Ahlulbayt ndani ya tafsiri za kisunni (sehemu ya tatu)

Page 1

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

AHLUL BAYT NDANI YA TAFSIR ZA KISUNNI SEHEMU YA TATU KWA MUJIBU WA IBN KATHIR, SUYUTI, BURUSAWI, ALUSI NA QASIMI

Kimeandikwa na: Sheikh Nizar al - Hasan

Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul)

Page A


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

B

7/1/2011

11:03 AM

Page B


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

ŠHaki ya kunakili imehifadhiwa na: AL-ITRAH FOUNDATION ISBN: 978 - 9987 - 512 - 97 - 3

Kimeandikwa na: Sheikh Nizar al - Hasan Kimetarjumiwa na: Hemedi Lubumba (Abu Batul) ] Kimehaririwa na: Ustadh Abdalla Mohamed Kimepangwa katika Kompyuta na: Hajat Pili Rajab Toleo la kwanza: April, 2011 Nakala: 1000 Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

11:03 AM

Page C


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

YALIYOMO Utangulizi..........................................................................................2 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Ibnu Kathir, Inayoitwa TafsirulQur’an Al-Adhim..............................................................................9 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsiri ya Suyuti, Inayoitwa Ad-DurulManthur Fit- Tafsir - U- Maathur ...................................................41 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Burusawi, Inayoitwa Tafsir Ruhul-Bayan Fi Tafsiril-Qur’an .....................................................93 Ahlul Bayt (a.s) ndani ya Tafsir ya Alusi, inayoitwa Ruhul - Ma’aniy Fittafsiril -Qur’an Al-Adhim Wasab’ul- Mathaniy.......................119

Page D


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

NENO LA MCHAPISHAJI Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiarabu kiitwacho, Ahlu ‘l-Bayti Fi Tafasiri Ahli ‘s-Sunnah kilichoandikwa na Sheikh Nazri Hasan. Sisi tumekiita, Ahlul Bayt Ndani ya Tafsiri za Kisunni. Hii ni sehemu ya tatu inayochambua tafsiri za wanavyuoni wakubwa wa Kisunni – Ibn Kathir, Suyuti, Burusawi, Alusi na Qasimi. Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Ni muhimu kukubaliana na kuziheshimu tofauti za kila mmoja na kutambua msimamo na mtazamo wa kila mmoja. Matatizo huja pale mtu anapolazimisha tabia, imani na mila zake zitawale wengine au kuzifisha itikadi na misimamo ya wengine. Ni muhimu kufikiria kila aina ya maoni katika E

Page E


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Wafuasi wa madhehebu nyingine wanaweza kuchambua uthibiti wa kitabu hiki ili kujenga maoni yao wenyewe kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe. Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inaweza ikasemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofauti, hawaelewi kwa ukamilifu mtazamo wa kwao wenyewe. Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu. Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeamua kuchapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili. Tunamshukuru ndugu yetu, Hemedi Lubumba (Abu Batul) kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwake. Ni matumaini yetu kwamba kitabu hiki kitakuwa ni changamoto kubwa kwa wasomaji wetu. Mchapishaji: Al-Itrah Foundation

F

Page F


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

NENO LA JUMUIYA Hakika mirathi ya Ahlul-Bait ambayo imehifadhiwa na kambi yao na wafuasi wao dhidi ya upotovu inaonyesha kambi iliyokusanya aina mbalimbali za taaluma za kiislamu. Kambi hii imeweza kulea nafsi mbalimbali zilizo tayari kunywa kutoka kwenye chemchemu hiyo, na kuupa umma wa kiislamu wanavyuoni wakubwa wenye kufuata nyayo za ujumbe wa AhlulBait. Wanavyuoni waliokusanya vidodosa na maswali mbalimbali ya madhehebu na mitazamo tofauti ya kifikira kuanzia ndani ya desturi ya kiislamu hadi nje ya desturi hiyo, huku wao wakitoa majibu na utatuzi makini juu ya maswali hayo ndani ya karne zote. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait imefanya hima kutetea utukufu wa ujumbe wa Uislamu na ukweli wake ambao umechafuliwa na makundi, madhehebu na wanaharakati mbalimbali wenye chuki na Uislamu. Jumuiya imefuata nyayo za Ahlul-Bait na za wafuasi wa kambi yao njema ambayo imefanya hima kujibu madai yenye kuendelea na daima ikajaribu kubaki ndani ya msitari wa mapambano kwa kiwango kinachohitajika ndani ya kila zama. Hakika uzoefu ambao umehifadhiwa ndani ya vitabu vya wanavyuoni wa kambi ya Ahlul-Bait katika dhamira hii ni wa aina ya pekee, kwa sababu una akiba ya kielimu inayotegemea akili na hoja, huku ukijiepusha na matamanio na upendeleo uliokatazwa. Unazungumza na wasomi na wanafikra wenye fani maalumu, mazungumzo ambayo yanakubalika kiakili na yanapokewa na maumbile yaliyo salama. Jaribio hili la Jumuiya ya kimataifa ya Ahlul-Bait limekuja kuwapa watafuta ukweli hatua mpya ya uzoefu wa thamani katika ulingo wa mazungumzo na maswali na kujibu hoja za utata zilizotolewa zama zilizopita au zinazotolewa leo kwa njia ya Tovuti, na hasa kwa kupewa nguvu na baadhi ya G

Page G


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

duru zenye chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu. Ikijiepusha na uchochezi uliyokatazwa, na ni yenye kuhangaikia kuzishauri akili zenye kufikiria na nafsi zenye kutafuta haki, ili ziweze kufikia kwenye haki ambayo inatolewa na Kambi ya Ahlul-Bayt ulimwengu mzima, ndani ya zama ambazo akili inaerevuka na nafsi na roho zinaboreka kwa kasi ya pekee. Ni lazima tugusie kuwa mfululizo huu wa tafiti hizi umeandaliwa na Kamati maalumu toka jopo la wanachuoni watukufu, hivyo tunatoa shukurani njema kwa hawa wote na kwa wasomi na wahakiki kwa kila mmoja miongoni mwao kwa kupitia sehemu ya tafiti hizi na kutoa mchango wao wa thamani kuhusu tafiti hizi. Na sote tunategemea na kutaraji kuwa tutakuwa tumetoa kile tulichokiweza katika juhudi za kutekeleza baadhi ya wajibu tulionao mbele ya ujumbe wa Mtukufu Mola Wetu Mlezi ambaye alimtuma Mtume Wake na uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi dhidi ya dini zote. Na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi. Jumuiya ya kimataifa ya Ahlu-Bait Kitengo cha utamaduni

H

Page H


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

I

7/1/2011

11:03 AM

Page I


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Page 1


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

UTANGULIZI Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Rehema na amani zimwendee Mtume Muhammad, yeye na aali zake watoharifu. Na daima laana iwe juu ya wote walio maadui zao na wakanushaji wa fadhila zao. Qur’ani iliteremkia katika nyumba tohara na safi, ambazo imeidhinishwa zitukuzwe, katika nyumba za aali Muhammadi watoharifu, ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu amezifanya makhsusi kwa ajili ya heshima na utukufu kuliko nyingine, na Mwenyezi Mungu akazitaja (nyumba hizo) kupitia Aya za Qur’ani tukufu ambazo zitaendelea kubaki muda wa dahari yote zikisomwa usiku na mchana, na si nyumba za viumbe wengine. Kwa ajili hiyo tunawaona (a.s.) wao ndio watambuzi na wajuzi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu kuliko wengine wote, na kwa ajili hiyo tunamwona Amirul-Muuminina Ali bin Abu Talib (a.s.) akisema: “Lau nikitandikiwa mto kisha nikaketi juu yake nitahukumu baina ya wanataurati kwa Taurati yao na wanainjili kwa Injili yao, na baina ya wanazaburi kwa Zaburi yao na wanafurqan kwa Furqani yao. Wallahi hakuna Aya yoyote iliyoteremshwa bara au baharini, katika tambarare au jabali, mbinguni au ardhini, usiku au mchana, ila mimi namjua ni nani wa iliteremka kwa ajili yake, na iliteremka kuhusu nini.”1 Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Imam Ali (a.s.) kwamba alisema: “Wallahi hakuna Aya iliyoteremka ila najua iliteremka kwa ajili ya nani, na wapi iliteremka, na hakika Mola Wangu Mlezi amenitunukia moyo wenye akili na ulimi wenye kudadisi.”

1 Matwalibus-Suul, cha Ibnu Talha as-Shafiiyu Juz. 1, Uk. 125, chapa ya Taasisi ya Ummul-Qura. 2

Page 2


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Na pia Abu Naiim ameandika katika kitabu Hilyatul-Awliyai kutoka kwa Ibn Mas’ud, amesema: “Hakika Qur’ani iliteremshwa kwa herufi saba, hakuna herufi yoyote ila ina dhahiri na batini, na hakika Ali bin Abu Talib ndiye mwenye dhahiri na batini.” Na kuna kauli moja inanasibishwa na Amirul-Muuminina (a.s.): “Lau nikitaka kuwapigisha magoti ngamia arubaini kwa tafsiri ya Qur’ani ninaweza.” Kisha wao ndio wafasiri wa wahyi wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, wenza wa Kitabu chake na Kitabu kitamkacho, haya ndio yathibitishwayo na Hadithi ya Vizito viwili: “Mimi ni mwenye kuacha kati yenu vizito viwili: Cha kwanza ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu, humo mna uongofu na nuru…., na Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu, nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu.”2 Hivyo wao ndio wabainishaji, wafafanuzi na wafasiri wa misamiati ya Qur’ani Adhimu. Kwa sababu Kitabu cha Mwenyezi Mungu kina haja ya kupata mfasiri, mfafanuzi na mbainishaji, hivyo ni aula kifani chake na mwenza wake ndiye mbainishaji, mfasiri, alimu na mjuzi wa Kitabu hicho na si mwingine. Kwa ibara nyingine tunaweza kusema: Hakika Ahlul-Baiti (a.s.) ndio waliokusudiwa, kuainishwa na kuashiriwa katika semi zake (s.w.t.). Bali ni katika nyumba zao ndimo kilimoteremka Kitabu, na wenye nyumba ndio wajuzi zaidi wa yale yaliyomo ndani ya nyumba yao. Kuanzia hapa tunawakuta Ahlul-Baiti (a.s.) siku zote wakiifasiri Qur’ani na Maneno ya Mwenyezi Mungu vizuri zaidi na kwa ukamlifu mno. Na watu wote wakirejea kwao bila kumtenga yoyote, na wala hatujaona tukio lililo kinyume na hali hiyo, hata Ibnu Abbas ambaye ni kinara na kiongozi wa wafasiri miongoni mwa sahaba yeye naye alikuwa ni mwanafunzi wa 2 Sahih Muslim, Juz. 4, Hadithi ya 1873. 3

Page 3


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ali (a.s.), yeye mwenyewe anasema: “Tafsiri ya Qur’ani niliyonayo ni kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.)”. Hapo hapo tunawaona ulamaa wa makundi mawili, Shia na Sunni wameifasiri Qur’ani Tukufu kupitia riwaya na nukuu, kama vile Tafsiri ya Ali bin Ibrahim al-Qummiy, Tafsirul-Ayyashiy na Furatil-Kufiy, KanzudDaqaiq ya Ibnu al-Mash’hadiy, al-Burhan ya Sayyid Hashim al-Bahraniy, Nurut-Thaqalayn ya Sheikh Abdu Ali al-Hawiziy, na wengineo miongoni mwa Maimamiya ambao wameifasiri Qur’ani kupitia Ahlul-Baiti (a.s.). Na miongoni mwa Masunni ni kama vile al-Haskaniy katika ShawahidutTanziil, Isfihaniy katika an-Nuru al-Mushtaalu na al-Wahidiy katika Asbabun-Nuzuul. Pia zipo tafsiri zilizozagaa huku na huko ambazo zinategemewa na Sunni katika utafiti na mchakato wa kielimu. Tafsiri hizi zimefasiri baadhi ya Aya tukufu kwamba walengwa halisi wa Aya hizo ni aali Muhammad (a.s.), hivyo tumejaribu kuzikusanya na kuziweka pamoja Aya hizi toka katika kabati za vitabu vya tafsiri muhimu zenye kutegemewa kwao. Miongoni mwazo ni: 1. Jamiul-Bayan Fii Tafsirul-Qur’ani ya Abu Jafar Muhammad bin Jarir bin Yazid bin Kathiir bin Ghalib atTabari, aliyefariki mwaka 310 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri yenye juzuu 30. 2. Al-Kashfu wal-Bayan Anitafsiril-Qur’ani ya Abu Is’haqa Ahmad ibnu Ibrahim at-Thaalabiy an-Nisaburiy al-Muqriu, aliyefariki mwaka 427 A.H. 3. Maalimut-Tanziil ya Abu Muhammad Husain bin Mas’ud bin Muhammad, maarufu kwa jina la Farrau al-Baghawi asShafiy, aliyefariki mwaka 516 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa yake ya Beirut ambayo ina juzuu 4 4

Page 4


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 4. Al-Kashaf Anihaqaiqit-Tanziil Wauyuunil-Aqawiil Fii Wujuhit-Taawiil ya Abu Qasim Mahmudu bin Umar bin Muhammad bin Umar al-Khawarazimiy al-Hanafiy alMuutazaliy az-Zamakhshariy, mwenye lakabu ya Jarullah, aliyefariki mwaka 538 A.H. Nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ya mwaka 1948 A.D. 5. Mafatihul-Ghaybi ya Abu Abdillah Muhammad bin Umar bin Husain bin Hasan bin Ali at-Tamimiy al-Bakriy atTarstaniy ar-Razi, mwenye lakabu ya Fakhrud-Din, maarufu kwa jina la Ibnul-Khatib as-Shafiy, aliyefariki mwaka 606 A.H. 6. An’warut-Tanziil Waasrarut-Taawiil ya Kadhi Mkuu Nasrud-Din (Abul-Khayri), Abdullah bin Umar bin Muhammad bin Ali al-Baydhawi as-Shafiy, aliyefariki mwaka 691 A.H. iliyo katika juzuu mbili, iliyochapishwa Misri mwaka 1968 A.D. 7. Al-Jamiu Liahkamil-Qur’an ya Abu Abdillah Muhammad bin Ahmad bin Abubakri al-Ansariy al-Khazrajiy alUndlusiy al-Qurtubiy, aliyefariki mwaka 761 A.H. iliyo katika juzuu ishirini, iliyochapishwa Misri mwaka 1950 A.D. 8. Tafsirul-Qur’ani al-Adhiim ya Hafidh Imadud-Din (AbulFidai), Ismail bin Amru bin Kathiir bin Dhaw’u bin Kathiir bin Zar’i al-Baswriy ad-Damashqiy, Ibnu Kathiir, aliyefariki mwaka 774 A.H. iliyo katika juzuu tano, iliyochapishwa Beirut. 9. Ad-Duru al-Manthur Fii Tafsiri Bil-Maathur ya Hafidh Jalalud-Din (Abul-Fadhli), Abdurahman bin Abubakri bin 5

11:03 AM

Page 5


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Muhammad as-Suyuti, aliyefariki mwaka 911 A.H. iliyo katika juzuu nne, iliyochapishwa Misri. 10. Ruhul-Bayan ya Allamah Sheikh Ismail Haqiyyu alBarusiyyu, aliyefariki mwaka 1137 A.H. iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Uthmaniya ya mwaka 1330 A.H. 11. Ruhul-Maaniy ya Allamah Abul-Fadhli Shihabud-Din, Sayyid Muhammad Al-Alusiy, aliyefariki mwaka 1270 A.H., iliyo katika juzuu thelathini, nasi hapa tumetegemea chapa ya Misri ambayo ilipigwa chapa na Al-Muniriyah mwaka 1345 A.H. 12. Tafsirul-Qummiy, maarufu kwa jina la Mahasinut-Taawiili ya Allamah as-Sham Muhammad bin Jamalud-Din alQasimiy, aliyefariki mwaka 1322 A.H., iliyo katika juzuu kumi na saba, nasi hapa tumetegemea chapa ya Beirut ya Ihyaut-Turathil-Arabiy ya mwaka 1415 AH. Tafsiri hizi zimepangwa kulingana na kipaumbele na umuhimu. Hivyo kutokana na wajibu wa kiitikadi na jukumu la kisheria, pia kutokana na kuwepo mapungufu ambayo ni lazima tuyazibe kwa kile kinachonasibiana na ukubwa wa mahitaji ya upungufu huo, na ili kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu Ambaye mara kwa mara ametangaza katika Qur’ani wito wa kuwapenda aali Muhammad (a.s.) aliposema: “Sema: Kwa haya siombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi katika kizazi changu” (Sura Shura: 23), tumefanya kazi hii iliyobarikiwa ambayo inamimina maji katika bahari ya aali Muhammad (a.s.) iliyojaa na yenye kububujika.

6

Page 6


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Na ni kutokana pia na umuhimu wa kazi hii katika kuthibitisha maarifa na nafasi ya Ahlul-Baiti (a.s.), ili uthibitisho huo uwe hoja yenye nguvu, na hapo utimie msemo “Nafuata kinywa chako.� Pia ni ili kuthibitisha kwamba wao ndio walioainishwa na kukusudiwa na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kazi hii imeendelea toka siku ya kumi na nane ya mfunguo pili mwaka 1420 A.H. mpaka siku ya ishirini na tatu ya mfunguo tatu mwaka 1426 A.H., lakini kazi hii ilikumbwa na matatizo mengi ikiwa ni pamoja na hali kutotulia, kutopatikana rejea, na nyudhuru nyingine mfano wa hizo. Pamoja na hayo yote tulivumilia kwa kalamu ya mahaba na upendo wetu kwa wateule Ahlul-Baiti (a.s.) nyudhuru zote zilizotukabili, tukazama katika kina cha tafsiri na wafasiri ili tutoe humo johari na vito vya aali Muhammad (a.s.) baada ya kuwa vimefichwa na kufunikwa na vumbi la historia kwa sababu za kisiasa na kidunia. Pia katika ziara yetu ya kitafsiri tumezitambua nafsi za wafasiri, hivyo tumegundua kwamba Ibnu Kathir ni ndiye mwenye maradhi makubwa ya nafsi na ndiye mwenye chuki kubwa dhidi ya Ahlul-Baiti (a.s.) na wafuasi wao wema. At-Thaalabiy ndiye mwadilifu na mwenye insafu kuliko wengine. Utafiti huu tuliuwakilisha kwenye kongamano la mwaka la Sheikh Tusiy ambalo lilifanyika katika Jamuhuri ya Kiislam ya Iran katika Jiji la Qum Takatifu, mwaka 1426 A.H. hatimaye ukapata tuzo katika kongamano hilo adhimu. Haya yote ni sehemu ya fadhila za Mola Wangu na neema kutoka Kwake (s.w.t.), na ni sehemu ya msaada toka katika roho toharifu (a.s.), kwa sababu kazi hii ni kwa ajili yao na si kwa ajili ya mwingine.

7

Page 7


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mwisho tunainua mikono yote kutoa shukurani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, tunamwomba maghufira dhidi ya utelezo na makosa yaliyotoka kwetu, kwa sababu umaasumu ni wa wenye nao. Pia tunamtaka msamaha msomaji mpendwa kutokana na makosa yasiyo ya kukusudiwa atakayoyakuta humu. Na kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote. Nizar Hasan 2 Mfunguo Nne 1427 A.H. Qum Takatifu

8

Page 8


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA IBNU KATHIR, INAYOITWA TAFSIRUL-QUR’AN AL-ÁDHIM

SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Sura Al-Baqarah: 274). Ibnu Abi Hatim amesema: “Ametusimulia Abu Said al-Ashji kwamba: ‘Alitupa habari Yahya bin Yaman kutoka kwa Abdul-Wahab bin Mujahid kutoka kwa Ibnu Jubayri kutoka kwa baba yake, amesema: ‘Ali alikuwa na dirhamu nne, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri, ndipo ikatremka: “Wale watoao mali zao…’”3 Lakini Ibnu Mardawayhi ameipokea kwa njia nyingine kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abutalib.4

3 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 281, Chapa ya Beirut ya D?rul-Qalam. 4 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 281, Chapa ya Beirut ya D?rul-Qalam 9

Page 9


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT A’ALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: “Ewe Maryam unatoa wapi hivi. “Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Sura Aali Imran: 37). Al-Hafidh Abu Ya’la amesema: “Ametusimulia Sahlu bin Zanjila amesema: “Ametusimulia Abdullah bin Salih amesema: Ametusimulia Abdullah bin Lahi’ah kutoka kwa Muhammad bin al-Mukandir kutoka kwa Jabir kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikaa siku kadhaa bila kula chakula mpaka hali hiyo ikawa nzito juu yake. Akaenda kwenye nyumba za wakeze lakini hakupata kwa yeyote chochote, ndipo akaenda kwa Fatima na kumwambia: “Ewe mwanangu mpendwa! Je una chochote ninachoweza kula kwani hakika mimi ni mwenye njaa?” Akamjibu: “Wallahi sina ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa haki ya baba yangu na mama yangu.” Mtume alipotoka, jirani wa Fatima alimletea Fatima vipande viwili vya mkate na finyango ya nyama, akavitwaa na kuviweka ndani ya bakuli lake, akasema: “Wallahi katika hiki nitampa kipaumbele Mtume wa Mwenyezi Mungu kabla ya nafsi yangu na kabla ya yule aliyopo kwangu.” Japokuwa wote walikuwa wanahitajia chakula lakini Fatima alimtuma Hasan au Husein aende kumwita Mtume (s.a.w.w.) naye alikuja. Fatima akamwambia: “Kwa haki yako na ya mama yangu, Mwenyezi Mungu ameleta kitu nami nimekihifadhi kwa ajili yako.” Akamwambia: “Kilete ewe binti yangu mpendwa.” 10

Page 10


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Akamletea bakuli na alipolifunua ghafla akakuta limejaa mikate na nyama, akapatwa na mshangao na akatambua kuwa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu. Akamuhimidi Mwenyezi Mungu, akamsalia Mtume na akamkabidhi chakula hicho Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) alipokiona alimuhimidi Mwenyezi Mungu na akasema: “Umetoa wapi hivi ewe binti yangu mpendwa? “Akajibu: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Mtume akamuhimidi Mwenyezi Mungu na kusema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya ewe binti yangu mpendwa kifani wa Seyida wa wana wa Israel (Mariam). Kwani hakika yeye alikuwa aruzukiwapo chochote na Mwenyezi Mungu kisha akiulizwa kakipata wapi husema: Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akampelekea ujumbe Ali aje. Akala Mtume, Ali, Fatima, Hasan, Husein na wakeze wote na AhlulBaiti wake wote mpaka wakashiba. Fatima alisema: “Bakuli lilibaki kama lilivyokuwa likiwa limejaa. Hivyo nikawagawia majirani zangu wote na Mwenyezi Mungu aliweka humo kheri nyingi na baraka tele. “5 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran: 42). 5 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 310. 11

Page 11


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:03 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Tirmidhi amesema: “Ametusimulia Abu Bakr bin Zanjawihi amesema: Ametusimulia Abdur-Razzaq amesema: ‘Ametusimulia Ma’amar kutoka kwa Qatadah kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha katika wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid, Fatima binti Muhammad na Asia mke wa Firaun.” Ameipokea Tirmidhi peke yake na amesema ni Hadithi Sahihi.6 Na amesema Abdullah bin Abi Jafar Razi kutoka kwa baba yake amesema: “Thabit al-Banani alikuwa akisimulia kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wanawake bora ulimwenguni ni wanne: Maryam binti Imran, Asia mke wa Firaun, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Ameipokea Ibnu Mardawayhi.7 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Abu Bakr bin Mardawayhi amesema: “Ametusimulia Sulayman bin Ahmad amesema: Ametusimulia Ahmad bin Daud al-Makkiy amesema: 6 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 313. 7 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 313. 12

Page 12


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ametusimulia Bashru bin Mahran amesema: Ametusimulia Muhammad bin Dinar kutoka kwa Daud bin Abi Hindi kutoka kwa as-Sha’biy kutoka kwa Jabir amesema: “Aqib na Tayib walimwendea Mtume (s.a.w.w.) naye akawaomba wafanye maapizano ya kuombeana laana, ndipo wakamwahidi kwamba maapizano hayo yafanyike kesho yake. Mtume akatoka siku iliyofuata akiwa na Ali, Fatima, Hasan na Husein, kisha akawatumia ujumbe waje kwenye maapizano, wakakataa lakini wakakubali kutoa kodi. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Lau wangekataa (kulipa kodi ya Jizya) basi bonde lao lingewaka moto toka mbinguni.” Jabir amesema: Na “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu….” iliteremka kwa ajili yao. Jabir amesema: “…na nafsi zetu na nafsi zenu…” ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ali. “…watoto wetu…” ni Hasan na Husein. Na “…. wanawake zetu….” ni Fatima. Na hivyo ndivyo alivyoipokea al-Hakim kwa maana hiyo katika kitabu chake al-Mustadrak kutoka kwa Ali bin Isa kutoka kwa Ahmad bin Muhammad al-Azhariy, kutoka kwa Ali bin Hajar kutoka kwa Ali bin Mus’har kutoka kwa Daud bin Abi Hindi. Kisha akasema: “Ni Hadithi sahihi kwa mujibu wa sharti za Muslim ijapokuwa hajaiandika.8

SURAT NISAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! msikaribie Sala hali ya kuwa mmelewa mpaka myajue mnayoyasema, wala mkiwa na janaba isipokuwa mmo safarini, mpaka muoge.” (Sura Nisai: 43). 8 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 319 13

Page 13


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Imepokewa kutoka kwa Ibnu Mas’ud kwamba baadhi ya Maansari milango yao ilikuwa ikitokea msikitini, hivyo baadhi ya nyakati walikuwa wakipatwa na janaba na hali hawana maji na hivyo watokapo kutafuta maji huwa hawana njia ila msikitini, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “…wala mkiwa na janaba isipokuwa mmo safarini.” Ama ile aliyoipokea Abu Isa Tirmidhi ambayo ni Hadithi ya Salim bin Abi Hafsa kutoka kwa Atiya kutoka kwa Abu Said al-Khudriy ni kwamba amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali! Haruhusiwi yeyote asiyekuwa mimi na wewe kupatwa na janaba ndani ya msikiti huu.” Ibnu Kathir amesema: “Yenyewe ni Hadithi dhaifu.”9

SURAT AL-MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini! Tekelezeni wajibu...” (Surat al-Maida: 1). Kutoka kwa Zayd bin Ismail as-Saighu al-Baghdadiy amesema: “Ametusimulia Muawiya, yaani Ibnu Hisham, kutoka kwa Isa bin Rashid kutoka kwa Ali bin Budhayma kutoka kwa Akrima kutoka kwa Ibnu Abbas, amesema: “Katika Qur’ani hakuna Aya yenye ibara ‘Enyi mlioamini!’ isipokuwa Ali ndiye kinara wake na kiongozi wake. Na hakuna Sahaba yeyote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ila alifokewa na Qur’ani ila Ali bin Abu ??lib, yeye hakufokewa kwa sehemu yoyote ya Qur’ani.10 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na 9 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 1, Uk. 430 na Uk. 431. 10 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2, Uk. 4, Chapa ya Beirut ya D?rul-Ma’rifa ya Mwaka 1412 A.H. 14

Page 14


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu..” (Surat Maida: 3). Imesemekana kwamba ilimteremkia Mtume wa Mwenyezi Mungu alipokuwa safarini kurudi toka Hija yake ya mwisho. Kisha imepokewa kwa njia nyingine na Abu Jafar Razi kutoka kwa Rabiu kutoka kwa Anas. Na pia ameipokea Ibnu Mardawayhi kwa njia ya Abu Harun al-Abdiy kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba ilimtremkia Mtume wa Mwenyezi Mungu Siku ya Ghadir Khum pale alipomwambia Ali: “Yule ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi Ali ana mamlaka juu yake.” Kisha ameipokea kutoka kwa Abu Huraira na katika maelezo yake ni kwamba ilikuwa ni siku ya kumi na nane ya Mfunguo tatu, yaani alipokuwa akirejea kutoka Hija yake ya mwisho.11 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui…..” (Surat al-Maida: 55). Ametusimulia Abu Said al-Ashji amesema: “Ametusimulia al-Fadhlu bin Dakin Abu Naim al-Ahwal amesema: ‘Ametusimulia Musa bin Qaysi alHadhramiy kutoka kwa Salma bin Kahil amesema: Ali alitoa sadaka pete yake na hali akiwa amerukuu ndipo ikateremka: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na…..” Ibnu Jariri amesema: al-Harith amenisimulia amesema: “Abdul-Aziz ametusimulia amesema: Ametusimulia Ghalib bin Ubaydullah amesema: 11 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2, Uk. 15. 15

