ambayo aliipata kwa “Taabi’in” mmoja jina lake Hammad Ibn Abi Salamah kwa miaka 18, kabla hajaanzisha Ijtihad yake na kupata wafuasi kama nilivyoeleza awali. Kwa kauli yake bwana Abu Hanifa anakaririwa akisema kuwa kama si miaka miwili aliyosoma kwa Imam Jaffar Sadiq (a.s.) yaani Imam wa sita wa Shia Ithna’asheri, angeangamia kielimu. Ina maana kuwa hata hiyo miaka 18 aliyosoma kwa ‘Taabi’in’ huyo isingemsaidia kitu kielimu. Inashangaza basi kwa nini hawa viongozi wawili wakuu wa Sunni hawakutaka moja kwa moja kuwa wafuasi wa Maimamu wa Shia ambao ndio walimu wao wakuu (kwa maana ya Abu Hanifa na Maliki). Elimu waliyopata Shafiii na Hambal asili yake pia inatoka kwa Maimamu wa Shia na ndiyo maana bwana Shafii alikiri wazi utukufu wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w). Tukirejea kwa bwana Abu Hanifa ni kwamba siku moja alimtembelea Imam Jafar as-Sadiq (a.s.), akawa anamsubiri nje atoke ndani. Akiwa anasubiri, alitokea mtoto mdogo. Abu Hanifa aliona apishe wakati kwa kuongea na mtoto huyo (ambaye alikuwa ni mtoto wa Imam Jafar Sadiq (a.s.) Abu Hanifa akamwuliza huyo mtoto, ‘Ewe mtoto, kitendo cha mtu kinatokana na nani?’ Mtoto alimjibu bila ya kusita, ‘Ewe Abu Hanifa kuna mawazo matatu tu yanayowezekana: Ama mtu mwenyewe ndiye mwanzilishi wa vitendo vyake; au Mwenyezi Mungu ni mtendaji wa kitendo kile; au wote wawili ni washiriki katika kitendo kile. Ikiwa Mwenyezi Mungu ni mshiriki wa vitendo vya mtu, kwa nini humwadhibu mtu kwa ajili ya madhambi? Je, hiyo si dhuluma? Na Mwenyezi Mungu anasema, ‘Hakika Mwenyezi Mungu si dhalimu kwa viumbe wake’ Na ikiwa wote wawili yaani mtu na Mwenyezi Mungu ni washirika katika vitendo vile, basi itakuwa dhuluma kubwa kwa Mwenyezi Mungu kumwadhibu mshirika dhaifu (mtu) kwa kitendo ambacho wameshiriki wote wawili! Kwa kuwa mambo haya mawili kiakili hayawezi kutendwa na Mwenyezi Mungu, hivyo basi ni wazi kuwa imebakia njia moja tu nayo ni kwamba mtu huten323


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 324

katika Uislamu

da vitendo vyake kwa uwezo wake na hiari yake mwenyewe.’ Kwa maelezo hayo ya ufasaha Abu Hanifa alibusu paji la uso wa mtoto huyo ambaye ndiye aliyerithi Uimamu toka kwa baba yake (Imam Jafar Sadiq) na kuwa Imam wa saba akiitwa Imam Musa Al-Kadhim (a.s.). Hapa tunathibitisha tena kwamba Ahlul-Bayt (a.s.) walizaliwa na elimu yao tangu utoto wao! Suala kama hili siyo “fiqih” bali lipo upande wa itikadi. Lakini kama tutakavyoona mbele, hawa viongozi wakuu wanne wa Sunni katika uhai wao wa uongozi wa miaka 131 hivi ukiongeza na miaka kama 30 hivi ya bwana Abul Hasan al- Ash’ari kusoma, kuhitimu na kuwa kiongozi wa Sunni kwa upande wa itikadi; ina maana kwamba Sunni walikaa miaka kama 161 bila kuwa na itikadi kama tutakavyoona mbele! Na dini haiwezi kukamilika kwa hukumu (shariah) bila itikadi. Hili ni tatizo la Waislamu kutofuata Ahlul-Bayt (a.s.) na badala yake kufanya ‘Ijtihad’ zao zenye upungufu mkubwa. Hakuna sababu ya msingi kwa nini Abu Hanifa hakufuata nyayo za mwalimu wake mkuu - Imam Jafar Sadiq (a.s.)! Mfano mwingine wa tukio lifuatalo, utatuonyesha jinsi ambavyo Abu Hanifa alikuwa na elimu duni, na pia pengo la kukosa elimu ya itikadi sahihi lilionekana wazi katika uongozi wa bwana Abu Hanifa. Wakati huo alitawala khalifa Harun al-Rashid ambaye alimchagua mtu mmoja aliyeitwa Bahlul ili kushughulikia migogoro fulani fulani. Huyu Bahlul alikuwa mtu mjanja na mwenye akili nyingi, kwa hiyo ili aweze kuwaingia watu wenye hadhi kubwa inapobidi, Bahlul alijifanya mwendawazimu na akawa anaitwa Bahlul Majnun (Bahlul Mwendawazimu). Kwa ujanja wake huo aliweza kuwalaumu na kuwakosoa hata wafalme kwa maovu au upotofu wao. Siku moja Bahlul alimsikia Abu Hanifa akiwafundisha wanafunzi wake kuwa amesikia mambo matatu toka kwa Imam Jafar Sadiq (a.s.) ambayo anafikiri kuwa ni makosa. Wanafunzi wakauliza ni mambo gani hayo? Abu 324


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 325

katika Uislamu

Hanifa akawajibu kuwa: (i) Kwanza kabisa Imam Jafar Sadiq anasema kuwa Mwenyezi Mungu haonekani. Lakini huo ni uongo kwa sababu kama kitu kipo lazima kionekane. (ii) Pili anasema kuwa shetani ataadhibiwa kwa kuchomwa motoni. Lakini hii ni upuuzi kwa sababu shetani kaumbwa kwa moto; vipi moto utakidhuru kitu au nafsi iliyoumbwa kwa moto huo huo? (iii) Tatu anasema kuwa kitendo cha mtu hutendwa kwa hiari na uwezo wake mwenyewe, na kwamba yeye mwenyewe ni juu yake vitendo hivyo. Lakini huo ni uongo, kwa sababu vitendo vyote vya mtu hutendwa kwa hiari na uwezo wa Mwenyezi Mungu ambaye kwa hakika ni mwenye dhamana ya vitendo vyote. Baada ya maelezo hayo, wanafunzi walianza kumshangilia Abu Hanifa. Hapo hapo Bahlul akaingia na akachukua donge la udongo na kumtupia Abu Hanifa na kumpiga kwenye paji la uso, naye Abu Hanifa akaanza kulia kwa uchungu na maumivu. Wanafunzi wakamkamata Bahlul na ikawa Abu Hanifa amempeleka mbele ya Kadhi. Kadhi alisikiliza mashitaka na akamwuliza Bahlul kama ni kweli. Bahlul: Ewe kadhi, Abu Hanifa anadai kuwa anasikia maumivu ya kichwa kutokana na udongo niliompiga nao. Lakini naona ni mwongo labda anionyeshe hayo maumivu. Abu Hanifa: Wewe Bahlul kweli ni mwendawazimu. Vipi nitakuonyesha wewe maumivu? Nani aliwahi kuona maumivu? Bahlul: Lakini ewe kadhi, muda si mrefu, sasa hivi tu, alikuwa akiwafundisha wanafunzi wake kwamba ikiwa kitu kipo basi lazima kionekane. Iwapo hawezi kunionyesha maumivu, basi hayapo kwa imani yake binafsi.

325


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 326

katika Uislamu

Abu Hanifa: We, kichwa changu kinaniuma kwa maumivu. Bahlul: Ewe kadhi nimesikia pia akiwafundisha wanafunzi wake sasa hivi tu kwamba, kwa kuwa Shetani kaumbwa kwa moto, basi moto wa Jahanamu hauwezi kumdhuru. Kwa vile mtu ameumbwa kwa udongo kama Qur’ani inavyotueleza, na mimi nimempiga kwa udongo, ninaona ajabu vipi huo udongo umdhuru naye kaumbwa kwa udongo? Abu Hanifa: Ewe kadhi, Bahlul anataka kukwepa adhabu, kwa kutoa maneno mengi, tafadhali chukua kisasi changu juu yake. Bahlul:

Ewe kadhi, nafikiri Abu Hanifa amekosea kunifikisha mahakamani kwa sababu ni sasa hivi tu, alikuwa akifundisha kwamba vitendo vyote vya mtu hutendwa na pia huongozwa na Mwenyezi Mungu ambaye ndiye mwenye dhamana ya matendo ya mtu. Sasa kwa nini ananileta hapa mahakamani? Ikiwa anasikia maumivu ya kupigwa na udongo basi akamshitaki Mwenyezi Mungu ambaye ameniongoza kumpiga na udongo!

Kadhi: Ewe Bahlul kwa maelezo yako ya haki nakuacha huru! Mpaka hapo tumeona nini maana ya itikadi katika dini na umuhimu wake. Pamoja na kwamba Abu Hanifa alikwishafafanuliwa jambo hili wazi wazi na mtoto wa Imam Jafar Sadiq (a.s.), kama tulivyoona hapo nyuma, bado alishikilia itikadi zake potofu ambazo mwisho wake zilimvunjia heshima akiwa kama kiongozi wa dini. Bahlul hasa alikuwa mfuasi na sahaba wa Imam Jafar Sadiq (a.s.) na aliishi hadi wakati wa Imam Ali Naqi (a.s.) yaani Imam wa kumi wa Shia. Baada ya kuanguka kwa utawala wa mfululizo wa Bani Umayyah, ulianza utawala wa Bani Abbas. Abu Hanifa alikataa kushirikiana na utawala wa Bani Abbas na hivyo alikamatwa tena, akafungwa kwa amri ya Al326


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 327

katika Uislamu

Mansuur (khalifa wa pili wa Bani Abbas) na akahukumiwa apigwe viboko. Alipopigwa viboko 110 alizidiwa na kufariki. Rejea: Kitabu, Abu Hanifah, cha Muhammad Abu Zuhrah, uk. 32-34. Habari hizo zilikaririwa kutoka kwenye kitabu cha, Mabadi’ul ‘Ammah lil-Fiq’hil-Ja’ fari, cha Hashim Ma’ruf al-Hasani. Bwana Malik Ibn Anas: Huyu alitokana na kabila la Banil-Asbah huko Yemen. Alizaliwa Madina mnamo mwaka 93 A.H (sawa na 714 A.D). Miongoni mwa walimu wake wakuu ni Imam Jafar as-Sadiq (a.s.) ambako alijifunza Hadithi na Hukumu (fiqh). Aliishi miaka 40 akiwa chini ya utawala wa Bani Umayyah na kupata umaarufu kama ulamaa. Baada ya kuanguka utawala wa Bani Abbas, alionyesha kuegemea upande wa wafuasi wa Imam Ali (a.s.) na haki yao ya Ukhalifa. Alitoa fatwa akiwataka watu kumuunga mkono bwana Muhammad Ibn ‘Abdillah Ibn al-Hasan Ibn Ali Ibn Abi Talib, ambaye alitangaza harakati za kupindua utawala wa Bani Abbas; kwa sababu hakuona uhalali wa kuwapa kiapo cha utii ambacho watu (raia) walilazimishwa kutoa. Gavana wa Bani Abbas wa Madina Ja’far Ibn Sulayman alimwamuru Imam Malik kupigwa viboko 50 ambavyo vilimtengua bega lake la kulia. Hata hivyo baadaye khalifa wa Bani Abbas Abu Ja’far al-Mansur alibadili mawazo na kurejesha uhusiano mzuri naye; na kumtaka aandike kitabu cha fiqh na kukisambaza kwa watu ili wakitumie. Kwa hiyo Imam Malik aliandika kitabu chake maarufu kiitwacho Al-Muwatta. Fiqh yake ilienea Afrika ya Kaskazini hadi Andalusia (Spain). Kuhusu msimamo wake wa ‘Ijtihaad’ alikuwa akisema kuwa, ‘Mimi ni binadamu, naweza nikawa sahihi au nikakosea kwa hiyo linganisha nisemayo na Qur’ani na Sunna.’ Bwana Malik alifariki hapo Madina mwaka 179 A.H.

327


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 328

katika Uislamu

Bwana Shafi’i: Jina lake kwa kirefu ni Muhammad Ibn Idris Ibn Abbas Ibn Uthman Ibn Shafi’i. Kizazi cha bwana Shafi’i kinatokana na Hashim Ibn Abdul Muttalib (babu yake Mtume). Alizaliwa mwaka 150 A.H (sawa na 771 A.D) huko Gaza. Mwaka huo huo ikawa bwana Abu Hanifa amefariki. Bwana Shafi’i alikuwa yatima na mama yake aliamua kumlelea huko Yemen. Alipofikia umri wa miaka 10 alisafiri kwenda Makkah ambako alijifunza kusoma na kuandika. Alisafiri jangwani ambamo aliishi miaka 17 na kuanza kujifunza Fiqh na mafunzo ya dini chini ya Maulamaa kadhaa kama Muslim Ibn Khalid al-Makhzumi na Malik Ibn Anas - alikosoma AlMuwatta juu ya Fiqh. Baada ya kufariki bwana Malik, bwana Shafi’i alirejea Yemen. Katika utawala wa khalifa Harun ar-Rashid mnamo miaka ya 148 A.H (sawa na 769 A.D) bwana Shafi’i pamoja na vikundi vingine vya harakati, walituhumiwa kuunga mkono wafuasi wa Imam Ali (a.s.). Aliyewatuhumu alikuwa gavana wa Yemen. Walikamatwa na kupelekwa Baghdad ili wafunguliwe mashitaka. Baadhi yao waliuawa lakini bwana Shafi’i alinusurika kifo na akasafiri kwenda Misri na kuishi huko. Madhehebu yake ilienea huko na katika nchi nyingi za kiislamu. Bwana Shafi’i alifariki huko Misri mwaka 204 A.H (sawa na 825 A.D). Bwana Hambal: Jina lake kwa kirefu ni Ahmad Ibn Muhammad Ibn Hambal. Ukoo wake unaonyesha kuwa asili yake ni kabila moja la kiarabu. Alizaliwa huko Baghdad - Iraq mnamo mwaka 164 A.H (sawa 785 A.D) na akaanza mafunzo ya dini akiwa na umri wa miaka 15. Alikuwa mwanafunzi wa Ash-Shafi’i, Abu Yusuf, na Ulamaa wengine. Madhehebu yake haikuenea sana kama hayo yaliyotangulia. Bwana Hambal alifariki huko Baghdad mwaka 241 A.H (sawa na 862 A.D). Mpaka hapo tumeona kuwa kihistoria, viongozi wakuu wa madhehebu ya Sunni walipata elimu yao toka kwa Imam Jaffar Sadiq (a.s.). Lakini viongozi hao wa Sunni wakaamua kufanya ‘Ijtihad’ zao binafsi hadi wakatoa hukumu za kutatanisha iwapo wafuasi wao wangechunguza na kufahamu hukumu zao zote kwa nia ya kuzifuata! 328


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 329

katika Uislamu

Mfano mmojawapo wa kusikitisha na kuchekesha ni fatwa ya bwana Abu Hanifa kuhusu Ulawiti. Fatwa yake hiyo inasema kuwa, Mtu yeyote anayemlawiti mtumwa wake au mtumishi wake hastahili adhabu kisharia! Bwana Malik naye anakubaliana na hukumu hiyo! Bwana Shafi anasema kuwa eti hakuna hukumu yoyote kuhusu suala hili katika Qur’ani lakini kwa maoni yake (Qiyas) - ni halali! Sisi Shia hatukubaliani na vitendo hivyo vya kutia aibu Uislamu! Rejea: (i) Hashiyah-Sharh al-Wiqayah, cha Allamah Chalapi, Kitabul Hudud - uk 212 (ii) Al-Mankhul - Imam al-Ghizal, Damascus, uk. 502. Katika nchi moja ya kiarabu yenye wafuasi wengi wa Abu Hanifa, kumekuwa na tuhuma nyingi za wenye nyumba kuwalawiti kwa nguvu watumishi wao wa nyumbani, wanaomiminika nchini humo kutafuta kazi! Kabla sijaendelea na maelezo mengine nataka nieleze tukio moja la kusikitisha wakati wa uongozi wa Imam Ali (a.s.) kuhusu uzito wa dhambi ya ulawiti mbele ya Mwenyezi Mungu. Siku moja mtumwa mmoja aliletwa mbele ya Imam Ali (a.s.) akikabiliwa na shitaka la kumwua bwana (mmiliki) wake. Mtumwa huyo alikiri kosa hilo na kusema kuwa hakuwa na njia yoyote ila kumwua bwana huyo, kwa sababu huyo bwana alimbaka huyo mtumwa kwa kumlawiti kwa kutumia nguvu. Imam Ali (a.s.) alimwuliza kama ana shahidi yeyote. Mtumwa alijibu kuwa hana, kwa sababu ilikuwa usiku wa manane wakiwa wawili tu nyumbani hapo. Imam Ali (a.s.) aliuliza kama huyo marehemu kabla hajafa alitubu kwa Mwenyezi Mungu. Mtumwa alijibu,’ Hapana’. Imam Ali (a.s.) kusikia hivyo alisema, ‘Allahu Akbar’ na kuongeza kuwa huyo mtumwa anasema kweli lakini hata hivyo aliamuru watu kwenda na kufukua kaburi la huyo marehemu na iwapo maiti itakutwa, huyo mtumwa ataadhibiwa. La, isipokutwa basi huyo mtumwa ataachwa huru. 329


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 330

katika Uislamu

Watu walikwenda na kufukua lakini hawakukuta maiti! Watu hao walirejea na kumweleza Imam Ali (a.s.) hali hiyo. Imam Ali (a.s.) aliamuru kuachiwa huru huyo mtumwa. Watu walishangaa na kusema, ‘Imam Ali (a.s.) anatawala watu walio hai na hata waliokufa’! Walimwuliza Imam Ali (a.s.) ni vipi alijua siri ya kaburi? Imam Ali (a.s.) alijibu, ‘Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema kuwa mwili wa basha au msenge ambaye hakutubu kabla ya kufariki, hata akizikwa popote pale duniani huwa unaondolewa na kupelekwa huko Sodoma kukaa huko na wenzao walioangamizwa hapo zamani hizo: na hubakia hapo hadi Kiyama watakapofufuliwa pamoja! Kwa hiyo tukipima uzito wa dhambi hiyo kulinganisha na dhambi nyinginezo, bila shaka tutatambua uzito wake mbele ya Mwenyezi Mungu. Rejea: The Holy Qur’ani (Full Commentary), ya Mir Ahmad Ali - M.A, B.O.L, BT - Jz .1 Lakini pamoja na hayo, dhambi hiyo inaongezeka sana hapa kwetu. Na huko Ulaya baadhi ya nchi kama Ubeligiji zimehalalisha kisheria ndoa ya mume kwa mume. Nchi nyingine huko Ulaya zimeruhusu kisheria kwa umri wa miaka 18 mtu awe huru kufanya uasi huo kwa misingi ya haki za binadamu! Nadhani baadhi yetu tumewahi kusikia baadhi ya Waislamu na viongozi kadhaa wakituhumiwa kwa vitendo vya ulawiti, hasa sehemu za pwani. Inawezekana ndugu zetu hao wanafuata ‘fatwa’ hizo potofu? Hayo tumwachie Mwenyezi Mungu, Mjuzi wa yote. Upotofu huo wa kutoa fatwa batili na kufasiri vibaya hukumu (Shariah), kumesababisha baadhi ya nchi za kiislamu siku hizi kutangaza kuwa zinatumia Shariah ya kiislamu. Matokeo yake kila mwizi anakatwa mkono! Hapo hapo nchi za Magharibi zinaanza kuushambulia Uislamu kuwa ni dini ya kinyama! Sheria ya kumkata mwizi mkono si halali kuitumia kwa kila mwizi; mpaka kwanza ieleweke kwa nini mtu huyo aliiba na taratibu nyinginezo muhimu. Iwapo aliiba kutokana na njaa hastahili kukatwa mkono kwa sababu katika nchi ya kweli ya kiislamu inayotawaliwa na 330


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 331

katika Uislamu

‘Shariah’ ni wajibu pia kwa serikali kuwalisha maskini au kuwapa Zaka! Mwizi anayestahili kukatwa mkono ni yule anayeiba ili atajirike au mwizi asiye na shida. Sharia sahihi ya kiislamu inazingatia vigezo mbalimbali katika kuadhibu wahalifu na ndiyo maana mzinifu mwenye ndoa anauawa kwa kupigwa mawe, wakati mzinifu asiye na ndoa anapigwa viboko 100! Kwa nini wote wasiuawe? Mara nyingi Uislamu unalaumiwa kwa vitendo vya watawala wajinga wa dini wasiotaka kukiri ujinga wao! Baadhi ya sheria za kiislamu zinazodaiwa kukandamiza wanawake katika ndoa na mirathi, ni sheria ambazo ziliwekwa na watawala wa dola ya kiislamu, katika utawala wao wa karne nyingi za ukandamizaji. Sheria halali za kiislamu zinapatikana kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w). Upotofu mkubwa tulionao katika Uislamu, ni matokeo mabaya ya kuwakataa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w) na kuwafuata watawala wasioheshimu dini. Tukitaka kufufua Uislamu, turejee haraka katika mafunzo yanayotokana na AhlulBayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w). Rejea: Sura ya 10, chini ya ‘Umar atoa hukumu bila ujuzi na kukosolewa.’ Maswali Muhimu ya Kujiuliza: Baada ya kufahamu historia fupi ya viongozi wakuu wa madhehebu ya Sunni, inabidi tujiulize maswali yafuatayo: (i) Tumeona kuwa Imam wa kwanza wa Sunni alizaliwa miaka 69 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Tukiongeza muda wa miaka kama 30 ya kumwezesha kuwa mtu mzima na kupata elimu ya kumwezesha kuwa kiongozi, tunafikia miaka 100. Je, katika hiyo miaka 100 kabla ya Abu Hanifa, Waislamu wa wakati huo walikuwa madhehebu gani? Ina maana Waislamu hao hawakuufahamu Uislamu ila Abu Hanifa aliyezaliwa miaka yote hiyo baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w)! Kwa nini Waislamu walioishi na Mtume (s.a.w.w) wakae miaka 100 bila kuwa na hukumu za dini (Fiqh) au itikadi? Maana yake ni kwamba Waislamu waliomwona Mtume (s.a.w.w) hawakuwa na madhehebu kwa sababu waliendelea kuishi wakiwa kitu kimoja kama alivyowaacha Mtume 331


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 332

katika Uislamu

(s.a.w.w.) bila madhehebu. Tatizo lililotokea ni utengano uliotokana na mgawanyiko kati ya Waislamu wanaosisitiza kuwa utekelezwe wasia wa Mtume (s.a.w.w) na kwa upande mwingine, wale walioangukia kutoa Bay’at kwa Abu Bakr Sidiq. Tofauti hiyo ilikuwa kwenye msimamo lakini siyo kwamba iliwazuia Waislamu kuswali msikiti mmoja na kushirikiana. Uzito wa Waislamu kujitenga kimadhehebu, ulitokea mbele kabisa enzi hizo za kuanzia uongozi wa viongozi wakuu wa Sunni na kuendelea hadi leo. Hata hivyo utengano huo haukuleta mfarakano mpaka enzi za ukoloni. Nina maana kwamba kama tungefuata wasia wa Mtume (s.a.w.w) kwa uaminifu, hadi leo hii tungekuwa kitu kimoja, tukiwategemea Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) kama viongozi wetu wakuu. (ii) Tumeona kuwa viongozi wakuu wanne wa Madhehebu ya Sunni ndio msingi mkuu wa Shariah (fiqh) Kisunni. Lakini viongozi hawa, hawakumwona kiongozi mkuu mwenzao Abul Husein al-Ashari ambaye ndiye msingi mkuu wa Itikadi! Maana yake ni kwamba muda wote wa uhai wa Abu Hanifa, Malik, Shafi na Hambal, Waislamu waliendesha dini kwa Fiqh peke yake bila Itikadi! Nasema hivi kwa sababu kiongozi mkuu wa mwisho - bwana Hambal alifariki mwaka 241A.H wakati ambapo Abul Husein al-Ash’ari alizaliwa mwaka 261 A.H, yaani tofauti ya miaka 20! Maana yake ni kwamba tukiongeza miaka kama 30, ili Abul Husein al-Ashari awe mtu mzima na awe na elimu ya kumwezesha kuwa kiongozi, tutaona kuwa Waislamu walikaa miaka isiyopungua 141 tangu alipofariki Abu Hanifa hadi Abul Husein al-Ashari awe mtu mzima mwenye elimu! Muda wote huo Waislamu walitumia Figh peke yake katika dini bila itikadi! Sasa huo ulikuwa Uislamu wa namna gani? Tumeona jinsi ambavyo bwana Abu Hanifa alivyojikuta katika matatizo kwa yeye kufundisha itikadi potofu! Umuhimu wa Itikadi ni kwamba kuna tofauti kubwa sana kati ya Waislamu wawili, ambao mmoja wao anaamini 332


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 333

katika Uislamu

kuwa Mwenyezi Mungu ataonekana na mwingine anayeamini kuwa Mwenyezi Mungu hawezi kuonekana. Kati ya hawa wawili, mmoja wao atakuwa na dhambi ya Shirk (Qur’ani 4:48) kwa kumpa Mwenyezi Mungu sifa isiyostahili! Kwa kifupi ni kwamba unapokuwa Mwislamu, uwe makini kuziepuka kabisa itikadi fulani fulani vinginevyo unaweza ukawa na imani za kikafiri! Kwa mfano Mwislamu akiamini kuwa Kiyama hakipo, tayari ni kafiri! Au tuseme iwapo Mwislamu ataamini kuwa kila tendo la binadamu hupangwa na kuongozwa na Mwenyezi Mungu, maana yake ni kwamba binadamu hawezi kuwa na dhambi kwa lolote atendalo! Na kwa maana hiyo kutakuwa hakuna haja ya Mwenyezi Mungu kuumba Pepo na Jahanamu kwa sababu itakuwa ni kuwaonea binadamu! Mwislamu asiyeamini kuwepo kwa Moto na Pepo sio Mwislamu tena! Imani kama hizi ndizo huitwa Itikadi. Sasa ni vigumu Uislamu wa mtu ukawa umekamilika bila itikadi zake kuwa wazi! Kama nilivyoeleza huko nyuma kwamba, makhalifa wengi walizuia hata kuelezea Hadithi za Mtume (s.a.w.w). Maana yake ni kwamba utawala wao haukutaka kuona dini inastawi na inaota mizizi katika jamii. Ndio maana Waislamu walikaa miaka yote hiyo zaidi ya 141 bila mwelekeo wowote! Na ndiyo maana wakatokea akina Abu Hanifa kujaribu kufufua dini upya kwa upande wa Sunni na kutumia Ijtihad zao kuandika vitabu vya Fiqh na kutoa Fatwa upya kama kwamba kuna jambo ambalo Mtume (s.a.w.w.) hakulifundisha huko nyuma! Na kama Mtume (s.a.w.w) alifundisha kila kitu, tusingetegemea Abu Hanifa awe mjuzi kuliko masahaba walioishi na Mtume (s.a.w.w)! Na tumeona wazi kuwa hata huyo Abu Hanifa alipotaka kuweka dini sawa, alikamatwa akafungwa na kupigwa viboko! Yote hayo yanaonyesha wazi wazi kuwa watawala hawakutaka kutawaliwa na dini japo walijiita viongozi wa Waumini! Kwa upande mwingine tumeona kuwa Waislamu wafuasi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w), kwa msimamo wao wa kutetea wasia wa Mtume (s.a.w.w) waliteswa na kuuawa kikatili, kwa hiyo wasingeweza kuleta 333


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 334

katika Uislamu

mabadiliko yoyote, zaidi ya kuendeleza harakati zao kwa kificho. Hata hivyo wafuasi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w) walikuwa wanaongozwa na misingi sahihi ya Uislamu, lakini walikuwa wachache na hawakuwa na madaraka yoyote juu ya umma mkubwa wa Waislamu. Kwa hiyo kazi ya watawala ilikuwa ni kukandamiza dini na kujinufaisha kwa Baitul Maal. Baadhi ya Waislamu wanahoji kwamba iwapo watawala hao walikandamiza Uislamu, mbona Uislamu ulipanuka na kuenea mpaka Ulaya, katika utawala wa viongozi hao hao? Jibu ni kwamba watawala hao walipenda sana vita na kupanua Dola ya kiarabu ili wapate kutawala sehemu kubwa na wapate mali nyingi za ngawira na waweze kukusanya Zaka nyingi pamoja na kutoza kodi ya Jiziya kwa raia wasio Waislamu! Ndio maana huko nyuma tumeona bwana Abu Bakr anaamuru kuwapiga vita Waislamu walioelekea kukataa au kusita kulipa Zaka, ingawa Mtume (s.a.w.w) hakuwahi kufanya hivyo! Nimeshaeleza kisa cha Tha’alabah kukataa kutoa Zaka, lakini Mtume (s.a.w.w) hakuamuru auawe! Wala Qur’ani haikuamrisha hivyo. (Qur’ani 9:75-77). Hiyo ilikuwa ni amri binafsi ya bwana Abu Bakr kinyume na amri ya Mwenyezi Mungu kwamba Mwislamu asiuawe vitani (Qur’ani 4:94). Kupanuka kwa dola ya kiarabu siyo kupanuka kwa Uislamu! Ndiyo maana uongozi wake uliendeshwa kwa ujanja wa hali ya juu wa siasa za kidunia zilizofunikwa na kilemba cha Uislamu! Kama tumezingatia maelezo ya nyuma, tutaona kuwa mali nyingi zilizokusanywa katika Hazina ya Taifa (Baitul Maal) zilikuwa kivutio kikubwa kwa watawala kuzitumia watakavyo pamoja na starehe zao za kupindukia. Kwa hiyo suala lolote lililowezesha kutunisha mfuko wa Baitul Maal lilipewa uzito mkubwa. Hata hivyo, katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri, vita vyovyote haviwezi kustahiki kuitwa ‘Jihad’ mpaka viwe vimeamrishwa na mmoja wa Maimamu 12 (a.s.) au ‘Mujtahid’ au viwe vita vya kujihami. Hii ni kuondoa uwezekano wa kuviita Jihad, vile vita visizo na mwelekeo wowote wa 334


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 335

katika Uislamu

misingi ya dini, isipokuwa tu kuteka ngawira na kutunisha Hazina (Baitul Maal) ili kugharimia anasa za watawala. Ukifikiri sana utaona kuwa kupanuka kwa dola ya kiislamu hakukuwa na maana yoyote wakati ambapo Uislamu wenyewe ulikuwa unadidimia! Kilichopanuka siyo Uislamu bali ni Dola ya kiarabu! Na ndiyo maana Uislamu uliporomoka huko Ulaya kwa sababu viongozi wa wakati huo walilenga kwenye maslahi ya kidunia badala ya kuimarisha Dini ya Mwenyezi Mungu. Mwisho kabisa wa somo hili, ningependa kutoa takwimu za mwaka 1975 za wafuasi wa viongozi wakuu wanne wa Suni duniani kote: 1. Abu Hanifa: (80 - 150 A.H) Ana wafuasi wapatao milioni 340 huko Uturuki, Pakistan, Bharat, Afghanstan, Transjordan, China, Indochina na Urusi ya zamani. 2. Malik bin Anas: (93 - 179 A.H) Ana wafuasi wapatao milioni 45 huko Morocco, Algeria, Tunisia, Sudan, Kuwait na Bahrain. 3. Shafi’i: (150 - 240 A.H) Ana wafuasi wapatao milioni 100 huko Palestina, Lebanon, Misri, Iraq, Saudi Arabia, Yemen, Indonesia, Tanzania, Kenya, Uganda na Somalia. 4. Hambal: (164 - 241 A.H) Ana wafuasi wapatao 300,000 huko Saudi Arabia, Lebanon na Syria. Rejea: Towards Understanding Islam - cha S.A.A. Maududi - Lahore Pakistan Kwa takwimu za wakati huu na kuendelea, ongeza wastani wa asilimia tatu kila mwaka kuanzia mwaka 1976 ili kupata makisio ya idadi ya wafuasi kwa wakati huu. 335


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 336

katika Uislamu

DINI SIYO NADHARIA POTOFU ‘DOGMA’ BALI NI TAALUMA Bila shaka uchambuzi huu umeonyesha kuwa yapo mambo mengi ambayo Waislamu wengi hatuyafahamu. Lakini kutofahamu jambo fulani hakulifanyi jambo hilo kuwa halipo. Mfano mzuri ni kwamba kila nchi inayo katiba lakini katika nchi zetu zinazoendelea, ni raia wachache wanaofahamu haki zao zilizomo kwenye katiba! Kwa hiyo akitokea mwananchi akadai haki yake fulani iliyomo kwenye katiba ya taifa lake, hata kama raia wenzake hawadai haki hiyo kwa kutoijua, sidhani kama haki hiyo itabatilika! Katiba ndiyo itahukumu. Katika mtazamo huo, niliyoyaandika hapa yasipuuzwe kwa kuwa walio wengi hawayajui! Mimi naamini kuwa Dini siyo ‘Dogma’ (nadharia potofu). Dini ya kiislamu ni sayansi ambayo hoja zake zote lazima zithibitishwe na zisiwe zenye kupingana na mantiki. Katika Qur’ani tunakuta hoja nyingi za kisayansi kuonyesha kuwa Uislamu siyo ‘Dogma’. Hivyo basi katika Uislamu wa kila siku hatuwezi kuingiza ‘Dogma’ yaani hatuwezi kutenda matendo ambayo hayana ushahidi wowote kuhusu ukweli na uhalali wake. Yawezekana hatuna elimu ya kutosha kutambua tufanye nini, lakini tusijenge hoja za kupingana na ukweli. Tusipoweka bidii kupata ukweli, tutatoa mwanya wa mtu yeyote kupenyeza ‘dogma’ katika dini, kwa kuzusha ibada au tendo lolote lisilo na uhusiano wowote na dini, kama nilivyotoa mifano mingi nyuma, kwa matendo kadhaa tuliyorithi bila uchunguzi wowote wa kielimu. Kama tunaamini kuwa tutahukumiwa Siku ya Kiyama, kwa nini wajibu wetu kiroho usiwe na kanuni maalumu hapa duniani? Vipi Mwenyezi Mungu atuhukumu kwa kukiuka sheria au kanuni ambazo hazikuwekwa wazi kwetu sote! Hiyo siyo sifa ya Mwenyezi Mungu kwa viumbe wake! Kama tunatetea madhehebu ambayo yanatawaliwa na kanuni tofauti, ina 336


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 337

katika Uislamu

maana kuwa Mwenyezi Mungu atatuhukumu kwa kutumia sheria tofauti wakati dini yake ni moja tu! Lakini hata hapa duniani, hakuna nchi huru inayowahukumu raia wake kwa aina tofauti za sheria kwa makosa yanayofanana! Uislamu ni ule ule mmoja mbele ya Mwenyezi Mungu; na kwa hiyo sheria zake pia ni aina moja tu. Migawanyiko hii tuliyonayo ni upotofu na ndiyo maana Mtume akasema kuwa tutagawanyika makundi mengi lakini ni kundi moja tu litakalonusurika. Watawala walidhibiti ijtihadi katika madhehebu ya Sunni: Iwapo Uislamu siyo ‘Dogma’ ina maana kuwa utafiti ufanywe ili kila tendo la ibada lithibitishwe na lipimwe katika mizani ya mantiki kwa kadri ya ushahidi wa Qur’ani na Sunna sahihi. Kinyume na hivyo tutajikuta tunatekeleza sunna potofu za watawala waovu wa ‘Dola ya kiarabu’. Watawala ambao hawakuwa hata na sifa yoyote njema ya kushika uongozi huo. Kwa upande mwingine tunaona kuwa tatizo la sunna potofu linatusababisha kufanya ibada batili zisizo na thawabu yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu. Sunna potofu zinatokana na Hadithi potofu kama tulivyoona katika Sura ya 15. Ukizidi kuchunguza utaona kuwa, mara nyingine watu waovu walitumia majina ya watu mashuhuri na kukariri kwao Hadithi za uongo lakini historia inawaumbua! Kwa mfano katika madhehebu ya Sunni, wanaelezea tukio la ‘Miraj’ kwa kukariri maelezo yanayodaiwa kutoka kwa bibi Aisha! Lakini tukirejea historia tunagundua kuwa, wakati huo (kabla ya Hijra) bibi Aisha alikuwa hajaingia kwa Mtume (s.a.w.w)! Ukweli ni kwamba wakati huo bibi Aisha alikuwa na umri wa miaka kati ya 8 na 9. Umri huo unatumiwa na maadui wa Uislamu kumdhalilisha Mtume (s.a.w.w) kwamba alikuwa mpenda wanawake sana kiasi cha kuoa binti mdogo kama huyo!

337


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 338

katika Uislamu

Kabla sijaendelea na maelezo juu ya kisa cha Miraj ningependa nitoe maelezo kidogo kupinga madai hayo ya kwamba Mtume (s.a.w.w) alikuwa na tamaa ya wanawake. Ukweli ni kwamba Mtume (s.a.w.w) hakuwachumbia bibi Aisha na bibi Hafsa. Kilichotokea ni kwamba Abu Bakr na Umar waliwatoa mabinti zao hao kwa Mtume (s.a.w.w) kama zawadi. Mtume (s.a.w.w) hakuwakatalia kwa sababu mabwana hao walikuwa ni watu maarufu hapo Makkah na kwa hiyo Mtume (s.a.w.w) aliona kuwa kwa kukubali kwake kuwaoa binti hao, kungeimarisha uhusiano mzuri na kisha kufanikisha kazi yake ya tabligh, wakati huo wa mwanzo wa Uislamu. Faida yake ni kwamba, ilitarajiwa kuwa watu watakapoona viongozi wao mashuhuri wameingia Uislamu, nao wataingia Uislamu. Baadaye Mtume (s.a.w.w) aliwaandikia barua wafalme kadhaa na kuwaalika waingie Uislamu. Na kila mahali ambapo kiongozi aliingia Uislamu, aliingia na wafuasi wengi waliomfuata. Hali hiyo ipo hata hivi leo, yaani nina maana kwamba Waislamu wengi humfuata shekhe wao bila hata kutumia akili zao! Tukirejea somo letu ni kwamba wakati wa tukio hilo la Miraj, bibi Aisha alikuwa bado mdogo mno kuweza kuolewa, na kwa hiyo japo alishapewa Mtume alikuwa bado kuishi naye. Bibi Aisha alianza kuishi na Mtume (s.a.w.w) kuanzia mwaka wa 1 A.H huko Madina wakati ambapo hiyo Miraj ilitokea mwaka mmoja nyuma, wakati Mtume (s.a.w.w) akiwa bado Makkah! Kwa hiyo Hadithi hiyo ambapo inadaiwa bibi Aisha alisema kuwa siku ya Miraj Mtume (s.a.w.w) alikuwa kitandani usiku wote - siyo kweli! Huo ni mfano mmojawapo kuonyesha kuwa Hadithi za uongo zipo nyingi mno na ni juu yetu kusoma sana historia ili kuepuka imani za ‘dogma’ ambazo hazitusaidii kitu. Waislamu kama hatutaki kubadili msimamo wetu kielimu, tutakuwa tunaendelea kupoteza muda kwa kuendeleza imani na ibada potofu.

338


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 339

katika Uislamu

Vile vile katika historia tunaona kuwa asili ya Waislamu kufunga mikono katika Swala, ni amri ya Muawiyah Ibn Abu Sufyan wala siyo Sunna ya Mtume (s.a.w.w)! Muawiyah aliponyakua madaraka aliamuru Waislamu wafunge mikono katika Swala badala ya kuiteremsha! Hata hivyo wanachuoni walioishi mbali na Madina walitekeleza amri hiyo potofu. Lakini Waislamu wa Madina walikataa kufunga mikono! Ndiyo maana hivi sasa kuna madhehebu ya Sunni ambayo wafuasi wake hawafungi mikono, na wakati huo huo kuna wanaofunga mikono! Lakini hapo hapo tukipitia hukumu (fiqh) za Imam Shafi’i tunaona kuwa ameruhusu kufunga mikono au kutofunga na kuita kwamba nip ambo tu la swala kufunga mikono. Rejea kitabu Hidayatul-Atfari. Sisi Shia tunasema kuwa kama Mtume (s.a.w.w) hakufunga mikono, basi hatuwezi kufunga mikono. Kwa kadri ya maelezo niliyotoa nyuma juu ya udhalimu na ukafiri wa Muawiyah, ni vipi mtu kama huyo akatoa fatwa ya kuongoza Waislamu? Sunna potofu kama hizo ndizo ninazoziiita ‘Dogma’ kwa sababu tunazifuata bila uhalali wowote! Ndiyo maana anakaririwa sahaba mmoja mwadilifu katika Sahihi al- Bukhari, bwana Anas Ibn Malik akiwa huko Damascus - Syria akisema kuwa, ‘Mimi sioni kitu chochote ila mnaswali tu na hii Swala imepotea’! Sahaba huyo mwaminifu aliyasema maneno hayo kwa kuwaona watu wanaswali kinyume na alivyoswali Mtume (s.a.w.w). Mwenyezi Mungu alishaukamilisha Uislamu (Qur’ani 5:3) mapema katika uhai wa Mtume (s.a.w.w) na kwa hiyo hakuna la kuongeza au kupunguza! Zaidi ya hayo wengi wetu tunaifahamu Hadithi maarufu alipokaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema, “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Pamoja na uzito wa maneno hayo na ucha Mungu wa hali ya juu wa Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) hatuoni popote katika historia ambapo Imam Ali (a.s.) aliongeza au kupunguza chochote katika yale yote aliyofundisha au kuamrisha Mtume (s.a.w.w). Vipi sahaba wengineo wawe na haki hiyo?

339


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 340

katika Uislamu

Tukirejea kwenye somo letu ni kwamba, tuchunguze ilikuwaje madhehebu ya Sunni wakawategemea viongozi wao watano tu yaani Abu Hanifa, Malik, Shafiii, Hambal, na Abul Hasan al-Ash’ari mpaka leo? Ukweli ni kwamba enzi hizo wasomi wa dini (Ulamaa) wa ngazi hiyo walikuwepo wengi kutokana na vuguvugu la kufufua dini lililokuwepo. Lakini hali hiyo iliwashtua watawala ambao waliona kuwa raia wanazidi kugawanyika na kutegemea zaidi hukumu (fatwa) za viongozi wa dini, badala ya amri za watawala. Kwa hiyo watawala hao walihofia kwamba madaraka yao kwa raia yatapungua, na mwisho wake ukusanyaji wa Zaka na utozaji kodi utapungua pia. Katika hali hiyo basi, watawala waliamuru kuwa watu wachague kufuata hukumu za mmojawapo yoyote kati ya hao viongozi wanne wa Sunni, na asitokee tena mwanachuoni mpya kufanya ‘Ijtihad’ mpya! Kwa upande wa madhehebu ya Sunni, hivyo ndivyo mlango wa fahamu ulivyofungwa yaani kuzuia watu kufanya utafiti katika dini kwa nia nzuri ya kuelewa na kusahihisha imani zao kama ni muhimu. Na hiyo ndiyo sababu ndugu zetu Sunni wanaendelea kuwategemea viongozi hao watano tu wa zamani. Je, ina maana miaka yote hiyo tangu enzi za hao viongozi watano wa Sunni, hakuna Sunni aliyesoma dini na kuhitimu na kustahiki kuwa kiongozi hai wa juu wa madhehebu ya Sunni? Kwa nini Waislamu waendelee kuongozwa na viongozi marehemu wakati matatizo mapya ya kidini yanazidi kujitokeza miongoni mwa Waislamu? Hiyo ni changamoto kwa ndugu zetu Sunni. Lakini tutaona kuwa viongozi hao wanne wa Sunni walitoa fatwa zao kulingana na matatizo yaliyokuwepo wakati huo wa uhai wao. Na tunafahamu kuwa Uislamu ni dini iliyo hai. Katika dini ambayo iko hai, hutokea matatizo mapya ambayo ni muhimu yatolewe fatwa ili kuwaongoza waumini wake. Lakini hatutegemei kuwa viongozi hao wakuu wa sunni walitoa hukumu (fatwa) za kutosha kutatua matatizo yote ya wafuasi wao hadi Siku ya Kiyama! Nina maana kwamba, iwapo kwa mfano, leo hii kutatokea tatizo jipya miongoni mwa Waislamu, ambalo linahitaji kutolewa 340


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 341

katika Uislamu

fatwa, vipi hao viongozi wakuu watano wa sunni watawasaidia wafuasi wao kwa wakati huu? Mfano wa tatizo linaloweza kujitokeza, ni kama vile ikitokea mji fulani ambao wakazi wake wamekuwa wengi kiasi ambacho hawawezi tena kutoshelezwa na mahitaji yao ya nyama za kuchinjwa ng’ombe kila siku kwa mikono. Ikawa umepita uamuzi wa kuchinja ng’ombe wengi kiwandani kwa kutumia mitambo ili kutosheleza mahitaji ya watu. Waislamu wakazi wa mji huo, watataka kujua uhalali wa kula nyama ya namna hiyo. Je, Waislamu hao watapata hukumu gani kutoka vitabu vya Abu Hanifa, Malik, Shafiii au Hambal? Wote hao ambao walikwishafariki zamani! Vile vile kutokana na maendeleo ya sayansi, tunasikia kuwa inawezekana sasa hivi kutumia taaluma ya kuumba kiumbe kinyume na maumbile (Genetic Engineering) kwa njia ya ‘Cloning’, kuzalisha binadamu au mnyama mwenye sifa sawa sawa za maumbile, sawa na mtu au mnyama mwingine anayeishi au aliyewahi kuishi! Maana yake ni kwamba zinatumika chembechembe nasaba (genes) ambazo zinapangiliwa kitaalamu katika yai la uzazi, na hivyo anazaliwa kiumbe mwenye sifa zote kama za yule mtu au mnyama zilikochukuliwa hizo chembehai, je ni halali kufanya hivyo kwa fatwa zao walizokwisha kutoa zamani! Inaeleweka kuwa kila binadamu ana michoro ya vidole (finger prints) ya aina yake tofauti na binadamu wote duniani! Lakini akizalishwa binadamu kwa njia hii, atakuwa na alama za vidole sawasawa na mtu aliyechukuliwa hizo chembechembe. Kwa hiyo sisi Waislamu wa enzi hizi za sayansi na teknolojia, ni lazima tuwe na kiongozi hai mwenye ujuzi wa kutosha wa dini, ambaye ataweza kututhibitishia uhalali au uharamu wa matumizi ya ‘Uzalishaji wa kinyume na maumbile’ kwa binadamu! Haifai kila shekhe au kiongozi yeyote wa nchi ya kiislamu kutoa fatwa yake bila ujuzi wa kutosha wenye misingi sahihi ya kiislamu! Vilevile siku hizi tunasikia huko Ulaya, kwamba inawezekana mwanamume akabadili jinsia yake na kuwa mwanamke, au 341


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 342

katika Uislamu

mwanamke kujibadili na kuwa mwanamume, ingawa sina taarifa kamili kuhusu sayansi hiyo, pamoja na asilimia ya kiwango cha ukamilifu wa badiliko hilo la maumbile asilia. Nani atatueleza athari zake kidini? Mfano mwingine ni hukumu (fatwa) juu ya binadamu aliyezaliwa nje ya tumbo la uzazi yaani (Test tube baby). Je, ni halali njia hiyo? Nani atoe fatwa leo hii wakati hao akina Shafi’i na Abu Hanifa wamekwishatutoka? Tuelewe kuwa Uislamu ulistahiki kuongoza maisha yote ya binadamu hadi Kiyama. Kama linatokea pengo la uongozi, huo ni upotofu wetu na siyo makusudio ya Mwenyezi Mungu. Kadri tunavyoendelea kuishi na kupata maendeleo ya kisayansi kutatokea matatizo mapya katika maisha yetu, yanayotaka ufumbuzi wa kidini. Na hiyo ndiyo maana ya Uislamu kuwa dini hai. Nataka kuonyesha kuwa ni muhimu wakati wote Waislamu wawe na kiongozi (Ulamaa) ambaye atatoa fatwa ya kuheshimiwa na Waislamu wote. Katika madhehebu ya Sunni, kiongozi kama huyo hayupo. Matokeo yake ni kwamba kila anayeitwa Sheikh hutoa fatwa yake hata kama hana ujuzi wa kutatua tatizo linalohusika! Kwani hao Mashekhe hawakuwepo wakati huo wa uhai wa hao Viongozi Wakuu? Mfano wa siku za karibuni ni pale ambapo marehemu Imam Khomeini alipotoa hukumu (fatwa) ya kuamuru kuuawa kwa Salman Rushidie, yule aliyetunga kitabu cha kashifa kilichoitwa Aya za Shetani. Kitabu hicho kilikashifu Uislamu na Mtume (s.a.w.w) na kilizua zogo dunia nzima, na kilisaidia Waislamu kupambanua kati ya viongozi halisi wa kiislamu na viongozi bandia. Baada ya Imam Khomeinii kutoa Fatwa hiyo, serikali za Magharibi na Marekani zilipinga vikali sana eti ni kinyume na haki za binadamu! Nchi za kiislamu za Uarabuni zilikaa kimya! Wakristo wajuzi watetezi wa Uislamu!: Lakini ajabu ni kwamba wakati huo huo alijitokeza kiongozi Mkristo 342


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 343

katika Uislamu

mwaminifu na mashuhuri - Bishop Lesslie Newbigin wa Birmingham Uingereza. Kiongozi huyo alikubaliana na fatwa ya Imam Khomeini kwa kutoa sababu zifuatazo:- (sababu zilizotolewa na Bishop). (i) Kashifa ya dini haipewi uzito sana hapa Uingereza kwa watu hawana tena imani nzito ya kuwepo kwa Mungu.

sababu

(ii) Sheria ya kuzuia kukashifu dini ipo Uingereza lakini inalinda Ukristo tu na siyo dini nyinginezo; na hiyo siyo haki kwa Waislamu kwa sababu Mungu ni yule yule. (iii) Binadamu hana uhuru wa kusema atakalo au kufanya atakalo iwapo kwa kufanya hivyo ataleta madhara kwa jamii; na ndiyo maana tunakataza mtu kuuza madawa ya kulevya. Uhuru una mipaka. (iv) Kwa kuwa Mungu ni Muumba na mtoa riziki (sustainer) wetu, kumkashifu ni sumu mbaya sana kwa jamii kuliko ubaya (sumu) wa wauzaji wa madawa ya kulevya. Sababu hizo muhimu za ucha Mungu zinajieleza wazi kwa watu wenye kufikiri. Lakini baadhi ya viongozi wa kiislamu wenye elimu duni, walidiriki kusema eti Imam Khomeini ana siasa kali! Baadhi ya viongozi Waislamu ndio wanaoutukanisha Uislamu na hata kuudhalilisha kutokana na elimu yao ndogo. Kimsingi ni kwamba wazungu wengi ni wakweli katika kufafanua mambo ya kitaaluma. Kwa mfano bwana William O. Beeman aliyekuwa mshauri katika Wizara ya Mambo ya Nje (State Department) Marekani. Bwana huyo pia alimuunga mkono Imam Khomeini juu ya fatwa hiyo kwa misingi ifuatayo: 1. Imam Khomeinii ametokea kuwa mtetezi imara wa Uislamu, na hilo ni jukumu muhimu katika Uislamu. 2. Uamuzi wa Imam Khomeini wa kutetea Uislamu hautofautiani na uamuzi wa Marekani wa kutetea na kulinda maslahi ya kidunia ya Kimagharibi. 3. Imam Khomeini si mzushi bali husisitiza lile jambo ambalo halipingani na sheria halisi za dini. 343


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 344

katika Uislamu

4. Migogoro na maandamano vilishaanza huko India na Pakistan na penginepo duniani kabla hata Imam Khomeini hajatoa fatwa yake! Tamko lake lilikuwa kuunga mkono wafuasi wake akiwa kama kiongozi wao. 5. Salman Rushidie alikuwa Mwislamu mzaliwa wa India; na aliyoandika kitabu chake ni kashifa ya kuifanya Qur’ani ionekane si neno la Mungu, na siyo tu kumkashifu Mtume Muhammad. Salaman alionekana wazi kuwa msaliti mwenye nia ya kuupiga vita Uislamu ndani kwa ndani, na hiyo ni dhambi kubwa kwa sheria za kiislamu; kwa h iyo adhabu ya kifo ni halali ikizingatiwa pia kuwa hakuna kiongozi mwingine maarufu kwa kiislamu aliyejitokeza angalau kumlaani Rushdie kwa usaliti huo! 6. Ingawa Imam Khomeini si kiongozi wa Waislamu wote kama Papa kwa Wakristo, lakini Imam Khomeini anakubalika kuwa mtetezi mkuu wa Uislamu na kwa hiyo pale ambapo Uislamu unakabiliwa na tishio kubwa, ni lazima atoe tamko ramsi kama ambavyo Papa angefanya iwapo Ukristo utatishiwa. 7. Lengo la Imam Khomeini kwa kutoa fatwa hiyo, ni kuueleza ulimwe gu kwamba huwezi kuushambulia Uislamu hivi hivi tu, bila wewe bina si kudhurika. 8. Ujumbe wa Imam Khomeini kwa Wamarekani ni kwamba Marekani imekuwa inadhibiti nchi fulani fulani kwa miaka mingi, siyo kwa kutetea dini bali kulinda siasa, na malengo (goals) ya Marekani ambayo Marekani inayathamini kama dini. Kwa mfano Marekani ilikula njama kwa kutumia C.I.A kutaka kumwua Fidel Castro wa Cuba miaka ya 1960. Vile vile Marekani katika miaka ya 1980 ilitumia ndege zake kupiga mabomu makazi ya Muammar Gaddafi huko Libya. Kwa hiyo kabla Magharibi haijamlaani Imam Khomeini, tujiulize kama sisi hatutoi hukumu kama hizo kulinda maslahi yetu ya kidunia? Kosa la Imam Khomeini liko wapi basi? Rejea: Africa Events Magazine, March 1989. 344


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 345

katika Uislamu

Sababu hizo zilitolewa na bwana William O. Beeman ambaye ni Mkristo, lakini elimu yake inampa uwezo wa kuchambua na kutetea Uislamu kwa mtazamo wa kitaaluma bila upendeleo au unafiki. Ndiyo maana ni muhimu Waislamu tupate elimu. Mfano wa tatu ni ule wa kiongozi mwingine maarufu - Prince of Wales huko Uingereza, katika hotuba yake aliyoitoa katika Sheldonian Theatre huko Oxford katika Taasisi ya Mafunzo ya kiislamu mnamo Oktoba tarehe 27, 1993. Katika hotuba yake hiyo nitanukuu vifungu muhimu kama ifuatavyo: 1. Pamoja na maendeleo makubwa ya teknolojia yaliyotuwezesha watu wa mataifa mbalimbali kuvuka mipaka ya nchi zetu, na kutembeleana kirahisi kuanzia nusu ya pili ya karne ya 18, bado kuna kutoelewana kati ya Uislamu na Magharibi. 2. Kuna Waislamu billioni moja duniani kote na kati yao wapo Waislamu milioni kumi hapa Ulaya na milioni moja hapa Uingereza. Uislamu umetuzunguka miongoni mwetu lakini hofu na kutoamini Uislamu kunaongezeka. 3. Inasikitisha sana kuona Waarabu wa Kusini mwa Iraq wanauawa kikatilina Saddam Husein. Kwangu mimi nasikitika kusikia maafa yanayowapata Waislamu Shia huko Karbala, Iraq. Pamoja na kwamba majeshi ya magharibi yalichukua tahadhari kubwa kutopiga mabomu sehemu takatifu za kiislamu huko Iraq; na ninakumbuka mimi binafsi kumwomba Jenerali Schwarzkopf nilipokutana naye huko Riyadh mnamo December 1990, kwamba majeshi yake yachukue tahadhari kulinda sehemu takatifu huko Iraq. Lakini ni Saddam Husein mwenyewe na utawala wake wa kutisha uliopiga mabomu na kuvunja sehemu hizo. 4. Uislamu umetangulia kuinua haki za wanawake katika nchi za kiislamu kama Uturuki, Misri na Syria kwa kuwapa wanawake mishahara sawa na wanaume na haki ya kupiga kura, mapema kuliko hapa Ulaya. Nchi hizo zimewapa wanawake haki ya kumiliki mali na urithi pamoja na 345


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 346

katika Uislamu

hifadhi wakipewa talaka. Haki hizo zilikuwa katika Qur’ani miaka 1400 iliyopita hata kama hazikutafsiriwa kwa vitendo na wanaohusika. 5. Tutakuwa tunajitumbukiza katika mtego wa majivuno ya uovu, kama tutafikiri kuwa maendeleo maana yake ni kwamba nchi za kiislamu zifanane na sisi! Kwa hakika ni kwamba mfumo wetu wa kuipenda dunia zaidi kuliko akhera, unaweza kupingana kabisa na maisha ya Mwislamu mwaminifu, ingawa sina maana ya wale Waislamu wa itikadi kali za kishabiki. Lakini tuwe makini na matumizi ya neno ‘Waislamu wenye siasa kali.’ Ni lazima tupambanue kati ya Waislamu wanaojaribu kwa uaminifu, kufufua Uislamu kwa kuzingatia yale yote yaliyoamrishwa; na kwa upande mwingine wale Waislamu mashabiki wanaotumia dini kufikia malengo yao ya kidunia au kisiasa. 6. Ufufuaji wa Uislamu ni hisia yenye nguvu kubwa ya kutoridhika na maendeleo pamoja na teknolojia za kimagharibi kwamba vitu hivi havitoshi; na kwamba maana halisi na lengo la kuumbwa binadamu linapatikana katika kuamini Uislamu na kanuni zake. Hata hivyo siasa kali ipo hata katika Ukristo na dini nyinginezo duniani. 7. Kutouelewa Uislamu hapa Magharibi, ni deni kwetu kwa kadri ya mchango mkubwa wa Uislamu kwenye ustaarabu na utamaduni wetu. Na hayo ni makosa ya historia potofu tuliyorithi. Ulimwengu wa kiislamu ambao leo tunauona kama adui yetu, ndio uliozaa wasomi wakuu wa taaluma zote muhimu tunazojivunia leo hii. Chini ya Uislamu, mji wa Cordoba ulikuwa ni mji uliostaarabika kuliko yote ya Ulaya mnamo karne ya kumi. Maktaba zilizoongoza kwa elimu zilijengwa na Waislamu nchini Hispania wakati mfalme Alfred akifanya uharibifu nchini humo. Sifa ambazo tunajivunia hapa Ulaya kama diplomasia, biashara huru na mipaka wazi ya nchi zinazopakana, utafiti wa kitaaluma n.k vimeletwa na Uislamu. 8. Ni muhimu tijifunze jinsi ya kuelewana na kubadilishana mawazo kama vile ambavyo mhandisi mzungu anafanya kazi katika visima vya mafu346


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 347

katika Uislamu

ta huko Ghuba, wakati ambapo daktari mpasuaji wa kupandikiza moyo ni Mmisri lakini anafanya kazi hapa Uingereza. Mwingiliano kama huo ni muhimu kimataifa ili kudumisha amani miongoni mwetu. Mpaka hapa ndugu Waislamu tumeyaona maelezo ya Wakristo wasomi na waaminifu juu ya Uislamu. Labda tujiulize kwamba ni viongozi wangapi wa kiislamu hapa kwetu, ambao wangeweza kuufafanua Uislamu kwa kiasi hicho? Kwa hiyo ninaposisitiza kuwa Waislamu tutafute elimu siyo kama ninawakashifu Waislamu wenzangu bali ni ukweli ulio wazi kwamba elimu yetu ni ndogo kwa wakati huu tulionao wa sayansi na teknolojia. Sasa turejee somo letu juu ya viongozi wengi kutoa fatwa katika Uislamu bila kuwa na ujuzi wa kutosha wa misingi muhimu ya dini yetu. Siku hizi siyo mashekhe tu wanaotoa fatwa, bali pia viongozi wa nchi za Waislamu (lakini ni wanasiasa)! Matokeo yake ni mgongano wa fatwa za kutatanisha! Umuhimu wa madhehebu ya Sunni kuwa na kiongozi mmoja duniani au walau Afrika nzima, bado haujazingatiwa. Ndiyo maana anatokea kiongozi mwanasiasa katika nchi ya kiislamu anaingiwa na tamaa ya kupanua mipaka ya nchi yake, anasimama jukwaani na kutangaza vita vya Jihad, na utawaona raia wake wanamiminika kujiunga na jeshi ili wakapigane na kufa kishahidi! Kumbe wanakufa vifo vya kijahilia! Kwa upande mwingine tatizo hili linasababishwa na kuichukulia dini kana kwamba siyo taaluma. Kwa maana kwamba kila mtu anajifanya kuifahamu dini! Ukweli ni kwamba dini ni taaluma kubwa sana na hakuna mtu awezaye kuipata taaluma bila kusoma kwanza na kuhitimu. Kama hatuheshimu na kuitambua taaluma ya dini, kwa kweli hiyo ni dharau kwa sababu tunapougua tunamwendea daktari na kuheshimu maelekezo yake. Tunapopata kesi tunamwendea wakili na tunamwacha kutusimamia bila kumwingilia uamuzi wake. Lakini tunashindwa kutambua kuwa kiongozi wa Dini mwenye ujuzi ni daktari wetu wa kiroho sawa na daktari wetu wa kimwili, kitaaluma! Kama nilivyoeleza nyuma, ni kwamba, madhehebu ya Shia Ithna’asheri hutegemea kiongozi mmoja mjuzi zaidi ya wote wa 347


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 348

katika Uislamu

wakati wake, kutuongoza na kutoa fatwa kwa waumini, katika mipaka ya Qur’ani na Sunna sahihi na wala siyo kwa misingi ya maoni yake binafsi, au kuwafurahisha watu wake au watu fulani mashuhuri. Msimamo huu wa Shia Ithna’asheri ni sahihi kwa sababu unaondoa uwezekano wa kuwapotosha waumini na fatwa zisizo na misingi yoyote ya dini. Kinyume na msimamo huu, itakuwa sawa na mtu yeyote kuingia hospitali chumba cha upasuaji; na kuchukua visu kupasua matumbo ya wagonjwa na kuwakata viungo fulani fulani bila ujuzi wowote! Matokeo yake ni kwamba hakuna mgonjwa atakayenusurika! Mifano ya imani zisizo na mantiki, ‘Dogma.’ Kutokana na wingi wa wafuasi wa madhehebu ya Sunni, utawasikia baadhi ya Waislamu wakisema kuwa Mtume (s.a.w.w) alikuwa Sunni! Wengine hudai kuwa al-Khulafau Rashidun walikuwa Sunni! Kwa kadri ya kumbukumbu za historia nilizotoa humu, Mtume (s.a.w.w) pamoja na akina Abu Bakr, Umar, Uthman na Imam Ali, hata wangefufuka leo, wasingejua maana ya Sunni! Nimeeleza kuwa kiongozi wa kwanza wa Sunni, bwana Abu Hanifa, alizaliwa miaka 69 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w) wakati ambapo al-Khulafau Rashidun wa mwisho (Imam Ali) alifariki mwaka 69 A.H, yaani miaka 11 kabla bwana Abu Hanifa hajazaliwa. Matumizi ya neno Sunni (Ahlul Sunna wal-Jamaa) yalianza katika utawala wa Muawiyah Ibn Abu Sufyan. Maana yake ni kwamba Waislamu wasio wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w) hawakuwa na uongozi maalumu na imara wa kutegemewa kidini baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Viongozi wao walikuwa wa kidunia tu. Kwa hiyo neno Sunni halina maana ya wafuasi wa sunna za Mtume (s.a.w.w) kama wengi wetu wanavyoamini! Ingekuwa maana yake ndiyo hiyo, basi neno hilo lingetumika sana katika uhai wa mabwana Abu Bakr, Umar na Uthman. Lakini tumeona pia kwamba katika uhai wa mabwana 348


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 349

katika Uislamu

hawa, ilikatazwa hata kuhadithia sunna za Mtume (s.a.w.w)! Kwa hiyo hatuwezi kuwaita hao kuwa ni wafuasi wa sunna za Mtume (s.a.w.w), watu ambao hawakutaka kusikia hata Hadithi za Mtume (s.a.w.w) (Qur’ani 58:22& 60:1) Hata hicho kipindi cha uhai wa Muawiyah ambapo neno hilo lilianza kutumika, hatuwezi kusema kuwa Muawiyah alikuwa na nia yoyote ile ya kuhamasisha watu kufuata Sunna za Mtume (s.a.w.w). Vitendo vya Muawiyah na kauli zake nimekwishavieleza huko nyuma kwa ushahidi wa kihistoria. Kwa hiyo tunabakia na ukweli kwamba, maana ya Sunni kwa kadri ya Muawiyah, ni wafuasi wa sunna zake mwenyewe! Waislamu walio wengi walilazimika kufuata sunna za Muawiyah ili kunusuru maisha yao! Baada ya Muawiyah kutawala miaka 20 mfululizo, bila shaka sunna zake hizo ziliota mizizi miongoni mwa Waislamu na kuwa sehemu ya dini (Qur’ani;10:36), hata baada ya kufariki Muawiyah. Isitoshe nimeeleza wazi na kwa ushahidi mzito, amri za makhalifa watatu wa kwanza, ambazo ni kinyume na mafunzo ya Mtume (s.a.w.w)! Tumeona kuwa Waislamu walitii amri hizo potofu na kuzipa uzito wa Sunna! Ni vipi tutawaita Waislamu hao kuwa ni wafuasi wa sunna za Mtume (s.a.w.w)? Kihistoria ni kwamba Muawiyah alitumia gharama kubwa katika kuinua heshima bandia ya kuwatukuza Bani Umayyah kinyume na sifa zao mbaya za kupindukia! Kwa hiyo ukizingatia upotofu wa kipindi cha hao makhalifa watatu wa kwanza, pamoja na upotofu wa miaka 20 ya utawala wa Muawiyah, sioni ni vipi tuwaite Waislamu wa wakati huo kuwa walikuwa wafuasi wa sunna za Mtume (s.a.w.w); ukiondoa wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.). Ushahidi wote muhimu nimeueleza wazi katika sura za nyuma. Pamoja na hayo, wapo Waislamu ambao wanaona kuwa Ahlul Sunna WalJamaa haikuwa na maana ya wafuasi wa sunna za Muawiyah. Kama tutakubaliana na hoja hiyo, tujiulize kwa nini kabla ya Muawiyah maneno 349


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 350

katika Uislamu

hayo hayakutumika? Au baada ya kufariki Muawiyah kwa nini Sunna zake potofu ziliendelea na Waislamu hawakuachana nazo hadi miaka 40 baada ya Muawiyah! Kisha tumeona kuwa baadhi ya Sunna hizo bado zinaendelea mpaka leo kama vile kufunga mikono katika swala! Tumeona pia kwamba Waislamu walitekeleza amri ya Muawiyah ya kumlaani Imam Ali (a.s.) katika Swala za Ijumaa na Idd kwa miaka 60 hata baada ya yeye Muawiyah kufariki! Hizo ndizo hoja muhimu kihistoria kuhusu Ahlul Sunna Wal- Jamaa. Kwa kadri ya historia sahihi ni kwamba, Waislamu waliomtii Muawiyah na wakaitwa Ahlul Sunna Wal-Jamaa (Sunni), waliendelea kujitambulisha hivyo na vizazi vyao, mpaka dini ikadidimia kabisa, na mwisho akazaliwa Abu Hanifa na harakati zake za kutaka kufufua Uislamu, miaka kama 100 baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w). Ni kitu gani kilichosababisha Abu Hanifa aanzishe harakati za kuufufua Uislamu baada ya miaka yote hiyo tangu kufariki Bwana Mtume (s.a.w.w.)! Bila shaka ni kwa sababu ya watawala wabovu waliodidimiza Uislamu hadi Waislamu wakapoteza muelekeo! Wafuasi wa Abu Hanifa, Malik, Shafii na Hambal ni Waislamu wale wale waliokuwa wanaitwa Ahlul Sunna wal-Jamaa. Kwa hiyo jina hilo likaendelea chini ya viongozi wapya na kurithishwa kwa vizazi mbalimbali hadi leo hii! Hata kama sasa hivi hatukubaliani na msimamo huo, lakini asili yake ni hiyo. Lakini kwa upande wa Shia Ithna’asheri tumeona jinsi ambavyo Sunna za Mtume (s.a.w.w) zilidumishwa muda wote wa uhai wa Ahlul-Bayt wake (a.s.). Ndiyo maana katika Shia Ithna’asheri matendo na mafunzo yote ya Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w) yanapewa uzito sawa na sunna za Mtume (s.a.w.w), kwa sababu nimeeleza alivyokaririwa Mtume (s.a.w.w) akisema kuwa, “Nawaachieni vizito viwili, (Qur’ani na Ahlul-Bayt wangu) ambavyo havitaachana hadi vinifikie katika kisima cha Kawthar huko Peponi. Jihadharini na mtakavyojihusisha navyo.” Nimeeleza pia jinsi ambavyo Ahlul-Bayt (a.s.) wanaongozwa na Mwenyezi Mungu na ambavyo wamelindwa na dhambi, kwa hiyo mafunzo na matendo yao hayawezi kuwa ya upotofu. (Qur’ani 33:33). 350


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 351

katika Uislamu

Lengo la utafiti huu Lengo la utafiti huu ni, kwanza kabisa, kuonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliacha Uislamu mmoja tu na wala hakuacha madhehebu. Pili nimeeleza maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba baada yake, umma wake utagawanyika katika makundi 73, na yote yataangamia isipokuwa kundi moja tu. Na nimeeleza hapo mwanzoni kabisa kuwa, Uislamu umegawanyika (kiitikadi) katika makundi mawili makuu nayo ni Sunni na Shia Ithna’asheri. Kwa hiyo nimechambua makundi haya mawili ili tuweze kufahamu asili zake kihistoria. Lengo langu siyo kuwavuta Waislamu wa madhehebu ya Sunni wawe Shia Ithna’asheri. Kazi yangu ni kuuweka wazi ukweli wa mambo na ni juu ya mtu yeyote, mwenyewe, kutumia akili yake na kuendelea ama kuwa Sunni, huku akielewa maana ya kuwa Sunni; au kuamua kuwa Shia Ithna’asheri akipenda. Mara nyingi utasikia viongozi wa Waislamu wanasisitiza kuwa Waislamu tuungane na tuwe kitu kimoja. Lakini hatuwezi kuungana kikwelikweli bila kwanza kuchunguza na kurejea katika mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.w.). Kama Waislamu wote tutakuwa waaminifu na kufuata nyayo sahihi za Mtume (s.a.w.w.), bila shaka tutajikuta tumekuwa kitu kimoja kwa sababu tutabakiwa na Uislamu mmoja uliosahihi. Vinginevyo madhehebu yatazidi kuongezeka na migongano itaongezeka, na mwisho wetu ni kuangamia. Maneno ya Mtume (s.a.w.w.) lazima yatatimia. Kwa kawaida utaona kuwa watetezi wa madhehebu na migawanyiko yote hii, ni viongozi ambao wanatetea maslahi yao ya kidunia. Wanaona kuwa muungano wa Waislamu wote na kuwa kwao kitu kimoja, kutawaondoa katika nafasi zao za uongozi walizoshikilia wakati huu. Hali kama hii haiwezi kutufikisha popote. Kama nilivyosema mwanzoni kwamba, hotuba ya Mtume (s.a.w.w.) aliyoitoa kama wasia pale Ghadiir Khum, inatosha kwa Waislamu waaminifu kurekebisha kasoro zetu. Hotuba hiyo inapatikana 351


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 352

katika Uislamu

katika kiarabu, kiswahili na kiingereza. Kwa maagizo ya Mtume (s.a.w.w.) juu ya hotuba yake hiyo, ni kwamba, ni wajibu kwa aliyeisikia kufikisha ujumbe huo kwa wale wasiowahi kuusikia. Sote tunafahamu kuwa kazi ya Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kufikisha ujumbe na siyo kuwalazimisha watu kuupokea na kuufuata. Waislamu tutafute elimu zote: Katika mijadala mbali mbali ya kidini na kidunia, ni wazi kwamba Waislamu wa hapa kwetu elimu yetu ni ndogo sana. Hali hii ni ya kusikitisha kwa sababu ulimwengu wa leo unaendelea haraka sana. Elimu zote zinazidi kurahisishwa kutokana na maendeleo makubwa ya ugunduzi na uendelezaji wa vyombo vya kompyuta n.k. Hivi sasa utaona kuwa kwa kutumia mfumo wa upashanaji habari wa Baruapepe (E-Mail) na Mtandao wa Internet ni rahisi kupata habari unazozitaka, dakika hiyo hiyo kutoka popote duniani! Habari kama hizo zimehifadhiwa katika kompyuta dunia nzima na wala huhitaji kuongea na mtu ili kupata habari hizo unazozitaka! Mnamo tarehe 24/10/99 saa kumi jioni, shirika la habari la BBC, Idhaa ya kiingereza, lilitangaza kuwa tayari walikuwepo watumiaji (wamiliki) wa vifaa vya Mtandao wa Internet wapatao milioni mia moja hamsini duniani kote na kwamba wanaongezeka kwa kasi sana. Baadaye shirika hilo lilitangaza pia kuwa, Encyclopedia Britanica tayari imewekwa katika Mtandao wa Internet. Maana yake ni kwamba mtu yeyote popote duniani anaweza kupata maarifa yaliyomo katika kitabu hicho maarufu, bila ulazima wa kukinunua kwa gharama kubwa sana au kwenda maktaba! Kitabu hicho kinayo maelezo ya wazi juu ya asili ya imani kadhaa muhimu za Kikristo ambazo Wakristo hudhani kuwa zilifundishwa na Nabii Isa (a.s.) kumbe sivyo! Je, sisi Waislamu tutaendelea kuyaficha yaliyomo katika vitabu vyetu vikuu kama Sahih Muslim na Sahih Bukhari n.k., mpaka lini? Hizi ni zama za ukweli na uwazi.

352


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 353

katika Uislamu

Kwa muda mrefu sasa kumekuwepo wahubiri wa kiislamu ambao wamekazania kuwahubiria Wakristo na kuwaingiza katika Uislamu. Hiyo ni kazi nzuri. Lakini Waislamu tumeweza kuifahamu Biblia vizuri kutokana na Biblia kuandikwa katika kiswahili. Kama viongozi wa Kanisa wangeacha Biblia ibakie katika Ki-Latin kama ilivyokuwa miaka ya hamsini (1950) kurudi nyuma, Waislamu tusingeifahamu Biblia. Lakini leo hii sisi Waislamu tumejenga kasumba ya kutukuza lugha ya kiarabu kama njia kuu ya kufahamu dini. Nimeeleza katika Dibaji yangu, kasoro nyingi za msimamo huu wa kutukuza kiarabu. Ni lazima mashekhe warekebishe kasoro hii ili mafunzo ya dini yaeleweke wazi kwa wote. Sambamba na kiarabu ni muhimu elimu ya dini katika kiswahili ipewe uzito maalumu kwa faida ya Waislamu wa kawaida kuweza kuelewa kwa urahisi zaidi. Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba katika kitabu hiki, nimetaja vitabu vingi sana kama ushahidi wa maelezo niliyotoa. Sitaona ajabu katika muda mfupi ujao, iwapo vitabu kama hivyo vitakuwa vimeingizwa katika mtandao wa kompyuta hizo na kuwawezesha watu wote wanaotaka kuifahamu historia sahihi ya Uislamu, kupata maelezo muhimu kwa urahisi, bila kuingia gharama kubwa ya kununua vitabu hivyo ambavyo ni vingi sana. Zaidi ya hayo wakati wa hatua za mwanzo za uchapishaji wa kitabu hiki, mwanzoni mwa mwaka 2000, tayari zimeshatengenezwa ‘Computer Programmes’ yaani taratibu za kompyuta, zenye uwezo wa kufasiri lugha ya kiarabu kwenda kiingereza au Kifaransa n.k! Miaka michache ijayo huenda lugha zote zikaeleweka kwa watu wote kwa kutumia njia hii! Je, hizo ‘siri’ zilizomo kwenye vitabu vikuu vya Uislamu zitafichika mpaka lini? Hao viongozi waliozoea kuficha ukweli ili kulinda maslahi yao, watadumisha utamaduni huo mpaka lini? Kwa hiyo muda si mrefu watu wengi wasio Waislamu, watapata nafasi ya kuufahamu Uislamu, pengine hata kuliko sisi Waislamu wenyewe! Ndiyo maana katika kitabu hiki nimeamua kueleza wazi mambo ambayo wengi 353


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 354

katika Uislamu

wetu hawajawahi kuyasikia! Na ninafahamu kuwa baadhi ya viongozi wa madhehebu ya Sunni hawatayafurahia ingawa mbele ya Mwenyezi Mungu ni ukweli mtupu. Ninaamini kuwa dunia nzima wakati huu, tumeingia katika kipindi cha ukweli na uwazi ndiyo maana siasa za kinadharia zimetelekezwa! Huu ni wakati wa Waislamu kuelezwa ukweli wa dini yao ili warekebishe kasoro zao. Iwapo tutaendelea kuficha ukweli, tufahamu kuwa njia za kupata ukweli zinaongezeka. (Qur’ani 2:146-147). Kuna kisa cha Mzungu mmoja aliyesoma sana vitabu vya Kiislam kwa lugha ya kiingereza mpaka akapendezewa na Uislam na kanuni zake. Akaenda kwa Sheikh kutaka kusilimu. Baada ya kusilimu, katika maingiliano mapya na Waislam, akakuta Waislam wanakwenda kinyume na vile alivyoona kwenye vitabu! Mambo ya ajabu ajabu na vitendo vyao yakamshangaza sana. Basi alinyanyua mikono yake juu na kumwambia Mwenyezi Mungu: “Ewe Mola wangu! Nakushukuru kwa kunionyesha Uislam na uzuri wake kabla ya kunikutanisha na Waislam wenyewe.” Kwa maana ya kwamba, kwa mambo yao hayo yeye asingevutiwa na Uislam na asingeweza kuipata neema hiyo! (Mhariri). Ni kweli kwamba ni viongozi wachache sana wa Waislamu, wanaofahamu kuwepo kwa vitabu nilivyovitaja humu. Lakini kwa upande mwingine, wapo viongozi ambao wanaficha ukweli ili kulinda maslahi yao ya kidunia! (Qur’ani 2:159). Miongoni mwa viongozi hao wafichao ukweli, wamekuwa wakiwaambia wafuasi wao wasio na elimu ya kupambanua mambo, kwamba madhehebu ya Shia Ithna’asheri ni Makadiani! Mara nyingine sisi Shia tunaitwa Makafiri eti tunadai kuwa Utume ulistahili kupewa Imam Ali (a.s.)! Astaghfirullah!!! Mungu aepushilie mbali uzushi huu. Madai yote haya tunayosingiziwa sielewi yamenukuliwa kutoka vitabu gani vya Shia Ithana’asheri? Katika kitabu hiki nimeeleza Hadithi muhimu za Mtume (s.a.w.w.) juu ya Imam Ali (a.s.). Kwa hiyo sisi tunamtambua Imam Ali (a.s.) katika misingi hiyo tu na siyo zaidi ya hapo,na tunatambua 354


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 355

katika Uislamu

kwamba yeye Imam Ali (a.s.) mwenyewe alisema kwamba yeye ni Mtumwa wa Muhammad Mustafa (s.a.w.w.). Na kwamba tunamfuata yeye kwa amri na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na anapotajwa jina lake yeye, mashia hufuatisha swala ya Mtume ambapo kunapingana na dhana hiyo potovu na kumtukuza zaidi nabii (s.a.w.w.). Tukirejea kwenye somo letu ni kwamba, kwa muda mrefu tumeshuhudia vikundi vya kiislamu vya Tabligh vikiendesha mikutano ya kuwavuta Wakristo, ili waingie Uislamu. Njia inayotumika ni kuchunguza maandiko ya Biblia ili kuonyesha kuwa manabii wote walileta dini moja tu inayofanana, nayo ni Uislamu. Anapotokea Mkristo kutoa hoja yake nje ya Biblia, haraka sana tunaikataa na kusisitiza kwa kumwambia “LETE ANDIKO! Lakini Waislamu hao hao, wanapochambua Uislamu, hawategemei ANDIKO tu, bali hujenga hoja zisizotokana na andiko lolote lile la Uislamu! Kwa mfano haya yote niliyoyataja humu kwa ushahidi, ni maandiko kutoka vitabu vyetu vya kutegemewa lakini tumeyafumbia macho! Kwa hiyo tutambue kwamba kazi ya Tabligh ni muhimu sana, lakini kazi hiyo ianzie kwetu wenyewe. ‘Kwanza tuufufue Uislamu kwa kurekebisha kasoro zote hizi nilizozitaja humu. Baada ya hapo ndipo tuwaendee wasio Waislamu na kuwaeleza Uislamu wa kweli. Si lazima kutumia Biblia katika Tabligh. Uislamu unazo hoja za kutosha kujitegemea, mradi tu wanaofanya kazi ya tabligh wawe tayari kuchukua mafunzo sahihi ya kutosha kuufahamu Uislamu. Nimeeleza hapo mwanzoni kwamba baadhi ya Wakristo wako tayari kuslimu lakini wanahoji kwa nini Uislamu uwe na madhehebu, iwapo ni Uislamu ule ule ulioletwa na manabii wote? Hili ni swali muhimu sana la hekima, lakini sijapata kusikia likijibiwa kiasi cha kumridhisha asiye Mwislamu! Ushahidi mkubwa uliopo ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuacha haya madhehebu tunayoyaona leo. Sasa kwa nini Mkristo akubali kuwa Mwislamu na kuyapokea madhehebu bila kuuliza swali?