Page 15


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Nilimsikia Mujahid akisema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake..” kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib alipotoa sadaka na hali akiwa amerukuu. Na Abdurazzaq amesema: Alitusimulia Abdul-Wahab bin Mujahid kutoka kwa baba yake kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake..” kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Ibnu Mardawayhi amepokea kwa njia ya Sufyan Thawri kutoka kwa Abu Sinan kutoka kwa Dhahak kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Ali alikuwa katika Sala ndipo muombaji akapita na hali akiwa katika rukuu akampa pete yake, ndipo ikateremka: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake…..” Kutoka kwa Abi Salih kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda msikitini akawakuta watu wakisali, baadhi wapo katika rukuu na wengine katika sijda, wangine katika kisimamo na baadhi wameketi, na ghafla akamwona masikini akiomba, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akamuuliza: “Je kuna yeyote amekupa kitu?” Akasema: “Ndio.” Akamuuliza ni nani? Akasema ni yule aliyesimama. Mtume akamuuliza: “Alikupa akiwa katika hali gani? “ Akasema: “Akiwa amerukuu.” Mtume akasema: “Yule ni Ali bin Abu Talib.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoa takbira huku akisema: “Na anayemtawalisha Mwenyezi Mungu, Mtume wake na wale walioamini, basi ajue hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lishindalo.” Ibnu Kathir amesema: “Njia hii ya upokezi haikutwi na dosari.”12

12 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 74. 16

Page 16


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-AN’AAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Surat An’aam:84 - 85). Ibnu Abi Hatim amesema: “Ametusimulia ibnu Yahya al-Askari amesema: Ametusimulia Abdur-Rahman bin Salih amesema: Ametusimulia Ali bin ‘?bis kutoka kwa Abdullah bin Atau al-Makkiy, kutoka kwa Abi Harbi bin Abil-As’wad amesema: Hajjaj alituma ujumbe kwa Yahya bin Ya’mur akasema: “Imenifikia habari kwamba wewe unadai kuwa Hasan na Husein ni kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kwa ushahidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nami nimekisoma kuanzia mwanzo hadi mwisho na wala sijaupata.” Akasema: Hujasoma Sura al-An’am: “Na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.”? Akasema: “Nimesoma.” Yahya akasema: “Basi Isa si kutoka

17

Page 17


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 kizazi cha Ibrahim na hali hana baba.” Akasema: “Umesema kweli.”13

Na wengine wamesema: “Watoto wa binti wanaingia katika kizazi cha mtu kutokana na riwaya iliyopo katika Sahih Bukhari kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwambia Hasan bin Ali (a.s.): “Hakika mwanangu huyu ni Sayyidi…”14

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe…” (Sura al-An’fal: 30). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Makuraishi walishauriana usiku mmoja huko Makka, baadhi yao wakasema: Akiamka mfungeni kwa kizuizi. Wakimkusudia Mtume (s.a.w.w.). Na wengine wakasema: Muuweni huku wengine wakisema: Mfukuzeni. Ndipo Mwenyezi Mungu akamjuza Nabii wake mkakati huo. Ali bin Abu Talib akalala usiku huo juu ya kitanda cha Mtukufu Mtume na Mtume akatoka mpaka pangoni, mushrikina wakakesha wakimlinda Ali wakidhani ndiye Mtume (s.a.w.w.), walipofika asubuhi walimvamia na walimuona kuwa ni Ali, Mwenyezi Mungu alizuia njama yao.15 13 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 160. 14 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 160. 15 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 316. 18

Page 18


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Imam Ahmad amesema: “Ametusimulia Affan amesema: Ametusimulia Hamad kutoka kwa Sammak kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma pamoja na Abu Bakr kuibalighisha Sura Baraa, walipofika Dhulhalifa akasema (s.a.w.w.): “Hapasi kuibalighisha ila mimi au mtu atokanaye na Ahlul-Baiti wangu.” Ndipo akamtuma Ali bin Abu Talibi akaibalighishe. Ameipokea pia Tirmidhi katika tafsiri yake.16 Abdullah bin Ahmad bin Hanbal amesema: “Ametusimulia Muhammad bin Sulayman amesema: Ametusimulia Muhammad bin Jabir kutoka kwa Sammak kutoka kwa Hasan kutoka kwa Ali (a.s.) amesema: Zilipoteremka kwa Mtume Aya kumi za mwanzo wa Sura Baraa Mtume (s.a.w.w.) alimwita Abu Bakr na kumkabidhi ili akawasomee wakazi wa Makka. Kisha akaniita na kusema: “Mdiriki Abu Bakr na popote utakapomkuta chukua Sura kutoka kwake na uende kuwasomea wewe wakazi wa Makka. Nikamkuta Juhfa na nikachukua Sura kutoka kwake. Abu Bakr akarejea kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Ewe Mtume wa Mweenyezi Mungu! Kuna chochote kimeteremka kunikhusu?” Akasema: “Hapana lakini Jibril amenijia na kuniambia: Hapasi kufikisha kwa niaba yako ila wewe mwenyewe au mtu kutokana na wewe.” 16 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 346. 19

Page 19


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kutoka kwa Abu Is’haqa kutoka kwa Zayd bin Yathighu amesema: “Baraa ilipoteremka Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr kisha baadae akamtuma Ali akaichukua. Abu Bakr aliporejea alisema: “Je kuna chochote kimeteremka kunihusu?” Akasema: “Hapana lakini nimeamrishwa niibalighishe mimi mwenyewe au mtu kutoka katika Ahlul-Baiti wangu.” (Ali) Akaenda Makka na kuwatangazia watu wake mambo manne: Baada ya mwaka huu mushriku haruhusiwi kuingia Makka, wala haruhusiwi kutufu akiwa uchi, wala hatoingia peponi ila mwislamu, na yule ambaye baina yake na Mtume wa Mwenyezi Mungu kuna mkataba basi mkataba huo utaendelea mpaka mwisho wa muda wake.17 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Abdu Razzaq amesema: “Ibnu Uyayna alitupa habari kutoka kwa Ismail kutoka kwa as-Sha’biy amesema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali na Abbas.”

Ibnu Jariri amesema: “Talha bin Shayba toka kizazi cha Abdudar, Abbas bin Abdul-Muttalib na Ali bin Abu Talib kila mmoja alijigamba. 17 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 346. 20

Page 20


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Talha akasema: ‘Mimi ndio mtunza Nyumba funguo zimo mikononi mwangu na hata nikitaka nalala humo.’ Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mgawa maji na msimamizi wake na hata nikitaka nalala msikitini.’ Ali akasema: ‘Sijui mtasema nini. Bila shaka nimeswali miezi sita kabla ya mtu yeyote na mimi ndiye mwanajihadi.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu….” Na hivyo ndivyo alivyoipokea as-Saddiy.18

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wakasema: Unastaajabu amri ya Mwenyezi Mungu? Rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka zake iko juu yenu enyi watu wa nyumba hii. Hakika Yeye ndiye Mhimidiwa Mtukuzwa.” (Sura Hud: 73). Amesema: “Imethibiti ndani ya Sahih mbili kwamba walisema: Tumeshajua namana ya kukusalimia basi ni vipi tutakavyokusalia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema:Semeni: “Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa).”19 18 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 355. 19 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 468. 21

Page 21


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT IBRAHIM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru na wakawafikisha watu wao katika nyumba ya maangamizo.” (Surat Ibrahim: 28). Ibnu Abi Hatim amesema: “Alitusimulia baba yangu alisema: Ametusimulia Ibnu Nufayli alisema: Nilisoma mbele ya Ma’qal kutoka kwa Ibnu Abi Husein kwamba: Ali bin Abu Talib alisimama na kusema: “Oh, yeyote aniulize kuhusu Qur’ani, na wallahi lau ningemjua leo yeyote aijuaye kuliko mimi hata kama yupo ng’ambo ya bahari basi ningemfuata.” Abdullah bin al-Kawau akasimama na kusema: “Ni akina nani wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru na wakawafikisha watu wao katika nyumba ya maangamizo?” Akasema: “Ni mushrikina toka kwa makuraishi, walijiwa na neema ya Mwenyezi Mungu ambayo ni Imani wakaibadili neema ya Mwenyezi Mungu kwa ukafiri na ndipo wakawafikisha watu wao katika nyumba ya maangamizo.”20

SURAT AN-NAHLI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na hatukutuma kabla yako ila wanaume tuliowapa wahyi. Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Surat an-Nahli: 43). 20 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 558 22

Page 22


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Abu Jafar al-Baqir (a.s.) alisema: “Sisi ndio wenye ukumbusho.”21 Ibnu Kathir amesema: “Ulamaa wa nyumba tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndio maulamaa bora kwani wao ndio waliokuwa katika Sunna ipasavyo, kama vile Ali, Ibnu Abbas, watoto wa Ali Hasan na Husein, Muhammad bin al-Hanafiyya, Ali bin Husein Zaynul-Abidin, Ali bin Abdullah bin Abbas, Abu Jafar al-Baqir ambaye ni Muhammad bin Ali bin Husein, na Mwanae Ja’far na mfano wao miongoni mwa wale wenye kushikamana vilivyo na kamba imara ya Mwenyezi Mungu na njia Yake nyoofu…..”22

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” (Sura Israi: 26). Al-Hafidh Abu Bakr al-Bazzar amesema: Ametusimulia Ibad bin Ya’kub amesema: Ametusimulia Abu Yahya at-Tamimiy amesema: Ametusimulia Fudhaylu bin Marzuq kutoka kwa Atiya kutoka kwa Abu Said amesema: Ilipoteremka: “Na mpe jamaa wa karibu haki…..” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Fatima na kumpa Fadak.23 Ibnu Kathir amesema: Na rai ya karibu zaidi ni kwamba yenyewe ni miongoni mwa uzushi wa marafidhi. Na Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye.24 21 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 591 na 592. 22 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 591 na 592. 23 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2, Uk. 34. 24 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2, Uk. 34. – Sielewi mpaka sasa ni kwa nini Ibnu Kathir umajununi wake unapanda pale anapoiona fadhila na heshima ya AhlulBaiti, na daima anajaribu kuidhoofisha ile iliyo mashuhuri, bila shaka si chochote bali ni uadui wake kwa Ahlul-Baiti (a.s.). Kisha riwaya hiyo wafasiri wakubwa wameitaja kabla yetu kama vile al-Haskaniy katika kitabu chake ShawahidutTanziil. 23

Page 23


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT MUUMINUNA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi litakapopulizwa parapanda, hapo hautakuwapo ujamaa baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.” (Sura Muuminuna: 101). Imam Ahmad amesema: “Ametusimulia Abu Sa’id huria wa Bani Hashim amesema: Ametusimulia Abdullah bin Ja’far amesema: ‘Ametusimulia Ummu Bakri binti ya al-Musawwar bin Makhrimah kutoka kwa Abdullah bin Abi R?fi’u kutoka kwa al-Musawwar amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ni pande la nyama yangu hunisononesha yale yanayomsononesha, na hunifurahisha yale yanayomfurahisha. Na hakika kila nasaba itakatika Siku ya Kiyama ila nasaba yangu na sababu yangu na ukwe wangu.” Hadithi hii ina asili katika Sahih mbili (Muslim na Bukhari) kutoka kwa alMusawwar kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ni pande la nyama yangu, hunikarahisha lile linalomkarahisha na huniudhi lile linalomuudhi.”25

25 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 3 Uk. 222. 24

Page 24


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT SHUA’RAU Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na uwaonye jamaa zako wa karibu.” (Sura Shu’arau: 214). Kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.), amesema: “Ilipoteremka Aya hii kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Na uwaonye jamaa zako wa karibu,” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Nikatambua kwamba nitakapowadhihirishia jamaa zangu jambo hili nitakumbana na nisiyoyapenda toka kwao. Nikanyamaza mpaka aliponiijia Jibril na kuniambia: ‘Ewe Muhammad! Hakika usipofanya unayoamrishwa Mola wako Mlezi atakuadhibu. Ewe Ali! Tuandalie pishi la chakula uweke mguu wa mbuzi na utujazie bilauri ya maziwa, kisha nikusanyie watoto wa Abdul-Mu??alib.’ Nikatekeleza, wakakusanyika kwake na wakati huo walikuwa wanaume arobaini, amezidi mtu mmoja au amepungua mmoja, humo walikuwemo ami zake: Abu Talib, Hamza, Abbas na Abu Lahabi kafiri khabithi. Nikawapelekea sinia la chakula, na ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akachukua kipande kidogo cha nyama akakikata kwa meno yake kisha akakitupia pembezoni mwa sinia, akasema: ‘Kuleni kwa Jina la Mwenyezi Mungu.’ Kaumu wakala mpaka wakatosheka na wala sikuona ila sehemu ambazo mikono yao ilikuwa ikimega. Wallahi, chakula nilichowapa wote ni cha kuweza kula mtu mmoja. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: ‘Wape watu kinywaji ewe Ali.’ Nikaja na ile bilauri wakanywa mpaka wakatosheka wote. Wallahi, kilikuwa ni kinywaji cha kutosheka mtu mmoja. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipotaka kuwaeleza Abu Lahabi alimtangulia kuongea, akasema: ‘Jamaa yenu amewaroga kwa karamu hii.’ Ndipo kaumu wakatawanyika na wala Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) hakufanikiwa kuwaeleza. Ilipowadia siku iliyofuata Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘Ewe Ali! tuandalie chakula na kiny25

Page 25


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 waji mfano wa kile ulichoandaa jana…..’ Nikatekeleza kisha nikawakusanya, naye Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akafanya kama alivyofanya jana, wakala mpaka wakatosheka, nikawaletea bilauri wakanywa mpaka wote wakatosheka. Wallahi, chakula na kinywaji nilichowapa wote ni cha kuweza kutosheka mtu mmoja. Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akaongea kwa kusema: ‘Enyi wana wa Abdul-Mu??alib! Hakika mimi wallahi simjui kijana wa kiarabu aliyewaletea jamaa zake kitu bora kuliko hiki nilichowaletea. Hakika mimi nimewaletea kheri ya dunia na akhera. Na hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru niwalinganie kwayo, basi ni nani kati yenu atanisaidia katika jambo hili, awe ndugu yangu na kadha wa kadha.’ Watu wote wakakaa kimya, nikasema na hali mimi nikiwa ndiye mdogo kiumri kuliko wote, mwenye tongotongo machoni (mtoto) kuliko wote, mwenye tumbo kubwa kuliko wote na mwenye muundi wenye majeraha madogo kuliko wote: ‘Mimi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nakuwa waziri wako.’ Akaishika shingo yangu kisha akasema (s.a.w.w.): ‘Hakika huyu ni ndugu yangu na kadha wa kadha, msikilizeni na mumtii.’ Kaumu wakaongea na hali wakicheka na wakimwambia Abu Taalib: ‘Bila shaka amekuamuru umsikilize na kumtii mwanao.’”26 26 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2, Uk. 302. Ibnu Kathir anaielezea habari hii kwa kusema: “Kaipokea kwa mtiririko huu Abdul-Ghaffar bin al-Qasim bin Abi Mariam pekee, naye ni muongo asiyefuatwa na ni Shia.” Maneno kama haya kutoka kwa Ibnu Kathir ni ya ajabu, na inashangaza kuona anajiita aalimu na hali yeye hajui bali anaharakia kuwahukumu wenzake. Hajui kwamba al-Hafidh al-Kunjiy as-Shafi’iyyu aliyefariki mwaka 658 A.H. ametaja tukio hili kwa njia mbili katika kitabu chake Kifayatut-Talib Uk. 304 mlango wa 51, na katika njia zote mbili hajataja jina la Abdul-Ghaffar bin al-Qasim bin Abi Layla, hii ni mosi. Pili: Tukio hili ni mashuhuri bali ni mutawatiri kwani limetajwa na wasimulizi wakubwa na wanahistoria wakubwa, miongoni mwao ni: Tabari katika kitabu chake cha historia Juz. 2, Uk. 62, al-Muttaqiy al-Hindiy katika kitabu Kanzul-Ummal Juz. 6, Uk. 392 na 397, Ahmad bin Hanbal katika al-Musnad Juz. 1, Uk. 195, al-Haythamiy katika Majmauz-Zawaid Juz. 8, Uk. 302, Tabari katika ar-Riyadhun-Nadhrah Juz. 2, Uk. 167, na wengineo. 26

Page 26


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na kama hamuwajui baba zao, basi ni ndugu zenu katika dini.” (Sura Ahzab: 5). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): “Wewe watokana na mimi na mimi natokana na wewe.”27 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na akawarithisheni nchi yao na majumba yao na mali zao, na nchi msiyoikanyaga, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo juu ya kila kitu.” (Surat Ahzab: 27). Amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwacha Ibnu Ummu Maktum Madina na akamkabidhi bendera Ali bin Abu Talib (a.s.).28 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33). 27 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 399. 28 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 408. 27

Page 27


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kutoka kwa Anas bin Malik amesema kwamba: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akipitia nyumbani kwa Ali muda wa miezi sita kila alipotoka kwenda kusali Sala ya alfajri, na alikuwa akisema: ‘Swala enyi Ahlul-Baiti. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’” Ameipokea Tirmidhi kutoka kwa Abdu bin Hamid kutoka kwa Affan, amesema: “Ni nzuri Gharib.”29 Ibnu Jarir amesema: “Ametusimulia Waki’u kutoka kwa Abu Is’haqa, amesema: Abu Daud amenipa habari kutoka kwa Abul-Hamrau, amesema: “Niliishi Madina miezi sita bila kutoka zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nilimwona Mtume kila ichomozapo alfajiri akienda kwenye mlango wa Ali na Fatima (a.s.) na kusema: ‘Sala Sala, Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”’30 Al-Awza’i amesema: “Ametusimulia Shaddad Abu Ammar amesema: “Niliingia kwa Wathila bin al-Asqau nikamkuta ameketi na baadhi ya watu, ndipo walipomtaja Ali na kumkashifu, nami nikamkashifu pamoja nao, walipoondoka akasema (Wathila): ‘Hivi kweli umethubutu kumkashifu huyu?’ Nikasema wamemkashifu ndipo nami nikamkashifu pamoja nao. Akasema: ‘Nikupe habari za yale niliyoyaona toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu?’ Nikasema ndio. Akasema: Nilikwenda kwa Fatima (a.s.) kumuulizia Ali (a.s.). Fatima akanijibu kwamba ameelekea kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), nikakaa namngojea mpaka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipokuja akiwa pamoja na Ali, Fatima, Hasan na Husain (a.s.) amemshika kila mmoja wao mkono, akaingia kisha akawasogeza Ali na Fatima na kuwakalisha mbele yake, na akamkalisha Hasan na Husein kila mmoja juu ya paja lake, kisha akawafunika nguo yake na kusoma Aya hii: “Hakika si mengineyo 29 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 413. 30 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 413. 28

Page 28


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Na akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio watu wa nyumba yangu, na watu wa nyumba yangu ndio wenye haki zaidi (kuliko mtu baki).’”31 Imam Ahmad amesema: Imepokewa kutoka kwa Ummu Salama kwamba alikuwa akitaja kuwa Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwake ndipo akaja Fatima akiwa na chungu chenye uji na kuingia nacho kwa Mtume. Mtume akamwambia mwite mumeo na wanao. Alikuja Ali, Hasan na Husein wakaingia kwa Mtume na wakaketi wakinywa uji huo na hali Mtume akiwa juu ya kitanda chake kilichotandikwa kishamia cha Khaibari. Nikiwa chumba kingine nasali ghafla Mwenyezi Mungu aliteremsha Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Mtume (s.a.w.w.) akashika pande za kishamia akawafunika, kisha akatoa mkono wake akauelekeza mbinguni kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu hawa ndio Ahlul-Baiti wangu na watu makhsusi kwangu. Waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’ Nikaingiza kichwa chumbani kwa Mtume na kumwambia: Je na mimi ni pamoja nanyi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: ‘Hakika wewe upo katika kheri. Bila shaka wewe upo katika kheri. ‘“32 Ibnu Jarir amesema: Imepokewa kutoka kwa A’mash kutoka kwa Hakim bin Sa’d amesema: Tulimtaja Ali bin Abu Talib (a.s.) mbele ya Ummu Salama, akasema: “Ndani ya nyumba yangu ndimo ilimoteremka: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” “Ummu Salama akasema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja nyumbani kwangu, akaniambia usimpe yeyote idhini ya kuingia. Akaja 31 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 413. 32 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 414. 29

Page 29


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Fatima sikuweza kumzuia na baba yake, kisha akaja Hasan sikuweza kumzuia asiingie kwa babu yake na mama yake. Akaja Husein sikuweza kumzuia asiingie kwa babu yake na mama yake. Kisha akaja Ali (a.s.) sikuweza naye kumzuia, walipokusanyika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawafunika kwa kishamia alichokuwa amejitanda, kisha akasema: ‘Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu. Waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.’ Ndipo ikateremka Aya hii walipokusanyika juu ya busati. Nikasema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Na mimi? Ummu Salama anasema: Wallahi hakukubali bali alisema: Hakika wewe utaelekea katika kheri.”33 Ibnu Jarir amesema: Ametusimulia Abu Karib kutoka kwa Abdullah bin Wahab bin Zam’at, amesema: Ummu Salama alinipa habari kwamba: “Hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwakusanya Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.) kisha akawafunika nguo yake, kisha akaelekea kwa Mwenyezi Mungu na kusema: ‘Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu.’ Ummu Salama akasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! (Allah) Amenijumuisha pamoja nao?’ akasema (s.a.w.w.): ‘Wewe ni miongini mwa wake zangu.”34 Imepokewa kutoka kwa Ummu Salama amesema: Siku moja Mtume akiwa nyumbani kwangu nilimwambia mfanyakazi: “Hakika Ali na Fatima wako mlangoni.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akaniambia: “Simama na wapishe Ahlul-Baiti wangu.” “Nikaketi kando kidogo pembezoni mwa nyumba.” Wakaingia Ali na Fatima wakiwa na Hasan na Husein (a.s.) wakiwa bado watoto wadogo, akawachukua watoto na kuwaweka mapajani mwake na akawabusu, akamshika Ali kwa mkono wake mmoja na Fatima kwa mkono wake mwingine, akambusu Fatima na kisha Ali, akawafunika shuka jeusi na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu tulete Kwako na si motoni, mimi na Ahlul-Baiti wangu.”35 33 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 414. 34 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 414. 35 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 414. 30

Page 30


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kutoka kwa Ibnu Abi Hatim kutoka kwa al-Awamu bin Hawshab, kutoka kwa ami yake amesema: Niliingia na baba yangu kwa Aisha, nikamuuliza kuhusu Ali (a.s.). Aisha akasema: “Umeniuliza kuhusu mtu aliyekuwa akipendwa sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuliko watu wote, na alikuwa mume wa binti yake aliyekuwa akipendwa sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu. Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akiwa amewaita Ali, Fatima, Hasan na Husein, akawafunika nguo na kisha akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, hivyo waondolee uchafu na uwatakase kabisa.’ Nikasogea na kusema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Je mimi ni miongoni mwa AhlulBaiti wako? Akasema: ‘Kaa pembeni, hakika wewe upo katika kheri.’”36 Ibnu Jarir amesema: Imepokewa kutoka kwa Atiyyah kutoka kwa Said amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Aya hii “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” iliteremka kwa ajili ya watu watano: Mimi, Ali, Fatima, Hasan na Husein.”37 Ametusimulia Bakir bin Mismar amesema: Nilimsikia Amir bin Sa’d akisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema pindi wahyi ulipomshukia, akamchukua Ali na wanae wawili na Fatima, akawafunika nguo yake kisha akasema: “Ewe Mola Mlezi! hawa ndio ndugu zangu na Ahlul-Baiti wangu.”38 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). Bukhari katika kutafsiri Aya hii amesema: Imepokewa kutoka kwa Ka’ab bin Ájrah amesema: Palisemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! 36 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 414. 37 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 415. 38 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 415 31

Page 31


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kukutolea salamu tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowarehemu aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’”39 Imam Ahmad amesema: Imepokewa kutoka kwa al-Hakam amesema: “Nilimsikia Ibnu Abi Layla akisema: Kaab bin Ajrah alikutana na mimi na kuniambia: Je nikupe zawadi? Siku moja alikuja Mtume wa Mwenyezi Mungu, nasi tukamuuliza, tukasema: Kukutolea salamu tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??? ???? ???? ????. ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowarehemu aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’”40

39 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 432. 40Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 432. 32

Page 32


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Bukhari amesema: “Ametusimulia Abdullah bin Yunus kutoka kwa Abu Said al-Khudriy amesema: Tulimwambia ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu basi ni ipi namana ya kukusalia? Akasema: “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?????? ??? ????? ??? ?? ???????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad mja Wako na Mtume Wako kama ulivyowarehemu aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’”41 Abdurahman bin Abu Layla, amesema: Kutoka kwa Ka’ab bin Ajrah, amesema: Ilipoteremka: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” Tulisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu ni ipi namana ya kukusalia? Mtume akasema: ‘’Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’’’42 41Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 432. 42 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 433. 33

Page 33


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kutoka kwa Ibnu Mas’ud al-Ansariy alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alikwenda na kutukuta tumeketi katika baraza la Sa’d bin Ubada. Bushru bin Sa’d akamwambia: Mwenyezi Mungu ametuamuru tukutolee salamu ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, basi ni vipi tutakavyokusalia? Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akakaa kimya mpaka tukatamani kwamba asingemuuliza. Kisha akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ???????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ?? ???????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowarehemu aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim katika walimwengu, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’’’ Pia ameipokea Abu Daud, Tirmidhi, Nasai na Ibnu Jariri kutoka katika hadithi ya Malik. Tirmidhi amesema: Ni nzuri na sahihi.43

SURAT YASIN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ikasemwa: Ingia peponi! Akasema: Laiti watu wangu wangejua. Jinsi Mola wangu alivyonighufuria na akanifanya katika waheshimiwa.” (Sura Yasin: 26 - 27). Al-Hafidh Abu Qasim Tabaraniy amepokea kwamba: “Alitusimulia Husein bin Is’haq at-Tusturiy kutoka kwa Ibnu Abi Najihi kutoka kwa Mujahid kutoka kwa Ibnu Abbas (a.s.) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Vinara ni watatu: Kinara kuelekea kwa Musa (a.s.) ni Yoshua bin Nun. Kinara kuelekea kwa Isa (a.s.) ni yule aliyezungumziwa na Sura Yasin, na kinara kuelekea kwa Muhammad (s.a.w.w.) ni Ali bin Abu Talib (a.s.).” 43 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 433. 34

Page 34


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Hakika yenyewe ni Hadithi isiyokubalika haijulikani ila kwa njia ya Husein al-As’haq naye ni Shia asiyefuatwa.44

SURAT AS-SSAFFAT Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amani kwa Ilyasin.” (Sura as-Saffat: 130).Ibnu Mas’ud amesema: Yaani Aali Muhammad (s.a.w.w.).45

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Kutoka kwa as-Sadiy, kutoka kwa Abu Daylam, amesema: “Alipoletwa Ali bin Husein na hali ni mateka na kusimamishwa katika barabara kuu ya Damascus alisimama mzee mmoja kati ya watu wa Sham, akasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amewauwa na kuwang’oeni na kung’oa mzizi wa fitina.” Ali bin Husein akasema: ‘Umewahi kusoma Qur’ani?’ akajibu ndio. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma Aali Haa Miim?’ Akajibu nimewahi kusoma Qur’ani na sijawahi kusoma Aali Haa Miim. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...”’ Mzee akasema: ‘Nyinyi ndio hao?’ Akasema (a.s.): ‘Naam ndio sisi.’46 Ibnu Abi Hatim amesema: Ametusimulia Ali bin Husein amesema: “Ametusimulia mtu aliyemtaja jina: Ametusimulia Husein al-Ashqar kutoka kwa Qaysi kutoka kwa al-A’mash, kutoka kwa Said bin Jubair, kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Ilipoteremka: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” walimuuliza: Ewe 44 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 2 Uk. 486. 45 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 21. 46 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 101. 35

Page 35


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni akina nani hawa ndugu ambao Mwenyezi Mungu ameamuru kuwapenda? Akasema: “ Fatima na kizazi chake.”47 Imepokewa kutoka kwa Zayd bin Arqam amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi ni mwenye kuwaachia kati yenu kile ambacho lau mkishikamana nacho katu hamtapotea baada yangu, kimojawapo ni kitukufu kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka toka mbinguni hadi aridhini. Na kingine ni kizazi changu watu wa nyumba yangu, na havitoachana mpaka vinikute kwenye hodhi, basi angalieni ni jinsi gani mtakavyobaki navyo.”48 Kutoka kwa Jabir bin Abdillah amesema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu Siku ya Arafa akiwa juu ya ngamia wake al-Qas’wau akiwahutubia watu, nikamsikia akisema: “Enyi watu! Hakika mimi nimeacha kati yenu kile ambacho lau mkishikamana nacho hamtapotea: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu.”49 Kutoka kwa Abu Dhari al-Ghaffariy alisema huku akiwa ameshikilia mlango: Enyi watu! Anayenitambua basi ameshanitambua na asiyenitambua basi mimi ni Abu Dhari, nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Hakika mfano wa Ahlul-Baiti wangu kwenu nyinyi ni sawa na safina ya Nuh (a.s.) aliyeipanda aliokoka.”50 47 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 102. 48 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 102. 49 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 102. 50 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4, Uk. 102. Lakushangaza sana ni kwamba Ibnu Kathir anaizingatia Hadithi mashuhuri kama hii kuwa ni dhaifu. Sijui amesahau au amejisahaulisha Hadithi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ardhi haijapata kumbeba wala mbingu haijapata kumfunika mtu mkweli kuliko Abu Dhari al-Ghaffariy.” 36

Page 36


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURA AD-DUKHAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Mbingu na ardhi hazikuwalilia; wala hawakupewa muda.” (Sura ad-Dukhan: 29). Ibnu Abi Hatim amesema: “Ametusimulia Ali bin Husein amesema: Ametusimulia Abdusalami bin Asim, amesema: Ametusimulia Ishaq bin Ismail, amesema: Ametusimulia al-Mustawridu bin Sabiq kutoka kwa Ubaydul-Maktabi kutoka kwa Ibrahim, amesema: “Dunia haijamlilia yeyote tangu kuumbwa kwake ila wawili.” Nikamwambia vipi? Akasema: “Inapatwa na wekundu na kuwa kama ua waridi. Hakika Yahya bin Zakariya alipouawa mbingu ilipatwa na wekundu na ikadondosha mvua ya damu. Na hakika Husein bin Ali (a.s.) alipouwawa mbingu ilipatwa na wekundu.”51 Ametusimulia Jarir kutoka kwa Yazid bin Abi Ziyad amesema: “Alipouwawa Husein bin Ali (a.s.) pande zote za mbingu zilipatwa na wekundu muda wa miezi minne. Na wekundu wake ndio kulia kwake.”52 Na wametaja katika habari za mauaji ya Husein (a.s.) kwamba siku hiyo hakuna jiwe lililoinuliwa au kugeuzwa ila chini yake kulikutwa damu nzito, na kwamba jua lilipatwa, mbingu ikawa nyekundu na ikanyesha mvua ya mawe.53 51 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 127. 52 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 127. 53 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 127. Ibnu Kathir katika habari hii anasema: “Dhahiri ni kwamba habari hii ni miongoni mwa uzushi wa mashia na uongo wao ili wakuze jambo….”. Nashangaa ni wepesi ulioje ulionao katika kuwatuhumu wengine? Na hilo tunakujibu nawe ndio wapasa zaidi kuwa muongo, kwa sababu si sisi pekee tuliopokea hadithi hii, hiyo ni mosi. Pili: Wewe mwenyewe katika tafsiri yako umepokea kwamba: Mbingu humlilia muumini siku arubaini. Je washakia Husein kuwa bwana wa waumini na kinara wao duniani na akhera baada ya babu yake, mama yake, baba yake na kaka yake? Tatu: Kwa nini wazikubali habari hizi zihusishwapo na Yahya bin Zakariya lakini si pale zinapomhusu Husein mtoto wa binti ya bwana wa Manabii na Mawasii? 37

Page 37


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-AHQAF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi watu wetu muitikieni Mwitaji wa Mwenyezi Mungu na muaminini, atakusameheni madhambi yenye kuumiza.” (Sura alAhqaf: 31). Imepokewa kutoka kwa Ibnu Mas’ud kwamba alisema: “Nilikuwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) usiku ndipo ukamfikia msafara wa majini, akavuta pumzi. Nikamwambia una nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ninajiomboleza mwenyewe ewe Ibnu Mas’ud.” Nikamwambia ainisha Khalifa. Akauliza nani? Nikamwambia Abu Bakr. Akakaa kimya, kisha ukapita muda kadhaa akavuta tena pumzi, nikamwambia kwa haki ya baba yangu na mama yangu, una nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ninajiomboleza mwenyewe ewe Ibnu Mas’ud.” Nikamwambia ainisha Khalifa. Akauliza nani? Nikamwambia Umar. Akakaa kimya muda kadhaa, kisha akavuta tena pumzi, nikamwambia una nini? Akasema: “Ninajiomboleza mwenyewe.” Nikamwambia ainisha Khalifa. Akauliza nani? Nikamwambia Ali bin Abu Talib. Akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi Mwake, lau wakimtii basi wote wataingia Peponi.”54

54 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 147. 38

Page 38


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Surat Mujadilah: 12). Imesemekana kwamba hakuna yeyote aliyeifanyia kazi Aya hii kabla ya hukumu yake kufutwa ila Ali bin Abu Talib (a.s.).55 Ibnu Abi Najihu amesema: Kutoka kwa Mujahidu, amesema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib, alitoa sadaka ya dinari kisha akasema siri na Mtume (s.a.w.w.) na alimuuliza mambo kumi, ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka.).”56 Kutoka kwa Mujahid amesema: Ali (a.s.) alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nilikuwa na dinari nikaibadili kwa dirhamu kumi, hivyo ikawa kila nina55 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 286. 56 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 286.