355


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 356

katika Uislamu

Zaidi ya hayo, iwapo Waislamu tungefuata Uislamu wa kweli kwa uaminifu na kwa vitendo, wasio Waislamu wangetufuata wenyewe kwa kuvutiwa na maadili mema ya kiislamu! Tabligh kwa Wakristo siyo tu Waislamu kuikariri Biblia. Waislamu lazima tujenge maadili mema (Akhlaq) ya kiislamu, ambayo yatawavutia wasio Waislamu kuwa Waislamu. Tabia ya baadhi ya Waislamu kupiga ramli, kuandika kombe na kuwapa wasio Waislamu; pamoja na baadhi ya mashekhe wa misikiti kujengeana uhasama na kushutumiana kwa ubinafsi; vile vile baadhi ya mashekhe wametuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uzinifu, hali ya kuwa mashekhe hao ndio viongozi wa Swala za jamaa, ni tabia zenye kuwavunja moyo wasio Waislamu! Kwa kadri ya hukumu za Shia Ithna’asheri, Swala zinazoongozwa na watu kama hao ni batili. Sifa nyingine mbaya kwa baadhi ya mashekhe iliyoenea sana, ni ile ya ushirikina, ambao huwafanya wasio Waislamu kuamini kuwa Qur’ani inahusiana na uchawi na siyo Neno la Mungu peke yake! Hapa nataka kuonyesha kuwa tunaweza kufanya tabligh kubwa ya nadharia (mihadhara) lakini tusiporekebisha matendo yetu, hatutawafanya watu kuthamini Uislamu. Tutakuwa tunajenga na kubomoa hapo hapo. (Qur’ani 7:179).

ASILI YA TOFAUTI KATIKA IBADA KATI YA SHIA NA SUNNI Mara nyingi hutokea migongano misikitini, anapotokea Shia kuswali katika msikiti wa Sunni, na hasa pale anapoonekana Shia anafanya vitendo fulani, ambavyo ndugu zetu Sunni hawajavizoea kutokana na uchache wa Waislamu wa ki-Shia. (1) Udhu - Kishia na Kisunni Katika kutawadha, utatuona Shia tunanawa uso na mikono halafu tunapakaza maji kichwani (sehemu tu ya kichwa) na pia tunapakaza sehemu ya 356


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 357

katika Uislamu

miguu - basi. Ndugu zetu Sunni wao huosha uso na mikono na miguu pia, na kupaka maji kichwa chote. Kusukutua na kuosha pua na masikio ni sunna kwa Shia na Sunni. Jambo la maana hapa tutajadili usahihi wa matendo hayo kwa kadri ya Sunna na Qur’ani. Nimetangulia kueleza huko nyuma, kuwa sisi Shia hatuna migongano miongoni mwetu juu ya matendo mbali mbali ya ibada au dini kwa ujumla kwa sababu Ahlul-Bayt (a.s.) walifafanua kila jambo baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. Miongoni mwetu wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) dunia nzima, ni vigumu kukuta tofauti za kuhitilifiana, labda uwe ni upotofu binafsi wa mtu au watu. Nina maana kwamba ninaweza kutoa ushahidi kutoka mafunzo ya Ahlul-Bayt (a.s.), lakini nasita kufanya hivyo kwa sababu hoja hizo hazitatosheleza na kuwaridhisha ndugu zetu Sunni. Kwa hiyo nitatumia Hadithi kutoka vitabu vinavyotegemewa na Sunni pamoja na Qur’ani. Ningependa nianze na maelezo ya Qur’ani juu ya udhu, (Qur’ani 5:6). Mimi si mtaalamu wa tafsiri sahihi ya Qur’ani. Hata hivyo ninayo maelezo ya kutosha juu ya tafsiri sahihi ya Aya hii. Lakini kawaida yangu huwa sipendelei malumbano ya kutumia Aya za Qur’ani peke yake, kwa sababu leo hii watu wengi waliohitimu usomaji wa Qur’ani, wao wanaamini kuwa wamehitimu pia misingi ya kufasiri Qur’ani! Kwa hiyo si lazima mtu aache misingi yake ya kufasiri na akubaliane na misingi yangu. Hilo litaendelea kuwa tatizo miongoni mwa Waislamu ingawa Mtume (s.a.w.w.) alishatuonya juu ya kufasiri Qur’ani kwa njia potofu kama nilivyoeleza huko nyuma - katika tukio la Ghadiir Khum. (2) Usomaji wa Qur’ani 5:6 (Rejea Msahafu) – kuhusu Aya ya Udhu Wajuzi wa kanuni za usomaji wa Qur’ani watakuwa wanafahamu kuwa kuna aina mbili maarufu za usomaji wa Qur’ani. Usomaji wa kwanza ni ule wa kutia kasra laamu, yaani ‘Wa ar-julikum’ ambao unawajibisha kupaka kichwa na miguu kwa sababu miguu ina lazima moja na kichwa kwa hukumu ya kawaida ya lugha yaani (At-fu). Aina ya pili ni usomaji wa kutia 357


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 358

katika Uislamu

fatiha laamu, yaani ‘Wa ar-julakum’. Usomaji huu pia unawajibisha kupaka kwa ajili ya amri ya ‘Imsahu’ ambayo maana yake ni kupaka miguu kwa kuwa ni ‘Maf-ulun bihi’. Msimamo wetu Shia Ithna’asheri ni kwamba fatiha katika Lamu - ‘Arjulakum’ haiondoi maana ya kupaka. Ni kweli kwamba zipo Hadithi zinazodai - kwamba Mtume (s.aw.w.) aliosha miguu katika udhu, lakini Hadithi hizo zinapingana na kanuni sahihi za kufasiri Qur’ani. Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa, ‘Achaneni na Hadithi inayopingana na Qur’ani.’ Rejea:(1) Wasaa’il - Jz. 1, uk. 289 (2) Tafsir al – Kabir, Jz. 3, uk. 370 (3) Ibid - uk. 371 Tukirejea tafsir ya Qur’ani ya Sheikh Swaleh Farsy (kiswahili), tutaona kuwa neno ‘kuosha’ miguu limewekwa kwenye mabano: (kuosha miguu) kuonyesha kuwa kwa kanuni za lugha za tafsiri, siyo tafsiri yake sahihi bali ni mazoea ‘kuosha’. Ingekuwa kuosha ndiyo sahihi, neno hilo lisingebanwa bali lingeachwa wazi. Kwa hiyo tunakubaliana na Hadithi zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.w.) alipaka maji miguu. Anakaririwa bwana Ibaad Bin Tamim akisema kuwa, “Nilimwona Mtume (s.a.w.w.) akifanya udhu na kupaka maji miguu.” Rejea:(1) Sahih al-Bukhari (2) Musnad Ahmad Ibn Hambal (3) Sunan Ibn Abi Shaybah (4) Mu’jamul Kabir, cha at-Tabarani. Walioisimulia Hadithi hii katika vitabu hivyo, wamethibitishwa kuwa ni waaminifu. Rejea: Al’Asqalani & Al-’Isabah, Jz. 1, uk.193 na pia Tahdhib at-Tahdhib. Anakaririwa pia sahaba mmoja maarufu - Abdullah Ibn Abbas akisema kuwa, “Mwenyezi Mungu ameamrisha miosho miwili (yaani uso na mikono) na mipako miwili (yaani miguu na kichwa) Je, hamwoni kuwa katika Tayammum ameamrisha mipako miwili (badala ya miosho miwili) 358


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 359

katika Uislamu

na kuacha kupaka miguu na kichwa? Rejea:Muttaqi al-Hind. Kanzu’l-’Ummal, Jz. 5, uk.103 - Hadithi namba 2213. Musnad Ahmad Ibn Hambal, Jz. 1, uk. 108. Ninaposema kuwa Shia hatuoshi miguu, sina maana kuwa tunaingia na miguu michafu msikitini! Kwa kweli usafi wa msikiti, kwa Shia Ithna’asheri ni jambo linalopewa uzito mkubwa sana. Kwa kawaida kila msikiti wa Shia, mlangoni utakuta dimbwi la maji yasiyopungua lita 357 hivi. Kila anayeingia msikitini ni lazima kwanza aingize miguu yake humo na kujisafisha na najisi yoyote ambayo anaweza kuwa ameikanyaga njiani au sehemu ya kuvulia viatu kabla hajaelekea mlango wa msikiti kuingia ndani sehemu ya kuchukulia udhu. Baada ya hapo ndipo akaushe miguu yake hayo maji na kuchukua udhu. Eneo la kuchukulia udhu huwa ni tohara kutokana na tahadhari hiyo. Baada ya udhu ndipo mtu huingia msikitini. Msikiti ukinajisika kwa vitu vinavyoitwa najisi, ni lazima ufungwe na usafishwe kwanza ndipo utumike kwa kuswalia, vinginevyo Swala zitakuwa batili. Hizo ni kanuni za ‘Fiqh’ ya Kishia. Sharti la kuweka maji lita 357, ni kanuni ya ‘Fiqh’ pia. Kiasi hicho cha maji hata kikiingia najisi huchukuliwa kuwa maji hayo ni tohara mpaka labda rangi yake au ladha ibadilike, ndipo yatakuwa najisi na hivyo yabadilishwe. Hukumu hiyo hiyo inaruhusu kuchukulia maji ya kisima kuwa tahir hata kama watumiaji wa kisima watakuta humo kiasi kidogo cha choo cha binadamu kinaelea, mradi wachote choo hicho na kukitupa kisha watumie maji yake kutawadha tu, sio kwa kunywa, mantiki yake ni kama vile ambavyo maji ya mto hayanajisiki japo uione najisi inaelea. Usafi wa msikiti unasisitizwa kwa sababu kusujudu juu ya kitu najisi au juu ya vitu vilivyokatazwa (kama tutakavyoona huko mbele), kunasababisha Swala kubatilika. Kwa hiyo ndugu zetu Sunni wako huru kutumia misikiti ya Shia mradi wazingatie kanuni hizo. 359


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 360

katika Uislamu

(3) Kufunga au kutofunga mikono katika Swala: Nimetangulia kueleza kuwa Muawiyah ndiye aliyeamuru kufunga mikono katika Swala lakini si Waislamu wote waliotii amri hiyo. Rejea Sura ya 16 chini ya: ‘Watawala walidhibiti ijtihad katika madhehebu ya Sunni.’ Kwa kuwa asili ya kufunga mikono siyo Sunna ya Mtume (s.a.w.w.), sisi Shia hatufungi mikono na ni wajib kuishusha. Lakini kwa upande wa Sunni, hukumu ya bwana Shafi’i inasema kuwa ni hiari ya mtu kufunga mikono au kuacha, na ni pambo. Waislamu wa Afrika Mashariki ni wafuasi wa Shafi’i kwa hiyo sielewi kwa nini baadhi ya ndugu zetu Sunni mara nyingi wanadiriki hata kuwafukuza misikitini Shia kwa vile hawafungi mikono! pamoja na kwamba yapo madhehebu ya Sunni ambayo pia hawafungi mikono kwenye Swala, kama Maliki na Ibadhi! Tatizo kubwa kwa Waislamu walio wengi ni kwamba, hata wale ambao wanaelewa kuwa wao ni Sunni Shafi’i, hawajui baadhi ya hukumu za Shafi’i kuhusiana na mambo mbalimbali wanayotakiwa kutekeleza katika dini! Lakini utawakuta watu hao hao wanamwandama Shia asiyefunga mikono! (4) Kusujudu ni juu ya ardhi au popote? Ukiingia misikiti ya Shia Ithna’asheri utaona saa ya kuswali, mbele ya kila mtu kuna muhuri wa udongo au kipande cha mbao. Suala hili limeleta malumbano yasiyofaa kati ya Shia na Sunni. Sunni wanadai kuwa hivyo vidongo ni vijisanamu na tunavisujudia (Astaghfiru-llah!) kama miungu yetu! Kwa hakika hayo siyo kweli kwa sababu tunasujudu juu ya vidongo hivyo, kama kusujudu juu ya mkeka, hatuvisujudii, kwani ujinga wa kiroho wa ngazi hiyo, si jambo linalowezekana kwa mtu yeyote anayeitwa Mwislamu kwa wakati huu! Ukweli ni kwamba nitatoa Hadithi kadhaa zinazoonyesha kuwa kusujudu juu ya ardhi (udongo) ni bora kuliko vitu vyote vilivyoruhusiwa kusujudu juu yake wakati wa kuswali:

360


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 361

katika Uislamu

(a) Bwana Bayhaq amepokea Hadithi kwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, ‘Nimefanyiwa ardhi kuwa ni tohara na mahali pa kusujudia. Na popote unapomfikia mtu wakati wa kuswali, basi aswali hapo alipo.’ Rejea:(1) Sahih Bukhari - Jz. 1, uk. 86 & 113 (2) Sahih Muslim - Jz. 2, uk. 64 (3) Sahih (Sunan) Nasai, Jz. 2, uk. 32 (4) Sahih (Sunan) Abu Daud, Jz. 1, uk. 79 (5) Sahih Tirmidh - Jz. 2, uk. 114 (6) Sunanul Kubra, Jz. 2, uk. 433 na 435 Zipo Hadithi nyingi juu ya maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu ubora wa kusujudu juu ya udongo kwa mfano pale anapokaririwa akisema kuwa:- “ ........ Inna Afdhal Ma Tusjadu Alayhi Al-Ardhu”. (Kilicho bora cha kusujudia juu yake ni ardhi). Kutokana na maelezo hayo ni wazi kwamba kusujudu juu ya ardhi ni bora zaidi. Lakini kama tunavyofahamu, sisi wakazi wa mjini si rahisi kila mmoja wetu akasujudu juu ya ardhi kwa sababu mbali mbali. Kwanza ardhi ya mjini au hata vijijini penye msongamano wa watu siyo ‘tohara’, yaani imenajisika. Kwa upande mwingine wakazi wa miji mikubwa huishi maghorofani milele. Ndiyo maana sisi Shia Ithna’asheri tukatengeneza vidongo maalumu vinavyoitwa Turba ili tuvitumie kusujudia na tupate huo ubora wa Swala zetu. Mara nyingi vidongo hivyo hutengenezwa kutokana na udongo wa Karbala ambao ni bora kusujudia kuliko udongo wa sehemu yoyote ile. Ubora wa udongo huo unatokana na tukio lililotokea hapo la kuuawa pale kishahidi kwa Imam Husein (a.s.) kama nilivyoeleza huko nyuma. Mfano wa ubora wa udongo wa Karbala ni kama ubora wa kuswali katika msikiti wa Mtume (s.a.w.w.) Madina au Makka, tofauti na misikiti yote duniani, au ubora wa maji ya kisima cha Zamzam kuliko visima vyote vya maji duniani n.k. Nafasi haitoshi kueleza kirefu lakini suala la msingi ni kwamba si lazima kutumia udongo wa Karbala 361


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 362

katika Uislamu

bali udongo wowote uliotoharika unafaa. Sababu ya pili ya Shia Ithna’asheri kutumia udongo misikitini au safarini, ni tahadhari yetu kuepuka kusujudu juu ya vitu vilivyokatazwa kwa kadri ya kanuni za ‘Fiqh’. Hukumu yenyewe ni kwamba inaruhusiwa kusujudu juu ya ardhi (udongo) pamoja na juu ya vitu vyote vinavyostawi katika ardhi ambavyo haviliwi wala kuvaliwa mwilini mradi viwe tohara. Maana yake ni kwamba kama angetokea mtu akatengeneza mkeka kwa mfano, kwa makuti ya mnazi au mtende jike, mkeka huo usingefaa kusujudia. Majamvi yaliyotengenezwa na mali ghafi japo kidogo ya kitu kinacholiwa, pia hayafai. Mabusati ya pamba hayafai kwa sababu pamba inavaliwa mwilini na pia mbegu za pamba ni chakula. Miswala iliyotengenezwa kutokana na vitu visivyoliwa inafaa mradi isiwe imepakwa rangi. Kwa hiyo tutaona kuwa, hata mabusati yanayowekwa misikitini siku hizi, hasa yale ya viwandani, hatuwezi kujua vitu gani viliyatengenezea! Kwa tahadhari ya yote hayo, ndiyo maana sisi Shia Ithna’asheri tunatumia hiyo mihuri ya udongo au ya mbao za miti isiyoliwa kwa kusujudia katika Swala zetu. Kusujudu juu ya sakafu ya ‘simenti’ kunakatazwa pia kwa sababu kanuni ya kusujudu kwenye udongo ni kwamba udongo huo usiwe umechomwa moto. Katika utengenezaji wa saruji, mali ghafi kubwa ni kuchoma chokaa kwa moto mkali sana kama hatua mojawapo ya utengenezaji saruji. Hata hivyo, Marjaa wa sasa hivi, Ayatullah Siistanii, anaruhusu kusujudu juu ya sakafu hiyo, alimradi iwe haina najisi. Waliokataza ni viongozi wa kabla yake. Iwapo Shia Ithna’asheri hana muhuri wa udongo au mbao anaweza kuchukua jani la mti usioliwa, la kutosha kusujudia kwa paji la uso, na akasujudia, kuliko kusujudia sehemu au mahali ambapo hakuna uhakika kama ni tohara (tahir) au hapana. Pamoja na hayo, zipo Hadithi pia zinazoonyesha kuwa masahaba waliruhusiwa kusujudu juu ya nguo zao au vilemba kutokana na joto kali la jangwani na siyo kwa sababu nyinginezo. Kwa 362


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 363

katika Uislamu

hiyo iwapo ardhi ina maji au matope ni lazima mtu asujudu hivyo hivyo bila kuweka kitu cha kumzuia asichafuke na matope. (5) Kukusanya Swala mbili za faradhi: Sisi Shia Ithna’asheri tuna hiari ya kuswali Swala ya Adhuhuri na Laasri, moja baada ya nyingine bila kusubiri katikati. Hivyo hivyo kwa Swala za Magharibi na Isha. Suala hili linawashangaza ndugu zetu Sunni ambao wanaona kuwa tumepotea au labda tunakosea! Kwa kawaida hakuna tendo lolote katika Shia ambalo tunatenda bila kuzingatia Qur’ani au Sunna. Zaidi ya hayo tufahamu kuwa, kanuni za mambo ya ‘wajibu’ hazibadiliki labda watu watie upotofu kama tulivyoona huko nyuma. Kwa hiyo tukirejea wakati wetu huu, tutaona kuwa madhehebu zote za Waislamu zinakubaliana kuwa, inajuzu kuunganisha Swala za Adhuhuri na Laasri katika ibada ya Hijja huko A’rafa. Tendo hili hujulikana kama ‘Jamuu Tak-diimi’. Vile vile madhehebu zote zinakubaliana kuhusu kuunganisha Swala za Maghribi na Isha huko Muzdalifa (Makkah) katika ibada hiyo hiyo ya Hijja. Tendo hilo huitwa ‘Jamuu Taakhiri’. Huo ni ushahidi wa kwanza wa kuthibitisha uhalali wa kuunganisha Swala katika Sharia, kwa sababu kama nilivyosema, kanuni za ‘Fardh’ hazibadiliki au kutofautiana kwa kutegemea mahali tofauti. Fardhi ya Makkah ni fardhi ya ulimwengu wote. Na ndio maana haiwezekani sisi Waislamu wa Afrika Mashariki tukaamua kuanzisha Swala yetu ya Adhuhuri ya rakaa 8 mathalan! Ushahidi wa pili ni tafsiri sahihi ya Qur’ani 11:114 kuhusiana na nyakati za kuswali. Maneno ya Aya hiyo yapo hivi: “Wa aqimis-Swalata Tarafan-Nahari wazulafan minal-laili.” ‘Na simamisheni Swala katika sehemu mbili za mchana na nyakati za usiku.’

363


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 364

katika Uislamu

Aya hii inaonyesha kuwa nyakati za Swala ni tatu. Kwa kulingana na maneno ya Aya hiyo, ni kwamba tumeamriwa kusimamisha Swala katika sehemu mbili za mchana - nazo ni Subhi peke yake; sehemu ya kwanza, halafu Adhuhuri pamoja na Laasri, sehemu ya pili. Aya inaongeza kuwa: na nyakati za usiku - kwa maana ya Magharibi na Isha. Ushahidi wa tatu ni Hadithi aliyoipokea bwana Muslim toka kwa Ahmad Yunus toka kwa Abu Zubairi toka kwa Said bin Jubair toka kwa Ibn Abbas kwamba: “Mtume (s.a.w.w.) aliswali Adhuhuri na Laasri zote pamoja huko Madina bila ya udhuru wowote.” Abu Zubair anasema kuwa alimwuliza Said kwa nini Mtume (s.a.w.w.) alifanya hivyo? Akajibu kuwa hata mimi nilimwuliza Ibn Abbas akanieleza kuwa Mtume (s.a.w.w.) alitaka asimpe taabu mtu yeyote katika umma wake. Hata hivyo si lazima kuunganisha Swala mbili mbili. Kama mtu ana nafasi ya kutenganisha Swala anaruhusiwa. Iwapo mtu mwingine ana udhuru anaruhusiwa kuuganisha ili awahi shughuli zake. Maana yake ni kwamba nyakati za Swala zinazounganishwa, zinaingiliana yaani ni pana. Hata kwa maelezo ya urefu wa kivuli cha mtu ili kupata wakati wa Swala, utaona kuwa Swala ya Adhuhuri inaingiliana na Laasri, kwani hata hivyo wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.) hazikuwepo saa za kuonyesha dakika na sekunde kama hivi leo! Maelezo hayo ni ya msingi sana kwa sababu mara nyingi wapinzani wa Uislamu wamedai kuwa Uislamu hauendi na wakati. Madai hayo yanatokana na matendo wanayoyaona ambayo kimsingi siyo Uislamu kama nilivyoeleza huko nyuma kwa kirefu. Mtu asiye Mwislamu akiangalia nyakati za Swala tano za Waislamu, ataona kama kwamba nyakati hizo hazimwezeshi Mwislamu kufanya shughuli nyingine kwa nafasi, kwa jinsi Swala zinavyoongozana! Lakini Mwislamu kapewa uhuru wa kuuganisha baadhi ya Swala au kuzipunguza rakaa zake akiwa safarini. Yote hayo ni kumrahisishia Mwislamu katika ibada zake. Lakini tukifuata Uislamu wa ‘Dogma’ bila shaka tutaona Uislamu ni mgumu. 364


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 365

katika Uislamu

Siku hizi wafanyakazi wengine hutumia muda mrefu kazini kiasi ambacho kuunganisha Swala kungewasaidia kupata ruhusa ya kuswali mara moja mchana badala ya ruhusa mbili zinazopoteza muda mrefu zaidi. Hata mkulima anaweza kutumia muda wake vizuri kwa kuswali kwa wakati mmoja mchana. – Cha ajabu ni kwamba, mfanyakazi ama mkulima huyo, utamuona jioni anaswali kadhaa nyingi kwa wakati mmoja! Je, hajaunganisha Swala hapo?. Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu aliufanya Uislamu kuwa dini nyepesi lakini Uislamu wa kweli hatujaufahamu bado. Tumebeba Uislamu wa kiutamaduni yaani wa urithi! (6) Maulidi na sherehe zake za Dufu: Shia Ithna’asheri husoma maulidi ya Mtume (s.a.w.w.) pamoja na maulidi ya Ahlul-Bayt wake (a.s.) wote 13; na ndiyo maana sisi Shia Ithna’asheri lazima tuhakikishe tarehe ya kuandama kwa kila mwezi wa kiislamu, ili tarehe zinazohusika na matukio muhimu ya kiislamu ziwe sahihi. Ndugu zetu Sunni wao huadhimisha maulidi ya Mtume (sa.w.w.) peke yake. Sisi Shia huadhimisha pia na vifo vya watukufu hao. Katika kusoma maulidi, sisi Shia Ithna’asheri hatukubaliani na kupiga dufu na zumari kwa sababu vifaa hivyo ni vyombo vya muziki vya Waarabu! Nimetangulia kueleza huko nyuma kwamba Uislamu wa leo umechanganyika kwa kiwango kikubwa na mila mbali mbali, kutegemea wanakoishi Waislamu wanaohusika. Waarabu walipotuletea Uislamu, walituletea na ngoma zao za utamaduni yaani dufu. Dufu siyo dini hata kama zinapigwa katika ‘Qasida’ zenye maneno ya kidini! Kama tutahalalisha dufu ya Mwarabu; hakuna sababu za msingi kwa nini tusihalalishe ngoma ya mdundiko, ilimradi wacheza mdundiko waimbe Qasida! Nataka kusisitiza kwamba Dufu ni ngoma ya utamaduni na mila ya Waarabu. Kama kila Waislamu wataamua waingize ngoma zao katika dini, sijui tutakuwa na Uislamu wa namna gani! Katika wakati huu wa maonyesho ya mikanda ya video, utawaona Waarabu katika sherehe zao za kimila wamevaa makanzu yao na majoho, huku 365


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 366

katika Uislamu

wanacheza ngoma zao za utamaduni, yaani dufu na nai (zumari), na mara nyingine wanarusha panga zao. Tofauti ni kwamba hawasomi Qasida! Katika ngoma hiyo ya Waarabu sisi huku tunaongeza Qasida na kuifanya sehemu ya dini! Uhalali wake uko wapi? Lakini ukichunguza makabila mbali mbali hapa Afrika Mashariki utaona kuwa Waislamu wanatumia aina mbali mbali za dufu, zenye kufanana na umbile la ngoma zao za jadi wanazotumia katika utamaduni wao wa kimila. Kwa mfano Wahaya na Waganda hutumia dufu kubwa sana zenye milio ya kusikika hadi umbali wa maili tano! Wakati zikipigwa dufu hizo, Waislamu hasa vijana wenye nguvu, hujipanga safu na kupiga magoti, na kucheza kwa kujirusha na kujitupa huku na kule, hadi mwili mzima kulowa jasho na huku wanasoma Qasida! Ngoma za utamaduni za Wahaya na Waganda, ni kubwa vile vile, na mlio wake husikika mbali sana; na uchezaji wake ni wa kutumia nguvu. Hivi ndivyo utamaduni unavyoingiliana na dini! Makabila ambayo ngoma zao za utamaduni ni ndogo na za mikononi, utawaona Waislamu wa makabila hayo wanatumia dufu ndogo za mikononi. Baadhi ya nchi zenye Waislamu wengi, kama Indonesia, kutokana na maendeleo yao makubwa ya kiuchumi, utakuta inauzwa mikanda mingi ya Qasida - ambazo zimesomwa kwa kutumia vifaa kamili vya bendi za kawaida za muziki! Maana yake ni kwamba katika nchi hizo, Qasida ya bendi ya muziki inaweza kuchezwa pengine hata msikitini! Kama tutakataa Qasida kama hizo zisisomwe msikitini, kwa nini turuhusu Qasida ya dufu na nai? Kwa kigezo gani? Waislamu wengine hudai kuwa Dufu ni halali eti kwa sababu wanawake wa Madina walimpokea Mtume (s.a.w.w.) kwa dufu! Mimi binafsi sijathibitisha madai hayo kihistoria, lakini tufahamu kuwa wakati huo 366


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 367

katika Uislamu

Uislamu ndio ulikuwa unachipua, kwa hiyo kibusara usingetegemea Mtume (s.a.w.w.) apige marufuku utamaduni wote unaopingana na dini, hata kabla hajawafundisha watu misingi yote ya dini! Zaidi ya hayo hata hivi leo katika kazi zetu za ‘tabligh’, iwapo unataka watu fulani wawe Waislamu, lakini ukawakuta wanapendelea sana kunywa pombe, huwezi kuwakataza pombe siku moja, bali hatua kwa hatua. Waislamu wengi hivi leo wanapendelea dufu kwa sababu dufu inafanana na ngoma zao za utamaduni zinazotumika katika sherehe mbali mbali kimila. Kwa hiyo tutaona kuwa ngoma na muziki katika Uislamu ni haramu. Asili ya muziki wa kisasa ni ngoma za asili za utamaduni. Nina maana kuwa katika jamii ya watu walioendelea (Kidunia), huvumbua vyombo vya kisasa vya kucheza muziki. Lakini jamii ya watu wanaoendesha maisha yao ya kiasili, hutumia ngoma na vifaa vya asili katika sherehe zao. Kwa lugha ya Qur’ani, vyote hivyo ni muziki, pamoja na kuimba kwa kubadili badili sauti. Yote haya katika Uislamu huitwa ‘Ghina’ na ni haramu kwa hukumu ya Shia Ithna’asheri. Isipokuwa aina fulani za muziki laini wa vyombo vitupu, au muziki wa kijeshi, au baadhi ya muziki unaoambatana na matangazo ya redio au televisheni, hasa taarifa za habari; huo unaruhusiwa, hasa muziki usio na waimbaji. Asili ya kwanza ya uharamu wa muziki na ngoma ni pale ambapo alipofariki Nabii Adam (a.s.). Mtoto wake muovu aliyeitwa Qa’abil (Cain) pamoja na Iblis walifurahi sana siku hiyo. Walikutana mahali fulani na kubuni vifaa vya kupiga kama ngoma, ili kusherehekea kifo cha Nabii Adam (a.s.)! Vifaa vyote vinavyotumiwa katika muziki siku hizi au kusherehekea sherehe mbali mbali asili yake ni hiyo na ni haramu. Maelezo haya yalitolewa na Imam Jafar Sadiq (a.s.) ambaye ni mmojawapo wa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.). Tukirejea tafsiri sahihi ya Qur’ani tutaona haya: “........kwa hiyo jizuie na uchafu wa masanamu na maneno machafu (yasiyo na faida).” (Qur’ani 22:30). Katika Aya hiyo neno la msingi ni ‘Zuur’ mwishoni mwa 367


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 368

katika Uislamu

Aya hiyo. Neno hilo katika lugha ya Qur’ani lina maana kadhaa na mojawapo ni upotofu na muziki. Kwa tafsiri ya Imam Jafar Sadiq (a.s.) ni kwamba, ‘uchafu wa masanamu’, maana yake ni michezo ya bao, draft, karata na chess; na maneno machafu (yasiyo na maana yenye faida), maana yake ni muziki. Katika Aya nyingine (Qur’ani 31:6) neno ‘Lah’wa’ lina maana ya kitu chochote kinachoelekeza mawazo ya binadamu mbali na lengo la kuumbwa kwake, yaani vitu vinavyomsahaulisha mtu asimkumbuke Mwenyezi Mungu na amri zake, kwa mfano mtu kuzama katika kusoma Hadithi za kubuni au Hadithi za mapenzi na maongezi yasiyo na faida pamoja na muziki. Kama tujuavyo au tuonavyo siku hizi katika video na televisheni, miziki mingi na ngoma, vyote vinalenga katika kuamsha au kufufua hisia za upotofu kwa binadamu. Mfano mzuri ni kwamba mikanda michafu ya video, hugombaniwa na kununuliwa kwa bei kubwa, kuliko kwa mfano, mkanda wa mawaidha ya dini. Rejea: Tafsir as-Safi, Al-Kafi, na Wasailu sh-Shi’ah, juu ya tafsiri sahihi ya Qur’ani 31:6. Aya ya Qur’ani 25:72 nayo inasisitiza uharamu wa muziki (ngoma): “Na wale ambao hawashuhudii uongo, na wanapopita penye upuuzi hupita kwa heshima.” (Qur’ani 25:72). Katika Aya hii, maneno ‘Zuur’ na ‘Laghw’ yametumika na yanafasiriwa kuwa, ‘Usisikilize muziki’. Kati ya maelezo (tafsiri) ya Maimamu wa Shia, wamesisitiza usahihi wa tafsir hiyo katika Aya hiyo ya Qur’ani. Kwa upande wa Hadithi, anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa:- “Umma wangu utakapoambukizwa tabia 13, watashukiwa na balaa, tabia hizo ni: (1) Wakati ngawira itachukuliwa kuwa mali binafsi ya mtu. (2) Dhamana (amana) itachukuliwa kama ngawira ya vita. (3) Sadaka itachukukiwa kama hasara. (4) Mume atamtii mke wake na kumuasi mama yake. (5) Mume atamkarimu rafiki na kuwa bahili kwa baba yake. (6) Sauti zitapanda misikitini. (7) Mtu ataheshimika kwa uovu wake. 368


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:24 PM

Page 369

katika Uislamu

(8) Kiongozi wa watu atakuwa mbaya kuliko watu wote. (9) Wanaume watavaa hariri. (10) Watu watamiliki wasichana waimbaji na wacheza muziki (11) Watu watamiliki vyombo vya muziki (12) Watu watakunywa vileo (pombe). (13) Uzinifu utaongezeka.” Katika Hadithi nyingine anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, katika dalili za kukaribia Kiyama ni kwamba: “Watu watapuuzia Swala tano au hawataswali kwa nyakati zake na wataegemea zaidi matakwa ya nafsi zao. Siku hizo, watakuwepo watu watakaosoma Qur’ani kwa manufaa yao ya kidunia na wataifanya Qur’ani kama muziki wa kuwaburudisha (Kusoma Qur’ani huku watu wanaongea mambo mengineyo au wanafurahia tu sauti ya msomaji)! Watakuwepo watu watakaosoma dini kwa ajili ya ufakhari wa kupata sifa na utajiri (Kama tuonavyo leo ambapo baadhi yetu husoma dini ili wawe wahutubu wazuri wa kuvuta watu na kulipwa kwa kazi hiyo). Watoto haramu wataongezeka na watu wataimba Qur’ani (wataisoma kwa madaha nje ya sheria zake za usomaji). Na watatamani vyombo vya muziki. Hawatapenda kuamrisha mema na kukataza maovu. Hawa wote wataitwa wachafu katika Ufalme wa Mwenyezi Mungu.” Ushahidi huo wa mafunzo ya dini, ndio unaotufanya sisi Shia Ithna’asheri tukatae dufu na muziki, iwe ni katika maulidi au popote pale. Jambo lingine tunalolikataa katika maulidi ni mchanganyiko wa wanaume na wanawake bila kizuizi. Amri ya kutochanganyika wanaume na wanawake imo hata katika Biblia (Zakaria;12:12). Amri hii haina maana kuwa inatosha wanawake wajitenge tu na wanaume, hali ya kuwa wanaonana, na kuja kwenye kinara, eti kusoma Qur’ani au mlango wa maulidi. Maana ya amri hii ni kwamba, kwanza wanawake wanatakiwa wawe na mavazi rasmi ya stara (Hijab), (Qur’ani 24:30-31), na pia wasionyeshe mapambo yao (Qur’ani 33:32-33), na zisisikike sauti zao (zisiwe juu) wala wasionane na wanaume bila kuwepo pazia kati yao (Qur’ani 33:53). 369


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 370

katika Uislamu

Ingawa baadhi ya Aya hizo zilishuka kwa ajili ya wake zake Mtume (s.a.w.w.), lakini kusudio lake zima ni wanawake wote Waislamu. Katika Aya hizo tutaona kuwa si halali kwa akina mama kusimama mbele ya wanaume na kusoma maulidi au Qur’ani, kama vile tunavyoona siku hizi. Wanawake wawe na maulidi zao. Kwa hiyo msimamo wa Shia Ithna’asheri ni kwamba Maulidi yanayosomwa bila kuzingatia kanuni hizi, siyo halali kuhudhuria. Maulidi yanayofaa ni yale ambayo hakuna upigaji dufu na kwamba wanawake wamewekewa pazia au ukuta na hawaonekani kwa wanaume, wala hawahusiki pia na kisomo chochote bali ni wasikilizaji tu. Vile vile kama kuna usomaji wa Qur’ani, miiko yake izingatiwe. (7) Kuosha na kukafini maiti na Talqin: Taratibu za Shia Ithna’asheri za kumuosha maiti zinatofautiana kidogo na zile za ndugu zetu Sunni lakini iwapo maiti wa ki-Shia ataoshwa ki-Sunni, inaswihi kwa Shia sio lazima aoshwe tena. Baadhi ya tofauti muhimu ni kwamba kwa upande wa Shia Ithna’asheri hairuhusiwi kumkamua maiti ngama kwa sababu mtu anapokufa, maiti yake inaumia kiroho japo watu walio hai hawalijui hilo! Isitoshe kama kukamua ngama ni kumwondoa kabisa uchafu, mbona mtu huswali hali ya kuwa amebanwa na choo au mkojo bila Swala yake kubatilika ingawa ni ‘Makruhu kuswali katika hali hiyo.’ Vile vile hairuhusiwi Mwislamu kuosha maiti ya Mwislamu kwa kulipwa ujira. Iwapo mtu atamuosha maiti kwa ujira hukumu yake ki-Shia ni sawa na kwamba maiti huyo kazikwa bila kuoshwa! Sababu kubwa ni kwamba ni wajibu kwa Waislamu wote wa mji au kijiji kinachohusika, kumwosha na kumzika Mwislamu mwenzao. Iwapo atazikwa bila kuoshwa ni dhambi kwa Waislamu wote wa hapo. Kwa hiyo siyo hiari kuosha maiti bali ni wajibu kama vile kufunga Ramadhani au kuswali Swala tano.