39

Page 39


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 posema siri na Mtume wa Mwenyezi Mungu natoa sadaka dirhamu moja, mpaka hukumu yake ikafutwa huku hakuna yeyote kabla yangu aliyeifanyia kazi na wala hakuna baada yangu atakayeifanyia kazi, nayo ni: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana…..””.57

SURA TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…..Basi Mwenyezi Mungu ni mlinzi wake, na Jibril na waumini wema na Malaika….” (Sura Tahrim: 4). Laythu bin Abi Salim amesema kutoka kwa Mujahid kwamba: ‘’Na waumini wema’’ ni Ali bin Abu Talib.58 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘’Na waumini wema’’ kuwa ni Ali bin Abu Talib.59

57 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 286. 58 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 340. 59 Tafsirul-Qur’an al-Adhim Juz. 4 Uk. 340. Mchakato toka katika tafsiri hii umetimia siku ya ishirini na tatu ya Mfunguo tatu Mwaka 1426 A.H. katika Jiji la Qum Takatifu. 40

Page 40


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA SUYUTI, INAYOITWA AD-DURUL-MANTHUR FIT-TAFSIRIL-MAATHUR SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na akamkubalia toba yake, hakika yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.” (Sura Al-Baqarah: 37). Ad-Daylami ameiandika katika Musnadul-Firdawsi kwa riwaya aliyoipokea kutoka kwa Ali, kwamba alisema: “Nilimuuliza Mtume (s.a.w.w.) kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Basi Adam akapokea maneno kwa Mola wake Mlezi, na akamkubalia toba yake.” Akasema (s.a.w.w.): ‘Hakika Mwenyezi Mungu alimshusha Adam huko India, Hawa huko Jiddah, Ibilisi huko Baysan, na nyoka huko Isfahani. Nyoka alikuwa na miguu kama ya ngamia, Adam akaishi huko India miaka mia moja huku akilia kwa kujutia kosa lake, mpaka Mwenyezi Mungu akampelekea Jibril na kumwambia: ‘Ewe Adam! Hivi sijakuumba kwa mkono wangu! Hivi sijakupulizia roho yangu! Hivi sikuwaamuru malaika wangu wakusujudie! Na hivi sijakuoza Hawa, kijakazi wangu!’ Akasema: ‘Ndio umenifanyia hayo.’ Akamwambia: ‘Basi ni kwa nini walia kiasi hiki?’ Akajibu: ‘Na ni kipi kitanizuia nisilie na hali nimetoka kwenye ujirani wa Rahman.’ Akamwambia: ‘Shikamana na maneno haya, hakika Mwenyezi Mungu ataipokea toba yako na kukughufiria dhambi yako.’ 41

Page 41


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Akasema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! hakika mimi nakuomba kwa haki ya Muhammad na aali Muhammad, Subhanaka hakuna Mungu apasaye kuabudiwa ila Wewe. Nimetenda uovu na nimeidhulumu nafsi yangu hivyo nighufirie hakika Wewe ni Ghafuru Rahimu. Ewe Mwenyezi Mungu! hakika mimi nakuomba kwa haki ya Muhammad na aali Muhammad, Subhanaka hakuna Mungu apasaye kuabudiwa ila Wewe. Nimetenda uovu na nimeidhulumu nafsi yangu hivyo nisamehe hakika Wewe ni Mwenye kupokea toba na ni Rahimu.’ Haya ndio maneno aliyoyapokea Adam (a.s.).”’60 Ibnu an-Najjar ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Nilimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kuhusu maneno ambayo aliyapokea Adam toka kwa Mola wake Mlezi na hatimaye akamkubalia toba yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Aliomba: Kwa haki ya Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein nikubalie toba yangu. Akamkubalia toba yake.”61 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Sura Al-Baqarah: 274). Abdurazzaq, Abdu bin Hamid, Ibnu Jarir, Ibnu al-Mundhir, Ibnu Abi Hatim, Tabarani na Ibnu Asakir wameandika kwa njia itokayo kwa AbdulWahab bin Mujahid kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Ibnu Abbas, ame60 Kwa maelezo zaidi rejea Tafsirul-Burhan Juz. 1 Uk. 86, Chapa ya Ismailiyyan. 61 Kwa uwazi kabisa inadhihiri kwamba Ahlul-Baiti ni Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s.) nao ndio Aali Muhammad na ndio waliokusudiwa katika Kisa cha Kishamia na katika Aya ya Utakaso. 42

Page 42


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 sema kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri..”: “Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib alikuwa na dirhamu nne, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri.”62

SURA AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu wote.” (Sura Aali Imran: 33). Ibnu Jarir, Ibnu al-Mundhir na Ibnu Abi Hatim wameandika kupitia njia ya Ali kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran” amesema: “Hao ni waumini kutoka katika aali Imran, aali Ibrahim, aali Yasin na aali Muhammadi (s.a.w.w.).”63 62 Rejea Shawahidut-Tanziil cha al-Haskaniy Juz. 1, Uk. 109, Chapa ya Beirut ya Kimataifa ya Mwaka 1974. Humo ameandika kutoka kwa al-Kalbiy kutoka kwa Abu Salih kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “”Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri..” kwamba aliteremka kwa ajili ya Ali pekee, katika kisa cha dirhamu zake nne alizozitoa sadaka, moja mchana nyingine usiku, nyingine kwa siri na nyingine kwa dhahiri. 63 Nasema: Aali Yasin ndio aali Muhammad (s.a.w.w.) kwa sababu Yasin ni moja ya majina ya Mtume (s.a.w.w.) kama alivyotamka wazi hilo Suyuti katika tafsiri hii Juz. 5, Uk. 258. Na al-Khazin ametaja hilo katika Juz. 4, Uk. 2 na Juz. 5, Uk. 286. Na limetajwa katika Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 118, Chapa ya Beirut. Kwa ziada rejea Tafsirul-’Ayyash Juz. 1, Uk. 191, Chapa ya Beirut ya mwaka 1991. 43

Page 43


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Sura Aali Imran: 37). Ameandika Abu Ya’la ameandika kutoka kwa Jabir kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikaa siku kadhaa bila kula chakula mpaka hali hiyo ikawa nzito juu yake. Akaenda kwenye nyumba za wakeze lakini hakupa kwa yeyote chochote, ndipo akaenda kwa Fatima na kumwambia: “Ewe mwanangu mpendwa! Je una chochote ninachoweza kula kwani hakika mimi ni mwenye njaa?” Akamjibu: “Wallahi sina.” Mtume alipotoka jirani wa Fatima alimletea Fatima vipande viwili vya mkate na finyango ya nyama, akavitwaa na kuviweka ndani ya bakuli lake, akasema: “Wallahi katika hiki nitampa kipaumbele Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kabla ya nafsi yangu na kabla ya yule aliyopo kwangu.” Japokuwa wote walikuwa wanahitajia chakula lakini Fatima alimtuma Hasan au Husein aende kumwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) naye alikwenda. Fatima akamwambia: “Kwa haki yako na ya mama yangu, Mwenyezi Mungu ameleta kitu nami nimekihifadhi kwa ajili yako.” Akamwambia: “Kilete ewe binti yangu mpendwa.” Akamletea bakuli na alipolifunua ghafla akakuta limejaa mikate na nyama, alipokitazama akapatwa na mshangao na akatambua kuwa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu. Akamhimidi Mwenyezi Mungu na akamkabidhi chakula hicho Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Mtume (s.a.w.w.) alipokiona alimhimidi Mwenyezi Mungu na akasema: “Umetoa wapi hivi ewe binti yangu mpendwa?” Akajibu: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ewe baba yangu mpendwa. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu. “ Mtume akamhimidi Mwenyezi Mungu na kusema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya ewe binti yangu mpendwa kifani 44

Page 44


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 wa Seyida wa wana wa Israel (Mariam). Kwani hakika yeye alikuwa aruzukiwapo chochote na Mwenyezi Mungu kisha akiulizwa kakipata wapi husema: Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.”64 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran: 42). Al-Hakima ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wanawake bora ulimwenguni ni: Khadija, Fatima, Maryam na Asia mke wa Firaun.” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘’Hakika Mwenyezi Mungu aliwateua wanne kwa ubora kuliko wanawake wote wa ulimwenguni: Asia binti Muzahim, Maryam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad (s.a.w.w.).” Ahmad, Tirmidhi, Ibnu al-Mundhir, Ibnu Habban na al-Hakim wameandika kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha toka katika wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid, Fatima binti Muhammad (s.a.w.w.) na Asia mke wa Firaun.” 64 Nasema: Hilo si zito kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, ikiwa Mariam ni mkweli wa Kizazi cha Israil na Fatima ni mkweli wa umma huu naye ni mbora wa wanawake wote wa ulimwengu. 45

Page 45


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Abi Shayba na Ibnu Jarir wameandika kutoka kwa Fatima (a.s.) kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliniambia: Wewe ndiye mbora kuliko wanawake wote wa peponi na si Mariam alBatul.” Ibnu Asakir ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wanawake bora wa peponi ni Maryam binti Imran, Fatima binti Muhammad (s.a.w.w.), Khadija binti Khuwaylid na Asia mke wa Firaun.” Ibnu Asakir ameandika kupitia njia ya Muqatil, kutoka kwa Dhahak kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Wanawake wanne ni wabora kuliko wanawake wote wa zama zao: Maryam binti Imran, Asia binti Muzahim, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad (s.a.w.w.) na yeye ndiye mbora wao kiulimwengu.”65 Ibnu Shayba ameandika kutoka kwa Abdurahman bin Abi Layla kwamba amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ndiye mbora wa wanawake wa ulimwenguni baada ya Maryam binti Imran, Asia mke wa Firaun na Khadija binti Khuwaylid.”66 65 Allama al-Muttaqiy al-Hindiy amepokea katika kitabu Kanzul-Ummal hadithi hii kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Ewe Fatima! Hivi hauridhii wewe kuwa ndiye mwanamke bora kuliko wanawake wote wa ulimwenguni na mbora kuliko wake wote wote wa waumini na mbora kuliko wanawake wote wa umma huu.” Tazama Kanzul-Ummal Juz. 12 Uk. 12, Namba 34232. 66 Allama al-Bahraniy amepokea katika al-Burhani Juz. 1 Uk. 281, Chapa ya Qum, kutoka kwa al-Mufadhal bin Umar kwamba amesema: Nilimwambia Abu Abdillah (a.s.): Nieleze kuhusu kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kwamba Fatima ni mbora wa wanawake wa ulimwenguni. Je ni ulimwengu wa zama zake? Akasema (s.a.w.w.): “Hali hiyo ni kwa Mariam yeye ndiye aliyekuwa mbora kwa wanawake wa ulimwengu wa zama zake. Ama Fatima yeye ni mbora wa wanawake wa ulimwengu mzima kuanzia wale wa mwanzo mpaka wa mwisho.” 46

Page 46


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Al-Hakim, Ibnu Mardawayhi na Abu Naiim katika ad-Dalail wameandika kutoka kwa Jabir kwamba alisema: al-Aqib na Seyyid walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.) naye akawalingania waingie katika Uislamu, wakasema: “Tumesilimu ewe Muhammad.” Akawaambia: “Mmesema uongo, na mkitaka nitawaambieni ni kipi kinachowazuia kuingia katika Uislamu.” Wakamwambia: “Tueleze.” Akawaambia: “Kuupenda msalaba, kunywa pombe na kula nyama ya nguruwe.” Jabir anasema: Ndipo akawaomba wafanye maapizano, nao wakamwahidi iwe siku itakayofuata. Mtume wa Mwenyezi Mungu akatoka siku iliyofuata akiwa amemshika mkono Ali, Fatima, Hasan na Husein, kisha akawatumia ujumbe waje lakini wakakataa kuitikia wito na baadaye wakamkubalia (kufanya suluhu). Mtume akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye alituma kwa haki! Lau wangethubutu kufanya (maapizano) basi bonde lingeteketea kwa moto.” Jabir anasema: Na kwa ajili yao iliteremka Aya: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu.” Nafsi zetu na nafsi zenu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ali. Watoto zetu ni Hasan na Husein. Na wanawake zetu ni Fatima (a.s.). Al-Hakim ameandika kutoka kwa Jabir kwamba: Ujumbe wa Najran ulifi47

Page 47


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 ka kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Unasemaje kuhusu Isa?” Akawaambia: “Yeye ni Roho wa Mwenyezi Mungu, Neno Lake, Mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.” Wakasema: “Upo tayari kuapizana nasi kwani ukweli si hivyo?” Akasema: “Je hilo mwaliridhia?” Wakasema ndio. Akasema: “Kama mnataka basi hakuna kizuizi.” Ndipo akaenda kuwakusanya watoto wake Hasan an Husein. Kiongozi wao akasema: “Msifanye maapizano na mtu huyu, Wallahi kama mtaapizana naye basi litaangamizwa moja kati ya makundi mawili.” Wakaja na kumwambia: “Ewe Abul-Q?sim! Hakika waliotaka kufanya maapizano na wewe ni wale masafihi miongoni mwetu, nasi tunapenda utusamehe.” Akaesema: “Nimeshawasamehe.” Kisha akasema: “Hakika adhabu imeshatanda Najran.” Muslim, Tirmidhi, Ibnu al-Mundhir, al-Hakim na al-Bayhaqiy katika Sunan yake wameandika kutoka kwa Sa’d ibnu Abi Waqqas kwamba alisema: Ilipoteremka Aya hii: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein, akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio ndugu zangu.” Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Aliyai bin Ahmar al-Yashkariy kwamba amesema: Ilipoteremka Aya hii: “Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima na watoto wao Hasan na Husein. Akawaita mayahudi waje kwenye maapizano na ndipo kijana toka kwa mayahudi akasema: “Ole wenu! Hivi jana ndugu zenu waliogeuzwa manyani na nguruwe hawakuwakatazeni kwamba msifanye maapizano.” Ndipo wakaacha. Al-Bayhaqiy katika ad-Dalail ameandika kupitia njia ya Salmah bin Abdu Yushu’ kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu yake, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliwaandikia barua watu wa Najran kabla ya kushushiwa Bismillahi ya Sulayman: “Kwa jina la Mungu wa Ibrahim, Is’haqa na Ya’qub. Kutoka kwa Muhammad Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenda kwa Askofu wa Najran na wakazi wa Najran. Ikiwa mtasilimu basi 48

Page 48


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 hakika mimi nitamhimidi Mwenyezi Mungu kwenu Mungu wa Ibrahim, Is’haqa na Ya’qub. Ama baad, hakika mimi nawaita kwenye ibada ya Mwenyezi Mungu na mtoke kwenye ibada ya waja, na nawaita kwenye mamlaka ya Mwenyezi Mungu na mtoke kwenye mamlaka ya waja. Hivyo mkikataa basi ni juu yenu kodi, na kama mkikataa nitaidhinisha vita dhidi yenu, wasalamu.” Askofu aliposoma barua hii aliisadiki na akaingiwa na hofu kubwa, ndipo akatuma ujumbe aitwe mtu mmoja mkazi wa Najrani aliyejulikana kwa jina la Sharhab?l bin Wid?’h, akampa barua ya Mtume (s.a.w.w.) naye akaisoma. Askofu akamuuliza ni ipi rai yako? Sharhab?l akasema: “Nimeyajua yale ambayo Mwenyezi Mungu alimwahidi Ibrahim ambayo ni unabii kutoka katika kizazi cha Ismail, hakuna kizuizi kinachozuia mtu huyu kuwa ndiye, hivyo sina rai katika unabii. Lau ingekuwa ni kuhusu mambo ya kidunia basi ningekupa rai na ningetoa juhudi zote kwako.” Askofu akamwita moja baada ya mwingine katika wakazi wa Najran, na wote walisema mfano wa yale aliyosema Sharhab?l, ndipo wakaamua kwa pamoja wamtume Sharhab?l bin Wid?’h, Abdullah bin Sharhab?l na Jabbari bin Faydh waende kumdadisi Mtume wa Mwenyezi Mungu na hatimaye wawaletee habari zake. Ujumbe ukasafiri hadi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wakamuhoji naye akawahoji, basi mahojiano yaliendelea mpaka wakamwambia: “Unasemaje kuhusu Isa bin Mariam?” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawaambia: “Leo hii sina kitu cha kuwaambieni kuhusu Isa, subirini mpaka kesho asubuhi ndipo nitawaelezeni yale nitakayoteremshiwa kuhusu Isa bin Mariam.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hizi: “Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, alimuumba kutokana na udongo, kisha akamwambia kuwa, basi akawa. Ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, basi usiwe miongoni mwa wenye kutia shaka. Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa 49

Page 49


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 59 - 61). Lakini wakakataa kuamini hilo. Siku iliyofuata baada ya kuwa tayari ameshawapa habari, Mtume wa Mwenyezi Mungu alitoka kwa ajili ya maapizano akiwa na Hasan na Husain ndani ya joho lake na Fatima akiwa nyuma ya mgongo wake, licha ya kwamba kipindi hicho tayari alikuwa ameshakuwa na wanawake wengi. Sharhab?l akawaambia marafiki zake: “Hakika kuna jambo ninaloliona mbele, ikiwa kweli huyu ni Nabii Mtume basi kitendo cha kuapizana naye hakitambakisha yeyote miongoni mwetu juu ya ardhi, hata unywele na ukucha bali ni lazima ataangamia.” Wakamwambia: Ni ipi rai yako? Akasema: “Rai yangu ni kwamba tumuombe abadili maamuzi kwani hakika mimi namwona ni mtu asiyehamia kwenye maamuzi ya kiupuuzi katu.” Wakamwambia hilo ni juu yako. Ndipo Sharhab?l akamwendea Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kumwambia: “Hakika mimi nimeona kheri nyingine kuliko kuapizana na wewe.” Akamuuliza ni ipi hiyo? Akasema: “Ubadili hatua yako ya leo mpaka kwenye ile ya usiku (wa jana), na toka kwenye ile ya usiku wako mpaka kwenye ile ya (jana) asubuhi, basi hatua yoyote utakayoichukua hapo kwa ajili yetu tutaipokea.” Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akabadili maamuzi akarejea bila kuapizana nao na akafanya nao suluhu kwa sharti walipe kodi.67 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote kwa pamoja wala msifarakane..” (Sura Aali Imran: 103). Ahmad ameandika kutoka kwa Zayd bin Thabit kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi ni mwenye kuacha 67 Ameiandika al-Haskani katika kitabu Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 120, chapa ya Beiruti. Na al-Manaqib cha Ibnu al-Mughazaliy, Hadithi ya 313. Na Ahamad bin Hanbal katika kitabu Fadhailus-Sahaba, Hadithi ya 27, mlango wa fadhila za Hasan na Husain (a.s.). 50

Page 50


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 kati yenu mirathi mbili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi, na kizazi changu watu wa nyumba yangu, na hakika hivyo viwili havitaachana mpaka vinikute kwenye hodhi.”68 Tabarani ameandika kutoka kwa Zayd bin Arqam kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Mimi nawatangulia nanyi mtanikuta katika hodhi, basi angalieni ni jinsi gani mtakavyoishi na vizito viwili nyuma yangu.” Pakasemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni vipi hivyo vizito viwili? Akasema: “Kikubwa ni Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba ambayo ncha moja imo mikononi mwa Mwenyezi Mungu na ncha nyingine mikononi mwenu, hivyo shikamaneni nacho hamtateleza wala kupotea. Na kidogo ni kizazi changu, na hakika hivyo viwili havitaachana mpaka vinifikie kwenye hodhi. Na hilo nilimuomba Mola wangu Mlezi hivyo msivitangulie mtaangamia na wala msivifundishe kwani hakika hivyo vina ujuzi kulikoni nyinyi.” Ibnu Sa’d, Ahmad na Tabarani wameandika kutoka kwa Abu Said alKhudri kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Enyi watu! Hakika mimi ni mwenye kuacha kati yenu mambo mawili ambayo lau mkishikamana nayo hamtapotea baada yangu, kimoja ni kikubwa kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi, na kizazi changu watu wa nyumba yangu, na hakika hayo mawili hayataachana mpaka yanikute kwenye hodhi.”69 68 Nasema: Baadhi ya wale ambao wana maradhi nyoyoni mwao miongoni mwa wale wenye chuki na uadui na Ahlul-Baiti (a.s.) wameondoa maneno ‘Kizazi changu’ na kuweka badala yake neno ‘sunna yangu’, na hii ni batili ya wazi, kwa sababu hata hiyo Sunna nayo inahitaji mfasiri na mfafanuzi, na hakuna ajuaye hayo ila Ahlul-Bait (a.s.) kwa sababu wao ndio wajuzi zaidi wa yale yaliyomo ndani ya nyumba. 69 Al-Haskani katika kitabu chake Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 130 anapotafsiri Aya hii, ameandika kutoka kwa Ali bin Musa Ridha (a.s.) kutoka kwa baba zake kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Anayetaka kupanda safina ya uokovu na kushikamana na shikio imara na kushikamana na kamba ngumu ya Mwenyezi Mungu basi amtawalishe Ali na awafuate viongozi toka katika kizazi chake.” 51

Page 51


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu..” (Sura Maida: 3). Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakir wameandika kwa sanad dhaifu kutoka kwa Abu Said al-Khudri kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipomsimika Ali Siku ya Ghadiri ya Mfunguo tatu alisema (s.a.w.w.): “Ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: Leo nimekukamilishieni dini yenu.70 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura al-Maida: 55). 70 Hadithi hii imepokewa na sahaba wakubwa mia moja na kumi, na tabiina thamanini na nne. Pia zaidi ya watu mia nne miongoni mwa wasomi, wanahadithi, wafasiri, wanahistoria na wataalamu wa fani ya wapokezi, wameiandika hadithi hii muhimu. Hivyo anayetaka maarifa zaidi ni juu yake kurejea Enklopedia ya Ghadiri ya Allama al-Amin Juz. 1. Humo ameipokea toka kwa wanazuoni mia tatu na sitini na toka katika vitabu ishirini na sita wote wakiwa ni wanazuoni wa kisunni na ni vitabu vya kisunni. 52

Page 52


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Al-Khatib ameandika katika al-Muttafaq kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Ali alitoa sadaka pete yake ndipo Mtume akamuuliza muombaji - ni nani aliyekupa pete hii? Akasema ni yule aliyomo kwenye rukuu, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Abdurazzaq, Abdu bin Hamid, Ibnu Jarir, Abu Shaykh na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui,” iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Tabarani katika al-Awsat na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ammar bin Yasir kwamba alisema: “Muombaji alisimama kwa Ali na hali akiwa katika rukuu ya Swala ya sunna, ndipo akavua pete yake na kumpa muombaji, naye akaenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumjulisha hilo, ndipo Aya hii ikateremka kwa Mtume (s.a.w.w.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawasomea sahaba zake kisha akasema: “Yule mbaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake. Ewe Mwenyezi Mungu! Mpende ampendaye na mfanyie uadui amfanyiaye uadui.” Abu Shaikh na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) kwamba alisema: “Aya hii ilimteremkia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nyumbani kwake: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui”, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoka na kuingia msikitini akawakuta watu wakisali, wengine wamo katika rukuu, wengine katika sijda na wengine katika kisimamo, ghafla akamwona muombaji, akamuuliza: Ewe muom53

Page 53


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 baji, je kuna yeyote aliyekupa kitu? Akajibu: ‘Hapana ila yule aliyemo katika rukuu naye ni Ali bin Abu Talib amenipa pete yake.”’ Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Mujahid kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib, alitoa sadaka na hali akiwa katika rukuu. Ibnu Mardawayhi ameandika kupitia njia ya al-Kalbiy kutoka kwa Abu Salih kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Abdullah bin Salam alikuja na kundi lake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) wakati wa Adhuhuri, wakasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika nyumba zetu ziko mbali na hatupati wa kuketi nasi na kujumuika nasi kinyume na msikiti huu, na hakika jamaa zetu walipoona tumemsadiki Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na tumeiacha dini yao wametudhihirishia uadui na wameapa kwamba hawatajumuika nasi na wala hawatakula pamoja nasi, jambo hilo limekuwa zito juu yetu.’ Wakiwa bado wanaendelea kumlalamikia hali hiyo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ghafla ilimshukia Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Sala ya Dhuhri ikanadiwa na akatoka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). akasema (kumuuliza muombaji): ‘Kuna yeyote aliyekupa kitu?’ Akajibu ndio. Akamuuliza: ‘Nani?’ Akajibu: Yule aliyesimama. Akamuuliza: ‘Alikupa akiwa katika hali gani?’ Akajibu: Akiwa katika rukuu. Akasema: ‘Yule ni Ali bin Abu Talib.’ Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoa takbira huku akisema: ‘Na mwenye kumtawalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini, basi kwa hakika kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kushinda.’ Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Ali bin Abu Talib alikuwa amesimama akisali ndipo muombaji akapita, 54

Page 54


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 naye akiwa katika rukuu, akampa pete yake, ndipo ikateremka Aya hii: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Iliteremka kwa ajili ya wale walioamini na Ali ndio kinara wao. Abdu bin Hamid, Ibnu Jarir na Ibnu al-Mundhir wameandika kutoka kwa Abu Ja’far kwamba aliulizwa kuhusu Aya hii kwamba ni akina nani walioamini? Akasema: “Ni wale walioamini. Akaambiwa imetufikia habari kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Akasema: Ali ni miongoni mwa wale walioamini.” Abu Naim ameandika katika al-Hilyah kutoka kwa Abdul-Malik bin Abu Sulayman kwamba alisema: Nilimuuliza Abu Ja’far Muhammad bin Ali kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” Nikasema hakika masahaba wa Muhammad (s.a.w.w.) wanasema kwamba ni Ali. Akasema: “Ali ni miongoni mwao.”71 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalim.” (Sura Maida: 67). Ibnu Abi Hatim, Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Said al-Khudriy kwamba alisema: Aya hii: “Ewe Mtume! Fikisha 71 Rejea pia Shawahidut-Tanziil Juz. 1, Uk. 161, Chapa ya Beirut. 55

Page 55


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako; na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalim.” Iliteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) Siku ya Ghadir Khum kwa ajili ya Ali bin Abu Talib. Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Mas’ud kwamba alisema: Zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu tulikuwa tukisoma: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola Wako; kwamba hakika Ali ni mwenye mamlaka juu ya waumini, na kama hutafanya, basi hukufikisha ujumbe Wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu.”72

SURAT AL-AN’AAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukampa Is’haka na Yakub, wote tukawaongoza, na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam:84 - 85). Ibnu Abi Hatim ameandika kutoka kwa Abu Harbi bin al-As’wad kwamba amesema: Hajjaj alituma ujumbe kwa Yahya bin Ya’mar kwamba: 72 Ad-Durul-Manthur Juz. 3, Uk. 28. Pia ameiandika Ibnu Asakir katika kitabu chake Tarikhud-Damashq katika wasifu wa Amirul-Muuminina (a.s.), Hadithi ya 452. 56

Page 56


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 ‘Imenifikia habari kuwa wewe unadai kwamba Hasan na Husein ni katika kizazi cha Mtume (s.a.w.w.) kwa ushahidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nami nimekisoma kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake lakini sijauona.’ Akamjibu: Hivi unasoma Sura An’am: “Na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa?” Akasema ndio nimesoma. Akamuuliza: ‘Huoni Isa ni kizazi cha Ibrahim na hali hana baba?’ Akasema: Umesema kweli. Abu Shaikh, al-Hakim na al-Bayhaqiy wameandika kutoka kwa AbdulMalik bin Umayri kwamba alisema: Yahya bin Ya’mar aliingia kwa Hajjaj na akamtaja Husein. Hajjaj akasema: “Hakuwa katika kizazi cha Mtume (s.a.w.w.).” Yahya akasema: “Umenena uongo.” Hajjaj akasema: “Niletee dalili juu ya hilo ulisemalo. “ Ndipo akamsomea: “…..na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa” hivyo Mwenyezi Mungu akatoa habari kwamba Isa ni katika kizazi cha Ibrahim. Hajjaj akasema: “Umesema kweli.”73

SURA AL-AA’RAF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na semeni: Tufutie dhambi zetu, na ingieni mlangoni kwa unyenyekevu, tutakusameheni makosa yenu tutawazidishia watendao mema.” (Sura Aa’raf:161).