370


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 371

katika Uislamu

Swala ya maiti inatofautiana kidogo kati ya Shia na Sunni, bali pia hata katika kuzika, usomaji wa ‘Talqin’ pia unatofautiana kama nilivyotangulia kueleza katika Sura ya 14 chini ya: ‘Mifano ya kuifasiri vibaya Qur’ani.’ Tatizo ni kwamba iwapo unafuata Uislamu ulio tofauti na ule alioamrisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ufahamu kuwa imani (itikadi) zako pia zitakuwa potofu. Kwa hiyo tufahamu kuwa, katika ‘Talqin’ huyo maiti roho yake hurejeshwa mwilini mwake ili aulizwe maswali yatakayothibitisha kama Uislamu wake umekamilika au hapana. Majibu ya kila marehemu, yatategemea alivyoamini katika itikadi zake hapa duniani muda wa uhai wake. Kwa hali hiyo, itikadi za Shia na Sunni zinatofautiana kwa kadri ya maelezo mengi yaliyotangulia katika Sura za nyuma. Ndiyo maana ‘Talqin’ nazo zinatofautiana. (8) Kusoma hitima na kuzuru makaburi: Katika madhehebu ya Shia, kumsomea khitima marehemu ni sawa. Hata hivyo tufahamu kuwa maana nzima ya khitima ni kwa ajili ya thawabu kwa marehemu. Waislamu wengi hupendelea kupika chakula kama sadaka. Utaratibu huu unafaa lakini unakosewa kwa sababu, unapotoa sadaka yoyote ile, uwape hiyo sadaka wanaostahili. Katika khitima zetu au sadaka utaona wengi wetu tunawaalika watu mashuhuri wasio na shida, tunawaandalia chakula wakati ambapo watu kama hao pengine chakula walichozoea kula ni bora kuliko vyakula vyetu! Matokeo yake baadhi ya hao waalikwa huondoka wakitoa kauli za kuonyesha kuwa labda pilau ilikuwa na nyama kidogo au viungo vichache! Hali hiyo hupunguza sana thawabu zilizokusudiwa kwa marehemu, ukilinganisha na vile ambavyo chakula hicho wangepewa watoto yatima au kundi la mafukara ambao hawajui hata harufu ya ugali na chumvi. Zaidi ya hayo tufahamu pia kuwa zipo njia nyingi za kumpatia thawabu marehemu, kama vile kununua misahafu na kuwapa watoto katika vyuo vyetu. Au kununua majamvi na kuyaweka kwenye misikiti yenye upungufu huo. Au kupanda miti ya matunda njiani sehemu za wazi na kuitunza hadi izae matunda, kuwalisha wapita njia. Yote haya unaweza kuyafanya 371


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 372

katika Uislamu

kwa kunuia thawabu kwa marehemu wako. Vile vile njia nyingine ya kumpatia marehemu wako thawabu nyingi ni kumsomea Qur’ani mara nyingi hata kwa kuajiri mtu afanye kazi hiyo. Tusiweke mkazo kwenye kupika pilao peke yake kama njia pekee. Kuhusu faida ya kuzuru makaburi ya ndugu zetu ni kwamba anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akiwaambia masahaba kuwa, “Watuzeni marehehmu wenu kwa sadaka na dua. Hakika roho za waumini hushuka mbingu ya kwanza siku ya Ijumaa na kupiga kelele kwa sauti ya kuhuzunisha na kulia wakisema, ‘Enyi watu wangu, watoto wangu, baba na mama yangu na jamaa zangu tuoneeni huruma na Mwenyezi Mungu Atakuoneeni huruma, kwani mali hiyo mliyokuwa nayo ilikuwa mikononi mwetu. Mateso na hesabu tunafanyiwa sisi lakini faida yake wanafaidi wengine.” Na kila marehemu roho yake humpigia kelele jamaa yake au jamaa zake, “Tuonee huruma japo kwa kutoa sadaka ‘dirham’ moja au kwa kutoa mkate kumpa masikini, au kwa nguo kumvisha maskini asiyekuwa na nguo na Mwenyezi Mungu atakuvisha nguo za ‘Janah’ (peponi).” Baada ya hapo Mtume (s.a.w.w.) akalia sana na masahaba wakalia. Baadaye akasema, “Hao ni ndugu zenu katika dini (imani) sasa wamekwishageuka kuwa udongo na mifupa imesagika, baada ya kuishi humu duniani kwa raha na furaha, basi wanapiga kelele na kusema, ‘Ole juu yetu, laiti katika uhai wetu tungalitoa sadaka na kutenda mazuri kwa (pesa zetu) hizo tulizokuwa nazo, katika njia ya Mwenyezi Mungu, leo tusingelikuwa wahitaji kwenu.’ Baada ya majonzi yao hayo ya kukosa msaada, wanarejea wakiwa wanyonge na huzuni wakipiga kelele, ‘Haraka toeni sadaka kwa marehemu wenu.” Inafaa kwa Mwislamu kila wiki, hasusan siku ya Alhamisi, awakumbuke marehemu wake kwa kufika kwenye makaburi yao. Hii ni Sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwaamrisha masahaba wake kuzuru makaburi na kuwafundisha dua za kusoma huko pamoja na sura za Qur’ani zinazofaa kuwasomea watu wa makaburini. 372


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 373

katika Uislamu

(9) Kufanya ibada za makelele misikitini: Siku hizi sio tatizo tena kununua kipaza sauti chenye nguvu yoyote ile. Hali hii imewezesha misikiti mingi kununua vipaza sauti ili kwenda na wakati. Lakini tufahamu kuwa ibada zinazoruhusiwa kusoma kwa sauti (hata bila kipaza sauti) msikitini, ni zile Swala za jamaa za sauti, ‘takbir’ za sikukuu za Idd, hotuba za Swala za Ijumaa na Swala za Idd; na msomaji mmoja wa Qur’ani wakati wengineo wote wanamsikiliza msomaji kwa unyenyekevu. Sauti ya kutoka nje iwe ni ya adhana tu. Kuna tabia ya siku hizi ya wanadi Swala mbali mbali kuamka saa kumi na nusu usiku na kuanza kutoa hotuba kwa sauti kubwa eti kuamsha watu! Maneno mengi kwenye hotuba zao hayana lazima ni sawa na makelele tu, wao wanadi swala tu kwa maneno ya kuamsha watu, basi! Kwa upande wa Hadithi, nimeeleza katika sura hii kifungu ya 5 kwamba Mtume (s.a.w.w.) alitaja kupiga makelele misikitini kuwa ni tabia mojawapo itakayosababisha Umma kushukiwa na mabalaa. Tabia hii ni miongoni mwa tabia mbaya 13 alizozitaja Mtume (s.a.w.w.). Rejea Na. 5. Kupiga makelele misikitini ni pamoja na kusoma ‘Dhikr’ katika vipaza sauti badala ya kila mtu kusoma kimya kimya peke yake (Qur’ani 7:205). Kuitangaza Swala katika vipaza sauti haifai kwa sababu walio ndani ya msikiti wanamsikia Imam. Na kama msikiti una ghorofa kwa wanawake au sehemu iliyojitenga ya wanawake, inatosha kupunguza sauti iwe ya kusikika tu kwa wanawake, kupitia kipaza sauti cha ndani kwa ndani kwa kutumia kinasa sauti cha radio kaseti, kinachonasa sauti ya mbali sana hata iwe ndogo. Wanaotaka kuhutubia kwa vipaza sauti watayarishe mihadhara nje ya misikiti au wajengewe kumbi za kufanyia mikutano ya kidini. Kwa kweli hata hizo adhana siku hizi zinaanza kuvuka mipaka. Wakati huu zinapatikana jedwali za nyakati za Swala. Kwa nini pale misikiti ilipokaribiana, usitumike msikiti mmoja kutoa adhana kwa wote badala ya kila msikiti na adhana yake? Tena kwa kupishana muda au kuingiliana adhana wakati huo 373


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 374

katika Uislamu

huo! Je, hiyo sio fujo? Huko Indonesia katika mji wao mkuu wenye watu milioni 10, karibu kila mtaa una msikiti kwa sababu misikiti hujengwa na serikali hasa mijini. Miaka ya hivi karibuni ilibidi serikali ipige marufuku adhana za vipaza sauti kwa sababu saa ya kuswali, mji mzima unapigwa radi za vipaza sauti! Hali hiyo inawatesa sana wagonjwa wa mioyo na shinikizo la damu n.k. Kwani katika miaka ya nyuma tulikuwa hatusali bila vipaza sauti?

10) Kumshuhudia Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) katika Adhana na Iqamah: Sisi Shia Ithna’asheri tunamshuhudia Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) katika Adhana kama Sunna tu, na siyo fardhi katika Adhana. Tunafanya hivyo kujitambulisha kama wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.), na kuwakumbusha Waislamuu juu ya cheo cha Imam Ali (Qur’ani; 5:55),3 lakini Shia yeyote atakayejenga imani kuwa maneno hayo ni sehemu ya fardhi katika adhana, basi adhana yake itabatilika. (11) Qur’ani ni moja tu – (Qur’ani 41:41-42; 15:9): Wapo maadui zetu wanaodai eti sisi Shia tuna Qur’ani yetu tofauti! Madai hayo ni uzushi na uzandiki kwa sababu taasisi kadhaa za Shia Ithna’asheri zimekuwa zinagawa misahafu karibu kila mwaka, na misahafu hiyo hutumika na Waislamu wote, lakini bado hatujapokea malalamiko kwamba misahafu yetu hiyo tuliyotoa ina kasoro yoyote! Pamoja na hayo, misikiti yetu ipo wazi kwa Mwislamu yeyote anayetaka kuona misahafu tunayotumia misikitini mwetu. Mwisho ifahamike kuwa madhehebu ya Shia Ithna’asheri haihusiani na Shia Ismailia. Ni vitu viwili tofauti. Wala hatuna uhusiano na Kadiani wala Bohora wala Mawahabi. Sisi ni wafuasi wa Kizazi cha Mtume (s.a.w.w.). 3 Hakika kiongozi wenu khasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na wale ambao wameamini; ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka hali ya kuwa wamerukuu (wameinama). 374


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 375

katika Uislamu

Vilevile hatuna uhusiano na Answari Sunna. Isipokuwa sisi Shia Ithnasheri tunavyo vitabu vikubwa kama msahafu, vya mkusanyiko wa dua zitokanazo na Ahlul-Bayt (a.s.). Vitabu hivyo ni kama Mafatihul Jinan na Al-Sahifat Sajadiyya au Jaushan Kabir. Baadhi ya ndugu zetu Sunni hudhani vitabu hivyo ni Qur’ani! Atakayedai kwamba Shia wana Qur’ani yao, basi mwambie akuonyeshe walau nakala moja ya Qur’ani hiyo badala ya maneno matupu! Bila ya hivyo ujue huyo ni mzushi, usimkubalie ewe ndugu Mwislam! (12) Wanawake kutoswali misikitini: Katika baadhi ya misikiti ya madhehebu ya Shia Ithnasheri, wanawake hawakutengewa sehemu yao ya kuswali msikitini ingawa ingewezekana kuwatenga kabisa wasionane na wanaume. Sababu yake ni kwamba wanawake wanapata thawabu nyingi kama wakiswali majumbani mwao, wakati ambapo wanaume wanapata thawabu nyingi kwa kuswali jamaa misikitini. Pamoja na kwamba si haramu kwa wanawake kuswali misikitini, lakini hali halisi ya misikiti yetu wakati huu ni kwamba, mara tu baada ya Swala, utaona wanawake na wanaume wanatoka na kuchanganyikana na kusalimiana hadi kupeana mikono na wanaume; wakati ambapo tunasoma kuwa pale ambapo ilimlazimu Mtume (s.a.w.w.) kupeana mkono na mwanamke ambaye si haramu kuolewa na Mtume (s.a.w.w.), yeye Mtume (s.a.w.w.) alifunga kitambaa mkononi kwanza. Kuchanganyika wanawake na wanaume popote pale ni haramu. Hata kwenye Biblia inakatazwa. (Zakariya 12:14). Wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.), alikuwa anawazuia wanaume kutoka msikitini, hadi pale wanawake wote watakapokuwa wametoka na kupotea kabisa, ndipo na wanaume wanaruhusiwa kutoka. Suala la kuchanganyika ovyo, wakati baadhi ya wanawake wenyewe wamevaa kanga mbili bila mavazi rasmi ya hijabu, ndilo linaloleta vishawishi vya 375


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 376

katika Uislamu

uzinifu. Hilo lazima lipigwe vita kwani sio mwenendo wa kiislamu. Hata hivyo katika misikiti ya Shia, kuna vyumba maalumu vya kukutania wanawakembali na wanaume mbali, kwa ajili ya kujifunza dini au mikutano. Sehemu hizo siyo misikiti, bali huitwa Huseiniyyah. (13) Faida za Qur’ani na miiko yake: Ni jambo la kusikitisha sana kuona kwamba kanuni za kuisoma na kuiheshimu Qur’ani hazizingatiwi hata kidogo. Sisi Shia Ithna’asheri tunayo mafunzo muhimu juu ya suala hili. Mafunzo hayo yanatokana na Mtume (s.a.w.w.) pamoja na Ahlul-Bayt (a.s.) wake: i. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa wakati mwalimu akimfundisha mtoto kutamka: Bismillahir-Rahma-nir-Rahiym, na mtoto akaweza kutamka, Mwenyezi Mungu humwandikia hati ya kumwacha huru (kumwepusha moto) yeye na wazazi wake na mwalimu wake. ii. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa yeyote atakayemfunza mwanawe kusoma Qur’ani, Mwenyezi Mungu atawavalisha wazazi wake (huyo mtoto) taji la kifalme pamoja na mavazi mazuri ambayo hakuna aliyewahi kuyaona. iii. Abil Jaruud anamkariri Imam Jafar Sadiq (a.s.) ambaye naye anamkariri Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa “Siku ya Kiyama nitakuwa wa kwanza kuja mbele ya Mwenyezi Mungu nikiwa na Qur’ani tukufu na Ahlul-Bayt wangu na wafuasi wangu. Kisha nitawauliza wafuasi wangu walivyojihusisha na Ahlul-Bayt wangu na Qur’ani Tukufu.” iv. Bashir Ibn Ghalib Al-Asadi anamkariri Imam Husein (a.s.) akisema kuwa, ‘Anayesoma Qur’ani katika Swala akiwa amesimama, Mwenyezi Mungu humwandikia thawabu mia moja kila herufi moja ya Qur’ani, na thawabu kumi kwa kila herufi iwapo Qur’ani itasomwa nje ya Swala. Msikilizaji huandikiwa thawabu moja kila herufi na hufutiwa dhambi moja na hupandishwa daraja moja. Mwenye kusoma Qur’ani kimya kwa kuangalia herufi hupata malipo hayo hayo.

376


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 377

katika Uislamu

v. Imam Hasan Askary (a.s.) anawakariri babu zake wakisema kuwa, “Surat Fatiha ina faida (thawabu) kubwa mno kuliko hazina zote za Arsh. Anayesoma sura hiyo akiwa na imani na mapenzi makubwa kwa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.), Mwenyezi Mungu humlipa thawabu moja kwa kila herufi moja. Kila thawabu moja ni bora kuliko thamani ya ulimwengu mzima na vyote vilivyomo. Msikilizaji wa msomaji, naye hulipwa kiasi hicho hicho.” vi. Anakaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa anayesoma Qur’ani yote ni sawasawa na kama vile kauvaa (kahusishwa na) utume isipokuwa tu kwamba hawezi kuletewa ‘wahyi’. vii. Ya’qub Al-Ahmar anamkariri Abi Abdullah akisema kuwa ‘Nimejifunza Qur’ani tukufu lakini hivi sasa nimesahau kiasi fulani’. Imam Jafar Sadiq (a.s.) aliombwa amwombee kwa Mwenyezi Mungu ili aweze tena kuisoma. Imam alionekana kushtuka na kusema, ‘Mwenyezi Mungu na sisi sote tukusaidie kuweza kusoma Qur’ani tena. Iwapo kati yetu kumi tulio hapa, mmoja wetu anaijua sura moja tu ya Qur’ani na kisha akaiacha asiisome, Siku ya Kiyama Sura hiyo ya Qur’ani itamtokea katika umbo zuri la kupendeza sana na kumsalimia. Mtu huyo atauliza: wewe ni nani? Nayo itasema: Mimi ni sura fulani ya Qur’ani. Kama usingenitelekeza, leo hii ningekupandisha daraja kubwa.’ viii. Husayn Ibn Zayd anamkariri Imam wa sita (a.s.) akisema kuwa, Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa (katika Hadithi al-Manahi): “Anayesoma Qur’ani na kisha akaisahau, atakutana na Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama akiwa amefungwa minyororo na kwa kila Aya aliyoisahau, Mwenyezi Mungu atamtumia nyoka ambaye atakaa naye Jahannam mpaka labda Mwenyezi Mungu amsamehe.’ (14) Miiko ya Qur’ani Tukufu: i. Muhammad Ibn Fuzail anasema kuwa alimweleza Imam Jafar Sadiq (a.s.) kwamba: 377


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 378

katika Uislamu

‘Mimi husoma Qur’ani kisha huenda haja na nikirudi huwa nimejisafisha kawaida ya usafi tu, halafu naendelea kusoma Qur’ani.’ Imam alijibu kuwa hivyo haifai mpaka kwanza utawadhe (Qur’ani 56:79) ndipo uweze tena kuendelea kusoma Qur’ani. ii. Anakaririwa Abu Dharr Ghiffari akimkariri Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema kuwa, ‘Abu Dharr teremsha sauti yako ukiwa unasindikiza jeneza, ukiwa vitani na unaposoma Qur’ani.’ iii. Abdullah Ibn Sinan anamkariri Imam wa Sita (a.s.) ambaye naye anamkariri Mtume (s.a.w.w.) kuwa, ‘Someni Qur’ani kwa kiarabu fasaha na sauti na msiisome kwa sauti za watenda madhambi, kwa kuwa baada yangu watakuja watu watakaorembua sauti zao wakati wa kusoma Qur’ani kama vile wanamuziki na waombolezaji na watu waovu.’ iv. Abdullah Ibn Abi Ya’fu’ur anamkariri Imam Jafar Sadiq (a.s.) akisema kuwa, ‘Mmoja wenu anaposoma Qur’ani ni wajibu kwa waliobaki kukaa kimya na kumsikiliza.’ v.

Al-Saku’uni anamkariri Imam Jafar Sadiq (a.s.) akisema kuwa, ‘Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa mfuasi wake asiyesoma Qur’ani kwa kiarabu ila kwa lugha yake ya asili, Malaika huinua hadhi yake kwa wao kusoma kwa kiarabu.’

(15) Faida zaidi za kusoma Qur’ani: i. Ibn Al-Qaddah anamkariri Imam Jaffar Sadiq (a.s.) ambaye naye anamkariri Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) akisema kuwa, “Nyumba ambayo Qur’ani tukufu inasomwa na Mwenyezi Mungu anatajwa kila mara, baraka huongezeka na Malaika huitembelea na shetani huikimbia, na nyumba hiyo hung’ara kwa walio akhera kama nyota zinavyong’ara kwetu kutoka angani. Nyumba ambayo Qur’ani haisomwi na pia Mwenyezi Mungu hatajwi, baraka hupungua na Malaika huondoka humo na mashetani huingia humo.” 378


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 379

katika Uislamu

ii. Ya’qub Ibn Yazid anamkariri Imam Jafar Sadiq (a.s.) akisema kuwa, “Anayesoma Qur’ani tukufu kwa maandishi atabarikiwa afya nzuri ya macho yake, na wazazi wake watapunguziwa dhambi hata kama ni makafiri.” iii. Is’haq Ibn Ummar anasema kuwa, ‘Nilimweleza Imam Jafar Sadiq (a.s.) kuwa nilikariri Qur’ani tukufu na ninaisoma kwa kukariri, je, nitapata thawabu zaidi au hapana? Imam alinijibu kuwa kuna thawabu nyingi kwa kusoma maandishi kuliko kusoma toka moyoni.’ iv. Abu Dharr Ghiffari anamkariri Mtume akisema kuwa, ‘Kuangalia uso wa Ali Ibn Abu Talib ni ibada, kuwaangalia wazazi wako kwa mapenzi ni ibada, na kuiangalia Qur’ani tukufu ni ibada na kuiangalia AlKaabah ni ibada.’ v. Anakaririwa Imam Jafar Sadiq (a.s.) akisema kuwa, ‘Vitu vitatu vitalalamika kwa Mwenyezi Mungu Mwingi wa ukarimu: Msikiti ambao umeharibika na watu wake hawaji kuswali humo, mjuzi wa dini (mwanazuoni) anayeishi miongoni mwa wajinga, na Qur’ani tukufu ambayo imewekwa hadi ikapata vumbi huku hakuna atakaye kuisoma. Tukizingatia maelezo hayo yote tutaona kuwa siku hizi usomaji wa Qur’ani Tukufu hauzingatii miiko na kanuni muhimu zinazotakiwa. Utakuta kwenye mgahawa imewekwa kanda (kaseti) ya Qur’ani huku watu wanaongelea mashindano ya mpira na maongezi mengine ya kidunia (Qur’ani 7:204). Utakuta msomaji anaisoma Qur’ani kwa mbwembwe na kwa sauti yenye lengo la kuwavutia watu; kama utenzi au mashairi, bila kuzingatia sheria za alama mbali mbali na vituo, huku wasikilizaji wakiingilia kati kwa takbir na sauti za kumshangilia msomaji kwa uzuri wa sauti yake! Hali hii inakuwa sawa na vile anavyoshangiliwa na kutuzwa mwimba mashairi, utenzi au taarabu. Ni vigumu kuwakuta wasikilizaji wa Qur’ani wakiwa katika masikitiko kwa kutafakari uzito wa Aya zinazosomwa! Ni muhimu tufahamu kuwa kitendo chochote cha kuichezea 379


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 380

katika Uislamu

Qur’ani, dhambi yake ni kubwa maradufu kuliko thawabu za kuisoma nilizozieleza hapa. Vile vile tutaona kuwa wakati wa kusoma hitima, kwanza wasomaji walio wengi hawachukui tahadhari ya tohara! Pili wanapoanza kusoma Qur’ani husoma kwa kubaraza kama cherehani. Vitendo kama hivyo, ndivyo vinavyoitwa kuichezea na kutoiheshimu Qur’ani. Sehemu nyingine inakochezewa Qur’ani ni utaratibu mzima wa Swala ya Taraweh ambapo msomaji mwenye kasi kubwa ndiye anasifiwa! Pamoja na kwamba taraweh siyo Swala ya wajibu lakini Swala yoyote ile ni lazima iswaliwe kwa unyenyekevu. Hayo makelele yanayopigwa misikitini katika Swala hiyo, vile vile ni makosa makubwa tukizingatia, kifungu namba 8 - Sura hii ya 20. Ni muhimu pia waalimu wa vyuo waanze kuwafundisha watoto wetu miiko ya Qur’ani tukufu ili baadaye watakapokuwa watu wazima wajenge utamaduni wa kuheshimu Qur’ani. Tabia ya watoto wa vyuo kuandika ovyo katika misahafu na pia kuichana na kutawanya ovyo maandishi yake, haina budi kukomeshwa. Tabia nyingine ya kusikitisha sana siku hizi, ni kuwasikia wanamuziki mbali mbali Waislamu duniani, ambao huimba Aya za Qur’ani katika muziki wao! Nimeeleza huko nyuma kwamba mojawapo ya dalili za kukaribia Siku ya Kiyama ni pale ambapo Qur’ani itaimbwa kama muziki! Hayo yalielezwa na Mtume (s.a.w.w.) karne 14 zilizopita! Inasikitisha pia kuona baadhi ya mashekhe wetu wanaandika kombe za Qur’ani na kuwauzia wasio Waislamu, au kuandika Aya za Qur’ani na kuwapa wasio Waislamu kama kinga. Yote haya ni katika kuichezea Qur’ani. Iwapo misahafu au juzu’amma zimechakaa, ni muhimu lichimbwe shimo mahali tohara ili zifukiwe humo na siyo kuacha kurasa zake zinapeperushwa ovyo na upepo.

380


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 381

katika Uislamu

Rejea: (Kuhusu miiko na faida ya Qur’ani) Islamic Laws of Worship and Contracts, cha Ayatullah Al-Uzma Sayyid M. Al-Shirazi. (16) Jinsi Qur’ani ilivyokusanywa na kufanywa Msahafu: Katika somo lililopita tumeona kuwa faida za Qur’ani ni nyingi. Faida hizo tumezipata toka katika mafunzo matukufu ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.). Kuna Waislamu wasio wafuasi wa Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ambao nasikia kuwa wanaitumia Qur’ani kwa faida za kishetani lakini ujuzi huo mimi sina kwa sababu ni haramu. Sasa tupate maelezo jinsi gani hii Qur’ani ilivyokusanywa na ukaandikwa msahafu baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), kwa sababu kuna watu wanapewa sifa za kukusanya Qur’ani kana kwamba ilikuwa imepotea! Tofauti za maoni juu ya suala hili kati ya Sunni na Shia ndizo zinazopelekea baadhi ya wachochezi na wazushi kudai kuwa Shia Ithna’asheri wana Qur’ani yao tofauti! Waislamu tusipoacha tabia ya kuchukulia juu juu kila jambo bila kuzama na kuchunguza undani wake, hatutaifahamu dini. Mara baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.), Qur’ani isingeweza kupotea kwa sababu Mwenyezi Mungu alishaahidi kuilinda (Qur’ani 15:9). Kazi iliyokuwepo ni kuiweka katika msahafu. Kwa kweli hata huo mpangilio wa sura na Aya zake zote, hayo yalishapangwa na Mtume (s.a.w.w.) katika uhai wake. Huko nyuma nimeeleza jinsi wasia wa Mtume (s.a.w.w) ulivyopuuzwa juu ya suala la uongozi baaada yake. Nimeeleza pia jinsi Mtume (s.a.w.w.) alivyosema kuwa, ‘‘Nawaachia vizito viwili ambavyo ni Qur’ani na Kizazi changu (Ahlul-Bayt wangu). Vitu hivyo havitatengana hadi vinifikie katika kisima cha Kawthar peponi. Jihadharini namna mtakavyojihusisha navyo.’ Hadithi nyingine maarufu ni pale aliposema kuwa, ‘Mimi ni Jiji la elimu na Ali Ibn Abu Talib ni lango lake.’ Kihistoria tunaona ajabu kwamba baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki mabwana Abu Bakr na Umar waliamua kumchagua Zayd Ibn Thabit eti kuku381


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 382

katika Uislamu

sanya Qur’ani wakati ambapo Imam Ali (a.s.) alikuwa anaiandika katika mpangilio alioelekezwa na Mtume (s.a.w.w.). Imam Ali (a.s.) alisema wazi kuwa hatatoka nyumbani kwake mpaka kwanza akamilishe uandishi huo. Baada ya Imam Ali (a.s.) kukamilisha kazi hiyo, aliwapelekea watawala ambao walikataa kupokea msahafu huo! Maoni yetu hapa ni kwamba tunafahamu kuwa wakati huo tayari walikuwepo masahaba wengi waliokuwa wamehifadhi (waliokariri) Qur’ani kwa usahihi kiasi ambacho hata kama ukusanyaji ungekuwa na kasoro, isingekuwa tatizo kuiandika Qur’ani. Na ndiyo maana hatuikatai hiyo Qur’ani iliyoandikwa enzi za utawala wa Uthman Ibn Affan. Nakala hiyo iliandikwa na bwana Ibn Mas’ood kisha ikachapishwa kwa idhini ya khalifa Uthman. Pamoja na kukataliwa nakala hiyo ya Imam Ali (a.s.), ninarudia kusisitiza kusema kuwa, Shia Ithna’asheri tunakubaliana na hiyo nakala ya Ibn Mas’ood. Sasa tuchunguze kwa nini nakala ya Imam Ali (a.s.) ilikataliwa pamoja na ukweli kwamba hapakuwepo sahaba yeyote mwenye elimu kama Imam Ali (a.s.)! Ni muhimu tufahamu kuwa Qur’ani ilipoteremshwa kwa Mtume (s.a.w.w.) haikuwa na irabu na kwa hiyo makabila tofauti ya Waarabu walikuwa wanaisoma kwa lafudhi tofauti na hivyo kupoteza maana yake, kama tuonavyo katika kanuni za kuisoma Qur’ani. Aliyefanya kazi ya kuweka irabu ni Imam Ali (a.s.) na hivyo mpaka leo Qur’ani inasomwa kwa lafudhi moja dunia nzima. Kwa hiyo inasikitisha kuona huyu lango la elimu ya Mtume (s.a.w.w.) anasukumwa pembeni katika kazi ya kuiandika Qur’ani baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.)! Na ndiyo maana Waarabu pia hulazimika kujifunza kusoma Qur’ani! Kujua kiarabu siyo urahisi wa kusoma Qur’ani! Ukweli ni kwamba katika nakala ya Imam Ali (a.s.) kulikwemo pia na ‘sherhe’ kuhusiana na sababu za kushuka Aya pamoja na matukio mengi ya unafiki wa baadhi ya masahaba uliosababisha kushuka Aya fulani fulani. Iwapo nakala hiyo ya Imam Ali (a.s.) ingepokelewa na kusambazwa, ina maana ingewasuta hata hao watawala! 382


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 383

katika Uislamu

Lakini kwa upande mwingine tutaona kuwa ukiiacha Qur’ani kama ilivyo (Jalalain) bila kuelezea sababu zote za kushuka Aya zake, inampa mwanya mtu yeyote kuzifasiri Aya zake atakavyo, kwa kutumia kanuni za kawaida za lugha ya kiarabu! Na hivyo ndivyo tufanyavyo siku hizi ambapo utamkuta kila mwenye ujuzi kidogo wa kiarabu anadai kuwa ni mjuzi wa kufasiri Qur’ani! Nimetoa mifano kadhaa huko nyuma kubainisha kasoro hii na bila shaka Waislamu waaminifu watakuwa wameona wazi kuwa, hatuwezi kuifasiri Qur’ani sawa na kitabu chochote kile cha kiarabu! Hayakuwa madhumuni ya kitabu hiki kidogo kutaja Aya zote za Qur’ani na kueleza sababu za kushuka kwake, ili tuweze kuona tofauti kati ya Jalalain na tafsiri halisi ya Qur’ani. Na wala siyo kama Mwenyezi Mungu alishindwa kuteremsha Qur’ani yote siku moja! Ingeteremshwa siku moja pengine zisingekuwepo sababu nyingi za kushuka Aya fulani fulani! Nasema hivi kwa sababu matukio katika miaka 23 ya kushuka Qur’ani ni mengi mno kuliko kama ingeshuka siku moja! Busara yake ni kwamba ni lazima mwenye kutaka kuifahamu Qur’ani ajitahidi sana kusoma historia sahihi ya Uislamu. Historia hiyo ni elimu pana sana. na inahitaji muda wa kutosha kuisoma na kuhitimu. Msimamo huu unatokana na maelezo machache niliyotoa katika kitabu hiki kutoka katika historia ya Uislamu. Bila shaka ni wachache kati yetu wanaoyafahamu machache haya! Isitoshe pia nimeeleza alivyokaririwa Mtume (s.a.w.w.) akisema kuwa, ‘Qur’ani ina maana iliyo wazi na maana iliyojificha na maana zote mbili anazifahamu Ali Ibn Abu Talib’. Zaidi ya hayo nilieleza huko nyuma katika sehemu ya Hotuba (wasia) ya Mtume (s.a.w.w.), miezi mitatu kabla hajafariki, akitokea Hijja yake ya mwisho, pale Ghadiir Khum, alipoeleza kuwa: “Enyi watu, someni na kutafakari Qur’ani na muelewe Aya zake. Fikirini juu ya Aya zake zilizo wazi na msijitahidi kuzitafsiri Aya zisizo wazi kwa sababu kwa jina la Mwenyezi Mungu, hapana atakayewaelezea maana yake isipokuwa huyu hapa ambaye ninainua mkono wake mbele yangu. Na ninawaeleza wazi kuwa yeyote ambaye mimi ni bwana wake, Ali ni bwana wake pia. ..........” 383


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 384

katika Uislamu

Kwa hiyo pamoja na maneno yote haya ya Mtume (s.a.w.w.) bado tumeona nakala ya Qur’ani ya Imam Ali (a.s.) inakataliwa na watawala! Natambua kuwa kuna Ulamaa wengi wa Sunni waliofasiri Qur’ani na kuisherehesha kwa nia nzuri ya kuelimisha Waislamu, lakini ni lazima tufikirie kwamba, kwa ushahidi wote huu niliotoa, tafsiri sahihi ya Qur’ani ni ile inayotokana na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo sisi Shia Ithnasheri tangu mwanzo tulitegemea tafsiri ya Qur’ani ya Ahlul-Bayt (a.s.) mpaka leo. Bila shaka huko nyuma tumeona elimu kubwa ya kuzaliwa nayo hao AhlulBayt. Kwa nini katika dini yetu tusiwategemee hao wenye elimu kubwa na ambao Mwenyezi Mungu amewatakasa na kuwalinda na madhambi (Qur’ani; 33:33)? Mbona katika mambo ya kidunia tunawategemea sana watu wenye ujuzi kama madaktari, marubani manahodha, wahandisi n.k.? Mwenyezi Mungu katuwekea viongozi maalumu wa kuifasiri Qur’ani kwa vitendo na kwa maneno ili kutuepusha na balaa la watu waovu kuifasiri kwa manufaa yao. (Qur’ani; 3:7)1 Tufahamu kuwa katika chuo chochote cha elimu hapa duniani, utakuta kuna vitabu vingi. Lakini hakuna chuo kinachowapatia vitabu wanafunzi bila viongozi wa kufundisha yaliyomo kwenye vitabu hivyo. Vitabu havitoshi bila wakufunzi wa kufafanua yaliyomo vitabuni humo.2 Lakini tunaelewa kuwa Uislamu ni dini ya Mwenyezi Mungu. Mwenye kutaka kuielewa na kutimiza wajibu wake, ni kheri kwake. Atakayetaka kujisifu kuwa amehitimu, bila shaka siku itafika ambapo atajikuta amesimama mbele ya Mwenyezi Mungu akiwa katika kundi la wajinga. Hayo yote niliyoyaandika ni mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.w.) lakini tunaona waliotutangulia walivyoyapa mgongo! Inasikitisha kuona baadhi ya Waislamu hawakubaliani na hali ya AhlulBayt kuwa wamelindwa na dhambi (Qur’ani 33:33). Hali hii imepelekea 1 ............Na wala hakuna ajuaye taawili ya Aya hizi ila Allah na wale waliozama katika elimu, .......... 2 Amirul-Muminin Ali (a.s.) anasema: "Hiyo ni Qur'ani iliyonyamaza, na mimi ni Qur'ani inayosema." 384


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 385

katika Uislamu

kuibuka itikadi mpya kwa baadhi ya Waislamu, wanaodai kuwa, “Mtume (s.a.w.w.) ni sawa na binadamu yeyote yule isipokuwa tu pale alipokuwa anapokea wahyi ndipo anakuwa na sifa ya Unabii!” Watu hao ambao ninasikitika kusema kuwa ama hawana elimu, au ni wanafiki, wao wanataja (Qur’ani 80:1) kama ushahidi wao! Eti Mtume (s.a.w.w.) kamkunjia uso kipofu!: Nimetangulia kueleza kuwa mojawapo ya kanuni za kufasiri Qur’ani ni kwamba tafsiri ya Aya yoyote ile isipingane na Aya nyinginezo katika Qur’ani. Hebu tuone Qur’ani inasemaje:- Na bila shaka (wewe) una tabia njema, tukufu. (Qur’ani 68:4). Ukilinganisha Aya hii na Sura ya Abasa, Aya isemayo kuwa: Alikunja uso na kugeuka nyuma (Qur’ani 80:1), utaona kuwa Mtume (s.a.w.w.) aliyesifiwa kwa tabia njema za hali ya juu, hawezi kumkunjia uso kipofu na kugeuka nyuma (kwa dharau)! Isitoshe, itakuwaje Mtume (s.a.w.w.) awe amelindwa na dhambi na uchafu wakati anamdharau kipofu? Waislamu kama tutadumisha tabia ya kukariri Qur’ani na kuighani (kuiimba) kama kasuku, bila kwanza kujifunza kanuni za kuifasiri kwa usahihi, pamoja na kujifunza historia sahihi ya Uislamu na dunia kwa ujumla; kamwe hatutaielewa dini yetu. Pamoja na kwamba Aya hiyo inasema kuwa: ‘alikunja uso’, maneno hayo kwa kadri ya kanuni za lugha ya kiarabu hayakumkusudia Mtume (s.a.w.w.)! Lakini tukianza kubishana kwa kutumia kanuni za lugha, kila mtu atatetea yale aliyofunzwa na shekhe wake hata kama shekhe huyo hana elimu ya kiwango cha kutegemewa. Matokeo yake ni kwamba kwa kiwango chetu kidogo cha elimu hatutapambanua ni nani mkweli. Kwa hiyo turejee msingi mwingine mkuu wa kuifasiri Qur’ani, ambao ni historia. Kwa kadri ya sababu za kushuka Aya hii ni kwamba siku moja Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekaa na machifu wa Quraish na ikawa kipofu mmoja, Abdullah Ibn Maktum amefika hapo. Kipofu huyo alikuwa rafiki sana wa Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimpokea kwa heshima kubwa na akampa nafasi ya kukaa karibu yake. Kwa kuwa Abdullah alikuwa masiki385


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 386

katika Uislamu

ni na pia kipofu, wale machifu wa Quraish walimdharau na hawakufurahia heshima aliyopewa na Mtume (s.a.w.w.) mbele yao. Wakati huo ndipo mmoja wa hao machifu alipokasirika na kukunja uso kisha akageuka na kumpa kisogo huyo kipofu Abdullah. Tabia hiyo ilimwudhi Mwenyezi Mungu na ndipo Malaika Jibril akateremsha Sura hiyo ya Qur’ani kwa Mtume (s.a.w.w.). Sura hii inamsifu Abdullah ingawa ni masikini na kipofu; na inakemea tabia mbaya ya majivuno ya hao masahaba. Tunawezaje kumtia kasoro hiyo Mtume (s.a.w.w.) wakati Mwenyezi Mungu anatuelekeza binadamu kufuata mfano mwema wa tabia njema za Mtume (s.a.w.w.) (Qur’ani 33:21)? Je, kama tutakutana na vipofu au vilema au mafukara tukawaangalia kwa dharau, tutakuwa tumetekeleza mwito au amri ya Qur’ani 33:21? Wanaojaribu kutumia nafsi ya tatu, ‘nominative pronoun’ katika Aya ya kwanza ili kumhusisha Mtume (s.a.w.w.) na tabia hiyo mbaya, hawana ujuzi kamili wa misingi yote muhimu ya kuifasiri Qur’ani; bali wanatumia kanuni za kawaida za lugha peke yake. Isitoshe wakati huo huyo Abdullah Ibn Maktum (kipofu) alikuwa tayari amesilimu lakini hao machifu wa Quraish walikuwa bado makafiri wakifanyiwa tabligh ili nao wasilimu pia! Vipi Mtume (s.a.w.w.) angemkunjia uso Mwislamu kwa kulinda heshima na majivuno ya makafiri! Rejea:The Holy Qur’ani; Full Commentary Vol. 2, cha S.V. Mir Ahmad Ali (M.A, B.O.L,B.T.) Pakistan. Eti Mtume (s.a.w.w.) alipasuliwa kifua na kusafishwa moyo na kutolewa nyongo! Mfano mwingine wa kupotosha tafsiri ya Qur’ani Tukufu, tunaupata katika Sura ya 94 (Al-Inshirah). Baadhi ya wafasiri (Mufasirun) wamepotosha Aya ya kwanza ya Sura hii kwa ujumla. Kutokana na upotofu huo wa miaka mingi, utawasikia hata Waislamu wa kawaida wanasema kuwa (na hata kwenye Qaswida), eti Malaika Jibril alimpasua kifua Mtume (s.a.w.w.) na kutoa moyo na kuusafisha kisha kuurudisha! Inadaiwa kuwa 386


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 387

katika Uislamu

uchafu ulioondolewa ni kama vile hizi kasoro tulizo nazo sisi binadamu wa kawaida kama chuki, uhasama na uovu! Kwa hiyo utasikia hata Mwislamu wa kawaida asiye na elimu yoyote ya dini anasema kuwa hajatolewa nyongo kama Mtume (s.a.w.w.) kwa maana kuwa hajakamilika kwa kuepukana na dhambi na uovu! Ukipitia historia ya maisha ya Mtume (s.a.w.w.) kabla hajapewa utume, huwezi kuona mahali popote ambapo Mtume (s.a.w.w.) alifanya tendo lolote la uovu japo uwe kidogo sana. Sababu kubwa ya Mwenyezi Mungu kumpa bi’tha ya (kutangaza) utume baada ya miaka 40, ni pamoja na kuwapa watu nafasi ya kuishi naye na kuhakikisha kuwa miaka yote ya nyuma kabla ya kutangaza utume, alikuwa mtu mwadilifu sana. Kwa kweli huo ndio ukweli tunaoupata katika historia. Na kama ndiyo hivyo, huo uchafu aliosafishwa Mtume (s.a.w.w.) ni uchafu gani; tukirejea maneno hayo ya Qur’ani yanayosema: “Je, Hatukukupanulia kifua chako!” Qur’ani 94:1. Maneno haya kusudio lake ni kuongeza uwezo wa Mtume (s.a.w.w.) wa kufikiri, kutafakari na kuelewa elimu pana zaidi. Kwa hiyo Mwenyezi Mungu amekusudia kueleza kuwa amekipanua kifua cha Mtume (s.a.w.w.) kwa kumwongeza elimu. Tufahamu kuwa katika lugha ya kiswahili utasikia mtu anasema kuwa, ‘Nimekariri Sura ya Alhamdu moyoni.’ Sote tunafahamu kuwa kichwa (ubongo) ndicho huweka kumbukumbu na siyo moyo! Lakini tunatumia ‘moyo’ kwa mazoea ya kilugha, na maana yetu inaeleweka. Wakati Nabii Musa (a.s.) alipoamrishwa na Mwenyezi Mungu kwenda kwa Firauni (Pharaoh) kumbashiria ukweli na kumkataza uovu na kumwonya dhidi ya uasi kwa Mungu wa kweli, nabii Musa (a.s.) alimwomba Mwenyezi Mungu kupanua kifua chake yaani kumwongeza elimu. Alisema: ‘Ee Mola Wangu! Nipanulie kifua changu’ (Qur’ani 20:25). Hakuna mahali panapoonyesha kwamba Musa alipasuliwa kifua chake! Na neno ni hilohilo lililotumika!