73 Rejea Tafsirul-Burhan ya Sayyid Hashim al-Bahraniy Juz. 1, Uk. 538, Chapa ya Qum. 57

Page 57


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Shayba ameandika kutoka kwa Ali bin Abu Talib kwamba alisema: Hakika mfano wetu katika umma huu ni kama mfano wa Safina ya Nuhu na mlango wa kufutiwa madhambi wa Kizazi cha Israil.

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na jueni kwamba chochote mlichopata ghanima, basi khumsi yake ni ya Mwenyezi Mungu na Mtume na jamaa na mayatima na masikini na msafiri……” (Sura al-An’fal: 41). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Zayd bin Arqam kwamba alisema: Aali Muhammad waliopewa khumsi ni wale Aali Ali, Aali Abbas, Aali Ja’far na Aali Aqil. Ibnu Abi Shayba ameandika kutoka kwa Mujahid kwamba alisema: Aali Muhammad si halali kwao sadaka hivyo akawawekea Khumsi.74 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na kama wakitaka kukuhadaa, basi Mwenyezi Mungu atakutosheleza. Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake na kwa waumini.” (Sura al-An’fal: 62). Ibnu Asakir ameandika kutoka kwa Abu Huraira kwamba alisema: “Arshi imenakishiwa kwa “Hapana Mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mimi pekee sina mshirika, Muhammad ni mja wangu na Mtume wangu, nimempa nguvu kupitia Ali.” Na hiyo ndio kauli ya Mwenyezi Mungu: “Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake na kwa waumini.” 74 Ad-Durul-Manthur Juz. 3, Uk. 185. 58

Page 58


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale walioamini na wakahama, na wakapigania dini ya Mwenyezi Mungu kwa mali zao na nafsi zao, na wale waliowapa mahala pa kukaa na wakainusuru, hao ndio marafiki wao kwa wao.” (An’fal: 72). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alifunga udugu baina ya Ansari na Muhajirina, hivyo akaweka udugu baina ya Hamza bin Abdul-Muttalib na Zayd bin Harith, baina ya Umar bin al-Khattab na Maadh bin Áfrau, baina ya Zubair bin al-Áwwam na Abdullah bin Mas’?d, baina ya Abu Bakr na ?alha bin Abdullah, baina ya Abdurahman bin Awfi na Sa’d bin Rabi’u. na akawaambia masahaba zake wengine fungeni udugu, nami ndugu yangu ni huyu, yaani Ali bin Abu Talib. Waislamu wakaendelea katika hali hiyo mpaka ikateremka Aya hii.75

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1).

75 Ad-Durul-Manthur Juz. 3 Uk. 205. 59

Page 59


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Abdullah bin Ahmad bin Hanbal katika Zawaidul-Musnad, na Abu Shaikh Ibnu Mardawayhi, wameandika kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: Zilipoteremka kwa Mtume Aya kumi za mwanzo wa Sura Baraa alimwita Abu Bakr ili akawasomee wakazi wa Makka. Kisha akaniita na kusema: “Mdiriki Abu Bakr na popote utakapomkuta chukua Sura kutoka kwake. Abu Bakr akarejea kwa Mtume (s.a.w.w.) na kumwambia: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kuna chochote kimeteremka kunikhusu?” Akasema: “Hapana lakini Jibril amenijia na kuniambia: Hapasi kufikisha kwa niaba yako ila wewe mwenyewe au mtu kutokana na wewe.” Ibnu Abu Shayba, Ahmad, Tirmidhi, Abu Shaikh na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Anas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr akiwa na Sura Baraa, kisha akamrejesha na kumwambia: “Haipasi yeyote yule kuibalighisha hii ila mtu kutoka katika ndugu zangu.” Ndipo akamwita Ali na kumkabidhi Sura hiyo. Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqqas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr aende na Sura Baraa kuwasomea wakazi wa Makka, kisha akamtuma Ali nyuma yake akaichukue toka kwake, basi Abu Bakr akahisi hali fulani moyoni mwake. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hafikishi kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe au mtu kutoka katika ndugu zangu.” Ibnu Habban na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Said al-Khudri kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtuma Abu Bakr akaifikishe Sura Baraa kwa niaba yake, baada ya kumtuma alimpeleka Ali bin Abu Talib (a.s.) akamwambia: “Ewe Ali! Hakika hafikishi kwa niaba yangu ila mimi mwenyewe au wewe.” Kisha akamwambia amfuate akiwa juu ya ngamia wake al-Ádhb?u, akaenda mpaka akamkuta Abu Bakr na akaichukua Sura Baraa toka kwake. Abu Bakr akaja kwa Mtume (s.a.w.w.) na hali kaingiwa na khofu kutokana na hilo kwamba huenda kuna chochote kimeteremshwa kumhusu yeye. Alipofika kwa Mtume akasema: “Nimefanya nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: 60

Page 60


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 “Hafikishi kwa niaba yangu asiyekuwa mimi au mtu kutokana na mimi.”76 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kususu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu” kwamba alisema: Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.). Ibnu Jariri ameandika kutoka kwa Muhammad Ka’b al-Qardhiy kwamba alisema: Talha bin Shayba, Abbas na Ali bin Abu Talib kila mmoja alijigamba. Talha akasema: ‘Mimi ndio mtunza Nyumba funguo zimo mikononi mwangu.’ Abbas akasema: ‘Mimi ndiye mgawa maji na msimamizi wake.’ Ali akasema: ‘Sijui mtasema nini. Bila shaka nimeswali kabla ya mtu yeyote na mimi ndiye mwanajihadi.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha 76 Hii yenyewe ni dalili tosha kwamba Abu Bakr hastahiki kuwa mwakilishi wa Mtume (s.a.w.w.) katika jambo kama hili, lakini cha kushangaza yeye mwenyewe alijitangaza kuwa ni Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu bila dalili wala tamko la Mtume au la Qur’ani. Na hali katika Umma yupo aliye mbora kushinda yeye naye si mwingine ni Ali bin Abu Talib. 61

Page 61


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wameridhia kuwa pamoja na wanaobakia nyuma, na nyoyo zao zimepigwa muhuri, kwa hiyo hawafahamu.” (Sura tawaba: 87). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Sa’d bin Abi Waqqas kwamba Ali bin Abu Talib alitoka na Mtume (s.a.w.w.) mpaka wakafika ThaniyatulWida’u akikusudia kwenda Tabuk na hali Ali akilia na akisema: “Unaniacha pamoja na wanaobaki nyuma.” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Hivi huridhii kuwa wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa ila ni kwamba hakuna unabii baada yangu.”77 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Muhajiri na Ansari...” (Sura Tawba: 100). Ibnu al-Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika Muhajiri ni: Ali, Salman na Ammar bin Yasir.” 77 Ad-Durul-Manthur Juz. 3 Uk. 266. 62

Page 62


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (Sura Tawba: 119). Ibnu al-Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” Kwamba alisema: “Yaani kuweni pamoja na Ali bin Abu Talib.” Ibnu Asakir ameandika kutoka kwa Abu Ja’far kuhusu kauli yake (s.w.t.): “Na kuweni pamoja na wakweli.” Kwamba alisema: “Yaani kuweni pamoja na Ali bin Abu Talib (a.s.).” Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hayo ni kwa sababu haiwafikii kiu wala taabu wala njaa katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawakanyagi njia iwachukizayo makafiri.” (Sura Tawba: 120). Al-Hakim na Ibnu al-Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alitoka kwenda kwenye moja ya vita na akamwacha Ali kama makamu wake kwa ndugu zake. Ali akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Unaniacha Maquraishi watasema nini, watasema amemtelekeza binamu yake mapema mno na amemwengua. Nami naona ni bora nitafute fadhila kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu nimemsikia Mwenyezi Mungu akisema: “wala hawakanyagi njia iwachukizayo makafiri.” Mtume akasema: “Ama kauli yako: Maquraishi watasema nini, watasema amemtelekeza binamu yake 63

Page 63


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 mapema mno na amemwengua. Bila shaka walishasema: Hakika mimi mchawi na kuhani. Wakasema: Hakika mimi mwongo. Hivyo una kigezo chema kwangu, huridhii kuwa wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa ila ni kwamba hakuna Nabii baada yangu.”

SURAT YUNUS Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Kwa fadhili za Mwenyezi Mungu na kwa rehema zake basi wafurahi, hiyo ni bora kuliko wanavyovikusanya.” (Yunus: 58). Al-Khatib na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Sema: Kwa fadhili za Mwenyezi Mungu” fadhila ni Nabii (s.a.w.w.). “na kwa rehema zake” rehema zake ni Ali bin Abu Talib.

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” (Sura Hud: 17). Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Ali kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndiye aliye na dalili itokayo kwa Mola Wake, na mimi ndiye shahidi atokaye kwake.” Ibnu Abi Hatim, Ibnu Mardawayhi na Abu Naim katika al-Ma’rifa wameandika kutoka kwa Ali bin Abu Talibi kwamba: Alisema Ali (a.s.): 64

Page 64


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 “Hakuna mtu yeyote miongoni mwa makuraishi ila kuna sehemu ya Qur’ani ilishuka kwa ajili yake.” Ndipo mtu mmoja akamwambia: ‘’Ni ipi iliyoteremka kwa ajili yako?’’Ali akasema: “Hivi hausomi Sura Hud: “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola Wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndiye aliye na dalili itokayo kwa Mola Wake, na mimi ndiye shahidi atokaye kwake.” Ibnu Mardawayhi ameiandika kwa njia nyingine kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Aliye na dalili itokayo kwa Mola Wake ni mimi, na shahidi atokaye kwake ni Ali (a.s.).”

SURAT AR-RAAD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiyochipua kwenye shina moja inayonyweshelezwa maji yaleyale.” (Raad: 4). Al-Hakim ameiandika na Ibnu Mardawayhi amesema ni hadithi sahihi, kutoka kwa Jabir kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Ewe Ali! Watu wanatokana na miti tofauti. Na mimi na wewe tunatokana na mti mmoja.” Kisha Mtume (s.a.w.w.) akasoma: “Na katika ardhi mna vipande vilivyokaribiana. Na zipo bustani za mizabibu na mimea mingine na mitende ichipuayo kwenye shina na isiy65

Page 65


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 ochipua kwenye shina moja inayonyweshelezwa maji yaleyale.”78 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Sura ar-Raad: 7). Ibnu Jariri, Ibnu Mardawayhi, Abu Naim katika al-Ma’rifa, Daylamiy, Ibnu Asakir na Ibnu Najjar wameandika kwamba: Ilipoteremka: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema: ‘Mimi ndiye mwonyaji.’ Kisha akaashiria mkono wake kwenye bega la Ali bin Abu Talib na kusema: ‘Ali wewe ndiye mwongozaji. Kupitia kwako wataongoka wenye kutaka kuongoka baada yangu.” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Abi Barzati al-Aslamiy kwamba alisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akisema: “Hakika wewe ni mwonyaji tu.” Akaweka mkono wake juu ya kifua chake. Kisha akauweka juu ya kifua cha Ali huku akisema: “Kila kaumu ina wa kuwaongoza.” Ibnu Mardawayhi na al-Dhiyau katika al-Mukhtar wameandika kutoka kwa ibnu Abbas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Mwonyaji ni mimi na Mwongozaji ni Ali bin Abu Talib (a.s.).” Abdullah bin Ahmad katika Zawaidul-Musnad, Ibnu Abi Hatim, Tabaraniy katika al-Awsat, al-Hakim na wamesema ni hadithi sahihi. Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakiri, hao wote wameiandika kutoka kwa Ali bin Abu Talib kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ndiye Mwonyaji, na mimi ndiye Mwongozaji.”79 78 Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 44. 79 Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 45 66

Page 66


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Utukufu ni wa yule ambaye alimpeleka mja wake usiku kutoka Msikiti Mtukufu mpaka msikiti wa mbali ambao tumevibariki vilivyoko pembezoni mwake, ili tumwonyeshe baadhi ya dalili zetu. Hakika yeye ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (Sura Israi: 1). Tabarani ameandika kutoka kwa Aisha kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Nilipopelekwa mbinguni niliingizwa peponi, nikaona mti mmoja miongoni mwa miti ya peponi ambao sijaona peponi mzuri kushinda wenyewe, wala wenye majani yang’aayo kushinda wenyewe, na wala wenye matunda matamu kushinda wenyewe, nikachuma moja ya matunda yake na nikala, ndipo mbegu za uzazi zikapatikana katika uti wa mgongo wangu kutokana na tunda hilo, nilipoteremka ardhini nilimwingilia Khadija na ndipo akashika mimba ya Fatima (a.s.), hivyo niwapo na hamu ya kunusa harufu ya pepo hunusa harufu ya Fatima.”80 Al-Hakim ameandika kutoka kwa Sa’d bin Waqqas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Jibril (a.s.) aliniletea pera nikalila usiku ambao nilipelekwa miraji, na ndipo Khadija akashika mimba ya Fatima, hivyo niwapo na hamu ya harufu ya peponi huinusa shingo ya Fatima.”81 80Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 153. Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Binti yangu Fatima ni Hurulaini wa kibinadamu, hajawahi kupata hedhi wala nifasi. Na hakika Mwenyezi Mungu alimpa jina la Fatima (Mwachanishi) kwa sababu Mwenyezi Mungu amemwepusha dhidi ya moto yeye na vipenzi vyake.” Tazama kitabu Kanzul-Ummal Juz. 12, Namba 3422. 81Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 153. 67

Page 67


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Adiy na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Anas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema: “Nilipopelekwa Miiraji niliona nguzo ya Arshi imeandikwa: Hapana Mungu apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wa Allah nimempa nguvu kupitia Ali.”82 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” (Sura Israi: 26). Al-Bazzar, Abu Ya’la, Ibnu Abi Hatim na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: Ilipoteremka Aya hii: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Fatima na kumkabidhi Fadak. Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Ilipoteremka: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” Mtume wa Mwenyezi Mungu alimpa Fatima Fadak.83

SURAT MARYAM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na amani iko juu yake siku aliyozaliwa na siku atakayofariki, na siku atakayofufuliwa hai.” (Sura Maryam: 15). Ahmad, Abu Ya’la, Ibnu Habban, Tabarani, al-Hakim na Dhayau wameandika kutoka kwa Abu Said kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi 82 Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 153. 83 Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 177. 68

Page 68


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hasan na Husain ni mabwana wawili wa vijana wa peponi, ila kwa wana wawili wa khalati: Isa bin Mariam na Yahya bin Zakariya.”84 Ibnu Asakir ameandika kutoka kwa Qurrat kwamba alisema: Mbingu haikuwahi kumlilia yeyote ila Yahya bin Zakariya na Husain bin Ali, na wekundu wake ndio kulia kwake.85 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” (Sura Maryam: 96). Ibnu Mardawayhi na Daylamiy wameandika kutoka kwa al-Barau kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali bin Abu Talib: “Ewe Ali sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hifadhi Kwako na niwekee mapenzi Kwako, na niwekee mapenzi katika nyoyo za waumini.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.).86 Tabarani na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib (a.s.): “Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” yaani mahaba katika nyoyo za waumini.”

84 Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 262. 85 Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 264. 86 Ad-Durul-Manthur Juz. 4 Uk. 287. 69

Page 69


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT TAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Akasema: Ee Mola wangu! Nipanulie kifua changu. Na unifanyie wepesi kazi yangu. Na ufungue fundo katika ulimi wangu. Wapate kufahamu kauli yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Harun. “ (Sura Twaha: 25 – 30) Salfiy ameandika katika Tuyuriyat kutoka kwa Abu Jafar Muhammad bin Ali kwamba alisema: “Ilipoteremka: “Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Harun. Nitie nguvu kupitia yeye.” Mtume wa Mwenyezi Mungu alikuwa juu ya kilele cha mlima, kisha akamwomba Mola wake kwa kusema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nitie nguvu kupitia ndugu yangu Ali. Mwenyezi Mungu akamkubalia ombi hilo.”87

87 Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 295. Kauli hiyo inaungwa mkono na kauli ya Mtume: “Wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa ila ni kwamba hakuna Nabii baada yangu.” Ambayo inatamka wazi kwamba Ali ndiye Khalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na ndiye Wasii, Waziri na Mwenye mamlaka baada yake. Hivyo kila aliyemwondoa katika nafasi yake ni mnyang’anyi. Kwa rejea zaidi rejea kitabu al-Aqdu At-Thamin cha Imam Shawkaniy. 70

Page 70


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT HAJJ Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Bila shaka Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na kufanya vitendo vizuri katika Bustani zipitazo mito chini yake, kwa hakika Mwenyezi Mungu hufanya atakavyo.” (Sura Hajj: 14). Abdu bin Hamid ameandika kutoka kwa Lahiq bin Hamid kwamba alisema: Iliteremka: “Bila shaka Mwenyezi Mungu atawaingiza wale walioamini na kufanya vitendo vizuri……na kuongozwa kwenye njia ya Mwenye kuhimidiwa.” (Sura Twaha: 14 - 24) kwa ajili ya Ali bin Abu Talib, Hamza, na Ubaydah bin al-Harith.88 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mwenyezi Mungu huchagua Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu, kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” (Sura Hajj: 75). Al-Baghawi ameandika katika Mu’jam, al-Barudiy, Ibnu Qaniu, Tabarani na Ibnu Asakir, wote wameandika kutoka kwa Zayd bin Abi Awfa kwamba alisema: “Niliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu katika Msikiti wa Madina, akaanza kusema yuko wapi bin fulani? Aliendelea kuwaita mpaka wakakusanyika kwake, kisha akasema: “Mimi nataka kuwasimulieni hadithi hivyo ihifadhini na muizingatie na mje kuwasimulia wale watakaokuja baada yenu: Hakika Mwenyezi Mungu aliteua kutoka mion71

Page 71


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 goni mwa viumbe Wake, viumbe maalumu: “Mwenyezi Mungu huchagua Wajumbe miongoni mwa Malaika na miongoni mwa watu,” viumbe atakaowaingiza peponi. Na mimi nachagua toka miongoni mwenu ambaye nimependa kumchagua, na ninaweka udugu baina yenu kama Mwenyezi Mungu alivyoweka udugu baina ya Malaika.” Kisha akamwita Sa’d bin Abi Waqqas na Ammar bin Yasir, akasema: “Ewe Ammar! Kundi ovu litakuuwa.” Kisha akaweka udugu baina yao. Ndipo akamwita Abu Dardau na Salman al-Farsiy na kusema: “Ewe Salman! Wewe ni katika watu wa nyumba.” Kisha akaweka udugu baina yao. kisha akatizama nyuso za masahaba zake akasema: “Furahini na tulieni.” Ali akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Roho yangu imenitoka na mgongo wangu umevunjika pale nilipokuona umewafanyia hayo sahaba zako na kuniacha, basi ikiwa ni kutokana na ghadhabu yako juu yangu basi onyo na heshima ni miliki yako. Mtume akasema: “Naapa kwa yule Ambaye amenituma kwa haki, sikukuacha ila ili uwe kwa ajili yangu mwenyewe, kwani wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa, na ni mrithi wangu.” Ali akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nitarithi nini toka kwako? Akasema: “Kile walichorithi warithi wa Manabii kabla yako: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Nabii wao, nawe pamoja na Fatima mtakuwa nami katika kasri la peponi, nawe ni ndugu yangu na rafiki89 yangu.” Kisha Mtume akasoma Aya hii: “Ndugu wakikaa juu ya viti kwa kuelekeana.” (Sura Hijri: 47).

88 Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 349. 72

Page 72


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT NURU Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu ziinuliwe na kutajwa humo jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.” (Sura Nuru: 36). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Anas bin Malik na Burayda kwamba walisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisoma Aya hii: “Katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu ameruhusu ziinuliwe na kutajwa humo jina lake, wanamtakasa humo asubuhi na jioni.” Akasimama mtu mmoja na kumuuliza: “Ni nyumba zipi hizi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Akasema: “Nyumba za Manabii.” Abu Bakr akasimama na kusema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nyumba hii ni miongoni mwazo, nyumba ya Ali na Fatima? “ Akajibu: “Ndio ni miongoni mwazo bali ndio iliyo bora kuliko nyingine.”

SURAT AS-SAJDA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa!” (Sura As-Sajda: 18). Abu al-Faraj al-Asbahani ameandika katika kitabu al-Aghaniy, al-Wahidiy, Ibnu Adiy, Ibnu Mardawayhi, al-Khatib na Ibnu Asakir, wamepokea kwa njia tofauti kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Walid bin Uqbah bin Abu Muit alimwambia Ali: ‘Mimi ni mfasaha kuliko wewe, mwenye meno makali kuliko wewe na shujaa kuliko wewe na hodari wa mapambano kuliko wewe.’ Ali akamjibu: ‘Nyamaza, bila shaka wewe ni fasiki.’ Ndipo 73

Page 73


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa.” Yaani Muumini ni Ali na Fasiki ni Walid bin Uqbah bin Abu Muit.90 Ibnu Is’haq na Ibnu Jariri wameandika kutoka kwa Atau bin Yasar kwamba alisema: Iliteremka Madina ikimuhusu Ali bin Abu Talib na Walid bin Uqbah. Kulikuwa na mzozo baina ya Walid na Ali, Walid bin Uqbah akamwambia Ali: ‘Mimi ni mfasaha kuliko wewe, mwenye meno makali kuliko wewe na shujaa kuliko wewe na hodari wa mapambano kuliko wewe.’ Ali akamjibu: ‘Nyamaza, bila shaka wewe ni fasiki.’ Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa!”91 Ibnu Abi Hatim ameandika kutoka kwa Abdurahman bin Abi Layla kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa,” kwamba alisema: Iliteremka ikimhusu Ali bin Abu Talib – yaani ndio Muumini, na Walid bin Uqbah – yaani Fasiki.92 Ibnu Mardawayhi, al-Khatib na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Je, aliye muumini ni sawa na aliye fasiki? Hawawi sawa,” kwamba alisema: Muumini ni Ali bin Abu Talib. Na Fasiki ni Walid bin Uqbah bin Abu Muit. Hiyo inatokana na sababu iliyokuwa baina yao, ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha aya hiyo.93

89 Ad-Durul-Manthur Juz. 4, Uk. 371. 90 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 178. 91 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 178. 92 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 178. 93 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 178.

74

Page 74


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Nabii ana mamlaka zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao…” (Sura Ahzab: 6). Ibnu Abi Shayba, Ahmad na Nasai wameandika kutoka kwa Burayda kwamba alisema: “Nilishiriki vita pamoja na Ali huko Yaman, nikaona kwake ambalo sikupendezwa nalo, nilipofika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nilimtaja Ali na nikaanza kumshusha hadhi, ghafla nikaona uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu umebadilika, akaniambia: “Ewe Buraydah! Mimi si mwenye mamlaka kwa waumini kuliko nafsi zao?” nikasema ndio ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: “Basi yule ambaye mimi ni mwenye mamlaka juu yake Ali ni mwenye mamlaka juu yake.”94 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita…” (Sura Ahzab: 25). Ibnu Abi Hatim, Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Ibnu Masu’d kwamba alikuwa akisoma hivi: “Na Mwenyezi Mungu amewatosheleza Waumini katika vita kupitia Ali bin Abu Talib.”95 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab:33). Ibnu Jariri, Ibnu Mundhir, Ibnu Abi Hatim, Tabaraniy na Ibnu Mardawayhi 94 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 182. 95 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 192. 75

Page 75


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 wameandika kutoka kwa Ummu Salama mke wa Mtume (s.a.w.w.) kwamba: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwake ameketi juu ya kitanda na hali kajifunika kishamia cha Khaibari, ndipo akaja Fatima akiwa na chungu chenye uji na kuingia nacho kwa Mtume. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamwambia mwite mumeo na wanao Hasan na Husain. Akawaita na ghafla walipokuwa wakila iliteremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.): “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Mtume akachukua sehemu iliyozidi ya kishamia chake na kuwafunika. Kisha akatoa mkono wake ndani ya kishamia akaunyoosha mbinguni na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu na watu makhsusi kwangu, hivyo waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.” Alisema hivyo mara tatu. Nikaingiza kichwa chumbani kwa Mtume na kumwambia: Je na mimi ni pamoja nanyi ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Hakika wewe utaelekea katika kheri.” Alisema mara mbili.96 Tabarani ameandika kutoka kwa Ummu Salama kwamba alisema: Fatima alikuja kwa baba yake akiwa amemletea uji uliokuwa ndani ya bakuli lake, akauweka mbele yake. Mtume akasema: “Yupo wapi mwana wa ami yako?” akasema yupo nyumbani. Akamwambia nenda ukamwite yeye na wanao. Akaja na wanae akiwa amemshika kila mmoja mkono na huku Ali akitembea nyuma yao, mpaka walipoingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), akamkalisha kila mmoja kati yao (Hasan na Husein) katika paja lake, Ali akakaa kuliani kwake na Fatima kushotoni kwake. Kisha kikachukuliwa kishamia kilichokuwa kimetandikwa juu ya kitanda chumbani kwangu. Tabarani ameandika kutoka kwa Ummu Salama kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema kumwambia Fatima (a.s.): Niitie mumeo na wanao. Akawaita na ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawafunika kishamia cha Fadaki, kisha akaweka mkono wake 96 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 198. 76

Page 76


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 juu yao na kusema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio Aali Muhammadi, hivyo weka Sala zako na baraka zako juu ya Aali Muhammadi kama ulivyoziweka juu ya Aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.” Ummu Salama anasema: Nikainua kishamia ili niingie pamoja nao, lakini akakivuta toka mikononi mwangu na kuniambia: Hakika wewe uko kwenye kheri.97 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ummu Salama kwamba alisema: Aya hii iliteremka nyumbani kwangu: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” na nyumbani kulikuwa na watu saba: Jibril, Mikail, Ali, Fatima, Hasan na Husein, nami nikiwa nimesimama mlangoni. Nikamwambia Mtume wa Mwenyezi Mungu je mimi sio katika AhlulBait? Akasema: “Hakika wewe upo katika kheri, wewe ni miongoni mwa wakeze Mtume.” Ibnu Mardawayhi na Khatib wameandika kutoka kwa Said al-Khudriy kwamba alisema: Ilikuwa ni siku ya Ummu Salama mama wa waumini, ndipo Jibril akateremka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu akiwa na Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.,” Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaita Hasan, Husein, Fatima na Ali, akawakumbatia na kuwafunika nguo ilihali kukiwa na pazia kati yao na Ummu Salama, kisha akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, hivyo waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.” Ummu Salama akasema: Na mimi ni pamoja nao ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Wewe una nafasi yako na bila shaka wewe upo katika kheri.” Tirmidhiy ameandika na kusema kwamba ni sahihi, Ibnu Jariri, Ibnu Mundhir, al-Hakim, Mardawayhi na Bayhaqi katika Sunnani Yake, wote wameandika kwa njia tafauti kutoka kwa Ummu Salama kwamba alisema: 97 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 198. 77

Page 77


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 “Nyumbani kwangu ndimo iliteremkia: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa,” na hali ndani ya nyumba alikuwemo Fatima, Ali, Hasan na Husein, Mtume wa Mwenyezi Mungu akawafunika kishamia alichokuwa amejitanda, kisha akasema: “Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, hivyo waondolee uchafu na watakase kabisa kabisa.”98 Ibnu Jarir, Ibnu Abi Hatim na Tabarani wameiandika kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa” imeteremka kwa ajili ya watano: Kwa ajili yangu, Ali, Fatima, Hasan na Husein.” Ibnu Abi Shayba, Ahmad, Muslim, Ibnu Jarir, Ibnu Abi Hatim, na Hakim wameandika kutoka kwa Aisha kwamba alisema: “Siku moja Mtume alitoka akajifunika shuka lililodariziwa na manyoya meusi. Wakaja Hasan na Husain akawafunika, kisha akaja Ali naye akamfunika, kisha akasema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.’” Ibnu Jarir, Hakim na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Sa’d kwamba alisema: Wahyi uliteremka na ndipo akawafunika Ali na Fatima shuka lake, kisha akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio ndugu zangu na Ahlul-Baiti wangu.” Ibnu Abi Shayba, Ahmad, Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir na Tabaraniy wameandika kutoka kwa Wathila bin Asqaf kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuja kwa Fatima akiwa pamoja na Hasan na Husain na Ali, akaingia kisha akamsogeza Ali na Fatim na kuwakalisha mbele yake, na akawakalisha Hasan na Husein kila mmoja wao juu ya paja 98 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 198. 78

Page 78


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 lake, kisha akawafunika shuka yake na hali mimi nikiwa nimewapa mgongo, kisha akasoma Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Ibnu Abi Shayba, Ahmad, Tirmidhi na amesema ni hadithi hasan, Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir, Tabaraniy, Hakim na amesema ni hadithi sahihi, na Ibnu Mardawayhi, wote wameandika kutoka kwa Anas kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akipita mlangoni kwa Fatima atokapo kwenda kuswali Sala ya Alfajri na husema: “Sala enyi Ahlul-Baiti, Sala enyi Ahlul-Baiti Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.”99 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: “Ali alipomuoa Fatima, Mtume alikwenda mlangoni kwake siku arobaini kila asubuhi, na alikuwa akisema: “Asalamu Alaykum Ahlul-Baiti Warahmatullah Wabarakatuhu. Mwenyezi Mungu akurehemuni. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa. Mimi ni mwenye kufanya vita na yule mwenye kuwapigeni vita nyinyi na ni mwenye amani na yule mwenye kufanya amani nanyi.” Tabarani ameandika kutoka kwa Abu Hamrau kwamba alisema: “Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu muda wa miezi sita akija kwenye mlango wa Ali na Fatima na kusema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Tulimshuhudia Mtume muda wa miezi tisa akija kila siku mlangoni kwa Ali bin Abu Talib wakati wa kila Sala na kusema: “Asalamu Alaykum 99 Ad-Durul-Manthur Juz. 5, Uk. 199 79

Page 79


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ahlul-Baiti Warahmatullah Wabarakatuhu. Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa. Mwenyezi Mungu akurehemuni.” Kila siku mara tano. Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na ulipomwambia yule ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha na wewe umemneemesha.” (Sura Ahzab: 37). Bazzar, Ibnu Hatim, Hakim, na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Usama bin Zayd kwamba alisema: Abbas na Ali bin Abu Talib walikwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumwambia: Tumekuja ili utueleze ni yupi umpendaye sana kati ya ndugu zako? Akasema: “Nimpendaye sana kati ya ndugu zangu ni Fatima.” Wakamwambia hatuulizi kuhusu Fatima. Akasema: “Ni Usama bin Zayd ambaye Mwenyezi Mungu amemneemesha nami nimemneemesha.” Ali bin Abu Talib akasema kisha nani ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Kisha wewe kisha Abbas.” Abbas akasema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hivi umemuweka ami yako mwisho!” Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Hakika Ali alikutangulia kwa kuhama.”100 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Sura Ahzab: 56). 100 Ad-Durul-Manthur Juz. 5, Uk. 201 80

Page 80


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Said bin Mansur, Abdu bin Hamid, Ibnu Abi Hatim na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ka’b bin Ajrah kwamba alisema: Ilipoteremka: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu,” tulisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kukutolea salamu tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’”101 Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Ka’b bin Ajrah kwamba alisema: Ilipoteremka Aya hii nilisimama na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kukutolea salamu tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim.’”

101 Ad-Durul-Manthur Juz. 5, Uk. 216 81

Page 81


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Yunus bin Khabab kwamba alisema: “Faris alitutolea khutba akasema: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” Hakika amenipa habari yule aliyemsikia Ibnu Abbas akisema: Hivyo ndivyo ilivyoteremka, nao (masahaba) walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kukutolea salamu tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ? ?? ??????? ???? ???? ????. ????? ?????? ? ?? ????? ??? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ? ???? ??? ????? ? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomsalia Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomrehemu Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim na aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’” Abu Daud, Ibnu Mardawayhi na al-Bayhaqiy katika Sunnan yake, wameandika kutoka kwa Abu Huraira kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Anayependa alingane sawasawa na kipimo kamili basi anapotusalia sisi Ahlul-Baiti aseme: Ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammad Nabii, yeye na dhuria wake na Ahlul-Baiti wake kama ulivyowasali Aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.” Ibnu Abi Shayba, Ahmad, Abdu bin Hamid, Bukhari, Nasai, Ibnu Majah, na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Said al-Khudriy kwamba alisema: Tulisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Kukutolea salamu

82

Page 82


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:04 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 tumeshajua basi ni ipi namna ya kukusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?????? ??? ????? ??? ?? ???????. ? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ???????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad mja Wako na Mtume Wako kama ulivyowasalia aali Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim.’”102 Abdu bin Hamid, Nasai na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Abu Huraira kwamba alisema: Walimuuliza Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni jinsi gani tutakavyokusalia? Akasema: “Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ? ???? ??? ????? ???? ?? ?????

‘Ewe Mwenyezi Mungu! Msalie Muhammad na aali Muhammad, na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyomsalia na kumbariki Ibrahim na aali Ibrahim juu ya walimwengu, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.’” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Abu Huraira kwamba alisema: “Tulisema ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, basi ni vipi tutakavyokusalia? Akasema: “Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Weka rehema na amani, na baraka Zako juu ya Aali Muhammad kama ulivyoziweka juu ya Aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ali kwamba alisema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni namna gani tutakusalia? Akasema (s.a.w.w.): “Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu msalie Muhammadi na Aali 102 Ad-Durul-Manthur Juz. 5 Uk. 218 83

Page 83


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Muhammad kama ulivyomsalia Ibrahim na Aali Ibrahim, hakika Wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.”

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Abu Naim na Daylamiy wameandika kwa njia ya Mujahid kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu, mnilindie heshima yangu kwa ndugu zangu na muwapende kwa ajili yangu.”103 Ibnu Mundhir, Ibnu Abi Hatim na Tabaraniy wameandika kwa njia ya Said bin Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Ilipoteremka Aya hii: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nani karaba zako hawa ambao tumewajibishwa kuwapenda? Akasema (s.a.w.w.): “Ali, Fatima na watoto wao.” Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Abu Daylam kwamba alisema: Alipoletwa Ali bin Husein bin Ali bin Abu Talib (a.s.) na hali ni mateka na kusimamishwa katika barabara kuu ya Damascus alisimama mzee mmoja kati ya watu wa Sham, akasema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amewauwa na kuwang’oeni na kung’oa mzizi wa fitina.” Ali bin Husein akasema: ‘Umewahi kusoma Qur’ani?’ akajibu ndio. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma Aali Haa Miim?’ Akajibu hapana. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...”’ Mzee akasema: ‘Nyinyi ndio hao?’ Akasema (a.s.): ‘Naam ndio sisi.’ 103 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 7 84

Page 84


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Muslim, Tirmidhiy na Nasai wameandika kutoka kwa Zayd bin Arqam kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Nawakumbusheni Mwenyezi Mungu kuhusu Ahlul-Baiti wangu, yaani Ali, Fatima, Hasan na Husein.” Ibnu Adiy ameandika kutoka kwa Abu Said kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Atakayetuchukia sisi Ahlul-Baiti basi ni mnafiki.” Tirmidhiy ameandika na kusema ni hadithi sahihi, na Ibnu al-Anbariy katika al-Masahifu wameandika kutoka kwa Zayd bin Arqam kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi ni mwenye kuwaachia kati yenu vile ambavyo lau mkishikamana navyo katu hamtapotea baada yangu, kimojawapo ni kitukufu kuliko kingine: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka toka mbinguni hadi ardhini. Na kingine ni kizazi changu watu wa nyumba yangu, na havitoachana mpaka vinikute kwenye hodhi, basi angalieni ni jinsi gani mtakavyobaki navyo.” Tabarani ameandika kutoka kwa Hasan bin Ali kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hatatuchukia yeyote wala kutuhusudu ila ataadhibiwa Siku ya Kiyama kwa mjeledi wa moto. Ahmad bin Habban na al-Hakim wameandika kutoka kwa Abu Said kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake kwamba hakuna mtu yeyote atakayetuchukia sisi Ahlul-Baiti ila ni lazima Mwenyezi Mungu atamwingiza motoni.

85

Page 85


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT MUHAMMAD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na kama tungependa tungekuonyesha hao na ungewatambua kwa alama zao, na hasa utawafahamu kwa namna ya usemi wao, na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyenu.” (Sura Muhammad: 30). Ibnu Mardawayhi na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Abu Said alKhudriy kwamba alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “….na hasa utawafahamu kwa namna ya usemi wao, na Mwenyezi Mungu anavijua vitendo vyao”: ni kwa kule kumchukia kwao Ali bin Abu Talib (a.s.).104 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Mas’ud kwamba alisema: Hatukuwa tunawafahamu wanafiki zama za Mtume wa Mwenyezi Mungu ila kwa kule kumchukia kwao Ali bin Abu Talib (a.s.).105

SURAT RAHMAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani. Basi nyinyi wawili mnakataa neema gani ya Mola wenu Mlezi? Katika hizo mbili hutoka lulu na marijani.” (Surat Rahman: 19 - 22). 104Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 66. 105 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 66. 86

Page 86


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amezikutanisha bahari mbili.” Ali na Fatima kati yao kuna kizuizi hawaingiliani, kwani Mtume alisema: “Hutoka kwao hao wawili lulu na marijani, Hasan na Husein.”106 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amezikutanisha bahari mbili”: “Ni Ali na Fatima, hutoka kwao hao wawili lulu na marijani, ambao ni Hasan na Husein.”

SURAT AL-WAQI’A Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na nyinyi mtakuwa namna tatu. Basi watu wenye kheri, watakuwa namna gani wenye kheri. Na watu wenye shari, watakuwa namna gani wenye shari. Waliotangulia ndio waliotangulia.” (Sura al-Waqi’a: 7 10). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Waliotangulia ndio waliotangulia” kuwa iliteremka kumuhusu Ali bin Abu Talib, na kila mtu miongoni mwao ni mtangulizi wa umma wake, na Ali ndiye mbora wao katika kutangulia.107

106 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 142 107Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 154. 87

Page 87


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Abi Hatim na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Waliotangulia ndio waliotangulia”: Yoshua bin Nun ndiye aliyetangulia kumwamini Musa, Muumini wa Aali Yasin ndiye aliyetangulia kumwamini Isa, na Ali bin Abu Talib ndiye aliyetangulia Muhammad (s.a.w.w.).

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). Abdu bin Hamid, Ibnu Mundhir na Ibnu Abi Hatim wameandika kutoka kwa Mujahid kwamba alisema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib, yeye alitoa sadaka ya dinari kisha akasema siri na Mtume (s.a.w.w.) na alimuuliza mambo kumi, ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka.).”108 Said bin Mansur ameandika kutoka kwa Mujahid kwamba alisema: “Ilikuwa anayesema siri na Mtume ni lazima atoe sadaka ya dinari, na wa awali aliyetekeleza hilo ni Ali bin Abu Talib, kisha ndipo ikateremka ruhusa: “…..na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” 108 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 185. 88

Page 88


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Abdu bin Hamid ameandika kutoka kwa Salmah bin Kuhayli kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu”: kuwa wa kwanza aliyeifanyia kazi ni Ali bin Abu Talib, kisha ikafutwa.

SURAT TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…..Basi Mwenyezi Mungu ni mlinzi wake, na Jibril na waumini wema na Malaika….” (Sura Tahrim: 4). Ibnu Abi Hatim ameandika kutoka kwa Ali kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema kuhusu ‘’Na waumini wema’’ kwamba ni Ali bin Abu Talib.109 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Asmau binti Umaysi kwamba alisema: “Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema: ‘’Na waumini wema’’ ni Ali bin Abu Talib.’” Said bin Mansur, Abdu Hamid na Ibnu Mundhir wameandika kutoka kwa Alau bin Ziyad kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: ‘’Na waumini wema’’ ni Ali bin Abu Talib (a.s.).

SURAT AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Sura al-Haqqah: 12). Said bin Mansur, Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir, Ibnu Abi Hatim na Ibnu Mardawayhi wameandika kutoka kwa Makhul kwamba alisema: 109 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 244. 89

Page 89


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ilipoteremka Aya hii: “…..na sikio lisikialo lisikie,” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: ‘’Nilimwomba Mwenyezi Mungu alifanye hivyo sikio la Ali.’’ Makhul anasema: Ali alikuwa akisema: “Sikusikia kitu chochote toka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kisha nikakisahau.”110 Ibnu Jarir, Ibnu Abi Hatim, al-Wahidiy, Ibnu Mardawayhi, Ibnu Asakir na Ibnu Najari wameandika kutoka kwa Burayda kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusogeze karibu nisikutenge mbali, na nikuelimishe nawe usikie vilivyo. Na Mwenyezi Mungu amehakikisha unasikia vilivyo.” Ndipo ikateremka Aya hii. Abu Naim ameandika ndani ya al-Hilyah kutoka kwa Ali kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali! Hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniamuru nikusogeze karibu na nikuelimishe nawe usikie vilivyo, ndipo ikateremka Aya hii: “…..na sikio lisikialo lisikie.” hivyo wewe ndio sikio lisikialo vilivyo elimu yangu.”

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat alInsan: 8-9). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kuhusu kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” Kwamba iliteremka kwa ajili ya Ali bin Abu Talib na Fatima binti ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.).111 110 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 360. 111 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 299. 90

Page 90


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-BAYYINA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” (Surat al-Bayina: 7). Ibnu Asakir ameandika kutoka kwa Jabir bin Abdillah kwamba alisema: Tulikuwa kwa Mtume na ndipo ghafla akaja Ali bin Abu Talib, Mtume akasema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakika huyu na Shia wake ndio wenye kufuzu Siku ya Kiyama.” Ndipo ikateremka: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” Basi masahaba wa Mtume wakawa atokeapo Ali husema: Amekuja kiumbe bora kushinda wote.112 Ibnu Adi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Ilipoteremka: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema kumwambia Ali: “Ni wewe na Mashia wako, Siku ya Kiyama mtakuja na hali mmeridhia nanyi mmeridhiwa.” Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ali kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu aliniambia: “Hivi hujasikia kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wale walioamini na kutenda mema, hao ndio wema wa viumbe.” Ni wewe na Mashia wako, ahadi yangu mimi na nyinyi ni kukutana kwenye Hodhi.

112 Ad-Durul-Manthur Juz. 6 Uk. 379. 91

Page 91


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT NASRI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Utakapofika msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi.” (Sura Nasri: 1 ). Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alipofika kutoka Vita vya Hunayni ilimteremkia Aya hii, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Ali bin Abu Talib! Na ewe Fatima binti Muhammad! Msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi vimefika, na nimeona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi.”113 Tabarani ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu alipofika kutoka Vita vya Hunayni ilimteremkia Aya hii: “Utakapofika msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi.” ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Ali bin Abu Talib! Na ewe Fatima binti Muhammad! Msaada wa Mwenyezi Mungu na ushindi vimefika na nimeona watu wakiingia katika dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi. Ametakasika Mola wangu Mlezi na kila sifa njema ni Yake na ninamuomba sana maghufira, hakika Yeye ni Mwenye kupokea toba. Ewe Ali! Lau ningekuwa namweka yeyote awe khalifa baada yangu basi yeyote asingekuwa na haki (ya ukhalifa huo) kuliko wewe,114 hiyo ni kutokana na ukaribu wako na Uislamu, ukaribu wako na Mtume wa 113 Ad-Durul-Manthur Juz. 6, Uk. 407. 114 Nasema: Ni wazi kwamba ziada hii ni nyongeza kutoka kwa wale wenye chuki na Ahlul-Baiti (a.s.), wale ambao kwa juhudi zao zote wamejitahidi kujaribu kuuondoa ukhalifa na uwasii toka kwa Imam Ali na hivyo wakadai kwamba eti Mtume hakuacha Wasii, alifariki bila kuusia. Lakini ukweli ni kama ulivyokwishatambua hapo mwanzo kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliusia ukhalifa kwa Ali na Siku ya Ghadir alimsimika rasmi mbele ya macho ya waumini, na kwa kinywa cha kheri, ulimi wa ukweli na matamshi ya Wahyi akasema: “Yule ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi huyu Ali ni mwenye mamlaka juu yake.”. 92

Page 92


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), ukwe wako, na kwako ndiko aliko mwanamke bora kushinda wote wa ulimwenguni.”115

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA AL-BARUSAWI, INAYOITWA TAFSIR RUHUL-BAYAN FI TAFSIRIL-QUR’AN BISMILAHI RAHMAN RAHIM Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye kurehemu Ukisema: Kuna hekima gani Mwenyezi Mungu kufungua Kitabu chake kwa herufi Bau na si kwa herufi nyingine yeyote? Jibu: Hakika kuna hikma kumi katika hilo la Mwenyezi Mungu kufungua Kitabu chake kwa herufi Bau.116 Ya Tisa: Hakika Bau ni herufi iliyokamilika kimaana yenyewe, kwani ni herufi inayoonyesha, mwambatano, msaada na usaidizi. Inakamilisha maana ya tamko lingine pale inapolifanya jina la mbele liwe na Jari na lichukue sifa yake (Bau). Nayo ina hadhi na heshima ya juu kutokana na kule kulikamilisha tamko lingine kwa kutoa maana ya Tauhidi na mwongozo, kama alivyoashiria Sayiduna Ali kwa kusema: “Mimi ni nukta chini ya herufi Bau.” Hivyo Bau ina cheo cha kuongoza na kuelekeza katika Tauhidi.117 115 Nimemaliza mchakato wa tafsiri hii siku ya tano ya Mfunguo nne wa Mwaka 1421 A.H. katika Jiji la Qum Takatifu. 116 Tumeichagua ya kumi kwa kuwa ndio inayohusu mazungumzo yetu. 117 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 1 Uk. 7.

93

Page 93


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na ambao huamini uliyoteremshiwa wewe, na yaliyoteremshwa kabla yako, na Akhera wakiisadiki.” (Surat Al-Baqarah: 4). Hakika mwenye kuvuka udhalili wa kizuizi cha dunia hupata utukufu wa kusadikisha mambo ya Akhera na huwa anayaamini bila hata kuyashuhudia kwa macho, hivyo huwa ni mwenye yakini baada ya kuondoa kizuizi, kama alivyosema Amirul-Muuminina Ali (a.s.): “Lau kizuizi kikiondolewa sintazidisha ila yakini.”118 Amesema: Tambua hakika sifa zinazomfanya mtu astahili kulaaniwa ni tatu. Baadhi yao wamesema kwamba Yazid amelaaniwa kutokana na ukafiri wake kuwa mashuhuri na kuenea kwa fedheha ya uovu wake pale alipokufuru pale alipoamuru Husein auwawe. Na pale aliposema huku akinywa pombe: “Ikiwa siku moja itaharamishwa na dini ya Muhammad basi ichukue kupitia dini ya Masihi mwana wa Mariam.” Wameafikiana kwamba inaruhusiwa kuwalaani wale waliomuuwa Husein, au aliyeamuru, au kuruhusu au kuridhia, kama alivyosema Taftazaniy: “Ukweli ni kwamba ridhaa ya Yazid juu ya kumuuwa Husein, furaha yake na kuwadhalilisha kwake Ahlul-Bait (a.s.) ni jambo mashuhuri kimaana ijapokuwa undani wake umetufikia kwa njia ya riwaya zisizokuwa mutawatiri. Sisi hatuna shaka na mambo yake bali na imani yake, laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na juu ya wasaidizi wake na wafuasi wake. Na Sahib bin Ubbad alipokuwa akinywa maji baridi husema: ‘Kiini cha 118 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 1 Uk. 42. 94

Page 94


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 ubaridi ni katika maji matamu, ambayo hutoa shukurani toka katika kina cha moyo.’ Kisha husema: ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Anza upya kumlaani Yazidi.”119 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii waliyoyatoa masimbulizi wala udhia, hao wana malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” (Sura Al-Baqarah: 262). Imepokewa kwamba Hasan bin Ali (a.s.) alitamani chakula hivyo akauza kanzu ya Fatima kwa dirhamu sita, muombaji akamwomba naye akampa. Kisha akakutana na mtu anauza ngamia akamnunua kwa mali kauli, kisha akamuuza kwa mtu mwingine, na Hasan alipotaka kumpelekea thamani yake yule aliyemuuzia kwa mali kauli hakumkuta. Ndipo akasimulia kisa kwa Mtume (s.a.w.w.), Mtume akasema: “Ama muombaji alikuwa ni Ridh’wan, Muuzaji alikuwa ni Mikail, ama Mnunuzi alikuwa ni Jibril.” Ndipo ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu: “Wale wanaotoa mali zao katika njia ya Mwenyezi Mungu, kisha hawafuatishii waliyoyatoa masimbulizi wala udhia, hao wana malipo yao kwa Mola wao Mlezi, wala haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.”120

119 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 1 Uk. 179. 120 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz.3 Uk. 419 95

Page 95


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Sura Aali Imran: 37). Mwandishi wa tafsiri hii anasema: “Katika Aya hii kuna dalili juu ya ruhusa ya kuwakirimu mawalii, …….imepokewa kutoka kwa Mtume kwamba Mtume alizidiwa na njaa zama za ukame na ndipo Fatima akamzawadia vipande viwili vya mkate na finyango ya nyama ambapo alimpa kipaumbele kabla ya nafsi yake mwenyewe, lakini Mtume alimrudishia Fatima na kusema: “Chukua ewe mwanangu mpendwa.” Alipofunua bakuli alilikuta limejaa mikate na nyama, ndipo Fatima akapigwa na butwaa na akatambua kuwa kimeteremka toka kwa Mwenyezi Mungu. Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Umetoa wapi hivi?” Akajibu: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Mtume akamhimidi Mwenyezi Mungu na kusema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya kifani wa seyida wa wana wa Israel (Mariam).”]

96

Page 96


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kisha Mtume (s.a.w.w.) akawakusanya Ali, Hasan na Husain. Akala Mtume na Ahlul-Baiti wake wote kwa pamoja mpaka wakashiba na chakula kikabaki kama kilivyokuwa kikiwa kimejaa. Ndipo Fatima akawagawia majirani zake wote.121 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Sura Aali Imran: 42). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wanawake bora ulimwenguni ni Maryam, Fatima, Khadija na Asia.” Ni Hadithi Hasan inaoana na Aya. Na kutoka kwa Anas amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Yakutosha kati ya wanawake wa ulimwenguni: Maryam binti Imran, Khadija binti Khuwaylid, Fatima binti Muhammad na Asia mke wa Firaun.”122 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake 121 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz.3 Uk. 29. 122 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz.3 Uk. 33 97

Page 97


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Imepokewa kwamba wakristo wa Najran walipoitwa kwenye maapizano walisema mpaka tutafakari. Walipoachana wakamwambia Aqib: “Unaonaje?” Akasema: Wallahi enyi wakristo mmeshaujua kwamba Muhammad ni Nabii aliyetumwa na bila shaka amewajieni na hoja yakinifu kuhusu mtu wenu (Yesu), wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Nabii kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Na kama mtafanya hivyo bila shaka mtaangamia, hivyo hakuna cha kufanya ila ni nyinyi kuendelea kubakia katika imani yenu na dini yenu, nendeni mkamuage mtu huyu na mrejee nchini kwenu. Ndipo kesho yake wakaja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na Mtume akatoka akiwa amemkumbatia Husein na amemshika mkono Hasan huku Fatima akitembea nyuma yake na Ali akiwa nyuma ya Fatima. Akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Askofu wao akasema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia, na wala juu ya uso wa ardhi hatobaki mkristo yeyote mpaka Siku ya Kiyama.” Wakasema: Ewe Abul-Qasim! Tumeona tusiapizane na wewe na tukuwache uendelee kuwa katika dini yako nasi tuendelee kubaki katika dini yetu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: Mkikataa kufanya maapizano basi msilimu mtapata haki waliyonayo waislamu na mtawajibikiwa na yale yaliyo wajibu kwa waislamu. Wakakataa, ndipo Mtume akawaambia: “Basi hakika mimi nitawapiga.” Wakasema: “Hatuna nguvu ya kupigana vita na waarabu, lakini sisi tunafanya suluhu na wewe usitushambulie kivita na wala usitufukuze na wala usitutoe katika dini yetu…...” 98

Page 98


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ambao hutoa katika raha na katika shida na wenye kujizuia na ghadhabu na wenye kuwasamehe watu, na Mwenyezi Mungu hupenda wafanyao wema.” (Sura Aali Imran:134). Imesimuliwa kwamba mtumishi alikuwa amesimama juu ya kichwa cha Husain bin Ali (a.s.) naye (a.s.) akiwa pamoja na wageni wake katika meza ya chakula, ndipo bakuli lililokuwa mikononi mwa mtumishi likamdondokea Hasan (a.s.). mtumishi akasema: “na wenye kuwasamehe watu,” Hasan (a.s.) akasema: “Nimeshakusamehe.” Mtumishi akasema: “Mwenyezi Mungu hupenda wafanyao wema.” Hasan (a.s.) akasema: “Uko huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na ninakuoza fulani.”123

SURAT AL-MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wale waliokufuru na kuzikadhibisha Aya zetu, hao ndio watu wa Motoni.” (Sura al-Maida: 10). Amesema: “Itakapofika Siku ya Kiyama bendera ya Mashuhadaa atakabidhiwa Ali, na kila Shahidi atakuwa chini ya bendera yake, na kila aliyeuawa pasi na haki atakuwa chini ya bendera ya Husain bin Ali, na hiyo ndio kauli ya Mwenyezi Mungu: “Siku tutakayowaita kila watu na Imam wao.”124 123 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 4 Uk. 95. 124 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 6 Uk. 360. 99

Page 99


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-AN’AAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na tukampa Is’haka na Yakub, wote tukawaongoza, na Nuh tulimwongoza zamani na katika kizazi chake, Daud na Sulaiman na Ayub na Yusuf na Musa na Harun. Na hivyo ndivyo tuwalipavyo wafanya wema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (Sura An’aam:84 - 85). Na katika kumtaja Isa ni dalili ya kwamba kizazi kinapitia watoto wa binti, hivyo Hasan na Husain ni miongoni mwa kizazi cha Bwana wa Mitume Muhammad (s.a.w.w.) japokuwa ni kwa nasaba ya mama. Na atakayewaudhi hao wawili bila shaka amekiudhi kizazi chake (s.a.w.w.). Fakiri125 anasema: “Ikiwa nasaba ya upande wa mama ni sahihi na inakubalika basi yule ambaye usharifu wake ni kupitia umamani naye anakubalika, kama ilivyo kwa yule mwenye kupitia upande wa baba. Hivyo kigezo (katika usharifu) ni nasaba yake kukomea kwa ima Hasan au Husain, kwa upande wowote ule (sawa uwe mama au wa baba).”126

125 Mwandishi wa Tafsiru Ruhul-Bayan 126 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 7 Uk. 61. 100

Page 100


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AARAF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wakamuuwa yule ngamia na wakaasi amri ya Mola wao Mlezi na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.” (Sura Aaraf: 77). Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Ewe Ali hivi wajua ni nani muovu kuliko wote waliotangulia?” Akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiye ajuaye.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ni yule aliyemchinja ngamia.” Kisha akasema: “Hivi wajua ni nani muovu kuliko wote watakaokuja?” Akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiye ajuaye.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ni yule atakayekuuwa wewe.”127