387


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 388

katika Uislamu

Maneno haya ya Qur’ani tunayakuta tena sehemu nyingine: “Kwa hiyo kwa yule ambaye Mwenyezi Mungu amekusudia kumwongoa, Humpanulia kifua chake kwa Uislamu .......” (Qur’ani 6:125)* Maelezo: Katika Aya zote hizi; 94:1; 20:25; na 6:125; neno lililokusuduwa hasa, mwote humo ni Kifua, wala sio moyo. Hapa tunaona wazi kuwa, kupanuliwa kifua maana yake ni kuongezwa elimu kwa sababu mtu yeyote hawezi kuongozwa katika Uislamu bila mtu huyo kupata elimu ya kumwezesha kufahamu dini ya haki. (17) Tahadhari kwa sisi Shia: Ukichunguza vitabu vya dini vya Shia Ithna’asheri, huwezi kukuta mafunzo au hukumu zinazohitilafiana au kugongana. Hali hii inatokana na Shia kumtegemea kiongozi mmoja (Mujitahid) kama nilivyoeleza huko nyuma. Lakini inasikitisha kuona kuwa, kuna baadhi ya Shia wanakiuka mafunzo ya dini hali ya kuwa baadhi yao ni wajuzi wa dini! Lengo la kitabu hiki ni kukemea imani na matendo ambayo ni kinyume na mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani; bila kujali kama yanatendwa na Sunni au Shia. Nakumbuka katika semina moja ya Shia mwaka 1991, alitokea mtoa mada mmoja ambaye alidai kuwa kutokana na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.), Shia wote, wafuasi wa Imam Ali (a.s.) ni watu wa peponi! Hoja hiyo ilizua mabishano makali kwa sababu ingawa kweli Hadithi hiyo ipo lakini kuwa mfuasi kwa maneno bila vitendo hakuwezi kumpeleka mtu peponi. Yawezekana mtu akawa na elimu zote za uongofu lakini vitendo vyake vikawa vya upotofu. Hali hiyo haitamsaidia kitu. Siku moja Imam Ali (a.s.) aliliona kundi la watu wamesimama mlangoni kwake, akamwuliza mtumishi wake Qambar ni watu gani hao. Mtumishi wake akajibu kuwa hao ni Shia wake (Imam). Imam Ali (a.s.) aliposikia hivyo alibadilika uso (alikunja uso) na kusema, “Kwa nini wanaitwa Shia? Hawana alama za Ushia.” Hapo ikawa Qambar ameuliza, “Ni alama gani za Ushia?” Imam Ali (a.s.) alijibu, “Matumbo yao yamerudi ndani kwa 388


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 389

katika Uislamu

njaa, midomo yao imekauka kwa kiu na macho yao yamedhoofika kwa kuomboleza.” Rejea:- Nahajul Balaghah (kiingereza) uk. 269. Hapa Imam Ali (a.s.) anaelezea alama za wafuasi wake zinazoonekana kwa sura tu! Alama hizo hata hivyo ni vigumu kuzipata kwa sisi tunaoitwa Shia! Iwapo alama hizo za nje zinatushinda, je, kama tutachunguzwa kwa alama kubwa zaidi za tabia zetu, tutastahili kuitwa Shia? Kwa hiyo tusidhani kuwa Ushia ni sawa na kupakwa rangi leo na kesho umeshakuwa Shia! Kama tunazo elimu za Ushia kikamilifu, kwa nini vitendo vyetu viwe kinyume na nyayo za Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) ambao ndio viongozi wetu? Ni bora kujiambatanisha na upotofu kuliko kujiambatanisha na Ahlul-Bayt (a.s.) kwa unafiki. Kuwafuata Ahlul-Bayt (a.s.) hakuishii kuswali Swala ndefu au ‘Salawat’ kwa wingi sana, wakati tunashindwa hata kuendeleza kazi yao tukufu, iliyowasababishia vifo vyao vya kishahidi. Tahadhari ni kwamba, tusije kuishia kuwa wapenzi wao wa kishabiki tu, bila kuwa wafuasi wao kivitendo! Kama kuna mfuasi wa Imam Ali (a.s.) anayepuuzia jambo hili, anakaririwa Imam Ali (a.s.) mwenyewe akisema kuwa “Fanyeni matendo mema na msitegemee sana Shafa’at (maombezi) na mkadharau adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwani mfahamu kuwa watakuwepo wafuasi wetu watenda madhambi ambao hatutaweza kuwaombea (Shafa’at) mpaka kwanza watumikie adhabu motoni miaka laki tatu! Rejea: Day Of Judgement, cha S.A. Rizvi. Bilal Muslim Mission Dar es salaam. Kwa hiyo ndugu zangu kama tutajiita Shia lakini vitendo vyetu vikawa kinyume na Ahlul-Bayt (a.s.) tuelewe kuwa kwenda peponi si jambo la moja kwa moja! (18) Hatima ya Waislamu watakaokanusha wasia wa Mtume (s.a.w.w.): Pamoja na maelezo yote niliyoyatoa kuhusu umuhimu wa Waislamu kutekeleza wasia wa Mtume (s.a.w.w.), bado ninaamini kuwa wapo Waislamu wenye uwezo wa kutafakari na kupambanua hoja, lakini hawako tayari kupokea ukweli. Upinzani wa binadamu kwa Mitume haukuanzia 389


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 390

katika Uislamu

kwetu bali ni wa tangu zamani sana. Tunasoma kwamba Nabii Nuhu (a.s.) katika umri wake mrefu wa miaka 2,500 alijitahidi sana kuwahubiria watu wafuate njia ya haki, lakini watu wake hao walimpiga mawe na kumfunika na takataka huku wakiongozana na watoto wao, ili utamaduni wa kumpiga Nabii Nuhu (a.s.) uendelee! Kila Nabii Nuhu (a.s.) alipopigwa na kufunikwa na takataka, Malaika Jibril alifika na kumwondoa na kuponya vidonda vyake. Kisha Nabii Nuhu (a.s.) aliendelea na kazi yake ya tabligh kwa watu wake kwa miaka 900 lakini watu wake hao hawakubadilika! Hapo ndipo Nabii Nuhu (a.s.) alipowalaani watu hao hadi wake zao wakawa wagumba. Mifugo yao ilikufa, na mashamba yao yalikauka. Kwa miaka 40-70 mfululizo kulitokea ukame mkubwa. Nabii Nuhu (a.s.) aliwataka watu wake wamwamini Mungu wa kweli na wabadili tabia zao mbaya ndipo adhabu hiyo itawaondokea, lakini walikataa ushauri wake. Nabii Nuhu (a.s.) aliamrishwa na Mwenyezi Mungu kujenga Safina ambayo ilichukua miaka 80 kuikamilisha, huku watu wake wakimwambia kuwa ana wazimu kwa kujenga hiyo Safina. Baada ya kukamilika hiyo Safina, ndipo adhabu ya gharika ilipowashukia watu wa Nabii Nuhu (a.s.) kama tunavyofahamu. Kwa hiyo tufahamu kuwa, kukataa kwetu kutii wasia huo wa Mtume (s.a.w.w), laana ya Mungu itadumu juu yetu kama Mtume (s.a.w.w.) alivyoeleza katika hotuba yake hiyo. Tumeona muda mrefu sana ambao Mwenyezi Mungu aliwavumilia watu wa Nabii Nuhu (a.s.) hadi akakasirika na kuwaangamiza kwa gharika. Katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.), wakati Quraysh walipokuwa wanakataa kupokea Uislamu, Mwenyezi Mungu aliwaletea ukame wa miaka saba. Katika ukame huo, walikula mizoga ya mbwa na hata kutwanga na kula mifupa ya wanyama waliokufa, wakaoza na kukauka. Walikula pia ngozi zilizokauka za wanyama waliokufa. Mwisho walimwendea Mtume (s.a.w.w.) na kumtaka awaombee waondolewe adhabu hiyo. Hizo ni baadhi tu ya laana. 390


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 391

katika Uislamu

Kwa hiyo Mwislamu anayejiona yupo katika kundi la walio wengi ambao hawakubaliani na wasia wa Mtume (s.a.w.w.); na kwa hiyo hataki kuachana na walio wengi; afahamu kuwa wingi si hoja mbele ya Mwenyezi Mungu. Ukisoma historia ya Vita vya Badr utaona kuwa Waislamu waaminifu walisaidiwa na Mwenyezi Mungu japo walikuwa katika hali ngumu. Maadui walipiga kambi kwenye ardhi ngumu, wakati ambapo Waislamu walikuwa kwenye eneo la mchanga ambao ulisababisha ugumu wa kutembea juu yake kutokana na kutitia miguu. Mwenyezi Mungu alisababisha mvua kunyesha na ikawa ardhi ngumu waliyokaa maadui ikageuka kuwa utelezi na matope, lakini mchanga kwa upande wa Waislamu, ukaimarika kwa mvua na kurahisisha utembeaji juu yake! Hizo ni neema za Mwenyezi Mungu kwa Waislamu waaminifu. Katika Vita vya Uhud, jeshi la makafiri lilikuwa kubwa sana na silaha nyingi imara. Jeshi la Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa na watu elfu moja tu lakini Abdullah Ibn Ubayy na wanafiki wenzake mia tatu, walimtoroka Mtume (s.a.w.w.) na hivyo kubakia Waislamu mia saba tu waaminifu wenye silaha duni, lakini wenye imani kubwa ya dini. Hata hivyo kulitokea Waislamu waliopuuza amri ya Mtume (s.a.w.w.) miongoni mwa wapiganaji. Hali hiyo ilisababisha makafiri kujipenyeza na kuwatia hasara kubwa Waislamu hadi mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kupoteza meno mawili kutokana na upanga aliopigwa kichwani ukavunja kinga (helmet) ya kichwa chake. Utiifu kwa Mtume (s.a.w.w.) ni wajibu. Mnafiki aliteremshiwa kifo kwa kupinga Imam Ali (a.s.) kuchaguliwa kiongozi: Uzito wa hotuba (wasia) ya Mtume (s.a.w.w.) ni kwamba, katika maelezo ya nyuma nimeeleza matukio mengi ambapo Waislamu wanafiki walimuasi Mtume (s.a.w.w.). Lakini siku ambayo Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza Imam Ali (a.s.) kuwa kiongozi wa Waislamu baada yake, mara Mtume (s.a.w.w.) aliporejea Madina, kulitokea mnafiki mmoja Harith Ibn Nu’man Fihri ambaye kwa chuki yake dhidi ya uchaguzi huo, alipanda 391


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 392

katika Uislamu

ngamia wake na kumwendea Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa na masahaba wake hapo msikitini Madina. Nu’man alishuka na kusimama mlangoni mwa msikiti na kumwambia Mtume (s.a.w.w.) kuwa: “Ewe Muhammad! Ulituamuru kuamini upweke wa Mweyenzi Mungu, kuswali, kufunga, kuhiji na yote haya tumeyakubali. Sasa ni vipi unampachika mtoto wa baba yako mdogo juu yetu awe bwana (Mawla) wetu baada yako?” Mtume (s.a.w.w.) alijibu kuwa, “Kwa jina la Mwenyezi Mungu nimefanya hivyo kwa amri ya Mwenyezi Mungu.” Pale pale Nu’man alianza kutaka kurejea apande ngamia wake huku akisema kuwa, “Ee Mungu, iwapo anayoyasema Muhammad ni kweli naomba jiwe linishukie toka mbinguni na kuniua.” Harith Ibn Nu’man kabla hajamfikia ngamia wake, jiwe lilishuka kweli na kumwua pale pale! Jiwe hilo lilimshukia utosini na kupenyeza likatokeza kwa chini (kwenye njia ya haja kubwa). Watu walipata habari juu ya tukio hilo lakini bado waliendelea kupinga uteuzi huo kama tulivyoona nyuma!1 Ndiyo maana siku alipofariki Mtume (s.a.w.w.), Waislamu wengi wanafiki walimtelekeza Imam Ali (a.s.)! Je, tukubaliane na unafiki huo eti kwa sababu umekubaliwa na walio wengi mpaka leo? Nimeeleza huko nyuma kuhusu maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba, “Utawatambua wanafiki kwa chuki yao juu ya Imam Ali (a.s.).” Ninachotaka kueleza hapa ni kwamba, kama kuna Waislamu ambao baada ya kusoma kitabu hiki, bado wanadai kuwa hawamtambui Imam Ali (a.s.) kama kiongozi wa kwanza halali wa Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w.); na kwamba hawako tayari kutambua haki ya Ahlul-Bayt (a.s.) juu ya 1 Na sisi tunaendelea kukumbushwa hadi leo ushahidi wa tukio hilo, ndani ya Qur’ani Tukufu, kwani ndio sababu ya kushuka kwa Aya za Qur’ani; 70:1-2. – ‘Muulizaji ameuliza adhabu juu ya adhabu itakayotokea; na kwa makafiri hakuna awezaye kuizuia.......’ 1 ......Au wanawahusudu wale watu kwa yale ambayo Mwenyezi Mungu amewapa katika fadhila Zake? Bila shaka tuliwapa kizazi cha Ibrahim Kitabu na Hekima, na tukawapa Ufalme mkubwa! Qur’ani; 4:54 392


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 393

katika Uislamu

Waislamu.1 Basi nawaomba Waislamu hao tukutane mahali fulani, tuchukue udhu na kila mmoja wetu aombe laana ya Mwenyezi Mungu imshukie, iwapo hayupo katika msimamo wa haki kwa kukubali au kukataa kwake haki ya Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.) juu ya Waislamu. Baada ya ushahidi wote niliotoa juu ya suala hili, hiyo ndiyo kauli yangu ya mwisho. Nimeeleza wazi msimamo wangu huo ili ieleweke wazi mbele ya Mwenyezi Mungu kwamba sikuandika kitabu hiki kwa nia ya kupoteza watu kama wafanyavyo hao wanaoitwa Mawahabi. Turejee Qur’ani: “Hakika, wale wasioamini hutumia utajiri wao kuwazuia (watu katika) njia ya Mwenyezi Mungu, wataendelea kugharimia; kisha watajuta katika hayo. Mwisho wake watazidiwa (nguvu), na makafiri watakusanywa motoni” (Qur’ani 8:160). Mimi nimefikisha ujumbe wa Ghadiir Khum kwa Waislamu kama alivyoamuru Mtume (s.a.w.w.) katika wasia wake kwa Waislamu wote hadi Siku ya Kiyama. Wajibu wangu umeishia hapo. Sikupata na wala sitarajii kunufaika kidunia kutokana na kuandika kitabu hiki, zaidi ya kumtarajia Mwenyezi Mungu - kesho akhera. Lakini kwa kuwa kazi ya binadamu haikosi makosa, iwapo kuna kosa katika maelezo niliyotoa humu, nitashukuru kusahihishwa. Vinginevyo mjuzi wa yote pekee, ni Mwenyezi Mungu. (16) Siku ya Miraj Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona adhabu za wanawake waovu: Chini ya Somo la ‘Tofauti za Ibada Kati ya Shia na Sunni’, nitapenda kusisitiza kwamba siku ya Miraj ambayo Mtume (s.a.w.w.) alipelekwa mbinguni kutembelea peponi na kuona Jahanamu; ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwakuta wanawake wengi sana wapo Jahannamu kuliko wanaume.

393


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 394

katika Uislamu

Kabla sijaeleza sababu zake ningependa kueleza masikitiko yangu kwamba katika madhehebu ya Sunni, viongozi wake hawatilii mkazo suala zima la Hijabu ya mwanamke wa kiislamu kama lilivyoamrishwa wazi wazi katika (Qur’ani 24:30-31), (Qur’ani 24:60), (Qur’ani 33:32-33) (Qur’ani 33:59). Baadhi ya Aya kama (Qur’ani 33:32-33) na (Qur’ani 65:1), zinazungumzia wake zake Mtume (s.a.w.w.) lakini kusudio lake ni kwa wanawake wote wa kiislamu. Nasema kwamba viongozi wa Sunni hawazingatii suala la Hijabu kwa sababu utaona wanawake wanaingia hata misikitini wakiwa wamevaa vazi la kanga mbili! Neno Hijabu hata hivyo, halihusiani na mavazi peke yake bali linahusu mwenendo mzima wa tabia za mwanamke wa kiislamu kama Qur’ani inavyoeleza katika Aya nilizozitaja hapa. Kwa kifupi kuhusiana na hijabu ya nguo ni kwamba, mwanamke avae nguo zinazofunika (zinazositiri) sehemu zote zinazokatazwa kuwa wazi. Ni muhimu nguo hizo zisiwe za kubana mwili wake na kuonyesha umbo lake, yaani nguo hizo ziwe za kupwaya. Ni muhimu pia nguo hizo ziwe nzito zisiwe za vitambaa vyepesi. Vile vile haifai nguo hizo ziwe zenye mapambo ya kuvuta macho ya wanaume! Ndiyo maana inafaa hijabu iwe ya kitamba cha rangi moja ya buluu au nyeusi au nyeupe. Ushungi ufunike kichwa, kifua (matiti) na shingo. Nywele zisionekane, kwa hiyo inabidi kufunga kitambaa cha kichwa kwanza kabla ya ushungi. Tabia ya sasa hivi ya wanawake (Waislamu na Wakristo) kuvaa mavazi yasiyofaa au mavazi yasiyo ya jinsia zao (Biblia: Kumbukumbu la Torati 22:5), pamoja na kuchanganyika ovyo na wanaume (Biblia: Zakaria 12:14) ndiko kunakosababisha vishawishi vya uzinifu pamoja na kudhalilishwa wanawake kijinsia, kwa kadri ya takwimu za miaka ya 1995 toka nchi zinazodaiwa kuwa zimeendelea kidunia. Huko Canada mwanamke mmoja hudhalilishwa kijinsia kila dakika sita; wakati ambapo mwanamke mmoja kati ya watatu atadhalilishwa kijinsia 394


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 395

katika Uislamu

katika maisha yake yote. Mwanamke mmoja kati ya wanne yuko hatarini kubakwa katika maisha yake. Mwanamke mmoja kati ya wanane atadhalilishwa kijinsia akiwa katika masomo ya juu au chuo kikuu. Utafiti ulionyesha kuwa asilimia 60 ya wanafunzi wa kiume wa chuo kikuu, wanakiri kuwa wangekuwa tayari kudhalilisha wenzao wa kike kama wangekuwa na hakika ya kutokamatwa! Takwimu hizi zilitolewa katika ‘Pamphlet’ na Dean of women’ s office, chuo kikuu cha, Queen’s University - Canada. Kuhusu hijabu ya mapambo ni kwamba hairuhusiwi mapambo yaonekane kwa watu. Mwanamke wa kiislamu hajakatazwa kujipamba isipokuwa kuna mipaka yake. Mapambo yake yote yawe ni kwa ajili ya mume wake tu, na siyo kama tuonavyo siku hizi wanawake wanashindana kujipamba ili pengine kuvutia wanaume au wasifiwe mitaani au waonekane wana uwezo. Mara nyingine wanaume Waislamu wasio na ujuzi wa dini au hata viongozi wa dini, utaona baadhi yao wanawahimiza wake zao kuvaa mavazi yasiyofaa kishariah, ili wanaume hao wapate sifa ya kuoa wanawake warembo! Hijabu ya tabia inahusiana na wanawake wasiojali kushusha sauti zao wanapoongea na wanaume walio haramu zao. Kuna wanawake ambao sauti zao ni za kuvutia (kimaumbile) kiasi ambacho sauti kama hizo zaweza kuwa kivutio cha uzinifu. Wanawake kadhaa wana tabia ya makusudi ya kuwalegezea sauti wanaume wasio waume zao. Haifai pia kwa mwanamke wa kiislamu kupayuka ovyo mitaani. Tabia ya wanaume na wanawake wa kiislamu kusalimiana kwa kupeana mikono inakatazwa kwa sababu inasemekana kuwa kila Mtume (s.a.w.w.) alipolazimika kupeana mkono na mwanamke, kwanza alifunga kitambaa mkononi ili asigusane naye! Je, vipi kwa sisi wenye udhaifu wa kila aina? Tufahamu kuwa kumiminika kwa vipodozi madukani pamoja na wanawake kuzidi kudai uhuru wa kuchanganyika ovyo na wanaume, ni kinyume kabisa na sheria za Mwenyezi Mungu, kwa maana kwamba wingi 395


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 396

katika Uislamu

wa vipodozi sio uhalali wa kuvitumia bila mipaka. Wanawake kuchanganyika ovyo na wanaume eti kwa kisingizio cha kuondoa unyanyaswaji wa wanawake, ni kujifurahisha duniani kwa muda mfupi, lakini kesho akhera ni maangamio ya milele kama tutakavyoona hapa. Sheria za Mwenyezi Mungu hazitabadilika au kupunguzwa eti kwa sababu ya maendeleo ya kidunia yanayoongezeka haraka. Tukitaka tuzifuate au tuziache, lakini mwisho wake tutauona huko akhera muda si mrefu. Hayo aliyoyaona Mtume (s.a.w.w.) huko mbinguni Siku ya Miraj, ni ushahidi wa kutukumbusha yale tunayoyapuuzia hapa duniani wakati ambapo yanatusubiri huko akhera! Adhabu zenyewe ni kama ifuatavyo: (1) Mwanamke amening’inizwa kwa nywele zake, na ubongo wake unachuruzika kwa moto (unachemka). Sababu? Katika uhai wake hakuwa mwenye kufunika kichwa kwa ushungi. (2) Mwanamke amening’inizwa kwa ulimi wake. Sababu?: Alikuwa akimuudhi mumewe kwa ulimi huo huo. (3) Mwanamke anamiminiwa maji machafu ya Jahannamu kinywani mwake. Sababu? Alikuwa si mtiifu kwa mumewe. (4) Mwanamke amening’inia miguu juu kichwa chini, kwa matiti yake. Sababu? Alikuwa akitoka nje ya nyumba bila idhini ya mumewe. (5) Mwanamke ambaye kwenye sehemu zake za siri moto ulikuwa unawaka huku anakula nyama yake mwenyewe. Sababu? Alikuwa akijipamba na kuvaa mavazi mazuri na kujionyesha kwa wanaume haramu yake. (6) Mwanamke kafungwa mikono na miguu pamoja, huku nyoka na nge wanamuuma. Sababu? Alikuwa hajali usafi (tohara) wala haogi majosho ya wajib ‘ghusl’ yaani janaba na hedhi, na pia haswali Swala tano. 396


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 397

katika Uislamu

(7) Mwanamke akiwa kipofu, kiziwi na bubu amefungiwa ndani ya sanduku la moto na ubongo wake ukitokota kwa joto. Sababu? Alikuwa akimdanganya mumewe kwamba watoto aliowazaa ni wa yule mume wakati ambapo ni watoto haramu watokanao na uzinifu. (8) Mwanamke ambaye Malaika walikuwa wanamkatakata nyama yake ya mbele na mgongoni kwa mkasi, vipande vipande. Sababu?: Alikuwa akipenda kuonyesha sura yake ili wanaume wamtamani. (9) Mwanamke aliyekuwa na kichwa kama nguruwe, mwili kama punda. Sababu? Alikuwa mfitini na mwongo. (10) Mwanamke ambaye mikono yake yote miwili ilikuwa inaungua huku anachomwa moto mwili wake wote na anakula utumbo wake mwenyewe. Sababu? Alikuwa kuwadi akiwapeleka na kuwafanyia mipango wanawake kwa wanaume ili wazini. (11) Mwanamke akichochewa moto kwenye sehemu zake za siri. Sababu? Alikuwa mwimbaji na mwenye kijicho. Mpaka hapo tumeona baadhi tu ya adhabu zinazowasubiri wanawake ambao hapa duniani wanajidai kwenda na wakati, kwa maana kwamba sheria za Mwenyezi Mungu zimepitwa na wakati! Kama ni hivyo basi, tusubiri hicho kifo ndipo tuone kama ahadi ya Mwenyezi Mungu itatimia au hapana. Kila mtu maarufu anapofariki utasikia watu wanasema, ‘Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi’. Hayo ni maneno ya kujifurahisha kwa sababu kuingia peponi ni matendo binafsi ya mtu katika uhai wake, na siyo maombi ya watu kumwombea marehemu! Kama wewe binadamu hutaki kutii amri za Mwenyezi Mungu, ufahamu kuwa wewe ni mtu wa kuteseka huko akhera hata ukiombewa na mji mzima au kijiji kizima au nchi nzima! Ukichunguza Aya za Hijabu nilizozitaja hapo nyuma, utaona kuwa yanayokatazwa humo ndiyo yanayopelekea wanawake wengi kwenda motoni! Kwa hiyo kama akina mama watazingatia makatazo katika Aya 397


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 398

katika Uislamu

hizo, watanusurika na adhabu hizo. Vinginevyo kama akina mama watajidai kwenda na wakati, wafahamu kuwa dunia hii ni hadaa na muda si mrefu wataingia kaburini na kuyakuta yote waliyoyapuuzia katika uhai wao mfupi duniani. Mungu atuepushe na laana hiyo. Tukumbuke pia kwamba Mwislamu yeyote asiyeamini tukio la Miraj si Mwislamu tena, kwa sababu ni sawa na kusema kuwa pepo na Jahannam havipo; na kwamba Mwenyezi Mungu hana uwezo wa kufanya lolote atakalo, japo liwe ni muujiza kwa binadamu hapa duniani, kwa kadri ya elimu ndogo tuliyonayo. (20) Asili na uhalali wa kufanya Taqiyah: Suala la sisi Shia kufanya ‘Taqiyah’ inapobidi, limezusha malumbano ya kutukashifu na kutuita wanafiki, bila kwanza kuchambua ukweli wa mambo. Kimsingi Taqiyah maana yake ni mtu kuficha imani yake ya dini kwa watu ambao wanaweza kumdhuru kwa imani yake hiyo. Kihistoria utaona kuwa Shia, yaani wafuasi wa Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.), siku zote waliishi katika mateso makubwa na ya kuuawa kikatili, kila walipobainika kuwa ni wafuasi wa kizazi cha Mtume (s.a.w.w.). Hali hiyo iliwalazimu kuficha ukweli huo ili kuokoa maisha yao. Katika maisha ya kawaida utasikia watu fulani wanaficha uraia wao au itikadi zao kisiasa ili kuepuka madhara fulani. Kwa watu kama hao wanapoondokana na madhara hayo, hudhihirisha wazi tena yale waliyoyaficha. Kwa hiyo Taqiyah haiwezi kuchukuliwa kuwa ni unafiki. Ushahidi wa Qur’ani kuhusu Taqiyah ni kama ifuatavyo: “Anayemkufuru Allah baada ya Uislamu wake (ni mwongo) isipokuwa yule aliyeshurutishwa, hali ya kuwa moyo wake umetulia juu ya imani, lakini anayekifungulia ukafiri kifua chake, hao ghadhabu ya Allah iko juu yao, na watapata adhabu kubwa”. (Qur’ani 16:106). Aya hiyo ilishuka kuhusiana na kisa cha sahaba mwadilifu Ammar bin Yassir (r.a) alipolazimika kutamka maneno dhidi ya Uislamu ili kuokoa 398


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 399

katika Uislamu

maisha yake toka ukafiri wa Quraish. Hao Quraish walishamuua kinyama shahidi Yassir na mkewe Sumaiyah kwa sababu tu ya imani yao ya Uislamu. Hao marehemu walikuwa mashahidi wa kwanza wa kiislamu. Mtoto wao - yaani Ammar alipoona wazazi wake wameuawa mblele ya macho yake, alijifanya kuukana Uislamu na hivyo akanusurika. Ndiyo maana Aya niliyotaja hapo juu haikumwita Ammar kuwa ni kafiri au mnafiki. Hata hivyo, katika tukio hilo, mtu mmoja alimwendea Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia kuwa “Ammar amekuwa kafiri.” Mtume (s.a.w.w.) akajibu kuwa, ‘Kamwe, hakika nyama na damu ya Amar vimekithiriwa na Imani ya kweli.’ Vile vile imeandikwa kuwa katika tukio hilo hilo, Ammar alimwendea Mtume (s.a.w.w.) huku akilia kwa uchungu kwamba ametoa kauli mbaya dhidi ya Uislamu ili anusurike na shari ya makafiri. Mtume (s.a.w.w.) akamuuliza, “Uliuhisi vipi moyo wako?” Ammar akajibu “Ulikuwa imara katika imani.” Mtume akamwambia asiwe na wasiwasi na akamshauri kufanya hivyo tena akikumbana na shari kama hiyo. Tukio hili limetajwa katika vitabu vifuatavyo vya tafsiri ya Qur’ani: 1. Ad-Durrul’-Manthur - cha Imam as-Suyuti Jz. 4, uk.132. 2. Tafsir Al-Kashshaf, Zamakhshari – Beirut, Jz. 2, uk. 430. 3. Tafsir Kabir - Imam ar-Razi Lakini msimamo wetu kuhusiana na suala hili ni kwamba Taqiyah hairuhusiwi itumike kuwadhuru watu au kificha uzinifu, wizi, dhulma, ushahidi wa uongo, kusingizia mtu au kutoa siri za udhaifu katika ulinzi wa Waislamu. Taqiyah inaruhusiwa pia katika kulinda mali za Waislamu kutokana na Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba, ‘Mali ya Mwislamu ni sawa na ubora wa damu yake.’ Mtume (s.a.w.w.) alisema pia kwamba, ‘Atakayeuawa katika kulinda mali yake (basi amekufa) akiwa ni shahidi.’ Lakini pale ambapo Mwislamu anatakiwa kukataza maovu na kuamuru mema hakuna takiyah! Nina maana kwamba iwapo kuwaamuru watu 399


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 400

katika Uislamu

fulani waache uzinifu hakuhatarishi maisha yako, ni lazima ukataze uovu huo vinginevyo utakuwa na hatia. Vile vile kama utaogopa kuwakataza ulevi rafiki zako ili urafiki wenu usivunjike, hiyo siyo Taqiyah bali ni shirk ya kuwaogopa watu badala ya kumwogopa Mwenyezi Mungu. (21) Shia na Maana ya Bad’a: Imani yetu ni kwamba elimu ya Mwenyezi Mungu imekamilika. Maana yake ni kwamba hatutegemei mabadiliko katika elimu ya Allah. Lakini elimu waliyopewa Malaika na Mitume, japo ni kamili zaidi na sahihi zaidi kuliko viumbe wote, bado siyo kamili ukilinganisha na elimu ya Allah. Kwa rehema za Allah daima huwajaza elimu tena na tena kwa usahihi na ukamilifu. Nabii Ibrahim (a.s.) alionyeshwa katika ndoto kuwa alikuwa anamtoa kafara mtoto wake wa pekee ili kutekeleza mapenzi ya Allah. Kwa kuwa ilikuwa ni ndoto, bila shaka alionyeshwa hasa jinsi alivyokuwa anamuuwa Ismail. Bila shaka alijiona yeye mwenyewe akiifunga mikono na miguu ya mtoto wake, kujifunga yeye mwenyewe kitambaa cha macho kisha akaweka kisu juu ya koo la mtoto na kuanza kuchinja. Katika hali hiyo hakuweza kuona ni nani au nini hasa kilichokuwa kinachinjwa kwa vile macho yake yalikuwa yamefunikwa. Kwa kuona ndoto hiyo aliamini kwamba anatakiwa amchinje mwanawe Ismail katika hali hiyo (ya ndotoni). Hivyo aliufanya mgumu moyo wake ili amtoe kafara mtoto wake wa pekee. Mtoto Ismail naye aliisikia hii ndoto na alijitayarisha kutolewa kafara kwa unyenyekevu kwa amri ya Allah. Baba na mtoto kwa pamoja walikuwa tayari kutoa muhanga kila kitu kwa jina la Allah. Nabii Ibrahim alifanya kama alivyoota kwa kumfunga mikono na miguu Ismail na kumlaza chini. Kisha naye alijifunga kitambaa cha macho akaweka kisu na kukata koo. Lakini alipoondoa kitamba machoni alimwona Ismail anatabasamu hali ya kuwa pembeni yupo kondoo amechinjwa badala yake. Nabii Ibrahim alidhani ameshindwa mtihani aliopewa. Lakini alitimiza ndoto yake. Hapa tunaona kuwa Mwenyezi Mungu hakumfahamisha Ibrahim matokeo ya 400


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 401

katika Uislamu

hatua ya mwisho. Kama Ibrahim angejua kuwa Ismail ataokolewa au Ismail angejua hivyo basi kusingekuwepo na maana yoyote katika mtihani huo waliopewa. Kusingekuwa na hali yoyote ya kuonyesha kukubali kwao kutoa kafara ya chochote kwa jina la Allah. Kwa hiyo Allah alimwonyesha Ibrahim katika ndoto yake matukio hayo kwa kiasi fulani tu, lakini alimwacha bila kujua nini kitatokea hatua ya mwisho. Kwa kuwa hawakujua matokeo, Ibrahim na Ismail walikuwa tayari kuonyesha kukubali kwao jinsi walivyotii amri ya Allah, japo iwe ni kutoa mhanga maisha yao kwa mapenzi ya Allah. Na hiyo ndiyo maana ya Bad’a. Mfano mwingine ni pale Nabii Musa alipopewa amri kwenda mlima Sinai akae huko na kufunga saumu siku thalathini kwa matayarisho ya kupokea mbao za Tawrat. Siku ya thalathini alipiga mswaki meno yake na akaenda mlima wa Sinai. Huko aliulizwa na Allah ni kwa nini alipiga mswaki meno yake. Alieleza kuwa kwa vile alikuwa akija sehemu takatifu aliona ni bora ajitengeneze kuwa nadhifu na msafi. Allah akamwambia kuwa harufu ya mdomo wa mtu aliyefunga ilikuwa ni nzuri mbele ya Allah kama harufu ya misk na ambari. Kisha aliambiwa arejee sehemu yake aliyokuwa anakaa na akafunge siku kumi zaidi, kisha aje mlima wa Sinai bila kupiga mswaki meno yake. Siku ya arobaini ndipo alipopewa mbao za Tawrat. Mwenyezi Mungu alijua tangu mwanzo kuwa Musa atakuja baada ya kupiga mswaki meno yake, na atatakiwa kufunga siku 10 zaidi. Lakini hakuna aliyeambiwa habari hizi si Musa wala Waisraeli. Wala Musa hakuambiwa kabla kuwa asipige mswaki meno yake katika siku ile ya thalathini. Wakati Allah anapozungumzia juu ya elimu yake, anaandika muda wote wa siku arobaini kwa pamoja:

“Na (kumbukeni) tulifanya ahadi na Musa kwa siku arobaini. Kisha ninyi (Bani Israil) mkafanya (sanamu ya ) ndama (kuwa Mungu wenu) baada ya kuondoka Musa na hivyo mkawa madhalimu.” (Qur’ani 2: 51) 401


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 402

katika Uislamu

Na pale anapozungumzia elimu ya Musa, Anataja siku thalathini na siku kumi kwa mbali mbali:

“Na tulifanya ahadi na Musa kwa siku thalathini na tukazikamilisha kwa (siku) kumi (zaidi), hivyo ukakamilika muhula wa Mola wake (wa) siku arubaini.” (Qur’ani 7:142). Sababu zilizoacha isitolewe taarifa mapema ziko wazi kutokana na tabia ya Bani Israel ambao kwa sababu ya kuchelewa kwake siku kumi waliacha kumuabudu Mwenyezi Mungu Mmoja wa kweli na wakaanza kuabudu sanamu ya ndama. Kisa hiki kinaelezwa kwa uwazi katika Qur’ani: Allah akasema (kumwambia Musa):

“Tumewatia mtihani watu wako baada yako; na Saamiriy amewapoteza.” (Qur’ani 20:85).

“Hivyo Musa akarudi kwa watu wake kwa ghadhabu (na) masikitiko. Akasema: ‘Enyi watu wangu! Je, Mola wenu hakukuahidini ahadi nzuri? Je, umekuwa mrefu kwenu (muda wa) ahadi hiyo au mlitaka ikushukieni ghadhabu kutoka kwa Mola wenu, hivyo mkavunja ahadi na mimi?’” (Qur’ani 20:86).

402


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 403

katika Uislamu

“Wakasema: Sisi hatukuvunja ahadi yako kwa hiari yetu” (Qur’ani 20:87). “Na yeye Saamiriy akawatolea ndama, kiwiliwili tu kinachotoa sauti (kinapopigwa na upepo). Na wakasema: Huyu ndiye Mungu wenu na Mungu wa Musa. Lakini (Musa) amesahau.” (Qur’ani 20:88). Hebu fikiria watu wote (umma) wa Nabii Musa (a.s.) wakiwa na msaidizi wake (Mrithi wake) Harun, wanaacha njia ya kweli ya dini na kuanza kuabudu sanamu kwa sababu tu ya Musa kuchelewa kurejea kwa siku chache. Mtihani huu wa imani usingeweza kufanyika kama Allah (s.w.t.) angemweleza Musa kuwa akae siku arobaini au kama angemweleza mapema kuwa asipige mswaki meno yake siku ya thalathini. Na kwa hakika hiyo ndiyo maana halisi ya Bad’a. Hakuna Shia anayesema kuwa elimu ya Allah hubadilikabadilika kwa maana ya kwamba Allah hajui kwa ukamilifu sababu (za mambo) na mwisho wa matokeo yake! La Hasha. Neno Bad’a na maana yake, vyote vinatokana katika Qur’ani. Allah anasema: “........... Na yaliwadhihirikia kwao kutoka kwa Allah ambayo hawakuwa wakiyafikiria” (Qur’ani 39:47). Na hiyo ndiyo maana ya Bad’a, na neno hili hutumika wakati Allah anapofanya kitu kitokee kwa viumbe, ambacho hawakukitazamia. Mabadiliko hutokea katika elimu ya kiumbe, siyo katika ujuzi wa Allah (s.w.t.) Ujuzi wa Allah umekamilika nyakati zote. Anayedai kuwa Bad’a maana yake ni upungufu katika ujuzi wa Allah, huyo hawakilishi mtazamo sahihi wa Shia kuhusu somo hili. Mara nyingi watu waovu wamekuwa wanazusha itikadi za uongo dhidi ya madhehebu ya Shia Ithna’asheri, badala ya kurejea mafunzo sahihi ya Ushia kutoka katika vitabu vinavyoongoza madhehebu yetu. Isitoshe kama nilivyotangulia kueleza huko nyuma ni kwamba Ushia unapatikana kikamilifu katika vitabu vinavyoongoza madhehebu ya ndugu zetu Sunni, hata kama Sunni hawavifahamu vitabu hivyo kutokana na sababu mbali mbali. Kwa maana hiyo ni kwamba sisi Shia tunafuata Uislamu asilia na kila mara tunasisitiza kuwa Waislamu wafuate mafunzo ya asili, kwa kadri 403


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 404

katika Uislamu

ya mwongozo wa Qur’ani na Sunna sahihi za Mtume (s.a.w.w.). (22) Migogoro ya kuandama mwezi wa kuanza au kumalizia Ramadhani: Hadi miaka ya karibuni Waislamu wa Afrika ya Mashariki tulikuwa na ushirikiano wa karibu kwa kufunga au kufungua Ramadhan iwapo mwezi umeonekana katika nchi mojawapo ya nchi zetu hizi tatu. Lakini siku za karibuni ushirikiano huo umevunjika baada ya vijana wetu kwenda Saudi Arabia kwa wingi na kusomeshwa bure itikadi potovu za elimu ya dini, kisha wakahitimu na kurejea hapa kushika uongozi katika taasisi za kiislamu. Kwa miaka mingi sana Uislamu wa hapa Afrika Mashariki, Waislamu wengi sana ni madhehebu ya Shafii, yaani tukizingatia hukumu mbali mbali za dini zinazofuatwa hapa kwetu hata kama wengi wetu hatujui. Huko Saudi Arabia Waislamu wengi ni madhehebu ya Hanafi yaani wafuasi wa bwana Abu Hanifa kama nilivyoeleza katika Sura ya 17. Hivi sasa (1999) Saudi Arabia inasherehekea miaka 100 ya kuundwa taifa hilo. Lakini miaka 250 hivi iliyopita, kulianzishwa madhehebu mpya kwa njama za majasusi wa kiingereza wa wakati huo kwa lengo la kuwagawanya Waislamu na kuwafarakanisha ili kuwatawala kirahisi kwa mgawanyo wa makoloni kama tunavyofahamu. Maana yake ni kwamba miaka hiyo Waislamu walikuwa kitu kimoja bila kujali mipaka ya utaifa iliyopo sasa hivi. Mipaka iliyoyatenga mataifa ya kiislamu sasa hivi ni mafanikio yaliyokusudiwa na wakoloni kwa kadri ya maelezo ya jasusi mkuu mhusika, aliyejulikana kama Mr. Humphrey na ambaye aliamua kuandika na kuacha kumbukumbu sahihi ya historia ya njama hiyo kabla hajafariki. Baada ya majasusi hao waliotumwa na Wizara ya Mambo ya nchi za nje ya Uingereza, kufanikisha njama ya kuwagawa Waislamu, miaka 250 hivi iliyopita, kulizaliwa madhehebu hiyo ambayo jina lake la Wahabi linahu404


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 405

katika Uislamu

sishwa na muasisi wake aliyeitwa Abdul Wahabu ambaye ndiye kibaraka aliyetumiwa na majasusi hao kuanzisha madhehebu hiyo potofu! Madhehebu hiyo inahusika na mauaji makubwa ya Waislamu waliopinga uanzishwaji wa madhehebu hiyo potofu. Kwa kipindi cha takriban miaka 150 hivi madhehebu hiyo ilistawi chini ya viongozi mbali mbali, hadi kufikia miaka kama 100 iliyopita, ambapo lilianzishwa taifa la Saudi Arabia na ikawa dhamana ya madhehebu hiyo ya Wahabi wamepewa Wafalme wa ukoo wa Saud yaani watawala wa Saudi Arabia ambao ndio ukoo ule ule unaoendelea kutawala hadi leo kwa maslahi ya Magharibi na Marekani katika mfumo wa ukoloni mamboleo. Ndiyo maana Saddam Husein aliendelea kuadhibiwa vikali kwa kujaribu kuingilia au kuhatarisha maslahi ya mataifa makuu katika eneo hilo. Ili kutimiza lengo la kudhoofisha Uislamu dunia nzima, vibaraka hao wa Saudi Arabia kwa kutumia utajiri wa mafuta yao, wamekuwa mstari wa mbele kueneza Uwahabi duniani ili kudhoofisha Uislamu na kwa hiyo kuzima harakati za Waislamu kufufua mshikamano wa kweli wa kiislamu. Njama hizo za kubomoa Uislamu zimefichwa katika misaada mingi mbali mbali kama elimu ya bure kwa vijana wetu huko Saudia, ujenzi wa misikiti mipya, misaada ya kiuchumi kwa Waislamu pamoja na zawadi mbali mbali kwa Waislamu dunia nzima. Kwa hiyo tukirejea nyuma ni kwamba, vijana wetu waendao kusoma huko Saudia, wanarejea hapa na itikadi za kiwahabi japo wasijijue! Tatizo letu ni kwamba Waislamu tulio wengi hapa kwetu, tunaposikia shekhe fulani kasomea Makka au Madina tunaamini kuwa huyo kahitimu kweli kweli na hasa tunapomwona anamwaga kiarabu fasaha misikitini! Tufahamu kuwa watawala wa Saudia ndio wanaongoza na kutoa mwelekeo wa vyuo vyao vya dini kwa maslahi yao na kamwe siyo kwa maslahi ya Uislamu. Njama hiyo imefichika na siyo rahisi kwa Mwislamu wa kawaida kuitambua, hasa sisi wenye elimu ndogo.