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Kama ilivyopokewa ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimpa uongozi wa Hija ya mwaka wa ukombozi wa Makka Itab bin Usaydi, na katika msimu huo walihiji waislamu na mushrikina pamoja, hivyo ulipowadia mwaka wa tisa Mtume alimpeleka Abu Bakr awe kion127 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 8 Uk. 195. 101

Page 101


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 gozi wa msimu wa Hija. Alipotoka Abu Bakr kuelekea Makka Mtume alimtumia Ali akiwa amepanda Adhbau128 ili aende kuwasomea Sura Baraa mahujaji. Akaambiwa (s.a.w.w.): “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! ungemtumia Sura hiyo Abu Bakr.” Akasema: “Hafikishi kwa niaba yangu ila mtu atokanaye na mimi.” Hiyo ni kwa sababu ada ya waarabu ni kwamba hawakilishi kabila katika uandishi au uvunjaji wa mkataba ila yule aliye chifu wa kabila hilo au mtu atokanaye na chifu wao au aliye ndugu wa chifu wao. Hivyo akamtuma Ali ili kuondoa dhana hiyo….129

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“…na zitakuwako umma tutakazo zistarehesha, kisha zitawashika kutoka kwetu adhabu zenye kuumiza.” (Sura Hud: 48). Amesema katika kitabu Uqad-Durar: “Ole wake muuwaji wa Husain vipi itakuwa hali yake pamoja na wazazi wake na babu yake.” Kisha akasoma shairi akisema: Lazima Fatima atafika Siku ya Kiyama na hali gauni lake likiwa limetapakaa damu ya Husain. Ole wake yule ambaye waombezi wake ndio mahasimu wake, na baragumu litapulizwa Siku ya Kiyama. Na katika Hadithi imesemwa: “Muuwaji wa Husain atakuwa katika sanduku la Moto na atapata nusu ya adhabu ya watu wa duniani.”130 Imepokewa kutoka kwa Sha’abiy kwamba: Ali (a.s.) alipita huko Karbala alipokuwa akielekea kwenye Vita vya Siffin, akasimama na akauliza jina 128 Jina la ngamia wa Mtume 129 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 10 Uk. 383. 130 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 12 Uk. 143. 102

Page 102


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 la eneo hilo, wakamwambia linaitwa Karbala. Akalia sana mpaka ardhi ikalowana kwa machozi yake, kisha akasema: “Niliingia kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) nikamkuta akilia. Akaniambia: ‘Punde tu Jibril alikuwa nami hapa na akanipa habari kwamba mwanangu Husain atauawa pembezoni mwa Mto Furati katika eneo linaloitwa Karbala. Kisha Jibril akatoa ukufi wa udongo na kuninusisha, ndipo sikuweza kuyazuia macho yangu mpaka yalipotoa machozi.’” Na imepokewa kwamba udongo huo Mtume wa Mwenyezi Mungu aliuweka katika chupa na akamwambia Ummu Salama: “Hakika huu ni udongo wa eneo la ardhi ambayo hapo atauawa Husain, hivyo pindi utakapouona umegeuka damu tambua kuwa ameuawa.” Ummu Salama alisema: “Ulipofika usiku ambao aliuawa Husain nilimsikia msemaji akinadi: ‘Enyi mliomuuwa Husain kwa ujahili, jibashirieni adhabu na udhalili. Mmelaaniwa kwa ulimi wa mwana wa Daud, Musa na aliyekuja na Injili.’131 Nikalia na nikatizama chupa nikakuta udongo umegeuka damu.” Imeelezwa pia kwamba mbingu ilipatwa na wekundu kutokana na kuuawa kwake. Ibnu Sirin amesema: “Wekundu ambao huwa kwenye mawingu haukuwepo hapo kabla mpaka pale alipouawa Husain, na hekima yake ni kama alivyosema Ibnu al-Jawziy kwamba: Hakika ghadhabu zetu husababisha wekundu usoni, na Haki (Mwenyezi Mungu) hana mwili, hivyo kupitia wekundu wa mawingu akadhihirisha ghadhabu yake juu ya yule aliyemuuwa Husain. Amefanya hivyo ili kudhihirisha ukubwa wa jinai. Na Siku hiyo aliyouawa hakuna jiwe lililoinuliwa duniani ila chini yake kulikutwa damu nzito.”132 Abu Shaykhi ameandika kwamba: Hakika kuna kundi la watu lilikumbushana kwamba hakuna yeyote aliyesaidia kuuawa Husain ila alisibiwa 131 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 12 Uk. 144. 132 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 12 Uk. 144. 103

Page 103


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 na balaa kabla ya kufariki kwake. Mzee mmoja akasema: ‘Mimi nilisaidia na sijapatwa na chochote.’ Ndipo aliposimama kwenda kutengeneza taa na ghafla akaanza kuwaka moto huku akipiga kelele ‘moto moto moto’, akajidumbukiza katika Mto Furati, lakini pamoja na hilo aliendelea kuwaka mpaka akafariki. Wengine walipatwa na kiu kali, ikawa wanakunywa wawezavyo lakini kiu haitulii. Wengine waliadhibiwa kuuawa au upofu au kusawijika uso au kunyang’nywa utawala baada ya muda mchache tu, na mengineyo kama hayo. Hivyo baada ya kuyajua hayo jiepushe na wale wanaowafanyia uadui Ahlul-Baiti, na wala usiwe rafiki yao, kwani kufanya nao urafiki ni kuwafanyia uadui Ahlul-Baiti na ni kuwachukia.133

SURAT AR-RAA’D Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Sura ar-Raad: 7). Mwonyaji ni Muhammad, na kiongozi wa kuwaongoza ni Ali. Hoja juu ya hilo ni kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Wallahi Mwenyezi Mungu kumuongoza mtu mmoja kupitia wewe ni bora kwako kuliko kuwa na ngamia mwekundu.”134 Na Tabarani ameandika kwamba Ali alimwambia Fatima (a.s.): “Nabii wetu ndio Nabii bora kushinda Manabii wote naye ni baba yako. Shahidi wetu ndiye shahidi bora kushinda mashahidi wote naye ni ami ya baba yako Hamza. Na kutoka kwetu amepatikana aliye na mbawa mbili anazorukia peponi atakavyo, naye ni mwana wa ami ya baba yako Ja’far. Na kutoka kwetu wamepatikana watoto wa umma huu Hasan na Husain, nao ni watoto wako. Na kutoka kwetu atapatikana al-Mahdi.”135 133 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 12 Uk. 144. 134 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 13 Uk. 346. 135 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 13 Uk. 346. 104

Page 104


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Kama mngezimiliki hazina za rehema ya Mola wangu Mlezi, hapo lazima nyinyi mngelizizuia kwa kuogopa kuzitumia, na mwanadamu ni mchoyo sana.” (Surat Israi: 100). Imepokewa kwamba Zainul-Abidin (a.s.) alikutana na mtu, ndipo mtu yule akaanza kumtukana. Watumwa wake wakakasirika na kutaka kumwadabisha, Zainul-Abidina akawaambia: “Mwacheni mtu huyu.” Kisha akamgeukia na kumwambia: “Yaliyositiriwa miongoni mwa mambo yetu ni mengi, je una haja yoyote tukusaidie?” mtu yule akaona aibu, basi Zainul-Abidina akamvulia kishamia chake na kumpa, na akaamrisha apewe dirhamu elfu moja. Basi tangu siku ile mtu yule akawa akisema: “Nashahidilia kwamba hakika wewe ni miongoni mwa watoto wa mitume, wala aliyepotezwa hadhani kwamba wao walikuwa ni watu wa dunia wenye kuzalisha humo mali, bali ni kwamba walikuwa wakarimu na wenye muruwa, dunia ilikuwa ikiwafuata nao wanaitoa kwa ajili ya kesho, na kwao wao ndipo inaposadikika kauli ya msemaji: ‘Na wao hutoa mali mwanzo wa utajiri na wanatanguliza subira mwisho wa ufakiri. Mgeni afikapo mtaani humkirimu, hivyo hutamjua ni yupi mkata kati yao na ni yupi tajiri.”’136

136 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 15 Uk. 207. 105

Page 105


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT KAHFI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi wakamkuta mja katika waja wetu, tuliyempa rehema kutoka Kwetu, na tuliyemuelimisha elimu kutoka Kwetu.” (Surat Kahfi: 65). Elimu ya siri ni sawa na mlango kwenye nyumba, na anayetaka kuingia ndani ya nyumba ni wajibu juu yake kupita mlangoni, na Jumba la elimu na Jiji lake ni Mtukufu Nabii (s.a.w.w.), na lango la Jumba hili na la Jiji hili ni Ali (a.s.) kama alivyosema Mtume (s.a.w.w.): “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.”137

SURAT TWAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Twaha.” (Sura Twaha: 1). Imam Ja’far as-Sadiq (a.s.) amesema: “Twaha ni kuapa kupitia utakaso wa Ahlul-Baiti na uongofu wao, kama alivyosema Mwenyezi Mungu: “Na kuwatakaseni kabisa.” (33:33)”138

SURAT HAJJ Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Anayedhani ya kwamba Mwenyezi Mungu hatamnusuru (Mtume) katika dunia na akhera, basi afunge kitanzi juu kisha ajinyonge, na aone je, hila yake yaweza kuyaondoa yale yaliyomghadhibisha?” (Sura Hajj: 15). 137 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 15 Uk. 272. 138 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 16 Uk. 361. 106

Page 106


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Imepokewa kutoka kwa Anas bin Malik kwamba alisema: “Kuna myahudi alikuja baada ya kufariki Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na akaingia msikitini na kusema: “Yuko wapi Wasii wa Muhammad?” hadhirina wakamwashiria kwa Abu Bakr, akasema: “Nakuuliza kuhusu mambo ambayo hayajui ila Nabii au Wasii wa Nabii.” Abu Bakr akasema uliza utakalo. Yahudi akasema: “Nieleze ni lipi asilolijua Mwenyezi Mungu, na lisilokuwa la Mwenyezi Mungu, na lisilokuwepo kwa Mwenyezi Mungu?” Abu Bakr akasema: “Akasema haya ni maneno ya wapagani.” Yeye na waislamu waliyokuwepo hapo wakamjia juu. Ibnu Abbas akasema: “Hamjamtendea haki mtu huyu ikiwa mnalo jibu lake, na kama hamna la kumjibu basi nendeni kwa yule atakayemjibu, kwani hakika mimi nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema kumwambia Ali (a.s.): ‘Ewe Mwenyezi Mungu upe nguvu moyo wake na uimarishe ulimi wake.’” Ndipo Abu Bakr na waliokuwa wamehudhuria hapo wakasimama na kumwendea Ali na wakamweleza hayo. Ali akasema: “Ama asilolijua Mwenyezi Mungu ni ile kauli yenu enyi Mayahudi ‘Hakika Uzayru ni mtoto wa Mwenyezi Mungu.’ Mwenyezi Mungu hajui kwamba ana mtoto. Ama lisilokuwa la Mwenyezi Mungu ni kwamba Yeye hana mshirika. Na ama lisilokuwepo kwa Mwenyezi Mungu ni kwamba kwa Mwenyezi Mungu hakuna uonevu wala ajizi.” Yahudi akasema: “Nashahidilia kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na hakika wewe ni Wasii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu.” Waislamu wakafurahi kwa hilo.139

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na 139 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 17 Uk. 14. 107

Page 107


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 kuwatakasa kabisa kabisa.” (Surat Ahzab: 33). Siku moja Mtume alitoka akiwa amejifunika shuka lililodariziwa kwa manyoya meusi, kisha akaketi. Akaja Fatima akamwingiza katika shuka hilo, kisha akaja Ali akamwingiza katika shuka hilo, kisha wakaja Hasan na Husain nao akawaingiza katika shuka hilo, kisha akasema: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume. Watu wa kishamia ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na binti yake na al-Murtadha (Ali), kisha ni watoto zake wawili pindi walipokusanyika.”140 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Surat Ahzab: 56). Ka’bi bin Ajrah, amesema: Ilipoteremka: “Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” tulisimama na kumwambia: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ni ipi namna ya kukusalia? Mtume akasema: ‘’Semeni: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ??????? ???? ?? ??????? ???? ???? ????. “Ewe Mwenyezi Mungu! Mpe rehma na amani Muhammad na aali Muhammad kama ulivyompa rehma na amani Ibrahim na aali Ibrahim. Hakika wewe ni Mhimidiwa Msifiwa.”141 140 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 22 Uk. 171. 141 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 22 Uk. 225. 108

Page 108


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Na katika Hadithi Mtume alisema: “Hakuna dua yoyote ila kati yake na Mwenyezi Mungu kuna kizuizi, mpaka pale atakapomsalia Muhammadi na Aali Muhammad. Likitekelezwa hilo ndipo kizuizi huondoka na dua kupita, na lisipotekelezwa hilo dua hurejea.”142 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Muogopeni Mwenyezi Mungu na semeni maneno ya sawa.” (Surat Ahzab: 70). Imeelezwa kwamba: “Hakika Yakub mtoto wa Is’haq aliyejulikana kwa jina la Ibnu Sikit ambaye ni miongoni mwa ulamaa wakubwa wa lugha ya Kiarabu, siku moja alikuwa ameketi na al-Mutawakil, ghafla akaja alMuutazu na al-Muayad watoto wa al-Mutawakil, akasema al-Mutawakil: “Ni yupi umpendaye sana, ni wanangu wawili au Hasan na Husain?” Ibnu Sikit akasema: “Wallahi hakika Qanbar mtumishi wa Ali (a.s.) ni bora kushinda wewe na kushinda watoto wako.” al-Mutawakil akasema: “Ng’oeni ulimi wake toka kinywani mwake.” Wakafanya hivyo na akawa amefariki usiku huohuo.143

SURAT ZUMARA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Mwenyezi Mungu amekupigieni mfano wa mtu mwenye washirika wanaogombana, na wa mtu mwingine aliyehusika na mtu mmoja, je wako sawa katika hali? Alhamdulillahi! Lakini wengine wao hawajui.” (Sura Zumar: 29). 142 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 22 Uk. 230. 143 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 22 Uk. 248. 109

Page 109


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Hasan na Husain (a.s.) walikuwa wakicheza mikononi mwa Mtume (s.a.w.w.), naye akavutiwa nao. Jibril akamjia akiwa na chupa na karatasi, na ndani ya chupa mlikuwa na damu na ndani ya karatasi mkiwa na sumu. Akasema: “Ewe Muhammad je wawapenda hawa, basi tambua kuwa mmoja wao atauwawa kwa upanga na hii ndio damu yake, na mwingine atanyweshwa sumu na hii ndio sumu yake, ghafla akaondoa moyo wake kwa watoto na kuuelekeza moja kwa moja kwa Mwenyezi Mungu….”144 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Sema: Ewe Mola Mlezi! Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana, wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.” (Sura Zumar: 46). Rabi’u alikuwa miongoni mwa wanahadithi, alikuwa hazungumzi ila lile linalomhusu yeye, basi alipouawa Husain wakasema sasa atazungumza, ndipo akasoma: “Sema: Ewe Mola Mlezi! Muumba wa mbingu na ardhi, Mjuzi wa yasiyoonekana na yanayoonekana, wewe utahukumu baina ya waja wako katika yale waliyokuwa wakikhitilafiana.” Na imepokewa kwamba alisema: “Ameuawa yule ambaye Mtume alikuwa akimkalisha mapajani mwake na akiweka ulimi wake ndani ya kinywa chake.”145

144 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 23 Uk. 104. 145 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 24 Uk. 120. 110

Page 110


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT GHAFIR Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na akasema mtu muumini aliyekuwa mmoja wa watu wa Firaun anayeficha imani yake; je, mtamuuwa mtu kwa sababu tu anasema Mola wangu Mlezi ni Mwenyezi Mungu?” (Sura Ghafir: 28). “Watatu hawajamkufuru Mwenyezi Mungu katu hata kidogo: Ezekiel Muumini toka aali Firaun, Habibu Najjari muumini toka aali Yasin, na Ali bin Abu Talib naye ndiye mbora wao.”146

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” (Surat as-Shura: 23). Imepokewa kwamba: Ilipoteremka palisemwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) ni akina nani hawa ndugu ambao ni imewajibishwa juu yetu kuwapenda. Akasema: “Ali, Fatima na wanangu Hasan na Husain.” Na hilo linathibitishwa na ile riwaya iliyopokewa kutoka kwa Ali kwamba: “Nilimshitakia Mtume wa Mwenyezi Mungu kuhusu husuda za watu dhidi yangu. Akasema: ‘Hivi huridhii kuwa wa kwanza kuingia Peponi.

146 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 24 Uk. 176. 111

Page 111


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mimi, Wewe, Hasan, Husein.�147 Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni shahidi. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ameghufuriwa. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ametubia. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali ni muumni aliyekamilika kiimani. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amekufa na hali malaika ameshambashiria Pepo, kisha Munkar na Nakir. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad atasindikizwa Peponi kama biharusi asindikizwavyo kwenda nyumbani kwa mumewe. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atamfungulia milango miwili ya Pepo kaburini. Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad Mwenyezi Mungu atawafanya malaika wa rehema wawe wenye kulizuru kaburi lake. 147Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 25 Uk. 312. 112

Page 112


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ehe! atakayekufa na hali awapenda aali Muhammad basi amefia ndani ya Sunna. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad atakuja Siku ya Kiyama na hali imeandikwa baina ya macho yake mawili: Amekata tamaa na rehema za Mwenyezi Mungu. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad basi amekufa na hali ni kafiri. Ehe! atakayekufa na hali awachukia aali Muhammad hatoipata harufu ya Pepo.”148

SURAT AZ-ZUKHRUF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na akalifanya neno hili liwe lenye kubaki katika kizazi chake ili warejee.” (Sura az-Zukhruf: 28). Baadhi wamesema kuhusu sababu ya kusema ‘Karamallahu Wajhahu’ pindi atajwapo Ali bin Abu Talib (a.s.), ni kwamba imepatikana nukuu kutoka kwa mama yake mzazi Fatima binti Asad bin Hashim kwamba kila alipokuwa akitaka kulisujudia sanamu wakati akiwa na mimba yake, Ali alikuwa akimzuia kufanya hivyo (akiwa angali tumboni).149

148 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 25 Uk. 312. 149 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 25 Uk. 364. 113

Page 113


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AL-FAT’HU Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu…..” (Sura al-Fat’hu: 29). Imam Zaynul-Abidina ambaye ni Ali bin Husain bin Ali (a.s.) alikuwa akiitwa: Mwenye sugu (sagamba). Na alikuwa na miti mia tano ya mizaituni, alikuwa akisali chini ya kila mti mmoja rakaa mbili kila siku. Mshairi akasema: “Nyumba za Ali, Husain, Ja’far, Hamza na Sajadi mwenye sugu”150

SURAT RAHMAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” (Sura Rahman: 19 - 20). Imesemwa kwamba bahari mbili ni Ali na Fatima, na kizuizi ni Mtume (s.a.w.w.), na hutoka kwao hao wawili Hasan na Husein.151

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). 150Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 26 Uk. 58. Ubeti huu ni wa Da’bal al-Khaza’i (Mwenyezi Mungu amrehemu). 151 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 27 Uk. 296. 114

Page 114


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Imepokewa kutoka kwa Ali bin Abu Talib (a.s.) kwamba alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nilikuwa nina dinari nikaichenji kwa dirhamu kumi, hivyo ikawa kila nisemapo siri na Mtukufu Mtume natoa sadaka dirhamu moja. Yaani nilikuwa kila siku nasema siri na Mtume kwa dirhamu moja mpaka siku kumi, na nilikuwa namuuliza kuhusu sifa moja miongoni mwa sifa njema.”152 Ibnu Umar alisema: “Ali alikuwa na mambo matatu, kuwa nalo moja kati ya hayo ni jambo nilipendalo mno kuliko kuwa na ngamia mwekundu: Kuozwa Fatima, kukabidhiwa bendera Siku ya Khaibar na Aya ya kuongea siri na Mtume.”153

SURAT TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Katika kitabu Mishkatul-Maswabihi imeandikwa kwamba: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hotuba na ghafla wakaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuamka, akateremka toka mimbarini akawafuata na kuwachukua na kuwaweka mbele yake, kisha akasema: ‘Mwenyezi Mungu amesema kweli. Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, nilipowaona hawa wawili wakitembea huku wakidondoka sikuweza kuvumilia mpaka nimekatisha mazungumzo yangu na kuwanyanyua.’ Kisha akaendelea na hotuba yake….”154 152 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 28 Uk. 405. 153 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 28 Uk. 40. 154 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 28 Uk. 18. 115

Page 115


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT TAHRIM Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…..Basi Mwenyezi Mungu ni mlinzi wake, na Jibril na waumini wema na Malaika….” (Sura Tahrim: 4). Imepokewa kutoka kwa Mujahid kwamba amesema: Waumini wema ni Ali bin Abu Talib. Fakiri155 anasema: Hiyo inaungwa mkono na kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Ewe Ali! Wewe kwangu mimi una nafasi ya Harun kwa Musa.” Hivyo ikiwa Ali ni sawa na Harun basi yeye ndio mwema mfano wake.156

SURAT NUH Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Ili mtembee humo katika njia zilizo pana.” (Sura Nuh: 20). Amirul-Muuminina Ali (a.s.) alikuwa akisema: “Niulizeni kuhusu njia za mbinguni kwani hakika mimi nazijua zaidi kushinda njia za ardhini.”157

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat al-Insan: 8 - 9). 155 Mwandishi wa tafsiri hii Tafsiru Ruhul-Bayan 156 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 28 Uk. 53. 157Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 29 Uk. 180. 116

Page 116


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: Hasan na Husein walipatwa na maradhi, babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona akiwa pamoja na baadhi ya watu. Wakamwambia Ali: “Ni vizuri lau ukiweka nadhiri kwa ajili ya wanao.” Ali, Fatima na mtumishi wao Fidha wakaweka nadhiri kwamba ikiwa watapona watafunga siku tatu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kutafuta radhi zake na kumshukuru. Wakapona, na wao wakafunga na hali hawana chochote cha kufuturu. Ali akaenda kwa Simon Myahudi wa Khaibari, akakopa toka kwake pishi tatu za ngano. Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano kulingana na idadi yao. Chakula kikawekwa mbele yao wakati wa kufuturu ili wafuturu, mara masikini akafika mlangoni kwao akasema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini miongoni mwa maskini wa kiislamu, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakampa chakula na wakashinda mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Asubuhi wakaamka wakiwa wamefunga, waliposhinda mchana kutwa na kukiweka chakula mbele yao ili waftari, mara akafika mlangoni kwao yatima, akasema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, yatima toka katika watoto wa muhajirana, baba yangu amekufa kishahidi Siku ya Aqabah, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakampa chakula. Asubuhi wakaamka wakiwa wamefunga, waliposhinda mchana kutwa na kukiweka chakula mbele yao ili waftari, mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao, akasema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya unabii, mimi ni mfungwa miongoni mwa wafungwa, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakampa chakula.

117

Page 117


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ilipofika siku ya nne wakiwa tayari wameshatimiza nadhiri yao Ali alimshika Hasan mkono wa kulia na Husein mkono wa kushoto na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na hali wao wawili wakitetemeka kama vifaranga kutokana na ukali wa njaa. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipowatizama alisema: “Hali niionayo yaniumiza mno.” Akasimama na kwenda nao, wakamkuta Fatima akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamebadilika, hilo likamuumiza sana. Ndipo Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Na akamsomea Sura hii.158 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Humo wataegemea viti vya enzi, humo hawataona jua wala baridi.” (Sura Insan: 13). Ibnu Abbas amesema: “Pindi watu wa Peponi watakapokuwa peponi ghafla wataona mwanga kama mwanga wa jua na Pepo imeangazwa kwa mwanga huo. Watasema: Ewe Ridhwan! Mola wetu Mtukufu amesema: “Hawataona jua wala baridi.” hii ni nuru ya nini? Ridhwan atawaambia: “Hili si Jua wala si Mwezi, lakini huyu ni Fatima na Ali wamecheka, na kutokana na nuru ya kicheko chao Pepo imeangaziwa.”159

SURAT SHAMSI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

158 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 29 Uk. 268. 159 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 29 Uk. 270. 118

Page 118


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 “Hapo Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaambia: Ni ngamia wa Mwenyezi Mungu na kinywaji chake. Lakini walimkadhibisha na wakamchinja. Kwa hiyo Mola wao Mlezi aliwaangamiza kwa sababu ya dhambi zao, na akifanya sawa.” (Sura Shamsi: 13 - 14). Katika Hadithi ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali: “Ewe Ali hivi wajua ni nani muovu kuliko wote waliotangulia?” Akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiye ajuaye.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ni yule aliyemchinja ngamia.” Kisha akasema: “Hivi wajua ni nani muovu kuliko wote watakaokuja?” Akasema: “Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiye ajuaye.” Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akasema: “Ni yule atakayekuuwa wewe.”160

AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA ALUSIY, INAYOITWA RUHUL-MA’ANIY FITTAFSIRIL-QUR’AN AL-‘ADHIM WASAB’ULMATHANIY. SURAT AL-BAQARAH Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na katika watu yuko auzaye nafsi yake kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mpole kwa waja.” (Surat Al-Baqarah: 207). Imamia na baadhi ya maulama wetu wamesema kwamba: Iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) pindi Mtume alipomwachia jukumu la kulala juu ya kitanda chake huko Makka pale alipoondoka kwenda Pangoni.161

160 Imeshatangulia riwaya kama hii katika Sura Aaraf Aya ya 77. 161 Tafsiru Ruhul-Bayan Juz. 2 Uk. 83. 119

Page 119


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Wale watoao mali zao usiku na mchana kwa siri na dhahiri, wana ujira wao kwa Mola wao Mlezi; wala haitakuwa hofu juu yao wala wao hawatahuzunika.” (Surat Al-Baqarah: 274). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali (a.s.) alikuwa na dirhamu nne, akatoa sadaka dirhamu moja usiku na nyingine mchana, nyingine siri na nyingine dhahiri.”162

SURAT AALI IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika Mwenyezi Mungu alimchagua Adam na Nuh na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu wote.” (Surat Aali Imran: 33). Imepokewa kutoka kwa Ahlul-Baiti (a.s.) kwamba wao husoma: “Na Aali Muhammad juu ya walimwengu wote.”163

162 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 41. 163 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 116. 120

Page 120


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Kauli ya Mwenyezi Mungu: “…Kila mara Zakariya alipoingia Mihrab hukuta vyakula. Akasema: Ewe Maryam unatoa wapi hivi. Akasema: Vinatoka kwa Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila hesabu.” (Surat Aali Imran: 37). Abu Ya’la ameandika kutoka kwa Jabir bin Abdullah amesema kwamba hakika Mtume (s.a.w.w.) alikaa siku kadhaa bila kula chakula mpaka hali hiyo ikawa nzito juu yake. Akaenda kwenye nyumba za wakeze lakini hakukuta chochote kwao ndipo akaenda kwa Fatima na kumwambia: “Ewe mwanangu mpendwa! Je una chochote ninachoweza kula kwani hakika mimi ni mwenye njaa?” Akamjibu: “Wallahi sina.” Mtume alipotoka, jirani wa Fatima alimletea Fatima vipande viwili vya mkate na finyango ya nyama. Fatima akapokea na kuweka ndani ya bakuli lake, akasema: “Wallahi katika hiki nitampa kipaumbele Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) kabla ya nafsi yangu na kabla ya yule aliyopo kwangu.” Japokuwa wote walikuwa wanahitajia chakula lakini Fatima alimtuma Hasna au Husein aende kumwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) naye alikuja. Fatima akamwambia: “Kwa haki yako na ya mama yangu, Mwenyezi Mungu ameleta kitu nami nimekihifadhi kwa ajili yako.” Akamwambia: “Kilete ewe binti yangu mpendwa.” Nikamletea bakuli na nilipolifunua ghafla nikakuta limejaa mikate na nyama, nilipolitazama nikapatwa na mshangao na nikatambua kuwa ni baraka toka kwa Mwenyezi Mungu. Nikamhimidi Mwenyezi Mungu na nikamkabidhi chakula hicho Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.). Alipokiona alimhimidi Mwenyezi Mungu na akasema: Umetoa wapi hivi ewe binti yangu mpendwa? Akajibu: “Ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu ewe baba yangu mpendwa. Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu. “

121

Page 121


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mtume akamhimidi Mwenyezi Mungu na kusema: “Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu Ambaye amekufanya ewe binti yangu mpendwa kifani wa seyida wa wana wa Israel (Mariam). Kwani hakika yeye alikuwa aruzukiwapo chochote na Mwenyezi Mungu kisha akiulizwa kakipata wapi husema: Hakika Mwenyezi Mungu humpa riziki amtakaye bila hesabu.” Kisha akawakusanya Ali, Hasan na Husein na Ahlul-Baiti wake wote wakala mpaka wakatosheka na chakula kikabaki kama kilivyokuwa, Fatima akawagawia jirani zake.164 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteua na akakutakasa na akakuteua juu ya wanawake wa ulimwenguni.” (Surat Aali Imran: 42). Ibnu Asakir ameandika kupitia moja ya njia zake kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Wanawake bora wa peponi ni Maryam binti Imran, Fatima, Khadija na Asia mke wa Firaun.” Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Fatima (a.s.) kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Wewe ni Seyida wa wanawake wa peponi ila Bikira Maryam.” Makusudio ni kwamba Mariam ni mbora kwa wanawake wa zama zake, na hiyo haipelekei yeye kuwa mbora kuliko Fatima (a.s.). Hilo linaungwa mkono na ile riwaya aliyoiandika Ibnu Asakir kwa njia ya Muqatil kutoka kwa Dhahak kutoka kwa Ibnu Abbas 164 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 124 122