405


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 406

katika Uislamu

Kwa hiyo Uwahabi umefika hapa kwetu miaka 250 baada ya kuazishwa huko Saudia! Sina maana kuwa Waislamu wote wa Saudia wanakubaliana na Uwahabi. Nasisitiza kwamba viongozi wakuu wa taasisi za kidini na uongozi wa nchi hiyo ndio wanatekeleza uwahabi kwa maslahi yao - kama tutakavyoona hapa katika maelezo yafuatayo chini ya somo hili. Hata hivyo, tayari baadhi ya Waislamu kama vile kutoka Kondoa vijijini hapa Dodoma wameshatambua upotofu wa Uwahabi. Mawahabi wamekuwa wanajificha kwa kubadilibadili majina ya madhehebu yao hiyo, lakini utawatambua kwa itikadi zao za kukataza maulidi na kisomo cha hitima na mengineyo tuliyoyazoea katika Uislamu wetu wa asili kama kusoma Talqin kaburini kwenye mazishi. Tabia ya kukimbiza jeneza la maiti ni ya kiwahabi - pia kwa wao kutoa tafsiri potofu ya Hadithi moja ya Mtume (s.a.w.w). Tukirejea hoja yetu ya msingi ni kwamba, tunasoma katika Hadithi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa, ‘Fungeni Ramadhan kwa kuuona mwezi na fungueni kwa kuuona mwezi.’ Rejea:- (1) Sahih Muslim (2) Sahih Bukhari. Nimeeleza katika Sura za nyuma jinsi ambavyo ni lazima Waislamu tutii amri (Sunna) za Mtume (s.a.w.w.) kama zilivyo. Waislamu wengi hapa kwetu wanaposikia kuwa Saudia wamefunga au wamefungua, huamini kuwa mwezi umeonekana huko! Ukweli ni kuwa huko Saudia, kalenda ya Kisaudia haiambatani na kuandama kwa mwezi bali hupangwa! Ndiyo maana siku zote tunasikia Saudia wanatangulia kufunga au kufungua bila mabadiliko! Mfumo huo ni kinyume na maumbile (ya asili) ya mizunguko ya sayari kwa sababu unapingana na takwimu sahihi za vituo vya uchunguzi wa anga vya Ulaya na Marekani, ambavyo vina mitambo ya kisasa iwezayo kutoa taarifa sahihi kuhusu lini, muda gani na mahali gani duniani ambapo mwezi au jua litapatwa japo iwe miaka 200 ijayo!

406


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 407

katika Uislamu

Kwa kutumia takwimu (data) za vituo hivyo, sisi Shia Ithna’asheri hutumia wataalamu kufanya mahesabu ya kutusaidia kujua nyakati sahihi za Swala na mwisho wa kula daku, kutegemea tupo sehemu gani duniani au kama ni hapa Tanzania tupo mkoa gani; kwani kila mkoa una nyakati zake tofauti, japo tofauti hiyo iwe ni dakika tatu! Ndiyo maana mara nyingine nyakati za adhana kati ya Shia na Sunni hutofautiana! Kwa maelezo haya machache nataka kuonyesha kuwa sisi Shia hutumia takwimu za vituo vya uchunguzi wa anga kujua ni sehemu gani ya dunia na ni muda gani ambapo mwezi unaweza kuonekana, na wala siyo Saudia peke yake kila mwaka! Kukubali kuwa lazima kila mara mwezi utangulie kuonekana Saudia, ni sawa na kulazimisha kuwa kila mwezi au jua likipatwa litapatwa katika anga ya Tanzania tu milele! Hata hivyo takwimu hizo toka vituo vya uchunguzi zinatusaidia tuweze kufahamu sehemu ya dunia inayofaa kuangalia mwezi lakini kuonekana kwa mwezi tukiwa ardhini, kunategemea anga isiyo na mawingu. Katika Hadithi niliyotaja nyuma, Mtume (s.a.w.w.) anatuamuru kuwa tufunge siku thalathini iwapo mwezi haukuonekana na siyo zaidi. Kalenda ya Saudia wanayoifanya kuwa kalenda ya kiislamu ijulikanayo kama Umm-ul-Qura ni kalenda potofu isiyohusiana na Uislamu hata kidogo kwa kadri ya Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) ya kufunga na kufungua kwa kuona mwezi. Kwa miaka mingi sasa, kalenda hiyo hutegemea tu mahesabu ya mwezi mpya wa kifalaki, kwa maana kwamba vituo vya uchunguzi wa anga kwa kutumia mitambo yao, wanafahamu siku na muda na mahali pa kuonekana mwezi mpya. Lakini mwezi mpya hauwezi kuonekana kwa macho ya binadamu duniani mpaka upite muda wa masaa 20! Katika masuala ya kuangalia mwezi hatuwezi kutegemea mwezi mpya wa kifalaki kuwa ndiyo mwezi umeonekana! Ni lazima tuone mwezi kwa macho au zipite siku 30 kabla ya kuanza mwezi wowote mpya wa kiislamu.

407


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 408

katika Uislamu

Lakini hata kama tungekubaliana na kigezo cha ‘mwezi mpya wa kifalaki’ kuwa sahihi, si lazima kuwa kila mwezi mpya unastahili kuonekana Saudi Arabia peke yake! Sasa ni kwa nini tukubaliane na Saudi Arabia hata kama vituo vya uchunguzi wa anga vyenye usahihi vinaonyesha uwezekano wa kuona mwezi mara ya kwanza sehemu nyinginezo duniani! Baada ya kutokea kasoro hii, Waislamu wa nje ya Saudia, walianza kuhoji msimamo wa chombo cha juu cha masuala ya dini hapo Saudia, kijulikanacho kama Majlis al-Ifta’al-Aala. Chombo hicho ni jopo la maulamaa viongozi. Viongozi hao ni vibaraka wa watawala. Mojawapo ya waliohoji msimamo huo potofu wa Saudia ni taasisi ya The Jordanian Astronomical Society kutoka nchi ya Jordan. Hilo jopo la maulamaa wa Saudia walijibu kuwa, ‘Tunataka kuwakumbusha kuwa kigezo cha kuamua siku ya kwanza ya mwezi wa kiislamu ni sawa na nyakati za Swala na kwa hiyo lengo la Mwenyezi Mungu lilikuwa ni taarifa tu na siyo tulichukulie kama ibada! Maana yao ni kwamba siku ya mwezi mpya wa kiislamu inaweza kupangwa kama tunavyobadili nyakati za Swala majira mbalimbali! Hata hivyo, nyakati hizo hubadilika kufatana na mahali linapokuwepo jua kuhusiana na dunia, yaani, kwa mfano tafsiri ya kivuli cha mtu kutoonekana akiwa amesimama wima, kuwa ndio wakati wa Adhuhuri, hubadilika miezi mbalimbali mwaka mzima na wala siyo muda wote huwa ni saa ileile, na ndio maana saa za Swala hubadilika sambamba na saa ambayo jua huwa utosini au jua kuchwa au kuchomoza. Kupanga saa za Swala kuna vigezo na sio uamuzi tu. Kwa jibu hilo la unafiki wa Saudia kuhusu kalenda yao potofu, sisi tunabakia kujiuliza kwamba, ni vipi tutaendesha Uislamu usiozingatia amri za Mtume (s.a.w.w.) na Mwenyezi Mungu? Waislamu tuwe macho na hujuma kama hizi pia tuache kasumba ya kukumbatia kila kitokacho Makkah na Madina kuwa ni sahihi bila kupata elimu kwa kurejea vitabu muhimu vyenye mafunzo sahihi ya Uislamu.

408


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 409

katika Uislamu

Unafiki huo wa jopo la maulamaa wa Saudia, umebainika wazi wazi mwaka wa 1999 mwezi wa Januari, wakati wa mwanzo wa mfungo wa Ramadhan! Kalenda ya Saudia ilionyesha kuwa Jumamosi, Desemba tarehe 19/12/98 ndiyo tarehe mosi ya Ramadhani! Lakini kutokana na takwimu za mahesabu ya kifalaki kamati ya Crescent Observation International ya New York - U.S.A. inapinga vikali uongo huo kutokana na ukweli kwamba eneo hilo la Saudia, mwezi ulitakiwa kutua dakika 12 kabla ya jua! Kwa maana hiyo mwezi usingeweza kuonekana Cairo wala Makka. Mahesabu hayo ya vituo vya uchunguzi wa anga yanaonyesha kuwa mwezi ulitakiwa kuonekana kwanza tarehe 19/12/98 huko Amerika ya Kaskazini; kwa hiyo Ramadhan ilitakiwa kuanza tarehe 20/12/98 Jumapili katika eneo hilo la dunia. Sehemu nyinginezo zilizobakia za dunia Ramadhan ilitakiwa kuanza tarehe 21/12/98, Jumatatu. Maana yake ni kwamba Waislamu wa hapa Tanzania waliwahi kufunga siku moja kabla ya Ramadhan ya kweli kuanza! Kwa mahesabu hayo hayo, ilibainika wazi mapema kuwa Idd-el-fitr itakuwa tarehe 19/1/99 Jumanne. Na hivyo ndivyo ilivyokuwa! Sisi Shia Ithna’asheri tuna kalenda zetu zinazozingatia Sunna sahihi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kila mwezi wa kiislamu huwa tunauangalia kwa uhakika wa kuandama sawa na mwezi wa Ramadhan ili tusipoteze tarehe sahihi za kuadhimisha matukio muhimu ya kiislamu, kama vile kuzaliwa au kufariki kwa viongozi wetu Maimamu 12 (a.s.) n.k. Kwa hiyo sisi Shia hupokea taarifa za kuandama kwa mwezi toka taasisi zetu zilizo dunia nzima juu ya suala hili, na siyo kutegemea Saudia au vigezo vinginevyo visivyozingatia misingi hii. Kufuatia mgogoro wa mwaka 1999 juu ya kuandama mwezi, sisi Shia tulianza kufunga tarehe 21/12/98 Jumatatu wakati wenzetu Sunni walianza Jumapili tarehe 20/12/98. Kufuatana na takwimu za Vituo vya Uchunguzi wa anga, zilizoeleza kuwa uwezekano wa kuonekana mwezi Jumamosi tarehe 19/12/98 ulikuwa ni katika eneo la Amerika ya Kaskazini 409


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 410

katika Uislamu

tu, sisi Shia hatukuafiki kuanza kufunga tarehe 20/12/98! Sababu zetu kubwa ni kwamba Saudia inapotosha Waislamu, na kisha tunaamini kuwa vituo vya uchunguzi wa anga ni vya kuaminika katika enzi hizi za sayansi na teknolojia kwa sababu vituo hivyo hivyo hutabiri kupatwa kwa jua au mwezi kwa uhakika wa mahali, wakati na muda na dakika za kupatwa! Kwa kweli hata hiyo Saudia hutegemea takwimu hizo hizo za mwezi mpya wa kifalaki kuwa ndiyo tarehe yao ya mwanzo wa mwezi wa kalenda yao ya Umm-ul-Qura! Msimamo huo siyo sahihi kwa sababu ni kinyume na mafunzo ya Mtume (s.a.w.w.) na ni kuvuruga kawaida tuliyozoea kwa karne 14 sasa! Ilimradi Saudia wanakubali kuwa hawafuati kuonekana kwa mwezi kwa macho kuwa kigezo muhimu, kwa nini basi sisi huku tukumbatie upotofu wao wa makusudi? Uislamu ni kanuni siyo utamaduni. Lengo la Uwahabi ni kuvuruga Uislamu ili kudhoofisha umoja wa kiislamu kwa faida ya Magharibi na Marekani na ufalme wao. Baadhi ya Mawahabi wanatumiwa bila kujijua kama alivyotumiwa muasisi wake Abdul Wahab pale mwanzoni kwa kadri ya historia yake. Kama tutadumisha Uislamu wa kurithi, bila kutumia akili kwa kupata elimu ya kutosha ya kutuwezesha kuifahamu dini, tutajikuta tumegeuka kuwa wafuasi wa shetani bila kujijua - (Qur’ani 14:22). Taarifa juu ya upotofu wa Saudia kuhusiana na suala hili, zimepatikana katika makala iliyoandikwa na bwana Athman Amran. Makala hiyo ilichapishwa katika toleo la gazeti la East African Standard – Kenya, la tarehe 11 Januari, 1999. Utatanishi wa kuandama mwezi ulitokea pia mwaka 1997 ambapo huko Amerika ya Kaskazini Waislamu wengi walisherehekea Idd-el-Adh’ha siku ya Ijumaa, tarehe 18 April, 1997. Lakini baadhi ya Waislamu walio chini ya taasisi ya Islamic Society of North America (ISNA) na misikiti yao, waliamua kufuata kalenda ya Saudia, na hivyo kusherehekea Idd el Hajj mapema kabla ya wakati wake halali, yaani tarehe 17 April 1997. Siku hiyo ilikuwa ni tarehe 9 Dhul-Hijjah kwa mujibu wa kalenda sahihi ya kiislamu. Kwa kawaida tangu uhai wa Mtume 410


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 411

katika Uislamu

(s.a.w.w.), Idd el Hajj husherehekewa tarehe 10 Dhul Hajj. Kwa hiyo tabia ya Saudia ya kujipangia tarehe za miezi ya kiislamu ni upotofu ulio dhahiri. (Qur’ani 14:22). Tukirejea Qur’ani (2:189) tutaona kuwa misingi ya kalenda sahihi ya kiislamu imeelezwa wazi pamoja na ibada ya Hijjah. Hakuna mahali popote katika Qur’ani au Sunna ambapo tumeamrishwa kufuata maoni ya watu wa Saudia badala ya kufuata Qur’ani na Sunna! Na hasa baada ya kubainika kuwa Saudia wanakiuka misingi halisi ya Uislamu. Tukijadili sula hili kisayansi, tutaona kuwa mwezi wa kiislamu ni mfupi kuliko mwezi wa kawaida; na kwamba dunia ni mviringo. Kwa hali hiyo ni wazi kuwa mwezi mpya wa kiislamu siku zote utaonekana nyakati tofauti sehemu mbali mbali za dunia. Kisayansi ni kwamba kwa kuwa dunia ni mviringo, eneo la dunia magharibi mwa Makka, wanastahili kuona mwezi mpya kabla ya Saudi Arabia! Kwa maana hiyo, Waislamu wa Amerika ya Kaskazini wanaweza kuwa wanasherehekea Idd-el-Hajj wakati huko Makka bado Waislamu wamo katika ibada ya Hijja huko Arafa! Hali hii ni sahihi iwapo tutazingatia misingi halisi ya kalenda ya kiislamu. Tusichukulie kuwa kwa kuwa Makka na Madina ziko Saudi Arabia, basi lazima tuwaabudu watu wa huko! Mtume hakuwahi kuamuru kuwa ni lazima Waislamu duniani kote kwanza wajue siku ya Arafa huko Makka ndipo warekebishe tarehe zao za siku ya Idd-el-Hajj! Utaratibu sahihi ni kwamba Idd-el-Hajj ni tarehe 10 mwezi wa Dhul Hijjah. Kwa hiyo Saudia inajitumbukiza katika uzushi (bidaa’) wa kupotosha Waislamu kwa sababu kuandama mwezi ni sawa na kuchomoza au kutua jua kwa nyakati tofauti popote duniani. Kama Waislamu duniani kote wataamua kufuata kalenda bandia ya kiislamu ya Saudia, watajikuta na tarehe mbili tofauti za tarehe 10 Dhul Hijjah! Tarehe moja kwa kadri ya kalenda bandia ya Saudia; na tarehe nyingine kwa kadri ya kuandama kwa mwezi mahali walipo! Je, watasherehekea Idd mbili? Si hivyo tu bali kwa kufuata kalenda ya Saudia isiyo na kanuni 411


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 412

katika Uislamu

maalumu wala vigezo vya dini, Waislamu watajikuta na mwezi wa Dhul Hijjah wa siku 28 tu (kama ilivyotokea mwaka huu)! Wakati mwingine katika misingi hiyo, twaweza kuwa na siku 31 za mwezi wa Dhul Hijjah, jambo ambalo haliwezekani kwa miezi sahihi ya kiislamu! Haya ni maajabu! Mwezi wa kiislamu lazima uwe na siku 29 au 30 basi, na si vinginevyo. Kwa mahujaji, jambo la busara ni kutegemea tarehe za kuonekana mwezi pale Makka na siyo tarehe za kuonekana mwezi za huko makwao, ili kuondoa hali ya utata. Na kwa maana hiyo haiwezekani mahujaji hao wawapangie siku ya Idd-el-Hajj Waislamu wengine wasiokuwepo hapo Makka! Hayo hayaingii akilini. Maelezo haya ya ziada yanapatikana katika: Crescent International Magazine, Vol.26 No.4, May 1-15, 1997 - Canada. (23) Uhalali au uharamu wa serikali za mataifa duniani: Kuna vikundi kadhaa vya Waislamu ambavyo hupita misikitini vikitoa hotuba kali za kupinga utawala wa serikali za kawaida za mataifa. Viongozi wa vikundi hivyo wangependa kuona nchi zote duniani zikiongozwa na Waislamu katika misingi ya kiislamu. Ni kweli kwamba Mwenyezi Mungu alikusudia Uislamu utawale dunia nzima. Lakini hali halisi tumeiona huko nyuma (Sura ya 6, 7 na 8) ambapo ni wazi kuwa Waislamu walio wengi hawakupenda kutawaliwa na Uislamu asilia. Hali hiyo inaendelea hadi wakati huu duniani. Mawazo yangu ni kwamba, sisi Waislamu kwa kiwango kikubwa hatuishi (kimaisha) kama Waislamu waaminifu. Hakuna serikali inayokataza Waislamu kuswali Swala tano au kutoa Zaka. Wala sijasikia Waislamu wamekatazwa kujenga misikiti au kupata mafunzo ya dini. Sijaona Waislamu wanalazimishwa na serikali kunywa pombe au kuzini. Nataka kubainisha kuwa kwa kiwango kikubwa sana, sisi Waislamu ndio tunaovunja Uislamu kwa kuacha kutekeleza yale yote tunayowajibishwa 412


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 413

katika Uislamu

katika dini, wakati ambapo serikali nyingi za mataifa hazijatuzuia kuishi katika mipaka ya dini yetu, kwa kiasi kikubwa. Madai ya kwamba serikali zote ziongozwe na Waislamu, hayana msingi kwa sababu kwanza tumeona nyuma (Sura ya 18 na 19) jinsi ambavyo viongozi Waislamu waovu walivyowatesa na kuwatendea uovu raia, kiasi ambacho ninaamini kuwa kiongozi Mkristo angewatawala Waislamu asingewatendea hivyo! Hata hivi leo zipo nchi nyingi za Waislamu wengi sana na viongozi wao ni Waislamu lakini nchi hizo hazitawaliwi na misingi thabiti ya kiislamu. Uislamu wa kweli ni ule wa vitendo. Tukizingatia kanuni za dini yetu tutaona kuwa, kama kwa mfano wangetokea viongozi waaminifu wa kiislamu wakaongoza nchi kwa misingi thabiti ya dini yetu, ni wazi kwamba wapinzani wakubwa wa utawala wa namna hiyo wangekuwa Waislamu! Sababu kubwa ni kwamba utaona kwa mfano katika mwezi wa Ramadhan wenye biashara za pombe wanalalamika kukosa wateja ambao wengi wao ni Waislamu! Iwapo Waislamu hatuko tayari kutawaliwa na Uislamu kwa nini tudai serikali za kiislamu? Isitoshe kama nilivyochambua historia sahihi ya Uislamu huko nyuma, tumeona kiwango ambacho Uislamu umepotoshwa kupitia tawala kadhaa za dola za kiarabu na mwisho Waturuki. Walioongoza upotofu huo ni Waislamu! Kwa hiyo tutaona kuwa kwa kadri ya hali halisi ya wakati huu duniani, ni vigumu kuwa na serikali halisi za kiislamu zenye uwezo kamili juu ya raia. Kwa ukweli huo, hatuna budi kuridhika na serikali zilizopo madarakani, ili mradi serikali hizo si za kidhalimu na zinajitahidi kudumisha amani ili Waislamu raia wa nchi hizo wawe na uhuru na usalama wa kumwabudu Mwenyezi Mungu. Tusidai uongozi wa kiislamu kwa manufaa yetu ya kidunia. Kwa upande mwingine hakuna faida yoyote kwa Waislamu ambao wanaishi nchi za Kislamu ambazo viongozi wake hawana ujuzi wa kutosha wa dini, na matokeo yake ikawa ni kuwakandamiza raia kwa matumizi ya sheria batili zinazodaiwa ni za kiislamu. Huko nyuma nimetangulia kueleza kuwa, kwa wakati huu ni nchi moja tu 413


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 414

katika Uislamu

duniani ambayo Katiba yake ni ya kiislamu na sheria zake vile vile. Nchi hiyo ni Jamhuri ya Kiislam ya Watu wa Iran. Pamoja na nia nzuri ya marehemu Imam Khomeini (R.A.) kuongoza harakati ndefu za kufufua Uislamu nchini humo, bado kuna makundi ya upinzani yanayopinga utawala huo! Je, nchi zetu ambazo tunaishi watu wa dini tofauti kwa miaka mingi, vipi itawezekana zitawaliwe na sheria za kiislamu? Faida gani kukazania malengo yasiyowezekana? Mwezi wa pili mwaka 2000, dunia nzima ilielekeza masikio nchini Iran ili kujua matokeo ya uchaguzi wa wabunge wapya. Vyombo vya habari vilitangaza kwa furaha kwamba matokeo yanaonyesha kuwa, wamechaguliwa wabunge wengi wapenda mageuzi, na kwamba wabunge wasiopenda mageuzi ni wachache, na kwa hiyo bunge litakuwa na uwezo mkubwa wa kupitisha maamuzi ya kuwapa raia uhuru zaidi wa mambo yao. Matokeo hayo yana maana kwamba raia wa Iran walio wengi hawapendi kubanwa na sheria za Mwenyezi Mungu bali wanataka kujitungia sheria kwa manufa yao ya kidunia. Lakini nimeeleza huko nyuma kuwa Taifa la Serikali ya kiislamu ni lile ambalo mambo yake yote yanaongozwa na Sharia sahihi ya kiislamu kwa ushahidi wa Qur’ani:

“Haiwi kwa muumin mwanamume au muumin mwanamke kuwa na uchaguzi katika mambo yao wakati Mwenyezi Mungu na Mtume Wake wameshakata shauri.” (Qur’ani 33:36)

“Sikuwaumba majini na binadamu ila waniabudu” (Qur’ani 51:56).

414


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 415

katika Uislamu

“Na Mola wako Huumba Alitakalo na Huchagua Alitakalo; wao viumbe hawana hiari....” (Qur’ani 28:68). Aya hizi zinatufundisha kuwa katika Uislamu wa kweli ni lazima binadamu watii amri zote za Mwenyezi Mungu na Mtume (s.a.w.w.) kama msingi mkuu wa maisha yao. Kwa mantiki hiyo ni kwamba hata kama Waislamu wa taifa fulani watapiga kura kwa wingi kuchagua mfumo usiozingatia Aya hizi, hatuwezi kuwapongeza bali kuwasikitikia. Kwa upande mwingine tunaona wazi kuwa Shariah ya kweli ya kiislamu ikitumika kwa usahihi na uaminifu, haina ukandamizaji wowote wa haki za binadamu kwa sababu Mwenyezi Mungu hana sifa ya udhalimu au ukandamizaji kwa viumbe wake! Kwa hiyo madai ya vyombo vya habari vya Magharibi kwamba wananchi wa Iran wamefanikiwa kuelekea kupata haki kamili za binadamu, siyo kweli kwa mtazamo sahihi wa kiislamu. Hata kama wananchi wote wa Iran au Waislamu wote wa dunia nzima wataunga mkono mwelekeo huo, bado ukweli unabakia ule ule kwamba ni kinyume na Uislamu. Kama Waislamu hawataki kutawaliwa na Uislamu; si tatizo kwa Mwenyezi Mungu ambaye anasubiri kutulipa Siku ya Kiyama. Zaidi ya hayo niemeeleza katika Sura ya tano na sita jinsi Waislamu walivyopinga wasia wa Mtume (s.a.w.w.) pale pale alipofariki hata kabla hajazikwa! Nimeeleza pia kwamba upinzani huo ulikuwa mkubwa kiasi kwamba ni asilimia kumi tu ya Waislamu wa wakati huo ambao walitii wasia wa Mtume (s.a.w.w.)! Je, hizo ndizo haki za binadamu? Baada ya kupita karne kumi na nne tangu kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), haishangazi kuona upotofu unazidi kuongezeka miongoni mwa Waislamu. Viongozi wachache wa Iran wanaotetea maslahi ya Uislamu, tusiwaone kama kikwazo kwa kupingana na raia walio wengi. Wajibu wa viongozi hao ni kutetea haki ya Mwenyezi Mungu hata kama raia walio wengi hawataki. Msimamo huo ni sawa na vile ambavyo serikali yoyote hutunga sheria na kuweka wasimamizi wa sheria, mahakama na magereza. Maana yake ni kwamba raia hawapendi kutii sheria yoyote ile iwe ya dini au dunia. Mahakama ya Mwenyezi Mungu ni Siku ya Kiyama. Gereza la 415


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 416

katika Uislamu

Mwenyezi Mungu ni Jahannam. Yote tutayaona muda wake ukiwadia. Sheria ya Mwenyezi Mungu haiwezi kujadiliwa na watu ili kuona kama wanaipenda au hawaipendi. Wajibu wetu ni kumtii Mwenyezi Mungu kwa kila hali. Umaarufu wa chaguo la watu siyo uhalali wake mbele ya Mwenyezi Mungu. Mnamo nusu ya kwanza ya mwezi wa tatu mwaka 2000, vyombo vya habari vilitangaza kuwa nchini Morocco, serikali ilikuwa inatayarisha kuidhinisha kutungwa sheria inayowazuia wanaume kuoa wake wawili! Tamko hilo liliwafurahisha wanawake ambao waliandamana kuunga mkono! Wanaume walipinga sheria hiyo kwamba inapingana na Qur’ani. Tukizingatia kwamba Morocco ni nchi ya kiislamu na ina Waislamu zaidi ya milioni 22, tunashangaa kuona mwelekeo huo wa serikali hiyo! Tunajiuliza vipi itungwe sheria inayokiuka mafunzo ya Qur’ani katika nchi ya kiislamu? Hapa tunapata fundisho kwamba ni Waislamu wachache ambao wako tayari kutawaliwa na sheria za Mwenyezi Mungu. Katika hali hiyo, suala la matakwa ya walio wengi halina maana yoyote katika misingi sahihi ya dini. Uislamu hautoi mwanya wa watu kupingana na Mwenyezi Mungu. Vile vile tunajifunza kuwa katika karne 14 za Uislamu, bila shaka viongozi wengi waovu waliopita, walitunga sheria zao zinazopingana na mafunzo sahihi ya dini, na kisha sheria hizo zikawa sehemu ya dini kwa vizazi vilivyofuatia. Ndiyo maana nimesisitiza katika kitabu hiki kwamba Waislamu tuachane na Uislamu wa kurithi kama msingi mkuu wa ibada zetu. Badala yake tutafute elimu sahihi ya dini kwa uhakika wa ibada zetu. (24) Eda ya kufiwa na mume na eda ya talaka kwa wanawake: Eda kwa wanawake ni ibada iliyotawaliwa na mila zisizo na msingi wowote wa dini, isipokuwa kuwatesa wanawake na mzigo wa mila za makabila zinazopingana na dini katika nchi mbali mbali za kiislamu. Kama

nilivyoeleza

mwanzoni

mwa 416

kitabu

kwamba

Uislamu


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 417

katika Uislamu

umechanganyika na mila kiasi ambacho si rahisi kutofautisha iwapo huna ujuzi wa dini. Nimeeleza pia kwamba Mtume (s.a.w.w.) alituamrisha kuwa tuachane na mila zinazopingana na dini. Lakini utaona kuwa Waislamu bado tunatanguliza mila na utamaduni wa makabila yetu, lakini dini tunaiweka nyuma. Tabia hii imeenea sana miongoni mwa jamii ya kiislamu kwa ujumla. Kwa upande wa madhehebu ya Sunni, nakumbuka marehemu Saleh Farsy alipinga vikali mlolongo wa masharti anayoamrishwa mwanamke katika eda ya kufiwa na mume. Kibaya zaidi ni kuyatekeleza masharti hayo kama sehemu ya dini wakati kimsingi ni mila potofu. Kanuni za eda ya mke kufiwa na mume ni chache na nyepesi kidini, nazo ni kwamba mwanamke akae eda ya maombolezo ya miezi minne na siku kumi. Eda hiyo ni wajibu kwa mwanamke hata kama mwanamke huyo amekwishakoma kupatwa na hedhi au hata kama ndoa ilifungwa lakini ikawa bado kukutana kimwili na mumewe. Masharti juu ya mwanamke kwa kadri ya madhehebu ya Shia Ithna’asheri ni kwamba mama huyo haruhusiwi kuolewa, kuvaa nguo za rangi mchanganyiko au mapambo, kujitia manukato na kushiriki starehe, mpaka muda wa eda uishe. Kumvalisha mwanamke mabaki ya kitambaa cha sanda ya mumewe na kumwamuru avae nguo hiyo milele hadi ichakae, siyo kanuni ya dini bali ni mila. Kumlazimisha mwanamke kukaa ndani asitoke wala asizungumze na watu fulani katika muda wa eda siyo dini bali ni mila. Iwapo mama huyo hana mtu wa kumletea riziki hakatazwi kwenda kujitafutia riziki kwa njia za halali. Kumvalisha mjane nguo za kusitiri mwili wake na kumkataza kuongea na wanaume wasiomhusu kisheria, hizo ni kanuni za kila siku za mwanamke wa kiislamu, na siyo wakati wa eda peke yake. Sehemu za pwani ya Afrika Mashariki, wajane wa kiislamu hukandamizwa na mila nyingi potofu katika eda zao, na hivyo kuwafanya waione dini kuwa ni ngumu. Mnamo katikati ya wiki ya pili ya mwezi wa nane mwaka 1999, kituo cha 417


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 418

katika Uislamu

radio cha BBC, Idhaa ya kiingereza kulikuwa na kipindi ambacho kilieleza jinsi ambavyo wanawake wa Nigeria hudhalilishwa mara wafiwapo na waume zao, kwa kisingizio cha sheria potofu za eda. Kwa mfano hulazimishwa kunywa maji yaliyooshea marehemu waume zao na kupelekwa mitoni kuoga maji ya baridi asubuhi wakiwa uchi hadharani! Kisha mali zote za marehemu huchukuliwa na ndugu wa marehemu bila hata kujali wajane na watoto! Hayo yana uhusiano gani na Uislamu? Labda yanafanyika maeneo ya wakristo! Tukizingatia kuwa Nigeria ni nchi ya Waislamu wengi sana, tunashangaa na kujiuliza kama kweli huo ndio Uislamu? Kama mila hizi potofu zingeendeshwa na wasio Waislamu ni sawa, iwapo msimamo huo haupingani na sheria za nchi zao. Lakini kwa sisi Waislamu lazima tutangulize Uislamu. Kwa hakika Uislamu wa kweli (Uslam asilia) unazo kanuni bora sana za usawa na haki kuliko sheria za nchi yoyote duniani. Kwa mfano huko Iran wafungwa wa kiume magerezani, hupewa fursa ya kukutana na wake zao kimwili mara kwa mara, kwa sababu kufungwa siyo kupoteza hadhi ya ubinadamu. Je, ni nchi gani nyingine zenye mifano kama hiyo, hata katika hizo nchi ambazo zinajiita ni za Kiislam? Kwa hiyo tutambue kuwa uzito wa kanuni za eda ya mke kufiwa na mume, utegemee dini na siyo mila au utamaduni. Mwenyezi Mungu ameleta Uislamu ili kuvunja mila potofu za makabila. Tufahamu kuwa kabla ya Uislamu kuletwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Waarabu walikuwa na mila chafu ambazo Mtume (s.a.w.w.) alizipiga vita. Wajibu wa Mwislamu ni kufuata nyayo za Mtume (s.a.w.w.). Kwa upande mwingine ninatambua kuwa Sunni wa hapa kwetu wanaitambua eda ya talaka lakini ni wachache wanaojali kuitekeleza ipasavyo au wanaoipa uzito. Masharti ya eda ya talaka kwa mwanamke ni kwamba muda wa eda hiyo ni miezi mitatu kuanzia pale anapopewa talaka. Kanuni sahihi za kutoa talaka nimetangulia kuzieleza nyuma (Sura ya 10). Akiwa kwenye eda, mwanamke hubakia nyumbani kwa mumewe na kutunzwa kikamilifu. Ni 418


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 419

katika Uislamu

lazima mama huyo awe mtiifu na asitoke nyumbani bila idhini ya bwana. Hairuhusiwi muda huo kukutana kimwili, lakini wakifanya hivyo, eda na talaka vinabatilika na hivyo ndoa inaendelea. Iwapo kuna uhasama kiasi ambacho mke hawezi kuvumilia kuishi na mume katika eda, anaweza kuishi penginepo chini ya masharti hayo hayo lakini kwa gharama ya mume. Hekima ya Mwenyezi Mungu kuamrisha utaratibu huo wa talaka, nimeieleza kwa ufasaha (Rejea Sura ya 10) chini ya ‘Talaka tatu kwa Mpigo.’ (25) Tofauti mchanganyiko katika hukumu za madhehebu matano: Kama nilivyotangulia kueleza huko nyuma kwamba Waislamu tuliowengi, katika uhai wetu wote, tunajiambatanisha na madhehebu ambayo hatujui hukumu zake kuhusiana na ibada zetu mbali mbali za kila siku! Tufahamu kuwa matendo yoyote tutendayo katika ibada zetu, yanatokana na hukumu fulani kutoka madhehebu fulani. Kinyume na hivyo ni sawa na mgonjwa kumeza dawa zozote bila maelekezo ya daktari. Kitendo kama hicho hakiwezi kumsaidia mgonjwa bali kumletea madhara. Ni ajabu kwamba baadhi ya Waislamu wa madhehebu fulani, katika msikiti wao, wakiona Mwislamu asiyefuata taratibu zao za ibada, humwandama na mara nyingine hata kumfukuza hapo msikitini! Migogoro kama hii inatokana na upungufu wa elimu juu ya madhehebu, ambapo Waislamu wengi hung’ang’ania mazoea kama walivyowaona babu zao wakifanya. Lakini mazoea siyo sheria! Na wala dini siyo utamaduni!1 Lakini kwa upande wa ndugu zetu wakristo, madhehebu zao tofauti hazijazua ugomvi kati yao. Utaona Wakristo kila mmoja anafuata kanisa lake bila migongano. Waislamu tunatakiwa tuige mfano huo wa kuheshimiana 1. Na wakiambiwa: Fuateni aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, husema: Bali tutafuata tuliyowakuta nayo baba zetu. Je, hata kama baba zao walikuwa hawafahamu chochote wala hawakuongoka? (Qur'ani; 2:170). 419


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 420

katika Uislamu

kimadhehebu na kuelimishana kwa hoja za kisayansi na akili katika yale tunayohitilafiana. Kuelimishana maana yake siyo kuachana na madhehebu zetu tunazozitaka au tulizozoea. Jambo la maana ni kila Mwislamu kufahamu misingi ya imani zake na ile ya Waislamu wenzake. Hukumu za dini huitwa ‘Fiqhi’, neno ambalo kwa kiswahili maana yake ni ‘Kuelewa’. Mjuzi wa ‘fiqhi’ huitwa ‘Faqih’. Tafsiri hii yaonyesha wazi kuwa, Mwislamu yeyote anayejidai kufuata kanuni ambazo hazielewi asili yake, huko siko kuelewa bali ni ujinga. Tunafahamu kuwa tendo lolote la ujinga, kidini na kidunia, haliwezi kumletea manufaa yoyote mwenye kulifanya. Baada ya maelezo hayo mafupi, hebu tujadili baadhi tu ya tofauti hizo. Kutokana na maelezo ya nyuma kuhusu asili ya Hadithi za uongo pamoja na amri batili za watawala mbali mbali waliovuruga Uislamu, ni juu ya Waislamu wenye kujali, kuamua ni hukumu gani za dini zilizo sahihi. Haiwezekani ‘Juisi’ ya zabibu ikawa sawa na mvinyo, ingawa rangi yake ni moja! 1. Usafi wa Tohara (At-Twaharah): Hapa tuna maana ya usafi wa lazima unaotakiwa kwa Mwislamu ili aweze kufanya ibada kama kuswali Swala tano, kuhiji, (Tawaf) kuzunguka AlKa’ba au pia kugusa Qur’ani. n.k. Iwapo mwili wako una najisi kama janaba, hedhi, mkojo, choo, pombe, damu ya jeraha, kugusa maiti baridi na shahawa; unatakiwa kunuia na kuoga ili utoharike. (a) Chini ya somo hili ni kwamba madhehebu ya Shia Ithna’asheri pamoja na Hanafi wanakubaliana kuwa maiti ni najisi, kama hajaoshwa, lakini Maliki, Shafii na Hambali wanaona siyo najisi. (b)

Ama kuhusu shahawa za wanyama ambao damu zao hazichiriziki kwa nguvu wanapochinjwa au kukatwa kwa chakula kama samaki, hiyo siyo najisi. Wanyama wengineo wanaochinjwa na kuchirizika damu taratibu, shahawa zao ni najisi. Hukumu hii inakubaliwa na madhehebu zote isipokuwa Shafii ambao wanachukulia shahawa za nguruwe na mbwa peke yake kuwa najisi. Hambal huchukulia shahawa za wanyama waliwao pekee kuwa ndiyo najisi. 420


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 421

katika Uislamu

2. Vitoharishaji (Mutwahiraat): Navyo ni maji, udongo, jua au Istikhaara (mabadiliko), na Uislamu. (a) Maji yanatakiwa kuwa na sifa zifuatazo : Yawe maji ya asili kama ya mvua, mito, bahari, visima au ya bomba. Yasiwe yamechanganywa na kemikali zinazoweza kuyabadili ladha au rangi yake. Yaani yasiwe na hata manukato au ‘juisi’ au sabuni au najisi japo kidogo. Maji ya kujitoharisha yasiwe yameibiwa au kudhulumiwa toka kwa mwenye kuyamiliki bila ruhusa yake. Kama ni maji yasiyo ya mto au kisima au bomba yatachukuliwa kama ni ya kutosha kutoharisha vitu mradi tu yasipungue lita 357 (Rejea mwanzoni mwa Sura ya 19 chini ya ‘Udhu - Kishia na Kisunni). Maaliki anasema kuwa kama chombo kimelambwa na mbwa inabidi kisafishwe (kitoharishwe) mara saba. Shia tunasema kuwa kama maji ya kutoharishia ni pungufu ya lita 357, chombo kisafishwe mara tatu. Vinginevyo kama maji yanatosha zaidi ya hapo, chombo kioshwe tu kwa kuondoa najisi hiyo basi. Hapa nimeeleza vifungu vya hukumu ambazo zinatofautiana kwa jambo lile lile kwa madhehebu tofauti. (b) Ulamaa wa Shia wanahukumu kuwa kuigusa maiti iliyopoa ni wajibu kuoga ‘Ghusl’ kujitoharisha. Lakini madhehebu mengineyo wanasema siyo wajibu. (Biblia: Hesabu 19:11-13). (c) Sunni wote hawaoni kuwa ni lazima kuoga Ghusl kwa utaratibu maalumu, lakini Shia huoga kwa utaratibu maalumu. Hanafi wanasema kuwa ni lazima baada ya Ghusl kusukutua maji na kuvuta maji puani. (d) Shafii na Hambal wanasema kuwa ukiwa na janaba, kupitia msikitini bila kukaa ni sawa. Maliki na Hanafi wanasema kuwa hairuhusiwi kuingia labda kwa dharura. 421


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 422

katika Uislamu

3. Umri wa kufunga hedhi (Menopause): Hambali wanasema kuwa ni miaka 50. Shia tunakubaliana na umri huo. Hanafi wanasema kuwa ni miaka 55. Maliki wanasema kuwa ni miaka 70. Shafii wanasema kuwa ni miaka 62. (a) Hambal na Shafii wanasema kuwa muda wa hedhi kwa mwanamke kwa chini kabisa ni siku moja na usiku mmoja, na kwa juu sana ni siku 15. Maliki wanasema kuwa hakuna kiwango cha chini ila kiwango cha juu ni siku 15 kwa mwanamke asiye mja mzito. Shia tunasema kuwa kuna hukumu nyingi tofauti kutegemea matatizo ya kiafya au maumbile ya wanawake tofauti. 4. Kuosha maiti: (a) Hambal wanasema kuwa Ghusl ni wajibu kwa kila hali. Hanafi wanasema kuwa kama marehemu amefariki na viungo vyake kamili, Ghusl ni wajibu; la sivyo siyo wajibu na haina haja. (b) Madhehebu nne za Sunni wanasema kuwa Ghusl ya wajibu kwa maiti ni moja tu inayofanyika kwa maji masafi yasiyochanganywa kitu; na kwamba Ghusl ya pili na ya tatu- hizo zinafaa (Mustahab) bali si wajibu. Shia tunasema kuwa Ghusl za wajibu ni tatu; ya kwanza ichanganywe na unga wa Sidri (majani ya mti fulani). Ya pili ichanganywe na karafuu maiti ‘camphor’, na ya tatu iwe maji peke yake. Kwa kadri ya hukumu za Shia, baada ya hapo ndipo maiti inatoharika na iwapo mtu ataishika hatalazimika kuoga ‘Ghusl Mass-ulMayyit.’ 5. Adhana na Iqamah: Suala hili limeshajadiliwa katika Sura hii nyuma. Hapa nitachambua msimamo wa madhehebu tano kuhusu somo hili: Sisi Shia huweka maneno ya ‘Hayya ‘Ala Khayril ‘Amal’ katika Adhana na Iqaamah. Ulamaa wa madhehebu tofauti wanakubali kuwa maneno hayo yalitumika vile vile katika uhai wa Mtume (s.a.w.w.) na ushahidi upo: (i) Allamah Qushji katika kitabu chake: ‘Sharhut Tajrid’ - sura ya ‘Imamah’. Huyu ni mwanachuoni mmojawapo maarufu wa Sunni. 422


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 423

katika Uislamu

(ii) Allamah Halabi katika kitabu chake:’ Sirat Ibn Umar’ - sura ya ‘Mwanzo wa Adhana’ - Jz. 2 uk. 110. Huyu naye ni mmojawapo wa wanachuoni maarufu wa Sunni. (iii) Ushahidi mwingine nimetangulia kuutoa nyuma kwamba maneno hayo yaliongezwa katika adhana na Mtume (s.a.w.w.), pale alipoamuru yatumike katika adhana pale Ghadiir Khum, kuwaita na kuwakusanya watu ili wasikilize ujumbe muhimu, katika hotuba yake ndefu, akitokea Hijja yake ya mwisho. (b) Madhehebu 4 za Sunni hawatumii maneno haya. Katika Swala ya Subhi, wao wameongeza maneno ya: ‘As-Swalaat Khayrum minanNawm’ kama nilivyoeleza nyuma kwamba maneno hayo maana yake ni: ‘Swala ni bora kuliko usingizi’, na yalianza kutumika kwa amri ya Umar Ibn Al-Khattab. Rejea:- Sura ya 10 Chini ya: ‘Kubadili Maneno ya Adhana.’ Kwa kadri ya hukumu za Shafii, alikataa maneno hayo: (Swala ni bora kuliko usingizi) yasiongezwe kwa kuwa hayakuwa maneno asilia ya adhana. Maulamaa kadhaa pia wameyakataa kwa mfano bwana Ibn Rushd katika kitabu chake: Bidayat ul-Mujtahid, Jz.1 toleo la 1935 A.D, anasema kuwa maneno hayo si maneno asilia ya adhana. Jambo la maana hapa ni kwamba, Waislamu wengi sana hapa Afrika Mashariki ni madhehebu ya Shafii. Iwapo Shafii hatambui maneno hayo, vipi wafuasi wake wayatumie? (c) Madhehebu ya Shia, Hanafi, Hambal na Shafii tunakubali kuwa maneno ya ‘Allahu Akbar’ mwanzoni mwa adhana yarudiwe mara nne. Madhehebu ya Maliki wanasema kuwa yarudiwe mara mbili basi. (6) Swala: (a)

Madhehebu zote tano zinaafikiana kuwa eneo la kuswalia lazima liwe halina najisi, liwe tohara.

(b)

Shafii anasema kuwa kila kigusacho mwili na nguo za mwenye kuswali lazima kiwe tohara. Hanafi wanasema kuwa sehemu za lazi423


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 424

katika Uislamu

ma kuwa tohara ni pale aliposimama (miguu) na pale awekapo paji la uso kusujudu basi. (c)

Madhehebu ya Sunni wanasema kuwa kuswali mahali palipodhulumiwa ni sawa ingawa mwenye kuswali hapo anapata dhambi. Shia tunasema kuwa Swala kama hiyo inabatilika.

(d) Shia tunasema kuwa hairuhusiwi kwa wanaume kuvaa hariri asilia au pete ya dhahabu katika Swala (wanawake wanaruhusiwa). Shafii anasema kuwa katika hali hiyo, mwenye kuswali hivyo Swala yake ni sahihi lakini atakuwa katika dhambi. (d)

Shia tunasema kuwa katika Swala lazima mwanamke afunike mwili wake wote, isipokuwa uso, viganja na miguu (nyayo) yake. Hanafi na Maliki wanasema kuwa mwanamke anaruhusiwa kufunua uso na mikono na miguu (nyayo) katika Swala. Hambal wanasema kuwa mwanamke anaruhusiwa tu kufunua uso katika Swala.

(e)

Malik wanasema kuwa kuteremsha mikono katika ‘Qiyaam’ ni wajibu. Sunni waliobakia wanasema kuwa kufunga mikono siyo wajibu bali mwenye kuswali ana hiari atakavyo. Shia tunasema kuwa kuteremsha mikono ni wajibu. Hanafi wanasema kuwa mwenye kuswali anaruhusiwa (katika rakaa ya tatu na ya nne) kusoma Sura ya Qur’ani au kusoma ‘dhikr’. Madhebu zilizobaki za Sunni wanasema kuwa kusoma Alhamdu kila rakaa ni wajibu. Shia tunasema kuwa ni uchaguzi wa mtu kusoma Suratul-Fatihah au kusoma dhikr: Subhan Allah, wal Hamdu Lillahi, wa laa ilaha ‘ilallahu wallahu Akbar - mara tatu, katika rakaa ya tatu na ya nne. Rejea: Al Fiqh ‘ala al-Madhaahib al-Khamsah - cha Muhhamad Jawad Mughniyyah.

(f)

(g)

Shafii, Hanafi na Maliki wanasema kuwa ‘Dhikr’ si wajibu katika rukuu. Madhehebu ya Hambal na Shia yanasisitiza hiyo dhikri isomwe. 424


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 425

katika Uislamu

(h) Kuhusu kusujudu nimeeleza msimamo wa Shia kwa ushahidi wa Suna na Qur’ani. Madhehebu za Sunni zinaruhusu kusujudu chini (aridhini) bila mipaka. Rejea Na: 3 ya Sura hii ya 19. (i) Hambal na Shia tunasema kuwa shahada ya kwanza katika Swala ni wajibu. Madhehebu mengineyo wanasema kuwa inasisitizwa (Mustahab) na siyo wajibu. Kuhusu shahada ya mwisho wa Swala, Shafii Hambal na Shia tunasema kuwa ni wajibu. Maliki na Hanafi wanasema kuwa ni Mustahab (yenye kusisitizwa tu). (j) Shia tunasema kuwa ni wajibu baada ya Tashahhud (shahada ya mwisho) kumsalia Mtume (s.a.w.w) na kizazi chake: Allahumma Swali alaa Muhammadin wa Aali Muhammad - mara tatu. Vinginevyo Swala yako haipokelewi! Shafii anasema kuwa salamu hiyo ni wajibu vile vile (kama Shia) na kwamba asiyeitoa, Swala yake haipokelewi. Je, Shafii wa hapa kwetu wanatekeleza hayo ? (Qur’ani 33:56) Je, Shafii alikuwa Shia? Rejea: (i) Sahih Tirmidhi - Jz. 45, Sura ya 64 (ii) Sunan Ibn Majah - Jz. 1, Sura ya 41 (iii) Al-Muwatta- Jz. 13, Sura ya 41-56 (k) Shafii na Maliki wanasema kuwa Qunut ni Mustahab katika Swala ya Subhi tu. Hanafi Shia na Hambal tunasema kuwa ni Mustahab katika Swala zote. (l) Shafii na Shia wanakubaliana juu ya Swala za kutoa sauti na zile za kuswali kimya. Hanafi wanasema kuwa mwenye kuswali ana uhuru atakavyo. Hambal wanasema kuwa ni Mustahab kwa rakaa mbili za mwanzo za Subhi, Maghrib na Isha. Madhehebu zote zinakubaliana kwamba ni sunnah kusoma kwa sauti baadhi ya rakaa za Swala hizo tatu kama tulivyozoea. Mpaka hapa nimejaribu kueleza kidogo tu juu ya baadhi ya tofauti zilizopo miongoni mwetu katika ibada, kutokana na hukumu tofauti za madhehebu 425


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 426

katika Uislamu

zetu tano. Sasa hivi tofauti hizo zimeongezeka miongoni mwetu, baada ya itikadi mpya za Kiwahabi kuingia katika Uislamu. Yote haya ni changamoto kwetu Waislamu. Inatubidi tujiulize: Kwa nini Qur’ani haijabadilika hata nukta, lakini kanuni nyingine (hukumu) za dini zinahitilafiana, wakati ambapo Mtume (s.a.w.w.) ni yule yule aliyetuletea Qur’ani na mafunzo mengineyo? Qur’ani ilishuka kwa miaka 23. Katika muda huo Mtume (s.a.w.w.) alionyesha kwa vitendo hukumu zote za dini. Kwa nini Qur’ani isalimike lakini mafunzo mengineyo yapotee? Kipi kigumu kati ya kukariri msahafu wote wa Qur’ani, na kukumbuka mafunzo ya ibada za kila siku za Mtume (s.a.w.w.) kama Swala tano? Hapa tunaona wazi kuwa, zilikuwepo njama za makusudi kupotosha dini baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.). Na huo ndio ukweli wa kihistoria kama nilivyoeleza kwa kirefu katika sura za nyuma, hasa katika historia juu ya ukusanyaji wa Hadithi mbali mbali za Mtume (s.a.w.w.) Kwa hiyo ni wajibu wetu kama Waislamu waaminifu, kuhakikisa kuwa, tunachunguza na kutekeleza mafunzo sahihi ya kiongozi wetu mpendwa Nabii Muhammad (s.a.w.w.). Waislamu tusiridhike na kurithi dini bila kuchunguza ukweli wake. Kwa mfano suala la kutoa Zaka ya mali na Zaka ya Khums - (Qur’ani 8:41), ni wajibu kwetu lakini hatujali kutoa. Hukumu za madhehebu yetu matano zinatambua Zaka hizi japo kwa viwango na kanuni tofauti. Baadhi ya Sunni wanaojali kutoa Zaka, hawatambui Zaka ya Khums! Kanuni sahihi za kutoa Zaka ya mali hazizingatiwi! Tukumbuke maneno ya Mtume (s.a.w.w.) aliposema kuwa, ‘Umma wangu baada yangu utagawanyika makundi 73 hadi siku ya Kiyama, na makundi yote yataangamia motoni (kwa upotofu) isipokuwa kundi moja tu litakalonusurika (kwa uongofu) Rejea: Sahihi Muslim, Jz.8 uk.7. Maana yake ni kwamba Uislamu ni mmoja tu mbele ya Mwenyezi Mungu. Je, ni Uislamu upi huo? Kuhusu hukumu tofauti miongoni mwa madhehebu, Rejea: Manhajul-Fiqhil-Islam - cha S.H. Al Musawi, Islamic Republic of Iran.

426


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 427

katika Uislamu

Mpaka hapa tumeona kuwa Mwislamu yeyote lazima atakuwa anafuata hukumu za kundi mojawapo, kati ya hukumu za madhehebu matano. Au ukichunguza zaidi utaona kuwa, huenda Waislamu walio wengi wanachaganya hukumu ambazo ni tofauti na madhehebu yao, kwa kutojua! Kisha tutaona kuwa Waislamu wengi zaidi hawatekelezi baadhi ya hukumu za madhehebu yao; na wanaona hukumu hizo kuwa ni ngeni kwa kutozifahamu! Nimeeleza huko nyuma kwamba kitendo cha Mwislam kufanya ibada asizozielewa asili yake, ukweli wake na uhalali wake; ni sawa na mgonjwa anayeamua kumeza dawa hivi hivi bila ujuzi wowote au maelekezo ya daktari. Maana yake ni kwamba mgonjwa huyo atapata madhara makubwa. Mwenyezi Mungu hapokei ibada yoyote inayofanyika katika ujinga. Mwanzoni mwa kitabu hiki nimetaja Hadithi ya Mtume (s.a.w.w.) kwamba: ‘Usingizi wa mtu mmoja mwenye elimu ni bora mbele ya Mwenyezi Mungu kuliko ibada ya usiku mzima ya kundi la wajinga elfu moja.’ Ibada za kurithi ni ibada za ujinga iwapo haziambatani na uchunguzi wa kuzihakikisha ukweli wake. Pengine Mwislamu wa kawaida anaweza kuchanganyikiwa kuhusu afanyeje, ili aione njia ya haki katika migongano ya hukumu za madhehebu! Kwa Mwislamu mwaminifu ni rahisi, kwa sababu tukirejea Sura ya 17 tutaona historia kamili ya chanzo cha madhehebu manne ya Sunni. Tumeona kuwa mwanzo wa madhehebu ya Sunni ni takriban miaka 100 na zaidi tangu alipofariki Mtume (s.a.w.w.)! Vile vile tumeona kuwa viongozi wa kwanza wa madhehebu ya Sunni walipata elimu yao kutoka kwa viongozi wa Shia Ithna’asheri. Kisha tumeona kuwa elimu ya viongozi wa Shia ni kubwa mno na inatokana na Mtume (s.a.w.w.). Maana yake ni kwamba Usunni ni itikadi mpya ambayo Mtume (s.a.w.w.) pamoja na al-Khulafau Rashidun hawaijui hata wakifufuka leo! Siandiki haya kufurahisha nafsi yangu, bali kwa kadri ya kumbukumbu sahihi za historia. Kwa kutojua historia, kuna ndugu zetu viongozi wa 427


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:25 PM

Page 428

katika Uislamu

Sunni ambao hudai kuwa Abu Hanifa, Maliki, Shafii na Hambal waliishi enzi za uhai wa Mtume (s.a.w.w.)! Kwa hiyo tutaona kuwa, itikadi na ibada zilizoanzishwa miaka 100 baada ya Mtume (s.a.w.w.), haziwezi kukosa kasoro, tukizingatia kuwa wakati huo hapakuwepo tena mtu yeyote aliyeonana na Mtume (s.a.w.w.) ana kwa ana! Isitoshe tumeona migogoro mikubwa iliyotokea katika kipindi hicho, ambapo viongozi watawala walikandamiza dini na kuivuruga kwa kiwango kikubwa. Lakini kwa upande mwingine tumeona sifa za pekee za Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.), ambao wanaongozwa na Mwenyezi Mungu wakati wote, na ambao walikusudiwa na Mwenyezi Mungu kutuongoza baada ya kufariki Mtume (s.a.w.w.) Nimetoa ushahidi mkubwa kuthibitisha ukweli huo. Kwa hiyo tunafikia ukweli kwamba, kwa Mwislamu mwenye kutafuta madhehebu inayofuata nyayo halisi za Mtume (s.a.w.w.), madhehebu hiyo si nyingine ila ni Shia Ithna’asheri. Dunia nzima katika ulimwengu wa wanavyuoni wa kiislamu, hakuna wajuzi wakubwa wa dini kama Shia. Msingi mkuu wa elimu ya Shia ni Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.).

“Mwenyezi Mungu ni Mlinzi wa wale walioamini. Huwatoa katika giza na kuwaingiza katika nuru, lakini waliokufuru, walinzi wao ni mashetani. Huwatoa katika mwangaza na kuwaingiza katika giza. Hao ndio watu wa motoni, humo watakaa milele.” (Qur’ani 2:257).

428


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 429

katika Uislamu

(26) Je! Tunaweza kubadili hukumu za Dini au Sunna eti kwa kwenda na wakati?: Siku hizi utawasikia baadhi ya mashekhe wetu katika hotuba zao, wakiwaeleza wafuasi wao kuwa baadhi ya sheria (fiqh) za dini zaweza kutenguliwa ili kukidhi mahitaji halisi ya wakati huu. Ukichukulia suala hili juu juu bila kuzama katika mafunzo sahihi ya dini, unaweza ukakubaliana na hoja hii potofu. Kwanza kabisa Qur’ani inasema: “Leo hii nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema Yangu, na kukuridhieni Uislamu uwe dini yenu.....” (Qur’ani 5:3). Aya hii inaonyesha kuwa Mwenyezi Mungu alikwishakamilisha Dini, kwa maana kuwa, hapana la kuongeza au kupunguza. Aya hiyo ilishuka miezi mitatu tu kabla ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki. Msimamo wa Shia Ithna’asheri ni kwamba baada ya Mtume (s.a.w.w.) kufariki, likitokea tatizo ambalo halina ufumbuzi wa wazi wazi katika Qur’ani au Sunna, kwa wakati huu baada ya Maimamu 12 (a.s.) ni lazima tatizo hilo apelekewe Mujitahid kulitatua (Rejea Sura ya 14 chini ya: ‘Kughibu kwa Imam Mahdi’ pia Sura ya 14 yote. Kwa hakika hakuna Imam au Mujitahid aliyewahi kutengua sehemu ya Qur’ani au Sunnah sahihi ya Mtume (s.a.w.w.). Sababu yake ni kwamba kitu kilichokamilika hakina haja ya kurekebishwa. Mtazamo huu wa baadhi ya Waislamu kuona kuwa Uislamu hauendi na wakati na hivyo urekebishwe, ni jambo la hatari kwa sababu siku zote binadamu hataki kutii sheria na ndiyo maana kuna mahakama na magereza. Siku zote binadamu hujitahidi kukwepa sheria ili kutimiza matakwa ya nafsi yake. Mfano wa mwelekeo huu potofu ni kwamba, nilimsikia Sheikh mmoja maarufu wa Sunni akiwaeleza wafuasi wake kuwa, ‘Kwa wakati huu hapa kwetu, hakuna haja ya ‘Udhu wa Tayammum, kwa sababu maji yapo tele na huwezi kutembea kilomita tano bila kupata maji, kama jangwani, na kwa hiyo ukitumia udhu huo utabatilisha Swala zako.’ Aliongeza kuwa Tayammum ilikusudiwa kwa wakazi wa jangwani wenye shida ya maji! 429


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 430

katika Uislamu

Kwa kadri ya Fiqh sahihi ya Ahlul-Bayt (a.s.), udhu wa Tayammum umekusudiwa pia kuwapunguzia matatizo waumini; na siyo tu ukosefu wa maji peke yake. Kwa mfano iwapo maji yaliyopo yanatosha kunywa tu na hakuna uwezekano wa kupata maji zaidi, ni lazima utumike udhu wa Tayammum. Iwapo mtu hawezi kutumia maji baridi kiafya, na wala hawezi pia kupasha joto maji hayo, anaruhusiwa kufanya Tayammum. Iwapo maji yaliyopo hayatimizi sifa za usafi unaotakiwa ili yaweze kutumika kwa udhu, itabidi utumike udhu wa Tayammum. Kwa hiyo tutaona kuwa Tayammum inategemea kanuni fulani fulani ambazo zimekusudiwa kurahisisha ibada. Zaidi ya hayo tufahamu kuwa hakuna amri ya Qur’ani au Sunna ambayo imekusudiwa kwa baadhi tu ya Waislamu wa sehemu fulani peke yake. (Qur’ani 5:6). Sheikh huyo wa Sunni aliendelea kuwafundisha wafuasi wake kuwa, ‘Hakuna haja ya kuswali Swala Qasr (kupunguza rakaa ukiwa safarini) kwa sababu eti siku hizi vyombo vya safari vinakwenda haraka sana na kwa hiyo unaweza ukaondoka Dodoma na ukafika Uingereza kabla ya jioni na ikawa umeharibu Swala zako kuzipunguza bila sababu za msingi’. Kwanza tufahamu kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anafahamu kuwa ingawa wakati huo alitumia ngamia kama chombo pekee cha usafiri, lakini siku zijazo vitakuwepo vyombo vya haraka zaidi vya usafiri. Kama tutakubaliana na madai ya Kwenda na Wakati ina maana kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawakufahamu dunia itakavyokuwa mbeleni! Imani kama hiyo ni shirk. Katika dini ya kiislamu zimo nafuu fulani fulani alizoweka Mwenyezi Mungu hata kama hakuna sababu za wazi kwetu binadamu kwa uchache wetu wa kufahamu. Jambo la maana ni kwamba kanuni zote za dini zinatumika hadi Kiyama bila nyongeza au upungufu. Ili mradi Warithi halali wa Mtume (s.a.w.w.) hawakupunguza au kuongeza chochote katika maisha yao yote, hakuna mwenye haki hiyo hadi Siku ya Kiyama. Isitoshe tukiendekeza upotofu huo wa ‘Kwenda na Wakati’, tufahamu 430


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 431

katika Uislamu

kuwa siku moja atatokea mtu na kudai kuwa kutokana na shughuli nyingi zitokanazo na maendeleo makubwa duniani, tupunguze Swala tano ziwe Swala tatu au mbili au moja kwa kutwa! Kwa mfano nchi za Ulaya utakuta mtu mmoja ana kazi mbili. Akirejea toka kazi ya kwanza hapo hapo anajitayarisha kuanza kazi ya pili, yaani waajiri tofauti. Kwa mtu kama huyo mwenye lengo la kupata mishahara miwili, ili aweze kumudu gharama kubwa za maisha, huenda akapendekeza kuwa Swala tano zipunguzwe ili apate muda wa kuinua kipato chake. Kwa kuwa dunia inazidi kusonga mbele, na maisha yanazidi kuwa magumu, tutapunguza na kuongeza mambo mangapi hadi Siku ya Kiyama? Na Uislamu utakuwaje dini iliyokamilika iwapo hauna kanuni maalumu? Nimeeleza huko nyuma kuwa, ‘Alilohalalisha Mtume (s.a.w.w.) ni halali hadi Siku ya Kiyama na aliloharamisha ni haramu hadi Siku ya Kiyama.’ Je, pana haja ya kufafanua Hadithi hiyo maarufu ya Mtume (s.a.w.w.). Mfano mwingine ni kwamba nimeeleza huko nyuma migogoro ya kuandama kwa mwezi. Iwapo tutadai kuwa siku hizi ni enzi za sayansi na teknolojia, na kwa hiyo tusiangalie mwezi tena, bali tutumie vituo vya ‘uchunguzi wa anga’ na kupanga kalenda yetu ya kiislamu. Matokeo yake ni kwamba tutajikuta na mwezi mmojawapo wa kiislamu wenye siku zaidi ya thalathini; jambo ambalo halistahiki. Sunna zote za wazi za Mtume (s.a.w.w.) zinabakia vile vile kama Qur’ani kwa sababu ni kitu kimoja. Masuala mapya miongoni mwa Waislamu ambayo Mtume (s.a.w.w.) hakuwahi kuyatolea hukumu, ndiyo pekee yatatafutiwa ufumbuzi na viongozi halali. Uislamu hauathiriki na nyakati bali huathiri nyakati zote hadi Kiyama. Ni lazima kwa Waislamu waaminifu kuupokea na kuutimiza Uislamu kama ulivyo. (27) Mila katika misiba na matanga: Kuzaliwa na kufariki ni jambo la kawaida kwa kila kiumbe. Lakini kwa sisi Waislamu tunatambua kwamba maisha ya duniani ni ya kimwili na ni ya muda mfupi sana. Maisha ya akhera ndiyo kituo cha kudumu cha safari 431


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 432

katika Uislamu

ya kiroho ya binadamu. Hata hivyo pamoja na ukweli huo, bado wengi wetu imani yetu ya maisha ya akhera ni ndogo sana. Na ndiyo maana utawasikia baadhi yetu wakisema kuwa, ‘Nani aliyewahi kwenda akhera na kushuhudia hayo ya huko?’ Kukosa imani kamili ya maisha ya akhera ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuwa wazembe katika masuala ya dini. Wengi wetu hudhani kuwa baada ya kufariki ndiyo mwisho wetu! Kutokana na imani hiyo potofu, wengi wetu huchukia kifo kwa kudhani kuwa aliyekufa kapotea milele. Laiti tungejua kuwa katangulia; na kwamba tunalo tumaini la kukutana naye akhera bila shaka tusingeomboleza na kuzirai kwa uchungu! Mbona hapa duniani watu huagana kwa furaha wanapotenganishwa na safari japo wanafahamu kuwa hawatawasiliana hata kwa miaka 20 mradi wanajua kuwa siku moja watakutana? Hapa tunaona wazi kuwa imani yetu ya kukutana akhera ni ndogo sana. Lakini tatizo siyo kuwa na imani peke yake. Kwa kweli suala zima la kukutana akhera na wale tuwapendao, linategemea sana maisha ya kiroho tunayoendesha hapa duniani. Kama tupo duniani ili tufaidi dunia, bila shaka thamani yetu kiroho itakuwa duni. Iwapo tutaishi katika uduni wa namna hiyo, maisha yetu yote duniani, ina maana kuwa huko akhera tutakutana Jahanamu katika mateso ya milele. Na bila shaka makutano hayo hayawezi kuwa ya furaha. Makutano ya furaha ni kukutana Peponi. (a) Mila ya kuomboleza na kulia kwa uchungu: Sina maana kuwa tusiwalilie marehemu wetu. Kwa hakika hata Mtume (s.a.w.w.) alionekana akiwalilia marehemu fulani fulani. Linalokatazwa ni kuomboleza na kujitupa ovyo na kugalagala. Utamwona mfiwa, anamlilia marehemu, huku anaomboleza kuwa, ‘Umeniachia upweke, nani atanitimizia mahitaji yangu.’ Maneno kama hayo ni kufuru kwa sababu mwenye kuruzuku ni Mwenyezi Mungu moja kwa moja au kupitia kwa mtu yeyote amtakaye. Sababu za mtu kumwomboleza marehemu ni kama ifuatavyo na majibu yake: (i) Kama mume anamwomboleza mke wake, afahamu kuwa kila mume wa peponi atapewa wanawake 70,000 wa peponi wenye sifa bora zisi432


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 433

katika Uislamu

zopatikana duniani. (ii) Kama mke anamwomboleza mume kwa uchungu wa kuadhirika kimaisha, afahamu kuwa kuna maelfu ya wanawake wajane au wasiowahi kuolewa, lakini kwa rehema za Mwenyezi Mungu hawakosi riziki zao za kila siku. (iii) Kama mtoto anamwomboleza mama au baba yake, afahamu kuwa wapo mamilioni ya watoto duniani ambao ni mayatima lakini kwa baraka za Mwenyezi Mungu, wanapata mahitaji yao muhimu. (iv) Kama wewe ni mzazi na unaomboleza kifo cha mwanao mchamungu, ufahamu kuwa mtoto mchamungu Siku ya Kiyama ataingia peponi na atamwomba Mwenyezi Mungu awasamehe wazazi wake nao waingie peponi. Maombi hayo yatakubaliwa. (v)

Iwapo wewe mzazi unaomboleza kifo cha mwanao asiyebalekhe au kuvunja ungo bado, ujue kuwa huyo hana dhambi kwenye daftari lake, na labda angefikia utu uzima angekuwa mtoto mwovu.

(vi)

Iwapo mke anamwomboleza mume au mume anamwomboleza mke kwa uchamungu wao, ieleweke kuwa hao wawili wataunganishwa tena peponi kwa ndoa yao hiyo, kwa ahadi ya Mwenyezi Mungu. Kwa maana hiyo, hapana haja ya kuomboleza bali huko ni kuagana tu. Uhusiano wowote peponi utakatika, isipokuwa huo wa mke na mume wachamungu basi, hao wataunganishwa tena.

Kwa mifano hiyo michache tutakuwa tumeona kuwa sababu zote za kidunia zinazotufanya kuomboleza kwa uchungu, hazina uzito wowote iwapo tutaishi duniani kwa misingi ya uchamungu, kwa kuweka matumaini yetu yote kwa Mwenyezi Mungu. Upungufu mkubwa katika imani zetu, ndio unaotufanya tushindwe kutambua uhusiano kati ya dunia na akhera. Kwa upande mwingine tuwe waangalifu katika kuwalilia marehemu wetu, kwa sababu huko nyuma nimetangulia kueleza kuwa, wengi wetu tume433


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 434

katika Uislamu

zoea kusikia kwa wenzetu kuwa eti ni haramu kumlilia marehemu ambaye inadaiwa huadhibiwa kwa vilio hivyo! Nimetangulia kusahihisha imani hiyo kwamba, bibi Aisha alimsahihisha Umar kwa kusema kuwa, ‘Mwenyezi Mungu amsamehe Umar, Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa kafiri huadhibiwa iwapo atakufa na watu wakamlilia.’ Kwa hiyo mtu anayefaa kuliliwa ni muumini peke yake. Ukweli ni kwamba kuwa Mwislamu siyo kuwa muumini moja kwa moja! Kuna matendo mengi na itikadi nyingi potofu ambazo ukizikumbatia unageuka kafiri bila kujijua! Mwenye kujua siri ya kila Mwislamu ni Mwenyezi Mungu. Kwa tahadhari ni bora tuache kuwalilia marehemu kwa kuwa hatujui matendo yao kama bado ni Waislamu au Waumini au Makafiri? Kwa mfano tunasikia Mashekhe wengi wanasema kuwa Mwislamu akiacha Swala tano huwa ni kafiri, na kwamba tofauti kati ya Mwislamu na Kafiri ni Swala tano. Tujiulize hilo peke yake linabakiza Waislamu wangapi miongoni mwetu? Zaidi ya hayo bado kuna kasoro nyingine nyingi kama kupiga ramli na ushirikina wa aina mbali mbali n.k. Je, tunapomlilia marehemu tuna hakika kuwa kasafika na hayo? (b) Kukusanyika Waislamu kwa wafiwa: Mkusanyiko unaotakiwa ni ule wa kutayarisha mazishi ya marehemu. Mambo ya wajibu kwa Waislamu ni kuosha maiti na kumkafini, kumsalia na kumzika. Gharama za sanda ni wajibu zitokane na mali za marehemu. Iwapo Waislamu watachanga pesa kugharimia sanda, siyo wajibu bali ni sadaka. Inasisitizwa kila Mwislamu anunue sanda akae nayo katika uhai wake; ni thawabu kuiangalia kila siku. Ni wajibu kwa Waislamu kumwosha maiti bure bila ujira. Kwa mafunzo sahihi ya dini, ni kwamba kumwosha maiti kwa ujira ni sawa na kumzika bila kumwosha! Kwa hiyo tabia ya siku hizi iliyoenea kote ya waoshaji kuweka viwango vya ujira, siyo sahihi. Waislamu wote tunapaswa kupata mafunzo ya kuosha na kukafini maiti na ndiyo maana wajibu huo ni juu ya Waislamu wote wa mji au kijiji alikofariki Mwislamu, mpaka apatikane japo Mwislamu mmoja atimize wajibu huo, la sivyo Waislamu wote wa 434


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 435

katika Uislamu

mahali hapo watabeba dhambi. Suala la mazishi ya Mwislamu halina haja ya vyama vya kufa na kuzikana bali ni wajibu kwa Waislamu kushiriki. (c) Matanga: Matanga ni sehemu ya dini bali mahali pengine huchanganyika na mila potovu ambazo lazima tahadhari ichukuliwe kuziepuka. Kwa kadri ya mafunzo sahihi ya dini, ni wajibu kwa majirani Waislamu, wa wafiwa, kupika chakula na kuwapelekea wafiwa kwa siku tatu, na siyo kwenda kukusanyika kwa wafiwa na kulishwa kwa gharama za marehemu au wafiwa. Katika somo hili, nimetangulia kueleza kuwa ni lazima Waislamu wakione kifo kama jambo la kawaida lisilozuilika. Kwa maana hiyo ni kwamba baada ya mazishi watu waendelee na shughuli zao za kawaida. Endapo wafiwa ni watu wasiohitaji kuletewa chakula na majirani, na iwapo wanataka kugharimia matanga, na kwamba watachukua tahadhari ya kuzingatia maadili ya kiislamu, basi wanaruhusiwa. Lakini, bado matanga hayo hayatamnufaisha marehemu! Ni bora iwapo katika mkusanyiko huo, itasomwa Qur’ani kwa faida ya marehemu. Ni bora hizo pesa za kugharamia matanga zingepewa kituo cha watoto yatima kwa thawabu ya marehemu. Mara nyingi kwa wafiwa wenye uwezo, hutumia matanga kama njia ya kutangaza uwezo wao kifedha! Kwa kweli hata hizo gharama kubwa za kisomo cha khitima, zingeweza kununulia vifaa vya kudumu vya msikiti kwa thawabu za milele za marehemu; badala ya vyakula vya siku moja ambavyo hata hivyo hupewa watu wasio na njaa! Bora vyakula vya khitima wangepewa kundi la masikini wasiojua harufu ya chakula zaidi ya kuokota jalalani. Suala zima la khitima ni kwa thawabu za marehemu kwa kisomo cha Qur’ani na kupika vyakula. Hapa tunajadili njia bora zaidi ya kumpatia thawabu nyingi marehemu. Suala hili nimeelezea huko nyuma kifungu Namba 7 cha mtiririko huu. Pengine sababu za ubaya au kasoro za matanga nilizoeleza hapa, huenda hazijawatosheleza baadhi ya wapenda ‘MILA’. Jambo la maana ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa 435


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 436

katika Uislamu

tuachane na mila zinazopingana na dini. Mwislamu mwaminifu ni yule anayejiambatanisha na dini kuliko mila za kabila au ukoo wake. (d) Kisomo cha Arobaini na sadaka zake: Kisomo hiki na sadaka zake hakina tofauti na Khitima. Imani kwamba kisomo hiki kinawiana na marehemu kukatika shingo kaburini, ni kichekesho kwa sababu hata kama madai hayo ni kweli, kukatika shingo siyo ibada. Jambo la maana ni kwamba, suala la kumsomea Qur’ani marehemu ili apate thawabu na nafuu kaburini, ni suala ambalo linafaa wakati wowote na siyo Arobaini tu. Kanuni zake ni zile zile kama za Khitima kwa maelezo yaliyotangulia nyuma. Kuna Waislamu wengi tu, ambao siku hizi huunganisha khitima na ibada ya AQIQA iwapo aliyefariki ni mtoto au kijana. Hayo ni makosa yaani, kumfanyia Aqiqa marehemu! Maelezo juu ya njia sahihi ya kufanya Aqiqa yatafuatia mbele. (e) Kanuni za Aqiqa ya kuzaliwa mtoto: Ibada hii hufanywa na Shia pamoja na baadhi ya Sunni. Kwa usahihi wake, ibada hii inapasika kufanywa siku ya saba baada ya kuzaliwa mtoto. Katika kutekeleza ibada hii, marafiki na Waislamu wengineo ni vizuri waalikwe. Mambo ya msingi ni kumpa jina mtoto, kumnyoa nywele na kutoa kafara. Kisha kusomwa dua maalumu. Baada ya hapo mtoto hunyolewa nywele. Kisha nywele hizo inabidi zipimwe kwa uzito wa madini ya ‘fedha’ na thamani yake wapewe mafukara au mayatima kama sadaka. Mbuzi au kondoo achinjwe kafara baada tu ya kunyoa nywele au muda ule ule, na siyo kabla. Wakati wa kuchinja husomwa dua maalum pia. Baada ya kafara hiyo, sehemu kubwa ya nyama wapewe mafukara. Nyama hiyo itafaa pia kuwapa wageni lakini haipasi kuliwa na wazazi na jamaa na wakazi wa nyumba hiyo. Iwapo kutokana na sababu fulani fulani, Aqiqa haikufanyika siku ya saba ya kuzaliwa mtoto, basi yaweza kufanyika baadaye hata na mtoto mwenyewe akifikia kuvunja ungo au kubalekhe. Ibada hii si wajibu ila inasisitizwa sana katika Hadithi. Dua za kuomba katika ibada hii zinapatikana kwa mwandishi wa kitabu. 436


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 437

katika Uislamu

(28) Mambo yanayomkuta mtu anayefariki dunia hadi kuzikwa kwake: Katika madhehebu ya Shia Ithna’asheri, tunazo kumbukumbu nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake, kuhusu mambo yanayomtokea mtu anayefariki dunia. Kwa watu wasio na imani thabiti ya dini, huchukulia kifo kama mwisho wa binadamu. Fikra potofu ya namna hii huwafanya watu kama hao kujitahidi sana hapa duniani kustarehe na kufaidi maisha kadri inavyowezekana. Hali kama hii haitoi mwanya wa mtu kuona huruma au kutoa sadaka au kujinyima kwa ajili ya watu wengine. Sababu yake ni kwamba watu kama hao huthamini sana maisha yao, kwa kuamini kuwa hakuna kuwajibika kwa matendo yao baada ya kifo; na kwa hiyo hapana sababu ya wao kuteseka kwa ajili ya watu wengine! Lakina tunaona kuwa imani ya kuwepo uhai mpya wa kiroho baada ya kifo, humfanya mtu kurekebisha maisha yake hapa duniani kwa kutambua kuwa ubora wa maisha yake kesho akhera, unategemea sana thamani ya matendo yake hapa duniani. Imani ya baadhi yetu kwamba maisha ya mtu huko akhera yalikwishapangwa na Mungu, ni imani potofu kwa sababu ni sawa na mtu anayejitahidi kuondoa ufukara katika maisha yake. Kama ufukara ni kudra ya Mwenyezi Mungu, kwa nini binadamu tunahangaika kujikwamua na ufukara? Kwa kadri ya mafunzo sahihi ya Uislamu, kifo ni maisha mapya katika makao mapya (Qur’ani 67:1-2). Imani hii inatufanya tutambue kuwa, wale watakaomtii Mwenyezi Mungu na kuishi maisha ya uadilifu, bila shaka watafurahia kifo ili waondoke katika dunia hii ya mateso na majaribu ili wakaishi maisha bora ya kudumu milele huko akhera. Kwa upande mwingine ni kwamba, wale waliotumia uhai wao hapa duniani kumuasi Mwenyezi Mungu, bila shaka watakuwa na hofu kubwa ya kwenda akhera na kuanza kuadhibiwa milele kwa uovu wao walioufanya duniani. Kwa kuwa maisha ya duniani ni mafupi sana, ndiyo maana Mtume (s.a.w.w.) anakaririwa akisema kuwa, “Hamkuumbwa ili kufa bali kuishi milele; kutoka dunia hii na kuhamia nyingine, na kwa hiyo roho zenu ni 437