Page 122


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 (a.s.) kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Wanawake wane ni wabora kushinda wanawake wa zama zao: Mariam binti Imran, Asia binti Muzahim, Khadija binti Khuwaylid na Fatima binti Muhammad, na mbora wao kiulimwengu ni Fatima.” Na ile aliyoipokea al-Harthi bin Usama katika Musnad yake kwa sanadi sahihi ijapokuwa ni Hadithi ya Mursal: “Mariam ni mbora kwa wanawake wa zama zake.” Na hii ndio rai ya Abu Ja’far (Imam al-Baqir) na ndio rai mashuhuri kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s.). Rai ambayo naipa kipaumbele mimi ni kwamba Fatima ni bora kushinda wanawake wote waliotangulia na watakaokuja, kwani yeye ni sehemu ya nyama ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), pili ni kutokana na wasifu mwingine ambao hauchafuliwi na Hadithi hizo zilizotangulia hata tuseme kwamba mwingine asiyekuwa yeye ni bora kumshinda…… Na kuanzia hapa ndipo unapojulikana ubora wake juu ya Aisha. Ama wengi wanaokhalifu rai hiyo, hoja yao ni kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Chukueni theluthi ya dini yenu toka kwa Hamayrau (Aisha).” Na kauli yake (s.a.w.w.): “Ubora wa Aisha juu ya wanawake wengine ni sawa na ubora wa mkate juu ya chakula.” Lakini wewe wajua kilichopo katika dalili hizi na ni kwamba hazielezi ubora wowote wa Aisha juu ya Fatima. Kwanza: Cha maana sana kilichomo katika Hadithi hii iwapo tukisema imethibiti ni kwamba yathibitisha kuwa yeye (Aisha) ni msomi hivyo theluthi ya dini inachukuliwa toka kwake, na hii haikanushi uwepo wa elimu mfano wa hiyo kwa kipande cha nyama ya Mtume (s.a.w.w.) (Fatima). Na kutokana na kujua kwake (s.a.w.w.) kwamba Fatima hatobaki muda mrefu ambao watu wataweza kuchukua elimu toka kwake huenda ndio maana hakusema, na laiti angejua (anao muda wa kutosha) angesema: “Chukueni dini yenu yote kutoka kwa Zahra.” 123

Page 123


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Na kutokutamka kauli hii kumhusu mtu ambaye akili na nukuu vyote vimethibitisha elimu yake haimaanishi kwamba yupo aliye bora zaidi yake, la sivyo Aisha angekuwa bora hata kushinda baba yake (Abu Bakr) kwani hakijapokewa chochote kutoka kwake kinachohusu dini ila kitu kichache. Zaidi ya hapo ni kwamba ile kauli ya Mtume (s.a.w.w.): “Hakika mimi ni mwenye kuwaachia vizito viwili kati yenu: Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, havitoachana mpaka vinikute kwenye hodhi,” inachukua nafasi ya ile riwaya ya ubora wa Aisha ambayo kama ilivyo wazi ni nyongeza (riwaya ya uwongo), kwani itawezekanaje iwe hivyo na hali Fatima ndiye Seyida wa kizazi cha Mtume. Pili: Kwa sababu Hadithi ya pili inapingana na zile zinazoonyesha kwamba wengine wasiyokuwa yeye (Aisha) ni bora kushinda yeye (Aisha). Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Ammar bin Sa’d kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Khadija amefanywa bora kushinda wanawake wa umma wangu kama Mariam alivyofanywa bora kushinda wanawake wa ulimwenguni.” Bali Hadithi hii ni dhahiri katika ubora, na inawasifu kamili kwa yule mwenye kutizama kwa akili yake na akajiepusha na ububusa na ulazimishaji. Ama kauli ya mwenye kusema kwamba hakika mabinti wengine wa Nabii ni bora kushinda Aisha, sioni kama ina tatizo. Na kwangu mimi mjadala wa ni nani aliye mbora kushinda wanawake wote wa ulimwenguni ni kati ya Mariam na Fatima tu. Na kutokana na wasifu uliotangulia tayari umeshajua rai yangu ninayoegemea. Imam as-Sabki aliulizwa kuhusu suala hili akasema: “Tunalolichagua na kulifuata ni kwamba Fatima binti Muhammadi ndiye bora kisha mama yake…”165

165 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 137 na Uk. 138.

124

Page 124


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Surat Aali Imran: 61). Kutoka kwa Ibnu Abbas amesema: “Ujumbe wa Wakristo wa Najran ulikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu, nao walikuwa ni watu kumi na wane wakiongozwa na Sayid ambaye alikuwa ndio mkubwa wao, kisha Aqib aliyekuwa akimfuatia kwa ukubwa na ndiye aliyekuwa mwenye uamuzi wa mwisho kwao, Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaambia: “Silimuni.” Wakasema tumeshasilimu. Mtume akawaambia: “Bado hamjasilimu.” Wakasema tumeshasilimu kabla ya kufika kwako. Mtume akawaambia: “Mnasema uongo, kuna mambo matatu yanawazuia kusilimu: Kuabudu kwenu msalaba, kula kwenu nguruwe, na kudai kwenu kuwa Mwenyezi Mungu ana mtoto.” Mwenyezi Mungu akateremsha:

“ “Hakika mfano wa Isa mbele ya Mwenyezi Mungu ni kama mfano wa Adam, alimuumba kutokana na udongo, kisha akamwambia kuwa, basi akawa. Ndiyo haki itokayo kwa Mola wako Mlezi, basi usiwe miongoni mwa wenye kutia shaka. (Surat Aali Imran: 59 - 60). 125

Page 125


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Alipowasomea Aya hiyo wakasema hatujui uyasemayo, ndipo ikateremka:

“Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Surat Aali Imran: 61). Mtume wa Mwenyezi Mungu akawaambia: “Hakika Mwenyezi Mungu ameniamuru ikiwa hamtakubali hili nifanye maapizano nanyi.” Wakasema: “Ewe Abul-Qasim! mpaka turejee na tutafakari jambo hili kisha tutakuja.” Walipoachana na wakasadikishana wao kwa wao, Sayid alimwambia Aqib: “Wallahi mmeshajua kwamba hakika mtu huyu ni Nabii na Mtume, na lau mkifanya naye maapizano basi atawateketeza, wallahi katu hakuna watu walioombeana laana na Mtume kisha mkubwa wao akaendelea kuishi au mdogo wao kuzaliwa. Kama hamtomfuata na mkikataa basi nyinyi endeleeni kubakia katika dini yenu, na nendeni mkamuage mtu huyu na mrejee nchini kwenu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa ametoka akiwa pamoja na Ali, Hasan, Husein na Fatima, akawaambia: “Mimi nitakapokuwa naomba nyinyi muwe mnaitikia.” Ndipo wakakataa kufanya naye maapizano na wakafanya suluhu kwa sharti la kutoa kodi.166 166 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 166 na Uk. 167. 126

Page 126


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Jabir amesema: Mtume alisema: “Naapa kwa Yule Ambaye aliyenituma kwa haki! Lau wangefanya maapizano bonde lao lingeteketea kwa moto.”167 Na imepokewa kwamba Askofu wa Najran alipomuona Mtume wa Mwenyezi Mungu akija akiwa na Ali, Fatima, Hasan na Husein alisema: “Enyi wakristo! Mimi naziona nyuso hizi kama zitamuomba Mwenyezi Mungu auondoe mlima kutoka mahala pake, atauondoa, msiapizane naye mtaangamia.”168 Na katika kadhia hii kuna dalili ya wazi juu ya unabii wake (s.a.w.w.), la sivyo wasingekataa kufanya naye maapizano, na kuna dalili juu ya ubora wa mawalii wa Mwenyezi Mungu na Aali wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, jambo ambalo hana shaka nalo yeyote aliye muumini.169 Muslim, Tirmidhi na weningineo wameandika kutoka kwa Sa’d bin Waqqas kwamba alisema: Ilipoteremka Aya hii: “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Surat Aali Imran: 61), Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husain, akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio watu wa nyumba yangu.”170 Ibnu Abi ‘Allani ambaye ni Muutazila ametoa dalili kupitia kisa hiki kwamba Hasan na Husain (a.s.) walikuwa Mukalafu katika hali hiyo, kwa sababu hairuhusiwi maapizano ila kwa waliobalehe. Kupatikana hali hiyo hakutegemei balehe, kwani ukamilifu unaweza kupatikana kabla yake, bali huenda ukashinda hata ule wa wale waliobale167 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 166 na Uk. 167. 168 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 166 na Uk. 167. 169 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 166 na Uk. 167. 170 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 168. 127

Page 127


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 he, hivyo hakuna kizuizi kinachozuia Hasan na Husain kutokuwa balehe kipindi hicho, isipokuwa tu iwapo ni katika miaka ambayo haiwezekani kwa wao kuwa tayari ni wakamilifu wa akili. Zaidi ya hapo ni kwamba inaewezekana Mwenyezi Mungu akavunja ada kwa hao mabwana hivyo akawapa lile ambalo hakuna mwingine yeyote atakayeshirikiana nao (yaani akawapa akili za utu uzima wangali watoto wadogo – kama ilivyokuwa kwa Nabii Isa alivyoongea akiwa kwenye kitenga cha utotoni), hivyo lau ikisihi kwamba ukamilifu wa akili huwa hauwi katika miaka hiyo, basi inajuzu kuwepo ukamilifu huo kwao kwa ajili ya kuwatofautisha wao na watu wengine, na kwa ajili ya kuwa dalili juu ya nafasi yao kwa Mwenyezi Mungu na umakhususi wao kwake, nao ni kaumu ambayo sifa zilizo makhususi kwao hazihesabiki.171 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu nyote wala msifarakane..” (Surat Aali Imran: 103). Ahmad ameandika kutoka kwa Zayd bin Thabit kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Hakika mimi ni mwenye kuacha kati yenu mirathi mbili: Kitabu cha Mwenyezi Mungu kamba iliyonyooka baina ya mbingu na ardhi, na kizazi changu watu wa nyumba yangu, na hakika hivyo viwili havitaachana mpaka vinikute kwenye hodhi.”172

SURAT NISAI Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wenye kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha Mwenyezi Mungu, miongoni mwa Manabii, na Masidiki, na Mashahidi na Watu wema, na hao ndio marafiki wema.” (Sura Nisai: 69). 171 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 3 Uk. 168. 172Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 4 Uk. 17. 128

Page 128


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Amesema: “Pili: Nafasi ya Masidiki nao ni wale ambao wanaowafuata Manabii (a.s.) katika maarifa, na mfano wao ni sawa na yule anayetazama kwa mbali kitu kilivyo, na hiyo ndiyo aliyomaanisha Ali (a.s.) pale alipoambiwa: “Je umemuona Mwenyezi Mungu?” Akajibu: “Siwezi kumwabudu Mola Mlezi nisiyemuona, macho hayamuoni kwa uono wa macho lakini nyoyo zinamuona kwa imani ya kweli.”173

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu..” (Sura Maida: 3). Imethibiti kwetu kwamba alisema huko174 kuhusu haki ya Ali (a.s.): “Yule ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi Ali ana mamlaka juu yake.” Na akaongeza zaidi ya hapo kama ilivyo katika baadhi ya riwaya.175 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). 173 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 5 Uk. 68. 174 Yaani katika bonde la Ghadir Khum. 175 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 6 Uk. 55. 129

Page 129


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Wanahadithi wengi wamesema kwamba yenyewe iliteremka kwa ajili ya Ali. al-Hakim, Ibnu Mardawayhi na wengineo wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwa sanad yenye kuungana kwamba alisema: Abdullah bin Salam na kundi lake waliokuwa wamemwamini Mtume (s.a.w.w.) walikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), wakasema: ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Hakika nyumba zetu ziko mbali na hatupati wa kuketi nasi wala kuzungumza nasi kinyume na kikao hiki, na hakika jamaa zetu walipoona tumemsadiki Mwenyezi Mungu na Mtume wake wametutenga na wameapa ndani ya nafsi zao kwamba hawataketi nasi, hawatatuozesha na wala hawatasema nasi, na jambo hilo limekuwa zito juu yetu.’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akawaambia: “Hakika Walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake.” Kisha (s.a.w.w.) akatoka na kuelekea msikitini na akawakuta watu wakiwa wamesimama na wengine wakiwa katika rukuu, ndipo akamuona muombaji, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akamuuliza: ‘Kuna yeyote aliyekupa kitu?’ Akajibu ndio, amenipa pete ya fedha. Akamuuliza: ‘Nani?’ Akajibu: Yule aliyesimama. Na akaashiria kwa Ali (a.s.). Mtume akamuuliza: ‘Alikupa akiwa katika hali gani?’ Akajibu: Akiwa katika rukuu. Ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoa takbira kisha akasoma Aya hii. Has?n akasimama na kusoma shairi: “Abul Hasan nafsi yangu ni fidia kwako, roho yangu na kila kizito na chepesi chenye kuelekea katika uongofu. Hivi kweli sifa zako njema zitakwenda bure bila faida, hapana; sifa njema zitokazo kwa Mungu hazipotei bure. Kwani wewe ndiye uliyetoa sadaka ulipokuwa katika rukuu, nafsi yangu ni fidia kwako ewe mwenye rukuu bora kushinda zote. Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha kwako uwalii bora, na akauthibitisha ndani ya Kitabu cha sheria.”176 130

Page 130


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AARAF Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na wakamuua yule ngamia na wakaasi amri ya Mola wao Mlezi na wakasema: Ewe Saleh! Tuletee unayotuahidi ikiwa wewe ni miongoni mwa Mitume.” (Sura Aaraf: 77). Imekuja katika Hadithi kwamba muovu kuliko wote waliotangulia ni yule aliyemchinja ngamia. Na muovu kuliko wote watakaokuja ni yule aliyemuua Ali (a.s.). Hilo ndilo Mtume alilomweleza Ali (a.s.). na kwa rai yangu mimi ni kwamba muovu kushinda wote watakaokuja ni muovu zaidi kushinda yule muovu mwenye kuwashinda wote waliotangulia. Na tofauti kati yao ni kama tofauti kati ya Ali na ngamia. Habari zimegusia bali zimetamka kwamba muuwaji wa Amiril-Muuminina alikuwa amehalalisha mauwaji hayo, bali alikuwa akiamini kuwa kufanya hivyo ni thawabu kwake, na masahiba zake wamemsifu kwa tukio hilo, ndipo Amran bin Hatwan (Ghadhabu za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake), akatoa shairi: “Pigo bora lilioje! Kutoka kwa mcha mungu, hakukusudia kwalo ila kupata ridhaa kutoka kwa Mkuu wa Arshi (Mwenyezi Mungu). Hakika mimi namtaja leo na ninamzingatia kwamba ni kiumbe chenye fungu kamili mbele ya Mwenyezi Mungu.” Na Mwenyezi Mungu ana neema kwa yule aliyemjibu: “Pigo ovu lilioje! Kutoka kwa muovu aliyejirithisha Moto, atakutana na Rahman akiwa Amemghadhibikia. 131

Page 131


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kana kwamba kwa pigo lake hajapata kitu ila kuingia motoni kesho Siku ya mkusanyiko. Hakika mimi namtaja leo na ninamlaani, na pia namlaani Imran bin Hatwan. Na kudai kwamba kitendo chake hicho ni shubha itakayomwokoa, ni kauli ambayo bila shaka ni sehemu ya kuweweseka. Kwani lau ikiwa mfano wa kitendo hicho ni chenye kumwokoa na adhabu ya dhambi hii, basi mtu afanye atakavyo! Umetakasika Mwenyezi Mungu na uzushi huu mkubwa.177

SURAT AL-AN’FAL Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na walipokupangia njama wale waliokufuru ili wakufunge au wakuue au wakutoe…” (Surat al-An’fal: 30). Jibril (a.s.) alimjia Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumwambia: “Usiku huu usilale kitandani kwako ambapo huwa unalala.” Ulipowadia usiku walijikusanya mlangoni kwake wakimvizia ni muda upi atalala ili wamvamie. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipoona nafasi yao alimwambia Ali (a.s.): “Lala kitandani kwangu na jifunike shuka hili la kijani la kihadhramiy, hakika hakitakupata chochote chenye kukuudhi toka kwao.” Na ilikuwa ni kawaida ya Mtume wa Mwenyezi Mungu kujifunika shuka hiyo alalapo. Ali (a.s.) akasoma shairi kuashiria neema aliyoneemeshwa na Mwenyezi Mungu, akasema: Nimemkinga kupitia nafsi yangu yule mbora kushinda wote waliowahi kukanyaga changarawe, na kuliko wote waliowahi kutufu Nyumba ya kale na kugusa Jiwe. Mtume wa Mwenyezi Mungu amekhofia wasimfanyie hila, ndipo Mungu Mwenye uwezo amemwokoa dhidi ya hila. 176 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 6 Uk. 149. 177 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 8 Uk. 147. 132

Page 132


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mtume wa Mwenyezi Mungu amelala kwa amani huko pangoni, akiwa chini ya ulinzi wa Mungu na sitara Yake. Nimelala nikiwafuatilia wao na yale wanayonituhumu, na hali nimeituliza nafsi yangu katika kuuawa na kufungwa.”178

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “(Tangazo la) Kujitoa Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wale mlioahidiana nao miongoni mwa mushrikina.” (Sura Tawba: 1). Alusiy amesema: “Riwaya zimetofautiana kuhusu je Abu Bakr alikuwa kaamrishwa kuisoma au la? Nyingi zinaona alikuwa ameamriwa kuisoma, na kwamba Ali alipomfuata na kuichukua toka kwake aliamriwa kuisoma. Na imekuja katika riwaya kutoka kwa Ibnu Habban na Ibnu Mardawayhi kutoka kwa Abu Said al-Khudri kwamba Abu Bakr aliponyang’anywa sura hiyo alikuja kwa Mtume na hali akiwa ameingiwa na khofu kwamba huenda kuna kitu kimeteremka kuhusu yeye. Alipofika kwa Mtume alisema: “Nina nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?” Mtume akasema: “Ni kheri tupu, wewe ni ndugu yangu na swahiba wangu pangoni, na wewe utakuwa pamoja nami katika hodhi, isipokuwa ni kwamba hafikishi kwa niaba yangu asiyekuwa mimi au mtu atokanaye na mimi.”179 Imekuja katika riwaya ya Ahmad na Tirmidhi, ambayo yeye Tirmidhi, Abu Shaikh na wengineo wameizingatia kuwa ni Hasana, kwamba Anas amesema: “Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Abu Bakr na Sura Baraa, kisha akamwita na kumwambia: “Haipasi yeyote kuifikisha hii ila mtu katika watu wa nyumba yangu.” Ndipo akamwita Ali na kumkabidhi.180 178 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 9 Uk. 176. 179 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 10 Uk. 40. 180 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 10 Uk. 40. 133

Page 133


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Je, mnafanya kuwanywesha mahujaji na kuamirisha msikiti mtukufu ni sawa na yule aliyemwamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na akapigana jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu? Hawawi sawa mbele ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu madhalimu.” (Sura Tawba: 19). Imepokewa kwa njia mbalimbali kwamba Aya hii iliteremka kwa ajili ya Ali na Abbas, hiyo ni pale Amirul-Muuminina alimwambia Abbas: “Ewe Ami yangu, ungehamia Madina.” Akamjibu: “Hivi mimi siko katika kazi bora kushinda kuhama, hivi mimi si ninatoa huduma ya maji kwa mahujaji na ninalinda Nyumba.”181 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Bila shaka Mwenyezi Mungu amekusaidieni katika mapigano mengi na Siku ya Hunayni.” (Sura Tawba: 25). Imepokewa kwamba al-Mutawakkil aliugua sana akaweka nadhiri iwapo Mwenyezi Mungu atamponyesha basi atatoa sadaka mali nyingi. Alipopona aliwauliza ulamaa kipimo cha wingi, ndipo kauli zao zikatofautiana, wakamshauri amuulize Abu Hasan Ali bin Muhammad bin Ali bin Musa al-Kadhim (a.s.), na alikuwa amemuweka kuzuizini huko nyumbani

181 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 10 Uk. 60. 134

Page 134


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 kwake, ndipo akaamuru aandikiwe barua. Akamrudishia jibu kwamba atoe sadaka dirhamu themanini. Walipomuuliza sababu alisoma Aya hii na kusema: Tumehesabu maeneo hayo yakafikia themanini.182

SURAT HUD Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake na anaifuata na shahidi atokaye kwake..” (Sura Hud: 17). Ibnu Mardawayhi ameandika kwa njia nyingine kutoka kwa Ali kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alisema: “Basi je, aliye na dalili wazi itokayo kwa Mola wake ni mimi. Na na anaifuata na shahidi atokaye kwake ni Ali.”183

SURAT AR-RAAD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe ni mwonyaji tu. Na kila kaumu ina wa kuwaongoza.” (Surat ar-Raad: 7). Ibnu Jarir, Ibnu Mardawayhi, Daylamiy na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: “Ilipoteremka Aya hii Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) aliweka mkono wake juu ya kifua chake na kusema: ‘Mimi ndiye mwonyaji.’ Akaashiria mkono wake kwenye bega la Ali na kusema: ‘Ali wewe ndiye mwongozaji. Kupitia kwako wataongoka 182 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 10 Uk. 65. 183 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 12 Uk. 26. 184 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 13 Uk. 97. 135

Page 135


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 wenye kutaka kuongoka baada yangu.”184 Abdullah bin Ahmad ameandika katika Zawaidul-Musnad, Ibnu Abi Hatim, Tabarani katika al-Awsat, al-Hakim katika Sahih yake, na Ibnu Asakir pia, wote wameandika kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: “Katika aya hii, Mtume wa Mwenyezi Mungu ndio Muonyaji, nami ndiye Mwongozaji.” Na katika kauli nyingine Mwongozaji ni mtu kutoka kizazi cha Hashim, yaani yeye mwenyewe.185

SURAT IBRAHIM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na mfano wa neno baya ni kama mti mbaya ambao umeng’olewa ardhini hauna uimara.” (Surat Ibrahim: 25 - 26). Imepokewa kutoka kwa Abu Ja’far katika tafsiri ya mti mbaya kwamba ni Bani Umaiya, na mti mzuri ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, Ali, Fatima na watoto wao.186

SURAT AN-NAMLI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “ Basi waulizeni wenye ukumbusho ikiwa nyinyi hamjui.” (Sura an-Namli: 43). Jabir amepokea na Muhammad bin Muslim kutoka kwa Abu Ja’far (a.s.) kwamba alisema: “Sisi ndio wenye ukumbusho.”187 185 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 13 Uk. 97. 186 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 13 Uk. 193. 136

Page 136


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT ISRAI Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake na maskini na mwana njia, wala usifanye ubadhirifu.” (Sura Israi: 26). Kutoka kwa as-Asadiy, na ameandika Ibnu Jarir kutoka kwa Ali bin Husain kwamba (a.s.) alimwambia mzee mmoja wa Sham: “Hivi umewahi kusoma Qur’ani?” akajibu ndio. Ali akasema: “Hivi hujasoma katika Surat Israi: “Na mpe jamaa wa karibu haki yake..”? Mzee akasema: ‘’Hivi nyinyi ndio jamaa wa karibu ambao Mwenyezi Mungu ameamuru wapewe haki yao?!!” Ali akasema: “Ndio sisi.”188

SURAT MARYAM Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika wale ambao wameamini na wakatenda mema Mwingi wa rehema atawajaalia mapenzi.” (Sura Maryam: 96). Ibnu Mardawayhi na Daylamiy wameandika kutoka kwa al-Barau kwamba alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali bin Abu Talib: “Ewe Ali sema: Ewe Mwenyezi Mungu! Nipe hifadhi Kwako na niwekee mapenzi katika nyoyo za waumini.” Ndipo Mwenyezi Mungu akateremsha Aya hii. Na Muhammad bin al-Hanafiya alikuwa akisema: Hutampata muumini ila ni yule anayempenda Ali na watu wa nyumba yake.189 187 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 14 Uk. 134. 188 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 15 Uk. 58. 189 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 16 Uk. 130. 137

Page 137


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT TWAHA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika wewe unatuona.” (Surat Twaha: 35). Ibnu Mardawayhi, al-Khatib na Ibnu Asakir wameandika kutoka kwa Asmau binti Umaysi kwamba alisema: Nilimuona Mtume wa Mwenyezi Mungu mbele ya Mlima wa Thabir akisema: “Thabir amechomoza, Thabir amechomoza. Ewe Mwenyezi Mungu! Ninakuomba lile alilokuomba ndugu yangu Musa kwamba unipanulie kifua changu. Unifanyie wepesi kazi yangu. Uniondolee fundo katika ulimi wangu. Ifahamike kauli yangu. Na uniwekee waziri katika jamaa zangu. Ndugu yangu Ali. Nitie nguvu kupitia kwake. na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutukuze sana. Hakika wewe unatuona.”190 Mfano wa hiyo ni ile kauli iliyosihi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema pindi alipompa umakamu juu ya watu wa nyumba yake siku alipokwenda katika Vita vya Tabuk: “Hivi huridhii kwamba wewe nafasi yako kwangu ni ile ya Harun kwa Musa ila ni kwamba hakuna Nabii baada yangu.”191

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Surat Ahzab: 33). 190 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 16 Uk. 169. 191 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 16 Uk. 169. 138

Page 138


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Tirmidhi na Hakim wameandika na kuizingatia kuwa ni riwaya sahihi, na Ibnu Jarir, Ibnu Mundhir, Ibnu Mardawayhi na al-Bayhaqiy katika Sunan yake, wote wameandika kutoka kwa Ummu Salama kwamba alisema: Aya hii: “Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab: 33) iliteremkia nyumbani kwangu, na humo alikuwemo Fatima, Ali, Hasan na Husain, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu akawafunika kishamia alichokuwa amejifunika, kisha akasema: “Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, waondolee uchafu na watakase kabisa.”192 Imekuja katika baadhi ya riwaya kwamba Mtume (s.a.w.w.) alitoa mkono wake toka katika kishamiya na kuunyoonsha mbinguni, akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio Ahlul-Baiti na wasiri wangu hivyo waondolee uchafu na watakase kabisa.” Alisema hivyo mara tatu.193 Na katika riwaya nyingine ni kwamba Mtume (s.a.w.w.) aliwafunika kishamiya cha Khaibar, kisha akaweka mkono wake juu yao kisha akasema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu.”194 Na katika lafudhi nyingine: “Ewe Mola wangu, shusha rehma zako na baraka zako juu ya aali Muhammad, kama ulivyoziweka juu ya aali Ibrahim, hakika wewe ni Mhimidiwa msifika.”195 “Na katika riwaya aliyoandika Tabarani kutoka kwa Ummu Salama ni kwamba alisema: Nilifunua kishamiya ili niingie pamoja nao lakini Mtume (s.a.w.w) akakivuta toka mikononi mwangu, na akasema: “Hakika wewe upo katika kheri.”196 192 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 193 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 194 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 195 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 196 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 139

Page 139


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Na katika riwaya nyingine iliyopokewa na Ibnu Mardawayhi kutoka kwa Ummu Salama ni kwamba alisema: “Je mimi sio katika Ahlul-Baiti wako? Mtume akajibu: “Hakika wewe waelekea katika kheri, hakika wewe ni miongoni mwa wakeze Mtume.”197 Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Hakika Mwenyezi Mungu na malaika wake wanamswalia Nabii. Enyi ambao mmeamini! Mswalieni na mumsalimu kwa salamu.” (Surat Ahzab: 56). Abdu Razaq, Ibnu Abi Shayba, Imam Ahmad, Abdu bin Hamid, Bukhari, Muslim, Abu Daud, Tirmidhiy, Nasaiy, Ibnu Majah na Ibnu Mardawayhi, wameandika kutoka kwa Ka’bi bin Ajrah, kwamba amesema: ‘’Mtu mmoja alisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ni ipi namna ya kukusalia? Mtume akasema: ‘’Sema: ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ?????? ???? ??? ????? ???? ?? ????? ??? ????? ??? ?? ??????? ???? ???? ????. ‘Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowarehemu aali Ibrahim, hakika wewe ni Mhimidiwa Msifika. Ewe Mwenyezi Mungu! mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyowabariki aali Ibrahim, hakika wewe ni Mhimidiwa Msifika.’”198 Imam Ahmad, Bukhari, Nasaiy, Ibnu Majah na wengineo, wameandika kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba alisema: Tulisema: Ewe Mtume 197 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 14. 198 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 72. 140

Page 140


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema: ‘Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Mrehemu Muhammad mja wako na Mtume wako kama ulivyomrehemu Ibrahim. Na mbariki Muhammad na aali Muhammad kama ulivyombariki Ibrahim.”’199 Imam Ahmad, Abdu bin Hamid na Ibnu Mardawayhi, wameandika kutoka kwa Ibnu Burayda kwamba alisema: “Tulisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Tumeshajua namna ya kukutolea salamu, ama sala tutakusaliaje? Akasema: ‘Semeni: Ewe Mwenyezi Mungu! Shusha rehema zako na baraka zako juu ya Muhammad na juu ya aali Muhammad, kama ulivyoziweka juu ya Ibrahim, hakika wewe ni Mhimidiwa Msifika.”’200

SURAT ZUMARA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na aliyeleta ukweli na aliyeusadikisha, hao ndio wamchao (Mwenyezi Mungu)” (Sura 33). Ibnu Jarir, al-Barudiy na Ibnu Asakir kwa njia ya Usayd bin Swaf’wan, wameandika kutoka kwa Ali (a.s.). Na Abu As’wad, Mujahid na jamaa miongoni mwa Ahlul-Baiti wamesema kwamba: Aliyeusadikisha ni Ali (a.s.).201

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” (Surat as-Shura: 23).