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 438

katika Uislamu

ngeni hapa duniani na zimekaa kama wafungwa miilini.” Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) akijibu swali kuhusu kifo, alisema, “Kifo ni moja ya mambo matatu yanayomtokea mtu anayefariki: Ama ni mwanzo wa maisha mapya ya starehe peponi, au adhabu ya kudumu akhera, au ni mashaka ya kutisha bila uhakika wa kundi gani ataingia. Kwa hiyo yule ambaye ni mtiifu na mpenzi wetu, ndiye atakayebashiriwa maisha ya raha peponi. Bali adui yetu hubashiriwa adhabu ya milele, lakini yule ambaye hajui ataingia kundi gani ni yule ambaye amejidhulumu nafsi yake kwa kutenda madhambi; lakini mwisho wake, Mwenyezi Mungu hatamchukulia kuwa adui yetu na hivyo atamtoa motoni kwa shufaa (maombezi) yetu. Hivyo msitegemee imani na shufaa peke yake bali mfanye bidii kutenda mema na msichukulie adhabu ya Mwenyezi Mungu kama mzaha kwani wapo baadhi ya waumini watenda madhambi ambao tutawaombea msamaha lakini watasamehewa baada ya kukaa motoni miaka laki tatu.” Imam Hasan (a.s.) anakaririwa akisema kuwa. “Kifo ni furaha kuu inayowafikia waumini wa kweli wanapoondoka hapa katika nyumba ya mateso (dunia) na kuhamia katika furaha ya milele peponi; lakini kifo ni balaa kubwa ambalo huwajia wasioamini wanapotoka na kuiacha pepo yao (dunia) na kwenda motoni milele, na moto huo hautazimika.” Imam Husain (a.s.) anakaririwa siku ya Ashura akisema kuwa, “Nilimsikia baba akimkariri Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema kuwa: ‘Hakika hii dunia ni gereza kwa waumini wa kweli na ni pepo kwa wasioamini. Ni daraja kwa waumini kwenda bustani za peponi na ni daraja kwa wasioamini kwenda motoni.’’ Nini maana ya kifo kizuri au kibaya?: Imam Ja’far Sadiq (a.s.) aliulizwa, “Inakuwaje tunawaona baadhi ya wasioamini ambao vifo vyao ni vyepesi bila mateso wanafariki huku wakicheka au kuongea? Kisha wapo pia waumini ambao hufariki katika hali kama hiyo? Kisha wapo wasioamini na pia waumini ambao hupata 438


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 439

katika Uislamu

mateso ya kukata roho?” Imam alijibu kwamba, “Raha au unafuu anaopata muumini wakati wa kukata roho ni malipo ya mwanzo; na iwapo atateseka wakati wa kifo ni kwa madhumuni ya kumsafisha madhambi ili aende akhera akiwa ametakasika bila kikwazo cha kumzuia raha ya moja kwa moja katika maisha ya akhera. Nafuu yoyote au raha yoyote anayopata asiyeamini wakati wa kifo chake, ni kukamilisha malipo yake hapa hapa duniani kutokana na mema yoyote aliyoyatenda katika uhai wake; kwa sababu asiyeamini hawezi kuingia peponi hata atende wema kiasi gani, hivyo ni lazima Mwenyezi Mungu amlipe hapa hapa duniani ili afikapo akhera asiwe na chochote ila kuadhibiwa tu. Na mateso yoyote ayapatayo asiyeamini wakati wa kifo chake ni mwanzo wa kukaribishwa aanze kuonja adhabu inayomsubiri akhera, baada ya Mwenyezi Mungu kumlipa kila kitu hapa duniani kwa kumpa afya njema, utajiri, cheo n.k. katika uhai wake. Yote haya hutendwa na Mwenyezi Mungu kwa uadilifu wake wa kumlipa kila mtu haki yake; huwalipa wasioamini kwa kuwapa kifo cha raha au kinyume chake”. Hatua anazopitia mtu anayefariki: Wakati huo, macho, masikio, ulimi na viungo vyote huacha kufanya kazi; kisha mtu huyo huona (kiroho) vitu vitatu ambavyo hudai kuwa ni rafiki zake. Cha kwanza humweleza kuwa, “Nitabakia na wewe hadi kifo chako”. Kitu hicho ni utajiri na mali zake. Cha pili hudai kuwa kitamsindikiza hadi kaburini; nacho ni familia yake. Cha tatu humweleza kuwa, “Niko nawe katika uhai na baada ya kifo chako”. Amali zake. Imam Zainul Abidiin (a.s.) anakaririwa akisema kuwa, “Mwenyezi Mungu hachelei amri yake isipokuwa kifo cha muumini; kwa kujua kwamba muumini anachukia kifo na kwa hiyo Mwenyezi Mungu hataki kumsononesha. Kwa hiyo muda wa kifo unapowadia, Mwenyezi Mungu hutuma Malaika wawili, mmoja anaitwa “Muskhiyah” – maana yake (mwenye kuleta ukarimu), na mwingine ni “Munsiyyah” – maana yake mwenye kusahaulisha. Hivyo Muskhiyah humfanya muumini kuwa mkarimu kwa kumfanya awe radhi kuacha mali zake (kurithisha); na huyo Munsiyyah 439


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 440

katika Uislamu

humfanya asahau upuuzi wote wa dunia.” Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) anakaririwa akisema, “Yeyote anayefariki ni lazima anione, awe muumini au awe mnafiki. Akiwa muumini hufurahi kuniona, na akiwa mnafiki husononeka.” Mara baada ya Malaika hao wawili niliowataja kumaliza kazi yao, hapo hapo huteremka Malaika wa Mauti ambaye humweleza muumini asiogope, na kisha humwambia afungue macho. Hapo huyo muumini hufungua macho na kuona sura ya Mtume (s.a.w.w) na Maimamu 12 (a.s.) yaani viongozi halali baada ya Mtume (s.a.w.w) na kuwatambulisha kwake na kuelezwa kuwa atakuwa nao akhera. Kisha huyo muumini husikia mwito:

“Ewe nafsi (roho) iliyotulia! Rejea kwa Mola wako hali ya kuwa umeridhika na umeridhiwa. Kisha ingia katika (kundi la) waja Wangu (wema). Na uingie katika Pepo Yangu.” (Qur’ani 89:27-30) Wakati huo muumini huwa amejawa na furaha akitamani kitu kimoja tu yaani kufariki haraka ili amfikie huyo mwenye kumwita. Katika hali hiyo muumini huondoka duniani akiwa hana majonzi yoyote wala kujali. Hivyo Mwenyezi Mungu humteremshia kifo wakati muumini tayari anatamani kifo, ili amwendee Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.s.). Lakini kwa wanafiki na wasioamini, hali yao ni kinyume cha hayo. Maswali kaburini: Suala hili ni mojawapo ya imani za msingi za Kiislam, na yeyote asiyeamini suala hili atakuwa ameuvua Uislamu wake. Tunasoma katika Hadithi kwamba baada ya mtu kuzikwa na watu wakaondoka; wakati huo hushuka Malaika wawili kaburini, mmoja anaitwa Munkar na mwingine ni Nakir. Roho ya marehemu hurejeshwa mwilini mwake ili ahojiwe. Malaika 440


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 441

katika Uislamu

humwuliza maswali makuu yafuatayo:Nani Mola wako? Nani Mtume wako? Ipi dini yako? Kipi kitabu chako? Nani Imamu wako? Ni wapi Kibla chako? Tunasoma katika Hadithi kwamba maswali mengineyo anayoulizwa ni juu ya Swala, Zaka, Hijja, Saumu na mapenzi yake kwa kizazi cha Mtume (s.a.w.w). Maswali hayo ndiyo huitwa “TALQIIN”. Iwapo mtu huyo ni muumini na ikawa amejibu maswali sawasawa, hapo hapo Malaika hao humwambia alale kwa amani, na wakati huo kaburi lake hugeuka kama chumba, ambapo Malaika hao humfungulia mlango unaoonyesha nafasi yake inayomsubiri Peponi Siku ya Kiyama. Baada ya hapo, roho yake huchukuliwa na kuwekwa miongoni mwa roho za watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w). Lakini iwapo huyo marehemu siyo muumini na hivyo akashindwa kujibu maswali sawasawa, basi hapohapo Malaika hao huanza kumwadhibu kwa rungu na humfungulia mlango kumwonyesha nafasi yake inayomsubiri Jahannam. Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) alielezwa na Mtume (s.a.w.w) kwamba, “Ewe Ali, wale wanaokupenda watafarijika sehemu tatu: Kwanza wakati wa kufariki, kwa sababu utahudhuria, pili, wakati wa kuhojiwa maswali kaburini kwa sababu utakuwepo kuwaongoza, tatu, siku ya hukumu (Kiyama), kwani utakuwepo ukiwatambulisha kwa Allah.” Kwa waumini wa kweli ambao Talqin imesomwa kaburini mwao kama kawaida, huwa hawaulizwi maswali ya kaburini kwa sababu Malaika huambizana kuwa huyo marehemu tayari amefuzu. Watu wengine hujiuliza vipi marehemu atasikia “talqiin” wakati ameshafariki? Mtu akiwa hai, roho yake inahitaji kutumia viungo vyake kama masikio, miguu n.k., 441


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 442

katika Uislamu

lakini akifariki, roho hujitegemea kila kitu, na ina uwezo wa kusikia lugha yoyote kwa sababu haitegemei kuongozwa na ubongo wa marehemu. Lakini hata hivyo, Mwislamu ambaye imani yake ni tofauti na mafunzo sahihi ya Mtume (s.a.w.w), hawezi kujibu maswali hayo sita kwa usahihi; na matokeo yake ni kwamba wengi wetu hatuwezi kunufaika na lengo zima la kusomewa Talqin kwa kuzingatia kwamba Malaika hawataridhika na majibu yetu yatokanayo na imani potofu. Adhabu ya kubanwa na Kaburi: Imam Ja’far Sadiq (a.s.) anakaririwa akisema kuwa, “Kila anayelazimika kuhojiwa kaburini na asifaulu, atakabiliwa na adhabu ya kubanwa na kaburi pamoja na adhabu nyinginezo kaburini. Lakini yule ambaye ataepushwa kuhojiwa kaburini kutokana na imani yake sahihi, basi ataepushwa pia na adhabu za kaburini.” Maelezo zaidi yanaonyesha kuwa kwa baadhi ya waumini, adhabu hiyo wataisikia kama vile marafiki wawili wanavyokumbatiana wakutanapo. Lakini waumini ambao madhambi yao hayakusafishwa yote na uchungu wa kukata roho (sakaratul-maut), adhabu hii itakuwa kali sana kiasi cha kubanwa na kuvunjwa mbavu! Imam Ja’far Sadiq (a.s.) anakaririwa akisema kuwa, “Tutawaombea msamaha (shafaat) wafuasi wetu, lakini kwa jina la Allah nina wasiwasi nanyi katika kipindi cha “Barzakh” (kati ya kuzikwa na kabla ya kufufuliwa Siku ya Kiyama). Hiki ndicho kipindi ambacho waumini watenda madhambi watapata adhabu yao. Ushahidi wa Uhalali wa Talqin: Vikundi vya Waislamu wanaojiita “Answar Sunna” wanakataza kisomo cha Talqin wakati wa mazishi. Hata hivyo Waislamu wengi bado wanaendeleza sunna hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Kihistoria, ushahidi wa Talqin unapatikana katika tukio la kifo cha mama yake Imam Ali Ibn Abu Talib (a.s.) yaani Bibi Fatima bint Asad – mke wa bwana Abu Talib, kilichotokea wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w). Msiba huo ulimhuzunisha sana Mtume (s.a.w.w) kwa sababu kama 442


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 443

katika Uislamu

tujuavyo, huyo mama ndiye aliyemlea Mtume (s.a.w.w) baada ya Mtume (s.a.w.w) kuwa yatima. Mama huyo alimtendea Mtume (s.a.w.w) kila ukarimu na kumpendelea. Mtume (s.a.w.w) alitoa nguo yake binafsi iwe sanda ya mama huyo baada ya akina mama kumwosha. Mtume (s.a.w.w) alibeba jeneza njia nzima hadi kaburini ambapo aliingia kaburini. Alipokea mwili na kuuweka kaburini na akainama kwa marehemu na kumnong’oneza kwa muda mrefu akimwambia, “Mtoto wako, mtoto wako”. Kisha alinyanyuka akatoka kaburini na ikawa wamefukia kaburi na kusawazisha. Mtume (s.a.w.w) aliinama tena kaburini, na watu walimsikia akisema, “Hapana Mola ila Allah, Ewe Allah nakukabidhi mama huyu kwa dhamana”. Kisha Mtume (s.a.w.w) akaondoka. Waislamu walimhoji, “Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, leo tumekuona ukifanya mambo ambayo hujawahi kufanya”. Mtume (s.a.w.w) alisema, “Leo hii nimempoteza mwongofu wa Abu Talib. Hakika alikuwa mkarimu kwangu kiasi kwamba alipokuwa na kitu kizuri alinipa badala ya kukitumia mwenyewe au kwa watoto wake. Niliwahi kusema kuwa Siku ya Kiyama watu watakusanywa wakiwa wako uchi na hivyo huyu mama akasema, ‘aibu iliyoje!’ Ndipo nilimhakikishia kuwa Mwenyezi Mungu atamfufua akiwa na nguo. Kisha nilielezea adhabu ya kubanwa na kaburi, na ikawa yeye amesema, ‘Ewe, unyonge.’ Nilimhakikishia kwamba Mwenyezi Mungu atamwepusha, na ndiyo maana nimetoa nguo yangu iwe sanda yake na nikainama kichwani kwake kumfundisha majibu ya maswali aliyokuwa akiulizwa wakati huo. Aliulizwa juu ya muumba wake akajibu kuwa ni Allah. Akaulizwa juu ya Mtume, na akajibu: ‘Muhammad (s.a.w.w).’ Kisha akaulizwa nani Imam wake na ikawa amechanganyikiwa na kusita, ndipo nilipomweleza, ‘Mtoto wako, mtoto wako.’ Hapo ndipo akajibu, ‘Mtoto wangu ndiye Imam wangu.’ Baada ya hapo Malaika wawili waliondoka na kusema, ‘Hatuna madaraka juu yako, lala kwa amani kama bibi harusi bila wasiwasi.’ Hapo ndipo Malaika walichukua roho na ikawa mama huyo amefariki tena.’”

443


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 444

katika Uislamu

Tukio hili linaonyesha mapenzi ya Mtume kwa bwana Abu Talib na bibi Fatima bint Asad, na mapenzi yao kwake. Tunaona pia utukufu alionao Mtume (s.a.w.w) mbele ya Allah, kiasi cha kumsamehe Mama Fatima bint Asad misukosuko ya Siku ya Kiyama na kaburini. Vilevile kutokana na tukio hili tunapata asili na uhakika wa Talqin pamoja na matukio ya kaburini kwa mtu anayefariki. Kisa cha Salman Farsi (r.a.): Wakati wa ukhalifa wa Imam Ali (a.s.), alimchagua bwana Salman Farsi kuwa gavana wa Madian. Bwana mmoja jina lake Asbagh bin Nubata (r.a.) alikuwa sahaba mwaminifu wa Imam Ali (a.s.). Bwana Asbagh anaeleza kuwa alikwenda kumtembelea bwana Salman Farsi (r.a.) na kumkuta anaumwa sana anakaribia kufariki. Bwana Asbagh anasema, “Bwana Salman alinieleza kuwa: ‘Ewe Asbagh, Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniusia kuwa karibu na kifo changu nitapata fursa ya kuongea na mtu aliyekufa zamani makaburini, kwa hiyo niweke kwenye machela unipeleke makaburini.” Nilipomfikisha makaburini, bwana Salman alielekea Kibla na kwa sauti akawatolea salamu hapo makaburini. Hakuna aliyejibu. Baada ya kuwatolea salamu mara kadhaa bila majibu, bwana Salman alisema: “Enyi wakazi wa makaburini, mimi ni Salman Farsi mtumwa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume aliniusia kuwa kukaribia kifo changu nitaongea na mtu aliyekufa zamani. Iwapo muda huo umewadia, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake tafadhalini ongeeni na mimi”. Mara ikawa sauti imeitikia salamu na kusema, “Enyi watu mnaojenga na kupandikiza mimea, na mwisho wake majengo huwa maghofu na bustani huoza; uliza unachotaka nitakujibu.” Bwana Salman aliuliza, “Wewe ni miongoni mwa watu wa Peponi au Motoni.” Sauti ilijibu kuwa yeye ni miongoni mwa watu wa Peponi. Bwana Salman alimwomba amweleze jinsi alivyofariki pamoja na uchungu wa mauti aliopitia. Sauti ikamjibu: “Ewe Salman, kwa jina la Allah ni bora mtu angechukua mkasi akawa ananikatakata nyama ya mwilini 444


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 445

katika Uislamu

mwangu mpaka ibakie mifupa, ningeona afadhali kuliko uchungu wa mauti. Ewe Salman, ziku zote nilitenda wema katika uhai wangu duniani, niliswali kwa wakati, nilizoea kusoma Qur’ani, nilikuwa mwema kwa wazazi, nilijipatia riziki ya halali. Siku moja niliugua na maisha yangu yakakatika. Wakati wa mauti yangu ulipowadia, mtu mrefu sana mwenye uso wa kutisha alisimama angani mbele yangu. Alinyoosha kidole machoni pangu na macho yakapoteza uwezo wa kuona. Akaninyooshea kidole masikio yakaacha kusikia, akanyoshea ulimi nikawa siwezi kusema. Nilimwuliza yeye ni nani na kwa nini ananitendea hayo, naye akajibu kuwa yeye ni Malaika wa mauti na kwamba uhai wangu wa duniani umekwisha na hivyo ilikuwa lazima niondoke niende ulimwengu mpya. Kisha watu wawili walinijia, mmoja akakaa kulia kwangu na mwingine kushoto kwangu. Walinieleza kuwa wao ni Malaika wawili waliokuwa wanaandika matendo yangu maisha yangu yote duniani. Mmoja jina lake “Raqiib” alinipatia kumbukumbu yangu ya matendo mema ambayo niliyasoma nikafurahi. Mwingine jina lake “Atiid” alinipa kumbukumbu ya matendo yangu maovu nikasoma na kusikitika. “Ndipo Malaika wa mauti alinisogelea na kuchukua roho yangu kupitia puani na sijasahau uchungu niliopata siku hiyo. Baada ya kufariki, familia na jamaa zangu walianza kulia. Malaika wa mauti alisema, ‘Mnalilia nini wakati sijatenda uovu wowote. Uhai wake umeisha hivyo nimeamrishwa na Allah kuchukua roho yake na nitarejea hapa mara nyingi kwa kazi kama hii.’ “Kisha Malaika mwingine alichukua roho yangu na nilipelekwa akhera ambako niliulizwa maswali kuhusu Swala, Funga, Zaka, Khums, Hajj, Jihaad, kusoma Qur’ani, kuwatii wazazi n.k. Niliulizwa pia kama niliwahi kumwua mtu au kula mali ya mtu bila idhini yake au kuwadhulumu watu n.k. 445


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 446

katika Uislamu

“Malaika huyo alirejesha roho yangu duniani na ndipo watu wakaanza kuniosha na kunivua nguo. Wakati huo roho yangu ilianza kuwasihi waoshaji: ‘Enyi watumishi wa Allah mhurumieni huyo ambaye mwili wake umevunjwavunjwa wakati roho yake ikitoka, na kuacha kiwiliwili kama kimepondwapondwa.’ Roho yangu ilikuwa inawasihi wanioshe taratibu kiasi kwamba kama waoshaji wangeweza kusikia maneno hayo wangeondoka na kuniacha. (Ndio maana haifai kuosha maiti kwa nguvu au kwa kivunja viungo vya marehemu vilivyokwisha kauka, pamoja na tabia ya kukamua ngama). “Kisha walinivalisha sanda na taratibu zote za “khunut” na Swala ya maiti. Waliponilaza kaburini niliogopa sana kiasi maneno hayatoshi kueleza. “Baada ya kufukia kaburi langu, roho yangu ilirejeshwa tena kwangu. Malaika jina lake Munabbih alinijia na kunifanya nikae. Aliniamuru niandike matendo yangu yote niliyofanya duniani. Alinieleza kuwa atanikumbusha, nianze tu kuandika. Nilimwuliza iko wapi karatasi, akasema, ‘ni sanda yako.’ Nilimwuliza iko wapi kalamu. Akajibu, ‘Kidole chako.’ Nilimwuliza kuhusu wino, akajibu, ‘Mate yako.’ “Baada ya kuandika matendo yangu yote, Malaika huyo alitundika maandishi hayo shingoni mwangu kama inavyoeleza Qur’ani 17:13-14. “Baada ya hapo akaingia Malaika wa kutisha jina lake Munkar akiwa amebeba rungu la kutisha na kuniuliza:Nani Mola wako? Nani Mtume wako? Nani Imam wako? Ni ipi Dini yako? Ni kipi Kitabu chako? Ni wapi Kibla chako? “Niliogopa sana mpaka nikachanganyikiwa na kutetemeka viungo vyote. Lakini rehma ya Allah ilinishukia na moyo ukatulia nikajibu maswali yote sawasawa.

446


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 447

katika Uislamu

“Malaika mwingine aitwaye “Nakir” alifika na kunihoji upya juu ya Imani zangu za dini. Nilimjibu, ‘Nashuhudia kwamba hapana mola ila Allah na kwamba Muhammad ni Mjumbe Wake, na Ali na kizazi chake (waliolindwa na dhambi) ni hoja za Allah, na Pepo ni haki, na moto ni haki, na sirat ni kweli ipo, na mizani ni kweli, na kuhojiwa kaburini ni kweli, na kufufuliwa kesho Kiyama ni kweli, kupewa vitabu vya amali Siku ya Kiyama ni kweli, na siku na saa ya Kiyama itawadia na ufufuo vyote ni kweli.’ “Malaika waliposikia majibu hayo ya kweli waliniambia, ‘Lala kama bibi harusi bila wasiwasi.’ Walifungua mlango kichwani kwangu kunionyesha nafasi yangu Peponi na harufu nzuri ya Peponi ilinifikia na upepo mwanana wa Peponi. Kaburi langu ambalo kabla ya hapo lilionekana kama chumba cha gerezani, ghafla liligeuka chumba kipana sana kama bustani kubwa upeo wa macho! “Ewe Salman, mtu amkumbuke Mola wake muda wote, na atumie muda wa uhai wake kwa utiifu Kwake kwa sababu kifo ni jambo la hakika kumtokea kila mtu, na kila mmoja atakumbana na mambo yote niliyokueleza hapa.’” Bwana Asbagh bin Nubata (msimuliaji wa kisa hiki) anasema kuwa mara sauti toka kaburini iliposimama, bwana Salman Farsi (a.s.) alinieleza nimrejeshe nyumbani. Tulipofika nyumbani alilala chini akiwa ameelekea angani, aliswali na hapo hapo akafariki. Mpaka hapa ndugu msomaji kama umesoma kwa makini, utakuwa umetambua hatari ya kukumbatia itikadi potofu za dini ambazo hazitakusaidia kujibu maswali ya kaburini kwa usahihi. Huko nyuma nimetangulia kueleza katika Sura ya 15, chini ya ‘Kufasiri vibaya Qur’ani,’ kwamba, kwa mfano, swali la Nani Imamu Wako linavyopotoshwa na wenzetu Sunni kwa sababu viongozi wao hawatambui haki ya Ahlul-Bayt (a.s.) kuongoza Waislamu baada ya Mtume (s.a.w.w). Tayari hiyo ni kasoro kwa Mwislamu ambaye atajibu swali hilo kinyume na ukweli wake.

447


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 448

katika Uislamu

Huko nyuma nimeeleza majibu wanayotoa viongozi wa Sunni juu ya swali hilo, kwa kudai kuwa Imam ni yule anayeongoza Swala! Uimamu unaokusudiwa hapa siyo huo wa kuongoza Swala bali ni ule wa kiongozi halali wa wakati wako baada ya Mtume (s.a.w.w). Kama jibu ni kiongozi wa Swala, je, huyo kiongozi akifariki, akiulizwa juu ya Imam wake, atamtaja nani? Au kiongozi wa Swala akiwa mtu mwovu atakuwa na manufaa gani kwa wanaomtaja kama Imam wao? Suala hili nimelieleza kirefu katika sura za nyuma. Nimeeleza pia hatari ya itikadi potofu kama vile kudai kuwa Talqin haina faida yoyote kwa marehemu, wakati ambapo jambo hilo ni mojawapo ya mambo yanayomkuta mtu kaburini. Nimeweka somo hilo mahali hapa kwa sababu matayarisho ya mazishi ni ibada yenye kanuni zinazotofautiana kati ya Shia Ithna’asheri na Sunni. Nimeeleza huko nyuma kuwa sisi Shia tunaweza kuzikwa na Sunni kwa kanuni zao, lakini kuzikwa siyo mwisho wa kila kitu, tukizingatia maelezo yaliyotangulia chini ya somo hili. Ibada ya mazishi ni pamoja na marehemu kuwa tayari kujibu maswali kwa usahihi. Marehemu hawezi kujibu yale ambayo hakuyafahamu katika uhai wake duniani. Kusomewa Talqin hakutoshi iwapo anayesomewa hakuwa na imani juu ya hayo anayosomewa. Talqin ni kukumbushwa tu.

MASWALI MUHIMU YA KUJIULIZA Baada ya hoja zote hizo kuwekwa wazi kwa ushahidi wa kitaaluma, ningependa kuwaomba Waislamu au wasomaji kwa ujumla, tujiulize maswali yafuatayo kwa sababu faida ya elimu ni kuitumia: (1)

Je, mpaka hapa unaona ni madhehebu ipi inayofuata nyayo za Mtume (s.a.w.w.) kwa uaminifu?

(2)

Je, unafikiri kuwa suala la madhehebu halina madhara yoyote katika Uislamu? 448


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 449

katika Uislamu

(3)

Je, umetambua tofauti na uzito kati ya Ahlul-Bayt (a.s.) wa Mtume (s.a.w.w.) na masahaba au Waislamu wengineo?

(4)

Je, unatambua hukumu zote za madhehebu yako na kuzifuata? Kama huzitambui, Uislamu wako una misingi gani?

(5)

Je, mpaka sasa madhehebu yako ni kwa misingi ya kurithi kwa wazazi wako, au wewe mwenyewe umechagua kwa ujuzi na utafiti wako?

(6)

Kama madhehebu yako ni kwa misingi ya kurithi, unadhani ni wewe utawajibika au hao wazazi wako waliokupoteza?

(7)

Unaonaje umuhimu wa kujifunza Historia sahihi ya Uislamu?

(8)

Unatambua kuwa Uislamu wa mtu haukamiliki kwa kutoa shahada, kukariri Qur’ani na kuswali Swala tano tu? Au hata kuhiji Makkah?

(9)

Unadhani viongozi wako wa dini wanayo elimu ya kutosha kukusaidia kutambua Uislamu wa kweli? (10) Je, viongozi wako wa dini ni waaminifu kiasi cha kuwa tayari kujadili hoja hizi bila jazba, na mwisho kukubaliana na ukweli ulio tofauti na matakwa au mazoea yao? (11) Unafahamu kuwa Mtume (s.a.w.w.) alituamuru kutafuta elimu kwa uwezo wetu wote, hata kama itatubidi tuitafute elimu hiyo hadi China? (12) Unaelewa kuwa Hadithi hiyo ya kutafuta elimu ina maana kwamba hakuna mtu atakayesamehewa kwa kuwa mjinga kama kisingizio chake cha kupotea?

449


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 450

katika Uislamu

(13) Wazionaje Aya zifuatazo za Qur’ani:-

(a) “Je! Yule afanyaye ibada wakati wa usiku kwa kusujudu na kusimama, na kuogopa Akhera na kutarajia rehma za Mola wake (ni sawa na yule asiyefanya hivyo?) Sema: Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanababi ni wale wenye akili tu.” (Qur’ani 39:9)

(b) “....... Na wasio hukumu kwa (kutumia) yale aliyoteremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri” (Qur’ani 5:44)

c) “Na wale wanaojitahidi kwa nguvu kwa ajili Yetu, bila shaka Tutawaongoza katika njia zetu.” (Qur’ani 29:69)

(d) “Wale ambao husikiliza kauli (nyingi zinazosemwa) kisha wakafuata zilizo nzuri zaidi, hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza, na ndio wenye akili.” (Qur’ani 39:18)

450


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 451

katika Uislamu

(e) “Huwezi kuwakuta watu wanaomwamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho wakiwafanya marafiki wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume Wake, hata kama ni baba (zao), au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao……” (Qur’ani 58:22) Jambo la Busara: Ndugu msomaji wa kitabu hiki, ninatumaini baada ya kujiuliza maswali hayo na kuzingatia Aya hizo za Qur’ani, Mwenyezi Mungu atakuongoza kuyajibu maswali hayo kwa uaminifu na mwisho wewe kutumia busara zako kuona ukweli na kuupokea bila kujali maoni ya mtu yeyote yule. Tufahamu kuwa hapo zamani enzi za ujinga huko ulaya, watu wengi sana au tuseme watu wote, waliamini kuwa umbo la dunia ni sawa na meza pana sana, kiasi kwamba ukisafiri mwendo wa kutosha utafika ukingoni na kutumbukia (kuporomoka)! Hakuna mtu aliyetambua kuwa dunia ni mviringo! Baada ya muda, alitokea bwana Galileo ambaye alifanya utafiti na kutangaza kuwa dunia ni mviringo! Watu walimpinga kwa kuleta mawazo yaliyotofautiana na walio wengi! Mwisho mtu huyo aliteswa na viongozi wa kidini, akituhumiwa kuanzisha imani mpya zinazopingana na dini yake! Baada ya miaka kupita ikawa ujinga umepita, na ukweli ukawa wazi kuwa dunia kweli ni mviringo kama chungwa! Kwa hiyo watu wajinga wanaweza kumdhuru msema kweli, lakini hatuwezi kuficha ukweli milele. Fundisho la maana ni kwamba hatuwezi siku zote kutegemea waliowengi kuwa ndio wakweli! Suala la msingi ni kila mtu kutumia akili vizuri na kutafuta ukweli.

451


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 452

katika Uislamu

Kiongozi mmoja aliyekuwa maarufu (sasa ni marehemu) huko Marekani bwana Abraham Lincoln aliwahi kueleza kuwa, “Unaweza kudanganya baadhi ya watu muda wote, au kudanganya watu wote kwa muda fulani, lakini huwezi kudanganya watu wote muda wote.” Viongozi wengi wa dini hawataki kufichua ukweli ambao unaweza kuwafanya wapoteze maslahi yao ya kidunia. Dini inatumiwa kama ajira. Waislamu tumefikia ujinga wa kukubaliana na baadhi ya madai ya vyombo vya kutetea haki za binadamu, kwamba eti sheria fulani za kiislamu ni za ukandamizaji kwa wanawake; wakati sheria kama hizo hazihusiani kabisa na Uislamu wa kweli!

“Anayesikia Aya za Mwenyezi Mungu zikisomwa juu yake kisha anazidi kushikilia kujivuna kama kwamba hakuzisikia; basi mpe habari ya adhabu yenye kuumiza..” (Qur’ani 45:8)

“Na kama ukiwatii wengi katika hawa waliomo ulimwenguni watakupoteza kutoka katika njia ya Mwenyezi Mungu; Hawafuati ila dhana tu, hawana ila (ni wenye kusema) uongo tu.” (Qur’ani 6:116). Baada ya binadamu kupewa akili, anatakiwa azitumie kwa faida yake ya kidunia na kiroho. Mara nyingi tunatumia akili zetu kuboresha maisha yetu ya kidunia kama vile kuongeza kipato na kuishi maisha mazuri. Lakini ni mara chache sana kuwaona watu wakifanya juhudi ya kuboresha maisha yao ya kiroho! Na hayo si matumizi mazuri ya akili tuliyopewa na Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo hakuna binadamu ambaye atadai kuwa kapotezwa na fulani au fulani. Kila mwenye kupewa akili atawajibika binafsi - peke yake:

452


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 453

katika Uislamu

“Na wote watahudhuria mbele ya Mwenyezi Mungu. Ndipo wanyonge watasema kuwaambia wale waliojivuna: ‘Hakika sisi tulikuwa tukikufuateni ninyi, je mnaweza kutuondolea kitu chochote katika adhabu ya Mwenyezi Mungu?’ Hao watasema: ‘Angalituongoza Mwenyezi Mungu bila shaka tungalikuongozeni. Lakini sasa ni mamoja kwetu, tuwe na subira au tusiwe na subira hatuna pa kukimbilia.” (Qur’ani 14:21)

“Na wale wanaokadhibisha hoja zetu ni viziwi na mabubu, waliomo katika giza; Mwenyezi Mungu humwachia kupotea amtakaye na humwongoa amtakaye.” (Qur’ani 6:39) Mpaka hapa ni matumaini yangu kwamba Mwislamu yeyote mwaminifu, mwenye kuzingatia yaliyoelezwa humu, na mwenye kuzingatia Aya za Qur’ani nilizozitoa hapa, bila shaka atafikia uamuzi wa busara utakaomnusuru na makundi 72 yatakayoangamia motoni kwa upotofu! - Insha Allah. Rehma na Amani zimshukie Bwana wetu Muhammad, mwisho wa Mitume na Aali Zake watukufu waliotakasika, na Sahaba Zake waaminifu waliofuata nyayo zake tukufu - Ilaahi Yaa Amin. 453


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

AL-LAAHUMMA TAQABBAL MINNAA TAMMAT BIL KHAYR. Isa Rwenchungura 24 Muharram, 1421 A.H. Dodoma, Tanzania 29 April, 2000 A.D

454

Page 454


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 455

katika Uislamu

BIBLIOGRAFIA 1. Shia’h - Allamah Sayyid Muhammad Husayn Tabatabai 2. The Holy Prophet - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 3. Sautu’l ‘Adalati’l Insaniyyah (Toleo la kiingereza) George Jordac Lebanon 4. Ask those Who Know - Muhammad at-Tijani Samawi 5. Bustani ya Elimu - Jz.1 - Bilal Muslim Mission - Dsm. 6. Manhaj Ul-Fiqh Il-Islam - Islamic Propagation Organisation - Iran 7. Then I was Guided - Muhammad at-Tijani Samawi 8. The Qur’ani - Tahrike Tarsile Qur’ani (English) vol.1 - S.V. Mir Ahmad Ali - Peermohamed Ebrahim Trust - Karachi, Pakistan 9. The Light Magazine - October 1991 - Bilal Muslim Mission -Dsm. 10. The Light Magazine - June 1992 - Bilal Muslim Mission -Dsm. 11. Muhammad The Messenger of Allah - A.B.C. - Arusha 12. Guidance From Qur’ani - Bilal Muslim Mission - Dsm. 13. The Ritual And Spiritual Purity - Sayyid Muhammad Rizvi - Canada 14. The Right Path (al-Muraaja’at) - Abdul-Husayn Sharafud- Din alMusawi (English) - Iran 15. Imamat - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 16. A Brief History of The Fourteen Infallibles - Ansariyan Publications Iran 17. Imam Zaman - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 18. Western Civilization Through Muslim Eyes - Sayyid Mujtaba Rukni Musawi Lari - Iran 19. Day of Judgement - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 20. Kwa nini Shia husujudu juu ya Udongo - Bilal Muslim Mission - Dsm 21. The Light Magazine - December, 1988 - Bilal Muslim Mission - Dsm 22. Ghadir-Khum - Dar ul Muslimin - Dodoma 23. Daily News - Tanzania - 23/6/92 24. Qur’ani and Hadith - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 25. Ulul Amr ni Nani - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 455


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 456

katika Uislamu

26. Islam - An Introduction - Begum Aisha Bawany Wakf -Karachi Pakistan 27. Holy Bible - By the Gideons - King James Version 28. Family Life of Islam - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 29. Husayn The Saviour of Islam - S.V. Mir Ahmad Ali - Shafagh Publications - Iran 30. Muhimu wa Hijab - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 31. Music and It’s Effects - By A.H. Sheriff - Bilal Muslim Mission 32. Mambo Yanayomhusu Maiti - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 33. The Independent (21-2-89) - U.K. 34. Africa Events - March, 1989 - U.K. 35. The Light - Vol. 28 No:1, February 1994 - Bilal Muslim Mission - Dsm. 36. The Muslim - March - April 1991 37. Qur’ani Takatifu - Saleh Farsi (Swahili) - Mombasa 38. Holy Qur’ani - English Translation (With Arabic) - M. H. Shakir - Iran, Published by Sayed Mujtaba M. Lari 39. Islamic Laws of Worship and Contracts - Ayatullah Al-Udhma Muhammad Shirazi. Al-Zahra Islamic Foundation - Canada - 1993 40. Bible, Qur’ani and Science - Maurice Bucaille - 1989 - France 41. Justice Of God - Bilal Muslim Mission of Dar es salaam 42. Sauti ya Bilal - No. 4 - July, 1990 43. Kitabu cha Tajwid - Amiraly M.H. Datoo - Bilal Muslim Mission Dsm 44. Sauti ya Bilal - No. 2 - Machi, 1991 45. Shia na Sahaba - Abdillahi Nassir - Kenya 46. Nahjul Balaghah - (English Version) - Imam Ali Ibn Abi Talib (a.s.) 47. Your Questions Answered - Vol. 6 - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 48. Slavery - From Islamic & Christain Perspective - S.S.A. Rizvi Canada, Vancouver - Islamic Education Foundation 49. The Seal of the Prophets and His Message - S. Mujtaba Musavi Lari Iran 50. Shia na Qur’ani - Abdillah Nassir Mombasa - Kenya 456


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 457

katika Uislamu

51. Women in Islam Versus The Judeo - Christian Tradition -Myth and Reality - Institute of Islamic Studies - U.K. - 1995 52. Fitina za Wahabi Zafichuliwa - Bilal Muslim Mission - Dar es salaam 53. The Prophet of Islam - Syed Muhammad Husain Shamsi - Kenya 54. Sauti ya Bilal - Na. 4 - July 1991.

457


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia 458

Page 458


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu 26. 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56.

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl 459

Page 459


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu 57. 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85.

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea 460

Page 460


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

86. 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Msahafu wa Imam Ali Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne 461

Page 461


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

katika Uislamu

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa

114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha 462

12:26 PM

Page 462


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

katika Uislamu

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje?

140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Elimu ya Ghaibu

152.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni Na.1

153.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni Na.2

154.

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni Na.3

155.

Kati ya Alama kuu za dini ni Swala ya Jamaa na Adabu za Msikiti na Taratibu zake

156.

Abu Huraira

157.

Mazingatio kutoka katika Qur’an

463

Page 463


Asili ya

ya madhehebu katika Uislamu final Lubumba.qxd

Asili ya Madhehebu

7/1/2011

12:26 PM

Page 464

katika Uislamu

BACK COVER Suala la madhehebu lilianza kuzungumzwa na Mtukufu Mtume SAW mwenyewe katika hadithi zake tukufu: “Mayahudi walikuwa madhehebu sabini na tatu baada ya Nabii Musa AS, na Wakristo madhehebu sabini na mbili baada ya Nabii Isa AS, na Umma wangu huu utakuwa na madhehebu sabini na moja baada yangu, na (madhehebu) zote (zitaingia) Motoni isipokuwa moja.� Kutokana na kauli hii ya Mtume SAW ni kwamba suala la madhehebu haliwezi kuepukika, lazima madhehebu zitakuwepo bali changamoto moja tu iliyoko katika kauli hii ni kwamba madhehebu zote hizo zitaingia Motoni isipokuwa moja. Suala hapa sasa ni kufanya utafiti ili kujua ni madhehebu ipi hiyo itakayokuwa salama, na sio kugombana kwa jambo ambalo lilikwishatabiriwa na Bwana Mtume mwenyewe - na hiki ndicho alichofanya mwandishi wa kitabu hiki. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

464


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.