Makusudio ya ndugu zake (s.a.w.w.) hapa ni Ali, Fatima na watoto wake 199 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 72 200 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 22 Uk. 72. 201 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 24 Uk. 3. 141

Page 141


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 (a.s.), na zimepokewa riwaya za kuvushwa kuhusu hilo. Ibnu al-Mundhir, Ibnu Abi Hatim, Tabarani na Ibnu Mardawayhi wameandika kupitia njia ya Ibnu Jubair kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Ilipoteremka: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” walisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni akina nani hawa karaba zako ambao tunapasa kuwapenda? Akasema: “Ni Ali, Fatima na watoto wao wawili.”202 Ibnu Jarir ameandika kutoka kwa Abu Daylam kwamba alisema: Alipoletwa Ali bin Husein (a.s.) na hali ni mateka na kusimamishwa katika barabara kuu ya Damascus alisimama mzee mmoja kati ya watu wa Sham, akasema: ‘Kila sifa njema ni ya Mwenyezi Mungu ambaye amewauwa na kuwang’oeni.’ Ali bin Husein radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee akasema: ‘Umewahi kusoma Qur’ani?’ akajibu ndio. Akasema (a.s.): ‘Umewahi kusoma Aali Haa Miim?’ Akajibu ndio nimewahi kusoma. Akasema (a.s.): ‘Hujawahi kusoma: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...”’ Mzee akasema: ‘Nyinyi ndio hao?’ Akasema (a.s.): ‘Naam ndio sisi.’”203 Dhadhan alipokea kutoka kwa Ali (a.s.) kwamba alisema: “Katika Aali Hamim (Sura Shura) kuna Aya inayotuhusu, hatupendi sisi ila muumini.” Kisha akasoma Aya hii: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” Na hili ndilo aliloashiria Kumayti katika shairi lake aliposema: “Tumewakuta mmo ndani ya Aya ya Aali Hamim, ameifasiri hivyo aliye mchamungu na mwarabu kati yetu.”204 Ibnu Habban na Hakim wameandika kutoka kwa Abu Said kwamba alise202 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 25 Uk. 28. 203 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 25 Uk. 28. 204 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 25 Uk. 29. 142

Page 142


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 ma: “Naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake, hakuna mtu atakayetuchukia sisi Ahlul-Baiti ila ni lazima Mwenyezi Mungu atamwingiza motoni.”205

SURA MUHAMMAD Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Na ndio Mwenyezi Mungu amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao.” (Sura Muhammad: 23). Hakuna kizuizi katika kumlaani Yazid kutokana na wingi wa sifa zake

chafu na kutenda kwake madhambi makubwa muda wote wa utu uzima wake. Inakutosha lile alilowafanyia watu wa Madina na Makka, amepokea Tabarani kwa njia hasan kwamba Mtume alisema: “Ewe Mwenyezi Mungu! Atakayewadhulumu wakazi wa Madina na kuwasababishia khofu, laana za Mwenyezi Mungu, Malaika na watu wote zitakuwa juu yake, haitakubaliwa fidia wala badala kutoka kwake.” Na msiba mkubwa ni kile kitendo alichowafanyia Ahlul-Baiti (a.s.) na kuridhia kuuawa Husain (a.s.) na kufurahia kitendo hicho, na kumdhalilisha yeye na watu wa nyumba yake, kama maana hiyo ilivyo mutawatiri. Jamaa miongoni mwa ulamaa wameamini na kutamka wazi kwamba inasihi kumlaani, miongoni mwao ni Hafidh Nasrus-Sunnah Ibnu al-Jawziy, na kabla yake ni al-Qadhiy Abu Ya’la. Allama Taftazaniy amesema: “Hatusiti kuhusu jambo lake, bali ni kuhusu imani yake, laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake na juu ya watetezi wake na wasaidizi wake.”206 205 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 25 Uk. 29. 206 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 26 Uk. 66. Anayetaka kwa undani suala la Yazid bin Muawiya kulaaniwa arejee kitabu Ar-Raddu ‘Alal-Muta’aswib al-‘Anid cha Hafidh Abul Faraj aliye mashuhuri kwa jina la Ibnu al-Jawziy, aliyefariki mwaka 597 A.H. 143

Page 143


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT RAHMAN Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Amezikutanisha bahari mbili. Baina yao kuna kizuizi haziingiliani. Basi nyinyi wawili mnakataa neema gani ya Mola wenu Mlezi? Katika hizo mbili hutoka lulu na marijani.” (Sura Rahman: 19 - 22).

Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Asakir kwamba alisema kuhusu: “Amezikutanisha bahari mbili.” ni Ali na Fatima. “Baina yao kuna kizuizi haziingiliani.” ni Mtume (s.a.w.w.) “Katika hizo mbili hutoka lulu na marijani.” Ni Hasan na Husein.” Nionalo mimi207 ni kwamba kauli hiyo ikisihi basi si miongoni mwa tafsiri bali ni taawili kama taawili nyingi za masufi katika Aya mbalimbali. Kwangu mimi wote Ali na Fatima ni watu adhimu mno kushinda bahari kuu kielimu na kifadhila, na pia wote wawili Hasan na Husain ni wazuri na wenye kung’ara kushinda lulu na marijani kwa kiwango ambacho kimevuka kipimo cha hesabu.208

SURAT AL-WAQI’A Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Waliotangulia ndio waliotangulia.” (Surat al-Waqi’a: 10). 207 Yaani mwandishi wa tafsiri hii. 208 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 27 Uk. 93. 144

Page 144


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Ibnu Mardawayhi ameandika kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba: “Iliteremka kwa ajili ya Ezekiel muumini wa aali Firaun, Habib Najar ambaye katajwa katika Sura Yasin, na Ali bin Abu Talib (a.s.)”209

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu: S

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12). Al-Hakim ameiandika na kuizingatia kuwa ni sahihi, Ibnu al-Mundhir, Abdu bin Hamid na wengineo, wote wameandika kutoka kwa AmirulMuuminina (a.s.) kwamba alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu, nayo ni Aya ya kusema siri na Mtume: “Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana…..” nilikuwa nina dinari nikazibadili kwa dirhamu, hivyo nikawa kila nisemapo siri na Mtume natoa dirhamu moja kabla ya kusema naye siri, kisha ikafutwa na hakuna yeyote aliyeifanyia kazi.”210

209 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 27 Uk. 114. 210 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 27 Uk. 28. 145

Page 145


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT TAGHABUN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, na kwa Mwenyezi Mungu kuna malipo makubwa.” (Sura Taghabun: 15). Imam Ahmad, Abu Daud, Tirmidhiy, Nasaiy, Ibnu Majah na Hakim ambaye ameizingatia kuwa ni sahihi, wote wameandika kutoka kwa Buraida kwamba alisema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alikuwa akitoa hotuba na ghafla wakaja Hasan na Husein wakiwa wamevaa kanzu mbili nyekundu na hali wakidondoka na kuamka, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka toka mimbarini akawafuata na kuwabeba kila mmoja katika bega lake, kisha akapanda juu ya mimbari na kusema: ‘Mwenyezi Mungu amesema kweli. Bila shaka mali zenu na watoto wenu ni mtihani, hakika mimi nilipowaona hawa wawili wakitembea na wakidondoka sikuweza kuvumilia mpaka nikakatisha mazungumzo yangu na nikashuka kwenda kuwachukua.”211 Na katika riwaya ya Ibnu Mardawayhi kutoka kwa Abdullah bin Umar ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alipokuwa akiwahutubia watu juu ya mimbari, Husain bin Ali alitokeza na kuanza kwenda kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) ndipo akakanyaga nguo yake aliyokuwa amevaa na akawa amedondoka na kuanza kulia, basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akateremka toka juu ya mimbari, watu walipomuona amefanya hivyo walimkimbilia Husain na kuanza kumbembeleza mpaka akafika mikono mwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na kusema: “Mwenyezi Mungu amuuwe shetani, hakika mtoto ni 211 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 27 Uk. 111. 146

Page 146


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 mtihani, naapa kwa yule ambaye nafsi yangu imo mikononi mwake sikuweza kujizuia212 hakika nimeteremka kutoka mimbarini kwangu.”213

SURAT AL-HAQQAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Ili tuifanye ukumbusho kwenu, na sikio lisikialo lisikie.” (Sura alHaqqah: 12). Katika habari ni kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) alimwambia Ali (a.s.): ‘’Hakika mimi nilimwomba Mwenyezi Mungu alifanye hivyo sikio lako ewe Ali.’’ Amirul-Mu’minin Ali (a.s.) alisema: “Baada ya hapo sikuwahi kusahau chochote na wala sikupasa kusahau.”

SURAT AL-INSAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na huwalisha chakula masikini na yatima na mfungwa hali ya kuwa wanakipenda. Tunakulisheni kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu tu, hatutaki kwenu malipo wala shukurani.” (Surat al-Insan: 8 - 9). 212 Katika maelezo ya Juz. 27 Uk. 112 Alusiy amesema: “Sijui ingekuwaje lau Mtume wa Mwenyezi Mungu angeiona hali ya Husain (a.s.) katika tukio la Karbala, sijui angefanya nini? Kwa kweli laana ya Mwenyezi Mungu, Malaika zake, Mitume wake na watu wote iwe juu ya yule aliyeamuru yale yaliyotokea, aliyerusha vimondo, kuwasha moto na akaridhia au kuongeza jeshi. 213 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 27 Uk. 111. 147

Page 147


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Riwaya ya Atau kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba alisema: Hakika Hasan na Husein walipatwa na maradhi, babu yao Muhammad (s.a.w.w.) alikwenda kuwaona, na masahaba nao pia walikwenda kuwaona. Wakasema kumwambia Ali: “Ewe Abu Hasan! Ni bora kama ungeweka nadhiri juu ya watoto wako.” Ali, Fatima na mtumishi wao Fidha wakaweka nadhiri kwamba ikiwa watapona watafunga siku tatu kumshukuru Mwenyezi Mungu. Vijana wawili wakapata afya njema na hali nyumbani kwa aali Muhammad hawana kitu si kichache wala kingi. Ndipo Ali akaenda kwa Simon Myahudi wa Khaibari, akakopa toka kwake pishi tatu za ngano. Akaja nazo na Fatima akachukua pishi moja akatwanga na kuoka mikate mitano kulingana na idadi yao. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume Sala ya Magharibi alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yake, mara masikini akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni maskini katika watoto wa umma wa kiislamu, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakampa na wao wakalala bila kuonja kitu ila maji, na siku ya pili wakaamka wakiwa na funga. Ilipofika siku ya pili Fatima akachukua pishi jingine akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) Sala ya Magharibi alikwenda nyumbani na kikawekwa chakula mbele yake, mara akafika mlangoni kwao yatima akagonga akisema: “Assalam Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, yatima toka katika watoto wa muhajirana, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula cha Peponi.” Wakampa chakula na wakashinda siku mbili mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji, na siku ya tatu wakaamka wakiwa na funga. Ilipofika siku ya tatu Fatima akachukua pishi la tatu akatwanga na kuoka mikate. Ali alipomaliza kuswali pamoja na Mtume (s.a.w.w.) Sala ya Magharibi alikuja nyumbani na kikawekwa chakula mbele yake, mara mfungwa wa kivita akafika mlangoni kwao akagonga akisema: “Assalam 148

Page 148


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Alaykum enyi watu wa nyumba ya Muhammad, mimi ni mateka wa Muhammad, nipeni chakula Mwenyezi Mungu atakupeni chakula.” Wakampa chakula na wakashinda siku tatu mchana kutwa na usiku kucha bila kuonja chochote ila maji. Ilipofika siku ya nne Ali alimshika mkono Hasan na Husein na kwenda nao kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.), alipowaona (s.a.w.w.) wakitetemeka kama vifaranga kutokana na ukali wa njaa, alisema: “Ewe Abal-Hasan! Hali niionayo kwenu yaniumiza mno.” Akasimama na kwenda nao kwa Fatima (a.s.), wakamkuta akiwa mihrabuni kwake na hali tumbo lake limeshikana na mgongo wake na macho yake yamebadilika kutokana na ukali wa njaa. Huruma ikamuingi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na ikamuumiza hali hiyo, ndipo Jibril (a.s.) akateremka na kusema: “Ewe Muhammad pokea, Mwenyezi Mungu anakupa pongezi kwa kitendo cha watu wa nyumba yako.” Mtume akasema: “Nichukue nini ewe Jibril?” Jibril (a.s.) akamsomea Surat Insan.214 AHLUL-BAIT (A.S.) NDANI YA TAFSIRI YA AL-QASIMIY, INAYOITWA MAHASINUT-TAAWIL

SURAT AAL IMRAN Kauli ya Mwenyezi Mungu:

214 Tafsir Ruhul-Ma’aniy Juz. 29 Uk. 157. 149

Page 149


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). Hafidh Abu Bakr bin Mardawayhi amepokeakutoka kwa Sha’abiy kutoka kwa Jabir kwamba amesema: Aqib na Tayib walikwenda kwa Mtume (s.a.w.w.), naye akawaomba wafanye maapizano, wakamwahidi wafanye maapizano naye kesho yake, ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) akatoka na hali amewashika mkono Ali, Fatima, Hasan na Husain, kisha akawatumia ujumbe waje lakini wakakataa na hatimaye wakakubali kutoa kodi. Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema: “Naapa kwa yule aliyenituma kwa haki! Lau wangesema la, basi bonde lao lingeteketea kwa moto.” Jabir anasema: Na kwa ajili ya hao iliteremka Aya hii: “Na watakaokuhoji baada kukufikia elimu hii, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake wenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo.” (Sura Aali Imran: 61). “….. nafsi zetu na nafsi zenu” ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Ali. “…..watoto wetu” ni Hasan na Husein. “…..wanawake zetu” ni Fatima. Hakim ameipokea kwa kuvushwa katika Mustadrak kutoka kwa Sha’bah kutoka kwa Mughira. Na hii ni sahihi zaidi.215

215 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 2 Uk. 71. 150

Page 150


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu na nimekupendeleeni Uislamu uwe dini yenu..” (Sura Maida: 3). Ibnu Mardawayhi amepokea kwa njia ya Abu Harun al-‘Abdiy kutoka kwa Abu Said al-Khudriy kwamba ilimteremkia Mtume wa Mwenyezi Mungu Siku ya Ghadir Khum pale aliposema kuhusu Ali: “Yule ambaye mimi nina mamlaka juu yake basi Ali ana mamlaka juu yake.” Kisha ameipokea kutoka kwa Abu Huraira na katika maelezo yake ni kwamba ilikuwa ni siku ya kumi na nane ya Mfunguo tatu.216

SURAT MAIDA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika walii wenu hasa ni Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wale walioamini ambao husimamisha Swala na hutoa Zaka wakiwa wamerukui.” (Sura Maida: 55). 216 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 7 Uk. 34. 151

Page 151


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:05 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Mpaka baadhi yao katika tendo hili wametaja athari inayomhusu Ali bin Abu Talib kwamba: Hakika Aya hii iliteremka kwa ajili yake, muombaji alipita kwake na hali akiwa katika rukuu yake ndipo akampa pete yake.217

SURAT TAWBA Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Na ni tangazo litokalo kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa watu Siku ya Hija kubwa.” (Sura Tawba: 3). Ibnu Is’haqa amepokea kwa sanadi yake kutoka kwa Abu Ja’far Muhammad bin Ali (a.s.) kwamba ilipoteremka Sura Baraa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) na alikuwa tayari ameshamtuma Abu Bakr akaongoze Hija, ndipo akaambiwa: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni vizuri lau ungemtuma nayo Abu Bakr. Akasema: “Hatekelezi kwa niaba yangu ila mtu toka katika Ahlul-Baiti wangu.” Kisha akamwita Ali bin Abu Talib na kumwambia: “Nenda na kisa hiki kuanzia mwanzo wa Sura Baraa, na nenda kawatangazie watu siku ya kuchinja pindi watakapokusanyika huko Mina, kwamba kafiri haingii peponi, baada ya mwaka huu haruhusiwi Mushriku kuhiji, haruhusiwi kutufu akiwa uchi, na yule ambaye ana mkataba na Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w.) utaendelea mpaka mwisho wa muda wake.”218

217 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 7 Uk. 156. 218 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 8 Uk. 85. 152

Page 152


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:06 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Imenukuliwa kwamba Bani Umaiyya walikuwa wakimtukana Ali katika hotuba zao, na ukhalifa ulipoangukia mikononi mwa Umar bin Abdul-Aziz aliondoa kipengele hicho (cha kumlaani Ali) na kuweka badala yake Aya hii. Nasir amesema: “Huenda Aya hii kuwekwa badala ya kashfa hizo ilikuwa ni kutokana na kuoana kati ya maana yake ambayo ni kukataza uovu na ile hadithi inayosema kwamba kumfanyia uadui Ali ni uovu, kwani Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Ammar aliyekuwa katika jeshi la Ali: “Litakuuwa kundi ovu.” Naye akauawa akiwa pamoja na Ali (a.s.) Siku hiyo ya Siffin.219

SURAT AHZAB Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Hakika si mengineyo Mwenyezi Mungu anataka kuwaondolea uchafu, enyi watu wa nyumba ya Mtume, na kuwatakasa kabisa kabisa.” (Sura Ahzab; 33:33). Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya Fatima, Ali, Hasan na Husain, kisha akawafunika kishamiya alichokuwa amejifunika, kisha akasema: “Hawa ndio Ahlul-Baiti wangu, waondolee uchafu.”220

219 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 10 Uk. 543. 220 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 13 Uk. 506. 153

Page 153


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:06 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

SURAT AS-SHURA Kauli ya Mwenyezi Mungu: “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” (Sura as-Shura: 23). Katika Sahih Bukhari imepokewa kutoka kwa Ibnu Abbas kwamba aliulizwa kuhusu “Sema: Kwa haya siwaombi malipo yoyote kwenu isipokuwa mapenzi kwa ndugu...” Said bin Jubair akasema: Ndugu ni aali Muhammad.221 Na aliyoipokea Ibnu Abi Hatim ni kwamba ilipoteremka Aya hii walisema: “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni akina nani hawa ambao Mwenyezi Mungu ameamuru tuwapende? Akasema: “Ni Fatima na kizazi chake.”222

SURAT MUJADILAH Kauli ya Mwenyezi Mungu:

“Enyi mlioamini! Mnaposema siri na Mtume, basi tangulizeni sadaka kabla ya kumsemesha hayo ni bora kwenu na ni safi sana, na ikiwa hamkupata basi Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.” (Sura Mujadilah: 12).

221 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 14 Uk. 172. 222 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 14 Uk. 172. 154

Page 154


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:06 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 Imepokewa kutoka kwa Mujahidu kwamba alisema: “Ali bin Abu Talib (radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee) alisema: “Hakika katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuna Aya ambayo hakuna yeyote aliyeifanyia kazi kabla yangu, wala hakuna yeyote atakayeifanyia kazi baada yangu.”223 Na imepokewa pia kutoka kwake (Mujahid) kwamba alisema: “Walikatazwa kusema siri na Mtume (s.a.w.w.) mpaka watoe sadaka. Hakuna aliyeweza kusema naye siri ila Ali bin Abu Talib (radhi za Mwenyezi Mungu zimwendee), alitoa sadaka ya dinari. Ndipo (baada ya sadaka hiyo) ikateremka ruhusa (iliyoondoa sharti la sadaka). “224 Na mwisho wa maombi yetu ni kumshukuru Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa viumbe wote.

223 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 16 Uk. 55. 224 Tafsirul-Qasimiy inayoitwa Mahasinut-Taawil Juz. 16 Uk. 55. 155

Page 155


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:06 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

ORODHA YA VITABU VILIVYO CHAPISHWA NA AL-ITRAH FOUNDATION 1. 2. 3. 4. 5. 6. 7. 8. 9. 10. 11. 12. 13. 14. 15. 16. 17. 18. 19. 20. 21. 22. 23. 24. 25. 26.

Qur'an Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka Thalathini Uharamisho wa Riba Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Kwanza Uharamisho wa uwongo Juzuu ya Pili Hekaya za Bahlul Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) Hijab vazi Bora Ukweli wa Shia Ithnaashari Madhambi Makuu Mbingu imenikirimu Abdallah Ibn Saba Khadijatul Kubra Utumwa Umakini katika Swala Misingi ya Maarifa Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia Bilal wa Afrika Abudharr Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu Salman Farsi Ammar Yasir Qur'an na Hadithi Elimu ya Nafsi Yajue Madhehebu ya Shia Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur'an Tukufu 156

Page 156


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 27. 28. 29. 30. 31. 32. 33. 34. 35. 36. 37. 38. 39 40. 41. 42. 43. 44. 45. 46. 47. 48. 49. 50. 51. 52. 53. 54. 55. 56. 57.

Al-Wahda Ponyo kutoka katika Qur'an. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii Mashukio ya Akhera Al Amali Dua Indal Ahlul Bayt Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna. Haki za wanawake katika Uislamu Mwenyeezi Mungu na sifa zake Amateka Na Aba'Khalifa Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) Adhana. Upendo katika Ukristo na Uislamu Nyuma yaho naje kuyoboka Amavu n’amavuko by’ubushiya Kupaka juu ya khofu Kukusanya swala mbili Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya Kusujudu juu ya udongo Kusheherekea Maulidi Ya Mtume (s) Tarawehe Malumbano baina ya Sunni na Shia Kupunguza Swala safarini Kufungua safarini Umaasumu wa Manabii Qur’an inatoa changamoto as-Salaatu Khayrun Mina -'n Nawm Uadilifu wa Masahaba Dua e Kumayl Sauti Ya Uadilifu wa Binadamu 157

11:06 AM

Page 157


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 58. 59. 60. 61. 62. 63. 64. 65. 66. 67. 68. 69. 70. 71. 72. 73. 74. 75. 76. 77. 78. 79. 80. 81. 82. 83. 84. 85. 86.

Umaasumu wa Mitume - Faida Zake Na Lengo Lake Umaasumu wa Mitume - Majibu Ya Aya Zenye Utata Umaasumu wa Mitume - Umaasumu wa Mitume Muhammad (s) Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Kwanza Nahju’l-Balaghah - Juzuu ya Pili Kuzuru Makaburi Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Kwanza Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Pili Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tatu Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Nne Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Tano Maswali Na Mishkili Elfu - Sehemu ya Sita Tujifunze Misingi Ya Dini Sala ni Nguzo ya Dini Mikesha Ya Peshawar Malezi Ya Mtoto Katika Uislamu Ubora wa Imam 'Ali Juu ya Maswahaba Na Ushia ndio njia iliyonyooka Hukumu za Kifikihi zinazowahusu Wanawake Liqaa-u-llaah Muhammad (s) Mtume wa Allah Amani na Jihadi Katika Uislamu Uislamu Ulienea Vipi? Uadilifu, Amani na Mtume Muhammad (s) Mitala na Ndoa za Mtume Muhammad (s) Urejeo (al-Raja’a ) Mazingira Utokezo (al - Badau) Sadaka yenye kuendelea Msahafu wa Imam Ali 158

11:06 AM

Page 158


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 87. 88. 89. 90. 91. 92. 93. 94. 95.

Uislamu na dhana Mtoto mwema Adabu za Sokoni Johari za hekima kwa vijana Maalimul Madrasatain Sehemu ya Kwanza Maalimul Madrasatain Sehemu ya Pili Maalimul Madrasatain Sehemu ya Tatu Tawasali Imam Mahdi katika Usunni na Ushia

96.

Maana ya laana na kutukana katika Qur’ani Tukufu

97.

Hukumu ya kujenga juu ya makaburi

98.

Swala ya maiti na kumlilia maiti

99.

Shiya na Hadithi (kinyarwanda)

100.

Mariamu, Yesu na Ukristo kwa mtazamo wa Kiislamu

101.

Hadithi ya Thaqalain

102

Fatima al-Zahra

103.

Tabaruku

104.

Sunan an-Nabii

105.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Kwanza)

106.

Historia na sera ya viongozi wema (Sehemu ya Pili)

107.

Mahdi katika sunna

108.

Kusalia Nabii (s.a.w)

109.

Ujumbe -Sehemu ya Kwanza

110.

Ujumbe - Sehemu ya Pili

111.

Ujumbe - Sehemu ya Tatu

112.

Ujumbe - Sehemu ya Nne

113.

Ngano ya kwamba Qur’ani imebadilishwa 159

11:06 AM

Page 159


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 114.

Iduwa ya Kumayili

115.

Maarifa ya Kiislamu.

116.

Ukweli uliopotea sehemu ya Kwanza

117.

Ukweli uliopotea sehemu ya Pili

118.

Ukweli uliopotea sehemu ya Tatu

119.

Ukweli uliopotea sehmu ya Nne

120.

Ukweli uliopotea sehmu ya Tano

121.

Johari zenye hekima kwa vijana

122.

Safari ya kuifuata Nuru

123.

Idil Ghadiri

124.

Myahudi wa Kimataifa

125.

Kuanzia ndoa hadi kuwa Wazazi

126.

Visa vya kweli sehemu ya Kwanza

127.

Visa vya kweli sehemu ya Pili

128.

Muhadhara wa Maulamaa

129.

Mwanadamu na Mustakabali wake

130.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Kwanza

131.

Imam Ali binamu ya Mtume Sehemu ya Pili

132.

Khairul Bariyyah

133.

Uislamu na mafunzo ya kimalezi

134.

Vijana ni Hazina ya Uislamu.

135.

Yafaayo kijamii

136.

Kusoma sura zenye Sijda ya wajibu

137.

Taqiyya

138.

Vikao vya furaha

139.

Shia asema haya Sunni asema haya Wewe wasemaje? 160

11:06 AM

Page 160


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3 140.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Kwanza

141.

Uislamu na Mazingatio Sehemu ya Pili

142.

Azadari-Kuhuzunika na Kuomboleza

143.

Sunna katika Kitabu Fiqhi al-Sunnah

144.

Mtazamo Mpya - Wanawake katika Uislamu

145.

Kuonekana kwa Allah

146.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Kwanza)

147.

Tabia njema kwa Mujibu wa Ahlul-Bayt (Sehemu ya Pili)

148.

Ndugu na Jirani

149.

Ushia ndani ya Usunni

150.

Maswali na Majibu

151.

Mafunzo ya hukmu za ibada

152

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni Na 1

153.

Ahlul Bayt ndani ya tafsiri za Kisunni Na 2

154.

Ahlul Bayt ndani ya tafsir za Kisunnu Na.3

155.

Kati ya Alama kuu za dini ni Swala ya Jamaa na Adabu za Msikiti na Taratibu zake

156.

Abu Huraira

157.

Uadilifu katika Uislamu

161

11:06 AM

Page 161


Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No 3 Check Lubumba.qxd

7/1/2011

11:06 AM

Ahlul Bayt ndani ya Tafsir za Kisunni No.3

BACK COVER Ahlul Bayt, yaani Watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ni viongozi ambao Mtume alituusia tuwafuate. Katika hotuba yake ndefu na maarufu aliyoitoa pale Ghadir Khumm katika msafara wake wa kurejea kutoka Hija yake ya mwisho, Mtukufu Mtume SAW alisema haya mbele ya masahaba na mahujaji zaidi ya laki moja: “...Nakuachieni vitu viwili vizito: Qur’ani na Ahlul Bayt wangu. Viwili hivyo havitaachana mpaka vinifikie katika [hodhi ya] Kawthar. Nawausia juu ya Ahlul Bayt wangu! Angalieni jinsi mtakavyojihusisha nao. Kama mkishikamana na viwili hivi hamtapotea kamwe...” (kwa maelezo zaidi soma kitabu cha al-Ghadir) Lakini bahati mbaya sana sio Waislamu wote wanaowafuata Ahlul Bayt AS pamoja na kwamba wanavyuoni wa madhehebu zote wameandika habari zao katika vitabu vyao na kuonesha kwamba hawa ni viongozi wa Umma huu wa Kiislamu. Mwandishi wa kitabu hiki anajaribu kuthibitisha hilo kwa kutoa rejea mbalimbali kutoka vitabu maarufu vya wanavyuoni wa Kisunni. Kimetolewa na kuchapishwa na: Alitrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 Simu/Nukushi: +255 22 2127555 Barua Pepe: alitrah@raha.com Tovuti: www.alitrah.org Katika mtandao: www.alitrah.info

162

Page 162


Issuu converts static files into: digital portfolios, online yearbooks, online catalogs, digital photo albums and more. Sign up and create your flipbook.